fbpx

Gombo la 1 Salamu Mwafaka Namba 25, 26

Gombo la 1 Salamu Mwafaka Namba 25, 26

                                    

AMANI YA PEKEE YA MAWAZO

Hati miliki, Kimechapishwa tena 1953

Haki zote zimehifadhiwa

V. T. HOUTEFF

                                    

NI MATAIFA GANI YATAACHA SILAHA, NA KWA NINI?

MVURUGO WA DUNIA YOTE, NA MATOKEO YAKE

                                    

1

WAZO LA SALA YA UFUNGUZI

Nitasoma kutoka katika “Mlima wa Baraka,” kuanzia ukurasa wa 182: {1TG25: 2.1}

M.B, uk. 182 — “Kristo hawa hawafukuzi lakini huwavuta watu Kwake. Shurutisho la pekee ambalo Yeye hu-tumia ni kizuizi cha upendo. Wakati kanisa linapoanza kutafuta msaada wa tawala za kidunia, ni thibitisho kwamba halina nguvu ya Kristo — kizuizi cha upendo wa Mungu. {1TG25: 2.2}

“Lakini ugumu upo kwa washiriki mmoja-mmoja wa kanisa, na hapa ndipo lazima tiba ifanyike. Yesu humwagi-za mshtaki kwanza kuiondoa boriti katika jicho lake mwenyewe, aikane roho yake ya udaku, kuungama na kuia-cha dhambi yake mwenyewe, kabla ya kujaribu kuwarekebisha wengine …. Unachohitaji ni badiliko la moyo. Lazima uwe na uzoefu huu kabla ya kufanywa wa kufaa kuwarekebisha wengine; kwa maana “kinywa hunena wingi wa yaliyo moyoni.” {1TG25: 2.3}

“Wakati tatizo linakuja katika maisha ya nafsi yoyote, na ujaribu kutoa ushauri au himizo, maneno yako yataku-wa tu na uzito wa mvuto kwa ajili ya wema ambao mfano wako na roho yako mwenyewe imekufaidisha. Lazi-ma uwe mzuri kabla ya kutenda mema. Huwezi kuudhihirisha mvuto ambao utawabadilisha wengine mpaka moyo wako uwe umenyenyekezwa na kutakaswa na kufanywa mpole kwa neema ya Kristo. Wakati mabadiliko haya yamefanyika ndani yako, itakuwa ni kawaida kwako kuishi kwa kuwabariki wengine kama ilivyo kwa mwaridi kutoa maua yake yenye manukato, au mzabibu vishada vyake vya rangi ya zambarau.” {1TG25: 2.4}

Tunahitaji kuomba kwa ajili ya badiliko la moyo; kuomba ili kugundua kwamba kuwa na roho ya udaku ni mba-ya zaidi kuliko kutafuta msaada wa utawala wa kidunia, na kwamba kuweka mfano mzuri unaweza kuwa uzito wa ushawishi wetu kwa ajili ya wema. {1TG25: 2.5}

2

NI MATAIFA GANI YATAACHA SILAHA, NA KWA NINI?

MATINI YA HOTUBA NA V. T. HOUTEFF

MCHUNGAJI WA WADAUDI WAADVENTISTA WA SABATO

SABATO, JANUARI 25, 1947

HEKALU LA MLIMA KARMELI

WACO, TEXAS

Ili kuendelea na mada ya masomo yetu ya awali — ufalme wa Yuda — tutafungua kitabu cha Mika. Kinaju-muisha kama unavyojua, sura saba, na hubeba kisa endelevu cha Yuda katika siku zake za mwanzo na za mwi-sho. Sura tatu za kwanza zinahusu Yuda katika siku zake za mwanzo, na nne za mwisho zinasheheni ahadi kwa Yuda wa uakisi, Yuda wa siku za mwisho, ambao maslahi yetu makuu sasa yanauhusu. {1TG25: 3.1}

Ili kuziunganisha sura tatu za kwanza za Mika na nne za mwisho, tutaanza na aya ya mwisho ya sura ya tatu. {1TG25: 3.2}

Mika 3:12 — “Basi, kwa ajili yenu, Sayuni utalimwa kama shamba lilimwavyo, na Yerusalemu utakuwa magofu; na mlima wa nyumba utakuwa kama mahali palipoinuka msituni.”

Kwa sababu hakukuwa na kitu kingine ambacho kingaliweza kufanywa ili kumshawishi Yuda kuwa alikuwa mkosaji na kwamba alikuwa na hitaji la kurudi kwa Bwana, Bwana hatimaye alionya kimbele kwamba uwanda wake wa kasri ungalilimwa kama shamba, na kwamba kasri na mji wake ungalikuwa marundo. Utimizo wa se-hemu hii ya unabii wa Mika ni shahidi mwaminifu mbele ya mataifa yote, na adhabu ya watu hao ni mfano mzuri

3

kwa ajili ya watu wote kujua kwamba Mungu humaanisha tu yale ambacho Yeye husema. Mungu, hata hivyo, hakuwatupilia kando wachache waaminifu Wake na uzao wao milele. Kwa ajili yao Aliacha ahadi hii ya faraja– {1TG25: 3.3}

Mika 4: 1 — “Lakini itakuwa katika siku za mwisho, ya kwamba mlima wa nyumba ya Bwana utawekwa imara juu ya milima, nao utainuliwa juu ya vilima; na watu wa mataifa watauendea makundi makundi.”

