20 Jul Gombo la 1 Salamu Mwafaka Namba 39, 40, 41
Gombo la 1 Salamu Mwafaka Namba 39, 40, 41
AMANI YA PEKEE YA MAWAZO
Hati miliki, Kimechapishwa tena 1953
Haki zote zimehifadhiwa
V. T. HOUTEFF
WATOTO WA ALIYE TASA NI WENGI KULIKO WATOTO WA MWANAMKE ANAYEZAA
ZAYUNI KATIKA UPEO WA UTUKUFU WAKE
MATUNDA YAKE ALIYETIWA-MAFUTA
1
ANDIKO LA SALA
Nitasoma kutoka katika “Mlima wa Baraka,” ukurasa wa 140, kuanzia aya ya kwanza. {1TG39: 2.1}
“Njia ya wakosaji ni ngumu,’ lakini njia za hekima ‘ni njia za kupendeza sana, na mapito yake yote ni amani. “Ki-la tendo la utiifu kwa Kristo, kila tendo la kujinyima kwa ajili Yake, kila jaribu lililohimiliwa vyema, kila mtu ushindi uliopatikana juu ya majaribu, ni hatua ya kwenenda kwa utukufu wa ushindi wa mwisho. Ikiwa tutam-chukua Kristo kuwa mwongozi wetu, Atatuongoza salama …. {1TG39: 2.2}
“Njia inaweza kuparuza, na mwinuko mkali; inaweza kuwa na mitego kwa mkono wa kulia na wa kushoto; tun-aweza hitajika kuvumilia kazi katika safari yetu; tunapokuwa na uchovu, tunapotamani kupumzika, tunaweza hitajika kuendelea kufanya kazi; tunapozimia, tunaweza hitajika kupigana; tunapovunjika moyo, lazima tuende-lee kutumaini; ila pamoja na Kristo kama mwongozi wetu, hatutashindwa kufikia bandari tuliyoitumaini mwishowe ….” {1TG39: 2.3}
Kwa mujibu wa andiko tunapaswa kuomba kwa ajili ya hekima na kwa azimio la kutembea katika njia za Bwa-na. Njia Zake tu ni za kupendeza na za amani. Tunapolazimika kujikana wenyewe kitu, au tunapolazimika kuhi-mili jaribu ili kuupata ushindi juu ya jaribu, tunapaswa kuhisi kwamba hizi ni hatua za kufikia ushindi wa mwi-sho. Na tunapaswa kuona kwamba kuishi maisha ya dhambi ni, kwa mfano, kuishi chini kwenye poromoko, chi-ni ambapo kwa kawaida tunajikuta tangu kuzaliwa. Ili kuishi kileleni kwa mlima (Ufalme) lazima mtu, kwa mfa-no, apande mwinuko mkali na njia inayoparuza ya mlima. Kuipanda njia inaweza kuonekana kuwa ngumu, lakini baada ya hatua ya mwisho kufanyika na kilele cha mlima kufikiwa, inakuwa furaha na starehe, ujasiri na ushindi ambao hakuna lugha inayoweza kuelezea. {1TG39: 2.4}
2
WATOTO WA ALIYE TASA NI WENGI KULIKO WATOTO WA MWANAMKE ANAYEZAA
MATINI YA HOTUBA NA V. T. HOUTEFF
MCHUNGAJI WA WADAUDI WAADVENTISTA WA SABATO
SABATO, MEI 3, 1947
HEKALU LA MLIMA KARMELI
WACO, TEXAS
Kabla tuanze somo letu la Isaya hamsini na nne aya kwa aya, tutasoma aya ya kwanza. {1TG39: 3.1}
Isa. 54: 1 — “Imba, wewe uliye tasa, wewe usiyezaa; paza sauti yako kwa kuimba, piga kelele, wewe usiyekuwa na utungu; maana watoto wake aliyeachwa ni wengi kuliko watoto wake yeye aliyeolewa, ase-ma Bwana.”
Wanawake wawili wameletwa hapa kwa mtazamo: Mmoja ni tasa, na mwingine la. Mwanamke aliye tasa anati-wa moyo aanze kuimba, kwa maana ameahidiwa kuwa na watoto wengi zaidi kuliko yule aliye na watoto. Ili kujifunza wanawake hawa ni nani, hebu tufungue sura ya nne ya Wagalatia. {1TG39: 3.2}
“Kwa maana imeandikwa ya kuwa, Abrahamu alikuwa na wana wawili mmoja kwa mjakazi, na mmoja kwa mwungwana. Lakini yule wa mjakazi alizaliwa kwa mwili, yule wa mwungwana kwa ahadi. Mambo haya husemwa kwa mfano; kwa maana hawa ndio kama maagano mawili, moja kutoka mlima Sinai, lizaalo kwa utumwa, ambalo ni Hajiri.” Gal. 4: 22-24. {1TG39: 3.3}
Mtume Paulo anatukumbusha kwamba Abrahamu alikuwa na wake wawili na wana wawili. Sote tunakijua kisa hiki, kwamba wakati
3
Mungu alimwita Abrahamu aondoke katika nchi yake na aende katika nchi asiyoijua, Mungu aliahidi kumpa mtoto wa kiume. Yapata miaka ishirini na tano ilipita na bado kuwasili kwa mwana hakukuonekana. Wakati huo Sara alikuwa karibu miaka tisini (Mwa. 17:17). Katika miaka hiyo ya Abrahamu na Sara kumngojea mtoto, Hajiri akawa mke wa Abrahamu na kupitia kwake Ishmaeli alizaliwa. Sara, kwa hivyo, ndiye yule mwanamke tasa (aliyeachwa pekee), na Hajiri ndiye aliye na mume. Kwa hivyo, Isaya 54: 1 inazungumza ki-mfano juu ya wanawake hawa wawili na watoto wao. Kama kwa mfano huu ni nini, Mtume anaelezea: — {1TG39: 3.4}
“Maana Hajiri ni kama mlima Sinai ulioko Arabuni, umelingana na Yerusalemu wa sasa; kwa kuwa anatumika pamoja na watoto. Bali Yerusalemu wa juu ni mwungwana, naye ndiye mama yetu sisi.” Gal. 4:25, 26. {1TG39: 4.1}
Hajiri huwakilisha Yerusalemu, mji wa Wayahudi, waliozaliwa kwa mwili, ilhali Sara huwakilisha Yerusalemu ambao unakuja, mji wa “waliozaliwa mara ya pili,” watoto wa ahadi. {1TG39: 4.2}
“Kwa maana imeandikwa, Furahi, wewe uliye tasa, usiyezaa; Paza sauti, ulie, wewe usiye na utungu; Maana wa-toto wake aliyeachwa pekee ni wengi Kuliko wa huyo aliye na mume. Basi, ndugu zangu, kama Isaka sisi tu wa-toto wa ahadi. Lakini kama vile siku zile yule aliyezaliwa kwa mwili alivyomwudhi yule aliyezaliwa kwa Roho, ndivyo ilivyo na sasa. Lakini lasemaje andiko? Mfukuze mjakazi na mwanawe, kwa maana mwana wa mjakazi hatarithi kabisa pamoja na mwana wa mwungwana. Ndiposa, ndugu zangu, sisi si watoto wa mjakazi, bali tu watoto wa huyo aliye mwungwana.” Gal. 4: 27-31. {1TG39: 4.3}
Uvuvio hufanya wazi kwamba ki-mfano Hajiri
4
na mwanawe, Ishmaeli, huwakilisha kanisa katika kipindi cha Agano la Kale, na kwamba Sara na mwanawe, Isaka, wanawakilisha kanisa katika kipindi cha Agano Jipya. Washiriki wa kanisa la Agano la Kale hakika walikuwa wa ki-mwili, kwa maana walijumuisha kila mtu aliyezaliwa kutoka kwa nasaba ya Yakobo; lakini washiriki wa kanisa la Agano Jipya, haswa wale wanaoonyeshwa hapa, ni watu ambao kwa Roho wa Kweli wameongoka kwa Kristo. Na kama haikuwezekana Isaka kuzaliwa kwa mapenzi ya mwili, hivyo tu haiwezekani kwa watoto hawa wa Roho wa Kweli kuzaliwa kwa mapenzi ya wanadamu. {1TG39: 4.4}
