fbpx

Gombo la 2 Salamu Mwafaka Namba 23, 24

Gombo la 2 Salamu Mwafaka Namba 23, 24

                                    

AMANI YA PEKEE YA MAWAZO

Hati miliki, Kimechapishwa tena 1953

Haki zote zimehifadhiwa

V. T. HOUTEFF

                                    

 

KUZISHIKA AMRI MOYO WA JIWE NA NIA YA MWILI

WATU AMBAO NI VIGUMU KUPATA NAFASI

                                    

1

ANDIKO LA SALA

Wapanzi Wa Mbegu

Nitasoma kutoka katika Mafunzo ya Kristo kwa Mifano, kuanzia kwa ukurasa wa 57. {2TG23: 2.1}

“Wapanzi wa mbegu wana kazi ya kufanya katika kuiandaa mioyo ili ipokee injili. Katika ukasisi wa dunia kuna kuhubiri kupita kiasi, na kazi halisi chache sana ya moyo kwa moyo…. Kwa hivyo wapanzi wana kitu cha kufanya ili mbegu hiyo isiweze kusongwa na miiba au kuangamia kwa sababu ya kukosa udongo wa kina…. Kila mwamini… anapaswa kufunzwa kwamba hawezi tu kuokolewa na dhabihu ya Kristo, ila kwamba anapaswa kufanya maisha ya Kristo kuwa maisha yake na tabia ya Kristo kuwa tabia yake. Acha wote wafunzwe kwamba wanapaswa kubeba mizigo na kuukana mwelekeo wa asili. Waache wajifunze baraka za kufanya kazi kwa ajili ya Kristo, wakimfuata Yeye kwa kujikana nafsi, na kuvumilia ugumu kama askari wema. Waache wajifunze kuuamini upendo Wake na wamtwike Yeye masumbuko yao. Waache waonje furaha ya kuongoa nafsi kwa ajili Yake. Katika upendo na hamu yao kwa ajili ya waliopotea, watapoteza mtazamo wa kibinafsi. Anasa za dunia zitapoteza nguvu zake za kuvutia na mizigo yake ya kuvunja mioyo.” {2TG23: 2.2}

Tuombe kwamba tutaweza kutambua kuwa hatujaokolewa tu kwa dhabihu ya Kristo lakini kwamba tuna-paswa kujitahidi kuwa kama Yeye katika maisha na tabia, na tunavyokuwa na hamu ya wokovu wa wengine, maisha yetu yataburudishwa; ya kwamba tutafanya zaidi kazi ya moyo kwa moyo; kwamba tutabeba mizigo na kuukana mwelekeo wa asili. Hivyo anasa za dunia zitapoteza nguvu zake za kuvutia, na mzigo wake kupoteza nguvu yake ya kuvunja mioyo. {2TG23: 2.3}

2

KUZISHIKA AMRI, MOYO WA JIWE NA NIA YA MWILI

ANDIKO LA HOTUBA NA V. T. HOUTEFF

MCHUNGAJI WA WADAUDI WAADVENTISTA WA SABATO

SABATO, JANUARI 17, 1948

HEKALU LA MLIMA KARMELI

WACO, TEXAS

Nakala yetu ya Maandiko inapatikana katika Ufunuo 22:14,15. {2TG23: 3.1}

Ufu. 22:14,15 — “Heri wazifuao nguo zao, wawe na amri kuuendea huo mti wa uzima, na kuingia mjini kwa milango yake. Huko nje wako mbwa, na wachawi, na wazinzi, na wauaji, na hao waabuduo sanamu, na kila mtu apendaye uongo na kuufanya.”

Hapa tunaona kwamba wale tu ambao huzishika amri Zake ndio wanayo haki ya kuingia Mjini. Wakati kazi ya wokovu imekamilishwa na watu kuwa wamekusanywa nyumbani, watakuwapo wale ambao wataendelea kuzishika amri za Mungu, hata baada ya dhambi kutokomezwa. Dhambi hata hivyo haiwezi kutokomezwa wa-kati ambapo sheria imevunjwa, kwa sababu uvunjaji wake ni dhambi. (1 Yohana 3: 3, 4.) Amri za Mungu, unaona, ni za milele, na wakati tu Wakristo wataanza kuishi maisha ambayo Neno la Mungu hutetea, watajikuta wakiishi juu ya sheria; wakati huo watakuwa tu huru kutoka kwa uasi. {2TG23: 3.2}

3

Mwishowe, ikiwa amri za Mungu ni za milele, basi lazima ziwe zimekuwepo daima. Sabato ambayo ilifanywa na kutakaswa katika juma la uumbaji, kabla ya dhambi kuja, iko katika zile amri. Na, pia, Adamu hangaliweza kuwa alifanya dhambi iwapo amri, “Usiwe na miungu mingine ila Mimi,” isingalikuwapo wakati huo. {2TG23: 4.1}

Warumi 7:7 — “Tusemeje, basi? Torati ni dhambi? Hasha! Walakini singalitambua dhambi ila kwa sheria; kwa kuwa singalijua kutamani, kama torati isingalisema, Usitamani.”

Taarifa iliyovuviwa ya Mtakatifu Paulo huziweka amri kumi, unaona, katika mfumo wa Injili. Bila amri, ana-tangaza , wafuasi wa Injili wasingalijua dhambi ni nini. {2TG23: 4.2}

Aya ya 8-10 — “Lakini dhambi ilipata nafasi kwa ile amri, ikafanya ndani yangu kila namna ya kutamani. Kwa maana dhambi bila sheria imekufa. Nami nalikuwa hai hapo kwanza bila sheria; ila ilipokuja ile amri, dhambi ilihuika, nami nikafa. Nikaona ile amri iletayo uzima ya kuwa kwangu mimi ilileta mauti.”

Hapa tunaona kwamba sheria haiokoi bali huwa inahukumu; na kwamba bila sheria pasingalikuwa na dhambi. Sheria haikumwokoa Adamu na Hawa, lakini iliwahukumu kuwa wasiostahili ule mti wa Uzima na makao ya Edeni. Kwa kweli, iliwahukumu kufa. Sheria ni mwalimu tu wa haki. Ni hilo tu. Si mwokozi. {2TG23: 4.3}

Aya ya 12-14 — “Basi torati ni takatifu, na ile amri ni takatifu, na ya haki, na njema. Basi je!

4

Ile iliyo njema ilikuwa mauti kwangu mimi? Hasha! Bali dhambi, ili ionekane kuwa ni dhambi hasa, ilifanya mauti ndani yangu kwa njia ya ile njema, kusudi kwa ile amri dhambi izidi kuwa mbaya mno. Kwa maana twajua ya kuwa torati asili yake ni ya rohoni; bali mimi ni mtu wa mwilini, nimeuzwa chini ya dhambi.”

