fbpx

Gombo la 1 Salamu Mwafaka Namba 31, 32

Gombo la 1 Salamu Mwafaka Namba 31, 32

                                    

AMANI YA PEKEE YA MAWAZO

Hati miliki, Kimechapishwa tena 1953

Haki zote zimehifadhiwa

V. T. HOUTEFF

                                    

MTI WA FAMILIA YA KALE

BABA WALIPENDA HILA WATOTO WAO WAPEWA NEEMA

                                    

1

ANDIKO LA SALA

Nitasoma kutoka katika “Mlima wa Baraka,” kuanzia ukurasa wa 188, aya ya mwisho. {1TG31: 2.1}

M.B., uk. 188 — “Yesu … alitamani sana kwamba umati mkubwa ungaliweza kuthamini rehema na fadhili za up-endo wa Mungu. Kama kielelezo cha hitaji lao, na cha hiari ya Mungu kutoa, Yeye huwasilisha mbele yao mtoto aliye na njaa akimuuliza mzazi wake wa duniani mkate. “Kuna mtu yupi kwenu,” Akasema, “ambaye mwanawe akimwomba mkate, atampa jiwe?” Yeye anarai upendo mwororo, wa asili wa mzazi kwa mtoto wake, kisha anasema, ‘Basi ikiwa ninyi, mlio waovu, mnajua kuwapa watoto wenu vipawa vyema; je! si zaidi sana Baba yenu aliye mbinguni atawapa mema wao wamwombao? Hakuna mtu mwenye moyo wa baba atamwacha mwanawe aliye na njaa ambaye anaomba chakula. Je! Wangeweza kufikiria kuwa anao uwezo wa kumchezea mtoto wake, kumtia uchungu kwa kuongeza matarajio yake ili kumvunja moyo?… Je! mtu yeyote aweze kumkosea heshima Mungu kwa kudhani kwamba Yeye hataitikia rai za watoto Wake? {1TG31: 2.2}

“… Roho Mtakatifu, mwakilishi wake Yeye mwenyewe, ndiye zawadi kuu zaidi kuliko zote. ‘Vitu vyote vyema’ hujumuishwa ndani yake. Muumbaji mwenyewe hawezi kutupatia chochote kikuu zaidi, hakuna bora zaidi …. “ {1TG31: 2.3}

Iwapo hatuamini yale Mungu hutuambia, ikiwa hatuamini kile Yeye husema alivyo Yeye, basi tunamdharau. Yeye anayo hamu sana kutupatia vipawa, ila tu ikiwa tunavihitaji. Anayo hamu sana hasa kutupatia zawadi kubwa zaidi — zawadi ya Roho Mtakatifu. Kwa kawaida, pamoja na zawadi hii zawadi zingine zote hutolewa. Ilikuwa zawadi hii ambayo Sulemani aliomba, na pamoja nayo akapewa kwa ukarimu zawadi zingine zote. Hebu vivyo hivyo tuombe kwa ajili ya zawadi hii kuu. Ni kile tu Mungu anataka kutupatia ikiwa tu tutaahidi kwa moyo wote na kwa uaminifu — kuitumia zawadi hiyo vyema kwa njia ambayo Yeye angalitaka tuitumie. {1TG31: 2.4}

2

MTI WA FAMILIA YA KALE

MATINI YA HOTUBA NA V. T. HOUTEFF

MCHUNGAJI WA WADAUDI WAADVENTISTA WA SABATO

SABATO, MACHI 8, 1947

HEKALU LA MLIMA KARMELI

WACO, TEXAS

Hebu tufungue sura ya kumi na moja ya Isaya, na tuanze somo letu na aya ya kwanza. {1TG31: 3.1}

Isa. 11: 1 — “Basi litatoka chipukizi katika shina la Yese, na tawi litakalotoka katika mizizi yake litazaa matunda.”

Hapa upo mti wa familia ambao watu watatu wanajulishwa. Aya hii haisemi fimbo inamwakilisha nani; haisemi Tawi linamwakilisha nani; lakini inasema kwamba shina ni Yese, baba ya mfalme Daudi. Fimbo, bila shaka, am-bayo ilichipuka kwenye shina, haingaliweza kuwa mwingine isipokuwa mwana wa Yese — Daudi, mfalme wa Israeli ya kale. Aya zinazofuatia aya hii zinaelezea kwamba Tawi ni Bwana Mwenyewe. Dhahiri, basi, mti huu wa familia unawakilisha Yese, Daudi, na Kristo. {1TG31: 3.2}

Aya zilizosalia za sura hii zinamhusu Kristo, kazi Yake, na ufalme Wake. {1TG31: 3.3}

Aya ya 2 — “Na roho ya Bwana atakaa juu yake, roho ya hekima na ufahamu, roho ya shauri na uweza, roho ya maarifa na ya kumcha Bwana.”

Juu ya zawadi hii moja — zawadi ya Roho — vitu vyote

3

huitegemea. {1TG31: 3.4}

Aya ya 3, 4 — “Na furaha yake itakuwa katika kumcha Bwana; wala hatahukumu kwa kuyafuata ayaonayo kwa macho yake, wala hataonya kwa kuyafuata ayasikiayo kwa masikio yake; bali kwa haki atawahukumu maskini, naye atawaonya wanyenyekevu wa dunia kwa adili; naye ataipiga dunia kwa fimbo ya kinywa chake, na kwa pumzi ya mdomo wake atawaua waovu.”

