fbpx

Gombo la 1 Salamu Mwafaka Namba 46, 47, 48

Gombo la 1 Salamu Mwafaka Namba 46, 47, 48

                                    

AMANI YA PEKEE YA MAWAZO

Hati miliki, Kimechapishwa tena 1953

Haki zote zimehifadhiwa

V. T. HOUTEFF

                                    

WATUMWA WA MUNGU KATIKA WAKATI WA KUKUSANYA

TAABU YA YAKOBO; YUDA NA ISRAELI WAENDA NYUMBANI

CHETI CHA MUNGU KUFUFUA, KUTAKASA, NA KUWAUNGANISHA YUDA NA ISRAELI

                                    

1

ANDIKO LA SALA

Kuwekwa Juu Ya Mwamba

Nitasoma kutoka “Mlima wa Baraka,” kuanzia ukurasa wa 211 — {1TG46: 2.1}

“Watu walikuwa wamevutiwa sana na maneno ya Kristo …. Maneno Yake yalikuwa yamegonga haswa kwenye mzizi wa itikadi na maoni yao ya zamani; kutii mafundisho Yake kungalihitaji badiliko katika tabia zao zote za mawazo na vitendo. Lingaliwaleta katika mgongano na waalimu wao wa kidini …. “ {1TG46: 2.2}

Kwa sababu mafundisho ya Kristo huhitaji badiliko la mawazo na vitendo, hatupaswi kushangazwa ikiwa hivyo ndivyo ujumbe Wake wa leo utataka kutoka kwetu. Wacha tuhitimishe usomaji wa leo kwa kufungua ukurasa wa 216. {1TG46: 2.3}

“… Yeye ambaye, kama Wayahudi katika siku ya Kristo, hujenga kwa msingi wa mawazo na dhana za mwana-damu, wa aina na sherehe za uvumbuzi wa mwanadamu, au juu ya kazi zozote ambazo anaweza kuzifanya huru kutoka kwa neema ya Kristo, anaijenga jengo la tabia kwenye mchanga unaohamishwa. Tufani kali za majaribu zitaufagilia mbali msingi wa mchanga, na kuiacha nyumba yake ikiwa gofu kwenye pwani ya wakati.” {1TG46: 2.4}

Hebu tuombe ili Mungu atusaidie kuhakikisha kwamba msingi wa imani yetu umejengwa juu ya Neno la Mungu, Mwamba thabiti; ili tuweze kujua kwamba kitu chochote pungufu kwalo kitaanguka upesi au baadaye; kwamba tumruhusu Bwana apate njia Yake ndani yetu; kwamba tumruhusu Yeye azibadilishe tabia na mazoea yetu kutoka kwa yalivyo hadi yanavyotakikana yawe. {1TG46: 2.5}

2

WATUMWA WA MUNGU KATIKA WAKATI WA KUKUSANYWA

MATINI YA HOTUBA NA V. T. HOUTEFF

MCHUNGAJI WA WADAUDI WAADVENTISTA WA SABATO

SABATO, JUNI 21, 1947

HEKALU LA MLIMA KARMELI

WACO, TEXAS

Tunaichambua sura ya arobaini na tisa ya Isaya. Sura hii inawaonyesha watumwa wa Mungu katika wakati wa kukusanywa, nasaba yao ya kijamaa, na hitaji lao la upanuzi wa mpaka. Tutaanza uchambuzi na aya tatu za kwanza. {1TG46: 3.1}

Isa. 49: 1-3 — “Nisikilizeni, enyi visiwa; tegeni masikio yenu, enyi kabila za watu mlio mbali sana; Bwana ameniita tangu tumboni; toka tumbo la mama yangu amenitaja jina langu. Naye anifanya kinywa changu kuwa kama upanga mkali; katika kivuli cha mkono wake amenisitiri; naye amenifanya kuwa mshale ulio-suguliwa; katika podo lake amenificha; akaniambia; Wewe u mtumishi wangu, Israeli, ambaye katika wewe nitatukuzwa.”

Roho wa Mungu ndani ya kiwiliwili cha Israeli, kupitia nabii Isaya anatangaza kwamba Israeli alizaliwa sio kwa sababu nyingine isipokuwa kuwa mtumwa wa Mungu, na husisitiza kwamba ukweli huu lazima sasa ufanywe kujulikana kote duniani, hata kwenye visiwa vya bahari. {1TG46: 3.2}

Kwa kuwa Yakobo mwenyewe alikuwa amekufa muda mrefu kabla ya nabii Isaya kuandika, ukweli unasimama wazi kwamba Roho wa Mungu katika andiko hili anasema, sio binafsi kwa Yakobo mwenyewe, ila kwa uzao wake, kwa wale ambao Ukweli huu umefanywa ujulikane na ambao sasa wanalibeba

3

jukumu la Kuutangaza kote kote; Ni wazi, basi, watu ambao Bwana atatukuzwa ndani yao, na ambao wanam-leta tena Yakobo Kwake (Isa. 49: 3, 5) ni wao wenyewe, pia, ili kufanywa wajulikane kimataifa. Wao ni wale ambao wanaikamilisha kazi ya injili — wa mwisho kabisa. Kwa wao Bwana anawapatia kinywa kama upanga mkali. {1TG46: 3.3}

Hawa watakuwa watumwa Wake wakati wa kuwakusanya watu, katika siku ambayo Bwana anatukuzwa. Ku-fichwa kwao, kwa mfano, katika podo Lake, kunaashiria kwamba kuja kwao kuwa maarufu kutakuwa mshangao kamili kwa wote: Kwa mara ya kwanza ulimwengu utajifunza kwamba hawa watumwa wa Mungu ndio wa mwisho kabisa wa uzao wa Yakobo, watumwa Wake waliofichwa, wale ambao watawakusanya watu Wake hata kutoka katika visiwa vya bahari. {1TG46: 4.1}

Tena imeandikwa – “Katika kazi ya uchaji ya mwisho watu wakuu wachache watahusishwa. Wamejitosheleza kwa ubinafsi, hawamtegemei Mungu, na hawezi kuwatumia. Bwana anao watumwa waaminifu, ambao katika wakati wa mtikiso, wa kupimwa watafunuliwa waonekane. Wapo sasa wa thamani sana waliofichwa ambao hawajamsujudia Baali. Hawajakuwa na nuru ambayo imekuwa ikiangaza kwa mng’ao thabiti juu yenu. Lakini, inaweza kuwa chini ya hali ngumu isiyopendeza ya nje ambapo waangavu wa tabia halisi ya Kikristo itafunu-liwa.” —”Shuhuda,” Gombo la 5, uk. 80, 81. {1TG46: 4.2}

Aya ya 4 — “Lakini nikasema, Nimejitaabisha bure, nimetumia nguvu zangu bure bila faida; lakini hakika hukumu yangu ina Bwana, na thawabu yangu ina Mungu wangu.”

Mwanzoni mwa kazi yao matokeo lazima yawe kama ya kuleta karibu kuvunjika moyo kabisa.

4

Wao hata hivyo wanajua kwamba wameteuliwa na Mungu, na kwa hivyo wanaacha hukumu yao, kazi yao na mafanikio yao pamoja Naye. {1TG46: 4.3}

Aya ya 5 — “Na sasa Bwana asema hivi, yeye aliyeniumba tangu tumboni niwe mtumishi wake, ili nimletee Yakobo tena, ingawa Israeli hawajakusanywa, bado mimi nitapata heshima mbele ya macho ya Bwana, na Mungu wangu atakuwa nguvu zangu.”

