20 Jan Gombo la 1 Salamu Mwafaka Namba 03, 04
Gombo la 1 Salamu Mwafaka Namba 3, 4
AMANI YA PEKEE YA MAWAZO
Hati miliki, Kimechapishwa tena 1953
Haki zote zimehifadhiwa
V. T. HOUTEFF
MAJADILIANO YA MASWALI NA MAJIBU
(Sehemu ya 1)
MAJADILIANO YA MASWALI NA MAJIBU
(Sehemu ya 2)
1
WAZO LA SALA YA UFUNGUZI
Alasiri hii la kufungua wazo letu la sala linapatikana kwenye kurasa za 149, 150 za Mlima wa Baraka. Tutasoma aya nne za kwanza. Hizi zina msingi kwa andiko, “Basi msisumbukie ya kesho … yatosha kwa siku maovu yake.” {1TG3: 2.1}
MB, kr. 149, 150 — “Ikiwa umejikabidhi kwa Mungu, kufanya kazi Yake, huna haja ya kuwa na wasiwasi kwa ajili ya kesho …. Tunapoccukua mikononi mwetu usimamizi wa mambo ambayo tunapaswa kufanya, na kutegemea hekima yetu wenyewe kwa mafanikio, tunachukua mzigo ambao Mungu hajatupatia …. Tunaweza kuwa na masumbuko, na kutarajia hatari na hasara; kwa maana ni hakika yaweza kutupata. Lakini tunapoamini kweli kwamba Mungu anatupenda, na anamaanisha kututendea mema, tutakoma kuwa na kusumbukia ya siku zijazo. Tutamtegemea Mungu kama mtoto anayemwamini mzazi mwenye upendo. Kisha taabu zetu na mateso yatatoweka; kwa maana mapenzi yetu yamemezwa katika mapenzi ya Mungu. {1TG3: 2.2}
“Kristo hajatupatia ahadi ya msaada wa kubeba leo mizigo ya kesho …. Siku moja tu ndiyo yetu, na katika siku hii tunapaswa kuishi kwa ajili ya Mungu. Kwa sababu siku hii moja tunapaswa kuweka mkononi mwa Kristo, kwa utumishi wa kicho, madhumuni na mipango yetu yote, tukimtwika Yeye mahitaji yetu yote, kwa maana Yeye hututunza. ‘Nayajua mawazo ninayowaza juu yenu, asema Bwana, mawazo ya amani, na sio ya uovu, ku-wapa mwisho wa matumaini.’ ‘… katika utulivu na kwa ujasiri utakuwa uwezo wako.’ “ {1TG3 : 2.3}
Hebu tuombe kwa ajili ya ufahamu wa kudumu kwamba Mungu ameahidi msaada wa kuibeba mizigo yetu, sio ya kesho, ila ya leo; tuombe kwamba sisi kila siku tuweke mikononi Mwake madhumuni na mipango yetu yote, mahitaji na masumbuko yetu. Hatimaye tu twaweza kutulia katika uhakikisho kwamba katika “utulivu na kwa ujasiri” utakuwa uwezo wetu. {1TG3: 2.4}
2
MAJADILIANO YA MASWALI NA MAJIBU
(Sehemu ya I)
MATINI YA HOTUBA NA V. T. HOUTEFF
MCHUNGAJI WA WADAUDI WAADVENTISTA WA SABATO
SABATO, AGOSTI 3, 1946
HEKALU LA MLIMA KARMELI
WACO, TEXAS
Baadhi yenu mmekuja kwangu hivi karibuni na maswali kadhaa yanayoonekana kuwa muhimu sana kwenu. Kwa sababu hii tutaweza kuitumia saa ya kujifunza alasiri hii ili kuyajibu. {1TG3: 3.1}
Sasa ninasoma swali: “Je, sisi, Ndugu Houteff, si wastahiki kamili kuagiza kati yetu
Mlo wa Bwana?” {1TG3: 3.2}
Hebu tuone. Kabla ya kuanzisha agizo la unyenyekevu, Yesu aliwaambia wanafunzi wake, “Ninyi ni safi, lakini sio nyote.” Mmoja hakuwa. Licha ya ukweli kwamba Yuda hakuwa anastahili, agizo halingeweza kusitishwa. Ingawa mara alipomaliza kushiriki sakramenti, akasimama, akaenda nje, na kufanya kazi yake ya ushetani. Baadaye macho yake yalifumbuliwa kwa uhalifu aliokuwa ameufanya, na akajinyonga. Wanafunzi wale wen-gine, hata hivyo, walikuwa tayari, au walistahili huduma takatifu kama walivyoweza kuwa hadi wakati huo. {1TG3: 3.3}
Mlo wa Bwana ulitawazwa kuwa ukumbusho wa dhabihu ya Bwana, sio kuwasafisha wanaoushiriki dhambi zao bali kuwatakasa kutoka kwa wadhambi, kama inavyoonekana kutoka kwa Pasaka huko Misri na kutoka kwa ukweli kwamba baada ya hapo Yuda hakutembea tena na
3
wanafunzi. Dhahiri, basi, uadhimisho wa agizo hilo uliisababisha baraka kwa kumi na moja, lakini maangamizo kwa moja. {1TG3: 3.4}
Zimekuwepo idadi kadhaa za mavuguvugu ya matengenezo miongoni mwetu kabla na wakati wetu. Bila shaka, yote yaliadhimisha Mlo wa Bwana kati yao. Lakini haukuwafaidi. Haukuwafanya au kazi yao kuwa ya kudumu na ya milele. Kwa kweli, walitoweka hata kwa kasi kuliko walivyoingia. Sasa hebu tusome kutoka — {1TG3: 4.1}
1 Kor. 11:17, 18 — “Lakini katika kuagiza haya, siwasifu, ya kwamba mnakusanyika, si kwa faida bali kwa hasara. Kwa maana kwanza mkutanikapo kanisani nasikia kuna faraka kwenu; nami nusu nasadiki.”
Wakorintho walikuwa na utata, uliosababisha migawanyiko miongoni mwao wenyewe, na hivyo kukusanyika kwao pamoja kanisani kulikuwa “sio kwa ubora,” ila kwa utata zaidi. {1TG3: 4.2}
Ikiwa tunakutana tu kwa “utata zaidi,” si ni bora zaidi kukaa nyumbani? {1TG3: 4.3}
Aya ya 27-30 — “Basi kila aulaye mkate huo, au kukinywea kikombe hicho cha Bwana isivyostahili, atakuwa amejipatia hatia ya mwili na damu ya Bwana. Lakini mtu ajihoji mwenyewe, na hivyo aule mkate, na kukinywea kikombe. Maana alaye na kunywa, hula na kunywa hukumu ya nafsi yake, kwa kutokuupambanua ule mwili. Kwa sababu hiyo wako wengi kwenu walio hawawezi na dhaifu, na watu kadha wa kadha wamelala.”
