10 Aug Gombo la 1 Salamu Mwafaka Namba 44, 45
Gombo la 1 Salamu Mwafaka Namba 44, 45
AMANI YA PEKEE YA MAWAZO
Hati miliki, Kimechapishwa tena 1953
Haki zote zimehifadhiwa
V. T. HOUTEFF
MAMBO AMBAYO YANAENEA KABLA NA BAADA YA DUNIA KUFANYWA UPYA
KINA ESAU WENYE UKUU MWINGI NA KINA YAKOBO WASIOJIVUNA
1
ANDIKO LA SALA
Kuwa Watendaji Wa Neno
Wazo letu la sala linapatikana katika “Mlima wa Baraka,” uk. 145 — {1TG44: 2.1}
“Sio wote wanaolikiri jina Lake na kuvaa Beji yake ni wake Kristo. Wengi ambao wamefundisha kwa jina Langu, alisema Yesu, watapatikana wapungufu mwishowe. Je! Wengi wataniambia Siku ile, Bwana, Bwana, hatukufanya unabii kwa jina lako? na kwa jina lako kutoa pepo? na kwa jina lako kufanya miujiza mingi? Ndipo nitawaambia dhahiri, Sikujua ninyi kamwe; ondokeni kwangu, enyi mtendao maovu.’ {1TG44: 2.2}
“Wapo watu ambao huamini kwamba wao wako sawa, ilhali wamekosea. Ambapo wanadai Kristo kama Bwana wao, na kwa madai kuwa wanafanya kazi kubwa kwa jina Lake, wao ni watendakazi wa uovu. ‘Na kwa vinywa vyao wanaonyesha upendo mwingi, lakini mioyo yao inafuata tamaa zao.’ Yeye ambaye hulitangaza Neno la Mungu kwa wao ni ‘kama wimbo wa kupendeza wa yule aliye na sauti tamu na anayeweza kucheza vyema kwenye chombo; kwa sababu huyasikia maneno Yako; lakini hawayatendi.’” {1TG44: 2.3}
Watu walioelezwa hapa hupenda kulisikia Neno la Mungu, lakini inaishia hapo mara tu wanapokwenda. Natu-mai hakuna yeyote hapa wa kusikiliza tu, ila wa kutenda jambo juu yake. Watendaji wa Neno tu ndio huhesabi-wa haki. Hebu tupige magoti na tuombe kwa bidii kwamba Mungu atusaidie tusiwe tu wanaoukiri Ukweli, bali watendaji wa kweli Yake. {1TG44: 2.4}
2
MAMBO AMBAYO YATATUKIA KABLA NA BAADA YA DUNIA KUUMBWA UPYA
Isaya 65
MATINI YA HOTUBA NA V. T. HOUTEFF
MCHUNGAJI WA WADAUDI WAADVENTISTA WA SABATO
SABATO, JUNI 7, 1947
HEKALU LA MLIMA KARMELI
WACO, TEXAS
Tunaichambua sura ya sitini na tano ya Isaya. Tunapojifunza tutaona kwamba inashuhudia mambo ambayo ya-natukia katika kipindi kabla ya dunia kufanywa upya, na katika kipindi baada ya kufanywa upya. Tutaanza so-mo letu na aya ya kwanza. {1TG44: 3.1}
Isa. 65: 1 — “Watu wasionitaka wanauliza habari zangu; nimeonekana na hao wasionitafuta; naliliambia taifa lisiloitwa kwa jina langu.”
Paulo, akiwaandikia Warumi, anaihusisha aya hii kwa Mataifa wanaokuja katika Injili (Rum. 10:20). Wao ni, kwa hivyo, wale ambao walimtafuta Bwana bila kumuuliza Yeye, na wale waliompata bila Kumtafuta. Hali hii imejaa matokeo, inaonyesha kwamba Bwana hupatikana kwa urahisi. {1TG44: 3.2}
Aya ya 2 — “Nitazameni, nitazameni. Mchana kutwa nimewanyoshea mikono yangu watu walioasi, watu waendao katika njia isiyo njema, wakifuata mawazo yao wenyewe.”
Hapa kuna tofauti kubwa kati ya walioelimishwa vizuri katika mambo ya Mungu, na Mataifa wasiojua. Wakati wale wa awali wanajiondoa, ingawa Bwana anateta nao kwa machozi, wa mwisho wanamkaribia
3
Yeye. Hapa tunaona jinsi Mungu alivyo na uvumilivu. Anaendelea kuwasihi daima. Ni vigumu Kwake kum-wachilia mdhambi kabla njia zote zinazowezekana kumwokoa zimemalizika. Hapa inaonekana wazi kwamba ni rahisi kumwokoa mshenzi kuliko ilivyo kumwokoa Mkristo aliyeridhika na kudanganyika. {1TG44: 3.3}
Aya ya 3 — “Watu wanikasirishao mbele za uso wangu daima, wakitoa dhabihu katika bustani zao, na kufukiza uvumba juu ya matofali.”
Kutoa dhabihu katika bustani ni kufanya wonyesho wa dini, na madhabahu za matofali (bidhaa ya mwanadamu, sio ya uumbaji wa Mungu kama lilivyo jiwe), ni matendo ya mwanadamu. Kaini alitoa dhabihu isiyofaa, lakini watu wanaoletwa kwa picha katika andiko hili hutoa kwenye madhabahu yasiyofaa. Moja ni mbaya kama ile nyingine. Na madhabahu ya matofali yanaweza kuwa nini ikiwa sio mahali pa ibada ambapo Mungu Mwenyewe hajaamuru pajengwe? {1TG44: 4.1}
Aya ya 4 — “Waketio kati ya makaburi, na kulala katika mahali pao pa siri; walao nyama ya nguruwe, na mchuzi wa vitu vinichukizavyo u katika vyombo vyao.”
