fbpx

Trakti ya Fimbo ya Mchungaji Gombo la 1

Trakti ya Fimbo ya Mchungaji Gombo la 1

1

Hati miliki 1930, 1945 na

V.T. Houteff

Haki zote zimehifadhiwa

Kwamba kila mtu aliye na kiu kwa ajili ya kweli aweze kupata, kijitabu hiki ni, kama huduma ya Kikristo, kinatumwa bila malipo. Tuma ombi lako. Kinaweka tu dai moja: wajibu wa nafsi kwa mwenyewe kuyajaribu mambo yote na kushika lililo jema. Nyuzi za pekee zinazounganishwa na toleo hili la bure ni ncha za dhahabu ya Edeni na kamba nyekundu ya Kalvari – mahusiano ambayo hufunga. {SR1P: 2.1}

Kilichapishwa tena 1997

2

FIMBO YA MCHUNGAJI

Kitabu cha 1

Toleo la pili

na V. T. Houteff

Huyu “mwandishi,” ameagizwa kwaUfalme wa mbinguni, “atoaye… vitu vipya na vya kale.” Mathayo 13:52. {SR1P: 3.1}

Sasa mtakaseni Bwana Mungu mioyoni mwenu, na kujiandaa kusimama na Mwana-Kondoo juu ya Mlima Zayuni. {SR1P: 3.2}

3

YALIYOMO

FIMBO YA MCHUNGAJI, NI NINI? 5

KUWATIA MUHURI MALIMBUKO – WALE 144,000 7

MAVUNO YA PILI — UMATI MKUBWA 17

Gwaride ya gwaride zote! Angalia Inapita 23

ESAU AU YAKOBO – YUPI? 25

Ndoto ya Yakobo 33

Mama za Wana wa Yakobo 34

Safari ya Yakobo kurudi Nyumbani 36

ISRAELI WAENDA MISRI 37

Mungu Aliulisha Ulimwengu wa Kale na Nafaka jinsi

Anavyolisha Dunia ya Sasa na Ukweli 39

Kutoka kwa Mazizi ya Kondoo hadi kwa yadi za Matofali 45

Hakuna tena Nyasi 47

Shifra na Puah 49

ISRAELI KUONDOKA MISRI 53

MAAJABU YA ELIMU YA MIFANO 56

MPANGILIO WA SANJARI 66

Muhtasari 70

EZEKIELI NNE 74

AKINA MAMA, SASA FANYA RUFAA YENU YA MWISHO 87

MIFANO

Kanisa na Ukuhani Wake 61

Ulinganifu wa Maongozi ya Mungu 72

4

FIMBO YA MCHUNGAJI

===========

NI NINI?

Kusudi la msingi la Fimbo ya Mchungaji ni kufungua siri iliyofichwa kwa muda mrefu juu ya suala lenye changamoto daima na linalojadiliwa zaidi la watu 144,000 (Ufunuo 14: 1), na jambo kuu kwa mtazamo la kuleta kuwahusu watu wa Mungu ” matengenezo ya kweli “yaliyotabiriwa na Roho ya Unabii (Shuhuda, Gombo la 8, uk. 251). {SR1P: 5.1}

Kweli hizi, zimefunuliwa na Mungu, ni muhimu sana kwa kanisa sasa tu kwa sababu ya hali za kujaribiwa, kupepetwa ambazo watu wa Mungu watapitia hivi karibuni. Kuwa ni wasiwasi za muhimu kwa wokovu, zinaitisha hatua za uamuzi kutoka kwa ukasisi sawa na waumini wajitenge na kuipenda dunia na kutia nanga kwenye Mwamba ulio Imara kwa kutii ukweli wote unaojulikana kwa kanisa, iwapo wangetaka kuukimbia uharibifu unaokuja ambao utamchukua kila mdhambi. {SR1P: 5.2}

Lengo kubwa la mafundisho likiwa ukweli wa watu 144,000, na ufahamu wake kwa usahihi likiwa suala la maisha na kifo kwa wote, Fimbo inalifunua kutoka pembe kadhaa tofauti, kila moja akilihimiza Dhehebu kujiandaa kwa ajili ya ukombozi wa utukufu

5

wa watakatifu na dhidi ya uharibifu wa wenye dhambi kama ulivyoashiriwa awali kwa kutiwa muhuri na kuuawa katika Ezekieli 9. {SR1P: 5.3}

Hakuna dhehebu jipya linaloshindaniwa hapa, kinyume chake, hili halikubaliki na kupingwa. Na hatimaye, uthibitisho dhahiri unaonyeshwa kwamba dhehebu la wa-Adventista wa Sabato limekuwa chombo cha Mungu tangu 1844 kuendeleza kazi Yake duniani, na kwamba Fimbo inaongeza “uwezo na nguvu” “kwa ujumbe wa tatu.” – Maandishi ya Awali, uk. 277. {SR1P: 6.1}

Ikionekana kuwa ni uakisi wa kutoka kwa kwanza, Fimbo ya Mchungaji inachukua jina lake kutoka kwa fimbo ya Musa, chombo ambacho Bwana alidhihirishia uwezo Wake kuwakomboa wana wa Israeli. Fimbo ya Mchungaji, ni Fimbo ya pekee ambayo imewahi kuzungumza, inatabiriwa na kuidhinishwa katika Mika 6: 9: “Isikieni hiyo fimbo na [Yeye] aliyeiagiza.” {SR1P: 6.2}

(Hili ndilo toleo jipya la Fimbo ya Mchungaji, Gombo la 1, lililochapishwa awali mwaka 1930. Kulifanya kitabu kidogo cha mfukoni, maana kwa toleo lililopita zimeshughulikiwa katika namba zingine za machapisho haya zimepunguzwa, na maneno ya somo kufupishwa.) {SR1P: 6.3}

Kwa kufuata amri ya Bwana, tunapaswa sasa na masikio yaliyo wazi tuusikie ujumbe wa Fimbo. (SR1P: 6.4}

6

KUWATIA MUHURI MALIMBUKO — WATU 144,000

“Nikamwona malaika mwingine, akipanda kutoka maawio ya jua, mwenye muhuri ya Mungu aliye hai; akawapigia kelele kwa sauti kuu wale malaika wanne waliopewa kuidhuru nchi na bahari, (SR1P: 7.1}

“akisema, msiidhuru nchi, wala bahari, wala miti, hata tutakapokwisha kuwatia muhuri watumwa wa Mungu wetu juu ya vipaji vya nyuso zao.” (SR1P: 7.2}

“Nikasikia hesabu yao waliotiwa muhuri katika kila kabila ya Waisraeli, watu mia na arobaini na nne elfu.” Ufu. 7: 2-4. {SR1P: 7.3}

Siri kuhusu kutiwa muhuri watu 144,000 pengine ni la kipekee kwa somo lolote la Biblia. Nadharia zimesongamana na nadharia, zaidi tu kuufumba na kuuchanganya ukweli wake. Hakuna dhehebu la Kikristo limeonekana kuepuka pambano ambalo, kwa kutoa maoni mengi yanayotofautiana, limeongeza tu ufa katika kinubi cha Uprotestanti. {SR1P: 7.4}

Hili limekuwa la kusikitisha sana, na zaidi hivyo miongoni mwetu kama wa-Adventista wa Sabato, kwa muda mrefu uliopita mjumbe wa Bwana alitupatia mawaidha “tujitahidi kwa nguvu zote ambazo Mungu ametupa kuwa miongoni mwa watu 144,000” (Mapitio na Kuhubiri, Machi 9, 1905), na kisha kwa neema kuweka mikononi mwetu maarifa muhimu kwa wakati wa sasa kwamba ni lini na wapi, kwa nini na ni nini, muhuri. {SR1P: 7.5}

7

“Hii kazi ya kutiwa muhuri watumwa wa Mungu,” Bwana alitangaza, “ni sawa na aliyo onyeshwa Ezekieli katika maono.” – Shuhuda kwa Wachungaji, uk. 445. (Soma Ezekieli 9). {SR1P: 8.1}

Na katika kuliimarisha somo mjumbe aliandika: “Hasa katika kazi ya kufunga kwa kanisa, wakati wa kutiwa muhuri watu mia na arobaini na nne elfu ambao watasimama bila waa mbele ya kiti cha enzi cha Mungu, watahisikwa undani sana makosa ya watu wanaodai kuwa wa Mungu. ” – Shuhuda, Gombo la 3, uk. 266. {SR1P: 8.2}

Kwa hiyo, kutia alama kunafanyika kanisani kwa sababu ya “machukizo” yanayofanyika katikati yake. Kwa hivyo, kuondolewa kwa wale wanaoendeleza machukizo ni kazi yake ya kufunga, si ya ulimwengu. {SR1P: 8.3}

Kwa ufunguo huu wa maarifa mkononi, kanisa lingekuwa limeendelea mbele kwa nuru na maendeleo ya Ukweli na kwa wakati ulioamriwa kuwezeshwa kuifungua siri. Lakini kwa kushindwa kutii sauti ya Bwana na hivyo kutembea katika Nuru na kukua kutoka kwa maarifa hadi maarifa, lilipoteza njia yake na hivyo limekuwa kwa miaka linatangatanga katika nyika ya nadharia, hivyo kwa kusema. {SR1P: 8.4}

Na ambapo lilikuwa katika kuchanganyikiwa juu ya somo, Roho wa Kweli alitamka kimya juu yake hatimaye kuwa “unenaji.” Lakini unenaji kwa muda gani? Milele? — Ni dhahiri hapana, bali tu mpaka Bwana Mwenyewe akifumue chuo, kutiwa muhuri kuanze,

8

na somo liwe ukweli wa sasa. Kisha kimya hakitakuwa tena unenaji; kwa kweli, hata haiwezekani — kama daima wataweza kuwa watu 144,000 waliotiwa muhuri na kuandaliwa kusimama na Mwana-Kondoo juu ya Mlima Sayuni (Ufunuo 14: 1). {SR1P: 8.5}

Ufahamu wa kina unaoendelea wa somo hili lazima uwe na umuhimu mkubwa kama vile ufahamu kamili wa Danieli 7, Ufunuo 13 na 17, Ujumbe wa Malaika watatu wa Ufunuo 14, au siri nyingine yoyote ya Biblia iliyofunuliwa au unabii. Na mmoja anawezaje kuokoka kuchinjwa isipokuwa mtu ajue ni nini kutiwa muhuri, kuwekwa alama, lini, na wapi? {SR1P: 9.1}

Hivyo ambapo kwa upande mmoja kunaonekana umuhimu mkubwa na hivyo uhakika kabisa wa Ufunuo unaofunua kikamilifu somo wakati wa kufunga kazi kwa kanisa, kwa upande mwingine yameonekana matokeo ya kutowezekana kabisa mtu yeyote kuugundua ukweli wote kabla ya wakati wake. {SR1P: 9.2}

Yeyote anayefikiria anajua kwamba ukweli ungefanywa ujulikane kabla ya wakati, kungeuacha kuwa bure, usio na thamani, na usio na ufanisi kama ukweli kuhusu sanamu ya mnyama miaka kabla au dakika moja baada ya kuifanya kazi yake ya udanganyifu. Lakini inapogonga saa iliyoamriwa kabla, wakati Uvuvio unafungua siri, wote wanaweza kuuona ukweli na kufaidika nao. Kwa furaha, tunaweza kwa akili kujitahidi kuwa miongoni mwa kundi hili lisilo na hila, iwapo kwa uaminifu na subira tunaendelea kufuata kuujua ukweli kwa wakati. {SR1P:9.3}

9

Mtu anauliza, “Ni lini ambapo kazi hii ya kufunga kwa kanisa itaanza?” — Ni dhahiri, tayari inaendelea. Mwanga unamimina juu ya somo hilo, ukilifukuza giza ambalo kwa muda mrefu limelifunika. Baada ya hivyo kuwa ukweli wa sasa kuiangaza njia ambayo watu 144,000 wata “mfuata Mwana-Kondoo popote aendako” (Ufunuo 14: 4), lazima utangazwe hata kutoka juu ya paa za nyumba. {SR1P: 10.1}

Katika mwaka wa 1844, jinsi wa-Adventista wa Sabato wote wanavyojua, Dada White alipewa njozi ya watu 144,000 wakiashiria safari ya malaika wa kutia muhuri akianza kupanda kutoka mashariki (Ufunuo 7: 2-4). Kutoka wakati huo alikuwa akipanda, na watakatifu wakisubiri kuwasili kwake. Hatimaye, mwaka wa 1929, kupitia Masomo ya Shule ya Sabato Bwana alitangaza kote katika dhehebu la wa-Adventista wa Sabato ya kuwa malaika amewasili. Kisha chuo kilianza kufumuka na uwepo wa malaika kuhisiwa na wengi wa wale waliokuwa wakiumia kutaka ukweli na haki. {SR1P: 10..2}

“Lakini tunawezaje kujua kwa hakika,” mwingine anauliza, “kwamba hiki na vitabu vyenza vilivvyochapishwa ni matunda ya kweli ya kufumua chuo na kuwasili kwa malaika anayetia muhuri? – Iwapo tu kama mdai hapa