Sababu ya Mungu kuchelewesha kuitimiza ahadi Yake kwa Sara, kwa hivyo, ni dhahiri sana: Alikuwa akiandika historia na unabii kwa maisha ya familia ya Abrahamu. Alisababisha kuzaliwa kwa Ishmaeli kwa kuchelewesha kuzaliwa kwa Isaka. Ishmaeli, kwa hivyo, mfano wa Waebrania, watoto wa ki-mwili, walimtangulia Isaka, mfa-no wa Wakristo, watoto wa ahadi. {1TG39: 5.1}
Shauku yetu kuu, hata hivyo, ni kujua wakati ambao Isaya 54 inapata utimizo wake wote na kizazi ambacho un-abii wake wa ki-mfano unakihusu hasa, kujua ikiwa uliandikwa haswa kwa manufaa kwa kanisa la kwanza la Kikristo, kwa kanisa katika Vizazi vya Kati, au kwa kanisa katika wakati wetu. Kwa kuwa hakuna hata mmoja wa waandishi wa Agano Jipya hutoa maelezo isipokuwa kwa aya ya kwanza ya Isaya 54, bila shaka sura hiyo haikuandikwa hasa kwa watu wa wakati huo. Zaidi ya hayo, aya ya kumi na nne inathibitisha zaidi wakati am-bao unabii huo unahusu. {1TG39: 5.2}
“Utathibitika katika haki; utakuwa mbali na kuonewa, kwa maana hutaogopa;
5
na mbali na hofu, kwa maana haitakukaribia.” Isa. 54:14. {1TG39: 5.3}
Ahadi kwa sehemu hii ya mwisho ya kanisa la Kikristo ni kwamba litakuwa mbali na kukandamizwa (halita-tawaliwa na watu wengine); kwamba hofu haitalikaribia; na kwamba halitakuwa na haja ya kuogopa. Kwa mta-zamo wa ukweli kwamba kanisa hapo awali halijawahi kuwa huru kwa lolote la haya, akili inahukumu kwamba bado litatambua ahadi hizi. Kwa hivyo, kizazi ambacho kimeelekezewa sura hii, kanisa ambalo litapokea ahadi hizi sio katika siku za zamani, ila katika siku zijazo. Na ukweli kwamba Uvuvio sasa kwa mara ya kwanza unazi-funua ahadi hizi zilizofichwa kwa muda mrefu, na sasa unazileta kwa usikivu, unazifanya kuwa “chakula kwa wakati wake,” ukweli ni dhahiri: kanisa, baada ya tangazo hili kufanya kazi yake, hivi karibuni litaingia katika kipindi hiki kitukufu cha wakati. Aidha, aya ya kumi na tano inasema: {1TG39: 6.1}
“Tazama, yamkini watakusanyana; lakini si kwa shauri langu. Watu wo wote watakaokusanyana juu yako wa-taanguka kwa ajili yako.” Isa. 54:15. {1TG39: 6.2}
Hapa ameonywa kwamba maadui zake watakusanyika pamoja dhidi yake, lakini sio na Bwana. Kwa hivyo, ha-watafanikiwa, lakini wataanguka kwa ajili yake. Maadui zake hawataweza kamwe kumchukua yeyote wa washiriki wake uhamishoni, sio gerezani, au kwa miali ya moto, au kwa mapango ya hayawani — hatamwona tena Mwashuri au Wakaldayo wakifanikiwa dhidi yake; Wala hataendelea tena kuteswa na Wayahudi na Warumi. Yote haya sasa yamepita na yakitukia tena hayatakuwa na athari kwake. {1TG39: 6.3}
“Tazama, nimemwumba mhunzi avukutaye moto wa makaa, akatoa
6
silaha kwa kazi yake; nami nimemwumba mharibu ili aharibu. Kila silaha itakayofanyika juu yako haitafanikiwa na kila ulimi utakaoinuka juu yako katika hukumu utauhukumu kuwa mkosa. Huu ndio urithi wa watumishi wa Bwana, na haki yao inayotoka kwangu mimi, asema Bwana.” Isa. 54:16, 17. {1TG39: 6.4}
Mpaka sasa, silaha ziliyofanyika dhidi ya kanisa zimefanikiwa, lakini kanisa hapa katika unabii litalindwa. Na likiwa kabisa mkononi mwa Mungu, kila mtu atakayeinuka dhidi yake katika hukumu litamhukumu kwa Ukweli na haki. Uwepo na kufaulu kwetu katika kazi ya Mungu, kwa hivyo, sio fumbo tena: Unabii unabainishia wazi kwamba wengi wanainuka dhidi yetu, ila hakuna ambaye amefanikiwa na kamwe atakayefanikiwa. Mungu ali-yemuumba mhunzi na mharabu wa kuharibu, anao uwezo pia kuumba amani na usalama. Roho ya Unabii inasisi-tiza hivi: {1TG39: 7.1}
“Watakatifu walipokuwa wakiondoka mijini na vijijini, walikimbizwa na waovu, ambao walitaka kuwaua. Lakini panga zilizoinuliwa kuwaua watu wa Mungu zilivunjika na kuanguka kwa udhaifu kama nyasi. Malaika wa Mungu waliwakinga watakatifu. Walipokuwa wakilia mchana na usiku ili kuokolewa, kilio chao kilikuja mbele ya Bwana.” — “Maandishi ya Awali,” uk. 284, 285. {1TG39: 7.2}
“… Lakini watu Wake wakisalia wamejitenga na kuwa tofauti mbali na dunia, kama taifa ambalo hutenda haki, Mungu atakuwa ulinzi wao, na hakuna silaha zitakazopangwa dhidi yao zitafanikiwa.” — “Shuhuda,” Gombo la 5, uk. 601. {1TG39: 7.3}
Somo liko wazi: Kanisa linaibuka kutoka kwa kipindi kimoja na kujiunga kuingia kingine. Liko mwanzoni mwa alfajiri ya siku mpya. Utukufu wake sasa utadhihirishwa,
7
kazi yake kubwa kukamilika, na watoto wake wote (umati mkubwa) kuokolewa. Badala ya maadui zake kul-ishinda, litashinda dhidi yao. {1TG39: 7.4}
Kwa sababu kanisa, kwa ujumla, hapa limewakilishwa na wote mama na watoto, tunapaswa kujua ni sehemu gani ya kanisa inayowakilishwa na mama na sehemu ipi na watoto. {1TG39: 8.1}
Kwa mujibu wa aya ya kumi na saba, sura hiyo inahitimisha kwamba “watumwa wa Bwana,” wale ambao hu-waleta waongofu, hujumuisha mama, na waongofu wao, walei, hujumuisha watoto. {1TG39: 8.2}
Je! Ni nini maana ya yeye kuwa na utungu wa kuzaa? — Kwa ajili ya jibu hebu turejee kwa Wagalatia 4:19: “Wa-toto wangu wadogo, ambao kwamba nawaonea utungu tena mpaka Kristo aumbike ndani yenu….” Wale ambao kwa ajili yao mtume Paulo alikuwa akitenda kazi ili kumleta Bwana kwa ufahamu wao, anasema kwamba alikuwa katika utungu wa kuzaa kwa ajili yao hadi Kristo aumbike ndani yao, hadi waongoke kikamilifu kwake – wazaliwe mara ya pili. {1TG39: 8.3}
Sasa kwa kuwa tunauelewa mfano wa wanawake hawa wawili, na wa watoto wao, pia wakati ambao Isaya 54 iliandikwa kutimia, tutaichambua sura hiyo aya kwa aya katika mapana yake yote kadiri Mungu anavyoruhusu. {1TG39: 8.4}
Isa. 54: 2, 3 — “Panua mahali pa hema yako, na wayatandaze mapazia ya maskani yako; usiwakataze; ongeza urefu wa kamba zako; vikaze vigingi vya hema yako. Kwa maana utaenea upande wa kuume na upande wa kushoto; na wazao wako watawamiliki mataifa; wataifanya miji iliyokuwa ukiwa kukaliwa na watu.”
