fbpx

Gombo la 2 Salamu Mwafaka Namba 21, 22

Gombo la 2 Salamu Mwafaka Namba 21, 22

                                    

AMANI YA PEKEE YA MAWAZO

Hati miliki, Kimechapishwa tena 1953

Haki zote zimehifadhiwa

V. T. HOUTEFF

                                    

 

WATOTO WALIOZALIWA KWA MAMA MZINZI WALETA AMANI NA FURAHA NYUMBANI

FUMBO KUU LA VIZAZI

                                    

1

ANDIKO LA SALA

Epuka Kunaswa Na Shetani Katika Mchezo Wake Kwa Nafsi

Nitasoma kutoka katika “Mafunzo ya Kristo katika Mifano,” ukurasa wa 55, kuanzia aya ya pili: {2TG21: 2.1}

“Masumbuko, utajiri, anasa, yote hutumiwa na Shetani katika kucheza mchezo wa maisha kwa nafsi ya mwa-nadamu. Onyo limetolewa, ‘Msiipende dunia, wala mambo yaliyomo duniani. Mtu akiipenda dunia, kumpenda Baba hakumo ndani yake…” Yeye asomaye mioyo ya wanadamu kama kitabu kilicho wazi anasema, “Basi jiangalieni, mioyo yenu isije ikalemewa na ulafi na ulevi na masumbufu ya maisha haya.’’ Na mtume Paulo kwa Roho Mtakatifu anaandika, “Wale watakao kuwa na mali huanguka katika majaribu na mtego, na tamaa nyingi zisizo na maana, zenye kudhuru, ziwatosazo wanadamu katika upotevu na uharibifu. Maana shina moja la maba-ya ya kila namna ni kupenda fedha; ambayo wengine hali wakiitamani hiyo wamefarakana na imani, na kujichoma kwa maumivu mengi.’”{2TG21: 2.2}

Tunataka kuomba kwa ajili ya kushinda kuipenda dunia na kukumbuka kwamba Shetani anacheza mchezo wa maisha kwa nafsi za watu wa Mungu; ili tupewe neema ya kutenda kazi na kuomba zaidi ya hapo awali; ili tushinde hila za Ibilisi; ili tujue kwamba yeye sio adui wa kuchezewa, na ya kwamba Yesu ndiye Nahodha Am-baye hajawahi kushindwa vita; kwamba iwapo tutaomba msaada Wake Yeye atatuwezesha kushinda. {2TG21: 2.3}

2

WATOTO WALIOZALIWA KWA MAMA MZINZI WALETA AMANI NA FURAHA NYUMBANI

ANDIKO LA HOTUBA NA V. T. HOUTEFF

MCHUNGAJI WA WADAUDI WAADVENTISTA WA SABATO

SABATO, JANUARI 3, 1948

HEKALU LA MLIMA KARMELI

WACO, TEXAS

Mada yetu ya leo inapatikana katika Hosea, sura ya kwanza na ya pili. Jambo la kwanza na muhimu zaidi ku-bainisha kuhusu sura hizi ni wakati ambamo maana yake ya unabii hufunuliwa. Ili kujua hili, tutasoma: {2TG21: 3.1}

Hos. 2:18 — “Nami siku hiyo nitafanya agano na wanyama wa mashamba kwa ajili yao, tena na ndege wa an-gani, tena na wadudu wa nchi; nami nitavivunja upinde na upanga na silaha vitoke katika nchi, nami nita-walalisha salama salimini.”

Hadi leo hii watu wa Mungu hawajawahi kupata usalama na uhuru kamili kama vile ulivyowekwa katika aya hii ya Maandiko. Inaonekana, kwa hivyo, upesi kwamba mada ya sura hiyo inafikia hata zaidi ya wakati wetu. Tunapozichambua sura hizi aya kwa aya, sehemu ya saa itaonekana bado iking’aa zaidi. {2TG21: 3.2}

Hos. 1:1,2 — “Hili ndilo neno la Bwana lililomjia Hosea, mwana wa Beeri, siku za Uzia, na Yothamu, na Ahazi, na Hezekia, wafalme wa Yuda; na siku za Yeroboamu, mwana wa Yoashi, mfalme wa Israeli. Hapo kwanza Bwana aliponena kwa kinywa cha Hosea,

3

Bwana akamwambia Hosea, Enenda ukatwae mke wa uzinzi na watoto wa uzinzi; kwa maana nchi imefanya uzinzi mwingi, kwa kumwacha Bwana.”

Nabii Hosea aliagizwa kumtwaa mke wa ukahaba bila sababu nyingine isipokuwa kuonyesha hali ya kusikit-isha na ya machukizo ambayo wakati huo ilikuwapo katika Israeli. {2TG21: 4.1}

Ndoa hii ni, bila shaka, ya maono tu kama ilivyo kwa nabii Ezekiel siku 40 kulalia upande mmoja, na siku 390 upande wa pili (Ezek. 4:4-6). {2TG21: 4.2}

Aya ya 3-5 — “Basi akaenda akamwoa Gomeri, binti Diblaimu; naye akachukua mimba, akamzalia mtoto mwanamume. Bwana akamwambia, Mwite jina lake Yezreeli; kwa maana bado kitambo kidogo, nitaipatiliza nyumba ya Yehu damu ya Yezreeli, na kuukomesha ufalme wa nyumba ya Israeli. Tena itakuwa siku ile, nitauvunja upinde wa Israeli katika bonde la Yezreeli.”

Mzaliwa wa kwanza mwana wa nabii katika ndoa yake ya maono, unaona, aliitwa Yezreeli ili kutabiri kile ambacho kingelipata taifa — si kutabiri tu kukomeshwa kwa ufalme, bali pia mahali haswa ambapo jeshi lake lin-gepata kushindwa — katika bonde la Yezreeli. Na uovu huu wa kuangamiza ulikuwa uje kwao kwa kuimwaga damu ya Yezreeli, lakini bila shaka si Yezreeli ambaye alikuwa amezaliwa wakati huo na kuitwa hivyo. Je! Yezreeli aliyechinjwa ni nani, tutamuona baadaye katika uchambuzi. {2TG21: 4.3}

Aya ya 6,7 — “Akachukua mimba tena, akazaa mtoto mwanamke. Bwana akamwambia, Mwite jina lake Lo-ruhama kwa maana sitairehemu nyumba ya Israeli tena,nisije nikawasamehe kabisa.

4

Lakini nitairehemu nyumba ya Yuda; nitawaokoa kwa Bwana, Mungu wao; wala sitawaokoa kwa upinde, wa-la kwa upanga, wala kwa silaha, wala kwa farasi, wala kwa wapanda farasi.”

