fbpx

Gombo la 1 Salamu Mwafaka Namba 01, 02

Gombo la 1 Salamu Mwafaka Namba 1, 2

                                    

AMANI YA PEKEE YA MAWAZO

Hati miliki, Kimechapishwa tena 1953

Haki zote zimehifadhiwa

V. T. HOUTEFF

                                    

NJIA YA KURUDI EDENI

NJIA MBILI TU

                                    

1

WAZO LA SALA YA UFUNGUZI

Nitasoma kutoka Mlima wa Baraka, ukurasa wa 147, aya ya 1 hadi 3. Aya hizi zinazingatia maandiko, “Uta-futeni kwanza Ufalme wa Mungu.” {1TG1: 2.1}

M.B. uk. 147 — “Watu walioyasikiliza maneno ya Kristo, walikuwa bado kwa shauku wakitazamia tangazo fula-ni la ufalme wa kidunia. Wakati Yesu alikuwa akiwafungulia hazina za mbinguni, swali la upeo katika mawazo ya wengi lilikuwa, Utawezaje uhusiano Naye kuendeleza matumaini yetu duniani? Yesu anaonyesha kwamba kwa kuyafanya mambo ya dunia kuwa shauku yao kuu, walikuwa kama mataifa ya kipagani yaliyowazunguka, wakiishi kana kwamba hakuna Mungu, ambaye utunzaji wake mwororo uko juu ya viumbe Vyake. {1TG1: 2.2}

“… ‘Baba yenu wa mbinguni anajua ya kuwa mnahitaji hayo yote. Bali utafuteni kwanza ufalme wa Mungu na haki Yake, na hayo yote mtazidishiwa.”… Fungueni mioyo yenu muupokee ufalme huu, na kuifanya huduma yake kuwa maslahi yenu ya juu. Ingawa ni ufalme wa kiroho, usiogope kwamba mahitaji yeko ya maisha haya hayatashughulikiwa. Ikiwa unajitoa kwa utumishi wa Mungu, Yeye aliye na mamlaka yote mbinguni na duniani ataweka tayari mahitaji yako. {1TG1: 2.3}

“Yesu hatuweki huru kutoka kwa hitaji la juhudi, ila Yeye hufundisha kwamba tumfanye Yeye kuwa kwanza na wa mwisho na bora katika kila kitu. Hatupaswi kushiriki katika shughuli, kutofuata miradi, wala anasa, ambazo zinaweza kuzuia kutimizwa kwa haki Yake katika tabia na maisha yetu. Chochote tunachofanya, kinapaswa kufanyika kwa moyo, kana kwamba ni kwa Bwana.” {1TG1: 2.4}

Hebu sasa tupige magoti na kusali kwamba tuweze kufanya ustawi wa Ufalme kuwa maslahi yetu ya juu; kwamba tusiyaruhusu masumbufu kuhitilafiana na utumishi wa mioyo yetu yote kwa Bwana; na kuamini kabisa kwamba Bwana ataweka tayari mahitaji yetu yote. Basi tu hatutaogopa siku zijazo. {1TG1: 2.5}

2

NJIA YA KURUDI EDENI

MATINI YA HOTUBA NA V. T. HOUTEFF

MCHUNGAJI WA WADAUDI WAADVENTISTA WA SABATO

SABATO, AGOSTI 3, 1946

HEKALU LA MLIMA KARMELI

WACO, TEXAS

Mwa. 3:17 — “Akamwambia Adamu, Kwa kuwa umeisikiliza sauti ya mke wako, ukala matunda ya mti ambao nalikuagiza, nikisema, Usiyale; ardhi imelaaniwa kwa ajili yako; kwa uchungu utakula mazao yake siku zote za maisha yako.”

Baada ya Adamu kuanguka dhambini, Bwana alimwambia nini? — “Kwa kuwa umeisikiliza sauti ya mke wako, umefanya yale haukustahili kufanya, ukala matunda ya mti ambao nalikuagiza usiyale; kwa sababu hiyo, ardhi imelaaniwa, si dhidi yenu, bali kwa ajili yenu.” {1TG1: 3.1}

Uongo, kwa kuwa ni kinyume cha Ukweli, ungalisema, “Imebarikiwa ardhi kwa ajili yako.” Na badala ya kus-ema, “Kwa uchungu utakula siku zote za maisha yako,” Uongo ungesema, “Kwa anasa utakula siku zote za mai-sha yako.” Kwa maneno mengine, wakati Mungu anatangaza laana, Shetani chini ya hali hiyo anatangaza baraka. Ndivyo ilivyo kwamba ulimwengu, kwa kawaida ukiwa unapenda kusikiliza hotuba ya Shetani, unatarajia kuishi katika anasa siku zake zote. Hata hivyo, unayo machungu tele. Mengi yake. {1TG1: 3.2}

Aya ya 18 — “Michongoma na miiba itakuzalia, nawe utakula mboga za kondeni.”

3

Ibilisi, bila shaka, angalisema, “Waridi na maua itakuletea.” Na badala ya kuamuru, “Utakula mbogaza kondeni,” angalisema “Utakula kila kitu unachopata kondeni.” Kweli, huwa hasemi hivyo katika kitabu, ila hunena ndani ya mioyo ya wote walio hai, na kwa bidii huitii sauti yake. {1TG1: 4.1}

Aya ya 19 — “Kwa jasho la uso wako utakula chakula, hata utakapoirudia ardhi, ambayo katika hiyo ulitwaliwa; kwa maana u mavumbi wewe, nawe mavumbini utarudi.”

Shetani angalisema: “Kwa anasa utakula chakula mpaka, katika mchakato wa nadharia ya mageuzi, utakuwa kama Mungu; maana kutoka kwa atomu ndogo ulitwaliwa, na kwa Mungu mwenye nguvu utatokea iwapo utaendelea na kuendelea. {1TG1: 4.2}

Mungu alisema nini, hata hivyo? — “Kwa jasho la uso wako utakula chakula chako siku zote za maisha yako; yaani, kwa ajili yako mwenyewe sasa utakuwa na shida katika maisha, na unapaswa pia kujipatanisha kwayo.” Ingawa hali hii haikuwa kura ya mtu kabla ya kutenda dhambi, ilikuwa sehemu yake mara tu alipoondolewa kwenye Bustani, mara tu alipopata laana. {1TG1: 4.3}

“Lakini,” unahoji, “kwa nini Mungu alikusudia kwamba sisi sote tuweze kupitia shida na huzuni kabla ku-rejeshwa ndani ya Edeni? Ikiwa Yeye ataturejesha huko, kwa nini Yeye hakufanya hivyo mwanzoni, katika siku za Adamu?” — Jibu kwa maswali haya yote lipatikana katika {1TG1: 4.4}

Luka 15: 11-13 — “Akasema, Mtu mmoja alikuwa na wana wawili; yule mdogo akamwambia babaye, Baba, nipe sehemu ya mali inayoniangukia.

4

Akawagawia vitu vyake. Hata baada ya siku si nyingi, yule mdogo akakusanya vyote, akasafiri kwenda nchi ya mbali; akatapanya mali zake huko kwa maisha ya uasherati.”

Kisa ni kwamba walikuwepo wana wawili katika familia. Mkubwa alichagua kusalia nyumbani, lakini mdogo alichagua kwenda mbali. Na unajua ni nini kilichotokea baadaye: Mwana mdogo alipoteza mali yake yote katika maisha ya anasa. {1TG1: 5.1}

Nina uhakika kwamba baba alijua kabla ya kwamba mwanawe alikuwa akienda katika shida. Alimpenda na ali-tamani kumwepushia kijana aibu, huzuni na majaribio mazito ambayo alikuwa anayaendea. Ukweli hasa kwamba wakati wa kijana kurudi, baba yake alimlaki akiwa bado mbali, na kumfanyia karamu, hata baada ya kupoteza mali ya baba yake na kulifedhehesha jina la familia, ni ushahidi wa kutosha kwamba baba alimpenda kijana sana. Mvulana huyo aliruhusiwa kuondoka nyumbani tu kwa sababu sio chochote ila ujuzi wake mwenyewe un-geweza kuonyesha upumbavu wake, na kuthibitisha upendo wa baba kwa ajili yake. {1TG1: 5.2}

Ni nini kilichomlazimisha mvulana asipende nyumbani? — Ilikuwa ni tamaa yake ya kuishi kwa anasa. Hakuna mvulana au msichana chini ya hali iyo hiyo hukimbia kutoka nyumbani isipokuwa kwa tumaini la kupata uhuru na kutekeleza maisha ya anasa, kufanya watakavyo kile moyo wa kimwili hutamani kufanya. {1TG1: 5.3}

Inaweza kuwepo furaha nyingi ya muda mfupi kwa upotevu ila huishia tu kwa madhila na fedheha. Ikiwa mpotevu angalikuwa anaiishi katika siku zetu, unadhani angeweza kufanya nini kuanza kwenye njia kuu ya bu-rudani, kuwa na wakati mzuri? — Kitu cha kwanza angeweza kufanya kwa hakika kingekuwa kununua, iki-wezekana, gari,

5

nguo nzuri, pete ya almasi, fimbo inayometameta, na kidude cha saa ya mkono. Oo, naam, hangalipuuza kuweka ua kwenye shavu la koti lake na kitambaa cha hariri mfukoni mwake. Inawezekana usikuwepo ubaya wa kuwa na baadhi ya vitu hivi, lakini hakika havistahili pongezi au hata kupendeza kujivika kila kitu kinachoweza kuva-liwa. Ni, kusema machache, upumbavu kujipamba katika mtindo wa tausi. {1TG1: 5.4}

Na angeweza kumchukua nani mvulana aliyepotoka kwa safari? — Wasichana, bila shaka. Na wangeweza kwen-da wapi? — Sio kule wahubiri waendako, na sio kanisani, ama. {1TG1: 6.1}

Aya ya 14 — “Alipokuwa amekwisha tumia vyote, njaa kuu iliingia nchi ile, yeye naye akaanza kuhitaji.”