Ijapokuwa Mika alinena kimbele habari za kusikitisha kwa ajili ya Yuda wa kale, alinena kimbele habari hizi za furaha kwa Yuda wa siku za mwisho. Kutaabisha, kwa kweli, lazima ilikuwa kwa Yuda kutarajia uharibifu wake mwenyewe. Kinyume chake, hata hivyo, ni lazima kuwa kulimtia moyo kujua kwamba wakati ungalimjia kurejea na “kupajenga mahali palipokuwa ukiwa,” “kuiinua misingi ya vizazi vingi” (Isa. 58:12). Na bado kwa furaha zaidi aweze sasa kujifunza kwamba wakati wake wa kumwelekea Mungu na kurejea nchini kwao kweli umekuja! {1TG25: 4.1}

Ili kuondoa shaka yoyote katika uhusiano huu Bwana analithibitisha tena Neno Lake kwa kusema: “Maana kama vile mvua ishukavyo, na theluji, kutoka mbinguni, wala hairudi huko; bali huinywesha ardhi, na kuizalisha na kuichipuza, ikampa mtu apandaye mbegu, na mtu alaye chakula; ndivyo litakavyokuwa neno langu, litokalo katika kinywa changu; halitanirudia bure, bali litatimiza mapenzi yangu, nalo litafanikiwa katika mambo yale niliyolituma. Maana mtatoka kwa furaha, Mtaongozwa kwa amani; Mbele yenu milima na vilima vitatoa nyimbo; Na miti yote ya kondeni itapiga makofi. Badala ya michongoma utamea msunobari, Na badala ya mibigili, mhadesi; Jambo hili litakuwa la kumpatia Bwana

4

jina, Litakuwa ishara ya milele isiyokatiliwa mbali.” Isa. 55: 10-13. Sisi, pia, tunapaswa kupiga makofi hata sasa kwa kuwa na fursa hii kubwa ya kushiriki katika kazi hii ya utukufu, na kwa fursa kuu na kubwa ya kuzitangaza habari njema hizi na kuitwa “Wenye kurejeza njia za kukalia.” Isa. 58:12. Hakika hizi ni “habari njema” za “ama-ni” ambazo nabii Nahum alinena kimbele. Nah. 1:15. {1TG25: 4.2}

Wakati ambapo ufalme wa Yuda unasimamishwa tena, kisha inakuwa kwamba andiko linatimizwa: {1TG25: 5.1}

Aya ya 2 — “Na mataifa mengi watakwenda na kusema, Njoni, twende juu mlimani kwa Bwana, na nyumbani kwa Mungu wa Yakobo; naye atatufundisha njia zake, nasi tutakwenda katika mapito yake; kwa maana katika Sayuni itatoka sheria, na neno la Bwana litatoka Yerusalemu.”

“Imba, ufurahi, Ee binti Sayuni; maana, tazama, ninakuja, nami nitakaa kati yako, asema Bwana. Na mataifa mengi watajiunga na Bwana katika siku ile, nao watakuwa watu wangu; nami nitakaa kati yako, nawe utajua ya kuwa Bwana wa majeshi amenituma kwako. Na Bwana atairithi Yuda, iwe sehemu yake katika nchi takatifu, naye atachagua Yerusalemu tena. Nyamazeni, ninyi nyote wenye mwili, mbele za Bwana; kwa maana ameamka, na kutoka katika maskani yake takatifu.” Zekaria 2: 10-13. {1TG25: 5.2}

“Na mataifa wataijilia nuru yako, Na wafalme kuujia mwanga wa kuzuka kwako. Inua macho yako, utazame pande zote; Wote wanakusanyana; wanakujia wewe; Wana wako watakuja kutoka mbali. Na binti zako watabebwa nyongani. Ndipo utakapoona na kutiwa nuru, Na moyo wako utatetemeka na kukunjuka; Kwa kuwa wingi wa bahari utageuzwa kukujia, Utajiri wa mataifa utakuwasilia. Wingi wa

5

ngamia utakufunika, Ngamia vijana wa Midiani na Efa; Wote watakuja kutoka Sheba; Wataleta dhahabu na uvumba; Na kuzitangaza sifa za Bwana. Makundi yote ya Kedari yatakusanyika kwako, Kondoo waume wa Nebayothi watakutumikia; Watapanda juu ya madhabahu yangu kwa kibali, Nami nitaitukuza nyumba ya utu-kufu wangu. Ni nani hawa warukao kama wingu, Na kama njiwa waendao madirishani kwao? Hakika yake visiwa vitaningojea, Na merikebu za Tarshishi kwanza, Ili kuleta wana wako kutoka mbali, Na fedha yao na dhahabu yao pamoja nao, Kwa ajili ya jina la Bwana, Mungu wako, Kwa ajili yake Mtakatifu wa Israeli, Kwa kuwa amekutukuza wewe. Na wageni watajenga kuta zako, Na wafalme wao watakuhudumu; Maana katika ghadhabu yangu nalikupiga, Lakini katika upendeleo wangu nimekurehemu. Malango yako nayo yatakuwa wazi daima; Hayatafungwa mchana wala usiku; Ili watu wapate kukuletea utajiri wa mataifa, Na wafalme wao wakiongozwa pamoja nao. Kwa maana kila taifa na ufalme wa watu Wasiotaka kukutumikia wataangamia; Naam, mataifa hayo wataharibiwa kabisa.” Isa. 60: 3-12. {1TG25: 5.3}

Hakika tuko kwenye pambazuko la siku mpya, siku ambayo kazi ya injili itatia fora katika ushindi na kuvuna mavuno mengi ya waongofu. Karibu mataifa yote yatajiunga kwa “mlima wa Bwana” wakati wa siku ya Huku-mu, siku ambayo sheria “itatoka katika Sayuni, na Neno la Bwana kutoka Yerusalemu,” kutoka kwa makao ma-kuu ya baadaye ya injili. {1TG25: 6.1}

Wakati u, kwa hivyo, karibu sana ili kwa kweli kwenda kanisani, mtu lazima aende Yerusalemu, na huko kufun-dishwa njia ya Bwana, na kwa hivyo kutembea katika mapito Yake. {1TG25: 6.2}

Aya ya 3 — “Naye atafanya hukumu kati ya watu wa kabila nyingi, naye atawakemea mataifa wenye nguvu walio mbali; nao watafua panga zao ziwe majembe, na mikuki yao iwe

6

miundu; taifa halitainua upanga juu ya taifa lingine, wala hawatajifunza vita tena kamwe.”