10

kwa kesi amethibitisha kwa Maandiko yote muhimu na ushuhuda mwingine ulioviviwa. Na ikiwa ni hivyo, basi hitimisho tu la kufaa linalohitajika ni kwamba saa iliyoamriwa na Mungu na iliyongojewa kwa muda mrefu imegonga, na kwamba kitabu hiki ni chombo kinachotumiwa na Uvuvio kulifanya tukio hilo lijulikane kwa watu wa Mungu. {SR1P: 10.3}

Tangu, kama tulivyokwisha ona kutoka kwa Roho ya Unabii, kutiwa muhuri na kuchinjwa kunatukia kanisani wakati wa kufunga kazi kwa ajili yake, hawangeweza kuharakisha tarehe ya wakati huu. Na unabii wenyewe unaonyesha kwamba kutiwa muhuri lazima kuanze wakati ambapo maisha yake ya kiroho yako chini kabisa, wakati limetiwa unajisi na dhambi — katika “mwingi sana … uovu.” Ezek. 9: 9. Kwa maana ni hali yake unajisi ambayo inasababisha Mungu Mtakatifu kufanya katikati yake kazi ya kuweka alama, kutia muhuri, watakatifu, na kuwaondoa wadhambi kati yao. {SR1P: 11.1}

Lilianzaje kufikia hali hii? – Mtumishi wa Bwana anajibu kwa huzuni: {SR1P: 11.2}

“Bwana hajaifunga Mbingu kwetu, lakini mwenendo wetu wa kurudi nyuma umeendelea kututenga na Mungu. Kiburi, tamaa, na kuipenda dunia vimeiishi ndani ya moyo bila hofu ya kupigwa marufuku au kuhukumiwa. Dhambi za kuudhi na za kiburi zimekaa kati yetu. Hata hivyo maoni ya jumla ni kwamba kanisa linanawiri, na ya kwamba amani na ustawi wa kiroho upo katika mipaka yake yote. {SR1P: 11.3}

11

“Kanisa limekengeuka na kuacha kumfuata Kristo Kiongozi wake, na badala yake linarudi pole pole kuelekea Misri. Lakini wachache wametiwa hofu au kushangaa kwa upungufu wao wa nguvu za kiroho. Shaka na hata kutoziamini shuhuda za Roho wa Mungu, kunachachisha makanisa yetu kila mahali.” — Shuhuda, Gombo la 5, uk. 217. {SR1P: 12.1}

“Tumetanga mbali na mipaka ya zamani. Hebu turudi. Ikiwa Bwana ni Mungu, mtumikie: iwapo ni Baali, mtumikie. Unachagua kuwa upande gani? — Shuhuda, Gombo la 5, uk. 137. {SR1P: 12.2}

“Jinsi Yesu anavyoitazama hali ya wanaokiri kuwa wafuasi wake leo, anaona msingi wa ukosefu wa shukrani, mashimo ya desturi, wanafiki sugu, majivuno ya Ufarisayo na uasi.” – ShuhudaGombo la 5, uk. 72. {SR1P: 12.3}

“Ni nani anayeweza kusema kwa kweli, ‘Dhahabu yetu imejaribiwa kwa moto; mavazi yetu hayajatiwa doa na ulimwengu’? Nalimwona Mwalimu wetu akionyesha mavazi ya kile kinachoitwa eti haki. Aliwavua, Akautandaza wazi uchafu uliokuwa chini yake. Kisha Akaniambia: ‘Je! Huoni jinsi walivyojifunika kwa hila uchafu wao na uozo wa tabia?’ Je! Ni vipi Mji mtakatifu kuwa kahaba?” Nyumba ya Baba yangu imefanywa nyumba ya biashara, mahali ambapo uwepo wa Mungu na utukufu umetoweka! Kwa sababu hiyo kuna udhaifu, na nguvu zimekosekana.” – Shuhuda, Gombo la 8, uk. 250. {SR1P: 12.4}

12

“Wakati umewadia kwa jitihada za bidii na za nguvu kuondoa kanisani tope la kunata na uchafu unaotia aibu usafi wake.” – Shuhuda kwa Wachungaji, uk. 450. {SR1P: 13.1}

Hivyo kwa hakika ya kudhalilisha tunafanywa kuona na kukubali kwamba hali ya kanisa “inasikitisha machoni pa Mungu.” – Shuhuda, Gombo la 3, uk. 253. {SR1P: 13.2}

Na ni ukweli wa kuhuzunisha kwa watu wote wenye elimu na waaminifu katika Dhehebu lote, kwamba ingawa kwa miaka mingi limekuwa likishuka daima kiroho, halijawahi kufikia kiwango chake cha chini cha sasa ambacho halihifadhi hata tofauti yoyote ya awali kutoka ulimwenguni. {SR1P: 13.3}

“Kifo cha kiroho,” yaomboleza sauti ya Uvuvio, “kimekuja juu ya watu ambao wangekuwa wanadhihirisha maisha na bidii, usafi na kujitia wakfu, na kujitolea kwa bidii kwa ibada ya kweli. Ukweli juu ya hali halisi ya watu wanaokiri kumwamini Mungu, unanena kwa sauti zaidi kuliko wanavyokiri, na unaweka wazi kwamba uwezo fulani umeikata amari ambayo iliwaunganisha kwenye Mwamba wa Milele, na kwamba wao wanaelea baharini, bila ramani au dira. ” – Kristo Haki Yetu, uk. 36 (toleo la 1941). {SR1P: 13.4}

“Wanaume na wanawake wako katika masaa ya mwisho ya majaribio, na bado hata sasa hawajali na ni wapumbavu, na wachungaji hawana nguvu ya kuwaamsha; wao wamelala.

13

Wachungaji wanaolala wanahubiri kwa watu wanaolala! “– Shuhuda, Gombo la 2, uk. 337. {SR1P: 13.5}

Kwa hakika, “imani inaota mizizi duniani kwamba Waadventista wa Sabato wanapuliza kwa tarumbeta sauti isiyo ya uhakika, kwamba wanaifuata njia ya ulimwengu.” — Shuhuda kwa Wachungaji, uk. 86. {SR1P: 14.1}

Kwa sababu hizi zote na zingine, baadhi ambazo hatuzijui, Mungu msafi na Mtakatifu ana “unoa upanga wake Mbinguni kuwakata” wale ambao hawaugui na kulia. “Oo, kila anayekiri wa-uvuguvugu angeweza kutambua kazi safi ambayo Mungu karibu anaifanya kati ya watu wake wanaojidai!” – Shuhuda, Gombo la 1, uk. 190. {SR1P: 14.2}

“Tia alama jambo hili kwa uangalifu: Wale wanaoipokea alama safi ya ukweli, uliofanywa ndani yao kwa nguvu ya Roho Mtakatifu, ikiwakilishwa na alama ya mtu mwenye kitani, ni wale wanaougua na kulia dhidi ya machukizo yote yanafanyika “katika kanisa.” – Shuhuda, Gombo la 3, uk. 267. {SR1P: 14.3}

“Muhuri wa Mungu utawekwa kwenye vipaji vya wale tu wanaoomboleza na kulia dhidi ya machukizo yanayofanyika katika nchi.” — Shuhuda, Gombo la 5, uk. 212. {SR1P: 14.4}

Lazima, “wakati hukumu ya upelelezi inaendelea mbinguni, wakati dhambi za waumini waliotubu zinaondolewa kutoka patakatifu, kutakuwa na kazi maalum ya utakaso, ya kuweka

14

mbali dhambi, miongoni mwa watu wa Mungu duniani. “– Pambano Kuu, uk. 425. {SR1P: 14.5}

Sasa kwa kuwa kazi hii maalum inaendelea, hakuna shaka tena kwamba “siku za utakaso wa kanisa zinaharakisha mbio. Mungu atakuwa na watu wasafi na wakweli. Katika mchekecho mkuu ambao utatukia hivi karibuni, tutakuweza vyema kupima nguvu za Israeli. Ishara zinaonyesha kwamba wakati unakaribia wa Bwana kudhihirisha kuwa pepeto lake liko mkononi mwake, naye ataisafisha sakafu yake kabisa. ” – Shuhuda, Gombo la 5, uk. 80. {SR1P: 15.1}

Katika maono mengine ya kukumbukwa ya kazi hiyo muhimu sana, Dada White “aliwaona malaika wakiharakisha huku na huko mbinguni, wakishuka duniani, na tena wakipanda mbinguni, wakiandaa kwa utimizo wa tukio fulani muhimu. {SR1P: 15.2}

“Kisha nalimuona malaika mwingine mwenye nguvu,” anasema, “ameagizwa kushuka duniani, kuiunganisha sauti yake na ya malaika wa tatu, na kupeana uwezo na nguvu kwa ujumbe wake. Uwezo mwingi na utukufu alipewa malaika, na aliposhuka, dunia ikaangazwa na utukufu wake …. Ujumbe huu ulionekana kuwa ni nyongeza kwa ujumbe wa tatu …. “- Maandishi ya Awali, uk. 277. {SR1P: 15.3}

Na “wale tu,” asema Roho wa Kweli, “ambao wamestahimili majaribu katika nguvu za Mwenye Uwezo wataruhusiwa kutenda sehemu kuutangaza

15

[Ujumbe wa Malaika wa Tatu] wakati utakapoingia kilio kikuu.”– Mapitio na Kuhubiri, Nov. 19, 1908. {SR1P: 15.4}

“Suala kubwa lililo karibu sana litawang’oa wale ambao Mungu hajawateua, naye atakuwa na ukasisi safi, wa kweli, uliotakaswa kwa ajili ya mvua ya masika.” — B-55-1886. {SR1P: 16.1}

Kwa nini wadhambi wanaondolewa miongoni mwa wenye haki kabla ya nchi kuangazwa na utukufu wa malaika? — Kwa sababu “mdhambi mmoja anaweza kueneza giza ambalo litaitenga nuru ya Mungu kutoka kwa mkutano wote.” — Shuhuda, Gombo la 3, uk. 265. {SR1P: 16.2}

Mlolongo dhahiri wa ukweli hapa umeonyesha kwa mkataa kwamba sasa tuko katika “kazi ya kufunga kwa kanisa, wakati wa kutiwa muhuri watu mia moja na arobaini na nne elfu”; kwamba kutiwa muhuri, kutia alama, kuchekecha, kupepetwa, “kazi maalum,” “tukio muhimu,” “kazi ya kufunga,” na “utakaso,” yote yana matokeo sawa kwa kuwaangamiza ambao hawakutiwa muhuri na katika utakaso wa waliotiwa muhuri. Ndiyo, haya ndiyo maandalio kwa wakati wa taabu, Kilio Kikuu, kufunga kazi kwa ulimwengu. {SR1P: 16.3}

Kwa hiyo basi, hatimaye,ujumbe wa mwisho kwa ulimwengu unatangazwa na waaminifu peke yao, na watu wa Mungu wakati wa mapigo wako kando pekee yao bila wasio waaminifu miongoni mwao. {SR1P: 16.4}

Hivyo somo la 144,000, pamoja na masomo yake yanayohusiana yanaanza kuwa wazi,

16

Na usawa kwa lengo, linaonyesha kuwa wito wa saa ya kumi na moja kwa watumwa katika shamba la mizabibu la Bwana sasa unaendelea, na kwamba sasa ndio wakati wa “kujitahidi kwa nguvu zote ambazo Mungu ametupatia kuwa miongoni mwa watu 144,000.” – Mapitio na Kuhubiri, Machi 9, 1905. {SR1P: 16.5}

Na sasa, utambulisho huu wa 144,000 umesababisha utambulisho wa umati mkubwa (Ufu. 7: 9) kuwa karibu kama swali la kubishania. Kwa hivyo jukumu ambalo limechukuliwa katika mfululizo huu kutambua wa awali, malimbuko, inalazimisha jukumu la kipimo sawa kutambua la pili — {SR1P: 17.1}

MAVUNO YA PILI – UMATI MKUBWA.