Ufalme wa makabila kumi, Israeli, ulinusurika hadi kuzaliwa kwa Lo-ruhama, lakini jina la mtoto huyu wa pili lilithibitisha kwamba Mungu asingalikuwa na huruma zaidi kwa nyumba ya Israeli, kwamba mwisho wake ulikuwa umefika. Hata hivyo, Yeye alipaswa kuwarehemu nyumba ya Yuda, ufalme wa makabila mawili, na alipaswa kuuokoa kwa muujiza. Na hivyo ndivyo ilivyofanyika: malaika aliwachinja 185,000 wa jeshi la Ashuru, na kwa hivyo Mungu akaiokoa nyumba ya Yuda (2 Wafalme 19:35). {2TG21: 5.1}

Aya ya 8,9 — “Basi, akiisha kumwachisha Lo-ruhama, akachukua mimba, akazaa mtoto mwanamume. Bwana akasema, Mwite jina lake Lo-ammi kwa maana ninyi si watu wangu,wala mimi sitakuwa MUNGU wenu.”

Mtoto wa tatu aliitwa Lo-ammi kuonyesha kwamba rehema za Mungu zingaliondoka kwa nyumba ya Yuda. Lakini badala ya kuwaacha washindwe kama watu Wake, kwanza Aliwakataa, na kwa hivyo hawakuwa watu Wake tena. Mtume Petro anataja aya hii ya Maandiko akirejelea Wayahudi wasioamini; Kama taifa walikataliwa baada ya kusulubishwa kwa Kristo, na kwa hivyo hawakuwa watu Wake tena (1 Petro 2: 9,10). Watu binafsi, hata hivyo, ambao walimwamini Bwana walikubaliwa tena, na wakawa “wana wa Mungu aliye hai.” (Tazama Rum. 9:26.) {2TG21: 5.2}

Sasa kumbuka kwamba mfano huu hadi sasa imetupeleka kwa njia ya kinabii na kihistoria kutoka siku za nyumba ya Israeli hadi kwa enzi ya Ukristo. {2TG21: 5.3}

Aya ya 10 — “Tena itakuwa ya kwamba hesabu ya wana wa Israeli

5

itafanana na mchanga wa bahari, usioweza kupimwa wala kuhesabiwa; tena itakuwa, badala ya kuambiwa, Ninyi si watu wangu, wataambiwa, Ninyi ndio wana wa Mungu aliye hai.”

“Tena,” yaani, licha ya ukweli kwamba wana wa Israeli walipaswa kutapanywa katika mataifa yote, na kukataliwa, wasiwe watu wa Mungu tena, tena licha ya haya yote, wazawa wa nyumba ya Israeli na wa nyumba ya Yuda (wana wote wa Yakobo) walipaswa kuongezeka kama mchanga wa bahari wakati watakapokubaliwa tena na hivyo kuwa wana wa Mungu aliye hai kupitia Mwokozi, Yesu Kristo. {2TG21: 6.1}

Kutoka kwa andiko hili unaona kwamba umati huu wa wana wa Yakobo sio Wayahudi wanaojulikana wa leo, ila badala yake ni wazawa waliopotea wa Yuda na Israeli, wa wale waliofyonzwa na nchi za Mataifa na kanisa la Kikristo la kwanza kwa kujichukulia jina “Wakristo,” wa wale ambao walipoteza hivyo utambulisho wao wa kabila na taifa. Kutoka kwa hao wote, baada ya kutawanywa katika nchi zote za Mataifa, na baada ya kupoteza utambulisho wao, watakuja wana wa Mungu ambao wameonyeshwa katika unabii huu wa ki-mfano. Kwa hivyo, wengi wetu ambao hudhani kuwa wa nchi za Mataifa, mwishowe tunaweza kugundua kwamba sisi ni wa yale makabila yaliyopotea ya Yuda na Israeli, na wa Wayahudi wa Wakristo wa mitume. Ingawa hakuna yeyote kati yetu anayejua ukoo wetu tangu jadi sana, lakini Mungu ambaye anajua hata idadi ya nywele kwenye kichwa cha mtu amehifadhi kumbu kumbu sahihi ya ukoo wa kila mmoja wetu. Hivyo anasema Yeye: “Nitataja Rahabu na Babeli miongoni mwao wanaonijua: tazama Filisti, na Tiro, na Kushi; huyu alizaliwa humo. Na Zayuni itasemwa, Huyu na mtu huyo alizaliwa ndani yake; Naam,

6

mintarafu Zayuni itasemwa, huyu na huyu alizaliwa humo. Na Yeye Aliye juu ataufanya imara. Bwana atahesa-bu, awaandikapo mataifa, huyu alizaliwa humo. Selah.” Zab. 87: 4-6. {2TG21: 6.2}

Aya ya 11 — “Ndipo wana wa Yuda na wana wa Israeli watakusanyika pamoja, nao watajiwekea kichwa kimoja, nao watakwea watoke katika nchi hii; kwa maana siku ya Yezreeli itakuwa kuu sana.”

Hapa tunaambiwa wazi wazi kwamba katika siku za mwisho, watakatifu wa Mungu, bila mdhambi kati yao, watakusanywa pamoja kutoka pembe nne za dunia, na kupangwa katika serikali ya Kitheokrasi, ambayo Daudi wa uakisi atakuwa mfalme. Hivyo inakuwa kwamba “…katika siku za wafalme hao [sio baada ya siku zao] Mun-gu wa mbinguni atausimamisha ufalme, ambao hautaangamizwa milele; wala watu wengine hawataachiwa enzi yake, utavunja falme hizi zote vipande vipande na kuziharibu, nao utasimama milele na milele. Na kama vile ulivyoona ya kuwa jiwe lilikatwa mlimani bila kazi ya mikono, na na ya kuwa lilivunja-vunja kile chuma, na ile shaba, na ule udongo, na ile fedha na ile dhahabu; basi Mungu aliye mkuu amemjulisha mfalme mambo yataka-yokuwa baadaye: na ndoto hii ni ya hakika, na tafsiri yake ni dhabiti.” Dan. 2:44, 45. {2TG21: 7.1}

Katika unabii mwingine wa ki-mfano, katika uhusiano na huu, tunaambiwa tena: {2TG21: 7.2}

Hos. 3: 4, 5 — “Kwa maana wana wa Israeli watakaa siku nyingi bila mfalme, wala mtu mkuu, wala sadaka, wala nguzo, wala naivera, wala kinyago; baada ya hayo wana wa Israeli watarejea, na kumtafuta Bwana, Mungu wao, na Daudi, mfalme wao; nao watamwendea Bwana na wema wake kwa kicho siku za mwisho.”