Mataifa mengi yatapokea kwa furaha makaripio Yake, yatafua panga zao kuwa majembe na mikuki yao kuwa miundu badala ya kuendelea kukimbia katika mbio za silaha. {1TG25: 7.1}

Kwa mujibu wa Mika, mataifa pekee ambayo yataacha silaha ni yale yatakayoupokea Ukweli wa Bwana wa leo na kwenda katika Nchi ya Ahadi. Hawatahitaji tena kamwe upanga au mikuki. {1TG25: 7.2}

Aya ya 4 — “Bali wataketi kila mtu chini ya mzabibu wake, na chini ya mtini wake; wala hapana mtu ata-kayewatia hofu; kwa kuwa kinywa cha Bwana wa majeshi kimesema hivi.”

Mataifa na watu sasa wanapata wakati mgumu wa kuufikia “mtini” wao, kwa mfano, sembuse kukaa kwa amani chini yake. Wako katika hofu ya daima kwamba mtu fulani anaweza hata kuwaondoa wasikae chini ya mti usi-okuwepo. Kwa hivyo watajaribu kulinda haki zao, au zisizo haki, kwa kuyafua “majembe yao yawe upanga, na miundu [yao] iwe mikuki.” Yoeli 3:10. Na hivyo kuuhukumu uwezo wao wenyewe kwa maandalizi yao ya vita, hata yale dhaifu yatasema, “Mimi ni hodari.” Lakini haitakuwa hivyo kwa yale mataifa yatakayoungana na watu wa Ufalme wa Bwana: Hawatahitaji kuamini katika nguvu zao wenyewe, kwa maana watakuwa na ulinzi wa Bwana. Kila mmoja atakaa starehe na salama chini ya “mtini” wake mwenyewe, akijua kwamba hakuna yeyote anayeweza kumfukuza kutoka chini yake. Hili litakuwa hivyo, kwa maana “kinywa cha Bwana wa majeshi ki-menena hivyo.” {1TG25: 7.3}

7

Aya ya 5 — “Kwa maana mataifa yote watakwenda, kila moja kwa jina la mungu wake, na sisi tutakwen-da kwa jina la Bwana, Mungu wetu, milele na milele.”

Wale walio nje ya Ufalme ambao Roho wa Mungu hawezi kuwashawishi kuhusu makosa yao, wataendelea kutembea katika jina la miungu yao ya uwongo. Lakini watu ndani ya Ufalme “wataenenda kwa jina la Bwana Mungu wetu milele na milele.” {1TG25: 8.1}

Aya ya 6, 7 — “Katika siku ile, asema Bwana, nitamkusanya yeye achechemeaye, nami nitamrudisha yeye aliyefukuzwa, na yeye niliyemtesa. Nami nitamfanya yeye aliyechechemea kuwa mabaki, na yeye ali-yetupwa mbali kuwa taifa lenye nguvu, na Bwana atawamiliki katika mlima Sayuni tangu sasa na hata milele.”

Katika siku ambayo watu wa Mungu wanakusanywa kutoka sehemu zote za dunia na kuletwa Zayuni ime-karibia, na Bwana atatawala juu yao tangu wakati huo hata milele. {1TG25: 8.2}

Aya ya 8 — “Na wewe, Ee mnara wa kundi, kilima cha binti Sayuni, utajiliwa; naam, mamlaka ya kwanza yatakuja, ufalme wa binti Yerusalemu.”

“Mnara wa kundi, ngome ya binti Zayuni,” utakuwa kivutio kikuu ndani ya Yerusalemu. Na unaweza kuwa ni-ni? — Vyema katika nyakati za zamani minara ilijengwa kwa kusudi la kuweka ulinzi juu ya mji, na hivyo “mnara wa kundi” lazima uwe kiti cha enzi juu ya Zayuni, kilima kilichoinuka, ngome ya Zayuni. Ngome hii, una-kumbuka, sio ya mama (sio ya Zayuni wa zamani) ila ya binti yake (Zayuni wa uakisi). {1TG25: 8.3}

Aya ya 9, 10 — “Sasa mbona unapiga kelele? Je!

8

Hakuna mfalme kwako, mshauri wako amepotea, hata umeshikwa na utungu kama mwanamke wakati wa kuzaa? Uwe na utungu, utaabike ili uzae, Ee binti Sayuni, kama mwanamke mwenye utungu; maana sasa utatoka mjini, nawe utakaa katika mashamba; utafika hata Babeli; huko ndiko utakakookolewa; huko ndiko Bwana atakakokukomboa katika mikono ya adui zako.”

Aya hizi mbili zinaturudisha nyuma wakati ambapo waaminifu wa Yuda wa kale walilia walipojiona wakiwa karibu kutawanywa kati ya mataifa, lakini ushauri unaomtia moyo afanye kazi na kuzaa watoto akiwa bado katika mashamba, na ahadi ya kumfariji ya ukombozi wake kutoka Babeli ya uakisi, iliyoachwa na manabii, ime-salia daima pamoja naye hata hivi leo. Zayuni, kanisa, lilikusudiwa kuingia katika nchi za Mataifa, huko ili ku-zaana, na hatimaye kuokolewa. Habari hizi njema, sasa tu kabla ya kukusanywa kuanza, Bwana anataka tuzitangaze kwa urefu na upana, tukisema: “Lisikieni neno la Bwana, enyi mataifa, litangazeni visiwani mbali; mkaseme, Aliyemtawanya Israeli atamkusanya, na kumlinda, kama mchungaji alindavyo kundi lake. Kwa maana Bwana amemweka huru Yakobo, amemkomboa mkononi mwake aliyekuwa hodari kuliko yeye. Nao watakuja, na kuimba katika mlima Sayuni, wataukimbilia wema wa Bwana, nafaka, na divai, na mafuta, na wachanga wa kondoo na wa ng’ombe; na roho zao zitakuwa kama bustani iliyotiwa maji; wala hawatahuzunika tena kabisa.” Yer. 31: 10-12. {1TG25: 9.1}

Aya ya 11, 12 — “Na sasa mataifa mengi wamekusanyika juu yako, wasemao, Na atiwe unajisi; macho yetu na yaone shari ya Sayuni. Lakini wao hawayajui mawazo ya Bwana; wala

9

hawafahamu shauri lake; kwa maana amewakusanya kama miganda sakafuni.”

Aya ya 13 — “Haya, simama upure, Ee binti Sayuni; kwa maana nitafanya pembe yako kuwa chuma, na kwato zako kuwa shaba; nawe utaponda-ponda mataifa mengi, na faida yao utaiweka wakfu kwa Bwa-na, na mali zao kwa Bwana wa dunia yote.”