Watu ambao hutii sheria ya serikali hufikiri kwamba ni maagizo bora ya uhuru, lakini wale hufurahia kufanya dhambi, kwa wao sheria ni chukizo. Muuaji yeyote ambaye kwa sheria amehukumiwa kifo, kwa kawaida hai-furahii sheria iliyomhukumu, wala kwa watu walioitekeleza hukumu yake. Iwapo mtu kama huyo angalikuwa na njia yake mwenyewe, angaliiondoa sheria. Wahalifu wote wangaliweza kuiondolea mbali sheria ya Mungu, pia, kwa maana sheria asili yake ni ya rohoni, na wao ni wa mwili, wameuzwa chini ya dhambi. {2TG23: 5.1}

Nini kingalitokea ikiwa hakungalikuwa na sheria katika Ufalme wa Mungu, bila sheria dhidi ya mauaji na wizi, au dhidi ya chuki na wivu? Ni nani angependa kuwa katika Ufalme hata kwa muda? Iwapo hivyo ndivyo ingalivyokuwa, basi, hakika, tungaliweza kuwa bora zaidi katika falme za dunia. {2TG23: 5.2}

Sheria, zaidi ya hayo, sio msimbo wa maadili tu, lakini pia ni wa mwili, kwa maana dhambi dhidi ya sheria huwahusisha wazawa wa mwenye dhambi, pia. Huwazungusha mwilini “maovu ya baba juu ya watoto hadi ki-zazi cha tatu na cha nne.” Kut. 20: 5. {2TG23: 5.3}

Kisha, pia, kila mzawa wa Adamu kiasili huzaliwa katika dhambi, ametolewa kwa dhambi: {2TG23: 5.4}

Aya ya 15 — “Maana sijui nifanyalo, kwa sababu lile nilipendalo, silitendi; bali lile nilichukialo ndilo ninalo-litenda.”

5

Kama hili likiwa fungu la mwanadamu, mwanadamu wa mwili huchukia sheria ya Mungu, na zaidi hivyo kwa sababu huingilia nia yake. {2TG23: 6.1}

Aya ya 16 — “Lakini kama nikilitenda lile nisilolipenda, naikiri ile sheria ya kuwa ni njema.”

Mtu akiuepuka wizi, hukiri kwamba sheria ni nzuri na ya ufanisi, ingawa kiasili anaweza kupenda wazo la kuiba. {2TG23: 6.2}

Aya ya 17-23 — “Basi sasa si mimi nafsi yangu ninayetenda hilo, bali ni ile dhambi ikaayo ndani yangu. Kwa maana najua ya kuwa ndani yangu, yaani, ndani ya mwili wangu, halikai neno jema; kwa kuwa kutaka na-taka, bali kutenda lililo jema sipati. Kwa maana lile jema nilipendalo, silitendi; bali lile baya nisilolipenda ndilo nilitendalo. Basi kama lile nisilolipenda ndilo nilitendalo, si mimi nafsi yangu nilitendaye, bali ni ile dhambi ikaayo ndani yangu. Basi nimeona sheria hii, ya kuwa kwangu mimi nitakaye kutenda lililo jema, lipo lililo ba-ya. Kwa maana naifurahia sheria ya Mungu kwa utu wa ndani, lakini katika viungo vyangu naona sheria iliyo mbali, inapiga vita na ile sheria ya akili zangu, na kunifanya mateka wa ile sheria ya dhambi iliyo katika viun-go vyangu.”

Hapa, unaona, tumezaliwa na sheria ya dhambi iliyo ndani yetu, na kwa hivyo ni muhimu kabisa kwa sheria ya Mungu kutuzuia kutenda dhambi. {2TG23: 6.3}

Aya ya 24, 25 — “Ole wangu, maskini mimi! Ni nani atakayeniokoa na mwili huu wa mauti? Namshukuru Mungu, kwa Yesu Kristo Bwana wetu. Basi, kama ni hivyo, mimi mwenyewe kwa akili zangu naitumikia she-ria ya Mungu, bali kwa mwili wangu sheria ya dhambi.”

Naam, Mungu na sheria Yake katika nia zetu, ambazo huwa tunapata tu kwa kulisoma Neno la Mungu

6

Ndilo tumaini letu pekee la ushindi kwa sheria ya dhambi na mwili. {2TG23: 6.4}

Warumi 8:1 — “Sasa, basi, hakuna hukumu ya adhabu juu yao walio katika Kristo Yesu.”

Wakati tunapompokea Kristo kama Mwokozi wetu, makosa yetu yote dhidi ya sheria yanafutwa, na kulipwa kwa kifo cha Kristo. Isingalikuwa hivi sisi wenyewe tungalipaswa kulipa adhabu ya kifo, ambayo hakuna ufufuo wa uzima wa milele. {2TG23: 7.1}

Warumi 8:2 — “Kwa sababu sheria ya Roho wa uzima ule ulio katika Kristo Yesu imeniacha huru, mbali na sheria ya dhambi na mauti.”

Hapa mtume hujulisha sheria nyingine, sheria ya Roho wa uzima — sheria tatu kwa ujumla: (1) sheria ya amri kumi, (2) sheria ya mwili, (3) sheria ya Roho wa uzima. Lakini sheria hii ya tatu, tukumbuke, i ndani ya Kristo, na hutufanya kuwa huru kutoka kwa sheria ya dhambi na kifo iwapo tu tunakaa ndani Yake. {2TG23: 7.2}

Warumi 8:3-11 — “Maana yale yasiyowezekana kwa sheria, kwa vile ilivyokuwa dhaifu kwa sababu ya mwili, Mungu, kwa kumtuma Mwanawe mwenyewe katika mfano wa mwili ulio wa dhambi, na kwa sababu ya dhambi, aliihukumu dhambi katika mwili; ili maagizo ya torati yatimizwe ndani yetu sisi, tusioenenda kwa kufuata mambo ya mwili, bali mambo ya roho. Kwa maana wale waufuatao mwili huyafikiri mambo ya mwili; bali wale waifuatao roho huyafikiri mambo ya roho. Kwa kuwa nia ya mwili ni mauti; bali nia ya roho ni uzi-ma na amani.”

“Kwa kuwa nia ya mwili ni uadui dhidi ya

7

Mungu: kwa maana haitii sheria ya Mungu, wala haiwezi kuitii. Kwa hivyo basi wale waufuatao mwili hawawe-zi kumpendeza Mungu. Lakini ninyi hamwufuati mwili, bali mwaifuata Roho, ikiwa Roho wa Mungu anakaa ndani yenu. Lakini mtu awaye yote asipokuwa na Roho wa Kristo, huyo si Wake. Na Kristo akiwa ndani yenu, mwili wenu umekufa kwa sababu ya dhambi; bali Roho i hai kwa sababu ya haki. Lakini ikiwa Roho wake Yeye aliyemfufua Kristo katika wafu anakaa ndani yenu, Yeye aliyemfufua Kristo katika wafu ataihuisha na miili yenu iliyo katika hali ya kufa kwa Roho Wake anayekaa ndani yenu.” {2TG23: 7.3}

Ni haki yetu kuwa na Roho yule yule ambaye alikuwa ndani ya Kristo. Kwa kweli, lazima tuwe na Roho huyu ikiwa tutatembea katika upya wa maisha, na iwapo tutashiriki katika ufufuo wa wenye haki. {2TG23: 8.1}

