fbpx

Gombo la 1 Salamu Mwafaka Namba 49, 50

Gombo la 1 Salamu Mwafaka Namba 49, 50

                                    

AMANI YA PEKEE YA MAWAZO

Hati miliki, Kimechapishwa tena 1953

Haki zote zimehifadhiwa

V. T. HOUTEFF

                                    

DINI NI NINI? JE! HUFAIDI SASA NA HAPO BAADAYE?

MAISHA NI KUMBE HUWA VILE SISI TUNAVYOYAFANYIZA

                                    

1

ANDIKO LA SALA

Mifano — Viunganishi Katika Mnyororo Wa Ukweli

Nitasoma kutoka katika “Mafunzo ya Kristo Kwa Mifano,” kwa ukurasa wa 17– {1TG49: 2.1}

“Katika mafundisho kwa mifano ya Kristo kanuni iyo hiyo inaonekana kama ilivyo katika utume Wake mwenyewe kwa ulimwengu. Ili tuweze kufahamu tabia na maisha Yake matakatifu, Kristo alichukua asili yetu, na akaishi kati yetu …. Wanadamu wangaliweza kujifunza yasiyojulikana kupitia yanayojulikana; mambo ya mbinguni yalifunuliwa kupitia kwa ya duniani; Mungu alidhihirishwa kwa sura ya wanadamu. Ndivyo ilikuwa katika fundisho la Kristo: lisilojulikana lilifafanuliwa kwa linalojulikana; kweli takatifu kwa mambo ya duniani ambayo watu walikuwa wanayajua sana …. Vitu vya asili vilikuwa njia ya vya kiroho; vitu vya maumbile na uzoefu wa maisha ya wasikilizaji Wake uliunganishwa na kweli za neno lililoandikwa. Hivyo kuongoza kutoka kwa ufalme wa asili hadi kwa wa kiroho, mifano ya Kristo ni viunganishi kwenye mnyororo wa ukweli ambao huunganisha mwanadamu kwa Mungu, na nchi kwa mbingu.” {1TG49: 2.2}

Tuombe ili tuweze kuelewa mafundisho ya Kristo yasiyojulikana kupitia kwa yanayojulikana — mambo ya mbinguni jinsi yanavyofunuliwa kupitia kwa ya duniani; kwamba tuige njia ya Kristo ya kufundisha, tukionye-sha kweli Takatifu kwa vitu vya duniani; tuombe kwamba tufaidike kikamilifu kwa mifano ya Kristo — viungan-ishi bora katika mnyororo wa Ukweli ambao huunganisha dunia na mbingu. {1TG49: 2.3}

2

DINI NI NINI? JE! HUFAIDI SASA NA HAPO BAADAYE?

MATINI YA HOTUBA NA V. T. HOUTEFF

MCHUNGAJI WA WADAUDI WAADVENTISTA WA SABATO

SABATO, JULAI 12, 1947

HEKALU LA MLIMA KARMELI

WACO, TEXAS

Ikiwa wanadamu  wanahitaji kujua kitu chochote juu ya kingine, ni jibu la maswali haya mawili: Dini ni nini? Je! Inafaidi sasa na hapo baadaye? {1TG49: 3.1}

Wengi wanafikiria kwamba dini hujumuisha kwenda kanisani, kusali, kuwa na tabia njema, kutoiba, kutoua, ku-tocheza michezo, kutocheza kamari, kutohudhuria maonyesho, kutokula vitu fulani, kufanya au kutofanya hivi, kile, na kingine. {1TG49: 3.2}

Wengine hufikiri dini sio kitu zaidi ya aina ya utaratibu fulani wa kijamii, na ya kwamba kanisa ni mahali pa kujuana, n.k, n.k. Hebu tuone: {1TG49: 3.3}

Yesu alikabiliwa na yule kijana tajiri, ambaye Alimwambia, nimezishika amri. Nifanye nini ili niurithi uzima wa milele? Hapa linafuata jibu: {1TG49: 3.4}

Luka 18:22 — “Yesu aliposikia hayo alimwambia, Umepungukiwa na neno moja bado; viuze ulivyo navyo vyote, ukawagawanyie maskini, nawe utakuwa na hazina mbinguni; kisha, njoo unifuate.”

Kulielewa andiko hili, lazima tusome lingine

3

pamoja nalo: {1TG49: 3.5}

Yohana 3: 1-3 — “Basi palikuwa na mtu mmoja wa Mafarisayo, jina lake Nikodemo, mkuu wa Wayahudi. Huyo alimjia usiku, akamwambia, Rabi, twajua ya kuwa u mwalimu, umetoka kwa Mungu; kwa maana hakuna mtu awezaye kuzifanya ishara hizi uzifanyazo wewe, isipokuwa Mungu yu pamoja naye. Yesu akajibu, akamwambia, Amin, amin, nakuambia, Mtu asipozaliwa mara ya pili, hawezi kuuona ufalme wa Mungu.”

Wote kijana tajiri na Nikodemo walikuwa watawala, na ingawa Nikodemo hakukuwa tajiri kama alivyokuwa yule kijana, hata hivyo hakuwa masikini. Lakini kwa nini mmoja aliulizwa kuugawa utajiri wake kwa masikini, na mwingine akaambiwa azaliwe mara ya pili? Kwa nini wote wasiweze kulipa gharama sawa kwa ajili ya wokovu? Hapa zipo sababu: {1TG49: 4.1}

Ili kuepuka kuonekana katika kundi la Yesu, Nikodemo alikuja Kwake, sio mchana, ila kwa siri usiku, ilhali yule mtawala kijana tajiri alikuja kwa Yesu sio tu wazi wakati wa mchana, lakini pia wakati umati wa watu ulikuwa na Yesu. Kizuizi cha msingi kwa mtawala kijana tajiri, kwa hivyo, kilikuwa utajiri wake, na kizuizi cha msingi kwa Nikodemo kilikuwa kiburi chake. Ni wazi, basi, maradhi ya mmoja yalihitaji tiba ya aina moja, na maradhi ya mwingine yalihitaji aina nyingine ya matibabu. {1TG49: 4.2}

Yesu kamwe hakumuuliza mtu yeyote achukue dini Yake, ila aliwauliza “wamfuate” Yeye, waweze kuwa mmo-ja wa wanafunzi wake. Mtawala kijana tajiri hakuweza kumfuata Bwana kwa sababu moyo wake ulitegemea utajiri wake. Na Nikodemo hakuweza kumfuata Bwana kwa sababu alikuwa na kiburi sana kuonekana katika kundi la asiye maarufu na aliyechukiwa Yesu aliyefuaswa na wavuvi wanyenyekevu. Kuondoa vizuizi, mmoja alipaswa

4

atupilie mbali utajiri wake, na mwingine ilibidi atupilie mbali kiburi chake. Ili kuondoa kiburi, mtu lazima az-aliwe mara ya pili, lazima awe mtu mpya. Lakini kuonolea mbali kupenda fedha mtu lazima apeane pesafedha zake kwa wale wanaozihitaji kwa kweli. {1TG49: 4.3}

Maandiko yanashuhudia kwamba Abrahamu alikuwa tajiri sana. Walakini anaitwa “rafiki wa Mungu.” Utajiri ndani yake, kwa hivyo, unaweza kuwa baraka, ingawa mara nyingi huwa laana. Kiburi, hata hivyo, sio kizuri kamwe. {1TG49: 5.1}

Kumbuka kwamba Ibilisi hupata ndani ya kila mmoja wetu angalau mwanya mmoja. Uwe mwanya uwayo wote, lazima uondolewe mbali — uwe utajiri au uwe kiburi. Bila shaka sio wote walio matajiri wamefungwa kwa utajiri wao, lakini kila mtu anaweza kufungwa kwa nafsi yake, “utu wa kale.” Na sio wote wanahitaji kuusalimisha uta-jiri, lakini wote wanahitaji kujitenga kwa “utu wa kale” ambao huwaingiza katika kila kitu isipokuwa kile wana-paswa kuwa ndani yake. {1TG49: 5.2}

Hebu tusome tena kutoka katika Yohana tatu– {1TG49: 5.3}

Aya ya 4-8 — “Nikodemo akamwambia, Awezaje mtu kuzaliwa, akiwa mzee? Aweza kuingia tumboni mwa mamaye mara ya pili akazaliwa? Yesu akajibu, Amin, amin, nakuambia, Mtu asipozaliwa kwa maji na kwa Roho, hawezi kuuingia ufalme wa Mungu. Kilichozaliwa kwa mwili ni mwili; na kilichozaliwa kwa Roho ni roho. Usistaajabu kwa kuwa nilikuambia, Hamna budi kuzaliwa mara ya pili. Upepo hu-vuma upendako, na sauti yake waisikia, lakini hujui unakotoka wala unakokwenda; kadhalika na hali yake kila mtu aliyezaliwa kwa Roho.”

