30 Jan Gombo la 1 Salamu Mwafaka Namba 05, 06
Gombo la 1 Salamu Mwafaka Namba 5, 6
AMANI YA PEKEE YA MAWAZO
Hati miliki, Kimechapishwa tena 1953
Haki zote zimehifadhiwa
V. T. HOUTEFF
LILE LITAKALOKUWAKO KATIKA SIKU ZA MWISHO
ZAYUNI NA BINTI ZAKE KATIKA SIKU ZA MWISHO
1
WAZO LA SALA YA UFUNGUZI
Kabla ya kujishughulisha katika maombi na kujifunza Biblia, nitasoma kutoka Mlima wa Baraka, kuanzia aya ya kwanza kwenye ukurasa wa 102. Sura hiyo imejengwa kwa Sala ya Bwana. {1TG5: 2.1}
M.B. kur. 151, 152 — “Sala ya Bwana ilitolewa mara mbili na Mwokozi wetu, kwanza kwa umati katika ma-hubiri juu ya mlima, na tena, miezi kadhaa baadaye, kwa wanafunzi pekee yao. Wanafunzi walikuwa hawako kwa muda mfupi kutoka kwa Bwana wao, wakati waliporudi walimpata Yeye amevutwa sana fikira katika ushirika na Mungu. Akionekana kuwa hana ufahamu wa uwepo wao, Aliendelea kuomba kwa sauti. Uso wa Mwokozi ulikuwa umenururishwa na uangavu wa mbinguni. Alionekana kuwa katika uwepo hasa wa Asiyeon-ekana: na kulikuwa na nguvu hai katika maneno Yake, kama ya mmoja aliyenena na Mungu. {1TG5: 2.2}
“Mioyo ya wanafunzi waliokuwa wakisikiliza iliguswa sana. Walikuwa wameweka alama jinsi ambavyo alitumia masaa mengi akiwa faraghani, katika ushirika na Baba Yake. Siku zake zilipita kwa kuwahudumia umati wa wa-tu Waliomsonga, na kwa kuifichua falsafa yenye hila ya marabi, na kazi hii isiyokoma mara nyingi ilimwacha Yeye akiwa amechoka kabisa kwamba mama na ndugu Zake na hata wanafunzi Wake, walihofia kwamba mai-sha Yake yangekuwa kafara.” {1TG5: 2.3}
Waliohofia nini? Waliogopa kwamba Yesu alikuwa akifanya kupita kiasi, na ya kwamba Iwapo Yeye anga-liendelea kuzichosha zaidi nguvu Zake, hangaliweza kuishi kwa muda mrefu. Walihisi kuwa Yeye hakika an-gekuwa mgonjwa na kufa. {1TG5: 2.4}
Je, Matarajio yao yalitimia? — Hapana. Kinyume cha yale waliyoyahofia yalitukia. Ni nini kilichomfanya awe sawa kwa kazi Yake? Haikuwa sala? Iwapo Yesu angeweza kupata nguvu za kutosha katika maombi ili kufanya kazi zake za kila siku, kwa nini hatuwezi? Hebu tupige magoti na kusali kwa mwisho huu. {1TG5: 2.5}
2
LILE LITAKALOKUWAKO KATIKA SIKU ZA MWISHO
MATINI YA HOTUBA NA V. T. HOUTEFF
MCHUNGAJI WA WADAUDI WAADVENTISTA WA SABATO
SABATO, SEPTEMBA 7, 1946
HEKALU LA MLIMA KARMELI
WACO, TEXAS
Masomo yetu ya alasiri hii ni kutoka kwa Isaya, sura ya tatu. Lakini maadamu hadithi, au unabii, wa sura hii huanzia katika sura iliyotangulia hatuwezi kujifunza kwa maufaa sura ya tatu bila kuitegemea ya pili. Hakuna yeyote kwa kuanza kujifunza somo kutoka katikati, akirudi nyuma au akienda mbele, anaweza kujifunza mwen-delezo wake na kujua linahusu nini. Iwapo mmoja anaweza kujifunza ukweli kamili wa somo, lazima ajifunze kwa ujumla wake. Mbwa na paka, sio wanadamu waliostaarabika, huanza kula kipande cha keki kuanzia katikati hadi nje. Kama wanadamu wenye akili, kama watu wa Mungu, tunapaswa kula keki kwa usahihi. {1TG5: 3.1}
Ninajuaje kwamba somo la kinabii la sura ya tatu huanza na sura ya pili? — Neno la kwanza kabisa la sura ya ta-tu, kihusishi “kwa maana,” linaonyesha kwamba kitu fulani kimepita awali. Ili kuchukua uendelezaji wa mzigo wa Uvuvio, na pia kupata msingi wa somo hilo, tunalazimika kuanza somo letu kwa aya hiyo hasa Isaya aliongozwa ili kuanza unabii: {1TG5: 3.2}
Isa. 2: 1 — “Hili ni neno aliloliona Isaya mwana wa Amozi katika habari za Yuda na Yerusalemu.”
Isaya aliongozwa kufunua nini? — Mambo kuhusu
3
Yuda na Yerusalemu, kanisa. Tunahitaji kujua, hata hivyo, kizazi halisi cha watu hao, kwa sababu ikiwa unabii unakihusu kizazi chetu, basi utakuwa na maana kubwa kwetu. Mafundisho yake basi yatakuwa haswa mwafaka kwa mahitaji yetu ya sasa na makubwa — yatakuwa “chakula kwa wakati mwafaka.” Kwa sababu hii hasa tunahitaji kuhakiki ni nani watu ambao Uvuvio unazungumzia. Hebu tusome {1TG5: 3.3}
Aya ya 2 — “Na itakuwa katika siku za mwisho, mlima wa nyumba ya Bwana utawekwa imara juu ya milima, nao utainuliwa juu ya vilima; na mataifa yote watauendea makundi makundi.”
Sio mtu, sio watu au taifa, ila Bwana Mwenyewe anatangaza hivyo. Nabii alionyeshwa mambo kuhusu nyumba ya Bwana (kanisa), “katika siku za mwisho,” — sio katika siku za Isaya. Taarifa “siku za mwisho,” yenyewe inat-uongoza hadi kwa “wakati wa mwisho.” Kama tulivyoonyeshwa Sabato iliyopita kwamba wakati wa mwisho ulianza katika karne ya 18, ni wazi basi, wakati umefika kwa ajabu hii ya vizazi kutukia. {1TG5: 4.1}
Aya ya 3 — “Na mataifa mengi watakwenda na kusema, Njoni, twende juu mlimani kwa Bwana, nyumbani kwa Mungu wa Yakobo, naye atatufundisha njia zake, nasi tutakwenda katika mapito yake maana katika Sayuni itatoka sheria, na neno la Bwana katika Yerusalemu.”
Kwa sababu hakuna mkusanyiko kama ule uliotabiriwa hapa umetukia, somo hili linakuwa dhahiri sana kwamba bado unakuja. {1TG5: 4.2}
Miaka michache iliyopita katika shauku yangu ya Isaya 2, nilimuhoji mhubiri mwenye ujuzi, ambaye pia alikuwa
4
msemaji mwenye ufasaha. Alijibu kwa mkazo kadri alivyoweza, kwa kusema, “Hilo halitatimizwa kamwe.” Wa-kati huo sikujua, na jibu lake kwa swali langu halikunisaidia kwa njia moja au nyingine, lakini sasa kwamba gombo limekunjua na Mungu Mwenyewe anatangaza kwamba Neno Lake halishindwi kamwe, na tunapaswa kumwamini Yeye, kwa maana iwapo unabii huu hauwezi kutimizwa, basi tuna uhakikisho gani kwamba unabii wowote utatimizwa? {1TG5: 4.3}
Zaidi ya hayo, iwapo unabii huu hautatimizwa, basi kazi ya injili haitamalizika aidha, kwa maana unabii huu un-aelezea jinsi kazi itakavyomalizika — kwamba sheria ya Bwana siku ya hukumu ya walio hai itatoka Sayuni, na Neno la Bwana kutoka Yerusalemu, — sio kutoka Takoma Park, sio kutoka Kituo cha Mlima Karmeli, na wala sio kutoka mahali pengine ama. {1TG5: 5.1}
Baada ya kazi ya hukumu katika nyumba ya Mungu (1 Pet. 4:17) kukamilika na watumwa 144,000 wa Mungu wasiokuwa na uongo, malimbuko (Ufu. 14: 4) kuchukua nafasi yao ya juu na iliyoinuliwa pamoja na Mwana-Kondoo juu ya Mlima Sayuni (Ufu. 14: 1), kisha kuanza kukusanywa ndani mavuno ya pili. Hatimaye macho ya ulimwengu yatafumbuliwa kwa hali hiyo, na kama taifa moja linaalika taifa lingine, kazi ya injili itashika kasi sana. Wengi watasema, “twende juu mlimani kwa Bwana, nyumbani kwa Mungu wa Yakobo, naye atatufun-disha njia zake.” Manabii wote wamezungumzia juu ya tukio hili kubwa na la ajabu, lakini kwa ajili ya ufupisho ninanukuu tu kutoka sura moja — Zekaria 2. {1TG5: 5.2}
“Naye akamwambia, Piga mbio, kamwambie kijana huyu, na kusema, Yerusalemu utakaliwa na watu, kama vijiji visivyo na kuta, kwa sababu ya wingi wa watu na mifugo iliyomo ndani yake. Kwa maana mimi, asema Bwana, nitakuwa ukuta wa moto kuuzunguka
5
pande zote, nami nitakuwa huo utukufu ndani yake …. Imba, ufurahi, Ee binti Sayuni; maana, tazama, ninakuja, nami nitakaa kati yako, asema Bwana. Na mataifa mengi watajiunga na Bwana katika siku ile, nao watakuwa watu wangu; nami nitakaa kati yako, nawe utajua ya kuwa Bwana wa majeshi amenituma kwako. Na Bwana atairithi Yuda, iwe sehemu yake katika nchi takatifu, naye atachagua Yerusalemu tena. Nyamazeni, ninyi nyote wenye mwili, mbele za Bwana; kwa maana ameamka, na kutoka katika maskani yake takatifu.” Zekaria 2: 4, 5, 10-13. {1TG5: 5.3}
Aya ya 4 — “Naye atafanya hukumu katika mataifa mengi, atawakemea watu wa kabila nyingi; nao wa-tafua panga zao ziwe majembe, na mikuki yao iwe miundu; taifa halitainua upanga juu ya taifa lingine, wala hawatajifunza vita tena kamwe.”