Sio binti wa Yerusalemu, bali binti Zayuni ndiye atakayepura. Na anayo ahadi ya pembe ya chuma — nguvu ya Mungu, aina ambayo haivunjiki. Aidha, ameahidiwa kwato za shaba, ujumbe maalum na tofauti ambao atatumia kuwavunja vipande vipande watu wengi; yaani, yeye anazo ili kupura na kuchagua ngano kutoka kwa makapi. “Kisha nalimwona malaika wa tatu. Akasema malaika aliyeambatana nami, Ya kutisha ni kazi yake. Wa kuo-gofya ni utume wake. Yeye ndiye malaika atakayeichagua ngano kutoka kwa magugu, na kutia muhuri, au kui-funga, ngano kwa ghala la mbinguni. Mambo haya yanapaswa kuyashughulisha mawazo yote, umakini wote.’” — “Maandishi ya Awali,” uk. 118. {1TG25: 10.1}

“Maana Bwana atakuja na moto, na magari yake ya vita kama upepo wa kisulisuli; ili atoe malipo ya ghadhabu yake kwa moto uwakao, na maonyo yake kwa miali ya moto. Kwa maana Bwana atateta na wote wenye mwili, kwa moto na kwa upanga wake; nao watakaouawa na Bwana watakuwa wengi.” Isa. 66:15, 16. Huu ni utengo wa kwanza. {1TG25: 10.2}

“Nami nitaweka ishara kati yao, nami nitawatuma hao waliookoka kwa mataifa, Tarshishi, na Puli, na Ludi, wavutao upinde, kwa Tubali na Yavani, visiwa vilivyo mbali; watu wasioisikia habari yangu, wala kuuona utu-kufu wangu; nao watahubiri utukufu wangu katika mataifa. Nao watawaleta ndugu zenu wote kutoka mataifa yote, kuwa sadaka kwa Bwana, juu ya farasi, na katika magari, na

10

katika machela, na juu ya nyumbu, na juu ya wanyama wepesi, mpaka mlima wangu mtakatifu Yerusalemu, asema Bwana; kama vile wana wa Israeli waletavyo sadaka yao nyumbani kwa Bwana katika chombo safi.” Isa. 66:19, 20. {1TG25: 10.3}

Wale ambao wanaokoka kutoka kwa mchinjo wa Bwana, unakumbuka, wanatumwa kwa nchi za Mataifa huko kuwahubiria sifa ya Bwana na utukufu Wake, na pia kuwaleta ndugu zao wote (wote ambao wanaweza kuo-kolewa) nyumbani mwa Bwana. Kutoka kwa hili unaweza kuona wazi kwamba wale wanaookoka lazima wawe malimbuko, Wayakobo 144,000 (Ufu. 14: 4). Wale wanaowaleta kutoka ndani ya nchi za Mataifa hadi kwa nyumba ya Bwana lazima, kwa hivyo, wawe mavuno ya pili (Ufu. 7: 9), hivyo pale ambapo ipo ya kwanza lazi-ma pia iwepo ya pili. Hatimaye unaona wazi kwamba kutoka kwa utakaso wa kanisa watu 144,000 wanaokoka na kuwa watumwa wa Mungu, masalia, wale ambao wanaikamilisha kazi ya Injili ulimwenguni kote. {1TG25: 11.1}

Sasa kwa muhtasari, hebu tuangalie tena hoja bora zaidi za somo hili: {1TG25: 11.2}

Ya kwanza ufalme wa Yuda ulipaswa kuvunjwa — Zayuni kulimwa kama shamba na Yerusalemu kuwa marun-do. {1TG25: 11.3}

Kisha katika siku za mwisho utasimamishwa tena, na kuinuliwa juu ya falme za Mataifa. {1TG25: 11.4}

Ya tatu, wakati “ukishasimamishwa” hivyo, mataifa mengi yataingia ndani yake, na hata kualikana kwenda huko ili kufundishwa njia ya Bwana na kutembea katika mapito Yake. Hii itakuwa hivyo kwa sababu “katika Sayuni itatoka sheria, na neno la Bwana litatoka Yerusalemu.” {1TG25: 11.5}

11

Ya nne, Bwana atahukumu kutoka Zayuni, na kutoka huko Yeye atakayakemea mataifa yenye nguvu mbali. Wale wanaopokea kemeo Lake watafua upanga wao kuwa jembe, na mikuki yao kuwa miundu. Mataifa ya-nayojiunga na Ufalme wa Bwana hayatainua kamwe tena upanga dhidi ya taifa, wala hawatajifunza vita tena. Wala hawatahitaji tena silaha, kwa maana watalindwa na “ukuta wa moto.” Zek. 2: 5. Kila mtu atakaa chini ya mtini wake, na hakuna yeyote atakayemfanya awe na hofu, “kwa maana Bwana wa majeshi amenena hivyo.” {1TG25: 12.1}

Ya tano, kila mmoja wa wale ambao hawatakwenda Yerusalemu, na ambao hawataacha silaha, atakwenda kwa jina la mungu wake wa uongo. Bali wote wanaojiunga na ufalme wa Yuda wataenda kwa jina la Bwana, Mungu wetu, milele na milele. {1TG25: 12.2}

Ya sita, Mungu atawakusanya na kuwakutanisha watu Wake, kanisa — yeye achechemeaye, na yeye aliyefuku-zwa, na yeye aliyeteswa. Yeye atamfanya kuwa taifa la nguvu “na Bwana atawamiliki katika mlima Sayuni tan-gu sasa na hata milele.” {1TG25: 12.3}

Ya saba, kwa Ufalme huu mamlaka ya kwanza yatakuja. {1TG25: 12.4}

Somo la alasiri hii linaonyesha jinsi ambavyo kukusanywa kutatimizwa na kazi ya injili kukamilika, na ulimwen-gu wa uovu kufikishwa kwa kikomo. Kweli, mpango kama huu kwa ajili ya kumaliza kazi haujakuwa mpango wetu, lakini wakati unakaribia tung’amue kwamba mipango yetu haijawahi kuwa na kamwe haitakuwa mipango ya Bwana. Ingalikuwa bora sasa tuipokee mipango Yake ikiwa tunatamani kwenda Zayuni na huko kusimama na Mwana-Kondoo. {1TG25: 12.5}