“Baada ya hayo nikaona, na tazama, umati mkubwa, ambao hapana mtu awezaye kuuhesabu, watu wa kila taifa, na kabila, na jamaa, na lugha, wamesimama mbele ya kile kiti cha enzi, na mbele za Mwana-Kondoo, wamevikwa mavazi meupe, wana matawi ya mitende mikononi mwao “Ufu. 7: 9. {SR1P: 17.2}

Kuongoza kwa utambulisho wa umati huu mkubwa, Uvuvio umepeana vidokezi kadhaa, mojawapo ni uainishaji wa waliokombolewa wa vizazi vyote, kutoka kwa mauaji ya Abeli hadi mwisho wa kipindi cha majaribio. {SR1P: 17.3}

Kundi la 1: “Karibu na kiti cha enzi ni wale ambao walikuwa wenye bidii kwa kazi ya Shetani, lakini ambao walinyakuliwa, kama kinga kutoka motoni, wamemfuata Mwokozi wao kwa ibada ya ndani, na kujitolea sana.” {SR1P: 17.4}

17

Kundi la 2: ” Kisha ni wale waliokamilika kwa tabia ya Kikristo katikati ya uongo na ukafiri, wale ambao waliheshimu sheria ya Mungu wakati ulimwengu wa ukristo uliitangaza kuwa ni bure.” {SR1P: 18.1}

Kundi la 3: “Na mamilioni, wa vizazi vyote, waliouawa kwa ajili ya imani yao.” {SR1P: 18.2}

Kundi la 4: “Na nyuma ya hao ni ‘umati mkubwa, ambao hakuna mtu anayeweza kuuhesabu, wa mataifa yote, na jamaa, na watu, na lugha, … mbele ya kiti cha enzi, na mbele ya Mwana-Kondoo, wamevaa mavazi meupe, na mitende mikononi mwao.'”– Pambano Kuu, uk. 665. {SR1P: 18.3}

Hapa kuna swali la kubwa linaloshinikiza jibu: Kwa kuwa tunaonyeshwa waziwazi kwamba “umati mkubwa” (kundi la 4) ni kundi tofauti na kinga kilichonyakuliwa (kundi la 1), kutoka kwa walioshinda uongo na ukafiri (kikundi cha 2), na kutoka wafia dini wa nyakati zote (kikundi cha 3), ni jinsi gani “umati mkubwa” unaweza kujumuisha watakatifu wa vizazi vyote, wote waliokombolewa? — Ni dhahiri sana hawawezi. {SR1P: 18.4}

Kwa hiyo, iwapo sio kundi la 1, 2, au 3, basi wanaweza kuwa nani isipokuwa watakatifu walio hai. Na kwa vile wao sio 144,000, malimbuko wa walio hai wanapaswa, kuwa, mavuno ya pili. Hakika,

18

lazima yawepo mavuno ya pili, kwa maana neno “malimbuko” linaita mavuno ya pili kama vile neno “ufufuo wa kwanza” (Ufunuo 20: 6) linaita ufufuo wa pili, na kama neno “mauti ya pili” (Ufunuo 20:14) huitwa na mauti ya kwanza. {SR1P: 18.5}

Hata hivyo, swali lingine la fumbo linahitaji jibu: Ikiwa swali la Kristo, ” atakapokuja Mwana wa Adamu, je! Ataiona imani duniani?” (Luka 18: 8), pia katika maneno yake, “Msiogope, enyi kundi dogo” (Luka 12:32), yanamaanisha kwamba wachache wataokolewa na kuwapata wakiwa hai Atakapokuja kwa walio Wake, basi kunawezaje kuwapo na umati usioweza kuhesabika? — Ingawa kwa mtazamo wa kwanza swali linaleta shida, linatatuliwa haraka, na wazo kwamba wachache tu watakatifu walio hai watamaki “angani” linapelekea ufanisi wakati sababu inachukuliwa kwa ukweli kwamba “mavuno kweli ni mengi” (Mat. 9:37), kwamba ni “mwisho wa dunia” (Mat. 13:39), na kwamba neno “mavuno” lenyewe linaashiria mkusanyiko mkubwa zaidi kuliko “msimu wowote” uliotangulia. {SR1P: 19.1}

Zaidi ya hayo, swali, “Je, Atapata imani duniani?” sio kuuliza idadi ya watakatifu wakati huu wa kuja, lakini imani yenyewe bila kujali idadi. Na ikiwa atakapoonekana katika mawingu kuwapeleka nyumbani waaminifu, Asiipate imani duniani, basi nini kuhusu kanisa Lake linalosubiri, ambalo lapaswa kuwa bila doa au kunyanzi au kitu kingine chochote, kiwe kidogo au kikubwa? {SR1P: 19.2}

19

Wazi, kuja Kwake ilivyoandikwa katika Luka 18: 8 hakuwezi kuwa kwa 1 Wathesalonike 4:17, kuja kwake “katika mawingu.” Lakini kwaweza kuwa kwa Malaki 3: 2, 3, na Mathayo 13:30, 47-48, kuongoza kwa Mathayo 25: 31-33. Kuja kwake kwa hekalu lake ni kuwatenganisha wadhambi kutoka kwa watakatifu, kwenye mwanzo ambao Uvuvio unauliza, “Ni nani atakayestahimili siku ya kuja Kwake?” {SR1P: 20.1}

Na sasa, kwa maneno ya nabii mwenyewe, unakuja ushahidi wa jumla wa kukusanywa ndani umati mkubwa wa watakatifu walio hai katika “wakati wa mavuno:” {SR1P: 20.2}

“Nao [144,000 wanaookoka kuchinjwa au kuistahimili siku (Isaya 66:16) katika mtengo wa magugu kutoka kwa ngano (Mathayo 13:30, 41), mavuno ya malimbuko (Ufunuo 14: 4), “watumwa” wa Mungu (Ufunuo 7: 3)] watawaleta ndugu zenu wote kuwa sadaka kwa Bwana kutoka kwa mataifa yote juu ya farasi, na magari, na machela, na juu ya nyumbu na juu ya wanyama wepesi, hadi kwa mlima Wangu mtakatifu Yerusalemu, asema Bwana, kama vile wana wa Israeli wanavyoleta sadaka katika chombo safi ndani ya nyumba ya Bwana. ” Isa 66:20. {SR1P: 20.3}

“Ndipo kile chuma, na ule udongo, na ile shaba, na ile fedha, na ile dhahabu, vikavunjwa vipande vipande pamoja vikawa kama makapi ya viwanja vya kupepetea wakati wa hari; upepo ukavipeperusha hata visionekane mahali pake; na lile jiwe lililoipiga hiyo sanamu

20

likawa mlima mkubwa, likaijaza dunia yote.” Dan 2:35. {SR1P: 20.4}

“Na itakuwa katika siku za mwisho, mlima wa nyumba ya Bwana utawekwa imara juu ya milima, nao utainuliwa juu ya vilima; na mataifa yote yatauendea.” (SR1P: 21.1}

“Na mataifa mengi watakwenda na kusema, Njoni, twende juu mlimani kwa Bwana, nyumbani kwa Mungu wa Yakobo.” Isa 2: 2, 3. {SR1P: 21.2}

Kuuweka utabiri huu wa matengenezo kwa mtazamo wa kasi, hakuna mtu isipokuwa kipofu anaweza kushindwa kuona kwamba wazo la wachache tu kuokolewa ni ukweli tu wa idadi iliyookolewa wakati wa kipindi chochote cha ujumbe kabla ya mavuno; ingawa,sio, idadi iliyookolewa kipindi cha “mavuno” yenyewe. {SR1P: 21.3}

Umati mkubwa, mavuno ya pili ya watakatifu walio hai, zaidi ya hayo, wanapatikana pia wameonyeshwa katika onyesho fulani la mfano: {SR1P: 21.4}

(1) “Musa juu ya mlima wa ugeuzi alikuwa shahidi wa ushindi wa Kristo juu ya dhambi na kifo. Aliwakilisha wale watakaotoka kaburini wakati wa ufufuo wa wenye haki.” –Tumaini la Vizazi Vyote, uk. 421. {SR1P: 21.5}

(2) “Na makaburi yakafununuka; ikainuka miili mingi ya watakatifu waliolala; nao wakiisha kutoka makaburini mwao,baada ya kufufuka kwake, wakauingia mji mtakatifu, wakaonekana kwa

21

wengi .. “Mathayo 27:52, 53. (Angalia Maandishi ya Awali, uk. 184, na Tumaini la Vizazi Vyote, uk.786.) {SR1P: 21.6}

(3) “Eliya, aliye hamishwa akaenda mbinguni bila kuona kifo, aliwaakilisha wale watakaoishi duniani wakati wa ujio wa pili wa Kristo, na ambao watahamishwa, kwa kufumba na kufumbua jicho, kwa tarumbeta ya mwisho …. ‘”– Tumaini la Vizazi Vyote, uk. 421. {SR1P: 22.1}

(4) “Kama Enoku alivyo hamishwa mbinguni kabla ya dunia kuangamizwa kwa maji, hivyo wenye haki watakao kuwa hai watahamishwa kutoka duniani kabla ya kuangamizwa kwa moto.” – Manabii na Mababa, uk. 89. {SR1P: 22.2}

Katika vifungu hivi tunaonyeshwa mifano minne, wito kwa makundi mawili ya watakatifu waliofufuliwa na kwa makundi mawili ya watakatifu waliohamishwa. {SR1P: 22.3}

Kwa kuwa kuna mifano miwili ya walio hai, na kama Enoku mwenyewe sio wa uzao wa Yakobo, hawezi kwa mantiki hii kuwakilisha wazawa wa Yakobo, 144,000. Kwa kweli, jina Yakobo, au jina la heshima “Israeli,” halikuwahi kuwapo karne nyingi baada ya Enoki kuhamishwa. Kwa hiyo, Eliya, Mwisraeli asilia, kwa mantiki anawakilisha watu 144,000, na Enoku anawakilisha umati mkubwa, ambao wanatoka “mataifa yote, na jamaa, na watu, na lugha” (Ufu 7: 9), kwa sababu tangu kizazi chake alishuka mataifa yote. {SR1P: 22.4}

22

Na wito wa Bwana wao wa mwisho, basi, unaonekana katika ulinganifu mzuri wa kumbu kumbu za Injili — majeshi mawili ya waliofufuliwa na mifano yao, na majeshi mawili ya walio hamishwa na mifano yao. {SR1P: 23.1}

Oo. nini yasioelezeka kwa kuwa ni mema na mazuri — majeshi yenye utukufu ya waliokombolewa yanajitokeza katika malango ya utukufu wakienda taratibu chini ya njia za dhahabu za mitaa ya Paradiso, kwa sauti za nyimbo za mbinguni ambazo sikio la mwanadamu halijawahi kusikia — {SR1P : 23.2}

GWARIDE YA GWARIDE ZOTE! ANGALIA INAPITA:

Ya kwanza, mamilioni ya malaika wapambe walio wahudumia waliokombolewa kwa vizazi vyote. {SR1P: 23.3}

Ya pili, Musa, mwandishi wa kwanza aliyevuviwa, jemedari na kiongozi asiye na kifani miongoni mwa watu, amevaa vazi jeupe na  taji ya dhahabu inayong’aa, akiongoza upande wa mbele ya waliofufuliwa, wakiwa wamevaa nguo nyeupe na taji za dhahabu. {SR1P: 23.4}

Ya tatu, Abeli, wa kwanza miongoni mwa walioifia-imani, akiliongoza jeshi la walioifia-imani wa vizazi vyote, wote wamevikwa nguo nyeupe za utukufu na pindo za rangi nyekundu. {SR1P: 23.5}

Ya nne, Henoko, kichwa chake kilichokuwa kimezindikwa na shada nyeupe ya ajabu ya kupendeza inayong’aa zaidi kuliko jua, na mkononi mwake alikuwa na mtende wenye utukufu; waliomfuata umati mkubwa, wote wamevalia nguo safi nyeupe, na mitende mikononi mwao na taji za dhahabu  vichwani mwao. {SR1P: 23.6}

23

Ya tano, Eliya, mwaminifu, amevaa vazi jeupe nyeupe kutoka mabegani mwake hadi kwa miguu yake, akiwaongoza wale 144,000, ukuhani wa kifalme, wote kama yeye, wamevaa mavazi meupe. {SR1P: 24.1}

Ya sita, kina Adamu, “wana wa Mungu,” kutoka kwa dunia zote za ulimwengu wa Mungu, na baba Adamu mbele yao. {SR1P: 24.2}

Ya saba, Yesu, Mfalme wa wafalme na Bwana wa mabwana, Mkuu wa viumbe vyote, wa kwanza na wa mwisho, na pamoja Naye elfu kumi mara elfu na elfu elfu za malaika. {SR1P: 24.3}

Katika ulimwengu wote usio na mwisho wa umilele kamwe mbingu haijawahi kuona na kamwe haitaona tena kama hii — gwaride ya Mungu! {SR1P: 24.4}

Ndugu, Dada, ni wetu wa kuchagua aidha mavazi ya waliookolewa au sanda za waliopotea; ama kutembea pamoja na waliolipiwa deni katika meupe[mavazi] au kulala pamoja na waliohukumiwa katika meusi. {SR1P: 24.5}

Ikiwa ni kwa la mwisho — Mungu anakataa usikuwemo — basi malipo ya kuogofya lazima iwe, sio kifo cha kwanza tu, bali pia kifo cha pili, ambapo hakuna kufunguliwa. {SR1P: 24.6}

Ndio, litakuwa gani – kulia kwa sauti kubwa katika ziwa la moto usiozimika, au nyimbo za hali ya heri katika chemi chemi ya furaha isiyoweza kuzimwa? Sasa, kwa saa ya mwisho utahitaji kuchagua aidha kundi la

24

ESAU AU YAKOBO — LIPI? {SR1P: 24.7}

” Isaka akamwomba Bwana kwa ajili ya mke wake, maana alikuwa tasa. Naye Bwana akamitikia, na Rebeka mkewe akachukua mimba. Watoto wakashindana tumboni mwake. Naye akasema, Ikiwa ni hivi, kuishi kwanifaa nini? Akaenda kumwuliza Bwana. {SR1P: 25.1}

“Bwana akamwambia, Mataifa mawili yamo tumboni mwako, na kabila mbili za watu watafarakana tangu tumboni mwako. Kabila moja litakuwa hodari kuliko la pili, na mkubwa atamtumikia mdogo.” (SR1P: 25.2}

