fbpx

Gombo la 1 Salamu Mwafaka Namba 07, 08

Gombo la 1 Salamu Mwafaka Namba 7, 8

                                    

AMANI YA PEKEE YA MAWAZO

Hati miliki, Kimechapishwa tena 1953

Haki zote zimehifadhiwa

V. T. HOUTEFF

                                    

NI NINI HUMFANYA MMOJA KUWA MTEULE?

MLAODEKIA AU MDAUDI — YUPI?

                                    

1

WAZO LA SALA YA UFUNGUZI

Nitaisoma kutoka Mlima wa Baraka, uk. 155, kuanzia aya ya pili. — {1TG7: 2.1}

“M.B. uk. 155, — 156 Hatua hasa ya kwanza ya kumwendea Mungu ni kujua na kuamini upendo ambao Yeye anao kwetu; maana ni kwa mvuto wa upendo Wake kwamba tunaongozwa kuja Kwake. {1TG7: 2.2}

“Ufahamu wa upendo wa Mungu hutenda kazi ya kuukataa ubinafsi. Kwa kumwita Mungu Baba yetu, tunawa-tambua watoto Wake wote kama ndugu zetu. Sisi sote ni sehemu ya utando mkubwa wa binadamu, wote washiriki wa familia moja. Katika sala zetu tunapaswa kuwajumuisha majirani zetu vile vile sisi wenyewe. Hakuna yeyote anayeomba kwa usahihi ambaye hutafuta baraka kwa ajili yake pekee. {1TG7: 2.3}

“’Uliye mbinguni.’ Yeye ambaye Kristo hutuhimiza tumwangalie kama Baba yetu,’ ‘yuko katika mbingu za mbingu; Yeye amefanya chochote alichopenda.’ Katika utunzi Wake tunaweza kupumzika kwa usalama, tukisema, Wakati ule ninaogopa, nitakutumini Wewe.’” {1TG7: 2.4}

Andiko linatuagiza tuombe kwa ajili ya nini? – Kwa ajili ya kuutambua upendo wa Mungu na kumfahamu Yeye vyema zaidi; kwa ajili ya ufahamu sahihi kuhusu maana ya kuomba sala ya Bwana; kwa ajili ya hekima tupate kujua kwa nini tunamtaja Mungu kama Baba yetu, kwa nini sisi ni washiriki wa familia moja, ndugu wa nyumba moja; kwa ajili ya neema ili kukumbuka kuomba sio kwa ajili yetu wenyewe tu bali kwa ajili ya jirani zetu, na hata kwa ajili ya adui zetu. {1TG7: 2.5}

2

NI NINI HUMFANYA MMOJA KUSTAHIKI?

ANDIKO LA HOTUBA NA V. T. HOUTEFF

MCHUNGAJI WA WADAUDI WAADVENTISTA WA SABATO

SABATO, SEPTEMBA 21, 1946

HEKALU LA MLIMA KARMELI

WACO, TEXAS

Ndugu kadhaa wameniandikia mara kwa mara, wakitaka kujua nini kinachoweza kuwafanya wawe wateule kuupokea Muhuri wa Mungu. Wengine wanataka kujua kama watatiwa muhuri kwa kutenda hili au kutenda lile. Wengine wanataka kujua kama wataachwa bila muhuri kwa kutofanya jambo hili au kutofanya jambo lingine. {1TG7: 3.1}

Maswali hakika ni ya wakati mwafaka na ya kupongezwa. Maswali muhimu kama haya yanastahili majibu thab-iti jinsi yalivyo maswali yenyewe. Na ni nani anayeweza kutoa jibu thabiti kuliko wale ambao wametangulia mbele yetu, wale ambao majukumu yao yalikuwa sawa na yetu, wale waliokuwa wakipita ndani ya uzoefu unaofanana, wale waliosafiri kwa barabara ile ile ambayo tunasafiria, wale waliokuwa wakijiandaa kwa ajili ya Ufalme kama sisi. {1TG7: 3.2}

Je, tunapata kwa nani usambamba kama huu? – Sio kwa wengine zaidi ya wale waliotoka Misri na kuanza safari ya nchi ya ahadi. Hapana, La, sio kwa wengine wowote. Wao ndio mfano wetu tu. Unasema Uvuvio: “Basi mambo hayo yaliwapata wao kwa jinsi ya mifano, yakaandikwa ili kutuonya sisi, tuliofikiliwa na miisho ya za-mani.” (1 Kor. 10:11). Majukumu yao, kwa hivyo, ni majukumu yetu, na kushindwa kwao kunapaswa kuwa ngazi yetu kwa ushindi. Hivyo ni kwamba matendo ya wale ambao waliingia katika nchi ya ahadi lazima yawe matendo

3

yetu, na iwapo tutatiwa muhuri, basi matendo ya wale ambao walishindwa kuingia humo, tunapaswa kuyaepuka kabisa na kwa haraka kama tungalivyoweza kuliepuka tundu la simba. {1TG7: 3.3}

Sasa tunataka kuangalia ni kwa nini baadhi yao waliingia katika nchi ya ahadi, na kwa nini wengine hawakuin-gia, kwa maana hili ndilo Uvuvio unatuamuru kulifanya. Andiko hili linamaanisha kwamba iwapo uzoefu wa Israeli ya zamani haukuwa kwa mifano, haungaliandikwa kamwe. Ni muhimu jinsi gani, basi, kwamba tujifunze kwayo kwa bidii. Naam, kusudi kwa ajili yetu tujue ni nini tunachopaswa kufanya ili kuupokea muhuri na kuin-gia katika Nchi ya Ahadi, sharti tulichunguze tendo la wote walioingia na la wale walioachwa nje. {1TG7: 4.1}

Hebu tuanze uchunguzi wetu kwa kuanza na Musa, na wakala wa kibinadamu, kiongozi anayeonekana wa lile vuguvugu. Alilelewa katika nyua za Farao, alipata elimu ya juu ya ulimwengu wakati huo. Na akishaelewa kwamba yeye ndiye wa kuwaweka huru ndugu zake kutoka utumwa wa Misri, alijihisi kwamba alikuwa na uwezo wa kuifanya kazi. {1TG7: 4.2}

Unakumbuka kisa cha jinsi alivyoanza kuwaokoa ingawa bado hakuwa ameambiwa kufanya hivyo. Alimuua Mmisri, akatumbukia kwa ugomvi na mmoja wa Waebrania, na kisha akakimbia kwa ajili ya maisha yake. Hivyo ilikuwa kwamba huko Midiani alipata kazi, akawa mchungaji, na kumwoa binti ya mwajiri wake. Katika hiyo miaka arobaini ya maisha ya uchungaji alisahau lugha ya Misri, na pamoja nayo elimu ya Misri. Katika nafasi yake, hata hivyo, alijifunza kuwatunza vizuri kondoo. Kwa hiyo, alitupilia mbali kutoka mawazoni mwake wazo la kuwaokoa watu wa Mungu kutoka kwa utumwa wao wa Misri. Kisha ikawa kwamba Mungu alimwona akiwa mwenye nguvu na hodari, na akamwamuru kurudi Misri na kuwatoa

4

watu Wake wanaougua. Unakumbuka kwamba Musa aliteta dhidi ya wazo hilo na akahoji kwamba alishindwa kwa jaribio lake la kwanza, wakati alipokuwa kijana na mwenye ujuzi sana na kwamba kwa wakati huo wa mwi-sho wa maisha yake alikuwa hawezi kujaribu tena, kwamba hangemudu tena hata kunena lugha ya huko. Baada ya mazungumzo ya muda mrefu Mungu aliondoa vikwazo vyake kwa kuahidi kumpa ndugu yake, Haruni, kuwa msemaji wake, na hatimaye Musa alikubali kurudi Misri. {1TG7: 4.3}

Huko na fimbo yake ya mchungaji alitenda ishara nyingi na maajabu mbele ya Wamisri na Waebrania. Na una-kumbuka kilichotukia usiku wa Pasaka, usiku kabla wao waondoke Misri: Musa alikuwa ametangaza kote kote nchini kwamba katika kila makao ambapo hakuna damu iliopatikana kwenye mwimo wa mlango, usiku huo mzaliwa wa kwanza katika kila nyumba kama hiyo angekufa. {1TG7: 5.1}