Siku mpya inapambazuka, Ndugu, Dada. Na

12

sasa, badala ya kudhani kwamba sisi ni matajiri na tumejitajirisha, wala hatuna haja ya kitu, tunajiona tukiwa na haja ya kila kitu. Je, hatutaupokea utajiri huu (Kweli) ambao umejaribiwa kwa moto, na mavazi haya ya haki yatuwezeshe kuufunika uchi wetu? Je, hatutaweza kujipaka mafuta ya macho yetu na mafuta haya safi ya dha-habu ya Kweli ili tuweze kuona na kuijua njia, ili tuweze kuufikia “mlango” kwa wakati? Hakuna sababu ya kukaa mnyonge, mwenye mashaka, maskini, kipofu, na uchi. Bwana anasubiri kwenye mlango wa mioyo yetu. Anayo hamu ya kumimina baraka, kukijaza kikombe kufurike. Hebu tusimkatishe Yeye tamaa kwa kumlazimisha Atupite. Hebu sasa tuache silaha na kwa ujasiri tujiandae kukaa kwa amani chini ya “mtini” tulio-pewa na Mungu. {1TG25: 12.6}

13

WAZO LA SALA YA UFUNGUZI

Nitasoma kutoka katika “Mlima wa Baraka,” kuanzia ukurasa wa 183, aya ya mwisho. {1TG26: 14.1}

M.B., uk. 183 — “Ikiwa Kristo yu ndani yako ‘tumaini la utukufu,’ hautakuwa na hulka ya kuwatazama wengine, kuyafunua makosa yao. Badala ya kutafuta kuwashtaki na kuwahukumu, litakuwa kusudi lako kuwasaidia, ku-wabariki, na kuwaokoa. Kwa kushughulika na wale ambao wamekosa, utalitii agizo hili, Jiangalie ‘mwenyewe usije ukajaribiwa pia.’ Utakumbuka mara nyingi ambapo umekosea, na jinsi ilikuwa vigumu kuipata njia sahihi wakati ulipokuwa umeiacha hapo awali. Hautamsukuma ndugu yako aingie kwenye giza kuu, bali kwa moyo wa huruma tele utamwambia juu ya hatari yake. {1TG26: 14.2}

“Yeye anayeutazama mara nyingi msalaba wa Kalvari, akikumbuka kwamba dhambi zake zilimtundika Mwokozi hapo, hatawahi kamwe kujaribu kukadiria kiwango cha hatia yake kwa kulinganisha na kile cha wengine. Hatapanda kwenye kiti cha hukumu kuleta mashtaka dhidi ya mwingine. Haiwezi kuwapo roho ya kukosoa au kujiinua nafsi kwa upande wa wale wanaotembea kwenye kivuli cha msalaba wa Kalvari.” {1TG26: 14.3}

Kutoka kwa hili tunaona kwamba hitaji letu ni kumwomba Kristo akae ndani yetu, ili kwamba badala ya kuta-zamia fursa za kuwashtaki au kuwalaumu wengine, na kuyafunua makosa yao, tutatafuta kila mara kuwasaidia, kuwabariki, kuwaokoa. Tunapaswa kuomba kwa ajili ya utambuzi wa kina wa dhambi zetu wenyewe; tuombe ili roho ya kukosoa na kujiinua nafsi ikomeshwe milele kutoka kwetu. Kisha hatutajihisi kuwa huru kuketi kwenye kiti cha hukumu na kumuhukumu mtu yeyote. {1TG26: 14.4}

14

MVURUGO WA DUNIA YOTE, NA MATOKEO YAKE

MATINI YA HOTUBA NA V. T. HOUTEFF

MCHUNGAJI WA WADAUDI WAADVENTISTA WA SABATO

SABATO, FEBRUARI 1, 1947

HEKALU LA MLIMA KARMELI

WACO, TEXAS

Alasiri hii tutaendelea na somo letu katika kitabu cha Mika. Hebu tufungue sura ya tano, na tuanze na aya ya kwanza. {1TG26: 15.1}

Mika 5: 1 — “Sasa utajikusanya vikosi vikosi, Ee binti wa vikosi; yeye amemhusuru; watampiga mwamuzi wa Israeli shavuni mwake kwa fimbo.”

Utagundua kwamba mbali na kujulisha viwakilishi kadhaa — yeye, sisi, wao, aya hii pia inaanzisha mada kadhaa tofauti: kwanza “binti wa vikosi,” kisha “mwamuzi wa Israeli” na “fimbo.” Masuala mengine yanaletwa zaidi katika sura hii. {1TG26: 15.2}

Sasa ili kufaidika na maono na somo ambalo Uvuvio unayo hamu kwamba tupate kutoka kwa andiko hili, ni muhimu kwamba tujifunze somo moja kwa wakati mmoja. Na ili kufanya hivyo, lazima tuzipange aya kwa ma-kundi kulingana na masomo. Kwa sababu mada ya aya ya kwanza ni sawa na aya ya 10-15, tutazinukuu kwa muunganisho: {1TG26: 15.3}

Aya ya 1, 10-15 — “Sasa utajikusanya vikosi vikosi, Ee binti wa vikosi: … Kisha itakuwa katika siku hiyo, asema Bwana, nitawakatilia mbali farasi zako watoke kati yako, nami nitayaharibu magari yako ya vita; nami nitaikatilia mbali miji ya nchi yako, na ngome zako

15

zote nitaziangusha; nami nitakatilia mbali uchawi, usiwe mkononi mwako; wala hutakuwa tena na waaguzi; nami nitakatilia mbali sanamu zako na nguzo zako, zitoke kati yako; wala hutaiabudu tena kazi ya mikono yako. Nami nitayang’oa maashera yenu, yasiwe kati yako; nami nitaiangamiza miji yako. Nami nitajilipiza kisasi katika hasira na ghadhabu juu ya mataifa wasiosikiliza.”