Mkate wa Bwana na kikombe ni lazima vichukuliwe na watu tu baada ya kujihoji, na
4
wameona kwamba hawasababishi shida; kwamba kukutana kwao pamoja ni kwa ajili ya ubora zaidi, sio “utata zaidi.” Sasa, iwapo tumefikia kiwango hicho cha haki, basi tunapaswa kwa njia zote kuagiza rasmi Mlo wa Bwana kati yetu. Lakini ikiwa hatujaafiki kiwango hicho hata sasa, basi kulianzisha rasmi agizo la unyenyekevu miongoni mwetu litakuwa tu kwa maangamizi yetu, sio kwa wokovu wetu. {1TG3: 4.4}
Kazi yetu kuu sasa sio kuhimiza uadhimishaji wa Mlo wa Bwana, ila badala yake kwanza kuinuka hadi kiwango cha ukamilifu ambacho ujumbe wa leo, pamoja na ujumbe wa jana huhimiza. Bwana haitishi kamwe “uamsho na matengenezo” wakati ambapo kanisa linafurahia maisha mazuri ya kiroho. Mlo wa Bwana, kwa hiyo, haupaswi kamwe kuagizwa mwanzoni mwa uamsho na matengenezo kama haya, ila kwenye upeo wake. Yesu hakuanzisha rasmi agizo hilo mwanzoni mwa huduma Yake, ila alifanya hivyo alipoifunga huduma yake. {1TG3: 5.1}
Na ikiwa tungeepuka kuchanganya kati yetu wenyewe, hatupaswi kamwe kuzungumza dhambi za wengine, wa-la tusitumie hukumu. Ikiwa hatuwezi kulia suala hilo kwa faragha na wale walio na kosa, basi tungependa kuzungumza na mtu yeyote au tutafuata maagizo yaliyopewa {1TG3: 5.2}
Mat. 18:16, 17 — “La, kama hasikii, chukua pamoja nawe tena mtu mmoja au wawili, ili kwa vinywa vya mashahidi wawili au watatu kila neno lithibitike. Na asipowasikiliza wao, liambie kanisa; na asipolisikiliza kanisa pia, na awe kwako kama mtu wa mataifa na mtoza ushuru.”
Hatuwezi kumuongoza Bwana. Yeye ndiye wa kutuongoza. Sisi wenyewe hatujui kilicho sahihi na kibaya
5
isipokuwa tumeambiwa. Rahisi vya kutosha, ikiwa tunafanya chochote tunachoambiwa kukifanya, tusiozidi na tusiopungua, tutahesabiwa kuwa tunaostahili. Hadi sasa, ujumbe wetu uliotumwa na Mungu haujaleta kwa umakini wetu agizo la Mlo wa Bwana, lakini unatusihi tuyaache machukizo, tutupe kando sanamu zetu zote, tuyaache mawazo yetu yote na maoni yetu ya kibinafsi, kwa moyo wote tumrudie Bwana. {1TG3: 5.3}
Ujumbe, zaidi ya hayo, hufundisha kwamba tunapaswa kusalia katika kanisa la mama na kufanya kazi hasa kwa ajili ya wokovu wake. Hitimisho basi ni kwamba kadri tunavyokaa pamoja naye, inaonekana hakuna haja ya kuagiza Mlo wa Bwana faraghani kati yetu, labda sio kabla ya saa ya waliotubu kutengwa kutoka kwa wale am-bao hawakutubu, kama ilivyofundishwa kwa mifano-kwa Pasaka huko Misri, na kwa Pasaka usiku ule Yuda an-geondoka, kutotembea tena na wale kumi na wawili. {1TG3: 6.1}
Isitoshe, hakuna yeyote huenda anajua ni lini na jinsi ya kuiadhimisha sakramenti. Wengine huiadhimisha kila Jumapili au kila Sabato, baadhi mara kwa mara, baadhi kila robo na kadhalika. Inaonekana kuwa ni busara kus-ema kwamba wakati Mungu atatuamuru tuianzishe upya Yeye atatuambia pia namna gani na wakati wa kuiad-himisha ifaavyo. {1TG3: 6.2}
—————0-0-0—————
Kadhaa wameniambia, “Ndugu Houteff, tunapokutana na wale wanaotupinga, hatujui jinsi ya kuyajibu maswali yao. Tunachanganyikiwa. Hatujui kama tuko sawa au kama tumekosea. Wanatukanganya hasa juu ya Ufasiri wa ‘Fimbo’ kuhusu
Tarumbeta na Mihuri.” {1TG3: 6.3}
Wale kati yenu ambao mnapata kuyajibu maswali yaliyobishaniwa, sema tu kwa wapinzani wenu: Moja wetu amekosea kwa hakika. Hatuwezi sote kuwa sahihi, kusema
6
machache, na hivyo kwa makini na kwa uangalifu bila ubaguzi tulichunguze jambo hilo. {1TG3: 6.4}
Ningaliwaambia kwamba tunafundisha tarumbeta kama ambavyo Yohana aliziona katika maono. Kwa mfano, Ufunuo Unasema, “Na hesabu ya majeshi ya wapanda farasi ilikuwa elfu ishirini mara elfu kumi; nilisikia hesabu yao. Hiyo ndivyo nilivyowaona hao farasi katika maono yangu, nao waliokaa juu yao, wana dirii kifuani, kama za moto, na za samawi, na za kiberiti; na vichwa vya farasi hao ni kama vichwa vya simba, na katika vinywa vyao hutoka moto na moshi na kiberiti. Theluthi ya wanadamu wakauawa kwa mapigo matatu hayo, kwa moto huo na moshi huo na kiberiti hicho, yaliyotoka katika vinywa vyao. Kwa maana nguvu za hao farasi ni katika vinywa vyao, na katika mikia yao; maana mikia yao ni mfano wa nyoka, ina vichwa, nao wanadhuru kwa hivyo.” Ufu. 9: 16-19. {1TG3: 7.1}
Hii ndio picha ya maelezo ambayo Waufunuo anatupatia kuhusu farasi na wapanda farasi, 200,000,000, farasi na wapanda farasi. Onyesho linalofuata ni kufanana na maelezo ya Yohana ya farasi na wapanda farasi kama tunavyoweza kulifanya, na ufasiri wetu kuwahusu ni barabara. Tazama Trakti Namba 5, “Onyo la Mwisho.” {1TG3: 7.2}
7
Hapa linafuata onyesho la farasi na wapanda farasi ambalo Baraza Kuu linaweka wazi kwa umma. {1TG3: 8.1}
Sasa linganisha maelezo ya Uvuvio kwa farasi na wapanda farasi na mchoro wa dhehebu kuwahusu kama lil-ivyoyatoa katika “Mawazo juu ya Danieli na Ufunuo,” uk. 510. Kwa nini Dhehebu kwa ufasiri wao wa Tarum-beta wasiyatumie maelezo ya Uvuvio kwa farasi na wapanda farasi? Kwa nini waliamua kuubuni wao wenyewe? — Jibu pekee ambalo linaweza kutolewa ni kwamba maelezo Ya Roho hayaafikiani na ufasiri wao ambao haujavuviwa. Kutoweza kwa mmoja kufasiri kwa usahihi, bila zawadi ya Mbinguni ya kufasiri, hata hivyo, kunatarajiwa na kusamehewa. Lakini kusema kwamba maono yalionyeshwa kwa Waufunuo kwa umbali sana, kwamba hakuweza kuona barabara aina ya vichwa na mikia ya farasi na ambako moto, moshi, na kiberiti zilitokea, ili kuyabadilisha maono yapatane na ufasiri wao kwayo, sio tu ukaidi kwa onyo la Kristo kuhusu kuongeza na kuondoa kwa Maandiko (Ufu. 22:18, 19), lakini pia ni kumkufuru wazi. {1TG3: 8.2}
