fbpx

Gombo 2021 Msimbo wa Nembo Nam. 4-5-6

The Symbolic Code 2021 Cover

Kwa Masilahi ya Dhehebu la SDA

“Kabila Kumi Na Mbili Waliotawanyika Ugenini”

Jarida hili ndogo limetiwa wakfu kujulisha habari na shughuli za matengenezo kwa waamini wa Ukweli wa Sasa; kujibu maswali kuhusiana na ujumbe wa kutiwa muhuri watu 144,000 (Ufu. 7:1-8) na umati mkubwa (Ufu. 7:9); kwa nabii za Isaya, Zekaria, Zefania, Mika, Hosea, Yoeli, Danieli, Ufunuo, Ezekieli, Yeremia, n.k., lakini kwa ukamilifu zaidi kwa vitabu vya kwanza vinane vilivyotajwa hapo juu; kwa mifano ya Kristo, kwa vivuli na nembo, na pia kwa maandishi ya Bi. E.G. White.

Hata hivyo, mgeni huyu wa kila robo mwaka anaahidi kujibu maswali kwa vifungu kama hivyo vya Maandiko jinsi tu ambavyo vimefunuliwa na Mungu na kutangazwa kwa mamlaka – yenye alama dhahiri ya ukweli. Kwa hivyo, ama atatoa jibu sahihi kwa maswali au sivyo akiri kutojua kwake kwa kusema “Sijui.

Lengo lake kuu ni kuufunua ukweli kwamba wakati umekuja Bwana audhihirishe uwezo Wake na kuliunganisha, na kulitakasa kanisa la Mungu – akiliita liamke kutoka kwa kitanda chake mavumbini na lijivike nguvu zake na zawadi ya mavazi yake mazuri, kwa maana “tokea sasa” hataingia ndani yako aliye najisi. (Isa. 52:1.) Kwa hivyo, anadai kwa udhahiri kwamba wajumbe wa “siku iliyo kuu na ya kutisha ya Bwana,” chini ya uangalizi wake, lazima watii kabisa matakwa, maagizo na ushauri wake wote ambao huwaletea mara kwa mara. Hatawafadhili wale wanaopuuza mamlaka yake matakatifu – kanisa linapaswa kuwa nuru kwa ulimwengu wote – zuri kama mwezi, – safi kama jua, na la kutisha kama jeshi lenye mabango. Isa. 62:1-7; Manabii na Wafalme, uk. 725.

Nembo zilizo kwa ukurasa wa jina la jarida ni nakala halisi ya Ufunuo, sura ya kumi na mbili na Tisa, na Isaya 7:21, ni nembo zinazofafanuliwa katika vitabu vyetu vinavyopatikana.

Mfariji huyu wa kila robo mwaka kwa furaha huwaita wa’S.D.A. ambao hufungua barua pepe zao au milango yao kukaribisha ziara yake. Hutoa kwa hiari wakati wake kuwahudumia wale wataokuwa warithi wa wokovu wala hakusanyi ada wala kutoza malipo kwa utumishi wake wa hisani. Huishi kwa zawadi za na sadaka za hiari – hamlemei mtu na huwafariji wote. Sala yake ya daima ni kwamba wateja wake wote wafanikiwe na kuwa na afya kama vile roho zao zifanikiwayo. (III Yohana 2.)

Eleza maswali yako kwa uwazi na dhahiri, ukitoa marejeo, na yatashughulikiwa mara tu zamu yayo kwa foleni inayosubiri itaruhusu.

Iwapo ungependa rafiki huyu aliyechapishwa aje nyumbani kwako siku zote, pia machapisho mengine bila fedha, tuma jina na anwani kwa info@gadsda.com au S.L.P. 23738, Waco, TX 76702.

Daudi Eliya Yezreeli

The 12 Tribes of Israel

Aprili – Mei – Juni 2021 | Msimbo wa Nembo, Gombo 2021, Nam. 4, 5, 6 | Ukurasa 2 wa 48

Table Of Contents.

Aprili – Mei – Juni 2021 | Msimbo wa Nembo, Gombo 2021, Nam. 4, 5, 6 | Ukurasa 3 wa 48

DPPS And QESS Logo. Volume 2021 The Symbolic Code Nos. 4-5-6

Aprili – Mei – Juni 2021 | Msimbo wa Nembo, Gombo 2021, Nam. 4, 5, 6 | Ukurasa 4 wa 48

Advert Of Midweek Prayer Meeting. Volume 2021 The Symbolic Code Nos. 4-5-6

BWANA ARUSI YUAJA

Wazo la Kutafakari

TN2: 67.1: Jifunzeni ujumbe ninyi wenyewe, na mzuie kwamba mwanadamu yeyote asihitilafiane na wokovu wenu. Fanya uamuzi wenu wenyewe bila kumtegemea mtu yeyote, na mjue wenyewe kwamba Mungu anawaongoza na kama Alivyofanya wakati mlitarajia kuwa wa S.D.A. Msimpokee kuhani wala askofu kama Mungu wenu. “Msiwe kama farasi, wala nyumbu, wasio na ufahamu: ambao vinywa vyao lazima vidhibitiwe kwa lijamu na hatamu, wasije wakawakaribia.” Zaburi 32:9. Kwa nini mjikwae na kuanguka juu ya kikwazo kile kile ambacho kimewatanguliza vichwa mamilioni kutumbukia kuzimuni? Tazama, Ndugu, Dada, epuka msiba ulio mbele, na uwasaidie wengine pia kuuepuka.

Tuanze na taarifa ifuatayo kutoka katika Pambano Kuu:

GC 399.4: Vivyo hivyo, mifano ambayo huhusiana na ujio wa pili lazima itimizwe kwa wakati ulioonyeshwa katika utumishi wa mfano. Chini ya mfumo wa Musa, kutakaswa kwa hekalu, au siku kuu ya Upatanisho, ilitukia siku ya kumi ya Mwezi wa saba wa Kiyahudi, [Walawi 16:29-34.] wakati kuhani mkuu, baada ya kufanya upatanisho kwa ajili ya Israeli, na hivyo kuziondoa dhambi zao kutoka patakatifu, alitoka ndani na kuwabariki watu. Basi iliaminika kwamba, Kuhani wetu Mkuu, angetokea kuitakasa dunia kwa kuiangamiza dhambi na wadhambi, na kuwabariki watu Wake waliomngojea kwa uhai wa milele. Siku ya kumi ya Mwezi wa saba, siku kuu ya Upatanisho, wakati wa kulitakasa hekalu, ambayo katika mwaka 1844 iliangukia siku ya ishirini na mbili ya Oktoba, ilionekana kwamba wakati wa kuja kwa Bwana. Huu ulikuwa katika uwiano na ushahidi uliowasilishwa tayari kwamba siku 2300 zingekoma katika vuli, na hitimisho hilo lilionekana kuwa lisilokanika.

Kumbuka kwa makini kwamba “Mifano ambayo huhusiana na Ujio wa Pili lazima itimizwe kwa wakati ulioonyeshwa katika utumishi wa mfano.” Nyakati zilizoonyeshwa wazi katika utumishi wa mfano hutegemea siku na miezi ya Kalenda ya Uumbaji na sio ile ya Gregoria. Tukio la kwanza linalohusiana na ujio wa Kristo lilikuwa kuja Kwake kwa Patakatifu Mno katika hekalu la mbinguni kuanza hukumu ya wanadamu, ambayo ilianza na wafu na itakamilika na walio hai. Siku ya kumi ya Mwezi wa saba, Siku ya Upatanisho katika utumishi wa mfano, iliangukia siku ya Ishirini na mbili ya Oktoba katika mwaka 1844, siku ambayo Kristo aliingia katika chumba kitakatifu mno cha Hekalu la Mbinguni.

Tuisikie Fimbo katika usanii wa kinabii katika chati ya “Mwaka Mtakatifu Na Sherehe Zake Kuu” kuhusiana ni lini Bwana atakuja kwa hukumu ya walio hai:

Chart Of Sacred Year Calendar. Volume 2021 The Symbolic Code Nos. 4-5-6

ABN3: 13.1: Chati hii hutuwezesha kuona kwamba kama vile msimu mmoja wa jua hulingana na mwingine (siku ya masika iliyo sawa mchana na usiku hulingana na siku ya vuli iliyo sawa mchana na usiku, na mageuzi ya majira ya kiangazi, mageuzi ya majira ya baridi),

Aprili – Mei – Juni 2021 | Msimbo wa Nembo, Gombo 2021, Nam. 4, 5, 6 | Ukurasa 6 wa 48

kwa mtindo kama huo sikukuu takatifu za msimu mmoja hulingana na sikukuu takatifu za msimu mwingine: siku ya kumi ya Mwezi wa kwanza, utengo wa mwana-kondoo mkamilifu kutoka kwa kundi (Kut. 12:3), sawa na siku ya kumi ya Mwezi wa saba, kazi ya Upatanisho, utengo wa wenye haki kutoka kwa waovu, ukiashiria katika matukio yote mawili siku ya hukumu, siku ya kuwatenga watakatifu kutoka kwa waovu; …

Kumbuka katika chati hii kwamba matukio yanayohusiana ni mkabala moja kwa moja na lingine na miezi sita kamili mbali mbali:

Chart Of Sacred Year Calendar. Volume 2021 The Symbolic Code Nos. 4-5-6

Kwa mtindo kama huo, sherehe takatifu ya siku ya kumi ya Mwezi wa saba hulingana na sherehe takatifu ya siku ya kumi ya Mwezi wa kwanza — zote zikiwa siku za hukumu — matukio yote ni ujio wa Bwana kwa hukumu. Kwa sababu ujio wa Bwana katika mwaka 1844 ulikuwa kwa wafu, basi ukilinganishwa ujio Wake ujao kwa siku ya kumi ya Mwezi wa kwanza lazima uwe kwa walio hai, jinsi ambavyo Fimbo husema katika taarifa zifuatazo:

“Kwa sababu utakaso unaotajwa katika mifano na katika unabii wa Malaki haujawahi kutukia, hukumu ya upelelezi ya walio hai ni dhahiri, basi bado ni wa baadaye. Kazi hii ya upelelezi kwa hivyo ni ya tukio la kazi ya kutenganisha katika hekalu la duniani (kanisa), jinsi inavyoletwa kwa mtazamo pia katika Ezekieli 9:” {TN3: 43.3} [218]

“Malaika ambao wanakizunguka kiti cha enzi katika hekalu la mbinguni wakati wa hukumu ya Danieli 7:9, 10 na Ufunuo 5:11, jinsi ambavyo mifano hufafanua, watashuka pamoja na “Mwana wa Adamu” wakati Atalijia “hekalu Lake” (kanisa Lake) kutenganisha kwa hukumu “waovu kutoka kati ya wenye haki,” na kuwasafisha kama dhahabu na fedha “lakini ni nani atakayestahimili siku ya kuja Kwake… nao watamtolea Bwana dhabihu katika haki.” Mal. 3:2, 3.”  {TN3: 46.2} [218]

“Katika onyesho la mchoro kwamba Atakuja kwa dunia pamoja na malaika Zake wote kutekeleza hukumu kwa walio hai, Bwana alijifunua Mwenyewe kinabii kwa Ezekieli akiletwa kama aliyeketi juu ya kiti cha enzi kwa dunia na viumbe wanne mara tu kabla ya mchinjo wa wanafiki ndani ya kanisa kutukia. Na kama vile kila kiumbe hai kina uso wa simba, uso wa ndama, uso wa mwanadamu, na uso wa tai (Ezek. 1:10), — nembo ile ile ya mahakama kama walivyo wanyama walio mbele ya kiti cha enzi katika hekulu la mbinguni (Ufu. 4:7) katika wakati wa hukumu ya wafu, — na wakati wanashuka kwa dunia wao hivyo kimfano wanaonyesha kwamba kazi ya kiti cha enzi ya upatanisho-ya hukumu ambayo inaitisha kikao cha kuongoza hukumu ya wafu inapanuliwa hadi duniani. ”  {TN3: 46.3} [218]

“Upanuzi huu, hadi hapa jinsi tumeweza kujua sasa, lazima utukie kwa ufunguzi wa muhuri wa

Aprili – Mei – Juni 2021 | Msimbo wa Nembo, Gombo 2021, Nam. 4, 5, 6 | Ukurasa 7 wa 48

saba (Ufu. 8:1), maana kwa wakati huo sauti za mbinguni , ambazo zilifungua hukumu ya walio kufa, zinanyamaza katika hekalu la mbinguni na kuanza, baada ya ukimya wa nusu saa, kuvuma duniani. Kwa maneno mengine kama vile mbinguni kwa wakati wa ufunguzi wa hukumu ya wafu, palikuwa na “umeme na sauti na ngurumo” (Ufu. 4:5), vivyo hivyo duniani kwa “ufunguzi wa hukumu ya walio hai,” zipo “sauti, na ngurumo, na umeme, na tetemeko la nchi.” Ufu. 8:5.” {TN3: 47.1} [218]
“Kwa hukumu ya waliokufa, hata hivyo, kazi ya utengo hutukia vitabuni katika hekalu la mbinguni ilhali kwa hukumu ya walio hai, utengo utatukia kati ya watu kanisani na kati ya majina yao ndani ya vitabu katika hekalu la mbinguni, hivyo kuonyesha kwamba hekalu zote mbili zitatakaswa mwishowe.”  {TN3: 47.2} [218]
“Bila shaka, kwa hivyo, ujio wa Bwana kwa hekalu Lake (Mal. 3:1-3), kuja Kwake pamoja na malaika Zake wote (Mat. 25), na kuja Kwake akiwa ameketi kwa kiti cha enzi juu ya viumbe hai (Ezek. 1), — wote mara tatu huwakilisha tukio lile lile jinsi ambavyo limeonyeshwa, — kutukia mwanzoni mwa hukumu ya walio hai: katika wakati ambamo shughuli za mahakama za hekalu la mbinguni zinapanuliwa hadi kwa hekalu la duniani — kanisa.”  {TN3: 47.3} [218]

Chart Of Sacred Year Calendar. Volume 2021 The Symbolic Code Nos. 4-5-6

SASA, KWA HIVYO kwa kuzingatia taarifa zilizotangulia, lazima sote hapa tukubali kwamba siku na ujio wa kuanza hukumu ya walio hai katika hekalu la mbinguni ni siku ya kumi ya Mwezi wa kwanza, itakayotukia hivi karibuni katika hii karne ya ishirini na moja ya kalenda ya Gregoria, 20??, jinsi ishara za nyakati zinavyotabiri. Tunakaribia nyumbani wapendwa.

Sasa ya kwamba twajua siku ambayo Kristo atalijia hekalu Lake la duniani, tuhimize ufunguzi wa Muhuri wa Saba tujiandae, maana Bwana arusi yuaja. Hivi karibuni sana, wapendwa wangu mno ndugu na dada, kilio kitafanywa “tazama, Bwana arusi yuaja; tokeni mwende Kumlaki” je! mtakuwa tayari? Basi lazima

Come Out Of Davidia. Volume 2021 The Symbolic Code Nos. 4-5-6

Aprili – Mei – Juni 2021 | Msimbo wa Nembo, Gombo 2021, Nam. 4, 5, 6 | Ukurasa 8 wa 48

Heaven's Appeal Advertisem

MTOKE DAVIDIA.

Swali ambalo huja akilini ni: I wapi au ni nini Davidia? Mahali pa kwanza tunaenda ni kwa ujumbe; ni wapi hunena kuhusu Davidia? La kushangaza, jina Davidia halipatikani katika ujumbe wa Fimbo, kwa hivyo ni wapi au kutoka wapi tunalipata? Jina hilo lilionekana mara ya kwanza katika Msimbo wa Nembo wa 1961 uliochapishwa na waamini wa Fimbo pekee 100%, mhariri mmoja na pekee M. J. Bingham. Alibuni jalada la Msimbo wa Nembo likiwa na ujumbe kwa washirika wake Majesuiti; Nadhani ni kuwajuza uwakilishi wao, au niseme kupenyeza. Hebu tulichunguze jalada:

Article of Come Out Of Davidia

Kwa kulichunguza jalada la msimbo wa nembo wa 1961 lililobuniwa na M. J. Bingham, utagundua ekaristi [nembo] katikati ikiwa imezungukwa na ujumuishaji wa majalada ya Msimbo wa Nembo wa 1954 na 1936. Jumuiya ya Bashani hufunza kwamba shirika lao ilianzia kwa Kikao hiki na hutumia huu Msimbo wa Nembo kama thibitisho, wewe kuwa mwamuzi.

Ukienda kwa ukurasa wa thelathini na tano wa Msimbo wa Nembo wa 1961, Napendekeza ufanye hivyo, nakala inapatikana kwenye tovuti yetu; Utapata barua kutoka kwa M. J. Bingham hadi kwa Ndugu aliyekuwa akihoji yaliyo katika Mwalimu wa Ukweli Mwafaka, baadaye kikawa chombo cha kinabii cha kilima cha Bashani. Kwa ukurasa wa thelathini na tisa ni pale ambapo jina Davidia huonekana haswa kwa mara ya kwanza katika Msimbo wa Nembo wowote:

Aprili – Mei – Juni 2021 | Msimbo wa Nembo, Gombo 2021, Nam. 4, 5, 6 | Ukurasa 10  wa 48

Volume 2021 The Symbolic Code Nos. 4-5-6

Sasa unajua ni nani aliyelipatia vuguvugu la Wadaudi jina hili linalopendwa, “Davidia.”

O, Davidia! Davidia! Umerogwa, kwa kukataa jina la heshima “Kanisa la Saa ya Kumi na Moja,” tulilopewa na Bwana katika mfano wa Mathayo Ishirini na Msajili wa Nyumba Nyeupe kwa ukurasa wa thelathini na tatu, ila kulipendelea jina Davidia. Uvuvio ulituonya kuhusu huku kupenyeza kwa Ujesuiti:

“Katika siku za wana-matengenezo, ili kuudumisha umati gizani akawawekelea vibanio vyake, kisha akakifungulia wazi kizima moto chake dhidi ya nuru iliyokuwa ikiwaka, na kiliposhindwa, aliwaweka “wahubiri waliolala wanahubiri kwa watu waliolala.’ Shuhuda, Gombo la 2, uk. 337.” {7SC7-12: 8.2.6} [490]

“Mwenendo huu wenye mafanikio ya juu sana ameufuata siku zote tangu zamani, hadi kama tokeo kanisa leo karibu linyongwe na magugu. Ni, kama kwa mfano, limepenyezwa ndani kwa safuwima humusi (ya tano).” {7SC7-12: 8.2.7} [490]

“Usiku huo niliota,” anasema mtumwa wa Bwana kwa mtazamo wa ajabu wa hali hii, “kwamba nalikuwa Battle Creek nikitazama nje kupitia kioo cha kando penye mlango, na nikaliona kundi likitembea

kuielekea nyumba, wawili wawili. Walionekana wakali na wenye azimio. Naliwajua vyema, na nikageuka kuufungua mlango wa sebule kuwapokea, lakini nalifikiri nitazame tena. Picha ilikuwa imebadilika. Kundi hilo sasa liliwasilisha muonekano wa maandamano ya Katoliki. Mmoja mkononi mwake alibeba msalaba, mwingine mwanzi. Na walipokaribia, yule aliyebeba mwanzi akafanya mduara kuizunguka nyumba akisema mara tatu, ‘Nyumba hii imepigwa marufuku. Bidhaa lazima zitaifishwe. Wamenena dhidi ya amri yetu takatifu.’ Nilishikwa na hofu, na nikakimbia ndani ya nyumba, hadi nje ya mlango wa kaskazini, na nikajikuta katikati ya kundi, baadhi ambao naliwajua, lakini sikuthubutu kusema neno kwao kwa kuogopa kusalitiwa. Nilijaribu kutafuta mahali pa kupumzikia ambapo ningeweza kulia na kusali bila kukutana na macho yenye ari, ya upekuzi popote nilipogeukia. Nilirudia mara kwa mara Iwapo tu ningaliweza kuelewa hili! Iwapo wataniambia lile nimesema, au lile nimefanya!’ {7SC7-12: 9.1.1} [491]

“Nalilia na kuomba sana nilipoona bidhaa zetu zimetaifishwa. Nilijaribu kusoma huruma au sikitiko kwa ajili yangu kwenye nyuso za walionizunguka, na nikatambua nyuso za baadhi ambao nalifikiri wangesema nami

Aprili – Mei – Juni 2021 | Msimbo wa Nembo, Gombo 2021, Nam. 4, 5, 6 | Ukurasa 11  wa 48

na kunifariji iwapo hawakuogopa kwamba wangetazamwa na wengine. Nilifanya jaribio la kukimbia kutoka kwa umati wa watu, lakini nikaona kwamba nalikuwa nikitazamwa, nikaficha nia yangu. Nikaanza kuomboleza kwa sauti, na kusema, “Iwapo wataniambia lile nimesema, au lile nimefanya!’ Mume wangu, ambaye alikuwa analala kitandani katika chumba kile kile, alinisikia nikiomboleza kwa sauti, na kuniamsha. Mto wangu ulikuwa umelowa kwa machozi, na huzuni ya kufadhaika roho ilikuwa juu yangu.” — Shuhuda, Gombo la 1, uk. 578. {7SC7-12: 9.1.2} [491]

“Kote kote katika Himaya ya Ukristo, Uprotestanti ulitishwa na maadui wa kutisha. Ushindi wa kwanza wa Matengenezo ulipita, Rumi uliita majeshi mapya, ukitarajia kufanikisha uharibifu wake. Kwa wakati huu amri ya Majesuiti ilitengenezwa, ya ukatili mno, fidhuli, na yenye nguvu ya mabingwa wote wa upapa. Ikiwa imekatwa kabisa kwa mafungamano ya ya duniani na maslahi ya wanadamu, ikiwa imekufa kwa madai ya mapenzi ya asili, kufikiri na dhamira vyote vikiwa vimezimishwa, hawakujua sheria, wala mshikamano, ilaule wa amri yao, na bila wajibu ila kupanua nguvu zake. Injili ya Kristo ilikuwa imewawezesha wafuasi wake kuikabili hatari na kuyastahimili mateso, bila kufadhaishwa na baridi, njaa, taabu, na umaskini, kuiinua bendera ya ukweli usoni pa kitanda cha kutesea, gerezani, na mlingoti wa kumtundika mtu. Ili kupambana na majeshi haya, Ujesuiti uliwavuvia wafuasi wake msimamo mkali uliowawezesha kustahimili hatari kama hizo, na kupinga uwezo wa ukweli dhidi ya silaha zote za udanganyifu. Haukuwapo uhalifu mkubwa sana ambao hawangeweza kutenda, udanganyifu mwovu sana wao kufanya, kuiga kugumu sana wao kuchukua. Waliapa kwa umaskini na unyenyekevu usiokoma, lilikuwa lengo lao walilosomea kujihifadhia utajiri na mamlaka, kujitolea kuupindua Uprotestanti, na kuusimamisha tena ubabe wa upapa.” {GC 234.2}

“Wanapojitokeza kama wanachama wa shirika lao, huvalia vazi la utakatifu, wakizuru magereza na hospitali, wakiwahudumia wagonjwa na maskini, wakikiri kwamba wameukana ulimwengu, wakilibeba

jina takatifu la Yesu, ambaye alienda huku na huko akitenda mema. Lakini chini ya maonekano haya ya nje bila lawama makusudi ya uhalifu na mabaya zaidi yalifichwa mara nyingi. Ilikuwa kanuni ya msingi ya shirika hilo kwamba kusudi huhalalisha njia ya kulifikia. Kwa alama hii ya siri, kudanganya, wizi, kusema uongo baada ya kuapa kusema ukweli, mauaji ya kukodiwa, hayakuwa tu ya kusamehewa bali ya kupongezwa, yalipotimiza maslahi ya kanisa. Chini ya miigo mbalimbali Majesuiti walifanyiza njia yao kuingia katika ofisi za serikali, wakipanda juu kuwa washauri wa wafalme, na kubadili sera za mataifa. Wakawa watumwa kutenda kama wapelelezi kwa mabwana zao. Walianzisha vyuo kwa ajili ya wana wa wakuu na wenye vyeo, na shule kwa watu wa kawaida; na watoto wa wazazi Waprotestanti wakavutwa kushika ibada za kipapa. Fahari zote za nje na wonyesho wa ibada za Kirumi uliletwa kukanganya akili na kupumbaza na kuvutia mawazo, na hivyo uhuru ambao wababa walijitaabisha na kutokwa damu ulisalitiwa na wana. Majesuiti walienea upesi kote Ulaya, na kotekote walikokwenda, ulifuata uamsho wa upapa.”{GC 235.1}

Majesuiti watendaji wa Davidia wanaojulikana wanaoongoza ni:

Kilima cha Bashani – Ufalme wa Bingham
UPA7.org – Eric Edstrom Dystopia
Daktari Mwanablogu – Robert Peralta

Wapo pia wanajeshi waendao kwa miguu, haswa kutoka kwa Ufalme, lakini msifadhaike mioyoni mwenu. Fimbo ya Mungu imepanga kimbele kushinda.