Aya hizi zinawasilisha kundi la watu — wema na wabaya waliochangamana — ambao Mungu atatakasa. Halafu andiko linafunga kwa ahadi ya Mungu ya kulipiza kisasi juu ya washenzi. Kundi la watu lililochangamana, “ngano” na “magugu,” ni dhahiri linajumuisha kanisa ambalo linakaribia “wakati wa mavuno” (Mat. 13:30), wa-kati ambamo waabudu sanamu wote watatoweka. “Ndivyo itakavyokuwa katika mwisho wa dunia; malaika wa-tatokea, watawatenga waovu mbali na wenye haki …. Ndipo wenye haki watakapong’aa kama jua katika ufalme wa Baba yao. Mwenye masikio, na asikie.” Mat. 13:49, 43. {1TG26: 16.1}

Sasa tunakuja katika sehemu ya mwisho ya Mika 5: 1. kirejelezi cha nomino “Yeye” kinapatikana katika aya ili-yotangulia — sura ya 4, aya ya 13. Hapo haraka tunaona kwamba ni Bwana mwenyewe. Kwa udhahiri, basi, kwa nomino “sisi” Mika anamaanisha yeye mwenyewe na watu wake — Yuda na Israeli, kanisa. {1TG26: 16.2}

Dhahiri ilivyo kwamba wakati Bwana na ujumbe Wake wa onyo na makaripio anawahusuru watu Wake maadui wanakusanyika pamoja katika makundi kuupinga. Ndivyo ambavyo imekuwa katika kuanzishwa kwa kila Ukw-eli mpya uliofunuliwa. {1TG26: 16.3}

Kanisa linaitwa “binti wa vikosi,” kwa sababu mama yake kanisa la Kiyahudi katika wakati huo

16

wa kuanzishwa kwa injili ya Kristo, walikusanyika pamoja katika vikosi, kumpinga Bwana. {1TG26: 16.4}

Zaidi ya hayo akiwa amepigwa usoni badala ya mgongoni, Mwamuzi wa Israeli (Kristo) lazima alikuwa akiwak-abili moja kwa moja — akizungumza nao, — sababu ambayo Wayahudi walimsulubisha Yeye. Aya zinazofuata aya ya kwanza zinathibitisha ukweli kwamba “Mwamuzi” ni Kristo. Wale wanaompiga Yeye, bila shaka, ni watesi Wake, adui Zake. Kuwahusu Uvuvio unasema: {1TG26: 17.1}

Aya ya 9 — “Mkono wako na uinuliwe juu ya adui zako, na adui zako wote wakauliwe mbali.”

Kwa mujibu wa mifano ya Kristo, wakati ambapo “watesi” Wake, maadui Zake wa Ukweli endelevu, wanauawa ni mwanzoni mwa kutakaswa kwa kanisa, wakati wa mavuno. Halafu, kwa mujibu wa unabii wa Ezekieli, Bwa-na anawaamuru watu wenye silaha za kuchinja mikononi, akisema, “Piteni kati ya mji nyuma yake, mkapige; jicho lenu lisiachilie, wala msione huruma; Waueni kabisa, mzee, na kijana, na msichana, na watoto wachanga, na wanawake; lakini msimkaribie mtu ye yote mwenye hiyo alama; tena anzeni katika patakatifu pangu. Basi, wakaanza kwa wazee waliokuwa mbele ya nyumba.” Ezek. 9: 5, 6. Roho ya Unabii inathibitisha hili tukio kwa kusema: {1TG26: 17.2}

“Hapa tunaona kwamba kanisa — hekalu la Bwana — lilikuwa la kwanza kuhisi pigo la ghadhabu ya Mungu. Wazee, wale ambao Mungu alikuwa amewapa nuru kubwa, na ambao walikuwa wamesimama kama walezi wa masilahi ya kiroho ya watu, walikuwa wameusaliti uaminifu wao. Walikuwa wamechukua msimamo kwamba hatuhitaji kutazamia miujiza na udhihirisho wa nguvu ya Mungu kama siku za zamani. Nyakati zimebadilika. Maneno haya huimarisha kutokuamini kwao, na wao husema,

17

Bwana hatatenda mema wala hatatenda mabaya. Yeye anayo rehema sana kuwazuru watu wake kwa hukumu. Hivyo amani na usalama ni kilio kutoka kwa watu ambao hawatapaza sauti zao tena kama tarumbeta kuonyesha watu wa Mungu makosa yao na nyumba ya Yakobo dhambi zao. Mbwa hawa bubu, ambao hawangaliweza kubweka, ndio ambao wanahisi ulipizi wa haki ya kisasi cha Mungu aliyekosewa. Wanaume, wanawake, na wa-toto wadogo, wote wanaangamia pamoja.” — “Shuhuda,” Gombo la 5, uk. 211. Na kupitia kwa mtume Petro, Uvuvio unatangaza: {1TG26: 17.3}

“Kwa maana wakati umefika wa hukumu kuanza katika nyumba ya Mungu; na ikianza kwetu sisi, mwisho wao wasioitii injili ya Mungu utakuwaje?” 1 Pet. 4:17. {1TG26: 18.1}

Aya ya 2 — “Bali wewe, Bethlehemu Efrata, uliye mdogo kuwa miongoni mwa elfu za Yuda; kutoka kwako wewe atanitokea mmoja atakayekuwa mtawala katika Israeli; ambaye matokeo yake yamekuwa tangu zamani za kale, tangu milele.”

Hakuna shaka kwamba aya hii inatabiri kuzaliwa kwa Kristo, “Mwamuzi wa Israeli,” “Ambaye matokeo yake yamekuwa kutoka milele. {1TG26: 18.2}

Aya ya 3 — “Kwa sababu hiyo atawatoa, hata wakati wa kuzaa kwake aliye na utungu; ndipo hayo mabaki ya nduguze watawarudia wana wa Israeli.”