Ikiwa unatumia yote uliyo nayo na yote unayopata, wewe pia, hivi karibuni au baadaye utakuwa na njaa. Majaaliwa yalileta njaa ili kumleta kijana “kwake binafsi,” kwa hisia zake. Hakika, hakuna mvulana anayekimbil-ia mbali kutoka nyumbani wakati yu mwenyewe; na, kinyume chake, wala harudi nyumbani kwa kuelewa kabla ya kujirudia mwenyewe. Hivyo anajifunza somo lake, lakini kwa gharama gani! Kwa gharama gani! {1TG1: 6.2}

Aya ya 15, 16 — “Akaenda akashikamana na mwenyeji mmoja wa nchi ile; naye alimpeleka shambani kwake kulisha nguruwe. Akawa akitamani kujishibisha kwa maganda waliyokula nguruwe, wala hapana mtu aliyempa kitu.”

Mpotevu alipata kazi ndiyo, lakini haikuweza “kulipia gharama,” bado alikuwa akihitaji. {1TG1: 6.3}

Aya ya 17-19 — “Alipozingatia moyoni mwake, alisema, Ni watumishi wangapi wa baba yangu

6

wanaokula chakula na kusaza, na mimi hapa ninakufa kwa njaa. Nitaondoka, nitakwenda kwa baba yangu na kumwambia, Baba, nimekosa juu ya mbingu na mbele yako; sistahili kuitwa mwana wako tena; nifanye kama mmoja wa watumishi wako.”

Mwishowe aligundua kwamba alikuwa akicheza upumbavu, na hivyo akaanza kuwaza juu ya kurudi nyumbani, akisema, “Fikiria tu ni watumishi wangapi walio katika nyumba ya baba yangu na wote wanakula na kusaza. Kwa nini nife kwa njaa? Lakini, nitasema nini wakati ninapofika huko?” Baada ya kujirudia mwenyewe, alihisi, bila shaka, kwamba lazima aseme jambo lililo sahihi, jambo ambalo litamstahikisha Mbinguni na duniani. {1TG1: 7.1}

Ikiwa mvulana huyo angaliuzingatia ushauri wa baba yake pale mwanzoni, hangaliweza kupata madhila. Ni ya namna gani aibu! Na ni somo la jinsi gani pia, sio tu kwa vijana, bali pia kwa wazima. Naam, wapo maelfu, vija-na na wazee sawa, ambao hujifunza masomo makuu, ila mara nyingi hulipia gharama kubwa tu kwa sababu wao daima wanausikiliza “ulaghai” wa Ibilisi. Kwa nini huchukuliwa kwa urahisi na ushawishi wake? — Kwa sababu tu chambo chake huvutia tabia ya dhambi na ubinafsi wa mwanadamu. {1TG1: 7.2}

Udhalilishaji wa mpotevu unawasubiri vijana wote ambao huwa hawafaidiki kwa shauri la wazee, na wazee wote ambao huwa hawafaidiki kwa shauri la Bwana. Hii ni moja ya sheria za Mungu ambazo hakuna yeyote ambaye amewahi kukwepa. {1TG1: 7.3}

Uzoefu wa mpotevu sasa unajibu maswali, Kwa nini Mungu alimwondoa Adamu kwenye Bustani? Maadamu Mungu atamsamehe siku fulani hata hivyo, kwa nini Yeye hakumsamehe mara baada ya kuanguka kwake na kumrudisha tena Edeni? Kwa nini watu wote hawangalikuwa wameweza kuokolewa hivyo wasipitie shida na mauti

7

kabla ya kurudi Edeni? {1TG1: 7.4}

Ikiwa Mungu angaliruhusu Adamu na Hawa kuishi katika Bustani baada ya kutenda dhambi na kuendelea kuu-fikia “mti wa uzima,” Yeye angalikuwa hapo ameyafanya ya milele maisha yao ya uovu katika hali yao ya dhambi. Lingalikuwa jambo la kutisha jinsi gani — wadhambi kupata kuishi milele na milele! Na kama Yeye an-galiwaepusha na wazao wao wasipitie shida na kifo, hawangalikuja tena kutambua ni vipi yalivyo maisha ya dhambi, la, hapana zaidi ya mpotevu angaliweza kabla ya kupitia uasherati, kufilisika, kazi ngumu na umasikini. {1TG1: 8.1}

“Lakini,” unasema, “Iwapo Bwana asingalikuwa amemleta Adamu na Hawa kwenye Bustani kabla ya kupitia kwanza kifo na ufufuo, kwa nini ilimpasa Yeye kuilaani ardhi na kuwafanya wapate chakula chao kwa jasho la nyuso zao?” Na kwa nini Yeye aliwasababisha wale chakula chao kwa huzuni kwa miaka 6,000? — Kwa sababu wote ambao milele wataingia katika Ufalme, hurudi Edeni, lazima kwanza wajirudie wenyewe alivyofanya mpotevu, kwa maana wote wanapaswa waletwe kutambua kwamba kila kitu mbali na Bustani si kitu zaidi ya maganda. {1TG1: 8.2}

Maadamu kazi ni muhimu na kwa sababu wadhambi kimaumbile huchukia kazi, miiba na michongoma iliumbwa kuwashurutisha wafanye kazi kwa ajili ya riziki. Iwapo tunayaacha magugu yachukizayo ardhini, na kutumia muda wetu kujiburudisha, yatayasonga mazao, na sisi, kama mpotevu, tutakuwa na njaa. Hivyo, hakuna kazi, hakuna kula. Mungu Ambaye anajua kilicho bora kwa ajili yetu amefanya kwamba tupate riziki yetu kwa njia ngumu, tufanye kazi kutwa nzima na ila pumziko kidogo. {1TG1: 8.3}

Wale wanaojirudia wenyewe, kwa wao kazi ni

8

starehe. Wapumbavu tu huchukia kazi. {1TG1: 8.4}

Kabla ya mitambo ya kisasa kubuniwa wakulima hawakuwa wakitaabishwa sana na magonjwa kama ilivyo sasa. Ila kama vile mitambo iliongezeka na kuboreshwa, hivyo wadudu waliongezeka, pia. Na kwa sababu gani? — Bado tuendelee kufanya kazi na hivyo kuwa nje ya upotovu. {1TG1: 9.1}

Nilipokuja Marekani miaka kadhaa iliyopita, naliona kila aina ya mitambo, mitambo ambayo ilifanya kazi kubwa sana kwa muda mfupi. Lakini pamoja na manufaa haya, ni nini kingine nilichokiona? — Naliona michongoma na miiba ikaongezeka mara elfu, na magonjwa ya kila aina yakiangamiza mimea. {1TG1: 9.2}

Katika Nchi ya Kale hatukuwa na mitambo, lakini kamwe hatukuhitajika kupulizia mimea yoyote dawa. Kwa nini? — Kwa sababu kufanya kazi bila mashine watu walikuwa wakishughulika kama ilivyokuwa. Iwapo wangepaswa kupigana na magonjwa pia, na bila chochote cha kutumia kupigana nayo, basi hawangaliweza ku-kuza chochote na wangekuwa na njaa. Hivyo inaonekana kwamba ikiwa mitambo hutuweka huru kwa kazi, Mungu hutuma wadudu ili kuturejesha kwa kazi. {1TG1: 9.3}