Wale ambao hawakulitii agizo la Mwenyezi Mungu, walikuwa, siku iliyofuata wakiomboleza na kuzika wafu wao, ilhali wale waliotii agizo walikuwa kwa furaha na kwa utaratibu wakiondoka mijini. Ndiyo, wale tu ambao waliweza kutii amri walifunguliwa kutoka utumwani. Kwa hiyo, ni, lazima tujifunze kutii amri ikiwa tunataka kupokea muhuri wa Mungu kwenye vipaji vya nyuso zetu. {1TG7: 5.2}

Hebu tusisahau, hata hivyo, kwamba wana wa Israeli waliondoka Misri kwa bidii kubwa na matazamio ma-kubwa. Lakini walipoiona Bahari ya Shamu mbele yao, na jeshi la Farao nyuma yao, wakajazwa hofu kuu. Wali-jiona katika mtego wa kifo ingawa walikuwa kwenye ukingo wa ukombozi mwingine wa ajabu. Kisha waka-mgeukia Musa na kumshutumu kwa kuwaleta baharini, kuwafanya kuokoka kutoka kwa adui zao kusiwezekane kabisa. {1TG7: 5.3}

5

Wakiitazama hali hiyo kibinadamu, walikuwa katika tatizo hatari. Wakati huo walisahau ukombozi wao wa muujiza kutoka kwa wasimamizi wa kazi wa Farao na macho yao yakiwa yamefumbwa kwa wingu la ajabu mchana na nguzo ya moto usiku ambayo iliwaongoza kotekote. Walivyoitazama hali, ushahidi dhidi ya uwezo wa Musa wa kuwaongoza kwa usalama ulikuwa mkubwa sana. Kadiri walivyoendelea kuwa na wasiwasi, mradi huo ulionekana kuwa wa kutofaulu. Matumaini yao ya kwenda mbele au ya kurudi hata nyuma yaliwaacha, na wote kwa sababu walidhani Musa, sio Mungu, alikuwa mkombozi wao! Ni jinsi gani wasioweza kuona mbali, wasio thabiti, wenye mashaka, na wasahaulifu wanadamu walivyo! Uzoefu katika kazi ya injili umenifundisha kwamba watu wa Mungu wa leo wanaye mjaribu yule yule wa kushindana naye, na majaribu yale yale ya kushinda iwapo wataweza kuupokea muhuri wa Mungu. {1TG7: 6.1}

Ingalikuwapo tofauti kubwa namna gani kama Waisraeli wangaliamini tu kwamba Mungu, sio Musa, alikuwa Nahodha wao, kwamba kile kilichoonekana kama mtego wao wa kifo, kilikuwa mlango wao wa matumaini. He-bu uzoefu wao utufundishe kukumbuka kwamba Mungu ama anatuongoza kabisa au sivyo kabisa, kwamba njia Zake sio; njia zetu, na kwamba kile ambacho kinaweza kuonekana kuwa kizuizi kikubwa zaidi, chaweza kweli kubadilika kuwa baraka yetu kubwa zaidi. {1TG7: 6.2}

Hatari halisi ya Israeli, sasa tunaona, haikuwa katika yale Musa alifanya, ila katika kutoamini kwao kwamba Mungu alikuwa amechukua mamlaka mikononi Mwake, kwa kutojua kwamba njia Zake hazichunguziki — kin-yume na zetu. Walikosa kuona kwamba Mungu angeweza tena na tena kufanya muujiza baada ya muujiza ili awaokoe kutoka kwa mkono wa adui zao, kwambaYeye angeikausha bahari kwa urahisi kama angalivyoweza kuigharikisha dunia. {1TG7: 6.3}

Tukiwa na kushindwa kwao mbele yetu, tunapaswa kuufanya

6

kuwa ngazi yetu ya mafanikio. Basi hebu tuamini kwa moyo wote kwamba Mungu ndiye ameshika hatamu ya wokovu wetu, ya maisha yetu na ya kifo chetu, pia. Kwamba Yeye anaweza kutupeleka kwenye usalama hata kama dunia inaweza kudondoka kutoka angani, kwamba hatuwezi kufa ikiwa Yeye anatutaka tuishi, na kwam-ba hatuwezi kuishi iwapo Yeye anatutaka tufe. Hebu tuweze daima kukumbuka kwamba sisi wenyewe hatujui chochote kuhusu mipango ya Mungu isipokuwa kama tunavyoelezwa kupitia kwa watumishi Wake aliowateua rasmi, manabii, na kadiri tunavyowashuhudia siku baada ya siku. Iwapo tunatembea kila siku pamoja na Mungu, ikiwa tunamkabidhi Yeye yote, basi wajibu wote ni Wake. {1TG7: 6.4}

Mungu, kwa hekima Yake, aliwaleta Israeli kwenye Bahari ya Shamu kwa manufaa yao wenyewe, na ingawa hawakuweza kuyaona kama Yeye, hata hivyo kwa ajili ya Jina Lake aliigawanya bahari, akawavusha salama, na kwa wakati huo huo, kwa Muujiza huo huo, Yeye aliwaangamiza adui zao! {1TG7: 7.1}

Iwapo Musa angalikuwa na shaka juu ya uwezo na uongozi wa Mungu kama lile la watu waliokuwa pamoja naye, fimbo yake ingekuwa na matokeo gani alipoipiga bahari kwayo? — Hakuna chochote. Ikiwa Hukumu ya Aishiye milele ingekuwa sawa na hukumu ya wale ambao hufa, basi jeshi la Farao ama lingewaua au kuwafanya Israeli kuwa watumwa tena. {1TG7: 7.2}

Ukombozi wao wenye nguvu unapaswa, kwa hivyo, kuweka daima uaminifu wetu kwa Mungu, na unapaswa kusimama kama kumbukumbu za milele kwamba hekima ya wanadamu ni upumbavu kwa Mungu, na kwamba imani ndani Yake kweli husongesha milima na bahari, pia. {1TG7: 7.3}

Licha ya mifano hii, hata hivyo, watu bado humtarajia Mungu kufanya kazi kwa mujibu wa hukumu zao, na ndiyo sababu wakati mwingine Yeye huwatumia watoto katika

7

kazi Yake badala ya watu wa busara na hodari. {1TG7: 7.4}

Jeshi la Waebrania lilijua vizuri kwamba waliongozwa baharini kwa kufuata wingu mchana na nguzo ya moto usiku. Bado hata wakati huo hakuna hata moja ya maajabu hayo yalionekana kuwa yamefanya chapa yoyote ya kudumu juu yao. Ipo hatari kwamba sisi pia tunaweza kusahau jinsi Bwana ametuongoza. {1TG7: 8.1}

Baada ya Israeli kuivuka bahari, na baada ya bahari kuwafunika maadui zao, wote waliimba na kumpa Mungu utukufu, ila ingawa jeshi la Farao na bahari havikuwa vitu vya hofu lakini vya kuvutia, majaribio yao, mashaka, na hofu haikuwa imekwisha: Karibu mara baada ya kuona bahari nyuma na jangwa mbele walianza kumshitaki Musa kwa kuwa amewaleta jangwani wafe njaa huko kwa kukosa maji na chakula. Haikuwahi kuingia mawa-zoni mwao ya kwamba iwapo Mungu anaweza kuikausha bahari, Yeye hakika kwa mafuriko anaweza kulighari-kisha jangwa na kulifanya lichanue kama waridi. Licha ya mashaka yao na maombolezo yao Mungu alifanya tena muujiza mkubwa zaidi: Yeye alisababisha maji yatoke mwambani na Akaleta mana kutoka Mbinguni! {1TG7: 8.2}

