fbpx

Gombo la 2 Salamu Mwafaka Namba 13, 14

Gombo la 2 Salamu Mwafaka Namba 13, 14

                                    

AMANI YA PEKEE YA MAWAZO

Hati miliki, Kimechapishwa tena 1953

Haki zote zimehifadhiwa

V. T. HOUTEFF

                                    

 

MIHURI NA BARAGUMU HUANZIA NA KWISHIA WAPI?

KUWEKA ORODHA YA MATUKIO YA UFUNUO SURA BAADA SURA — MUHTASARI

                                    

1

ANDIKO LA SALA

Utakatifu Wa Kweli Ni Uzima Katika Utumishi

Nitasoma kutoka katika Mafunzo Ya Kristo Kwa Mifano, ukurasa wa 48, kuanzia aya ya 2: {2TG13: 2.1}

“Wengi huhisi hali ya kutengwa na Mungu, utambuzi kwamba wao ni watumwa kwa nafsi na dhambi; wao hufanya juhudi za matengenezo; lakini hawaisulubishi nafsi. Hawajikabidhi kabisa mikononi mwa Kristo, wakitafuta nguvu ya Mungu kutenda mapenzi Yake. Hawataki kufinyangwa kulingana na mfano wa kiungu. Kwa ujumla wao hutambua mapungufu yao, lakini hawaziachi dhambi zao maalum…. Tumaini la pekee kwa nafsi hizi ni kutambua ndani yao ukweli wa maneno ya Kristo kwa Nikodemo, ‘Lazima uzaliwe mara ya pili.’ ‘Mtu asipozaliwa kutoka juu, hawezi kuuona ufalme wa Mungu.’ Utakatifu wa kweli ni uzima katika utumishi wa Mungu. Hili ndilo takwa la kuishi kwa Ukristo wa kweli. Kristo anaomba kujitoa wakfu kukunjufu, kwa huduma isiyokengeuka. Anadai moyo, nia, nafsi, nguvu. Ubinafsi haupaswi kuthaminiwa. Yeye anayeishi kwa ajili yake mwenyewe sio Mkristo.”{2TG13: 2.2}

Tumeamriwa hapa kumkaribia Kristo na kuuacha ubinafsi, na kwamba kabla ya “kuzaliwa mara ya pili” lazima kwanza tufe kwa dhambi. Hebu tuombe ili tutambue kwamba iwapo tunahisi kuwa tumetengwa na Mungu, kosa ni letu, na ya kwamba lazima tufanye jambo ili kurekebisha hali hiyo; kwamba lazima tuupokee mwaliko wa Kristo wa neema: “Njooni Kwangu, nyote… kulemewa na mizigo, Nami nitawapumzisha” — Amani. {2TG13: 2.3}

2

MIHURI NA BARAGUMU HUANZIA NA KUISHIA WAPI?

ANDIKO LA HOTUBA NA V. T. HOUTEFF

MCHUNGAJI WA WADAUDI WAADVENTISTA WA SABATO

SABATO, NOVEMBA 1, 1947

HEKALU LA MLIMA KARMELI

WACO, TEXAS

Alasiri hii tutaona pale ambapo kila Muhuri na Baragumu huanzia na kwishia. Hebu kwanza tusome maelezo ya mihuri mitano ya kwanza: {2TG13: 3.1}

Ufu. 6:1-11 — “Kisha nikaona napo Mwana-Kondoo alipofungua moja ya zile muhuri saba, nikasikia mmoja wa wale wenye uhai wanne akisema, kama kwa sauti ya ngurumo, Njoo! Nikaona, na tazama, farasi mweupe, na yeye aliyempanda ana uta, akapewa taji, naye akatoka, ali akishinda tena apate kushinda. Na alipoifungua muhuri ya pili, nikamsikia yule mwenye uhai wa pili akisema, Njoo! Akatoka farasi mwingine, mwekundu sa-na, na yeye aliyempanda alipewa kuiondoa amani katika nchi, ili watu wauane, naye akapewa upanga mkubwa. Na alipoifungua muhuri ya tatu, nikamsikia yule wa tatu mwenye uhai akisema, Njoo! Nikaona, na tazama, farasi mweusi, na yeye aliyempanda ana mizani mkononi mwake. Nikasikia kama sauti katikati ya hao wenye uhai wanne, ikisema, Kibaba cha ngano kwa nusu rupia, na vibaba vitatu vya shayiri kwa nusu ru-pia, wala usiyadhuru mafuta wala divai. Na alipoifungua muhuri ya nne, nikasikia sauti ya yule mwenye uhai wa nne akisema, Njoo! Nikaona, na tazama, farasi wa rangi ya kijivujivu, na yeye aliyempanda jina lake

3

ni Mauti, na Kuzimu akafuatana naye. Nao wakapewa mamlaka juu ya robo ya nchi, waue kwa upanga na kwa njaa na kwa tauni na kwa hayawani wa nchi. Na alipoifungua muhuri ya tano, nikaona chini ya madhabahu roho zao waliochinjwa kwa ajili ya neno la Mungu, na kwa ajili ya ushuhuda waliokuwa nao. Wakalia kwa sauti kuu, wakisema, Ee Mola, Mtakatifu, Mwenye kweli, hata lini kutokuhukumu, wala kuipatia haki damu yetu kwa hao wakaao juu ya nchi? Nao wakapewa kila mmoja nguo ndefu, nyeupe, wakaambiwa wastarehe bado muda mchache, hata itakapotimia hesabu ya wajoli wao na ndugu zao, wa-takaouawa vile vile kama wao.”