“Siku zake za kuzaa zilipotimia, tazama! Mapacha walikuwamo ndani mwake. Wa kwanza akatoka, naye alikuwa mwekundu mwili wote kama vazi la nywele. Wakamwita jina lake Esau. Baadaye ndugu yake akatoka, na mkono wake unamshika Esau kisigino. Akaitwa jina lake Yakobo. ” Mwa. 25: 21-26. {SR1P: 25.3}

Katika kuzaliwa kwa ajabu na maisha ya Esau na Yakobo, kuna elimu ya mifano na ubunifu usiokosea wa Mungu. Makosa ya ajabu kwa uzoefu wa familia hii kwa uwazi umeigizwa kwa udogo uzoefu ambao kanisa la Mungu lingeweza kupitia siku moja. Rebeka mwenyewe alikuwa amefahamishwa bara bara ukweli huu wakati “Bwana akamwambia, Mataifa mawili yamo tumboni mwako, na kabila mbili za watu watafarakana tangu tumboni mwako. Kabila moja litakuwa hodari kuliko la pili, Na mkubwa atamtumikia mdogo. ” Mwanzo 25:23. {SR1P: 25.4}

Je, ni elimu gani ya mifano katika kupiga piga kwa maisha haya ya kuigiza? — Kimsingi kile ambacho kinasimama katika ufafanuzi wa Paulo wa usawa

25

Mkali wa tamasha ya Hajira na Ishmaeli, Sara na Isaka. Uvuvio unafichua ukweli kwamba jozi ya awali inawakilisha Kanisa la Agano la Kale na waumini wake, Wayahudi; na jozi ya mwisho inawakilisha Kanisa la Agano Jipya na waumini wake, Wakristo (Wagalatia 4: 22-31). {SR1P: 25.5}

Vivyo hivyo, ingawa katika awamu nyingine, Rebeka pia anawakilisha kanisa, wakati Esau na Yakobo wanawakilisha uzao wake, waumini. Na kwa kuwa hao wawili walishindana ndani ya mama kabla hawajazaliwa (kuokolewa), somo muhimu ni kwamba wakati kanisa linapokuwa lina utungu na watoto wake kabla ya kuwazaa, kupata kuzaliwa mara ya pili (Yohana 3: 3) na kuongozwa hadi katika ufalme, watashindana ndani. Kwa hiyo, Rebeka kuwabeba wana wawili ni kidokezo kwamba kanisa linabeba ndani yake makundi mawili ya watu – akina Esau na Yakobo. {SR1P: 26.1}

“Kuna mivuto miwili hasimu,” unathibitisha Uvuvio, “inayoendelea kuvutana juu ya washiriki wa kanisa. Mvuto mmoja unafanya kazi kwa ajili ya utakaso wa kanisa, na mwingine kwa ajili ya kuwapotosha watu wa Mungu.” – Shuhuda kwa Wachungaji, uk. 46. {SR1P: 26.2}

Namna ambayo Esau na Yakobo walizaliwa — Yakobo akimfuata Esau akiwa amemshika kisigino — ina umuhimu sana: Esau akiwa ametagulia inamfanya kuwa aina ya viongozi wanaomiliki tabia kama yake, na Yakobo akiwa yuamfuata inamfanya aina ya wafuasi

26

wanaomiliki tabia yake. Mfano huu bila kukosea unaashiria pia, kwamba mmoja unawakilisha daraja la watu linalotangulia lingine katika ushirika wa kanisa. Kusema kwa mapana, kwa hivyo, wote pamoja wanawakilisha wagombea wa urithi wa ukasisi na waumini kwa mtiririko huo. {SR1P: 26.3}

Pia kuna umuhimu wa kawaida kwa ukweli zaidi kwamba Esau alizaliwa na nywele na Yakobo laini. Uwazi huu wa ajabu wa nje husababisha dhahiri aina fulani ya utambulisho unaoonekana wazi kwa makundi mawili yaliyo kwa mfano. {SR1P: 27.1}

Mungu alimchagua mwanamume kuongoza na mwanamke kufuata, na hivyo Aliumba mwanamume mwenye nywele nyingi na mwanamke mwororo. Alama hizi za Mungu za kutofautisha zinadhibitisha Esau kuwa daraja analowakilisha wanamiliki vifaa vya asili kwa uongozi, wakati Yakobo na daraja analowakilisha hawana. Mbali na hilo, akiwa mzawa wa kwanza, Esau kwa haki ya kuzaliwa angekuwa kuhani wa familia. Kwa uzao wake wangekuja mababa wa kabila kumi na mbili, manabii, wakuu, wafalme wa Israeli, na hata Mfalme wa wafalme Mwenyewe, Mwokozi wa ulimwengu. {SR1P: 27.2}

Lakini hamu, matamanio, na malengo ya Esau na Yakobo, yalikinzana na nafasi zao za urithi. Esau hakuvutiwa na umuhimu maalum katika sehemu ya kazi ambayo haki yake ya kuzaliwa iliruhusu, wakati ambapo Yakobo aliitamani. Akizuiwa, hata hivyo, kwa sheria ya urithi

27

kuimiliki sehemu ya Esau, Yakobo kwa hamu kupita kiasi kwa ajili ya urithi wa mzawa wa kwanza aliweza kuununua kwa wakati ufaao. Kisha ili kupokea baraka za baba yake, aliukubali ushirika wa mama yake ili kuupata kwa udanganyifu. {SR1P: 27.3}

Somo la kutisha linaonekana kwa machungu: daraja la Esau ambao huhudhuria kazi za ofisi zao kwa kiwango cha chini ya madai ya utakatifu wake, kwa kutojali huiacha iponyoke kutoka mikononi mwao na kuingia mikononi mwa daraja la Yakobo wanaoidaka kwa hamu, ambao kwa kweli hushukuru na kuyathamini majukumu yake, lakini ambao, sio viongozi asili kwa kuzaliwa , wanapaswa kupata vifaa vya ofisi takatifu kwa kupitia mafunzo ya kuwatia adabu ya uzoefu fulani wa kuipima nafsi jinsi kivuli cha mafunzo ya Yakobo alipokuwa mkimbizi kutoka nyumbani. Hivyo katika kura yao ya maongozi, hutupwa nje ya kanisa na ndugu zao wakubwa, kama vile Yakobo alifukuzwa nyumbani na ndugu yake mkubwa, kwa sababu ya bidii yao kwa utumishi wa Mungu, wanapata mafunzo kwa kazi ya upendeleo wao ambayo itakuwa yao . {SR1P: 28.1}

Ni baraka ya thamani isiyoweza kukadiriwa ambayo mzaliwa wa kwanza, ukasisi wa sasa, wanapoteza! Wao ni upendeleo usio na kifani kusimama juu ya Mlima Sayuni na Mwana Kondoo na wa kuzalisha raia wa Ufalme siku za mwisho, kuongoza hadi kwa Ufalme wenyewe, kuuleta ujio wa pili wa Kristo, na hatimaye kuliongoza jeshi la waliokombolewa hadi Kanaani ya mbinguni, katika ulimwengu wa

28

utukufu usio na mwisho. Lakini wao karibu wanapoteza — janga la majanga! {SR1P: 28.2}

Kwa baadhi ya mchanganyiko wa kutamanisha wa ndengu wanaiacha iwaponyoke fursa hii ya mwenye enzi! La kusikitisha, hata sasa wanaruhusu kuenea kwa daraja la Yakobo, washirika waaminifu, wale 144,000 watumwa wa Mungu wa baadaye (Ufunuo 7:3; 5:10, Shuhuda, Gombo la 5, uk. 475, 476) {SR1P : 29.1}

“Jinsi Esau alipozinduka kuona upumbavu wake wa kubadilisha bila kufikiri alipokuwa amechelewa sana kurudisha alichokuwa amepoteza, ndivyo itakavyokuwa siku ya Mungu kwa wale ambao wameuza urithi wao wa kwenda mbinguni kwa ajili ya kutosheleza tamaa.” – Wazee wa Imani na Manabii, uk. 182. (Soma Pia Shuhuda, Gombo la 2, uk. 38, 39.) {SR1P: 29.2}

“Wandugu,” miaka mingi iliyopita aliteta Roho wa Kweli pamoja na mzaliwa wa kwanza kwa kuwaonya juu ya hatari yao ya kupoteza haki yao ya uzawa, “ikiwa mnaendelea kuwa walegevu, wa kidunia, wabinafsi jinsi ambavyo mmekuwa, Mungu hakika atawapita, na kuwachukua wale wasiojijali sana, wasio na tamaa ya heshima ya kidunia, na ambao hawatasita kwenda, alivyofanya Mwalimu wao, nje ya kambi, akibeba shutuma. Kazi itapeanwa kwa wale watakaoichukua, wanaoithamini, ambao hufuma kanuni zake katika uzoefu wao wa kila siku. Mungu atawachagua watu wanyenyekevu, wanaotafuta kulitukuza jina lake na kuendeleza kazi yake badala ya kujiheshimu na kujiendeleza wao wenyewe. Atawainua watu ambao hawana hekima nyingi ya kidunia, ila ambao

29

wameungana naye, na wanaotafuta nguvu na ushauri kutoka juu. “– Shuhuda, Gombo la 5, uk. 461. {SR1P: 29.3}

“Mwito kwa kazi hii kuu na ya uchaji uliwasilishwa kwa watu wasomi na wenye nyadhifa; kama hili lingekuwa dogo machoni mwao wenyewe, na kumtegemea kikamilifu Bwana, angaliwaheshimu kwa kuinua kiwango Chake katika shangwe hadi kwa ushindi…. {SR1P: 30.1}

“Mungu atafanya kazi katika siku zetu ambayo ni wachache huitazamia. Atawaamsha na kuwainua miongoni mwetu wale ambao wamefundishwa na kupakwa mafuta ya Roho Wake, badala ya kwa mafunzo ya nje ya taasisi za kisayansi.” — Shuhuda, Gombo la 5, uk. 82. {SR1P: 30.2}

“Hapa [Ezek. 9:5,6] tunaona kwamba kanisa — hekalu la Bwana — lilikuwa la kwanza kuhisi pigo la ghadhabu ya Mungu. Wazee, ambao Mungu alikuwa amewapa nuru kubwa, na ambao walisimama kama walezi wa masilahi ya kiroho ya watu, walikuwa wameisaliti imani yao. Walikuwa wamechukua nafasi kwamba hatuhitaji kutazamia udhihirisho wa nguvu za Mungu kama ilivyokuwa zamani. Nyakati zimebadilika. Maneno haya yanaimarisha kutoamini kwao, wao husema, Bwana hatatenda mema, wala hatatenda mabaya.” Yeye ni mwenye rehema sana kuwaadhibu watu wake kwa hukumu. Hivyo amani na usalama ni kilio kutoka kwa watu ambao kamwe hawatapaza sauti zao kama tarumbeta kuwaonyesha watu wa Mungu makosa yao na nyumba ya Yakobo

30

dhambi zao. Mbwa bubu hawa, ambao hawangeweza kubweka, ndio wanaohisi kisasi walichostahili cha Mungu aliyeudhiwa. Watu, wajakazi, na watoto wadogo, wote waangamia pamoja. “– Shuhuda, Gombo la 5, uk. 211. {SR1P: 30.3}

Sasa jinsi awamu nyingi za hii elimu ya mifano inapozunguka kwa sura yake ijayo, Esau na Yakobo wanaonekana katika uwakilishi zaidi wa madaraja mawili ya dhambi: Esau, kwa rangi ya ngozi yake na kwa maana ya jina lake baada ya kubadilishwa kutoka kwa Esau hadi Edomu; Yakobo, kwa maana ya jina lake kabla ya kubadilishwa kutoka Yakobo hadi Israeli. {SR1P: 31.1}

Ajabu kabisa, kama vile rangi ya ngozi ya Esau ilikuwa nyekundu, ndivyo ilivyokuwa maana ya jina lake jipya, Edomu. Na kama alivyoshindwa kuthamini na kuitunza zawadi ya wa-baba, kamwe kutotimiza maana ya jina lake la kuzaliwa (“yeye anayekamilisha”), inaonekana kwamba jina lake jipya, tofauti na jina jipya la Yakobo, linaashiria, si maendeleo, ila kushindwa kuendeleza, aliendelea bila kuzizuia njia zake za kimwili – akitulia katika tabia ya kuzaliwa kwake, “nyekundu,”. Kwa hivyo, daraja la viongozi analoashiria watapoteza, kamwe hawataikamilisha kazi aliyowateulia Mungu, na kamwe kutobadilishwa kutoka kwa wadhambi kuwa watakatifu! Kupoteza kwa jinsi gani! {SR1P: 31.2}

Sivyo, hata hivyo, na daraja la Yakobo. Kama vile asili wao, ambaye aliwatunza kondoo, kwa uangalifu aliifanya kazi yake, na kwa shangwe akaushinda utu wake wa