7

Hapa tena ahadi ziko wazi jinsi maneno yanavyoweza kuonyesha kwamba baada ya kutawanywa na kutekwa, zile “siku nyingi,” watu waliotawanyika wa Mungu watarudi wakati huo katika nchi yao, na kisha watamtafuta Bwana Mungu wao, na Daudi mfalme wao. Hivyo, hawa wana wa Mungu si Wayahudi waliotambuliwa na wa-sioamini wa leo ambao wanajaribu kutengeneza makao ya kitaifa ya kudumu katika Nchi ya Ahadi. {2TG21: 7.3}

Wakristo kwa karne nyingi wamehubiri Ufalme wa Mungu, lakini haujaeleweka kwa wengi wao iwapo Utakuwa halisi kama dunia yenyewe, au Utakuwa kitu fulani cha povu, kitu fulani kinachoelea angani, au nini? Uvuvio, hata hivyo, unatangaza wazi kwamba Ufalme wa Kristo (kanisa lililosafishwa — lililotakaswa, Dan. 8:14) utakuwa halisi kama ufalme wowote wa dunia. {2TG21: 8.1}

Sasa tutaendelea na uchambuzi wetu katika Hosea sura ya pili, kwa sababu, jinsi nilivyosema hapo awali, yali-yomo ni endelezo la yale yaliyo ndani ya sura ya kwanza. {2TG21: 8.2}

Hos. 2: 1-3 — “Waambie ndugu zako wanaume, Ammi na ndugu zako wanawake, Ruhama. Msihini mama yenu, msihini; kwa maana yeye si mke wangu, wala mimi si mume wake; na ayawekee mbali mambo ya uasherati wake yasiwe mbele ya uso wake, na mambo ya uzinzi wake yasiwe kati ya maziwa yake; nisije ni-kamvua nguo zake akawa uchi, nikamweka katika hali aliyokuwa nayo siku ya kuzaliwa kwake, na kumfanya kama jangwa, na kumweka kama nchi kame, na kumfisha kwa kiu.”

Tukumbuke kwamba sura ya kwanza ilituleta katika mkondo wa wakati, hadi kwa enzi ya Ukristo. Sasa, kati-ka sura ya pili umakini wetu umeelekezwa tena kwa watoto wa maono wa Hosea, lakini kiambishi “Lo” kimeon-dolewa kutoka kwa majina Loruhamah na Loammi ili kubadili maana kutoka kwa sitairehemu, na sio watu Wangu, kuwa “nitairehemu,” na “Watu wangu.”

8

Hapa katika mfano huu wa kipekee, uliofanyizwa miaka ya zamani kabla ya kipindi cha Ukristo, Uvuvio ulionyesha neema ambayo ingalipewa watu katika enzi ya Ukristo, na kwamba badala ya kuendelea kuitwa Wayahudi, wangaliitwa kwa jina lingine — Wakristo: Rehema, na watu wangu. {2TG21: 9.1}

Amri, “Waambie ndugu zako, Ammi; na dada zako, Ruhama,” ndani yake yenyewe huelezea kwamba Mungu ananena kwa Yezreeli, (ndugu ya Ammi na Ruhama), na kwamba Yezreeli naye anene kwa Ammi na Ruhama. Na ukweli kwamba Mungu humwita mke wa Hosea wa maono mke Wake Mwenyewe, mada hii inazidi kuwa wazi: Hosea, unaona, humwakilisha Mungu, na mke wa Hosea huwakilisha kanisa la Mungu; Yezreeli, yule am-baye Mungu hunena naye, huwakilisha kipaza sauti Chake, nabii, na ndugu wa Yezreeli, Ammi na Ruhama, hu-wakilishawashiriki wa kanisa, wote wa kiume na wa kike. Sasa, kwa sababu Ammi na Ruhama huwakilisha walei, ni wazi kwamba mama huwakilisha ukasisi, wale ambao huzalisha waongofu ndani ya kanisa. Hapa tuna uwakilishi kamili wa nyumba ya Mungu. {2TG21: 9.2}

Ukweli kwamba Yezreeli atawahimiza ndugu zake, walei, wamsihi mama (ukasisi, ambao huzalisha waongo-fu), kwamba auweke mbali uasherati wake, ukweli unasimama wazi kwamba uamsho na matengenezo haya hayaji kwa washiriki kupitia kwa ukasisi, ila kwa ukasisi kupitia kwa washiriki. {2TG21: 9.3}

Washiriki watafafanua kwamba ikiwa wachungaji watashindwa kufanya matengenezo, Mungu atawavua nguo — kuwafanya uchi kama siku ile walipozaliwa. {2TG21: 9.4}

Mstari wa 4, 5 — “Naam, sitawaonea rehema watoto wake; kwa maana ni watoto wa uzinzi.

9

Maana mama yao amezini; yeye aliyewachukua mimba ametenda mambo ya aibu; maana alisema, Nitafuat-ana na wapenzi wangu, wanipao chakula changu na maji yangu, sufu yangu na kitani yangu, mafuta yangu na vileo vyangu.”

Aya hizi zinaweka mbele maana ya neema ya Mungu: kwamba iwapo “mama” atashindwa kufanya maten-genezo, ashindwe kuuacha uasherati wake na dunia na mazoea yake, basi sio mama tu bali pia watoto wake wanaoshirikiana naye wataanguka kutoka kwa neema milele. {2TG21: 10.1}

Mama yule, hapa tunaambiwa, anadhani kwamba wapenzi wake haramu ndio humsambazia mahitaji ya kawa-ida ya maisha, na ndio udhuru wake wa kufanya chochote nao. {2TG21: 10.2}

Kwa kuongezeaZaidi ya hayo, tunaambiwa tena kwamba wakati yeye anaendelea kucheza hivi ukahaba, an-awazaa watoto haramu, waongofu wasio wa kweli. Hapa lipo onyo ambalo bila maneno ya kusitasita linadai matengenezo au sivyo familia nzima ya kanisa, isipokuwa kwa wale ambao wanafanya matengenezo, itaangamizwa kabisa kama vile Yerusalemu wa zamani uliharibiwa miaka kadhaa baada ya kusulubishwa Kristo. {2TG21: 10.3}

Aya ya 6-13 — “Basi kwa ajili ya hayo, angalia, Nitaiziba njia yako kwa miiba, nami nitafanya kitalu juu yake, asipate kuyaona mapito yake. Naye atawafuata wapenzi wake, lakini hatawapata; atawatafuta, lakini hatawaona; ndipo atakaposema, Nitakwenda nikamrudie mume wangu wa kwanza; kwa maana hali yangu ya zamani ilikuwa njema kuliko hali yangu ya sasa. Maana hakujua ya kuwa mimi ndiye aliyempa ngano, na di-vai, na mafuta, na kumwongezea fedha na dhahabu, walivyovitumia kwa ajili ya Baali. Basi kwa ajili ya hayo, Nitaitwaa tena ngano Yangu kwa wakati wake, na divai Yangu kwa wakati wake, nami

10

nitamnyang’anya sufu Yangu na kitani Yangu, vya kumfunika uchi wake. Na sasa Nitaifunua aibu yake mbele ya macho ya wapenzi wake, wala hapana mtu atakayemwokoa katika mkono Wangu. Tena Nitaikomesha fu-raha yake yote, na sikukuu zake, na siku zake za mwandamo wa mwezi, na sabato zake, na makusanyiko yake yote yaliyoamriwa. Nami nitaiharibu mizabibu yake na mitini yake, ambayo alisema, Hii ndiyo ujira wangu niliopewa na wapenzi wangu; Nami nitaifanya kuwa msitu, na wanyama wa mashamba wataila. Nami nitam-wadhibu kwa sababu ya siku za Mabaali, aliowafukizia uvumba; hapo alipojipamba kwa pete masikioni mwake, na kwa vito asema Bwana.”

