fbpx

Gombo la 1 Salamu Mwafaka Namba 33, 34, 35

Gombo la 1 Salamu Mwafaka Namba 33, 34, 35

                                    

AMANI YA PEKEE YA MAWAZO

Hati miliki, Kimechapishwa tena 1953

Haki zote zimehifadhiwa

V. T. HOUTEFF

                                    

KUTAWANYWA, WAKATI, NA KUOKOLEWA

MATEKA WA MHARABU WACHUKULIWA NA WACHECHEMEAO NA WADHAIFU

MATAIFA YANAONA EDOMU UKIANGAMIA, JANGWA LACHANUA, NA NJIA KUU KWEN-DA ZAYUNI

                                    

1

ANDIKO LA SALA

Mahitaji Yetu Yatimizwa

Nitasoma kutoka katika “Mlima wa Baraka,” uk. 190, aya inayoanzia katikati ya ukurasa: {1TG33: 2.1}

M.B., uk. 190 — “Kila ahadi katika Neno la Mungu hutupatia mada ya sala, ikiwasilisha neno lililoahidiwa na Yehova kama hakikisho letu. Baraka iwayo yote ya kiroho tunayohitaji, ni fursa yetu kuidai kupitia kwa Yesu. Tunaweza kumwambia Bwana, kwa unyenyekevu wa mtoto, kile hasa tunachohitaji. Tunaweza kumweleza Yeye mambo yetu ya kawaida; kumwomba chakula na mavazi na mkate wa uzima na vazi la haki ya Kristo. Ba-ba yenu wa mbinguni anajua kwamba mnavihitaji vitu hivi vyote, na mmealikwa kumwomba Yeye kuvihusu. Ni kwa kupitia jina la Yesu kwamba kila neema inapokelewa. Mungu ataliheshimu jina hilo, na atayakidhi mahitaji yenu kutoka kwa utajiri wa ukarimu Wake.” {1TG33: 2.2}

Hebu tufanye muhtasari wa yale tunapaswa kuomba kwa ajili yake alasiri hii. Tunahitaji kuomba kwa ajili ya imani thabiti katika uhakikisho kwamba bila kujali ni baraka gani za kiroho na za kawaida tunaweza kuhitaji, ni fursa yetu kumwendea Bwana kwa unyenyekevu wa mtoto na kudai baraka hizi kwa jina la Yesu. Tunahitaji kuomba kwa ajili ya msaada wa kumwamini Mungu kwa neno Lake; Tuombe kwa kugundua kwamba Yeye humaanisha tu kile ambacho husema wakati Anaahidi kuliheshimu jina la Yesu na kuyatimiza mahitaji yetu kutoka kwa utajiri Wake usio na kifani. {1TG33: 2.3}

2

KUTAWANYWA, WAKATI, NA KUOKOLEWA

MATINI YA HOTUBA NA V. T. HOUTEFF

MCHUNGAJI WA WADAUDI WAADVENTISTA WA SABATO

SABATO, MACHI 22, 1947

HEKALU LA MLIMA KARMELI

WACO, TEXAS

Alasiri hii tutajifunza Isaya, sura ya 31 na 32. Katika sura hizi tutaona sababu ya kutekwa kwa Zayuni na Ma-taifa, kikomo chao cha wakati, na ukombozi wa Israeli wa uakisi: {1TG33: 3.1}

Isa. 31: 1-4 — “Ole wao watelemkao kwenda Misri wapate msaada, na kutegemea farasi; watumainio ma-gari kwa kuwa ni mengi, na wapanda farasi kwa kuwa ni hodari sana; lakini hawamwangalii Mtakatifu wa Israeli, wala hawamtafuti Bwana! Lakini yeye naye ana akili, naye ataleta uovu, wala hatayatangua maneno yake; bali ataondoka juu ya nyumba yao watendao mabaya, na juu ya msaada wa hao watendao maovu. Basi Wamisri ni wanadamu wala si Mungu, na farasi zao ni nyama wala si roho; na Bwana atakaponyosha mkono wake, yeye asaidiaye atajikwaa, na yeye asaidiwaye ataanguka, nao wote pamoja watakoma. Maana Bwana aniambia hivi, Kama vile ilivyo simba angurumapo na mwana-simba juu ya mawindo yake, wachungaji wengi wakiitwa ili kumpiga, lakini hatiwi hofu na sauti zao, wala kufanya woga kwa sababu ya mshindo wao; ndivyo Bwana wa majeshi atakavyoshuka ili kufanya vita juu ya mlima Sayuni, na juu ya kilima chake.”

Ingawa Bwana aliruhusu ufalme Wake wa zamani

3

kutekwa na Mataifa, andiko hili linaonyesha kwamba Yeye ataukomboa hivi karibuni. Sio tu kwamba Yeye atawaokoa watu Wake na Mlima Zayuni, lakini Atawalinda, pia. {1TG33: 3.2}

Aya ya 5, 6 — “Kama ndege warukao, Bwana wa majeshi ataulinda Yerusalemu; ataulinda na kuuokoa, atapita juu yake na kuuhifadhi. Mwelekeeni yeye mliyemwasi sana, enyi wana wa Israeli.”

Kwa kuwa sasa wameufikia wakati wao wa ukombozi, Bwana anawasihi watu Wake wamwelekee Yeye — wafanye matengenezo. {1TG33: 4.1}

Aya ya 7 — “Maana katika siku hiyo kila mtu atatupa sanamu zake za fedha, na sanamu zake za dhaha-bu, ambazo mikono yenu imezifanya, zikawa dhambi kwenu.”

Kumwelekea Yeye, Anafafanua, ni kutupilia mbali kila sanamu. Wakati uamsho na matengenezo makubwa ka-ma hayo yanatukia kati ya watu wa Mungu, Anaendelea: {1TG33: 4.2}

Aya ya 8, 9 — “Ndipo huyo Mwashuri ataanguka kwa upanga ambao si wa mtu; na upanga usio upanga wa mtu utamla; naye ataukimbia upanga, na vijana wake watashindwa. Na ataikimbilia ngome yake kwa sababu ya hofu, nao wakuu wake wataionea bendera hofu kuu, asema Bwana, ambaye moto wake u katika Zayuni, na tanuru yake katika Yerusalemu.”