Sio mataifa, ila Uvuvio Wenyewe unatangaza kwamba katika siku ambayo Mungu anawahukumu walio hai, basi mataifa hayo yanayoenda mlimani (Kanisa la Ufalme lililotakaswa) la Bwana “watawafua panga zao ziwe majembe, na mikuki yao iwe mundu” — watakuwa wakulima badala ya kutumia nguvu zao vitani. Mataifa am-bayo hayatapokea “kemeo” la Bwana, katika siku hiyo, hata hivyo, kwa wenda wazimu yatainuka dhidi ya “mlima” wa Bwana, kama ilivyotabiriwa na nabii Yoeli, akisema: “Tangazeni haya kati ya mataifa; takaseni vita; waamsheni mashujaa; watu wa vita na wakaribie; na wapande juu. Yafueni majembe yenu yawe panga, na mi-undu yenu iwe mikuki; aliye dhaifu na aseme, Mimi ni hodari. Fanyeni haraka, mje, enyi mataifa yote, wa pande zote, jikusanyeni pamoja; na huko watelemshe mashujaa wako wote, Ee Bwana. Mataifa na wajihimize, waka-pande juu katika bonde la Yehoshafau; maana huko ndiko nitakakoketi niwahukumu mataifa yote yaliyo pande zote.” Yoeli 3: 9-12. {1TG5: 6.1}
6
Maadamu Uvuvio umeyaweka wakfu machapisho haya kwa kulitangaza tukio hili muhimu zaidi kuhusiana na injili — kilele na ushindi wake, mtengo wema kutoka kwa wabaya (Mat. 13:30, 47, 48), mbuzi kutoka kwa kon-doo (Mat. 25:32); na kuanzishwa kwa mlima wa nyumba ya Bwana; basi hakuna kukwepa hitimisho kwamba sura hizi za Isaya ziliandikwa hasa kwa kanisa leo. Sasa kwa kuwa sisi ni watangulizi wa tukio hili kubwa na la utukufu, tunapaswa kutoa tahadhari maalum kwa yale sura hizi zitasema. Hili tunapaswa kulifanya iwapo tuna-paswa kuiandaa njia ya Bwana (Mat. 3: 3, Isa. 4: 3-5). Ujumbe huu kwa kanisa, unaona wazi, ni kuandaa washiriki wake kwa Hukumu kabla ya “siku kuu na ya kutisha ya Bwana” kuanza (Mal. 4: 5). Kwa sababu hii hasa Maandiko kwa wakati huu yanafunuliwa. Hebu sasa tuisikie maombi ya Bwana. {1TG5: 7.1}
Aya ya 5 — “Enyi wa nyumba ya Israeli, njoni, twende katika nuru ya Bwana.”
Kwa sababu kanisa linahitaji sana nuru hii, nuru ambayo sasa inaangaza Siku ya Hukumu, Bwana ameifanya rai ambayo imepita kwa “nyumba ya Yakobo” ya uakisi, nyumba ambayo wamo Wayakobo 144,000, wazao wa ka-bila 12 za Israeli, ambao mfululizo kwa njia ya vizazi walifyonzwa na nchi za Mataifa, na hivyo wakapoteza utambulisho wao wa taifa. {1TG5: 7.2}
Kujali kwa Bwana, kwamba kanisa litembee katika nuru ya Bwana (katika nuru ya Uvuvio ya leo) kwa udhahiri ina maana kwamba sasa halitembei katika nuru Yake; na amri Yake, inayopatikana katika aya ya mwisho ya sura ya Isaya, inaonyesha dhahiri kwamba linatembea katika cheche za watu ambao hawajavuviwa. Bwana, kwa hivyo, anaamuru: {1TG5: 7.3}
7
Aya ya 22 — “Mwacheni mwanadamu ambaye pumzi yake i katika mianzi ya pua yake; kwa maana hudhaniwaje kuwa ni kitu?”
Sababu kwamba washiriki wake wanapaswa mara moja kuwaacha wanadamu imenenwa katika aya zifuatazo: {1TG5: 8.1}
Isa. 3: 1-4 — “Kwa maana, tazama, Bwana, Bwana wa majeshi, awaondolea Yerusalemu na Yuda egemeo na tegemeo; tegemeo lote la chakula na tegemeo lote la maji; mtu hodari na mtu wa vita; mwamuzi na nabii; mpiga ramli na mzee; jemadari aliye juu ya watu hamsini, na mtu mstahifu, na mshauri, na fundi aliye mstadi, na mganga ajuaye uganga sana. Nami nitawapa watoto kuwamiliki, na watoto wachanga kuwatawala.”
Kwa zaidi ya karne sisi kama Waadventista wa Sabato tumekuwa tukihubiri kazi ya Hukumu ya Wafu, na sasa tunapaswa kwa urahisi kuona kwamba wakati Hukumu ya Walio Hai itakapoanza itawatenganisha watakatifu kutoka kwa wadhambi — ngano kutoka kwa magugu (Mat. 13:30), samaki wazuri kutoka samaki wabaya (Mat. 13:47, 48), kondoo kutoka kwa mbuzi (Mat. 25: 32-46), wanawali wenye hekima kutoka kwa wale wapumbavu (Mat. 25: 1-13). {1TG5: 8.2}
Dhahiri basi, Isaya 3: 1-4 inafunua kwamba kati ya wale wanaopatikana wamepungukiwa, ni baadhi ya watu wenye nguvu, watu wa vita, waamuzi na manabii (walimu wa dini), wenye busara na wakongwe, maakida na waheshimiwa, washauri na mafundi werevu na wasemaji stadi, na kwamba Mungu sio wa kuwaheshimu watu, bali wadhambi wanaotubu tu pekee; kwamba Yeye hawezi kuwategemea watu wanaoitwa eti watu wakuu. {1TG5: 8.3}
Wale ambao wamekuwa wakijikweza na ambao wamewafanya watu Wake kufuata watu wasomi badala ya Uvuvio na kwa hivyo Ukweli wa Bwana
8
unaoendelea, wote watapeperushwa mbali kama makapi! {1TG5: 8.4}
Ndugu ambao kwa miaka mingi wamekuwa wakihubiri Hukumu kwa Wafu wamekuwa vipofu kiroho na wap-umbavu, hawatarajii hata ujumbe wa Hukumu kwa Walio Hai na wanasema kwa ujeuri. “Unabii huu hauwezi kutimizwa!” Sasa ni saa yao ya kutafakari juu ya nuru hii pamoja na taarifa: “Katika kazi ya mwisho ya uchaji watu wakuu wachache watahusishwa.” — Shuhuda, Gombo la 5, uk. 80. {1TG5: 9.1}
Hebu turudi katika sura ya 2. {1TG5: 9.2}
Isa. 2: 6 — “Maana wewe umewaacha watu wako, nyumba ya Israeli, kwa sababu wamejaa kawaida za mashariki, nao ni wapiga ramli kama Wafilisti, na wanapana mikono na wana wa wageni.”
Kwa wakati wa kukusanywa ndani kukuu ambako kumeonyeshwa hapa kunakaribia kutukia, watu Wake wanaomkiri, Yeye anatangaza, hujifurahisha wenyewe kati ya wale ambao hawajaongoka na wanatuhumiwa kuwa waaguzi, kwa uhodari wakiufafanua visivyo Ukweli wa Mungu uliofunuliwa kwa wakati huu badala ya kuutukuza na kuutangaza . {1TG5: 9.3}
Aya ya 7 — “Tena nchi yao imejaa fedha na dhahabu, wala hapana mwisho wa hazina zao; tena nchi yao imejaa farasi, wala hapana mwisho wa magari yao.”
Nyumba ya Yakobo ambayo Mungu anazungumzia hapa inatambulishwa tena kwa ukweli kwamba inakaa kati-ka nchi iliyojaa fedha, dhahabu, na magari, kwamba hakuna mwisho wa idadi yake. Maadamu hakuna
9
nchi katika ulimwengu wote wa Mungu ambayo ni tajiri kwa fedha, dhahabu na msongamano wa magari kama ilivyo nchi hii ya Majimbo Yaliyouangana ya Amerika, ni wazi kabisa Amerika, nchi ambamo makao makuu ya injili yapo, ndiyo nchi ambayo Mungu anataja. Yeye, kwa hivyo, siku hii, Ndugu, Dada, kwa njia ya pekee Ana-zungumza nawe, kwa dhehebu lote na hasa kwa Baraza Kuu (nyumba ya Yakobo) katika Ukweli uliofunuliwa upya, na kwa lugha isiyokosa kueleweka. Je, wewe, mimi, kwa furaha tutayazingatia mapenzi ya Bwana? ni swali kuu mbele yetu. Hivi karibuni Hukumu itaanza na lazima tuhakikishe kwamba kesi zetu zitasimama. {1TG5: 9.4}
Aya ya 8 — “Tena nchi yao imejaa sanamu [Anatangaza]; huabudu kazi ya mikono yao, vitu vilivyofany-wa kwa vidole vyao wenyewe.”
Nchi ambamo injili sasa inatokea pia imejaa sanamu, Anatangaza, aina ambayo mikono yao wenyewe imezifan-ya; yaani, wanajivunia ibada zao za sanamu, na mafanikio yao wanayaabudu kama kwamba yamekuwa Mungu wao. Wote wanyonge na wakuu wanatenda desturi za unafiki. Usiwasamehe Yeye anapaza sauti, isipokuwa wao watubu. {1TG5: 10.1}
Aya ya 10 — “Ingia ndani ya jabali; ukajifiche mavumbini mbele za utisho wa Bwana, mbele za utukufu wa enzi yake.”