Aya hizi huelezea njia na nguvu ya Mungu ya kuokoa: Kabla hajaitisha matengenezo Yeye huandaa njia: Ana-leta kanisa Lake kwa kujaribu na hali ngumu ambazo haziwezi kujitenga mwenyewe. Yeye hulileta kanisa Lake kwa hali za kujihoji na kutatanisha ambazo ni vigumu kujinasua kujinasua. Yeye hulileta katika hali sawa am-bayo Yeye alimleta mwana mpotevu. Yeye hufanya hivi ili kwamba aweze kulileta litambue pale ambapo hakika msaada wake kwa kweli hutoka, kujua kwa hakika kwamba hautoki kwa wapenzi wake. Basi, wakati huo tu, litaweza kufanya jambo jambo lile ambalo mwana mpotevu alifanya wakati alipojifahamu mwenyewe. {2TG21: 11.1}

Kwa kuutimiza unabii ulio katika aya ya kumi na moja, Mungu aliiruhusu hiyo pembe ndogo ya Danieli ibad-ilishe nyakati na sheria, na akawaruhusu watakatifu wake Aliye Juu kuwa mikononi mwake kwa “wakati na nyakati mbili na nusu wakati.” Dan. 7:25. {2TG21: 11.2}

Aya ya 14,15 — “Kwa hiyo angalia, mimi nitamshawishi, na kumleta nyikani, na kusema naye maneno ya kumtuliza moyo. Nami nitampa mashamba yake ya mizabibu toka huko, na bonde la Akori kuwa mlango wa

11

tumaini; naye ataniitikia huko, kama siku zile za ujana wake, na kama siku ile alipopanda kutoka nchi ya Misri.”

Baada ya kumleta katika hali ngumu na za kuaibisha kama zile mtu anaweza kuwa ndani yake, Mungu anaahidi kumshawishi, na kumpeleka nyikani, na kuzungumza naye maneno ya kumtuliza. Akizungumza hasa, baada ya kutoka katika “dhiki kubwa, ambayo haijatokea namna yake tangu mwanzo wa ulimwengu” (Mat. 24:21), Mungu anamleta, sio ndani ya shamba lake la mizabibu, sio katika Nchi ya Ahadi, bali “nyikani” (katika nchi za Mataifa), kusema naye maneno ya kumtuliza, na kumsaidia afanye matengenezo. Baada ya mkutano huu wa kumfariji kutukia atayapokea mashamba yake ya mizabibu kutoka huko, na Bonde la Akori kuwa mlango wa tumaini; huko ataimba na kufurahi kama katika siku za ujana wake, na kama siku ile alipopanda kutoka Misri. {2TG21: 12.1}

Bonde la Akori, unakumbuka, ni mlango wake wa tumaini — ndio njia pekee ya kutoka katika shida yake. Bonde lina umuhimu mmoja tu: huwakilisha kusafisha kabisa, kuwaangamiza wadhambi ambao wako kati yake kabla kuimiliki nchi — tumaini lake la pekee la kuwa mke wa adabu wa Mungu. {2TG21: 12.2}

Ilikuwa katika Bonde la Akori ambapo Yoshua aliwapiga mawe wadhambi wa mwisho katika Israeli — Akani na nyumba yake. Kisha ikawa kwamba taifa la Israeli liliruhusiwa kuitwaa nchi ya ahadi, shamba la mizabibu. Kusafisha kwa namna hii tu ndio “mlango wa tumaini” wa kanisa pekee, unasema Uvuvio, kuokoka kwake kwa pekee kutoka kwa shida yake ya sasa. Wakati huo atarudi katika nafasi yake ya zamani na neema. Kisha atapata baraka iliyoahidiwa kama vile Israeli wa zamani alipokea yake. Tukio hilo la ajabu katika Bonde la Akori sasa linaonekana kuwa ishara ya utakaso kwa ajili ya kuimiliki tena nchi ya ahadi — likiashiria Hukumu kwa Walio Hai,

12

kuwakusanya watakatifu, na uangamizwaji wa wadhambi — mtengo wa ngano kutoka kwa magugu, mbuzi kutoka kwa kondoo, samaki wazuri kutoka kwa samaki wabaya. “Ghala” (Mat. 13:30), humaanisha Ufalme ulioonyeshwa hapa kama ilivyo kuume kwa Bwana, na vile vile vyombo. {2TG21: 12.3}

Aya ya 16 — “Tena siku hiyo itakuwa, asema Bwana, utaniita Ishi, wala hutaniita tena Baali.”

Naam, badala ya kuwa bwana wake, kwa kweli Mungu atakuwa mume wake, kwa maana mmoja anaweza kuwa na mabwana wengi, ila mume mmoja tu. {2TG21: 13.1}

Aya ya 17 — “Kwa maana nitayaondoa majina ya Mabaali kinywani mwake, wala hawatakumbukwa tena kwa majina yao.”

Majina ya Mabaali ni muhimu kwa watu wanaomiliki tabia za ubinafsi kama wa Baalamu — waalimu wa dini, manabii ambao wangaliweza kulaani Israeli kuliko kupoteza fursa ya pato la pesa, au ya upumbavu mwingine fulani, ya kuendeleza ubinafsi unaokwezwa na kusifiwa. Wa aina hii wakati huo hawatajulikana tena kwa ya ubwana, majina yao yaliyotukuka sana. {2TG21: 13.2}

Wakati Kanisa litakuwa limetakaswa hivyo sanamu zake zote, ndipo litapata amani ya milele. {2TG21: 13.3}

Aya ya 18-22 — “Nami siku hiyo nitafanya agano na wanyama wa mashamba kwa ajili yao, tena na ndege wa angani, tena na wadudu wa nchi; nami nitauvunja upinde na upanga na silaha vitoke katika nchi, nami nita-walalisha salama salimini. Nami nitakuposa uwe wangu kwa milele; naam, nitakuposa kwa haki, na kwa hukumu, na kwa ufadhili, na kwa rehema. Nami nitakuposa kwa uaminifu;

13

nawe utamjua Bwana. Tena itakuwa siku hiyo, mimi nitaitika, asema Bwana; nitaziitikia mbingu, nazo zitaiitikia nchi; nayo nchi itaiitikia nafaka na divai na mafuta; nayo yataiitikia Yezreeli.”