Kwa sababu ya ibada ya sanamu, Mwashuri aliruhusiwa kuwateka watu wa Mungu wa kale na nchi yao ya uz-uri. Na hakika ni kwamba Mwashuri ataendelea kuimiliki nchi tu wakati watu wa Mungu wataendelea katika ibada ya sanamu. Lakini, mara tu sanamu zote zinapotupwa kando, — naam, mara tu uamsho na matengenezo makubwa yanapotukia

4

mioyoni mwa watu, — kisha Mwashuri (dola ambayo inawatawala sasa) ataanguka hakika, na watu wa Mungu watarejea kwa hakika. Mwashuri ataanguka hivyo, sio kwa upanga wa mtu hodari, na sio kwa wa mtu dhaifu, ila “kwa sauti ya Bwana, Mwashuri atavunjika-vunjika, yeye apigaye kwa bakora.” Isa. 30:31. {1TG33: 4.3}

Isa. 32: 1-8 — “Tazama, mfalme atamiliki kwa haki, na wakuu watatawala kwa hukumu. Na mwanadamu atakuwa kama mahali pa kujificha na upepo, na mahali pa kujisitiri na dhoruba; kama mito ya maji ma-hali pakavu, kama kivuli cha mwamba mkubwa katika nchi yenye uchovu. Tena macho yao waonao hayatakuwa na kiwi, na masikio yao wasikiao yatasikiliza. Tena moyo wa mtu mwenye hamaki uta-fahamu maarifa, na ndimi zao wenye kigugumizi zitakuwa tayari kunena sawasawa.”

“Mpumbavu hataitwa tena mwungwana, wala ayari hatasemwa kwamba ni karimu. Maana mpumbavu atanena yaliyo upumbavu, na moyo wake utafanya maovu, ili kutenda hila na kusema yasiyo kweli juu ya Bwana, ili ku-ziacha nafsi za watu wenye njaa hazina kitu, na kukikomesha kinywaji chake mwenye kiu. Tena vyombo vyake ayari ni vibaya; hutunga hila mbaya, ili kuwaangamiza wanyonge kwa maneno ya uongo, mtu mhitaji ajaposema maneno yenye haki. Bali mwungwana huwaza mambo ya kiungwana, naye hushika sana mambo ya kiungwana.” {1TG33: 5.1}

Ukiwaelekea tena watu Wake wa zamani, Uvuvio ulitangaza, kwamba ingawa ufalme wao ungalianguka, lakini siku moja Mfalme atatawala kwa haki, na wakuu watatawala kwa hukumu; kwamba katika siku hiyo Mtu atakuwa kama mahali pa kujificha, kama maji mahali pakavu, na kama kivuli cha mwamba mkubwa katika nchi yenye uchovu (Isa. 32: 2); kwamba ingawa watu walikuwa vipofu kiroho na hawangaliweza kuona, bado ipo siku inakuja

5

ambapo wale wenye macho wataona wazi, na wale walio na masikio watasikia wazi; kwamba moyo wa upele utaelewa maarifa na ulimi wa kigugumizi utakuwa tayari kunena vizuri; ya kuwa huyo mtu mwovu atatambuliwa kuwa muovu, na ayari hatatajwa tena kuwa mkarimu; kwamba watu wabaya na wanafiki watajulikana kama wale wanaosema uongo dhidi ya Bwana na ambao hujaribu kuidanganya nafsi iliyo na njaa na kiu cha kiroho; kwamba, kwa upande mwingine, ayari wataonekana kuwa wale hupanga njia mbaya ambazo hutumia kumfanya maskini kuwa maskini zaidi (Isa. 32: 7). {1TG33: 5.2}

Aya ya 9-14 — “Inukeni, enyi wanawake wenye raha, isikieni sauti yangu; enyi binti za watu msiokuwa na uangalifu, tegeni masikio yenu msikie matamko yangu. Maana mtataabishwa siku kadha wa kadha zaidi ya mwaka, enyi wanawake mliojikinai; kwa sababu mavuno ya mizabibu yatakoma, wakati wa kuvuna vitu vya mashamba hautakuja. Tetemekeni, enyi wanawake wenye raha; taabikeni, enyi msiokuwa na uangalifu; jivueni, jivueni nguo zenu kabisa, jivikeni viuno nguo za magunia.

“Wataomboleza kwa ajili ya chuchu, kwa ajili ya mashamba mazuri, kwa ajili ya mzabibu uliozaa sana. Juu ya nchi ya watu wangu itamea michongoma na mibigili; naam, juu ya nyumba za furaha katika mji ulio na shangwe; maana jumba la mfalme litaachwa; mji uliokuwa na watu wengi utakuwa hauna mtu; kilima na mnara utakuwa makao ya wanyama milele, furaha ya punda-mwitu, malisho ya makundi ya kondoo.” {1TG33: 6.1}

“Wanawake” waliotajwa hapa bila shaka ni “Aholah” na “Aholiba” (Ezek. 23), majina ya mfano ya Yuda na Is-raeli. Hapa ni maelezo ya kutawanywa kwao kati ya Mataifa, adhabu ambayo wangaliichukua. {1TG33: 6.2}

Aya ya 15 — “Hata Roho itakapomwagwa juu yetu kutoka

6

juu; hata jangwa litakapokuwa shamba lizaalo sana; nalo shamba lizaalo sana litakapohesabiwa kuwa msitu.”

Hapa tunaambiwa kwamba watu watakuwa miongoni mwa Mataifa, na nchi ibaki ukiwa mpaka Roho atakapomwagwa kutoka juu. Wakati huo ndipo watarejea. {1TG33: 7.1}

Tumeona tayari sababu ya kutawanywa na kwamba kumiminwa kwa Roho ni alama ya ukombozi wa watu. Naam, basi nchi yao haitakuwa tena utekwani, nyumba zao hazitakuwa tena ukiwa. Hata jangwa litakuwa shamba lenye matunda, na shamba lizaalo litahesabiwa kuwa msitu – yatakuwapo wakati huo mavuno mengi ya roho. {1TG33: 7.2}

Sasa tumejifunza nini kutoka kwa sura hizi mbili za Isaya? Kwa kweli tumekuwa na muhtasari wa mada ambayo sura za awali zilishughulikia. Sasa hata kwa uwazi zaidi kuliko awali tunaona kwamba ibada ya sanamu ya Israe-li wa zamani ilimlazimisha Mungu kuwaruhusu watawaliwe na Waashuri. Yeye, hata hivyo, anaweza kuwaokoa wakati watu Wake wanaposikia rai Yake na kuziacha sanamu zao; wanapomwelekea tena Bwana, wakati uams-ho na matengenezo haya makubwa yaliyoitishwa katika sura hii hatimaye yametekelezwa. Hivi divyo ilivyo