Bwana alitoa amri kwamba tunapaswa kwa jasho tupate riziki zetu, ila Yeye alijua kwamba wengi wetu hatungefanya hivyo kama hatungehitaji. Na Yeye pia alijua kwamba iwapo hatungalikuwa na kazi nyingi ya kufanya, tungeweza kuingia katika upotovu, katika maisha ya anasa, na kwa hivyo kamwe kutojirudia wenyewe, wala kamwe kurudi Edeni. Kwa hivyo Yeye alilaani ardhi kwa faida yetu. {1TG1: 9.4}

Zaidi ya hayo, kwa mwanamke anayeketi chini na kufanya ila kidogo tu kuidumisha nyumba yake, Mungu huleta kunguni na mende, panya buku na panya, nzi na siafu, chawa na viroboto, na mbu, pia. Hawa watamweka afanye kazi ndani

9

na nje iwapo chochote hakitaweza. {1TG1: 9.5}

Wasingalikuwa wadudu, mtu angeweza kuwa nini! Mungu, unaona, alivifanya vitu hivi vyote kwa kusudi nzuri lakini licha ya wadudu kuwahimiza wavivu kuinuka na kuanza kwenda, bado wengine wanapendelea kuishi kama nguruwe! Kwa nini usubiri hadi Yeye atume jeshi lake kubwa la wadudu? Kwa nini usiupokee ushauri Wake, kujishughulisha, na kutenda kile unachoweza kuwafanya wengine kuwa na furaha, kuifanya dunia kuwa bora zaidi ilivyo, kuiruhusu ijue kwamba wewe u ndani yake kuitendea wema, usiwe mzigo juu yake? Kisha ma-laika watafurahia kufanya kituo kukuzunguka pande zote, na Bwana Mwenyewe atakuja na kula pamoja nawe. {1TG1: 10.1}

Ikiwa tunaifanya shughuli ya Mungu kuwa yetu, Ufalme Wake nyumbani kwetu, basi vitu vingine vyote am-bavyo tunajitahidi na kusumbukia vitasambazwa kwetu kwa wingi. Hebu, basi, tusiwe Wakristo kwa nje na Wapagani mioyoni, lakini badala yake bila “uongo vinywani mwetu” na “mitende mikononi mwetu.” {1TG1: 10.2}

Kwa nini wanadamu walilazimika kungoja miaka elfu sita kabla ya kurudi Edeni? — Kwa sababu inachukua mu-da huo mrefu kupata idadi kubwa ya kutosha ya wapotevu wenye kutubu, wapotevu ambao wamejirudia wenyewe, ambao wanatambua kwamba ni bora kuwa mlinzi mlangoni nyumbani kwa Baba kuliko kuzamishwa katika kinachoitwa eti kujiburudisha mbali na nyumbani Mwake. Mungu hamrudishi yeyote kati yetu kurudi Edeni katika hali ya mawazo tuliyozaliwa nayo. La, hapana zaidi ya Yeye kumrudisha Adamu Edeni katika hali yake ya kuanguka. Wote sharti wajirudie wenyewe. “… mateso hayatainuka mara ya pili.” Nah. 1: 9. {1TG1: 10.3}

Sasa tunaweza kuona kwa nini ni rahisi kwa ngamia kupita katika jicho la sindano kuliko ilivyo kwa tajiri kuin-gia katika Ufalme. Ni wale wapotevu tu ambao kupitia

10

uzoefu wanatambua kwamba ulimwengu huu sio nyumba ya Baba yao, wale tu ambao huanza kurudi Edeni na aina hiyo ya mawazo na kwa aina hiyo ya kuungama kama ile ya mpotevu watajumuika kuwa Ufalme. {1TG1: 10.4}

Zaidi ya hayo, wana wa Israeli walipoingia katika nchi ya Misri, waliishi maisha mazuri huko Gosheni. Waliishi kama wafalme. Naam, walikuwa na maisha bora zaidi kuliko Wamisri. Mungu alijua, hata hivyo, kwamba iwapo wakati ulipokaribia wa ukombozi wao wangaliendelea kuishi kama wafalme, iwapo kila kitu kingaliendelea ku-wa rahisi kwao kama wakati ilivyokuwa Yusufu akiwa hai, wao kamwe, hawangeazimia kurudi katika nchi ya ahadi. Kwa hiyo ilikuwa kwamba Majaaliwa yalileta hali ya majaribu ili kuwasababisha kulia mchana na usiku kwa ajili ya ukombozi. Kisha walikuwa tayari kwenda. Ili kuhakikisha, hata hivyo, kwamba wote wangetoka Misri, Bwana aliruhusu wasimamizi wa kazi wa Misri kuicharaza migongo yao na kufanya kazi yao kuwa ngumu zaidi wakati Musa alipokuwa katika nchi. Vivyo hivyo, lazima kuupenda ulimwengu kucharazwe kutoka ndani mwetu, pia, iwapo daima tutaanza kurudi nyumbani Edeni. {1TG1: 11.1}

Ikiwa ninyi wavulana na wasichana mnataka kuwa na maisha ya anasa, mnaweza kuyapata. Kwa hakika, yapo zaidi mnayoweza kupata leo kuliko ilivyokuwa katika siku za mpotevu halisi. Lakini kumbuka kwamba iwapo utawahi kurudi nyumbani kwetu Edeni unapaswa kulipa gharama ile aliyolipa. Hakutakuwa na tiketi ya bure kwa yeyote, mzee au mchanga. {1TG1: 11.2}

Mhu. 4: 5 — “Mpumbavu huikunja mikono yake, Naye hula chakula chake mwenyewe.”

Mpumbavu huikunja mikono yake; huidharau kazi. Huula mwili wake mwenyewe: Badala ya kufanya kazi, atakuwa na njaa, na kulisababisha tumbo lake kutumia

11

hifadhi ya mafuta yake, na hivyo anazidi kuwa mwembamba. Ni nani anataka kuwa mpumbavu? {1TSM: 11.3}

Muh. 7: 2 — “Heri kuiendea nyumba ya matanga, Kuliko kuiendea nyumba ya karamu. Kwa maana huo ndio mwisho wa wanadamu wote, naye aliye hai atautia moyoni mwake.”

Nyumba ya karamu huleta mwisho wa watu wote wanaoishi kwa ajili ya kujifurahisha, kwa ajili ya maisha ya anasa. “Aliye hai atautia moyoni mwake.” Wale, basi, ambao hawautii moyoni kwa hakika hawaishi, na wanahitaji kuhuishwa. {1TG1: 12.1}

Aya ya 3 — “Huzuni ni afadhali kuliko kicheko, Maana simanzi ya uso ni faida ya moyo.”

Iwapo utajiingiza katika “burudani,” basi moyo wako siku fulani utafadhaika, lakini ikiwa moyo wako huzuni, uta-fanywa kuwa na furaha. Mpumbavu tu huchagua kuwa katika nyumba ya kicheko. Lakini mimi, badala yake niwe katika nyumba ya maombolezo, “kupata mateso pamoja na watu wa Mungu kuliko kujifurahisha katika dhambi kwa kitambo.” Ebr. 11:25. {1TG1: 12.2}

Walikuwepo watu wawili ambao walifanya ushirikiano baada ya Bwana kuwauliza wahamie nchi ya mbali na nchini kwao. Huko wakawa matajiri. Kwa kweli, walikuwa matajiri kiasi kwamba walipaswa kujigawanywa katika makundi mawili. {1TG1: 12.3}

Yule aliyechagua kuishi milimani, ambaye alichagua kujipatia riziki yake kwa ugumu, alithibitisha kuwa mwenye hekima. Ila yule aliyechagua kuishi kwenye uwanda, ambako angeweza kujipatia riziki kwa urahisi, alithibitisha kuwa mpumbavu zaidi. Wa mwisho alikuwa mdogo, pia, unajua. Alijenga hema yake kuelekea Sodoma, na kwa kadri alivyoendelea kuutazama mji huo, ndivyo alivyoukaribia zaidi. Hatimaye aliamua kuhamisha hema yake hadi ndani

12

Yake ambapo angeweza kuona yote kwa ushwari. {1TG1: 12.4}

Alipopata kuwa mtu mkuu, labda meya wa mji kama wanavyofikiri watu wengine, na kwamba hivyo ilikuwa huko alikoketi kwenye lango la Sodoma. Uwezekano mkubwa, hata hivyo, aliketi hapo akiwasubiri wageni ku-wakaribisha nyumbani. Kweli, familia ya Lutu ilikuwa na maisha ya kusisimua, ya anasa miongoni mwa watu wa Sodoma, lakini burudani halikudumu milele, na Lutu kwa usiku mmoja alipoteza kila kitu alichokuwa amemiliki; alitoka humo masikini zaidi ya maskini. Lutu, unaona alilipia zaidi kwa ajili ya kujifurahisha kwake, na iwapo unataka kulipa gharama kama hiyo kwa anasa zako, unaweza kufanya alivyofanya. {1TG1: 13.1}

Mtu ambaye kutoka kwa maandishi yake ambayo tunasoma sasa alikuwa na bado ni, unajua, mtu mwenye heki-ma zaidi ulimwengu haujawahi kuwa naye. Sasa, alisema mpumbavu hufanya nini? — Mpumbavu huingia katika nyumba ya kicheko. Je! Unataka kufaidika na uzoefu wa wengine? Je! Unataka kuchukua shauri la mtu mwenye hekima? Ikiwa unataka, basi hekima inatulia pamoja nawe {1TG1: 13.2}

Muh. 10:18 — “Kwa sababu ya uvivu paa hunepa; Na kwa utepetevu wa mikono nyumba huvuja.”