Aya hizi, ninao uhakika, hazihitaji maelezo yoyote isipokuwa kutaja kwamba “fimbo ya kinywa Chake” na “pumzi ya mdomo Wake” lazima kumaanishe Neno la Mungu, Ukweli Wake. Ukweli huu hasa ambao tunasikili-za alasiri hii, kwa hivyo, kwa upande mmoja utawaua wale ambao Wanaukataa pamoja na wale ambao Hawautii, ila kwa upande mwingine utawaokoa wale ambao Wanautii, na kuyazingatia matakwa Yake. Tokeo moja ni la asili kama lile lingine. Kwa mfano, je! Kuhubiriwa kwa Injili ya Kristo haikuwaokoa Mitume, lakini wakati uo huo ikasababisha Yuda kujinyonga? Na je! Haikuwaokoa wanafunzi ila ikawaangamiza makafiri wote wa Ye-rusalemu mwaka wa 70 B.K.? {1TG31: 4.1}

Katika Ufalme uliotabiriwa hapa, sio tu watu watakuwa na amani na watu, bali watu na wanyama, na wanyama kwa wanyama pia. Sababu iliyotolewa kwa ajili ya amani kamilifu kama hii ni kwamba nchi itajawa na maarifa ya Bwana. Maarifa, basi, ndiyo tunayohitaji, na je! tutayakataa sasa wakati ambapo yanaletwa bila gharama kwa milango yetu? {1TG31: 4.2}

Mara tu watu wa Mungu wanapopata maarifa haya ya Bwana, mara tu wakati huo ufalme utakuja. Kwa hivyo inakuwa kwamba wakati tunajifunza kwa Mungu na hekima Yake,

4

wakati uo huo tunaleta amani kwa dunia. Kwa udhahiri, basi, wale ambao hawana maarifa haya ya Bwana ha-wawezi kuwa raia wa ufalme Wake. Ni muhimu kama nini, kwamba tujifunze wenyewe; ni muhimu kama nini kwamba tujue Ukweli ni nini kupitia uzoefu wetu binafsi, sio kupitia kwa uzoefu wa wengine! {1TG31: 4.3}

Aya ya 10 — “Na itakuwa katika siku hiyo, shina la Yese lisimamalo kuwa ishara kwa kabila za watu, yeye ndiye ambaye mataifa watamtafuta; na mahali pake pa kupumzikia patakuwa na utukufu.”

Yaani, katika siku ya Tawi (katika kipindi cha Ukristo), katika siku ambayo mti huu wa familia unakamilishwa, kisha inakuwa kwamba ufalme wa amani (kanisa lililotakaswa) unachipuka, kwa mfano, kutoka chini hadi juu. Unasimama basi kuwa ishara kwa watu, na kwa Huo Mataifa watautafuta kwa ajili ya wokovu. Bila shaka, basi, mti huu wa zamani wa familia, Ufalme, utasimamishwa wakati muda wa rehema ungalipo. Zaidi ya hayo, mahali ambapo Utasimama (kupumzikia) patakuwa na utukufu. Kwa hivyo Utakuwa na eneo Lake, na msitari Wake wa mpaka. Utakuwa kwa ajili ya kuwakusanya watu, safina ya leo kama ilivyokuwa safina ya Nuhu katika siku ya Nuhu. Hivyo tunaletwa tena kwa ukweli ule ule ambao Isaya, sura ya 2, na Mika, sura ya 4, hufundisha: {1TG31: 5.1}

Aya ya 11, 12 — “Na itakuwa katika siku hiyo, Bwana atapeleka mkono wake mara ya pili, ili ajipatie wa-tu wake watakaosalia, kutoka Ashuru, na kutoka Misri, na kutoka Pathrosi, na kutoka Kushi, na kutoka Elamu, na kutoka Shinari, na kutoka Hamathi, na kutoka visiwa vya bahari. Naye atawatwekea mataifa bendera, atawakutanisha watu wa Israeli waliotupwa, atawakusanya watu wa Yuda waliotawanyika, kutoka

5

ncha nne za dunia.”

Bwana atawaokoa masalia (wale ambao wamesazwa) wa watu Wake katika siku ambapo Ufalme huu unasimamishwa; yaani, Ufalme unaanzishwa, kisha wale ambao wameachwa kati ya watu wa Mataifa, wale wanaoitafuta ishara hiyo, Bwana atawaokoa. Uokozi huu wa pili wa watu Wake unatangaza Uvuvio, utakuwa kutoka ncha nne za dunia. Wa kwanza, kama unavyojua, ulikuwa kutoka Misri tu. {1TG31: 6.1}

Aya ya 13-15 — “Na wivu wa Efraimu utaondoka, na wale wanaomwudhi Yuda watakatiliwa mbali; Efraimu hatamhusudu Yuda, wala Yuda hatamwudhi Efraimu. Nao watashuka, watalirukia bega la Wa-filisti upande wa magharibi; nao pamoja watawateka wana wa mashariki; watanyosha mkono juu ya Edomu na Moabu; na wana wa Amoni watawatii. Na Bwana atauangamiza kabisa ulimi wa bahari ya Misri; na kwa upepo wake uteketezao atatikisa mkono wake juu ya Mto, naye ataupiga, uwe vijito saba, na kuwavusha watu wenye viatu vikavu.”

Falme zote mbili, Israeli (wakati mwingine huitwa nyumba ya Efraimu) na Yuda, zitarejeshwa na kuunganishwa katika uakisi. Hawatawahi tena kuoneana kijicho au kuudhiana. Na kupitia kwa Ezekieli anaamuru Bwana: {1TG31: 6.2}

“Waambie, Bwana MUNGU asema hivi; Tazama, nitakitwaa kijiti cha Yusufu, kilicho mkononi mwa Efraimu, na kabila za Israeli wenzake, nami nitawaweka pamoja nacho, yaani, pamoja na kijiti cha Yuda, na kuvifanya kuwa kijiti kimoja; navyo vitakuwa kimoja mkononi mwangu. Navyo vijiti, ambavyo uliandika juu yake, vitakuwa mkononi mwako mbele ya macho yao. Ukawaambie,

6

Bwana MUNGU asema hivi; Tazama, nitawatwaa wana wa Israeli toka kati ya mataifa walikokwenda, nami nitawakusanya pande zote, na kuwaleta katika nchi yao wenyewe; nami nitawafanya kuwa taifa moja katika nchi hiyo, juu ya milima ya Israeli; na mfalme mmoja atakuwa mfalme wao wote; wala hawatakuwa tena mataifa mawili, wala hawatagawanyikana kuwa falme mbili tena, hata milele. Wala hawatajitia uchafu tena kwa vinyago vyao, wala kwa vitu vyao vichukizavyo, wala kwa makosa yao mojawapo; lakini nitawaokoa, na kuwatoa katika makao yao yote, ambayo wamefanya dhambi ndani yake, nami nitawatakasa; basi watakuwa watu wangu, nami nitakuwa Mungu wao.” Ezek. 37: 19-23. {1TG31: 6.3}