Aya hizi zinaonyesha wazi kwamba uwepo wa Mungu siku hiyo utakuwa katika kanisa Lake, kwamba hata mbingu zote zitakuwa zikiisikia sauti ya Mungu wakati Yeye anaongea na watu Wake hapa duniani. Dunia pia itaisikia “nafaka, na divai, na mafuta”; Yaani, dunia itausikia Ukweli — Ukweli ambao huridhisha nafsi kama vile chakula kilicho bora kinachoboresha. Zaidi ya hayo, sio tu nafaka, divai, na mafuta — Ukweli wote — lakini Yezreeli, pia, dunia itamsikia. Kwa kweli, ahadi hizi zote zitatimizwa katika wakati wa rehema, kwa sababu haziwezi kuitendea dunia wema baada ya muda wa rehema kumalizika. {2TG21: 14.1}

Yezreeli ambaye damu ya Israeli wa kale ulishtumiwa kuwa na hatia, unaona, alikuwa mfano wa manabii am-bao Israeli uliwakataa na kuwaua. Hivyo ni kwamba nyumba ya Israeli iliyowachukia manabii ilishindwa katika Bonde la Yezreeli, ambalo kwa ufasiri wake ni bonde la manabii waliouawa. {2TG21: 14.2}

Aya ya 23 — “Nami nitampanda katika nchi kwa ajili Yangu mwenyewe; nami nitamrehemu yeye asiyepewa rehema; nami nitawaambia wale wasiokuwa watu wangu, Ninyi ndinyi watu wangu; nao watasema, Wewe ndiwe Mungu wangu.”

‘Kumpanda katika nchi kwa ajili Yangu,” humaanisha kumzidishia watoto wake kwa mpangilio wa Mungu baada ya kupata baraka hizi zote zilizoahidiwa. Wakati huo atakuwa kwa kweli na rehema ya Mungu, rehema kubwa kama hii hajawahi kupata. Hivyo kwa wale ambao iliambiwa “Ninyi si watu Wangu,” basi katika,

14

uhalisi mtukufu, itasemwa, “Ninyi ni wana wa Mungu aliye hai.” {2TG21: 14.3}

Sasa kwamba ukweli wote wa sura hizi unafunuliwa kwa mara ya kwanza tangu nabii alipouandika, na kwa sababu hakuna unabii wowote wa Maandiko upatao kufasiriwa kama apendavyo mtu fulani tu, sio kwa mapenzi ya mwanadamu, ila kwa mapenzi ya Roho (2 Pet. 1:20, 21), ukweli ni kwamba Mungu alikuwa nasi moyoni (sisi ambao sura hizi zinafanuliwa kwetu) Aliposababisha mambo haya kuandikwa. Zaidi ya hayo, kwa sababu aya za kwanza za sura ya pili zinatuleta hadi kwa wakati wa uamsho na matengenezo yanayotukia katika wakati wetu, yakidhaminiwa na Mungu Mwenyewe na kuletwa nuruni kupitia Yezreeli, kisha kupelekwa kanisani na walei, ni kazi ambayo inajitimiza tu katika vuguvugu hili la mlei ambalo sasa linafagilia kote kote katika ulimwengu wa Waadventista wa Sabato. Ukweli huu, kwa hivyo, unasimama juu sana kama mlima kwamba Mungu sasa yu kazini, kwamba mambo yanapaswa kusonga kulingana na kusudi Lake Takatifu. Hivyo inakuwa kwamba “wa-tamsikia Yezreeli,” na kwamba Mungu Mwenyewe atawaambia, “Ninyi ni watu Wangu,” na wao, pia, watasema, “Wewe ndiye Mungu wetu.” {2TG21: 15.1}

Uvuvio unaonyesha hivi kwamba juhudi zetu pamoja na ujumbe huu ni hakika kabisa zitaleta matengenezo makubwa ya nyakati zote; kwamba kemeo la watoto kwa mama hakika litaleta amani na furaha katika nyumba ya Mungu. Sisi, kwa hivyo, tuna kila sababu ya kuwa na uhakika wa kushinda na kuwa na hamu ya kufanya ka-zi, kama alivyokuwa Daudi wa zamani wakati alipolikabili jitu Goliathi. Wazi ni kwamba watoto (walei) wali-ozaliwa na mwanamke mzinzi (kanisa) waleta amani na furaha katika familia ya Mungu. Lazima, kwa hivyo, usishindwe kwa moyo wote na kwa kweli ujiunge na vuguvugu hili hodari kwa ajili ya uamsho na matengenezo kote kote Laodekia na kukamilisha kazi ya injili na kanisa, “’…Zuri kama mwezi, safi kama jua na la kutisha ka-ma jeshi lililo na mabango, ‘litasonga mbele ulimwenguni kote, likishinda na kushinda.” — “Manabii na Wafal-me,” uk. 725. Hauwezi kumudu kupoteza. {2TG21: 15.2}

15

ANDIKO LA SALA

Upasue Udongo Mgumu

Nitasoma kutoka ukurasa wa 56 wa “Mafunzo ya Kristo kwa Mifano”: {2TG22: 16.1}

“Katika mfano wote wa mpanzi, Kristo huwakilisha matokeo tofauti ya upanzi kulingana na udongo. Katika kila kisa mpanzi na mbegu ni sawa. Kwa hivyo hufundisha kwamba iwapo neno la Mungu hushindwa kutimiza kazi yake mioyoni na maishani mwetu, sababu itapatikana ndani yetu wenyewe. Lakini lile tokeo haliko zaidi ya udhibiti wetu. Kweli, hatuwezi kujibadilisha sisi wenyewe; lakini uwezo wa uchaguzi ni wetu, na hubaki kwetu kuamua vile tutakavyokuwa. Kando ya njia, udongo penye miamba, wasikilizaji wa udongo penye miiba ha-wahitaji kubaki hivyo…. Udongo mara moja ukifunikwa na miiba unaweza kubadilishwa tu kwa kazi ya bidii. Kwa hivyo mielekeo miovu ya moyo wa asili inaweza kushindwa tu kwa juhudi za dhati katika jina na nguvu za Yesu. Bwana hutuhimiza kupitia kwa nabii Wake, ‘Upasue udongo wako mgumu, usipande kati ya miiba.’ ‘Ji-pandieni katika haki; vuneni kwa fadhili.’ Kazi hii Yeye anataka kuitimiza kwa ajili yetu, na Yeye hutuuliza ku-shirikiana Naye.” {2TG22: 16.2}

Sasa tutapiga magoti na kusali ili tuweze kuwa macho daima kwa Sauti ya Roho wa Mungu; tujue kwamba ingawa hatuwezi kujibadilisha sisi wenyewe, ila uwezo wa kuchagua ni wetu; kukumbuka daima kwamba Mun-gu ametuumba sisi mawakala huru wa maadili, kwamba sisi wenyewe tunawajibika kwa ugumu wa mioyo yetu; kumruhusu Yeye aupasue udongo wetu mgumu ili tuweze kujipandia katika haki; tujue kwamba kupitia sala na kujifunza tunaweza kuweka hai tumaini letu la mambo ya kiroho. {2TG22: 16.3}