Nyumba ya mtu mvivu huchakaa, nyumba yake huwa mbovu hata kabla kuikamilisha, au kabla hajairekebisha. Yeye ni wa kuchelewa katika kila kitu — tabia mbaya ya mtu kujiingiza ndani yake. Unaposafiri nje mashambani, kando ya barabara utatambua kwamba nyumba ambazo zimeharibika sana na zilizochafuka, ni nyumba za wale unaowaona kwenye kumbi wakipoteza wakati ambapo wangekuwa wakifanya kazi. Lakini huwezi kuona mtu yeyote ameketi bila kufanya kazi karibu na nyumba zilizotunzwa vyema. Iwapo utawaona watu, utawaona wakifanya kitu. Unafanya nini, Ndugu, Dada? — Unajua njia ya kurudi Edeni? {1TG1: 13.3}

13

Hebu tena turejee kwa Mhubiri. {1TG1: 14.1}

Muh. 3:17 — “Nikasema moyoni mwangu, Mungu atawahukumu wenye haki na wasio haki; kwa kuwa kuna wakati huko kwa kila kusudi na kwa kila kazi.”

Mungu atawahukumu waovu na wenye haki, kwa sababu kuna wakati kwa kila kusudi na kila kazi. Kila mtu atatoa hesabu kwa muda wake pamoja na matendo yake. {1TG1: 14.2}

Muh. 8: 6 — “ Kwa maana kwa kila shauri kuna wakati na hukumu; kwa sababu mashaka ya mwana-damu yaliyo juu yake ni makubwa.”

Kwa sababu kuna wakati wa kila kusudi na kila kazi, kwa hiyo kuna wakati wa hukumu kwa wote kanisani na duniani. Na kwa sababu kuna wakati na msimu kwa kila kusudi, taabu ya mwanadamu huongezeka iwapo haitii sheria hii ya Mungu. Lazima afanye kila kitu kwa wakati, ili taabu zake zisije zikaongezeka. {1TG1: 14.3}

Mit. 6: 6 — “Ewe mvivu, mwendee chungu, Zitafakari njia zake ukapate hekima.”

Mtu, mwanafunzi; chungu mdogo mwalimu! Ni taarifa ya kudhalalisha jinsi gani dhidi ya mvivu! {1TG1: 14.4}

Aya ya 7, 8 — “Kwa maana yeye hana akida, Wala msimamizi, wala mkuu, Lakini hujiwekea akiba ya chakula wakati wa jua; Hukusanya chakula chake wakati wa mavuno.”

Chungu anajua nini cha kufanya na wakati wa kukifanya na kukitekeleza. Hawezi kamwe kutafuta riziki ingawa hana bosi. Laiti ungeenda ndani ya nyumba yake, ungepata vyakula zaidi ya msimu unavyohitaji. Anajua wakati mavuno huja, na anajua jinsi ya

14

kuutumia vyema zaidi. Iwapo mwanadamu hawezi kufanya kama chungu, ikiwa hawezi kutambua wakati na msimu, basi taabu zake zitaongezeka bila shaka. {1TG1: 14.5}

Ushauri huu ungalikuwa umetoka kwa wanadamu, labda hatungaliweza kuuhitaji; ila ulitoka kwa Mungu, kuto-ka kwa Yeye Aliye na udhibiti wa kila kitu. Anajua maisha yako tangu wakati unapozaliwa hadi wakati una-pokufa. Anajua ni aina gani ya maisha utakayopitia. Unaweza kujisababisha kwenda njia ya mpotevu, lakini ni bora zaidi kama hautaiendea. Iliyo bora kwako ni kwenenda katika njia ya Baba. {1TG1: 15.1}

Kumbuka daima kwamba wapo waongozaji wawili tu wa mawazo katika ulimwengu — mawazo ya Mungu na mawazo ya Shetani. Sisi, kama wadhambi, tunazaliwa na mawazo ya Shetani, na hukaa pamoja nasi mpaka tun-apozaliwa mara ya pili, kuzaliwa kwa Roho na kwa mawazo ya Mungu. Kutenda haki, basi, lazima tufanye kin-yume cha kile ambacho mawazo yetu ya asili hutuambia, na basi tutakifanya kile mawazo ya Mungu yanajitahidi kutuwezesha kutenda. {1TG1: 15.2}

Vijana wanajua kile ninyi watu wazima mnafanya. Wanajua ni kiasi gani mnafikiri juu ya Mungu na Ufalme Wake. Wanajua jinsi gani mnavyofikiria mahali hapa na kazi Yake. Kwa vile wanayajua yote hayo, na mengi zaidi, basi ni wakati wa sisi sote kutambua kwamba hatuwezi kuwaongoza watoto karibu na malengo ya Mungu kuliko sisi wenyewe tulivyo; hatuwezi kuhamasisha ndani yao imani na bidii katika chochote wakati ambapo sisi wenyewe hatunayo. {1TG1: 15.3}

Ninatumaini kwamba wale ambao wameenda kwa njia ya mpotevu, waweze kujirudia wenyewe kabla ya uzoefu wa taabu kuwajia. {1TG1: 15.4}

Hivyo ndivyo ilivyo njia ya kurudi Edeni ilivyotengenezwa wazi kwa kila mmoja anayekuja duniani. {1TG1: 15.5}

15

WAZO LA SALA YA UFUNGUZI

Tutaendelea kusoma kuanzia pale tulipoachia Sabato iliyopita: Mlima wa Baraka, ukurasa wa 148 — {1TG1: 16.1}

M.B, uk. 148 — “Yesu, wakati Alipokaa duniani, aliishi maisha ya heshima katika historia yake yote kwa kuweka mbele ya wanadamu utukufu wa Mungu, na kwa kutiisha kila kitu kwa mapenzi ya Baba Yake. Iwapo tunafuata mfano Wake, uhakiksho Wake kwetu ni kwamba vitu vyote tunavyovihitaji katika maisha haya tutaongezewa.’ Umaskini au mali, ugonjwa au afya, unyenyekevu au hekima, — vyote atatukirimia kwa ahadi ya neema Yake. {1TG1: 16.2}

“Mkono wa milele wa Mungu huizunguka nafsi inayorudi Kwake kwa msaada, hata hivyo, dhaifu nafsi hiyo inavyoweza kuwa. Vitu vya thamani vya vilima vitaangamia; ila nafsi inayoishi kwa ajili ya Mungu, itakaa pamoja Naye. ‘Dunia inapita, na tamaa zake; lakini yeye ayafanyaye mapenzi ya Mungu anakaa milele.’ Mji wa Mungu utayafungua malango yake ya dhahabu kumpokea yule aliyejifunza wakati alipokuwa duniani kumwe-gemea Mungu kwa uongozi na hekima, kwa ajili ya faraja na matumaini, kati ya kupoteza na mateso. Nyimbo za malaika zitampokea huko, na kwa ajili yake mti wa uzima utazaa matunda yake. ‘Mlima itatoweka, na vilima kuondolewa; bali wema Wangu hautaondoka kwako, wala agano la amani Yangu kuondolewa, asema Bwana anayekurehemu.” {1TG1: 16.3}

Na sala yetu itakuwa kuhusu nini alasiri hii? — Naam, tuombe kwa ajili ya kutambua kwamba ikiwa tunaweka utegemezi wetu kamili kwa Bwana, kumtegemea Yeye kwa uongozi na hekima, Yeye hatatuacha; tunapaswa kuomba kwa ajili ya kutambua kwamba mikono Yake ya milele daima iko tayari kuizunguka nafsi ambayo inar-udi Kwake kwa msaada; na tunapaswa kuomba kwa imani kamili katika ahadi Yake ya kwamba ikiwa tunatiisha kila kitu kwa mapenzi ya Baba, basi vitu vyote vinavyohitajika katika maisha haya, “vitaongezwa” kwa maslahi yetu ya milele. {1TG1: 16.4}

16

NJIA MBILI TU

ANDIKO LA HOTUBA NA V. T. HOUTEFF

MCHUNGAJI WA WADAUDI WAADVENTISTA WA SABATO

SABATO, AGOSTI 3, 1946

HEKALU LA MLIMA KARMELI

WACO, TEXAS

Mara nyingi husikia kwamba zipo njia nyingi za kuingia katika Ufalme wa amani na ustawi wa milele, kwamba tunaweza kuchukua yoyote kati yazo na kufika huko. Mimi, kwanza, namini kwamba zipo njia mbili pekee, kwamba moja huongoza kwenye uzima wa milele na ile nyingine kwa mauti ya milele. Kuwapa sababu yangu ya kuamini kwamba zipo njia hizi mbili pekee, nitasoma kutoka Kitabu kisichokosa kamwe: {1TG2: 17.1}

Mat. 7:13, 14 — “Ingieni kwa kupitia mlango ulio mwembamba; maana mlango ni mpana, na njia ni pana iendayo upotevuni, nao ni wengi waingiao kwa mlango huo. Bali mlango ni mwembamba, na njia ime-songa iendayo uzimani, nao waionao ni wachache.”