Maneno haya yote — kupanua, kutandaza, usiwakataze, kuongeza urefu, na kukaza — yanamaanisha kufanya kila linalowezekana
8
sasa kukidhi hali hiyo, kufanya makao kwa ajili ya idadi kubwa ya waongofu, kufanya kila linalowezekana sasa ili wakati unapokatika upande wa kulia na kushoto, wakati umati wa waongofu unapoanza kumiminika ndani, usifadhaike na kutoweza kutoa makao. Usiwavunje moyo watu. Na zaidi ya hayo, anahakikisha Bwana: “na wazao wako watawamiliki mataifa; wataifanya miji iliyokuwa ukiwa kukaliwa na watu.” Unabii huu, kwa hivyo, unatuleta kwa siku za kurejeshwa kwa mambo yote (Mat. 17:11). {1TG39: 8.5}
Aya ya 4 — “Usiogope; maana hutatahayarika; wala usifadhaike; maana hutaaibishwa; kwa kuwa utaisahau aibu ya ujana wako, pia mashutumu ya ujane wako hutayakumbuka tena.”
Naam, amehakikishiwa kwamba hahitaji tena kuhofu, hahitajiki kutupwa katika machafuko na kiwewe tena, kwamba atasahau kulaimiwa na ujane wake (Mungu kumwacha). {1TG39: 9.1}
Aya ya 5 — “Kwa sababu Muumba wako ni mume wako; Bwana wa majeshi ndilo jina lake; na Mtakati-fu wa Israeli ndiye Mkombozi wako; Yeye ataitwa Mungu wa dunia yote.”
Maadui zetu wanaweza kusema chochote wanachotaka, lakini Mungu mwenyewe anashuhudia kwamba Yeye ndiye Mungu wetu, Mungu aliyetuumba, Mkombozi, Mungu wa dunia yote. {1TG39: 9.2}
Aya ya 6, 7 — “Maana Bwana amekuita kama mke aliyeachwa na kuhuzunishwa rohoni, kama mke wa-kati wa ujana, atupwapo, asema Mungu wako. Kwa kitambo kidogo nimekuacha; lakini kwa rehema nyingi nitakukusanya.”
9
Taarifa, “kwa kitambo kidogo nimekuacha,” ikiwa imewekwa kinyume cha taarifa, “lakini kwa rehema nyingi nitakukusanya.” inaonyesha kwamba Mungu kumwacha ni kutawanywa kwake kati ya Mataifa, na kwamba ku-kusanywa kwake ni kurejea kwake katika nchi yake, kuimiliki miji iliyo ukiwa. {1TG39: 10.1}
Aya ya 8, 9 — “Kwa ghadhabu ifurikayo nalikuficha uso wangu dakika moja; lakini kwa fadhili za milele nitakurehemu, asema Bwana, Mkombozi wako. Kwa maana jambo hili limekuwa kama maji ya Nuhu kwangu; maana kama nilivyoapa ya kwamba maji ya Nuhu hayatapita juu ya dunia tena, kadhalika nimeapa ya kwamba sitakuonea hasira, wala kukukemea.”
Yale ambayo amekwisha yapitia hatayapitia tena, — ahadi ya uhakika kama ilivyokuwa kwa Nuhu: “Mimi nau-weka upinde wangu winguni, nao utakuwa ni ishara ya agano kati yangu na nchi.” Mwa. 9:13. {1TG39: 10.2}
Aya ya 10, 11 — “Maana milima itaondoka, na vilima vitaondolewa; bali wema wangu hautaondoka kwako, wala agano langu la amani halitaondolewa; asema Bwana akurehemuye. Ewe uliyeteswa, uli-yerushwa na tufani, usiyetulizwa, tazama, nitaweka mawe yako kwa rangi nzuri, nitaweka misingi yako kwa yakuti samawi.”
Je! Ni nini kingine ambacho “mawe” yake yanaweza kuwakilisha iwapo sio kwa ajili ya washirika wake (wato-to)? Je! Misingi yake inaweza kuashiria nini iwapo sio Mitume wake (waasisi), wale ambao Bwana huwatumia kwa kazi ya uamsho na matengenezo? Kama huu ulikuwa upendeleo wa mitume kumi na wawili mwanzoni mwa kanisa la Kikristo. Kwa kuutambua ukweli huu mtukufu, Uvuvio uliandika: {1TG39: 10.3}
“Na ukuta wa mji ulikuwa na misingi kumi na miwili, na katika ile misingi majina kumi na mawili ya wale mi-tume kumi na wawili wa Mwana-Kondoo.” Ufu. 21:14. {1TG39: 11.1}
10
Taarifa, “nitaweka misingi yako kwa yakuti samawi,” inaashiria kwamba sasa ameanzishwa, ya kuwa Bwana sasa anajenga kuanzia chini kwenda juu. {1TG39: 11.2}
Aya ya 12 — “Nami nitaifanya minara yako ya akiki nyekundu, na malango yako ya almasi, na mipaka yako yote ya mawe yapendezayo.”
Ikiwa utumizi halisi wa madirisha ni kutoa nuru na hewa, basi nembo hii inaweza kumaanisha nini ikiwa sio “waonaji” wake, wale wanaoleta nuru na Ukweli kwa kanisa la Mungu? Na iwapo malango halisi hutumika kuzuilia nje vitu visivyofaa, basi katika ufalme wa kiroho lazima lazima yawakilishe walinzi wake, ukasisi. {1TG39: 11.3}
Ni mfano wa ajabu kama nini! Ni kama nini kikundi cha watu waliotakaswa ambao unaonyesha kwa udhahiri! — Mawe ya rangi nzuri, na misingi ya yakuti samawi, madirisha ya lulu, malango ya almasi, na mipaka yake yote ya mawe ya kupendeza! kila nafsi kito! “Nitafanya wanadamu kuadimika kuliko dhahabu safi, na watu kuliko dha-habu ya Ofiri.” Isa. 13:12. {1TG39: 11.4}
“Kwa ajili ya Zayuni” asema BWANA, “ sitanyamaza, na kwa ajili ya Yerusalemu sitatulia, hata haki yake itaka-potokea kama mwangaza, na wokovu wake kama taa iwakayo. Na mataifa wataiona haki yako, na wafalme wote watauona utukufu wako; nawe utaitwa jina jipya, litakalotajwa na kinywa cha Bwana. Nawe utakuwa taji ya uzuri katika mkono wa Bwana, na kilemba cha kifalme mkononi mwa Mungu wako. Hutaitwa tena Ali-yeachwa, wala nchi yako haitaitwa
11
tena, Ukiwa; bali utaitwa Hefsiba; na nchi yako Beula;kwa kuwa Bwana anakufurahia ,na nchi yako itaolewa.” Isa. 62: 1-4. {1TG39: 11.5}
Sasa inaonekana wazi wazi kwamba Ulaodekia utatoweka milele, kwamba Mungu atakuwa na kanisa lisilokuwa na doa, kunyanzi, au kitu chochote kama hicho. Huwezi kumudu kuachwa nje yake. Lazima ujiunge na watetezi wa Ukweli huu iwapo unataka kuwa sehemu ya vuguvugu hili tukufu. {1TG39: 12.1}
Aya ya 13-17 — “Na watoto wako wote watafundishwa na Bwana; na amani ya watoto wako itakuwa nyingi. Utathibitika katika haki; utakuwa mbali na kuonewa, kwa maana hutaogopa; na mbali na hofu, kwa maana haitakukaribia. Tazama, yamkini watakusanyana; lakini si kwa shauri langu. Watu wo wote watakaokusanyana juu yako wataanguka kwa ajili yako. Tazama, nimemwumba mhunzi afukutaye moto wa makaa, akatoa silaha kwa kazi yake; nami nimemwumba mharabu ili aharibu. Kila silaha itakayofan-yika juu yako haitafanikiwa na kila ulimi utakaoinuka juu yako katika hukumu utauhukumu kuwa mkosa. Huu ndio urithi wa watumishi wa Bwana, na haki yao inayotoka kwangu mimi, asema Bwana.”