Kutoka kwa mahubiri ya Paulo unaona kwamba kuwa Mkristo humaanisha kuchunga kila hatua unayopiga, na kufanya vita na mwili wako mwenyewe, usije kimakusudi ukaanguka katika shimo ambalo hakuna kuokoka. Mkristo, zaidi ya hayo, hawezi kutenda dhambi; haki yake katika Kristo imehifadhiwa kabisa, kwa maana Kristo amelipa adhabu ya dhambi zake za zamani. Zaidi ya hayo, ikiwa atafanya dhambi tena bila kukusudia, anaye Wakili wa kuitetea kesi yake, Yesu Kristo, mwenye haki. Hivyo ni kwamba ingawa mwenye haki ataanguka ma-ra saba kwa siku, yeye huinuka, bado huendelea mbioni na mwishowe hushinda. {2TG23: 8.2}

Lakini tuseme kwamba ikupase kupambana kuzishika amri za Mungu katika Ufalme wa Mungu milele yote, utapambana kwa bidii unavyojitahidi sasa? Tuseme sheria ya mwili iweze kukaa nawe milele? — Nini

8

basi? Je! Ungaliweza wakati huo kuwa na hamu kama ulivyo sasa kwa ajili ya nafasi katika Ufalme? Mungu hu-tuambia cha kutarajia. {2TG23: 8.3}

Yer. 31:31-34 — “Angalia, siku zinakuja, asema Bwana, nitakapofanya agano jipya na nyumba ya Israeli, na nyumba ya Yuda. Si kwa mfano wa agano lile nililolifanya na baba zao, katika siku ile nilipowashika mkono, ili kuwatoa katika nchi ya Misri; ambalo agano langu hilo walilivunja, ingawa nalikuwa mume kwao, asema Bwana. Bali agano hili ndilo nitakalofanya na nyumba ya Israeli, baada ya siku zile, asema Bwana; Nitatia sheria yangu ndani yao, na katika mioyo yao nitaiandika; nami nitakuwa Mungu wao, nao watakuwa watu wangu. Wala hawatamfundisha kila mtu jirani yake, na kila mtu ndugu yake, wakisema, Mjue Bwana; kwa maana watanijua wote, tangu mtu aliye mdogo miongoni mwao hata aliye mkubwa miongoni mwao, asema Bwana; maana nitausamehe uovu wao, wala dhambi yao sitaikumbuka tena.”

Hapa ipo ahadi ya mkataba mpya, agano jipya. Sio kama lile Mungu alifanya na watangulizi wetu katika siku waliyotoka Misri, siku ambayo Yeye aliziandika zile amri kwenye mbao za mawe na hivyo kuzishika. Badala yake Yeye anafanya agano jipya, agano la kuziandika haswa kwa mioyo yetu. Wakati huo kila mmoja wetu at-amjua Yeye bila kufunzwa. {2TG23: 9.1}

Tambua, hata hivyo, Yeye hatafanya sheria mpya, ila agano jipya, mkataba mpya wa kutunza sheria. Tofauti ni kwamba badala Yeye kuiandika sheria juu ya mbao za mawe, Yeye ataiandika kwa mbao za

9

moyo, kiti ambacho sheria ya dhambi sasa humiliki. {2TG23: 9.2}

Agano hili, unaona, litafanywa na nyumba zote ya Israeli na ya Yuda, — na watu wote wa Mungu. {2TG23: 10.1}

Andiko, kumbuka, halisemi kwamba hatuwezi kutunza sheria ikiwa bado imeandikwa kwenye mbao za mawe, lakini inasema wazi kwamba tunaweza, kwa sababu wale walioivunja sheria wanakemewa kwa kufanya hivyo. Tunaweza, kwa hivyo, hata sasa kwa taabu kuzishika amri ingawa bado zimeandikwa kwa mawe. Kwa minajili ya raha Wakristo wengi wangetaka sheria itanguliwe, na wengine hujifanya waamini kwamba imeon-dolewa, ingawa sheria ya pekee ambayo imeondolewa ni sheria ya sherehe, ya kafara, kivuli cha Mwana-Kondoo wa Mungu. {2TG23: 10.2}

Je! itakuwapo tofauti gani iwapo sheria itaandikwa kwa mawe, au kwa mioyo yetu? — Uzoefu wa Nebukad-nezza, mfalme wa Babeli unafichua jibu. {2TG23: 10.3}

Iwapo mfalme kwa sharti angalilazimishwa kuishi na ng’ombe, katika hori au kondeni, angalijiua iwapo inga-liwezekana. Lakini mara tu Mungu alipouondoa moyo wa kibinadamu kutoka kwake, na kuweka moyo wa ng’ombe maksai ndani yake, mfalme huyo aliridhika kabisa kuwa pamoja na ng’ombe, na hakuridhika kabisa kuishi katika ikulu yake. {2TG23: 10.4}

Laiti kitu kama hicho kingalifanywa kwa yeyote kati yetu, tamaa zetu zingalikuwa sawa na za mfalme. Vivyo hivyo, wakati ambapo moyo wa jiwe umeondolewa kutoka kwetu, na moyo wa nyama pamoja na

10

sheria ya Mungu iliyoandikwa juu yake umewekwa ndani yetu, wakati huo itakuwa vigumu mno kutenda dhambi, na kupendezwa sana kuzishika amri za Mungu. Na kwa hivyo hautahitaji kupambana kuitunza sheria ya Mungu katika Ufalme, kama unavyofanya hapa. Wakati huo utaridhika kabisa kuishi maisha yasiokuwa na dhambi. Kwa kweli hautataka kufanya dhambi zaidi ya vile usingetaka kufa sasa. {2TG23: 10.5}

Ajabu kweli! lakini ni lini tunaweza kutarajia muujiza huu kutukia? Ili kupata jibu la swali hili, tunahitaji kuunganisha unabii wa Yeremia na unabii wa Ezekieli wa tukio hilo hilo: {2TG23: 11.1}

Yer. 31:8 — “Tazama, nitawaleta toka nchi ya kaskazini, na kuwakusanya katika miisho ya dunia, na pamoja nao watakuja walio vipofu, na hao wachechemeao, mwanamke mwenye mimba, na yeye pia aliye na utungu wa kuzaa; watarudi huko, jeshi kubwa.”

Ezek. 36:24–28 — “Maana nitawatwaa kati ya mataifa, nami nitawakusanya na kuwatoa katika nchi zote, na kuwarudisha katika nchi yenu wenyewe. Nami nitawanyunyizia maji safi, nanyi mtakuwa safi; nitawatakaseni na uchafu wenu wote, na vinyago vyenu vyote. Nami nitawapa ninyi moyo mpya, nami nitatia roho mpya nda-ni yenu, nami nitatoa moyo wa jiwe uliomo ndani ya mwili wenu, nami nitawapa moyo wa nyama. Nami nitatia roho yangu ndani yenu, na kuwaendesha katika sheria zangu, nanyi mtazishika hukumu zangu, na kuziten-da. Nanyi mtakaa katika nchi ile niliyowapa baba zenu, nanyi mtakuwa watu wangu, nami nitakuwa Mungu wenu.”