Kwa ajili ya wao kutiwa moyo wanaambiwa kwamba ingawa Israeli hajakusanywa (atakusanywa, hata hivyo), lakini watapata heshima machoni pa Bwana, na Bwana Mungu atakuwa nguvu yao. Kwa sababu sasa wako (sio kwa wakati mwingine ila katika siku ambayo unabii huu unatimizwa) wameitwa kumletea tena Bwana Yakobo, inaonyesha kwamba Yakobo (watu wa Mungu katika hali yao ya Uyakobo) lazima wawe walimwacha Bwana. Sasa lazima warudishwe Kwake kwa njia ya uamsho na matengenezo makuu. {1TG46: 5.1}

Aya ya 6 — “Naam, akasema hivi, Ni neno dogo sana wewe kuwa mtumishi wangu ili kuziinua kabila za Yakobo, na kuwarejeza watu wa Israeli waliohifadhiwa; zaidi ya hayo nitakutoa uwe nuru ya mataifa, upate kuwa wokovu wangu hata miisho ya dunia.”

Andiko hili lilikuwa na mfano wake wakati ambapo Mitume waliagizwa hatimaye kuhubiri injili kwa Mataifa na kwa Wayahudi. Sasa kuziinua kabila za Yakobo, ni kwanza kuwainua malimbuko, 144,000 — 12,000 kutoka katika kila kabila za Israeli (Ufu. 7: 3). Zaidi ya hayo, kuwa nuru na wokovu hadi miisho ya dunia, humaanisha kwamba hawa watumwa wa siku za mwisho wa Mungu wataikamilisha kazi ya injili, watahubiri injili ya Ufalme katika ulimwengu wote kuwa ushuhuda kwa mataifa yote, na hivyo kuuleta mwisho (Mat. 24:14). {1TG46: 5.2}

Ni haki yetu, kwa hivyo, sio tu kuleta nuru ya Mungu kwa Dhehebu ambamo “malimbuko” (watu 144,000 – Ufu. 14: 4) ya mavuno makubwa ya kiroho yapo, lakini hata kuleta nuru ile ile kwa mavuno ya pili, kwa umati mkubwa ambao unakusanywa kutoka mataifa yote, umati ambao hakuna mtu awezaye kuuhesabu (Ufu. 7: 9). {1TG46: 6.1}

5

Wale ambao wamepewa haki hivyo ni, jinsi Mungu mwenyewe anavyoshuhudia, wazawa wa Yakobo, “kabila zilizopotea za Israeli” ambao sasa wanakuja kwenye mwanga. {1TG46: 6.2}

Aya ya 7 — “Bwana, mkombozi wa Israeli, Mtakatifu wake, amwambia hivi yeye anayedharauliwa na wanadamu; yeye anayechukiwa na taifa hili; yeye aliye mtumishi wao watawalao; Wafalme wataona, wa-tasimama; wakuu nao watasujudu; kwa sababu ya Bwana aliye mwaminifu, Mtakatifu wa Israeli ali-yekuchagua.”

Bwana anaonekana hapa akinena kwa watu ambao watu huwadharau, kwa wao ambao taifa linawachukia, kwa watumwa wa watawala – kwa walei, sio wachungaji wanaotambuliwa na Dhehebu. Mtumwa huyu wa Bwana, Andiko lasema wazi, amedharauliwa na kuchukiwa kama vile Bwana Mwenyewe. Chuki, basi, ambayo imerun-dikwa juu yetu na ndugu zetu Walaodekia, sio lazima iwe ya kutuvunja moyo, ila badala yake ya kutia moyo sana. Na kwa Nini? — Kwa sababu Roho wa Bwana Mwenyewe anashuhudia ya kuwa sisi ni watumwa wa Mungu kwa wakati huu, kwamba ataibariki kazi yetu sana ya kuwa hata wafalme wataona kuinuka kwetu na wakuu pia watakuja na kuabudu. {1TG46: 6.3}

Aya ya 8 — “Bwana asema hivi, Wakati uliokubalika nimekujibu, na siku ya wokovu nimekusaidia; nami nitakuhifadhi, nitakutoa uwe

6

agano la watu hawa, ili kuiinua nchi hii, na kuwarithisha urithi uliokuwa ukiwa.”

Mungu ametusikia katika wakati wa rehema, katika wakati ambao tunaweza kutiwa muhuri na kuhifadhiwa ku-wa agano la watu, kuianzisha nchi, kurithi urithi uliokuwa ukiwa – kuyarejesha mambo yote. {1TG46: 7.1}

Aya ya 9 — “Kuwaambia waliofungwa, Haya, tokeni; na hao walio katika giza, Jionyesheni. Watajilisha katika njia, na juu ya majabali watapata malisho.”

Haijalishi ni wapi watu wa Mungu walipo, au chini ya hali gani watakayowekwa, hata hivyo wote watasikia wa-tumwa Wake wakitangaza mwaka wa Yubile ya mwisho, na wote wataachwa huru, wote watashiriki sikukuu hii ya kiroho inayoongezeka daima. {1TG46: 7.2}

Aya ya 10, 11 — “Hawataona njaa, wala hawataona kiu; hari haitawapiga, wala jua; kwa maana yeye ali-yewarehemu atawatangulia, naam, karibu na chemchemi za maji atawaongoza. Nami nitafanya milima yangu yote kuwa njia, na njia kuu zangu zitatukuzwa zote.”

Bwana hapa anahakikisha kwamba sasa katika wakati wa kukusanywa hakutakuwa na kizuizi cha aina yoy-ote, kwamba Yeye ndiye Bwana wa hali hiyo. {1TG46: 7.3}

Aya ya 12 — “Tazama, hawa watakuja kutoka mbali; na tazama, hawa kutoka kaskazini, na kutoka ma-gharibi, na hawa kutoka nchi ya Sinimu.”

Njia kuu ya Mungu itajazwa na kuinuliwa, na umati wa watu, ambao wamekusanywa kutoka pembe nne za dunia, watatembea kwa usalama ndani yake. {1TG46: 7.4}

7

Aya ya 13 — “Imbeni, enyi mbingu; ufurahi, Ee nchi; Pazeni sauti ya kuimba, enyi milima; Kwa kuwa Bwana amewafariji watu wake, Naye atawahurumia watu wake walioteswa.”

Sio kwamba Bwana atawafariji watu Wake, ila kwamba tayari Amewafariji, Yeye amewajaza Ukweli. {1TG46: 8.1}

Aya ya 14 — “Bali Zayuni alisema, Bwana ameniacha, Bwana amenisahau.”

Kabla hawajatiwa muhuri, wale ambao watakuwa wenyeji wa Zayuni (watu 144,000) wanafikiria Mungu ame-waacha. Jibu la Mungu kwao, hata hivyo, ni hili: {1TG46: 8.2}

Aya ya 15 — “Je! Mwanamke aweza kumsahau mtoto wake anyonyaye, hata asimhurumie mwana wa tumbo lake? Naam, hawa waweza kusahau, lakini mimi sitakusahau wewe.”

Hata ingawa baadhi, badala ya kuomba kwa ajili ya kuusimamisha upya Zayuni, kwa kweli wanaomba dhidi yake, hata hivyo wao, pia, watagundua punde kuwa Mungu yu kwa ajili yake kabisa. {1TG46: 8.3}

Aya ya 16 — “Tazama, nimekuchora katika vitanga vya mikono yangu; kuta zako ziko mbele zangu dai-ma.”

Kutoka kwa mandhari yote ya asili inaonekana kwamba Mungu ameusahau Zayuni, mahali pa kiti Chake cha enzi cha duniani; ya kwamba Yeye amewaacha maadui Zake kuwanyanyasa watu Wake na kuuharibu mlima ulioinuliwa wa Zayuni, ila Bwana Mwenyewe huhakikishia kwamba kwa ajili ya Zayuni na kwa ajili ya uhuru wa watu Wake, Alitundikwa msalabani. {1TG46: 8.4}

Aya ya 17 — “Watoto wako wafanya haraka, hao wakuharibuo,

8

nao waliokufanya ukiwa, watatoka kwako.”