Hivyo ni kwamba “… katika siku za wafalme hao Mungu wa mbinguni atausimamisha ufalme ambao hau-taangamizwa milele, wala watu wengine hawataachiwa enzi yake [ufalme] bali utavunja falme hizi zote vipande vipande na kuziharibu, nao utasimama milele na milele. Na kama vile ulivyoona ya kuwa jiwe lilichongwa mli-mani bila kazi ya mikono, na ya kuwa lilivunja-vunja kile chuma, na ile shaba na ule udongo, na ile fedha, na ile dhahabu; basi Mungu aliye mkuu amemjulisha mfalme mambo yatakayokuwa baadaye; na ndoto hii ni ya haki-ka, na tafsiri yake ni thabiti.” Dan. 2:44, 45. {1TG31: 7.1}

Ikiwa Ufalme utazivunja falme hizi zote, basi lazima Usimamishwe kabla ya falme hizi kuharibiwa. Jiwe ambalo limekatwa kutoka “mlimani” katika siku za wafalme hao, litakuwa mlima mkubwa, Nao, Ufalme huo, utaujaza ulimwengu wote (Dan. 2:35, 45). {1TG31: 7.2}

Katika siku za Musa Bwana alipiga kijito kimoja tu, Bahari ya Shamu, na taifa moja, Misri. Lakini sasa

7

Bwana anaahidi kupiga kila mto (yote “saba”) na kusababisha watu Wake kutoka pembe nne za dunia wafike katika nchi yao bila hata kulowesha miguu yao. Ingawa leo kama ilivyokuwa katika siku za Musa, jambo kama hilo linaonekana haliwezekani kabisa, lakini ni hakika kwamba kama vile Mungu alivyoliwezesha wakati huo, Ataliwezesha sasa, pia. Vita ni vya Bwana, mapenzi ni yetu. Hatuna chochote cha kufanya ila kutii sauti Yake. Hilo ndilo jukumu letu Ndugu, Dada. {1TG31: 7.3}

Hakuna Ukweli wa Bibilia ulio wazi kuliko huu, na hakuna ukweli muhimu kwa wakati huu kama ulivyo Ukweli huu. Hizi ndio hasa sababu ambazo ama huokoa au kuangamiza — Kuupokea ni kupata dhambi zako zote zimefutwa; Kuukataa, ni kutenda dhambi dhidi ya Roho Mtakatifu. “Leo kama mtasikia Sauti Yake, msifanye migumu [mioyo yenu]” ni ushauri wa Mungu kwako na kwangu. Unajua sasa kwamba Ukweli huu hauwezi kup-ingwa. Jaribu na ujionee mwenyewe. {1TG31: 8.1}

Aya ya 16 — “Itakuwako njia kuu kwa mabaki ya watu wake watakaobaki, watokao Ashuru, kama vile ilivyokuwako kwa Israeli, katika siku ile waliyotoka katika nchi ya Misri.”

Baada ya malimbuko na Mwana-Kondoo kwenda Mlima Sayuni, itakuwako barabara kuu ya mavuno ya pili, kwa wale ambao bado wako “Ashuru,” ulimwengu. Kwa maneno mengine, vizuizi vyote vitaondolewa. Imani yetu haitatuangusha, na tumaini letu halitakuwa bure, kwa maana Mungu hajaiacha nchi. Yeye ambaye huzita-wala na kuziongoza nyota kwenye njia yazo isiyokosea, anao uwezo wa kutuongoza salama hadi kuingia katika nchi yetu. Hakika, kama vile hakuna hata moja kati yazo hukosa kwenye mkondo wake, hivyo hakuna ahadi mo-ja ya Mungu ambayo itashindwa kutimika. Mtu asiwadanganye kwa hili. Jifunze aya kwa aya, neno kwa neno, soma, tulia na waza,

8

usipitie haraka huu chanya, Ukweli wa dharura, kwa maana vile ilivyokuwa siku za mafuriko ndivyo itakavyokuwa sasa, asema Bwana (Mat. 24:37). Mzaliwa wa kwanza (limbuko) ambaye alishindwa kupaka mwimo wa mlango kwa damu ya dhabihu katika kutoka kwa kwanza, mfano, aliangamia. Hivyo yeyote wa malimbuko wa leo ambaye anashindwa kutii matakwa ya ujumbe wa leo, hakika ataangamia kwa silaha za ku-chinja za malaika (Ezek. 9: 5, 6). {1TG31: 8.2}

Isa 12: 1-3 — “Na katika siku hiyo utasema, Ee Bwana, nitakushukuru wewe; Kwa kuwa ijapokuwa ulinikasirikia, Hasira yako imegeukia mbali, Nawe unanifariji moyo. Tazama, Mungu ndiye wokovu wangu; Nitatumaini wala sitaogopa; Maana Bwana YEHOVA ni nguvu zangu na wimbo wangu; Naye amekuwa wokovu wangu. Basi, kwa furaha mtateka maji katika visima vya wokovu.”

“Katika siku hiyo,” yaani, siku ambayo watu Wake wanakusanywa kutoka ncha nne za dunia, katika siku hiyo Watamsifu hivyo, kwa sababu wataona wazi kabisa kwamba hasira Yake imeondolewa kwao. Kwa kweli wa-tajua kwamba Yeye ndiye wokovu wao, kicho chao, na nguvu yao. Kwa hivyo watakunywa kwa furaha kubwa katika kweli mpya zilizofunuliwa za Bibilia. {1TG31: 9.1}

Aya ya 4 — “Na katika siku hiyo mtasema, Mshukuruni Bwana, liitieni jina lake; Yatangazeni matendo yake kati ya mataifa, Litajeni jina lake kuwa limetukuka.”