11

Zile kumbu kumbu kutoka kwa manabii wote wawili zinaonyesha wazi wakati muujiza huu utakapotekelezwa mioyoni mwa watu wote wa Mungu. Manabii wote wawili wanaifanya iwe wazi kama inavyoweza kufanywa, kwamba badiliko hili la moyo litatukia katika Nchi Takatifu, Palestina, mwanzoni mwa ufalme ambao Mungu ameahidi kuusimamisha “katika siku za wafalme hao” (Dan. 2: 44), sio baada ya siku zao. Yeye zaidi ya hayo nasema kwamba Atatuchukua kutoka kwa mataifa na kutukusanya kutoka nchi zote, na kutupeleka katika nchi yetu (Ezek. 36:24), nchi ambayo baba zetu waliishi (Ezek. 36:28). “Basi,” kwa wakati huo, Uvuvio husema, sio kabla, Atatunyunyizia maji safi, Atatusafisha uchafu wetu wote, na sanamu zetu zote. Pia, moyo mpya Yeye atauweka ndani yetu (Ezek. 36:26). Yeye atatupa Roho wake na kusababisha tuyafuate maagizo Yake, na kuzishika hukumu Zake (Ezek. 36:27). Uyasome mwenyewe maandiko haya na uone iwapo yanasema yote ni-nayojaribu kuwaambia yanasema. {2TG23: 12.1}

Yer. 31:35-40 — “Bwana asema hivi, awapaye watu jua, ili kuwa nuru wakati wa mchana, na amri za mwezi na nyota, ili kuwa nuru wakati wa usiku, aichafuaye bahari, hata mawimbi yake yakavuma; Bwana wa majeshi, ndilo jina lake; Amri hizi zikiondoka, zisiwe mbele yangu, asema Bwana, ndipo wazao wa Israeli nao wataacha kuwa taifa mbele yangu milele. Bwana asema hivi, Kama mbingu zikiweza kupimwa, na misingi ya dunia ikiweza kugunduliwa huko chini, ndipo wazao wa Israeli pia nitawatupilia mbali, kwa ajili ya hayo yote waliyoyatenda, asema Bwana. Tazama, siku zinakuja, asema Bwana, mji huu utakapojengwa kwa ajili ya Bwana, toka buruji ya Hananeli hata lango la pembeni. Na kamba ya kupimia itaendelea moja kwa moja hata mlima Garebu,

12

tena itazunguka na kufika Goa. Na bonde lote la mizoga, na majivu, na mashamba yote mpaka kijito Kidroni, mpaka pembe ya lango la farasi, upande wa mashariki, patakuwa patakatifu kwa Bwana; hapatang’olewa, wala hapatabomolewa, hata milele.”

Watu wanaweza kuamini chochote wanachotaka kuamini, lakini tutaamini Bibilia. Ninajua kwamba hili ndilo Biblia hufundisha, na kwamba hii ndio ratiba ya Mungu kwa matukio haya. Na kwa sababu huu ni mpango wa Mungu wa kuwatakasa watu Wake, na kwa ajili yao kuupokea moyo mpya, ujumbe wetu unakuwa muhimu sana kwa wote wanaotamani kuwa katika Ufalme. Tunaweza kuweka moyo na nafsi yetu katika kazi hiyo, hata hivyo, na kumwachia Mungu matokeo. Iwapo tungaliweza daima kuwa wote kwa ajili ya Mungu na bila yeyote kwa unafsi, ni sasa. {2TG23: 13.1}

13

WATU AMBAO NI VIGUMU KUPATA NAFASI

ANDIKO LA HOTUBA NA V. T. HOUTEFF

MCHUNGAJI WA WADAUDI WAADVENTISTA WA SABATO

SABATO, JANUARI 24, 1948

HEKALU LA MLIMA KARMELI

WACO, TEXAS

Nakala ya mada yetu ya alasiri hii inapatikana katika Mithali 29:18. {2TG24: 14.1}

Mit. 29:18 — “Pasipo maono, watu huangamia; Bali ana heri mtu yule aishikaye sheria.”

Mwanzoni mwa uchambuzi wetu hebu tuhakiki ni kwa kadiri gani maandishi haya yametimizwa. Katika siku za Musa, unakumbuka, Wamisri hawakuwa na maono, lakini Waebrania walikuwa na maono na nabii wa kuyafasiri maono. Pamoja na kipawa hiki kati yao wakati walipokuja dhidi ya Bahari ya Shamu Waebrania wali-hifadhiwa, lakini Wamisri waliangamia. “Mtu mwenye hekima,” unaona, hakuwa akikisia aliponena “Pasipo maono, watu huangamia.” {2TG24: 14.2}

Tuseme, hata hivyo, watu waweze kuwa na maono, lakini hakuna mfasiri kwa yale maono. Nini basi? Wacha tuone: Unakumbuka kwamba Nebukadnezza, mfalme wa Babeli, alikuwa na maono usiku lakini hakuwa na mfa-siri, la, hapakuwa hata mmoja kati ya watu wake wote wenye busara katika ufalme. Kwa hivyo, kwa vile ha-wakuweza kuyafasiri maono yake (Dan. Sura ya 2), iliamuriwa kwamba wauawe, na wangeangamia ikiwa Dan-ieli, mtu wa Mungu, asingalikuwa katika nchi kuyafasiri maono ya mfalme. {2TG24: 14.3}

14

Farao pia alikuwa na maono lakini hapakuwa na mfasiri. Na kama Yusufu asingalikuwa katika nchi ya Misri kuyafasiri maono ya mfalme, Wamisri na dunia yote ya zamani wangaliangamia wakati wa ile miaka saba ya njaa. Lile ambalo Biblia husema, ni kweli asilimia mia moja, unaona. {2TG24: 15.1}

Sasa hebu nikuulize swali rahisi. Ikiwa watu bila maono na bila mfasiri huangamia, basi watayapataje maono na mfasiri? Mtakatifu Petro hutoa kidokezi: {2TG24: 15.2}

2 Pet. 1:19, 20 — “Nasi tuna lile neno la unabii lililo imara zaidi, ambalo, mkiliangalia, kama taa ing’aayo ma-hali penye giza, mwafanya vyema, mpaka kutakapopambazuka, na nyota ya asubuhi kuzuka mioyoni mwenu. Mkijua neno hili kwanza, ya kwamba hakuna unabii katika maandiko upatao kufasiriwa kama apendavyo mtu fulani tu.”

Hapa tunaambiwa kwamba unabii, maono, ni kipimo cha tindi kali ambacho unaweza kuhukumu unaodaiwa kuwa Ukweli wa Bibilia; yaani, iwapo jambo hilo haliko katika unabii, ikiwa hamna maono yake yanayopa-tikana katika maandishi ya manabii, basi, hamna ukweli ndani yake. Naam, maono ya manabii yanapaswa ku-wa maono yetu iwapo ni lazima tuhifadhiwe. Unabii, hata hivyo, anateta sio ufasiri wa apendavyo mtu tu kul-iko yalivyokuwa maono ya Nebukadnezza na ya Farao, kwamba wenye hekima wa watu wowote hawawezi kuufasiri unabii wa Mungu uliositirika. Kwa nini? — {2TG24: 15.3}

Aya ya 21 — “Maana unabii haukuletwa po pote kwa mapenzi ya mwanadamu; bali wanadamu walinena yali-yotoka kwa Mungu, wakiongozwa na Roho Mtakatifu.”