8
Je! Sasa unaona kile watu wale wanaoitwa wakuu, “watu wenye ujuzi,” wanafanya? Matendo haya ya walaghai yanashutumu majivuno yao kwamba watu watakatifu wanaliendesha Dhehebu; na kuzungumzia kwa majivuno mamilioni ya dola Dhehebu hukusanya kila mwaka kutoka kwa masikini sio kitu iwapo zinaweza kutumika kwa kazi kama hiyo. Wanahitaji kutubu na kusahihisha makosa wanayopitisha kama Ukweli kabla waweze kudha-miria kuwahukumu wengine. {1TG3: 9.1}
Iwapo Yohana hakuweza kuona vizuri jinsi farasi walivyoonekana, basi angewezaje kuona kwamba samaki wote baharini walikufa (Ufu. 8: 9)? Na kama kitangulizi cha kujiinua nafsi cha kuyapekua Maandiko kama aina ya Baraza Kuu limekianzisha, mtu anawezaje kuwa na hakika kwamba yeyote kati ya manabii aliona kitu chochote sahihi? Je! Hautambui kwamba ufasiri kama huu na uliyopindwa wa maandiko ni majaribio ya Shetani kudhoof-isha imani ya wanadamu ndani ya manabii na uwezo wa Kristo wa kufunua kwa usahihi na kuonyesha Ukweli kwa watumwa Wake? Fikiria jinsi linavyoharibu shtaka dhidi ya Uvuvio, jinsi linavyoharibu nafsi, na la kukufu-ru dhidi ya Roho Mtakatifu Ambaye huongoza katika Kweli yote! na lazima kuwa la kuchukiza namna gani kwa Kristo, hasa kwa kuwa linakuja kutoka kwa wale wanaojidai kumtumikia Yeye! Hili pekee linapaswa kuwa la kutosha kuonyesha kwamba malaika (ukasisi) wa Laodekia ni wa upofu na uchi na unahitaji kila kitu. Kwa ajili ya maisha yako na kwa maisha ya wengine, usiunge mkono mafundisho kama haya ya mashetani. Hayo sio chochote isipokuwa Ukweli, sio chochote isipokuwa ishara za Roho ya Unabii kazini. Jiulizeni wenyewe ni lini Uturuki au taifa lolote limewahi kuwa na askari wapanda farasi 200,000,000! Na kama bado unashangaa kwa nini Mungu aliruhusu makosa kutambaa hadi kanisani, jibu ni: Kusudi wao kwa kuyakuza na kuyaeneza Yeye aweze kwa wakati kama huu kuwafunua watenda kazi wa uovu na kuwathibitishia waumini kwamba kanisa
9
Lake sasa limefurika sana na Ibilisi kama lilivyokuwa kanisa la Kiyahudi wakati wa Kristo, hivyo kuwaamsha waaminifu na kuwaweka huru kutoka kwa udanganyifu wa ubinfsi wa Ulaodekia, na hivyo kutoka kwa pigo lifurikalo (Isa 28: 13-15). {1TG3: 9.2}
Je! Sasa huoni sababu ya jina “makufuru” juu ya vichwa vyote saba vya mnyama kama chui (Ufu. 13)? Na kwamba ikiwa kichwa kimoja kinawakilisha mfumo wa kidini, basi vyote vinapaswa kufanya hivyo, kwa maana vyote ni sawa isipokuwa kwa kimoja chenye jeraha, na vyote viko kwa mnyama (dunia) kwa wakati mmoja, sio kimoja baada ya kingine. {1TG3: 10.1}
Kwa shtaka lao kwamba “Fimbo” hufundisha kwamba kanisa ni Babeli, tunawapa changamoto watoe taarifa hiyo. Na kama hawajui Babeli ni nini, basi ni bora wasome “Fimbo ya Mchungaji.” {1TG3: 10.2}
Kweli, kanisa ni kanisa la Mungu, lakini wale ambao wamechukua usimamizi wake sio bora kuliko Sanhed-rini katika siku za Kristo. Ni kwa sababu Mungu anao ustahiki mkuu kwa kanisa Lake kwamba Yeye hivi kwa Ukweli Wake amelivamia, na ni hivi kuwakomboa watu Wake kwa kuwakata waanguke wale ambao kinyume cha sheria wanawafanya kuwa watumwa, wakiwafunza mafundisho ya mashetani yalivyoonyeshwa katika funzo hili; na kuwazuia wasikutane na Ukweli wa Mbinguni kwa wakati huu wa hatari. Je! Unaona kwa nini Ba-raza Kuu sasa sio tena Sauti ya Mungu kwa watu (Matangazo ya Baraza Kuu, kikao cha 34, Gombo la 4, Ziada Namba 1, Aprili 3, 1901, uk. 25, Safu 1, 2) kuliko ilivyokuwa Sanhedrin kwa Wayahudi wakati wa Kristo? Na-tumaini hamtaendelea kujidanganya kuwa “Fimbo ya Mchungaji” inabomoa chochote ambacho Mungu amejenga. Sasa
Mihuri Saba {1TG3: 10.3}
Walaodekia hufundisha kwamba mihuri huanza na
10
kufufuka kwa Kristo, ambapo, kama mnavyojua, ilikuwa karibu miaka sabini kabla ya Yohana Waufunuo kuwa na maono ya mihuri. Hebu sasa tusikie ni nini Sauti ya Ufunuo Yenyewe inasema: {1TG3: 10.4}
Ufu. 4: 1 — “Baada ya hayo naliona, na tazama, mlango ukafunguka mbinguni, na sauti ile ya kwanza niliyoisikia kama sauti ya baragumu ikinena nami, ikisema, Panda hata huku, nami nitakuonyesha mam-bo ambayo hayana budi kuwako baada ya hayo.”
Sauti ilinena kwa dhati kwamba vitu ambavyo Yohana alikuwa karibu kuonyeshwa havikuwa vimetukia, na havikuwa kwa wakati huo vinatukia, ila kwamba vingetukia baadaye katika mkondo wa muda. Kwa sababu vil-ipaswa kutukia baada ya Yohana kuwa na maono (baada ya 96 B.K., sio katika karne ya kwanza ya enzi ya Ukristo), basi sio kukufuru kufundisha kinyume cha kile Sauti ilisema — kusema kwamba mihuri ilianza zaidi ya miongo mitatu kabla ya Yohana kuonyeshwa? Hapana, mihuri haiwezi, kwa hivyo, kuanza na kanisa la Kikristo. Ili kujua Ukweli unaoihusu, soma Trakti Namba 15, “Kwa Makanisa Saba.” {1TG3: 11.1}
—————0-0-0—————
“Je Vipi Kuhusu Ufunuo Kumi na Mbili?”