Leo kama katika siku za Musa wengi wanazirudufisha dhambi za watu hao: Baadhi wote wanakuwa moto kwa siku, na wote kwa barafu siku ijayo. Wengine humtukuza Mungu kwa sauti zao za juu wakati meli yao inaelea kwa ulaini, lakini wakati bahari inachafuka na mawimbi kuanza kupiga dhidi yao, basi wanamwona tu mtu kwenye usukani na badala ya kumtarajia Mungu kuituliza bahari wanaanza msako wa kuruka kutoka hapo. Wengine bado wanajaribu daima kujikweza wenyewe kwa kuendelea kutafuta makosa dhidi ya wale ambao hu-beba uzito wote wa mzigo. Kwa hiyo ni kwamba lazima wapo kati yetu leo – wanamashaka, wanaolalamika

8

watafuta-ofisi na watafuta makosa wa uakisi, wakiukubali ukweli mmoja siku moja na kuusahau siku ijayo – na bado wanatarajia kutiwa muhuri wa Mungu na kusimama na Mwana-Kondoo juu ya Mlima Zayuni! {1TG7: 8.3}

Bwana aliwalisha watu Wake wa kale chakula cha Malaika, aina ambayo kazi yao na hali ya hewa ilihitaji. Al-ikiwasilisha kikiwa kipya kila siku, na hakikuwagharimu senti yoyote. Yote waliotakiwa kufanya ni kuiingiza ndani ya hema zao na kula. Lakini hawakupenda mana, na walitamani kwamba wangerudi Misri kula kutoka kwenye vyungu vyake vya nyama, “vitunguu vya majani, na vitunguu, na vitungu saumu.” Katika macho yao, Musa alikuwa mkuu wa wadhambi, na walimlaumu kwa kila jaribio la imani yao. Laiti Mungu angaliwapa kitu kingine chochote isipokuwa mana, wasingaliridhika kwacho kwa sababu roho mwovu alikuwa ndani yao. Hebu tufurahi na kwa shukrani tule na kunywa kile ambacho Bwana hutupatia na wakati ambao Yeye anatupatia. {1TG7: 9.1}

Mnakumbuka kwamba kwa kutamani chakula cha nyama walifanya hali isiyovumilika kwa Musa. Hivyo, kwa mshangao wao mkubwa kware walifurika kambini, na umati wa watu ukawaingiza katika hema zao. Lakini kwa gharama gani! Maelfu yao walikufa hata wakati nyama ilikuwa bado kati ya meno yao. Kisha wakaelewa kwamba mana ilikuwa chakula bora. Lilikuwa somo kuu, lakini ghali mno. Vipi kuhusu sisi Walaji wa mboga? {1TG7: 9.2}

Manung’uniko yao, hata hivyo, hayakukoma hata wakati huo. Walipata kitu kingine cha kunung’unikia. Waliku-za wivu dhidi ya Musa na Haruni. “Wanajishughulisha sana,” watafuta-ofisi walilalamika. “Sisi pia tunacho kibali cha Mungu kama vile Musa na Haruni. Mungu hunena nasi kama vile ambavyo Yeye hunena nao,” wakasema. Na ni nani waliokuwa walalamishi wakuu? — Wakuu wa mataifa,

9

watu ambao walikuwa wenye uwezo zaidi, ndio hasa waliopaswa kuwa wamejua zaidi. Wale ambao wangeku-wa msaada mkubwa zaidi kwa Musa walikuwa kikwazo kikubwa kwake. Walitaka ofisi ya Haruni; walitaka ofisi ya Musa. Walikataa kuridhika na chochote kidogo. Bwana Mwenyewe hakwenda popote pamoja nao. Kitu cha pekee Yeye angeweza kufanya ni kuisababisha nchi kuwameza. Hivyo kwa siku moja maelfu — kivitendo wote wanaoitwa eti wenye hekima — wakaanguka ndani ya kina cha nchi. Je, sisi pia, tunatafuta ofisi ili tuitumie kuikweza nafsi na je, sisi pia, tunajaribu kukinyakua kiti cha Roho wa Kweli? {1TG7: 9.3}

Hatimaye, wana wa Israeli waliowekwa huru walifika kwenye mipaka ya nchi ya ahadi. Na ingawa walikuwa wameshuhudia miujiza mikubwa, bado hawakuamini kwamba Mungu angaliweza kuwapatia nchi! Walikuwa wameona kwamba Yeye alikuwa na uwezo wa kuwaokoa kutoka kwa yadi za matofali za Farao, kuwapeleka nchi kavu kupitia baharini, kuwaangamiza adui zao, kuwapa chakula na maji jangwani ambako hakuwa na mtu yeyote, bado hawakuamini kwamba Yeye alikuwa na uwezo wa kuichukua nchi kwa ajili yao na kwamba An-geweza kukikamilisha kile alichoanzisha! {1TG7: 10.1}

Wapo maelfu leo ambao wanafanya sawa wakati wanaposema, “Isaya, sura ya 2, Mika, sura ya 4, Yeremia, sura ya 31 na Ezekieli, sura ya 36 na 37 hazitatimizwa kamwe.” Ni wale ambao walikuwa wa umri, wale ambao walipaswa kuwa wamejua vyema, walioanzisha kuufingirisha mpira kuelekea chini ya kilima kwa uharibifu. Vi-jana, bila shaka, lazima waliunga mkono manung’uniko ya wazee wao, lakini Bwana hakuhesabu hatia dhidi yao. Na ili kuwaokoa vijana, Mungu ilibidi awazike wazazi wao wote wa kulalamika isipokuwa wawili waamini-fu, wanaume wasadikifu walioipinga ripoti ovu ya wapelelezi wengine kumi. Maki wewe, kila mtu mzima am-baye

10

aliondoka Misri, isipokuwa Kalebu na Yoshua, ilibidi wazikwe kabla ya vijana wangaliweza kuvuka Yordani! Kwa nini? — Kwa sababu ingawa Mungu aliwaondoa kwa urahisi kutoka Misri, Yeye hakuweza kuiondoa Misri ndani mwao. Je, bado unashangaa kwa nini nabii Eliya lazima “aigeuze mioyo ya baba iwaelekee watoto wao, na mioyo ya watoto iwaelekee baba zao,”? (Mal 4: 6.) {1TG7: 10.2}

Wakristo mara kwa mara hufikiri kwamba Waisraeli walikuwa waovu sana na watu watukutu, lakini baada ya kuwa na uzoefu wao ili uwafaidishe, fikiria ni vibaya zaidi jinsi gani tutakavyokuwa ikiwa tunafanya kama walivyotenda! Iwapo hatutendi vizuri zaidi kuliko wao, tunawezaje kutarajia kuwa wateule kwa ajili ya muhuri na kwa Ufalme maadamu hawakustahiki? {1TG7: 11.1}

Katika hali ya ukubwa wa maisha, Musa alijiona kuwa mwenye uwezo wa kuwaokoa wana wa Israeli. Lakini Majaaliwa yakasema: “Wewe hujafaa kwa kazi hiyo, toka na Nitakufanya uwe wa kufaa.” Na Musa akatoka akaenda. {1TG7: 11.2}

Hakuhitaji elimu ya Farao ili aifanye kazi ya Mungu. Ilikuwa kizuizi kwake! Kwa nini? Kwa sababu ilimfanya wa kujitegemea nafsi, asiyemtegemea Mungu. Mtu kama huyo angalikuwa wa kufaa kuwaongoza watu wa Mungu mbali kutoka Kwake na kuwaingiza dhambini, lakini asiyefaa kuwaongoza kwa Mungu na mbali na dhambi. {1TG7: 11.3}

Ni kweli namna gani taarifa katika Shuhuda, Gombo la 5, uk. 80: “… Katika kazi ya mwisho ya uchaji watu wakuu wachache watahusishwa. Wanajitegemea nafsi, hawamtegemei Mungu, na hawezi kuwatumia. Bwana anao watumwa waaminifu, ambao katika mtikiso, wakati wa kupimwa watafunuliwa waonekane.” {1TG7: 11.4}

Mungu anaweza kuwasaidia tu wale wanaojua kwamba hawalingani na kazi yao, wale wanaojua kwamba wanahitaji msaada Wake. Hivyo, basi, wale ambao hufikiri kwamba wanaweza kufanya maajabu