15

Hii ndio haswa unabii hauwezi kufasiriwa kama apendavyo mtu, sio bila Roho Ambaye aliuandikisha unabii kupitia watu watakatifu wa zamani. Hivyo, basi, unabii haufasiriwi kwa mapenzi ya wanadamu, ila kwa Roho wa Kweli, “Roho ya Unabii,” Roho yule yule ambaye aliuandikisha unabii. Hili, unaona, sio wazo langu. Ni lugha wazi ya Bibilia. Lakini labda lipo shaka katika akili zenu, na ikiwa ni hivyo tutaweza kufanya vyema kui-patia Biblia kipimo kingine cha tindi kali. {2TG24: 16.1}

Hebu, kwa hivyo, tena tuwatazame mfalme wa Babeli na wa Misri. Wafalme wote wawili waliwapatia wenye hekima wao nafasi ya kuyafasiri baadhi ya mambo ambayo tunapata sasa katika Bibilia. Wafalme wa nchi hizo za zamani hawakuwapa wenye hekima wao sio fursa yenye chambo cha tuzo nono kwa kuyafasiri maono, ila hata wakatishia kuwachinja iwapo wangeshindwa kufanya hivyo. Hii ilikuwa kweli haswa katika Babeli. Wenye hekima wao walishindwa na hata kwa uwazi na kwa busara wakakiri kwamba kuyafunua mambo ya siri ya Mungu haikuwa shughuli yao. {2TG24: 16.2}

Je! Vipimo hivi havina nguvu ya kutosha kumshawishi yeyote kati yenu kwamba mambo ya siri ya Mungu, kama vile unabii uliositirika, hayafunuliwi na watu wafaji, — la, wala sio na Ibilisi, kwamba wakati Mungu analitaka jambo liwe siri, hilo hubaki siri mpaka Yeye Mwenyewe alifunue? Basi, linapofunuliwa wote watajua kwamba Mungu Mwenyewe yu kazini. Je! Wenye hekima wa leo huwajifanyi kuwa wapumbavu kwa kuzianika fasiri zao kama wapendavyo za Maandiko ambayo hayajafunuliwa? {2TG24: 16.3}

Iwapo ni vigumu kabisa kwa akili ya kawaida kukiri kwamba amekosea, basi unambie

16

itakuwa rahisi namna gani wenye hekima wetu, ambao hufikiri wao husimama bila rika, kukiri makosa yao? Kwa maana hili ndilo haswa lazima wafanye kwa wasikilizaji wao iwapo wao wenyewe wataweza kuupokea unabii utakapofunuliwa na Roho Mtakatifu Mwenyewe. Na ikiwa hawawezi kuziacha fasiri zao za kibinafsi na kuchukua fasiri za Roho, je! hawatatenda dhambi dhidi ya Roho Mtakatifu? {2TG24: 16.4}

Wenye hekima wa Ukaldayo na wa Misri hawakuruhusiwa kuendeleza mawazo yao ya kibinafsi kuhusu kile maono ya wafalme yangaliweza kumaanisha, hivyo mwishowe ilikuwa rahisi wao kusema, “Hatujui.” Lakini hai-kuwa rahisi hata kidogo kwa makuhani, waandishi, na Mafarisayo katika siku ya Kristo kughairi yale waliokuwa wamewafunza watu, na wala haitakuwa rahisi kwa wafasiri wa kibinafsi wa leo, hata ingawa wanajua kwamba kukiri kwao kwa uaminifu na kwa taabu kunaweza kuwafanya kuwa mashujaa wakuu. {2TG24: 17.1}

Leo Fasiri za kibinafsi zimeidhuru na kuikanganya dunia zaidi kuliko wakati mwingine wowote. Tazama dunia ya leo iliyovunjika kwa madhehebu. Zimeugawanya Ukristo katika mamia ya madhehebu, chenga chenga za vipimo vyote, moja likihitilafiana na lingine. Ni nani awezaye kusema kwamba fasiri zao mbalimbali za kibin-afsi za Maandiko zimevuviwa, za kutegemewa, au zinafaa kwa kitu chochote isipokuwa kusababisha Wakristo kugombana na kuzozana kati yao juu ya nadharia na mafundisho? Je! Hawa wa kimbelembele wafasiri wa Maandiko wanawaleta Wakristo kwa umoja, wakiwaandaa kwa Pentekoste ya pili? au wanawagawanya na ku-wafanya wasifae? Je! Hawajifanyi kuwa wapumbavu wenyewe machoni pa ulimwengu ambao sio wa Ukristo? Ni wazi kuona kwamba wao si hata wenye hekima kama wenye hekima wa siku ya

17

Yusufu au ya Danieli. Inasikika vikali, najua, lakini itakuwa vibaya sana kuwaacha wakilala bila kufanya jambo la kuwaamsha. Hakuna mtu anayeweza kumtazama kipofu akitembea hadi ndani ya daraja lililo wazi bila kufan-ya jambo kumzuia asitumbukie kwenye mto. Iwapo hawawezi kuyafumbua macho yao sasa, basi ni nani anayeweza kusema kwamba wao sio watu ambao ni vigumu kupata nafasi? {2TG24: 17.2}

Fasiri zao za kinadharia za Maandiko zinaleta chokochoko ndani ya kila dhehebu, na wakati uo huo wafuasi wayo huomba na kuongea kuhusu kwamba wamepokea, au kuhusu kutarajia kupokea zawadi ya Roho! Wao hu-omba, sio wapate zawadi ya ufasiri uliovuviwa, sio kuruhusu ufasiri wao wa kibinafsi urekebishwe, au kuujua Ukweli vyema zaidi, lakini huomba wapokee zawadi ya kutenda miujiza! Naam, hilo ndilo wote wanafuata. Ufidhuli kama nini! na dhulma kama nini kwa Uwelekevu! {2TG24: 18.1}

Miujiza kwa kusudi gani? — Si kwa lengo lingine isipokuwa kuwakanganya hata umati mkubwa zaidi na fasiri zao za kibinafsi. Wanaweza kuwapumbaza wanadamu lakini ninakuambia hawawezi kamwe kumpumbaza Mun-gu, na ingalikuwa bora wasiendele kujaribu hilo. {2TG24: 18.2}

Sasa, tuseme tunayo maono na pia mfasiri, lakini tusiwe na imani. Basi nini? — Ikiwa hii ndio hali yetu, basi ninaamini kwamba katika hali ya akili kama hiyo isiyo na furaha tungalikuwa bora iwapo hatungalikuwa na maono wala mfasiri, kwa sababu iwapo tunayo maono na mfasiri, ila hatuna imani tutawajibishwa kwa kukataa yote mawili, na hivyo kutenda dhambi maradufu dhidi ya Roho Mtakatifu. Wakati huo tungalijikuta katika nafasi isiyofaa zaidi