Nikodemo kukiri kwamba Yesu alikuwa

5

Mwana wa Mungu aliifanya kesi yake kuwa mbaya sana. Kujua Yesu alikuwa nani, hangalipaswa kuaibika kuonekana katika kundi Lake, wala hangalipaswa kuwaogopa maadui Zake. Angaliweza kuona huo ulikuwa up-endeleo wa kushirikiana na Mwana wa Mungu, na kiumbe wa Mbinguni. Lakini kwa kadri Nikodemo alikuwa na aibu kuonekana pamoja Naye, na alikuwa na fahari ya kuwa pamoja na Mafarisayo, alihitaji kuuzika “utu wa kale,” na kuamka katika upya wa uzima — alihitaji kuzaliwa mara ya pili. {1TG49: 5.4}

Kwa swali, “Awezaje mtu kuzaliwa, akiwa mzee?” Yesu akajibu, “Mtu asipozaliwa kwa maji na kwa Roho, hawezi kuuingia Ufalme wa Mungu.” Nikodemo alihitajika kubatizwa, alihitajika kukiri hadharani Yesu kuwa ni Mwana wa Mungu, na apokee Roho wa Kweli. {1TG49: 6.1}

Na mfano, “upepo huvuma upendako, na sauti yake waisikia, lakini hujui unakotoka wala unakoenda; kadhalika na hali yake kila mtu aliyezaliwa kwa Roho,” bila shaka unabainisha kwamba kujua hakika ni nini kuzaliwa kwa Roho ni kuwa na uzoefu wa kuwa mmoja wa wanafunzi Wake, wa kujazwa kwa Roho Mtakatifu, na wa kuutangaza Ukweli Wake. Yesu, kuwalinganisha wafuasi Wake, wale ambao wamezaliwa mara ya pili, na up-epo, huufanya ukweli huu kuwa wazi zaidi; kwa maana ikiwa wanafunzi Wake ni kama upepo, ikiwa hakuna yeyote anayejua wanakotoka na waendako, basi njia pekee ya kujua ni kuwa mmoja pamoja nao. {1TG49: 6.2}

Ili Yesu kuwa mmoja pamoja nasi Ilimpasa azaliwe mara ya pili; Ilimbidi awe mtu wa duniani. Na ili sisi tuweze kuwa wamoja pamoja Naye, hatuna budi kuzaliwa mara ya pili, kuzaliwa kwa Roho. Tofauti ni kwamba Yesu mwanzo alizaliwa wa kiroho, kiumbe Kitakatifu, na pili mwanadamu;

6

ilhali mwanzo tumezaliwa wanadamu, na pili viumbe wa kiroho. Kunena kinabii juu ya kuzaliwa kwa Yesu, nabii Isaya aliandika: {1TG49: 6.3}

Isa. 66: 7 — “Kabla hajaona utungu alizaa; Kabla maumivu yake hayajampata, Alizaa mtoto mwana-mume.”

Kanisa la Kiyahudi, kanisa ambamo na kwalo Yesu alizaliwa, Uvuvio hutangaza, halikuona utungu wala maumivu; yaani, halikuhisi hitaji wala mzigo kwa ajili ya Mwokozi, na licha ya hayo, Yeye alizaliwa. {1TG49: 7.1}

Lakini tukizungumza kuwahusu watoto ambao watajumuika kuwa Ufalme, tunasoma: {1TG49: 7.2}

Aya ya 8 — “Ni nani aliyesikia neno kama hili? Ni nani aliyeona mambo kama haya? Je! Nchi yaweza ku-zaliwa siku moja? Taifa laweza kuzaliwa mara? Maana Sayuni, mara alipoona utungu, Alizaa watoto wake.”

Ingawa kanisa la Kiyahudi katika siku za Yesu halikuhisi utungu, lakini lilimzaa Mwana wa Mungu! Lakini Za-yuni anapohisi utungu atazaa watoto wake wote mara moja, taifa zima! Muujiza katika kila tukio. {1TG49: 7.3}

Je! Zayuni anaweza kuzaa vipi? — Hebu turejee kwenye ufalme wa maumbile: Katika maumbile, mama humbeba mtoto, kisha huhisi utungu na kuzaa. Vipi vinginevyo, basi, katika ufalme wa kiroho Zayuni anaweza kuhisi utungu bila kwanza kuwabeba watoto wake kabla wazaliwe? Kubainisha, wakati mtu anajiunga kwa kanisa, linakuwa ujauzito naye kwa mfano. Wakati linabeba watoto wake hivyo, basi wote watazaliwa mara moja, — wote kwa wakati mmoja watapokea kuzaliwa kwao mara ya pili, kuzaliwa kunakotajwa hapa. {1TG49: 7.4}

7

Na jinsi Uvuvio huweka wazi kwamba lazima wazaliwe mara ya pili, wote mwanzoni lazima wawe katika hali sawa ya nia kama alivyokuwa Nikodemo – wanaona aibu kuonekana katika kundi la waamini wa Ukweli wa sasa, wanaona haya kuhusishwa na waamini wa Ukweli usio maarufu. {1TG49: 8.1}

Kwa uwazi, basi, juhudi zetu za kuwafikia watu na ujumbe wa “kuzaliwa mara ya pili” hazitakuwa bure: Zayuni atawazaa watoto wake wote, kama ilivyo, katika siku moja. Na ndio sababu hatuwezi kusukumwa kukata tamaa au kuvunjika moyo. Tunahakikishiwa kwamba “uamsho na matengenezo” yatatukia kati ya watu wote wa Mun-gu, kwamba Neno Lake halitarudi Kwake bure. {1TG49: 8.2}

Sasa, watoto wanaweza kuwa nani? — Ili kuwa watoto wa Zayuni, lazima siku moja wasimame Zayuni. Wao kwa hivyo sio wengine isipokuwa “malimbuko” ambao Wa-ufunuo husema: “Kisha nikaona, na tazama, huyo Mwana-Kondoo amesimama juu ya mlima Sayuni, na watu mia na arobaini na nne elfu pamoja naye, wenye jina lake na jina la Baba yake limeandikwa katika vipaji vya nyuso zao.” Ufu. 14: 1. {1TG49: 8.3}

Kutoka kwa Maandiko sasa inaonekana wazi kwamba katika mfano huu wakati mtu anajiunga na kanisa, kanisa linakuwa ujauzito na huyo mshiriki. Hivyo ni kwamba tangu wakati mtu anakuwa mshiriki wa kanisa hadi wa-kati “anazaliwa mara ya pili,” yeye anakua kiroho kwa ajili ya saa ya huku kuzaliwa mara ya pili. Kisha, baada ya “kuzaliwa mara ya pili” bado anaendelea kukua hadi kuwa mtu mzima, aliyekomaa, kiumbe cha kiroho — mtu mkamilifu, hadi kwa kipimo cha kimo cha Kristo, bila waa wala kunyanzi au kitu kama hicho. Kwa hivyo, hali ya kuwa hivi hakuna yeyote hata sasa ameifikia, lakini wakati umekaribia sasa ambapo umati utaifikia, kwa maana asema Bwana: {1TG49: 8.4}

8

Isa. 66: 9 — “Je! Mimi nilete wana karibu na kuzaliwa, nisizalishe? Asema Bwana; mimi nizalishaye, je! Nilifunge tumbo? Asema Mungu wako.”