Kuketi kati ya makaburi ni kunyimwa kuwa na sehemu katika ufufuo wa watakatifu. Na kulala katika makaburi ni kuishi katika kinachoitwa eti mwamba uliokwezwa wa maisha — wafu kwa Mungu na hai kwa dunia. {1TG44: 4.2}
Wayahudi walikuwa waangalifu mno kwa kile walichokula, lakini hapa upo utabiri wa watu ambao hamu zao ni legevu kama iliyokuwa ya Adamu na Hawa walipokuwa wakila tunda lililokatazwa. {1TG44: 4.3}
Ingawa sisi kama watu hudai kuwa wa msimamo mkali katika kuvizuilia mbali vyakula najisi kutoka kwa meza zetu, andiko
4
hili, hata hivyo, linafunua ukweli wa kuaibisha. Linaarifu kwamba wengi wanapendelea mambo ya machukizo. Katika sehemu moja ya dunia labda wanapendelea chukizo moja, na katika sehemu nyingine ya ulimwengu wanapendelea chukizo lingine. {1TG44: 4.4}
Aya ya 5 — “Watu wasemao, Simama peke yako, usinikaribie mimi, kwa maana mimi ni mtakatifu kuliko wewe; watu hao ni moshi puani mwangu, moto uwakao mchana kutwa.”
Kwa upande mmoja wao ni wasiojali wanavyoweza kuwa, wanakula chochote na kila kitu, kilicho safi na najisi sawa. Na kwa upande mwingine wanayo maoni yao ya juu – hufikiri wenyewe ni watakatifu kuliko wengine wowote. Kwa udhahiri, basi, wale ambao hupendelea machukizo ambayo aya ya nne inazungumzia, ndio hasa wale ambao hupinga kushirikiana na wale ambao hujaribu kuishi maisha yanayopatana na madai yao, wakihofia kwamba matengenezo yanaweza kutukia. Ushetani kweli kweli! Mungu huchukia wanafiki zaidi ya Anavyo-chukia aina nyingine yoyote ya wadhambi. Wale ambao wanasukumwa hivi kulia na kushoto, wanaona utimizo kamili wa andiko hili kwa wakati huu. {1TG44: 5.1}
Aya ya 6, 7 — “Tazama, neno hili limeandikwa mbele yangu. Sitanyamaza, lakini nitalipa, naam, mimi nitawalipa ujira wao vifuani mwao; maovu yenu na maovu ya baba zenu pamoja, asema Bwana, ninyi mliofukiza uvumba juu ya milima, na kunitukana juu ya vilima; basi, kwa ajili ya hayo nitawapimia kwanza kazi yao vifuani mwao.”
Aya ya sita haihitaji maelezo, na ila sentensi kwenye aya ya saba inatosha. Mafarisayo wa jana na Mafarisayo wa leo, kwa mfano, tunaona watapata thawabu sare. {1TG44: 5.2}
5
Aya ya 8, 9 — “Bwana asema hivi, Kama vile divai mpya ipatikanavyo katika kichala, na mtu mmoja husema, Usikiharibu kwa maana mna baraka ndani yake; ndivyo nitakavyotenda kwa ajili ya watumishi wangu, ili nisiwaharibu wote. Nami nitaleta uzao toka Yakobo, na mrithi wa milima yangu toka Yuda, na mteule wangu atairithi, na watumishi wangu watakaa huko.”
Uzao wa Yakobo, mrithi kutoka Yuda, ni, bila shaka Kristo. Wateule, watumwa Wake, ni wale ambao wanaokoka maangamizi yaliyotajwa hapa. Watakuwa baraka kwa wengine. Kunena ki-mfano, milima ni falme za Yuda na Israeli zilizokusanywa pamoja kama ilivyotabiriwa katika Ezekieli 37: 16-28. Lakini ikichukuliwa kwa uhalisi, milima ni ile iliyo katika Nchi ya Ahadi. Kirai, “Mteule Wangu atairithi,” kinabadilisha kitu kutoka kwa wingi “milima” hadi kwa umoja “atairithi”, na hufanya nembo kuyabeba mawazo yote mawili, Ufalme na eneo Lake. Aya ambayo inafuata inathibitisha wazo hili haswa. {1TG44: 6.1}
Aya ya 10 — “Na Sharoni itakuwa zizi la makundi ya kondoo, na bonde la Akori mahali pa kulala ma-kundi ya ng’ombe, kwa ajili ya watu wangu walionitafuta.”
Aya ya tisa na kumi zinatupeleka kutoka kipindi cha Kiyahudi hadi kuingia enzi ya Ukristo, kisha hadi kwenye urejesho na kuunganishawa kwa falme za Yuda na Israeli katika nchi ya baba zetu, Sharoni na Akori. {1TG44: 6.2}
Aya ya 11 — “Bali ninyi ndio mmwachao Bwana, na kuusahau mlima wangu mtakatifu, na kuandaa meza kwa ajili ya hicho kikosi, na kuweka tayari sadaka ya kinywaji kwa idadi hiyo.”
6
Wale watakaoangamizwa ni wale ambao hawajali haswa mlima Wake mtakatifu, Ufalme uliotajwa katika maandiko haya. Ni wale wanaoiandaa meza, au wanaoyakusanya mafungu ya Maandiko yaliyoondolewa katika muktadha wake, na kwayo hulisha (hufundisha) kikundi, au kikosi ambacho kina nia moja kama wao. “Kuweka tayari sadaka ya kinywaji” ni sawa na kusema kwamba kikosi kinakunywa chochote kile ambacho walimu wao hutoa. {1TG44: 7.1}
Aya ya 12 — “Mimi nitawaandikia kuuawa kwa upanga, na ninyi nyote mtainama ili kuchinjwa; kwa sababu nilipoita hamkuitika; niliponena, hamkusikia; bali mlitenda yaliyo mabaya machoni pangu, mlich-agua mambo nisiyoyafurahia.”
Kwa mwito huu wa Mungu hawaitiki. Wala hawamsikii Akiongea, kwa sababu wanao mwelekeo wa kufanya uovu. Hupendezwa katika njia zao wenyewe na huzichukia za Bwana. Kwa dhambi hii wao yawezekana ha-wajui. {1TG44: 7.2}
Aya ya 13-15 — “Kwa hiyo Bwana MUNGU asema hivi, Tazama, watumishi wangu watakula, bali ninyi mtaona njaa; tazama, watumishi wangu watakunywa, bali ninyi mtaona kiu; tazama, watumishi wangu watafurahi, bali ninyi mtatahayarika; tazama, watumishi wangu wataimba kwa furaha ya moyo, bali ninyi mtalia kwa huzuni ya moyo; mtapiga kelele kwa sababu ya uchungu wa roho zenu. Nanyi mtaliacha jina lenu kuwa laana kwa wateule wangu. Na Bwana MUNGU atakuua; naye atawaita watumishi wake kwa jina lingine.”