Kumsulubisha Kristo na kukataa kwao kumwelekea Bwana, hakuna kitu ambacho kingaliweza kufanywa kwa ajili ya Wayahudi wakati huo isipokuwa kuwaachilia “hata wakati wa kuzaa kwake aliye na utungu.” {1TG26: 18.3}

Kiwakilishi “kwake” kinamwonyesha binti Zayuni

18

(Mika 4:10). Yeye atawazaa watoto wake akiwa bado shambani; katika nchi za Mataifa. Halafu wakati wa kukaa kwake kutakoma na yeye atakombolewa. “Katika siku ile, asema Bwana, nitamkusanya yeye achechemeaye, … Nami nitamfanya yeye aliyechechemea kuwa mabaki … na Bwana atawamiliki katika mlima Zayuni tangu sasa na hata milele.” Mika 4: 6, 7. {1TG26: 18.4}

Aya ya 4, 5 — “Naye atasimama, na kulisha kundi lake kwa nguvu za Bwana, kwa enzi ya jina la Bwana, Mungu wake; nao watakaa; maana sasa atakuwa mkuu hata miisho ya dunia. Na mtu huyu atakuwa amani yetu; wakati Mwashuri atakapoingia katika nchi yetu, na kuyakanyaga majumba yetu, hapo mta-ondokesha wachungaji saba juu yake, na wakuu wanane.”

Wakati ambapo watoto wa binti Zayuni wanarejea kwenye Mlima Zayuni, watakaa milele. Kamwe hawatatup-wa nje tena kati ya nchi za Mataifa. Kamwe hawataachiliwa tena. Bwana jinsi hii atajitambulisha Mwenyewe kuwa “mkuu hata miisho ya dunia.” Wakati ambapo yeye aliye na utungu atakuwa amezaa, wakati huo watakati-fu watainuka dhidi ya Mwashuri “wachungaji saba, na wakuu wanane”; yaani, wachungaji wote wa Mungu na watu Wake wakuu, pamoja na Kristo, wa nane. {1TG26: 19.1}

Aya ya 6 — “Nao wataiharibu nchi ya Ashuru kwa upanga, na nchi ya Nimrodi katika malango yake; naye atatuokoa na Mwashuri, atakapoingia katika nchi yetu, na kukanyaga ndani ya mipaka yetu.”

Ufalme wa Israeli ambao uliangamizwa na Ashuru, na pia ufalme wa Yuda ambao uliharibiwa na Babeli, hata kabila zote kumi na mbili za

19

Israeli wataokolewa. {1TG26: 19.2}

“Nami,” atangaza Bwana, “nitawafanya kuwa taifa moja katika nchi hiyo, juu ya milima ya Israeli; na mfalme mmoja atakuwa mfalme wao wote; wala hawatakuwa tena mataifa mawili, wala hawatagawanyikana kuwa fal-me mbili tena, hata milele. Wala hawatajitia uchafu tena kwa vinyago vyao, wala kwa vitu vyao vichukizavyo, wala kwa makosa yao mojawapo; lakini nitawaokoa, na kuwatoa katika makao yao yote, ambayo wamefanya dhambi ndani yake, nami nitawatakasa; basi watakuwa watu wangu, nami nitakuwa Mungu wao. Na mtumishi wangu, Daudi, atakuwa mfalme juu yao, nao wote watakuwa na mchungaji mmoja; nao wataenenda katika hukumu zangu, na kuzishika amri zangu, na kuzitenda.” Ezek. 37: 22-24. {1TG26: 20.1}

Aya ya 7 — “Na hayo mabaki ya Yakobo yatakuwa kati ya kabila nyingi mfano wa umande utokao kwa Bwana, mfano wa manyunyu katika manyasi; yasiyomngojea mtu, wala kuwakawilia wanadamu.”

Baada ya Hukumu katika nyumba ya Mungu kutukia, basi inakuwa kwamba “mabaki,” wale ambao wamesalia, wataikamilisha kazi ya injili. {1TG26: 20.2}

“Wale ambao wameamini katika akili, ubunifu, au talanta, wakati huo hawatasimama kuwa askari mbele ya safu. Hawakusonga mbele sambamba na nuru. Wale ambao wamejithibitisha kwamba sio waaminifu hawataka-bidhiwa kundi. Katika kazi ya mwisho takatifu watu wakuu wachache watashirikishwa. Wamejitosheleza nafsi, hawamtegemei Mungu, na hawezi kuwatumia. Bwana anao watumwa waaminifu, ambao katika wakati wa kupepetwa, wa kupimwa watafunuliwa waonekane.” — “Shuhuda,” Gombo la 5, uk. 80. {1TG26: 20.3}

20

Kisha inakuwa kwamba wao, masalia wa Yakobo, watakusanywa katika nchi yao, baada ya hapo wanatumwa kama wamishonari kwa Mataifa ambao hawajawahi kulisikia jina la Mungu na sifa Zake. Hivi ndivyo inakuwa kwamba watakaookoka wakiwa hai kutoka kwa Hukumu ya Bwana, masalia, watakuwa kama umande kutoka kwa Bwana, kama manyunyu katika manyasi. Hawatamngojea yoyote katika kazi yao ya umishonari. Watawale-ta ndugu zao wote kutoka katika mataifa yote “kuwa sadaka kwa Bwana.” Isa. 66:15, 16, 20. {1TG26: 21.1}

Aya ya 8 — “Na hayo mabaki ya Yakobo yatakuwa kati ya mataifa, kati ya kabila nyingi, mfano wa simba kati ya wanyama wa msituni, kama mwana-simba kati ya makundi ya kondoo, ambaye, akiwa anapita katikati, hukanyaga-kanyaga na kurarua-rarua, wala hakuna wa kuokoa.”

Wakati watu wa Mungu ni kama umande na kama manyunyu kwa wenye haki (Mika 5: 7), kwa waovu ni kama simba kati ya wanyama na makundi ya kondoo. Kwa maneno mengine, injili yao itawaokoa watakaotubu, lakini iwaangamize wakaidi. {1TG26: 21.2}

Aya ya 9-14 — “Mkono wako na uinuliwe juu ya adui zako, na adui zako wote wakauliwe mbali. Kisha itakuwa katika siku hiyo, asema Bwana, nitawakatilia mbali farasi zako watoke kati yako, nami nitayaha-ribu magari yako ya vita; nami nitaikatilia mbali miji ya nchi yako, na ngome zako zote nitaziangusha; nami nitakatilia mbali uchawi, usiwe mkononi mwako; wala hutakuwa tena na watu waaguzi; nami nita-katilia mbali sanamu zako na nguzo zako, zitoke kati yako; wala hutaiabudu tena kazi ya mikono yako. Nami nitayang’oa maashera yenu, yasiwe kati yako; nami nitaiangamiza miji yako.”