Andiko hili linajaribu kuondoa mashaka yote. Wacha tumwamini Bwana na tujue hakika kwamba wakati wa huku kuzaliwa upya hasa kumewadia na kwamba Bwana anaweza na atawezesha hivyo bila kujali ni kunaweza kuonekana vipi kwetu. {1TG49: 9.1}

Kutoka kwa uchambuzi huu tunaona kwamba dini haijafanyizwa kwa lazima na usifanye; ya kwamba hakuna yeyote atakayefungwa kwa mtu, ila kwa Ukweli wa Mungu ambao daima unakunjuka; ya kwamba dini in-amaanisha kuwa wa kumfuata Bwana, na kuwa wa kuyafanya mambo ambayo Yeye humwongoza mmoja kutenda; kwamba tangu wakati mtu anapompokea Bwana kama Mwokozi wake, — tangu wakati huo anaanza kukua kiroho, kwanza kuzaliwa mara ya pili, kisha kiumbe wa kiroho aliyekomaa, sio yote kwa wakati mmoja, lakini kukua kila siku. Ili kuifikia hali ya juu ya ukamilifu, mmoja lazima kwa hivyo awe akijikamilisha mwenyewe kila siku na kuenenda pamoja na Ukweli wa Mungu, kwamba kila cheche ya Ukweli inaweza kuongeza kiwango cha ukuaji wa kiroho msimu unavyohitaji, au sivyo mmoja ataanguka nyuma asiufikie uko-mavu wa kiroho. Ni hivyo tu kwamba mmoja anaweza kuvuna faida zote ambazo dini hutoa. {1TG49: 9.2}

Hapana, dini sio kitu cha ziada, kitu cha hiari. Ni kitu ambacho kila mtu lazima awe nacho. Dini ya kweli na ya kisasa ni kitu muhimu kama macho katika kichwa chako. {1TG49: 9.3}

Kwa mifano niruhusu niwapeleke kwenye mkondo wa wakati, kuanza na Nuhu. Dini yake sio tu ilimuokoa yeye na familia yake kutokana na kuzama katika gharika ya kutisha, lakini pia ilimfanya kuwa mzazi wa ulimwengu baada ya gharika, — naam, mzazi wa dunia

9

yetu. Ulimwengu katika siku yake, hata hivyo, uliangamia kwa sababu haukuhisi hitaji la dini ya kisasa, bila hitaji la ukweli wa Sasa. Ni aibu kama nini! Ni upuuzi kama nini kwa mtu kujaribu kuishi bila dini, bila ushauri wa Mungu, na bila ujumbe wa saa! {1TG49: 9.4}

Hebu tuangalie jambo kuu lingine katika historia ya Bibilia. Mama ya Musa aliamini katika dini ya sasa. Aliamini kwamba wakati ulikuwa umekuja kwa ajili ya ukombozi wa taifa la Waebrania, na alitenda yote aliyoweza kufanya uwezekane. Alipoona kwamba hangaliweza tena kumficha mwana wake mchanga kutoka kwa mkono wa Farao, aliacha dini yake itende yaliosalia. Matokeo yalikuwa makubwa, sio tu kwamba alimpokea mwanawe tena mikononi mwake ameokolewa milele kwa kutotupwa katika mto Nile, lakini pia dhamana ya msaada wake, elimu, na yote — bora ambayo Misri ingaliweza kumudu — yalilipwa kutoka katika hazina ya Farao! Aina sahihi ya dini, unaona, hufanya mambo makubwa. {1TG49: 10.1}

Miaka themanini baadaye Dini ya Musa iliongoza taifa lote la Waebrania kutoka kwenye yadi za matofali ya Farao hadi kwa Bahari ya Shamu. Bahari iligawanyika kwa ajili yao, na mara walipokuwa wamepita, iliwafunika wasimamizi wao wa kazi. Ukombozi kama nini! Ushindi ulioje! {1TG49: 10.2}

Zaidi ya hayo, mamilioni ya wanaume, wanawake, na watoto, na mifugo yao, walipoingia katika jangwa hatari mahali ambapo hapakuwa na chakula wala maji, dini ilifanya miamba ibubujike vijito, na mawingu yakadon-dosha mana — sio kwa siku moja , wala kwa mwezi, ila kwa miaka yote arobaini! Kisha muujiza wa Bahari ya Shamu ulirejelewa kwa mto Yordani, na watengeneza matofali waliowekwa huru wakawa manabii, wafalme, na makuhani! {1TG49: 10.3}

10

Bila kujali matukio haya yote makubwa, wakati walipokuwa walegevu na wasiojali, walipojihisi hawahitaji man-abii, hawana haja ya Ukweli wa sasa, hawana hitaji la chakula kwa wakati wake, wakawa tena watumwa na mateka! Ndio sababu tunahitaji aina sahihi ya dini, na ndio sababu tunahitaji kushikamana na dini na kukua nayo. {1TG49: 11.1}

Wayahudi walitekwa nyara na kupelekwa Babeli. Walakini, wale ambao walikuwa waaminifu kwa dini yao walitunzwa vizuri hata katika utumwa wao. Danieli, kwa mfano, badala ya kutumika kama mtumwa, badala yake alishugukuliwa kama bwana, na mwishowe akafanywa kuwa mtawala na wote Wakaldayo na Wamedi-Waajemi. Na wakati licha ya chuki alitupwa ndani ya tundu la simba, aliokolewa, wakati ambapo maadui zake waliliwa na wale hayawani wa porini. {1TG49: 11.2}

Wakati Waebrania watatu, kwa ajili ya uaminifu kwa dini yao, walitupwa katika tanuru la moto, Mwana wa Mungu alikuja na kuwaokoa na sio hata unywele wa vichwa vyao uliangamia. Adui zao, hata hivyo, walichom-wa hadi kufa, lakini Waebrania wakafanywa watawala katika ufalme. {1TG49: 11.3}

Gideoni alipaswa kushinda vita. Baada ya kuajiri askari 22,000, aliambiwa kwamba walikuwa wengi sana! Kwa hivyo wapoteza muda waliondolewa, na mwishowe walikuwapo tu mia tatu walioachwa kupigana dhidi ya umati ulioufunika uwanda! Licha ya jeshi lake dogo, Gideoni alishinda vita usiku kucha, na bila kumpoteza mtu! Dini, Ndugu, Dada, ukiishi kwayo, ni pendekezo linalolipa. {1TG49: 11.4}

Wote wangaliweza kuwa akina Danieli na akina Gideoni. Naam, hata Wayahudi wa leo wangaliweza kuwa kitu fulani, lakini wao ni nini? — Taifa lililochukiwa na watu wote

11

ulimwenguni, taifa bila mfalme, bila bendera, bila nchi, — taifa pekee la namna hiyo duniani. {1TG49: 11.5}

Acha niwaambie kuhusu uzoefu ambao ni wa kibinafsi sana, na habari kwa wengi wenu. Miaka kadhaa iliyopita wakati nalikuwa nikivuka moja ya barabara za shughuli nyingi Los Angeles, California, mwanamke mmoja kutokea kwangu kushoto akiliendesha gari alinigonga dafrao. Kisha akaingiwa na wasiwasi hata hakuweza kuli-simamisha gari lake lakini aliendelea kwenda kwa nusu ya nyumba nyingi pamoja. Gari, hata hivyo, hai-kunipindua; mkono usioonekana ulinibeba mbele yake. Na gari liliposimama kulia kwenye njia ndogo ambayo ilivuka barabara, nilisimama, pia! Kufikia wakati huo mamia ya watazamaji pamoja na waandishi wa habari na askari magari matatu, walikuwa wamekusanyika kulizunguka gari. Walipokosa kupata yeyote amelala barabara-ni, amekufa au amejeruhiwa, basi waliamua kwamba mwathiriwa lazima amebanwa chini ya gari. Nalipowaam-bia kuwa ni mimi ambaye alikuwa amegongwa, walishangaa. Kama nilivyowaambia kwamba sikuwa nimeumia, na kwa vile nilikataa kupelekwa hospitalini, walinifanya niiue juu mikono na miguu yangu, na waliuliza dazani za maswali. Penseli katika mfuko wa koti langu ilikuwa imevunjika kwa athari za gari ilikuwa vipande karibu dazani, lakini mbavu zangu hazikuguswa! Kisha mmoja kati ya umati wa watu akasema, “Lazima awe ameumb-wa kwa mpira.” {1TG49: 12.1}

Dini, mnaona, ni bora kuliko sera ya bima. {1TG49: 12.2}

Kutoka kwa somo letu tunang’amua kwamba nguvu ya Mungu ambayo iliulinda uhai hata katika tanuru la moto na kwenye tundu la simba, bado inatenda kazi; ya kwamba Mungu bado anavutiwa sana na watu Wake leo ka-ma vile Alivyokuwa kwa Danieli au kwa siku nyingine yoyote. Sisi kwa hivyo tunahitaji dini ya sasa kila siku. Hatuwezi kumudu kuwa bila nayo, — la, sio hata kwa muda mfupi tu. {1TG49: 12.3}