Zaidi ya jina Davidia, msingi wa fundisho la uongo ulianzishwa katika Msimbo wa Nembo wa 1961 unaopatikana kwa ukurasa wa nane na tisa:

Msimbo wa Nembo Gombo la 1, Namba 1, Agos. – Des. 1961, uk. 8, aya ya 5: “Mapema kwenye ajenda lilikuja jambo kuhusu eneo la makao makuu. Hili lilithibitisha kuwa tatizo gumu la Kikao. Baadhi walikuwa na maoni kwamba lazima, kaw mtazamo wa taarifa moja au mbili katika Fimbo, yawe ni mapenzi ya Bwana kwamba kwa namna fulani tupate udhibiti wa Mlima Karmeli wa zamani, ili tuweze kuendeleza na kukamilisha kazi kutokea

Aprili – Mei – Juni 2021 | Msimbo wa Nembo, Gombo 2021, Nam. 4, 5, 6 | Ukurasa 12  wa 48

hapo. Uchambuzi kutoka katika Biblia na Fimbo uliwasilishwa kwetu na Ndugu Bingham, ulithibitisha kabisa kwamba yapo maeneo matatu ya malisho ya kiroho ambamo watu wa Mungu watalisha (tazama 2SR 243:2). Uchambuzi uliendelea kuonyesha kwamba kwa vile Karmeli wa Fimbo (Mlima Karmeli wa zamani) haupo tena, na kwa vile Gileadi ni Ufalme (tazama Yer. 51:8 na Yer. 46:11, 12) kwa hivyo sasa tuko katika kipindi cha Bashani na lazima, ndiposa, tupate chakula chetu kwa wakati wake kutoka kwa Fimbo katika BASHANI. (Uchambuzi huu wote utachapishwa haraka iwezekanavyo.)”

Hapa tunaona chimbuko la Mlima Karmeli wa Fimbo haupo tena, likiweka msingi wa wote ambao hawana makao makuu kwa Mlima Karmeli wa Uakisi leo.

Udanganyifu mwingine uliotangazwa katika huu Msimbi wa Nembo ni ujanja mwingine wa muundo wa kiserekali wa naibu rais bila rais. M. J. Bingham alikuwa dhidi ya muundo huu wa kiserikali kabisa. Lengo lake kwa Kikao lilikuwa kuanzisha jumuiya ya kikatiba, ambayo ingehitaji rais, naibu rais, katibu, na mhazini, kama maafisa wake wanne. Pamoja na kutumaini kuwa rais, alikuwa pia anatumaini kuwa nabii wa leo, anavyothibitishwa na kuleta kwake Kikao cha kwanza baada ya pigo la 1959 na uhariri wake wa Mwalimu wa Ukweli Mwafaka. Ndugu Bingham alifanikiwa kupata nyadhifa zote mbili baada ya waamini wa Fimbo pekee 100% kukataa mfano wake usiovuviwa wa Leah and Raeli, ambao Wabashani hudhani ni uzinduzi wake wa kazi ya kinabii.

Jina Davidia lilienea nje ya nchi kotekote katika ulimwengu wa Wadaudi, na likawa jina la kuliunganisha vuguvugu lililogawanyika. Katika 1961, Davidia ilijumuisha Kundi la Dada Houteff huko Elk, Texas, Mlima Karmeli Mpya, na vichipuko viwili: Branch, ambacho baadaye kiliongeza Wadaudi kwa jina lake ili kikubalike zaidi na Wadaudi; na kile cha Wadaudi Fimbo pekee 100%.

Ben Roden, kiongozi wa Branch, alikufa, na mkewe akawa nabii mke mrithi. Baada ya kifo chake, mavuguvugu karibu matatu ya Branch yalichipuka. Branch la David Koresh, lililo maarufu sana kwa yote, likaleta aibu duniani kote kwa Vuguvugu la Wadaudi. Yapo sasa karibu makundi saba tofauti ya Branch, na la Trent Wilde huongoza yaliyo maarufu. Umaarufu wa la Wilde utakuwa

mbaya zaidi ya la Koresh.

Davidia ulifanza mgawanyiko mwingine wa amiba wakati M. J. Bingham aligawanyika kutoka kwa Wadaudi Fimbo pekee 100% baada ya wao kukataa mfano wake wa Leah na Raeli, ambao ulikizalisha kichipuko cha Bashani katika 1962 chini ya jina la shirika Jumuiya ya Wadaudi Waadventista wa Sabato. Kichipuko cha Gileadi kilichipuka kutoka kwa kichipuko cha Bashani. Kichipuko cha Bashani baadaye kibakteria kikazalisha vichipuko huru vingi, ambavyo cha kuchukiza zaidi ni Mustard Seed Advent cha msharika wake wa awali Derek West.

Katika 1970 amiba, Davidia, katika maumbo ya watu Wadaudi Fimbo pekee 100%, walihamia Salem, Carolina Kusini, kutoka Vesta, California, wakatumia Mto Mkubwa wa Sura ya Ezekieli 47 kama kiunga mkono chao kuhama. Miaka minne mifupi baadaye, Davidia ikagawanyika tena. Don Adair, mshirika wa awali wa M. J. Bingham, akahamia magharibi hadi Tamassee, Carolina Kusini, na wengine wakarudi magharibi hadi Yucaipa, California. Kumbuka kwamba mwelekeo wa mashariki uliachwa na makundi yote mawili, ambako mto huo awali uliwaelekeza, maana yote yalienda magharibi ya Salem. Ardhi iliyonunuliwa na Ndugu Don Adair kule Tamassee, Carolina Kusini, ilitangazwa kuwa Mlima Karmeli na ikaendelea kuitwa Jumuiya ya Salem. Ndugu Don alichaguliwa kama naibu rais wa Salem, kwa hivyo akaendeleza urithi wa muundo wa kiserekali wa Dada Florence Houteff. Katika 1980 baad ya kuwapoteza vijana wengi, washarika mahiri walioondoka na kuanzisha Jumuiya ya sasa ya Mt. Dale, Ndugu Don naibu rais wa kudumu wa Jumuiya ya Salem/Tamassee. Tumkumbuke Ndugu Don katika sala zetu; sasa yu mkongwe, na taabu za maisha zimemdhoofisha. Itaonekana kwamba kundi la Salem lazima limtafute naibu rais mwingine au liimbe wimbo wa mgawanyiko wa Davidia.

Katika 1980 Mt. Dale ikawa nyongeza mpya kwa Davidia. Wakati huo huo, nyuma kule Yucaipa, utumbo wa amiba ulikuwa ukitaharuki kugawanyika, na katika 1983 Wanda O’Berry na wenza aliligawanya kundi la Yucaipa na wakahama hadi Calimesa, California, wakaanzisha Jumuiya ya Uchapishaji ya Ulimwengu, DSDA, na walioachwa nyuma waliungana na Mt. Dale, muungano wa kwanza katika Davidia. Muungano huu ulipigiwa hesabu, maana duka la kuchapisha la Mt. Dale lilikuwa limeharibiwa kwa kuchomwa moto na watenda kazi wa SDA, na Yucaipa ilikuwa na

Aprili – Mei – Juni 2021 | Msimbo wa Nembo, Gombo 2021, Nam. 4, 5, 6 | Ukurasa 13  wa 48

matbaa bora. Aina hii ya muungano utaonekana tena hivi karibuni katika Davida, wakati wafungwa wa mafundisho haya ya uongo wanawekwa huru kutoka kwa anamu zao wanapoanza kusoma taarifa kama hii:

“Je! Mwenendo wa Dhehebu uliopotoshwa wa kutafuta Ukweli uliofunuliwa na Mbingu hauthibishi kwako kwamba halimjali Mungu, kwamba badala Yake wamewekwa wale ambao wanastahili kuwa watumwa Wake? Inaweza kuwaje iwapo mwanadamu anaulizwa ushauri wakati ambapo Roho wa Mungu anapaswa kutafutwa? Je! Hatujaambiwa na Maandiko kwamba Roho Mwenyewe atatuongoza mmoja mmoja katika Kweli yote? Kwamba tusiufanye mwili kuwa kinga yetu kwa kumruhusu mtu mwingine atuamulie Ukweli ni nini na uongo ni nini? Je! Sisi hatumkani Roho na muunganisho wetu kwa Mbingu tunapochukua mbadala? Na bado iliyo mbaya zaidi ni kutafuta ushauri kwa mtu ambaye tayari yu dhidi ya lile unalotarajia akubali au asikubali. Iwapo Mungu anaweza kumfunza ng’ombe mmoja mmoja kutafuta maji katika nyanda za chini, na sio juu ya milima na vilima, na kutafuta mahali pa joto ambapo upepo hauvumi, basi kwa nini Yeye mwenyewe asiweze kutuonyesha kibinafsi Ukweli ni nini? na uongo ni nini?” {2TG41: 6.5} [459]

Katika 1991 amiba, Davidia, ilichipuka tena baada ya Kikao Maalum cha Mt. Dale cha 1991 kilipigia kura kuhamisha Makao Makuu hadi Waco, Texas. Nini kilichosababisha kugeuza kura ya Kikao cha Kawaida cha 1990 kutohamishwa hadi Waco, Texas? Jambo pekee nasema kwa wakati huo ni mazingira mazuri. Sikutaja kichipukizi cha 1988 kwa wakati huu kwa sababu nitafanya mtiririko wa chati ya kichipukizi baadaye. Hapa upo mtiririko wa kuona wa Davidia:

Flowchart of Davidan Movements, Associations and Groups.

Tangu 1955 hadi karibu 2008, migawanyiko mingi ya Davidia kamwe haikuwashtua wakazi, maana jina Davidia lilitumika kama muungano wa udanganyifu. Kisha kikaja kichipukizi Ukasisi wa Mganda wa Kutikisa ukionyesha wazi migawanyiko katika Davidia, ukileta Davidia karibu na mazigazi.

Ni hatari zipi za kukaa katika Davidia? Ya kwanza, mafundisho ya uongo yanayofundishwa humo; na haya yanaweza kuwa yapi? Hapa yapo baadhi yake: 1) Malisho ya kiroho ni maeneo ya makao makuu. 2) Karmeli ulinyauka. 3) Ndugu Houteff, kabla ya mauti yake, aliagiza Mlima Karmeli wa Uakisi wote uuzwe. 4) Hotuba za Msimbo wa Nembo Mpya zilizochapishwa na Dada Houteff na washirika ni hotuba zilizowasilishwa na marehemu Ndugu Houteff. 5) Taabu ya Yakobo itatukia kabla ya Kanisa kutakaswa. 6) Muungano wa Ashuru sio muungano wa kanisa na serikali wa “Alama ya Mnyama.” 7) Hatuko

Aprili – Mei – Juni 2021 | Msimbo wa Nembo, Gombo 2021, Nam. 4, 5, 6 | Ukurasa 14  wa 48

School Of The Prophets Advert Of The Symbolic Code 2021

katika saa ya kumi na moja ya Kanisa. 8) Vuguvugu la Wadaudi si kanisa. 9) Ipo sehemu moja pekee ya malimbuko ya mavuno ya walio hai, watakaohamishwa bila kuonja mauti, kwa hivyo ukakaso mmoja pekee katika Dhehebu la SDA. 10) Kuchagua maafisa kwa kura ya washarika na kuungana. 11) Kulitesa kanisa la SDA na mbinu za Florence Houteff, kusambaza vitabu mbele ya makanisa, mikutano ya kambi, makongamano ya Baraza Kuu, etc. 12) Ndugu Houteff ni Eliya, Daudi, Yoshua, Zerubbabeli wa Uakisi, n.k. 13) Chemchemi ya Zekaria Sura ya Tatu imefunguliwa kwa Nyumba ya Daudi. 14) Chati zilizobadilishwa za Zekaria Nne na Ezekieli Arobaini na Saba. 15) Kutunza siku kuu za mfano. 16) Watu 144,000 pekee wataokolewa kutoka katika dhehebu la SDA.

Ya pili, hautakuwa tayari Bwana arusi ajapo. Ya tatu, hautamtambua Eliya wa uakisi:

“Na iwapo yeyote ataweza kukwambia kwamba nabii wa awali ametimiza ahadi hii, ingawa nabii mwenyewe hajanena hivyo, basi pasipokujua kwa hakika kwamba kama hao hawamfanyii kazi Mungu wa Eliya, bali ibilisi, ni Ulaodekia wa aina mbaya sana.”{GCS: 23.1}

Kwa sababu upo Davidia, basi lazima liwepo jina na vuguvugu la kweli, maana lilipo la uongo, lazima liwepo la kweli. Hebu tuisikie Fimbo:

“Kwa mfano: Hata majina ya kibinafsi ya mababu, ambayo mavuguvugu mbalimbali ya zamani yalitajwa kwayo, yalibadilishwa kadiri muda ulivyoendelea. Abramu, unakumbuka, katika mchakato wa wakati aliitwa Abrahamu; na Yakobo aliitwa Israeli. Basi, pia, Kanisa la wakati wa Musa liliitwa Waisraeli, wakati wa Kristo liliitwa Yudea, na baada ya hilo la Kikristo. Hatimaye ukafika wakati ambao liliitwa ama Katoliki au la Kiprotestanti. Kisha ama la Walutheri au jingine fulani. Kila mmojawapo la haya lilikuwa uzao wa lile la zamani. Sio wale ambao hubakia nyuma, ila wale ambao huenenda pamoja na jumbe za Mungu, kadiri wakati unavyoendelea, daima hutambuliwa na Mbingu kama Kanisa.  {2TG34: 24.1} [430]

“Mwanzoni mwa kila ujumbe watu ambao walisonga mbele na Ukweli walikuwa washiriki mmoja mmoja wa kanisa ambalo lilikuja kuwa kanisa kwa njia ya kuupokea ujumbe, ujumbe ambao mwasisi wake aliuleta. Kwa mfano, kanisa lote la Kiyahudi halikuja kuwa kanisa la Kikristo, lakini kanisa la Kikristo liliwakokota washiriki wake kutoka katika kanisa la Kiyahudi na kuwaleta katika Ukweli ulioendelea, Ukweli mwafaka haswa kwa ajili ya wakati na watu wa wakati huo. {2TG34: 24.2} [430]

“Jinsi tunavyoishi sasa katika wakati wa Ufunuo, katika wakati wa kufunuliwa kwa unabii ambao huonyesha kuanzishwa kwa Ufalme na vile vile kwa ujio wa pili wa Kristo, Kanisa wakati huu, kwa hivyo, haliwezi kwa busara kuitwa kwa jina lingine isipokuwa jina ambalo linafaa awamu yake ya sasa (ya juu) ya kazi ya injili. {2TG34: 24.3} [430]

“Kwa udhahiri, basi, jina lake lazima lionyeshe kweli ambazo huzitetea: yaani, kuzishika amri, ujio wa pili wa Kristo, na pia urejesho wa Ufalme wa Wadaudi kwa mujibu wa unabii. Kwa hivyo jina la busara ambalo linawakilisha kazi yake kuanzia wakati huu hadi kwa wakati Ufalme unapoanzishwa, litakuwa Wadaudi Waadventista wa Sabato, — jina ambalo hushuhudia ujumbe wa Ufalme, kuzishika amri ambazo ile Sabato ya siku ya saba ni sehemu yazo, na ujio wa pili wa Kristo.  {2TG34: 24.4} [430]

“Sasa unaona kwamba kila Ukweli wa nyongeza mwafaka huleta jina la nyongeza mwafaka. Na wewe ambaye hujabatizwa katika jina la Kanisa, ila katika jina la Kristo kupitia Ukweli wa Roho, wewe ambaye hujafungwa kwa mtu yeyote, ila kwa Kristo, huwezi kumudu kuendelea na Roho ya Unabii Ambayo huufunua Ukweli na kuwapa jina watu Wake. Hutaweza kwa hivyo, kumudu kusimama kwa utulivu, kuota ndoto ya kwamba u tajiri na umejitajirisha, hauhitaji chochote ilhali kwa kweli wewe ni maskini na uchi kiroho. Na utakaa hivyo iwapo utapuuza kuendelea na Ukweli wa

Aprili – Mei – Juni 2021 | Msimbo wa Nembo, Gombo 2021, Nam. 4, 5, 6 | Ukurasa 17  wa 48

wakati huu.” {2TG34: 25.1} [431]

Hadi Ufalme utakaposimamishwa, jina la Kanisa la Mungu ni “Wadaudi Waadventista wa Sabato”, sio “Davidia.”

Come Out Of Davidia

“Iwapo Kristo kwa kuyakusanya makanisa haya saba katika kundi la vinara saba vya taa na kutoa rekodi chafu kabisa kwa lile la mwisho, Yeye hawaiti Walaodekia Babeli, basi wala ufasiri wa “vichwa” haufanyi hivyo. Si kwa sababu Walaodekia ni bora hivi kwamba hawajaitwa Babeli, kwa sababu rekodi yao ni mbaya zaidi, lakini ni kuonyesha kwamba kwa mujibu wa nuru yao iliyoongezeka, Yeye atashughulika nao kwa njia tofauti. Ni ya kudhihirisha kwamba iwapo “malaika” (uongozi) wa kanisa la Walaodekia ataukataa ujumbe wa “Shahidi wa Kweli,” Yeye hawezi kuwaita watu 144,000 kutoka kati yao kuingia katika vuguvugu lingine kwa mwito wa Ufunuo 18. “Tokeni kwake enyi watu Wangu, msishiriki dhambi zake, wala msipokee mapigo yake,” (Ufu. 18:4), lakini badala yake kwa ujumbe wa Ufunuo 7 na Ezekieli 9. Hivyo kuwafungua watu Wake, na kwa haraka “Atakamilisha kazi na kuifupisha katika haki: kwa maana kazi fupi Bwana ataifanya katika nchi.” (Rum. 9:28.) {SR2: 94.2} [88]

Advert Of Isaiah 2:22 In

Aprili – Mei – Juni 2021 | Msimbo wa Nembo, Gombo 2021, Nam. 4, 5, 6 | Ukurasa 18  wa 48

SHULE YA KIKOSI CHA MBELE, KENYA

Historia ya Shule ya Watangulizi Kenya hurejea nyuma Julai 2013 baada ya mkutano wa siku kumi uliyoendeshwa na Ndugu Lennox Sam, uliofanyika Rongai, Kenya. Liligundulika hitaji la dharura la kuwa na shule ambayo watoto Wadaudi wangefunzwa kulingana na kanuni za mbingu. Dada Beatrice Owitti aliamua kuasisi mradi huo, na shule ikaanzishwa na binti yake, Ellen Gould, akiwa mwanafunzi pekee. Darasa lilikuwa nyumba iliyokodiwa kama kituo cha shughuli za Jumuiya iliyokuwa imeanzishwa ya Ukasisi wa Mganda wa Kutikisa nchini Kenya.

Baraka hii Ellen hangeifurahia kwa muda mrefu yeye pekee. Wanafunzi wengine, ambao wazazi wao walikuwa na hamu kuvuna baraka hiyo, walijiunga nayo muda mfupi baadaye, kuthibitisha: Philip Mzee Daniels, Gilbert Mogoi and Bildad Mogoi. Baraka zilikuwa zinatiririka, na wengi walikuwa wanagundua wao na watoto wao wadogo walikuwa wanakosa hizi baraka!