16

FUMBO KUU LA VIZAZI

ANDIKO LA HOTUBA NA V. T. HOUTEFF

MCHUNGAJI WA WADAUDI WAADVENTISTA WA SABATO

SABATO, JANUARI 10, 1948

HEKALU LA MLIMA KARMELI

WACO, TEXAS

Zek. 6: 1-8 — “Nikainua macho yangu tena, nikaona, na tazama, yanatokea magari ya vita manne, yanatoka kati ya milima miwili, na milima hiyo ilikuwa ni milima ya shaba. Katika gari la kwanza walikuwa farasi we-kundu; na katika gari la pili walikuwa farasi weusi; na katika gari la tatu walikuwa farasi weupe; na katika gari la nne walikuwa farasi wa rangi ya kijivujivu. Nikajibu, nikamwuliza yule malaika aliyesema nami, Hawa ni nini, Bwana wangu? Malaika akajibu, akaniambia, Hawa ni pepo nne za mbinguni, zitokeazo baada ya kusimama mbele ya Bwana wa dunia yote. Gari lile lenye farasi weusi latoka kwenda hata nchi ya kaskazini; nao farasi weupe wakatoka wakafuata nyuma yao; na wale wa rangi ya kijivujivu wakatoka kwenda hata nchi ya kusini. Na wale farasi wa rangi ya damu ya mzee, wakataka kwenda huko na huko katika dunia; naye akawaambia, Haya! Tokeni, mwende huko na huko katika dunia. Basi wakaenda huko na huko katika dunia. Ndipo akaniita, akaniambia akisema, Tazama, wale waendao mpaka nchi ya kaskazini wameituliza roho yangu katika nchi ya kaskazini.”

17

18

Fumbo katika mfano huu wa kinabii liko kwa gari la nne, unaona: Limeunganishwa kwa makundi mawili, la kijivujivu na la farasi wa rangi ya damu ya mzee, kundi moja likijaribu kulipeleka kwa mwelekeo mmoja (kusini), na lingine katika mwelekeo mwingine (kwenda na huku na huko katika dunia)! Je! itakuwaje kwa gari, na ni kundi gani litakaloweza kulichukua? Hilo ndilo fumbo, kwa maana yote hayawezi kulichukua isipokuwa yatem-bee pamoja. Kwa sababu huu ni mfano wenye fumbo la utata, umekuwa fumbo siku zote tangu wakati nabii ali-uandika, na kwa kuwa umefunuliwa sasa kwa mara ya kwanza, Uvuvio ni dhahiri unamwonya mtu umbele ku-husu jambo zito sana ambalo linatukia kwa wakati huu. Linaweza kuwa nini? — {2TG22: 19.1}

Nabii Zekaria alikuwa na hamu ya kujua kama tulivyo, kwa maana aliuliza, “hawa ni nini, Bwana wangu”? Na kwa swali lake likaja jibu, “Hawa ni pepo nne za mbinguni, zitokeazo baada ya kusimama mbele ya Bwana wa dunia yote.” {2TG22: 19.2}

Jibu la malaika ni wazi. Magari, Alitangaza ni roho za mbinguni, ambazo zimesimama mbele ya Bwana, na ambao wametumwa kwenda huko na huko duniani. Dhahiri, basi, makundi haya manne na magari yanawakilisha jumbe nne (Roho nne) zilizotumwa kutoka kwa uwepo wa Mungu. Na kwa sababu jumbe zote kutoka kwa Mungu hupelekwa huku na huko kote duniani na Ukasisi na Kanisa, yale magari na makundi yao, kwa hivyo, yanaonekana kuwakilisha kanisa likiwa kazini katika vipindi vinne tofauti. {2TG22: 19.3}

Swali linalofuata ni, Je! Ni wapi katika mkondo wa wakati ambapo tunaweza kulitafuta kanisa hili lili-losheheni ujumbe na mzigo wa taabu? katika wakati wetu, zamani au nini? Milima ya shaba inatoa kidokezi, kwa maana magari yalitokea kati yake. Tuweze, kwa hivyo, kwanza kujua ni nini milima huwakilisha, na

19

ni wapi inasimama katika wakati. Na kwa sababu magari yalitokea kati ya ile milima, mmoja ukisimama kushoto kwayo (katika siku za baadaye) na ule mwingine upande wayo kulia (zamani), ni muhimu kujua mahali ilipo kwanza. Ufasiri wa Kibibilia wa mlima wa mfano ni kama ifuatavyo: “Yerusalemu utaitwa mji wa Kweli; na mlima wa BWANA wa majeshiutaitwa, mlima mtakatifu.” Zek. 8: 3. Ile milima katika unabii wa Zekaria, kwa hivyo, kama mahali pengine katika Bibilia, inaonekana kuashiria serikali mbili, makanisa, sawa katika maumbile (yote ya shaba) na kwa nyakati mbili tofauti (mmoja kulia kwa magari na mmoja kushoto kwayo). Ikiwa ya sha-ba, chuma kilicho na ubora wa kudumu, ambao hauharibiki, huonyesha kwamba huwakilisha kitu cha milele. Zaidi ya hayo milima ikiwa ya nyenzo sawa za mfano kama zile za miguu ya Kristo (Ufu. 1:15) iliyoonyeshwa kuwa ya (shaba), huonyesha milima katika enzi ya Ukristo. {2TG22: 19.4}

Serikali za pekee kama hizo takatifu za Mungu katika enzi ya Ukristo, moja zamani na moja katika siku za baadaye ambayo kati yake njia ya magari ipo, ni kanisa la Pentekoste na wanafunzi 120 waliojazwa Roho, lililo-fananishwa na mlima kulia kwa yale magari, na kanisa kwenye Pentekoste ya pili (Yoeli 2:28,29, bado la baadaye) na wanafunzi 144,000 waliojazwa Roho wamesimama juu ya Mlima Zayuni na Mwana-Kondoo (Ufu. 14:1), wakiwakilishwa na mlima kushoto kwa yale magari. {2TG22: 20.1}

Inaeleweka vyema kwaamba kanisa la leo limetengenezwa kwa kila aina ya nyenzo, sio vya shaba madhubuti — sio la Wakristo wa kweli pekee, bali limechamana na wazuri na wabaya — ngano na magugu. Ukweli ni dha-hiri: Itakuwepo Theokrasia nyingine ya kuangamiza dhambi na kuwapepeta wadhambi kama ile katika siku ya Anania na Safira ambao kwa dhambi walikata

20

roho walipoanguka miguuni pa mtume (Mdo. 5: 1-11). {2TG22: 20.2}

Kwa uwazi, magari huwakilisha kanisa la wanamgambo likiwa kazini kati ya hizo Pentekoste mbili. {2TG22: 21.1}

Gari la nne likiwa la mwisho, litapatikana likitenda kazi kabla tu ya Pentekoste ya pili. {2TG22: 21.2}