“Je Mwanamke aliyevikwa jua anaashiria kanisa kuanzia Pentekoste na kuendelea, likiwa limevikwa Injili (jua) ya Kristo?” {1TG3: 11.2}
Wakati joka lilimshambulia mwanamke, alikuwa tayari amevikwa jua, na mtoto wake, Bwana, alikuwa bado hajazaliwa. Hii ikiwa hivyo, je, vazi lake la jua linawezaje kuwa nembo yake kuwa amevikwa injili ya Kristo na kwa jinsi gani angeweza kuwa analiwakilisha kanisa la Kikristo, kuona kwamba injili wala kanisa wakati huo halikuwepo. Na anawezaje kuwa mama wa Kristo kabla ya kanisa la Kikristo lenyewe kuzaliwa? Hawezi kuwa ni jumla
11
ya jibu. {1TG3: 11.3}
Nadharia, basi, kwamba mwanamke huchukua mwanzo wake kwa Pentekoste, ni kama vile kufikiri kama ni kusema kwamba kifaranga huanguliwa kabla ya yai kutagwa. {1TG3: 12.1}
—————0-0-0—————
“Je mchinjo wa Ezekieli 9 utatukia ulimwenguni au kanisani? Je ni mapigo saba ya mwisho, au ni
Utakaso Wa Kanisa? “ {1TG3: 12.2}
Ezek. 9: 1, 4, 9 — “Kisha akalia kwa sauti kuu masikioni mwangu, akisema, Waamuru wale wanaousimamia mji wakaribie, kila mmoja na awe na kitu chake cha kuangamiza mkononi mwake. 4 Bwana akamwambia, Pita kati ya mji, kati ya Yerusalemu, ukatie alama katika vipaji vya nyuso vya watu wanaougua na kulia kwa sababu ya machukizo yote yanayofanyika kati yake. Ndipo akaniambia, Uovu wa nyumba ya Israeli na Yuda ni mwingi sana, nayo nchi imejaa damu, nao mji umejaa kupotosha hukumu; maana husema, Bwana ameiacha nchi hii, naye Bwana haoni.”
Malaika wanaulinda “mji,” Yerusalemu, sio ulimwengu, wala sio Babeli. Hata Mkristo ambaye hajaelimishwa kabisa anajua kwamba majina Yerusalemu, Yuda, na Israeli, yanamaanisha kanisa, kamwe hata kwa mfano hayamaanishi “ulimwengu.” Daima yamemekuwa yakimaanisha kanisa na daima yatamaanisha kanisa, kwa kuwa ndivyo yalivyo . {1TG3: 12.3}
Mchinjo wa Ezekieli 9 hakika sio sawa na mapigo saba ya mwisho (Ufu. 16), kwa sababu mapigo yanaanguka Babeli, lakini mchinjo, kwa Yuda na Yerusalemu. Zaidi ya hayo, malaika wa Ezekieli 9
12
wanaua kila mmoja asiye na alama, lakini mapigo hayamchinji yeyote. Kwa kuyapotosha maandiko ya Musa, Wayahudi walijaribu kuyapinga mafundisho ya Kristo na ni yakini kwamba iwapo Walaodekia wanaendelea kuyapotosha maandishi ya Dada White katika wakijaribu kuupinga ujumbe wa leo, basi mwisho wao utakuwa wa kuomboleza zaidi kuliko ilivyokuwa kwa Wayahudi. Kuhusu kile ambacho husema juu ya Ezekieli 9 soma Shuhuhuda, Gombo la 3, uk. 267; Kimenukuliwa, Gombo la 5, uk. 211; pia Pambano Kuu, kur. 656, 657. Ezeki-eli tisa huwakilisha Hukumu ya Walio Hai ndani ya nyumba ya Mungu (1 Pet. 4:17) – Kutiwa muhuri kwa wa-takatifu na kuangamizwa kwa waovu ndani ya kanisa. {1TG3: 12.4}
——0——
Nafikiri ninao wakati kwa swali lingine: Swali hili limeulizwa katika sehemu tano, na kwa hivyo nitalijibu ipasavyo. {1TG3: 13.1}
Swali la 1: “Je, unabii wa Nahumu unatabiri Vita Kuu vya 2 au Vita Vingine?”
Kwa ajili ya jibu hebu tuende moja kwa moja kwa unabii wa Nahumu. {1TG3: 13.2}
Nah. 2: 1 — “Yeye asetaye vipande vipande amepanda juu mbele ya uso wako; zishike silaha, ilinde njia, vitie nguvu viuno vyako, uongeze uwezo wako sana.”
Nahumu anatabiri kwamba yeye atakayeanza vita, “yeye asetaye vipande vipande,” atakuwa amejiandaa vizuri kabla ya kuanza vita, lakini dola inayompinga, Ashuru, haitakuwa tayari hadi baada ya vita kuanza; yaani, baada ya “asetaye vipande vipande” kuja mbele ya uso wa Ashuru, kisha inakuwa kwamba Ashuru anafanya maandalio ya kumkabili. Kisha inakuwa kwamba anavitia nguvu viuno vyake, na kuimarisha “uwezo wake sana.” {1TG3: 13.3}
13
Sasa, ya kuwa ni ukweli unaojulikana kwamba Uingereza Kuu na Ufaransa walikuwa hawajajiandaa kupigana na Hitler alipofyatua bunduki zake dhidi yao, na kama vile kila mmoja wa Muungano walianza kujitayarisha kwa nguvu baada ya Hitler kuanza kuseta vipande vipande, ukweli unasimama wazi kama kioo kwamba “yeye asetaye vipande vipande” sio mwingine isipokuwa Hitler, yeye aliyekuwa tayari mwanzoni mwa vita, yeye ali-yevunja Ujerumani yenyewe vipande vipande, Ufalme wa Uingereza na nchi zingine nyingi. Muungano, kwa hiyo, lazima wawe Ashuru ya uakisi. Hiki ni kidokezi namba moja. {1TG3: 14.1}
Kwa kidokezi namba mbili tutasoma kuhusu mbinu za safari na usafirishaji katika siku ambayo maandalizi ya vita yanafanywa na vita vyenyewe kupiganwa. {1TG3: 14.2}
Aya ya 3, 4 — “… magari ya vita yametameta kwa taa za umeme siku ya kujitengeza kwake, … Magari ya vita yanafanya mshindo njiani, Yanasongana-songana katika njia kuu; Kuonekana kwake ni kama mienge, Yanakwenda upesi kama umeme.”
Aya hizi zinaonyesha mbinu za safari na usafirishaji za pekee katika historia ambazo maandalizi yaliyoelezwa na Nahumu yalifanywa na kutumika wakati “magari” (usafiri wa magari) yanapokwenda kwa kasi isiyo na kifani, kasi “kama ya umeme”, wakati usafiri wa mitambo angani na baharini, mijini na mashambani (mitaa na njia kuu), “inasongana-songana.” Hizi zote ishara za wakati, zinaweka alama wakati ambapo vita vinapiganwa, haziachi nafasi ya mashaka. Zote kwa maneno kamili zinathibitisha kwamba Nahumu anatabiri Vita Kuu vya 2. Kwa kidokezi cha tatu tutasoma. {1TG3: 14.3}
14
Nah. 1:15 — “Tazama, juu ya milima iko miguu yake aletaye habari njema, atangazaye amani. Zishike sikukuu zako, Ee Yuda, uziondoe nadhiri zako; kwa maana yule asiyefaa kitu hatapita kati yako tena kamwe; amekwisha kukataliwa mbali.”