4

Kupata pale ambapo Mihuri huanzia, tutakumbuka kwa uangalifu kwamba Historia hurekodi kipindi kimoja tu cha mauaji ya kufia-imani kama yale yaliyoelezwa katika muhuri wa nne na wa tano — mauaji ya kufia-imani yaliyoanzia kwa Yohana Mbatizaji na, ila pamoja na kukatizwa kidogo, yaliendelea hadi karibu katikati ya karne ya kumi na nane. {2TG13: 5.1}

Bila shaka, basi, muhuri wa nne ulifunguliwa pamoja na kufungwa kwa wakati wa Agano la Kale na mwanzo wa Jipya. Kwa sababu hii ni hivyo, na kwa vile Mihuri hufuatana, mihuri mitatu ya kwanza hupata kutimizwa kwayo, sio katika kipindi cha Agano Jipya, ila katika kipindi cha Agano la Kale. {2TG13: 5.2}

Sasa hebu tuone wakati muhuri wa pili ulipoanza. Tunaambiwa kwamba mpanda farasi wa muhuri wa pili alikuwa “aiondoe amani juu ya nchi,” kumaanisha kwamba amani ilikuwapo awali. Ili kujifunza wakati wa mu-huri wa pili, kwa hivyo, tunahitaji kujibu swali: Amani iliondolewa lini duniani? — {2TG13: 5.3}

Sote tunajua kwamba vita havikuwapo kabla ya gharika, kwamba vita vilianza baada ya mchafuko wa lugha kwenye mnara wa Babeli, baada ya familia ya wanadamu kugawanyika katika lugha, mataifa, na jamii nyingi. Vita vya kwanza vilivyoandikwa katika historia takatifu, vilipiganwa katika siku za Abrahamu, na vita vime-dumu nasi tangu wakati huo. Kabla ya siku hiyo amani ilikuwapo. Je! Ni wapi pengine, basi, muhuri wa pili un-galiweza kutumika ila baada ya gharika, wakati ambapo amani iliondolewa duniani? Mwishowe, historia ya mu-huri wa kwanza lazima itafutwe katika kipindi kabla ya gharika. Rangi (nyeupe) ya farasi yenyewe huzungumza juu ya amani, na kwa hivyo ni wazi kwamba mihuri huanza na uumbaji. {2TG13: 5.4}

5

Je! Farasi, wakiendeshwa na watu, wangeashiria nini? — Wanaweza kuashiria tu kitu ambacho mtu hutawala, kwa maana kila mwendeshaji hutawala kile anachokipanda. Wapanda farasi, basi, lazima wawe nembo ya uta-wala wa mwanadamu juu ya uumbaji wa Mungu. {2TG13: 6.1}

Rangi za farasi na kazi za waliowapanda huonyesha maendeleo katika tamaa na uhalifu. Ni dhahiri kutoka kwenye nembo kwamba mwanadamu kuitawala dunia hakujaiboresha. {2TG13: 6.2}

Farasi mweupe huashiria amani na usafi ambao ulikuwepo tu mwanzoni mwa uumbaji wa Mungu. Kwa mpandaji wa farasi mweupe huonekana kusudi kuu la mwanadamu kuitiisha na kuijaza dunia. Na kwa farasi mwekundu na mpandaji wake tunaona umwagaji wa damu na vita. Ukatili huu uliiongoza njia ya farasi mweusi kuja kwenye eneo. Rangi nyeusi ina umaana wa kuwafanya mataifa watumwa, na mizani ni dhihirisho la ubuni-fu wa miradi ya biashara kujipatia utajiri. Farasi wa nne, wa kijivujivu, huonyesha mfumo wa tabia isiyoweza kueleweka — ngumu kutofautisha iwapo ni Mkristo au Mpagani — unafiki. Muhuri wa tano huonyesha kwamba mateso kwa watakatifu yaliendelea hadi kufunguliwa kwa muhuri wa sita. Je! Hivi sio vichwa vya habari vya historia? Mihuri, kwa hivyo, huanza na mwanzo wa mambo haya. {2TG13: 6.3}

Ufu. 6: 12-17 — “Nami nikaona, alipoifungua muhuri ya sita, palikuwa na tetemeko kuu la nchi; jua likawa jeusi kama gunia la singa, mwezi wote ukawa kama damu, na nyota zikaanguka juu ya nchi kama vile mtini upukutishavyo mapooza yake, utikiswapo na upepo mwingi. Mbingu zikaondolewa

6

kama ukurasa ulivyokunjwa, na kila mlima na kisiwa kikahamishwa kutoka mahali pake. Na wafalme wa dunia, na wakuu, na majemadari, na matajiri, na wenye nguvu, na kila mtumwa, na mwungwana, wakajificha katika pango na chini ya miamba ya milima, wakiiambia milima na miamba, Tuangukieni, tusitirini, mbele za uso wake yeye aketiye juu ya kiti cha enzi, na hasira ya Mwana-Kondoo. Kwa maana siku iliyo kuu, ya hasira yao, imekuja; naye ni nani awezaye kusimama?”