Pamoja na ongezeko la idadi ya wanafunzi, lilikuwapo hitaji la kuongeza wafanyakazi. Dada Deborah Cheruiyot alijiunga na shule kama mwalimu na Dada Felister Wambua aliingia kama mpishi mwasisi. Shule wakati huo ilikuwa kituo cha bweni, na ilikuwa inakua haraka.

Kuongeza usajili shuleni kwa siku na maelfu ya shughuli zingine za Kanisa zikafanya mahali pale kuwa padogo sana, na sehemu kubwa ya kituo cha shughuli ilitafutwa katika mtaa huo. Uaminifu wa Bwana uliandaa sehemu moja iliyokuwa karibu Februari 2014.

Tuliona idadi ya wanafunzi ikiumuka hadi zaidi ya hamsini katika eneo hili jipya, shukrani kwa mpango na viongozi wa Kanisa kwa kuwaita watoto wa waamini wa Ukweli wa Sasa kusajiliwa. Wakati huo tulikuwa na wafanyakazi kumi na moja: Mwalimu mkuu:

Dada Beatrice Owitti; Naibu Mwalimu mkuu: Ndugu Dennis Mutiso; Walimu: Ndugu Joshua Cheruiyot, Michael Murunga, Patrick Omogi, Felix Ombasa, Ezekiel Tunya, kina Dada Sophiey Tunya, Agnes Mueke, Lydia Odero na Deborah Cheruiyot; na Wapishi: Ndugu Albanus Wambua na Dada Lilian Omogi.

Mwaka 2015 ulipokaribia kufunga, Bwana aliibariki Tarafa ya Kenya na ardhi yenye ekari kumi na sita na nusu kule Ochoria, Kaunti ndogo ya Muhoroni, Kaunti ya Kisumu (zilivyoonyeshwa kwenye mpango hapo juu). Majengo yasiyo ya kudumu yalijengwa haraka kuiifadhi shule maana lilikuwapo hitaji la dharura kuhamishwa.

Kisha shule ilihamishiwa kwenye ardhi mpya iliyokuwa imenunuliwa ambako ipo mpaka leo. Wanafunzi wengi wamehitimu kutoka Shule ya Kikosi cha Mbele na matokeo mazuri na kujiunga na shule zingine za upili katika nchi. Tunampa Mungu utukufu na heshima.

Marekebisho makubwa ya shirika tangu wakati huo yamefanywa na wafanyakazi kwa sasa ni kama ifwatavyo: Meneja wa Kambi: Ndugu. Isaac Misiani; Mhazini: Ndugu Nelson Getanda; Mwalimu Mkuu: Dada Nerries Nyaga; Naibu Mwalimu Mkuu: Dada Vane Osiemo; Walimu: Ndugu Ezekiel Tunya, kina Dada Agnes Mueke na Sophiey Tunya; Manaibu Walimu: kina Dada Patience Kamene na Karen Nyamvula; Wapishi: Ndugu Geoffrey Kamwara na Dada Pauline Andeso; Mlezi: Ndugu Benard

Aprili – Mei – Juni 2021 | Msimbo wa Nembo, Gombo 2021, Nam. 4, 5, 6 | Ukurasa 19  wa 48

Momanyi; Mlezi wa kike: Dada Immaculate Wangui; Wachapa kazi Shambani: kina Ndugu Elvas Maritim, Emmanuel Imbali na Charles Mwai.

Usajili wa sasa hujumuisha wanafunzi walioenea kote katika madarasa tisa ya kiwango cha msingi. Kwa kuufanya mzigo wa mzazi kuwa mwepesi iwezekanavyo, tumeweka ada ya mafunzo dola za Marekani thelathini na tano kwa kila mwezi, zikigharamia chumba, malazi, kufua nguo, vyakula, na kila kitu! Isitoshe, kwa kuufuata mfano wa Msamaria mwema, taasisi hii huchukua jukumu kamili kwa gharama za watoto ambao wazazi wao hawawezi kabisa kulipia chochote kwa ajili ya utunzi wa watoto wao ili kwamba mtoto wa kila msharika apate fursa ya kupata elimu ya Mdaudi Mkristo. Mkoba huu wa Msamaria pia hufadhiliwa kwa mfuko wa udhamini ambao washarika wote wanaweza kushiriki.

Shule kwa sasa ina uwezo kamili wa wafanyakazi na wanafunzi, na iwapo tunaweza kuyaongeza majengo yetu na hivyo kutoa makazi kwa wanafunzi wachache zaidi, twaweza kuwaleta ndani zaidi. Usajili ukiwa kwenye mwendo unaopanda, tunaitazama shida ambapo wanafunzi wanaweza kutoruhusiwa kuingia kwa ukosefu wa makao. Ili kwamba hili lisitukie, tunatoa mwito kwa sala na michango yenu, maana hivi karibuni

tutahitaji majengo ya kudumu kwa makao na madarasa yachukue nafasi ya yale ya muda yanayotumika kwa sasa.

Kufikia sasa, vyoo vya shimo sita vya kudumu vilijengwa mwaka uliopita, na tunapanga hivi karibuni kuanza ujenzi wa jiko na ukumbi mkubwa na ofisi za kudumu ili kupunguza hali ya msongamano na kurahisisha kazi kwa ujumla.

Tunapotazama mbele kwa ukubwa wa kazi inayosubiri kufanywa, inaonekana kwamba tunakwenda kwa mwendo wa konokono hadi sasa katika kufanya maboresho muhimu. Hata hivyo, hili huongeza kwa ujasiri wetu na ukweli kwamba kila idara ya ujumbe wa kutia muhuri imekuwa na mwanzo mdogo sana na wa polepole lakini thabiti. Hakika, ni kama mbegu ya haradali, bali kwa mujibu wa Neno, maboresho yatakapokamilishwa, zitakuwa kama mmea wa haradali, mkubwa kwa mimea yote.

Kwa vile shule ni yako na haina msaada kwa mwingine ila wewe, kwa hivyo ni lazima kwamba ujitwike mzigo wake wa kifedha; iwapo taasisi yenyewe italitekeleza jukumu lake kubwa la kuikamilisha kazi teule ya Mungu ya kuwakusanya ndani na kuwaelimisha watoto wako. Usithubutu kushindwa katika hili na hivyo kumruhusu adui wa Mungu na mwanadamu ashinde. Na tunayo imani yote kwamba hautaruhusu hili litukie, maana watu 144,000 “watafanya agano Naye kwa dhabihu.” Kama shule, tunajitahidi, Ndugu na Dada, kuwaokoa watoto. Je! Wewe, dhidi ya mapenzi ya Mungu, utawaacha waangamie katika “maangamizo ya jumla,” yote kwa sababu ya “kupenda ubinafsi wa mimi na yangu?”

Aprili – Mei – Juni 2021 | Msimbo wa Nembo, Gombo 2021, Nam. 4, 5, 6 | Ukurasa 20  wa 48

Tumekuwa pia tukiiendesha bila umeme tangu tulipohamia eneo letu jipya, chanzo chetu cha umeme kikiwa jenereta, ambayo ni ghali mno. Ombi la muunganisho kwa mfumo umeme wa taifa lilifanywa Aprili, usoroveya ulifanywa na kampuni ya umeme Mei, na tukapewa dondoo ya malipo takribani $18,545 Juni. Ni ghali mno kwa sababu tuko zaidi ya kilomita moja mbali kutoka kwa fito umeme iliyo karibu. Unapomkaribia Baba wa Mianga, utukumbuke, tulio katika giza la usiku, ya kwamba Awashe taa za umeme. Pia, kumbuka kuuombea mradi wetu wa maji safi.

Ardhi ni yenye rutuba na katika nyanda ambazo mvua ni ya kutosha kwa mwaka mzima. Upo tu msimu mmoja mfupi wa karibu mwezi mmoja ambao mvua haishuhudiwi, lakini katika msimu huu unyunyiziaji maji hufanywa kutoka katuka Kipchoria ambao hupakana na ardhi. Pia hujulikana kama “mto usiokauka kamwe.”

Shughuli kadhaa zimefanyika katika idara ya shamba, zikiwa ni pamoja na kufyeka vichaka, kujenga matuta (kuchimba mitaro), kulitayarisha shamba kwa upanzi, kupanda aina mbalimbali za mazao (viazi mbatata, sukuma, malenge, ndizi, vitunguu, matango, kokwa siagi, alizeti, mipapai, n.k.), kuvuna, na kuhifadhi.

Crops have produced good yields and are helping us have a balanced diet.

Tumeongeza uzalishaji mwaka baada ya mwaka, na Bwana kwa ajabu ameibariki kazi. Tunayo mazao yaliyopangwa kwa namna mbalimbali, ingawa kwa sababu ya vizuizi vya kuchapisha hatuwezi kila jambo katika picha hizi.

Jaribio letu la kwanza kwa nyanya lilifanywa mwaka huu na linaonekana la ufanisi. Mavuno yatasaidia kupiga jeki idara ya Biashara kwa sababu wakazi wa kambi hawawezi kutumia mavuno yote. Msifuni Mungu ambaye baraka zote zatoka Kwake!

Aprili – Mei – Juni 2021 | Msimbo wa Nembo, Gombo 2021, Nam. 4, 5, 6 | Ukurasa 21  wa 48

HISTORIA YA WADAUDI NDANI YA KENYA

USHUHUDA WA KIBINAFSI

Salamu za Kikristo!

Ujumbe wa Fimbo ya Mchungaji ulianza kuvuma hapa mwishoni mwa miaka ya 1970. Nalijifunza kutoka kwa Ndugu Charles Oyando, aliyenijuza Fimbo, ya kwamba alianza kusoma vitabu vya Fimbo katika mwaka 1983. Alikuwa mwajiriwa wa kanisa la S.D.A. wakati huo katika makao makuu ya shamba la Magharibi mwa Kenya mjini Eldoret. Ni hapa, katika ofisi ya kanisa, alikopata ujumbe wa Fimbo kupitia vijitabu viwili vilivyochapishwa na Jumuiya ya Yucaipa. Kimojawapo kilikuwa na kichwa “Hukumu ya walio Hai, Vipi na Lini?” Jinsi vijitabu hivi viliingia katika ofisi ya kanisa; hajui hadi leo.

Ilikuwa kwa kusoma kijitabu kilichotajwa hapo juu ndipo macho yake yakafumbuliwa kwa Ukweli kuhusu hukumu ya walio hai. Alivutiwa sana hivi kwamba alichukua anwani kwenye jalada la nyuma na kuwasiliana na wachapishaji. Aliendelea kuwasiliana nao hadi mwaka 1985/1986, walipomtumia anwani mpya na kumwelekeza kwa Jumuiya ya Mountain Dale. Alipokea makasha ya vitabu na pia alikuwa na mawasiliano ya kawaida nao.

Katika mwaka 1995, nalipata vitabu kadhaa vimejaa vumbi katika nyumba ya Ndugu yangu mkubwa. Nikakiokota kimojawapo na kuanza kusoma; sikujua kwamba nalikuwa nikisoma kitabu cha Fimbo. Hivi vitabu vilinipa ari ya kusoma Biblia na maandishi ya Dada White. Jambo moja lilikuwa wazi akilini mwangu: Hivi havikuwa vitabu vya kawaida; vilikuwa vikielimisha sana na vilikidhi mahitaji yangu ya kiroho ya wakati huo na ya muda mrefu.

Wakati fulani baadaye mwaka uo huo, Ndugu Charles Oyando alinialika kwa mafunzo ya Biblia katika nyumba alimokuwa akiishi na Ndugu Elijah Natili, ambaye pia alikuwa mwamini wa Fimbo. Sote tulikuwa waajiriwa katika Chuo Kikuu cha Afrika Mashariki, Baraton; taasisi ya S.D.A. ya elimu ya juu. Tulijifunza “Wanyama” wa Dan. 7 na Ndugu Oyando alionyesha wazi mafundisho yenye makosa yanayotangazwa rasmi na kanisa na walimu wa unabii kwa ujumla: kwamba mabawa huwakilisha kasi na mbavu huwakilisha falme ambazo hazikutekwa na

Wamedi. Siku iliyofuata tulijifunza Ufu. 7 na akaonyesha tena mafundisho potofu ya kanisa kuihusu sura hii: kwamba namba 144,000 ni nembo.

Baada ya fundisho hili alinipa Msimbo wa Nembo wenye kichwa “Orodha ya Machukuzo ya Kuugua na Kulia Dhidi Yake,” uliochapishwa na Jumuiya ya Njia ya 2500, Mlima Karmeli. Baadaye alinipa trakti kadhaa za Fimbo baada ya kusadiki kwamba sikuwa na pingamizi kwa yale aliyokuwa amewasilisha hadi hapo. Tuliendelea kujifunza, na mwishowe aliweka wazi kwamba vitabu tulivyokuwa tukisoma vilikuwa ujumbe wa Fimbo uliotabiriwa katika Mika 6:9. Nilipoisoma aya hiyo, ari yangu katika ujumbe iliongezeka maradufu, na naliomba vitabu zaidi; alinigawia chochote alichokuwa nacho. Hii haikumpendeza ndugu yangu mkubwa, na nalianza kujifunza Fimbo kwa siri hadi wakati alipoipoteza kazi yake katika mwaka 1996 chini ya hali za kiajabu. Aliondoka kwenye taasisi hiyo, na nalilazimika kutafuta nyumba yangu mwenyewe; hii ilinipa fursa ya kuisoma Fimbo bila macho ya kudadisi.

Februari 27, 1997: Ndugu aitwaye Errol Stanford aliwasili Kenya na akaja katika Chuo Kikuu cha Baraton katika mwezi Machi. Ndugu Oyando alikuwa amehama katika taasisi hiyo na nalimpa hifadhi. Mafunzo yote yaliendeshwa katika nyumba hii. Kadiri idadi ilipoanza kuongezeka, adui alighadhibishwa na akawaajiri mawakala wake kutupeleleza. Walitaka kujua mtu huyu Mmarekani alikuwa nani, alikuwa na lengo gani, na ni nani waliokuwa wanahudhuria mikutano. Ilianza kufahamika kwa utawala wa taasisi hiyo kwamba Ndugu Oyando alikuwa akimhifadhi mwalimu Mdaudi kutoka Marekani, na ya kwamba baadhi ya washarika wa kanisa walikuwa kwa uaminifu wakihudhuria mikutano. Tuliitwa mbele ya mchungaji wa kanisa letu, kasisi wa chuo kikuu, na wasimamizi wetu wa karibu katika idara zetu katika kampeni ya kuonya, kutuwekea vikwazo, na kututia hofu ya kupoteza kazi zetu iwapo tungeendelea kuhudhuria mikutano. Baadhi ya ndugu walirudi nyuma na mbali na Ndugu Oyando na Natili, ni wanne tu tulisalia. Kati ya hao wanne, Ndugu yangu Franklin Webuye na Ndugu mmoja Peter wamepoteza ari katika ujumbe; binamu yangu, Ndugu

Aprili – Mei – Juni 2021 | Msimbo wa Nembo, Gombo 2021, Nam. 4, 5, 6 | Ukurasa 22  wa 48

Leonard Kochwa, ambaye alikuwa ameongoka wakati huo kwa imani ya Uadventista, sasa ni mchungaji huko Mountain Dale.

Ndani ya majuma mawili, taasisi yote ilihisi nguvu ya Fimbo, na viongozi wa kanisa haraka wakabuni mpango wa kukomesha shughuli za Fimbo. Kila Sabato kwenye mimbari ilitolewa fursa ya shutuma dhidi ya Fimbo na wafwasi wake. Walisimulia bila tumaini kisa cha David Koresh na video za moto mkubwa huko Elk, Texas, lakini ujasiri wetu uliongezeka kila siku. Chuo kikuu chote kilisisimuka na kuamshwa – baadhi waliunga mkono ujumbe na wengine waliupinga.

Nakumbuka kwamba Sabato tatu ziliwekwa wakfu ili kufichua “mafundisho ya uongo” ya Wadaudi. Kila alasiri, uwanja wa michezo ulifurika kuliko hapo awali. Kama juhudi za pamoja za kukomesha na kupunguza shughuli za Fimbo, walimu wote wa theolojia na wanafunzi walitakiwa kuhudhuria; pamoja na wale wa kitivo walioonekana kuwa na uzoefu katika imani. Katika Sabato ya kwanza, walipanda jukwaani kwanza, na ndugu kutoka Kushi alijaribu kukanusha mafundisho ya Fimbo bila kufaulu: ilikuwa kupoteza muda tu na onyesho la bure.

Zamu yetu ilipokuja kuwasilisha, mkutano wote ulisisimka chini ya dakika 6. Kila mtu alitaka kunena jambo dhidi ya Ndugu Stanford na vuguvugu la Kidaudi. Nafasi yake ilikatizwa sana hivi kwamba hakuna jambo muhimu lililoshughulikiwa. Adui aliyapanga majeshi yake yote dhidi ya “Ukweli wa Sasa.” Yalikuwapo makelele kutoka ndani kumtaka yeye na wafuasi wake watimuliwe na kuzuiwa wasihudhurie ibada za kanisa. Naweza kukumbuka tukio moja baya ambapo mhadhiri mkuu alimwendea mbio Ndugu Natili, aliyekuwa akipiga picha, akanyakua kamera kutoka kwake na kuondoa mkanda wa filamu. Ilikuwa dhahiri kwamba Shetani alikuwa akiudhibiti kabisa mkutano.

Ndugu Stanford aliogopa kwamba tungekimbia kwa sababu bado tulikuwa wachanga katika ujumbe na katika mwanzoni mwa ujana wetu, bali Roho wa Bwana alikuwa juu yetu, na ujasiri wetu uliinuka na hali ilivyodai. Ndugu yetu alitiwa nguvu, lakini maagizo kutoka juu yaliamuru kwamba asiruhusiwe kuingia katika chuo kikuu na asipitie tena katika malango yake. Siku iliyofuata, Jumapili, tulipokea barua kutoka

kwa kasisi wa chuo kikuu akituita ofisini kwake, ambamo onyo kali lilitolewa dhidi ya mtu yeyote kuhudhuria mikutano ya Wadaudi. Maneno yake ya kuagana yalikuwa: “Acha kuhudhuria mikutano hiyo au sivyo mhatarishe kufukuzwa kazi.” Kilikuwa kisa kile kile katika kituo changu cha kazi Jumatatu; bwana wangu alifupisha jambo hili kwa muhtasari hivi: “Amatete, hatuwezi kukulisha chakula ilhali unatutupia mawe; nenda ufikirie maradufu kuhusu jambo hili la Udaudi.

Ndugu Oyando na Natili walikuwa wameshawishi Mountain Dale kununua kipande cha ardhi na kuanzisha makao makuu (kambi) ya shughuli nchini Kenya. Walifanya hili kuwa sharti la shughuli za Mountain Dale nchini. Ndugu Stanford alikuwa ametoka Marekani na lengo moja kwa mtazamo: kuendesha DLI kwa miezi mitatu na kisha arudi. Jumuiya ya Mountain Dale haikuwa na mipango wala makadirio ya kuanzisha kambi wakati huo, lakini Uvuvio ulikuwa unaamuru mambo kwa Hekima Yake Wenyewe, na wakati ulikuwa umekuja wa Mungu kuanzisha shughuli za Fimbo ndani ya Kenya. Kipande cha ardhi kilinunuliwa mnamo Aprili 1997. Ndugu Stanford alitupasha hiyo habari njema na kutuomba tusali na tujiandae kuondoka Chuo Kikuu cha Baraton tujitahidi kuendeleza kazi ya Bwana. Kwa furaha tuliupokea mwito huo – ilikuwa njia pekee ambayo Mungu angependezwa – kwa sababu dalili zote zilikuwa wazi kwamba uaminifu wetu kwa ujumbe ungeidhinisha tufutwe kazi.

Alhamisi, asubuhi na mapema, tuliondoka Baraton kuelekea Chimoi mahali ambapo ardhi ilikuwa imenunuliwa. Hapakuwa na jengo lolote kwa hiyo ardhi, vilikuwapo tu vichaka na miti michache ya asili. Tulikaa kwa muda katika makao ya Ndugu Natili ambayo yalikuwa jirani kwa hiyo ardhi na tulifanya kazi Kambini mwetu kutokea kwenye makao hayo kwa karibu miezi miwili, tulifyeka na kujenga majengo rahisi kutuwezesha kuanza. Kisha tukapokea barua kutoka kwa kanisa zikituarifu kwamba tulikuwa tumekaguliwa vitabuni na kutengwa na kanisa.

Naweza kusimulia kwa uzoefu kwamba kuasisi katika kazi ya Bwana si jambo rahisi hasa wakati ni lazima uanzie mwanzoni bila fedha. Tuliishi kwa imani, na Mungu alikuwa pamoja nasi. Tulikuwa na majengo matatu: kanisa, ambalo lilikuwa na nafasi ya jiko la muda na vyumba viwili vya kulala; bweni; na jengo moja ambalo lilipaswa kutumika kama jiko / ghala katika siku zijazo, na pia

Aprili – Mei – Juni 2021 | Msimbo wa Nembo, Gombo 2021, Nam. 4, 5, 6 | Ukurasa 23  wa 48

vyumba rahisi vya kuogea. Hivyo Kambi ilisimamishwa na kwa furaha ikaitwa Kituo cha Mlima Karmeli, Tawi la Kenya. Madarasa ya DLI yaliyokuwa yamesalia yaliendeshwa humo na yalikamilika mwezi wa Juni.

Muda mfupi kabla ya Ndugu Stanford kusafiri kwenda Marekani, tulikuwa na Bodi ya Wadhamini na kundi lililopangwa kikamilifu, na sisi wanne, waasisi, tulikuwa Watenda kazi wa Biblia. Tuliendelea kuitangaza Fimbo katika makanisa ya S.D.A. viungani mwa Kambi na mbali. Wachungaji wa S.D.A. na washarika wa kanisa walihisi “joto” la ujumbe kwa maana tulikuwa tumekamilisha masomo yetu ya DLI, kwa hivyo tulikuwa “moto sana,” kwa mfano.