Hapa tunaambiwa kwamba wakati ambapo vita vitapiganwa mtu fulani atakuwa anachapisha mafunuo yali-yovuviwa ya Ukweli uliofunuliwa, Ukweli wa Hukumu ya Walio Hai, ambao utatenganisha milele ngano kutoka kwa magugu (Mat. 13:30). ), samaki wazuri kutoka kwa wabaya (Mat. 13:47, 48), kondoo kutoka kwa mbuzi (Mat. 25:32), na wanawali wenye busara kutoka kwa wale wapumbavu (Mat. 25: 1-12). Hawa “hawatapita kati yako tena” kanisa, yanatangaza maandiko, “wamekwisha kukataliwa mbali.” Kwa hivyo, yanamuhimiza Yuda, kanisa, kuiadhimisha hii ya upatanisho karamu ya uakisi na kuzitenda nadhiri zake kwa Mungu ili apatikane anastahili kuokoka hukumu za Mungu. Hivyo, rai ya Mungu kwa kanisa Lake sasa inatoa sauti kote kote katika nchi, ikisema, “Amka, amka, jivike nguvu zako, Ee Sayuni; Jivike mavazi yako mazuri, Ee Yerusalemu, mji mta-katifu; Kwa maana tokea sasa hataingia ndani yako Asiyetahiriwa, wala aliye najisi.” (Isa. 52: 1) {1TG3: 15.1}
Pamoja na hizi hakika ishara za nyakati Uvuvio humwacha kila mtu kujiamlia iwe ni kuweka imani katika Sauti ambayo Uvuvio Wenyewe hupendekeza, au katika sauti ambayo wanadamu ambao hawajavuviwa hupendekeza. Tokea sasa hakutakuwepo kuchanganyikiwa miongoni mwa watu wa kweli wa Mungu. Wake “… walinzi wa-tapaza sauti zao, wataimba pamoja; Maana wataona jicho kwa jicho, Jinsi Bwana arejeavyo Sayuni.” (Isa. 52: 8.) {1TG3: 15.2}
——0——
Swali la 2: “Nahumu asema nani atashinda vita — ‘asetaye vipande vipande’ au ‘Ashuru’?”
Ingawa unabii wa Nahumu unasisitiza zaidi
15
juu ya anguko la Ashuru, hata hivyo unasema kwamba wote watapoteza, kwa maana kunena juu yake “asetaye vipande vipande,” maandiko yanasema: {1TG3: 15.3}
Nah. 2: 5 — “Awakumbuka watu wake wenye heshima; Wanajikwaa katika mwendo wao; Wanafanya haraka waende ukutani; Nacho kitu cha kuwafunika kimewekwa tayari.”
“Kuwakumbuka watu wake wenye heshima” kunayo maana kwamba idadi ya watu wake – viongozi na majem-adari na watu wengine wenye uwezo pamoja na jeshi lake bora – wanakupungua na hivyo haja ya kuhesabu, na kwamba “wakuu wake” wanajikwaa katika kutembea kwao; yaani watafanya aina fulani ya makosa wakipam-bana kuelekea kwa ushindi na kuwasababisha kuanguka. Na hili ndilo hasa lililotokea: jeshi la Hitler lilijikwaa kwa kupambana na Urusi wakati akipigana na Uingereza Kuu. Wakati huo hatari wa taaluma yake ulikuwa upumbavu mkubwa wa Hitler. Uingereza ilikuwa karibu kujisalimisha, lakini jeshi la Ujerumani liliondoka na kwenda kupigana na Urusi! Na, pia, kuanguka kwa wakuu wake kutajwa kabla ya kuanguka kwa Ashuru kutajwa, unabii hivi unafichua kwamba “yeye asetaye vipande vipande,” Hitler, alikuwa wa kwamza kuanguka. {1TG3: 16.1}
——-0——
Swali la 3: “Kwa nini jina la Hitler ‘yeye asetaye vipande vipande’?”
Naam, hayo ndiyo yote Hitler alifanya. Alianza kuvunja vipande vipande kutoka mwanzoni mwa vita, — hakuna aliyeweza kusimama dhidi yake, na hata baada ya kutoweka, na Ujerumani kujisalimisha, kuvunja vipande vipande kuliendelea na hata sasa hakujakoma. Matokeo yake dunia yote imevunjwa vipande vipande, sio tu kiji-ografia, ila kisiasa na kijamii na kiuchumi pia. Ufalme wa Kiingereza bado unatikisika, na ya kuogofya “milio” inaendelea kusikika zaidi na zaidi kila siku inayopita. Hitler, kwa hivyo, anastahili jina (“asetaye vipande vipande”) kwa njia nyingi. {1TG3: 16.2}
16
——0——
Swali la 4: “Je, unabii wa Nahumu haufundishi kwamba Ashuru itaanguka kabisa?”
Naam, hilo ndilo tu tunaloelewa hufundisha. Dhahiri kabisa, basi, unabii wa Nahumu huonya umbele kwamba Vita Kuu vya Pili vya Dunia hata sasa havijakoma. Dunia yenyewe inajua kuwa havijaisha, na kwamba Muun-gano, isipokuwa Urusi, haukushinda chochote, kwamba ingalikuwa bora zaidi wangalimpa Hitler sehemu ya Po-land kuliko kupambana katika vita na kisha kupoteza kwa Urusi sio tu sehemu ila Poland yote na pamoja nayo Ulaya Mashariki yote. Aidha, Urusi sasa imekuwa adui wao mkubwa zaidi kuliko Hitler. Walimwondolea mbali Hitler, lakini vita vikali kamwe havikukoma, na vita baridi vimeongeza hivi karibuni juu yake. Kila mtu anajua kwamba vita havijatulia, na kwamba amani haijakuja, kwamba vita vinaweza kuzuka moto kabisa siku yoyote. {1TG3: 17.1}
——0——
Swali la 5: “Je, trakti zenu hufundisha nini kuhusu vita?” –
Trakti hazisemi mengi. Hazisemi dhahiri “yeye asetaye vipande vipande” ni nani, wala hazisemi hakika kwamba Vita Kuu vya 2 ni vita vya Nahumu. Na ambapo Trakti Namba 14, Utabiri wa Habari za Vita, inasema kwamba jeshi lake yeye asetaye vipande vipande, “pia pamoja na hayo litaanguka,” haisemi kwa kweli kwamba ni jeshi la nani litaanguka kwanza. (Angalia Trakti Namba 14, uk. 12, — maelezo juu ya Nahumu 2: 5.) {1TG3: 17.2}
Trakti Namba 12, Dunia, Jana, Leo, Kesho, kilichapishwa miaka miwili kabla Trakti Namba 14, hata hivyo, inasema: {1TG3: 17.3}
“Kwa sasa inaonekana kwamba hema za maskani yake’ zinadhaniwa kuwakilisha utakatifu, na kwamba mwa-namke kumwendesha
17
mnyama ni kiashirio cha yeye kuyatatua matatizo ya dunia ya kijamii, kiuchumi, kisiasa, na kidini, ukweli ni dhahiri kwamba serikali za sasa za Kikristo zitapangwa upya, na kutawaliwa na kiongozi wa kanisa — sio na Hit-ler.” {1TG3: 17.4}
Trakti hazisemi kila kitu, ila kile zinachosema, huwa zinasema moja kwa moja. {1TG3: 18.1}
18
MASWALI NA MAJIBU KUADILIANA
(Sehemu ya 2)
Walaodekia ni nani?