Watoto wa Zayuni watakuwa na hamu ya kufika kwake, lakini maadui zake, wadhambi watafukuzwa mbali kutoka kwake. {1TG46: 9.1}

Aya ya 18, 19 — “Inua macho yako, tazama pande zote; hao wote wanajikusanya na kukujia. Kama niishivyo, asema Bwana, hakika utajivika na hao wote, kama kwa uzuri, nawe utajifungia hao, kama bibi arusi. Maana katika habari za mahali pako palipokuwa ukiwa, pasipokaliwa na watu, na nchi yako iliyo-haribika hakika sasa utakuwa mwembamba usiwatoshe wenyeji wako, nao waliokumeza watakuwa mba-li.”

Neno “tazama” yanavuta uangalifu kwa idadi maridhawa ya nafsi za thamani tayari zinajiandaa kuja. Ndani yao watumwa wa Mungu watajitukuza. Zaidi ya hayo, licha ya idadi kubwa ya wadhambi wasiotubu ambao wa-taondolewa, nchi kwa wakati huo hata itakuwa nyembamba sana kwa sababu ya umati mkubwa unaokuja ndani. {1TG46: 9.2}

Aya ya 20 — “Watoto ulionyang’anywa watasema masikioni mwako, Mahali hapa ni pembamba, hapani-toshi; nipe nafasi nipate kukaa.”

Kutoka kwa aya hii tunakusanya kwamba watoto ambao Zayuni atapoteza, ni wale ambao wanakataa kuongoka. Hasara yake, hata hivyo, itabadilishwa na idadi kubwa kutoka kwa mataifa yote na kwa hivyo nchi itakuwa nyembamba sana. Aya zinazofuata, zinathibitisha mtazamo huu: {1TG46: 9.3}

Aya ya 21-23 — “Ndipo utasema moyoni mwako,

9

Ni nani aliyenizalia watoto hawa, na mimi nimefiwa na watoto wangu, nami ni peke yangu, nimehamish-wa, ninatanga-tanga huko na huku? Tena ni nani aliyewalea hawa? Tazama, naliachwa peke yangu; ha-wa je! Walikuwa wapi? Bwana MUNGU asema hivi, Tazama, nitawainulia mataifa mkono wangu, na kuwatwekea kabila za watu bendera yangu; nao wataleta wana wako vifuani mwao, na binti zako wa-tachukuliwa mabegani mwao. Na wafalme watakuwa baba zako za kulea, na malkia zao mama zako za kulea; watainama mbele yako kifudifudi, na kuramba mavumbi ya miguu yako; nawe utajua ya kuwa mimi ni Bwana, tena waningojeao hawatatahayarika.”

Ingawa sasa tunaweza ama kuchukiwa au kutojulikana, siku inakuja ambayo tutafarijiwa. Watu wakuu wa dunia wakati huo, kwa mfano, “watayaramba mavumbi” ya miguu yetu. {1TG46: 10.1}

Aya ya 24, 25 — “Je! Aliye hodari aweza kunyang’anywa mateka yake, au jeshi lao waliofungwa halali wataokoka? Naam, Bwana asema hivi, Hata jeshi la wafungwa wake aliye hodari watapokonywa miko-noni mwake, na mateka yake aliye jabari wataokoka; kwa maana nitateta na yeye atetaye nawe, nami nitawaletea wana wako wokovu.”

Hakuna utawala wowote ulimwenguni ambao utaweza kuwashikilia watu wa Mungu chini mavumbini. {1TG46: 10.2}

Aya ya 26 — “Na hao wanaokuonea nitawalisha nyama yao wenyewe, nao watalewa kwa kuinywa damu yao wenyewe, kama kwa mvinyo mpya; na wote wenye mwili watajua ya kuwa mimi, Bwana, ni mwokozi wako, na Mkombozi wako ni Mwenye enzi wa Yakobo.”

Adui zetu watauana kwa bidii kubwa kana kwamba wamejinywesha divai tamu. {1TG46: 10.3}

10

Ndipo wale waliosalia watatambua kwamba Bwana, aliye hodari wa Yakobo, ni Mwokozi na Mkombozi wetu. Je! Tuweze kwa hivyo kuendelea kulala? Au tutaondoka katika haki ya Kristo na kujiandaa kukutana na Bwana na kuwa pamoja Naye katika Ufalme Wake? Fursa yako na wakati wa uamuzi wako ni sasa umekuja na hauwezi kuahirishwa. Lazima uchukue msimamo thabiti na amilifu pamoja na vuguvugu hili la walei, katika hili kazi am-bayo kwanza ni kwa ajili ya kanisa, kisha kwa ajili ya ulimwengu. {1TG46: 11.1}

*******

Wakati ambapo unaagiza nakala za ziada za “Trakti za Vuli,” tafadhali bainisha gombo na namba ya somo bada-la ya tarehe au jina. Hili litawezesha kuingiza agizo lako bila kukawia. {1TG46: 11.2}

Usiyakose Manufaa Juu ya Hili

Iwapo haujatuma kwa ajili ya nakala yako iliyotangazwa na iliyojadiliwa sana kijitabu cha afya cha kurasa 96 (Kabari Inayoingia) ambacho kimefanya uamsho mkubwa katika dunia ya Waadventista na ambacho kimeliweka Shirika la K.I. katika mwangaza, usikikose iwapo afya, nyumba, na furaha yako inamaanisha kitu kwako. Kwa maoni yetu kitabu hiki ndicho bora hatujawahi kuona juu ya su-ala hili. Kwa kweli tunahisi kwamba kimetumwa na Mungu, na kwamba nakala yake inapaswa kuwa katika kila nyumba. Tumejulishwa kwamba sasa unaweza kukipata bila kuagizia. Tuma jina lako, anwani, na jina la kanisa ambalo wewe ni mshiriki (unaombwa kuchap-isha), na senti 15 kwa sarafu au stempu kwa Shirika La Kabari Inayoingia La Marekani, Kituo cha Mlima Kar-meli, Waco, Texas, Marekani na kitatumwa kwako. {1TG46: 11.3}

11

DUKA LA KUTUMIA

Rai Ya Rehema Ya Mungu

Nitasoma kutoka katika “Mlima wa Baraka,” ukurasa wa 217, kuanzia aya ya kwanza– {1TG47: 12.1}

“Lakini hadi leo rehema humrai mdhambi. ‘Jinsi niishivyo, asema Bwana MUNGU, sifurahii kufa kwake mtu mwovu; si afadhali kwamba aghairi njia yake akaishi: ghairini, ghairini kutoka kwa njia zenu za uovu; mbona mfe?’ Sauti ambayo hunena kwa wasiotubu hadi leo ni sauti yake Yeye ambaye katika uchungu wa moyo alipaaza sauti aAlipouona mji wapendo Lake: ‘Ee Yerusalemu, Yerusalemu, uwauaye manabii, na kuwapiga kwa mawe wale waliotumwa kwako! Ni mara ngapi nimetaka kuwakusanya pamoja watoto wako, kama vile kuku avikusanyavyo pamoja vifaranga vyake chini ya mabawa yake, lakini hamkutaka! Angalieni, nyumba yenu mmeachiwa hali ya ukiwa!’’ Katika Yerusalemu, Yesu aliona ishara ya ulimwengu ambao ulikuwa umekataa na kuidharau neema Yake. Alikuwa akiomboleza, Ee moyo mkaidi, kwa ajili yako! Hata wakati machozi ya Yesu yalimtiririka mlimani, Yerusalemu ungaliweza kuwa umetubu, na kuokoka maangamizi yake. Kwa muda mchache Zawadi ya mbinguni bado ilingojea kukubaliwa kwake. Kwa hivyo, Ee moyo, kwako wewe Kristo bado ananena kwa lafudhi za upendo: ‘ Tazama, nasimama mlangoni, nabisha; mtu akiisikia sauti yangu, na kuufungua mlango, nitaingia kwake, nami nitakula pamoja naye, na yeye pamoja nami. Sasa ni wakati ulioku-baliwa; tazama, sasa ni siku ya wokovu.’” {1TG47: 12.2}