Neno lilisambazwa kwamba “kikundi cha vichipuko kimejianzisha na ya kwamba walikuwa wametimuliwa kutoka Chuo Kikuu cha Baraton baada ya kuanzisha uasi dhidi ya kanisa na taasisi hiyo; basi jihadharini nao.” Tuliendeleza “kuhusuru,” Bwana alifanikisha juhudi zetu dhaifu, na tuliongezeka kwa idadi katika sehemu mbali mbali za nchi.

UKWELI WA ENEO MAALUM

Wakati mwingine wa maamuzi ulikuja katika mwaka 1999. Hadi hapo, hatukuwa tumesikia kuhusu mavuguvugu mbali mbali ya Kidaudi. Asubuhi moja Ndugu Natili alikuja na wazo lenye lengo na kumuuliza Ndugu Kochwa na Mimi iwapo tulikuwa tunajua kwamba yapo Makao Makuu Mawili katika vuguvugu la Kidaudi – na yawezekana yapo mengine – na ya kwamba moja linapingana na lingine katika mafundisho: haswa kuhusu eneo maalum la makao makuu ya kweli, na iwapo chemchemi ya utakaso ya Zek. 13 imefunguliwa au la.

Asubuhi iliyofuata, alikuja na vijitabu vya Waco na vya Mountain Dale vilivyogusia maswala hayo mawili ya mafundisho. Aliweka wazi kwetu kwamba Jumuiya hizi mbili zilikuwa zinapigana juu ya maswala haya na ya kwamba wito wa umoja ulikuwa umeshindwa. Nalianza kudurusu hati hizo hatua kwa hatua. Katika kudurusu kwangu kwa kawaida, ilikuwa dhahiri kwamba ndugu wa Waco walikuwa sahihi kwa msingi wa Neno lililoandikwa, na ya kwamba ndugu wa Mountain Dale walipungukiwa na walitumia ustadi mwingi ili nadharia zao zisimame. Walionekana kuwa wazuri sana kupuuza maana, kuondoa na kuongeza kwa taarifa za mamlaka sana katika Fimbo, na kutumia taarifa za Roho ya Unabii ambazo zilionekana kuwa zinaaminika kuunga mkono nadharia zao. Sikumaliza kudurusu kwangu hadi baadaye wakati mambo yalichukua mwelekeo tofauti.

Ilitukia kwamba katika mwaka uo huo, Ndugu Arthur, Anthony Hibbert na Terry Harrison wa Mountain Dale walikuwa kwa utume wa kuzuru na kuwatia moyo washarika wao katika Shamba la Afrika. Ilitokea kwamba Ndugu Norman Archer wa Waco pia alikuwa kwa utume wa kuwafikia washarika wao katika Shamba la Afrika, akitoa mwito wa umoja katika “Davidia.” Nyuma ya pazia, Ndugu Oyando na Natili walikuwa wamemwandikia Ndugu Archer kumwalika azuru Kenya. Kwa Ndugu Archer, hili halikuwa jingine zaidi ya “habari njema” kwa maana alikuwa anajua kabisa kwamba Mountain Dale tayari walikuwa wamekita mizizi nchini. Ilimpa fursa ya kuwageuza-imani ndugu wa Mountain Dale.

Ndugu Archer aliwasili nchini akitokea Zambia na Ndugu Natili na Webuye walimpokea kutoka Uwanja wa Ndege; walielekea moja kwa moja Kambini. Walipofika, alisisimka sana, na maneno ya kwanza yaliyotoka kinywani mwake yalikuwa mwito wa umoja katika “Davidia,” haswa kati ya Mountain Dale na Waco. Kisha akagusia masuala mawili ya ubishani: eneo maalum na chemchemi. Tulimsikia tukaanza kuona nuru na tukasadiki. Mambo haya yote yalikuwa yakitukia Ndugu Hibbert na Terry walipokuwa nchini Zambia.

Kwa msingi wa kusadikishwa kwetu “kwa muda,” neno lilifika Mountain Dale kwamba Ndugu Archer alikuwa amevamia Kambi yao na kuwaongoa washarika wote na ndugu kwa mafundisho yake. Ndugu Hibbert alituandikia kwa uhakikisho kwamba watakuja kulishughulikia jambo hilo. Wakati uo huo, Ndugu Archer aliondoka kwenda Zambia, akijua kwamba Kenya ilikuwa eneo lao jipya.

Ndugu Hibbert na Terry mwishowe waliwasili kutoka Zambia na, bila kupoteza muda wowote, waliitisha mkutano na ndugu wote. Ndugu Hibbert “alilishughulikia” jambo hilo kama alivyoahidi. Mwito ukafanywa, na sote tukabadilika kurudi Mountain Dale. Tena, habari ilimfikia Ndugu Archer, ambaye tayari alikuwa amerudi Marekani, kwamba ndugu wa Kenya walikuwa wameshawishwa kurudi Montain Dale. Kwa maendeleo haya mapya, Ndugu Archer aliomba radhi kwa kutozama katika maelezo wakati alikuwa Kambini maana alisadiki kwamba yote yalikuwa shwari, lakini aliahidi kutuma maelezo yote yaliyoshughulikia masuala hayo mawili.

Maelezo yalitumwa, na tukarejea

Aprili – Mei – Juni 2021 | Msimbo wa Nembo, Gombo 2021, Nam. 4, 5, 6 | Ukurasa 24  wa 48

mezani, tukasoma kwa uangalifu kila jambo juu ya suala hili. Baada ya kugundua kwamba Waco walituma maelezo, Mountain Dale mara moja wakatuma yao pia. Mvutano dhahiri kati ya hizi Jumuiya mbili ulijulikana vyema, na ilikuwa dhahiri kwamba ulikuwa na athari kwa ndugu. Waasisi wanne waliokuwa wanaishi Kambini wote walisadikishwa kwamba Waco walipata alama juu ya masuala haya kwa msingi wa yale yaliyoandikwa katika Fimbo na ya kwamba Mountain Dale walikuwa na sufuri, lakini baadhi walikabiliwa na lile lingewapata kama Watenda kazi wa Biblia, ikizingatiwa kwamba hayakuwapo matarajio ya Waco kumwajiri mtu yeyote.

Lakini wakati ulikuwa umekuja Mungu kuchukua hatua nyingine na wale waliokuwa na nia na tayari kusonga mbele katika ngazi ya Ukweli bila kujali matokeo. Sikusita na nikatangaza msimamo wangu mbele ya waasisi wenzangu kwamba Waco ndio mahali pa kuwa kwa mujibu wa “Bwana asema hivi.” Naliendelea kusimulia usadikisho wangu, na waongofu wetu walionekana kuelewa yale yaliyokuwa yakikunjua mbele yao. Ikawa lazima kwetu kuitisha mkutano wa jumla kwa washarikam wote walichunguze upya jambo hili.

Ndugu Natili na Mimi tulikuwa watoa hoja wakuu wa mawasilisho hayo. Aliwasilisha kwanza, nami nikawasilisha mwisho; kisha mwito ukafanywa, na ndugu wakachukua misimamo yao juu ya jambo hilo. Ndugu waliunga mkono Waco kwa wingi. Mountain Dale walikuwa na waunga-mkono wanne tu, na kati ya hao, watatu walikuwa waasisi ambao walisadikishwa kwa Ukweli katika mioyo yao. Bado, suala la papo hapo lililowakabili lilikuwa ajira yao, ikizingatiwa kwamba Waco hawakuwa na ofa yoyote. Kwa ufupi, Mountain Dale walipoteza yote.

Pamoja na mgawanyiko huu uliodhihirika, Kambi ilikuwa hainistahimili. Ilikuwa dhahiri kwamba ilibidi nianze kujiandaa kuondoka haraka iwezekanavyo. Barua za aina zote zilitumwa Makao Makuu ya Mountain Dale zikinishtaki kwa kuwashawishi ndugu kuhamia Waco. Naweza kukumbuka shtaka moja duni kwamba Ndugu Archer alinihonga $ 100. Huu ulikuwa uongo. Ndugu Archer bado yu hai na anaweza kutoa ushahidi kwa jambo hilo.

Ndugu Stanford aliandika barua nyingi akinisihi niache [imani niliyokuwa nayo] na nifanye kazi ya kukomesha shughuli za Waco nchini Kenya. Barua hizo zilikuwa za sifa ya kuniponza na kunifanya nijihisi mwenye hatia. Nalisisitiza kwamba yote niliyofanya

yalikuwa tu kuwasilisha, na wote waliitwa kuchukua misimamo yao. Hili halikumshawishi. Kisha nikawaandikia Waco kuhusu maendeleo ya hivi punde, na wakachukua hatua baadaye.

Ndugu Maswabi Samutumwa, mchungaji wa Waco kutoka Tarafa ya Zambia, aliitwa asafiri kuja Kenya na kutupanga. Aliwasili nchini Disemba na baadaye akaenda Kambini. Tulipanga mkutano mwingine, na ndugu wote waliombwa kuhudhuria. Mchungaji alifanya wasilisho pamoja na vipengele vya ziada vilivyogusa historia ya Udaudi. Kama mkutano wa kwanza, wote walichukua msimamo na Waco isipokuwa wale ndugu wanne. Baada ya mkutano huo ilikuwa lazima kwetu kujipanga kama kundi la Waco. Mchungaji aliongoza uchaguzi na kusimika Bodi mpya ya Wadhamini.

Nalikuwa nimepanga kutoka Kambini nihamie mji ulio karibu wa Webuye kufikia Januari 1, 2000, kwa uwezekano wa njia yoyote ya kujitafutia riziki na kuendelea katika kazi ya Bwana – sikujua kwamba Makao Makuu ya Waco yalikuwa yakinuia kuniajiri kama Mtenda kazi wa Biblia kuanzia tarehe iyo hiyo kwa Makao Makuu yao Nairobi! Baadaye, Bodi ya Wadhamini iliitisha kikao cha bodi na kupiga kura Ndugu David Wamalwa (sasa mchungaji wa Waco 2500) ajiunge nami Nairobi kama Mtenda kazi wa Biblia. Kazi ilifanikiwa jijini Nairobi na viunga vyake, maeneo ya Mashariki na Naivasha, na sehemu ya Magharibi mwa Kenya yalikoanzia yote – na kazi imeendelea kustawi tangu wakati huo.

MGANDA WA KUTIKISA 2013/2014

Mwaka 2013 ulitia alama sura mpya tena kwa shughuli za Fimbo ndani ya Kenya. Jumuiya zote, Njia ya 2500 Mlima Karmeli na Mountain Dale zilipoteza washarika wao wengi kwa “Ukasisi wa Mganda wa Kutikisa” wakati huo na sasa “Jumuiya ya Wadaudi Waadventista wa Sabato” Uvuvio ulipokikunjua chuo kwa kufunua Ukweli wa utakaso wa kanisa katika sehemu mbili, kama ulivyoonyeshwa katika “sheria na shuhuda.” Jumuiya mpya ilizaliwa, na sasa mimi ni sehemu yake. Ndugu wa Njia ya 2500 Kituo cha Mlima Karmeli walijaribu kunibembeleza nirudi huko, lakini nalikuwa sipatikani – Ukweli ulikuwa umeniweka kwa jukwaa tofauti hakika; Naomba kwamba nisianguke kutoka njiani.

Hii ni historia ya Vuguvugu la Udaudi nchini Kenya tangu mwaka 1983 hadi 2013 kadiri ninavyoweza kukumbuka.

Aprili – Mei – Juni 2021 | Msimbo wa Nembo, Gombo 2021, Nam. 4, 5, 6 | Ukurasa 25  wa 48

Ni mimi pekee kati ya waasisi ambaye niko katika Jumuiya ya Mungu leo, na ombi langu ni kwamba Mungu atawaongoza wenzangu katika Kweli yote ili tuweze kuwa kitu kimoja tena kama tulivyokuwa mwanzoni. Ndugu Natili tangu wakati huo aliutema ujumbe, lakini nilikutana na kuzungumza naye katika mwaka 2014; hakuwa na taabu kwa yale niliyowasilisha lakini hakuwa na nia katika shughuli za Fimbo. Ndugu Weslay Mochama nami tulikutana na Ndugu Oyando katika mwaka 2014 lakini ilionekana kwamba haukuwa wakati wake wa kuufahamu ujumbe katika umbo lake la upeo; Nalikutana naye mwaka huu mwezi wa Februari, na alionekana kuwa msikivu na tayari kuupokea sasa.

Kwa ukosefu wa nafasi na wakati, nimewasilisha tu mambo muhimu kwa muhtasari. Bwana mwema abariki na kufanikisha shughuli za Fimbo safi kote ulimwenguni.

Ndugu yenu katika Kazi ya Bwana wetu Mpendwa Yesu,
Edwin A. Amatete,
Kenya.

Advert of Dyaya In

Aprili – Mei – Juni 2021 | Msimbo wa Nembo, Gombo 2021, Nam. 4, 5, 6 | Ukurasa 26  wa 48

SHUHUDA

Dada Gina Dambrevil

Salamu katika Kristo Yesu, Ndugu na Dada zangu wa Kanisa la saa ya 11,

Namshukuru Mungu kwa ujumbe wa Fimbo ya Mchungaji ambao naliupokea kupitia Dada mmoja kutoka Marekani mwaka 2006. Nalifurahishwa mno kwa namna alivyoliwasilisha fundisho la Zekariah Sura ya 4, “Bakuli la Dhahabu,” ambalo lilinishangaza kwa sanbabu awalinalikuwa Mpentekoste na sikujua nabii hizi. Hili liliniongoza kuvitafiti vitabu vya Dada White na tangu wakati huo nimevuviwa kusoma vitabu vya Roho ya Unabii kama Pambano Kuu na Jumbe kwa Vijana.

Kwa vile wakati huo hatukuwa na teknolojia ya sasa, ilitupasa kuwasubiri walimu watupatienakala zilizorudufishwa baada ya kilawasilisho ili tusome tena; hizi hazikunifurahisha maana sikuwa na mawasilisho mkononi ili niweze kuifuatilia mada. Hili lilitamausha sana. Naliondoka nchini kwenda Chile na nikaolewa kwa Ndugu Mdaudi. Maadamu tulivyozijua familia zingine za Wadaudi, tulijifunza masomo yale yale ya msingi hadi tulipokutana na Dada Mdaudi kutoka Martinique.

Tulianza fundisho la siku 2300 hadi tukawasili kwa mganda wa kutikiswa; kwa hatua hiyo, Nalitiwa moyo sana kujifunza Fimbo ya Mchungaji. Sasa nimesoma hadi Salamu Mwafaka, Gombo la 1. Nampa Mungu shukrani kwa maarifa yote ambayo nimepata kupitia kususoma kibinafsi. Pamoja na pambazuko la uzoefu huu, naliweza kuuelewa ujumbe vyema na kuyatengeneza maisha yangu.

Bwana anisaidie nimalize kusoma, nifanye matengenezo kabisa, na niwe mtenda kazi pamoja Naye katika ujumbe huu.

Santiago de Chile.

DADA Pierre Mendjee

Amani iwe kwenu Ndugu katika jina la thamani la Mwokozi wetu Yesu,

Nalikuwa nikiitafuta Kweli na Mungu alinisikia. Ilikuwa

kwa hatua hiyo maishani mwangu nilipojihisi kwamba nalikuwa katika usahaulifu wa kina, nalihisi kwamba maombi yangu hayangesikika. Nalikuwa nikilia na kuomba siku moja asubuhi, nikimwomba Bwana anisamehe dhambi zangu na kuniosha. Nalikuwa nikiomba upendo Wake, rehema Yake, na msamaha Wake. Nalimwomba Amtume mtu njiani mwangu aniletee nuru katika jina Lake.

Sabato iliyofuata nalikutana na dada ambaye sikuwa nimemwona zaidi ya mika miwili. Hakuwa amepanga kwenda Kanisani siku hiyo, lakina alikuwa karibu na akaamua kuhudhuria. Nalimwambia kwamba namjua, lakini alikuwa akinitazama, akijaribu kuitambua sura yangu. Baada ya ibada ya Kanisa, alinialika kwa chajio.

Mume wake alikuwa na Ukweli, lakini kwa sababu fulani alikuwa hajawahi kunigawiza hata neno. Nalisisimka sana na kuwaambia kuhusu sala yangu na jinsi nilivyowapata baada ya muda huo mrefu! Nalimwambia jinsi nilivyokuwa nikilitazama Kanisa na jinsi nilivyohisi (ya kwamba nilihitaji kitu kingine). Yeye aliniuliza ikiwa nina ari kujifunza nabii na baadaye akanitambulisha kwa Fimbo ya Mchungaji – na msifuni Bwana! Tangu siku hiyo, Naliijua Kuwa ni Ukweli; na nimeamua kujifunza na Kuufanya uwe Nguzo ya maisha yangu.

Ndugu, tangu niujue Ukweli, nimekuwa na furaha maishani mwangu hata katika nyakati za taabu. Nina tabasamu usoni mwangu ambayo hakuna mtu awezaye kufuta. Mambo si rahisi maishani mwangu; labda yako katika hali yake mbaya zaidi: lakini huona kila wakati mgumu kama baraka fiche kutoka kwa Mungu.

Niliamua kuyabadilisha maisha yangu yote, na Baba yangu alinipa hiyo amani niliyokuwa nikitafuta. Mungu aliniponya kimwilli na kunigusa kiroho. Alinichagua, na najua kwamba mimi ni binti Yake.

Nimekuja kutoka mbali, na bado nina mwendo mrefu wa kwenda. Msifuni Bwana kwa Fimbo ya Mchungaji! Msifuni kwa upendeleo ambao Ametupatia! Ndugu, tusaideni katika sala zenu kwa sababu sisi ni kikundi kidogo na tunapaswa kuitenda kazi ya Mungu.

Santiago, Chile.

Aprili – Mei – Juni 2021 | Msimbo wa Nembo, Gombo 2021, Nam. 4, 5, 6 | Ukurasa 27  wa 48

DADA Sherline Francius

Salamu katika Kristo Yesu, Ndugu na Dada zangu,

Nalipokea ujumbe wa Uadventista wa Sabato katika mwaka 2014 na kubatizwa mwaka uo huo. Nalivumilia muda mrefu kwa sababu yalikuwapo mengi niliyokosa katika hali yangu ya kiroho – lakini sikujua ni yapi – kama vile kutojua kwangu vitabu vya Dada White vya Roho ya Unabii, ambavyo hufunza kuhusu maisha ya Kanisa, lakini hayakufunzwa Kanisani.

Mwanzoni mwa mwaka 2020, Mungu alinielekeza maskani kwa Ndugu Jean Edvard Louis. Alinifanyia utangulizi wa jumla na baadaye aliendea kujifunza pamoja nami. Alinitambulisha kwa Maandishi ya Dada Ellen G. White na akanifafanulia mambo muhimu sana kama matengenezo ya afya na mavazi n.k. Kisha akanitambulisha kwa vitabu vya Fimbo ya Mchungaji na kuniomba nisome Vyote. Nilipokuwa nikisoma, Naliona kwamba iliwezekana kuvisoma na Kuvimaliza. Sikutaka nisome sana, lakini nilianza kusoma Fimbo na kuona kwamba ilikuwa inavutia sana, na nikaendelea kusoma ili nimalize hivyo vitabu.

Ujumbe huu umeyabadilisha maisha yangu, na sasa mimi ni msharika wa Kanisa la Saa ya Kumi na Moja: utukufu wote ni kwa Mungu wetu!

Chile, Santiago

Ushuhuda wa Dada ROLLÉ Patricia

Kama M’adventista, Nimekuwa nikijiuliza nawezaje kuwa tayari kupelekwa mbinguni papo hapo – kwa kufumba na kufumbua – bila maandalio. Hakika, Biblia hufundisha kwamba lazima mtu awe bila lawama ili auone uso wa Mungu. Nilijua kwamba Kanisa katika hali yake ya sasa halingeweza kuniandaa kwa tukio muhimu kama hilo. Nafsi yangu ilikuwa na kiu cha kitu ambacho sikuweza kupata Kanisani. Nalihudhuria ibada zote, lakini mahubiri yalikuwa yakizidi kukosa mvuto.

Kwa hivyo, nalichagua kuyapokea mafunzo kwa vikundi ambavyo vilikuwa vikijifunza Ukweli wa ziada kutoka katika Biblia na Roho ya Unabii. Mimi hufurahia kusoma na kusikiliza yale wengine husema. Yohana hutuambia, “Lakini Yeye, atakapokuja, Roho wa Kweli, Atawaongoza awatie kwenye Kweli yote: kwa maana Hatanena kwa shauri Lake Mwenyewe; lakini yote Atakayoyasikia Atayanena, na mambo yajayo Atawapasha

habari yake.”

Vifungu vingine vimeitegemeza imani yangu, pamoja na hiki: “…iwapo ujumbe unakuja usiouelewa, vumilia ili uweze kusikiza sababu ambazo mjumbe anaweza kutoa…kwa maana msimamo wako hautatikiswa kwa kukutana na makosa… Hakuna hata mmoja wao ambaye hudhani kwamba anajua yote ni mzee au mwerevu sana kutojifunza kutoka kwa aliye mnyenyekevu zaidi wa wajumbe wa Mungu aliye hai.” – Shuhuda kwa Kazi za Shule ya Sabato, uk. 60-66. Hivyo, naliendelea kujifunza Ukweli huu.

Dada kutoka Guadeloupe alinigawiza Ukweli kuhusu “Mganda wa Kutikisa,” na tangu siku hiyo nimekuwa nikijifunza na kuupokea ujumbe wa Fimbo katika usafi Wake wote. Ujumbe huu ulikata kiu changu, tangu wakati huo, nimelifanya Neno la Mungu kuwa furaha yangu.

