fbpx

Barua Iliyojumuishwa na Cheti cha Ushirika

Barua Iliyojumuishwa na Cheti Cha Ushirika

Mpendwa Mshiriki Mwenza:

Katika kutuma Cheti chako cha Ushirika cha mwaka huu, tunapenda kushiriki pamoja nawe mawazo machache ya Maandiko ambayo tumeyapata kuwa yenye msaada sana siku baada ya siku tunaposafiri njia ya Ukristo. {CFL: 1.1}

Kila mmoja wetu, unajua, katika maumbile yetu ya mwili kawaida hupitia vipindi vitatu: (1) utoto, (2) ujana, na (3) ukomavu. Vivyo hivyo, katika hali yetu ya kiroho, jinsi ilivyoonekana katika Salamu Mwafaka, Gombo la 2, No. 39, na Trakti Namba 14, Utabiri wa Habari za Vita, uk. 31-39, tunapitia katika vipindi vitatu kama hivi vya ukuaji: (1) Haki kwa Neema, kilicho sawa na utoto wa kiroho (kuzaliwa mara ya pili), (2) Haki kwa Imani, kilicho sawa na ujana, na (3) Haki ya Kristo, ambacho kwa kweli ni ukomavu wetu wa kiroho. Na kwa kuwa kipindi cha “utoto”, haki kwa neema sasa ki katika wakati wa zamani kwa mujibu wa Salamu Mwafaka, Gombo la 2, Namba 39, na sasa tumekuja kwa kipindi cha haki kwa imani cha “ubalehe,” ambacho ndani yake usalama wetu na maslahi ya milele yamo, hatupaswi kupuuza kufikia ukomavu kamili wa Ukristo, haki ya Kristo, ikiwa tunatarajia kutuzwa uzima wa milele pamoja na makao katika Ufalme Wake. Basi kwa hivyo tunapaswa kufanya vyema kukumbuka kwa uangalifu baadhi ya alama za mkristo mkomavu — Mdaudi wa kweli. Kama huyo hana budi ila

Kuchangia Kitu Kinachofaa kwa Dunia. {CFL: 1.2}

Mkristo mkomavu anajua vyema kwamba alizaliwa duniani ili kuiboresha, kiroho na kimaumbile, kwamba hakuja tu kuishi kwa ubinafsi ndani yake na kuondoka kwayo na “asante” kubwa ila kuibariki, kuacha ukumbusho wa yale ambayo Mungu ameweza kufanikisha kupitia kwake kwa ajili ya wanadamu, kiroho na kimaumbile; kwamba yeye ni kama tawi la kuzaa matunda katika nchi yenye jangwa, kwa maana anajua ya kuwa “kila mti usiozaa matunda mema hukatwa na kutupwa motoni.” Mat. 3:10. Kisha, pia, Mkristo mkomavu kama huyo

Ana Maono na Lengo. {CFL: 1.3}

Yeye huona kwamba anapata maono ya yale ambayo Mungu angemtaka afanye. Yeye hatembei katika mtindo wa kipepeo; yeye hujua kinachohitajika kufanywa na kukifanya. Yeye haitoi nafasi yoyote kwa mwaliko ambao itaweza kuvuta umakini wake na nguvu asilifikie lengo lake. Yeye anajua vyema kwamba “pale ambapo hakuna maono, watu huangamia.” Mit. 29:18. Yeye, isitoshe,

1

Huwajali Wengine. {CFL: 1.4}

Jicho lake hujali mahitaji ya wengine, na hufanya yote awezayo kukidhi mahitaji hayo bila kujali usumbufu na juhudi ya kibinafsi inayoweza kuhitajika kwake mwenyewe. Yeye hujali wa wengine wakati, hisia, umri, sifa, na uwezo, haswa mali ya watu wengine, kwa maana “upendo haumfanyii jirani neno baya.” Rum.13:10. “Msitende neno lo lote kwa kushindana wala kwa majivuno; bali kwa unyenyekevu, kila mtu na amhesabu mwenziwe kuwa bora kuliko nafsi yake. Kila mtu asiangalie mambo yake mwenyewe, bali kila mtu aangalie mambo ya wengine.” Filp. 2:3, 4. Yeye