“Katika siku hiyo,” yaani, katika wakati wa kuwakusanya watahimizana kumsifu Bwana, kuliitia jina Lake, na kuyatangaza matendo Yake kati ya watu. Kisha kwa moyo wote na kwa maarifa watakuwa wakifanya kazi hali-si na yenye manufaa ya umishonari. {1TG31: 9.2}

9

Aya ya 5, 6 — “Mwimbieni Bwana; kwa kuwa ametenda makuu; Na yajulikane haya katika dunia yote. Paza sauti, piga kelele, mwenyeji wa Sayuni; Maana Mtakatifu wa Israeli ni mkuu kati yako.”

Kwa kweli hautaruhusu chochote kizuie au kuizima sauti yako sasa kwamba Mungu anaamuru kupaza sauti na kupiga kelele. {1TG31: 10.1}

“Tazama, mfalme atamiliki kwa haki, na wakuu watatawala kwa hukumu. Na mwanadamu atakuwa kama maha-li pa kujificha na upepo, na mahali pa kujisitiri na dhoruba; kama mito ya maji mahali pakavu, kama kivuli cha mwamba mkubwa katika nchi yenye uchovu.” Isa. 32: 1, 2. {1TG31: 10.2}

La, hili sio theolojia maarufu hufundisha, lakini unakiri kwamba hili ndilo Biblia hufundisha, na kwamba ni lazima Tuiamini badala ya wanadamu. {1TG31: 10.3}

Hadi hapa imani katika ahadi za Mungu haijatuangusha, na kwa nini Yeye atuangushe sasa? – Kamwe Hawezi. Imani iliyo na matendo italeta kila kitu kwa majira yake mwafaka. Maadui wa Ukweli watashindwa, ila Ukweli utashinda, na waaminifu pamoja Nao. {1TG31: 10.4}

“Basi imani ni kuwa na hakika ya mambo yatarajiwayo, ni bayana ya mambo yasiyoonekana. Maana kwa hiyo wazee wetu walishuhudiwa. Kwa imani twafahamu ya kuwa ulimwengu uliumbwa kwa neno la Mungu, hata vitu vinavyoonekana havikufanywa kwa vitu vilivyo dhahiri. {1TG31: 10.5}

“Kwa imani Habili alimtolea Mungu dhabihu iliyo bora kuliko Kaini; kwa hiyo alishuhudiwa kuwa ana haki; Mungu akazishuhudia sadaka zake, na kwa hiyo, ijapokuwa amekufa, angali akinena. Kwa imani Henoko ali-hamishwa,

10

asije akaona mauti, wala hakuonekana, kwa sababu Mungu alimhamisha; maana kabla ya kuhamishwa alikuwa ameshuhudiwa kwamba amempendeza Mungu. Lakini pasipo imani haiwezekani kumpendeza; kwa maana mtu amwendeaye Mungu lazima aamini kwamba yeye yuko, na kwamba huwapa thawabu wale wamtafutao. {1TG31: 10.6}

“Kwa imani Nuhu akiisha kuonywa na Mungu katika habari za mambo yasiyoonekana bado, kwa jinsi alivyom-cha Mungu, aliunda safina, apate kuokoa nyumba yake. Na hivyo akauhukumu makosa ulimwengu, akawa mrithi wa haki ipatikanayo kwa imani. Kwa imani Ibrahimu alipoitwa aliitika, atoke aende mahali pale ataka-popapata kuwa urithi; akatoka asijue aendako. Kwa imani alikaa ugenini katika ile nchi ya ahadi, kama katika nchi isiyo yake, akikaa katika hema pamoja na Isaka na Yakobo, warithi pamoja naye wa ahadi ile ile. Maana alikuwa akiutazamia mji wenye misingi, ambao mwenye kuubuni na kuujenga ni Mungu. {1TG31: 11.1}

“Kwa imani hata Sara mwenyewe alipokea uwezo wa kuwa na mimba; alipokuwa amepita wakati wake; kwa kuwa alimhesabu yeye aliyeahidi kuwa mwaminifu. Na kwa ajili ya hayo wakazaliwa na mtu mmoja, naye alikuwa kama mfu, watu wengi kama nyota za mbinguni wingi wao, na kama mchanga ulio ufuoni, usioweza kuhesabika. Hawa wote wakafa katika imani, wasijazipokea zile ahadi, bali wakaziona tokea mbali na kuzishangilia, na kukiri kwamba walikuwa wageni, na wasafiri juu ya nchi. Maana hao wasemao maneno kama hayo waonyesha wazi kwamba wanatafuta nchi yao wenyewe. Na kama wangaliikumbuka nchi ile waliyotoka, wangalipata nafasi ya kurejea. Lakini sasa waitamani nchi iliyo bora, yaani, ya mbinguni. Kwa hiyo Mungu haoni

11

haya kuitwa Mungu wao; maana amewatengenezea mji. {1TG31: 11.2}

“Kwa imani Ibrahimu alipojaribiwa, akamtoa Isaka awe dhabihu; na yeye aliyezipokea hizo ahadi alikuwa akimtoa mwanawe, mzaliwa pekee; naam, yeye aliyeambiwa, Katika Isaka uzao wako utaitwa, akihesabu ya kuwa Mungu aweza kumfufua hata kutoka kuzimu; akampata tena toka huko kwa mfano. Kwa imani Isaka akawabariki Yakobo na Esau, hata katika habari ya mambo yatakayokuwa baadaye. Kwa imani Yakobo, ali-pokuwa katika kufa, akambariki kila mmoja wa wana wa Yusufu, akaabudu akiegemea kichwa cha fimbo yake. Kwa imani Yusufu, alipokuwa amekaribia mwisho wake, alitaja habari za kutoka kwao wana wa Israeli, akaagi-za kwa habari ya mifupa yake. {1TG31: 12.1}

“Kwa imani Musa, alipozaliwa, akafichwa miezi mitatu na wazazi wake, kwa sababu waliona kwamba ni mtoto mzuri; wala hawakuiogopa amri ya mfalme. Kwa imani Musa alipokuwa mtu mzima, akakataa kuitwa mwana wa binti Farao; akaona ni afadhali kupata mateso pamoja na watu wa Mungu kuliko kujifurahisha katika dhambi kwa kitambo; akihesabu ya kuwa kushutumiwa kwake Kristo ni utajiri mkuu kuliko hazina za Misri; kwa kuwa aliyatazamia hayo malipo. Kwa imani akatoka Misri, asiogope ghadhabu ya mfalme; maana alistahimili kama amwonaye yeye asiyeonekana. Kwa imani akaifanya Pasaka, na kule kunyunyiza damu, ili yule mwenye ku-waangamiza wazaliwa wa kwanza asiwaguse wao. {1TG31: 12.2}