Muhuri wa sita unasheheni ishara za nyakati na huleta mwisho wa dunia. Na kwa sababu sura ya sita ya Ufunuo inatuleta kwa mwisho wa dunia, na maadamu mambo ya sura ya saba yanatukia kabla ya mwisho, ni dhahiri kwamba mada ya sura ya 7 — kutiwa muhuri kwa watu 144,000 kutoka kwa makabila ya Israeli, na ku-kusanywa kwa umati mkubwa kutoka kwa mataifa yote (malimbuko kutoka kwa kanisa, na mavuno ya pili kutoka kwa mataifa) — hurudi nyuma hadi katika kipindi cha muhuri wa sita. Zaidi ya hilo, muhuri wa saba huanza na sura ya 8. {2TG13: 7.1}

Sasa, muhuri wa saba huanzia wapi? Kwanza tukumbuke kwamba muhuri wa sita ulituleta hadi mwisho wa dunia. Bila shaka, kwa hivyo, muhuri wa saba, ambao hushughulikia mada kadhaa, lazima uingiliane na wa sita. Tukumbuke kwamba mwanzo wa muhuri wa saba ulifichua Baragumu Saba. {2TG13: 7.2}

7

8

Namba saba katika Maandiko daima hubeba maana ya ukamilifu. Baragumu Saba kwa hivyo hubeba, kama vile Mihuri Saba, mada yazo kamili. Neno “baragumu” lina maana ya kutangaza ujumbe. Na hivyo Baragumu Saba haswa huonyesha tokeo ambalo wasiotii jumbe hizi walipatwa nalo tangu mwanzo hadi mwisho. Kwamba tarumbeta ya saba huwakilisha ujumbe wa mwisho huonekana upesi kutoka kwa andiko– {2TG13: 9.1}

Ufu. 11:15 — “Malaika wa saba akapiga baragumu, pakawa na sauti kuu katika mbingu, zikisema, Ufalme wa dunia umekwisha kuwa ufalme wa Bwana wetu na wa Kristo wake, naye atamiliki hata milele na milele.”

Hapa tunaona kwamba ujumbe wa mwisho kwa dunia ni ujumbe ambao hutangaza mwisho wa serikali zote za kidunia. {2TG13: 9.2}

Baragumu ziko katika sehemu mbili — tatu za mwisho ni Baragumu za “Ole”, wala sio nne za kwanza. Kwamba Baragumu Saba hufunika nyakati zote za Agano la Kale na Jipya zinaweza kuonekana kwa urahisi katika uchambuzi mfupi wa tarumbeta ya tano– {2TG13: 9.3}

Ufu. 9: 1-4 — “Malaika wa tano akapiga baragumu, nikaona nyota iliyotoka mbinguni, imeanguka juu ya nchi; naye akapewa ufunguo wa shimo la kuzimu. Akalifungua shimo la kuzimu; moshi ukapanda kutoka mle shimoni kama moshi wa tanuru kubwa; jua na anga vikatiwa giza kwa sababu ya ule moshi wa shimoni. Nzige wakatoka katika ule moshi, wakaenda juu ya nchi, wakapewa nguvu kama nguvu waliyo nayo nge wa nchi. Wakaambiwa wasiyadhuru majani ya nchi, wala kitu cho chote kilicho kibichi,

9

wala mti wo wote, ila wale watu wasio na muhuri ya Mungu katika vipaji vya nyuso zao.”

Kwa ile Nyota iliyoanguka kutoka mbinguni imehusishwa na kitenzi jina cha kiume “Yeye”. Kwake Yeye al-ipewa ufunguo wa shimo la kuzimu. Nyota inaweza kumwashiria nani? — Tufungue Ufunuo 20:1 {2TG13: 10.1}

Ufu. 20:1 — “Kisha nikaona malaika akishuka kutoka mbinguni, mwenye ufunguo wa kuzimu, na mnyororo mkubwa mkononi mwake. “

Hapa tumeambiwa kwamba malaika huyu mwenye nguvu, adui wa Shetani, anao “ufunguo wa shimo la kuz-imu.” Iwapo Yeye yu nao, basi Kwake yeye lazima “alipewa” ufunguo. Nyota iliyopokea ufunguo, kwa hivyo, ni mfano wa huyu malaika. {2TG13: 10.2}