31

kutamani, na jina lake lililobadilishwa kutoka kwa Yakobo (mnyakuzi) kwa Israeli (mshindi na hivyo Mwana wa Mfalme), hivyo pia, mwishowe, wanapoushinda utu wao wa asili ya kimwili, majina yao yamebadilishwa kutoka kwa wa-Yakobo hadi Waisraeli, kutoka kwa wanyakuzi hadi washindi, — kutoka kwa watumwa wa ubinafsi hadi watumwa wa Mungu, kutoka kwa Wakristo wa-Laodekia wa kawaida hadi wakuu waliokwezwa juu ya Mlima Sayuni. Hivyo, kwa haki yao wenyewe wa-Yakobo akisi wanakuwa Waisraeli akisi, kwa kujipatia haki ya uzawa wa ukuhani wanakuwa wakamilishaji wa kazi ya injili na wakiwa watumishi wa Mungu wanasimama juu ya Mlima Sayuni na Mwana Kondoo. {SR1P: 31.3}

Kwa hiyo inaonekana kwamba madaraja yote, kama mifano yao, majina yao yamebadilishwa: daraja la Yakobo, kwa sababu wanathamini, kama vile Yakobo alivyokuwa haki ya kuzaliwa isiyoharibika; daraja la Esau, kwa sababu wanadharau, kama vile Esau, haki ya kuzaliwa isiyoharibika, na kuthamini utukufu unaoharibika wa maisha haya. Mmoja ana hisia imara, sahihi ya maadili ya maisha; mwingine, hisia butu, isiyo sahihi. {SR1P: 32.1}

Na ingawa Yakobo alizikosa sifa za asili za kutekeleza majukumu ya ofisi yake, ukosefu huo uliondolewa zaidi na bidii yake kubwa. Kwa hiyo, bila kujali, ni ukubwa au udogo gani wa talanta asili na kupata mafunzo ambayo mtu anaweza kuyapata kwa nafasi yoyote, hataweza kuyapata mafanikio kwayo isipokuwa awekeze ndani yake kila kitu alicho nacho — auelekeze moyo wote na nafsi yake ndani. Hii ni mojawapo wa sheria ya maisha isiyoweza kutanguliwa,

32

na inapaswa kukumbukwa na wote kwamba inathibiti ustawi katika kila nyanja za jitihada ikiwa ni kwa anayeamini au asiyeamini. {SR1P: 32.2}

Kwa kuwa hasara ya mtu daima ni faida ya mtu mwingine, kama vile hasara ya Esau ilikuwa ni faida ya Yakobo, hivyo kwa kutisha, kusivyoweza kurekebishwa, na isiyo na thamani hasara kwa daraja la Esau itakuwa ni faida ya utukufu wa milele kwa daraja la Yakobo. {SR1P: 33.1}

Katika majuto ya kujisaga juu ya kutambua hasara yake isiyoweza kukadiriwa, Esau ” alikataliwa (maana hakuona nafasi ya kutubu), ijapokuwa aliitafuta sana kwa machozi. ” Heb. 12:17. Hatma yake isiyotanguka inaashiria kile kitakacho wapata wote ambao kwa matendo yao wanajiweka wenyewe katika daraja la Esau. {SR1P: 33.2}

Katika mkondo wa elimu hii ya mifano juu ya somo, sasa tunaelekezwa kwa na kipengele chake cha kilele

NDOTO YA YAKOBO. {SR1P: 33.3}

Usiku wa kwanza wa kukimbia kwake kutoka kwa hasira ya kuua ya Esau, Yakobo, akitumia jiwe kama mto, akalala kupumzika: {SR1P: 33.4}

” Akaota ndoto; na tazama, ngazi imesimamishwa juu ya nchi, na ncha yake yafika mbinguni. Tena, tazama, malaika wa Mungu wanapanda, na kushuka juu yake.” Mwanzo 28:12. {SR1P: 33.5}

Ndoto ina maana gani? – Ikiwa ni upande mwingine wa hiyo elimu ya mifano, ni lazima iwe inaonya mbele tukio la kustahili kukumbukwa kuwafikia watu wa Mungu, wana Yakobo. {SR1P: 33.6}

33

Kwa kuwa ngazi hiyo, mwisho mmoja duniani na mwingine mbinguni, ni mfano wa Kristo (Mababu na Manabii, uk. 184), na tangu malaika wakipanda na kushuka chini ya ngazi ni wajumbe Wake (Pambano Kuu, uk. 512) , yote inaashiria kuwa Kristo ataweka kupitia kwake Mwenyewe mawasiliano ya uhakika na thabiti kati ya mbingu na dunia. {SR1P: 34.1}

” Tena itakuwa siku hiyo, mimi nitaitika, asema Bwana; nitaziitikia mbingu, nazo zitaiitikia nchi;” Hos. 2:21 {SR1P: 34.2}

Hatua inayofuata katika elimu ya mifano inazingatia – {SR1P: 34.3}

KINA MAMA ZA WANA WA YAKOBO

Pamoja na njia ya kihistoria ya awamu nyingi za elimu ya mifano, sasa katika mawazo tunamfuata Yakobo Padan-Aramu. Huko alijitwalia wake wanne, Lea na Raeli, binti za Labani; kisha Zilpa na Bilha, wajakazi wao husika. Hawa wanne walikuwa mama za wana kumi na wawili wa Yakobo, ambao pia walikuwa baba wa kabila kumi na mbili za Israeli. {SR1P: 34.4}

Katika mfano huu unaoendelea wa Israeli wa kiroho, mmoja tu kati ya wanne, Leah, kisheria alikuwa mke wa Yakobo. Kwa hivyo, yeye tu ndiye anayeweza kuwakilisha kanisa la kweli na la kisheria — ambalo liliasisiwa huko Yerusalemu na ufalme wa kabila kumi na mbili, na ambao hatimaye ilibadilika kuwa Kanisa la Kikristo. {SR1P: 34.5}

34

Raeli lazima awakilishe kanisa dada –lililoasisiwa Samaria kwa ufalme wa kabila kumi na kutawanywa nao kati ya Mataifa. {SR1P: 35.1}

Zilipa na Bilha, wakiwa “wageni” na watumishi kwa Leah na Rachel, lazima wayawakilishe makanisa ya baadaye ya asili ya Mataifa. {SR1P: 35.2}

Kutoka kwa safu hizi nne huja wazawa wa Israeli akisi. Na cha kweli katika uzao wa kimwili lazima kuwa kweli pia katika uzao wa kiroho. Kwa hivyo, wakati wa akisi, kama wa mfano, makabila kumi na mawili huja kwa njia ya mama wote wa Israeli na wa Mataifa, lakini wanazaliwa na baba mmoja yule — Mwisraeli. {SR1P: 35.3}

Walitawanywa na Mungu katika mataifa yote, Wote Yuda (ufalme wa kabila mbili) na Israeli (ufalme wa kabila kumi) walimezwa nayo. Kisha, pia, Kanisa la Kikristo, lenyewe likiwa chipukizi la Kanisa la Kiyahudi (wafuasi wa Kristo na mitume, pamoja na waongofu wa kanisa la kwanza, walikuwa Wayahudi asilia, kumbuka), waliacha jina la heshima la “Agano la Kale” jina la “Wayahudi” wakati lilipochukua jina la heshima la Agano Jipya “Wakristo.” Kisha polepole lilipoteza majani yake ya Wayahudi katikati ya majani ya pandikizi la Mataifa lililoingizwa. {SR1P: 35.4}

Sasa tunapoiacha awamu hii ya elimu ya mifano, tunaingia ya

35

SAFARI YA YAKOBO KURUDI NYUMBANI. {SR1P: 35.5}

Baada ya miaka ishirini ya utumishi wa uaminifu huko Padan – Aramu, kwa uajiri mkali, wa kupunja wa Labani, mjomba wake, Yakobo hatimaye akaugeuza uso wake na hatua zake kuelekea nyumbani kurudi kwa nyumba ya baba yake katika nchi ya ahadi. {SR1P: 36.1}

Lakini taabu ikampata. Alipokuwa akishikana na hofu yake kuhusu matokeo ya mkutano wake uliokuwa ukikaribia na Esau  na mtu mmoja akashindana naye hata alfajiri.” Mwanzo 32:24 {SR1P: 36.2}

Hapa alilala mtu Yakobo na akainuka mtu Israeli, akiashiria uzoefu wa kuteseka kwa uchungu ambao wazawa wake wanapaswa kupitia kwa ushindi, pia, kupokea jina jipya, kutoka kwa wana wa Yakobo kuwa wana wa Mungu, Waisraeli kweli kweli. Wakisha pata ushindi juu ya mtihani huu, “wakati wa taabu ya Yakobo,” watafika nyumbani, nchi ya ahadi — mwisho wa furaha wa safari yao ndefu na ya taabu. {SR1P: 36.3}

Katika kipindi hiki cha kutahiniwa na kupimwa Roho ya Unabii inasema: “Amri ilitangazwa kuwaua watakatifu, iliyowasababisha kulia mchana na usiku kwa ajili ya ukombozi. Huu ulikuwa ni wakati wa taabu ya Yakobo” — Maandishi ya Awali, uk. 36, 37. (Tazama pia; Mababu na Manabii, uk. 202, 203.) {SR1P: 36.4}

Sasa, kama kustaafu kwa Yakobo kutoka utumwa wake huko Padan – Aramu kunatamatika na kurudi kwake

36

nyumbani, elimu ya mifano inaendelea na —

ISRAELI WAENDA MISRI {SR1P: 36.5}

Kwamba Biblia huufunua ukweli wake mwingi ajabu kwa njia mbalimbali — kwa hesabu, kwa mifano na takwimu, katika mithali na mafumbo, katika ndoto na maono, katika taipolojia na majaaliwa ya Mungu — zinajulikana zaidi katika uzoefu wa kipekee wa Israeli asilia kuingia Misri. Katika hili kila mwanafunzi wa Biblia mwenye ufahamu anaelewa, si tu tukio la kuigiza, bali mpango wa kusudi kwa mkono wa Mwenyezi Mungu na majaaliwa yake. Hakika, Yusufu mwenyewe, mkuu katika tamasha kubwa, anakiri hivi: “Mungu alinipeleka mbele yenu,” anasema, “kuhifadhi maisha ya watu.” Mwanzo 45: 5. {SR1P: 37.1}

Kwa kulitambua hili, Paulo katika maongozi ya Uvuvio anaelezea kuwa ” Basi mambo hayo yaliwapata wao kwa jinsi ya mifano, yakaandikwa ili kutuonya sisi, tuliofikiliwa na miisho ya zamani.” 1 Wakor. 10:11. Kwa hivyo ni muhimu sana, basi, tuchunguze kabisa, tuelewe, na kuuthamini mfano huu wa ajabu ambao Mungu alifanya kwa ajili ya maslahi yetu. {SR1P: 37.2}

Kuanzia na uzoefu wa Yakobo, tunayaona majaaliwa ya Mungu yakitukia kuyaelekeza maisha yake wakati wote, hata kutangulia kumpenda Yusufu zaidi kuliko watoto wengine (Mwanzo 37: 2-11) — sababu ya haraka ya wivu wao na kumuondoa awe mbali

37

kijana. Hivyo, miaka kabla wao kuondoka Kanaani kwenda Misri, Mungu katika majaaliwa yake alimtuma Yusufu, jinsi mwenyewe baadaye alivyogundua, kuiandaa njia yao. Kisha kwa kuileta miaka saba ya chakula, ikifuatwa na miaka saba ya njaa katika nchi yote,

Mwenyezi Mungu halikadhalika aliumba hali zaidi ili kuleta nyumba nzima ya Israeli chini katika Misri. Na hapo ndipo baadaye walipunguzwa mpaka utumwa, ambayo iliwagharimu magumu yasiyoelezeka na mauaji ya idadi kubwa ya watoto wao wa kiume. {SR1P: 37.3}

Kutoka kwa kuuza kwa Yosefu katika utumwa, hadi kuuawa kwa mzaliwa wa kwanza huko Misri – mlolongo wa mabadiliko ya kusikitisha ya aina gani! Kwa nini ilikuwa lazima kwamba nyumba ya Yakobo ipitie uzoefu wa utakaso vile? Kwa nini? – Kwa sababu “haya yote,” tena unakumbusha Uvuvio, “yalitokea kwao kwa mifano: na yameandikwa kwa onyo kwetu sisi, ambao miisho ya ulimwengu imewadia.” 1 Kor. 10:11. {SR1P: 38.1}

Kwa hekima Yake isiyofikika, Mungu aliwaruhusu wana wa Yakobo waende kwa njia ngumu, ili waweze kuwa mfano, mfano, somo kuu la kuokoa siku atakapoweka “mkono wake tena mara ya pili ili kuwarudisha mabaki ya watu wake, watakaoachwa, kutoka Ashuru, na kutoka Misri, na kutoka Pathros, na kutoka Kushi, na kutoka Elamu, na kutoka Shinari, na kutoka Hamathi, na kutoka visiwa vya bahari. Isa. 11:11. {SR1P: 38.2}
38
Kwetu sisi, basi limetwikwa jukumu la, kwa umakini, busara, na kwa uaminifu kufanya vishindo vyao kuwa mawe ya kukanyagia kufikia ushindi. Ajabu kweli kujua kwamba njia yetu imeorodheshwa karne nyingi mapema! {SR1P: 39.1}

Kama sehemu muhimu ya “mfano” hizi za ubunifu, Mbuni wao alimkuza Joseph kwenye kiti cha enzi cha Wamisri kwa kumwezesha kutabiri miaka saba ya mengi na miaka saba ya njaa, ambayo–

MUNGU ALIULISHA ULIMWENGU WA KITAMBO KWA MAHINDI JINSI ANAVYOULISHA ULIMWENGU WA SASA NA UKWELI. {SR1P: 39.2}

“Na ikaja kuwa… kwamba Farao aliota: na, tazama, amesimama kandoni mwa mto. Na, tazama, wakapanda kutoka mtoni ng’ombe saba wazuri na wanono; na wakajilisha manyasini. {SR1P: 39.3}

Na, tazama, ng’ombe saba wengine wakapanda nyuma yao kutoka mtoni, wabaya na wamekonda; na wakasimama karibu na wale ng’ombe wengine ukingoni mwa mto. {SR1P: 39.4}

Kisha wale ng’ombe wabaya na waliokonda wakawala wale ng’ombe saba wazuri na wanono. Basi Farao akaamka… {SR1P: 39.5}

“Ikawa asubuhi, roho yake ikafadhaika, akawatuma wachawi wote wa Misri, na wenye hekima wote; Farao akawaambia ndoto yake, lakini hakuna aliyeweza kutafsiri kwao. Farao …. {SR1P: 39.6}

39

” Ndipo Farao akapeleka watu, akamwita Yusufu, wakamleta upesi kutoka gerezani. Akanyoa, akabadili nguo zake, na kuingia kwa Farao.