“Kwa imani wakapita kati ya Bahari ya Shamu, kama katika nchi kavu; Wamisri walipojaribu kufanya vivyo wa-katoswa. Kwa imani kuta za Yeriko zikaanguka, zilipokwisha kuzungukwa siku saba. Kwa imani Rahabu, yule kahaba, hakuangamia

12

pamoja na hao walioasi; kwa kuwa aliwakaribisha wale wapelelezi kwa amani. {1TG31: 12.3}

“Nami niseme nini tena? Maana wakati usingenitosha kuleta habari za Gideoni na Baraka na Samsoni na Yeftha na Daudi na Samweli na za manabii; ambao kwa imani walishinda milki za wafalme, walitenda haki, walipata ahadi, walifunga vinywa vya simba, walizima nguvu za moto, waliokoka na makali ya upanga. Walitiwa nguvu baada ya kuwa dhaifu, walikuwa hodari katika vita, walikimbiza majeshi ya wageni. {1TG31: 13.1}

“Wanawake walipokea wafu wao waliofufuliwa. Lakini wengine waliumizwa vibaya hata kuuawa, wasikubali ukombozi, ili wapate ufufuo ulio bora; wengine walijaribiwa kwa dhihaka na mapigo, naam, kwa mafungo, na kwa kutiwa gerezani; walipigwa kwa mawe, walikatwa kwa misumeno, walijaribiwa, waliuawa kwa upanga; walizunguka-zunguka wakivaa ngozi za kondoo na ngozi za mbuzi; walikuwa wahitaji, wakiteswa, wakitendwa mabaya; (watu ambao ulimwengu haukustahili kuwa nao), walikuwa wakizunguka-zunguka katika nyika na katika milima na katika mapango na katika mashimo ya nchi. {1TG31: 13.2}

“Na watu hao wote wakiisha kushuhudiwa kwa sababu ya imani yao, hawakuipokea ahadi; kwa kuwa Mungu alikuwa ametangulia kutuwekea sisi kitu kilicho bora, ili wao wasikamilishwe pasipo sisi.” Waebrania 11. {1TG31: 13.3}

Sasa wakati kumbukumbu za milele zinafanywa, je! Hautasababisha jina lako kuandikwa kati ya mashujaa wakuu wa Mungu? Je! Unawezaje kumudu kupoteza milele saa ya mwisho kama hii? {1TG31: 13.4}

13

BABA WALIPENDA HILA WATOTO WAO WAPEWA NEEMA

MATINI YA HOTUBA NA V. T. HOUTEFF

MCHUNGAJI WA WADAUDI WAADVENTISTA WA SABATO

SABATO, MACHI 15, 1947

HEKALU LA MLIMA KARMELI

WACO, TEXAS

Tutajifunza sura ya thelathini ya Isaya, kuanzia aya ya kwanza. {1TG32: 14.1}

Hapa, kama ilivyo katika sura zingine za unabii wa Isaya, utagundua kwamba sehemu ya sura hiyo (kwa mfano, aya kumi na saba za kwanza) hunena juu ya dhambi za Israeli wa kale, baba za Israeli wa uakisi, na kuhusu an-guko lao kutoka kwa utawala. Lakini salio la sura hiyo hunena juu ya Israeli katika siku za mwisho, siku ambazo Israeli wa uakisi unainuka kutawala. Hebu sasa tuangalie {1TG32: 14.2}

Isa. 30: 1, 2 — “Ole wa watoto waasi; asema Bwana; watakao mashauri lakini hawayataki kwangu mimi; wajifunikao kifuniko lakini si cha roho yangu; wapate kuongeza dhambi juu ya dhambi; waendao kutelemkia Misri wala hawakuuliza kinywani mwangu; ili wajitie nguvu kwa nguvu za Farao, na kutu-mainia kivuli cha Misri.”

Ni dhahiri watu wa Mungu katika siku hizo walikuwa na hatia ya dhambi hizi. Badala ya kumwamini Mungu awaokoe kutoka kwa maadui zao, walimwamini Farao. Ni msaada maskini kama nini wa kuegemea! Kama tokeo waliambiwa wazi: {1TG32: 14.3}

14

Aya ya 3-7 — “Basi, nguvu za Farao zitakuwa aibu yenu, na kutumainia kivuli cha Misri kutakuwa kufadhaika kwenu. Kwa maana wakuu wake wako Soani, na wajumbe wake wamefika Hanesi. Wote wa-tawaonea haya watu wasioweza kuwafaidia, wasio na msaada wala faida, bali ni aibu na sababu ya kushutumiwa. Ufunuo juu ya hayawani wa Negebu. Katikati ya nchi ya taabu na dhiki, Ambayo hutoka huko simba jike na simba, Nyoka na joka la moto arukaye, Huchukua mali zao mabegani mwa punda wachanga, Na hazina zao juu ya nundu za ngamia Waende kwa watu ambao hawatawafaa kitu. Kwa maana Misri huwasaidia bure, bila faida; Kwa hiyo nimepiga kelele, Nguvu yao itakaa kimya.”

Hivi, kama unavyojua, ndivyo ilivyowapata watu wa kale wa Mungu. Ni bora namna gani kukaa kimya, kumngojea Bwana kwa ajili ya msaada wakati umeshindwa kabisa, kuliko kuomba msaada wa maadui Zake! {1TG32: 15.1}

Aya ya 8 — “Haya, enenda sasa, andika neno hili katika kibao mbele ya macho yao, lichore katika kitabu ili liwe kwa ajili ya majira yatakayokuja, kwa ushuhuda hata milele.”