18

kuliko Wayahudi. {2TG24: 18.3}

Hakuna msamaha wa kufanya dhambi dhidi ya Roho Mtakatifu, dhidi ya Uvuvio, kwa sababu ukikataliwa mara moja hakuna kitu kingine ambacho kwacho kinaweza kutumiwa kumleta mdhambi kwa Kristo. Kwa hivyo hakuna tumaini lingine kwa ajili ya mtu kama huyo, maana hakuna kitu zaidi ambacho Mbingu inaweza kufanya kumwaamsha kwa umasikini wake, na kwa hivyo hakuna tiba zaidi, hakuna msamaha wa dhambi. {2TG24: 19.1}

Lakini mmoja anaweza kusema, “Nina imani katika Bibilia, katika Neno la Mungu.” Tunaweza kuwa na imani zaidi katika Bibilia kuliko Wayahudi, lakini iwapo imani ya upande mmoja ilikuwa hasara kwa Wayahudi, basi itakuwaje kwa wengine? La, Wayahudi hawakuhukumiwa kwa ukosefu wa imani katika Bibilia, lakini kwa ku-kosa imani katika wajumbe wa Mungu, bila imani katika manabii na fasiri zao za Maandiko. Zaidi ya hayo, imani katika Bibilia bila imani kwa Mfasiri Ambaye aliiandikisha Bibilia ni vizuri kama kukiri kwamba mkate ni chaku-la cha maisha, lakini ukatae kuutafuna! Hebu tuone Biblia yenyewe inasema nini kuwahusu wa shari kama hawa: {2TG24: 19.2}

2 Nya. 36:14-17 — “Na zaidi ya hayo wakuu wote wa makuhani, na watu, wakakosa mno sawasawa na ma-chukizo yote ya mataifa; wakainajisi nyumba ya Bwana aliyoitakasa katika Yerusalemu. Naye Bwana, Mungu wa baba zao, akatuma kwao kwa mikono ya wajumbe wake, akiondoka mapema, na kutuma; kwa sababu ali-wahurumia watu wake, na makao yake; lakini waliwadhihaki wajumbe wa Mungu, na kuyadharau maneno yake, na kuwacheka manabii wake, hata ilipozidi ghadhabu ya Bwana juu ya watu wake, hata kusiwe na kuponya. Kwa hiyo akaleta juu yao mfalme

19

wa Wakaldayo, aliyewaua vijana wao kwa upanga nyumbani mwa patakatifu pao, asiwahurumie kijana wala mwanamwali, mzee wala mkongwe; akawatia wote mkononi mwake.’’

Waasi waliotajwa humu, unaona, hawakuachiliwa kwa mchinjo kwa sababu tu walikuwa wadhambi wakuu; Mungu aliwahurumia wakati walipokuwa wakitenda dhambi, na akatuma wajumbe kuwarekebisha na kuwapatia nuru. Lakini baada ya kuzikataa jumbe Zake, na kuwaua wajumbe Wake waliojazwa na Roho, walitenda dhambi dhidi ya Roho Mtakatifu, kisha hapakuwa na kitu kingine zaidi ambacho Yeye angalifanya isipokuwa kuwaru-husu maadui zao wawaangamize. {2TG24: 20.1}

Hebu tuuangalie mfano mwingine, huu nao katika wakati wa Yesu. Wayahudi katika wakati Wake walikuwa na imani kubwa zaidi katika Maandiko kuliko yeyote kabla yao. Kwa Maandiko walimshtaki, wakamhukumu, na wakamsulubisha Bwana. Kitu ambacho hawakuwa nacho imani kilikuwa fasiri za Yesu za Maandiko. Kama tokeo, miaka kadhaa baadaye mji wao uliharibiwa, na kila mmoja aliyepatikana ndani yake aliungua kama panya, kwa sababu tu walishindwa kutii maagizo ya Yesu: {2TG24: 20.2}

Luka 21:20-22 — “Lakini, hapo mtakapoona mji wa Yerusalemu umezungukwa na majeshi, ndipo jueni ya kwamba uharibifu wake umekaribia. Ndipo walio katika Uyahudi na wakimbilie milimani, na walio katikati yake wakimbilie nje, na walio katika mashamba wasiuingie. Kwa kuwa siku hizo ndizo za mapatilizo, ili yati-mizwe yote yaliyoandikwa.”

Pasipo maono, unaona, watu huangamia. Na pia bila mfasiri na bila imani

20

wao pia huangamia. Na hii ndio sababu “Roho ya Unabii” ni hitaji la lazima kabisa kwa watu wa Mungu katika vizazi vyote. {2TG24: 20.3}

Ulaodekia leo, unajua, u katika hali mbaya zaidi kuliko watu wowote katika wakati wowote mwingine, kwa kuteta kwamba hakuna hitaji la manabii, hakuna hitaji la ukweli zaidi, tayari wamewakataa, naam, kwa kweli wamewaua. Iwapo hawautarajii ukweli zaidi na ikiwa Yesu Kristo Mwenyewe aweze kuja na ukweli zaidi je! Hawatamsulubisha Yeye pia? Najua kwamba sitoi taarifa ya haraka, wala kutilia chumvi, na pia najua kwamba Bibilia itanitegemeza katika yale ninayosema, la sivyo nisingaliyasema. {2TG24: 21.1}

Tumeona tayari kwamba Maandiko sio ya ufasiri wa apendavyo mtu tu, na kwamba Ukristo kwa ujumla hauna aliyevuviwa, mfasiri aliyeteuliwa na Mungu, hata haudai kuwa na mmoja, na kwamba watu wamekan-ganyikiwa kama walivyokuwa wapumbavu kwa mnara wa Babeli wakati lugha yao ilipobadilishwa na lugha nyingi. {2TG24: 21.2}

Sasa, basi, iwapo ni Ukweli unaomfanya mtu yeyote kuwa huru, na ikiwa unakuja kupitia Uvuvio pekee, na iwapo Ukristo unashindwa kutambua hili na hivyo kumpa Mungu nafasi ya kuuokoa, basi nini itakuwa hatma yake, na pia hatma ya Kanisa lenyewe? Unalijua jibu {2TG24: 21.3}

Mzizi wa makosa , hata hivyo, unatoka ndani ya moyo wa kanisa ambalo linadai kuwa ni nuru ya ulimwengu, kwa maana linajihisi tajiri na limeongezeka na bidhaa, bila hitaji la Ukweli wala manabii licha ya ukweli kwamba Bwana Mwenyewe inaliambia kwamba ni nyonge, lenye mashaka, lenye upofu, umaskini na uchi, na karibu kutapikwa, na linahitaji kila kitu (Ufu. 3:14-18).