Hawa watenda maovu hawawezi sasa kutoa hata wazo kwa onyo hili kuu, bali hakika kama vile mchana hu-fuatwa na usiku, jinsi hiyo hakika kwamba hitaji lao, aibu, huzuni na msiba hivi karibuni vitakuja. {1TG44: 7.3}
7
Jina la dhehebu wataliacha kwa watumwa wa Mungu; yaani, kwa wale ambao wataokoka upanga wa Bwana kwa sababu hiyo wataachiwa jina. Jina, hata hivyo, limeachwa tu kama laana, na watumwa Wake wataitwa kwa jina lingine ambalo “kinywa cha Bwana kitanena.” {1TG44: 8.1}
Aya ya 16 — “Hata itakuwa yeye atakayejibariki duniani, atajibariki kwa Mungu wa kweli; naye ataka-yeapa duniani, ataapa kwa Mungu wa kweli. Kwa kuwa taabu za kwanza zimesahauliwa, na kwa kuwa zimefichwa machoni pangu.”
Katika aya hii imeonyeshwa kwamba Bwana anachukua hatua hii ya kushangaza kwa sababu watumishi Wake wasio waaminifu hawajakuwa wakijibariki kwa Mungu wa Kweli. Kwa sababu hiyo, lazima wamekuwa waki-jibariki katika mungu wa uongo; yaani, wamekuwa wakifundisha, kuidhinisha, na kueneza uongo wakati am-bapo Bwana anajaribu kuwabariki watumwa Wake wote kwa Ukweli mpya kutoka kwa kiti Chake cha enzi. Kwa wale ambao wanaukumbatia Ukweli Wake kwa wakati huu, Yeye kamwe hatayakumbuka mambo yao ya zamani. {1TG44: 8.2}
Aya ya 17 — “Maana, tazama, mimi naumba mbingu mpya na nchi mpya, na mambo ya kwanza hayata-kumbukwa, wala hayataingia moyoni.”
Hapa tunaletwa hadi kwa wakati ambao Bwana mwishowe anaiumba upya mbingu na nchi. {1TG44: 8.3}
Aya ya 18, 19 — “Lakini furahini, mkashangilie daima, kwa ajili ya hivi niviumbavyo; maana, tazama, naumba Yerusalemu uwe shangwe, na watu wake wawe furaha. Nami nitaufurahia Yerusalemu, nita-waonea shangwe watu wangu; sauti ya kulia haitasikiwa ndani yake tena, wala sauti ya kuomboleza.”
8
Tunatiwa moyo tufurahi kwa sababu Yerusalemu, pamoja na watu wake, wameumbwa kwa ajili ya shangwe. {1TG44: 9.1}
Aya ya 20 — “Hatakuwapo tena mtoto wa siku chache, wala mzee asiyetimia siku zake; kwa maana mtoto atakufa mwenye umri wa miaka mia; bali mtenda dhambi mwenye umri wa miaka mia atalaaniwa.”
Kuhusu waovu katika nchi iliyoumbwa upya, wanaokuja katika ufufuo wa pili, ufufuo wa wasio haki (Ufu. 20: 5), hakutakuwapo kuzaliwa wala kifo kati yao kwa miaka mia moja. Kwa hivyo watoto wa pekee watakaokuwa kati yao watakuwa wale ambao wamefufuliwa kutoka kwa wafu. Vivyo hivyo wale ambao ni wakongwe na wale ambao ni wachanga watakuwa wameishi miaka mia kuanzia kwa ufufuo wa wasio haki hadi kwa mauti ya pili. Kwa hivyo mtoto na mdhambi, wakiwa na umri wa miaka mia moja katika nchi iliyoumbwa upya, wote wa-takufa mwishoni mwa karne. Kisha wenye haki wataimiliki dunia yote. {1TG44: 9.2}
Aya ya 21, 22 — “Nao watajenga nyumba, na kukaa ndani yake; watapanda mizabibu, na kula matunda yake. Hawatajenga, akakaa mtu mwingine ndani yake; hawatapanda, akala mtu mwingine; maana kama siku za mti ndivyo zitakavyokuwa siku za watu wangu, na wateule wangu wataifurahia kazi ya mikono yao muda wa siku nyingi.”
Tena tunaona kwamba Maisha yanayofuata ni ya kweli na ya asili kama yalivyokuwa Bustani ya Edeni katika siku ile iliyoumbwa. Kwa hivyo ujumbe wa Eliya hakika utayarejeshea mambo yote — yote yaliyopotea kupitia dhambi. {1TG44: 9.3}
Aya ya 23 — “Hawatajitaabisha kwa kazi bure, wala hawatazaa kwa taabu; kwa sababu wao ni wazao wa hao waliobarikiwa na Bwana, na watoto wao pamoja nao.”
9
Kazi yetu nyingi hapa duniani imefanywa bure, na wana na binti zetu pia wamezaliwa bure. Lakini katika nchi iliyoumbwa upya, hakuna yeyote atakayefanya kazi bure, na hakuna kitu kitakachozalishwa kwa shida. {1TG44: 10.1}
Aya ya 24 — “Na itakuwa ya kwamba, kabla hawajaomba, nitajibu; na wakiwa katika kunena, nitasikia.”
Kwa majibu ya baadhi ya sala zetu mara nyingi hungojea muda mrefu, na nyingi ya sala hizo huwa hazijibiwi jinsi tunavyotaka ziwe. Lakini katika inchi iliyofanywa upya hakutakuwapo kuchelewa na kuvunjika moyo. {1TG44: 10.2}
Aya ya 25 — “Mbwa-mwitu na mwana-kondoo watalisha pamoja, na simba atakula majani kama ng’ombe; na mavumbi yatakuwa chakula cha nyoka. Hawatadhuru wala kuharibu katika mlima wangu mtakatifu wote, asema Bwana.”