7

“maana kwa sauti ya Bwana, Mwashuri atavunjika-vunjika, yeye apigaye kwa bakora.” Isa. 30:31. Tangu hapo Mfalme atatawala kwa haki. Ndipo watu wabaya na wanafiki watatendewa kama hivyo. Katika siku hiyo yatakuwapo mavuno ya roho makubwa na matukufu. Sasa kwamba tumeona wazi wakati, hitaji, na ukombozi, hebu Ndugu, Dada, tuilete siku hiyo karibu kwa kuachana na sanamu zetu zote, na kuigeuza mioyo yetu kika-milifu na kabisa kwa Mungu wetu. {1TG33: 7.3}

8

ANDIKO LA SALA

Njooni Kwa Mungu Kama Watoto Wadogo

Alasiri hii tutaendelea kusoma kutoka katika “Mlima wa Baraka.” Tutachukulia pale tulipoachia juma lililopita, ukurasa wa 191. {1TG34: 9.1}

M.B., uk. 191 — “Lakini usisahau kwamba kumwendea Mungu kama baba, unatambua uhusiano wako kwake Yeye kama mtoto. Hauuamini tu wema Wake, bali katika mambo yote nyenyekea kwa mapenzi Yake, ukijua kwamba upendo Wake haubadiliki. Unajitolea kuifanya kazi Yake. Ilikuwa ni kwa wale alikuwa amewaambia wautafute kwanza ufalme wa Mungu na haki Yake ambao Yesu alitoa ahadi, ‘Ombeni, nanyi mtapokea.’ {1TG34: 9.2}

“Zawadi zake Yeye aliye na mamlaka yote mbinguni na duniani zimehifadhiwa kwa ajili ya watoto wa Mungu. Zawadi za thamani sana hivi kwamba hutujia kupitia kafara ya gharama kubwa ya damu ya Mkombozi; zawadi ambazo zitaridhisha hamu ya ndani ya moyo; Zawadi za kudumu kama umilele, zitapokelewa na kufurahiwa na wote watakaokuja kwa Mungu kama watoto wadogo. Zichukue ahadi za Mungu kama zako mwenyewe, sihi mbele Yake kama maneno Yake mwenyewe, na utapokea ujazi wa furaha.” {1TG34: 9.3}

Hebu tuombe kwa ajili ya kugundua kwamba uhusiano wetu na Mungu ni kama uhusiano wa mtoto na wazazi wake; ya kwamba tunamwamini Mungu katika mambo yote kama vile mtoto huwaamini wazazi wake; ili tujue kwamba iwapo tukijikabidhi kikamilifu kufanya mapenzi Yake na kazi, basi tunaweza kuomba na kupokea; kwamba ametuhifadhia zawadi ili kutosheleza hamu ya ndani ya moyo, zawadi za kudumu kama umilele; na kwamba iwapo tutamwendea Yeye tu kama watoto wadogo na kumwamini Yeye kwa neno Lake, ahadi hizi zote katika Neno Lake zitakuwa zetu. {1TG34: 9.4}

9

MATEKA WA MHARABU WACHUKULIWA NA WACHECHEMEAO NA WADHAIFU

MATINI YA HOTUBA NA V. T. HOUTEFF

MCHUNGAJI WA WADAUDI WAADVENTISTA WA SABATO

SABATO, MACHI 29, 1947

HEKALU LA MLIMA KARMELI

WACO, TEXAS

Mada hii inapatikana katika Isaya 33. Tutaanza somo letu na— {1TG34: 10.1}

Isa. 33: 1 — “Ole wako uharibuye ila hukuharibiwa, utendaye hila wala hukutendwa hila! Utakapokwisha kuharibu, utaharibiwa wewe; na utakapokwisha kutenda kwa hila, wao watakutenda hila wewe.”

Kuzingatia kinachofuata katika sura hii na katika sura mbili zijazo (kwa sura ya 34 na 35 ni sehemu ya mada am-bayo iko katika sura ya 33), inabainika kuwa yule ambaye juu yake “ole” imetamkwa ni kanisa linalotangulia “Siku kuu na ya kutisha ya Bwana,” katika siku ambayo wahambi wa Sayuni wataangamia, katika siku ambayo wale waliotubu wanapewa thawabu yao, — “Maana ni siku ya kisasi cha Bwana, mwaka wa malipo, ili kushinda-nia Sayuni.” Isa. 34: 8. {1TG34: 10.2}

Kanisa linaonyeshwa haswa kwa ukweli kwamba, tofauti na Kanisa la Agano la Kale, limekuwa likiharibu lakini halijaharibiwa; ya kwamba limekuwa likifanya hila lakini lenyewe halijashughulikiwa. Uvuvio, hata hivyo, unaendelea kutabiri

10

kinyume cha hali hii: Kanisa litaharibiwa na kushughulikiwa kwa hila. Waaminifu Wake walio kati yake, hata hivyo, watapata neema, kwa sababu wanasihi: {1TG34: 10.3}

Aya ya 2 — “Ee Bwana, uturehemu; tumekungoja wewe; uwe wewe mkono wetu kila asubuhi,na wokovu wetu pia wakati wa taabu.”

Aya hii inaonyesha kwamba wakati ambapo matamshi ya ole (Isa. 33: 1) yanafanywa, wakati huo huo maten-genezo yaliyokita mizizi yatakuwa yanafanyika kati ya watu watafuta Ukweli wa Mungu. Wanaomba, sio kwa ajili yao wenyewe, ila kwa ajili ya ndugu zao pia. Wanatambua kikamilifu kwamba wanaujongea wakati wa taa-bu, na tumaini lao liko katika ukweli kwamba wamemngojea Bwana. Nguvu ya Mungu itahisiwa duniani kote: {1TG34: 11.1}

Aya ya 3 — “Kabila za watu wamekimbia wakisikia kelele za fujo; mataifa wametawanyika ulipojiinua nafsi yako.”

Aya hii inafichua kwamba wakati Mungu ambapo anaonyesha nguvu Yake miongoni mwa watu Wake, ulim-wengu utahisi athari zake. {1TG34: 11.2}

Aya ya 4 — “Na mateka yako yatakumbwa kama wadudu wakumbavyo, wataruka juu yake kama arukavyo nzige.”

Nyara ambazo kanisa limechuma, Yeye anazikusanya kama mkusanyiko wa viwavi. Kisha itanenwa: {1TG34: 11.3}

Aya ya 5 — “Bwana ametukuka; kwa maana anakaa juu; amejaza Sayuni hukumu na haki.”