11

ni wale hasa ambao hawawezi kufanya chochote ila madhara. {1TG7: 11.5}

Dhahiri, wale ambao Mungu atatumia katika kazi Yake ya mwisho, katika wakati wa mwisho, hawapaswi kuwa chochote kama mkuu wa taji wa Misri, sio kitu chochote kama Musa msomi. Wale ambao wanaweza kujifunza kuwalisha na kuwachunga kondoo vyema na kuwa tayari kutii maagizo, ni wale ambao wanaweza kufundishwa jinsi ya kuwatunza na kuwalisha watu wa Mungu. {1TG7: 12.1}

Mke wa Musa ndiye pekee aliyekuwa Mkushi katika kundi lote. Kwa sababu hii baadhi walifikiri walikuwa bora kuliko yeye. Walifikiri kwamba Musa alikuwa amefanya dhambi isiyoweza kusamehewa kwa kuoa nje ya taifa lake, kana kwamba rangi ilikuwa na kitu cha kuwafanya na kutowafanya watu kuwa bora au duni. Dadake Mu-sa, Miriamu, alinaswa katika dhambi hiyo. Hapo alikuwa, akijaribu kuivunja familia yake, hata hivyo Musa ali-omba kwa ajili ya uponyaji wake alipokuwa amepatwa na ukoma. {1TG7: 12.2}

Ni nani walioingia nchi ya ahadi? — Wote isipokuwa wanung’unikaji. Je, unadhani kwamba unaweza kuikuza roho hiyo ya kunung’unika na kulalamika, na licha yake kuupokea muhuri? — Jinsi gani la upumbavu wazo hilo! Je, isingalikuwa sawa kwa Mungu mwenye haki kuwaangamiza wasiotii wa siku hiyo, lakini awaokoe wasiotii wa siku hii. {1TG7: 12.3}

Ni nini kilicholifanya kundi moja lihitimu kuvuka Yordani? — Ilikuwa imani yao kwa Mungu, walijua kwamba Yeye alikuwa Kiongozi wao Mkuu. Walimtambua Musa na Yoshua kama wale ambao Mungu alikuwa akiwasil-iana nao. Hawakuwatazama kuwa kama mtu yeyote isipokuwa ambavyo walivyokuwa hakika. Waliridhika kwa kura yao. Walitii maagizo jinsi yalivyokuwa yakitolewa. Hivyo ilikuwa kwamba wao ndio pekee yao walioingia ndani ya nchi. {1TG7: 12.4}

12

Tukiwa na mifano hii mbele yetu, taswira hii ya kukumbuka, naweza kusema kwa ujasiri iwapo ninaelekea katika Ufalme au ikiwa ninaelekea katika vina vya nchi (Ufu. 12:16). Na nina uhakika kwamba wewe, pia, unaweza kueleza ni njia ipi unaelekea. Bwana hahitaji zaidi au pungufu kutoka kwetu kuliko vile Alivyotaka kutoka kwa walio mifano yetu. Kwa hivyo hakuna fumbo kuhusu kile tunachopaswa kufanya, na kile ambacho hatupaswi kufanya ili kuupokea muhuri wa Mungu. {1TG7: 13.1}

Hatupaswi kwenda katika nchi ya maajabu, hatuhitaji kuliburudisha wazo kwamba sharti tuwe na hisia ya ajabu, hisia ya kusisimua, hatuhitaji kugaagaa mavumbini au kuruka kwenye dari. La, hatuhitaji kujifanya wapumbavu. Yote tunayohitaji kufanya ni kuwa wanyoofu. Kuwa watulivu, wa adabu, wa kuheshimika, viumbe kama wa mbinguni, kujitahidi kufanya mapenzi ya Mungu duniani kama yanavyofanyika mbinguni. Hatuhitaji kujifanya wonyesho, ila tunahitaji kuijali shughuli yetu tuliyopewa na Mungu na kujiepusha na shughuli za watu wengine. {1TG7: 13.2}

Wakati tumefanya tu yote tunayoweza kwa kuyazingatia matakwa ya ujumbe wa leo, sio wa jana, tutatiwa mu-huri na kusimama na Mwana-Kondoo juu ya Mlima Sayuni. {1TG7: 13,3}

Je, hatupaswi kufurahi kwamba wakati tunapoalikwa kwenye Ufalme, tunaambiwa pia jinsi ya kufika huko? Kwa kuyaona haya yote, hatupaswi kamwe kuruhusu imani yetu kwa Mungu ififie. Tunapaswa kuwa thabiti, imara katika kila kitu, bila upungufu wa kitu chochote. Watumwa wa Mungu wa saa kumi na moja, unanea Uvuvio, watakuwa “ni wakuu, tena wenye nguvu, mfano wao haukuwako kamwe, wala hautakuwako baada ya hao, hata katika miaka ya vizazi vingi.” Yoeli 2: 2. Wanakijua wanachoamini, na wanaamini kile wanachokijua. La muhimu zaidi ya yote, wanajua kwamba wanaongozwa na Mungu, sio na mwanadamu. {1TG7: 13.4}

13

Wao sio kama Mafarisayo ambao waliokuwa wakijenga makaburi kuwakumbuka manabii waliokufa (Mat. 23: 29-31) na wakati huo huo walikuwa wakiwaua walio hai! Kwa mwanga huu unaoangaza kwa njia yetu, Wae-brania, sura ya 3, 4, 10 na 11 zinakuwa za kujifafanua zenyewe. {1TG7: 14.1}

14

Ukurasa Mtakatifu

Utukufu unafunika ukurasa mtakatifu,

Wenye fahari kama jua;

Unatoa nuru kwa kila kizazi,

Hutoa, lakini hauombi yeyote.

Roho hupuliza juu ya neno,

Na huleta ukweli uonekane;

Maagizo na ahadi zinapatikana

Nuru ya kutakasa.

Mkono ambao ulitoa, bado husambaza

Mwanga wa neema na joto;

Kweli zake juu ya mataifa huinuka,

Huinuka, wala hazitui kamwe.

 

Shukrani za milele ziwe zako,

Kwa wonyesho mwangavu kama huu;

Unafanya ulimwengu wa giza kuangaza

Pamoja na miale ya siku ya mbinguni.

 

–Wm. Cowper

15

WAZO LA SALA YA UFUNGUZI

Nitasoma kutoka kwa Mlima wa Baraka, kuanzia aya ya kwanza kwenye ukurasa wa 157. {1TG8: 16.1}

M.B, uk. 157– “Kulitukuza jina la Bwana linahitaji kwamba maneno ambayo tunatamka juu ya Aliye Mkuu Kul-iko wote yatamkwe kwa utiifu. “Takatifu na la kuogopwa ndilo jina Lake.” Kamwe hatupaswi kwa namna yoy-ote kuchukulia kihivi-hivi majina ya Mungu. {1TG8: 16.2}

“Lakini kulitukuza jina la Bwana humaanisha zaidi ya hili …. Kulihusu kanisa la Kristo imeandikwa, ‘Na jina lake atakaloitwa ni hili, Bwana ni Haki yetu.’ Jina hili linawekwa juu ya kila mfuasi wa Kristo. Ni urithi wa mtoto wa Mungu. Familia huitwa kwa jina la Baba. Nabii Yeremia, katika wakati wa dhiki kali ya Israeli na mateso, ali-omba, ‘Tumeitwa kwa jina Lako; usituache.’… {1TG8: 16.3}

“Katika kila tendo la maisha unapaswa kulidhihirisha jina la Mungu. Ombi hili linakuita uimiliki tabia Yake. Huwezi kulitukuza jina Lake, huwezi kumwakilisha Yeye kwa ulimwengu, isipokuwa katika maisha na tabia un-awakilisha kwa uhalisi maisha na tabia ya Mungu. Hili unaweza kulitenda tu kwa njia ya kuipokea neema na haki ya Kristo.” {1TG8: 16.4}

Kwa kutambua kwamba Mungu ametukubali mbele ya wanadamu na malaika kama watoto Wake, hebu tuombe ili “hatuwezi kufanya aibu kwa” jina lililostahili ambalo mmeitwa. ‘”Hebu tuombe ili tuwe wawakilishi Wake wa kweli. {1TG8: 16.5}

16

MLAODEKIA AU MDAUDI — YUPI?