Hana Ubinafsi Kabisa. {CFL: 2.1}

Yeye hushangilia bahati nzuri ya wengine, na hupenda wengine wapokee sifa kwa jambo ambalo yeye mwenyewe ameweza kutekeleza. Yeye hutarajia sifa yake kutoka kwa Bwana pekee. Lile mkono wake wa kulia hufanya mkono wake wa kushoto haulijui (Mat. 6:3, 4). Yeye pia

Jasiri na Bila Hofu. {CFL: 2.2}

Yeye hajui hofu ila kumcha Mungu. Ana ujasiri wa kusimama kidete ila kwa busara kwa msimamo sahihi bila kujali athari kwake mwenyewe. Yeye hujua kwamba hakuna mtu anayeweza kumdhuru iwapo Mungu hawezi kuruhusu. Isitoshe, anajua kwamba ingawa wanadamu wanaweza kuua mwili wake, hawawezi kuigusa roho yake (Mat. 10:28). Mungu pekee ndiye ngao yake. Yeye zaidi, ni,

Mwenye Hisani. {CFL: 2.3}

Yeye ni mwaminifu katika tathmini binafsi ya mwenyewe na mwenye hisani kwa wengine wote, akitambua kwamba iwapo maisha yake yangekuwa sawa na yao yeye mwenyewe angekuwa sawa sawa kama wao; kwamba wakati wengine wakikosea katika jambo moja yeye mwenyewe anaweza kukosea katika kingine. Anajua kwamba Mungu anaweza kurekebisha mtumwa Wake mwenyewe (Rum. 14:4-7), na huzuia mikono yake. Yeye ni

Bwana wa Hali. {CFL: 2.4}

Yeye hushukuru mbele ya hali ngumu aumazingira yanayovunja moyo. Yeye hapotezi nguvu zake kwa kunung’unika na kununa, na hatafutii kukwepa jukumu la kutowajibika na kweli zisizopendeza. Wala hajiruhusu kuangushwa chini wakati wa matatizo, lakini yeye yu karibu kila wakati “kusimama kwa zamu yake,” na huteka rasilimali zake za kiroho kufikia ustadi hali zake. Habaki nyuma ya Yusufu wa zamani, yuko hata mbele yake kwa maana anajua kwamba anaishi katika msimu uliostawi. Bado zaidi, yeye

Kamwe si wa Hisia nyepesi. {CFL: 2.5}

Mashtaka ya upumbavu kamwe hayamtaabishi. Yeye hakasirishwi nayo. Hahitaji kamwe kubebwa na glavu za mikononi. Hakazii nia yake kamwe kwa kitu chochote kitakachomfanya ajihisi ameumia. Iwapo jambo fulani limesemwa dhidi yake,

2

yeye kamwe haumizwi nalo, haswa ikiwa hana hatia ya jambo hilo. Yeye halipizi kisasi, yeye huliacha jambo lisilofaa life lenyewe. Yeye haruhusu kukata tamaa kuingia ndani ya mawazo yake, si hata ikiwa wote watamwacha. Yeye hukumbuka vyema kwamba hata Bwana Mwenyewe aliachwa na wafuasi Wake mwenyewe, na ya kwamba kati ya watu milioni kadhaa walikuwako watu wawili tu asilimia mia moja kwa Musa — Kalebu na Yoshua tu. Yeye daima hukumbuka andiko ambalo husema: “Sio kwa uwezo, wala si kwa nguvu, bali kwa Roho Yangu, asema Bwana wa majeshi.” Zek. 4:6. Yeye kwa hivyo

Hatafuti Sifa au Huruma. {CFL: 2.6}

Yeye hatafuti huruma kutoka kwa wengine, wala hajihurumii; hukataa kupoteza muda akiwalaumu wengine kwa hali zisizopendeza au kushindwa au vizuizi; wala yeye hatarajii sifa kwa matendo yake ya thamani. Yeye kamwe hapulizi pembe yake mwenyewe. Huridhika kujua kwamba yeye anamtumikia Mungu, kwamba Mungu atamjazi waziwazi. Kwa kuongezea, pia, yeye yu tayari siku zote kusikia; yeye ni