Ukweli Mwafaka sio tu unaokoa roho zetu kwa ajili ya umilele,

12

lakini Hutulinda siku baada ya siku. Husambaza mahitaji yetu leo na hutupatia tumaini la baadaye. Hakuna usalama katika kitu kingine chochote, na imani kwa Mungu ndio amani yetu ya mawazo, haswa katika siku na kizazi hiki. {1TG49: 12.4}

Dini bila shaka inayo faida sio tu baadaye, ila hakika kwa ajili ya leo vile vile. Usichipumbaze kwa kujaribu kuendelea pasipo kuwa nayo. {1TG49: 13.1}

Usiyakose Manufaa Juu ya Hili

Iwapo haujatuma kwa ajili ya nakala yako iliyotangazwa na iliyojadiliwa sana kijitabu cha afya cha kurasa 96 (Kabari Inayoingia) ambacho kimefanya uamsho mkubwa katika dunia ya Waadventista na ambacho kimeliweka Shirika la K.I. katika mwangaza, usikikose iwapo afya, nyumba, na furaha yako inamaanisha kitu kwako. Kwa maoni yetu kitabu hiki ndicho bora hatujawahi kuona juu ya su-ala hili. Kwa kweli tunahisi kwamba kimetumwa na Mungu, na kwamba nakala yake inapaswa kuwa katika kila nyumba. Tumejulishwa kwamba sasa unaweza kukipata bila kuagizia. Tuma jina lako, anwani, na jina la kanisa ambalo wewe ni mshiriki (unaombwa kuchap-isha), na senti 15 kwa sarafu au stempu kwa Shirika La Kabari Inayoingia La Marekani, Kituo cha Mlima Kar-meli, Waco, Texas, Marekani na kitatumwa kwako. {1TG49: 13.2}

13

ANDIKO LA SALA

Mdhihirishe Mungu; Usimfiche

Nitasoma kutoka katika “Mafunzo ya Kristo Kwa Mifano,” ukurasa wa 18, kuanzia aya ya kwanza– {1TG50: 14.1}

“Katika mafundisho Yake kutoka kwa maumbile, Kristo alikuwa akizungumza juu ya vitu ambavyo mikono Yake mwenyewe imeumba, na ambavyo vilikuwa na ubora na nguvu ambazo Yeye Mwenyewe alikuwa amezi-weka. Katika ukamilifu wavyo wa asili, vitu vyote vilivyoumbwa vilikuwa dhihirisho la wazo la Mungu …. Dunia sasa imeharibiwa na kutiwa unajisi kwa dhambi …. Masomo ya mifano ya Mungu haijafutiliwa mbali; ya-kieleweka kwa usahihi, maumbile hunena kumhusu Muumba wake. Katika siku za Kristo masomo haya yaliku-wa yamesahaulika …. Udhambi wa wanadamu ulikuwa umeharibu uso mzuri wa uumbaji; na badala ya kum-dhihirisha Mungu, kazi Zake zikawa kizuizi kilichomficha Yeye …. Hivyo katika Israeli, mafundisho ya mwana-damu yalikuwa yamewekwa mahali pa ya Mungu. Sio tu vitu vya maumbile, bali huduma ya kafara na Maandi-ko yenyewe, — vyote vilitolewa kumfunua Mungu, — vilipotoshwa sana hata vikawa njia ya kumficha Yeye.” {1TG50: 14.2}

Hushangaa iwapo dunia sio karibu sawa leo jinsi ilivyokuwa katika siku ya Kristo. Wayahudi walipewa fursa kuu ya kumfunua Mungu kwa wanadamu, lakini badala yake Walimficha. Wakristo wanaogombana na kuzoza-na, wakiyaleta mafundisho ya wanadamu katika mafundisho ya Mungu, hawamdhihirishi Mungu kwa washenzi lakini Wanamficha, wakiwageuza dhidi Yake. Wa namna hii hawawafanyi kuwa waongofu kwa Kristo ila wanazifukuza nafsi mbali kutoka Kwake. Lazima tuombe kwamba tufanye vyema zaidi; kwamba tusimfiche Kristo bali tumfunue Yeye katika kazi zetu zote na kupitia kwa maisha yetu. {1TG50: 14.3}

14

MAISHA NI KUMBE HUWA VILE SISI TUNAVYOYAFANYIZA

MATINI YA HOTUBA NA V. T. HOUTEFF

MCHUNGAJI WA WADAUDI WAADVENTISTA WA SABATO

SABATO, JULAI 19, 1947

HEKALU LA MLIMA KARMELI

WACO, TEXAS

Ili kujua kwamba maisha ni kumbe huwa vile sisi tunavyoyafanyiza, nitaleta kwa umakini mifano saba, kuanzia siku ya Nuhu na kumalizia katika siku yetu: {1TG50: 15.1}

Mfano Namba 1: Nuhu aliagizwa kujenga safina, na kuuambia ulimwengu kwamba gharika ingaliifunika dunia, kwamba wale tu ambao wangaliweza kuingia ndani ya safina wangaliweza kuokoka wakiwa hai. Miaka mia mo-ja na ishirini baadaye wanyama walionekana kwa kushangaza wakiandamana wawili wawili wakiingia ndani ya safina! Nuhu na familia yake pia waliingia ndani, ilhali wengine wa dunia walicheka na kumdhihaki. Lakini mvua ilipoanza kumiminika, hali ilikoma kuwa “ya ucheshi.” Waliokuwa nje ya safina walilia, wakaomboleza, na kusihi. Lakini wote waliangamia kama wapumbavu tu kwa sababu walikuwa wameshindwa kutii Ukweli wa sasa, walikuwa wameshindwa kula “chakula kwa wakati wake.” Upumbavu kama nini! Janga kama nini! {1TG50: 15.2}

Mtu angalifikiri kwamba baada ya gharika, ulimwengu ungalikuwa na heshima kubwa kwa dini na kwa manabii wa Mungu. Lakini haikuwa hivyo. Walioishi kabla ya gharika hawakuamini utabiri wa Nuhu kwamba mafuriko yangalikuwapo, kwa hivyo walikataa kuingia ndani ya safina! Lakini gharika ilikuja na wakangamia. Walioishi baada ya gharika hawakuamini utabiri wake kwamba hapangalikuwapo mafuriko mengine kwa hivyo walianza kujenga mnara wa Babeli! Lakini Mungu alipouona mnara ukijengwa kuelekea juu angani,

15

Yeye alikilipua kilele chake, na kuichafua lugha ya wajenzi. Yaani, Aliifuta lugha yao kutoka kwa akili zao na kutia ndani yao lugha za leo. Hivyo Alisababisha kuzaliwa kwa jamii na lugha mbali mbali ambazo sisi leo hu-pata hata sehemu za mashambani zaidi za dunia. {1TG50: 15.3}

Halikuwa kusudi la Mungu kwamba watu wajirundike katika nyanda za Shinari, ila kwamba waweze kuenea na kuijaza dunia. Na hivyo walipokataa kutii amri Yake aliwapatia ijayo bora zaidi Aliokuwa nayo kwa ajili yao, na kwamba walipaswa kutii. {1TG50: 16.1}

Kazi ya mwanadamu bila kumtegemea Mungu na kinyume chake, unaona hakika itakutana na janga. Nyumba iliyojengwa kwa mchanga haiwezi kustahimili dhoruba, na hakuna mtu anayeweza kushinda kusudi la Mungu kwa wanadamu. Usijipumbaze kwa kujaribu. {1TG50: 16.2}

Huchukua miaka katika shule za wanadamu kujifunza lugha, lakini katika shule ya Mungu, huchukua tu sekun-de. Anaweza kufuta lugha moja kutoka katika akili za mwanadamu na kutia ndani nyingine, na wakati huo huo abadilishe umbo la uso wake na rangi ya ngozi yake. Naam, Mungu anaweza kufanya haya yote haraka kuliko daktari wa meno anavyoweza kung’oa jino. Lakini ikiwa badiliko litafanywa kwa ajili ya ubora au ubaya, yote humtegemea mtu mwenyewe. {1TG50: 16.3}