Kwa uwazi tu wazembe kushawishika kwamba Mungu Mtukufu wa Yakobo anaweza kutulinda na kutukinga na maovu yote vinginevyo Yeye asingalikuwa anajaribu mara kwa mara kutuhakikishia uwezo wake kwa kufafanua zaidi kwamba kwa vile Yeye amemuumba “mhunzi” Na “mharabu” na amewaruhusu wafanye kazi, vivyo hivyo Yeye anao uwezo wa kuvifanya vyombo na juhudi zao kuwa bila faida. Ushawishi wa Mungu, unaona, ni kwamba hata mtoto mdogo anaweza kuelewa. {1TG39: 12.2}
12
Ahadi hizi zote ni urithi wa watumwa wa Bwana. Je! Tunawezaje kumudu kuziacha zitoweke? Je! sio za bei rahisi vya kutosha? Kwa sababu zinagharimu imani tu, hebu basi tuamini na zitakuwa zetu milele. {1TG39: 13.1}
Tumejifunza sasa kwamba wake wawili wa Abrahamu na wana wawili ni utabiri ki-mfano wa makanisa ya Agano la Kale na Jipya; kwamba kuwasili kwa Ishmaeli kuliwakilisha kimbele Israeli wa asili na kwamba ku-wasili kwa Isaka kuliwakilisha kimbele Israeli wa kiroho, Wakristo; kwamba Ishmaeli alivyomtesa Isaka ulikuwa utabiri wa Wayahudi kuwatesa Wakristo; kwamba tendo la Abrahamu kumnyima urithi na kumfurusha Hajiri na mtoto wake kutoka nyumbani, lilitabiri tendo la Mungu kuwaondolea mbali na kuwanyima urithi Israeli wa mwili — kwamba ni wale tu “waliozaliwa mara ya pili,” waliozaliwa kwa Roho, ndio watakaourithi Ufalme; kwamba Isaka, aliyekuja katika ulimwengu huu tu kwa uwezo wa Mungu, aliwakilisha kimbele kanisa la Kikris-to, lakini haswa kanisa la Ufalme linalokuja hivi karibuni ambalo halitakuwamo Mwishmaeli — hakuna mtu ata-kayeletwa ndani kwa mapenzi ya mwili — hamna “magugu,” hamna “samaki wabaya,” hamna “mbuzi” — wa-takatifu tu, “wale tu wanaopaswa kuokolewa,” na hakuna mtu anayeweza kuwa kama “wale tu wanaopaswa kuokolewa” iwapo hayaamini yale ambayo Neno husema, ikiwa yeye hauchukui msimamo wake kwa upande wa Ukweli. Wale tu walio na njaa ya Ukweli na haki watajazwa na kuwa vyombo vyake vya thamani, watafaa ku-wa sehemu ya jengo hili la Kito. “Nao watakuwa wangu, asema Bwana wa majeshi, katika siku ile niifanyayo vito Vyangu; naam, watakuwa hazina yangu hasa; nami nitawaachilia, kama vile mtu amwachiliavyo mwanawe mwenyewe amtumikiaye. Ndipo mtakaporudi, nanyi mtapambanua kati ya wenye haki na waovu, na kati ya yeye amtumikiaye Mungu na yeye asiyemtumikia.” Mal. 3: 17,18. Ni jambo la kutisha kutoliamini Neno la Mun-gu, au kuwa asiye na msimamo, wa kusitasita na mzembe. {1TG39: 13.2}
13
WAZO LA SALA
Vita Na Mwendo
Tutasoma kutoka katika “Mlima wa Baraka,” ukurasa wa 141, kuanzia aya ya pili. {1TG40: 14.1}
“Maisha ya Kikristo ni vita na mwendo. Lakini ushindi unaopatikana hauvutwi na uwezo wa kibinadamu. Shamba la vita ni uwanja wa moyo …. Utu wa kale, uliozaliwa kwa damu na kwa mapenzi ya mwili, hauwezi kuurithi ufalme wa Mungu. Maelekeo ya kurithi, tabia za zamani lazima ziachwe. {1TG40: 14.2}
“Yeye ambaye huazimia kuingia katika ufalme wa kiroho atapata kwamba nguvu na tamaa zote za asili isiyoongoka, zikiungwa mkono na nguvu za ufalme wa giza, zimekusanyika dhidi yake. Ubinafsi na kiburi vi-tasimama dhidi ya kitu chochote kitakacho onyesha kwamba wao ni wadhambi. Hatuwezi, sisi wenyewe, kushinda tamaa na tabia za uovu ambazo hujitahidi kufanikiwa. Hatuwezi kumshinda adui hodari ambaye hu-tushikilia katika utumwa wake. Mungu pekee ndiye anayeweza kutupatia ushindi. Anayo shauku tuwe na uwezo wa kushinda juu yetu, juu ya mapenzi na njia zetu wenyewe. Lakini Yeye hawezi kufanya kazi ndani yetu bila idhini na ushirikiano wetu. Roho wa Mungu hutenda kazi kupitia kwa uwezo na nguvu aliyopewa mwanadamu. Nguvu zetu zinahitajika kushirikiana na Mungu.” {1TG40: 14.3}
Utu wa kale, asili ambayo tumezaliwa nayo, haiwezi kuurithi Ufalme wa Mungu. Kwa mujibu wa andiko hili hitaji letu ni kuomba kwa ajili ya uwezo wa kuisalimisha mioyo yetu, yote yetu kwa Mungu. Tunapofanya hivi, tutakuwa tofauti kabisa kuliko vile tulivyo sasa – utu wetu wa kale utatoweka. {1TG40: 14.4}
14
ZAYUNI KATIKA UPEO WA UTUKUFU WAKE
MATINI YA HOTUBA NA V. T. HOUTEFF
MCHUNGAJI WA WADAUDI WAADVENTISTA WA SABATO
SABATO, MEI 10, 1947
HEKALU LA MLIMA KARMELI
WACO, TEXAS
Uchambuzi wetu alasiri hii ni kutoka katika sura ya sitini ya Isaya. Humo tunasoma: “Ondoka, uangaze; kwa kuwa nuru yako imekuja, Na utukufu wa Bwana umekuzukia.” Isa. 60: 1. {1TG40: 15.1}
Jambo la kwanza tunalohitaji kujua katika uchambuzi huu ni mtu ambaye Uvuvio huuliza kuondoka. Sura hii ikiwa ni endelezo la sura ya hamsini na nne, kwa hivyo, tutaangalia humo habari hiyo. Humo inaonyesha kwam-ba ni mwanamke tasa, watumwa wa Mungu katika kanisa la Kikristo. Yeye analiita kanisa Lake liondoke na kuangaza kwa sababu yake “nuru imekuja.” Kuhusu ikiwa ananena kwa waja wake wakati huu wa sasa, wa za-mani, au wa siku zijazo, hebu tusome tena– {1TG40: 15.2}
“Watu wako nao watakuwa wenye haki wote, Nao watairithi nchi milele; chipukizi la upandaji wangu, kazi ya mikono yangu, ili nipate kutukuzwa.” Isa. 60:21. {1TG40: 15.3}
Aya hii haisemi kwamba watu wake tayari ni watakatifu, ila kwamba watakuwa watakatifu. Haisemi kwamba wamerithi nchi, lakini kwamba watairithi. Kanisa Lake, kwa hivyo, litatakaswa na kufanywa jeupe Mungu atakapoyaondolea mbali “magugu.” {1TG40: 15.4}
15
Kwa sababu watu wake hawajawahi kuwa watakatifu wote hata leo, ni wazi kuona kwamba utimizo wa unabii huu ni wa baadaye. Na kwa mtazamo wa ukweli kwamba ujumbe wetu unatangaza utakaso wa kanisa ulio kari-bu sana, wakati ambao malaika wanapaswa kuwaondoa wanafiki kutoka miongoni mwa waaminifu, wakati am-bapo juya linavutwa pwani na samaki wabaya kutupwa nje, kutakaswa kwa patakatifu — Hukumu kwa Walio Hai katika “nyumba ya Mungu” (1 Pet. 4:17) i karibu kuanza, Uvuvio, kwa hivyo, katika sura hii unanena kwa kanisa la Mungu hasa kwa wakati huu. Maadamu sasa tunaona kwamba sura hii inasheheni Ukweli muhimu mwafaka, tutaisoma aya kwa aya. {1TG40: 16.1}
Isa. 60: 1 — “Ondoka, uangaze; kwa kuwa nuru yako imekuja, Na utukufu wa Bwana umekuzukia.”