Njia ngapi? – mbili tu: njia sahihi na njia mbaya. Njia hizi mbili zimekuwa pamoja nasi na daima zitakuwa kwa kadri muda wote mwanadamu wa asili na wa kiroho atakuwa anaishi duniani. Zilikuja kuwepo na ndugu wawili wa kwanza ambao waliishi duniani — Kaini na Abeli. Wale ambao husafiri kwenye njia nyembamba ni Waabeli, na wale ambao husafiri kwa njia pana ni Wakaini. Wapo wasafiri wengi kwenye ya mwisho kwa sababu wote wanaokuja katika uliwengu huu huanzia kwayo, na wengi wao hukaa daima kwayo. {1TG2: 17.2}

Hivi ndivyo ilivyo maana kwa kuanza sisi tumezaliwa kwa mwili — “Wakaini” kwa asili. Kwa hiyo, kabla

17

kuzaliwa mara ya pili, kuzaliwa kwa Roho, na hivyo kuwekwa kwenye njia nyembamba, sisi sote husafiri kwenye njia pana. Mbali na hilo, njia pana ni pana zaidi kwa mmoja kubeba yote ambayo dhambi hutoa, lakini njia nyembamba ni finyu sana kutoruhusu kila kitu ila msafiri mwenyewe. Kwa hiyo, kunena kwa kulinganisha, kunao wachache ambao huchagua kuzikana tamaa za mwili na kuacha dhambi katika namna zake zote. Kwa kawaida, basi, wengi husafiri kwenye “njia ionekanayo kuwa sawa machoni pa mtu,” ingawa “… mwisho wake ni njia za mauti.” Mit. 14:12. Sasa hebu twende kwa Injili ya Yohana, sura ya 9: {1TG2: 17.3}

Aya ya 39 — “Yesu akasema, Mimi nimekuja ulimwenguni humu kwa hukumu, ili wao wasioona waone, nao wanaoona wawe vipofu.”

Hapa tunaambiwa kwamba Yesu alikuja kwa hukumu ambayo itawasababisha wale wanaoona, kuwa vipofu; na wale walio vipofu, kuwezeshwa kuona! Msemo huu ni wa kipekee, ila maana ni wazi: Alikuja kumbadilisha kila mwanadamu — kupindua hali ya kila mtu — walio vipofu waone, na wale wanaona kuwa vipofu. {1TG2: 18.1}

Hebu sasa tuhukumu kesi yetu wenyewe. Ikiwa maono yetu kwa wakati huu ni sawa na siku zote, basi dhahiri kabisa kuja Kwake bado hakujatufaidi: Ikiwa katika kututembelea Kwake tunadhani kwamba tayari tunaona na kujua zaidi, hatuhitaji kitu chochote zaidi, na hatuwezi kushawishika vinginevyo, basi tutakuwa vipofu milele, hatutaweza kuona kile Yeye anachotaka tuone. Lakini iwapo tunakubali kwamba sisi ni vipofu kwa mambo ya kiroho, kwamba macho yetu yanahitaji kufumbuliwa, basi Kristo atatuwezesha kuona. Kama hao kwa uzoefu watasema, “Nilikuwa kipofu, lakini sasa ninaona.” Uzoefu wa kipofu lazima uwe wetu. {1TG2: 18.2}

18

Aya ya 40; 41 — “Baadhi ya Mafarisayo waliokuwapo pamoja naye wakasikia hayo, wakamwambia, Je! Sisi nasi tu vipofu? Yesu akawaambia, Kama mngekuwa vipofu, msingekuwa na dhambi; lakini sasa mwasema, Twaona; basi dhambi yenu inakaa.”

Iwapo unasema unaona, na bado unaendelea kufanya dhambi, basi wewe mwenyewe unawajibikia dhambi yako. Lakini ikiwa huoni, Yeye atakufanya uone, ili uweze kuiacha dhambi. {1TG2: 19.1}

Yoh. 10: 1 — “Yesu aliwaambia, Amin, amin, nawaambieni, Yeye asiyeingia mlangoni katika zizi la kon-doo, lakini akwea penginepo, huyo ni mwivi naye ni mnyang’anyi.”

Je! Unataka kuingia kwenye “zizi la kondoo”? Ikiwa unataka, unapaswa kuingia kupitia “Mlango.” Iwapo utaingia kwa njia nyingine fulani, hatimaye utatupwa nje katika giza, huko kusaga meno yako. Kutoka kwa njia mbadala hizi sisi sote lazima tufanye uchaguzi wetu. {1TG2: 19.2}

Aya ya 2 — “Aingiaye mlangoni ni mchungaji wa kondoo.”

Katika aya ya 9 Kristo alisema, “Mimi ni mlango.” Unganisha aya ya 9 na ya 2, na utaona kwamba wale wanaoingia ndani kupitia njia ya Bwana ni wao tu ambao Yeye huwatambua kama wachungaji wa kundi Lake. Bwana, kwa hiyo, inaashiria kwamba wapo wachungaji ambao hawajaidhinishwa wanaochunga kondoo Wake. {1TG2: 19.3}

Aya ya 3 — “Bawabu humfungulia huyo, na kondoo humsikia sauti yake; naye huwaita kondoo wake kwa majina yao, na kuwapeleka nje.”

Bawabu, yule msimamizi, huwafungulia mlango tu

19

wale ambao wameyazingatia mahitaji ya kuingia. Kwa maneno mengine, Bwana anatuambia wazi kwamba hakuna mtu anayeweza kuukwepa ukaguzi wa bawabu na milele kufaulu. Na bado licha ya onyo hili, na licha ya ukweli kwamba kupitia mlangoni ni rahisi zaidi kuliko kupanda juu ya ukuta, baadhi huchagua kuichukua nafasi ya kuiba njia yao ya kuingia — kujifanya kuwa katika “imani” hivyo kuingia ndani ya zizi la kondoo na kutarajia kumiliki au kupata wafuasi. Haiwezekani, hata hivyo, kuwashawishi kondoo wa kweli wa Mungu kuwafuata kwa sababu wanaijua Sauti ya Mchungaji wa kweli. {1TG2: 19.4}

Ni wale tu wanaopata kiingilio kwa njia ya Mlango na ambao “bawabu” (ambaye kupitia kwake Roho ya Unabii imedhihirishwa) huwafungulia ndio wachungaji walioidhinishwa ambao sauti zao kondoo wa Mungu husikia. Wachungaji wote kama hawa huwaita kondoo kwa majina: Wao wanafahamiana vizuri na makundi yao kwa sababu wanapendezwa sana na maslahi yao, nao huwaongoza kwa makini ndani na nje. {1TG2: 20.1}

Hapa mwanafunzi wa Ukweli wa sasa atakumbuka kwamba kwa mfano huu Kristo anaonyesha kwamba wa-chungaji pekee ambao Yeye hutambua kuwa Wake ni wale ambao “bawabu” hufungulia mlango na kuwaalika ndani. Mwanafunzi atakumbuka pia kwamba wengine wote wamepigwa chapa matapeli. Na kondoo ambao hus-ikia sauti ya mchungaji wa uongo, Yeye anatangaza, sio kondoo Wake. {1TG2: 20.2}

Aya ya 4 — “Naye awatoapo nje kondoo wake wote, huwatangulia; na wale kondoo humfuata, kwa maa-na waijua sauti yake.”