Aya hizi zinaweza kumaanisha kitu kimoja tu, nacho ni, kwamba Mungu ataisafisha sakafu Yake kabisa. Yeye atachukua pepeto mikononi mwake na kuyapeperusha makapi, Yeye

21

atawaangamiza wadhambi ambao wako kati ya watu Wake. Kwa kulitakasa hivyo kanisa Lake, Atawaumba wa-tu wasafi, ukasisi ulio na umoja na uliojazwa bidii. “Sauti ya walinzi wako! Wanapaza sauti zao;” Anatangaza, “wanaimba pamoja; Maana wataona jicho kwa jicho, Jinsi Bwana arejeavyo Sayuni.” Isa. 52: 8. {1TG26: 21.3}

Aya ya 15 — “Nami nitajilipiza kisasi katika hasira na ghadhabu juu ya mataifa wasiosikiliza.”

“Kwa maana wakati umefika wa hukumu kuanza katika nyumba ya Mungu; na ikianza kwetu sisi, mwisho wao wasioitii injili ya Mungu utakuwaje? Na mwenye haki akiokoka kwa shida, yule asiyemcha Mungu na mwenye dhambi ataonekana wapi?” 1 Petro 4:17, 18. {1TG26: 22.1}

Ili tusikose sehemu yoyote katika somo hili, wacha tujikumbushe mambo makuu. {1TG26: 22.2}

La kuanzia, kundi la watu — wema na wabaya waliochangamana – wanaletwa kwenye mtazamo. Wao jinsi am-bavyo tumeona, wanajumuisha kanisa ambalo linakaribia wakati wa mavuno ambamo waovu watatengwa kuto-ka kati ya wenye haki. (Mat. 13:49). {1TG26: 22.3}

Wakati ambapo Bwana anao ujumbe wa maonyo na makaripio anawahusuru watu Wake, maadui wanakusanyika pamoja katika vikundi (“vikosi”) kumpinga. Kisha watakatiliwa mbali. Farasi (viongozi) watakatwa kabisa (wa-taachishwa kazi) na magari (sehemu za kutaniko) yataharibiwa. Watu wa Mungu watatakaswa kabisa kwa kuondolewa dhambi na wadhambi na waliotubu tu ndio watakaosazwa. Hao ni mabaki ya Yakobo ambao “ha-watatenda uovu, wala kusema uongo; wala ulimi wa hadaa hautaonekana kinywani mwao;

22

kwa maana watakula na kulala, wala hapana mtu atakayewaogofya.” Zef. 3:13. Watakusanywa katika nchi yao, kutoka huko watakwenda kama wamishonari kwa Mataifa. Kwa wenye kutubu watakuwa kama umande na kama manyunyu, lakini kwa wakaidi, watakuwa kama simba kati ya wanyama na makundi. {1TG26: 22.4}

Kwa hivyo mvurugo unaosababishwa na uhusuru wa Ukweli kwa kanisa na maadui Wake kufanya vita dhidi Yake, ambao tayari umeanza kunasa umakini wa dunia, utasababisha kutakaswa kwa kanisa, “Hekalu.” Mal. 3: 1-3. {1TG26: 23.1}

Hivi ndivyo Bwana atakavyomaliza kazi Yake duniani, kuwakusanya watu Wake, kuwaangamiza wadhambi na washenzi kwa usawa. Lazima, “… siku za utakaso wa kanisa zinaharakisha kwa kasi. Mungu atakuwa na watu wasafi na wakweli.” — “Shuhuda,” Gombo la 5, uk. 80. {1TG26: 23.2}

23

Kina cha Rehema

Kina cha rehema! inaweza kuwapo

Rehema bado niliyohifadhiwa?

Je! Mungu wangu hasira Yake yaweza kunivumilia,

Mimi, mkuu wa watenda dhambi kukolewa?

Nimeipinga neema yake kwa muda mrefu,

Muda mrefu Nimemkasirisha usoni Mwake,

Sikuweza kusikiliza wito Wake,

Nalimuhuzunisha na anguko maelfu.

Huko kwa ajili yangu Mwokozi husimama,

Huonyesha vidonda Vyake na kueneza mikono Yake,

Mungu ni upendo! Najua, nahisi;

Yesu hulia na bado ananipenda.

24

Usiyakose Manufaa Juu ya Hili

Iwapo haujatuma kwa ajili ya nakala yako iliyotangazwa na iliyojadiliwa sana kijitabu cha afya cha kurasa 96 (Kabari Inayoingia) ambacho kimefanya uamsho mkubwa katika dunia ya Waadventista na ambacho kimeliweka Shirika la K.I. katika mwangaza, usikikose iwapo afya, nyumba, na furaha yako inamaanisha kitu kwako. Kwa maoni yetu kitabu hiki ndicho bora hatujawahi kuona juu ya su-ala hili. Kwa kweli tunahisi kwamba kimetumwa na Mungu, na kwamba nakala yake inapaswa kuwa katika kila nyumba. Tumejulishwa kwamba sasa unaweza kukipata bila kuagizia. Tuma jina lako, anwani, na jina la kanisa ambalo wewe ni mshiriki (unaombwa kuchap-isha), na senti 15 kwa sarafu au stempu kwa Shirika La Kabari Inayoingia La Marekani, Kituo cha Mlima Kar-meli, Waco, Texas, Marekani na kitatumwa kwako. {1TG26: 25.1}

25

Jumuiya ya Wadaudi Waadventista wa Sabato

(Ushirika Huru Unaojumuisha Kanisa)

Mlima Karmeli, Waco, Texas

S.L.P. 23738, Waco, TX 76702

+ 1-254-855-9539

www.gadsda.com

info@gadsda.com

Gombo la 1, Namba 25, 26

Kimechapishwa nchini Marekani

26

>