MATINI YA HOTUBA NA V. T. HOUTEFF

MCHUNGAJI WA WADAUDI WAADVENTISTA WA SABATO

SABATO, SEPTEMBA 28, 1946

HEKALU LA MLIMA KARMELI

WACO, TEXAS

Alasiri hii nitajibu swali: Ninajuaje kwamba mimi sio bado Mlaodekia, kwamba sasa mimi ni Mdaudi wa kweli? Ili kwa busara tulijadili swali hili, lazima kwanza tuwe na picha ya akili kuhusu kile walivyo Walaodekia, na kile ambavyo Wadaudi wanavyopaswa kuwa. Nitasoma {1TG8: 17.1}

Ufunuo 3: 14-18 — “Na kwa malaika wa kanisa lililoko Laodikia andika; Haya ndiyo anenayo yeye aliye Amina, Shahidi aliye mwaminifu na wa kweli, mwanzo wa kuumba kwa Mungu. Nayajua matendo yako, ya kuwa hu baridi wala hu moto; ingekuwa heri kama ungekuwa baridi au moto. Basi, kwa sababu una uvuguvugu, wala hu baridi wala moto, nitakutapika utoke katika kinywa changu. Kwa kuwa wasema, Mimi ni tajiri, nimejitajirisha, wala sina haja ya kitu; nawe hujui ya kuwa wewe u mnyonge, na mwenye mashaka, na maskini, na kipofu, na uchi. Nakupa shauri, ununue kwangu dhahabu iliyosafishwa kwa moto, upate kuwa tajiri, na mavazi meupe upate kuvaa, aibu ya uchi wako isionekane, na dawa ya macho ya kujipaka macho yako, upate kuona.”

Ni nini kibaya na malaika wa Laodekia? — Yeye ni vuguvugu. Yeye si baridi wala moto. Bwana anapendekeza kwamba awe baridi au moto, — asiyejitosheleza, kwa kutafuta kitu bora kuliko kukaa

17

vuguvugu, akiwa ametosheka na mafanikio yake ya kiroho, akidhani kwamba yeye ni tajiri na amejitajirisha (kwa Ukweli). Hajui kwamba ni masikini kiroho, kipofu na uchi, ameonywa juu yake na Yeye Ajuaye Yote na kuulizwa kutubu. Iwapo onyo la Bwana mwenyewe linashindwa kuibadilisha nia yake, basi jambo la pekee lili-loachwa kwa ajili ya Bwana kulifanya ni kumtapika kutoka katika kinywa hake. {1TG8: 17.2}

Kwa maneno, “Mimi ni tajiri, na nimejitajirisha,” malaika wa Laodekia anasema kwamba anao ufahamu mzuri wa Biblia na anazo “Shuhuda za Kanisa,” na kwamba hizi zinamfanya kuwa tajiri. Na kwamba zaidi ya hizo, anayo machapisho mengine ya kidini, utajiri wake. Hivi anajidanganya mwenyewe kwamba anao ukweli wote kumpeleka moja kwa moja hadi katika Malango ya Lulu, kwamba hahitaji kitu chochote zaidi. Shauri la Bwana, hata hivyo, kwamba anunue Kwake dhahabu iliyosafishwa kwa moto ili aweze kuwa tajiri, linafunua ukweli kwamba utajiri wa Walaodekia sio “dhahabu safi,” na kwamba kinachoitwa eti utajiri sio utajiri wa Ukweli, ila ni usio na maana, ufafanuzi ambao haujavuviwa wala kujaribiwa kwa moto. {1TG8: 18.1}

Malaika wa Laodekia yu uchi, pia. Yeye hajajivika vazi la harusi hana haki ya Kristo. Na kuwa kwake uchi, bila kujivika nguo yoyote, kunaashiria kwamba hana utakatifu isipokuwa wake mwenyewe — haki ambayo alizaliwa nayo — ngozi yake tupu. Zaidi ya hayo, yeye ni kipofu kiroho. Na kwamba kwa ajili ya ugonjwa wake dawa ya macho ya Bwana ndiyo tiba ya pekee. Iwapo angaliweza tu kuupokea ushauri wa Bwana na kupaka dawa kwa macho yake yanayougua, basi angeweza kuona. {1TG8: 18.2}

Nini kinachowakilishwa na dawa ya macho? Kwanza hebu tuone kile ambacho humfanya mtu awe kipofu kiroho. Yule Ambaye anajua hata idadi ya nywele juu ya vichwa vyetu, anabainisha kwamba “Basi ile nuru ili-yomo ndani yako ikiwa giza,

18

si giza hilo!” Mat. 6:23. Iwapo uzembe wa kutumia vyema nuru ya kiroho humfanya mkosaji kuwa kipofu, basi kitu chenye uwezo wa kufufua ndani yake juhudi za kugundua hali yake ya kweli, ndio dawa yake ya pekee. Dawa ya macho kama hiyo tu inaweza kuyafumbua macho yake. Hebu nifafanue kwa uthabiti: {1TG8: 18.3}

Watu mara kwa mara huandika kwa ofisi wakisema: “Nilisikia sana dhidi ya ‘Fimbo ya Mchungaji,’ na yale nili-yoyasikia yalinifanya nichukizwe bila rehema. Lakini naliweza kushika moja ya trakti zako ndogo, … na kwa ajili ya heshima, nilifikiri ningeweza kuona inahusu nini. Lakini niliposoma kurasa zake chache, na kadri macho yangu yalipoanza kufumbua, nilisoma trakti yote. Sasa nina hamu kusoma vitabu vyako vyote vilivyosalia. Ta-fadhali unaweza kunitumia kitu chochote cha kusoma unachoweza?” {1TG8: 19.1}

Tukio lingine la Majaaliwa kama hili lilikuja kwa umakini wetu kutoka mbali sana China: “Naliokota nusu ya trakti yako (Trakti Namba 13) mtaani, na mke wangu siku chache baadaye aliokota nusu nyingine kando ya ki-zuio cha njia iyo hiyo. Niliziunganisha pamoja, na nikapata anwani yako. Ninavutiwa sana na yote yaliyomo, na ninajitahidi kusubiri kusikia kutoka kwako. Je, Unaweza kuniambia kila kitu kitakachonisaidia kupata furaha?” {1TG8: 19.2}

Hawa ndugu wachunguzi wa ukweli bila shaka wanawakilisha wale ambao wanaweza kung’olewa kutoka kwa Ulaodekia wao. Uzoefu wao unaonyesha vyema kwamba “dawa ya macho” inawakilisha Ukweli wa Uvuvio kwa wakati mwafaka. {1TG8: 19.3}

Sasa hebu niwambie kuhusu daraja lingine la watu ambao mara kwa mara huwa nasikia kutoka kwao. Sikiliza kile wao husema: “Tafadhali jiwekee ‘Fimbo’ kwako mwenyewe, ondoa jina langu kwenye orodha yako ya ba-rua. Mimi sina hamu hata kidogo ya kile unachofanya. Vijitabu vyako hutupwa

19

motoni mara tu vinapofika. Kamwe huwa sivisomi na sitavisoma kamwe — la, sio hata mstari. Nimeridhika [vuguvugu] na dini yangu. Mimi ni wa kanisa la kweli la masalia na ninatarajia kuendelea nalo. Je, unadhubutu vipi kujaribu kunidanganya?” {1TG8: 19.4}

Mwingine anasema: “Tafadhali usinitumie tena vitabu vyako, kwa kuwa nimeridhika na maoni yangu mwenyewe.” {1TG8: 20.1}