Ni Akina Nani Mfalme wa Kaskazini Na
Mfalme wa Kusini?
Je, Vita vya 2 viko katika Danieli Kumi na Moja?
Jinsi Ya Kuugeuza Wakati Uliopotea Kwa Matumizi Mazuri
MATINI YA HOTUBA NA V. T. HOUTEFF
MCHUNGAJI WA WADAUDI WAADVENTISTA WA SABATO
SABATO, AGOSTI 3, 1946
HEKALU LA MLIMA KARMELI
WACO, TEXAS
Alasiri hii mimi najibu maswali ambayo yamekuja kwangu kutoka kwa wandugu katika kanisa la mama. Lakini unapoyasikiliza majibu nataka uangalie kwamba sisi, pia, tulikuwa mahali pao; kwamba sisi pia tulikuwa Wala-odekia asili; na kwamba wanavyofanya sasa, sisi pia tulifanya hivyo wakati huo. Sisi, pia, labda tulihoji kila kitu ambacho hatukuwa na sehemu kwacho; tulitenda na kunena kwa namna ile ile kama wao. Ni jambo la kutisha na lisilofaa namna gani kwa Mkristo kutoamini hata unenaji wa Bwana Mwenyewe kwa Walaodekia, hata sisi, pia, tulifikiri hatukuhitaji kitu, bali kwamba wengine wote walituhitaji sisi. {1TG4: 19.1}
Unajua kwamba hatukuwa welekevu wakati huo kama tulivyo sasa. Na wakati mafundisho yetu yalipohojiwa sisi, pia, kama ndugu zetu, hatukutoa kwa uaminifu na bila ubaguzi usikivu mzuri kwa maoni ya wengine. {1TG4: 19.2}
Wakati tulipokuwa mahali pao sisi, pia, katika uvuguvugu wetu tulitetea kwa bidii kila fundisho, hata
19
ingawa sisi wenyewe hatukuwa na ufahamu katika baadhi yake. Hili tulifanya tu kwa sababu mafundisho yali-yofundishwa kanisani na ndugu zetu Wachungaji sisi, pia, labda tuliamini yalikuwa sahihi. Na hivyo sisi, kwa upofu kama walivyoamini asilimia mia moja ya chochote kilichofundishwa kanisani, bila kuzingatia kwamba mengi ya hayo yalikuja kupitia kwa watu ambao hawakuvuviwa. Yaliyovuviwa au yasiyovuviwa hayakufanya tofauti yoyote kwetu wakati huo, kwa vile hayafanyi tofauti kwa wao sasa. Sisi, pia, tulikuwa katika wa kutisha udanganyifu wa kusikitisha na kwa hakika pamoja nao hatukujua au hatukuamini, kwamba tulikuwa wanyonge, wenye mashaka, maskini, vipofu, na uchi, ingawa Bwana mwenyewe alisema hivyo! Ufu. 3: 14-18. Tuliendelea katika hali hiyo ya mawazo mpaka gombo likakunjua. Kisha macho yetu yalifumbuliwa: mafundisho na ufafa-nuzi ambao haukuja kupitia Uvuvio wakati huo tuliona wazi kwamba yalikuwa tu “ubunifu wa wanadamu.” Wa-la hatukuona mbeleni ya kuwa Sabato na kanisa ziligeuzwa kuwa taasisi za kuongeza malengo na biashara — njia ya kutomheshimu Mungu na kuwanyang’anya masikini kuwalisha na kuwavika wale wanaoliweka kanisa lote katika wa kutisha udanganyifu wa kusikitisha wa Ulaodekia. {1TG4: 19.3}
Kwa hiyo tukiliangalia kutoka kwenye pembe hii, hatukuwa hata afadhali kuliko aliye bora wa Walaodekia. Kinachofanya tofauti kati yetu na wao ni kwamba nuru imeangaza njia yetu, ila bado haijawafikia. Sifa, basi, kwa maendeleo tumeweza kuwa tumefanya katika juhudi hii ya uamsho na matengenezo sio yetu, bali ni ya Mungu. {1TG4: 20.1}
Swali la kwanza lijibu alasiri hii linatupeleka kwenye sura ya kumi na moja ya Danieli, huko
20
Kumtambua Mfalme Wa Kaskazini Na Mfalme Wa Kusini {1TG4: 20.2}
Swali ni: “Ni akina nani mfalme wa kaskazini na mfalme wa kusini katika siku zetu?” – Kwa vile ni wajibu wetu kumtakasa Bwana Mungu mioyoni mwetu, na kuwa tayari kutoa jibu sahihi kwa wakati mwafaka kwa kila mtu aulizaye habari ya tumaini lililo ndani yetu, hebu tusome– {1TG4: 21.1}
Dan. 11: 40-43 — “Na wakati wa mwisho mfalme wa kusini atashindana naye; na mfalme wa kaskazini atamshambulia kama upepo wa kisulisuli, pamoja na magari ya vita, na wapanda farasi, na merikebu nyingi; naye ataingia katika nchi hizo, na kufurika na kupita katikati. Tena ataingia katika hiyo nchi ya uzuri, na nchi nyingi zitapinduliwa; lakini nchi hizi zitaokolewa na mkono wake, Edomu, na Moabu, na wakuu wa watu wa Amoni. Naye ataunyosha mkono wake juu ya nchi hizo, hata na nchi ya Misri haitaokoka. Lakini atakuwa na nguvu juu ya hazina za dhahabu na fedha, na juu ya vitu vyote vya Misri vyenye thamani; na Walibia na Wakushi watafuata nyayo zake.”