Farao akamwambia Yusufu, Nimeota ndoto, wala hakuna awezaye kunifasiria; nami nimesikia habari zako, ya kwamba, usikiapo ndoto, waweza kuifasiri…..  [Kisha Farao akamwelezea Yusufu ndoto]. {SR1P: 39.7}

” Yusufu akamjibu Farao,… Mungu amemwonyesha Farao atakayoyafanya hivi karibu.

Wale ng’ombe saba wema ni miaka saba…. Na wale ng’ombe saba, dhaifu, wabaya, waliopanda baada yao, ni miaka saba … {SR1P: 40.1}

Tazama, miaka saba ya shibe inakuja, katika nchi yote ya Misri…. Wala shibe ile haitajulikana katika nchi kwa sababu ya njaa inayokuja baadaye, maana itakuwa nzito sana …. Farao akamwambia Yusufu …. Tazama, nimekuweka juu ya nchi yote ya Misri…. {SR1P: 40.2}

“Ikawa katika miaka ile saba ya shibe, nchi ikazaa kwa wingi.” Akakusanya chakula chote cha miaka ile saba katika nchi ya Misri. Akaweka chakula katika miji; chakula cha mashamba yaliyouzunguka kila mji, akakiweka ndani yake.

Yusufu akakusanya nafaka kama mchanga wa pwani, nyingi mno, hata akaacha kuhesabu, maana ilikuwa haina hesabu.” Mwanzo 41: 1-49. {SR1P: 40.3}

Nini maana ya kiroho ya somo hili la kielezo? — Hii tu: kwa kuwa katika Maandiko Matakatifu nambari saba daima huashiria ukamilifu wa aina inayowakilishwa, miaka saba ya wingi na miaka saba ya njaa inaashiria moja moja kwa vipindi viwili vinavyofuatana na kamili. {SR1P: 40.4}

Cha kwanza ni kwa muujiza kuzalisha kwa wingi sana sio tu kwa wakati uliopo awali lakini kwa wakati utakaokuja, na cha pili ni ki-muujiza kuzalisha kidogo sana, kama si chochote. {SR1P: 40.5}

Na ni nini kingine katika nyanja ya mifano ambacho “nafaka” iliyohifadhiwa inawakilisha ila chakula cha kiroho, Neno la Mungu lililohifadhiwa katika Biblia (Zaburi 78:24)? Kwa hiyo, mfano unaonyesha kwamba vitabu sitini na sita vya Biblia ni maghala ya Mungu ya Ukweli, na kwamba yalijazwa chakula cha kuilisha n Ya kwanza ni kwa muujiza kuzalisha kwa wingi sana si kwa wakati tu sasa lakini kwa wakati ujao, na pili ni ajabu kwa kuzalisha kidogo sana, kama si chochote. {SR1P: 40.5}

40

Na ni nini kingine chochote ambacho kinaweza kuhifadhiwa “nafaka” bali chakula cha kiroho, Neno la Mungu limehifadhiwa katika Biblia (Zaburi 78:24)? Kwa hiyo, mfano huo unaonyesha kwamba vitabu sitini na sita vya Biblia ni maghala ya Mungu ya Haki, na kwamba vilikuwa vimejaa chakula cha nafsi wakati wa kipindi cha manabii — kipindi akisi cha wingi — kuyahifadhi maisha ya kiroho wakati huo na wakati wa kipindi kinachofuata, kipindi cha injili, kipindi akisi cha njaa. {SR1P: 41.1}

Kwa hiyo, Ukweli uliohifadhiwa ambao utaendeleza kila kizazi katika vipindi vya Agano la Kale na Jipya ni maandishi ya manabii yanayofunuliwa kama mafunuo ya wakati wake katika kipindi chote cha injili. Na hivyo ni jinsi kila mwanafunzi wa Biblia anavyojua, ukweli halisi. {SR1P: 41.2}

Wazi kabisa, somo kubwa la elimu ya mifano ni kwamba katika yapata miaka mingi ambayo imetokea tangu Biblia ilipoandikwa, na ambapo hakujakuwapo chakula cha kiroho cha ziada, lazima kingenunuliwa kutoka hifadhi ya kale, Ghala kubwa la Bwana, Biblia, na bado kinapaswa kununuliwa kutoka Mle hata sasa kama awali, kwa njia pekee ya wasambazaji Wake Aliowateua, wafafanusi Wake Waliovuviwa. {SR1P: 41.3}

41

“Haya, kila aonaye kiu, njoni majini,” sasa anaita Roho “ Naye asiye na fedha; njoni, nunueni mle; Naam, njoni, nunueni divai na maziwa, Bila fedha na bila thamani.” Isa. 55: 1. {SR1P: 41.4}

Mfano huo bila kukosa unaonyesha kwamba kama ilivyokuwa siku ya Yosefu hakuna mtu angeweza kujisaidia kwa nafaka, ila angeweza kuipata tu kupitia watumishi waliochaguliwa na Yusufu, kwa hivyo hata siku zetu yule tu hutoa “chakula kwa majira yake,” ni Mwokozi kupitia watumishi Wake aliowaliowateua. Ni kupitia kwao tu Yeye huufunua, kuutafsiri, na kuusambaza ukweli wa wakati. {SR1P: 42.1}

Hivi ni kwamba ingawa sasa tuko katika miaka akisi ya njaa, kipindi ambacho hakuna ufunuo wa moja kwa moja kutoka Mbinguni, hakutakuwapo na ukosefu wa chakula, ukweli wa sasa. Kuna cha kutosha kilichohifadhiwa katika Biblia kutuwezesha kupita miaka ya njaa ikiwa tu tunatuma ombi letu kwa wasambazaji wake aliowachagua. Hili ndilo somo la maana sana, la haraka, na linalohitajika zaidi kufundishwa katika mfano huu wa majaaliwa ya Mungu kwa ajili ya watu wake. {SR1P: 42.2}

Ukweli kwamba nafaka ni mfano wa Neno la Muumba, na kwamba maghala ya kuhifadhi ni mfano wa vitabu vya Biblia, humfanya Yusufu kuwa mfano wa Kristo, ambaye huthibiti Maandiko na ambaye peke Yake huusambaza Ukweli kwa wale wanaolipa gharama — wanaoacha maelekeo yao ya kutenda maovu waliorithi na walioyakuza (Mafunzo ya Kristo kwa Mifano, uk. 330; Manabii na Wafalme, uk. 97.) {SR1P: 42.3}

Hivyo ni kwamba kama Yusufu alivyokuwa mtawala mwenza na Farao, Kristo ni Mtawala mwenza na

42

Mungu: na kama vile Yusufu, mwokozi wa kimwili wa ulimwengu, alihifadhi nafaka kwenye maghala ya Misri, Kristo, Mwokozi wa kiroho wa ulimwengu, aliuhifadhi Ukweli katika vitabu vya Biblia. Kwa hiyo, heshima ambayo Farao alimpa Yusufu ilionyesha mbele heshima ambayo Mwalimu Mkuu wa Elimu ya Mifano alimpa Kristo. {SR1P: 42.4}

Baada ya kutayarisha njia, Yosefu aliwaita baba yake, ndugu zake, na jamaa zao: {SR1P: 43.1}

” Akasafiri Israeli, pamoja na yote aliyokuwa nayo, akaja Beer-sheba, akamchinjia sadaka Mungu wa Isaka babaye. (SR1P: 43.2}

” Mungu akanena na Israeli katika ndoto ya usiku, akasema, Yakobo, Yakobo. Akasema, Mimi hapa. ” (SR1P: 43.3}

” Akasema, Mimi ni Mungu, Mungu wa baba yako, usiogope kushuka mpaka Misri;… {SR1P: 43.4}

Farao akamwambia Yusufu, akisema, Baba yako na ndugu zako wamekujia; nchi ya Misri iko mbele yako, palipo pema pa nchi uwakalishe baba yako na ndugu zako; na wakae katika nchi ya Gosheni. {SR1P: 43.5}

” Naye Yusufu akawalisha babaye na nduguze na nyumba yote ya babaye…. Israeli akakaa katika nchi ya Misri, katika nchi ya Gosheni. Wakapata mali humo, wakaongezeka na kuzidi sana.” Mwanzo 46: 1-3; 47: 5, 6, 12, 27. {SR1P: 43.6}

Nchi ya Goshen, ambayo Mungu alimwelekeza Yusufu kuwapa Israeli kwa kuhama kutoka nchi yao, ilikuwa bora zaidi katika nchi ya Misri. Huko katika mazingara mazuri na hali zingine zilizowafaa,

43

Yusufu aliwapa mahitaji yao yote (Mwanzo 45:10). {SR1P: 43.7}

Kwa hivyo, katika miaka akisi ya njaa, — katika kipindi cha injili, — Kristo lazima awe na, jinsi mfano, unavyoonyesha aliliandalia kanisa lake ardhi bora iliyokuwapo muda akisi wa kukaa katika nchi za Mataifa — “nyika.” Ufu. 12: 6. Huko, katika Gosheni ya uakisi, lili ” lishwa kwa wakati, na nyakati, na nusu wakati,” Ufu. 12:14. {SR1P: 44.1}

Zaidi ya hayo, kama Yakobo na uzao wake, mababa wa makabila kumi na mawili ya Israeli, waliingia nchi ya Gosheni, sio mwanzoni mwa miaka ya njaa, ila katika mwaka wa pili, inaonyesha tena kwamba somo wao hawapaswi kutafutwa mwanzoni mwa enzi ya Kikristo, lakini baadaye. {SR1P: 44.2}

Zaidi ya hayo, tunapata kwamba Mzee White, jina lake alilopewa “Yakobo” linamaanisha sawa na Yakobo, aliwazaa (alitengeneza ushirika) wazawa (waongofu na washirika), mababa waasisi wa Kanisa la Waadventista wa Sabato wazazi wa kiroho wa makabila kumi na mawili akisi — wale 144,000 — katika ardhi ya Goshen akisi, mbali na nchi ya ahadi. {SR1P: 44.3}

Na Farao kumhifadhi Yusufu upande wake wa kulia juu ya kiti cha enzi cha Misri akiwa sawa na Mungu kumudumisha Kristo upande wake wa kuume juu ya kiti cha enzi cha

44

dunia zote, elimu mifano humfafanua Farao kama mfano wa Mungu. {SR1P: 44.4}

Lakini baada ya muda Farao huyo mwenye mkarimu na mwenye huruma alilala, na akainuka badala yake Farao mwenye chuki na mkatili ambaye aliamua kuwaangamiza Waebrania kwa kuwaondoa —

KUTOKA KWA MAZIZI YA KONDOO HADI KWA YADI ZA MATOFALI (SR1P: 44.5}

” Basi akainuka mfalme mpya kutawala Misri, asiyemjua Yusufu. Akawaambia watu wake, Angalieni, watu wa wana wa Israeli ni wengi tena wana nguvu kuliko sisi…. Basi wakaweka wasimamizi juu yao wawatese kwa mizigo yao. Nao wakamjengea Farao miji ya kuwekea akiba, Pithomu na Ramesesi. Lakini kwa kadiri ya walivyowatesa ndivyo walivyoongezeka na kuzidi kuenea. …. Wamisri wakawatumikisha wana wa Israeli kwa ukali; wakafanya maisha yao kuwa uchungu kwa kazi ngumu; kazi ya chokaa na ya matofali, na kila namna ya kazi ya mashamba; kwa kazi zao zote walizowatumikisha kwa ukali.” Kut. 1: 8-14. {SR1P: 45.1}

Kwa mantiki sambamba, huyu Farao “mpya” ambaye hakumjua Yusufu na ambaye alitaka kuwaangamiza watu wa Bwana, Waisraeli, ni mfano wa adui mkuu, si mwingine ila Shetani, mungu wa uongo, anayejiinua katika dunia hii, katika Misri akisi. {SR1P: 45.2}