Aina hii ya mazungumzo aghalabu ni ya Ulaodekia. Yanaonyesha kikamilifu uvuguvugu wao. Bwana, hata hivyo, yu kinyume na mwenendo wao. Je, kipo chochote ambacho chaweza kabisa na kwa haraka kuutenga mwunganisho wa mawasiliano na Mungu milele kuliko mwenendo wa kuwa na Ukweli wote na wa kutohitaji zaidi? Ikiwa lugha katika barua ambazo nimekuwa nikisoma kwenu hazisemi, “Mimi ni tajiri, nimejitajirisha, na sina haja ya kitu,” basi ni nini kingaliweza kusema hayo? {1TG8: 20.2}

Kundi hili la Walaodekia halitawahi kamwe, kamwe kufumbuliwa macho yao, kamwe halitakuwa kitu chochote ila wanyonge, wenye mashaka, na maskini, na kipofu, na uchi. Hawawezi kufikiwa kamwe na Mbingu, sio hata na Bwana Mwenyewe. Iwapo wanaendelea hivi, basi jambo la pekee ambalo Kristo anaweza kufanya ni ku-watapika kutoka kinywani Mwake, kamwe kutoyataja majina yao penye Kiti cha Enzi cha Neema. Chochote kipya kutoka kwa Biblia ambacho hutolewa na mtu yeyote isipokuwa wao wenyewe, hata ingawa kinadai kuwa kwa njia ya Uvuvio, kwa haraka wao hukipiga chapa “udanganyifu,” ingawa tayari wako katika udanganyifu wa jumla wa ubinafsi. Wao huisoma Biblia kwa tumaini la kupata ushahidi wa kutumia kuhitilafiana na kila mtu isipokuwa wao wenyewe. {1TG8: 20.3}

Hebu nifanye mfano: Ninaweza kuwa njiani kwenda benki na dola milioni moja, na ninaweza kuamini kwa bidii kwamba mimi ni millionaire. Lakini waza mwanabenki aniambie,

20

“Pesa zako ni ghushi,” na waza sina zingine. Basi nitakuwa tajiri namna gani? — Ningekuwa tajiri kama alivyo malaika wa Laodekia. Hasa uzoefu kama huu wa kufumbua jicho ndio ambao Walaodekia wanahitaji. Isipoku-wa kitu kama hiki kitukie kwao, watadhani milele kwamba wao wamejitajirisha na hawana haja ya kitu. Baadhi husema, hata hivyo, sio muda mrefu basi, Mlinzi wa mbinguni Mwenyewe atawaonyesha ana kwa ana kwamba dhahabu yao haijajaribiwa katika moto. Kisha macho yao yatafumbuliwa, lakini sio muda mchache kuwatendea wema wowote. {1TG8: 20.4}

Wanachokiona sasa kwa mbali, kinaonekana kwao kwa hakika kuwa ni “bahari ya kioo.” Lakini wanapofikia mwisho wa njia, na waangalie kwa ukaribu, watakuwa na huzuni isiyoelezeka na kwa sauti ya kutetemeka kulia “Mazigazi, mazigazi! Sio bahari ya kioo!” Ndipo watakuwa na hamu ya kujua Ukweli; na hawatalipa chochote kuupata, lakini watakuwa wamechelewa sana na, kubadilisha umbo, wataufikia mlango tu kusikia Sauti kutoka ndani ikisema, “Siwajui ninyi.” Mat. 25:12. {1TG8: 21.1}

Kwa tabia za uso wa mtu tunaweza kutambua jamii yake; na vivyo hivyo tunaweza kuhukumu taaluma ya mtu kwa aina ya nguo ambazo huvaa: Ikiwa mtu huvaa nguo nzuri na hajajipamba kwa kila kitu anachoweza kujivi-ka, tunamhukumu kuwa mwana biashara. Iwapo huvaa mavazi ya daraja la chini na mwilini mwake anacho kila kitu anachoweza kujipamba kwacho, basi tunamhukumu kuwa mwana tafrija. Ikiwa amejivika vazi la kupwaya, tunamhukumu kuwa mfanyakazi. Iwapo amevaa vinginevyo, tunamhukumu kuwa mfanyakazi wa ofisini. Lakini iwapo huwa havai nguo yoyote, basi hakuna mtu ila Mungu anayeweza kujua yeye ni nani. Kama huyo ni Mla-odekia. {1TG8: 21.2}

Sasa, iwapo vazi jeupe huwakilisha Haki ya Kristo, basi ikiwa mtu hajavaa nguo yoyote,

21

yu uchi, basi ni haki ya nani atakuwa nayo? — haki ya ubinafsi, ngozi tu aliyozaliwa nayo. Uchi wa Walaodekia unawakilisha tu hiyo, lakini hawajui. Kwa heshima yote, natambua hili linasema mengi, lakini halisemi mengi sana, kwa sababu ni Bwana Ambaye ananena. {1TG8: 21.3}

Anawaalika Walaodekia wanunue Kwake dhahabu, aina ambayo imejaribiwa kwa moto (Ukweli uliovuviwa), ili kwamba waweze kuwa matajiri kweli. Yeye anawaalika wajivike vazi la harusi, ili wasitupwe katika “giza la nje,” huko kulia na kusaga meno yao. Ikiwa hawaupokei mwaliko wake sasa — naam, sasa — uchi wao utafunu-liwa na hivyo kuaibishwa. {1TG8: 22.1}

Iwapo utafanya kinyume cha vile ambavyo Walaodekia hufanya, basi bila shaka huwezi kuwa bado ni Mlaode-kia. Na ni rahisi tu kujua kama wewe ni Mdaudi au la. Ili kujua kama wewe ni Mdaudi, lazima kwanza ujue Mdaudi ni nini. Naam, kueleza kwa ufupi, Mdaudi anatambulika kwa vazi lake, na chanzo ambacho yeye hu-lipata, na kwa kile yeye kutoa ili kubadilisha kwa ajili ya vazi hilo. Nabii Zekaria anafafanua: {1TG8: 22.2}

Zek. 3: 1-4 — “Kisha akanionyesha Yoshua, kuhani mkuu, amesimama mbele ya malaika wa Bwana, na Shetani amesimama mkono wake wa kuume ili kushindana naye. Bwana akamwambia Shetani, Bwana na akukemee Ewe Shetani; naam, Bwana, aliyechagua Yerusalemu, na akukemee; je! Hiki si kinga kili-chotolewa motoni? Basi, Yoshua alikuwa amevaa nguo chafu sana, naye alikuwa akisimama mbele ya ma-laika. Naye huyo akajibu, akawaambia wale waliosimama mbele yake, akisema, Mvueni nguo hizi zenye uchafu. Kisha akamwambia yeye, Tazama, nimekuondolea uovu wako, nami nitakuvika mavazi ya tha-mani nyingi.”

22

Yule wa kwanza kupewa vazi ni Yoshua, kuhani mkuu, afisa mkuu katika kanisa. Iwapo hana lile vazi, basi hakuna mwingine aliye nalo aidha. Kutoka kwa hili tunaona kwamba uamsho na matengenezo halisi huanzia kwa kichwa, sio kwa miguu, na kwamba kabla ya mtu kupewa haki ya kujivika vazi, uovu wake unaondolewa — anatubu dhambi zake, na Bwana anazifuta. Shetani, hata hivyo, yuko hapo kumpinga na kumshtaki; lakini, shukrani kwa Mungu kwamba Bwana pia yuko hapo kumkemea adui. Je, Unalipata somo, Ndugu, Dada? Wa-kati ambapo unalipata vazi utahitajika kupambana na upinzani mkali. Lakini ni nini? Je, ni vigumu sana kusimama imara kwa ajili ya Ukweli na haki wakati wengi wanaacha? Na ni jinsi gani utakuwa shujaa kwa ajili ya Mungu? (Soma Mathayo 5: 10-12.) {1TG8: 23.1}

Mitume na manabii sio tu waliustahimili upinzani kutoka kwa ndugu zao, lakini hata walifurahi kufa kwa ajili ya vazi lao jeupe. Wewe, hata hivyo, sasa hujaulizwa kuyatoa maisha yako, bali kuyahihifadhi. “Meza” sasa zime-geuzwa. Bwana hataruhusu uangamizwe kwa kuchomwa moto. Yeye atakuokoa kama “kinga kilichonyakuliwa kutoka motoni.” {1TG8: 23.2}

Kutoka kwa hili tunaona kwamba Yoshua wa leo aliye na mavazi yake machafu yanabadilishwa kwa mavazi meupe, kwa ajili ya haki ya Kristo. {1TG8: 23.3}

Aya ya 5 — “Nikasema, Na wampige kilemba kizuri kichwani pake. Basi, wakampiga kilemba kizuri kichwani pake, wakamvika mavazi; naye malaika wa Bwana akasimama karibu.”