Itakuwapo amani pande zote. Hatutawaona watu wakigombana wala wanyama wakipigana na mmoja kumla mwenziwe. Itakuwapo amani halisi na kamili kati yao wote. {1TG44: 10.3}
Iwapo tungaliweza kutambua tu yale ambayo Mungu amewaandalia wapendao kusoma Neno Lake na kutembea katika Nuru Yake inayoongezeka daima, basi tungalifanya shughuli ya Mungu iwe shughuli yetu kuu; basi hatungaliweza kupoteza nguvu zetu tena kusumbukia mambo ya maisha haya. Tutaongezewa wakati tunafanya bidii kwa ajili ya kuujenga Ufalme Wake, kwa maana Yeye Mwenyewe husema: “Mtenda kazi anastahili ujira wake.” {1TG44: 10.4}
10
ANDIKO LA SALA
Mtihani Wa Uanafunzi
Nitasoma kutoka katika“Mlima wa Baraka,” kuanzia ukurasa wa 209, aya ya mwisho. {1TG45: 11.1}
“Madai tu wa uanafunzi hayana thamani …. imani ambayo haiongozi kwa utiifu ni kiburi. Mtume Yohana huse-ma, ‘Yeye asemaye, Nimemjua, wala hazishiki amri Zake, ni mwongo, wala kweli haimo ndani yake.’ Yeyote asikuze wazo kwamba majaaliwa maalum au udhihirisho wa kimiujiza utakuwa thibitisho la uhalali wakazi yao au kauli wanazotetea. Wakati watu watazungumza ki-vivi-hivi juu yakuhusu Neno la Mungu, na kuweka chapa, hisia, na mazoea yao juu ya kiwango cha Uungu, tunaweza kujua kwamba hawana nuru ndani yao. {1TG45: 11.2}
“Utiifu ni mtihani wa uanafunzi. Ni utunzaji wa amri ambao huthibitisha uaminifui wa madai yetu ya upendo. Wakati ambapo fundisho tunalopokea linaua dhambi moyoni, huisafisha nafsi kutoka kwa unajisi, huzaa matun-da kwa utakatifu, tunaweza kujua kwamba ni ukweli wa Mungu. Wakati ukarimu, fadhila, moyo wa upole, zi-najidhihirisha katika maisha yetu; wakati furaha ya kutenda haki i mioyoni mwetu; tunapomwinua Kristo, na sio nafsi, tunaweza kujua kwamba imani yetu ni ya utaratibu sahihi. ‘Na katika hili twajua ya kuwa tumemjua Yeye, ikiwa tunashika amri Zake.’ {1TG45: 11.3}
Hebu tuombe kwa ajili ya nguvu ambayo itatuwezesha kuacha kuwa wanafiki, kutoka kuwa wanaodai tu uana-funzi na kuwa wafuasi halisi wa Kristo, kuishi namna Alivyoishi na kutenda kazi – asili hasa ya Ukristo. {1TG45: 11.4}
11
KINA ESAU WENYE UKUU MWINGI NA KINA YAKOBO WASIOJIVUNA
MATINI YA HOTUBA NA V. T. HOUTEFF
MCHUNGAJI WA WADAUDI WAADVENTISTA WA SABATO
SABATO, JUNI 14, 1947
HEKALU LA MLIMA KARMELI
WACO, TEXAS
Tunataka kuichambua sura ya sitini na sita ya Isaya. Katika sura hii Bwana ananena kwa makundi mawili ya wa-tumwa: watumwa hadi kwa utakaso wa patakatifu (Dan. 8:14) — hadi kwa Hukumu ya Walio hai, utakaso wa kanisa (“Shuhuda,” Gombo la 5, uk.80), katika wakati ambapo wanapatikana “wakiwapiga” watumwa wenzao, wakila na kunywa na walevi. Watumishi wengine ni watumwa wa baadaye. Ili kusikia yale Bwana anayo kunena kwa watumwa Wake wa awali unapojongea utakaso, tutaanza uchambuzi wetu na aya mbili za kwanza za sura hiyo. {1TG45: 12.1}
Isa. 66: 1, 2 — “Bwana asema hivi, Mbingu ni kiti changu cha enzi, na dunia ni mahali pa kuweka miguu yangu; mtanijengea nyumba ya namna gani? Na mahali pangu pa kupumzikia ni mahali gani? Maana mkono wangu ndio uliofanya hivi vyote, vitu hivi vyote vikapata kutokea, asema Bwana; lakini mtu huyu ndiye nitakayemwangalia, mtu mhitaji, mwenye roho iliyopondeka, atetemekaye asikiapo neno langu.”
Kwa kusema “mbingu ni kiti Changu cha enzi, na dunia ni mahali pa kuweka miguu Yangu,” Bwana anasema haswa kwamba Yeye hajaiacha dunia; kwamba ingawa kiti Chake cha enzi kiko mbinguni, miguu Yake bado i duniani; ya kwamba bado Anapendezwa na watu Wake. Lakini maswali, “mtanijengea
12
nyumba ya namna gani? Na mahali pangu pa kupumzikia ni mahali gani?” kwa huzuni yanafunua kwamba kazi imepuuzwa, kwamba nyumba wala mahali pa kupumzika hapajaandaliwa kwa ajili Yake. Taarifa ijayo ya Bwana inathibitisha zaidi ukweli huu, kwa maana Anasisitiza kwamba mambo ambayo Yeye amepata yalikuwa tu ni mambo ambayo yalikuwapo sikuzote, na ambayo mkono Wake Mwenyewe, sio mikono ya watumwa Wake, imefanya. {1TG45: 12.2}
Kisha kwa kusema, “Lakini mtu huyu ndiye Nitakayemwangalia, mtu mhitaji, mwenye roho iliyopondeka, ate-temekaye asikiapo Neno Langu,” hakika Yeye anajulisha kwamba watumwa Wake wasio waaminifu wameach-ishwa kazi Yake, na kwamba wengine, wahitaji wenye roho iliyopondeka na watetemekao kwa Neno Lake, wamechukua nafasi zao, kwamba yale watumwa wa awali wameshindwa kufanya, wa mwisho watafanya. Wa-kati huo huo Anawatuhumu watumwa wa awali kwamba hujihisi wamejitajirisha na hawahitaji kitu zaidi; kwamba hawatetemeki kwa Neno Lake. Hivyo, watumwa ambao Watamjengea nyumba na Kumfanyia mahali pa kupumzika, watakuwa watu wahitaji na wa roho iliyopondeka; watu ambao hutetemeka kwa Neno Lake; wa-tu wasio na kiburi na majivuno, ila ambao wanaweza kufundishwa na wanaolizingatia Neno Lake; watu ambao hutubu na kujiona wanahitaji kila kitu badala ya kutohitaji. Mwishowe Bwana anatangaza kwa hasira: {1TG45: 13.1}
Aya ya 3, 4 — “Yeye achinjaye ng’ombe ni kama yeye amwuaye mtu; na yeye atoaye dhabihu ya mwana-kondoo ni kama yeye avunjaye shingo ya mbwa; na yeye atoaye matoleo ni kama yeye atoaye damu ya nguruwe; na yeye afukizaye uvumba ni kama yeye abarikiye sanamu; naam, wamezichagua njia zao wenyewe, na nafsi zao zafurahia machukizo yao. Mimi nami nitachagua mapigo yao, nitaleta hofu zao juu yao; kwa sababu nilipoita, hawakuitika; na niliponena, hawakusikia; bali walifanya yaliyo maovu machoni pangu, na kuyachagua
13
nisiyoyafurahia.”