Juzijuzi, nalibatizwa tena, na Bwana aliimarisha imani yangu kwa sababu naliinunua “dhahabu iliyosafishwa kwa moto.” Kwa neema Yake, natii, naishi, na kuwagawia walio karibu nami Ukweli huu, na natumaini kwamba washarika wote wa familia yangu pia Wataupokea. Kwa kweli namshukuru na kumbariki wa Kuabudiwa Bwana na Mwokozi wangu Yesu kwa kunileta katika nuru Yake ya ajabu.

Nawaomba mniombee na familia yangu ili kwamba ushuhuda wetu uwaaongoze Ndugu na Dada wengine waupokee huu Ukweli.

Ufaransa.

USHUHUDA WA MWANDISHI WA NYIMBO

Tangu wakati nilipozaliwa mara ya pili, Kristo kihalisi amekuwa Rafiki yangu bora, katika maisha yangu, na katika mambo yangu yote. Nikiwa mwenye bidii sana kumtumikia Bwana katika njia mbalimbali, Nalijiunga na kwaya mbili tofauti katika kanisa la Laodekia. Nasikitika, walimu wangu wa kwaya walitambua kwamba sikuwa mwimbaji mwenye kipaji. Nalianza kwa maombi kuizoesha sauti yangu, lakini haikuwezekana haraka sana nilivyofikiri ingekuwa, na siku moja mwalimu wetu alikosa uvumilivu na kunipigia kelele katika mazoezi kwa sababu sauti yangu haikuwa inaimarika. Nikalia kwa sababu nalikuwa nimetenda niwezavyo kuimarika.

Baadaye, Bwana akanikutanisha na ujumbe wa Fimbo ya Mchungaji, na kwa neema Yake

Aprili – Mei – Juni 2021 | Msimbo wa Nembo, Gombo 2021, Nam. 4, 5, 6 | Ukurasa 28  wa 48

Katika kipindi hiki, nalikabiliwa na changamoto kadhaa za kifedha lakini kwa majaliwa ya Mungu nalipata ofa ya kazi katika mji wa Kenya uitwao Eldoret. Nalisafiri huko, lakini ofa hiyo haikutimia nilivyokuwa nimetarajia. Jambo la kufurahisha, nalipata nyumba ya udongo niliyoweza kumudu hapo mjini na ingawa ilikuwa na matundu duni ya kupitisha hewa, nalishukuru kuwa na nyumba.

Siku moja, katika nyumba hiyo ya udongo, nilipokuwa nikitafakari mintarafu ya Ufalme unaokuja hivi karibuni, nilipata vifungu viwili vya wimbo wangu wa kwanza. Niliugawia washarika wa Eldoret, na wakabarikiwa. Usiku uliofuata naliota kwamba nalikuwa nikiuimba wimbo huo, lakini ajabu, pamoja na kibwagizo ambacho sikuwa nimekisikia awali. Naliamka upesi na kukiandika hicho kibwagizo. Hivi ndivyo Bwana alinifunulia kwamba nina kipaji cha kuandika nyimbo na hata kuziimba. Ninazo karibu nyimbo 50za Ukweli wa Sasa leo ambazo Mungu alinisaidia kuandika kwa msingi wa uzoefu tofauti tofauti. Pia Amenibariki kwa kipaji cha ushairi ambajo kilikuja kama tokeo la jaribu fulani nililopitia.

Kalamu haiwezi kuandika yote ambayo Bwana amenitendea. Naweza tu kusema: “Neema ya ajabu! Ni ilioje sauti tamu, iliyomwokoa mnyonge; kama mimi! Nalikuwa nimepotea, ila sasa nimepatikana, nalikuwa kipofu ila sasa naona.” Utukufu, heshima, kuabudu na sifa kwa Malme wetu Yesu atupendaye.

Dada Edna Twara,
Kenya.

 

Wapendwa Ndugu,

Salamu Changamfu katika Jina la thamani la Bwana wetu Yesu Kristo. Nchukua fursa hii kumshukuru Bwana kwa ujumbe wa Fimbo ya Mchungaji ambao umenipa matumaini mengi na amani ndani ya Kristo. Nashuhudia kwamba afya yangu imekuwa njema tangu nalijifunza jinsi ya kutekeleza matengenezo ya afya yanavyofundishwa Kabari Inayopenyeza. Nathibitisha kwamba yakifuatwa kikamilifu, haya matengenezo ya afya ni ya kutekelezwa na baraka halisi kwa maisha yetu.

Shukrani, na Mungu awabariki nyote.

Ndugu Evans Mogoi,
Kenya.

Malachi 4:5.

Naliupokea ujumbe wa Fimbo ya Mchungaji kati ya mwaka 2002 na 2003 na kuwa msharika wa Njia ya 2500 Mlima Karmeli baada ya mmoja wa Ndugu zangu kuwasilisha Mathayo 20 na kuonyesha wazi kwamba ulikuwapo mwito mwingine wa watenda kazi baada ya mwaka 1844. Lilikuwa la kushangaza na la kusisimua kwa sababu siku zote nalifikiri kwamba wa’S.D.A. walikuwa kundi la mwisho la watenda kazi.

Takribani miaka kumi baadaye, ndugu mwingine wa Njia ya 2500 Mlima Karmeli akiwa ameandamana na ndugu na dada walizuru na kunialika kwa fundisho baada ya ibada ya kanisa la Laodekia ili tujadili nuru fulani waliyokuwa nayo mintarafu ya Ukweli wa Sasa. Tuliamua kulifanyia nyumbani mwa rafiki ya Mdaudi mwingine. Wakati huo mada ya uchambuzi ilikuwa “Mavuno.” Tuliifungua mioyo yetu kusikia na kupokea yale yule ndugu aliwasilisha, na ilikuwa shangwe na furaha moyoni mwangu nilipoona wazi kwamba yale aliyokuwa akiwasilisha yalithibitishwa kwa Neno lililoandikwa, haswa Trakti Namba 3, ambayo kwa hakika sikuwa na uelewa wake bora awali.

Tuliuza maswali, na aliweza kujibu yote kwa msaada wa Bwana. Alitupeleka kwa chati ya“Mavuno” na kutuonyesha “Siku ya Kutoa Hesabu, Mathayo 25:19,” na kulifafanua andiko hilo kwa uhusiano na hiyo chati. Uthibitisho huo ulitosha kutusadikishia Hukumu katika Jumuiya ya Wadaudi wa S.D.A. kabla ya ile katika kanisa Mama. Baada ya kuagana, tuliendelea kusoma na kudurusu ujumbe kupitia baadhi ya DVD, tulizopewa baadaye.

Katika mwaka 2013, tulipokea habari kwamba mtunzi wa hizo DVD alikuwa anapanga kuzuru Kenya na ya kwamba washarika wote wamealikwa kuhudhuria mkutano, ambao ungefanyika nje ya Nairobi katika eneo la Rongai. Tulikuwa na wakati wa kutosha kujifunza ujumbe na Ndugu Sam kwa siku kumi. Ukweli uliwasilishwa katika njia wazi na iliyoeleweka kwa urahisi. Nalihisi nguvu ya Roho Mtakatifu ikitusadikisha kwamba tulikuwa tukiusikiza Ukweli wa Mungu: Fimbo ya Mchungaji katika usafi wake. Maswali mengi yalijibiwa, ambayo awali yalikuwa tu fumbo. Moto wa uamsho na matengenezo makubwa uliwashwa.

Katika mwaka 2014, tulikuwa na warsha nyingine ya mwezi mmoja ambapo Ndugu Sam aliongoza

Aprili – Mei – Juni 2021 | Msimbo wa Nembo, Gombo 2021, Nam. 4, 5, 6 | Ukurasa 29  wa 48

usharika kwa kuugawia mkate wa mbinguni. Wakati huo idadi kubwa ilihudhuria, na kambi iliangazwa nuru ilipong’aa kutoka kwa Neno la Mungu. Nalishangilia kwa sababu familia yangu yote ilihudhuria warsha hiyo na kula kweli za ajabu zilipokuja moja kwa moja kutoka kwenye kiti cha enzi cha rehema.

Baada ya hiyo warsha, tulihudhuria kanisa la S.D.A. la eneo letu la Kinoo, na baada ya wakati fulani, Nalipokea barua kutoka kwa uongozi wa kanisa, ulioniita mbele ya baraza la kanisa nijibu mashtaka kadhaa. Ingawa barua hiyo ilielekezwa kwangu, nalishuku kwamba ndugu zangu pia walikuwa wamepokea zao maana sisi watano tulishtakiwa kusababisha mchafuko kanisani kwa kuongoza katika matengenezo.

Siku hiyo ilikuja, na tukauona mkono wa Mungu jinsi mambo yalivyotukia. Mchungaji, akiwa amesimama kwenye ardhi iliyojazwa kokoto nje ya kanisa, aliamua kutupatia maagizo kabla tuingie ukumbini mwa mkutano. Kwa makusudi lituambia tukiwa bado kwa ardhi hiyo yenye kokoto na tukajua kwamba hili lilikuwa jaribio iwapo tungepiga magoti kwa eneo kama hilo. Kwa mshangao wake, aliona tukipiga magoti, na alichanganyikiwa sana ya kwamba hakuweza kuomba kwa ufahamu.

Baada ya ombi, alitoa maagizo fulani akitumia Kanuni ya Kanisa la S.D.A. akatuonya tusiseme jambo lolote au kuuliza maswali yoyote. Utaratibu huu ulipaswa kufuatwa hata tukiwa katika “Chumba cha Mashtaka,” kama walivyokiita. Baraza la karibu washarika 30 walikuwapo mchungaji alipokuwa akiongoza kesi. Alitumia karibu masaa mawili akisoma, akikemea, na kutoa maonyo makali dhidi yetu. Yeye na mzee mwandamizi walikuwa wakali mno. Baada ya kumaliza kazi yao ovu, mchungaji aliomba akitulaani tufe ili tusiweze kuvuruga watu wake.

Mashtaka yaliyowekwa mbele yalikuwa: 1) Kukosa kusalimiana hekaluni hata baada ya kuombwa kufanya hivyo; 2) Kupiga magoti kwa maombi ya ushirika wakati wengine wamesimama; 3) Kutoagiza Masomo ya Shule ya Sabato ya kila Robo wengine wanapoyaagiza; na 4) Kutotoa zaka kanisani.

Mchungaji wa wilaya alituamuru tusije kwa kanisa hilo ikiwa tulitaka kuwa na amani naye, au sivyo ataweka walinzi

kutuchunga na kutuzuilia langoni. Hiyo ilikuwa siku ya mwisho nilipomwona huyo mchungaji, maana alipata uhamisho, na yule mzee mwingine ambaye alitukasirikia aliugua pamoja na mkewe na akafa baada ya miezi michache.

Kwa sasa, Ukweli unaenea kutoka sehemu moja hadi nyingine katika Tarafa, tumekuwa na maeneo mapya yaliyoanzishwa na washarika wanashangilia katika Kweli. Bwana ametenda kwa ajabu sana, na ninayo kila sababu kutoa utukufu kwa Jina Lake takatifu na Kuu. Aweze kutusaidia tusimame kwa ajili Yake katika masaa haya ya mwisho ya wakati wa rehema.

Ndugu Shadrack Mauta,
Eneo la Kinoo, Kenya.

Wapendwa Ndugu na Dada,

Namshukuru Mungu kuniongoza hadi kwa hatua hii leo. Ujumbe wa Fimbo ya Mchungaji unakuwa wazi na wazi zaidi kwa uelewa wangu. Nilipoanza kusoma na kujifunza maandishi ya Fimbo ya Mchungaji, ilionekana kwangu kwamba singeweza kuelewa yale yalionekana wazi kwa wengine. Nalimwomba sana Bwana kwa msaada wa Roho Mtakatifu ili niuelewe mpango Wake ulio katika ujumbe Wake uliovoviwa. Naam, Mungu, akiwa ameahidi kutuongoza katika Kweli yote kupitia Roho Mtakatifu, ni mwaminifu kwa ahadi Zake: Kamwe Yeye hamwachi au kumtupa yeyote ambaye Humwinulia sauti yake kwa unyenyekevu na kutambua tegemeo lake Kwake. Bwana ni Mtakatifu, na Neno Lake ni Takatifu. “Vivyo hivyo na mambo ya Mungu hakuna afahamuye, ila Roho wa Mungu.” {SR2 :14.2}

Fimbo ya Mchungaji ni chanzo cha Ukweli kisichoweza kumalizika! Namshukuru Mungu bado nina mengi ya kujifunza na kuelewa. Roho Mtakatifu aweze kuniongoza na kunielekeza na kila mmoja wetu kadiri tunavyosoma, kujifunza, na kutekeleza mashauri ya Shahidi Mwaminifu na wa Kweli.

Dada Suivant-Oncins Huguette,
Ducos, Martinique.

LILE NILILOJIFUNZA KATIKA KANISA LA SAA YA 11

Namshukuru Bwana kwa kuwa sehemu ya Kanisa la saa ya Kumi na Moja. Mpaka hapo nalikuwa Mdaudi Mountain dale ambaye sikuujua ujumbe wa Fimbo katika ukamilifu wake kwa sababu sikusoma

Aprili – Mei – Juni 2021 | Msimbo wa Nembo, Gombo 2021, Nam. 4, 5, 6 | Ukurasa 30  wa 48

Msimbo wa Nembo. Kila wakati niliposoma Msimbo, ulikuwa mafumbo ambayo sikutaka kushughulika nayo kwa sababu haukupigiwa debe kwa nguvu na walimu wengi huko Mountain dale.

Ni kwa kukutana na Mawasilisho ya mtandaoni kupitia kwa Ndugu yangu mpendwa Iwan Kortram ya kwamba nilijifunza Ukweli ulio nyuma ya Msimbo na Kweli zingine muhimu katika Fimbo ambazo zimefanya Niuelewe zaidi na bado ni wa ajabu kwangu. Nashangilia sasa katika kusoma Msimbo wa Nembo safi kwa sababu umechochea roho yangu kuyafanya matengenezo na kuishi kulingana na matakwa ya Ukweli wa sasa wa Mungu kwa wakati huu. Kila siku hujifunza kumjua Yesu Mwokozi wangu vyema zaidi kuliko awali, na Anavyotaka ili niwe sehemu ya Ufalme Wake unaokuja hivi.

Namshukuru Bwana ya kwamba nilijifunza katika Kanisa hili nisiwafuate wanadamu bali kwa kweli niidurusu Fimbo mwenyewe! Sikujua hata kilichomaanisha kwa kweli kudurusu ujumbe wa Fimbo ya Mchungaji: hili, pia, nilijifunza katika Kanisa la Saa ya Kumi na Moja.

Bwana atupate sote tukiwa waaminifu Atakapokuja kufanya hesabu na watumwa Wake wa Saa ya Kumi na Moja ndiyo matamanio na ombi langu.

Ndugu Lloyd van Niel,
Berlijn, Suriname.

NAMNA UJUMBE WA “SIKU YA KUTOA HESABU” ULINIJIA KWA NGUVU.

Nataka kumshukuru Mungu kwa Ukweli wa Siku ya Kutoa Hesabu, ambao nilipokea kupitia DVD kadhaa zilizotumwa kutoka Zambia na Ndugu Fidelis Mutale. Ujumbe ulikuja kwa nguvu. Nilipokuwa nikizisikiliza video hizo mfululizo mchana na usiku katika juma, Naliona mkono wa Mungu ukitenda kazi kwa kujibu maswali yote niliyokuwa nayo tangu niongoke na kuingia katika vuguvugu la Kidaudi. Sehemu kubwa ya historia sikuijua na hakika nilidanganywa kwa mafundisho ya wanadamu, nikiyaamini kuwa ni kweli. Nalikuwa nimefunzwa kwamba Ndugu Houteff alikufa kifo cha ghafla; ya kwamba Mountain Dale ilihama kutoka Waco 2500; ya kwamba msimbo mpya ulikuwa sehemu ya Fimbo; na ya kwamba ni watakatifu 144,000 pekee watakaookolewa katika mavuno ya malimbuko. Masuala haya yote yalishughulikiwa na nikafurahi sana.

Siwezi kuusahau msimu huo wa kujifunza kwa sababu, hata wakati wowote nilipokwenda nje ya nyumba kujituliza, ningeisikia sauti ya mwasilishaji akihutubu masikioni mwangu! Ni vigumu kufafanua huo uzoefu, lakini ulikuwa halisi. Ujumbe huu umebadilisha maisha yangu na familia yangu yote. Ingawa bado tunapambana na udhaifu kadhaa katika maisha yetu, Nina furaha hakika kwamba Mungu anatuongoza katika Ufalme Wake kupitia ujumbe huu wa ajabu mkononi mwa msemaji kama alivyoahidiwa katika Mtoa Jibu [ABN3: 32.2]. Bwana atuongoze kupanda ngazi ya ukamilifu hata Siku hiyo tukufu ije.

Ndugu Ibrahim Sekabira,
Busunju, Uganda.

NALIKUWA KIPOFU, LAKINI SASA NAONA

Salamu, Kanisa la 11:

Namshukuru Bwana kwamba sasa mimi ni Mdaudi katika Ukweli wa Sasa. Awali, nalikuwa sehemu ya “Davidia” chini ya Mountain Dale. Viongozi wa kanisa la S.D.A. la eneo letu walitutesa vikali mara kwa mara wakiwa na azma ya kutufanya tuuache Ukweli wa Sasa: Mungu asifiwe kamwe hawakushinda! Baadhi yetu tulipigwa, tukapelekwa kwa polisi, nyakati zingine kutupwa gerezani, au kupelekwa kwa baraza la kanisa – lakini Bwana alikuwa pamoja nasi katika hayo yote. Ulikuwapo mtengano nilipokuwa ndani ya Davidia na huu ulikuwa njia ya Mungu ya kunifumbua macho; Njia Zake si njia zetu! Karibu miaka saba imepita tangu nilipojifunza kuhusu Siku ya Kutoa Hesabu, ambayo naamini kabisa, na nampa Mungu utukufu maana Yeye huwaongoza watu Wake hatua kwa hatua. Mungu atusaidie tuwe waaminifu hadi mwisho. Amina.

Dada Martha Kabalwanyi,
Busunju, Uganda.

WAKATI MMOJA NALIPOTEA, SASA NIMEPATIKANA

Wapenzi Ndugu,

Namsifu Bwana kwa rehema Zake na upendo mkuu katika shughuli Yake ya kuziokoa roho. Namshukuru kwa Ujumbe wa Fimbo; ulinipata katika hali ya kusikitisha: Nilikuwa katika kanisa la S.D.A. kwa karibu miaka 15 na Fimbo ilinitendea lile kanisa mama halikunitendea – hakika ilinifumbua macho. Mungu asifiwe kwa Ujumbe huu wa Fimbo! Amina.

Dada Tabitha Bisembo,
Busunju, Uganda.

Aprili – Mei – Juni 2021 | Msimbo wa Nembo, Gombo 2021, Nam. 4, 5, 6 | Ukurasa 31  wa 48

Wapenzi Wapendwa Ndugu,

Umekuwa uzoefu mkubwa kwa familia yangu nami katika Ukweli wa Sasa kwa vile tumeshuhudia kwanza utamu wa ujumbe. Ujumbe wa Fimbo umeleta furaha nyingi na maana kwa maisha yangu. Sasa, nimeazimia zaidi kuliko wakati mwingine wowote kumfanyia Bwana kazi kadiri Anaponiongoza.

Kwa huzuni, inaonekana wengi wetu kama Wadaudi bado hatujalielewa pendeleo ambalo tumeitiwa, na kwa sikitiko, ndugu zetu wapenzi katika “Davidia” wanaupiga vita Ukweli wa Sasa kwa bidii ya ukatili. Mwalimu fulani kutoka Njia ya 2500 Mlima Karmeli alihisi vibaya sana baada ya kuwapoteza wanafunzi wake kwa Fimbo safi hata akamshinikiza mmoja wao akome kujifunza nasi, akamwambia kwamba sisi tulikuwa wezi tulitaka kumuiba kutoka kwa Jumuiya ya kweli; lakini huyo mwanafunzi aliweza kumdhibiti kwa sababu tulikuwa tumeweka msingi thabiti. Alimwambia huyo mwalimu kwamba mambo mengi wanayofundisha hayajaandikwa katika Fimbo, bali ya kwamba wale ndugu wengine (akimaanisha sisi) siku zote hunukuu kutoka katika Fimbo.

Yule mwalimu aliendelea kumshutumu huyo mwanafunzi kwa kuleta makosa kwa wazazi wake waliokuwa wachanga katika ukweli na kumwamuru akome kufanyia mafunzo ndani ya nyumba yao. Tunafikiri kwa kweli amri hiyo ilikuwa inavuka mpaka wa mamlaka

yake kama mwalimu. Hata hivyo, yule ndugu mchanga alijibu kwa unyenyekevu akisema: “Siwezi kuwaamuru wazazi wangu waache kuuchunguza Ukweli; wao wana umri wa kutosha kujifanyia uamuzi.” Huyo mwalimu alikumbushwa zaidi kwamba alipokuwa akiendesha mafunzo katika nyumba ile ile, mama wa hiyo nyumba pamoja na watoto wachanga, walikuwa wameacha kuhudhuria mafunzo, ila sasa, Mungu asifiwe, yeye na hao watoto tena wanashiriki katika mafunzo kwa bidii kubwa.

Mwongofu mpya kwa Fimbo safi alimfafanulia mwalimu wake wa awali hivi: “Sababu pekee ambayo polisi wanazo bunduki ni ya kwamba ili waweze kuwadhibiti watu.” Hili alilinena kumaanisha kwamba sababu ya wao kutotaka kuwapa wanafunzi Fimbo hawakutaka wajisomee wenyewe na wagundue makosa yanayofundishwa; hivyo wao huwadhibiti kwa njia hii. Huyo mwalimu alikasirika, na kama wafanyavyo siku zote, alianza kuharibu heshima ya washarika wa Kanisa la Saa ya Kumi na Moja. Hili lilikuwa la kututia moyo, tulipomwona Bwana akilikusanya jeshi la vijana ambao wanaweza kusimama kwa Ukweli.