Zaidi ya hayo, tuone kwamba mara tu ufunguo ulipolifungua shimo la kuzimu, nzige wakatoka. Mwishowe, ukweli kwamba nzige ni maadui kwa wale ambao hawana muhuri wa Mungu kwenye vipaji lvya nyuso zao, basi ile “Nyota” (malaika) aliyetoka mbinguni na kulifungua shimo ili kuwaachilia nzige ni rafiki wao na adui hodari wa Shetani. Hakuna kwa hivyo kukwepa hitimisho hili: Nyota ya mbinguni inawakilisha Kiumbe aliyetumwa kutoka mbinguni, “malaika” yule yule Ambaye tulimsoma tena katika sura ya 20:1, nao nzige ni umati uliook-olewa na Mbingu. Ni Nani mwingine, basi, ambaye “Nyota” na nzige wanaweza kuwakilisha ila Kristo na Wa-kristo? Shetani alikuwa amelifungia ndani ya shimo la kuzimu taifa lote la Kiyahudi, — taifa la pekee ambalo hapo awali lilikuwa nje ya shimo. Kristo kwa hivyo alikuja kulifungua shimo na kuwaweka huru mateka. Kwa dunia kama hii ndio Bwana wa Mbingu alitumwa, na Yeye alipokuja Alitangaza bila kukawia: {2TG13: 10.3}

10

Luka 4:18,19 — “Roho wa Bwana yu juu yangu, Kwa maana amenitia mafuta kuwahubiri maskini habari njema. Amenituma kuwatangazia wafungwa kufunguliwa kwao, Na vipofu kupata kuona tena, Kuwaacha hu-ru waliosetwa, Na kutangaza mwaka wa Bwana uliokubaliwa.”

Hapa unayo habari katika msimbo wa mafumbo ya Uvuvio wenyewe, ambayo yamefichua upya kwamba Yesu Kristo ni Kiumbe aliyetumwa na mbingu, Mwokozi wa ulimwengu. {2TG13: 11.1}

Sasa ukweli bayana kwamba enzi ya Ukristo ilianza na kuvuma kwa baragumu ya tano, ukweli wa Baragumu nne za kwanza lazima utafutwe katika enzi ya Agano la Kale. {2TG13: 11.2}

Tumeona sasa asili na wakati ambapo Mihuri Saba na Baragumu Saba huanzia na kwishia, na wale ambao wanataka kuzijua mada katika maelezo yazo yote wanaweza kufanya hivyo kwa kusoma trakti hizi , — “Onyo la Mwisho,” na “Kuifungua Mihuri,” — ambayo itatumwa bure kwa ombi. {2TG13: 11.3}

11

ANDIKO LA SALA

Dini Ya Uzembe Husababisha Kuyumba

Nitasoma kutoka kwa ukurasa wa 49 wa Mafunzo ya Kristo Kwa Mifano: {2TG14: 12.1}

“Ikiwa tunampenda Yesu, tutapenda kuishi kwa ajili Yake, kutoa sadaka zetu za shukrani Kwake, kutenda kazi kwa ajili Yake. Kazi yenyewe itakuwa nyepesi. Kwa ajili Yake tutatamani maumivu na taabu na kafara. Tutakuwa na huruma pamoja na shauku Yake kwa ajili ya wokovu wa wanadamu. Tutahisi uchu mwororo ule ule kwa ajili ya nafsi ambazo Yeye ameacha. {2TG14: 12.2}

“Hii ndiyo dini ya Kristo. Chochote kipungufu kwayo ni udanganyifu. Hakuna nadharia tu ya ukweli au dai la uanafunzi litaiokoa nafsi yoyote. Sisi sio wafuasi wa Kristo isipokuwa sisi ni Wake kabisa. Ni kwa moyo wa uzembe katika maisha ya Kikristo kwamba watu huwa wadhaifu kwa madhumuni na vigeugeu katika shauku. Juhudi ya kuwahudumia wote unafsi na Kristo humfanya mtu kuwa msikilizaji wa penye miamba, na hataweza kuvumilia wakati mtihani utamjia.” {2TG14: 12.3}

Sasa tupige magoti na tuombe kwamba tusiweze kusahau kwamba kitu chochote kilichopungukiwa kafara kwa ajili ya nafsi sio dini ya Kristo; ya kwamba ikiwa tu wazembe katika kazi zetu, tutayumba zaidi na zaidi; kwamba dini kamilifu na matendo ya makamilifu unaweza kuwa ushahidi pekee kwamba damu ya Kristo imefanya kazi yake ndani yetu, na kitu cha pekee kuhakikisha haki yetu kwa Mji Mtakatifu. {2TG14: 12.4}

12

KUWEKA ORODHA YA MATUKIO YA UFUNUO SURA BAADA YA SURA — MUHTASARI

ANDIKO LA HOTUBA NA V. T. HOUTEFF

MCHUNGAJI WA WADAUDI WAADVENTISTA WA SABATO

SABATO, NOVEMBA 8, 1947

HEKALU LA MLIMA KARMELI

WACO, TEXAS

Masomo yetu ya zamani yameonyesha kwamba vitabu vyote vya Bibilia hukutana na kwishia katika Ufunuo (Matendo ya Mitume, uk. 585); kwamba Ufunuo hushughulikia historia yote ya wanadamu. {2TG14: 13.1}