11

Wakati ambapo mambo haya yatatukia, basi Zayuni (kanisa lililotakaswa) litajazwa na hukumu na haki. Zaidi ya hayo, waaminifu wa Mungu wanao uhakikisho huu: {1TG34: 12.1}

Aya ya 6 — “Nyakati zako zitakuwa nyakati za kukaa imara; za wokovu tele na hekima na maarifa; kum-cha Bwana ni hazina yake ya akiba.”

Lakini kuhusu hodari wao ambao hawakutubu, Uvuvio unatangaza: {1TG34: 12.2}

Aya ya 7 — “Angalia, mashujaa wao wanalia nje, wajumbe wa amani wanalia kwa uchungu.”

Hapa tunaona kwamba wale wanaotangaza amani badala ya siku ya Mungu, watalia “kwa uchungu.” {1TG34: 12.3}

Aya ya 8 — “Njia kuu zimeachwa, msafiri amekoma; ameyavunja maagano, ameidharau miji, hamjali mtu.”

Katika usemi wa leo aya hii ingalisomwa: Njia za wamishonari zimeachwa; mmishonari mwenyewe amekoma; ameuvunja mkataba wake; ameidharau miji; hamjali mtu. {1TG34: 12.4}

Aya ya 9 — “Nchi inaomboleza, na kulegea; Lebanoni imetahayarika na kunyauka; Sharoni imekuwa kama jangwa; Bashani na Karmeli zimepukutika majani.”

Nomino katika aya hii zikiwa ni za mfano sana, na wakati wa utimizo bado ni baadaye, hatujajiandaa kutoa maelezo yoyote. {1TG34: 12.5}

Aya ya 10 — “Basi, sasa nitasimama; asema Bwana; sasa nitajiinua, sasa nitajitukuza.”

12

Wakati ambapo hali zilizoelezwa hapa zinatukia, kisha inakuwa kwamba Bwana atainuka na kutukuzwa na kuinuliwa. Lakini kwa wale walio na makosa Yeye anaonya kimbele: {1TG34: 13.1}

Aya ya 11 — “Ninyi mtachukua mimba ya makapi, mtazaa majani makavu; pumzi yenu ni moto uta-kaowateketeza wenyewe.”

Akiwaelekea wadhambi na wanafiki kati ya watu Wake, wale ambao juu yao ole ya aya ya kwanza hasa imenenwa, Mungu anafichua kwamba matunda ya matendo yao yatakuwa makapi na majani makavu, kwamba pumzi yao itawaangamiza kana kwamba ni moto. Zaidi ya hayo, juu ya wafuasi wao Yeye anaongeza: {1TG34: 13.2}

Aya ya 12 — “Nao mataifa watakuwa kama kuchoma chokaa, kama miiba iliyokatika, iteketezwayo mo-toni.”

Baada ya kuanza kazi Yake ya utakaso ndani ya Zayuni, Yeye anatangaza: {1TG34: 13.3}

Aya ya 13, 14 — “Sikieni, ninyi mlio mbali, niliyoyatenda; na ninyi mlio karibu, kirini uweza wangu. Wenye dhambi walio katika Sayuni wanaogopa; tetemeko limewashika wasiomcha Mungu; Ni nani kwetu sisi awezaye kukaa na moto ulao; ni nani kwetu sisi awezaye kukaa na moto uteketezao milele?”

Wakati Hakimu mwenye haki atakapoinuka kuwapepeta watu, wakati huo wanafiki hawatakuwa wakijigamba kwamba wao “ni Wakristo wazuri kama yeyote.” Wala hawatasema tena, “Hatuhitaji Ukweli zaidi.” Badala yake, hofu na mshangao utawapata. Swali kubwa na la heshima sana basi litakuwa, “Ni nani kwetu sisi awezaye kukaa na moto ulao; ni nani kwetu sisi awezaye kukaa na moto uteketezao milele?” {1TG34: 13.4}

13

Na hapa lipo jibu la jumla: {1TG34: 14.1}

Aya ya 15-17 — “Ni yeye aendaye kwa haki, anenaye maneno ya adili; ni yeye anayedharau faida ipatika-nayo kwa dhuluma; akung’utaye mikono yake asipokee rushwa; azibaye masikio yake asisikie habari za damu; afumbaye macho yake asitazame uovu. Huyu ndiye atakayekaa juu; majabali ni ngome yake; atapewa chakula chake; maji yake hayatakoma. Macho yako yatamwona mfalme katika uzuri wake, yataona nchi iliyoenea sana.”

Kupita kutoka kwa usemi huu wa malezi ya Mungu na mandhari ya uzuri, wanaambiwa ifuatayo: {1TG34: 14.2}

Aya ya 18 — “Moyo wako utatafakari hofu ile; Yuko wapi yeye aliyehesabu? Yuko wapi yeye aliyeupima ushuru? Yuko wapi yeye aliyeihesabu minara?”

Wa kutisha hakika ni utambuzi kwamba wale wanaopatikana bila vazi la harusi (kati yao ni wale ambao wana-shikilia ofisi za juu kanisani, katibu na mtunza hazina) wanatupwa nje kulia na kusaga meno yao. Lakini masalia, wale waliosazwa, watainuliwa. Kwa wao Bwana anasema: {1TG34: 14.3}

Aya ya 19 — “Hutawaona watu wale wakali; watu wa maneno magumu usiyoweza kuyafahamu; wenye lugha ya kigeni usiyoweza kuelewa nayo.”

Wageni wanaopita ukaguzi wa Mwalimu kwa kweli watafanywa kuwa wakuu. Iwe ni katika ufahamu wa usemi wa kina, au iwe ni katika ufahamu wa usemi wa kigugumizi, hakuna atakayekuwa mkuu kuliko wao. Macho ya waaminifu kisha yanaelekezwa kwa mji wa Mungu. {1TG34: 14.4}

14

Aya ya 20 — “Angalia Sayuni, mji wa sikukuu zetu; macho yako yatauona Yerusalemu umekuwa kao la raha; hema isiyotanga-tanga; vigingi vyake havitang’olewa, wala kamba zake hazitakatika.”

Baada ya wakorofi kuondolewa, wakati huo watu wa Mungu wataonekana wamesimama imara na kwa uhakika, wakisimama bila hata nafasi ndogo kabisa ya kusumbuliwa. Na watakatifu watajaa furaha. Hata sasa wanapaaza sauti: {1TG34: 15.1}

Aya ya 21, 22 — “Bali huko Bwana atakuwa pamoja nasi, mwenye adhama; mahali penye mito mipana na vijito, pasipopita mashua na makasia yake; wala hapana merikebu ya vita itakayopita hapo. Kwa maana Bwana ndiye mwamuzi wetu; Bwana ndiye mfanya sheria wetu; Bwana ndiye mfalme wetu; ndiye ataka-yetuokoa.”