Mfano Namba 2: Nebukadneza alipewa ndoto. Alipokwisha taabishwa nayo, aliwaita wenye hekima wa ufalme wake wamweleze tafsiri yake. Walikuja lakini hakuna kitu ambacho wangaliweza kufanya. Mwishowe, Danieli aliletwa mbele ya mfalme. Baada ya kusikia kisa cha ndoto ya mfalme, Danieli alisema: {1TG50: 16.4}

Dani. 4: 24-26, 28 — “Tafsiri yake ni hii, Ee mfalme, nayo ni amri yake Aliye juu, iliyomjia

16

bwana wangu, mfalme; ya kuwa utafukuzwa mbali na wanadamu, na makao yako yatakuwa pamoja na wanyama wa kondeni, nawe utalazimishwa kula majani kama ng’ombe, nawe utatiwa maji kwa umande wa mbinguni, na nyakati saba zitapita juu yako; hata utakapojua ya kuwa Aliye juu ndiye anayemiliki katika ufalme wa wanadamu, naye humpa yeye amtakaye, awaye yote. Na kwa kuwa waliamuru kukia-cha kisiki cha shina lake; ufalme wako utakuwa imara kwako, baada ya wewe kujua ya kuwa mbingu ndizo zinazotawala …. Hayo yote yakampata mfalme Nebukadneza”

Mfalme alisikia tafsiri yake, na akaelewa amri hiyo. Walakini hakuwa tayari kukubali kwamba alikuwapo Mmoja mkuu kuliko yeye. Kisha ikawa kwamba {1TG50: 17.1}

Dan. 4:29, 30 — “Baada ya miezi kumi na miwili, alikuwa akitembea ndani ya jumba la kifalme katika Babeli. Mfalme akanena, akasema, Mji huu sio Babeli mkubwa nilioujenga mimi, uwe kao langu la ki-falme, kwa uwezo wa nguvu zangu, ili uwe utukufu wa enzi yangu?”

Taarifa kama nini ya kufanya baada ya kusikia amri ya Mungu! Mfalme alikuwa bado ajifunze kwamba Mungu hutawala mataifa, huwasimamisha wafalme na kuwauzulu wafalme. Hebu tusikie sasa jibu la Mungu kwa upumbavu wa mfalme: {1TG50: 17.2}

Aya ya 31-33 — “Hata neno lile lilipokuwa katika kinywa cha mfalme, sauti ilikuja kutoka mbinguni, ikisema, Ee mfalme Nebukadneza, maneno haya unaambiwa wewe; Ufalme huu umeondoka kwako. Na-we utafukuzwa mbali na wanadamu, na makao yako yatakuwa pamoja na wanyama wa kondeni; utal-ishwa majani kama ng’ombe, na nyakati saba zitapita juu yako, hata utakapojua ya kuwa Aliye juu ndiye anayemiliki katika ufalme wa wanadamu, naye humpa

17

amtakaye, awaye yote. Saa iyo hiyo jambo hilo likatimizwa, likampata Nebukadneza; alifukuzwa mbali na wanadamu, akala majani kama ng’ombe, na mwili wake ulilowa maji kwa umande wa mbinguni, hata nywele zake zikakua, zikawa kama manyoya ya tai, na kucha zake kama kucha za ndege.”

Wengine hata hivi leo hawatambui kwamba Mungu hutawala, kwamba wanadamu hawako huru bila Kumtegemea ingawa wanaruhusiwa kuchagua iwapo watamtumikia Yeye au la. Haikuwa lazima kwa mfalme wa Wakaldayo kuishi na hayawani wa porini, lakini kwa vile hakuweza kujifunza somo lake kwa maneno, kwa njia rahisi, aliondolewa kutoka kwenye ikulu yake ya kifalme na kuwekwa kwenye mazizi, huko ili kujifunza kwa uzoefu, kwa njia ngumu. Mwishoni mwa miaka saba, baada ya kuhitimu, kwa mfano, kutoka shule ya Mungu ya mapigo magumu, mfalme alirudi ndani ya ikulu yake, akasema: {1TG50: 18.1}

Aya ya 34-37 — “Hata mwisho wa siku hizo, mimi, Nebukadneza, nikainua macho yangu kuelekea mbingu, fahamu zangu zikanirudia; nikamhimidi Yeye aliye juu, nikamsifu na kumheshimu Yeye aishiye milele; kwa maana mamlaka yake ni mamlaka ya milele, na ufalme wake hudumu toka kizazi hata kizazi; na watu wote wanaokaa duniani wamehesabiwa kuwa si kitu, naye hufanya kama atakavyo, katika jeshi la mbinguni, na katika hao wanaokaa duniani; wala hapana awezaye kuuzuia mkono wake, wala kumwu-liza, Unafanya nini wewe? Basi wakati uo huo fahamu zangu zikanirudia, na kwa ajili ya utukufu wa ufalme wangu, enzi yangu na fahari yangu zikanirudia; na mawaziri wangu, na madiwani wangu, wakaja kunitafuta; nami nikathibitika katika ufalme wangu, nikaongezewa enzi kupita kiasi. Basi mimi, Nebukadneza, namhimidi Mfalme wa mbinguni, namtukuza na kumheshimu; maana matendo yake yote ni kweli, na njia zake ni za adili; na wale waendao

18

kwa kutakabari, yeye aweza kuwadhili.”

Kupitia kiburi na ukosefu bwa uaminifu kwa Mungu Nebukadneza alifanya maisha kuwa mabaya kwake, lakini mwishowe alizinduka. {1TG50: 19.1}

Mfano Namba 3: Ufalme wa Nebukadneza uliendelea hadi utawala wa mjukuu wake, Belshaza. Belshaza alijua historia ya babu yake na uzoefu wake na Mungu, lakini alishindwa kufaidika nao. Alifanya karamu kubwa kwa mabwana zake elfu, na akaamuru kwamba vyombo ambavyo Nebukadneza alikuwa amevichukua kutoka Hekaluni huko Yerusalemu, viletwe kwenye karamu, ili mfalme mwenyewe, na wakuu, wake na masuria wake waweze kuvinywea. {1TG50: 19.2}

Mara tu sherehe hii ilipofanyika, vilitokea vidole vya mkono wa mtu, ambavyo viliandika kando ya kinara cha taa kwenye chokaa ya ukuta wa kasri la mfalme. Belshaza alifadhaika sana, na uso wake ukabadilika ndani mwake, na mabwana wake walishangaa. Basi Danieli akaletwa mbele ya mfalme. Na Danieli alitangaza kwa nguvu: {1TG50: 19.3}

Dan. 5: 18-31 — “Kwa habari zako, Ee mfalme, Mungu Aliye juu alimpa Nebukadreza, baba yako, ufal-me, na ukuu, na fahari, na utukufu; na kwa sababu ya ule ukuu aliompa, watu wa kabila zote, na ma-taifa, na lugha, wakatetemeka na kuogopa mbele yake; aliyetaka kumwua alimwua; na aliyetaka kumwa-cha hai, alimwacha hai; aliyetaka kumtukuza, alimtukuza; na aliyetaka kumshusha, alimshusha. Lakini moyo wake ulipoinuliwa, na roho yake ilipokuwa ngumu akatenda kwa kiburi, aliuzuliwa katika kiti chake cha enzi, nao wakamwondolea utukufu wake. Akafukuzwa mbali na wanadamu, moyo wake ukafanywa kuwa kama moyo wa mnyama, na makao yake yalikuwa pamoja na punda-mwitu; akalishwa majani kama ng’ombe, mwili wake ukalowa maji

19

kwa umande wa mbinguni; hata alipojua ya kuwa Mungu Aliye juu ndiye anayetawala katika ufalme wa wanadamu, na ya kuwa humweka juu yake yeye amtakaye, awaye yote. Na wewe, mwanawe, Ee Bel-shaza, hukujinyenyekeza moyo wako, ijapokuwa ulijua hayo yote. Bali umejiinua juu ya Bwana wa mbingu; nao wamevileta vyombo vya nyumba yake mbele yako; na wewe, na wakuu wako, na wake zako, na masuria wako, mmevinywea; nawe umeisifu miungu ya fedha na ya dhahabu na ya shaba, na ya chu-ma, na ya mti, na ya mawe; wasioona, wala kusikia, wala kujua neno lo lote; na Mungu yule, ambaye pumzi yako i mkononi mwake, na njia zako zote ni zake, hukumtukuza. Ndipo kile kitanga cha ule mkono kikaletwa kutoka mbele zake, na maandiko haya yameandikwa. Na maandiko yaliyoandikwa ni haya; MENE, MENE, TEKELI, NA PERESI. Na tafsiri ya maneno haya ni hii; MENE, Mungu ameuhesabu ufalme wako na kuukomesha. TEKELI, umepimwa katika mizani nawe umeonekana kuwa ume-punguka. PERESI, ufalme wako umegawanyika, nao wamepewa Wamedi na Waajemi. Ndipo Belshaza akatoa amri, nao wakamvika Danieli mavazi ya rangi ya zambarau, wakatia mkufu wa dhahabu shingoni mwake, wakapiga mbiu kutangaza habari zake, ya kwamba yeye ni mtu wa tatu katika ufalme. Usiku uo huo Belshaza, mfalme wa Wakaldayo, akauawa. Na Dario, Mmedi, akaupokea ufalme, naye umri wake alikuwa na miaka sitini na miwili.”