Kwa kuwa kondoo Wake hawazijui nyuso, lakini huzijua sauti, basi, wale wanaokazia uangalifu kwa nyuso na ambao hawawezi kutofautisha kati ya sauti na sauti wana hakika ya kupotoshwa na wachungaji waliojiteua. Ila wale tu ambao

20

huitii Sauti, Sauti ya Kweli, kwa upole huongozwa ndani kwa ajili ya makao na nje kwa malisho ya majani ma-bichi. Watu wa Mungu huwa hawajishughulishi na nyuso, ila hutii kwa bidii sauti zilizoteuliwa na Mungu zinaz-otamka Ukweli. {1TG2: 20.3}

Aya ya 5, 8, 10 — “Mgeni hawatamfuata kabisa, bali watamkimbia; kwa maana hawazijui sauti za wageni …. Wote walionitangulia ni wevi na wanyang’anyi; lakini kondoo hawakuwasikia …. Mwivi haji ila aibe na kuchinja na kuharibu; mimi nalikuja ili wawe na uzima, kisha wawe nao tele.”

Kondoo wa Mungu hivyo huongozwa kwa makini ndani na nje, wote kwa ajili ya makao na “chakula kwa msi-mu unaofaa,” kwa ukweli wa Sasa. “Mbuzi,” hata hivyo, wale ambao humkwepa bawabu wakati wakiingia, lazima, bila shaka, wafanye hivyo wakati wa kutoka nje, pia. Kwa hiyo, hawawezi kuongozwa na wachungaji walioteuliwa na Mungu. Hebu twende kwa Yohana 14 na tusome ila aya moja. {1TG2: 21.1}

Yohana 14: 6 — “Yesu akamwambia, Mimi ndimi njia, na kweli, na uzima; mtu haji kwa Baba, ila kwa njia ya mimi.”

Kutoka kwa hii tunaona kwamba Yesu ndiye njia pekee ya kuingia kwa Ufalme. Wazo, basi, kwamba zipo njia nyingi ilhali yupo Yesu mmoja, na kwamba zote huongoza kwa Ufalme wa Milele, ni “uvumi wa walaghai” am-bao mioyo ambayo haijatakaswa hupenda kuusikiliza. Wao ni miongoni mwa wale wanaomkwepa bawabu “Mlangoni,” wa wale wanaojua kwamba matendo yao hawezi kuustahimili ukaguzi. {1TG2: 21.2}

Ikiwa tunapaswa kuwa na makao katika Ufalme, hatupaswi kamwe kuwa kama wao. Lazima tujue ubaya zaidi wa

21

kesi yetu. Hatupaswi kamwe kusema kwamba ikiwa “yule na yule” atafika huko, tutaweza, pia. Unaweza kuwa ukweli kwamba iwapo “yule na yule” wangeweza kufika huko, sisi sote tungeweza, pia, lakini “yule na yule” haendi huko. Hatupaswi, kwa hivyo, kucheza upumbavu kwa kuwafanya “yule na yule” kuwa mifano yetu. Sharti tumfuate Bwana kupitia Ukweli Wake, Ukweli ambao inatufanya kuwa huru. {1TG2: 21.3}

Maadamu ipo Njia moja tu sahihi na Mlango mmoja, na kwa sababu Wakristo wote hawaoni sawa na hawatem-bei pamoja, inakuwa ni kwamba sisi sote tumekosea? sote tunaenda kwenye mwelekeo usio sahihi? — Hapana, hilo halingaliweza kuwa kamwe kadri ambavyo Bwana haitelekezi dunia. Hakika la, kwa maana Yeye lazima awe na watu ambao huwafunulia Ukweli Wake na ambao kupitia kwa wao awaokoe wale wanaochagua kwenda kwa njia Yake. Kwa hivyo, wale wanaochagua kwenda kwa njia nyingine mwishowe watagundua kwamba Ibil-isi, sio Bwana, yuko nyuma yao, na kwamba kuzimu, sio Ufalme, kupo mbele yao {1TG2: 22.1}

Tunapaswa kufanya vyema kujadili kwa dakika chache sifa ambazo mchungaji lazima awe nazo ili kupita ukaguzi wa bawabu. Nitaweza kutumia mifano michache, labda miwili au mitatu tu. {1TG2: 22.2}

Unakumbuka kwamba palikuwa na mtoto mmoja jina lake Samweli ambaye mwanzoni mwa maisha alikuja kutembea kwenye “Njia,” na ndani yake alifundishwa. Sasa fikiria juu ya kile kilichotokea: Usiku mmoja Sam-weli, unakumbuka, mara ghafla iliamshwa kwa Sauti. Akidhani kwamba ilikuwa ya Eli, aliruka haraka kutoka kitandani na kwenda kumwuliza Eli. Bila shaka Eli alishangaa, lakini alisema kwa upole, “Sikukuita. Nenda tena kitandani.” Kwa vile hapakuwa na mtu mwingine ila Eli karibu. Samweli alikuwa na uhakika kwamba mzee huyo alikuwa amemwita. Hata hivyo, aliitii na mara moja akarudi kitandani. {1TG2: 22.3}

22

Kabla ya muda mrefu, hata hivyo, labda mara tu Samweli alipokuwa amelala tena, Sauti hiyo iliita mara ya pili. Unajua kwamba Samweli angeweza kwa urahisi kuwa alisema moyoni mwake, “Mzee huyo lazima awe anaota. Hapa ananiita tena. Lakini mimi sitaki kusumbuliwa naye zaidi; Nitamruhusu apige mayowe yote anavyoweza.” Samweli, hata hivyo, aliharakisha iwezekanavyo mbele ya kitanda cha mwalimu wake, kusikia tena tu maneno, “Nenda tena kitandani, sikukuita!” Bado mara ya tatu alimsikia mtu akiita, na kwa hiari na kwa heshima kama hapo awali, alienda karibu na kitanda cha mwalimu wake mara ya tatu! Eli hatimaye aking’amua kwamba Bwa-na lazima awe amemwita mtoto, kwa hiyo alimwagiza Samweli atakachofanya. Na Samweli alifanya nini? — Ha-sa alivyoambiwa. {1TG2: 23.1}

Samweli asingalikuwa tayari, mwenye heshima, na mwenye subira jinsi alivyokuwa, unafikiri angaliweza kuja na kushikilia ofisi ya juu zaidi katika nchi? — Bila shaka hapana. Hapakuwa na kitu chochote isipokuwa sifa za uta-katifu za tabia ambazo Samweli alionyesha usiku huo zilizomkweza hadi kwa ofisi ya nabii, kuhani, na mwamuzi. {1TG2: 23.2}

Bado tunashangaa kwa nini Samweli aliitwa kutoka kitandani mara tatu mfululizo na kwa nini yeye na Eli wa-lisumbuliwa usiku? — Kwa sababu mbili: (1) Ili kuthibitisha kwamba bila kujali usumbufu, Samweli asingaliweza kusita kuinuka anapoitwa, na kwamba asingaliweza kuwa na hasira, kwamba hangaliweza “kumkejeli” Eli. (2) Bwana alitaka kumsaidia Eli; Alitaka kuzuia uwezekano wa Eli kuhitimisha kwamba Samweli alikuwa akipotoka na kuhoji uwezo wake wa kuwaadhibu wanawe. Laiti Eli asingalikuwa amepewa fursa ya kujua yakini kwamba Bwana alinena kwa mtoto huyo, basi angaliweza kuamua kwa urahisi kwamba Samweli alikuwa akitenda hila dhidi ya wana wa Eli. Lakini

23

hali ya majaaliwa kuwa kama ilivyokuwa, Eli hakika alijua bila shaka kwamba Mungu alikuwa na ujumbe kwa ajili yake. Hapakuwa na nafasi ya shaka. {1TG2: 23.3}

Wavulana leo, kama nyakati zilizopita, wanahangaika kufika mahali fulani maishani, hata sasa mamilioni kati yao hushindwa kufikia lengo lao na wengi huharibu maisha yao. Wanataka kuwa watu wakuu, lakini hushindwa hata kufanya watu wa wastani. Na sababu? — Ni rahisi kwa sababu huwa wanautathmini kuwa wa juu zaidi uwezo wao wenyewe, na kuutathmini kuwa wa chini zaidi uwezo wa Mungu. Hawajui kwamba pamoja na Mungu hakuna kushindwa, na kwamba pamoja Naye “wanaweza kuyafikia maeneo.” {1TG2: 24.1}

Enyi wavulana na wasichana jitolee kwa Mungu maishani mwenu. Yeye anawahitaji watu wakuu, na Anaweza kukufanya uwe hivyo. Unapojifunza njia ya Mungu na kuwa mvulana au msichana wa kutegemewa alivyofanya Samweli, Mungu hatapuuza bidii yako, uadilifu, na uaminifu. Atakupa kitu kikubwa kwa ajili ya thawabu yako. Naam, basi utakuwa mkuu kweli kweli. {1TG2: 24.2}