Tuweze kuomba kwamba tuitikie kwa furaha rai ya rehema ya Mungu; kwamba tung’amue kuwa kusudi Lake ni kutuokoa kutoka kwa uharibifu wa milele; kwamba tuweze kuitika sasa katika siku ya wokovu; kwamba tujue Yeye anaturai leo kama Alivyousihi Yerusalemu wakati wa ujio Wake wa kwanza; kwamba mlango wa mioyo yetu usifungwe kamwe kwake. {1TG47: 12.3}

12

TAABU YA YAKOBO; YUDA NA ISRAELI WAENDA NYUMBANI

MATINI YA HOTUBA NA V. T. HOUTEFF

MCHUNGAJI WA WADAUDI WAADVENTISTA WA SABATO

SABATO, JUNI 28, 1947

HEKALU LA MLIMA KARMELI

WACO, TEXAS

Sasa tunaendeleza mada ile ile ambayo tumekuwa tukiichambua kutoka katika kitabu cha Isaya, ila leo tu-taichambua kutoka katika kitabu cha Yeremia. {1TG47: 13.1}

Kwa kuanza, tutaona kwamba sura za kwanza za kitabu hicho hushughulika na Yuda na Israeli wa kale, pamoja na dhambi zao na ukaidi wa moyo, na tokeo la kutawanywa kwa nchi zote za Mataifa. Sura ya thelathini, hata hivyo, haishughuliki, na kutawanywa kwa Yuda na Israeli ya kale, bali na kukusanywa kwa Yuda na Israeli katika siku yetu. {1TG47: 13.2}

Sasa tutaanza uchambuzi wetu na aya tatu za kwanza– {1TG47: 13.3}

Yer. 30: 1-3 — “Neno hili ndilo lililomjia Yeremia, kutoka kwa Bwana, kusema, Bwana Mungu wa Israeli, asema hivi, ya kwamba, Uyaandike kitabuni maneno hayo yote niliyokuambia. Kwa maana, tazama, siku zinakuja, asema Bwana, nitakapowarejeza watu wangu wa Israeli na Yuda waliofungwa, asema Bwana; nami nitawarudisha hata nchi niliyowapa baba zao, nao wataimiliki.”

Kumbuka kwamba wote Yuda na Israeli pamoja wanayo ahadi ya kurejea katika nchi yao. Kwa

13

sababu hili haijawahi kutimia, unabii bado utatimizwa. {1TG47: 13.4}

Aya ya 4-6 — “Na haya ndiyo maneno aliyosema Bwana, katika habari za Israeli, na katika habari za Yuda. Maana Bwana asema hivi, Tumesikia sauti ya tetemeko, na ya hofu, wala si ya amani. Ulizeni sasa, mkaone kwamba mwanamume aona utungu wa uzazi; mbona, basi, ninaona kila mtu anaweka mikono yake viunoni, kama mwanamke aliye na utungu, na nyuso zote zimegeuka rangi?”

Sababu ya hofu iliyotabiriwa hapa haina msingi na isiyokuwa muhimu, asema Bwana. {1TG47: 14.1}

Yer. 30: 7 — “Ole! Maana siku ile ni kuu, hata hapana inayofanana nayo, maana ni wakati wa taabu yake Yakobo; lakini ataokolewa nayo.”

Watu ambao wamekuja hadi kwa wa uakisi wakati huu wa taabu wanarejea nchini kwao, wamefarijiwa. Ina-vyoonekana ni vibaya kuwatisha wote, ila shauri la kutia moyo la Mungu ni, “Usiogope.” {1TG47: 14.2}

Kwa udhahiri, mzigo wa sura hii ni kuhusu wa uakisi kurejea katika nchi yao. Ingawa ya kutisha taabu ina-vyoweza kuonekana, bado matokeo yake yatakuwa sawa na ulivyokuwa mfano. Hivi sasa hatuwezi kuuthamini uchambuzi huu kama tunavyopaswa kufanya, lakini wakati unakuja hivi karibuni ambapo tutauchimba upesi sa-na na kwa bidii kama vile tungaliweza ili kutoka chini ya poromoko. Wale ambao wanayo imani haba tu katika Neno la Mungu, uchambuzi huu hautawafaa sana. Sasa ni wakati wa kuanza kuikuza imani tunayohitaji kuwa nayo wakati huo. {1TG47: 14.3}

14

Yakobo, mfano wetu, alijua vyema kwamba Mungu alikuwa ameelekeza kurejea kwake kutoka Padan-aram kwenda nyumbani, hata hivyo alitetemeka aliposikia kwamba Esau, na wanaume mia nne walikuwa njiani kuku-tana naye. Mbali na hilo, aliongozwa kushindana na malaika usiku kucha. Alishinda tu kwa sababu hangalimru-husu Malaika aende hata Ambariki. Tokeo la mwisho lilikuwa kwamba kesho yake, Esau, badala ya kuliangami-za kundi lote, kwa upole mno alimsalimu Yakobo kwa kumbusu, na akamkaribisha kwa ukunjufu arudi nyumba-ni! Kwa hivyo wakati yote yalipojisuluhisha, Yakobo aliona wazi kwamba hapakuwa na haja yoyote kuwa ali-hofia. Inatia moyo kama nini kwamba “Basi mambo hayo yaliwapata wao kwa jinsi ya mifano, yakaandikwa ili kutuonya sisi, tuliofikiliwa na miisho ya zamani.” 1 Kor. 10:11. Kile kilichotokea kwa Yakobo ni hakika kitatukia kwetu, na ni faraja jinsi gani kuyajua haya yote kabla ya wakati. Sasa, iwapo hatujawahi awali tuna-paswa kuona kwamba pale ambapo upo mfano hapo pia upo uakisi, na kwamba pale ambapo hakuna mfano, haupo Ukweli. {1TG47: 15.1}

Aya ya 8 — “Na itakuwa katika siku ile, asema Bwana wa majeshi, nitaivunja nira yake itoke shingoni mwako, nami nitavipasua vifungo vyako; wala wageni hawatamtumikisha tena.”

Aya hii inasema wazi kuwa Mungu atawaweka huru watu Wake kutoka kwa nira ya Mataifa, na kwamba wa-geni [wasio waongofu] hawatawataabisha tena. {1TG47: 15.2}

Aya ya 9 — “Bali watamtumikia Bwana, Mungu wao, na Daudi, mfalme wao, nitakayemwinua kwa ajili yao.”

Wafuasi wa Ukweli hawatawatumikia tena wengine, lakini watamtumikia Bwana, na mfalme ambaye Mungu Mwenyewe atatoa. {1TG47: 15.3}

15

Aya ya 10 — “Kwa sababu hiyo usiogope, Ee Yakobo, mtumishi wangu, asema Bwana; wala usifadhaike, Ee Israeli; kwa maana, tazama, nitakuokoa toka mbali, na wazao wako toka nchi ya uhamisho wao; na Yakobo atarudi, naye atatulia na kustarehe, wala hapana mtu atakayemtia hofu.”

Kwa hivyo hakuna haja ya hofu, lakini kuna haja ya imani katika ahadi za Mungu. {1TG47: 16.1}

Aya ya 11 — “Maana mimi ni pamoja nawe, asema Bwana, nikuokoe; maana nitawakomesha kabisa ma-taifa yote huko nilikokutawanya, bali sitakukomesha wewe kabisa; lakini nitakurudi kwa hukumu, wala sitakuacha bila adhabu.”