Katika masomo haya pia tumejifunza kwamba tukio ambalo lilisababisha kitabu chenye Mihuri Saba kufungu-liwa, liliufichua Ufunuo wenyewe, na kwamba kusema kihalisi, “Ufunuo wa Yesu Kristo aliyopewa na Mungu” huanza na sura ya 6 na huisha na sura ya 22 — sura kumi na saba kwa ujumla, ambazo kufunguliwa kwa Mihuri kulifichua. Pia tulijifunza kwamba mambo ambayo hayana budi kuwako”upesi” kutoka kwa wakati wa Mtakati-fu Yohana, baada ya 96 B.K., ni mambo ambayo tukio hilo lilileta, kusanyiko kubwa lenyewe kukizunguka Kiti cha Enzi likiwa limekutana kuyachunguza mambo ambayo yalikuwa ndani ya Kitabu. {2TG14: 13.2}

Sasa ningependa mtambue kwamba Ufunuo husheheni masomo kadhaa, ambayo kila moja ni kamilifu lenyewe, ingawa sura moja au mada zinaweza kulaliana au kuingiliana na zingine; yaani, mada na sura zote hazi-fuatani kulingana na mpangilio wa matukio na nyingine.

13

Kweli hizi zitaonyeshwa tunapoendelea katika uchambuzi wetu. {2TG14: 13.3}

Hapo awali tulipata kwamba tukio kama la mahakama lilifunguliwa na Ufunuo wa Yesu Kristo aliyopewa na Mungu, Kitabu kilichofungwa na ile mihuri saba. Liliufichua Ufunuo, na kwa hilo baraza la mbinguni lilianza kazi yake ya kupitia ya zamani, ya sasa, na ya siku zijazo ya mwanadamu. Sasa tutasoma aya za mwisho za sura ya sita. {2TG14: 14.1}

Ufu. 6:14-17 — “Mbingu zikaondolewa kama ukurasa ulivyokunjwa, na kila mlima na kisiwa kikahamishwa kutoka mahali pake. Na wafalme wa dunia, na wakuu, na majemadari, na matajiri, na wenye nguvu, na kila mtumwa, na mwungwana, wakajificha katika pango na chini ya miamba ya milima, wakiiambia milima na mi-amba, Tuangukieni, tusitirini, mbele za uso wake yeye aketiye juu ya kiti cha enzi, na hasira ya Mwana-Kondoo. Kwa maana siku iliyo kuu, ya hasira yao, imekuja; naye ni nani awezaye kusimama?”

Kwa sababu sura ya sita inamaliza kisa chake kwa mwisho wa dunia, ni bayana kwamba kwa mpangilio sura ya saba imepachikwa kati ya tukio ambalo sura ya sita huanzia, na tukio ambalo hukwishia. {2TG14: 14.2}

Sura ya saba huanza na kutiwa muhuri watu 144,000, na kwishia na kukusanywa kwa umati mkubwa, ikugusa umilele. {2TG14: 14.3}

Sura ya 8, ufunguzi wa muhuri wa saba, huanza kwa kujulisha mada nyingine, mada ya Baragumu Saba. Baragumu jinsi

14

tulivyojifunza katika masomo yetu ya awali huenea kupitia sura ya 9 hadi ya 11. {2TG14: 14.4}

Tulijifunza zaidi kwamba Baragumu huzifunua jumbe za Mungu na matokeo kwa wadhambi wasiotubu; kwamba Baragumu huanza na ujumbe wa kwanza kama huo, ujumbe wa Nuhu, na humalizika na ujumbe wa mwisho katika wakati wa rehema, ujumbe ambao unatangaza kwamba Siri ya Mungu, kazi ya Injili imekamilika, kwamba wakati wa rehema umekwisha. Hili linaonekana zaidi kutoka kwa ukweli kwamba wanadamu wengine ambao hawakuuawa na moto, moshi, na kiberiti uliotoka vinywani mwa farasi (Ufu. 9:18) hawakutubu. Kwa kweli, isingalisemwa, “Hawakutubu,” iwapo wakati wao wa kutubu ulikuwa haujapita. Hivyo ni kwamba sura ya 8 na ya 9 hutuleta kwa mwisho wa rehema. Sura ya 10 na ya 11 kwa hivyo hujipachika katika sura ya 8 na ya 9. {2TG14: 15.1}

Baragumu zenyewe zinaonyeshwa kuwa katika migawanyo miwili, nne katika wakati wa Agano la Kale, na tatu katika Jipya; yaani, tatu za mwisho ni Baragumu za “ole”. Ya kwanza kati ya Tarumbeta za ole huanzisha kushuka kwa Nyota ya mbinguni Ambayo ilipewa ufunguo wa shimo la kuzimu. Ni wazi kwamba Nyota ni nembo ya Malaika ambaye mwanzoni mwa millenia atamfunga Shetani ndani ya shimo la kuzimu, kwa maana Yeye, Malaika wa Ufunuo 20:1, Ndiye Malaika ambaye ana ufunguo wa shimo la kuzimu. Hangaliweza kuwa na ufunguo ikiwa ungalikuwa umepeanwa kwa mwingine. {2TG14: 15.2}