Je! Ingalikuwapo tofauti gani katika chuo cha historia ikiwa Belshaza angalikuwa amefaidika na somo la tha-mani ambalo babu yake alikuwa amejifunza. Naam, ni tofauti gani lingalikuwa limefanya! Hili ni somo muhimu kwa ajili yetu sote, wafalme na wakulima sawa. {1TG50: 20.1}

Mfano Namba 4: Ufalme wa Wakaldayo ukawa ufalme wa Wamedi na Waajemi, sio kwa sababu Wamedi na Waajemi walikuwa na nguvu na hodari zaidi, lakini kwa sababu

20

Mungu alikuwa ameamuru. Wacha tuone: {1TG50: 20.2}

Isa. 45: 1 — “Haya ndiyo Bwana amwambiayo Koreshi, masihi wake, ambaye nimemshika mkono wake wa kuume, ili kutiisha mataifa mbele yake, nami nitalegeza viuno vya wafalme; ili kufungua milango mbele yake, hata malango hayatafungwa.”

Koreshi, ambaye chini ya amri yake jeshi la Wamedi na Waajemi liliingia Babeli, alikuwa hajazaliwa wakati nabii Isaya aliandika kumhusu. Lakini Mungu alikumbuka ahadi Yake na wakati Belshaza alijihisi salama kabisa usiku ule wa sherehe na upotovu, Mungu alifungua mbele ya Koreshi malango yenye pande mbili na kuwezesha ku-tekwa kwa ufalme. Huko Wamedi na Waajemi walikutana na Danieli na wenzake, ambao waliuita usikivu wa Koreshi kwa Maandiko ambayo hayakutabiri tu ushindi wake, lakini hata yalibashiri jina lake. Baada ya kuona na kuhisi nguvu ya Mungu, Koreshi alichochewa kuamuru: {1TG50: 21.1}

Ezra 1: 2-11 — “Koreshi, mfalme wa Uajemi asema hivi; Basi kila mtu katika ninyi nyote mlio watu wake, Bwana, Mungu wake, na awe pamoja naye, na akwee mpaka Yerusalemu, ulioko Yuda, akaijenge nyumba ya Bwana, Mungu wa Israeli, (yeye ndiye Mungu), iliyoko Yerusalemu. Na mtu awaye yote aliye-salia mahali po pote akaapo hali ya ugeni, na asaidiwe na watu wa mahali pake, kwa fedha, na dhahabu, na mali, na wanyama, zaidi ya vitu vitolewavyo kwa hiari ya mtu, kwa ajili ya nyumba ya Mungu, iliyoko Yerusalemu. Ndipo wakaondoka wakuu wa mbari za mababa, wa Yuda na Benyamini, na makuhani, na Walawi, naam, watu wote ambao Mungu amewaamsha roho zao kukwea, ili kuijenga nyumba ya Bwana, iliyoko Yerusalemu. Na watu wote

21

waliokaa karibu nao pande zote wakawatia nguvu mikono yao, kwa vyombo vya fedha, kwa dhahabu, kwa mali, na kwa wanyama, na vitu vya thamani, zaidi ya vile vilivyotolewa kwa hiari ya mtu. Tena Kore-shi, mfalme, alivitoa vyombo vya nyumba ya Bwana, alivyokuwa amevileta Nebukadneza toka Yerusale-mu ,na kuvitia katika nyumba ya miungu yake. Naam, vyombo vile ndivyo alivyovitoa Koreshi, mfalme wa Uajemi, kwa mkono wa Mithredathi, mtunza hazina; naye akavihesabu mbele ya Sheshbaza, mkuu wa Yuda. Na hii ndiyo hesabu yake; sinia za dhahabu thelathini, sinia za fedha elfu, visu ishirini na ken-da. mabakuli ya dhahabu thelathini, mabakuli ya fedha ya namna ya pili mia nne na kumi, na vyombo vingine elfu. Vyombo vyote vya dhahabu na vya fedha vilikuwa jumla yake elfu tano na mia nne. Hivyo vyote Sheshbaza akakwea navyo, hapo walipokwea wale wa uhamisho kutoka Babeli mpaka Yerusale-mu.”

Sio vigumu kuona kwamba iwapo watawala wa milki ya Wamedi na Waajemi wangaliendelea kutawala katika roho ile ile kama ya Koreshi, ufalme huo ungalikuwa umesimama hadi leo. Ufalme huo, hata hivyo, ulitoa nafasi kwa Uyunani; Uyunani, kwa Rumi; na Rumi, kwa mataifa ya leo. Ni dhahiri kabisa kuona kwamba falme za leo bado zinasimama kwa sababu Mungu amekusudia hivyo. {1TG50: 22.1}

Kuendelea kwao zaidi na zaidi bila kumtegemea Mungu punde au baadaye kutaleta mwisho wao pia, kwa kuta-zama chini ya mkondo wa wakati, chini hadi kwa falme za leo ambazo zinaonyeshwa kwa nyayo na vidole vya sanamu kubwa, Roho wa Kweli aliandika: “Na kama vile ulivyoziona hizo nyayo za miguu na vidole vyake, ku-wa nusu udongo wa mfinyanzi, na nusu chuma, ufalme ule utakuwa ufalme uliogawanyika; lakini ndani yake zitakuwako nguvu za chuma, kama vile ulivyoona kile chuma kimechanganyika na udongo wa matope. Na kama vidole vya zile nyayo vilikuwa nusu chuma na nusu udongo, kadhalika ufalme ule utakuwa nusu yake una nguvu,

22

na nusu yake umevunjika. Na kama vile ulivyokiona kile chuma kimechanganyika na udongo wa matope, wa-tajichanganya nafsi zao kwa mbegu za wanadamu; lakini hawatashikamana, kama vile chuma kisivyoshikamana na udongo. Na katika siku za wafalme hao Mungu wa mbinguni atausimamisha ufalme ambao hautaangamizwa milele, wala watu wengine hawataachiwa enzi yake; bali utavunja falme hizi zote vipande vipande na kuziha-ribu, nao utasimama milele na milele. Na kama vile ulivyoona ya kuwa jiwe lilichongwa mlimani bila kazi ya mikono, na ya kuwa lilivunja-vunja kile chuma, na ile shaba na ule udongo, na ile fedha, na ile dhahabu; basi Mungu aliye mkuu amemjulisha mfalme mambo yatakayokuwa baadaye; na ndoto hii ni ya hakika, na tafsiri yake ni thabiti.” Dan. 2: 41-45. Badala ya kujiunganisha kwa Ufalme wa Mungu, zitalazimika kuangamizwa. {1TG50: 22.2}

Mfano Namba 5: Sasa hebu tuone ni faida gani falme na mataifa yalivuna kutokana na kukutana na kanisa. Babeli, Umedi-Uajemi, Uyunani, na Rumi, ambazo zilikutana na kanisa, hujumuisha ulimwengu uliostaarabika wa leo. {1TG50: 23.1}

Tazama mataifa na watu (wapagani katika sehemu tengwa za dunia) ambao hawakuwa na bahati nzuri ya kuku-tana na kanisa mapema kama mataifa mengine. {1TG50: 23.2}

Bado zaidi, angalia wale ambao bado wametengwa zaidi katika sehemu za mbali zaidi za dunia ambao ha-wajakutana na kanisa, sio hadi hivi majuzi tu. Wengi wao ni bora kidogo kuliko wanyama sio kwa akili tu ila hata katika ustawi. {1TG50: 23.3}