Hapa tunaambiwa wazi kwamba watenda dhambi hatimaye watajikuta hawajajiandaa kwa siku kuu na ya kutisha ya Bwana, na wakati Mungu akizidhihirisha hivyo Nguvu Zake watahofu kweli kweli. Watakuwa kama watu washenzi wataikimbilia miamba na milima ili kujificha. Tukio la aya hii linafanana na lile la Ufunuo:
10
“Na wafalme wa dunia, na wakuu, na majemadari, na matajiri, na wenye nguvu, na kila mtumwa, na mwungwana, wakajificha katika pango na chini ya miamba ya milima, wakiiambia milima na miamba, Tu-angukieni, tusitirini, mbele za uso wake yeye aketiye juu ya kiti cha enzi, na hasira ya Mwana-Kondoo. Kwa maana siku iliyo kuu, ya hasira yao, imekuja; naye ni nani awezaye kusimama?” Ufu. 6: 15-17. {1TG5: 10.2}
Ni dhahiri sana unabii wa Isaya unakutana na utimilifu wake katika wakati wa muhuri wa sita, wakati ambapo Bwana anakaa juu ya Kiti cha Enzi cha Utukufu Wake, sio juu ya mawingu, kiti cha enzi ambacho mbele yake yanakusanywa mataifa yote, ambapo kazi ya Hukumu inaanza: mtengo unafanyika, watakatifu (kondoo) wana-wekwa wakati huo kuume Kwake na wadhambi (mbuzi) kwa kushoto Kwake (Mat. 25:33). Nabii Yoeli anai-tangaza siku kwa maneno haya: {1TG5: 11.1}
“Haya! Utieni mundu, maana mavuno yameiva; njoni, kanyageni; kwa maana shinikizo limejaa, mapipa nayo yanafurika; kwani uovu wao ni mwingi sana. Makutano makubwa, makutano makubwa, wamo katika bonde la kukata maneno! Kwa maana siku ya Bwana i karibu, katika bonde la kukata maneno. Jua na mwezi vimetiwa giza, na nyota zimeacha kuangaza. Naye Bwana atanguruma toka Sayuni, atatoa sauti yake toka Yerusalemu; na mbingu na nchi zitatetemeka; lakini Bwana atakuwa kimbilio la watu wake, na ngome ya wana wa Israeli.” Yoeli 3: 13-16. {1TG5: 11.2}
Ni wakati ambapo itanenwa, {1TG5: 11.3}
“Wenye dhambi walio katika Sayuni wanaogopa; tetemeko limewashika wasiomcha Mungu; Ni nani kwetu sisi awezaye kukaa na moto ulao; ni nani kwetu sisi awezaye kukaa na moto uteketezao milele? Ni yeye aendaye kwa haki
11
anenaye maneno ya adili; ni yeye anayedharau faida ipatikanayo kwa dhuluma; akung’utaye mikono yake asipokee rushwa; azibaye masikio yake asisikie habari za damu; afumbaye macho yake asitazame uovu. Huyu ndiye atakayekaa juu; majabali ni ngome yake; atapewa chakula chake; maji yake hayatakoma. Wala hapana mwenyeji atakayesema, Mimi mgonjwa; watu wakaao humo watasamehewa uovu wao.” Isa. 33: 14-16, 24. {1TG5: 11.4}
Waovu ndani ya Zayuni ndio wa kwanza kuililia miamba na milima, wakati huo kutangazwa kwa siku kuu na ya kutisha ya Bwana kutaenda mbele mbali na kwa upana kusema: “Sikieni, ninyi mlio mbali, niliyoyatenda; na ninyi mlio karibu, kirini uweza wangu.” Isa. 33:13. {1TG5: 12.1}
Sasa ndio wakati wa kuacha kujipumbaza wenyewe, tuamue kumtumikia Bwana kwa moyo wote, na Yeye peke yake. {1TG5: 12.2}
Ninajuaje kwamba siku kuu ya Bwana imekaribia hapa? — Naijua kwa sababu tangazo la kuihusu liko hapa tayari, na kwa sababu ujumbe wa kutiwa alama uliotabiriwa katika Ezekieli sura ya tisa, kazi ya Hukumu, tayari inatengeneza njia yake kote katika ulimwengu wa Waadventista. Naijua pia kwa sababu habari za utukufu unaofuata mara baada ya hapo (habari ambazo zitaiangaza dunia kwa utukufu wa malaika, Kilio Kikuu – Ufu. 18: 1) ziko tayari na zinasubiri. {1TG5: 12.3}
Na ni nini kinachotokea basi? — kilio kinaenda kwa himaya yote ya Babeli, “kikisema, Tokeni kwake, enyi watu wangu, msishiriki dhambi zake, wala msipokee mapigo yake.” Ufu. 18: 4. Watu wa Mungu wanatoka Babeli ili kujiunga na kanisa Lake
12
lililotakaswa lisilo na dhambi, watumwa Wake wasio na hila, watu 144,000, malimbuko ya mlima wa nyumba ya Bwana. {1TG5: 12.4}
Kisha itakuwa kwamba kutoka kwa mataifa yote watakatifu wataingia ndani yake. “Maana, tazama, giza litaifunika dunia, Na giza kuu litazifunika kabila za watu; Bali Bwana atakuzukia wewe [kanisa lililotakaswa, mlima wa Bwana], Na utukufu wake utaonekana juu yako. Na mataifa wataijilia nuru yako, Na wafalme kuujia mwanga wa kuzuka kwako. Inua macho yako, utazame pande zote; Wote wanakusanyana; wanakujia wewe; Wana wako watakuja kutoka mbali. Na binti zako watabebwa nyongani. Ndipo utakapoona na kutiwa nuru, Na moyo wako utatetemeka na kukunjuka; Kwa kuwa wingi wa bahari utageuzwa kukujia, Utajiri wa mataifa utakuwasilia. Wingi wa ngamia utakufunika, Ngamia vijana wa Midiani na Efa; Wote watakuja kutoka Sheba; Wataleta dhahabu na uvumba; Na kuzitangaza sifa za Bwana. Makundi yote ya Kedari yatakusanyika kwako, Kondoo waume wa Nebayothi watakutumikia; Watapanda juu ya madhabahu yangu kwa kibali, Nami nitaitukuza nyumba ya utukufu wangu. Ni nani hawa warukao kama wingu, Na kama njiwa waendao madirishani kwao? Hakika yake visiwa vitaningojea, Na merikebu za Tarshishi kwanza, Ili kuleta wana wako kutoka mbali, Na fedha yao na dhahabu yao pamoja nao, Kwa ajili ya jina la Bwana, Mungu wako, Kwa ajili yake Mtakatifu wa Israeli, Kwa kuwa amekutukuza wewe. Na wageni watajenga kuta zako, Na wafalme wao watakuhudumu; Maana katika ghadhabu yangu nalikupiga, Lakini katika upendeleo wangu nimekurehemu. Malango yako nayo yatakuwa wazi daima; Hayatafungwa mchana wala usiku; Ili watu wapate kukuletea utajiri wa mataifa, Na wafalme wao wakiongozwa pamoja nao.” Isa. 60: 2-11. Kisha itatokea kwamba {1TG5: 13.1}
13
Aya ya 11 — “Macho ya mwanadamu yaliyoinuka yatashushwa chini, na kiburi cha mwanadamu kitain-amishwa, naye Bwana, yeye peke yake, atatukuzwa siku hiyo.”
Mwanadamu kwa muda mrefu amekuwa akijikweza; sana hivi, kwa kweli, kwamba wapo labda Wakristo wachache tu ulimwenguni ambao kweli wanaifuata “nuru ya Bwana.” Wengi wao wanafuata cheche za wana-damu, kuyafuata mafafanuzi ambayo hayavuviwa ya Maandiko, — ubunifu wa wanadamu, watu wanaodharau wazo la Uvuvio; hawaoni haja ya Ukweli zaidi au ya manabii, ingawa wanajua vyema kwamba Ukweli pekee ambao umewahi kuja umekuja kupitia watumwa waliochaguliwa na Mungu. Hata wauaminio Ukweli wa sasa bado hawajaamka kwa ufunuo huu wa kushangaza, wengi wao wanachukuliwa na kila upepo wa mafundisho, mengi ambayo yametengenezwa na walaghai kama Kora, Dathani na Abiramu (Hes. 16: 9-11) wakiitamani ofisi ya Musa — wanyakuzi wa Kiti cha Enzi cha Uvuvio – wakiunga mkono, mmoja wa Paulo na mwingine wa Apo-lo, kama ilivyokuwa! Jicho la Uvuvio likitazama hadi siku hii na ujumbe, linafichua kwamba wingi wa udanganyifu huu wa ubinafsi ni matokeo ya kile Roho anachoelezea, unafiki wa sura maradufu, akisema: “Na-we, mwanadamu, wana wa watu wako husimulia habari zako karibu na kuta, na ndani ya milango ya nyumba zao, na kuambiana, kila mtu na ndugu yake, wakisema, Haya! Twende tukasikie ni neno gani hilo litokalo kwa Bwana. Nao huja kwako kama watu wajavyo, nao hukaa mbele yako kama watu wangu, nao husikia maneno yako, wasiyatende; maana kwa vinywa vyao hujifanya kuwa wenye upendo mwingi, lakini mioyo yao inatafuta faida yao. Na tazama, wewe umekuwa kwao kama wimbo mzuri sana, wa mtu mwenye sauti ipendezayo, awezaye kupiga kinanda vizuri; maana, wasikia maneno yako, lakini hawayatendi. Na hayo yatakapokuwapo (tazama, yanakuja), ndipo watakapojua ya kuwa
14
nabii amekuwapo kati yao.” Ezek. 33: 30-33. Tunahitaji kuwa watendaji wa Neno sio wasikilizaji tu. {1TG5: 14.1}
Aya ya 12, 13, 15, 16 — “Kwa maana kutakuwa siku ya Bwana wa majeshi juu ya watu wote wenye ki-buri na majivuno, na juu ya yote yaliyoinuka; nayo yatashushwa chini. Na juu ya mierezi yote ya Leba-noni iliyo mirefu na kuinuka, na juu ya mialoni yote ya Bashani, na juu ya kila mnara mrefu, na juu ya kila ukuta ulio na boma,… na juu ya merikebu zote za Tarshishi, na juu ya kila taswira ipendezayo.”
Haya bila shaka ni maelezo ya ki-mfano, yakimaanisha watu wenye kiburi na wenye kujitegemea ambao machoni pa watu ni kama mierezi ya Lebanoni, na kama mialoni ya Bashani. {1TG5: 15.1}
Aya ya 17-20 — “Na majivuno ya mwanadamu yatainamishwa, na kiburi cha watu kitashushwa; naye Bwana, yeye peke yake, atatukuzwa siku hiyo. Nazo sanamu zitatoweka kabisa. Na watu wataingia ndani ya pango za majabali, na ndani ya mashimo ya nchi, mbele za utisho wa Bwana na utukufu wa enzi yake, atakapoondoka ili aitetemeshe mno dunia. Siku hiyo kila mtu atazitupilia mbali sanamu zake za fedha, na sanamu zake za dhahabu, walizojifanyia ili kuziabudu, kwa fuko na popo.”
Je, Sanamu gani zitakazoondolewa? — Sanamu ambazo hutembea. Ni, kwa hivyo, wanadamu ambao watu hu-waabudu. Wao, na wale wanaowaabudu watakimbilia “mapango ya majabali, na ndani ya mashimo ya nchi.” Wale tu ambao wanazitupilia mbali sanamu watasazwa. Katika aya hizi aina tatu za sanamu zinatajwa: (1) kazi za mikono ya wanadamu, (2) watu wanaoheshimiwa, (3) dhahabu na fedha ambazo zinaabudiwa. Hizi zitaon-dolewa, hazitakuwepo sanamu tena. {1TG5: 15.2}
15
Wao na wanaowaabudu; {1TG5: 16.1}
Aya ya 21 — “wataingia ndani ya pango za majabali, na ndani ya tundu za miamba iliyopasuka, mbele za utisho wa Bwana na utukufu wa enzi yake, atakapoondoka ili aitetemeshe mno dunia.”
Ikiwa sasa hatuzitupi nje kwa hiari sanamu zetu zote, tutalazimika kuzitupa baadaye, lakini manufaa gani zitat-utendea wakati huo basi? {1TG5: 16.2}
Isa. 3: 1 — “Kwa maana, tazama, Bwana, Bwana wa majeshi, awaondolea Yerusalemu na Yuda egemeo na tegemeo; tegemeo lote la chakula na tegemeo lote la maji.”
Wakati umekaribia ambapo wadhambi huko Yerusalemu na katika Yuda – watu wa Baraza Kuu na kanisa kwa ujumla, hawatakuwa na tone la kunywa au kula cha kutafuna. Ni nani aliye miongoni mwao? {1TG5: 16.3}
Aya ya 2-4 — “mtu hodari na mtu wa vita; mwamuzi na nabii; mpiga ramli na mzee; jemadari aliye juu ya watu hamsini, na mtu mstahifu, na mshauri, na fundi aliye mstadi, na mganga ajuaye uganga sana. Nami nitawapa watoto kuwamiliki, na watoto wachanga kuwatawala.”
Ishara za nyakati zitatambuliwa na hali zilizofunuliwa katika {1TG5: 16.4}
Aya ya 5 — “ Nao watu wataonewa, kila mtu na mwenziwe, na kila mtu na jirani yake;
16
mtoto atajivuna mbele ya mzee, na mtu mnyonge mbele ya mtu mwenye heshima.”