Kwa sababu yale magari yanaongozwa na farasi, farasi wenyewe lazima wawakilishe uongozi wa lile gari (wa kanisa), na abiria ndani ya yale magari lazima wawakilishe walei. {2TG22: 21.3}

Ule mfano, hata hivyo, utafichua fumbo la hali ya utata ambalo liko na gari la nne, la mwisho, na hivyo kanisa la Laodekia na ujumbe wa Hukumu, jinsi jina lake linavyoashiria. {2TG22: 21.4}

Gari la kwanza, unakumbuka, linaongozwa na farasi wekundu; la pili na farasi weusi; la tatu na weupe; na la nne na aina mbili — wa kijivujivu na farasi wa rangi ya damu ya mzee. Rangi ya kila farasi ikiwa ni alama ya aina, lazima iwe ishara ya hali zao za asili na za matokeo yao. Na kama ilivyobainishwa hapo awali, ni mifano ya ukasisi katika kila sehemu ya historia ya kanisa. Nyekundu kwa uwazi huashiria kufia-imani; nyeusi huashiria utumwa; nyeupe huashiria uhuru; ya kijivujivu (rangi isiyotambulika, si nyeusi wala nyeupe) huwaakilisha wa-chungaji ambao si Wakristo wa kweli au Wapagani wa kweli — wanafiki. Rangi ya damu ya mzee, hata hivyo, huashiria nguvu, jinsi maelezo ya pambizoni huonyesha. {2TG22: 21.5}

Unabii huu wa mfano unaonekana kupatana na historia. Unabainisha kwamba Kanisa la Kikristo mwanzoni liliathirika na wafia-imani, walionyeshwa kwa rangi, nyekundu. Kisha vikafuata Vizazi vya Giza la dini wakati ambapo

21

kanisa lilikuwa utekwani (nyeusi). Kufuatia kikaja kipindi cha Kiprotestanti, kipindi cha uhuru wa kidini (kundi jeupe). Na mwishowe linakuja gari la nne pamoja na makundi yake farasi wa rangi ya damu ya mzee na ki-jivujivu. Timu hizo zinaonekana kuwa na mzozo wa utata juu ya gari. Kijivujivu ikiwa rangi isiyotambulika — si nyeusi wala nyeupe, humaanisha unafiki, aina ambayo haijulikani tangu hapo awali, ilhali rangi, ya damu ya mzee, humaanisha nguvu ya kiroho (pambizo) aina ambayo haijulikani tangu hapo awali. {2TG22: 21.6}

Kwa sababu Kanisa lilianzia Akaya, Yerusalemu haswa, gari la kwanza linaonekana lilibaki hapo, maana halikwenda popote. “Nchi ya kaskazini,” kijiografia kaskazini mwa Palestina ni mahali ambapo magari mengine yalikwenda; yaani, nchi ambazo mataifa ya Kikristo sasa yanamiliki. Gari la nne, hata hivyo, linastahili kwenda huku na huko katika dunia yote — kwa kila taifa, na jamaa, na lugha na watu. Lakini kinyume na hili, farasi wa kijivujivu “wakatoka kwenda hata nchi ya kusini” ambayo, kwa usemi wa mfano, ingekuwa Misri ya kiroho — udunia. {2TG22: 22.1}

Roho wa Mungu akishatulizwa katika nchi ya kaskazini, lazima imaanishe kwamba jumbe za Mungu katika nchi ya kaskazini zilikataliwa kwa ujumla, haswa ule wa gari la nne, ambao ulisababisha Roho wa Ukweli kuondoka na kutouleta Ukweli tena kupitia wao — kuwa kimya huko — na kwamba, kwa hivyo, haupaswi kuta-rajiwa Ukweli wowote kupitia wao. {2TG22: 22.2}

Timu maradufu za farasi, na aina zao mbili za rangi, zikivuta pande mbili tofauti zinaonekana mara moja kuashiria jozi mbili za viongozi wa kanisa (viongozi wa Waadventista wa Sabato na viongozi wa Wadaudi Waadventista wa Sabato) tofauti katika tabia na lengo. Kunena ki-mfano, farasi wa kijivujivu, wale ambao walitokea kwanza kwa

22

tukio la kinabii, linaongoza gari kwenda Misri — udunia ambao wanapaswa kutoka ndani badala ya kurudi ndani yake. Farasi wa rangi ya damu ya mzee, hata hivyo, wanajitahidi kujiondoa kwalo na kwenda huku na huko du-niani kama ilivyoamriwa — kukamilisha kazi ya injili kulingana na mpango wa Mungu. Lakini hili haliwezi kutu-kia iwapo timu zote mbili zimefungwa kwa gari, kwa maana gari haliwezi kwenda upande wowote wakati timu moja inavuta kwa mwelekeo mmoja na nyingine kwa mwelekeo mwingine. {2TG22: 22.3}

Hitaji la haraka, kwa hivyo, ni kufungua (kuiuzulu) moja, ili nyingine iweze kuwa huru kwenda huku na huko duniani mara tu watakapoambiwa “Haya! Tokeni.” Wakati hili litakapotukia fumbo halitakuwa fumbo tena. {2TG22: 23.1}

Ni nini kilichoweka aina mbili tofauti za viongozi kufanya kazi kwa makusudi yanayokinzana? — Nitaruhusu Roho ya Unabii itoe jibu. Hapa yanafuata maelezo ya jozi moja ya viongozi wa kanisa: {2TG22: 23.2}

“Wale ambao wametoa heshima kubwa kwa ‘sayansi inavyoitwa kwa uongo,’ hawatakuwa viongozi baadaye. Wale ambao wameamini kwa akili, ustadi, au talanta, hawatasimama baadaye kuwa viongozi wa askari. Ha-wakufululiza mwendo na nuru. Wale ambao wamejithibitsha kuwa sio waaminifu baadaye hawatakabidhiwa kundi…” — “Shuhuda,” Gombo la 5, uk. 80. {2TG22: 23.3}

Bila shaka, viongozi hawa wa kujiona kuwa bora, wanaopenda kulala katika nchi ya uvuguvugu, wana-wakilishwa na farasi wa kijivujivu. {2TG22: 23.4}

Sasa tutasoma kuwahusu viongozi ambao farasi

23

wa rangi ya damu ya mzee huonyesha, wale wa mwisho kuja kwenye eneo: {2TG22: 23.5}

“… Bwana anao watumwa waaminifu, ambao katika wakati wa mtikiso, wa kupimwa watafunuliwa waon-ekane. Wapo sasa wa thamani sana waliofichwa ambao hawajamsujudia Baali. Hawajakuwa na nuru ambayo imekuwa ikiangaza kwa mng’ao thabiti juu yenu. Lakini, inaweza kuwa chini ya hali ngumu isiyopendeza ya nje ambapo waangavu wa tabia halisi ya Kikristo itafunuliwa. Wakati wa mchana huwa tunaangalia mbinguni, lakini hatuzioni nyota. Ziko pale, imara angani, lakini jicho haliwezi kuziona. Usiku tunaona mng’ao wazo halisi.” — “Shuhuda,” Gombo la 5, uk. 80-81. {2TG22: 24.1}