Ni nani awezaye kusema kwa kweli kwamba taa yetu haijakuja? kwamba ujumbe wetu sio Ukweli kwa wakati mwafaka? Hakuna yeyote ambaye amekutana nao, ninao uhakika. Uvuvio, kwa hivyo, unawaalika watu wa Mungu, Dhehebu, pamoja nasi, kuondoka na kuangaza. Neno “uangaze” ndilo tunapaswa kulichambua ijayo ili tujue kinachohitajika kwetu. {1TG40: 16.2}
Kitu cheusi, kichafu kamwe huwa hakiakisi, hufyonza nuru yote chenyewe. Mwezi huangaza kwa sababu uso wake ni wa vitu vyeupe. Iwapo ungalitengenezwa kwa vitu vyeusi haungaliweza kuakisi nuru yoyote. Ndivyo ilivyo kweli na nuru ya kiroho: Ikiwa tunatamani kuangaza, lazima tuamke na kusafisha, tuyavue mavazi yetu meusi, na machafu — tuchukue sehemu amilifu katika uamsho na matengenezo haya chini ya usimamizi wa Roho Mtakatifu. Upumbavu, ushabiki wa dini, na uzembe lazima uachwe na mawazo ya Matakatifu yawekwe kwa utendaji, hivyo anaamuru Bwana: {1TG40: 16.3}
“Mtu mbaya na aache njia yake, Na mtu asiye haki
16
aache mawazo yake; Na amrudie Bwana, Naye atamrehemu; Na arejee kwa Mungu wetu, Naye atamsamehe kabisa. Maana mawazo yangu si mawazo yenu, wala njia zenu si njia zangu; asema Bwana. Kwa maana kama vile mbingu zilivyo juu sana kuliko nchi, kadhalika njia zangu zi juu sana kuliko njia zenu, na mawazo yangu kul-iko mawazo yenu. Maana kama vile mvua ishukavyo, na theluji, kutoka mbinguni, wala hairudi huko; bali huinywesha ardhi, na kuizalisha na kuichipuza, ikampa mtu apandaye mbegu, na mtu alaye chakula; ndivyo litakavyokuwa neno langu, litokalo katika kinywa changu; halitanirudia bure, bali litatimiza mapenzi yangu, nalo litafanikiwa katika mambo yale niliyolituma.” Isa. 55: 7-11. {1TG40: 16.4}
Lazima tuyasafishe mawazo yetu, njia zetu, miili yetu, nguo zetu, makao yetu ndani na nje. Usafi ni Uungu; Serikali ya Mungu ni sheria na utaratibu, amani na haki, furaha na kuridhika. Hivyo tunahitaji kung’arishwa na Roho wa Mungu, kuwa Wakristo kweli kweli iwapo tutaweza “kuangaza,” ikiwa tutaweza daima kuliakisi Neno la Mungu kwa wale ambao hukaa gizani. Iwapo umewajibikia mambo yote ambayo ujumbe hufundisha, basi kama jukumu lako la juu na fursa Takatifu, chukua kile Uvuvio unasema: “Ondoka, uangaze; kwa kuwa nuru yako imekuja, Na utukufu wa Bwana umekuzukia.” Leo ni fursa yako. {1TG40: 17.1}
Aya ya 2 — “Maana, tazama, giza litaifunika dunia, Na giza kuu litazifunika kabila za watu; Bali Bwana atakuzukia wewe, Na utukufu wake utaonekana juu yako.”
17
Neno “tazama” humaanisha kwamba ukiangalia, unaweza kuziona ishara za giza zikiwa tayari zinaelea juu yako. “Giza kuu” humaanisha kwamba watu watakuwa kwa hasara kabisa kujua ni njia ipi ya kufuata, kwamba wa-tachanganyikiwa kabisa na kutatizwa. Sasa ni fursa yetu kuitikia mwito wa Bwana na kujitayarisha kuikabili hali hiyo. Tunapaswa sasa kutambua kikamilifu kwamba kwa uhalisi tunaitwa kuwa nuru kwa Dhehebu, na mwishowe kwa ulimwengu. Ajabu kweli kweli kwamba tunapaswa kuwa wateule kutoka kati ya halaiki kubwa za dunia! Hauwezi kumudu kuikosa fursa hii. Chukua hatua sasa. {1TG40: 18.1}
Aya ya 3 — “Na mataifa wataijilia nuru yako, Na wafalme kuujia mwanga wa kuzuka kwako.”
Sisi sasa ni watu wasiojulikana zaidi duniani, lakini siku imekuja ambayo tutajulikana sana. Hapa ipo ahadi ya uhakika kwamba ikiwa sasa tunaweza kuinuka na kufanya juhudi kulifikia lengo ambalo Mungu ameweka kwa ajili yetu, tokeo litakuwa kwamba Mataifa wataijia nuru yetu na wafalme kwa mwanga wa kuzuka kwetu. Hii ndio siku inayokubalika kwa ajili yako. {1TG40: 18.2}
Aya ya 4 — “Inua macho yako, utazame pande zote; Wote wanakusanyana; wanakujia wewe; Wana wako watakuja kutoka mbali. Na binti zako watabebwa nyongani.”
Hata sasa iwapo tunayainua macho yetu ya kiroho, asema Bwana, tutaona kwamba mambo yote yako tayari. Mwito, pamoja na ishara za nyakati ni wazi sana kwa mtu kudhani kwamba siku hiyo iko mbali. Wana na binti zetu katika ujumbe huu watakusanywa hivi karibuni kutoka katika miisho ya dunia. {1TG40: 18.3}
Aya ya 5 — “Ndipo utakapoona na kutiwa nuru,
18
Na moyo wako utatetemeka na kukunjuka; Kwa kuwa wingi wa bahari utageuzwa kukujia, Utajiri wa mataifa utakuwasilia.”
Wakati haya yatakapotukia, basi masalia wataona wazi na kukunjuka pamoja, utajiri wa Mataifa utawawasilia. {1TG40: 19.1}
Aya ya 6-9 — “Wingi wa ngamia utakufunika, Ngamia vijana wa Midiani na Efa; Wote watakuja kutoka Sheba; Wataleta dhahabu na uvumba; Na kuzitangaza sifa za Bwana. Makundi yote ya Kedari yata-kusanyika kwako, Kondoo waume wa Nebayothi watakutumikia; Watapanda juu ya madhabahu yangu kwa kibali, Nami nitaitukuza nyumba ya utukufu wangu. Ni nani hawa warukao kama wingu, Na kama njiwa waendao madirishani kwao? Hakika yake visiwa vitaningojea, Na merikebu za Tarshishi kwanza, Ili kuleta wana wako kutoka mbali, Na fedha yao na dhahabu yao pamoja nao, Kwa ajili ya jina la Bwa-na, Mungu wako, Kwa ajili yake Mtakatifu wa Israeli, Kwa kuwa amekutukuza wewe.”
Wana na binti zetu katika imani watakuja kama kimbunga angani na baharini. Watakuja kwa sababu Bwana atawatukuza watu Wake wote. Mwito, “Tokeni kwake, enyi watu wangu, msishiriki dhambi zake, wala msipokee mapigo yake.” (Ufu. 18: 4), hakika pamoja na utajiri wa Mataifa watawatoa nje “umati mkubwa ambao hapana mtu awezaye kuhesabu.” Ufu. 7: 9. {1TG40: 19.2}
Aya ya 10 — “Na wageni watajenga kuta zako, Na wafalme wao watakuhudumu; Maana katika ghadha-bu yangu nalikupiga, Lakini katika upendeleo wangu nimekurehemu.”
19
Katika wakati wa Ezra na Nehemia watu wa Mungu, Wayahudi, wenyewe walipaswa kujenga dhidi ya hali ngumu, lakini kwa ajili ya kanisa lililotakaswa, Mataifa watajenga kwa furaha. Sio tu watu wa kawaida bali hata wafalme wao watawahudumia watumwa wa Mungu. Wafalme sasa ni mabwana, lakini siku i karibu hapa am-bayo watumwa wa Mungu watakuwa mabosi wa wafalme, na wafalme watafurahi kuajiriwa na wao. {1TG40: 20.1}
Aya ya 11 – “Malango yako nayo yatakuwa wazi daima; Hayatafungwa mchana wala usiku; Ili watu wapate kukuletea utajiri wa mataifa, Na wafalme wao wakiongozwa pamoja nao.”