Wapenzi wapendwa, tunaomba msali kwa ajili ya hawa wanafunzi wapya, maana Shetani yuajishughulisha sana awanyakue. Bwana aweze kuwalinda katika viganja vya mikono Yake.

Ndugu Denis Mwaba,
Lusaka, Zambia.

IBADA

KATIKA MAENEO YA MBINGUNI (ELLEN G. WHITE)

Sura ya 187 – “Ibada Yetu Yenye Maana”

“Basi ndugu zangu, nawasihi, kwa huruma za Mungu, itoeni miili yenu iwe dhabihu iliyo hai, takatifu, ya kumpendeza Mungu, ndiyo ibada yenu yenye maana.” Rum. 12:1.

Mtume huwasihi ndugu zake waitoe miili yao kwa Mungu. . . . Wakati tunafuata mwenendo wa kudhoofisha nguvu za akili na mwili — kila tulapo, tunywapo, au tunapofanya lolote katika mazoea yetu — tunamfedhehesha Mungu, maana huwa tunamnyang’anya ibada ambayo Yeye hudai kutoka kwetu. Tunaporidhisha ulafi bila kujizuia kwa gharama ya afya, au tunaporidhisha mazoea ambayo hudhoofisha uhai na nguvu za akili, hatuwezi kuthamini upeo wa upatanisho na tathmini sahihi ya mambo ya milele. {HP 193.2}

Wakati akili zetu zimekanganywa na kufishwa ganzi kwa sehemu na maradhi tunashindwa kwa urahisi na majaribu ya Shetani. Ulaji wa chakula kisicholeta afya kuridhisha ulafi bila kujizuia una mwelekeo wa moja kwa moja kuchafua

Aprili – Mei – Juni 2021 | Msimbo wa Nembo, Gombo 2021, Nam. 4, 5, 6 | Ukurasa 32  wa 48

mzunguko wa damu, kusababisha udhaifu wa neva, na kama tokeo unakosekana uvumilivu na upendo, wa kweli ulioinuliwa. Nguvu za mwili, na vile vile mwelekeo wa tabia na uwezo wa akili timamu, hudhoofishwa kupitia kuridhisha ulafi bila kujizuia. . . . {HP 193.3}

Hazina zote za ulimwengu huzama na kuwa si kitu zinapolinganishwa kwa thamani ya nguvu za akili na tabia. Na utendaji kiafya wa viungo hivi hutegemea afya ya mwili. Basi ni umuhimu ulioje kwamba tujue jinsi ya kudumisha afya, ya kwamba wajibu wetu kwa Mungu na mwanadamu utekelezwe kulingana na amri Zake. Sheria za Mungu ni rahisi na wazi. Hakuna kutokuwa na uhakika huzifunika yoyote kati yazo. Kamwe hakuna hata moja kati yazo inahitaji kutoeleweka. Wale

ambao hawawezi kuzitambua wamefanywa wapooze kwa mazoea yao mabaya yanayodhoofisha ubongo wao. {HP 193.4}

Mungu hunuia kutufunza umuhimu wa kuwa na kiasi katika mambo yote. Kwa sababu kutokuwa na kiasi kulisababisha anguko la wazazi wetu wa kwanza kutoka kwa hali yao takatifu na ya furaha, kwa kuiasi sheria ya Mungu, hivyo kuwa na kiasi katika mambo yote kitadumisha viungo vyetu katika hali nzuri kiafya inavyowezekana, ya kwamba hakuna ukungu au kutokuwa na uhakika hakuwezi kuifunika yoyote kati yazo, ya kwamba akili ziongoze kuchukua hatua sahihi katika kutunza sheria Yake. . . . Lazima tutende kazi kwa upatano na sheria za asili iwapo tungependa kutambua iliyonenwa kutoka madai ya kisheria ya sheria ya Mungu iliyonenwa kutoka Sinai. {HP 193.5}

Imewasilishwa na Dada Gloria Nalls,

Marekani.

Maswali na Majibu

KUUNGANA AU KUTOUNGANA?

Swali Namba 1

Kuungana kuwa shirika ni nini na mbona Jumuiya za Kidaudi haziruhusiwi kuungana?

Jibu:

Shirika ni taratibu maarufu sana ya majina ya kibiashara Marekani, lakini laweza kuwa limezidiwa na lililo bora sasa Kampuni yenye Dhima ya Kikomo (KDK). Kwendesha biashara katika mojawapo wa majimbo hamsini Marekani, mtu lazima afanye muundo wa jina la biashara na asajiliwe katika jimbo la chaguo lake, na atii sheria za Kampuni za jimbo hilo. Ili kuhalalisha misimamo ya Kuungana, uongozi wa Jumuiya za Wadaudi hudai kwamba mashirika yasiyo ya kibiashara lazima yaungane na yapate hati 501(c) ondoleo la kodi kutoka kwa Utumishi wa Kodi ya Ndani; huu ni udanganyifu.

Mbona wao huridhia kuungana? Kwa sababu mali za watu binafsi za wanachama wao zinalindwa kutokana na uwezekano wa madai yoyote ya kesi. Iwapo kampuni yoyote iliyoungana itashtakiwa na hukumu kutolewa dhidi ya shirika, ni mali za shirika pekee ambazo hutiishwa chini ya mashtaka; mali za kibinafsi za wamiliki au wenye hisa zinalindwa katika tukio ambapo mali za shirika hazitoshi kufidia hukumu. Marekani ni jumuiya inayopenda kufungua kesi mahakamani; kila mmoja anajitahidi kumshtaki mwenziwe, kwa hivyo ulinzi huu unatafutwa na wengi.

Jumuiya ya Bwana imekatazwa kuungana kuwa shirika kwa sababu Bwana alisema hivyo:

TN8: 48.2 [SRS: 168]: Wakati umeonyesha kwamba shirika la S.D.A. linatimiza ule mfano. Kwa kupenda zaidi kushirikisha, na kuchagua maofisa kwa njia ya kura za watu, kwa hivyo wameonyesha kwamba hawakujali sana kumpendeza Mungu ili waweze kuwa “watu wa milki ya Mungu,” jinsi Yeye angetaka wawe, maadamu wanataka kujifurahisha iwezekanavyo kuwa kama madhehebu mengine – kama katika wakati wa Sauli watu walitaka kuwa kama mataifa waliowazunguka pande zote (1 Sam. 8:5, 7). Na ingawa wamechaguliwa na watu, bado maofisa wa Baraza Kuu hata hivyo walikubaliwa na Mungu kuwa watawala kwa watu Wake sasa, alivyokuwa Sauli zamani.

Aprili – Mei – Juni 2021 | Msimbo wa Nembo, Gombo 2021, Nam. 4, 5, 6 | Ukurasa 33  wa 48

Jinsi alivyousaliti uaminifu wake, hata hivyo, kwa kutolitii Neno la Mungu lilivyonenwa kwake na nabii Samweli, hivyo uongozi wa sasa wa kanisa, “wazee wa kale…walio mbele ya nyumba,” asema nabii kwa kanisa leo, “wameisaliti imani yao.” – Shuhuda, Gombo la 5, uk. 211.

Fimbo hapa hutuhimiza kwamba tumeitwa tuwe watu wa milki ya Mungu, na sio kama walimwengu wengine. Kanisa la Kiadventista liliamua kuunganisha na kuchagua maofisa kwa njia ya kura za watu kwa sababu madhehebu mengine yalikuwa yakifanya hivyo. Jumuiya nyingi za Kidaudi zimeungana kuwa shirika vivyo hivyo haswa Njia ya 2500 Mlima Karmeli, Waco, Texas, Jumuiya ya Mountain Dale, Jumuiya ya Salem, Jumuiya ya Bashani, n.k.

Swali hili lingekuwa la sehemu tatu, sehemu ya tatu ikiwa, mbona Jumuiya za Kidaudi zinachagua maofisa wao kwa njia ya kura za watu. Jumuiya tatu za kwanza zilizotajwa hapo juu, zaidi ya kuungana kuwa shirika, pia zinachagua viongozi wao kuingia ofisini. Kwa mujibu wa ile taarifa katika Trakti Namba 8, yote yameshtumiwa.

Jinsi Mungu alivyomkataa Sauli kwa kutotii, Amezikataa pia hizi zote zinazoitwa eti Jumuiya— haswa Njia ya 2500 Mlima Karmeli, Waco, Texas — kwa sababu wanakataa kulitii Neno Lake. Katika mwaka 2002 Kikao chao kilipiga kura kulivunja shirika. Miaka kumi na tisa baadaye, bado wameungana kuwa shirika kwa sababu sanamu ambazo hunena zilisema, “sahau lile Kikao kilipigia kura, tuendeshe Makao makuu haya,” na waabudu wakasema “amina.” Sababu kuu abayo viongozi waliukataa uamuzi wa Kikao ilikuwa kwa sababu ya wasilisho la kuungana lililoletwa na Ndugu lennox Sam. Hakuamini Ndugu Houteff aliwasilisha hotuba zilizochapishwa na Dada Houteff baada ya kifo cha nabii. Ndiposa, vuguvugu la “asiye mwingine ila Sam” lilianza na limezibomoa kuta za utengano kati ya makundi mbali mbali ya Wadaudi. Vuguvugu la “asiye mwingine ila Sam” limegeuka na kuwa vuguvugu “lazima tumkomeshe Sam.” Pambano lao kubwa ni kwamba hawawezi kumpata yeyote kati yao ambaye atakubali kukutana na Sam na ajibu maswali yake.

KISAWE AU NENO LINALOTUMIKA BADALA YA LINGINE?

Swali Namba 2:

Uvuvio husema kwamba “Bwana sasa haitishi sasa dhehebu”: Je! Ipo tofauti gani kati ya kanisa na dhehebu? Je! Makanisa yote ni madhehebu, na je! madhehebu yote ni makanisa?

Answer:

Maana ya neno “dhehebu” ni:

Dhehebu:

A Jumuiya ya kidini ambayo washarika huungana katika utiifu wao kwa imani na taratibu.

Tabaka, jumuiya au mkusanyiko wa watu, wanaoitwa kwa jina moja; kama dhehebu la Wakristo.

Maana ya neno “kanisa” ni:

Kanisa:

1 :  jengo la umma na haswa la ibada ya Ukristo

2 :  ukasisi au uongozi wa mwili wa kidini

3 aghalabu huandikwa kwa herufi kubwa : mwili au jumuiya ya waamini wa kidini: kama

Aprili – Mei – Juni 2021 | Msimbo wa Nembo, Gombo 2021, Nam. 4, 5, 6 | Ukurasa 34  wa 48

a :  mwili wote wa Wakristo

bdhehebu <kanisa la Kiprestiberi>

cusharika

Dhehebu ni mwili wote au mkusanyiko wa makanisa (usharika) yanayoitwa kwa jina moja. Je! Madhehebu yote ni makanisa? Naam. Je! Makanisa yote ni madhehebu? La: Kila dhehebu ni kanisa, ila kila kanisa si dhehebu. Kwa mfano, kanisa la S.D.A. Texas si dhehebu bali ni kanisa ndani ya dhehebu la S.D.A. Kanisa kwa urahisi ni tawi la dhehebu, na katika lugha ya Kiingereza, yote huitwa kanisa.

Hali yetu ni sawa na ya Israeli ya kale. Kwa sababu ya dhambi, Ufalme wa Israeli uligawanywa katika falme mbili, wa kabila mbili, na wa kabila kumi. Kabila kumi ziliendelea kuitwa Israeli kwa sababu walikuwa wengi, ilhali kabila mbili waliitwa Yuda (Wayahudi) kwa sababu wafalme wao walitoka kabila la Yuda. Sisi sote tuko katika dhehebu la S.D.A. (Israeli), na kwa sababu ya dhambi (kukataa Ukweli), Bwana alianzisha kanisa la Kidaudi ndani ya dhehebu la S.D.A., kama lilivyotabiriwa katika mfano wa Mathayo 20; kwa hivyo, sisi ni kanisa ndani ya kanisa.

KANISA AU JUMUIYA?

Swali Namba 3:

Mbona ninyi husema sisi ni kanisa ilhali Ulawi husema sisi ni jumuiya?

Jibu:

Ulawi hufafanua kwa usahihi kwamba sisi ni jumuiya, ukifunua aina ya chombo cha kibiashara tulivyo. Makanisa mengi yanayofanya shughuli Marekani lazima yaendeshwe kama chombo fulani cha kibiashara; mengi huchagua kufanya shughuli kama shirika, kama tunavyoliona Baraza Kuu la Waadventista wa Sabato. Iwapo msaili angalisoma ukurasa wa themanini na saba wa Ulawi, angekuwa amesoma kichwa “Sifa za Washarika wa Kanisa.” Siamini hata kidogo kwamba Ulawi unanena kuhusu sifa za washarika wa kanisa mama; kwa hivyo, ushahidi wako wa kwanza kwamba sisi ni kanisa ndani ya kanisa, zaidi haswa linavyofafanuliwa katika fimbo kama “Vuguvugu ndani ya Vuguvugu.”

Fimbo I wima moja kwa moja juu yetu kuwa kanisa katika Salamu Mwafaka Gombo la Pili, Namba 34:

“Mwanzoni mwa kila ujumbe watu ambao walisonga mbele na Ukweli walikuwa washarika mmoja mmoja wa kanisa ambalo lilikuja kuwa kanisa kwa njia ya kuupokea ujumbe, ujumbe ambao mwasisi wake aliuleta. Kwa mfano, kanisa lote la Kiyahudi halikuja kuwa kanisa la Kikristo, lakini kanisa la Kikristo liliwakokota washiriki wake kutoka katika kanisa la Kiyahudi na kuwaleta katika Ukweli ulioendelea, Ukweli mwafaka haswa kwa ajili ya wakati na watu wa wakati huo.  {2TG34: 24.2} [430]

“Jinsi tunavyoishi sasa katika wakati wa Ufunuo, katika wakati wa kufunuliwa kwa unabii ambao huonyesha kuanzishwa kwa Ufalme na vile vile kwa ujio wa pili wa Kristo, Kanisa wakati huu, kwa hivyo, haliwezi kwa busara kuitwa kwa jina lingine isipokuwa jina ambalo linafaa awamu yake ya sasa (ya juu) ya kazi ya injili. {2TG34: 24.3} [430]

“Kwa udhahiri, basi, jina lake lazima lionyeshe kweli ambazo huzitetea: yaani, kuzishika amri, ujio wa pili wa Kristo, na pia urejesho wa Ufalme wa Wadaudi kwa mujibu wa unabii. Kwa hivyo jina la busara ambalo linawakilisha kazi yake kuanzia wakati huu hadi kwa wakati Ufalme unapoanzishwa, litakuwa Wadaudi Waadventista wa Sabato, — jina ambalo hushuhudia ujumbe wa Ufalme, kuzishika amri ambazo ile Sabato ya siku ya saba 

Aprili – Mei – Juni 2021 | Msimbo wa Nembo, Gombo 2021, Nam. 4, 5, 6 | Ukurasa 35  wa 48

ni sehemu yazo, na ujio wa pili wa Kristo.”  {2TG34: 24.4} [430]

Iwapo kumbukumbu ilyo hapo juu haitoshi, tunakazia fikira za msaili kwa Msajili wa Nyumba Nyeupe ukurasa wa thelathini na tatu, ambamo Fimbo inaonya kuhusu jaribio la kutoa pigo la mtoano kwa vuguvugu. Jaribio lililonenwa lilitukia katika mwaka 1959 wakati Dada Houteff alitangaza kwa Baraza Kuu kwamba iwapo utabiri wake wa mchinjo wa Ezekieli Sura ya Tisa halitatukia Aprili 22, 1959, Fimbo ni ya uongo. Kumbuka, katika taarifa hii, badala ya kutuita kwa jina letu, Fimbo hutuita kwa namba ya Kanisa letu katika mfano wa Mathayo sura ya ishirini, hebu tuisikie Fimbo:

“Kila kitu ambacho kinaweza kufanywa dhidi ya ujumbe wa Mungu wa leo kitafanywa na kisasi kikubwa kuliko kilivyodhihirishwa dhidi ya ujumbe wa Mbingu siku za ujio wa Kristo mara ya kwanza, kwa maana Ibilisi anajua kwamba ikiwa atapoteza sasa, atapoteza milele — kwamba yeye hawezi kupata nafasi nyingine. Usio na kifani, kwa hivyo, ni hima kila mshiriki wa kanisa la saa ya kumi na moja sasa kwa upesi na kidete ajikaze dhidi ya jitihada za Adui kutoa pigo la mtoano. Lazima tuwe chonjo, pia, kutambua kwamba hilo pigo kwa kushangaza litakuja kutoka kwa adui tusiowatuhumu — kutoka kwa wanaodai kuwa ni marafiki wa injili, ambao ni wacha Mungu zaidi kuliko walivyokuwa makuhani katika siku ya Kristo. Zaidi ya hayo ni kutarajia kwamba Adui atatumia kila chombo iwezekanavyo kumzuia Bwana asiwafunue waonekane Wake sasa wasiojulikana 144,000 watumwa malimbuko, ambao watakwenda kukusanya ndani mavuno ya pili (Ufu. 7:9). Yule Adui atajaribu kila kitu atakachofikiri kukanganya, na kuufunika Ukweli, hasa kwa mada ya watu 144,000.” {WHR: 33.2} [498]

Je! sasa ni ya kumi na moja?

Swali 4:

Je! Sasa tuko katika saa ya saa 11, au ni baada ya Kanisa kutakaswa?

Jibu 4:

Ili kuelewa kwa usahihi iwapo au la tuko katika saa ya saa 11, lazima kwanza tuelewe vipengee viwili muhimu: 1) saa ya 11 ni nini, na 2) kwamba vipo vipindi viwili vya saa ya kumi na moja katika siku ya mfano ya muda wa rehema, kimoja kwa Kanisa na kimoja kwa ulimwengu. Taarifa ifuatayo husema kwamba saa ya mwisho ya siku ya mfano au wakati wa rehema ni saa ya 11:

“Hivyo, muda mfupi baada ya kusimamishwa, shirikisho hili la kanisa na serikali litatoweka kabisa, kama “jiwe la kusagia” kubwa ambalo linatupwa katika bahari (Ufu. 18:21). Na kilio cha waombolezaji wake kitakuwa: “kwa kuwa katika saa moja utajiri mwingi namna hii umekuwa ukiwa.” Ufu. 17:12; 18:10, 17. Hii saa ambayo inaleta maumivu ya kifo cha Babeli, haiwezi kuwa nyingine isipokuwa ile ambayo, kulingana na mfano wa Yesu (Mat. 20:11-16), ni ya mwisho kwa saa ya mfano (kipindi) cha kutwa (muda wa rehema); yaani, kutoka kwa mwito wa watumwa wa saa ya kumi na moja (ujumbe wa mwisho kwa ulimwengu — Mal. 4:5), hadi saa ya kumi na mbili (jua likitua saa za kale), mwisho wa siku — kufungwa kwa kipindi cha injili (Mat. 24:14), mwisho wa mavuno (Yer. 8:20), kufungwa kwa muda wa rehema (Ufu. 22:11). {TN12: 34.1} [145]

The last hour, the eleventh–the most momentous in history–is about to strike, when the billions of earth are to hear the gospel’s final plea, and Mercy’s farewell cry to unrepenting sinners. Upon the purity of this final message and the force given to it now in the sealing time of the first fruits, hangs the fate of the Church and the world. If it goes forth in company with pet theories and fanatical ideas (unsound doctrines), with faultfinding, talebearing, reporting, backbiting, and slandering (evil speaking), how can we dare think that it will charm the ear and turn the heart Zionward”? {9SC1-12: 8.2.8} [538]

“Kufikia hapa, ukweli unasimama wazi kwamba mwito huu wa mwisho unakuja kwa saa ya mwisho ya siku ya mfano, kabla tu kazi ya injili kufunga. Ukiwa ni ujumbe wa mwisho wa rehema kwa dunia, na pia mwito wa mwisho kwa watumwa, basi lazima utangazwe na nabii Eliya, naye atakayeonekana tu

Aprili – Mei – Juni 2021 | Msimbo wa Nembo, Gombo 2021, Nam. 4, 5, 6 | Ukurasa 36  wa 48

kabla ya “siku iliyo kuu na ya kuogofya ya Bwana.” Mal. 4:5; Mat. 17:11. Vivyo hiyo, watumwa wa saa ya kumi na moja lazima waitwe kazini naye anapoitangaza siku ya Bwana, siku ambayo Bwana anachukua pepeto mkononi Mwake (Mat. 3:12; Shuhuda, Gombo la 5, uk. 80; Shuhuda kwa Wachungaji, uk. 373), na kuusafisha “uwanda Wake” — kuyapeperusha makapi na kuyachoma magugu. Mara tu anapoiweka ngano katika “ghala” Lake (Mat. 13:30), ndani ya kanisa Lake la Ufalme, linadumu bila magugu, na hivyo “kanisa tukufu, lisilo na waa, kunyanzi, au kitu kingine chochote; … takatifu lisilo na mawaa.” Efe. 5:27. Nyumba Nyeupe ya Mungu kweli kweli! (Tazama Isa. 52:1, Yoeli 3:17, Nah. 1:15).”  {WHR: 29.1} [497]

Taarifa zifuatazo husema kwamba kupo kufungwa kuwili kwa wakati wa rehema:

“Itagunduliwa kwamba ufungwaji wa mlango wa rehema kwa kanisa na ule wa ulimwengu ni matukio mawili tofauti. La awali ni uwakilishi mdogo wa la mwisho. Andiko la kwa lililotangulia linapatikana katika Mathayo 25:11, 12; lakini kwa la mwisho tunasoma: “Mwenye kudhulumu, na azidi kudhulumu: na mwenye uchafu, na azidi kuwa mchafu: na mwenye haki na azidi kufanya haki: na mtakatifu, na azidi kuwa mtakatifu. Tazama, naja upesi, na ujira wangu u pamoja nami, kumlipa kila mtu kama kazi yake ilivyo.” (Ufu. 22:11, 12.) Wakati huu wale ambao walikuwa kama wanawali watano wapumbavu, watasema, “Mavuno yamepita, wakati wa hari umekwisha, wala sisi hatukuokoka.” (Yer. 8:20.) “Nao watatanga-tanga toka bahari hata bahari, na toka upande wa kaskazi hata upande wa mashariki, watapiga mbio wakienda huko na huko, kulitafuta neno la Bwana, wasilione.” (Amosi 8:12.)” {SR2: 186.1} [111]