Kwa sababu mambo haya yanatukia sasa, hatupaswi kukosa ufahamu wa ukweli kwamba “siku kuu na ya kutisha ya Bwana” iko karibu. Watukutu na wajeuri hawataishi siku hiyo. {1TG5: 17.1}
Aya ya 6 — “Mtu atakapomshika ndugu yake ndani ya nyumba ya baba yake, akisema, Wewe una nguo, ututawale wewe; na mahali hapa palipobomoka pawe chini ya mkono wako.”
Kusema “wewe una nguo, ututawale wewe,” labda ni sawa na kusema, “Iwapo utatutawala unaweza angalau kutupatia kitu cha kuvaa, na uharibifu huu utakuwa chini ya udhibiti wako, unaweza kuisuluhisha hali hiyo.” {1TG5: 17.2}
Namna watu wanavyofikiri na kutenda katika wakati huu unaokuja wa taabu, uharibifu, na hali ngumu ya kila aina, wanaonyesha wazi kwamba sio waangalifu kwa Mungu, — la, hapana kabisa. Wanawaamini wanadamu na bidhaa. Wanatarajia kwamba mtu fulani anaweza kutatua hali hiyo, anaweza kuwaokoa kutokana na maangamizi. Hivyo wao kwa kuwaita wanadamu kuwasaidia badala ya kumwita Mungu, wanatenda kana kwamba Mungu ameacha nchi. {1TG5: 17.3}
Aya ya 7 — “Basi, siku ile atainua sauti yake, akisema, Mimi sitakuwa mponya watu; kwa maana ndani ya nyumba yangu hamna chakula wala mavazi; wala hamtanifanya kuwa mtawala juu ya watu hawa.”
Yule ambaye ameitwa kutawala, pia anaushiriki mwelekeo wa watu. Anatangaza kwamba hawezi kuponya uovu, kwamba yeye, pia, ni maskini. Mungu, hata hivyo, anaweka wazi sababu ya taabu: Hebu tuisome {1TG5: 17.4}
Aya ya 8 — “Kwa maana Yerusalemu umebomolewa na Yuda wameanguka:
17
kwa sababu ulimi wao na matendo yao ni kinyume cha Bwana, hata wayachukize macho ya utukufu wake.”
Sio dunia, ila Yerusalemu umeharibiwa, na Yuda ameanguka. Kwa nini? — Kwa sababu matendo yao na ndimi zao ziko kinyume na Bwana; yaani, wako kinyume cha Ukweli Wake wa Hukumu. Ni nini macho ya utukufu Wake? Kulingana na Isaya 62: 3 na 4: 5, utukufu Wake ni Zayuni iliyo hai daima, kanisa Lake lililonururishwa Ukweli. Ghala la Ukweli Wake uliofunuliwa ni, kwa hivyo, utukufu Wake, waonaji Wake ni “macho” Yake. Angalia 1 Samweli 9: 9. Yaani watumwa wa Mungu waliojazwa Roho ambao huongoza katika Kweli yote, ndiyo macho ya utukufu Wake ambao wadhambi bila kuona haya huwachokoza. {1TG5: 18.1}
Unajua kwa ukweli kwamba hakuna mtu ambaye hujiita mwenyewe Mkristo ambaye hunena kwa wazi dhidi ya Mungu. Kile wanaodai kuwa ni Wakristo hufanya kweli, kusema mambo dhidi ya Ukweli wa Mungu uliofunu-liwa, bila kutambua kwamba wananena na kutenda dhambi dhidi ya “Roho Mtakatifu,” na hivyo dhidi ya Mun-gu Mwenyewe, pia. {1TG5: 18.2}
Hata baadhi ya wanaouamini Ukweli wa sasa mara kwa mara hutamka neno la lawama, wakisema mambo am-bayo yanaweza kuimarisha heshima yao na kushusha ya mtu mwingine au kumvuta mtu kwa njia yao ya kufikiri kwa hasara ya kazi ya Mungu! Aina hizi za dhambi ni za kisiri sana. Na uwezo mkubwa wa yule anayehusika katika mazoea kama haya, ndivyo mkubwa zaidi uharibifu. {1TG5: 18.3}
Je, ndimi hizi zetu hatujapewa kumtukuza Mungu kupitia kwa Ukweli Wake, au tumepewa tuzitumiie kwa Ukweli wa Mungu uliofunuliwa kwa njia ya kujiinua nafsi, kuwafanya wengine wafikiri tunavyotaka? {1TG5: 18.4}
Labda uharibifu zaidi ya wote ni lawama zisizo za haki ambazo mara kwa mara hunenwa wanaposikia
18
watoto na vijana, au mbele ya wasio na ujuzi na wasio na ufahamu. Haya ni madhara ambayo hayawezi ku-badilishwa kamwe! Wazazi kwa upande mmoja hufanya kazi kwa bidii kuwaokoa watoto wao, na kwa upande mwingine kwa mazungumzo yasiyo ya busara huwafukuza mbali kutoka kwa Mungu na Ukweli wake. {1TG5: 18.5}
Aya ya 9 — “Kuonekana kwa nyuso zao kwashuhudia juu yao, wafunua dhambi yao kama Sodoma, ha-waifichi. Ole wa nafsi zao, kwa maana wamejilipa nafsi zao uovu.”
Dhambi zinazotendwa, sio aina ambayo watu kama sharti hufanya faraghani, ila badala yake ni aina ambayo wa-tu hujivunia, kwa maana huwa hawazifichi, wao huzifanya wazi na kukosa haya kwao huendelea kushuhudia dhidi yao. Watu wale hasa ambao wangeweza kuwa msaada mkubwa kwa Musa, walikuwa kizuizi kikubwa, walisababisha shida na manung’uniko. Hata Bwana Mwenyewe hakuweza kuwarudisha katika hisia zao kwa hivyo nchi ikafunua kinywa chake ikawameza wote. (Angalia Hes. 16: 26-33; Mababu na Manabii, uk. 400-405.) {1TG5: 19.1}
Wakati umekuja kwa ajili yetu tutoke katika utoto wetu, kuwa wanaume na wanawake imara — wakomavu ka-mili katika imani. Wakati umekuja kwa ajil yetu sote kula “chakula kigumu,” na kutambua kikamilifu kwamba kazi tunayoifanya ingekuwa imetupwa kwenye “jaa la taka” kabla ya kuafikia hili, iwapo ingetegemea hekima ya binadamu. {1TG5: 19.2}
Aya ya 10-12 — “Waambieni wenye haki ya kuwa watakuwa heri, kwa maana watakula matunda ya matendo yao. Ole wake mtu mbaya; shari itakuwa kwake, kwa maana atapewa ijara ya mikono yake. Katika habari za watu wangu, watoto ndio wanaowaonea, na wanawake ndio wanaowatawala. Enyi watu wangu, wakuongozao wakukosesha, waiharibu
19
njia ya mapito yako.”
Mungu mwenyewe hawezi kuwatawala wenye kiburi, wanajiona kuwa wa maana, na wa kujitegemea. Lakini kwa watu Wake, hata watoto na wanawake huwatawala. Kwa hiyo wao sasa wanaonywa kwamba wenye kiburi ambao wanawatawala sasa wanawakosesha, wakiuharibu mpango wa Mungu kwa ajili yao. {1TG5: 20.1}
Ndugu fulani alisema, “Natumaini Bwana hivi karibuni atachukua mamlaka mikononi Mwake Mwenyewe ili kuwaokoa Israeli.” Hata baada ya kufika Bahari ya Shamu, umati wa watu haukujua kwamba Mungu alikuwa amechukua mamlaka mikononi Mwake Mwenyewe. Wao, pia, walidhani kila kitu kilikuwa mikononi mwa Mu-sa. Ingawa kwa muujiza waliivuka Bahari, na ingawa waliimba wimbo wa ukombozi, na kuelewa kwamba mkono wa Mungu ulikuwa umewaokoa, lakini baadaye, walisahau, na tena wakaanza kumlaumu na kumlaani Musa kwa kuwaleta jangwani waangamie. Walikwama hata kwenye mipaka ya nchi ya ahadi, na matokeo yake iliwapasa kutumia miaka arobaini jangwani. {1TG5: 20.2}
Hata manna iliyoshuka kwa nchi kila siku haikuweza kuwashawishi umati kwamba Mungu alikuwa amechukua mamlaka mikononi Mwake Mwenyewe. Hivyo ilikuwa kwamba mizoga yao ilianguka jangwani, lakini watoto ambao walidhani kwamba kamwe hawangelifikia lengo lao waliimiliki nchi (Hes. 14: 1-3, 27-32; 26: 63-65). {1TG5: 20.3}
Kipo watu wa asili fulani ambao hata Mungu mwenyewe hawezi kuwashawishi kwamba amechukua amlaka mikononi Mwake Mwenyewe. Hawatii kamwe maagizo kutoka kwa yeyote isipokuwa wao wenyewe. Wa nam-na hii wanaojitegemea wataendelea kuhoji na kulaumu kila kitu ambacho wao wenyewe hawana sehemu. Hivyo bila kujali taaluma yao, wanachokifikiria au kusema, sio watu wa Mungu. Watu wake halisi, Anatangaza, wana-weza kutii maagizo
20
hata kutoka kwa wanawake na watoto. {1TG5: 20.4}
Watu wa Mungu hutii maagizo kutoka kwa mtu yeyote ambaye Mungu huteua kwa sababu wao huenenda kati-ka nuru ya Bwana, sio katika cheche za wanadamu. Anafafanua wazi kwamba wale ambao sasa wanawatawala, wanawakosesha watu Wake, na wanaiharibu njia ya mapito yao ya haki! {1TG5: 21.1}
Aya ya 13, 14 — “Bwana asimama ili atete, asimama ili awahukumu watu. Bwana ataingia katika ku-wahukumu wazee wa watu wake na wakuu wao; Ninyi ndinyi mliokula shamba la mizabibu; vitu mlivyowateka maskini vi ndani ya nyumba zenu.”