Watu ambao walikuwa na bahati sana kuwa karibu zaidi na dini ya Kristo, ni, utapata,

23

wenye busara zaidi, waliofanikiwa zaidi. Uingereza, kwa mfano, ambayo ilitafsiri Bibilia na kuichapisha na kui-eneza kote ulimwenguni kwa watu na lugha zote, ilikuwa kuu zaidi kati ya mataifa kwa wakati wake. Kisha Ma-rekani (lakini taifa umbu kwa Milki ya Uingereza), ambayo chini ya karne mbili zilizopita ilianzisha utawala wake kwa kanuni za Bibilia na kuandika kwa dola yake, KATIKA MUNGU TUNAAMINI, na ambayo pia ali-anzisha Jumuiya za Bibilia za Marekani, ni kwa ulinganifu miaka michache ikawa kuu zaidi ya mataifa, kama walivyokuwa Waebrania katika siku yao. {1TG50: 23.4}

Kwa upande mwingine wale ambao waliasi dini ya Bibilia, waliachwa ukiwa — baraka zao zikawa laana kwao. Wayahudi waliochukiwa, ambao hawana eneo duniani, ni mfano bora. Ujerumani, ambayo iliongoza katika Matengenezo lakini ikakengeuka kwayo, imevuna mavuno ya majonzi, pia. {1TG50: 24.1}

Na kile ambacho ni kweli kwa mataifa, bila shaka, ni kweli hasa kwa watu binafsi, maskani, familia, na jamii. {1TG50: 24.2}

Ikiwa utachukua muda mchache kuangalia, utaiona sheria hii ya baraka na laana katika wonyesho kila mahali bila ubaguzi. {1TG50: 24.3}

Ulimwengu ulianzishwa juu ya dini, na unaweza kutulia umehakikishiwa kwamba wakati dini itatoweka duni-ani, dunia itatoweka pamoja nayo. Wale ambao wanakuwa wapenzi na Ukweli watapata kuwa baraka, vivyo hivyo, zitakuwa wapenzi nao. Hebu tusome: {1TG50: 24.4}

2 Thes. 2: 8-12 — “Hapo ndipo atakapofunuliwa yule asi, ambaye Bwana Yesu atamwua kwa

24

pumzi ya kinywa chake, na kumwangamiza kwa ufunuo wa kuwapo kwake; yule ambaye kuja kwake ni kwa mfano wa kutenda kwake Shetani, kwa uwezo wote, na ishara na ajabu za uongo; na katika madanganyo yote ya udhalimu kwa hao wanaopotea; kwa sababu hawakukubali kuipenda ile kweli, wapate kuokolewa. Kwa hiyo Mungu awaletea nguvu ya upotevu, wauamini uongo; ili wahukumiwe wote ambao hawakuiamini kweli, bali walikuwa wakijifurahisha katika udhalimu.”

Tunaona kwamba ikiwa hatuwezi kuwa wapenzi na Ukweli, udanganyifu hauwezi kuepukika. La, hakuna yeyote hudanganywa kwa kukutana na uongo (kwa maana tumekutana nao hata hivyo tangu wakati tunapoza-liwa hadi wakati tunapokufa), ila kila mtu asiyependa Ukweli ni hakika atadanganywa, bila kujali atakachoweza kufanya ili Kuuepuka. {1TG50: 25.1}

Na wale ambao wameridhika kwa Ukweli wa jana, ambao hawautafuti Ukweli mpya kwa ajili ya leo kutoka kwenye kiti cha enzi cha Mungu, hawatafuti “chakula kwa wakati wake,” – watu kama hao watajikuta katika shida ya kutisha kama walivyofanya Wayahudi – kutapikwa nje. {1TG50: 25.2}

Kumbukumbu la Torati 30:15, 19 — “Angalia, nimekuwekea leo mbele yako uzima na mema, na mauti na mabaya; … Nazishuhudiza mbingu na nchi juu yenu hivi leo, kuwa nimekuwekea mbele yako uzima na mauti, baraka na laana; basi chagua uzima, ili uwe hai, wewe na uzao wako.”

Mfano Namba 6: Iwapo tutashindwa kufaidika kwa yale Mungu hutuambia tutashindwa vibaya kama, ikiwa sio vibaya zaidi, kama wale wote ambao wameshindwa kabla yetu. Nafikiri baadhi yenu ambao wamekutana kibin-afsi na Mungu, wanayajua mambo haya kupitia uzoefu wao wenyewe. Bila shaka mmegundua kwamba hamwe-zi kuzuia mlipuko kwa muda mrefu

25

wakati mnaendelea kuweka moto na baruti katika chumba kimoja; ya kuwa humwezi kumtumikia Ibilisi na bado muwe na amani na usalama. Acha nifafanue kwa tukio halisi: {1TG50: 25.3}

Mtu fulani aliota kwamba farasi alimwua kwa kumpiga teke. Ili kukinga maisha yake daima alikaa mbali na fara-si wote. Walakini siku moja yenye upepo alipokuwa akitembea barabarani, akapita penye kibanda cha mhunzi ambacho mbele yake kilikuwa kikining’inia ishara ya chuma cha kwato za farasi zimechorwa juu yake. Ishara ghafla ilianguka kichwani mwake na akafa kutokana na kipigo hicho. {1TG50: 26.1}

Hatuwezi kuendelea kuyaepuka matokeo ya dhambi na ya kutengwa na Mungu, kuliko vile yule muota ndoto angaliepuka kifo kwa kukikwepa. Hatujui kamwe ni nini siku itazalisha, na hatuwezi kumudu kujitenga na Mun-gu hata kwa nukta. Wala hatuwezi kusema bayana kwamba tutaweza au hatutaweza kufanya hili, lile, au lingine. {1TG50: 26.2}

Mfano Naamba 7: Miaka kadhaa iliyopita nilipokuwa Uropa, nalisikia kwamba mmoja wa binamu zangu alikuwa ameondoka kwenda Marekani. Kisha nikanena moyoni, “Masikini binamu, sitaondoka nyumbani kamwe na kwenda kuishi popote mbali kama Marekani kwa sababu yoyote.” Lakini karibu na wakati huo, mimi, pamoja na wengine, tulituhumiwa isivyo kweli kwa njama. Ilikuwa katika msimu ambao usiku ulikuwa mrefu, na tu-lipowasha taa kwenye duka letu asubuhi moja kabla maawio, umati wa watu ulikusanyika ukiwa na bunduki na mawe, na kuyapiga madirisha. Hivyo ilikuwa kwamba miezi michache tu baada ya kusikitikia kujitenga kwa maskini binamu yangu kutoka katika nchi yake nilijikuta nikiwa Marekani katika nyumba moja naye. Ilikuwa kuvunjika moyo mwanzoni, la sio kidogo kuliko Yusufu wa zamani, ila ilikuwa fadhili kama nini mwishowe! Mungu ubariki umati! {1TG50: 26.3}

26

Mungu tu ndiye ajuaye siku za baadaye, na tunapaswa kuweka matumaini na matarajio yetu katika mkono Wake hodari. Kisha, na wakati huo tu, tutakuja “juu.” Na ikiwa tumejaribiwa kusema tutafanya au kutofanya hili au lile, basi tumkumbuke Yona: Alisema hatautangaza ujumbe kwa Ninawi, na mara akachukua mashua kwenda Tarshishi. Lakini wenye mashua wakamtupa baharini na samaki mkubwa akamchukua na kumrudisha mahali hapo alipokuwa akijaribu kukimbia. {1TG50: 27.1}

Nebukadneza, mfalme wa Babeli, alifikiria kuudumisha ufalme wake kwa kuwaamuru raia wake wote waisuju-die sanamu yake ya dhahabu. Waebrania watatu, hata hivyo, walikataa kusudi lake na wakabadilisha mkondo wa historia. Wanaume ambao waliwatupa Waebrania katika tanuru ya moto wenyewe walichomwa wakafa, ila hakuna uywele wa vichwa vya Waebrania ulichomeka wakati wote walikuwa ndani ya tanuru la moto. Hebu sisi pamoja na Mtunga Zaburi tuinue sauti zetu na kusema: {1TG50: 27.2}

Zaburi 8: 1-6 — “Wewe, MUNGU, Bwana wetu Jinsi lilivyo tukufu jina lako duniani mwote! Wewe umeuweka utukufu wako mbinguni; Vinywani mwa watoto wachanga na wanyonyao Umeiweka misingi ya nguvu; Kwa sababu yao wanaoshindana nawe; Uwakomeshe adui na mijilipiza kisasi. Nikiziangalia mbingu zako, kazi ya vidole vyako, Mwezi na nyota ulizoziratibisha; Mtu ni kitu gani hata umkumbuke, Na binadamu hata umwangalie? Umemfanya mdogo punde kuliko malaika; Umemvika taji ya utukufu na heshima; Umemtawaza juu ya kazi za mikono yako; Umevitia vitu vyote chini ya miguu yake.”