Vitu hivi vyote vitakuwa vyetu ikiwa tutakuwa waaminifu hadi mwisho. Tena akihutubia kanisa ambalo linai-jonea siku kuu na ya kutisha ya Bwana, Yeye anatangaza — {1TG34: 15.2}

Aya ya 23 — “Kamba zako zimelegea; hawakuweza kukaza sana shina la mlingoti wao; hawakuweza kulikunjua tanga; ndipo mapato ya mateka yaligawanywa, hata wachechemeao walipata mateka.”

Wale ambao hawaitii sauti ya Bwana, hapa wameonywa kimbele kwamba siku iko karibu ambapo watajikuta hawawezi tena kukusanya mateka. Halafu inakuwa kwamba mateka wao watagawanywa, na wachechemeao — wanaoonekana wadhaifu na hohe hahe — watachukua mateka. {1TG34: 15.3}

Aya ya 24 — “Wala hapana mwenyeji atakayesema, Mimi mgonjwa; watu wakaao humo watasamehewa

15

uovu wao.”

Hebu fikiria! Kitambo kidogo, iwapo tutakuwa waaminifu, hakuna tena mmoja wetu atahitaji kusema, mimi ni mgonjwa. {1TG34: 16.1}

Sasa kupitia tena kauli chache za somo letu: {1TG34: 16.2}

Juu ya wale wasio waaminifu ambao wanaikaribia “siku kuu na ya kutisha ya Bwana,” Mungu anatamka laana: Kanisa litatwaliwa mateka ambao limepata na litashughulikiwa kwa hila kama vile ambavyo limeshughulika na wengine. {1TG34: 16.3}

Ni wazi kabisa, wakati ambapo matamshi haya yanafanywa, matengenezo yaliyokita mizizi yanafanyika kati ya watu watafuta Ukweli wa Mungu. Wanatambua ukweli kwamba wanaujongea wakati wa taabu, na wanahakikishiwa kwamba uthabiti wao na nguvu ya wokovu utapatikana katika hekima na maarifa, katika Roho na ndani ya Ukweli wa siku hiyo. Kumcha Bwana itakuwa hazina yao kuu. {1TG34: 16.4}

Wakati ambapo Mungu anaidhihirisha nguvu Yake kati ya watu Wake, hata ulimwengu utahisi athari zake. Njia za wamishonari zimeachwa, mmishonari mwenyewe anakoma; hamjali mtu. Mungu anafichua kwamba matunda ya wenye dhambi na wanafiki kati ya watu wake, yatakuwa makapi na majani makavu; pumzi yao wenyewe itawaangamiza kana kwamba ni moto. Hofu na mshangao utawapata. {1TG34: 16.5}

Kisha inakuwa kwamba Zayuni, kanisa lililotakaswa, litajazwa hukumu na haki. Mungu wakati huo atatukuzwa na kuinuliwa. Watu Wake ambao wametembea kwa unyofu, watabarikiwa na utunzi Wake Mtakatifu. Macho yao yatamwona Mfalme na uzuri Wake; kanisa litakuwa thabiti na la uhakika, halitasumbuliwa

16

tena kamwe; mateka ambao dhehebu limepata, yatachukuliwa na wachechemeao — na watu wa kweli wa Mun-gu. Watasamehewa maovu yao, na afya yao itarejeshwa. Naam, ahadi kwa ajili yako ni ya uhakika:… afya yako itatokea mara: na haki yako itakutangulia; utukufu wa BWANA utakufuta nyuma ukulinde ” (Isa. 58: 8), ikiwa utatii onyo hili kuu na kusalia mwaminifu kwalo. {1TG34: 16.6}

*******

Wakati ambapo unaagiza nakala za ziada za “Trakti za Vuli,” tafadhali bainisha gombo na namba ya somo bada-la ya tarehe au jina. Hili litawezesha kuingiza agizo lako bila kukawia. {1TG34: 17.1}

Usiyakose Manufaa Juu ya Hili

Iwapo haujatuma kwa ajili ya nakala yako iliyotangazwa na iliyojadiliwa sana kijitabu cha afya cha kurasa 96 (Kabari Inayoingia) ambacho kimefanya uamsho mkubwa katika dunia ya Waadventista na ambacho kimeliweka Shirika la K.I. katika mwangaza, usikikose iwapo afya, nyumba, na furaha yako inamaanisha kitu kwako. Kwa maoni yetu kitabu hiki ndicho bora hatujawahi kuona juu ya su-ala hili. Kwa kweli tunahisi kwamba kimetumwa na Mungu, na kwamba nakala yake inapaswa kuwa katika kila nyumba. Tumejulishwa kwamba sasa unaweza kukipata bila kuagizia. Tuma jina lako, anwani, na jina la kanisa ambalo wewe ni mshiriki (unaombwa kuchap-isha), na senti 15 kwa sarafu au stempu kwa Shirika La Kabari Inayoingia La Marekani, Kituo cha Mlima Kar-meli, Waco, Texas, Marekani na kitatumwa kwako. {1TG34: 17.2}

17

ANDIKO LA SALA

“Nanyi Watendeeni Vivyo Hivyo”

Andiko letu alasiri hii linapatikana kwenye ukurasa wa 192 na 193 wa “Mlima wa Baraka” — {1TG35: 18.1}

“Juu ya uhakikisho wa upendo wa Mungu kwetu, Yesu huagiza upendo mtu kwa mwenzake, kwa kanuni moja kamili inayoufunika mahusiano yote ya ushirika wa wanadamu. {1TG35: 18.2}

“Wayahudi walikuwa wamehangaika juu ya ni nini walipaswa kupokea; mzigo wa hangaiko lao ulikuwa kuhifadhi kile walichofikiria ni haki yao ya mamlaka na heshima na huduma. Lakini Kristo hufundisha kwamba hangaiko letu halipaswi kuwa, Tunaweza kupokea kiasi gani? ila, tunaweza kutoa kiasi gani? Kiwango cha waji-bu wetu kwa wengine kinapatikana katika yale ambayo sisi wenyewe tungaliona kama wajibu wao kwetu. {1TG35: 18.3}

“Kila mtu ambaye amefanywa kuwa wakili wa neema nyingi za Mungu, ameitwa kupeana kwa roho zilizo kwa ujinga na gizani, kama vile, angalivyokuwa katika nafasi yao, angetumaini wao wampe yeye …. {1TG35: 18.4}