Hivi ndivyo inavyotukia sasa: Wale ambao wanaukataa ujumbe ambao unatangaza Hukumu kwa Walio Hai; wale ambao “hawakufululiza mwendo na nuru,” na wameridhika kukaa katika Misri ya uakisi; ukasisi wa Waadventista wa Sabato ‘watachishwa kazi (watafunguliwa); na wale “waliofichwa”, ambao wanawakilishwa na farasi wa rangi ya damu ya mzee, ukasisi wa Wadaudi Waadventista wa Sabato, wanakuja mbele. Sasa ‘wanafunuliwa waonekane,’ na wako tayari kulichukua lile gari! Kisha mara tu watakapoambiwa “Haya! To-keni,” watasonga bila kusitasita na kwa upesi kwenda “huku na huko duniani” na ujumbe wa saa hii, Hukumu kwa Walio Hai. {2TG22: 24.2}

Sasa ruhusu mwasisi wa Dhehebu la Waadventista wa Sabato afafanue kwa uthabiti ni nini na iko wapi nchi ya kusini: {2TG22: 24.3}

“Nimejawa na huzuni ninapofikiri hali yetu kama watu …. Kanisa limekengeuka na kuacha kumfuata Kristo Kiongozi wake, na pole pole linarudi

24

kuelekea Misri. Lakini wachache wameshtuka au kushangaa kwa upungufu wao wa nguvu za kiroho. Shaka na hata kutoziamini Shuhuda za Roho wa Mungu, kunatia chachu makanisa yetu kila mahali. Shetani anatazamia iwe hivyo. Wachungaji wanaohubiri ubinafsi badala ya Kristo wanatazamia iwe hivyo. Shuhuda hazisomwi na haziwekwi maanani. Mungu amenena kwenu. Nuru imekuwa ikiangaza kutoka kwa neno lake na katika Shuhu-da, na zote mbili zimedunishwa na kupuuzwa. Matokeo ni dhahiri kwa ukosefu wa usafi na moyo wa ibada na imani thabiti miongoni mwetu.” — “Shuhuda,” Gombo la 5, uk. 217. (Maneno yaliyopigwa mistari ni yetu.) {2TG22: 24.4}

Je! Nini kitakachowafungua farasi wa kijivujivu kutoka kwa gari? — Isaya nabii anajibu: {2TG22: 25.1}

Isa. 66:16,19,20 — “Kwa maana Bwana atateta na wote wenye mwili, kwa moto na kwa upanga wake; nao watakaouawa na Bwana watakuwa wengi…. Nami nitaweka ishara kati yao, nami nitawatuma hao waliooko-ka kwa mataifa, Tarshishi, na Puli, na Ludi, wavutao upinde, kwa Tubali na Yavani, visiwa vilivyo mbali; wa-tu wasioisikia habari yangu, wala kuuona utukufu wangu; nao watahubiri utukufu wangu katika mataifa. Nao watawaleta ndugu zenu wote kutoka mataifa yote, kuwa sadaka kwa Bwana, juu ya farasi, na katika magari, na katika machela, na juu ya nyumbu, na juu ya wanyama wepesi, mpaka mlima wangu mtakatifu Yerusale-mu, asema Bwana; kama vile wana wa Israeli waletavyo sadaka yao nyumbani kwa Bwana katika chombo safi.”

Hapa umeonyeshwa mchinjo, ukitukia kati ya wale ambao wameagizwa kujitenga kula vyakula najisi, ila mi-ongoni mwo wengi wanakiuka amri ya Mungu. Wasio watiifu, wale ambao miungu yao ni tumbo, pamoja na wale wajitakasao

25

na kujisafisha, (wanaojihesabia haki) katika bustani nyuma ya mti mmoja (nyuma ya mchungaji wao anayechukia Ukweli, Isa. 66: 17, pambizo), wanaondolewa na Bwana Mwenyewe kutoka kwa Wake wanaoutafuta Ukweli. {2TG22: 25.2}

Baada ya wakosaji kuondolewa hivyo, kisha wale ambao wanaachwa, “masalia,” waliookoka, wanakuwa wa-tumishi wa Mungu na wanatumwa kwa mataifa yote, haswa kwa wale ambao bado hawajaisikia sifa ya Mungu au habari njema ya Ufalme Wake. Hawa waliookoka watawaleta katika nyumba ya Bwana ndugu zao wote, wote ambao wataongoka kwa Kristo — “umati mkubwa sana, ambao hapana mtu awezaye kuuhesabu, watu wa kila taifa, na kabila, na jamaa, na lugha.” Wao watasimama “mbele ya kile kiti cha enzi, na mbele ya Mwana-Kondoo, wamevikwa mavazi meupe, na matawi ya mitende mikononi mwao.” Ufu. 7:9. {2TG22: 26.1}

Hivi ndivyo Injili itakavyokamilishwa na wale ambao wataokoka mchinjo wa Bwana (Isa. 66:15,16) na watu wa Mungu watakusanywa upesi kutoka pembe nne za dunia, wakiletwa kwa furaha kama sadaka kwa nyumba ya Bwana (Isa. 66:19,20). {2TG22: 26.2}

Sasa ni nafasi ya kila mtu kuamua kuwa ama upande mmoja au mwingine, ama kufanya matengenezo na kuongozwa na farasi waaminifu wa rangi ya damu ya mzee, au kushikamana na wanaojiona bora farasi wa ki-jivujivu na kukaa nao katika nchi ya kusini, huko kuangamia. Hapa hakika ni uamuzi muhimu sana unaopaswa kufanywa na kila mshiriki wa Dhehebu. Unahitaji kuchukua hatua ambayo itaamua hatma ya walei na vile vile ya ukasisi. {2TG22: 26.3}

Sasa ni nafasi yako ya kuchukua hatua, na ni tarajio langu na ombi kwamba wewe, na kila mshiriki wa dhehe-bu,

26

Achague kuwa upande ambao fumbo hili la vizazi lililofunuliwa wazi linakuagiza kwa dhati kuwa. Usiwaruhusu farasi wa kijivujivu waendelee kukudanganya. Kutana na hotuba zao laini na “Bwana asema hivi.” Watoe ki-jasho kwa Ukweli huu halisi wa Bibilia. {2TG22: 27.1}

27

Jumuiya ya Wadaudi Waadventista wa Sabato

(Ushirika Huru Unaojumuisha Kanisa)

Mlima Karmeli, Waco, Texas

S.L.P. 23738, Waco, TX 76702

+ 1-254-855-9539

www.gadsda.com

info@gadsda.com

Gombo la 2, Namba 21, 22

Kimechapishwa nchini Marekani

28

>