Mgogoro unaoletwa kwa mtazamo katika aya hii, unaotukia kati ya wafalme, sio kabla ya wakati wa mwisho, au katika wakati wa mwisho, ila “mwanzoni mwa wakati wa mwisho.” Mfalme wa kusini kumbuka, ndiye atakaye-shindana na mfalme wa kaskazini, na mfalme wa kaskazini ndiye atakayeshinda vita, na kuiteka kutoka kwa mfalme wa kusini nchi ya uzuri (Palestina) na Misri kando na nchi ambazo hazijatajwa kwa majina. Vipengele hivi kama tunavyoona sasa ni vya kutosha kuwatambua kabisa wafalme wawili, vita, na wakati ambapo vitapi-ganwa. Na kwa sababu vita vitaanza mwanzoni mwa wakati wa mwisho, na kwa vile mfalme wa kusini
21
ndiye atakayeshindwa vitani, nchi ambazo zimeshindwa lazima kwa hivyo zitawaliwe na mfalme wa kaskazini katika wakati wa mwisho. (Kwa maelezo ya kina ya Danieli kumi na moja, soma Trakti Namba 12, Dunia, Jana, Leo, Kesho, kur. 57-91. {1TG4: 21.2}
Kwa sababu wale ambao waliuliza maswali hukubaliana nasi kwamba sasa tunaishi katika “wakati wa mwisho,” hatuhitaji kusema zaidi juu ya awamu hiyo ya somo, lakini tunawahitaji watuambie ni utawala gani hasa kwa wakati huu, katika wakati wa mwisho, umeongeza “nchi ya uzuri” (Palestina), Misri, na nchi zingine kwa ufalme wake. Jibu ambalo yeyote anaweza kutoa ni kwamba Uingereza Kuu ilizichukua hizi kutoka kwa Uturuki na kweli imezitawala tangu wakati huo. Kwa hakika, wakati wa mwisho Uingereza ni mfalme wa kaskazini na Uturuki ni mfalme wa kusini. Kwa hakika hivyo, pia, maana Uislamu kwa asili uliinukia kusini mwa Mediterania na kuzitawala kwa kipindi kisicho na tarehe iliyoandikwa nchi za kaskazini hadi kwa wakati wa mwisho. Kisha meza zilipinduka na utawala wa Uturuki ukaanza kudidimia ilhali wa Ungereza ukaanza kupanuka. {1TG4: 22.1}
Maadamu hakuna njia ya yeyote kuukwepa ukweli wa somo, hakuna haja ya kulijadili zaidi. Kwa ajili ya utafiti wa kina juu ya Danieli kumi na moja soma sehemu ya mwisho ya Trakti Namba 12. Dunia, Jana, Leo, Kesho. {1TG4: 22.2}
Usitarajie mengi sana kwa ajili ya Walaodekia, hata hivyo, kwa maana ili ujue kuwa ni vigumu kwao kuukubali Ukweli kama ilivyokuwa kwa wengi wetu wakati tulipokuwa mahali pao. Kwa nini? — Sababu kwa wanadamu wengi ni vigumu kusema, “tumekosea.” Wachache tu wanaweza kuyakataa majivuno ya maoni na kuyakubali makosa yao. Kwa sababu hii hasa kwamba Ukweli uliofunuliwa upya kamwe sio maarufu. Wakati Ukweli wa leo ulitujia, hatukuuamini kwa sababu wengine waliuamini, ila kwa sababu sisi
22
wenyewe tuliuona wazi. Hebu tuendelee hivyo, lakini tuwe na subira, wavumilivu, na wenye kuwapenda wote. {1TG4: 22.3}
——0——
Swali letu lijalo la kujibiwa —
“Je, Vita vya 2 vya Dunia Viko Katika Unabii wa Danieli?” {1TG4: 23.1}
Dan. 11:44, 45 — “Lakini habari zitokazo mashariki na kaskazini zitamfadhaisha; naye atatoka kwa ghadhabu nyingi, ili kuharibu, na kuwaondolea mbali watu wengi. Naye ataweka hema zake za kifalme kati ya bahari na mlima mtakatifu wa uzuri; lakini ataifikilia ajali yake, wala hakuna atakayemsaidia.”
Katika vita hivi hasa mfalme wa kaskazini anaondoka kuwaangamiza wengi kwa sababu habari zisizofurahisha kutoka mashariki na kutoka kaskazini, zinafika masikioni mwake. Mfalme wa kusini kusini kwa hivyo hahusiki katika hilo. {1TG4: 23.2}
Tangu Hitler na Urusi (dola za kaskazini) walianza Vita Namba 2 huko Poland, kisha Japan (dola ya mashariki) ilijiunga nazo, na maadamu Uturuki, mfalme wa kusini alijitenga navyo, ni dhahiri sana kwamba vita vya Dan. 11:44 ni Vita vya 2 vya Dunia ambapo habari zilizotajwa hapa ziliivuta Uingereza (mfalme wa kaskazini). Vita vya 2 vya Dunia ni hakika vita vilivyotabiriwa katika Dan. 11:44, 45, vita vya mwisho vya Daniel kumi na moja. Zaidi ya hayo, ukweli kwamba aya ya 44 hadi sasa imetimizwa, kwamba mfalme bado hajafikia mwisho wake, ni ushahidi wazi kwamba Vita vya Dunia bado havijakwisha, kwamba haitakuwepo amani sasa, na hakuna ma-kubaliano ya maafikiano kati ya mataifa ingawa vita vinadhaniwa vimekoma tangu kutoweka kwa Hitler. {1TG4: 23.3}
Taarifa, “Ataifikilia ajali yake, wala hakuna
23
atakayemsaidia,” inayo maana kwamba mtu fulani amekuwa akimsaidia, na ulimwengu unajua kwamba ya-mekuwa Majimbo Yaliyoungana ya Marekani. Tunajikuta, kwa hivyo, tukiishi kati ya aya 44, na 45 za Danieli kumi na moja. {1TG4: 23.4}
——0——
Swali letu lijalo ni,
“Wakati Wa Mwisho Unaanza Lini?” {1TG4: 24.1}
Hebu tusome– {1TG4: 24.2}
Dan. 11:35 — “Na baadhi yao wenye hekima wataanguka, ili kuwatakasa, na kuwasafisha, na kuwafanya weupe, hata wakati wa mwisho; kwa maana ni kwa wakati ulioamriwa, ambao haujaja.”