“Vivyo hivyo na zawadi na baraka za maisha haya: chochote unachoweza kumiliki zaidi ya wenzako, hukuweka kwenye deni, kwa kiwango hicho, kwa wale wote ambao wamejaaliwa kidogo.” {1TG35: 18.5}

Je! Tuombe kwa ajili ya nini alasiri hii? – kwamba tuweze kuinywa kanuni kuu ya Sheria ya Upendo, na tugun-due kuwa hangaiko letu halipaswi kuwa ni kwa kiasi gani tutapokea, ila ni kwa kiasi gani tunaweza kutoa. Hebu tuombe kwa ajili ya ufahamu kwamba kiwango cha wajibu wetu kwa wengine kinapatikana katika yale ambayo sisi kibinafsi tungaliweza kuona kama wajibu wao kwetu; na pia kwamba chochote tunachomiliki zaidi ya wen-zetu hutuweka katika kiwango hicho cha deni kwa wale waliojaaliwa kidogo. {1TG35: 18.6}

18

MATAIFA YANAONA EDOMU UKIANGAMIA, JANGWA LACHANUA, NA NJIA KUU KWEN-DA ZAYUNI

MATINI YA HOTUBA NA V. T. HOUTEFF

MCHUNGAJI WA WADAUDI WAADVENTISTA WA SABATO

SABATO, APRILI 5, 1947

HEKALU LA MLIMA KARMELI

WACO, TEXAS

Mada yetu alasiri hii inapatikana katika Isaya 34 na 35. Juma lililopita, mnakumbuka, tulisoma sura ya thelathini na tatu, mzigo wa Bwana kulihusu kanisa wakati ambapo linajongea wakati wa “mavuno” — wakati ambapo “ngano” inawekwa ghalani, na “magugu” kuchomwa (Mat. 13:30); wakati ambapo “samaki wazuri” wanawekwa ndani ya “vyombo” na “samaki wabaya” kutupwa nje (Mat. 13: 47-49) kama ilivyo kwa wale ambao hawana “vazi la harusi” (Mat. 22: 1-13) ). Kuendelea sasa katika sura ya thelathini na nne, tunaona humo kwamba Mun-gu anayaalika mataifa ya ulimwengu kukaribia na kuisikia kazi Yake yenye nguvu ya kusafisha: {1TG35: 19.1}

Isa. 34: 1-3 — “Karibuni, enyi mataifa, mpate kusikia; sikilizeni, enyi kabila za watu; dunia na isikie, na-cho kiijazacho, ulimwengu na vitu vyote viutokavyo. Maana Bwana ana ghadhabu juu ya mataifa yote, na hasira kali juu ya jeshi lao lote; amewaangamiza kabisa, amewatoa waende kuchinjwa. Watu wao waliou-awa watatupwa nje, na uvundo wa maiti zao utapaa juu, na milima itayeyushwa kwa damu yao.”

Je! Ni kwa nini Mungu anayaalika mataifa ya ulimwengu wote yakaribie na kusikia? — Ili wapate kuiangalia hasira Yake dhidi ya waovu katika kanisa Lake na wajue

19

watakachotarajia wakati ambapo Hukumu Yake itakapoenea kati ya mataifa yote; ili wapate kujua nini wa-takachotarajia wakati kazi Yake ya kusafisha itakapoanza kati yao; kwamba wapate kimbele kuhesabu gharama. Hukumu Yake, Anasema, tayari imetangazwa juu ya majeshi ya ulimwengu — “Kwa maana wakati umefika wa hukumu kuanza katika nyumba ya Mungu; na ikianza kwetu sisi, mwisho wao wasioitii injili ya Mungu utaku-waje?” — 1 Pet. 4:17. {1TG35: 19.2}

Aya ya 4 — “Na jeshi lote la mbinguni litafumuliwa, na mbingu zitakunjwa kama karatasi, na jeshi lao lote litanyauka kama vile jani la mzabibu linyaukavyo na kupukutika, na kama jani la mtini linyaukavyo na kupukutika.”

Wakati aya ya 3 inaonyesha kuwa matukio muhimu ya sura hii yanatukia katika siku ya mpango mkubwa wa kujihami wa ulimwengu wote, aya ya 4, ikiwa kwa usambamba na Ufunuo 6: 14, inafichua kwamba yanatukia katika kipindi cha muhuri wa sita, Katika siku za kutiwa muhuri kwa watu 144,000 na kukusanywa kwa umati mkubwa usioweza kuhesabika kutoka kwa mataifa yote, muhuri ambao sasa tunaishi ndani yake. Muhuri wa sita unaweza kuingiliana na wa saba. {1TG35: 20.1}

Aya ya 5-11 — “Maana upanga wangu umekunywa na kushiba mbinguni; tazama, utashukia Edomu, na juu ya watu wa laana yangu, ili kuwahukumu. Upanga wa Bwana umeshiba damu, umenona kwa unono, kwa damu ya wana-kondoo na mbuzi, kwa mafuta ya figo za kondoo waume; maana Bwana ana dhabihu huko Bozra, machinjo makubwa katika nchi ya Edomu. Na nyati watatelemka pamoja nao, na mahasai pamoja na mafahali, na nchi yao italewa kwa damu, na mavumbi yake yatanoneshwa kwa shahamu. Maana ni siku ya kisasi cha Bwana, mwaka wa malipo, ili kushindania Sayuni.

20

Na vijito vyake vitageuzwa kuwa lami, na mavumbi yake yatageuzwa kuwa kiberiti, na ardhi yake itaku-wa lami iwakayo. Haitazimwa mchana wala usiku, moshi wake utapaa milele; tangu kizazi hata kizazi itakuwa ukiwa; hapana mtu atakayepita kati yake milele na milele. Mnandi na nungu wataimiliki, bundi na kunguru watakaa huko, naye atanyosha juu yake kamba ya ukiwa na timazi ya utupu.”

Laana ya haraka, tunaona, inatua juu ya Edomu. Kunena ki-uakisi, ni nchi ya Waesau wa uakisi — wale ambao kwa haki wangalikuwa wameihifadhi ofisi ambayo Wayakobo wa uakisi wanaichukua kutoka kwao. Wao wanaipuuza thamani yake hivi kwamba, kama Esau wa zamani, huuza haki zao kwa ajili ya bakuli la mchuzi wa ndengu kwa mfano. (Kwa masomo zaidi juu ya mada hii, angalia “Fimbo ya Mchungaji,” Gombo la 1, uk. 52-111.) {1TG35: 21.1}

Aya ya 12 — “Watawaitia wakuu wake ufalme, lakini hawatakuwapo; wakuu wake wote wamekuwa si kitu.”