Haijalishi sadakazinaweza kuwa nzuri au muhimu namna gani, maadamu tunamtumikia Yeye katika njia yetu zawadi na dhabihu zetu ni chukizo Kwake. Njia za mwanadamu mwenyewe lazima ziachwe, hata ingawa itakuwa kazi ngumu kuikabili, ikiwa atataka kufanya amani na Mungu. {1TG45: 14.1}
Hakuna swali ila kwamba sasa Mungu ametuma ujumbe huu wa onyo kwa watumwa Wake wasio waaminifu wenye majivuno, ingawa hawasikii na hawatasikia. Baada ya kusema Alichotaka kusema kwao, sasa Ana-wageukia watumwa Wake wapya aliowaajiri hivi karibuni: {1TG45: 14.2}
Aya ya 5, 6 — “Lisikilizeni neno la Bwana, ninyi mtetemekao kwa sababu ya neno lake; Ndugu zenu wa-wachukiao ninyi, waliowatupa kwa ajili ya jina langu, wamesema, Na atukuzwe Bwana, tupate kuiona furaha yenu; lakini watatahayarika. Sauti ya fujo itokayo mjini! Sauti itokayo hekaluni! Sauti ya Bwana awalipaye adui zake adhabu.”
Baadhi tayari wamepata uzoefu wa kunyanyuliwa nje ya makanisa bila sababu nyingine isipokuwa wamesoma “Fimbo ya Mchungaji,” na kwa kuwa wamesema, “Ninaamini kile huwa Inasema.” Bila shaka, ni ajabu mno kwamba watu waweze kutenda kama mashetani. Hata hivyo ni hivyo, na Mungu Mwenyewe hushuhudia dhidi ya mazoea yao ya ushetani. Hatujionei huruma, na hatuna hasira kwa watesi wetu, lakini tunasikitika juu ya upo-fu, unyonge, umaskini, na uchi wao wa kiroho, kwa maana tunajua kwamba furaha inayokuja itakuwa yetu, na huzuni na aibu na kusaga meno, yao. Hili twajua amini kama vile Yakobo alivyojua ya kwamba Mungu alikuwa pamoja naye katika kukimbia kwake kutoka kwa uso wa Esau. {1TG45: 14.3}
14
Kina Esau wa leo, hata hivyo, hawajui hili. La, hawalijui zaidi kama vile Esau wa zamani hakujua juu ya maono ya Yakobo usiku ya ngazi ambayo ilitandawaa kutoka mbinguni hadi kwenye kitanda cha Yakobo kilicholowa umande. {1TG45: 15.1}
Iwapo sehemu yoyote ya Bibilia imekuwa Ukweli wa sasa, bila shaka ni Isaya 66: 5. Kwa hivyo, kutoka katika mji kuna kelele na ipo sauti kutoka hekaluni dhidi yetu; lakini sauti ya Bwana, ujumbe wa leo, ndio muhimu na unaotatua mambo yote. Unahofia kutupwa nje? au unatetemeka kwa Neno la Mungu? Sasa unatakiwa ufanye uchaguzi wako dhidi ya upinzani iwapo unatarajia kuwa katika Ufalme wa milele. {1TG45: 15.2}
Aya ya 7 — “Kabla hajaona utungu alizaa; Kabla maumivu yake hayajampata, Alizaa mtoto mwana-mume.”
Kwa mwanamke kujifungua mtoto kabla ya kuona utungu na kabla maumivu yake hayajampata, ni jambo la kushangaza — muujiza. Na hivyo ndivyo ilivyotokea kwa kanisa wakati Bwana alizaliwa katika hori la Bethle-hemu: Kanisa halikujua kujiliwa kwake, na ingawa alihisi hitaji la Mwokozi (halikuona utungu), lakini likamzaa mtoto. Lakini kwa mujibu wa aya inayofuata, kanisa katika siku hii litapata muujiza mkubwa kuliko lilivyopata kanisa katika siku ya Kristo: {1TG45: 15.3}
Aya ya 8 — “Ni nani aliyesikia neno kama hili? Ni nani aliyeona mambo kama haya? Je! Nchi yaweza ku-zaliwa siku moja? Taifa laweza kuzaliwa mara moja? Maana Zayuni, mara alipoona utungu, Alizaa wato-to wake.”