Andiko hili kwa mkazo linatangaza kwamba Bwana anateta wakati Anaposimama kuwahukumu watu, kuonye-sha kwamba Hukumu ya Walio Hai inaanza baada ya tangazo hili lake limesikika kote kote Laodekia. Shtaka dhidi ya wazee na wakuu (viongozi na wachungaji) ni kwamba wamekula wakamaliza shamba la mizabibu, kwamba wametumia mapato yote, na kwamba wamewanyang’anya watu Wake ili kujitajirisha wenyewe. Ni ukweli unaojulikana kwamba sio tu zaka (posho la pekee halali kwa ajili ya ukasisi) lakini pia sadaka (sehemu ya maskini) na mengine yote yanaliwa na ukasisi, na kwamba wameigeuza hata Sabato na nyumba ya ibada kuwa taasisi za kuchanga fedha, wakitumia kila aina ya njia na mbinu kwa jina la dini wanalolitumia kuwafanya maskini maskini zaidi na wao wenyewe matajiri zaidi. Si mimi, ila Bwana ndiye Yule Anayesema hivyo. Sitilii chumvi, kwa hivyo, kusema kwamba nyumba ya Mungu imekuwa nyumba ya biashara, inayoendeshwa na wezi, kwamba mahali pa makao ya wazee na wakuu kati yake yanatumiwa kama pakiti za viota vya panya, na kwamba siku ya Sabato imegeuzwa kuwa siku ya soko. “Ni nani anaweza kusema kwa kweli, ‘Dhahabu yetu imejaribiwa kwa moto; mavazi yetu
21
hayajatiwa doa na ulimwengu’? Nalimwona Mwalimu wetu akiyaonyesha mavazi ya kile kinachoitwa eti uta-katifu. Aliyararua, Akaufunua wazi unajisi uliokuwa chini yake. Kisha akanambia: ‘Je, huoni jinsi walivyoji-funika kwa hila unajisi wao na uozo wa tabia?’ “Je, Mji mwaminifu umekuwaje kahaba?” Nyumba ya Baba Yangu imefanywa kuwa nyumba ya biashara, mahali ambapo uwepo wa Mungu na utukufu umetoweka! Kwa sababu hii upo udhaifu, na nguvu inakosekana.’” — Shuhuda, Gomo la 8, uk. 250. {1TG5: 21.2}
Kuona kwamba karibu wote wananaswa na Adui wa roho, tunapaswa, kwa hivyo, kumcha sana Mungu na tutembee karibu Naye, tusije, pia, tukatumbukia ndani ya mfuko wa kuteka nyara wa Shetani. Tunapaswa kuwa wachungaji waangalifu na wanaojali, sio wafisadi wakatili. {1TG5: 22.1}
Utapata kwamba Ibilisi atapambania maisha na kushindana na ujumbe huu wa Hukumu kwa ujeuri, na atajaribu kuwashawishi wote kwamba huu unabii hautatimizwa. Watu wa kweli wa Mungu, hata hivyo, wataona umuhi-mu wa utimizo wake wakati huu maalum, na kwa furaha watapokea kile ambacho Neno la Mungu linasema. {1TG5: 22.2}
Tumeitwa kuwa wana matengenezo, sio wa kupoozesha, wakusanyaji pamoja na Mungu, sio wa kutawanya pamoja na Shetani. Hebu tuwe tu kile tunachokiri kuwa, na hivyo kusimama bila hatia mbele ya Kiti cha enzi cha Mungu, bila hila vinywani mwetu na hatimaye bila wadhambi kati yetu. {1TG5: 22.3}
Aya ya 15 — “Ni nini maana yake, ninyi kuwaonea watu wangu, na kuseta nyuso za maskini? Asema Bwana, Bwana wa majeshi.”
Ni shtaka la kutisha namna gani kwa mmoja kujifaidi mwenyewe akiwatumia maskini. Ni vibaya sana kwamba ndugu zetu wameanguka chini sana. Na bado kibaya zaidi ni kwamba hawazijali
22
hata kidogo jumbe hizi zilizotumwa kutoka Mbinguni, na badala ya kuzipokea, wanafanya yote ili kuzikwepa na kuwazuilia mbali washiriki wasije wakakutana nazo. {1TG5: 22.4}
Makosa yao yaweze kuwa ngazi yetu ya kufaulu. Kwamba pale wanaposagia nyuso za maskini, tuweze ku-wafanya kuwa na furaha, na tupate kutambua kwamba kumpokea mmoja aliye mdogo wa watu wa Mungu, ni kumpokea Mungu Mwenyewe. Tunastahili kuwa wenye shukrani jinsi gani kwa ajili ya pendeleo hili kuu. {1TG5: 23.1}
23
WAZO LA SALA YA UFUNGUZI
Kabla ya kushiriki katika wakati wa sala, nitasoma kutoka Mlima wa Baraka, uk. 154, kuanzia aya ya kwanza: {1TG6: 24.1}
M.B, uk. 154 — “Yesu hutufunza kumwita Baba Yake Baba yetu. Yeye haoni aibu kutuita sisi ndugu. Yuko tayari, wa shauku kubwa, ni moyo wa Mwokozi kutupokea kama washiriki wa familia ya Mungu, kwamba kati-ka maneno hasa ya kwanza tutakayotumia kumkaribia Mungu, Yeye anaweka uhakikisho wa uhusiano wetu wa Mungu, — ‘Baba yetu.’ {1TG6: 24.2}
“Hapa ni tangazo la ukweli huo wa ajabu, uliojaa himizo na faraja, kwamba Mungu anatupenda jinsi Yeye anavyompenda Mwanawe. Hili ndilo lile Yesu alisema katika sala Yake ya mwisho kwa wanafunzi Wake, Wewe “umewapenda kama Ulivyonipenda Mimi.” {1TG6: 24.3}
“Dunia ambayo Shetani amedai na kuitawala kwa udhalimu wa ukatili, Mwana wa Mungu, kwa ufanisi mmoja mkubwa, ameizungushia upendo Wake, na kuiunganisha tena na kiti cha enzi cha Yehova. Makerubi na Maser-afi, na majeshi yasiyo na idadi ya dunia zote ambazo hazikuanguka, waliimba nyimbo za sifa kwa Mungu na kwa Mwana-Kondoo wakati ushindi huu ulihakikishwa. Walifurahi kwamba njia ya wokovu ilikuwa imefungu-liwa kwa taifa lililoanguka, na kwamba dunia itaweza kukombolewa kutoka kwa laana ya dhambi. Wanawezaje kufurahi sana wale ambao ni walengwa wa upendo wa ajabu sana kama huu!” {1TG6: 24.4}
Kusema “Baba yetu,” sio Baba Yangu, hasa wakati wa kuomba hadharani, hutusaidia kutambua kwamba sisi sote ni ndugu. Mungu anatupenda sote kama Anavyompenda Kristo, na Yeye hatatuvunja moyo ikiwa tunaom-ba na kuishi kama sala ya Kristo na mfano Wake unavyofundisha. Yeye hawezi kutunyima jibu la sala zetu iwapo tunakijua kile tunachoomba, — ikiwa tunaomba vitu ambavyo kweli tunahitaji kuwa navyo, vitu ambavyo Yeye Mwenyewe anayo shauku kwamba sisi tuwe navyo. Kabla ya kusali kwa chochote, lazima tujifunze juu yake kwanza, ili sala zetu, pia, ziweze kusimama milele na milele. Hebu tupige magoti. {1TG6: 24.5}
24
ZAYUNI NA BINTI ZAKE KATIKA SIKU ZA MWISHO
MATINI YA HOTUBA NA V. T. HOUTEFF
MCHUNGAJI WA WADAUDI WAADVENTISTA WA SABATO
SABATO, SEPTEMBA 14, 1946
HEKALU LA MLIMA KARMELI
WACO, TEXAS
Mnakumbuka kwamba katika somo letu Sabato iliyopita, tulipata kwamba unabii wa sura ya tatu ya Isaya kweli huanza na sura ya pili, linaendelea kupitia ya tatu, na hufikia mwisho na sura ya nne. Na pia mnakumbuka kwamba habari ndani yake, ni kwa ajili ya kanisa “katika siku za mwisho,” katika sehemu ya mwisho ya wakati wa mwisho. Kwa maneno mengine, mnakumbuka kwamba katika sura hizi Mungu anazungumza moja kwa moja kwa watu Wake wanaoishi hasa wakati huu. {1TG6: 25.1}
Maadamu habari za sura hizi zimeelekezwa kwa Yuda, Yerusalemu, na Zayuni ya siku za mwisho, hebu kwa kifupi tuyapindue majina haya hadi katika lugha ya leo. {1TG6: 25.2}
Jina “Yuda” (ufalme wa Yuda), bila shaka, linabeba taifa hilo kwa ujumla. Kutumia jina hili kwa kanisa kwa wakati wetu, linamaanisha Dhehebu kwa ujumla, watu ambao wataujumuisha ufalme wa Yuda wa uakisi. Jina “Zayuni,” eneo la kale la kasri linafananishwa kama lilivyo katika sura hii, na mbali kutoka kwa nchi ya ahadi, linamaanisha Baraza Kuu, makao makuu ya Dhehebu. Kwa mujibu wa Nehemia 11: 1, jina “Yerusalemu” zamani lilimaanisha mji wa watawala wa taifa. Kutumia jina hili kwa wakati wetu, na mbali na
25
nchi ya baba zetu, jinsi Uvuvio hufanya, humaanisha watawala walio chini ya Baraza Kuu. Kurudia, Yuda huchukua ndani washiriki; Yerusalemu huchukua ndani viongozi wa mabaraza ya mitaa na wa muungano; Za-yuni huchukua ndani viongozi wa Baraza Kuu. Haya ndiyo tu matumizi yanayowezekana na ya kimantiki ya-nayoweza kufanywa kwa majina haya. {1TG6: 25.3}
Kujua sasa kwamba sura ya 3 inawasilisha habari za Bwana kwa ajili yetu leo, tutaanza somo letu na {1TG6: 26.1}
Aya ya 16 — “Bwana akasema tena, Kwa sababu binti za Sayuni wana kiburi, na kuenenda na shingo zili-zonyoshwa, na macho ya kutamani, wakienenda kwa hatua za madaha, na kuliza njuga kwa miguu yao.”
Mbali na masuala ambayo tuliangalia juma lililopita, Bwana anao ujumbe huu leo kwa “binti za Sayuni.” {1TG6: 26.2}
Katika aya hii hasa, kwa hivyo, Mungu anawaambia hasa mabinti za viongozi wa juu ndani ya Dhehebu, ukasisi, wale walio kwenye uongozi wa kazi. Kwa hivyo, Yeye yu karibu kufanya kitu kwa sababu binti za Sayuni ni “wenye kiburi,” majivuno. Kiburi chao kinafanywa wazi kwa ukweli kwamba wanatembea na shingo zili-zonyooshwa na macho ya kutamani; wameachiliwa, watovu, wasio faa. Kisha, pia, wanapotembea, kwa hatua za maringo na kuliza njuga kwa miguu yao, — hawatembei kwa kawaida, huigiza kama ilivyokuwa, ili kuvutia uan-galizi wa umma. Hivyo Mungu anawaona wako njiani, sio safari ya kufika walikokuwa wakienda, sio kupata kazi yao imefanyika, ila wako hapo waonekane. Hivi ndivyo Mungu anavyoitazama hali ya mambo ambayo ipo kati ya binti za Sayuni. Anawaona kama viongozi wakuu katika uasherati kanisani. {1TG6: 26.3}
26
Mnakumbuka katika somo letu la awali kile ambacho Bwana anateta dhidi ya wazee wa watu Wake, dhidi ya mtu hodari na mtu wa vita; mwamuzi na nabii; mpiga ramli na mzee; jemadari aliye juu ya watu hamsini, na mtu mstahifu, na mshauri, na fundi aliye mstadi, na msemaji mwenye ufasaha (Isa. 3: 2, 3). Wao ni “wapiga ramli,” Anatangaza (Isaya 2: 6); “wamekula shamba la mizabibu; vitu mlivyowateka maskini vi [ndani ya] nyumba zenu.” Isa. 3:14. Hivi Uvuvio unabainisha kwamba wao kwa uovu wanatumia nyara za maskini. Lugha nzito, hakika, lakini ni Mungu anayeinena. {1TG6: 27.1}
Aya ya 17 — “Basi, kwa hiyo, Bwana atawapiga binti za Sayuni kwa pele za utosini, na Bwana ataifunua aibu yao.”