Kweli, waliwaua manabii kwa kuwaonya watu dhambi zao, lakini Mungu aliamuru kwamba maandishi ya man-abii dhidi ya dhambi zilizopo lazima yadumishwe bila kuguswa yasomwe kama mafunzo yenye kielezo kwa vizazi ambavyo vingalifuata baadaye. Watu wa Mungu wa leo, kwa hivyo, hawana udhuru kwa kurudia makosa ya watangulizi wao. Ikiwa watarudia dhambi za watangulizi wao, hata hivyo, basi hatia yao itawaletea adhabu kubwa kuliko ile iliyoletwa kwa Wayahudi. Na iwapo hakuna yeyote anayeweza kukataa kwamba unabii wa Isaya dhidi ya Wayahudi ulitimizwa, basi ni nani anayeweza kuthubutu kusema kwamba hautatimizwa

15

dhidi yetu ikiwa tutashindwa kama wao? {1TG32: 15.2}

Aya ya 9, 10 — “Kwa maana watu hawa ni watu waasi, watoto wasemao uongo, watoto wasiotaka kuisikia sheria ya Bwana; wawaambiao waonaji, Msione; na manabii, Msitoe unabii wa mambo ya haki, tuambi-eni maneno laini, hubirini maneno yadanganyayo.”

Kuwaua manabii kwa kuunena ukweli, watu wa kale wa Mungu walikuwa kwa kweli wakisema, Tuhubirie udanganyifu. Tuambie mambo laini, hatutaki kuujua ukweli unaotuhusu. Je! jambo hili bado lingalipo kati yetu? — Acha niwaambie tukio ambalo litajibu haraka swali hili. {1TG32: 16.1}

Hivi juzi tu kutoka kwa ndugu mchungaji nilipokea barua iliyoandikwa kwa unyenyekevu sana, ambayo kwa uaminifu anaelezea maoni yake kuhusu vitabu vyetu. Kwa upole alieleza kwamba yote aliyo nayo dhidi yake ni kwamba ndani yake huwa tunazungumza juu ya dhambi na makosa ambayo viongozi wa kanisa hutenda. Ikiwa mnawapenda alisema, mtasema tu wema wao. {1TG32: 16.2}

Ninathamini uaminifu wa ndugu huyu katika jambo hili, lakini siithamini hukumu yake juu kuvihusu. Iwapo at-avichunguza tena vitabu hivyo, ninao uhakika atapata kwamba hatukusema chochote ila tu kile Maandiko ya-navyosema juu ya mada hiyo kwa wakati wetu. Kwa hivyo mzigo wake kwa kweli umeelekezwa, sio dhidi yetu bali dhidi ya Mungu Mwenyewe! {1TG32: 16.3}

Shyghuli yetu, Ndugu, Dada, sio kutafuta makosa ama kwa ukasisi au washiriki, bali kwa ukweli kuleta nuruni kile Maandiko yanavyosema kwa watu wa Mungu wa leo. Hatuwezi kufanya vinginevyo, Mungu akitusaidia. Agizo la Ezekieli ndilo agizo letu: {1TG32: 16.4}

16

“Nimwambiapo mtu mbaya, Hakika utakufa; wewe usimpe maonyo, wala husemi na huyo mtu mbaya ili kum-wonya, kusudi aache njia yake mbaya na kujiokoa roho yake; mtu yule mbaya atakufa katika uovu wake; lakini damu yake nitaitaka mkononi mwako.” Ezek. 3:18. {1TG32: 17.1}

Wakati ambapo Wayahudi walitafuta makosa kwa manabii kwa ajili ya kunena juu ya dhambi ambazo makuhani walikuwa wakijifurahisha, kwa kweli walisema: {1TG32: 17.2}

Aya ya 11 — “Tokeni katika njia, geukeni mtoke katika mapito; mkomesheni Mtakatifu wa Israeli mbele yetu.”

Upofu wa kiroho ni kitu cha ukatili. Waathiriwa wake ni vigumu kufanywa wazione dhambi zao au wema wa Mungu. Wanafafanua vibaya na kupotosha kila kitu ambacho kimekusudiwa kwa manufaa yao. {1TG32: 17.3}

Aya ya 12, 13 — “Basi kwa ajili ya hayo Mtakatifu wa Israeli asema hivi, Kwa sababu mwalidharau neno hili, na kutumainia jeuri na ukaidi, na kuyategemea hayo; basi, uovu huu utakuwa kwenu kama mahali palipobomoka, palipo tayari kuanguka patokezapo katika ukuta mrefu, ambapo kuvunjika kwake huja ghafula kwa mara moja.”

Kama macho ya kiroho ya watu wa kale wa Mungu yangaliweza kufumbuliwa, kama wangaliona kwamba dhambi zao zilikuwa zinaudhoofisha msingi ambao walikuwa wamesimama juu yake, wasingalizitemea mate nyuso za manabii kwa kuwaonya kuhusu shida yao. Hakika hapana. Badala yake, wangaliwapokea manabii. {1TG32: 17.4}

Isa. 30:14 — “Naye atapavunja kama chombo cha mfinyanzi kivunjwavyo, akikivunja-vunja asiache kukivunja, hata hakipatikani katika

17

vipande vyake kigae kitoshacho kutwaa moto jikoni, au kuteka maji kisimani.”

Ni nani anayethubutu kukanusha kwamba ufalme wao ulianguka hivyo? Mambo haya yote yaliwajia tu kwa sababu walikataa kuwasikia manabii. {1TG32: 18.1}

Aya ya 15-18 — “Kwa maana Bwana MUNGU, Mtakatifu wa Israeli, asema hivi, Kwa kurudi na kus-tarehe mtaokolewa; nguvu zenu zitakuwa katika kutulia na kutumaini; lakini hamkukubali. Bali ninyi mlisema, La! Maana tutakimbia juu ya farasi; basi, ni kweli, mtakimbia; tena, Sisi tutakimbia juu ya wan-yama waendao upesi; basi, wale watakaowafuatia watakuwa wepesi. Elfu moja watakimbia kwa kuke-mewa na mtu mmoja; kwa kukemewa na watano mtakimbia; hata mtakapoachwa kama mlingoti juu ya kilele cha mlima, na kama bendera juu ya kilima. Kwa ajili ya hayo Bwana atangoja, ili awaonee huruma, na kwa ajili ya hayo atatukuzwa, ili awarehemu; kwa maana Bwana ni Mungu wa hukumu; heri wote wamngojao.”