Kwa udhahiri baada ya uharibifu kuanguka juu ya Edomu, hakuna hata mmoja wa wale wanaoitwa watawala wake atakayepatikana huko kushiriki katika kutoka (Isa. 11: 11) kwenda kwa Ufalme wa uakisi (kanisa lili-lotakaswa), na wakuu wake watakuwa kama sio kitu. Kisha, lazima iwe kwamba wale ambao wanaokoka na kuingia ndani ya Ufalme ni kwa wingi kutoka kwa watu wa kawaida, wale wa kutoka njia kuu na vichochoro (Luka 14: 16-21). “… Katika kazi ya kicho ya mwisho watu wakuu wachache watahusishwa. Wamejitosheleza kwa ubinafsi, hawamtegemei Mungu, na hawezi kuwatumia.” — “Shuhuda kwa Kanisa,” Gombo la 5, uk. 80. “… Wale tu ambao wameweza kuyahimili majaribu katika Uwezo wake Mwenye Nguvu ndio wataruhusiwa kuten-da sehemu kuutangaza

21

[Ujumbe wa Malaika wa Tatu] wakati ambapo utakuwa umeumuka kuingia Kilio Kikuu.” — “Mapitio na Kuhubiri,” Novemba 18, 1908. {1TG35: 21.2}

Aya ya 13 — 15 — “Miiba itamea majumbani mwake, upupu na mbigili ndani ya maboma yake; nayo itakuwa kao la mashetani, na ua la bundi. Na hayawani wa nyikani watakutana na hayawani wa kisiwani, na jini anamwita mwenziwe; mtiti anakaa huko na kujipatia raha. Huko bundi mkubwa atafanya kioto chake na kuzaa na kuotamia, na kukusanya watoto wake katika kivuli chake: naam, huko watakusanyika tai, kila mmoja na mwenzake.”

Mungu haiachi nchi. Yeye haipotezi nguvu Yake wala shauku Yake katika Ukweli na haki. Yeye hauachi ulim-wengu utoweke. Kile ambacho Hufanya, hata hivyo, ni kuifanya mifano ya baadhi ili Awaokoe wengine wengi, maana wakati ambapo hukumu za Mungu zikiwapo duniani, watu wakaao duniani watajifunza haki. (Isa. 26: 9.) {1TG35: 22.1}

Je! Ni kujihami kwa silaha basi kwamba mataifa ya leo yanahitaji amani na usalama? Je! Vita vya atomiki ni wo-ga wao? — Wanachohitaji kuogopa ni “upanga wa Bwana,” kwa maana “upanga Wake utaogeshwa mbinguni,” “utashuka juu ya Edomu, na juu ya watu wa laana [Yake].” Hawahitaji kuhofia chochote iwapo wanamcha Bwana. Hebu wamfanye kuwa hofu yao, utisho wao na kinga yao (Isa. 8:13). Kwa hivyo Anaamuru: {1TG35: 22.2}

Aya ya 16 — “Tafuteni katika kitabu cha Bwana mkasome; hapana katika hao wote atakayekosa kuwapo, hapana mmoja atakayemkosa mwenzake; kwa maana kinywa changu kimeamuru, na roho yake imewa-kusanya.”

Hapa Mungu anatushauri tuichunguze Biblia na kuamini

22

kabisa kwamba hakuna mmoja wa unabii Wake utakaoshindwa, — la, hakuna mmoja utakaoshindwa kuufuata mwingine kwa zamu yake. Na kwa nini tunapaswa kuwa na imani hii? — Kwa sababu Mungu mwenyewe ame-amuru, na kwa sababu Roho Wake, sio hekima au juhudi za wanadamu zimekusanya katika gombo moja, maandishi ya manabii wa zamani, “kitabu cha Bwana” — Bibilia isiyo ya kidhehebu tunavyoijua leo. {1TG35: 22.3}

Aya ya 17 — “Naye amewapigia kura, na mkono wake umewagawanyia kwa kamba; wataimiliki hata milele, watakaa ndani yake kizazi hata kizazi.”

Bila kujali ikiwa tunachukua aya hii kusema kwamba wanyama wa porini “watamiliki milele,” au ikiwa tun-aichukua kusema kwamba wale wanaotafuta “kutoka kwa kitabu cha Bwana” “wataimiliki milele,” hangaiko letu kuu lazima liwe kumfahamu ki-binafsi Bwana na ukweli Wake ikiwa tungetaka kupata kibali Chake na kukingwa katika wakati huu wa taabu. {1TG35: 23.1}

“Tazama, mfalme atamiliki kwa haki, na wakuu watatawala kwa hukumu. Na mwanadamu atakuwa kama maha-li pa kujificha na upepo, na mahali pa kujisitiri na dhoruba; kama mito ya maji mahali pakavu, kama kivuli cha mwamba mkubwa katika nchi yenye uchovu.” Isa. 32: 1, 2. {1TG35: 23.2}

Sasa tutaendelea kwenye sura ya thelathini na tano ya Isaya, ambayo ni endelezo la ya thelathini na nne. {1TG35: 23.3}

Isa. 35: 1 — “Nyika na mahali palipo ukiwa patafurahi; jangwa litashangilia na kuchanua maua kama waridi.”

Ni tofauti kama nini wakati ambapo Mungu anaidhihirisha nguvu Yake na kulitakasa kanisa Lake! Kisha nchi za watu wa mataifa (nyika) na nchi ya wapagani (mahali

23

palipo ukiwa) zote zitafurahi kuwaona watu watakatifu wa Mungu. Mwishowe kama Ukweli wa Mungu wa wakati huu unavyopenyeza katika nchi ambazo hakuna Wakristo, maeneo ya nyika yatakua kama waridi, kwa mfano, na hivyo kutoa mavuno mengi ya nafsi. {1TG35: 23.4}

Aya ya 2-4 — “Litachanua maua mengi, na kufurahi, naam, kwa shangwe na kuimba; litapewa uzuri wa Lebanoni, utukufu wa Karmeli na Sharoni; watauona utukufu wa Bwana, ukuu wa Mungu wetu. Itieni nguvu mikono iliyo dhaifu, yafanyeni imara magoti yaliyolegea. Waambieni walio na moyo wa hofu, Jipeni moyo, msiogope; tazama, Mungu wenu atakuja na kisasi, na malipo ya Mungu; atakuja na ku-waokoa ninyi.”