Kwa sababu binti za Sayuni kwa upande mmoja ni kwa hasara ya maskini wakijifanya wapumbavu wenyewe, na kwa upande mwingine wanadai wanaiwakilisha Mbingu, Bwana atawapiga kwa pele za utosini. Hapana, ha-waondoki ama na nyara za maskini, au kwa upumbavu, uovu, upuuzi wao usiofaa. {1TG6: 27.2}
“Bwana atazifunua sehemu zao za siri” ikiwa hawatubu sasa. Kwa majivuno wanatumia vibaya vichwa vyao na shingo zao, viwiko vyao na miguu yao. Wanajivunia kufanya maonyesho ya bidhaa zao. Kwa sababu hii Bwana ataviweka wazi viungo ambavyo hawangetaka viweze kufunuliwa. Yeye atawafanya kuwa uchi. Atawafanya wao kuwa mfano wa watu wote. {1TG6: 27.3}
Aya ya 18-23 — “Katika siku hiyo Bwana atawaondolea uzuri wa njuga zao, na kaya zao; na pete za masikio, na vikuku, na taji zao; na dusumali, na mafurungu,
27
na vitambi, na vibweta vya marashi, na matalasimu; na pete, na azama, na mavazi ya sikukuu, na deb-wani; na shali, na vifuko; na vioo vidogo, na kitani nzuri, na vilemba, na utaji.”
“Katika siku hiyo,” siku ambamo hali hizi zitaenea kati ya watu wanaojidai kuwa wa Mungu, Yeye atauondoa ujasiri wao, ataondoa urembo ambao wanautumia kujipumbaza wenyewe. Atayaondoa mapambo ya uovu ya nyayo, miguu, na shingo zao. Hawa binti za Sayuni, mbele ya uongozi wa kazi, wanampinga Bwana, na ku-wapotosha watu Wake kwa hasara ya Ukweli Wake, ya shamba Lake la mizabibu, na jasho la maskini. Lakini sasa Yeye atazipindua meza. Yeye atawapinga. {1TG6: 28.1}
Je, kaya zao kama mwezi zinaweza kuwa nini? – Basi, huenda zikawa visigino vikubwa chini ya nyayo zao, visi-gino ambavyo huzifanya shingo zao ndefu na migongo yao dhaifu, lakini uwezekano mkubwa, kaya zao kama mwezi zinaweza kuwa vitu vya urembo ambavyo huvaliwa vichwani mwao, na ambavyo wao huviita kofia pen-gine tu kwa sababu huvalishwa pale ambapo kofia inapaswa kuwa. {1TG6: 28.2}
Kwa kufuata sana mitindo ya dunia ni sahihi kabisa kwa wasioamini, lakini hakika ni makosa kwa wote wale ambao taaluma yao ya kidini inahukumu mazoea yao. {1TG6: 28.3}
Orodha hii ya mapambo huingiza ndani kila kitu kinachodhaniwa, kila kitu kisichofaa ambacho mtu anaweza kuvaa kwa ajili ya kujionyesha. Kwa nini sio sasa, Ndugu, Dada, mvue kutoka milini mwenu vitu visivyofaa ambavyo vinashusha heshima ya taaluma yenu, na ambavyo huufanya ujumbe wa Mungu usiweze kuwa na ma-tokeo yoyote? Kwa nini sasa usivae nadhifu, safi, kwa adabu, kwa kiasi — kwa
28
kupatana na taaluma yako? Kwa nini usubiri hadi Bwana akupige kwa laana fulani ambayo huwezi kupona kamwe? Kwa nini usiyatekeleze maslahi ya uhai wako na Mungu, Yule Ambaye ni Rafiki wako wa pekee wa kweli, Mwokozi wako wa pekee, Yeye pekee ambaye anajua matatizo yako yote, Yule wa pekee ambaye ana-weza kuzifuta dhambi zako? {1TG6: 28.4}
Mbona usichukue ushauri wa Mungu mwenye hekima yote? Kwa nini uruhusu unafiki ukushushe hadi kwa ki-wango cha waovu, wasio na adabu, na wasio na heshima, — unafiki unaoongoza kwenye bonde la kusitasita kuamua, la kutokuwa na uhakika, la msiba, la aibu? Kwa nini wewe kwa jina la Bwana ufume utando wa shetani kwa miguu isiotambua inaswe ndani? Kwa nini wewe umutumikie Adui yako wakati ambapo unakiri kwamba unamwakilisha Kristo? {1TG6: 29.1}
Je, unadhani kwamba tunaweza kuwaongoa washenzi hadi kwa kiwango cha juu cha Kristo na namna ya kuishi iliyoinuliwa tusipovaa bora zaidi kuliko wao, hasa wanapojua kwamba mavazi yetu hayapatani na kukiri kwetu wenyewe? Hadi sasa, inaonekana kama washenzi wanalifanya kanisa kuwa la kishenzi, badala ya kanisa ku-wafanya kuwa Wakristo. {1TG6: 29.2}
Iwapo Mungu alitaka uwe tofauti na jinsi ulivyo, Yeye angaliweza kukuumba tofauti. Ikiwa Angalikutaka uwe kama ndege bata mzinga, angaliweza kwa urahisi kukupa kito cha pua, pete za masikio, na bizimu. Iwapo Anga-likutaka uwe kama tausi, Angalikupa mkia wa tausi na taji ya tausi. Ikiwa Angalikutaka uwe na shingo ili-yonyooshwa, Angalikupa shingo la twiga. Ikiwa Angalikutaka kuliza njuga unapotembea, angalikupa mkia wa nyokakayamba. Angaliweza kukuumba njia yoyote ambayo Angetaka. Lakini hufurahi kwamba Yeye ameku-umba tu jinsi ulivyo? {1TG6: 29.3}
29
Sio miaka mingi iliyopita ikiwa mmoja wa binti za Sayuni angalionekana mitaani amejivika aina ya nguo wanazovaa leo angaliweza kuharakishwa kuingia jela. Lakini iwapo mmoja wao aweze kuonekana katika mavazi ya siku hiyo kwa mitaa ya leo, hakuna yeyote anayeweza kujushughulisha naye. Je, hilo linamaanisha nini kwako? Je, halimaanishi kwamba mavazi ya leo sio ya adabu? kwamba mitindo ya dunia inazidi kuwa mibaya zaidi? {1TG6: 30.1}
Je, ninyi Wanadaudi, pia, mnaenda kuanguka kwa njia ya binti wenye kiburi wa Sayuni? Je, mmekuja humu du-niani ili kuvutia macho ya wazembe wa mitaani? au ninyi mpo hapa kufanya mema kwa ulimwengu, na kumpendeza Bwana? Je, Ni yupi kati yenu ndugu anataka mke wake au binti yake kwenye maonyesho ili kuya-furahisha macho ya kutamani ambayo hujaza mitaa? {1TG6: 30.2}
Kwa nini Mungu atawavua binti za Sayuni kwa sababu ya ubatili wao? — Hebu tumsikie Akijibu: “…kwa sababu binti za Sayuni wana kiburi, na kuenenda na shingo zilizonyoshwa, na macho ya kutamani, wakienenda kwa hatua za madaha, na kuliza njuga kwa miguu yao.” {1TG6: 30.3}
Njia ya mitindo ya kuvaa huwafanya kuwa wenye kiburi, wenye majivuno; huwafanya wazinyooshe shingo zao, na kuwafanya watembee na kuliza njuga kwa miguu yao; huwafanya watende chochote ili wavutie — naam, kila kitu ambacho watatumia kuwafanya waonekane wasiokuwa nadhifu, wanafiki, na wa tabia za kutiliwa shaka. Je, ni ajabu kwamba upo uovu mwingi sana kanisani? Mmoja lazima kama ingalikuwa ajihami kwa bunduki ili kumlinda mkewe mitaani. Inawezaje kuwa vinginevyo wakati namna ya wanawake ya kuvaa yenyewe inaalika shida? {1TG6: 30.4}
Zaidi ya hayo, iwapo ninyi dada hamwezi kuvaa kwa uwiano wa mapenzi ya Bwana, kulingana na Ukweli Wake uliostawi, hata ulimwengu, ikiwa unajua chochote kuhusu
30
kukiri kwenu, hautafikiria sana juu yenu. Wanawatafuta wanafiki hata hivyo, na iwapo ninyi sio waaminifu kwa dini yenu, machoni mwao mtaonekana kuwa wanafiki bora zaidi. {1TG6: 30.5}
Aya ya 24 — “Hata itakuwa ya kuwa badala ya manukato mazuri kutakuwa uvundo, na badala ya mishipi, kamba; na badala ya nywele zilizosukwa vizuri, upaa; na badala ya kisibau, mavazi ya kigunia; na kutiwa alama mwilini kwa moto badala ya uzuri.”
Vaa ifaavyo na utaona sio tu kwamba watu waovu hawatakufuata, ila wala laana za Bwana hazitakuangukia. {1TG6: 31.1}
Aya ya 25 — “Watu wako waume wataanguka kwa upanga, na mashujaa wako vitani.”
Iwapo binti za Sayuni watashindwa kufanya matengenezo, basi waume zao wataanguka kwa upanga. Je, Una-taka nikuambie kwa nini waume zao wataanguka kwa upanga? — Kwa sababu hakuna mvulana Mkristo wa kweli katika hisia zake sahihi, kamwe ataweza hata kufikiria kumwoa msichana anayevaa nguo kama ambavyo mnafiki huvaa. Na hivyo ikiwa msichana wa nia ya kidunia kama huyu ataweza kuolewa, atapata aina gani ya mwanamme? — Sio Mkristo aliye na ufahamu katika Ukweli wa sasa, ninao uhakika. Atapata aina ya mwa-namme ambaye hana ulinzi wa Mungu juu yake, aina ambayo itaanguka katika vita, vita ambavyo vitapiganwa wakati ambapo watu wa Mungu wanaokolewa. (Soma tena Trakti Namba 14.) Iwapo mnataka kuwaokoa waume zenu, basi acheni kujipumbaza na Ibilisi. Mpate kuwa wawakilishi wa kweli wa Mungu. {1TG6: 31.2}
Ungefikiriaje kama malaika wangalishuka chini mitaani wakiwa wamejivika kama hawa binti za Sayuni? Je, ungefikiri walikuwa malaika, au ungefikiri walikuwa ni mashetani? Je, ungefikiri kwamba Mbinguni ni
31
mahali pazuri pa kuishi? Kwa kweli, sasa, ungeweza kufikiria nini? Je, ungaliwapa heshima wanayostahili? La, ninao uhakika haungaliweza. Kwa nini usivae kama vile malaika wangaliweza kuvaa ikiwa wangalikuwa mahali pako? Iwapo malaika wanaweza sasa kuonekana, hawataweza kuaibika kutazamwa, lakini wengi mwanamke wangeweza kuaibika kuonekana karibu na malaika. Ukweli ni Ukweli, na hisia ni hisia; hebu tuwe navyo vyote viwili. {1TG6: 31.3}
Aya ya 26 — “Na malango yake yatalia na kuomboleza, naye atakuwa ukiwa, atakaa chini.”