Sura ya 10 hufichua kwamba malaika aliyekifunua (kifungua) kile “kitabu kidogo” ndiye malaika ambaye huleta mvua ya kiroho kwa ajili ya kukuza na kuikomaza nafaka ya kiroho (kwa maana hiyo ndiyo

15

maana ya wingu na upinde wa mvua). Alisababisha pia kile kitabu kidogo kuliwa (kilizingatiwa moyoni), am-bacho baadaye kikawa kichungu ndani ya yule aliyekila. {2TG14: 15.3}

Utamu wa asali kitabu hicho kilipokuwa kikiliwa bila shaka huashiria kwamba mambo yaliyoandikwa humo yalipokelewa kwa furaha. Lakini kwa yule aliyekila kitabu hicho baadaye kilisababisha kuvimbiwa, kwa mfano, na hivyo kuvunjika moyo; yaani, mambo kitabuni hayakueleweka kikamilifu, na hivyo, furaha ikatoweka, na kuvunjika moyo kukajiingiza. Baada ya hilo, waliokila kitabu waliamriwa “kutoa unabii tena,” kuhubiri tena. {2TG14: 16.1}

Malaika huyu kwenye mkondo wa wakati, kwa hivyo, anaonekana mwanzoni mwa kufunuliwa kwa kitabu cha Danieli, kwa sababu ndicho kitabu pekee cha Bibilia ambacho kiliwahi kufungwa na kutiwa muhuri, na am-bacho hakingefunuliwa kamwe tangu wakati kilipoandikwa hadi “wakati wa mwisho.” {2TG14: 16.2}

Mada ya sura ya 10 hukoma na aya ya pili ya sura ya kumi na moja, aya ambayo hutuleta wakati wa kuwapi-ma (kuwahesabu) watu, ambao kwa udhahiri ni kuwahesabu watu 144,000 (Ufu. 7:3-8), kwa maana wao ndio kundi pekee lililohesabiwa la watu katika safu ya unabii. Hivyo ni kwamba sura ya kumi, pamoja na aya ya 1 na ya 2 kutoka sura ya 11, huanzia mwanzoni mwa “wakati wa mwisho,” na kukoma kwa kuwahesabu watu 144,000. {2TG14: 16.3}

Sura ya kumi na moja (isipokuwa aya mbili za kwanza ambazo ni za sura ya kumi) bado hurejea nyuma kwa wakati kuliko sura ya kumi. Inasheheni mada ya mashahidi wawili waliotoa unabii wakati wa siku 1260 za un-abii. Nayo, pia, hutuleta mbele

16

hadi mwisho wa dunia, wakati ambapo falme za dunia”zinapokuwa falme za Bwana wetu na Kristo Wake.” Ufu. 11:15. {2TG14: 16.4}

Sura ya 12 huturudisha nyuma zaidi kwa wakati kuliko sura ya 11, mbali zaidi ya kuzaliwa kwa Kristo, kisha mbele hadi wakati ambapo nchi itafunua kinywa chake na kuyameza mafuriko, na hadi kwa wakati wa masalia (masalia ni wale ambao wameachwa baada ya wengine kumezwa na nchi). Wao kama watu huzishika amri za Mungu, na wanao ushuhuda wa Yesu Kristo. Wanateswa na yule joka mara baada ya nchi kuyameza mafuriko. {2TG14: 17.1}

Hata sasa hatuwajui watu katika dunia yote, ambao Uvuvio unaweza kusema kwamba wao kama watu (wote) kwa kweli wanazishika amri za Mungu. Kundi la pekee la watu kama hao ambalo linaweza kupatikana katika wakati ni watu 144,000. {2TG14: 17.2}

Ushuhuda wa Yesu Kristo, Uvuvio hueleza ni “Roho Ya Unabii.” Ufu. 19:10. Kuwa na Roho ya Unabii, ni kuwa na Roho Ambaye aliutamka unabii huo na pekee anayeweza kuufasiri, kwa maana “hakuna unabii katika Maandiko upatao kufasiriwa kama apendavyo mtu,” au bila uvuvio wa Roho yule yule. “Maana unabii haukule-twa popote kwa mapenzi ya mwanadamu; bali wanadamu walinena yaliyotoka kwa Mungu wakiongozwa na Roho Mtakatifu.” (2 Pet. 1:20, 21), na kwa hivyo ni watu watakatifu wa Mungu katika Roho wanaweza kuyafasiri Maandiko. {2TG14: 17.3}

Kwa hivyo ni kwamba sura ya 12 inamaliza kisa chake na masalia, watumwa wa Mungu, malimbuko, watu 144,000. Wanakuwa masalia baada ya wanafiki kati yao kumezwa