Kwa sababu hapakuwa na kitu chochote ambacho kingaliweza kufanywa kuwaokoa mababu zetu kutoka kwa aibu, Bwana aliwaruhusu mataifa kuwapiga watu Wake na kuwatawanya kwa pepo nne. Walakini Yeye aliacha ahadi kwamba Angengojea hadi wao kama watu wamepitia kipindi chao cha upotevu, hadi wao kama mtu mmoja mmoja wagundue makosa yao na kumpa Bwana fursa ya kuionyesha neema Yake kwao. Wale wanaom-ngojea Yeye hakika watapata baraka Zake. {1TG32: 18.2}

Kwa aya ya kumi na nane unakuja mgawanyo kati ya simulizi la watu wa Mungu wa zamani na utabiri wa siku za baadaye za watu Wake katika siku za mwisho. Kufikia hatua hii ni kumbukumbu ya wa awali; sasa kuhusu ahadi kwa la mwisho, tunasoma: {1TG32: 18.3}

18

Aya ya 19 — “Kwa maana watu watakaa katika Sayuni huko Yerusalemu; wewe hutalia tena; hakika yake atakuonea rehema nyingi kwa sauti ya kilio chako; asikiapo ndipo atakapokujibu.”

Je! Ni kwa sababu gani Mungu anasubiri kwa uvumilivu? na kwa nini Yeye anaahidi neema Yake kwa watu Wake? — Kwa sababu Ameazimia kwamba watakaa Zayuni huko Yerusalemu. Kusudi Lake ni kuwarejesha hu-ko, na kuwapa pumziko. Kusudi Lake ni kukikomesha kilio chao, kusikia sala zao, na kuwapa mahitaji yao. {1TG32: 19.1}

Hivyo ni kwamba wakati watu wa Mungu wa zamani walikabiliwa na uharibifu, adhabu, na ukiwa, sasa tuna-tazamia urejesho, huruma, na neema. Leo tunayo ahadi ile ile ambayo watu walikuwa nayo katika siku ya Musa — naam, kubwa zaidi. {1TG32: 19.2}

Aya ya 20 — “Na ingawa Bwana atawapeni chakula cha shida na maji ya msiba, lakini waalimu wako hawatafichwa tena, ila macho yako yatawaona waalimu wako.”

Ijapokuwa Mungu zamani aliwaruhusu waalimu wa watu (manabii wao) kusukumwa pembeni, kunyanyaswa, na kuchinjwa, Yeye hataruhusu hilo tena. Macho ya watu Wake yatawaona walimu wao walioteuliwa na Mungu wanapoletwa mbele. {1TG32: 19.3}

Aya ya 21 — “Na masikio yako yatasikia neno nyuma yako, likisema, Njia ni hii, ifuateni; mgeukapo kwenda mkono wa kulia, na mgeukapo kwenda mkono wa kushoto.”

Kwa hivyo hakuna haja ya yeyote kati yetu kwenda kombo. Hakuna kisingizio cha kufanya makosa ambayo hatupaswi kutenda. {1TG32: 19.4}

19

Aya ya 22 — “Nanyi mtakitia najisi kifuniko cha sanamu zenu za fedha zilizochongwa, na mabamba ya sanamu zenu za dhahabu zilizoyeyushwa; utazitupilia mbali kama kitu kilicho najisi; utasema, Haya, toka hapa.”

Hapana, watu waaminifu wa Mungu hawatashikilia kitu chochote kisichompendeza Bwana. Sio tu kwamba wa-tavitupilia mbali vitu vyote vya sanamu, ila kwa kweli watavichukia. {1TG32: 20.1}

Aya ya 23 — “Naye atatoa mvua juu ya mbegu zako, upate kuipanda nchi hii; na mkate wa mazao ya nchi, nayo itasitawi na kuzaa tele; katika siku hiyo ng’ombe zako watakula katika malisho mapana.”

Tunapoyazingatia matakwa yote ya Mungu, basi inakuwa kwamba tutafanikiwa. Kisha inakuwa kwamba yule wa kunyafua atakemewa, na laana kuzuiliwa mbali kutoka kwetu. Tunapaswa kwa hivyo kugundua kwamba ufanisi hautegemei uwezo wa mtu mmoja tu, ila kwamba unategemea zaidi kibali cha Mungu kwa matendo ya mtu. {1TG32: 20.2}

Aya ya 24 — “Ng’ombe pia na wana-punda wailimao nchi watakula chakula kilichokolea, kilichopepetwa kwa ungo na kwa pepeo.”

Ikiwa ng’ombe wetu watakuwa na lishe safi, basi ni muhimu zaidi kama nini sisi wenyewe kuwa na chakula cha kiroho ambacho kimepepetwa na Roho wa Kweli. Hiki ndicho watapata. {1TG32: 20.3}

Aya ya 25 — “Na juu ya kila mlima mrefu, na juu ya kila kilima kilichoinuka, itakuwapo mito na vijito vya maji, katika siku ya machinjo makuu itakapoanguka minara.”

20

Ni wazi, wakati ambapo maji ya wokovu ya Mungu yanaifunika dunia — hata juu ya milima, kwa mfano — basi minara ya walinzi (mimbari), ambayo watu wameijenga kwa mpango wao wenyewe, itaanguka. Bila shaka siku ya machinjo ni siku kuu na ya kutisha ya Bwana. Kwa hivyo tena tunaletwa dafrao kwa uhalisi kwamba Ukweli hufanya mojawapo wa mambo mawili — iwapo Hauwezi kuokoa, Huangamiza. {1TG32: 21.1}

Ukweli huu ambao mnausikiliza leo hakika utaenea ulimwenguni kote kama moto unavyosambaa kwenye mabua makavu. Haijalishi kuwa ni nani anayejaribu kuuzuia Ukweli wa Mungu, najua kwamba wote kama hao wa-tajikwaa na kuanguka na hawatapatikana, ila kwamba Ukweli utaifunika dunia. {1TG32: 21.2}

Aya ya 26 — “Na tena nuru ya mwezi itakuwa kama nuru ya jua, na nuru ya jua itaongezeka mara saba, kama nuru ya siku saba, katika siku ile Bwana atakapofunga mapigo ya watu wake, na kuliponya pigo la jeraha yao.”