Mwelekevu. {CFL: 3.1}

Yeye yuachunguza siku zote kumjua Mungu zaidi na yale ambayo Yeye angetaka afanye, bila kujali njia ambayo nuru inakujia. Yeye kamwe hashutumu wazo la mtu yeyote kabla ya uchunguzi wa uaminifu na wa kusali. Hakimbii mbali kutoka kwa lolote, maana yeye humtegemea Roho wa Kweli wa Mungu kumlinda kutoka kwa makosa yote, ushupavu, na majivuno. Yeye kamwe haufanyi mwili kuwa kinga yake ya Ukweli yeye humtegemea Roho wa Mungu kumwonyesha Ukweli ni nini na kosa ni nini. Yeye hakika ni Mberoya (Matendo 17:10,11). Kuzitunza amri na Ushuhuda wa Yesu Kristo (Ufu. 12:17) ni ramani yake hadi kwa Ufalme. Zaidi ya hilo, yeye ni

Mtoa Hoja Timamu wa Busara. {CFL: 3.2}

Maamuzi yake katika mambo yote ni ya uhuru, kwa msingi wa busara na akili, sio kwa hisia, upendeleo, au “heshima kwa watu,” wala kwa faida ya ubinafsi. Njia ya Mungu siku zote ni fimbo yake ya kupimia. Yeye kwa hivyo kamwe haishi akijutia kitu chochote isipokuwa dhambi zake. Pamoja na haya, yeye ni

Imara {CFL: 3.3}

Yeye hajajulikana kuyumbayumba. Yeye hubadilisha mawazo yake wakati tu atajikuta mbaya au amekosea. Kwa kweli yeye ni Daudi wa siku hii. Yeye ni asiyebadilika na wa kutegemewa katika yote anayopewa kufanya, na daima

Hukubali Marekebisho. {CFL: 3.4}

Yeye hahisi uchungu anapokosolewa, lakini hushukuru kwa hilo na huweka kwa matumizi yote ambayo ni ya kujenga. Yeye hatoi udhuru kwa makosa yake, bali huyatumia kama ngazi kwa maendeleo. Anayo

3

Ujasiri Usiotikisika. {CFL: 3.5}

Yeye husahau yaliyopita, na daima anakaza mwendo afikilie mede ya thawabu ya mwito mkuu. Yeye kwa hivyo hufanya yote awezayo kurekebisha chanzo cha taabu zake, na ile isiyoweza kurekebishwa yeye hukubali na kujibadilisha kupatana nalo. Yeye ndiye Musa wa siku hii. Anaweza kuanguka mara saba kwa siku, lakini upesi huinuka na kukimbia mbele, na daima ana matumaini na

Hutazamia Majaliwa ya Mungu. {CFL: 4.1}

Kupitia imani na uzoefu ana imani kwamba Mungu anamwongoza na ya kwamba atatoa kwa ukarimu atatoa hekima na nguvu inayohitajika kuhimili hata matatizo magumu sana ya maisha. Katika hali hii yeye ni kama Ruthu, Mmoabu. Yeye haachi fursa imponyoke, na anayo

Amani Kamili ya Akili. {CFL: 4.2}

Akili yake imewekwa tayari kushinda na kuendeleza Ufalme wa Mungu na, kwa hivyo, haogopi njaa wala kifo. Yeye hana hata wasiwasi kwa wakati ujao. Yeye kamwe halalamikii udhaifu wake; daima ni mwenye kushukuru na anajua kuwa zipo kesi mbaya maelfu kuliko yake. Anajua kwamba hawezi kufa iwapo Mungu anataka aishi, na ya kwamba hawezi kuishi ikiwa Mungu anataka afe. Yeye ndiye Ayubu na yeye ndiye Paulo wa siku hii. Anangojea kwa uvumilivu, akijua kwamba “Mungu hufanya kazi pamoja na wale wampendao katika kuwapatia mema, yaani wale walioitwa kwa kusudi Lake.” Rumi.8:28. Yeye anajua kabisa kwamba kila wingu lenye giza, jeusi na lenye dhoruba pia lina upande mwangavu wa faraja, na daima hutazama upande mwangavu. Yeye ni