17

na nchi, kwa mfano. Masalia hawa kama watu watakuwa wakizishika amri za Mungu, na hawatakuwa na hila vinywani mwao. Wao wakiwa malimbuko, Uvuvio hivyo unaonyesha kwamba yatakuwapo mavuno ya pili, kwa sababu pasipo ya pili haiwezi kuwa hapo ya kwanza. Na hivyo tunaona kwamba sura ya 12 inatuleta kwa wakati ambapo kanisa limetakaswa, wakati likiwa kwa kweli kama kanisa linazishika amri za Mungu. {2TG14: 18.1}

Ni lini katika wakati ambapo sura ya kumi na mbili huanza? — Vyema, huanza na siku ambayo mwanamke ali-yetajwa humo alipata mimba ya mtoto wa kiume. Kunena kweli tupu, kupata kwake mimba ya mtoto kuna-zungumzia wakati ambapo Uvuvio uliahidi kumtuma Mkombozi kwa Kanisa. {2TG14: 18.2}

Sura ya 13 inaanza na kuvunjika kwa Ufalme wa Kirumi, na kwa wafalme ambao waliinuka kutoka kwake, ambao walizitwaa taji zao, kama inavyofananishwa na pembe zenye vilemba za mnyama-kama chui. Sura hii hu-koma na amri ya mnyama mwenye pembe mbili, amri ya kuwaua wote ambao watathubutu kutoipokea alama ya mnyama. Ndivyo joka litamkasirikia huyo mwanamke, na hivyo kuwatesa masalia. {2TG14: 18.3}

Sura ya kumi na nne huanza na watu 144,000 wakiwa wamesimama na Mwana-Kondoo juu ya Mlima Zayuni. Kisha hufuata Jumbe za Malaika Watatu katika utumizi wazo wa moja kwa moja na wa mwisho kwa ajili ya kuyakusanya mavuno ya pili. Hivyo sura hufunga pamoja na mavuno ya nchi. Sura yenyewe huonyesha kwamba mavuno yako katika sehemu mbili, ya kwanza ambayo huvunwa na “Mwana wa Adamu,” na ya pili na malaika. Kwa udhahiri mavuno haya mawili huzalisha malimbuko na mavuno ya pili. {2TG14: 18.4}

18

Sura ya 15 huelezea matukio ambayo huleta kikomo cha wakati wa rehema, na sura ya 16 husimulia mapigo saba ya mwisho. {2TG14: 19.1}

Sura ya 17 huanza na kuinuka kwa Babeli Mkuu na utawala wake. Kusema ki-mfano, mnyama-mwekundu sana, mnyama anayemwendesha, anayemtawala, ni ufalme wake. Serikali hii ya kidini ya ulimwengu hustawi baada ya nembo ya mnyama kama chui (sura ya 13) kumaliza kazi yake, kwa maana pembe za mnyama mwe-kundu sana hazina vilemba, ilhali pembe za mnyama kama chui zina vilemba. Pembe zake zenye taji huonyesha dunia inayotawaliwa na wafalme wenye taji, ambao tayari karibu wanatoweka, na pembe za mnyama mwekun-du sana zisizo na taji huonyesha dunia isiyo na taji ambayo inatawaliwa na Babeli ambaye humwendesha yule mnyama, humtawala. Mnyama huyu, unasema Uvuvio, “aliyekuwako naye hayuko, naye yuko.” Yaani, aliishi kabla ya miaka 1000, na kwa hivyo “alikuwako”; haishi wakati wa miaka 1000, na kwa hivyo “hayuko”; anaishi kwa kufufuliwa baada ya millenia, na kwa hivyo “naye yuko.” {2TG14: 19.2}

Yeye ni wa nane na ni mmoja wa wale saba; yaani, wanyama wanne wa Danieli sura ya 7, na wawili wa Yo-hana wa sura ya 13, kwa ujumla sita, mnyama mwekundu sana wa sura ya 17 kwa hivyo ni wa saba mwanzoni mwa millenia, na ni wa nane baada ya millenia. Ni wa wale saba kwa sababu, nilivyosema hapo awali, atakufa kifo chake cha kwanza mwanzoni mwa millenia, na katika ufufuo baada ya millenia anaishi tena kwa kipindi kifupi kabla kukumbana na mauti yake ya pili, na ufufuo unamfanya kuwa wa nane katika awamu yake ya pili, na wa saba katika awamu yake ya kwanza. Sura ya 17 kwa hivyo inaanza na Babeli Mkuu akimpanda yule mnyama, awamu yake ya kwanza, na kwishia kwa upande mwingine wa