Kanisa sasa limejaa magugu, na samaki wabaya na mbuzi. Ni vigumu kuwapata watakatifu. Hata
15
hivyo litawaleta wote kwa wakati mmoja umati wa waongofu ambao hakuna mtu awezaye kuuhesabu. Dhehebu haliamini hili; la, hapana zaidi ya Wayahudi ambao hawakuamini kwamba Mwokozi amezaliwa kwenye hori, wala sio zaidi ya walivyotarajia kwamba wavuvi wa Galilaya wangalizichukua nafasi za makuhani wachaji na za viongozi wa dini waliokwezwa wa siku hiyo, na sio zaidi ya walivyotarajia Mataifa kushiriki katika ahadi za Is-raeli. Dhehebu la leo, pia, hufikiria kwamba kesho itakuwa kama leo, ya kwamba Bwana Mungu amewaacha wanadamu milele wafanye kama watakavyo. Halijui ya kuwa Bwana anachukua mamlaka mikononi Mwake Mwenyewe (“Shuhuda kwa Wachungaji,” uk. 300). Bado linafikiria kwamba ni tajiri na limejitajirisha (Ukweli), wala halihitaji chochote zaidi. Kanisa, hata hivyo, litaona ahadi zote zimetimilika. Litaona kwamba maandiko haya hayamo katika Bibilia kujaza nafasi tu. Mara tu litakapoona utungu na kuhisi hitaji lake, mara hiyo tu nyua zake zitajazwa watakatifu na kazi yake kukamilika. {1TG45: 15.4}
Aya ya 9 — “Je! Mimi nilete wana karibu na kuzaliwa, nisizalishe? Asema Bwana; mimi nizalishaye, je! Nilifunge tumbo? Asema Mungu wako.”
Je! Bwana angalikuwa amezifanya ahadi hizi ikiwa Asingaliweza kuzitimiza? Hili ndilo swali kuu mbele yako, mbele yangu. Na angaliweza kuanzisha kitu ikiwa Yeye hawezi kukitenda na kukimaliza? Usiweze kuyapitia kihivi-hivi maswali haya, kwa maana majibu yako yataamua hatima yako. {1TG45: 16.1}
Aya ya 10-14 — “Furahini pamoja na Yerusalemu, shangilieni kwa ajili yake, ninyi nyote mmpendao; fu-rahini pamoja naye kwa furaha, ninyi nyote mliao kwa ajili yake; mpate kunyonya, na kushibishwa kwa maziwa ya faraja zake, mpate kukama, na kufurahiwa
16
kwa wingi wa utukufu wake. Maana Bwana asema hivi, Tazama, nitamwelekezea amani kama mto, na utukufu wa mataifa kama kijito kifurikacho, nanyi mtapata kunyonya; mtabebwa; na juu ya magoti mtabembelezwa. Mfano wa mtu ambaye mama yake amfariji, ndivyo nitakavyowafariji ninyi; nanyi mta-farijiwa katika Yerusalemu. Nanyi mtaona, na mioyo yenu itafurahi, na mifupa yenu itasitawi kama ma-jani mabichi; na mkono wa Bwana utajulikana, uwaelekeao watumishi wake, naye atawaonea adui zake ghadhabu.”
Hapa tunaambiwa kwamba ni wale tu ambao huomboleza kwa ajili ya Yerusalemu, wale wanaoomba kwa ajili ya kuanzishwa kwa cha uakisi kiti Chake cha ufalme cha Daudi, na ufalme, ndio watakaofurahia pamoja naye. Wao, na wao tu, watanufaika kutokana na wingi wa utukufu wake. Hakuna wengine watakaoshiriki amani yake na utukufu wake mwingi. La, hakuna wengine watakaobembelezwa juu ya magoti yake. Wadhambi hawatafari-jiwa kule Yerusalemu, na uvuguvugu wao utakuwa moto sana na kuwafanya wakimbilie vilima na kwa miamba ya milima (Ufu. 6: 14-17). {1TG45: 17.1}
Ayaya 15-17 — “Maana Bwana atakuja na moto, na magari yake ya vita kama upepo wa kisulisuli; ili atoe malipo ya ghadhabu yake kwa moto uwakao, na maonyo yake kwa miali ya moto. Kwa maana Bwana atateta na wote wenye mwili, kwa moto na kwa upanga wake; nao watakaouawa na Bwana watakuwa wengi. Watu wale wajitakasao, na kujisafisha katika bustani, nyuma yake aliye katikati; wakila nyama ya nguruwe, na machukizo, na panya; watakoma pamoja, asema Bwana.”
Baada ya Mungu kufanya yote Anayoweza kufanya kuielekeza njia ya watumwa Wake, wakati “hakuna tiba” zaidi, basi wakati huo, kisasi cha Mungu kutatekelezwa. Wale wanaoendelea kutembea kwa njia yao wenyewe wakati huo
17
hujipata katika njia pana ambayo hakuna rehema ya Mungu, ambapo Mlipiza kisasi wa haki atachukua idadi Yake. {1TG45: 17.2}
Ni wale ambao hujitakasa na kujisafisha katika bustani nyuma ya mti mmoja (nyuma ya kiongozi); yaani, wana-jifanya kuwa waamini sana katika sehemu zao za kukusanyika, wakiamini kwamba mchungaji atawaongoza hadi kwa Ufalme. Wanajifurahisha katika matumizi ya vyakula vilivyokatazwa na wakati huo huo kwa majivuno wakijifanya kuwa wametakaswa na kutakasika. Kwa Bwana, hata hivyo, wanaonekana kama makaburi yaliyo-pakwa chokaa nyeupe yaliyojaa mizoga iliyooza, kama vikombe ambavyo ni safi kwa nje lakini vichafu ndani. {1TG45: 18.1}
Aya ya 18, 19 — “Nami nayajua matendo yao na mawazo yao; wakati unakuja nitakapokusanya mataifa yote na lugha zote; nao watakuja, nao watauona utukufu wangu. Nami nitaweka ishara kati yao, nami nitawatuma hao waliookoka kwa mataifa, Tarshishi, na Puli, na Ludi, wavutao upinde, kwa Tubali na Yavani, visiwa vilivyo mbali; watu ambao hawajaisikia habari yangu, wala kuuona utukufu wangu; nao watahubiri utukufu wangu katika mataifa.”