Kwa sababu ya itikio letu kwa mwito wa Mungu na kwa sababu ya kuondoka kwetu ili kuangaza kwa ajili Yake, watu wengi watasema: “… Njoni, twende juu mlimani kwa Bwana, nyumbani kwa Mungu wa Yakobo, naye atatufundisha njia zake, nasi tutakwenda katika mapito yake maana katika Sayuni itatoka sheria, na neno la Bwana katika Yerusalemu.” Isa. 2: 3. Kwa sababu hii ilio wazi malango kama mfano, yataweza kuwa wazi mchana na usiku ili kuwakaribisha watu watakaopitapita — watakatifu wanaokuja, utajiri wa Mataifa, na wafal-me wao. Kwa udhahiri, basi, hitaji kubwa sio kampeni ya “Kuyakusanya Mavuno”, sio michango mingi, sio siku za kuuza vitabu — sio kampeni zozote za kukuza malengo — bali kuyachukua haya “mafuta ya dhahabu” kwa ajili ya taa zetu na “kuondoka na kuangaza” ni kile kanisa linahitaji leo. {1TG40: 20.2}
Aya ya 12, 13 — “Kwa maana kila taifa na ufalme wa watu wasiotaka kukutumikia wataangamia; Naam, mataifa hayo wataharibiwa kabisa. Utukufu wa Lebanoni utakujia wewe, Mberoshi na mtidhari na mteashuri pamoja; Ili kupapamba mahali pangu patakatifu, Nami nitapatukuza mahali pa miguu yangu.”
20
Mahali ambapo miguu ya Bwana itasimama wakati huo “bonde la milima” (Zek. 14: 5); patafanywa pa utukufu zaidi. {1TG40: 21.1}
Aya ya 14-16 — “Na wana wa watu wale waliokutesa Watakuja kwako na kukuinamia; Nao wote wali-okudharau Watajiinamisha hata nyayo za miguu yako; Nao watakuita, Mji wa Bwana, Sayuni wa Mta-katifu wa Israeli. Na kwa kuwa umeachwa na kuchukiwa, Hata ikawa hapana mtu aliyepita ndani yako, Nitakufanya kuwa fahari ya milele, Furaha ya vizazi vingi. Utanyonya maziwa ya mataifa, Utanyonya matiti ya wafalme; Nawe utajua ya kuwa mimi, Bwana, ni mwokozi wako, Na mkombozi wako, Mwenye enzi wa Yakobo.”
Kama watoto wanavyotendewa na kubembelezwa kwa kutamaniwa, vivyo hivyo Mataifa na wafalme wao wa-tawangojea kwa furaha watakatifu na kutokana na wingi wao watawalisha watumwa wa Mungu kwa furaha. {1TG40: 21.2}
Aya ya 17 — “Badala ya shaba nitaleta dhahabu, Na badala; ya chuma nitaleta fedha, Na badala ya mti, shaba, Na badala ya mawe, chuma; Tena nitawafanya wasimamizi wako wawe amani, Na hao wakutozao fedha kuwa haki.”
Naam, bora zaidi ya iliyo bora nyumba ya Mungu itajengwa. {1TG40: 21.3}
Aya ya 18 — “Jeuri haitasikiwa tena katika nchi yako, Ukiwa na uharibifu hazitakuwa mipakani mwako; Bali utaziita kuta zako, Wokovu, Na malango yako, Sifa.”
Sasa wakati ambapo dunia inahitaji na kutamani amani zaidi kuliko hapo awali, Mungu, Ambaye pekee aliye na uwezo wa kuitoa anatangaza kwa sauti kwamba wale ambao wanataka hakika amani
21
wanaweza ipata ikiwa wanakuja Kwake. Tumaini hili na imani katika ahadi za Mungu hata sasa litakuwa amani yetu ya mawazo iwapo kweli tunaamini. {1TG40: 21.4}
Aya ya 19-22 — “Jua halitakuwa nuru yako tena wakati wa mchana, Wala mwezi hautakupa nuru kwa mwangaza wake; Bali Bwana atakuwa nuru ya milele kwako, Na Mungu wako atakuwa utukufu wako. Jua lako halitashuka tena, Wala mwezi wako hautajitenga; Kwa kuwa Bwana mwenyewe atakuwa nuru yako ya milele; Na siku za kuomboleza kwako zitakoma. Watu wako nao watakuwa wenye haki wote, Nao watairithi nchi milele; Mdogo atakuwa elfu, Na mnyonge atakuwa taifa hodari; Mimi, Bwana, nitayahimiza hayo wakati wake.”
Wakati ambapo watumwa wote wa Mungu kama kitu kimoja “wataondoka na kuangaza,” basi mtu mdogo atakuwa elfu, na mtu mnyonge atakuwa taifa hodari. Kisha Watakatifu watakusanywa haraka na uovu utak-omeshwa. Hii ndio njia ya Mungu ya kuikamilisha kazi ya injili na ingalikuwa bora kuacha dhana zetu za kibinadamu na kuitikia kwa moyo wote mwito wa Mungu iwapo tunatarajia kuokoka katika “siku kuu na ya kutisha” ya Bwana, ikiwa tunatarajia kufurahi katika upeo wa utukufu wa Zayuni. Iwapo tunasimama waamini-fu kwa Neno la Mungu, mwishowe tutayaona maajabu haya yote na kuishi milele. {1TG40: 22.1}
-0-0-0-0-0-
Ili kuleta furaha hii isiyoneneka ya ahadi za Mungu, tarajio la vizazi, masomo haya yanachapishwa na kutumwa bila malipo au wajibu kwa wote wanaotaka kuwa nayo. Tuma jina na anwani yako kwa Shirika la Uchapishaji a Ulimwengu, Kituo cha Mlima Karmeli, Waco, Texas. {1TG40: 22.2}
22
ANDIKO LA SALA
Wepesi Kufanywa Wa Moyo
Nitasoma kutoka katika “Mlima wa Baraka,” kuanzia ukurasa wa 142, aya ya kwanza: {1TG41: 23.1}
“Ushindi haupatikani bila maombi ya dhati, bila kujinyenyekeza nafsi kwa kila hatua. Nia zetu hazipaswi ku-lazimishwa kushirikiana na vyombo vya Mungu, lakini lazima zitiishwe kwa hiari. Ingaliwezekana ushinikizwe juu yako kwa nguvu kubwa mara mia moja ushawishi wa Roho wa Mungu, haungekufanya kuwa Mkristo, raia wa kufaa mbinguni …. Nia lazima iwekwe kwa upande wa mapenzi ya Mungu . Hauwezi, mwenyewe, kuleta maazimio na tamaa na mwelekeo wako kwa utiifu wa mapenzi ya Mungu; lakini ikiwa u ‘mwepesi kufanywa wa moyo,’ Mungu ataikamilisha kazi kwa ajili yako …. Lakini wengi wanavutiwa na uzuri wa Kristo na utukufu wa mbinguni, ambao bado huogopa maagizo ambayo kwayo pekee huo unaweza kuwa wao wenyewe …. Ili kuzika-na nia zao, vitu walivyovichagua vya mahaba au masumbuko, huhitaji kafara ambayo wao husita, na kujikwa, na kurudi nyuma. Wengi ‘watatafuta kuingia ndani, na hawataweza.’” {1TG41: 23.2}
Je! Tuombe kwa ajili ya nini jioni hii? — Tukumbuke kwamba ubinafsi ndicho kizuizi cha pekee kati yetu na Mungu, na kwamba Mungu hatatulazimisha kuja Kwake. Hebu tumwombe Yeye uwezo wa kuitumia neema ambayo Yeye hutoa kwa hiari. Asingalikuwa ametuumba mawakala huru wa maadili kama Asingalitarajia tu-tumie nia zetu. Tunapaswa kumwomba Yeye atusaidie kuwa “wepesi wa moyo,” na kisha kuziunganisha nia zetu na Yake, na hivyo “kuufanyia kazi wokovu wetu wenyewe.” Tunahitaji nguvu ya Mungu ili kuupinga uovu wote, kuushinda ulimwengu jinsi Yesu alivyoushinda. {1TG41: 23.3}
23
MATUNDA YAKE ALIYETIWA-MAFUTA
MATINI YA HOTUBA NA V. T. HOUTEFF
MCHUNGAJI WA WADAUDI WAADVENTISTA WA SABATO
SABATO, MEI 17, 1947
HEKALU LA MLIMA KARMELI
WACO, TEXAS
Tutaichambua sura ya sitini na moja ya Isaya, tukianza na aya ya kwanza: {1TG41: 24.1}
Isa. 61: 1, 2 — “Roho ya Bwana MUNGU i juu yangu; kwa sababu Bwana amenitia mafuta niwahubiri wanyenyekevu habari njema; amenituma ili kuwaganga waliovunjika moyo, kuwatangazia mateka uhuru wao, na hao waliofungwa habari za kufunguliwa kwao. Kutangaza mwaka wa Bwana uliokubaliwa, na siku ya kisasi cha Mungu wetu; kuwafariji wote waliao.”