19

millenia, awamu ya pili ya yule mnyama. {2TG14: 19.3}

Kama tokeo la kutakaswa kwa kanisa, kutiwa muhuri kwa watu 144,000, watumwa wa Mungu, dunia inaangazwa kwa utukufu wa malaika (Ufu. 18:1), na “injili ya milele” (Ufu. 14:6). Kisha watu wa Mungu wanaitwa kutoka kwa himaya ya Babeli ili wasizishiriki dhambi zake (Ufu. 18:4). Wakati huo wanaletwa kuin-gia mahali ambapo hakuna dhambi, pale ambapo masalia huzishika amri za Mungu, na pale ambapo hakuna hofu ya mapigo kuwahi kuanguka (Ufu. 18:4). Na kwa hivyo sura ya 18 inaanza baada ya kutiwa muhuri kwa wa-tumwa wa Mungu, na kwishia na kuangamizwa kwa mwanamke, Babeli Mkuu. Hili linatukia baada ya watakati-fu kuitwa watoke na kupelekwa nyumbani. {2TG14: 20.1}

Sura ya kumi na tisa hufichua kuvunjika kwa yule mnyama na yule nabii wa uongo, pia kwa masalia (ya wale wameachwa Babeli, wengine wote wa dunia). Kwa hivyo millenia, iliyoletwa kwa mtazamo katika sura ya ishir-ini, huanza baada ya yule mnyama na nabii wa uongo, pia wengine wote wa dunia ambao hawakutubu, kuangamia. Na wakazi pekee walioachwa juu ya dunia mwanzoni mwa millenia ni mavuno ya kwanza na ya pili (watakatifu) ya shamba kubwa la mavuno la ulimwengu, na “walio heri na watakatifu” ambao wanainuka katika ufufuo wa kwanza. Hivyo ni kwamba Shetani hawezi kuwadanganya mataifa wakati wa millenia, na kwa hivyo ni kwamba millenia ni wakati wa amani. Lakini tangu siku ambayo mataifa watafufuliwa mwishoni mwa mille-nia hadi kwa mauti yao ya pili, mwasi mkuu wa vizazi vyote atawadanganya tena. Wafu, wakati huo, ambao hawatatoka makaburini mwao katika ufufuo wa kwanza (sura ya 20:5), hawataishi tena hadi miaka elfu imeka-milika. {2TG14: 20.2}

20

Kutoka kwa haya tunaona kwamba pale ambapo sura ya kumi na tisa huachia, sura ya ishirini inaanzia hapo. {2TG14: 21.1}

Sura ya ishirini na moja inaonyesha dunia iliyoumbwa upya na Yerusalemu mpya. {2TG14: 21.2}

Sura ya ishirini na mbili husimulia kiti cha enzi cha Mungu na mto wa uzima, na hufunga na maonyo dhidi ya wale ambao kwa ufasiri kulingana na mapenzi yao huongeza na kuondoa ili kubuni nadharia zao. Kizuio dhidi ya kuongeza na kuondoa huonyesha kwamba Ufunuo ni kamili jinsi ulivyo, kwamba hauhitaji hekima ya mwa-nadamu, wala msaada wake. Iwapo watakiuka amri hii, Mungu ataondoa sehemu yao katika kitabu cha uzima. {2TG14: 21.3}

Kuelezea waziwazi na kwa mfuatano yale nimejaribu kuwasilisha kwenu, nitawaruhusu sasa muyachambue kwa mapumziko yenu kupitia kwa msaada wa ramani iliyo kwa ukurasa unaofuata. {2TG14: 21.4}

(Wale ambao wangependa kuuchambua Ufunuo kwa undani zaidi wanaweza kufanya hivyo kutoka kwa trakti, Kwa Makanisa Saba. Somo la Baragumu Saba, hata hivyo, kamilifu kwa kila jambo kwa undani, mtapata ndani ya Trakti namba 5, Onyo la Mwisho.) {2TG14: 21.5}

21

22

Usiyakose Manufaa Juu Ya Hili

Iwapo haujatuma kwa ajili ya nakala yako iliyotangazwa na iliyojadiliwa sana kijitabu cha afya cha kurasa 96 (“Kabari Inayoingia”) ambacho kimefanya uamsho mkubwa katika dunia ya Waadventista na ambacho kimeli-weka Shirika la K.I. katika mwangaza, usikikose iwapo afya, nyumba, na furaha yako inamaanisha kitu kwako. Kwa maoni yetu kitabu hiki ndicho bora hatujawahi kuona juu ya su-ala hili. Kwa kweli tunahisi kwamba ki-metumwa na Mungu, na kwamba nakala yake inapaswa kuwa katika kila nyumba. Tumejulishwa kwamba sasa unaweza kukipata bila kuagizia. Tuma jina lako, anwani, na jina la kanisa ambalo wewe ni mshiriki (unaombwa kuchapisha), na senti 15 kwa sarafu au stempu kwa Shirika La Kabari Inayoingia La Marekani, Kituo cha Mlima Karmeli, Waco, Texas, Marekani na kitatumwa kwako. {2TG14: 23.1}

23

Jumuiya ya Wadaudi Waadventista wa Sabato

(Ushirika Huru Unaojumuisha Kanisa)

Mlima Karmeli, Waco, Texas

S.L.P. 23738, Waco, TX 76702

+ 1-254-855-9539

www.gadsda.com

info@gadsda.com

Gombo la 2, Namba 13, 14

Kimechapishwa nchini Marekani

24

>