Adhabu iliyoshughulikiwa kwa Israeli ni kutawanywa kwao kati ya Mataifa kama ilivyofafanuliwa katika aya zinazofuata. Wakati wa uhuru hata hivyo umekuja, na kwa hili tunapaswa kufurahi na kumpa Mungu utukufu. {1TG47: 16.2}

Aya ya 12-19 — “Maana Bwana asema hivi, Maumivu yako hayaponyeki, na jeraha yako ni kubwa. Hap-ana mtu wa kukutetea; kwa jeraha yako huna dawa ziponyazo. Wote wakupendao wamekusahau; ha-wakutafuti; maana nimekujeruhi kwa jeraha ya adui, kwa adhabu ya mtu mkatili; kwa sababu ya ukubwa wa uovu wako, kwa sababu dhambi zako zilikuwa zimeongezeka. Mbona unalilia maumivu yako? Hayaponyeki maumivu yako; kwa sababu ya ukubwa wa uovu wako, kwa sababu dhambi zako zimeongezeka, nimekutenda haya. Basi, watu wote wakulao wataliwa; na adui zako wote watakwenda kufungwa; kila mmoja wao; na hao waliokuteka nyara watatekwa; na wote waliokuwinda nitawafanya kuwa mawindo. Maana nitakurudishia

16

afya, nami nitakuponya jeraha zako, asema Bwana, kwa sababu wamekuita, mwenye kutupwa, wakise-ma, Ni Sayuni, ambao hapana mtu autakaye. Bwana asema hivi, Tazama, nitarudisha tena hema za Yakobo zilizohamishwa, na kuyahurumia makao yake; nao mji huo utajengwa juu ya magofu yake wenyewe, nalo jumba litakaliwa, kama ilivyokuwa desturi yake. Tena kwao itasikiwa shukrani, na sauti yao wachangamkao; nami nitawazidisha, wala hawatakuwa wachache; tena nitawatukuza, wala ha-watakuwa wanyonge.”

Baada ya kupitia utumwani, watu watatambua kabisa rehema ya Mungu na hekima Yake ya kuwaokoa. Wa-takuwa na furaha milele, kwa maana Atawazidisha katika nchi ya baba zao, na huko Yeye atawafanya kuwa wakuu. {1TG47: 17.1}

Aya ya 20 — “Watoto wao nao watakuwa kama zamani, na kusanyiko lao litathibitika mbele zangu, nami nitawaadhibu wote wawaoneao.”

Ufalme (kanisa lililotakaswa na lililotengwa na ulimwengu) utakuwa wa asili na halisi kama ulivyokuwa ufalme wa Israeli wa kale, lakini hautakuwa na wadhambi ndani yake. {1TG47: 17.2}

Aya ya 21-23 — “Na mkuu wao atakuwa mtu wa kwao wenyewe, naye mwenye kuwatawala atakuwa mtu wa jamaa yao; nami nitamkaribisha, naye atanikaribia; maana ni nani aliye na moyo wa kuthubutu ku-nikaribia? Asema Bwana. Nanyi mtakuwa watu wangu, nami nitakuwa Mungu wenu. Tazama, tufani ya Bwana, yaani, ghadhabu yake, imetokea tufani ya kudumu; itawaangukia waovu vichwani.”

17

Mkuu wao atakuwa wa kwao wenyewe; yaani, Ufalme huu utajitawala chini ya Mungu. Neno “tazama” linavuta umakini kwa kitu ambacho kinaweza kuonekana na kwa hivyo linamaanisha kwamba kimbunga cha Bwana tayari kinafanya kazi yake. Si ajabu, basi, kwamba sasa tunapata usumbufu wa kila aina, na hasara kubwa ya maisha na mali duniani kote. {1TG47: 18.1}

Aya ya 24 — “Hasira kali ya Bwana haitarudi, hata atakapokwisha kutenda, hata atakapokwisha kuyati-miza makusudi ya moyo wake; katika siku za mwisho mtayafahamu haya.”

Ukweli haswa kwamba kweli hizi zimefunuliwa sasa, na pia ukweli kwamba mambo yaliyotabiriwa na Maandi-ko sasa yanatukia, unaonyesha wazi kwamba sasa tunaishi katika siku za mwisho, — siku ambazo lazima tuanga-lie chanzo cha maovu ambayo yanaufunika ulimwengu wote, na kufanya mwito na uteuzi wetu kuwa hakika. {1TG47: 18.2}

Tunapaswa kushukuru sana kuwa Bwana anatulisha kwa “chakula kwa wakati wake”! Ijapokuwa watu wanauana kwa mamilioni ili wajikomboe kutoka kwa nira ya taifa fulani lingine, Musa aliwakomboa Israeli wa kale bila majeruhi. Tunapaswa kujua sasa kwamba imani huondoa milima, ambapo shaka huangamiza mataifa. Tusiendelee tena kuwa wapumbavu na goigoi wa moyo kuamini yote ambayo manabii wameandika (Luka 24:25) “Amini” ulikuwa mwito wa Yesu, na unapaswa kuwa wetu pia. Kamwe hakuna wenye mashaka wa-takaoingia katika Ufalme Wake. {1TG47: 18.3}

Mambo haya yameandikwa “ili mpate kuamini ….” Yohana 20:31. {1TG47: 18.4}

Lipo hitimisho moja la busara ambalo unaweza kufikia, nalo ni kukubali kwa moyo wote na kutimiza ambayo manabii wote wameandika. Usiache mtu yeyote augeuze umakini wako kutoka kwa Ukweli huu. {1TG47: 18.5}

18

ANDIKO LA SALA

Jenga Kwa Msingi Thabiti

Nitasoma kutoka katika “Mlima wa Baraka,” ukurasa wa 217, kuanzia aya ya pili. Kushtukia, hii ndiyo sura ya mwisho katika kitabu. {1TG48: 19.1}

“Ninyi mnaoegemeza tumaini lenu kwa ubinafsi, mnajenga kwa mchanga. Lakini bado hamjachelewa sana kuo-koka maangamizi yanayokuja. Kabla ya tufani kuvuma, ukimbilie msingi thabiti. Bwana MUNGU asema hivi, Tazama, naweka katika Zayuni jiwe kuu la pembeni, teule, lenye heshima, Na kila amwaminiye hatatahayarika. Nitafute mimi, na muokolewe, miisho yote ya dunia; kwa kuwa mimi ni Mungu, na hapana mwingine. Usiogope; kwa kuwa Mimi ni pamoja nawe; usifadhaike; kwa kuwa Mimi ni Mungu wako; nitakuimarisha; naam, nitaku-saidia; naam, nitakushikilia kwa mkono wa kuume wa haki Yangu. Hautaaibika wala kufadhaika dunia bila mwisho.’” {1TG48: 19.2}

Tunataka sasa kuomba kwamba tuachane na ubinafsi na kumtegemea Mungu kabisa; kwamba tujenge, sio juu ya msingi wa mchanga, ila juu ya Mwamba thabiti, juu ya msingi hakika ambao hautaweza kufagiliwa mbali wakati dhoruba itakapokuja. {1TG48: 19.3}

19

CHETI CHA MUNGU KUFUFUA, KUTAKASA, NA KUWAUNGANISHA YUDA NA ISRAELI

MATINI YA HOTUBA NA V. T. HOUTEFF

MCHUNGAJI WA WADAUDI WAADVENTISTA WA SABATO

SABATO, JULAI 5, 1947

HEKALU LA MLIMA KARMELI

WACO, TEXAS

Alasiri hii tutachambua Yeremia 31. Inasheheni hakikisho la Uvuvio kwa watu wa Mungu kurejea katika nchi yao. Sura hii, utatambua, inasheheni unabii wa siku za mwisho: {1TG48: 20.1}

Yer. 31: 1 — “Wakati huo, asema Bwana, nitakuwa Mungu wa jamaa zote za Israeli, nao watakuwa watu wangu.”

Kirai, “wakati huo,” kinarudisha mawazo yetu kwa Yeremia 30, aya ya 24, ambapo kinaelezea kwamba ule wa-kati ni siku za mwisho, wakati wetu. Sio muda mrefu, kwa hivyo, Mungu wetu atakuwa Mungu wa familia zote za Israeli, Mungu wa kanisa lote. Mtakatifu na mdhambi wakati wa Hukumu kwa Walio Hai hawataendelea kuchangamana tena. {1TG48: 20.2}

Aya ya 2 — “Bwana asema hivi, Watu wale walioachwa na upanga walipata neema jangwani; yaani, Is-raeli, hapo nilipokwenda kumstarehesha.”