Nabii Malaki aliagizwa aandike kwa ajili ya watu ambao wangaliishi katika wakati wa mwisho. {1TG50: 27.3}

27

Hebu tusome kutoka katika sura ya nne: {1TG50: 28.1}

Mal. 4: 1-3 — “Kwa maana, angalieni, siku ile inakuja, inawaka kama tanuru; na watu wote wenye kiburi, nao wote watendao uovu, watakuwa makapi; na siku ile inayokuja itawateketeza, asema Bwana wa majeshi; hata haitawaachia shina wala tawi. Lakini kwenu ninyi mnaolicha jina langu, jua la haki lita-wazukia, lenye kuponya katika mbawa zake; nanyi mtatoka nje, na kucheza-cheza kama ndama wa maz-izini. Nanyi mtawakanyaga waovu; maana watakuwa majivu chini ya nyayo za miguu yenu; katika siku ile niifanyayo, asema Bwana wa majeshi.”

Je! Sio bora kuwa mwanadamu kwa mpangilio wa Mungu, kiumbe mzuri anayeishi daima, kuliko kuwa majivu chini ya nyayo za watakatifu? Je! Kwa nini usiitike mwito Wake na kuyafanyiza maisha yawe ambayo yana-paswa kuwa? {1TG50: 28.2}

Aya ya 4-6 — “Ikumbukeni torati ya Musa, mtumishi wangu, niliyomwamuru huko Horebu kwa ajili ya Israeli wote, naam, amri na hukumu. Angalieni, nitawapelekea Eliya nabii, kabla haijaja siku ile ya Bwa-na, iliyo kuu na kuogofya. Naye ataigeuza mioyo ya baba iwaelekee watoto wao, na mioyo ya watoto iwaelekee baba zao, ili nisije nikaipiga dunia kwa laana.”

Je! Unangojea, unakesha, unaomba na kutarajia kwamba wakati huyu wa uakisi nabii Eliya atakapoonekana na kukuita, moyo wako uwaelekee watoto wako na mioyo yao ikuelekee wewe, au unatambaa chini ya ganda lako, kwa mfano, kwa kuogopa kwamba utadanganywa iwapo unaweza kukutana naye? {1TG50: 28.3}

Maisha, unaona, ni kumbe unavyoyafanyiza. Watu wengi hawajui jinsi ya kuyafanya yawe bora, lakini “ikiwa mnayajua mambo haya, mna heri ninyi mkiyatenda.” {1TG50: 28.4}

28

Kufanya muhtasari wa uchambuzi huu: Tumejifunza kwamba tumewekwa katika ulimwengu huu kwa kusudi, kwamba ikiwa tunataka wokovu na baraka lazima tushirikiane na Mungu. Hili tunaweza kufanya kwa kuifuata mifano ya watu wenye njaa ya Ukweli wa Mungu. Ili kutuwezesha kufanya hili Yeye amehakikisha kwamba utukufu na majanga ya madaraja yote mawili yamenakiliwa katika Kitabu Chake. {1TG50: 29.1}

Iwapo tutalinganisha kazi zetu na kazi za Nuhu tutaona ikiwa tunapatana naye katika kutii Ukweli wa sasa. La walioishi kabla wala baada ya gharika hawakufaidika na mahubiri ya Nuhu. Wa awali hawakuamini ingaliweze-kana kuigharikisha nchi na wakaangamia; wa mwisho hawakuamini ingaliwezekana kwa dunia isigharikishwe tena. Waliujenga mnara wa Babeli kwa sababu waliogopa mafuriko mengine ingawa waliambiwa wazi wazi kwamba hakutakuwa na mafuriko kama hayo tena. Mungu, hata hivyo, hakuangamiza kazi yao tu, lakini pia aliichanganya lugha yao, na badala yake akawapa lugha zote tofauti ili wachache waweze kuelewana. Ikiwa tutafanya kazi kuitimiza mipango ya Mungu kwa ajili yetu kamwe hatutachanganyikiwa au kufedheheshwa. {1TG50: 29.2}

Nebukadneza, mfalme wa Babeli mwishowe aliona mambo haya kama ambavyo Mungu huyaona, lakini kwa njia ngumu — sio kabla ya Mungu kumfanya huru kwa miaka saba akila nyasi kama ng’ombe. Baadaye ali-pojifahamu mwenyewe, alimtambua Mungu kama Mungu Anayetawala mbingu na nchi. Hebu tufanye vyema kuliko alivyofanya Mfalme. {1TG50: 29.3}

Kisha Belshaza, mfalme ambaye alishindwa kufaidi kutokana na uzoefu wa Nebukadneza, usiku mmoja alijipo-teza, ufalme wake na yote yake. {1TG50: 29.4}

Mtawala alimfuata mtawala na mwishowe ufalme ukapishwa kwa Wamedi–Waajemi, kisha kwa Wayunani, ijayo kwa Warumi na mwishowe kwa mataifa ya leo.

29

Mataifa, unaona, ni ya Mungu, na Yeye huyaacha yatawaliwe na Yeyote Amtakaye. {1TG50: 29.5}

Mataifa ambayo yalikuja karibu kwa Mungu na mafundisho Yake yakawa mataifa makuu na yenye kuheshimi-wa, na yale ambao yalijiweka mbali kutoka Kwake sio bora zaidi kuliko wanyama. {1TG50: 30.1}

Ni bora kujifunza kile Mungu anataka ufanye, basi fanya tu hivyo. Maisha kwa kweli ni kumbe huwa vile tuna-vyoyafanyiza — sio pungufu na sio zaidi. Sasa ni nafasi yako, sasa u kwenye nji panda mbili. Itakuwa ni ipi kwa ajili yako? Pana, au nyembamba, ipi? {1TG50: 30.2}

-0-0-0-0-0-

Ili kuleta furaha hii isiyoneneka ya ahadi za Mungu, tarajio la vizazi, masomo haya yanachapishwa na kutumwa bila malipo au wajibu kwa wote wanaotaka kuwa nayo. Tuma jina na anwani yako kwa Shirika la Uchapishaji la Ulimwengu, Kituo cha Mlima Karmeli, Waco, Texas. {1TG50: 30.3}

*******

Wakati ambapo unaagiza nakala za ziada za “Trakti za Vuli,” tafadhali bainisha gombo na namba ya somo bada-la ya tarehe au jina. Hili litawezesha kuingiza agizo lako bila kukawia. {1TG50: 30.4}

30

Zawadi za Mungu

Zawadi Zake ni kubwa kuliko ndoto zangu,

Zawadi za Mungu kwangu;

Zisizohesabika kama mihimili ya dhahabu ya jua linapotua,

Isiyo na mwisho kama bahari.

Huomba sehemu, Yeye hutoa zote–

Mwenyewe, na yote kando;

Fadhili Zake hufurika nafsi yangu,

Zikiingia ndani kama wimbi.

Ndani ya moyo wangu Atapata nafasi

Kumiliki na kutawala upeo;

Sauti yangu Itamsifu milele kwa neema hiyo

Ambayo siwezi kamwe kuota.

Zawadi zake ni kubwa kuliko ndoto zangu,

Zawadi zake Yeye aliyeniweka huru;

Zaidi na zaidi tele kila siku huonekana

Neema ya Mungu kwangu.

—J. B. Pound

31

Jumuiya ya Wadaudi Waadventista wa Sabato

(Ushirika Huru Unaojumuisha Kanisa)

Mlima Karmeli, Waco, Texas

S.L.P. 23738, Waco, TX 76702

+ 1-254-855-9539

www.gadsda.com

info@gadsda.com

Gombo la 1, Namba 49, 50

Kimechapishwa nchini Marekani

32

>