Kwa uwazi watumishi wa Farao mwenye mjeuri ambao walimwezesha kuyatekeleza makusudi yake maovu, ni mfano wa watumishi wa

45

Shetani, ambao wanamwezesha kuifanya kazi ya kuharibu makusudi ya Mungu kwa kanisa Lake. {SR1P: 45.3}

Kwa mtazamo huu Yusufu alikuwa ametafuta milele kufunga uwezekano wa kujumuika kijamii kati ya Waebrania na Wamisri, kwa kuwaagiza ndugu zake kumwambia Farao kwa msisitizo kwamba walikuwa wachungaji, maana wachungaji walikuwa chukizo kwa Wamisri. Hata hivyo, baada ya muda, Farao mwovu aliwatoa kwa mazizi ya kondoo na kuwaweka wafanye kazi katika yadi za matofali. {SR1P: 46.1}

Kweli kwa mfano, Waadventista wa Sabato wamekuwa tangu mwanzo wao wakijiwakilisha kama wachungaji, kauli mbiu yao ni: “Kila mu-Adventista wa Sabato ni mmishonari, na kila mmishonari ni mhubiri na mchungaji” — wachungaji wa kundi la Mungu. {SR1P: 46.2}

Roho wa Kweli, hata hivyo, aliweka bayana miaka ambayo imepita kwamba vikwazo juu ya mazoea hayo tayari vilikuwa vimeanza. Alifichua, “Jambo la kigeni, limeingia katika makanisa yetu. Watu ambao wamewekwa katika nafasi za majukumu kwamba waweze kuwa wasaidizi wa busara kwa watenda kazi wenzao, wamedhani kwamba wamewekwa kuwa wafalme na watawala katika makanisa kumwambia ndugu mmoja, Fanya hili; kwa mwingine, Fanya Lile; na kwa mwingine, Hakikisha kufanya kazi kwa njia hii na hii.” — Shuhuda kwa Wachungaji, uk. 477. {SR1P: 46.3}

46

Hivyo, kama vile Waebrania walivyolazimishwa kutoka kwenye mazizi ya kondoo hadi katika yadi za matofali, Waadventista wa Sabato kwa namna hiyo wanalazimika kuacha kuhubiri Injili ili kuongeza vikomo na vikomo zaidi. Ndiyo, hata ambapo wanafanya kazi yao kuwa kali, Farao mamboleo, pia, anadai kwamba

HAKUNA TENA NYASI. {SR1P: 46.4}

” Na siku ile ile Farao akawaamuru wasimamizi wa watu, na wanyapara wao, akisema, Msiwape watu tena majani ya kufanyia matofali, kama mlivyofanya tangu hapo; na waende wakatafute majani wenyewe…. Hao wasimamizi wa watu na wanyapara wao wakatoka, wakasema na watu, wakanena,… Enendeni wenyewe, jipatieni majani hapo mtakapoyaona; kwa maana kazi yenu haitapunguzwa hata kidogo. ” Kut. 5: 6, 7, 10; 11. {SR1P: 47.1}

Na sasa, kabla ya ukombozi wao kutoka kwa utumwa wao akisi, Waadventista wa Sabato wanahitajika kwa ukubwa kufanya bajeti zao, vikomo, na ada mbalimbali na matumizi mengine, lakini wakati wanapohitaji, hawapati kivitendo msaada wowote wa Kidini. Jinsi ilivyo na mifano yao, kila kitu — muda, nguvu, pesa, na vyote — huchukuliwa kutoka kwao, ambapo kwa mbadala hawapati kitu. {SR1P: 47.2}

“Katika nambari za zamani za Shuhuda kwa Kanisa,” anasema mwasisi wa Dhehebu, “Nimesema juu ya umuhimu wa Waadventista wa Sabato kuanzisha taasisi kwa manufaa ya

47

wagonjwa, hasa kwa wanaoteseka na wagonjwa miongoni mwetu. Nimesema juu ya uwezo wa watu wetu, kuhusu raslimali, kutekeleza hili; na nimewahimiza kwamba, kwa mtazamo wa umuhimu wa tawi hili la kazi kubwa ya maandalizi ya kukutana na Bwana kwa furaha ya moyo, watu wetu wanapaswa kujihisi wameitwa, kwa mujibu wa uwezo wao, kuweka sehemu ya raslimali zao katika taasisi ya aina hii…. {SR1P: 47.3}

“Nilipowaona wale ambao walisimamia na kuelekeza, wakiingia katika hatari nilioonyeshwa, ambayo nilikuwa nimewaonya kwa umma, na pia katika mazungumzo ya faraghani na barua, mzigo mkubwa ulikuja juu yangu. Kile ambacho nilikuwa nimeonyeshwa kuwa ni mahali ambapo wagonjwa wanaoumia miongoni mwetu wangeweza kusaidiwa, palikuwa pale ambapo sadaka, ukarimu, imani, na uchaji lazima ziwe kanuni za uongozi …. {SR1P: 48.1}

“Kwa kadiri ninavyoweza kuhukumu, nusu ya waathirika kati ya watu wetu, ambao wanapaswa kukaa wiki au miezi kwenye Taasisi, hawawezi kulipa gharama zote za safari na kukaa pale. Je, umaskini utawatenga hawa marafiki wa Bwana wetu kutoka kwa baraka ambazo amezitoa kwa wingi? Je! Wao waachwe waendelee kupambana na mzigo mara mbili wa udhaifu na umaskini? … {SR1P: 48.2}

“Kwa walio adhirika miongoni mwa watu wetu napenda kusema, Msikate tamaa. Mungu hajawaacha watu wake na kazi yake.” – Shuhuda, Gombo la 1, uk. 633, 641, 643. {SR1P: 48.3}

48

Halafu kwa mfano tunaongozwa kuwafikiria wakunga waaminifu –

SHIFRA NA PUAH. {SR1P: 49.1}

Kwa kuthibitisha kwamba Farao mamboleo anafanya kazi yote anayoweza kufanya ili kuwadanganya watu wa Mungu dhidi ya mkombozi siku hii. ” Kisha mfalme wa Misri akasema na wakunga wa Waebrania, mmoja jina lake aliitwa Shifra, na wa pili jina lake aliitwa Pua; akasema, Wakati muwazalishapo wanawake wa Kiebrania na kuwaona wa katika kuzaa, ikiwa ni mtoto mwanamume, basi mwueni, bali ikiwa ni mtoto mwanamke, na aishi. Lakini wale wazalisha walikuwa wakimcha Mungu, wasifanye kama walivyoamriwa na huyo mfalme wa Misri, lakini wakawahifadhi hai wale wanaume. {SR1P: 49.2}

” Basi mfalme wa Misri akawaita wale wakunga na kuwauliza, Kwa nini kufanya jambo hili, na kuwahifadhi watoto waume wawe hai? Wakunga wakamwambia Farao, Ni kwa sababu hao wanawake wa Kiebrania si kama wanawake wa Kimisri; kwa kuwa ni hodari hao, nao huzaa kabla mkunga hajapata kuwafikilia. {SR1P: 49.3}

” Basi Mungu akawatendea mema wale wakunga; na hao watu wakaongezeka sana, wakaendelea na kuzidi kuwa na nguvu nyingi. {SR1P: 49.4}

” Kisha huyo Farao akawaagiza watu wake, akisema, Kila mtoto mwanamume atakayezaliwa mtamtupa mtoni, na kila mtoto mwanamke mtamhifadhi hai. Kut. 1: 15-22. {SR1P: 49.5}

Wakunga wanaweza kuwakilisha nani kwa kawaida? — Hebu mantiki na haki kutoa jibu: Watoto waliozaliwa na wanawake Waebrania katika nchi ya Misri, mbali na nchi yao, wanaweza tu kuwakilisha watoto waliozaliwa kwa kanisa wakati lingali ugenini mgeni miongoni mwa nchi za mataifa. {SR1P: 49.6}

Wajibu wa mkunga ni kupokea kwa neema, kumuosha vizuri, na kwa usafi

49

kumvika, pia kumpa lishe bora, mtoto aliyezaliwa. Hivyo wakunga wa kale lazima wawakilishe, wale ambao wajibu wao wa kiroho wa siku hii ni kumtakasa mwanafunzi-kijana kutokana na dhambi za kurithi, kuwavika mavazi ya haki ya Kristo, na kuwalisha chakula cha kiroho — kuwafunza mafundisho kwa mwanga wa Ukweli wa sasa. Uharaka huu tu kwa vijana, bila shaka, ni shule ya kanisa. {SR1P: 49.7}

Kwa hiyo wakunga ‘kukataa kuua watoto wa Kiebrania, kwa hivyo, hakuonyeshi kitu kuliko ukweli kwamba walimu katika shule za dhehebu za leo wanajitahidi kufanya jambo la haki hata kama wana, kama ilivyo, kukiuka amri mbaya ya Farao. {SR1P: 50.1}

Na ufafanuzi huu wa elimu ya mifano unasisitizwa kikamilifu katika dondoo kutoka kwa Gazeti la Elimu ya Kikristo Nyumbani na Shuleni, Jarida la Baraza Kuu ambalo kila mwalimu katika dhehebu la Waadventista wa Sabato anatakiwa kujiandikisha. {SR1P: 50.2}

Toleo la Desemba, 1929, la gazeti hili, lililojaa kutunza Krismasi na mipango ya Krismasi na zawadi, ni mfano mzuri wa mwenendo wa Baraza wakati Fimbo ya Mchungaji alianza kufunuliwa. Kwa vile ni la urefu mno kunukuu kwa ukamilifu, tuna nukuu msitari wa mwisho tu, maneno ya kufunga chini ya aya, “Kile Krismasi Inaweza Kumaanisha Daima”: {SR1P: 50.3}

50

“Na, kwa ujumla, ubatizo wa ukweli, unyenyekevu, na uaminifu katika ukumbusho wa sikukuu ya kuzaliwa ya dunia.” {SR1P: 51.1}

Kwa jarida la Baraza Kuu kuwaamuru walimu kuinua mbele ya vijana siku kuu ya sanamu ya kidunia kama siku ya kuzaliwa ya Kristo, ni ajabu. Lakini, kama wote wanaweza kuona hasa, ni kama vile ilivyokuwa amri ya Farao kwa wakunga. {SR1P: 51.2}

Matakwa yake kwamba watoto wa kiume watupwe ndani ya mto, halikuwa na matokeo kuzuia maendeleo ya ongezeko la haraka la taifa la Waebrania, lakini lilikuwa ni jitihada katili ya kumwangamiza mkombozi aliyeahidiwa. Na kushindwa kwa azimio ovu la Farao siku hiyo ulikuwa mfano wa kushindwa kwa jitihada ya hila ya Farao mamboleo ili kumuondolea mbali nabii wa leo, ambaye atawaokoa Waisraeli mamboleo ambapo nyakati za Mataifa zitakapotimia. {SR1P: 51.3}

Kuthibitisha kwamba Farao mamboleo anafanya kazi yote ambayo inaweza kufanywa kuwadanganya watu wa Mungu dhidi ya mkombozi leo, tunasoma ukweli kwamba wakati rekodi ya Uvuvio ya Dhehebu imeelezea wazi kuja kwa nabii (Shuhuda kwa Wachungaji, uk. 475), ujumbe, ukweli wa ziada (Maandishi ya awali, uk. 277), washiriki wa kanisa hawajaachwa tu kwa kutokuujua pia hata wanaonywa dhidi yake, — wamefundishwa kuwa hawana haja ya kitu, kwamba wana ukweli wote wa kuwapeleka kwa Ufalme! {SR1P: 51.4}

51

Ili kufichua, kwa maneno ya Uvuvio, matamshi ya majivuno na ya hila ya Farao mamboleo na udanganyifu wa aina hii, tuna nukuu: {SR1P: 52.1}

“Unabii lazima utimizwe.” Asema Bwana: Angalieni, nitawatumia Eliya nabii kabla haijaja ile siku kuu na ya kutisha ya Bwana.’ Mtu atakuja katika roho na nguvu ya Eliya, na wakati atapoonekana, watu wanaweza kusema: ‘Wewe ni wa bidii sana, hutafsiri Maandiko kwa njia sahihi. Hebu nikuonyeshe jinsi ya kuufundisha ujumbe wako.’ ” – Shuhuda kwa Wachungaji, uk. 475, 476. {SR1P: 52.2}

“Hali ya sasa ya kanisa haimpendezi Mungu. Kumeingia kujiamini nafsi ambapo kumewaongoza kujihisi hawana haja ya ukweli zaidi na nuru kubwa. Tunaishi wakati ambapo Shetani anafanya kazi mkono wa kulia na wa kushoto, mbele na nyuma yetu; na bado kama watu tumelala. Mungu anakusudia kwamba sauti itasikika kuwaamsha watu Wake kutenda. ” — Shuhuda, Gombo la 5, uk. 709. (Angalia pia Watenda Kazi wa Injili, uk. 300.) {SR1P: 52.3}