Watu ambao wataokoka uhamisho wao, watapata neema katika nchi za Mataifa — “nyikani,” mbali na shamba la mizabibu. (Kwa sababu Nchi ya Ahadi ni shamba la mizabibu — Isaya 5 — basi nyika ingaliweza kuwa nini isipokuwa nchi za watu wa Mataifa?) Watu wa Mungu

20

watapata neema hii wakati ambapo Bwana atasababisha wapumzike kutoka kwa ugeni wao — baada ya “Huku-mu katika nyumba ya Mungu” kutukia. (1 Pet. 4:17). {1TG48: 20.3}

Aya ya 3 — “Bwana alinitokea zamani, akisema, Naam nimekupenda kwa upendo wa milele, ndiyo maana nimekuvuta kwa fadhili zangu.”

Katika utimizo wa unabii huu watu watatambua kwamba Bwana amewapenda kwa kweli, na ya kuwa Yeye an-awavuta Kwake kwa fadhili zenye upendo. {1TG48: 21.1}

Aya ya 4 — “Mara ya pili nitakujenga, nawe utajengwa, Ee bikira wa Israeli mara ya pili utapambwa kwa matari yako, nawe utatokea katika michezo yao wanaofurahi.”

Bwana huwahakikishia watu Wake kwamba ingawa nchi za Mataifa zimeuangusha ufalme wao, Yeye ataureje-sha kwao, na tena watakuwa taifa lenye utukufu na furaha. Ahadi hizi hunamaanisha kwamba watu sasa ha-wajapambwa na kufurahi. Huenda tusilitambue hili kikamilifu, lakini Mungu anajua vyema zaidi ya tujuavyo. {1TG48: 21.2}

Aya ya 5 — “Mara ya pili utapanda mizabibu juu ya milima ya Samaria; wapanzi watapanda, nao wa-tayala matunda yake kama kawaida.”

Wengi wa ulimwengu hufikiri kwamba kama kabila kumi, Ufalme wa Israeli, zimepotea kati ya nchi za Mataifa, kwamba ufalme wao umetoweka milele, lakini Mungu Ambaye hutenda kulingana na mapenzi Yake mema ana-tangaza wazi kwamba waaminifu, baada ya kutengwa kwao kutoka kwa wasio waminifu, watakusanywa na ku-rejeshwa katika milima ya Samaria; na kwamba watapanda na kula matunda ya upanzi wao kama jambo la kawa-ida. {1TG48: 21.3}

21

Aya ya 6 — “Maana kutakuwa siku moja, ambayo walinzi watalia juu ya vilima vya Efraimu, Inukeni, tu-kaende Zayuni, kwa Bwana, Mungu wetu.”

Walinzi wa siku zijazo wa Mlima Efraimu, badala ya kujitenga na wale wa Mlima Zayuni walivyofanya zamani, watawaongoza walei kwa furaha kurudi Zayuni. Halitaibuka tena swali, Je! Ni kwanini “Baba zetu waliabudu katika mlima huu, nanyi husema ya kwamba huko Yerusalemu ni mahali patupasapo kuabudia.”? Yohana 4:20 {1TG48: 22.1}

Aya ya 7 — “Maana Bwana asema hivi, Mwimbieni Yakobo kwa furaha, mkampigie kelele mkuu wa ma-taifa, tangazeni, sifuni, mkaseme, Ee Bwana, uwaokoe watu wako, masalia ya Israeli.”

“Masalia” ni wale watakaokoka “Hukumu katika nyumba ya Mungu.” Watu wa Mungu sasa, wakati wanakaa kati ya wakuu wa mataifa, wanahimizwa kutangaza habari hii njema miongoni mwao pamoja na kuimba, furaha na sifa, wakisema. , “Ee Bwana, uwaokoe watu Wako.” Ukweli huu sasa ndio haswa Ukweli wa sasa, na Una-paswa kutangazwa na kuzingatiwa. Kutenda kazi na kuomba kwa kusudi hili, ndio ujumbe wa saa. {1TG48: 22.2}

Aya ya 8 — “Tazama, nitawaleta toka nchi ya kaskazini, na kuwakusanya katika miisho ya dunia, na pamoja nao watakuja walio vipofu, na hao wachechemeao, mwanamke mwenye mimba, na yeye pia aliye na utungu wa kuzaa; watarudi huko, jeshi kubwa.”

Hatuhitaji kuogopa; juhudi zetu hazitakosa matunda. Watu waaminifu wa Mungu watausikia na kutii ujumbe wa siku hii, na Bwana kwa hivyo atawakusanya kutoka pembe nne za dunia. Wawe ni vipofu au viwete, wawe wanawake au watoto, wote

22

watarejea kwenye shamba la mizabibu la Bwana. {1TG48: 22.3}

Aya ya 9 — “Watakuja kwa kulia, na kwa maombi nitawaongoza; nitawaendesha penye mito ya maji, katika njia iliyonyoka; katika njia hiyo hawatajikwaa; maana mimi ni baba wa Israeli, na Efraimu ni mzaliwa wangu wa kwanza.”

Efraimu mwenyewe, Uvuvio unasema, angaliweza kuwa “umati wa mataifa.” Mwa 48:19, 20. {1TG48: 23.1}

Aya ya 10 — “Lisikieni neno la Bwana, enyi mataifa, litangazeni visiwani mbali; mkaseme, Aliyemtawanya Israeli atamkusanya, na kumlinda, kama mchungaji alindavyo kundi lake.”

Mungu ananena na ni nani anayethubutu kutoliweka Neno Lake moyoni? Nani anayethubutu kutojali na kunyamaza? Ili mataifa waweze kusema, “Aliyemtawanya Israeli atamkusanya, na kumlinda,” lazima yawe ni mataifa ambayo yanaamini, mataifa ambayo yanauelewa unabii huu na ahadi. Wanapaswa kutenda tunachofan-ya. Lakini kwa sababu hakuna taifa linalofanya hivi kwa wakati huu, na kwa kuwa ni sisi pekee ndio tunao-husika katika kazi hii, ukweli unakuwa bayana kwamba ujumbe wetu utayaamsha mataifa kwa ukweli kwamba sisi, wazawa wa mwisho wa kabila kumi na mbili za Israeli, tumeitwa kuutangaza Ukweli huu sio tu kwa ndugu zetu wote, bali hata kwa mataifa. Kisha mataifa Yatautangaza tena kwa mataifa mengine, hivyo yananena Maandiko. Watatangaza kwamba watu wa Mungu watakusanywa, na kulindwa, pia. {1TG48: 23.2}

Sisi, kwa hivyo, hatupaswi kushindwa katika uaminifu wetu. Lazima tuthibitike kuwa tunastahili mwito wetu. {1TG48: 23.3}

Aya ya 11 — “Kwa maana Bwana amemweka huru Yakobo,

23

amemkomboa mkononi mwake aliyekuwa hodari kuliko yeye.”

Hatuwezi kujikomboa, wala wenyewe hatuwezi kurudi katika nchi yetu. Mungu atafanikisha haya yote kwa ajili yetu. Tunapaswa kwa hivyo kuwa wa shukrani kwamba uhuru na ukombozi wetu haututegemei sisi wenyewe. Wajibu ni wa Mungu. Yeye atatukomboa kutoka kwake aliye hodari kuliko sisi. {1TG48: 24.1}

Aya ya 12-14 — “Nao watakuja, na kuimba katika mlima Zayuni, wataukimbilia wema wa Bwana, nafa-ka, na divai, na mafuta, na wachanga wa kondoo na wa ng’ombe; na roho zao zitakuwa kama bustani ili-yotiwa maji; wala hawatahuzunika tena kabisa. Ndipo bikira atafurahi katika kucheza, na vijana na wazee pamoja; maana nitageuza masikitiko yao kuwa furaha, nami nitawafariji, na kuwafurahisha waache huzuni zao. Nami nitaishibisha roho ya makuhani kwa unono, na watu wangu watashiba kwa wema wangu, asema Bwana.”