Hizi ndizo aya mbili ambazo Yesu alisoma Aliposimama katika sinagogi la mji wa Nazareti, mahali Alipolelewa. Yeye alizisoma aya hizi kisha akaketi bila kutoa maelezo yoyote. Wakati wasikilizaji Wake walipokuwa bado wameduwaa kuhusu kwa nini Yeye alikuwa amesoma kisha akaketi bila kuongeza neno, Yesu akainuka tena akasema, “Leo hii andiko hili limetimia masikioni mwenu.” {1TG41: 24.2}
Sababu iliyotolewa kwa ajili ya nguvu ya Roho kuwa juu yake ni kwamba Bwana Mungu alikuwa Amemtia ma-futa aihubiri habari njema kwa wanyenyekevu, kumaanisha kwamba iwapo Bwana alikuwa Hajamtia mafuta kuhubiri, Roho wa Bwana asingalikuwa juu Yake. Zaidi ya hayo, Alitiwa mafuta ahubiri kwa wapole, kwa wale ambao
24
hawajajitosheleza kwa ubinafsi, wasio jitakia makuu, ila wanyenyekevu na wasikivu; daraja lile lingine halinga-liweza kufundishwa. Yeye alipaswa kuwafariji wote wanaoomboleza, kuwaganga waliovunjika moyo, kuwatan-gazia mateka uhuru wao (sio kuwaweka huru mara moja). “Mwaka wa Bwana uliokubaliwa” ni bila shaka, kwa wakati ambapo andiko hili linatimizwa, wakati linapofunuliwa na kutangazwa. Wale ambao hawatalitii wa-tafagiliwa mbali katika “siku ya kisasi.” Hizi ndizo habari njema ambazo kwa ajili yazo Yesu alitiwa mafuta. Kutokuamini na kutojali katika Ukweli uliofunuliwa ni chukizo kwa Mungu na dhambi dhidi ya Roho Mtakatifu ambaye huongoza kwenye Kweli yote. {1TG41: 24.3}
Eti kwa sababu Mwokozi alihubiri aya hizi mbili, hata hivyo, sio lazima kuhitimisha kwamba sura nzima iliti-mizwa wakati huo au kwamba utimizo wa aya hizi mbili haungaliweza kutimizwa tena kwa wakati ambapo aya zingine za sura hiyo zinatimizwa. Kama vile Roho yule yule alikuwa pia juu ya Mitume — juu ya wale waliouendeleza ujumbe wa Bwana katika siku hiyo, hivyo pia lazima iwe katika siku hii, katika siku ambayo sura yote inatimizwa. {1TG41: 25.1}
Jukumu la wale wanaoutangaza ujumbe wa sura hii ni: {1TG41: 25.2}
Aya ya 3 — “Kuwaagizia hao waliao katika Sayuni, wapewe taji ya maua badala ya majivu, mafuta ya fu-raha badala ya maombolezo, vazi la sifa badala ya roho nzito; wapate kuitwa miti ya haki, iliyopandwa na Bwana, ili atukuzwe.”
Mzigo wa Roho ni kuboresha hali ya kiroho ya wale wanaoomboleza katika Zayuni, kanisa: kuwapa uzuri badala ya majivu (kwa toba na unyenyekevu), mafuta ya furaha badala ya kuomboleza (Ukweli wa Sasa ambao kwa matumaini huangazia njia iliyosalia) na mavazi (tabia)
25
ya sifa ili wawe kama mapambo hai ya haki, viumbe wapya wa Mungu, ili Atukuzwe. {1TG41: 25.3}
Hapa inaonekana kwamba uumbaji wa asili wa Mungu ambao umepotezwa kupitia dhambi, utarejeshwa. Sasa ni siku inayokubalika kuufungua moyo wako, kuupokea Ukweli wa sasa, kuumba upya na kurejesha kile kilichop-otea kupitia dhambi. {1TG41: 26.1}
Aya ya 4 — “Nao watajenga mahali pa kale palipoharibiwa, watapainua mahali palipokuwa ukiwa za-mani, watatengeneza miji iliyoharibiwa, mahali palipoachwa kizazi baada ya kizazi.”
Wale ambao wamefanywa wafurahi na wazuri, ambao wamevikwa sifa na wanaokuwa miti ya haki — wali-opandwa na Bwana. Watumwa Wake walioshinda, kina Ezra na Nehemia wasio na hila wa leo, watayarejesha mambo yote. {1TG41: 26.2}
Aya ya 5 — “Na wageni watasimama na kulisha makundi yenu, na watu wa kabila nyingine watakuwa wakulima wenu, na watunzaji wa mizabibu yenu.”
Wageni na watu wa kabila nyingine waliotajwa hapa, wao kwa kweli sio wageni na watu wa kabila nyingine kwa Ufalme wa Mungu, lakini kitaifa wasio na uhusiano wa damu na Yuda na Israeli, sio wa ukoo wa Yakobo, sio wale 144,000 ambao wanasimama kwanza juu ya Mlima Zayuni, ila pamoja nao. {1TG41: 26.3}
Aya ya 6 — “Bali ninyi mtaitwa makuhani wa Bwana; watu watawaiteni wahudumu wa Mungu wetu; mtakula utajiri wa mataifa, na kujisifia utukufu wao.”
26
Katika Ufalme wa Yuda wa uakisi unaokuja, kwa hiyo, kutakuwa na makundi mawili ya watu — wachungaji na walei. {1TG41: 27.1}
Kutoka kwa maandiko haya tunaona kwamba Ufalme wa Mungu, kanisa lililotakaswa, huru kwa “magugu” ni kitu halisi. Sio kitu cha kuwaza, sio kitu cha povu kinachoelea na kutoweka hewani, ila papa hapa duniani. {1TG41: 27.2}
Aya ya 7 — “Badala ya aibu yenu mtapata maradufu, na badala ya fedheha wataifurahia sehemu yao; basi katika nchi yao watamiliki maradufu; furaha yao itakuwa ya milele.”
Wachungaji hawa wa Mungu watapata maradufu kwa sababu ya aibu ambayo wamevumilia, wote kama hao hu-furahia fungu lao. Je! unayo nia ya kuteseka kwa ajili ya Kristo? Je! wewe ni kama au sio kama wale wanaotafu-ta furaha na urafiki kutoka kwa dunia na ambao hivi karibuni au baadaye watajikuta katika kuvunjika moyo ku-kuu? Amini! Ni hilo tu. {1TG41: 27.3}
Aya ya 8 — “Maana mimi, Bwana, naipenda hukumu ya haki, nauchukia wizi kwa sadaka ya kuteketez-wa; nami nitawalipa malipo katika kweli, nitaagana nao agano la milele.”