“Kanisa huonekana linafahamu sana kuhusu wakati wa rehema kufungwa kwa ulimwengu, lakini halina ufahamu kwamba rehema kwa washiriki wake hufunga hasa kwa wakati wanapoukataa ujumbe uliotumwa na mbingu. Hapa inaonyeshwa kwa nini wanawali watano wapumbavu waliupata mlango umefungwa ingawa walikuwa wameyapata baadaye mafuta na kufika mlangoni: Rehema yao ilikuwa imefungwa wakati waliposhindwa katika fursa ya kwanza kuvijaza vyombo vyao na mafuta ya ziada, ujumbe wa ziada.”  [394]

Kutoka kwa taarifa ambazo zimenukuliwa mpaka sasa, ni wazi kama kioo kwamba saa ya kumi na moja kwa Kanisa na saa ya kumi na moja kwa ulimwengu ni vipindi vya wakati vilivyotengana na dhahiri. Kwa maarifa haya mkononi, twaweza kuelewa kwa usahihi taarifa zinazohusu saa ya kumi na moja au kabla ya saa ya kumi na moja katika mpangilio wa muktadha wazo. Taarifa zifuatazo hutuambia wakati saa ya kumi na moja ilianza kwa Kanisa:

“Kazi takatifu ambayo tumekabidhiwa hutushurutisha tutete kwa bidii na wote ambao wameupokea huu wa thamani “ukweli wa sasa” kwamba wawe waaminifu, maana kuipokea tu nadharia ya ujumbe hukutamsaidia yeyote kati yetu. Hakika sasa tuko katika mwito wa “saa ya kumi na moja,” na jinsi Bwana alivyofanya wonyesho kwa Wayahudi wa kale namna “Hukumu na Rehema zilikutana na Haki na Amani kubusiana ,” hivyo hivi karibuni tutaona jinsi Mungu atalijibu swali lililozushwa na wa kale nabii wa injili alipouliza:” {2SC2: 2.9} [170]

“Hakuna, Mwaadventista wa Sabato mkweli na mtiifu ambaye macho yake yamefumbuliwa kwa hali ya kanisa, na ambaye husoma hizi taarifa za kushtua mintarafu ya hatma yake ya kusikitisha anaweza ila kuomboleza, naam, hata “kuugua na kulia kwa sababu ya machukizo yanayotendeka kati” yake. Iwapo sisi waamini wa ukweli wa Sasa hakika tunaamini yale tunayotangaza, kwa kweli “Tutapiga kelele, wala hatutaacha.” Tutaharakisha kwa ndugu zetu ambao wanajishughulisha sana na utaratibu wa kanisa, na kuwasihi waisikilize sauti ya rehema ambayo inavuma sasa katika “mwito wa saa ya kumi na moja.” {3SC11-12: 11.1.1} [369]

“Je! Tunautangaza ujumbe wa saa ya 11 sasa au hautatangazwa hadi baada ya kutimizwa Ezek. 9? Je! Malaika ambaye ataangaza nchi kwa utukufu wake (M.A. 277) tayari amekuja?” Iwapo musaili atatafuta habari kwa chati ukurasa wa 224 wa Gombo la 2 la Fimbo, ataona kwamba malaika wa Ufu. 7 na 18 wanawakilishwa kama wanaokuja saa ya 11, na kwa vile tuko katika wakati wa kutiwa muhuri, unathibitisha kwamba sasa tuko katika saa ya 11. {1SC6: 10.9} [43]

Aprili – Mei – Juni 2021 | Msimbo wa Nembo, Gombo 2021, Nam. 4, 5, 6 | Ukurasa 37  wa 48

At the 11th Hour: Matthew 20

Kutoka kwa hizi kumbukumbu za ziada, twaweza kuona dhahiri kwamba sasa tuko katika saa ya 11 ya Kanisa. Tumekuwa katika saa ya 11 ya Kanisa tangu ujumbe ulipoanza kuvuma katika mwaka 1929; na wakati uliotajwa u karibu kukoma, rehema ya Kanisa la 11 I karibu kufunga kwa Kanisa kama mwili. Bali kama inavyoonekana katika 2TG11: 11.2, rehema kwaprobation kwa baadhi imefungwa tayari. Twamshukuru Mungu kwamba bado I wazi kwa baadhi, maana walikuwa wakidanganywa; tunaomba majibu haya yatawaamsha.

Kwa mujibu wa WHR: 29.1, iliyonukuliwa hapo juu, tunaona kwamba Eliya wa Uakisi lazima awe katika Kanisa na watumwa lazima waitwe kazini wakati Eliya wa uakisi anatangaza kwamba Bwana yu karibu kulitakasa Kanisa, Eliya aliyetajwa hataonja mauti maana mfanowe hudai kuhamishwa hadi mbinguni bila kufa. Kumbuka kwamba wapo malaika wawili kwa saa ya 11 katika chati ya Mathayo 20, mmoja akimwakilisha Eliya, aliyeuleta ujumbe katika mwaka 1929, na yule mwingine Eliya wa uakisi. Yeye anaitayarisha njia ya ujio wa Bwana kulitakasa Kanisa.

NDOA ZA UMBALI MREFU

Swali Namba 5:

Je! Inafaa wanandoa kuishi katika miji mbalimbali kwa ajili ya kazi au sababu zinginezo kama hiyo?

Jibu:

Haifai kwa mme na mke kuishi katika miji mbalimbali. Iwapo ni hali ya muda mfupi ambayo ni lazima kabisa kwa kuitegemeza familia, wanandoa wote lazima wakubaliane na wakati ulio kati ziara zisikawishwe kwa muda mrefu. Unapaswa kuzuru nyumbani mara kwa mara, na mawasiliano lazima yawe ya daima ili kuepuka kufarakana. Isiwe hali ya muda mrefu.

Advert Of Hosea 2:2. Volume 2021 The Symbolic Code Nos. 4-5-6

ANGALIA: Makala ya Kuzaa Watoto yatakuwa katika toleo lijalo la Msimbo wa Nembo.

Aprili – Mei – Juni 2021 | Msimbo wa Nembo, Gombo 2021, Nam. 4, 5, 6 | Ukurasa 38  wa 48

KONA YETU YA AFYA

Wapendwa wasomaji wa Msimbo, leo tutajikumbusha lile ambalo Bwana katika upendo Wake na utunzi alitushauri tutende zaidi ya miaka mia moja iliyopita:

JIFUNZE KUJIFANYIA MWENYEWE

Tiba Salama, Rahisi

“Kuhusu yale tunayoweza kujifanyia wenyewe, lipo jambo ambalo huhitaji busara ya kuzingatia kwa uangalifu. Lazima nijifahamu mwenyewe, Lazima niwe mwanafunzi siku zote jinsi ya kulitunza jengo hili, mwili Mungu amenipa, ili niuhifadhi katika hali bora kabisa ya afya. Lazima nile vyakula ambavyo vitakuwa vya manufaa yangu bora kimwili, na lazima nichukue tahadhari maalum nguo zangu ziridhishe mzunguko wa damu yenye afya. Nisijinyime mazoezi na hewa. Lazima nipate mwanga wote wa jua ambao inawezekana niupate.{ {2SM 296.3}

“Lazima niwe na hekima ili niwe mlezi mwaminifu wa mwili wangu. Nitafanya jambo lisilo la hekima kuingia katika chumba cha hewa baridi wakati mwili unatoa jasho; Nitaonyesha kwamba mimi si wakili mwenye hekima kukaa katika mazingira ya hewa iliyofungwa, na hivyo kujiachilia nishikwe na mafua. Nitakuwa sina hekima kukaa nyayo na miguu ikiwa baridi, na hivyo kuisukuma damu nyuma kutoka pembezoni hadi kwa ubongo au viungo vya ndani. Lazima siku zote nikinge nyayo zangu katika tabia nchi yenye unyevu. {2SM 296.4}

“Napaswa kula mara kwa mara chakula bora zaidi ambacho kitatengeneza damu bora zaidi, na nisifanye kazi bila kiasi iwapo ni katika uwezo wangu kuepuka kufanya hivyo.” {2SM 297.1}

“Na ninapozikiuka sheria, ambazo Mungu ameweka katika uhai wangu, Napaswa kuungama na kufanya matengenezo, na kujiweka katika hali nzuri zaidi chini ya madaktari ambao Mungu ametoa – hewa safi, maji safi, na mwanga wenye thamani unaoponya wa jua. {2SM 297.2}

“Maji yanaweza kutumika kwa njia nyingi ili kutuliza maumivu. Minywo ya maji moto, safi yanayonywewa kabla kula (zaidi au chini ya nusu lita), kamwe hayatafanya madhara yoyote, lakini badala yake yatazalisha mema. {2SM 297.3}

“A Kikombe cha chai kilichotengenezwa kutoka kwa mtishamba mnanaa hutuliza mishipa.” {2SM 297.4}

“Chai ya mhopi italeta usingizi. Dawa-bandika ya mhopi juu ya tumbo itaondoa maumivu. {2SM 297.5}

“Iwapo macho ni dhaifu, ikiwa kuna maumivu machoni, au mwasho, vitambaa laini vya fulana vilivyoloweshwa katika maji moto ya chumvi, yataleta afueni haraka. {2SM 297.6}

“Wakati kichwa kina msongo, iwapo nyayo na miguu itaoshwa kwa maji yaliyo na haradali kidogo, afueni itapatikana. {2SM 297.7}

“Zipo tiba rahisi nyingi zaidi ambazo zitafanya mengi kurejesha utendaji kiafya wa mwili. Kwa matayarisho haya yote rahisi Bwana hutarajia tuyatumie kwa ajili yetu wenyewe, lakini kupita kiasi kwa mwanadamu ni fursa za Mungu. Iwapo tunapuuza kufanya lile lililo karibu ambalo kila familia inaweza, na kumwomba Bwana atuondolee maumivu wakati tu wavivu sana kutumia dawa hizi zilizo katika uwezo wetu, ni kiburi tu…” {2SM 297.8}

Hili ndilo Baba yetu atupendaye na kututunza alitupatia kama watoto Wake kutusaidia tuwe “watu wa kushangaza.” Alihakikisha kwamba ipo mitishamba ya madawa yenye thamani inayokua tele duniani kote ambayo twaweza kutumia kwa uhuru kwa kila aina ya njia.

Aprili – Mei – Juni 2021 | Msimbo wa Nembo, Gombo 2021, Nam. 4, 5, 6 | Ukurasa 39  wa 48

Mara nyingi, huidharau hii mitishamba tunapoiona kwenye bustani zetu au yadi, huing’oa, na kuitupa. Uzoefu wangu baada ya kuishi katika maumbile asili kwa muda sasa ni kwamba Mponyaji wetu Mkuu alitoa kila kitu kuzuia magonjwa na kutuponya kupitia tiba asili. Tunaambiwa pia tufanye utafiti wa miili yetu, kwa vile ni lazima sisi sote tuwe wana-matengenezo wa afya. Njia moja wapo ya kujifahamu ni kujifunza sayansi ya viungo vya mwili wa mwanadamu.

TUANZE KWA KUJIBU HII CHEMSHA BONGO YA MWILI:

Taja sehemu 24 za mfumo umeng’enyaji wa mwanadamu:

Ni mangapi unajua kuuhusu mfumo umeng’enyaji wako? Ng’amua kwa kujibu hili swali!

Chemsha bongo ya Afya Namba 1:

Ni mrefu kiasi gani utumbo mdogo wa mtu mzima?
Futi 22
Inchi 30
Maili 30
Futi 17

Utapata majibu katika toleo lijalo.

Jifunze Kujitibu Mwenyewe!

“Njia ya kweli ya kuwaponya wagonjwa ni kuwaambia miti shamba ambayo hukua kwa ajili ya manufaa ya mwanadamu. Wanasayansi wameambatisha majina makubwa kwa matayarisho haya rahisi, bali elimu ya kweli itatuongoza kuwafunza wagonjwa kwamba hawahitaji kumwita daktari tena kuliko vile wangemwita wakili. Wao wenyewe wanaweza kutumia miti shamba rahisi ikiwa ni lazima.” {PH144 13.1}

“Kuielimisha familia ya mwanadamu kwamba daktari pekee yuajua magonjwa yote ya watoto wachanga na watu wa kila umri ni fundisho la uongo, na punde sisi kama watu tukisimama juu ya kanuni za matengenezo ya afya, baraka itakuwa kubwa itakayowajia wale ambao watafanya kazi ya kweli ya matibabu. Ipo kazi ya kufanywa kuwatibu wagonjwa kwa kutumia maji na kuwafunza watumie kabisa mwanga wa jua na mazoezi ya mwili. Hivyo kwa lugha rahisi, twaweza kuwafunza watu jinsi ya kudumisha afya, jinsi ya kuepuka magonjwa. Hii ndiyo kazi ambayo zahanati zetu zinahitajika kufanya. Hii ni sayansi ya kweli.” – M.S. 105, (uliandikwa Agosti 26, 1898) {PH144 13.2}

Jifunze Njia za Mungu

Chochote kisiingizwe ndani ya mwili wa mwanadamu ambacho kitaacha nyuma mvuto wa kuumiza. {MM 228.3}

“Hii ndiyo njia ya Mungu. Miti shamba ambayo hukua kwa manufaa ya mwanadamu, miti shamba kiasi kidogo michache iliyotiwa ndani na kuloweshwa na kutumika kwa maradhi ya ghafla, imetimiza lengo mara kumi, naam malengo mara mia moja vyema, kuliko madawa yote yaliyofichwa chini ya majina ya ajabu na kuuondoa ugonjwa.” {PH144 12.2}

“Ni udanganyifu na upuuzi, na Bwana amenifichulia kwamba utendaji huu hautadumisha uhai, bali utaingiza katika mwili vitu ambavyo havistahili kuwa humo, maana vitafanya kazi mbaya kwa mwili wa mwanadamu.” – Barua 59, 1898 (iliandikwa Agosti 29, 1898) {PH144 12.3}

Aprili – Mei – Juni 2021 | Msimbo wa Nembo, Gombo 2021, Nam. 4, 5, 6 | Ukurasa 40  wa 48

JUMUIYA YA WADAUDI MAKUHANI NA WANA-MFALME

DPPS ni Jumuiya ya Ndugu katika Kanisa la saa ya Kumi na moja. Lengo lake ni kuwatia moyo, kuwainua, kuwashauri na kuwaunganisha Ndugu kuombeana kwa heshima ya changamoto zote ambazo sisi, kama Ndugu, hupitia katika safari yetu ya Ukristo – iwe ni katika useja, ndoa, ubaba, au katika hali nyingineyo ya kifamilia.

Twamshukuru Bwana kwa jukwaa hili la ajabu ambapo kwalo twaweza kugawiana mawazo: kama jinsi ya kupata riziki; jinsi ya kusimamia imani yetu; jinsi ya kwendesha familia zetu; jinsi ya kuwatunza wake zetu, watoto, na wote walio katika mzingo wa mvuto wetu n.k.

Kati ya baraka zetu nyingi sasa ni kuanzishwa kwa Shirika la Ajira la Watunza Sabato (SKEA), ambalo litasaidia kukidhi mahitaji ya Ndugu zetu ambao hawana ajira na pia kuwasaidia Walaodekia na waamini wengine wote watunza Sabato kujiandikisha kutangaza ajira ya aina yoyote. Tunatamani sala zenu kwa ajili ya mradi huu uliobarikwa kwa sababu pia hakika utakuwa “kabari Inayopenyeza” ya kuwafikia ndugu wengi na Ukweli wa sasa.

“Hali ya mambo kama hiyo ilikuwapo katika siku, za Eliya. Kanisa, nyumbani na shule “zilikuwa zimeoza katika miaka ya uasi wa Israeli,” na zikasalia hivyo hadi Eliya alipokuja na kuzirejesha. Kazi yake ya

kuzisimamisha tena shule za manabii, “kufanya uandalizi kwa vijana kupata elimu ambayo ingewaongoza kuitukuza sheria ya Mungu na kuifanya iheshimiwe,” ilikuwa msingi mmojawapo wa kuifanya taasisi ya shule kuwa chombo katika kurejesha na kuliunganisha kanisa na nyumba, na kuwapatanisha wazazi na watoto. {3SC3-4: 5.1.2}

Sasa, katika siku hii ya uasi-imani mkubwa, wakati kanisa, nyumbani, na shule ziko haswa katika maumivu ya kifo cha kuoza, Eliya lazima arejeshe tena jinsi Maandiko yanavyosema, “vitu vyote.” Na, kwa mujibu wa mfano, taasisi iliyorejeshwa ya shule za manabii inapaswa kusimama kama mvuto wa kushirikisha kati ya kanisa na nyumba, mzazi na mtoto. {3SC3-4: 5.1.3}

“Angalieni, Nitawatumia nabii Eliya kabla haijaja siku ile ya Bwana, iliyo kuu na ya kuogofya. Naye ataigeuza mioyo ya baba iwaelekee watoto wao, na mioyo ya watoto iwaelekee baba zao, ili nisije nikaipiga dunia kwa laana.” (Mal. 4:5, 6.) {3SC3-4: 5.1.4}

Kwa hivyo DPPS ni Shule ambayo itawaamsha wanawali wenye busara watu walio ishara — waache kusinzia na kwa haraka wajiandae kwa ujio wa Bwana arusi hivi karibuni. Imekuwa

baraka ya ajabu kukua pamoja hadi tuifikilie Haki ya Kristo tangu kuanzishwa kwa Idara hii mwezi wa Mei 2019, na sasa tumekuwa Wadaudi Makuhani na Wana-Mfalme bora kwa kujadili masuala ya Undugu.

Kila mmoja wetu, unajua, katika maumbile yetu ya mwili kawaida hupitia vipindi vitatu: (1) utoto, (2) ujana, na (3) ukomavu. Vivyo hivyo, katika hali yetu ya kiroho, jinsi ilivyoonekana katika Salamu Mwafaka, Gombo la 2, No. 39, na Trakti Namba 14, Utabiri wa Habari za Vita, uk. 31-39, tunapitia katika vipindi vitatu kama hivi vya ukuaji: (1) Haki kwa Neema, kilicho sawa na utoto wa kiroho (kuzaliwa mara ya pili), (2) Haki kwa Imani, kilicho sawa na ujana, na (3) Haki ya Kristo, ambacho kwa kweli ni ukomavu wetu wa kiroho. Na kwa kuwa kipindi cha “utoto”, haki kwa neema sasa ki katika wakati wa zamani kwa mujibu wa Salamu Mwafaka, Gombo la 2, Namba 39, na sasa tumekuja kwa kipindi cha haki kwa imani cha “ubalehe,” ambacho ndani yake usalama wetu na maslahi ya milele yamo, hatupaswi kupuuza kufikia ukomavu kamili wa Ukristo, haki ya Kristo, ikiwa tunatarajia kutuzwa uzima wa milele pamoja na makao katika Ufalme Wake. {CFL: 1.2}

Ndugu Jerry Cox,

Kaimu Katibu DPPS.