Kitu hasa kinachompepeta nje yule ambaye hajaongoka, kwa sababu kiwango cha kukiri kwake kinatupwa kwa pepo, malango ya maeneo yake ya mikusanyiko, italalama na kuomboleza. Mkiwa atakaa chini, sio juu ya kiti cha enzi. Kwa nini hupata hasara kama hiyo? {1TG6: 32.1}
Bila shaka watu watakutazama, lakini hawatakuangalia kama mtenda maovu, au kama mtu asiyefaa au wa mzaha, ila badala yake kama Mkristo wa kuheshimiwa. Ikiwa watakuchukia, itakuwa kwa sababu tabia yako inawafanya waaibike. Na, zaidi ya hayo, utawezaje kuwaongoa waingie katika dini yako ambayo wanapaswa kuwa nayo ili waokolewe, isipokuwa uiwakilishe kwa usahihi? {1TG6: 32.2}
Wakati ninapoenda nje na mke wangu, watu ambao hawajawahi kuniona awali, ambao hawajui naweza kuwa nani, lakini kwa kusitasita kidogo huniita “Wa kuheshimiwa” kwa sababu wanamchukulia kuwa mke wa mhubiri. Hilo huonyesha kile watu wa ulimwengu hufikiri wakati wanapowaona wanawake waliovaa ifaavyo. Ni bora kuwa nao wafikiri kwamba wewe ni mke wa mhubiri au binti yake, kuliko kuwa nao wakikisia unaweza kuwa ni nani. {1TG6: 32.3}
Kwa nini usitii kilio cha kuamsha cha Bwana? Usiahirishe kutii mwito huu wa dharua hadi kesho, Ndugu,
32
Dada. Iwapo unashindwa leo, kesho haitakuja kamwe. Hii ndio fursa yako. {1TG6: 32.4}
Kama ilivyoelewa awali, kama vile Isaya sura ya 3 ni endelezo la sura ya 2, sura ya 4 ni endelezo la sura ya 3. Tutaendelea kwa hivyo somo hili katika sura ya 4. {1TG6: 33.1}
Isa. 4: 1 — “Na siku hiyo wanawake saba watamshika mtu mume mmoja wakisema, Tutakula chakula chetu, na kuvaa nguo zetu wenyewe, lakini tuitwe tu kwa jina lako; utuondolee aibu yetu.”
Yaani, katika siku za mwisho, wakati binti za Sayuni ni wenye majivuno, basi wanawake saba (makanisa yote ya siku hiyo) mioyoni yatasema kwa Kristo, yule Mtu mme mmoja, “Tutakula chakula chetu, na kuvaa nguo zetu wenyewe, Tutakuwa huru kabisa kwako Wewe. Kipo kitu kimoja tu tunachotaka kutoka kwako: Tuitwe tukwa Jina Lako, Mkristo, ili utuondolee aibu yetu.” Hivi ndivyo Mungu anavyoliona kanisa Lake likiwa limefanywa mtumwa wa ulimwengu. {1TG6: 33.2}
Sasa, hadi hapa, nataka kuwasomea shairi. Linaelezea kikamilifu jinsi anguko lilivyokuja. {1TG6: 33.3}
KANISA LINATEMBEA NA ULIMWENGU
Kanisa na Dunia walitembea mbali mbali
Kwenye pwani za mabadiliko ya wakati,
Dunia alikuwa ikiimba wimbo wa kizunguzungu,
Na Kanisa wimbo wa utukufu.
“Njoo, nipe mkono wako,” alisema Dunia ya kufurahisha,
“Na utembee nami kwa njia hii!”
Lakini Kanisa nzuri alificha mikono yake ya theluji
Na kwa makini akajibu “Hapana,
Sitakupa mkono wangu kabisa,
Nami sitatembea pamoja nawe;
33
Njia yako ni njia inayoongoza kwenye kifo;
Maneno yako yote si ya kweli. “
“Bali, tembea nami lakini muda mchache,”
Alisema Dunia kwa pumzi ya upole;
“Njia ninayotembea juu yake ni barabara njema,
Na jua huangaza daima huko;
Njia yako ni ya miiba ya kukwaruza na isiyopitika,
Lakini yangu ni pana na wazi;
Njia yangu ina lami na maua na umande,
Na yako ina machozi na maumivu;
Anga kwangu daima ni samawati,
Hutahitaji kitu, hakuna kazi ninayoijua;
Anga juu yako daima ni giza,
Fungu lako ni fungu la ole nyingi;
Ipo nafasi ya kutosha kwa ajili yako nami
Kusafiri sambamba.”
Nusu kwa haya Kanisa alimwendea Dunia,
Akampa mkono wa theluji;
Na Dunia wa zamani aliufumbata na kutembea pamoja,
Akisema, kwa lafudhi za chini,
“Mavazi yako ni rahisi sana hayaridhishi ladha yangu;
Mimi nitakupa lulu uvae,
Bahameli ghali na hariri kwa umbo lako zuri,
Na almasi kupamba nywele zako.”
Kanisa liliangalia chini kwa mavazi yake meupe,
Na kisha kwa Dunia yenye kumetameta,
Na kuwaziawazia alipouona mdomo wake mzuri
Kwa tabasamu ya dharau ameukunja.
Nitayabadilisha mavazi yangu kwa moja la gharama kubwa,”
Alisema Kanisa, kwa tabasamu ya neema;
Kisha mavazi yake meupe yakapeperuka mbali,
Na Dunia ikapeana, mahali pake,
Atlasi nzuri na hariri zinazong’aa,
34
Waridi na vito na lulu za gharama kubwa;
Ambapo juu ya kipaji la uso wake nywele zake safi zilianguka
zilipambwa kwa kusukwa songa elfu.
“Nyumba yako ni wazi sana,” alisema Dunia ya majivuno ya zamani,
“Mimi nitakujengea moja kama yangu,
Yenye kuta za gololi na minara ya dhahabu,
Na samani nzuri sana daima.”
Basi akamjengea nyumba nzuri ya gharama ya juu;
Ya kifalme ilikuwa ya kuona;
Wanawe na binti zake warembo walikaa humo
Waking’aa kwa rangi ya zambarau na dhahabu:
Maonyesho ya ukwasi na tamasha kwenye kumbi yalifanyika,
Na Dunia na watoto wake walikuwa hapo.
Vicheko na muziki na karamu zilisikika
Katika mahali ambapo palikusudiwa kuwa pa sala.
Kulikuwa na viti vya magodoro kwa matajiri na mashoga,
Wakae katika mbwembwe zao na majivuno;
Lakini maskini waliokuwa wamevikwa mavazi chakavu,
Waliketi chini kwa unyenyekevu nje.
“Unawapa maskini sana,” alisema Dunia.
“Zaidi ya unapvyopaswa kufanya;
Ikiwa wanahitaji makazi na chakula,
Kwa nini hayo yakutaabishe?
Nenda, chukua pesa zako na ununue mavazi ya gharama kubwa,
Nunua farasi na magari mazuri;
Nunua lulu na vito na vyakula vitamu,
Nunua divai adimu sana na ya gharama kubwa zaidi;
Watoto wangu, wanavipenda vitu hivi vyote,
Na kama wewe upendo wao ungeweza kushinda
Lazima ufanye kama wanavyofanya, na utembee katika njia
Ambazo wanatembea ndani.”
Hivyo maskini waligeuzwa kutoka kwa mlango wake kwa dharau,
Naye hakusikia kilio cha yatima,
Lakini akayavuta mavazi yake mazuri kando,
35
Wajane walipokuwa wakienda wakilia.
Kisha wana wa Dunia na Wana wa Kanisa
Walitembea kwa ukaribu mkono na moyo,
Na Mwalimu tu, ajuaye yote,
Angeweza kuwaambia wawili watengane.
Kisha Kanisa akaketi kwa ushwari wake, na akasema,
“Mimi ni tajiri na bidhaa zangu zimeongezeka;
Sina haja ya chochote, au ninachopaswa kufanya,
Ila kucheka, na kucheza, na kusherehekea. “
Dunia ya ujanja ilisikia, na akacheka kindanindani,
Na kwa dhihaka akasema, pembeni–
“Kanisa limeanguka, Kanisa nzuri;
Na aibu yake ni majivuno yake na kiburi chake.
Malaika alikikaribia kiti cha rehema,
Na akanong’oneza kwa maombolezo jina lake;
Kisha mpasuko wa sauti kubwa za nyimbo ukatulia,
Na vichwa vilifunikwa kwa aibu;
Na sauti ikasikia mwishowe pembeni mwa Kanisa
Kutoka kwake Yeye aliyeketi juu ya kiti cha enzi,
“Nayajua matendo yako, na jinsi ulivyosema,
‘Mimi ni tajiri,’ na hujui
Kuwa u uchi, na maskini na kipofu,
Na mnyonge mbele ya uso Wangu;
Kwa hivyo kutoka kwa uwepo Wangu nakutupa nje,
Na kulifuta jina lako kutoka mahali pake.”
–Matilda C. Edwards.
Simjui mwandishi wa shairi hili, lakini linaonekana kuwa lililovuviwa kama yale ambayo nimewasomea kutoka kwa Biblia. Shairi hili linaelezea hadithi sawa na Biblia inavyofanya. Wale wanaopenda kuvaa na kuonekana kama ulimwengu, hufanya hivyo tu kwa sababu mkono wao ni, kama ingalivyokuwa katika mkono wa dunia, na kwa sababu dunia hukataa kutembea pamoja nao isipokuwa wavae jinsi dunia inavyovaa. Kwa kushangaza — dunia iko sawa kwa kujidai kwake,
36
lakini binti za Sayuni sio wakweli kwa kukiri kwao! {1TG6: 36.1}
Dunia iliendelea kubembeleza. Kanisa mwanzoni liliendelea kujiepusha nayo. Lakini ulimwengu uliendelea ku-bembeleza na kurai mpaka hatimaye ukashinda. Wale wanaonaswa kwa sehemu moja ya inchi, siku kwa siku, ni, kwa hivyo, wale hasa ambao kwa mvuto wao Shetani anatumia kusabisha kanisa kuanguka. Amka Ndugu! Amka Dada! Shetani asije akatufanya sote kuwa wapumbavu wa milele wote. {1TG6: 37.1}
Mungu hatuulizi tujivike kitu chochote ambacho kitaunguza miili yetu. Ila Yeye anatuuliza tuvae kitu cha heshima ambacho kitamwakilisha Yeye na ujumbe Wake wa sa ya sasa. Tusipofanya hivi, ulimwengu hautaamini kwamba Yeye ametupeleka, na sisi wenyewe tutaanza kuwa na shaka. Mtindo wetu wa mavazi hunena kwa sauti zaidi kuliko maneno. {1TG6: 37.2}
Ibilisi, bila shaka, anafanya kazi pande zote — yeye mwenyewe hajali ni ipi, lakini yeye ni mwangalifu wa kum-hifadhi mdhambi ili kumvuta kwa upande wake. Ikiwa moja kupita kiasi haiwezi kufanya, Adui anamruhusu apate kitu kingine — chochote cha kumzuia asitembelee katikati ya barabara, chochote cha kumzuia kumfuata Bwana. {1TG6: 37.3}
Aya ya 2 — “Siku hiyo chipukizi la Bwana litakuwa zuri, lenye utukufu, na matunda ya nchi yatakuwa mema sana, na kupendeza, kwa ajili ya Waisraeli wale waliookoka.”