Kile ambacho Bwana yu karibu kukitenda hakitafanyika kwa siri. Sio jambo la kufikiria sio kitu kilichofunikwa kwa siri ya kukisia; lakini ni tendo la wazi na bayana mbele ya mataifa yote. {1TG45: 18.2}
Sasa kwa uangamizi wao wenyewe, watu huhoji kwamba huu ni mchinjo wa kiroho, (Ni nini mchinjo wa kiroho? — hakuna ajuaye.) Ingawa ni wazi kuona kwamba hiyo ni Hukumu kwa Walio Hai. Ukweli kwamba kwa zaidi ya karne moja Dhehebu limekuwa likifundisha kuwa Hukumu ya Wafu ni kutenganisha wema kutoka kwa wabaya (magugu na ngano) ubishi
18
wao wa kipumbavu sasa unathibitisha kwamba wao sio tu hawaijui, ila hata ni vipofu sana (Ufu. 3:17) kwamba hata baada ya kuambiwa na kuonyeshwa ni nini hawawezi kuiona! Ingawa wanadai wanajua kuwa Hukumu ni kutenganisha ngano kutoka kwa magugu, wazuri kutoka kwa wabaya, kwamba itapatakasa patakatifu kwa kuyaondoa majina ya wabaya na dhambi za wazuri, hawakubali kwamba tendo hili la kushangaza la Mungu sio kitu pungufu kuliko Hukumu kwa Walio Hai ndani ya nyumba ya Mungu (1 Pet. 4:17), kupatakasa patakatifu (Dan. 8:14), utakaso wa kanisa (“Shuhuda,” Gombo la 5, uk. 80), kulisafisha hekalu (Mal. 3: 1-3). {1TG45: 18.3}
Msiendelee kufarijiana wenyewe kwamba huu mchinjo wa Bwana ni jambo la kubuni, au kwamba utatukia baada ya kufungwa kwa mlango wa rehema. Sasa jitayarishe usije ukaanguka. Usimruhusu mtu yeyote aukengeushe usikivu wako kutoka kwalo. {1TG45: 19.1}
Aya ambayo tumesoma tu inaelezea kwamba wale ambao “wataokoka” upanga wa Bwana, Atawatuma kwa Ma-taifa, kwa wale ambao hawajausikia umaarufu Wake au kuuona utukufu Wake, nao watautangaza utukufu Wake kati ya Mataifa; wataleta katika nyumba ya Bwana wale wote watakaokolewa. Hapa hebu tusome mane-no halisi ya Bwana: {1TG45: 19.2}
Aya ya 20, 21 — “Nao watawaleta ndugu zenu wote kutoka mataifa yote, kuwa sadaka kwa Bwana, juu ya farasi, na katika magari, na katika machela, na juu ya nyumbu, na juu ya wanyama wepesi, mpaka mlima wangu mtakatifu Yerusalemu, asema Bwana; kama vile wana wa Israeli waletavyo sadaka yao nyumbani kwa Bwana katika chombo safi. Na baadhi ya hao nitawatwaa kuwa makuhani na Walawi, asema Bwana.”
Sasa, kwa mtazamo wa ukweli kwamba wale ambao wataokoka mchinjo wa Bwana watatumwa kama wamish-onari,
19
wahubiri, na wachungaji kwa mataifa yote na watu ambao bado hawajamjua Mungu na injili Yake, lipo bali hitimisho hili: kwamba mchinjo unatukia tu kati ya watu wa Mungu; ya kwamba ni Hukumu kwa Walio Hai katika “nyumba ya Mungu” (1 Pet. 4:17); kwamba wachungaji wameuawa kwa sababu wamewaweka kondoo mbali na malisho ya kijani kibichi ya Bwana (Ukweli wa sasa); kwamba walei waaminifu wanachukua nafasi zao; kwamba wakati huo kanisa, “safi kama jua, zuri kama mwezi, na la kutisha kama jeshi lenye mabango,” “linaenda mbele ulimwenguni kote, likishinda na kushinda.” Hivi ndivyo kazi ya injili itamalizika na ulimwengu wa uovu kuletwa kwa kikomo {1TG45: 19.3}
“Wale tu ambao wameyastahimili na kuyashinda majaribu kupitia kwa nguvu zake Mwenye Uwezo wataruhusi-wa kutenda sehemu katika kuutangaza [Ujumbe wa Malaika Watatu] utakapokuwa umeumuka na kuingia katika Kilio Kikuu.” — “Mapitio na Kutangaza,” Novemba. 19, 1908. {1TG45: 20.1}
“… Tumekuwa na maelekeo ya kufikiri kwamba pale ambapo hakuna wachungaji waaminifu, hapawezi kuwa na Wakristo wa kweli; lakini hili sivyo. Mungu ameahidi kwamba pale ambapo wachungaji sio wa kweli atali-simamia kundi mwenyewe. Mungu kamwe hajawahi kulifanya kundi litegemee kabisa vyombo vya kibinadamu. Lakini siku za utakaso wa kanisa zinaharakisha kwa upesi. Mungu atakuwa na watu wasafi na wakweli. Katika kupepetwa kukuu kutakakotukia hivi karibuni, tutaweza vyema zaidi kuupima uthabiti wa Israeli. Ishara zi-naonyesha kuwa wakati unakaribia ambapo Bwana atadhihirisha kwamba pepeto lake li mkononi mwake, naye atausafisha uwanda wake kabisa.” — “Shuhuda,” Gombo la 5, uk. 80. {1TG45: 20.2}
Aya ya 22 — “Kama vile mbingu mpya na nchi mpya, nitakazofanya, zitakavyokaa mbele zangu, asema
20
Bwana, ndivyo uzao wenu na jina lenu litakavyokaa.”
Pamoja na aya hii Uvuvio sasa unaanza kuyafichua mambo ambayo yatatukia katika nchi iliyoumbwa mpya. {1TG45: 21.1}
Aya ya 23 — “Na itakuwa, mwezi mpya hata mwezi mpya, na sabato hata sabato, wanadamu wote wa-takuja kuabudu mbele yangu, asema Bwana.”
Sabato, unaona, ni ya milele kama vile ilivyo dunia. Inastahili kutunzwa sio sasa tu, bali hata baada ya dunia hii iliyolaaniwa na dhambi kuumbwa upya. Na sio sasa tu watu wa Mungu wanapaswa kukusanyika pamoja katika nyumba ya Bwana kila Sabato, lakini wataendelea kufanya hivyo kwa furaha milele yote. {1TG45: 21.2}
Aya ya 24 — “Nao watatoka nje na kuitazama mizoga ya watu walioniasi; maana funza wao hatakufa, wala moto wao hautazimika nao watakuwa chukizo machoni pa wote wenye mwili.”