21

Kupuuza shtaka hili na kuendelea kusema hatuhitaji chochote ni kumtukana Bwana, na kumshtaki Mungu ya kuwa ameiacha dunia, Kanisa, na watu, na kuwaacha wote wafanye kadri wanavyoweza katika machafuko yao na kuutegemea mwili, wakitarajia kujiinua kutoka katika udanganyifu wao na gidamu za vyatu vyao! {2TG24: 21.4}

Lipo jambo moja tu ambalo watu wake wamefunzwa kulitafuta, nalo ni kuwatafuta manabii wa uongo, na kwa sababu watu hawatambui kwamba hapawezi kuwapo la uongo pale ambapo hakuna la ukweli, hamuwezi kuona mambo yao yasiyopatana? Na ni udanganyifu wa kutisha kama nini kwa watu kufikiri wako sawa ilhali wote wamekosea! — Shuhuda kwa Kanisa, Gombo la 3, uk. 253. Nasema wa kutisha, na namaanisha wa kutisha, kwa sababu iwapo wanaendelea kudhani kwamba wao ni matajiri na wamejitajirisha, wakiwa hawana haja ya kitu, ilhali wao wamepungukiwa kila kitu, hakika “watatapikwa nje.” {2TG24: 22.1}

Iwapo hawataamka kwa umaskini wao, utakuwa muujiza mkubwa tangu mwanzo wa ulimwengu. Nasema utakuwa mkubwa zaidi, kwa sababu wanahisi hawana msaada wa Mungu kupitia Uvuvio, hawatarajii wowote, wanachukia bila sababu, wenye kushuku, na wanamwogopa kila mtu ambaye hakubaliani na wazo lao waliloji-jengea. Wao kwa hivyo ni wagumu zaidi kuwafikia na Ukweli wa kuokoa wa leo kuliko walivyokuwa Waya-hudi wa jana. {2TG24: 22.2}

Je! Kanisa litabaki milele katika udanganyifu wake, au litaamka kwa hitaji lake kuu? Maswali haya yatajibiwa iwapo tutafungua Ufunuo: {2TG24: 22.3}

“Nchi ikamsaidia mwanamke, nchi

22

ikafunua kinywa chake ikaumeza mto ule alioutoa yule joka katika kinywa chake. Joka akamkasirikia yule mwa-namke, akaenda zake afanye vita juu ya wazao wake waliosalia, wazishikao amri za Mungu, na kuwa na ushuhuda wa Yesu.… kwa maana ushuhuda wa Yesu ndio Roho ya Unabii.” Ufu 12:16,17; 19:10. {2TG24: 23.1}

Hapa lipo jibu la Bibilia yenyewe, ambalo linasema kwamba watakuwako watu ambao watakuwa na Ushuhu-da wa Yesu Kristo wakati ambapo nchi itayameza mafuriko, wanafiki. Na kwa sababu tukio hili bado ni la baadaye, linaonyesha kwamba atakuwako nabii katika Kanisa, kwa maana ufasiri wa Bibilia yenyewe “Ushuhu-da wa Yesu Kristo,” ni “Roho ya Unabii” (Ufu. 19:10). Sehemu ya kwanza ya sura ya 19 utaona inaelezea kwamba Roho ya Unabii inaletwa kwao na mtu, “mtumwa mwenza,” na ya kwamba wale wanaompokea hujihisi kama wamwabudu yeye, lakini huwaelekeza wamwabudu Mungu, sio mwanadamu. {2TG24: 23.2}

Masalia walioachwa, watakatifu ambao hawakumezwa na mafuriko ya Joka wakati ambapo nchi ilifunua kin-ywa chake, unakumbuka wanao “ushuhuda wa Yesu Kristo,” iliyo hai Roho ya Unabii amilifu kati yao. Kanisa kwa hivyo halitalala milele, watu wa kweli wa Mungu wataamka kwa umaskini wao, watafaidika kwa mwito huu wa kuamsha, lakini mafuriko ya Joka yatayajaza matumbo ya nchi. {2TG24: 23.3}

Mtu yeyote asijidanganye kwa kufikiria kwamba Bibilia yenyewe ndio amilifu Roho ya Unabii. Hebu tuwe watu wa Mungu wa kweli, welekevu wa kufikiri, sio wawindaji wa chambo. Bibilia, unajua, bila njia ya kibinadamu, sio amilifu kana kwamba Ni wino na karatasi tu. Zaidi ya hayo, Roho, pia, mbali na mwanadamu, pia sio amilifu:

23

Naye, pia, hutenda kazi kupitia chombo cha kibinadamu. Kwa hivyo, bila mfasiri aliyevuviwa unabii uliositirika na Roho ambaye huufunua sio amilifu. Zaidi ya hayo, itawezaje kusemwa kuhusu kundi haswa moja kwamba lina Roho ya Unabii, ilhali madhehebu yote katika Jumuiya ya Kikristo yana Bibilia? {2TG24: 23.4}

Masalia, ambao wana roho ya Unabii kati yao wameelekezwa kuzishika amri za Mungu, ilhali wengine wote wa dunia, kupitia ushawishi wa lile Joka, unawatesa. Katika nuru hii, unaona tena kwamba masalia wataokoka kutoka kwa udanganyifu wa kibinafsi ambao sasa umeupotosha ulimwengu wote wa Kikristo. {2TG24: 24.1}

Mwishowe, yanaweza kuwa nini mto kama mafuriko yanayotoka kinywani mwa lile Joka iwapo sio wafasiri wa Maandiko waliochochewa na lile Jokaambao kupitia kwao hutarajia kusababisha Kanisa lichukuliwe? {2TG24: 24.2}

Kweli manabii waliojiteua wenyewe katika Israeli ya leo ni wengi kwa idadi kuliko manabii katika siku ya Eliya. Hapa upo ukweli ambao ni watu viziwi na vipofu pekee watajaribu kuukana. Hapana, sineni kimzaha kwa kuufichua Ukweli huu, ninafanya hivyo tu kwa sababu ni lazima. Mungu anataka watu Wake wawe na Ukweli, na kwa hivyo sina budi ila kuusema. {2TG24: 24.3}

Mafuriko haya ambayo Kanisa lililo hai milele linapambana kutengeneza njia yake, tunaambiwa, yatamezwa, na nchi. Yataondolewa mbali kama walivyokuwa manabii waliojiteua wenyewe katika siku ya Musa: ambao ni Kora, Dathani, na Abiramu, “wakuu wa mkutano, waliokuwa wateule wa mkutano, watu wenye sifa.” Hes. 16:2. Hawa na wafuasi na wamana wao wote

24

“Nchi ikafunua kinywa chake, na kuwameza, na watu wa nyumba zao, na wote walioshikamana na Kora, na vyombo vyao vyote.” Hes. 16:32. {2TG24: 24.4}

Hapa tuna kivuli, na mfano, pia, ukionyesha kwamba kile kilichofanyika katika siku ya Musa kwa watu am-bao walijaribu kujikweza wenyewe hadi kwa ofisi ya Roho ya Unabii, kitafanywa kwa watu ambao wanaitamani ofisi hiyo katika siku yetu. Wao ni watu ambao ni vigumu kupata nafasi. {2TG24: 25.1}

Hivyo ni kwamba yeyote ambaye ameitwa kufunza lile Roho ya Unabii huwafunulia, hapaswi kutamani ufasiri ambao haujavuviwa wa Maandiko. Ikiwa watafanya hivyo, wao na wote wanaowafuata watapata tha-wabu yao isipokuwa watubu. {2TG24: 25.2}

Gal. 3:1-3; 4:16 — “Enyi Wagalatia msio na akili, ni nani aliyewaloga, ninyi ambao Yesu Kristo aliwekwa wa-zi mbele ya macho yenu ya kuwa amesulibiwa? Nataka kujifunza neno hili moja kwenu. Je! Mlipokea Roho kwa matendo ya sheria, au kwa kusikia kunakotokana na imani? Je! Mmekuwa wajinga namna hii? Baada ya kuanza katika Roho, mnataka kukamilishwa sasa katika mwili?” “Je! Nimekuwa adui wenu, kwa sababu na-waambia yaliyo kweli?”