Katika siku hiyo, — katika siku ambayo binti za Sayuni watakuwa na majivuno, katika siku wanawake saba wa-tamshika yule mtu mme mmoja, wakati huo chipukizi la Bwana litakuwa zuri na la utukufu, na matunda ya nchi yatakuwa mema sana na kupendeza kwa ajili ya Waisraeli waliookoka. Watu Wake wataokoka kutoka kwa nini? Hapa lipo jibu: {1TG6: 37.4}
37
Isa. 3: 1-3 — “Kwa maana, tazama, Bwana, Bwana wa majeshi, awaondolea Yerusalemu na Yuda egemeo na tegemeo; tegemeo lote la chakula na tegemeo lote la maji; mtu hodari na mtu wa vita; mwamuzi na nabii; mpiga ramli na mzee; jemadari aliye juu ya watu hamsini, na mtu mstahifu, na mshauri, na fundi aliye mstadi, na mganga ajuaye uganga sana.”
Ni dhahiri kwamba wanaokoka maangamizi ya wadhambi ndani ya kanisa. {1TG6: 38.1}
Isa. 4: 3 — “Tena itakuwa ya kwamba yeye aliyebaki katika Sayuni, na yeye aliyeachwa ndani ya Yerusal-emu, ataitwa mtakatifu; yaani, kila mmoja aliyeandikwa miongoni mwa hao walio hai ndani ya Yerusale-mu.”
Watakatifu tu pekee yao, wale ambao majina yao yameachwa yameandikwa katika Kitabu wanaokoka maangamizi yanayoanguka juu ya waovu ndani ya kanisa. Wao tu ndio wanaojumuisha “masalia,” wale ambao wameachwa. Hili litakuwa lini? — Bwana Mwenyewe analo jibu: {1TG6: 38.2}
Aya ya 4-6 — “Hapo Bwana atakapokuwa ameuosha uchafu wa hao binti za Sayuni na kuisafisha damu ya Yerusalemu kati yake, kwa roho ya hukumu na kwa roho ya kuteketeza. Tena juu ya makao yote ya mlima Sayuni, na juu ya makusanyiko yake, Bwana ataumba wingu na moshi wakati wa mchana, na mwangaza wa miali ya moto wakati wa usiku; kwa maana juu ya utukufu wote itatandazwa sitara. Kisha kutakuwa na hema kuwa uvuli wakati wa mchana kwa sababu ya hari, na kuwa mahali pa kukimbilia na kujificha wakati wa tufani na mvua.”
Litakuwa wakati ambapo utakaso wa kanisa utafanyika, wakati wa Hukumu ya Walio Hai ndani ya nyumba
38
ya Mungu (1 Pet. 4:17), wakati wa mtengo wa ngano kutoka kwa magugu, katika wakati wa mavuno, wakati ambapo samaki wazuri wanatengwa kutoka kati ya wabaya, mbuzi kutoka kati ya kondoo (Mat. 25:32) ). {1TG6: 38.3}
Katika wakati huu wa taabu, wakati kila kitu kinafanya kazi ili kuleta wakati wa taabu mfano wake haukuwapo (Dan. 12: 1) Mungu atalitakasa kanisa Lake ili kuwalinda watu Wake kutokana na taabu ambayo linaenda kuku-tana nayo. Watu waliosalia baada ya wadhambi kutwaliwa, “masalia,” watakuwa na amani kamilifu. {1TG6: 39.1}
Bwana sasa anawaita wanaume na wanawake “Roho ya Bwana MUNGU i juu yangu; kwa sababu Bwana amenitia mafuta niwahubiri wanyenyekevu habari njema; amenituma ili kuwaganga waliovunjika moyo, ku-watangazia mateka uhuru wao, na hao waliofungwa habari za kufunguliwa kwao. Kutangaza mwaka wa Bwana uliokubaliwa, na siku ya kisasi cha Mungu wetu; kuwafariji wote waliao; kuwaagizia hao waliao katika Sayuni, wapewe taji ya maua badala ya majivu, mafuta ya furaha badala ya maombolezo, vazi la sifa badala ya roho nzito; wapate kuitwa miti ya haki, iliyopandwa na Bwana, ili atukuzwe. Nao watajenga mahali pa kale pali-poharibiwa, watapainua mahali palipokuwa ukiwa zamani, watatengeneza miji iliyoharibiwa, mahali palipoachwa kizazi baada ya kizazi. {1TG6: 39.2}
“Na wageni watasimama na kulisha makundi yenu, na watu wa kabila nyingine watakuwa wakulima wenu, na watunzaji wa mizabibu yenu. Bali ninyi mtaitwa makuhani wa Bwana; watu watawaiteni wahudumu wa Mungu wetu; mtakula utajiri wa mataifa, na kujisifia utukufu wao. Badala ya aibu yenu mtapata maradufu, na badala ya fedheha wataifurahia sehemu yao; basi katika nchi yao watamiliki maradufu; furaha yao itakuwa ya milele. Maana mimi, Bwana, naipenda hukumu ya haki, nauchukia wivi na uovu; nami nitawalipa
39
malipo katika kweli, nitaagana nao agano la milele. Na kizazi chao kitajulikana katika mataifa, na uzao wao kati-ka kabila za watu; wote wawaonao watakiri ya kuwa wao ni kizazi kilichobarikiwa na Bwana. {1TG6: 39.3}
“Nitafurahi sana katika Bwana, nafsi yangu itashangilia katika Mungu wangu; maana amenivika mavazi ya wokovu, amenifunika vazi la haki, kama bwana arusi ajipambavyo kwa kilemba cha maua, na kama bibi arusi ajipambavyo kwa vyombo vya dhahabu. Maana kama nchi itoavyo machipuko yake, na kama bustani ioteshavyo vitu vilivyopandwa ndani yake; ndivyo Bwana MUNGU atakavyootesha haki na sifa mbele ya mataifa yote. {1TG6: 40.1}
“Kwa ajili ya Sayuni sitanyamaza, na kwa ajili ya Yerusalemu sitatulia, hata haki yake itakapotokea kama mwangaza, na wokovu wake kama taa iwakayo. Na mataifa wataiona haki yako, na wafalme wote watauona utukufu wako; nawe utaitwa jina jipya, litakalotajwa na kinywa cha Bwana. Nawe utakuwa taji ya uzuri katika mkono wa Bwana, na kilemba cha kifalme mkononi mwa Mungu wako. Hutaitwa tena Aliyeachwa, wala nchi yako haitaitwa tena, Ukiwa; bali utaitwa Hefsiba; na nchi yako Beula;kwa kuwa Bwana anakufurahia ,na nchi yako itaolewa. Maana kama vile kijana amwoavyo mwanamwali, ndivyo wana wako watakavyokuoa wewe; na kama vile bwana arusi amfurahiavyo bibi arusi, ndivyo Mungu wako atakavyokufurahia wewe. Nimeweka wal-inzi juu ya kuta zako, Ee Yerusalemu; hawatanyamaza mchana wala usiku; ninyi wenye kumkumbusha Bwana, msiwe na kimya; wala msimwache akae kimya, mpaka atakapoufanya imara Yerusalemu, na kuufanya kuwa sifa
40
duniani. Bwana ameapa kwa mkono wake wa kuume, na kwa mkono wa nguvu zake, Hakika sitawapa adui za-ko nafaka yako tena kuwa chakula chao; wala wageni hawatakunywa divai yako, uliyoifanyia kazi. Lakini wali-oivuna, ndio watakaoila, na kumhimidi Bwana; na walioichuma, ndio watakaoinywa, ndani ya nyua za patakati-fu pangu. Piteni, piteni, katika malango; Itengenezeni njia ya watu; Tutieni, tutieni barabara; toeni mawe yake; Twekeni bendera kwa ajili ya kabila za watu. Tazama, Bwana ametangaza habari mpaka mwisho wa dunia, Mwambieni binti Sayuni, Tazama, wokovu wako unakuja; Tazama, thawabu yake i pamoja naye, Na malipo yake yako mbele zake. Nao watawaita, Watu watakatifu, Waliokombolewa na Bwana; Nawe utaitwa, Ali-yetafutwa, Mji usioachwa.” Isa. 61: 1-11; 62: 1-12. {1TG6: 40.2}
Kwa nini usimrudie Mungu? Haijalishi wewe ni mdhambi mbaya kiasi gani Yeyekwa furaha atakusamehe. Mbona usiupokee sasa mwito Wake? Huwezi kumudu kupoteza milele, kwa hakika hutaki kuupoteza utukufu huu ujao ambao unaonyeshwa na manabii, na ambao sasa umeletwa upya kwa nuru. “Msiipende dunia, wala mambo yaliyomo katika dunia. Mtu akiipenda dunia, kumpenda Baba hakumo ndani yake. Maana kila kilichomo duniani, yaani, tamaa ya mwili, na tamaa ya macho, na kiburi cha uzima, havitokani na Baba, bali vyatokana na dunia. Na dunia inapita, pamoja na tamaa zake, bali yeye afanyaye mapenzi ya Mungu adumu hata milele.” 1 Yoh. 2: 15-17. “Kwa hiyo (kama anenavyo Roho Mtakatifu, Leo, kama mtaisikia sauti yake, Msifanye migumu mioyo yenu, Kama wakati wa kukasirisha, Siku ya kujaribiwa katika jangwa:)” Ebr. 3: 7, 8. {1TG6: 41.1}
Hii ndio fursa yako. Leo unaweza kuichukua au unaweza kupita mbali nayo, lakini kesho aidha utaruka kwa
41
kwa furaha, au kusaga meno yako katika giza la nje. Sasa yote yanakutegemea wewe. {1TG6: 41.2}
Hakika hutaweza kuuza kwa bei nafuu zaidi ya kuuacha utukufu huu kuliko wote na rai ya Mungu ya kuutoa moyo kuiacha dunia na kurudi kwa moyo wote kwake Yeye sasa katika wito Wake wa mwisho. {1TG6: 42.1}
Je, ulimwengu unaweza kumwona Yesu ndani yako?
Je, Tunaishi karibu na Bwana leo,
Tukipita huku na huko kwa njia ya shughuli za maisha,
Kwamba ulimwengu ndani yetu unaweza kuona mfano
Kwa Mtu wa Kalvari?
Je, Tunapenda, na upendo kwa ujamaa wake Mwenyewe,
Viumbe Vyake vyote waliopotea katika matope ya dhambi?
Tutaweza kufikia mkono, kwa gharama yoyote,
Kumkomboa mdhambi aliyepotea?
Kama kitabu kilicho wazi maisha yetu watasoma,
Kwa maneno na matendo yetu kutoa kila siku tahadhari;
Je, watavutiwa, au kugeuzwa mbali
Kutoka kwa mtu wa Kalvari?
Je, ulimwengu unaweza kumwona Yesu ndani yangu?
Je, ulimwengu unaweza kumwona Yesu ndani yako?
Je! Upendo wako Kwake ni mlio wa kweli,
Na maisha yako na huduma yako pia?
Je, ulimwengu unaweza kumwona Yesu ndani yako?
–Bi. C. H. Morris
42
[Ukurasa mtupu]
43
Jumuiya ya Wadaudi Waadventista wa Sabato
(Ushirika Huru Unaojumuisha Kanisa)
Mlima Karmeli, Waco, Texas
S.L.P. 23738, Waco, TX 76702
+ 1-254-855-9539
www.gadsda.com
info@gadsda.com
Gombo la 1, Namba 5, 6
Kimechapishwa nchini Marekani
44