Ijapokuwa aya zilizotangulia za sura hii hazijachambuliwa sana na yeyote, hizi mbili za mwisho mara nyingi zimejadiliwa na kufanyiwa mdahalo na wengi. Kwa baadhi wanamaanisha kwamba kutakuwa na mateso ya milele. Lakini je! Andiko linaunga mkono wazo kama hilo hata kidogo? — La, hasha. Ufafanuzi wa “mizoga” ni “miili isiyokuwa na uhai.” Na nabii Malaki husema: “Kwa maana, angalieni, siku ile inakuja, inawaka kama ta-nuru; na watu wote wenye kiburi, nao wote watendao uovu, watakuwa makapi; na siku ile inayokuja itawate-keteza, asema Bwana wa majeshi; hata haitawaachia shina wala tawi. Lakini kwenu ninyi mnaolicha jina langu, jua la haki litawazukia, lenye kuponya katika mbawa zake; nanyi mtatoka nje, na kucheza-cheza kama ndama wa
21
mazizini. Nanyi mtawakanyaga waovu; maana watakuwa majivu chini ya nyayo za miguu yenu; katika siku ile niifanyayo, asema Bwana wa majeshi.” Mal. 4: 1-3. {1TG45: 21.3}
Mizoga mwanzoni na majivu mwishowe ya watumwa wasio waaminifu wakiwa chini ya miguu ya watakatifu, haiwezi kuashiria kwamba wasio waaminifu wamesukumwa katika “moto wa jahanamu,” humo kuishi milele. Zaidi ya hayo kwa sababu wenye haki tu wanapewa uzima wa milele, basi waovu lazima wapewe kifo cha milele. Isitoshe, “mauti ya pili” (Ufu. 20: 14) haiwezi kumaanisha “uzima wa pili.” {1TG45: 22.1}
Dhana ya mateso ya milele imetokana kijujuu na ukweli kutoka kwa taarifa, “funza wao hatakufa.” “Funza wao,” funza ambaye hula mizoga yao, ingawa, haiwezi kumaanisha nafsi za watu. Angalau haiwezi kumaanisha hivyo kwake yeye ambaye huchimba kwa kina ndani ya kisima cha wokovu, na anayeweza kufikiri na kutumia akili mwenyewe. Mtu kama huyo husoma kati ya mistari na huandika thamani kamili ya kila neno. Ikiwa “funza” hu-maanisha chochote, basi humaanisha kwamba funza hupanda juu ya mzoga, kwamba ni chombo ambacho hu-punguza sehemu za mizoga kuwa vipengee vyake vya asili. Kwa kweli, “funza wao hatakufa”; hakika atatimiza kazi yake ya kula; mizoga Yeye atairudisha kwa mavumbi, “kwa maana u mavumbi wewe,” andiko lasema, “na-we mavumbini utarudi.” Mwa. 3:19. Ni chombo cha kusambaratisha, funza anayekula ambaye hafi. Zaidi ya hayo, tunaambiwa kwamba nafsi itendayo dhambi, itakufa. (Ezek. 18: 4). {1TG45: 22.2}
Inaonekana wazi kwamba mahubiri ya mateso ya milele katika moto wa kuzimu badala ya kifo cha milele, hu-chochewa na walaghai waitwao eti waongoaji wa nafsi
22
wakijaribu kuwaongoza wasikilizaji wao kanisani kwa kuwatisha. Lakini iwapo wangalijua kwamba ni walioza-liwa mara ya pili tu kupitia kuupenda Ukweli ndio wanapewa haki ya kuingia katika Mji Mtakatifu, iwapo wan-galijua kwamba wale ambao lazima watishwe ili kuingia ndani wametengwa nao, ikiwa wangalijua kuwa kitu chochote ambacho hufanya uwongo pia hakijapewa haki ya kuingia ndani yake, — iwapo wao wangaliyajua haya yote kwa moyo wote, labda wangaliacha kuhubiri uzima wa milele katika moto wa jahanamu, na kuanza kuhubiri upendo wa milele wa Ukweli. Hebu sasa tufunge uchambuzi wetu kwa kusoma ombi la mwisho la Bwana: {1TG45: 22.3}
“Kesheni basi; kwa maana hamjui ni siku ipi atakayokuja Bwana wenu. Lakini fahamuni neno hili; kama mwenye nyumba angaliijua ile zamu mwivi atakayokuja, angalikesha, wala asingaliiacha nyumba yake kuvun-jwa. {1TG45: 23.1}
“Kwa sababu hiyo ninyi nanyi jiwekeni tayari; kwa kuwa katika saa msiyodhani Mwana wa Adamu yuaja. Ni nani basi yule mtumwa mwaminifu mwenye akili, ambaye bwana wake alimweka juu ya nyumba yake, awape watu chakula kwa wakati wake? Heri mtumwa yule, ambaye bwana wake ajapo atamkuta akifanya hivyo. Amin, nawaambieni, atamweka juu ya vitu vyake vyote. {1TG45: 23.2}
“Lakini mtumwa yule mbaya akisema moyoni mwake, Bwana wangu anakawia; akaanza kuwapiga wajoli wake, na kula na kunywa pamoja na walevi; bwana wake mtumwa huyo atakuja siku asiyodhani, na saa asiyojua, ata-mkata vipande viwili, na kumwekea fungu lake pamoja na wanafiki; ndiko kutakuwako kilio na kusaga meno.” Mat. 24: 42-51. {1TG45: 23.3}
Lipo chaguo moja tu sahihi kwa ajili yako kufanya, na hilo ni kukataa kushirikiana na kina Esau wenye ukuu mwingi, na kujiunga na kina Yakobo wasiojivuna waliojaa Ukweli. {1TG45: 23.4}
23
Jumuiya ya Wadaudi Waadventista wa Sabato
(Ushirika Huru Unaojumuisha Kanisa)
Mlima Karmeli, Waco, Texas
S.L.P. 23738, Waco, TX 76702
+ 1-254-855-9539
www.gadsda.com
info@gadsda.com
Gombo la 1, Namba 44, 45
Kimechapishwa nchini Marekani
24