Makini Sana kwa Kile Hufanya na Jinsi ambavyo Hukifanya. {CFL: 4.3}

Yeye husaka na kupata uzuri ulio katika uumbaji wote wa Mungu, na hutafuta kuweka sanaa katika yote atendayo. Yeye ni

Mwenye Uwezo wa Kutofautisha Sana. {CFL: 4.4}

Yeye haketi kamwe na wenye mizaha (Zab. 1:1), hali kamwe pale walevi hukulia, ni mahsusi kwa kuchagua kundi lake. Vitabu vyake vya kusoma, muziki, sanaa, nk, haviwezi kutiliwa shaka. Yeye kwa hivyo hujikuta

Akihitajika Sana. {CFL: 4.5}

Yeye hafanzi maadui, na siku zote hutafuta kufanza marafiki. Hufikiri kwa uchanya, mawazo ya kusaidia, na kwa hivyo yeye ni mtu mkunjufu, wa manufaa, mtu mwenye furaha, mwenye kuhitajika sana. Hata maadui zake wanayo heshima fulani kwake. Bado yu

Mwenye Adabu. {CFL: 4.6}

Yeye huwa hajaribu kuvuta uangalifu kwake mwenyewe, ila badala yake

4

kwa chimbuko lake. Yeye ni mwenye adabu katika mavazi, semi, na tabia, na yeye hukataa kujifurahisha katika kuakisi kwa utukufu wa mwingine. Katika ufanisi yeye ni mnyenyekevu na mwenye shukrani humpa Mungu utukufu kwa matendo na mafanikio yake yote, na iwapo utukufu wowote wa kibinadamu, hugawana na wanadamu wenzake. Zaidi ya yote, yeye ni mwangalifu na

Mtiifu kwa Sheria za Mungu. {CFL: 4.7}

Yeye hudumisha imani katika siku za baadaye njema. Yeye hutenda yote kuishi na kutumika, na kwa hivyo hula ili makusudi apate nguvu, si kwa ajili ya ulevi. Yeye huzuia mikono yake mbali na kile ambacho Mungu ametamka kuwa najisi. Yeye kamwe si mshupavu, wala yeye si mlegevu. Yeye hutembea katikati ya barabara ambapo nuru hung’aa angavu. Yeye hachukuliwi na kila upepo wa mafundisho; hukumbuka mamlaka, na huepuka utapeli. Kabla ya aingie ndani ya chumba cha “wageni” (Mat. 22:11), huhakikisha kwamba yeye

Amejivika Vazi la Harusi. {CFL: 5.1}

Yeye anajua kwamba Ufalme wa Mungu unaundwa na Wakristo “waliokomaa”, “wasiokuwa na doa, au kunyanzi, au kitu kama hicho.” Kwa hivyo yeye haupotezi wakati wake kutafuta kibanzi au boriti katika jicho la mwingine (Mat. 7:1-5). Ikiwa kuna chochote, hutafuta ili kuona kwamba hakuna chochote katika jicho lake. Yeye hujua ya kwamba Mungu hajamfanya kuwa mwamuzi wa watu Wake, au murekebishaji wa wazushi. Yeye hutenda lile Ukweli husema, na wale wanaotamani kuiga wanaweza kufanya hivyo, bali yeye kamwe huwa hajaribu kuwasukuma upande wake. {CFL: 5.2}

Natumaini katika sala kwamba mawazo haya kwa Maandiko yatakuwa ya msaada na himizo kwako na kwa wote wanaokuzunguka pande zote. Mungu akubariki. {CFL: 5.3}

Wako mwaminifu katika imani na ujasiri mwema,

V.T. Houteff

5

>