Aya hizi, nina uhakika, hazihitaji ufafanuzi au maelezo. {1TG48: 24.2}

Aya ya 15, 16 — “Bwana asema hivi, Sauti imesikiwa Rama, kilio, na maombolezo mengi, Raheli akiwalilia watoto wake; asikubali kufarijiwa kwa watoto wake, kwa kuwa hawako, Bwana asema hivi, Zuia sauti yako, usilie, na macho yako yasitoke machozi; Maana kazi yako itapata thawabu, nao watakuja tena toka nchi ya adui; Ndivyo asemavyo Bwana.”

Ili kuzielewa aya hizi lazima kwanza tuangalie katika mandhari ya historia yake. Raheli, mke

24

wa Yakobo, alikuwa na wana wawili wake mwenyewe, Yusufu na Benyamini. Walikuwa wana pekee ambao walizaliwa kwa Yakobo katika Nchi ya Ahadi. Raheli alikufa alipokuwa akimzaa Benyamini, na kwa hivyo yeye mwenyewe asingaliweza kulia kwa kuwapoteza watoto wake. Wote walikuwa pamoja naye alipokufa. Kwa hivyo, hitimisho la pekee ambalo mtu anaweza kufikia, ni kwamba Raheli katika andiko hili ni mfano. {1TG48: 24.3}

Baada ya kifo cha Sulemani, ufalme uligawanywa, kabila kumi zikachukua kaskazini, na kabila mbili zikachukua kusini. Kabila la Yusufu lilikuwa katika ufalme mmoja, na kabila la Benyamini katika mwingine. Raheli, kwa hivyo, lazima awe mama wa mfano wa watoto wa falme zote mbili — Yuda na Israeli. {1TG48: 25.1}

Tukio la Yer. 31:15 Mathayo alilihusisha kwa Herode kuwaua watoto katika jaribio la kumuua Bwana (Mat. 2:18). Uchunguzi wa aya hii pamoja na muktadha wote wa sura hiyo, hata hivyo, utafichua kwamba ina ma-tumizi ya moja kwa moja hata zaidi ya kutawanywa kwa falme zote mbili, Yuda na Israeli, na kurudi kwao kutoka katika nchi za maadui wao kwenda nchi ya baba zao. {1TG48: 25.2}

Aya ya 17, 18 — “Tena liko tumaini kwa siku zako za mwisho, asema Bwana; na watoto wako watarejea hata mpaka wao wenyewe. Hakika nimemsikia Efraimu, akijililia hivi, Umeniadhibu, nami nikaadhibika, kama ndama asiyeizoelea nira; unigeuze, nami nitageuzwa; kwa maana wewe u Bwana, Mungu wangu.”

Mawazo mawili tofauti yanaletwa kwa mtazamo katika aya hii: kwanza, kwamba wana wa Ufalme watakuja tena kwenye mpaka wao; na pili, kwamba watakuwa awali wamepata uzoefu wa uamsho mkubwa

25

na matengenezo. Watakuwa wametambua kwamba adhabu ya Mungu ilikuwa kwa faida yao wenyewe, na kwamba Bwana ndiye Mungu wao. Matengenezo haya, pamoja na rehema za Mungu, yanaonekana zaidi katika aya zifuatazo. {1TG48: 25.3}

Aya ya 19, 20 — “Hakika baada ya kugeuzwa kwangu, nalitubu; na baada ya kufundishwa kwangu, nali-jipiga pajani; nalitahayarika, naam, nalifadhaika, kwa sababu naliichukua aibu ya ujana wangu. Je! Efraimu siye mwanangu mpendwa? Je! Siye mtoto apendezaye? Maana kila nisemapo neno juu yake, ningali nikimkumbuka sana; kwa sababu hiyo moyo wangu unataabika kwa ajili yake; bila shaka nitamrehemu, asema Bwana.”

Aya zifuatazo zinasheheni agizo na ushauri wa Mungu kwa watu Wake: {1TG48: 26.1}

Aya ya 21 — “Jiwekee alama za njia; jifanyie miti ya kukuongoza; uuelekeze moyo wako kwenye njia kuu, njia ile ile uliyoiendea; rudi tena, Ee bikira wa Israeli, irudie hii miji yako.”

Uvuvio hapa kwa dhati huwahimiza watu waaminifu wa Mungu kujiandaa kurudi kwa Nchi ya Ahadi, na unaendelea: {1TG48: 26.2}

Aya ya 22 — “Hata lini utatanga-tanga, Ee binti mwenye kuasi? Kwa maana Bwana ameumba jambo ji-pya duniani; mwanamke atamlinda mwanamume.”

Kwa kuwa haiwezekani kwa mwanamke kumzunguka mwanaume, mwanamke anayetajwa hapa lazima awe nembo ya kanisa. Na mwanamume ambaye atakuwa amezungukwa, kwa mujibu wa Uvuvio, Bwana mwenyewe. Kanisa, kwa hivyo litafanywa kumzunguka Bwana na kwa hivyo kuingia katika uzoefu wake mpya na wa furaha. {1TG48: 26.3}

“Imba, ufurahi, Ee binti Zayuni; maana, tazama,

26

ninakuja, nami nitakaa kati yako, asema Bwana. Na mataifa mengi watajiunga na Bwana katika siku ile, nao wa-takuwa watu wangu; nami nitakaa kati yako, nawe utajua ya kuwa Bwana wa majeshi amenituma kwako. Na Bwana atairithi Yuda, iwe sehemu yake katika nchi takatifu, naye atachagua Yerusalemu tena. Nyamazeni, ninyi nyote wenye mwili, mbele za Bwana; kwa maana ameamka, na kutoka katika maskani yake takatifu.” Zek 2: 10-13. {1TG48: 26.4}

Aya ya 23, 24 — “Bwana wa majeshi, Mungu wa Israeli, asema hivi, Watatumia tena neno hili katika nchi ya Yuda, na katika miji yake, nitakapowarudisha mateka yao; Bwana na akubariki, Ee kao la haki, Ee mlima wa utakatifu. Na Yuda, na miji yake yote, watakaa humo pamoja; wakulima, nao waendao huko na huko pamoja na makundi yao.”

Tena na tena tunaambiwa ya kwamba Ufalme wa Bwana, kanisa lililotakaswa, bila magugu sio kitu cha kifum-bo, ila kwamba Ni halisi kabisa. {1TG48: 27.1}

Aya ya 25, 26 — “Kwa maana nimeishibisha roho yenye uchovu, nami nimeiridhisha kila roho yenye huzuni. Basi, nikaamka, nikaangalia; na usingizi wangu ulikuwa mtamu kwangu.”

Inaonekana kwamba kuamka kwa nabii lazima kuonyeshe uamsho wa kiroho wa watu. Na utamu wa usingizi wake lazima uonyeshe kupenda kwa watu kuendelea kusinzia na kulala, kusitasita kwao kuamka kwa ukweli huu. {1TG48: 27.2}

Aya ya 27 — “Tazama, siku zinakuja, asema Bwana, nitakapoipanda nyumba ya Israeli, na nyumba ya Yuda, mbegu ya mwanadamu na mbegu

27

ya mnyama.”