D  P  P  S

Aprili – Mei – Juni 2021 | Msimbo wa Nembo, Gombo 2021, Nam. 4, 5, 6 | Ukurasa 41  wa 48

KUTAFUTA DOSARI

Mazungumzo ya Asubuhi na Bi. E. G. White
Ottawa, Kansas, Mei 12, 1889

Adui yu kazini na wale ambao wamejitia katika kutilia shaka na kutoamini; na hawaridhiki kuwa tu pale wenyewe, bali wakati wote huwaimarisha wengine katika msitari huo, na hutaka wengine waamini kama wao. Kutoka katika nuru Mungu amenipa, kamwe haikuwapo nuru mpya yoyote iliyokuja kutoka mbinguni bila Shetani kuweza kupata jambo ndani yake la kuchambua. Na ndivyo ilivyo na baadhi ya watu leo – huyachambua mambo madogo. Wao hutaka nuru, lakini huja adui kama alivyofanya kwa watu wa Nazareti, na ingawa Roho wa Mungu aliwaambia kwamba Yesu alikuwa ndiye mtiwa mafuta na Kristo aliwaambia iliyokuwa kazi Yake –kuzivunja nguvu za adui na kuwaweka huru waliodhulumiwa, kuvifungua vifungo vya uovu na kuwahubiri maskini habari njema [tazama Luka 4:18]–[walibaki katika mashaka na kutoamini]. {1SAT 93.1}

Lakini huonekana kwangu kwamba hatuyapokei mambo haya na kupata mafunzo kutoka kwayo tunavyopaswa. Wasioamini waliinuka na ibilisi akatumia fursa hiyo na kuanza kazi, na wakaanza kusemezana, ni nani Huyu? Huyu si mwana wa Yusufu na Maria? Na dakika ile ile wazo hili liliwajia akilini wakaanza kulitekeleza. Na mwajua jinsi lilivyotenda kazi. Waliinuka na kumkamata Kristo na kumpeleka mpaka ukingo wa kilima Wamtupe chini. Sasa, hayajafanywa maboresho yoyote katika asili ya mwanadamu tangu wakati huo. Asili ya mwanadamu bado ni ile ile. Iwapo kuna jambo ndogo ambapo wanaweza kukengeuza nia zao, wao hulitumia kabisa. Huonekana katika mashauri. Limeonyeshwa kwangu tena na tena. Wao [viongozi wa kanisa] wanaweka mipango kwa kazi ya Mungu, wakijaribu kufanya mipangilio ambayo kwayo wanaweza kuiendeleza kazi ya Mungu, na hapo husimama mtu fulani akijaribu kuzuia magurudumu. Kama nilivyosema kwa ndugu yetu mmoja si muda mrefu uliopita, “Umefanya zaidi

kuzuia kazi ya Mungu kuliko maadui zetu kumi au ishirini, kwa sababu huifafanua hoja fulani kuwa jambo la ajabu, na umeshikilia kamati kwa masaa bure, kwa kutupa ndani tu kibao kulizuia gurudumu, wakati uliopotezwa na maazimio mazuri ambayo yangetekelezwa yamepotea. Wewe huingia ndani na wao hufikiri wewe ni mtu mzuri, mwenye maadili, na ulisemalo ni sawa, na kila mara ukiwa na kipande cha kutupa ndani, na wanatiwa hofu kwa mashauri yao na hakuna jambo linafanikishwa ambalo lingetekelezwa, kwa sababu ya hicho kizuizi.” {1SAT 93.2}

Sasa ndugu nataka niwaambie, Roho wa Mungu anapokuja kati yetu, atagusa nia zilizo tayari kumpokea. Lakini nia zao zisipokuwa wazi kumpokea, zote zitakuwa tayari kupitisha hukumu kwa mjumbe na kwa maneno yanayonenwa. Badala ya kuja kwa Mungu na Kumwomba awape moyo mpya na nia mpya, ili mvuto unaobadilisha wa neema ya Mungu iwe juu yao, wao huanza kutafuta makosa na kuchambua dosari. Roho hawagusi, na lazima apatane na mawazo yao na watasimama papo hapo hadi mambo haya yaondolewe njiani, na wajikite papo hapo kuhukumu. Hivi ndivyo ilivyokuwa Minneapolis. {1SAT 94.1}

Ni kwa sababu najua roho ile ile i hapa, na ya kwamba hatupaswi kuipatia nafasi hata kidogo ndiposa nasema mambo haya. Najua kwamba Roho wa Mungu atakapozishawishi nia za wanadamu, adui ataingia ndani na kutumia sana jambo lolote ndogo sana ambalo anaweza kufanya na chachu itaanza kazi kwa sababu ibilisi anataka hivyo. Sasa ndugu na dada nataka niwaweke mjilinde. Nataka niwaulize iwapo mmeridhika na ubaridi wenu, kutoamini kwenu, ukengeufu wenu. Je! Hamjatosheka nao? Iwapo sivyo, ibilisi atawapatia yote mtamanio. Hatutaki tena. {1SAT 95.1}

Aprili – Mei – Juni 2021 | Msimbo wa Nembo, Gombo 2021, Nam. 4, 5, 6 | Ukurasa 42  wa 48

Tunaona kwamba hatuko katika hali bora kuliko Wayahudi. Mungu aliwapa nuru wazi ili wasimae kama watu Wake watakatifu, wa milki ya Mungu. Aliwapa manabii, kisha Kristo Mwenyewe alikuja ili Auwasilishe ukweli kwao. Lakini taifa Lake lenyewe Lilimkataa, Akageuka. Akawaambia, “Mlio na masikio, lakini hamsikii, mlio na macho ila hamwoni.” (Yeremia 5:21.) Wakahoji, “Je!

Picking Flaws pg 43.

sisi nasi tu vipofu?” Kristo akawaambia, “Kama mngekuwa vipofu msingekuwa na dhambi, lakini sasa nuru imekuja na mmechagua giza badala ya nuru.” (Tazama Yohana 9:41) Je! lilikuwa giza halisi? La, halikuwa. Nuru ya ilikuwa imewaangazia, lakini Shetani alikuwa akiwatupia kifumba macho mbele ya macho yao, na hawakuipokea. {1SAT 95.2}

Sasa ndugu, ipo hapa baraka kwa ajili yenu. Mwaweza kufikiri ni ajabu kwamba nanena nanyi kuhusu mambo haya, bali ni wajibu wangu. Kamwe hatutaki jambo hili litendwe tena kwa dunia ya Mungu; na Mungu akinipa nguvu nitatenda. Nataka muulize, Iko vipi nafsi yangu? Utaipokea nuru, au utasimama ukilalamika? Ni wakati tunapaswa kujua tulipo. Tunapaswa kuwa na nafasi ya kuomba na kunena na kumtafuta Mungu. Tunamtaka Bwana, na hututaki kitu kingine chochote. Lakini tunapata hapa katika maneno ya Zekaria. Yoshua alisimama mbele ya Bwana, na Shetani akasimama mkono Wake wa kuume ili kushindana naye. “Bwana na akukemee,” Akasema, “je! hiki si kinga kilichotolewa motoni?” (Zekaria 3:2). . {1SAT 95.3}
Sasa hapa wapo watu wa Mungu na Mungu anawahitaji

mwe mkijitayarisha kwa siku kuu ya wokovu, kwamba mwe mkiwawezesha wengine kuwa tayari. Yeye anataka mwe mnajiweka sawa, ili mweze kuwa na ujumbe kwa ajili ya watu utakaokata kwa kupita katika moyo wa nyama, na ya kwamba mweze kupiga kelele ukumbini na madhabahuni, “Uwaachilie watu Wako, Ee Bwana, wala usiutoe uridhi Wako upate aibu” (Yoeli 2:17). Sasa fungueni masikio yenu kwa ukweli ambao mmesikia na mweke mbali mashaka yenu, kutoaamini, na mawazo yasiyo ya Kristo.{1SAT 96.1}

Mungu ataka mje na mnywe maji safi ya vijito vya Lebanoni, na mkiisha kuyanywa mtataka kuwaita wengine wanywe. Mwongofu baada ya mwongofu huonyeshwa kwangu asiyejua ni nini kuwa na imani ndani ya Kristo. Inaonekana wako tayari kufa; hamna nuru ndani yao; wanakufa kwa kumkosa Mungu. {1SAT 96.2}

Nalienda katika mkutano ambako nilikaa siku tatu tu, na katika wakati huo nalinena kwao mara saba. Waliniomba nikae zaidi; walionekana kuwa na njaa, na walisimama na kuzungumza jinsi waliutaka ukweli huu na nuru hii, lakini ibilisi alikuwa tayari kuleta ndani jambo fulani kuifungia nje nuru, na wengi wako radhi iwe hivyo. Hawajui ni vipi angahewa safi ilivyo, bali Bwana atusaidie ili nuru wazi ya utukufu Wake ituzunguke. Mungu atusaidie tusimame mahali pafaapo kabla ya adui ili nia zetu zitengwe kutokana na mambo ya chini na tuyashikilie yatokayo juu. {1SAT 96.3}

Kristo, alipokuwa akinena kwa watu wa wakati Wake, aliwaambia kwamba walikuwa wameyafumba macho yao na kuziba masikio yao wasije wakaona kwa macho yao wakasikia kwa masikio yao wakaelewa kwa mioyo yao wakaongoka Akawaponya. (Tazama Mathayo 13:15). Walipewa nuru, lakini hawakutaka kuipokea. Giza liliwafunika, na walikuja na kutafuta dosari ndogo ndogo, na kuvuta nia za watu mbali kutoka kwa ukweli mzito uliokuwa wao. Sasa, itakuwaje nasi? Hatutaki kujiua hapa kuwatendea kazi, lakini hamtatenda kazi wenyewe? Tunataka tujue iwapo tutapata baraka tele za Bwana zikitua juu yetu, na tunatambua kwamba Yeye huiangaza nuru Yake kubwa na utukufu juu yetu. Hili ndilo ombi langu. –Muswada 2, 1889. (MR 900.22) {1SAT 97.1}

Aprili – Mei – Juni 2021 | Msimbo wa Nembo, Gombo 2021, Nam. 4, 5, 6 | Ukurasa 43  wa 48

QESS

Mabinti Jumuiya ya Malkia Esta (QESS) ilibuniwa Februari 24, 2019 kutokana na hitaji la kuwatia moyo Mabinti watembee katika nuru ya Ukweli wa sasa ili waweze kuwa wanawake wema na wawakilishi wa Kristo. Jukwaa ambalo mabinti wanaweza kujadili mambo yanayowahusu pekee.

Usharika katika QESS upo tu kwa Mabinti walio na hati ya usharika wa Kanisa la saa ya 11. Kuwapatia nafasi na kuwasaidia Mabinti ambao ni sehemu ya Kanisa lakini ambao hawajahitimu kuwa washarika wa QESS, kikundi kidogo, Mabinti kwa ajili ya Mabinti (SFS) kilibuniwa.

Idara ya QESS/Mabinti kwa ajili ya Mabinti ina Mwenyekiti, Naibu Mwenyekiti, Katibu, na Wanakamati sita: Roho Mtakatifu akiwa ndiye Kiongozi wa Jumuiya hii.

Kamati ya QESS hutafuta kutoa jukwaa salama ambalo kwalo Neno la Mungu huchambuliwa na majadiliano yenye maana kufanywa juu ya mada yoyote. Maadamu mawazo na mitazamo inagawianwa katika vikao, washarika hupokea habari za thamani ambazo ikiwa zitatekelezwa zitaboresha kila kipengele cha maisha yao.

OWITO WETU: Tukiangamia, na tuangamie.

MADA YETU: Tawala kwa imani na uchaji Mungu.

UTUME WETU: Kuuendeleza Ufalme wa Mungu ndiyo shughuli yetu kuu.

TABIA ZA BINTI MMALKIA ESTA

Ili kuwa kama Malkia Esta ni mwito wa upeo mno. Binti LAZIMA:

1. Amche Mungu Aliye Juu Sana.
2. Awe na uhusiano na Yesu Kristo.
3. Ahatarishe uhai wake kwa ajili ya kazi ya watu wa Mungu.
4. Awe mwajibikaji na kuwafanya wengine kuwajibika.
5. Amtegemee Mungu.
6. Awe mtendaji mwepesi.
7. Awe mwenye bidii na asiyesita kuomba.
8. Awe anayeomba bila kukoma.
9. Awe anayechukua muda kuwa pamoja na Mungu.
10. Amtambue Mungu kama Chanzo cha nguvu.
11. Afunge na kuomba kwa hatari ambayo inaweza kuwa inaendelea kati yetu.
12. Ajidhabihu.
13. Awe mwanamke aliye ishara.
14. Amtegemee Bwana.
15. Ahimize katika nyayo za Kristo.
16. Awe kielelezo kumcha Mungu.
17. Ajifunze na kuliamini neno la Mungu kikamilifu.

TAFADHALI KUMBUKA: QESS na SFS hukutana kila Jumatano ya 1 na ya 3 ya kila mwezi kwa Zoom saa 2 usiku saa za Kati [Marekani]. Mabinti, tutafurahi iwapo mtajiunga nasi!

Aprili – Mei – Juni 2021 | Msimbo wa Nembo, Gombo 2021, Nam. 4, 5, 6 | Ukurasa 44  wa 48

HISTORIA YA UJUMBE WA FIMBO YA MCHUNGAJI KATIKA SHAMBA LA UHOLANZI

Katika mwanzoni mwa miaka ya 1980, Ndugu Otmar Kortram, mcha Mungu mhubiri m’S.D.A. wa Suriname aliyezaliwa katika Ukweli wa Ujio na kuishi Marekani kwa miaka kadhaa, aliupokea ujumbe wa Fimbo ya Mchungaji kupitia kwa ndugu Mdaudi kutoka Mountaindale, New York. Baada ya kuukumbatia kwa shukrani na kwa bidii kuusambaza Ujumbe huo katika makanisa kadhaa huko Marekani, alisafiri kwenda Uholanzi na kuendelea kuutangaza Ujumbe katika makanisa ya S.D.A. huko. Ingawa wengi waliupinga, baadhi waliupokea – akiwemo nduguye wa damu, Iwan Kortram.

Kisha Ndugu Iwan kwa kuchangamkia kazi alianza kuutangaza ujumbe wa Fimbo katika makanisa ya S.D.A. nchini Uholanzi na kusambaza machapisho wakati wa kongamano la Baraza Kuu lililofanyika Utrecht katika mwaka 1995 bega kwa bega na Ndugu Antony Hibbert, Ishmael Rodrigues, Joseph Serafin, Terry Harrison, Jim Kakouri, na Glenroy Matthews. Ndugu hawa walikuwa wakimtembelea wakati huo, na katika mwaka 1996 alihudhuria DLI huko Mountain Dale. Walilikuwapo ndugu kadhaa waliojiunga na Ndugu Iwan kujifunza Ukweli, na wengine pia walikuwa wakiutangaza hata ingawa walikabiliwa na changamoto nyingi kutoka kwa viongozi wapinzani katika kanisa la S.D.A.

Umuhimu mkubwa wa Kweli za ajabu zilizo katika

Fimbo ya Mchungaji zilichochea moyo wa Ndugu Iwan na Bwana akamtwika mzigo maalum wa kutafsiri machapisho ya Fimbo kwa Kidachi ili ndugu wote wanaozungumza Kidachi waweze kusikia na kusoma Kweli hizi muhimu sana katika lugha yao na waokolewe kwa kuzipokea na kuzitenda. Hili lilisababisha Fimbo ya Mchungaji, Gombo la 2, kutafsiriwa kabisa, na machapisho mengine kadhaa yakafuata baadaye. Tafsiri ya Kidachi ya vitabu vya Fimbo ilikamilishwa katika mwaka 2016, ingawa kusahihisha bado ni mradi unaoendelea. Tunamsifu na kumshukuru Bwana kwa mafanikio haya.

History Of The Srod Message In The Dutch Field.

Karibu Desemba wa 1996, Ndugu. Iwan alijongelewa katika kanisa la S.D.A. huko Amsterdam na Dada Helga van Niel. Alikuwa ameelekezwa kwake na binamu yake kutoka Suriname, Ndugu Ricardo Kortram, ambaye pia alikuwa amepokea Fimbo kutoka kwa Ndugu Otmar na pia alikuwa amehudhuria DLI huko Mountain Dale. Dada Helga alikuwa ameupokea Ukweli kuhusu watu 144,000 kwa kujifunza na Ndugu Ricardo na alikuwa amehamia Uholanzi na mzigo maalum moyoni mwake kuutangaza

Ukweli wa Ujio na familia yake. Ilikuwa baada ya kufariki kwa mama yake ndipo familia yake (ambao walikuwa Wamoravia) wakawa tayari na nia ya kujifunza naye.

Alitaka pia kuutangaza Ukweli kuhusu watu 144,000 na familia yake lakini hakuwa na uhakika angeweza kufanya hivyo kwa vile hakuwa amepokea masomo yote na hakuwa amesoma vitabu vyote. Akiwa amesadikishwa kwamba huo ulikuwa Ukweli na ya kwamba familia yake ilihitaji kuusikia, aliomba kwamba mtu fulani aweze kupatikana ambaye aliufahamu Ujumbe huo vyema aushiriki pamoja nao. Bwana alijibu sala yake kwa kukutana na Ndugu Iwan na Otmar Sabato moja katika kanisa la S.D.A. huko Amsterdam Kusini-Mashariki.

Karibu familia yote – Binti wawili wa Dada Helga (Vanessa na Perla Pahlad); Dada Selma van Niel na watoto wake watatu; Dada Phili van Niel na watoto wake watatu; Ndugu Lloyd van Niel; Dada Norma Gilliot-van Niel, mumewe, Ndugu Wilco Gilliot (aliyefariki 2014) na binti yao Gabriella; na baba, Elwin van Niel (aliyefariki 2001) – aliukumbatia Ukweli wa kanisa la S.D.A. na Fimbo ya Mchungaji wakati uo huo baada ya mfululizo wa masomo na Ndugu Iwan. Ndugu Lloyd na Dada Phili pia walianza kusaidia kutafsiri Ujumbe kwa Kidachi. Ndugu Iwan na Dada Helga walifunga ndoa katika mwaka 1998.

Though there were many trials

Aprili – Mei – Juni 2021 | Msimbo wa Nembo, Gombo 2021, Nam. 4, 5, 6 | Ukurasa 45  wa 48

Ingawa yalikuwapo majaribu mengi na upinzani mwingi kutoka kwa uongozi wa kanisa la S.D.A.A., familia ya Kortram van Niel ilikuwa ikiutangaza Ujumbe kwa bidii na ndugu wengine waliopendezwa ilhali waliendelea kujifunza Ujumbe wenyewe. Katika mwaka 1998, upinzani kutoka kwa uongozi wa kanisa ulimlazimu Ndugu Lloyd, Dada Selma, na Dada Phili na wanawe wawili: Jahfaar na John, wabatizwe na Ndugu Anthony Hibbert, mchungaji Mdaudi kutoka Mountain Dale, katika kanisa la Wababtisti wa Sabato badala ya mchungaji wa S.D.A. katika kanisa la S.D.A. Katika mwaka 1999, Ndugu Lloyd pia alihudhuria DLI, akifuatiwa na Ndugu Jahfaar na Dada Perla katika mwaka 2000.

Karibu mwaka 2001, Ndugu Iwan alipokea kijitabu kutoka kwa Ndugu Don Adair ambamo mada ya “watu 144,000 na wale pamoja nao” ilishughulikiwa sana. Ndugu Iwan alikisambaza na kusoma kijitabu hiki na familia ya van Niel-Kortram na baada ya kuuona Ukweli,

familia iliupokea. Katika mwaka 2002, Ndugu Iwan na Lloyd walihudhuria Kikao huko Mountain Dale ambako waliwasilisha sababu zao kuamini “watu 144,000 na wale pamoja nao.” Hao ndugu hawakuupokea Ukweli huu, na tangu wakati huo familia ya Kortram-van Niel na ndugu wa Mountain Dale wakaachana kimafundisho, lakini kwa njia ya urafiki.

Hali hii iliendelea hata baada ya Dada Phili kufunga ndoa na Ndugu Ricardo na kuhamia Suriname kabisa katika mwaka 2008. Baadaye, katika mwaka 2011, Ndugu Lloyd, Iwan na Dada Helga pia walihamia Suriname kabisa, wakifuatiwa na Dada Selma katika mwaka 2013. Bwana alimwongoza tena Ndugu Iwan na Dada Helga kwa mawasilisho ya Ukasisi wa Mganda wa Kutikisa katika mwaka 2014-2015, na baada ya maombi yasiyokoma kutoka kwa Ndugu Iwan, Ndugu Sam mwishowe aliridhia na kuwazuru washarika wa Suriname katika mwaka 2015.

Tangu wakati huo na kwendelea, kundi la

washarika Suriname na Uholanzi (ambalo ni pamoja na familia ya van Engel / Bouterse / Vreds / Johnson huko Suriname na kina dada 3 wamchao Mungu wa’S.D.A. kutoka Rotterdam, Uholanzi – wote ambao familia ya Kortram-van Niel ilikuwa ikiwasambazia na kujifunza nao Ujumbe) walijiunga na masomo ya kanisa la saa ya Kumi na Moja. Twamshukuru sana Bwana ya kwamba tumekuwa tukishiriki katika mafunzo haya na katika kazi hii ya ajabu tangu wakati huo.

Tunaomba sala zenu kwa unyenyekevu, kwamba tutiishe vyote tulivyo navyo kwa maagizo ya Roho wa Kweli, ili tuweze kuendelea kutenda sehemu yetu kwa uaminifu na kwa kumcha Mungu katika shamba la Uholanzi ili tuendeleze kuanzishwa Ufalme wa Bwana, ambao unaharakisha kwa kasi.

Kwa moyo mnyofu kuusambaza Ujumbe wa ajabu sana,

Ndugu L. E. E. van Niel.

Matukio Yajayo

Shule ya Manabii ya Walimu, Sabato ya kwanza ya kila mwezi

Saa 1 asubuhi saa za Kati, Tuma Barua pepe kwa mwaliko, Rekebisha kulingana na eneo lako

Shule ya Manabii kwa washiriki wote, Sabato ya 2 ya Kila Mwezi

Saa 1 asubuhi saa za Kati, Rekebisha kulingana na eneo lako
Nambari ya Zoom: 940 2826 1432, Nenosiri: 1

Fundisho la Sabato Mchana, Saa 9 alasiri saa za Kati, Rekebisha kulingana na eneo lako

Nambari ya Zoom: 940 4716 3414, Nenosiri: 1

Mkutano wa Maombi wa Jumanne Jioni, Saa 2 Usiku saa za Kati

Nambari ya Zoom: 989 2478 5827, Nenosiri: 1

Wana-Mfalme na Makuhani Wadaudi (DPPS) Jumatano ya 2 na ya mwisho

Saa 2 usiku saa za Kati, Nam. ya Zoom: 964 6277 5768, Nenosiri: 1

Jumuiya ya kina dada ya Malkia Esta (QESS) Saa 2 usiku saa za Kati, Jumatano ya 1 na ya 3

Nambari ya Zoom: 959 0403 4695, Nenosiri: 7

Shule ya Manabii ya Walimu, Sabato ya kwanza ya kila mwezi

Saa 9 alasiri saa za Afrika Mashariki, Tuma Barua pepe kwa mwaliko, Rekebisha kulingana na eneo lako

Shule ya Manabii kwa washiriki wote, Sabato ya 2 ya Kila Mwezi

Saa 9 alasiri saa za Afrika Mashariki, Rekebisha kulingana na eneo lako

Nambari ya Zoom: 940 2826 1432, Nenosiri: 1

Fundisho la Sabato Mchana, Saa 4 Usiku saa za Afrika Mashariki, Rekebisha kulingana na eneo lako

Nambari ya Zoom: 940 4716 3414, Nenosiri: 1

Mkutano wa Maombi wa Jumatano Asubuhi, Saa 10 Alfajiri saa za Afrika Mashariki

Nambari ya Zoom: 989 2478 5827, Nenosiri: 1

Wana-Mfalme na Makuhani Wadaudi (DPPS) Alhamisi ya 2 na ya mwisho

Saa 10 alfajiri saa za Afrika Mashariki, Nam. ya Zoom: 964 6277 5768, Nenosiri: 1

Jumuiya ya kina dada ya Malkia Esta (QESS) Saa 9 alfajiri saa za Afrika Mashariki, Alhamisi ya 1 na ya 3.

Nambari ya Zoom: 959 0403 4695, Nenosiri: 7

Aprili – Mei – Juni 2021 | Msimbo wa Nembo, Gombo 2021, Nam. 4, 5, 6 | Ukurasa 46  wa 48

P
Picture
>