Sio tu amevikwa mavazi meupe, lakini pia amevikwa kilemba cha haki. Na kilemba kama hicho kingeweza kuashiria nini isipokuwa mamlaka yaliyowekezwa

23

ndani yake kama mtawala aliyeteuliwa na Mbingu? Kwa hivyo amevikwa kutoka kichwani mwake hadi miguuni mwake, “na malaika wa Bwana akasimama karibu.” Ni zawadi ya namna gani! na ni mpambe wa jinsi gani kwa ajili ya mtu kuwa naye katika ulimwengu kama wetu huu! Licha ya hayo, hata hivyo, wanadamu si wepesi sana na wa kusitasita kusimama upande wa Bwana. Wengi wao badala yake wangeridhia kumwegemea mwanadamu. {1TG8: 23.4}

Aya ya 8 — “Sikiliza sasa, Ee Yoshua, kuhani mkuu, wewe na wenzako waketio mbele yako; maana hao ni watu walio ishara; kwa maana, tazama, ninamleta mtumishi wangu, aitwaye Chipukizi.”

Sio Yoshua tu, bali pia wale waketio mbele yake (ushirika) wanashauriwa kusikia agizo hili. Na ni watu wa aina gani? – Watu wa kushangaza. Ishara hii inaonyesha kwamba katika utimilifu wa unabii huu malaika wa kanisa la Laodekia sio tena msimamizi wa nyumba ya Bwana, na kwamba watu wa Mungu watafanywa kuwa watu wa kushangaza kabisa! {1TG8: 24.1}

Kwa udhahiri, basi, kama matokeo ya uamsho na matengenezo haya ndani ya kanisa la Laodekia, kanisa lingine linajitokeza ambalo Yoshua ni msimamizi, sio malaika wa Laodekia. Ndani yake hayatakuwamo “magugu” (Mat. 13:30), “samaki wabaya” (Mat. 13:47, 48), au “mbuzi” (Mat. 25:32). Laodekia, la saba, ndilo la mwisho ambalo limechangamana na wanafiki, watakatifu na wadhambi. {1TG8: 24.2}

Ni nani atakayeleta uamsho na matengenezo haya, mabadiliko haya makubwa? — CHIPUKIZI. Na kwa mujibu wa Isaya 11: 1 hadi 5, Chipukizi ni Bwana, Mwana wa Daudi. Sasa tunasoma– {1TG8: 24.3}

Aya ya 9 — “Maana, litazame jiwe hili Nililoliweka mbele ya

24

Yoshua; katika jiwe moja yako macho saba; tazama, nitachora machoro yake, asema Bwana wa majeshi, Nami nitauondoa uovu wa nchi ile katika siku moja.”

Wale ambao wameketi mbele ya Yoshua ni “watu wa ishara.” Kwa vile wanawakilishwa na lile “jiwe” (kanisa, au Ufalme) ambalo liko mbele ya Yoshua. Linayo macho saba — maono makamilifu. Wakati ambapo utakaso huu wa kanisa unatukia basi dhambi katika nchi inaondolewa haraka — “kwa siku moja.” {1TG8: 25.1}

Hapa unaonekana uamsho na matengenezo ya kweli yakiambatana na utakaso wa kanisa. Bwana atkuwa na ka-nisa safi na watu wasafi. {1TG8: 25.2}

Aya ya 10 — “Katika siku ile, asema Bwana wa majeshi, ninyi mtamwalika kila mtu jirani yake chini ya mzabibu, na chini ya mtini.”

“Katika siku hiyo,” siku ambayo utakaso huu unatukia, kazi ya injili itakamilishwa haraka kwa kuwa kila mshiriki wa nyumba ya Bwana atamwita jirani yake kwenye kipande chake cha ardhi, kwa kile ambacho Mungu amepanga kimbele kwamba kila mtu apate. Kila mshiriki, kwa hivyo, anapaswa kuwa mmishonari kwa nafasi moja au nyingine. Hakika hili ni vuguvugu la washiriki ambalo litakamilisha kazi ya Injili. {1TG8: 25.3}

Taarifa hiyo, “mtamwalika kila mtu jirani yake chini ya mzabibu, na chini ya mtini,” inaonekana pia katika Mika 4. Inafundisha kitu kimoja ambacho Zekaria anafundisha. {1TG8: 25.4}

Somo hili, hata hivyo, halikomi kwa Zekaria tatu, linaendelea. {1TG8: 25.5}

25

Zek. 6:11 — “Naam, pokea fedha na dhahabu, ukafanye taji, ukamvike kichwani Yoshua, mwana wa Ye-hosadaki, kuhani mkuu.”

Malaika ameagizwa kuchukua fedha na dhahabu, na kutengeneza vilemba — sio kimoja, lakini zaidi ya kimoja. Hivi vinawekwa juu ya kichwa cha Yoshua. {1TG8: 26.1}

Aya ya 14 — “Na hizo taji zitakuwa za Heldai, na Tobia, na Yedaya; na kwa fadhili za mwana wa Sefania; ziwe ukumbusho katika hekalu la Bwana.”

Aya ya 14 inafichua kwamba Yoshua atapeana taji kwa wasaidizi wake ambao Bwana Mwenyewe atawataja. Hili litakuwa ukumbusho, ukumbusho wa milele katika hekalu la Bwana. {1TG8: 26.2}

Je, Haya yote yanamaanisha nini? – Hili tu: Yoshua ni hakimu, mtawala aliyeteuliwa na Mbingu,. Yeye mwenyewe amevikwa taji hivyo. Na kwa kuitikia amri ya Bwana Mwenyewe, Yoshua anawavika (anaidhinisha) wasaidizi wake ambao Bwana Mwenyewe anataja. Kwa maneno mengine, kama washiriki wa “nyumba ya Daudi,” Yoshua anawaidhinisha kushiriki katika kazi. Kwa hivyo, Yoshua anawajibika kwa Bwana, bali wa-saidizi wake wanawajibika kwa Yoshua. Hapa linaonekana shirika lililo na Kiongozi Mkuu na kiongozi mdogo — Bwana na Yoshua. Hivi ni kwamba chochote kitakachofungwa duniani, pia kitafungwa Mbinguni (Mat. 16:19.) {1TG8: 26.3}

Kwa uthabiti kama Mbingu inavyoweza kuifanya, ishara hii inaonyesha kwamba watu wa Mungu katika kazi hii ya mwisho hawataifanya kazi kwa kuhitilafiana. Wote watanena mamoja. Hivyo ni kwamba “Sauti ya walinzi wako! Wanapaza sauti zao, wanaimba pamoja; Maana wataona jicho kwa jicho, Jinsi Bwana arejeavyo Sayuni.” Isa. 52: 8. Ndipo watu Wake wataitwa

26

“Watu Mtakatifu, Waliokombolewa na Bwana,” “Waliotafutwa, Mji usioachwa” (Isaya 62:12). {1TG8: 26.4}

Aya ya 12 — “Ukamwambie, ukisema, Bwana wa majeshi asema hivi, ya kwamba, Tazama, mtu huyu ndiye ambaye jina lake ni Chipukizi; naye atakua katika mahali pake, naye atalijenga hekalu la Bwana.”