Hukumu na haki ni kauli mbiu ya Mungu kwa viumbe Vyake vyote. Taarifa, “Nauchukia wizi kwa sadaka ya kuteketezwa,” inamaanisha kwamba mambo kama haya yasiyofaa sasa yanafanywa kati ya watu Wake. Katika uhusiano huu, miaka kadhaa iliyopita nalimsikia mshiriki fulani wa kanisa akisema kwamba katika aina fulani ya kamari alikuwa ameshinda fedha kidogo na kadri dhamiri yake ilivyomuumiza kuzihifadhi, alizitoa kama sadaka kwa kanisa lake! Pia, nimewasikia kadhaa wakisema
27
kwamba wao hufanya kazi siku ya Sabato, ila kwamba huyaelekeza mapato yao ya Sabato kwa kanisa! Matukio haya yaweza kutumika kama sampuli za jinsi walivyo watu wa Mungu wajinga, wasio na elimu katika mambo ya Mungu. Kwa kuleta sadaka kama hizo Kwake wanamfanya Mungu kuwa mcheza kamari na mvunja Sabato, na kwa wakati huo huo wanadhani kwamba wanamtendea Yeye fadhili kubwa! {1TG41: 27.4}
Ahadi ya Mungu kwa watu wake ni: “Nami nitawalipa malipo katika kweli.” Je! Basi tunapaswa kuhoji uwezo Wake wa kutekeleza na kwa wakati huo huo kumtarajia Yeye atupe makao katika Ufalme Wake? {1TG41: 28.1}
Aya ya 9 — “Na kizazi chao kitajulikana katika mataifa, na uzao wao katika kabila za watu; wote wa-waonao watakiri ya kuwa wao ni kizazi kilichobarikiwa na Bwana.”
Ni tumaini lililobarikiwa kama nini! Je! Ni kama nini nguvu ya kuokoa vijana na wazee na kuyafanya majina yao yajulikane duniani kote! Kwa umaarufu kama huu, watu walipitia karibu mateso yoyote ambayo yanajulikana kwa wanadamu. Mungu, hata hivyo, anakuuliza uamini tu na kulifuata Neno Lake, — naam, hilo tu. {1TG41: 28.2}
Ukristo utakuwa kitu halisi, halisi sana kwamba Mataifa watatambua kwamba Wakristo kama hao wanaweza kuwa tu mpando wa Bwana, na kwamba nguvu ya Mungu pekee ndio inayoweza kuleta badiliko katika moyo wa mwanadamu, na kusababisha watakatifu Wake kusema. : {1TG41: 28.3}
Aya ya 10 — “Nitafurahi sana katika Bwana, nafsi yangu itashangilia katika Mungu wangu; maana amenivika mavazi ya wokovu, amenifunika vazi la haki, kama bwana arusi ajipambavyo kwa kilemba cha maua, na kama bibi arusi ajipambavyo kwa vyombo vya dhahabu.”
28
Sura hii ya Isaya nabii ni kweli italeta “uamsho na matengenezo” ambayo hayajawahi kutukia tangu mwanzo wa dhambi. Mungu anakataza kwamba yeyote mmoja wetu asikose uzoefu na baraka ambazo zinazokuja kupitia uamsho huu na matengenezo. {1TG41: 29.1}
Aya ya 11 — “Maana kama nchi itoavyo machipuko yake, na kama bustani ioteshavyo vitu vilivyopandwa ndani yake; ndivyo Bwana MUNGU atakavyootesha haki na sifa mbele ya mataifa yote.”
Kupitia katika mbegu ya Ukweli moyoni uzoefu huu utawajia watu wa Mungu kwa kawaida kama ifanyavyo ardhi kusababisha mbegu zilizopandwa ndani yake kumea na kuzaa matunda. Hii kwa kweli ni “haki ya Kristo,” sio nguvu ya wanadamu. {1TG41: 29.2}
Kutoa muhtasari wa uchambuzi huu, tunajifunza kwamba matunda yake Aliyetiwa-mafuta ni haya: {1TG41: 29.3}
Kwamba Yesu alitiwa mafuta kuhubiri habari njema, habari kwamba Yeye angaliufungua mlango wa kifungo cha dhambi, kuwaganga watu wa Mungu, kuutangaza mwaka wa Bwana uliokubaliwa, kuwafariji wale wanaoomboleza, na kuwapa wote fursa ya kuokoka “siku ya kisasi”; kwamba kwa sababu Yeye alitiwa-mafuta hivyo, Aliwezeshwa kuwafariji wale wanaoomboleza katika Zayuni, wapewe taji ya maua badala ya majivu, ma-futa ya furaha badala ya maombolezo, vazi la sifa badala ya roho nzito; wapate kuitwa “miti ya haki,” na ya kwamba Mungu atukuzwe hapo; kwamba kupitia zawadi ya Roho watu Wake watawezeshwa kujenga mahali palipokuwa ukiwa kwa vizazi vingi; kwamba wale ambao wameitwa sasa watakuwa wachungaji wa Mungu “nao watakula utajiri wa Mataifa,” na kujisifia utukufu wao, na “wageni na watu wa kabila nyingine” watakuwa wakulima wao na
29
“watunzaji wa mizabibu yenu”; kwamba wakati huo fedheha yao na fujo zitabadilishwa kuwa furaha ya milele; kwamba jinsi Mungu anavyochukia wizi, Ataongoza kazi katika Kweli na kufanya agano la milele pamoja na wale wanaomjua Yeye; kwamba basi uzao wao utajulikana kwa Mataifa na kati ya watu na watakiri kwamba Mungu amewabariki watu Wake; kwamba kwa sababu Mtiwa-mafuta huwavika watu Wake nguo ya wokovu, na vazi la haki, ushuhuda wa watoto Wake utakuwa, “Nitafurahi sana katika Bwana”; na kama bibi arusi ajipam-bavyo na vito hivyo mapambo ya kiroho, yaliyotolewa kupitia zawadi hizi yataleta “uhuisho na matengenezo”; na ya kwamba, kama vile maumbile yanavyoleta matunda kwa mbegu zilizopandwa ardhini, hivyo Mtiwa-mafuta atasababisha haki na sifa kuchipuka mbele ya mataifa yote. {1TG41: 29.4}
“Maandalizi tele yametengenezwa kwa ajili ya wote ambao kwa uaminifu, kwa bidii, na kwa makini wame-anzisha kazi ya utimilifu wa utakatifu katika kumcha Mungu. Nguvu, neema na utukufu zimetolewa kupitia Kristo, kuletwa na malaika wanaowahudumia warithi wa wokovu. Hakuna aliye goigoi sana, aliye mpotovu na mfisadi sana na wa kuchukiza, kwamba hawawezi kupata ndani ya Yesu, aliyekufa kwa ajili yao, nguvu, usafi, na haki, ikiwa wataziweka mbali dhambi zao, kukoma mwenendo wao wa uovu, na kugeuka kwa kusudi kamili la moyo kwa Mungu aliye hai. Yeye anasubiri kuwavua mavazi yao, yaliyotiwa doa na unajisi wa dhambi, na kuwavika mavazi meupe maangavu ya haki; na kuwahimiza waishi na wasife. Katika yeye wanaweza kustawi. Matawi yao hayatanyauka wala kukosa matunda. Ikiwa watakaa ndani yake, wanaweza kupata chakula na lishe kutoka kwake, kujazwa na Roho wake, kutembea kama alivyotembea, kushinda kama alivyoshinda, na kuinu-liwa hadi kwa mkono wake wa kuume.” — “Shuhuda,” Gombo la 2, uk. 453. {1TG41: 30.1}
30
UPO UPANA KATIKA NEEMA YA MUNGU
Upo upana katika neema ya Mungu,
Kama upana wa bahari;
Ipo fadhila katika haki Yake,
Ambayo ni zaidi ya uhuru.
Yapo mapokezi kwa ajili ya mdhambi.
Na neema zaidi kwa wazuri;
Ipo rehema na Mwokozi
Kunao uponyaji katika damu Yake.
Maana upendo wa Mungu ni mpana
Kuliko kipimo cha akili ya mwanadamu
Na moyo wa yule wa milele
Ni wa ajabu sana mpole.
Ikiwa upendo wetu ungalikuwa wa unyenyekevu zaidi,
Tunapaswa Kumwamini kwa Neno Lake;
Na maisha yetu yote yaweze kuwa jua
Katika utamu wa Bwana wetu.
-Frederick W. Faber.
31
Jumuiya ya Wadaudi Waadventista wa Sabato
(Ushirika Huru Unaojumuisha Kanisa)
Mlima Karmeli, Waco, Texas
S.L.P. 23738, Waco, TX 76702
+ 1-254-855-9539
www.gadsda.com
info@gadsda.com
Gombo la 1, Namba 39, 40, 41
Kimechapishwa nchini Marekani
32