Hapa unatambua kwamba watu wa Mungu walipaswa kuanguka, kuteswa, kuuawa na kujaribiwa hata mpaka wakati wa mwisho. Walipaswa kupitia matatizo hayo ili kusafishwa, kujaribiwa, na kufanywa weupe. Kumbuka kwamba kusafishwa kulipaswa kuendelea “mpaka wakati wa mwisho,” na kwamba mfalme wa kusini an-geshindana naye mfalme wa kaskazini “mwanzoni mwa wakati wa mwisho.” Sasa maki kihusishi “mpaka” kina-koma kwenye kihusishi “mwanzoni,” ndipo ambapo kusafishwa kunamalizikia, mfalme akaanza ushindani. Maelezo haya yaliletwa kwenye nuru mwanzoni mwa somo hili. {1TG4: 24.3}
Hadi hapa ninavyoweza kupata, historia inafundisha kwamba mauaji ya waumini yalikoma mwaka wa 1700 B.K., na kwamba ufalme wa Uturuki ulianza kusambaratika mwaka wa 1699. (Angalia Ramani Namba 10 ya Trakti 12, Dunia, Jana, Leo, Kesho.) Wakati wa mwisho, kwa hivyo, ulianza mwishoni mwa karne ya kumi na saba, wakati ambapo mauaji ya waumini yalikoma, na wakati ufalme wa Uturuki ulianza kusambaratika. {1TG4: 24.4}
24
Zaidi ya hayo, akizungumza kuhusu dhiki ambayo mamilioni waliuawa kwa imani, Yesu alisema: “Lakini mara baada ya dhiki ya siku zile jua litatiwa giza ….” Mat. 24:29. Siku ya giza ilikuja mwaka wa 1780 B.K. Na wakati Ufalme wa Uturuki uliendelea kusambaratika, Waingereza waliendelea kupanuka. Hapa inaonekana kwamba unabii unathibitsha kikamilifu historia. Sasa jifunze–
“Jinsi Ya Kuugeuza Wakati Uliopotea Kwa Matumizi Mazuri” {1TG4: 25.1}
Unafahamu ukweli kwamba tumepewa kazi kuu na kwamba wakati wa kuifanya ni mfupi sana; kwamba tuna-paswa kwa hivyo kujifunza jinsi ya kuugeuza wakati uliopotea kwa matumizi mazuri. Mtu fulani amesema kwamba kwa wastani, zaidi ya nusu ya maisha ya wanadamu na nguvu hupotezwa juu ya kuzungumza ovyo maana na kuwadhibiti wengine. Mojawapo ya mahitaji yetu makubwa ni kwamba tujifunze kuzitawala ndimi zetu na kujiepusha na shughuli za watu wengine ili kuhifadhi wakati na kawi, amani na uadilifu. {1TG4: 25.2}
Ni vyema kukumbuka pia, kwamba ndimi zetu tumepewa kwa kusudi la kunena Ukweli wa Mungu na sifa Zake, na nguvu zetu kuutangaza Ukweli Wake na kuwabariki watu Wake. Hebu tuwe tukizizungumzia na kuzifanyia kazi kanuni hizi za kutoka mbinguni. Ikiwa kwa kushtukia upate kuona au kusikia kwamba mtu fula-ni anafanya kitu ambacho kulingana na hukumu yako bora sio sahihi kwa Mkristo kukifanya, na iwapo unadhani unaweza kumsaidia, basi usijifanyie kuwa msengenyaji kumwaambia kila mtu yeyote ila badala yake suluhisha na mwenye hatia. {1TG4: 25.3}
Usijifanye kuwa kigezo ama kwa yeyote, wala msimlazimishie yeyote mawazo yenu bali juu yenu mwenyewe. Sio wajibu wa mmoja kumdhibiti mwingine. Elewa
25
kwamba hakuna mtu aliye katika deni la kuyaleta maisha yake kwa viwango na maadili ya yeyote. Sikiliza unachosema Uvuvio: “Wewe u nani unayemhukumu mtumishi wa mwingine? Kwa bwana wake mwenyewe yeye husimama au huanguka. Naam, atasimamishwa, kwa kuwa Bwana aweza kumsimamisha.” (Rum. 14: 4) ila kwa sababu huwezi, basi kwa nini ujaribu! {1TG4: 25.4}
Msijifanyie maadui kwa ndimi zenu. Tengeneza Marafiki. Na usiwe na hisia zako kwenye ncha za vidole. Ikiwa utafanya hivyo, wewe mwenyewe utahisi kuwapoteza marafiki, furaha ya kijamii, na fursa na haki za kuziongoa roho kwa Kristo. Usiikamilishe siku bila sifa ya kunakiliwa kwenye ukurasa wako wa daftari ya Mbinguni. Usiyafafanue visivyo maazimio ya watu wengine ama. Jaribu kuona na kufafanua kila kitu kwa njia sahihi, mpe kila mtu nafasi. Angalia yaliyo mema kwa kila mtu na uyafumbe macho yako kwa uovu wote. {1TG4: 26.1}
Hebu mazungumzo yako yawe juu ya kuutangaza Ukweli wa Mungu wa leo. Utakushughulisha uendelee kuzungumza juu ya kitu kinachofaidisha na cha kupongezwa. Fikiria na kujifunza, na unapozungumzia dini, kwa njia zote usiwe wa kuchosha. Endelea na masimulizi yako tu kwa umbali ule wasikilizaji wako wanavyokufuata — “Msiwape mbwa kilicho kitakatifu, wala msitupe lulu zenu mbele ya nguruwe, wasije wakazikanyaga chini ya miguu yao, wakageuka na kuwararua.” Mat . 7: 6. {1TG4: 26.2}
Ndimi ni ngumu kuzidhibiti, na masikio daima hutamani kusikia. Itakuwa bora kwa hivyo iwapo utafanya kuzuru kuchache. Kuzuru sana ni kupoteza muda tu na jaribio la kuzungumzia vibanzi machoni mwa wengine na kutotazama boriti iliyo ndani ya jicho lako mwenyewe. {1TG4: 26.3}
Kila unapokuwa pekee yako unaweza kufanya
26
kitu. Unaweza basi aidha kufanya kazi au kujifunza. Lakini unapojumuika na wengine, uwezekano ni kwamba hutafanya kitu chochote ila madhara kwako mwenyewe na wengine. Sasa ni wakati wa kuuchunguza na kuji-funza Ukweli wa wakati huu, kujua jinsi ya kuwasilisha somo na jinsi ya kuyajibu maswali kwa njia rahisi, bila kwenda katika historia nyingi au wasifu. Na iwapo umeamua kutembea na Mungu kila siku na kujifunza mapen-zi Yake juu ya kazi zako mwenyewe, sio kazi za wengine, utapata mengi ya kukufanya uendelee kujisughulisha na nje ya fitina. {1TG4: 26.4}
Kumbuka pia kwamba ninyi ni wagombea kwa ajili ya malimbuko, kuwa ama mmoja na au mmoja wa watu 144,000, kwamba hamtakuwa na uongo vinywani mwenu (Ufu. 14: 5). {1TG4: 27.1}
Yapime maneno yako kwa kanuni ya dhahabu. Iwapo utawatendea wengine yote utakayotaka wao wakutendee, utakuwa na taabu kidogo, furaha kubwa maishani, marafiki wengi kukuzunguka, na miganda mizuri kwa ajili ya Ghala la Mbinguni. {1TG4: 27.2}
Usiyakose Manufaa Juu ya Hili
Iwapo haujatuma kwa ajili ya nakala yako iliyotangazwa na iliyojadiliwa sana kijitabu cha afya cha kurasa 96 (Kabari Inayoingia) ambacho kimefanya uamsho mkubwa katika dunia ya Waadventista na ambacho kimeliweka Shirika la K.I. katika mwangaza, usikikose iwapo afya, nyumba, na furaha yako inamaanisha kitu kwako. Kwa maoni yetu kitabu hiki ndicho bora hatujawahi kuona juu ya suala hili. Kwa kweli tunahisi kwamba kimetumwa na Mungu, na kwamba nakala yake inapaswa kuwa katika kila nyumba. Tumejulishwa kwamba sasa unaweza kukipata bila kuagizia. Tuma jina lako, anwani, na jina la kanisa ambalo wewe ni mshiriki (unaombwa kuchap-isha), na senti 15 kwa sarafu au stempu kwa Shirika La Kabari Inayoingia La Marekani, Kituo cha Mlima Kar-meli, Waco, Texas, Marekani na kitatumwa kwako. {1TG4: 27.3}
27
Jumuiya ya Wadaudi Waadventista wa Sabato
(Ushirika Huru Unaojumuisha Kanisa)
Mlima Karmeli, Waco, Texas
S.L.P. 23738, Waco, TX 76702
+ 1-254-855-9539
www.gadsda.com
info@gadsda.com
Gombo la 1, Namba 3, 4
Kimechapishwa nchini Marekani
28