Baada ya Ufalme huu kusimamishwa katika nchi ya ahadi, Utakua na wanadamu na wanyama jinsi ambavyo mfano wa sura ya pili ya Danieli unavyoelezea: “Na lile jiwe lililoipiga hiyo sanamu likawa mlima mkubwa, ukai-jaza dunia yote.” Dan. 2:35 “Katika siku za wafalme hao,” sio baada ya siku zao, “Mungu wa mbinguni atausimamisha ufalme, … bali … [Ufalme] Utavunja vipande vipande na kuziharibu falme hizi zote …” Dan. 2:44 {1TG48: 28.1}

Je! Wataongezeka vipi na kuijaza dunia? — Ruhusu nabii Isaya atoe jibu: {1TG48: 28.2}

“Na itakuwa katika siku za mwisho, mlima wa nyumba ya Bwana utawekwa imara juu ya milima, nao utainuliwa juu ya vilima; na mataifa yote watauendea makundi makundi. Na mataifa mengi watakwenda na kusema, Njoni, twende juu mlimani kwa Bwana, nyumbani kwa Mungu wa Yakobo, naye atatufundisha njia zake, nasi tutakwenda katika mapito yake maana katika Sayuni itatoka sheria, na neno la Bwana katika Yerusalemu.” Isa. 2: 2, 3. {1TG48: 28.3}

Aya ya 28 — “Tena itakuwa, kwa kadiri nilivyowaangalia, ili kung’oa, na kubomoa, na kuangusha, na kuangamiza, na kutesa; kwa kadiri iyo hiyo nitawaangalia, ili kujenga, na kupanda, asema Bwana.”

Kutoka kwa vifungu hivi vya Maandiko tunaona jinsi Bwana atajenga na kuuongeza Ufalme, na kuufanya Ui-jaze dunia. {1TG48: 28.4}

Aya ya 29, 30 — “Siku zile, hawatasema tena,

28

Baba za watu wamekula zabibu kali, na meno ya watoto wao yametiwa ganzi. Bali kila mtu atakufa kwa sababu ya uovu wake mwenyewe; kila mtu alaye zabibu kali, meno yake yatatiwa ganzi.”

Ufalme wa kale ulibomolewa kwa sababu ya dhambi za wale ambao waliongoza na kutawala mataifa; na kwa hivyo wote, wazuri na wabaya sawa, waliteseka. Mmoja wa watu wazuri ambao waliteseka kwa dhambi za wa-baya, alikuwa Danieli. Na daima imekuwa hivyo. Lakini sasa tunakuja kwa siku ambayo kila mtu atakufa kwa uovu wake mwenyewe. Mikaeli atasimama na “kila mmoja atakayeonekana ameandikwa katika kitabu kile” ataokolewa (Dan. 12: 1). {1TG48: 29.1}

Aya ya 31-33 — “Angalia, siku zinakuja, asema Bwana, nitakapofanya agano jipya na nyumba ya Israeli, na nyumba ya Yuda. Si kwa mfano wa agano lile nililolifanya na baba zao, katika siku ile nilipowashika mkono, ili kuwatoa katika nchi ya Misri; ambalo agano langu hilo walilivunja, ingawa nalikuwa mume kwao, asema Bwana. Bali agano hili ndilo nitakalofanya na nyumba ya Israeli, baada ya siku zile, asema Bwana; Nitatia sheria yangu ndani yao, na katika mioyo yao nitaiandika; nami nitakuwa Mungu wao, nao watakuwa watu wangu.”

Hili agano jipya, unaona, litatumika katika wakati wa kukusanywa. Wakati huo watu wote wa Mungu watajua tofauti kati ya wema na uovu. Kwa hivyo watajua ni nini mapenzi ya Bwana na njia. Na hivyo wataweza kuten-da mema na kuyaepuka uovu. Kwa uasilia na kwa shangwe watakuwa na mwelekeo wa kutenda mema, kama vile wao sasa walivyo na mwelekeo wa kutenda uovu. {1TG48: 29.2}

Nebukadneza, mfalme wa Babeli, alikuwa mfalme mkuu sana. Aliutawala ufalme mkubwa, na kuishi ndani ya

29

kasri la ajabu. Lakini mara tu moyo wake wa kibinadamu ulipoondolewa kwake na moyo wa mnyama kuwekwa ndani yake, mara hiyo tu tamaa zake mwenyewe na njia zake zikamtoka na tamaa na njia za mnyama zikaingia ndani yake. (Tazama Danieli 4:16). Ndivyo ilivyo na watu wa Mungu: Punde tu Yeye anapoitia sheria Yake ndani yao, na kuiandika katika mioyo yao, mara hiyo tu hamu ya moyo wa mwili na uadui dhidi ya sheria ya Mungu utatoweka. Watu wa Mungu hawatahitaji tena kusema, Wakati “tunataka kufanya mema, uovu upo.” “Ole wangu maskini mimi! ni nani atakayeniokoa na mwili huu wa mauti? ” Rom. 7:24. {1TG48: 29.3}

Aya ya 34 — “Wala hawatamfundisha kila mtu jirani yake, na kila mtu ndugu yake, wakisema, Mjue Bwana; kwa maana watanijua wote, tangu mtu aliye mdogo miongoni mwao hata aliye mkubwa miongoni mwao, asema Bwana; maana nitausamehe uovu wao, wala dhambi yao sitaikumbuka tena.”

Kumbuka kwamba wadhambi na wale ambao hawamjui Mungu hawatakuwa tena kati ya watu wa Mungu. Hakika badiliko linakuja. Hali ya sasa ya mambo haitaendelea muda mrefu, wadhambi wataondolewa milele. Na tunapaswa kufurahi kama nini kwamba ikiwa tunatubu sasa, dhambi zetu zitasamehewa na kusahaulika, na ya kwamba hakuna mtu atakayetukumbusha tena kuzihusu! {1TG48: 30.1}

Aya ya 35, 36 — “Bwana asema hivi, awapaye watu jua, ili kuwa nuru wakati wa mchana, na amri za mwezi na nyota, ili kuwa nuru wakati wa usiku, aichafuaye bahari, hata mawimbi yake yakavuma; Bwa-na wa majeshi, ndilo jina lake; Amri hizi zikiondoka, zisiwe mbele zangu, asema Bwana, ndipo wazao wa Israeli nao wataacha kuwa taifa mbele zangu milele.”

30

Hapa kuna dhamana halisi ya Mungu dhidi ya shaka na kutokuamini. Kwa hakika kama watia shaka hawawezi kubadilisha amri za mbingu, hakika jinsi hiyo watu wa Mungu watakuwa tena taifa la Kutawaliwa na Mungu. {1TG48: 31.1}

Aya ya 37- 40 — “Bwana asema hivi, Kama mbingu zikiweza kupimwa, na misingi ya dunia ikiweza ku-gunduliwa huko chini, ndipo wazao wa Israeli pia nitawatupilia mbali, kwa ajili ya hayo yote wali-yoyatenda, asema Bwana. Tazama, siku zinakuja, asema Bwana, mji huu utakapojengwa kwa ajili ya Bwana, toka buruji ya Hananeli hata lango la pembeni. Na kamba ya kupimia itaendelea moja kwa moja hata mlima Garebu, tena itazunguka na kufika Goa. Na bonde lote la mizoga, na majivu, na mashamba yote mpaka kijito Kidroni, mpaka pembe ya lango la farasi, upande wa mashariki, patakuwa patakatifu kwa Bwana; hapatang’olewa, wala hapatabomolewa, hata milele.”

-0-0-0-0-0

Ili kuleta kwa wote furaha hii isiyo na kifani ya ahadi za Mungu, tarajio la vizazi vyote, masomo haya yanachap-ishwa na kutumwa bila malipo au wajibu kwa wote wanaotaka kuwa nayo. Tuma jina lako na anwani kwa Shiri-ka la Uchapishaji la Ulimwengu, kwa anwani iliyo nyuma ya jalada. {1TG48: 31.2}

31

Jumuiya ya Wadaudi Waadventista wa Sabato

(Ushirika Huru Unaojumuisha Kanisa)

Mlima Karmeli, Waco, Texas

S.L.P. 23738, Waco, TX 76702

+ 1-254-855-9539

www.gadsda.com

info@gadsda.com

Gombo la 1, Namba 46, 47, 48

Kimechapishwa nchini Marekani

32

>