Daudi wa kale pia alikuwa mvulana mdogo na sio kitu zaidi ya mchungaji wa kawaida. Lakini alikuwa mchungaji mwema, bora zaidi katika nchi. Mungu aliona kwamba alikuwa akizingatia na mwaminifu kwa kazi zake, na hivyo Yeye aliazimu kumfanya kijana awe mfalme juu ya watu Wake. Hakika, wakati mtu anapolifanya jambo moja vyema, inawezekana kwamba atalifanya jambo lingine vyema pia. Daudi alikuwa mzuri katika kazi zake kama vile Samweli alivyokuwa. Ndiyo sababu aliiinuliwa kutoka kwenye zizi la kondoo na kuwekwa ndani ya kasri. {1TG2: 24.3}

Ninamfikiria kijana mwingine, kijana mchanga katika utineja wake — Yusufu. Bwana aliona kitu ndani yake am-bacho Yeye hangaliweza kukipata katika ndugu za Yusufu. Sio tu alikuwa mwana mpendwa wa baba yake, ila alikuwa mpendwa wa Mungu, pia. Mungu mawazoni alikuwa na kitu kizuri kwa ajili ya Yusufu

24

— kikubwa zaidi kuliko ambavyo dunia ingeweza kufikiria. Ili kuthibitisha kwamba alistahili kuaminiwa Yusufu ilikuwa kwanza awe mtumwa. Alihitaji kufundishwa kwa ajili ya kazi kubwa. {1TG2: 24.4}

Kwa hivyo namna ambavyo Majaaliwa yalitenda, ilikuwa kwamba ndugu zake walimuuza awe mtumwa. Wakati huo alikumbuka kile Bwana alikuwa amemwahidi katika ndoto — kwamba kando na ndugu zake, hata baba yake na mama yake wangalimsujudia. Unaweza kudhani ni fursa gani nzuri sana ya kumlaani Mungu alipojiona kwenye njia ya utumwa? Angaliweza kuwa alisema, “Kwa nini nimtumikie Mungu anayeahidi utukufu lakini badala yake anatoa kuaibishwa, shida na kutengwa?” Lakini Yusufu alitenda kwa hekima kama Ayubu: Kwa kumtakasa Mungu moyoni mwake, kwa tokeo alisema, “Ingawa Yeye aniangamize, bado katika Yeye nitamtegemea.” {1TG2: 25.1}

Yusufu haraka alijipatanisha kwa hali yake, akiwa na ujasiri kwamba Mungu wa baba yake alizijua taabu zake zote. Kwa hiyo mabwana wake wa watumwa, Waishmaeli, mara moja walitambua kwamba walikuwa wana-mumiliki mtumwa mzuri, mtumwa ambaye wangemuuza kwa vipande vya fedha maridhawa. Ninajuaje hili? — Najua kwa sababu Waishmaeli walimpeleka mara moja kwa mtu ambaye hangaliweza kununua kitu chochote ila kilicho bora, kwa mtu tajiri zaidi Misri, kwa mtu ambaye angeweza kulipa bei. Watu matajiri, unajua, huwa ha-wanunui vitu duni, wala wauzaji huwa hawawasambazii bidhaa duni. {1TG2: 25.2}

Hata wakati akiwa na huzuni, Yusufu lazima aliuonyesha uwezo wake wa utumishi, na lazima alionyesha heshima kubwa kwa mabwana wake wa watumwa wakiwa safarini kwenda Misri, kwa sababu wakati huo ilikuwa kwamba wachuuzi waligundua thamani ya mateka wao, na kisha wakang’amua kwamba wangeweza kumuuza kwa mtu aliyehitaji kitu kizuri na ambaye angaliweza kulipa bei. Potifa, pia, si kitambo aligundua kwamba Yusufu alikuwa katika hali zote wa kuaminika. {1TG2: 25.3}

25

Hivyo ndivyo alivyokuwa mtu wa Potifa namba 1. Hata Bi. Potifa kwa mahaba akasisimka kwa ajili yake. Ilikuwa kwa hatua hii, unakumbuka, kwamba alikuja kwenye kilele cha mtihani wake wa kuhitimu. Kwa kuupitia mtihani mkubwa zaidi wa maisha yake, alihitimu kutoka kwa nyumba ya Potifa, kisha kutoka gerezani, ambako alikwezwa kwenye kiti cha enzi cha Misri, kikuu zaidi duniani. Katika kukwezwa au kushushwa Yusu-fu alimpa Mungu utukufu na alifanya uaminifu wake kwa ubora. Kwa kila kitu alichowekwa, alikuwa wa pili kwa sifuri, na hivyo akawa mkuu kati ya waliokuwa hai wote duniani. {1TG2: 26.1}

Kuhusiana na siri halisi ya mafanikio yake utaipata katika kanuni moja rahisi — uthabiti dhidi ya majaribu kwa dhambi, na uaminifu kwa wajibu: “Ah! Siwezi kufanya jambo hili ovu. Siwezi kufanya dhambi dhidi ya wana-damu wala dhidi ya Mungu,” lilikuwa jibu lake kwa jaribu. {1TG2: 26.2}

Hii ndio sababu Yusufu alikuwa mkuu katika nyumba ya baba yake, mikononi mwa Waishmaeli, katika nyumba ya Potifa, katika chumba cha gereza, kwenye kiti cha Farao, na duniani kote. Ndio sababu ulimwengu wote wa kale ulimsujudia. {1TG2: 26.3}

Kutoka kwa kweli hizi za maisha inaonekana kwamba kanuni rahisi ambazo zilileta mafanikio kwa Samweli, Daudi na Yusufu, bila shaka zinaweza kuleta mafanikio kwetu sote. Na kumbuka kwamba mafanikio huanza mara popote pale unapokuwa, iwe ni katika nyua za hekalu, katika zizi la kondoo, katika yadi ya bwana wa mtumwa, gerezani, au katika kasri la mfalme – hakuna tofauti popote. Hauhitaji kukimbia ili kupata mafanikio, ila unahitaji kuinama na kuichukua. Naam, kwa kweli, mafanikio hudondoka kutoka angani, lakini kuyachukua unapaswa kuinama chini sana. Hili lazima ufanye ikiwa unataka kufanikiwa kweli katika chochote. {1TG2: 26.4}

26

Hivi sasa Bwana anatangaza kwa ajili ya angalau waokozi wa uhai 144,000, pamoja na makao makuu juu ya Mlima maarufu Zayuni — nafasi kubwa zaidi kuliko aliyoshikilia Yusufu. Utakuwa mmoja wao? Zipo fursa kuu leo kuliko hapo awali. Kwa nini usithubutu katika kitu ambacho hakuna nafasi ya kubahatisha? Mtu yeyote an-aweza kufanikiwa iwapo yuko tayari kulipa gharama {1TG2: 27.1}

Kwa mtazamo wa njia hizi mbadala zisizikosea kwa nini, nakuomba niambie, kwamba vijana leo ni wazembe na wasiojali? Kwa nini? Wao sio wavulana na wasichana mbaya; wamezaliwa kwa maumbile sawa na kizazi kingine chochote. Kwa kweli, wale walio juu ya kilima hiki ni wavulana na wasichana wazuri, lakini wanahitaji wazaliwe mara ya pili, wazaliwe kwa njia ya Roho — wabadilishwe, wafanywe kuona. {1TG2: 27.2}

Vijana kwa kawaida ni vipofu kwa mambo ya kiroho kama vile paka wachanga walivyo vipofu kwa vitu vya kimwili. Vijana wanahitaji kufundishwa njia ya kiroho ya maisha, wanahitaji kutenganishwa na asili ya kutamani dhambi ndani mwao, na asili ya kuchukia dhambi kuingizwa ndani mwao. {1TG2: 27.3}

Wazazi ambao tayari wamefanywa kuona, wanahitaji sasa kuamka kwa wajibu wao. Wanahitaji kuelimisha wa-toto wao kwa njia ya Kristo kama wanavyohitaji kuwaelimisha kwa njia ya kijamii. Hili wanaweza kulifanya tu kwa maagizo na mfano. {1TG2: 27.4}

Mfano wetu mkuu alikuja kutoka Mbinguni hadi duniani, akatembea na kufanya kazi na watu miongo mitatu, akafa na kufufuka tena. Hili Yeye alifanya ili kuwabadilisha watu, kuumba upya mfano wa Mungu ndani yao na kuwapa uzima wa milele. Ikiwa wavulana na wasichana hawa wanajitahidi kufanya kitu kwa ajili yao wenyewe, basi kwa hakika tunapaswa kuwasaidia kwa furaha kufikia lengo lao. {1TG2: 27.5}