Utume huu mkubwa na fursa ya kutangaza kulipiza kisasi cha Mungu ni yetu. Tusishindwe kuchukua manufaa ya fursa hizi. Pamoja na ujumbe wenye nguvu wa wakati huu lazima tuwaimarishe wadhaifu; lazima tuimarishe magoti ambayo yanalegea. Wale ambao hawawezi kusimama na kushikilia yaliyo yao lazima waimarishwe. Lazima tuwahakikishie tena wanaogopa kwamba Mungu atakuja na kisasi dhidi ya wasioamini na thawabu kwa waaminifu. {1TG35: 24.1}

Aya ya 5, 6 — “Ndipo macho ya vipofu yatafumbuliwa, na masikio ya viziwi yatazibuliwa. Ndipo mtu aliye kilema ataruka-ruka kama kulungu, na ulimi wake aliye bubu utaimba; maana katika nyika maji yatabu-bujika; na vijito [vya ukweli] jangwani. “

Wakati mambo haya yanatukia, basi itakuwa kawaida kwa vipofu kuona, viziwi kusikia, viwete kurukaruka, na bubu kuimba, naam, kawaida kama ambavyo maua hufuatwa na matunda. Ukweli wa Mungu kwa wakati huu utaenea kila mahali na kuvuna mavuno makubwa ya nafsi. {1TG35: 24.2}

24

“Naliona mishale ya nuru iking’aa kutoka mijini na vijijini, na kutoka kwenye maeneo ya juu na maeneo ya chini ya dunia. Neno la Mungu lilifuatwa, na matokeo yake zilikuwapo kumbukumbu kwa ajili Yake katika kila mji na kijiji. Ukweli Wake ulitangazwa ulimwenguni kote.” — “Shuhuda”, Gombo la 9, uk. 28. Iwapo ni roho moja tu inaokolewa kutoka kwa kila mji na kijiji zingalikuwapo nafsi mara kadhaa za watu 144,000. {1TG35: 25.1}

Aya ya 7 — “Na mchanga ung’aao mfano wa maji [maeneo ambayo sasa hayana Ukweli] utakuwa ziwa la maji, na nchi yenye kiu [ardhi inayotamani Ukweli wa Mungu] itakuwa chemchemi za maji; katika makao ya majoka, walipokuwa wamelala, patakuwa na majani, pamoja na mianzi na manyasi.”

Yatakuwapo matunda, mnaona, hata mahali ambapo majoka hulala. {1TG35: 25.2}

Aya ya 8 — “Na hapo patakuwa na njia kuu, na njia, nayo itaitwa, Njia ya utakatifu; wasio safi hawatapi-ta juu yake; bali itakuwa kwa ajili ya watu hao; wasafirio, wajapokuwa wajinga, hawatapotea katika njia hiyo.”

Hakuna atakayeachwa “nyikani,” kwa maana patakuwa na njia kuu kwa wafuasi wote wa Ukweli wa Mungu. Haijalishi waaminifu watakuwa nini, wasiojua kusoma wala kuandika au vinginevyo, hawatakosea. Hakika, “ngano” yote itakusanywa na kuwekwa “ghalani,” Ufalme. (Tazama Trakti Namba 3, “Hukumu na Mavuno.”) {1TG35: 25.3}

Aya ya 9 — “Hapo hapatakuwa na simba, wala mnyama mkali hatapanda juu yake; hawataonekana hapo; bali waliokombolewa watakwenda katika njia hiyo.”

Mara tu wanafiki wanapotupwa nje, hawataruhusiwa

25

kurudi na kuhatarisha amani ya watu wa Mungu. Waliokombolewa tu ndio watakaotembea kwenye Njia kuu ya Utakatifu. Na Njia kuu inaongoza wapi? – Aya inayofuata inatoa jibu: {1TG35: 25.4}

Aya ya 10 — “Na hao waliokombolewa na Bwana watarudi, watafika Sayuni wakiimba; na furaha ya milele itakuwa juu ya vichwa vyao; nao watapata kicheko na furaha, huzuni na kuugua zitakimbia.”

Naam, Njia kuu inaelekea Zayuni. Kwa nyimbo na furaha ya milele watakaokombolewa wataingia ndani yake, hawatahuzunika au kuugua kamwe. “Kwa maana anakuja aihukumu nchi. Atauhukumu ulimwengu kwa haki, Na mataifa kwa uaminifu Wake.” Zab. 96:13. {1TG35: 26.1}

Ndugu, Dada, dhabihu ambazo tunaweza kuitwa kutoa ni kama bure kulinganisha na fursa ya kwenda Zayuni kupitia kwa Njia kuu ya Utakatifu. Tafakari juu ya hili, kisha uchukue hatua. Usiruhusu chochote kikuzuie kufu-ata Ukweli wa Mungu kwa ajili ya wakati huu — siku ambayo ndani yake mataifa wataona Edomu ukiangamia na jangwa kuchanua. Tenda sasa wakati ambapo njia kuu ya kwenda Zayuni inatayarishwa. {1TG35: 26.2}

“Sote tulienda chini ya mti na tukaketi kuutaxama utukufu wa mahali hapo, wakati ndugu Fitch na Stockman, ambao walikuwa wamehubiri injili ya ufalme, na ambao Mungu alikuwa amewalaza kaburini ili kuwaokoa, wakaja kwetu na kutuuliza tumepitia nini wakati ambapo walikuwa wamelala. Tulijaribu kuyakumbuka majaribu yetu makubwa zaidi, lakini yalionekana ni madogo sana yakilinganishwa na uzani mzito zaidi na wa milele wa utukufu ambao ulituzunguka kwa nguvu ambayo hatukuweza kutamka, na sote tukapiga kelele, ‘Alleluya, mbingu ni rahisi kwetu!’ na tulivigusa vinubi vyetu vya utukufu na tukayafanya matao ya mbinguni kuvuma.” — “Maandishi ya Awali,” uk. 17. {1TG35: 26.3}

26

-0-0-0-0-0-

Ili kuleta furaha hii isiyoneneka ya ahadi za Mungu, tarajio la vizazi, masomo haya yanachapishwa na kutumwa bila malipo au wajibu kwa wote wanaotaka kuwa nayo. Tuma jina na anwani yako kwa Shirika la Uchapishaji a Ulimwengu, Kituo cha Mlima Karmeli, Waco, Texas. {1TG35: 27.1}

27

Jumuiya ya Wadaudi Waadventista wa Sabato

(Ushirika Huru Unaojumuisha Kanisa)

Mlima Karmeli, Waco, Texas

S.L.P. 23738, Waco, TX 76702

+ 1-254-855-9539

www.gadsda.com

info@gadsda.com

Gombo la 1, Namba 33, 34, 35

Kimechapishwa nchini Marekani

28

>