Huu usingalikuwa usemi wa mfano, kama jua lingaliweza kuwa moto mara saba kuliko lilivyo, basi dunia yenyewe ingeteketea. Bila shaka jua katika mfano huu limetumika kuonyesha kwamba nuru ya Neno la Mungu sasa wakati ambapo Yeye analifunga “jeraha” la watu Wake, itaongezeka mara saba — nuru yote ambayo ipo itachomoza juu ya nchi kama vile lifanyavyo jua baada ya siku ya mawingu. Zaidi ya hayo, mwezi (kanisa), chombo ambacho huakisi mionzi ya jua ndani ya maeneo yenye giza ya dunia, matokeo yake litatosheleza watu, sio bora zaidi kuliko ambavyo limekuwa hapo awali, ila kikamilifu. Tayari tunaiona nuru ya Neno la Mungu ikiongezeka zaidi na zaidi kila juma linalopita. {1TG32: 21.3}

Aya ya 27 — “Tazama, jina la Bwana linakuja kutoka

21

mbali sana, linawaka kwa hasira yake, kwa moshi mwingi sana unaopaa juu; midomo yake imejaa ghadhabu, na ulimi wake ni moto ulao.”

Tazama! Anaamuru Bwana, kufunuliwa kwa kweli hizi kunaonyesha ila kitu kimoja — kwamba tunakaribia siku kuu na ya kutisha ya Bwana, siku ambayo atakuwapo Bwana mmoja tu, na jina Lake moja. {1TG32: 22.1}

Aya ya 28 — “Na pumzi yake ni kijito kifurikacho, kifikacho hata shingoni, kupepeta mataifa kwa ungo wa ubatili; na lijamu ikoseshayo itakuwa katika taya za watu.”

Pumzi ya Bwana, Neno Lake lililoandikwa, litainuka (Ukweli uliofunuliwa utaongezeka) juu hadi juu mpaka Litafikia “hata shingoni,” kana kwamba, kuwapepeta mataifa. Wa ubatili wataanguka, bali wanyenyekevu, wanaomngojea Bwana, watasimama. {1TG32: 22.2}

Aya ya 29 — “Mtakuwa na wimbo kama vile wakati wa usiku, ishikwapo sikukuu takatifu, mtakuwa na furaha ya moyo kama vile mtu aendapo na filimbi katika mlima wa Bwana, aliye Mwamba wa Israeli.”

Naam, wanaolikataa Neno la Mungu wataweza kuomboleza na kusaga meno yao kwenye giza la nje, lakini wa-tiifu, wale wanaomngojea Bwana, wataimba kama wakati sherehe takatifu inavyoadhimishwa, na, kama il-ivyokuwa, watacheza na filimbi “kama vile mtu aendapo katika mlima [ufalme] wa Bwana.” {1TG32: 22.3}

Aya ya 30 — “Naye Bwana atawasikizisha watu sauti yake ya utukufu, naye atawaonyesha jinsi mkono wake ushukavyo, na ghadhabu ya hasira yake, na mwako wa moto ulao, pamoja na dhoruba, na tufani, na mvua ya mawe ya barafu.”

22

Mungu yu karibu kuidhihirisha nguvu Yake hivyo na kuietea kazi Yake. Siku za ukimya Wake ziko karibu kupi-ta. {1TG32: 23.1}

Aya ya 31-33 — “Maana kwa sauti ya Bwana, Mwashuri atavunjika-vunjika, yeye apigaye kwa bakora. Na kila pigo la fimbo iliyoamriwa, ambayo Bwana ataliweka juu yake, litakuwa pamoja na matari na vi-nanda, na kwa mapigano yenye kutikisa atapigana nao. Maana Tofethi imewekwa tayari tokea zamani, naam, imewekwa tayari kwa mfalme huyo; ameifanya kubwa, inakwenda chini sana; tanuru yake ni mo-to na kuni nyingi; pumzi ya Bwana, kama mto wa kiberiti, huiwasha.”

Iwapo watu wa Mungu katika siku za zamani wangaliyaamini yale ambayo manabii waliwaambia, yangalifanya tofauti kama nini! Makosa yao lazima sasa yawe maarifa yetu, ngazi yetu ya kuokoka. {1TG32: 23.2}

“Kwa hiyo, ndugu watakatifu, wenye kuushiriki mwito wa mbinguni, mtafakarini sana Mtume na Kuhani Mkuu wa maungamo yetu, Yesu, aliyekuwa mwaminifu kwake yeye aliyemweka, kama Musa naye alivyokuwa, katika nyumba yote ya Mungu …. Basi, ikiwa ingaliko ahadi ya kuingia katika raha yake, na tuogope, mmoja wenu asije akaonekana ameikosa. Maana ni kweli, sisi nasi tumehubiriwa habari njema vile vile kama hao. Lakini neno lile lililosikiwa halikuwafaa hao, kwa sababu halikuchanganyika na imani ndani yao waliosikia. Aweka tena siku fu-lani, akisema katika Daudi baada ya muda mwingi namna hii, Leo; kama ilivyonenwa tangu zamani, Leo, kama mtaisikia sauti yake, Msifanye migumu mioyo yenu.” Ebr. 3: 1, 2; 4: 1, 2, 7. {1TG32: 23.3}

Babu zetu walipendelea hila. Sisi, hata hivyo, tunapaswa sasa kuitikia kwa furaha ombi la Rehema, na hivyo kuipata neema. {1TG32: 23.4}

23

Jumuiya ya Wadaudi Waadventista wa Sabato

(Ushirika Huru Unaojumuisha Kanisa)

Mlima Karmeli, Waco, Texas

S.L.P. 23738, Waco, TX 76702

+ 1-254-855-9539

www.gadsda.com

info@gadsda.com

Gombo la 1, Namba 31, 32

Kimechapishwa nchini Marekani

24

>