Hebu tena niwaonyeshe watu ambao wako kwenye hatari kubwa ya kushindwa kumtumikia Bwana jinsi Roho huelekeza. Hili tunaweza kuona tena kutoka kwa mifano ya zamani. Naweza kurejea nyuma mbali kabisa kwa Kaini na Abeli. Kaini alikuwa mzaliwa wa kwanza wa Adamu, na kwa mujibu wa kanuni ya Bibilia, mzali-wa wa kwanza alipaswa kuwa kiongozi, kuhani. Kutoka kwa uzoefu wake tunajua kwamba yeye, kiongozi, mchungaji katika familia, alikuwa wa kwanza katika historia kuabudu kulingana na ufasiri wake wa kibinafsi wa dini. Na Abeli kushindwa kuifuata njia ya ibada ya Kaini, Abeli aliuawa mikononi mwake Kaini. {2TG24: 25.3}

25

Ijayo, nitawapeleka kwa wakati wa Abrahamu. Mnajua kwamba Ishmaeli alikuwa mzaliwa wa kwanza wa Abrahamu, na Isaka mzaliwa wake wa pili. Ishmaeli, mzaliwa wa kwanza, akiwa wa mwili alimtesa Isaka, yule aliyezaliwa kwa roho. {2TG24: 26.1}

Kisha, tukija kwa mapacha wa Isaka, Esau na Yakobo: Esau alikuwa mtu hodari wa siku hiyo, na mzaliwa wa kwanza nyumbani; yake ilikuwa haki ya kuzaliwa kuongoza katika huduma ya Mungu. Lakini yeye, pia, alikuwa na tamaa ya uwindaji kuliko kazi ya Roho. Hivyo aliweka thamani ndogo sana kwa kazi ya Roho hivi kwamba aliuza haki yake ya kuzaliwa kwa mchuzi wa ndengu. Licha ya hili, bado alitarajia baraka zilizoahidiwa kutoka kwa baba yake, lakini Majaaliwa yaliingilia kati! Alipogundua hasara yake, yeye, kwa kweli, kama Kaini wa za-mani, alitafuta kumuua ndugu yake. {2TG24: 26.2}

Katika wakati wa Musa tunapata roho ile ile akitenda kazi kupitia kwa wazaliwa wa kwanza, kwa maana wale wote waliokuwa na miaka ishirini au zaidi walipoondoka Misri, waliangamia jangwani, isipokuwa Kalebu na Yoshua. {2TG24: 26.3}

Kutoka kwa hivi vielelezo katika siku za mifano yetu, tunaona kwamba wale ambao ni wa kwanza, na wale ambao ni hodari, ambao haki yao ya kuzaliwa kanisani huwapa upendeleo wa kuwaongoza watu, wako kwenye hatari kubwa ya kukosea au kupoteza nafsi zao. Lakini wa kiwa na picha wazi kama hii mbele yao kupitia mifano hii ya Bibilia, tunatumai kwamba watamgeuka dhidi ya yule Joka mzee na kuponyoka kutoka katika mifumbato yake. Iwapo watatoka, hakika watatambuliwa kama mashujaa watu wa Mungu kama walivyokuwa Waebrania watatu baada ya kutoka katika tanuru la moto na kama Danieli baada ya kutoka kwenye tundu la simba. {2TG24: 26.4}

“Mwacheni mwanadamu, ambaye pumzi yake i katika mianzi ya pua yake;

26

kwa maana hudhaniwaje kuwa ni kitu?” Isa. 2:22. Ukweli uliovuviwa, Ndugu, Dada, ndilo jambo pekee ambalo ni muhimu, na wakati wewe tu unapouchunguza mwenyewe na kibinafsi uamue kuchukua msimamo wako kwa ajili yake hata kama dunia nzima iukatae na kukukasirikia. Hebu kwa hivyo sisi tusiendelee kuelea kwa mwele-keo kama changarawe pamoja na mawimbi ya bahari. Lazima tuwe wanaume na wanawake wa nguvu na uthab-iti iwapo tutamfuata Mungu na Ukweli Wake. {2TG24: 26.5}

Tumeona sasa wazi kwamba wale waliochukua msimamo kama huu ambao Ukweli hapa unawasilisha, walikuwa mashujaa wa Mungu wa zamani, na kama hao lazima wawe mashujaa Wake wa leo, hata ingawa wateswe, wachekelewe, na kutupwa nje kama wale waliowatangulia. {2TG24: 27.1}

Ushindi juu ya kila ukosefu unaweza kupatikana kwa maono ya Mungu, Ufasiri wa Mungu, imani ya Mungu. Haya matatu, unaona, hayawezi kutenganishwa, na haya matatu tu huongoza kwa Kristo na uzima wa milele. Hili hakika ni haki ya Kristo, ambayo haijachafuliwa na zari ya wanadamu. {2TG24: 27.2}

Bila shaka, utaweza kukumbana na upinzani, lakini alifanya hivyo Bwana Mwenyewe. Je! Wewe ni mkuu kul-iko Yeye? Lipo, hata hivyo, jambo moja ambalo maadui wa Ukweli hawawezi kulifanya, nalo ni, hawawezi kushinda hoja dhidi ya Ukweli, sembuse kutoa chochote kizuri kama hicho. Kusudi lao pekee ni kuitwaa lulu yako ya thamani kubwa. Na lengo lako linapaswa kuwa kuihifadhi ingawa utalazimika kupoteza kila kitu kingine iwapo unakusudia kuwaepuka watu ambao ni vigumu kupata nafasi na kushinda katika mbio na wenye haki. Maono ya Mungu, mfasiri aliyejazwa Roho, na imani isiyotindika, ndio tunayohitaji sote kuwa nayo, tusije sote kuangamia. {2TG24: 27.3}

27

Jumuiya ya Wadaudi Waadventista wa Sabato

(Ushirika Huru Unaojumuisha Kanisa)

Mlima Karmeli, Waco, Texas

S.L.P. 23738, Waco, TX 76702

+ 1-254-855-9539

www.gadsda.com

info@gadsda.com

Gombo la 2, Namba 23, 24

Kimechapishwa nchini Marekani

28

>