27

Ninyi, wanaume na wanawake, mulikuja juu ya kilima hiki, sio kwa sababu mtu aliwaleta, lakini kwa sababu mulifikiri ni wajibu wenu. Ninyi hata hivyo, mmewaleta pamoja nanyi wadogo hawa. Kwa hiyo ni kwamba mlikuja kupitia “Mlangoni,” lakini wavulana na wasichana walikujia kwenye mizigo yenu, kama ilivyokuwa. Na sasa, iwapo watataka kuwa washirika wa kudumu katika hili “zizi la kondoo” wao pia, sharti wapitie ukaguzi. Mnaona, wanapitia mapambano yao sasa kama vile ninyi watu wazima mlivyopitia yenu kabla ya mje hapa. Na kama vile mtu fulani alivyojitahidi kwa ajili yenu huko, vivyo hivyo sasa mnapaswa kuweka juhudi kwa ajili ya vijana hapa. {1TG2: 28.1}

Tunahitaji wainjilisti wachanga, wavulana na wasichana walioongoka kufanya kazi kwa ajili ya wasioamini, ili kuweka mvuto sahihi juu ya wavulana na wasichana wengine. Hii ni muhimu kwa sababu wavulana na wasichana waongofu hufanya zaidi kwa ajili ya rika lao kuliko watu wazima. Kisha, pia, tunawahitaji vijana wanaume na vijana wanawake kuwasaidia wavulana na wasichana katika kazi ya kuziongoa nafsi — sio ku-wahubiria, ila kuwaongoza. {1TG2: 28.2}

Uliona jinsi wavulana walivyokuwa karibu D______ alipokuwa hapa. Ikiwa D______ angalikuwa ameongoka, iwapo angalikuwa ameamua kumtumikia Bwana kama alivyofanya Daudi wa zamani, fikiria ni nguvu gani kwa wema ambayo angeweza kuwa! Angaliweza kuwa mvuto wa ajabu sana miongoni mwa vijana. Angaliweza ku-wa kiongozi mkuu. Alikuwa na nafasi nzuri kama yeyote wa watu wakuu wa Mungu wa nyakati zilizopita. Lakini fursa D______ aliyokuwa nayo, kila mvulana na msichana anayo. Mvulana mmoja au msichana ali-yeongoka anaweza kuyageuza mazungumzo mabaya na yasiyofaa kuwa yenye thamani. Mfano mmoja mwema unaweza kufanya zaidi ya mahubiri. {1TG2: 28.3}

Wavulana na wasichana, ipo fursa kwa ajili yenu kutulia kwa biashara na Mungu, na kuamua

28

mnachotaka kuwa. Hamuhitaji kuwa wahubiri kwa kuanza, lakini sasa mnaweza kuwa wainjilisti wa kijamii. Ninyi wavulana na wasichana mnaweza kuwageuza wavulana na wasichana wengine kutoka kwa upumbavu wao, kutoka kwa vitendo vyao visivyo vya hekima na mazungumzo maovu. Wengine watafuata mifano yenu. Ni fursa yenu kuu sana iwapo tu mtajiweka tayari kwayo! {1TG2: 28.4}

Tunatamani kuwaona ninyi wavulana na wasichana mkiwa na wakati mwema. Tumechozwa na kuweka vikwazo juu yenu. Ninyi imarisha imani yetu ndani yenu, na kwa hivyo mtajiweka huru kwa masharti na vikwazo. {1TG2: 29.1}

Ikiwa mtatuonyesha kwamba mmeamua kuwa vile Samweli na Yusufu walivyokuwa, hatutaweza kuwa na wasiwasi juu ya kile mnachofanya au mnakokwenda. Naam, imarisha imani yetu ndani yenu, na kamwe hamta-taabishwa nasi. Ni kwa njia ya imani ya mtu kwenu kwamba mnaweza kupata chochote kwa vyovyote. {1TG2: 29.2}

Yusufu na Samweli walifanya kitu muhimu. Waliiweka mioyo yao yote katika chochote walichokifanya. Watu wote wakuu ulimwenguni hufanya na ndio sababu wao ni wakuu. Chochote ninyi wavulana na wasichana mnafanya, kifanye kweli. Msifanye udanganyifu juu yake. Mwishoni mwa kila siku mnapaswa kusema, “Kazi yangu ilikuwa karibu kamilifu, na matendo yangu hayana shaka.” Hili mwaweza kufanya. Nenda kwa “Mlango,” na umwambie Yeye mahitaji yako na majaribio yako. Sema, “Bwana, majaribio yangu ni majaribio Yako. Siwezi kuyaacha yanitaabishe tena. Nitauweka moyo wangu na nafsi yangu katika kazi Yako.” {1TG2: 29.3}

Fanyeni hili, wavulana na wasichana, na mtaona mambo tofauti ya kushangaza. Mtaona kwamba njia zenu za zamani zilikuwa njia za upumbavu. Wewe utajiambia, “Mimi sikuwa mpumbavu kufanya hicho na

29

kile?” Najua ninachokizungumzia. Ninawaambia hivi kutokana na uzoefu. {1TG2: 29.4}

Kwa nini wengi husafiri kwenye njia pana? — Kwa sababu huko unaweza kuwa chochote. Lakini kwa njia nyembamba, lazima uwe kitu kikuu sana. {1TG2: 30.1}

Idadi ya wavulana na wasichana hawapo tena nasi kwa sababu walikuwa wameamua kuendelea kwa njia pana. Wanaweza kupata uradhi fulani pale, lakini wanaelekea kwa mtihani mkubwa, na kwa hasara kubwa, pia. Ila wote ambao “hawajazaliwa mara ya pili” wajirudie wenyewe alivyofanya mpotevu, watasafiri mwendo wote mpaka mwisho wa barabara. Na nini basi? — Ibilisi nyuma na mwamba mkubwa mbele. Kutakuwako na kilio na kusaga meno. Kwa nini uendelee katika njia ya mpumbavu? {1TG2: 30.2}

Ni vyema usiipishe fursa yako wakati inapogonga langoni pako. Chukua “njia nyembamba” na ukae ndani yake, na utakuwa na ustawi na kuridhika siku zote za maisha yako. Hautapungukiwa wala kujuta. Hii amani ya mawazo unayohitaji. Kwa nini usiichukue? {1TG2: 30.3}

 

Usiyakose Manufaa Juu ya Hili

Iwapo haujatuma kwa ajili ya nakala yako iliyotangazwa na iliyojadiliwa sana kijitabu cha afya cha kurasa 96 (Kabari Inayoingia) ambacho kimefanya uamsho mkubwa katika dunia ya Waadventista na ambacho kimeliweka Shirika la K.I. katika mwangaza, usikikose iwapo afya, nyumba, na furaha yako inamaanisha kitu kwako. Kwa maoni yetu kitabu hiki ndicho bora hatujawahi kuona juu ya suala hili. Kwa kweli tunahisi kwamba kimetumwa na Mungu, na kwamba nakala yake inapaswa kuwa katika kila nyumba. Tumejulishwa kwamba sasa unaweza kukipata bila kuagizia. Tuma jina lako, anwani, na jina la kanisa ambalo wewe ni mshiriki (unaombwa kuchap-isha), na senti 15 kwa sarafu au stempu kwa Shirika La Kabari Inayoingia La Marekani, Kituo cha Mlima Kar-meli, Waco, Texas, Marekani na kitatumwa kwako. {1TG2: 30.4}

30

MKRISTO

Je! Ninaweza kuitwa Mkristo
Ikiwa kila mtu alijua
Mawazo yangu ya siri na hisia
Na kila kitu ninachofanya?

Oo, wangeweza kuona mfano
Wa Kristo ndani yangu kila siku?
Oo, wanaweza kumsikia Akinena
Katika kila neno nilisemalo?

Je! Ninaweza kuitwa Mkristo
Ikiwa kila mtu angeweza kujua
Kwamba mimi hupatikana katika maeneo
Ambapo Yesu hangeweza kwenda?

Oo, wanaweza kusikia Mwangwi Wake
Katika kila wimbo mimi huimba?
Katika kula, kunywa, kuvaa
Wanaweza kumwona Kristo ndani yangu?

Je! Ninaweza kuitwa Mkristo
Ikiwa nikihukumiwa kwa kile ninachokisoma
Kwa starehe zangu zote
Na kila wazo na tendo?

Je, ninaweza kuhesabiwa kuwa kama Kristo
Sasa ninavyofanya kazi na kuomba
Mkarimu, mwenye fadhili, wa kusamehe
Kwa wengine kila siku?

– Evangel.

31

Jumuiya ya Wadaudi Waadventista wa Sabato

(Ushirika Huru Unaojumuisha Kanisa)

Mlima Karmeli, Waco, Texas

S.L.P. 23738, Waco, TX 76702

+ 1-254-855-9539

www.gadsda.com

info@gadsda.com

Gombo la 1, Namba 1, 2

Kimechapishwa nchini Marekani

32

>