Yoshua anaagizwa vyema kwamba mzigo na ustadi wa kujenga hekalu hili la kiroho, ni wake Yeye ambaye jina lake ni “CHIPUKIZI.” Yeye atakua kutoka mahali Pake. Utukufu kwake Yeye. Yeye pekee ndiye wa kuinu-liwa. Yeye ndiye atakayelijenga hekalu la Bwana. {1TG8: 27.1}

Aya ya 13, 15 — “Naam, yeye atalijenga hekalu la Bwana; naye atauchukua huo utukufu; ataketi akimiliki katika kiti chake cha enzi; na kutakuwa na kuhani katika kiti chake cha enzi; na shauri la amani litakuwa kati ya hao wawili …. Nao walio mbali watakuja na kujenga katika hekalu la Bwana, nanyi mtajua ya kuwa Bwana wa majeshi amenituma kwenu. Na haya yatatokea, kama mkijitahidi kuitii sauti ya Bwana, Mungu wenu.”

Hivyo unabii wa Isaya, sura ya pili na ya nne, pia sura ya nne ya Mika utatimizwa. {1TG8: 27.2}

Hatimaye, tunajuaje yakini kwamba ujumbe huu ulipangwa na ukanakiliwa hasa kwa kanisa la leo? — Tunajua hili kutoka kwa ukweli kwamba ufunuo wa maandiko haya sasa, kuliko wakati mwingine wowote, umefunuliwa na kutangazwa. Sasa utangazaji wake unajulisha kwamba Bwana “anayachukua mamlaka mikononi Mwake Mwenyewe” (Shuhuda kwa Wachungaji, uk 300); kwamba wakati wa utakaso wa kanisa (Hukumu ya Walio Hai katika nyumba ya Mungu — 1 Pet 4:17) iko karibu (Ushuhuda, Gombo la 5, uk. 80); kwamba wale waliota-kaswa, watu 144,000 (ngano) — Ufu. 14: 1 watawekwa ghalani (Mat. 13:30), hawatachangamana tena na magugu; kwamba umati wa watu wasiohesabika kutoka

27

katika Mataifa yote (Ufu. 7: 9), wataletwa ndani ya nyumba ya Bwana (Isa. 66:19, 20). {1TG8: 27.3}

Wewe, mwenyewe, unaweza sasa kujibu swali ikiwa kama wewe ni Mdaudi au bado ni Mlaodekia. Iwapo umej-iridhisha, na mafanikio yako ya kiroho, na mpangilio wako wa injili uliofanywa na mwanadamu; ikiwa unafikiri kwamba Bwana anazungumza nawe kwa chochote kinachotokea kwa “bonyeza” akilini mwako; ikiwa unafikiri unao Ukweli wote, na kwamba hauhitaji kitu chochote zaidi; iwapo unafikiri kwamba kila mtu ambaye hana chapa ya kibali chako kwa imani yake, ni nabii wa uongo; na kama wewe unayo hofu ya daima kwamba mtu anajaribu kukudanganya siku zote kwa sababu hufundisha kitu kipya; iwapo hautakifikiria kwamba unaweza kuwa unaufunga mlango wako dhidi ya mbeba Ukweli ambaye anawezakuwa anakuletea “dawa ya macho” ya Bwana, na “vazi la harusi” — iwapo hutenda haya yote au sehemu yake, basi ni lazima ulivyo inawezekana uwe Mlaodekia, sio Mdaudi. {1TG8: 28.1}

Lakini ikiwa unajua kwamba mavazi yako ni machafu, na uovu wako haujafutwa; ikiwa unatambua kwamba un-atakikana kutembea katika njia za Mungu anavyoongoza kupitia kwa Yoshua wa leo, ikiwa wewe ni yote kwa ajili ya Mungu na sio yote kwa ajili ya nafsi au ya ulimwengu, basi, bila shaka, wewe aidha unakuwa, Mdaudi. Iwapo haujaafikia haya yote, unapaswa kuona kwamba unafanya hivyo; na ikiwa umeafikia tayari, basi endelea kustawi katika nuru, na kwa hakika mwishowe utasimama juu ya Mlima Zayuni na Mwana-Kondoo. {1TG8: 28.2}

Sasa chukua shauri la Bwana, wala usiwe tena kama kipande cha gome kinachoelea baharini na kila upepo wa mafundisho. {1TG8: 28.3}

“… Watu wa Mungu wanawakilishwa katika ujumbe

28

kwa Walaodekia kama walio katika nafasi ya usalama wa kimwili. Wako shwari, wanajiamini kuwa katika hali ya juu ya kiroho …. {1TG8: 28.4}

“Ni udanganyifu mkubwa jinsi gani unaoweza kuja juu ya akili za binadamu kuliko kujiamini kwamba wako sawa, wakati ambapo wote wamekosea! ujumbe wa Shahidi wa Kweli huwapata watu wa Mungu katika udanganyifu wa kusikitisha, hata sasa wao ni waaminifu katika udanganyifu huo. Hawajui kwamba hali yao ni mbaya machoni pa Mungu. Wakati wale wanaolengwa wanajidanganya kwamba wako katika hali ya juu ya kiroho, ujumbe wa Shahidi wa Kweli huuvunja usalama wao kwa mashtaka ya kushtusha juu ya hali yao ya kweli ya upofu wa kiroho, umasikini, na unyonge. Ushuhuda, unaokata na mkali, hauwezi kuwa kosa, kwa maa-na ni Shahidi wa Kweli anayesema, na ushuhuda wake lazima uwe sahihi.” — Shuhuda kwa Kanisa, Gombo la 3, uk. 252, 253. {1TG8: 29.1}

Hatuna haki ya kumhukumu mtu

Mpaka ahukumiwe kwa haki;

Je, haitupasi kulipenda kundi lake,

Twajua ulimwengu ni mpana.

Baadhi wanaweza kuwa na makosa — na nani hana?

Wazee na pia vijana;

Pengine twaweza, kwa sifuri tunayojua,

Kuwa na hamsini kwa lao moja.

–Joseph Kronthal

29

Amini na Utii

Tunapotembea na Bwana

kwa nuru ya Neno Lake,

Utukufu wa jinsi gani Yeye huangaza juu ya njia yetu!

Wakati tunafanya mapenzi yake mema,

Hukaa nasi bado,

Na wote ambao watakaomwamini na kumtii.

Sio mzigo tunaobeba,

sio huzuni tunayoshiriki,

Lakini kazi yetu Yeye atalipa sana.

Sio sikitiko wala kupoteza,

sio kununa wala msalaba,

Lakini ni baraka kama tunaamini na kutii.

Lakini hatuwezi kamwe kuthibitisha

furaha ya upendo Wake,

Mpaka yote juu ya madhabahu tuweke,

Kwa neema Yeye huonyesha,

na furaha Yeye hutoa,

Ni kwa wao ambao wataamini na kutii.

–J. H. Sammis

30

Usiyakose Manufaa Juu ya Hili

Iwapo haujatuma kwa ajili ya nakala yako iliyotangazwa na iliyojadiliwa sana kijitabu cha afya cha kurasa 96 (Kabari Inayoingia) ambacho kimefanya uamsho mkubwa katika dunia ya Waadventista na ambacho kimeliweka Shirika la K.I. katika mwangaza, usikikose iwapo afya, nyumba, na furaha yako inamaanisha kitu kwako. Kwa maoni yetu kitabu hiki ndicho bora hatujawahi kuona juu ya su-ala hili. Kwa kweli tunahisi kwamba kimetumwa na Mungu, na kwamba nakala yake inapaswa kuwa katika kila nyumba. Tumejulishwa kwamba sasa unaweza kukipata bila kuagizia. Tuma jina lako, anwani, na jina la kanisa ambalo wewe ni mshiriki (unaombwa kuchap-isha), na senti 15 kwa sarafu au stempu kwa Shirika La Kabari Inayoingia La Marekani, Kituo cha Mlima Kar-meli, Waco, Texas, Marekani na kitatumwa kwako. {1TG8: 31.1}

31

Jumuiya ya Wadaudi Waadventista wa Sabato

(Ushirika Huru Unaojumuisha Kanisa)

Mlima Karmeli, Waco, Texas

S.L.P. 23738, Waco, TX 76702

+ 1-254-855-9539

www.gadsda.com

info@gadsda.com

Gombo la 1, Namba 7, 8

Kimechapishwa nchini Marekani

32

>