Kwamba Farao mamboleo atakumbana na mwisho kushindwa kabisa katika jitihada zake za hila, inaonyeshwa wazi katika kweli sio tu kwamba maisha ya Musa yaliokolewa na binti wa Farao wa kale, bali pia alilelewa kwa gharama ya mfalme mwenyewe! Elimu ya mifano inafichua, kwa hivyo, kushindwa kwa kutisha ambapo maadui wa kazi ya mkombozi akisi wataadhibishwa: jaribio lao kwa upumbavu kumshinda Mungu kwa kusudi lake kwa

52

Ajili ya watu Wake, ni kwa gharama zao wenyewe hakika watageuza kuwa ushindi wa utukufu kwa Bwana. {SR1P: 52.4}

Kwa kuwa sasa tumeona kuwa Waisraeli kuingia Misri ni kwa mfano, mantiki huamua kwamba hivyo pia lazima kuwepo

ISRAELI KUONDOKA MISRI {SR1P: 53.1}

Kwamba kule kutoka kwa siku ya Musa ni onyesho sawa sawa lakini ndogo la kutoka kwa hivi karibuni, Roho kupitia Isaya nabii anatangaza: {SR1P: 53.2}

“Na itakuwa katika siku hiyo, shina la Yese lisimamalo kuwa ishara kwa kabila za watu, yeye ndiye ambaye mataifa watamtafuta; na mahali pake pa kupumzikia patakuwa na utukufu. {SR1P: 53.3}

“Na itakuwa katika siku hiyo, Bwana atapeleka mkono wake mara ya pili, ili ajipatie watu wake watakaosalia, kutoka Ashuru, na kutoka Misri, na kutoka Pathrosi, na kutoka Kushi, na kutoka Elamu, na kutoka Shinari, na kutoka Hamathi, na kutoka visiwa vya bahari. {SR1P: 53.4}

“Naye atawatwekea mataifa bendera, atawakutanisha watu wa Israeli waliotupwa, atawakusanya watu wa Yuda waliotawanyika, kutoka ncha nne za dunia..” (SR1P: 53.5}

“Na wivu wa Efraimu utaondoka, na wale wanaomwudhi Yuda watakatiliwa mbali; Efraimu hatamhusudu Yuda, wala Yuda hatamwudhi Efraimu. [Kutakuwa na amani kamili kati yao]. {SR1P: 53.6}

53

“Nao watashuka, watalirukia bega la Wafilisti upande wa magharibi; nao pamoja watawateka wana wa mashariki; watanyosha mkono juu ya Edomu na Moabu; na wana wa Amoni watawatii.” (SR1P: 54.1}

“Na Bwana atauangamiza kabisa ulimi wa bahari ya Misri; na kwa upepo wake uteketezao atatikisa mkono wake juu ya Mto, naye ataupiga, uwe vijito saba, na kuwavusha watu wenye viatu vikavu.”{SR1P : 54.2}

” Itakuwako njia kuu kwa mabaki ya watu wake watakaobaki, watokao Ashuru, kama vile ilivyokuwako kwa Israeli, katika siku ile waliyotoka katika nchi ya Misri.” Isa. 11: 10-16. {SR1P: 54.3}

Dhahiri sana,zamani zile, nguzo ya wingu mchana na nguzo ya moto usiku ambayo iliongoza kwa utukufu jeshi la Waebrania kutoka Misri lilionyesha mbele na hata kubwa zaidi na yenye utukufu mkubwa zaidi wa kinga, kwa ushindi kuwaongoza Waisraeli wa leo sio tu kwa safari yao ya kwenda nchi ya ahadi lakini wakati wote wanapokaa huko. {SR1P: 54.4}

Kwa maana “Tena itakuwa,” anafunua nabii, ” ya kwamba yeye aliyebaki katika Sayuni, na yeye aliyeachwa ndani ya Yerusalemu [baada ya mwovu kuchukuliwa], ataitwa mtakatifu; yaani, kila mmoja aliyeandikwa miongoni mwa hao walio hai ndani ya Yerusalemu; hapo Bwana atakapokuwa ameuosha uchafu wa hao binti za Sayuni na kuisafisha damu ya Yerusalemu kati yake, kwa roho ya hukumu na kwa roho ya kuteketeza. {SR1P: 54.5}

54

“Na Bwana ataumba juu ya kila makao ya Mlima Sayuni, na juu ya makusanyiko yake, wingu na moshi mchana, na mwangaza wa moto wa moto usiku; kwa maana utukufu wote utakuwa ulinzi.” (SR1P: 55.1 }

“Kisha kutakuwa na hema kuwa uvuli wakati wa mchana kwa sababu ya hari, na kuwa mahali pa kukimbilia na kujificha wakati wa tufani na mvua.” Isa. 4: 3-6. {SR1P: 55.2}

Mafungu haya ya unabii kwa hakika yanaonya mbele kwamba kwa muda mfupi wadhambi watachukuliwa kutoka Yerusalemu (“uchafu wa binti za Sayuni” utatakaswa), na hivyo yana ahidi kwamba watakatifu tu kutoka pembe nne za dunia watakuwa na sehemu katika safari inayokuja ya kutoka akisi. {SR1P: 55.3}

Pasaka, pia, ambayo waliangamia wazawa wa kwanza wa mwanadamu na wanyama waliopatikana katika makao ambayo hayakuwa na damu kwenye miimo ya milango, ilisema mbele ya Pasaka akisi ambayo wote watakao achwa bila alama kwa sababu ya kutougua na kulia kwa sababu ya machukizo kati yao hakika wataanguka chini ya vyombo vya kufisha vya malaika (Ezek. 9: 2). {SR1P: 55.4}

Je, hii itatukia lini? — Mfano bila shaka unaonyesha wakati kupitia ukweli kwamba wazawa wa kwanza tu walikuwa kwa

55

hatari. Vivyo hivyo, Pasaka akisi itafanyika wakati wa mavuno ya malimbuko — kutiwa muhuri watu 144,000, malimbuko, wa kwanza kwenda Yerusalemu akisi, wa kwanza kusimama juu ya Mlima Sayuni na Mwanakondoo, wazawa wa kwanza kwa Roho. Wazi kabisa, malimbuko wote watakao pokea alama wataendelea kuishi, na wote watakao shindwa kupokea alama wataangamia hakika kama vile wazawa wa kwanza ambao wakati wa Pasaka asili walishindwa kupaka damu kwenye miimo ya milango . {SR1P: 55.5}

Mbali na mifano hii ya kushangaza na masomo yake ya thamani, Wa Ajabu amefanya, kwa ajili ya kuerevuka kwetu, kwa usahihi zaidi

MAAJABU YA ELIMU YA MIFANO. {SR1P: 56.1}

Jicho la uangalifu kwa nuru ya mbinguni linaona kwamba Yehova Mungu, Msanii Bora, ametumia katika Maandiko kila njia inayojulikana kwa wanadamu ya kuufunua muundo wa ajabu wa Ukombozi. Na sasa anapowaongoza watu wake kwa Ufalme wa milele, Yeye hutumia nuru kwa njia yao hata elimu ya mifano — maisha ya watu ambao wamekuwapo awali na uzoefu ambao wamepitia — na unaamuru kwamba kushindwa na ushindi wao unapaswa uwe mawe mtoni ya watakatifu kuvukia. {SR1P: 56.2}

Na kuziamsha roho za wanadamu kwa ufahamu wa Nguvu kazi Yake ya ajabu na kutoweza kwao kutoyaona ya baadaye

56

na kwa hivyo kutembea katika njia nyembamba, Yule Wa Kujua Yote anatupa changamoto: {SR1P: 56.3}

“Haya, leteni maneno yenu, asema Bwana; toeni hoja zenu zenye nguvu, asema mfalme wa Yakobo.” (SR1P: 57.1}

Wayatangaze na kutujulisha yatakayokuwa; watuonyeshe mambo ya zamani, ni mambo gani, tukapate kuyatia moyoni, tukajue mwisho wake; au wamdhihirishie yatakayotokea baadaye. {SR1P: 57.2}

Tujulisheni yatakayokuwa baadaye, nasi tutakiri ya kuwa ninyi ni miungu; naam, tendeni mema au tendeni mabaya, ili tujipime, tukaone pamoja. ” Isa. 41: 21-23. {SR1P: 57.3}

“Ni nani aliyetenda na kufanya jambo hilo, aviitaye vizazi tangu mwanzo? Mimi, Bwana, wa kwanza na wa mwisho, mimi ndiye.” Isa. 41: 4. {SR1P: 57.4}

Eleza chanzo, sababu, umuhimu wa mambo ya zamani, Anadai. Tuambie, yanamaanisha nini? Je, ni ya nini? Je! Unaweza kutabiri wakati ujao kwa ya zamani, yawe mazuri au mabaya? Onyesha uwezo wa Mungu ikiwa unaweza. {SR1P: 57.5}

Kimya kwa hoja kinapeana idhini ya ukweli kwamba Mimi Niko tu anaweza hivyo kuonya mbele vizazi, cha kwanza hadi cha mwisho. Na hufanya ijulikane kwamba ingawa uzoefu ambao watangulizi wetu waliruhusiwa kupitia ulikuwa kwa ajili yetu mifano, bado hata sasa sisi wenyewe hatuwezi kuitafsiri kwa usahihi. {SR1P: 57.6}

57

Lakini sasa kwa wakati uliowekwa, Yeye Mwenyewe anafunua umuhimu wake kwa wale walengwa ambao awali hasa iliyoundwa kwa ajili yao. Hivi kwa “vitu vya zamani,” ulimwengu wa jana, Mkuu wa pekee Mtaalamu wa elimu ya mifano ameonyesha “mwisho unaofuata” wa, dunia ya leo: {SR1P: 58.1}

Mwanzoni mwa elimu ya mifano hii, imeonekana kwamba “mwanamke,” Hawa ambaye kwa njia ya uzao wake mwenyewe (kanisa hai) litakiponda kichwa cha nyoka (Mwanzo 3:15), unaashiria kanisa lililotangulia kipindi cha Waebrania; ijayo, kwamba hajira anaashiria kanisa kipindi cha waebrania, na mwisho, kwamba Sara anaashiria Kanisa la Kikristo. {SR1P: 58.2}

Kufuatilia haya, elimu ya mifano inaonyesha kwamba Melkizedeki, kuhani

wa Mungu aliye Juu Sana, Ambaye hana mwanzo wala mwisho wa siku, anamuashiria Kristo Kuhani wetu Mkuu na kazi Yake ya milele, na kwamba Haruni, kuhani mkuu katika kipindi cha Wayahudi, anamuashiria Kristo, Kuhani wetu Mkuu na kazi ya ukuhani wa muda. {SR1P: 58.3}

Wakati wa kujenga elimu ya mifano, Majaaliwa ya Mungu yalimleta Hajira ndani ya nyumba ya Ibrahimu, na kupitia kutovumilia kwa Sarah kusubiri mwana, yalimleta Ishmaeli kuwapo. Hivyo ulikuwa utabiri wa maadili na tabia ya taifa akisi. {SR1P: 58.4}

“Kwa maana imeandikwa, Ibrahimu alikuwa na wana wawili, mmoja kwa mjakazi, na mwingine kwa mke huru. Lakini yeye aliyekuwa wa

58

mjakazi alizaliwa kwa mwili; lakini yeye wa mke huru alikuwa wa ahadi. {SR1P: 58.5}

“Mambo haya husemwa kwa mfano; kwa maana hawa ndio kama maagano mawili, moja kutoka mlima Sinai, lizaalo kwa utumwa, ambalo ni Hajiri. Maana Hajiri ni kama mlima Sinai ulioko Arabuni, umelingana na Yerusalemu wa sasa; kwa kuwa anatumika pamoja na watoto. Bali Yerusalemu wa juu ni mwungwana, naye ndiye mama yetu sisi. {SR1P: 59.1}

“Kwa maana imeandikwa, Furahi, wewe uliye tasa, usiyezaa; Paza sauti, ulie, wewe usiye na utungu; Maana watoto wake aliyeachwa pekee ni wengi Kuliko wa huyo aliye na mume. {SR1P: 59.2}

Basi, ndugu zangu, kama Isaka sisi tu watoto wa ahadi. Lakini kama vile siku zile yule aliyezaliwa kwa mwili alivyomwudhi yule aliyezaliwa kwa Roho, ndivyo ilivyo na sasa. {SR1P: 59.3}

“Lakini lasemaje andiko? Mfukuze mjakazi na mwanawe, kwa maana mwana wa mjakazi hatarithi kabisa pamoja na mwana wa mwungwana. Ndiposa, ndugu zangu, sisi si watoto wa mjakazi, bali tu watoto wa huyo aliye mwungwana.”Wagal. 4: 22-31. {SR1P: 59.4}

“Ni wazi kwamba Hajiri na Ishmaeli waliingia katika nyumba ya Ibrahimu waliwakilisha watu waliozaliwa kwa mwili ( sio wazaliwa kwa roho), wazawa wa Yakobo (Israeli wa zamani), kuingia katika nyumba ya Mungu,

59

Sio kupitia kuzaliwa kwa kiroho, bali kwa sababu ya ki-asili. {SR1P: 59.5}

Pia ni kwamba uasi wa Hajiri kwa Sara ulinena mbele dhidi ya uasi wa marabi dhidi ya Kanisa la Kikristo, na kwamba utesi wa Ishmaeli kwa Isaka ulionyesha mateso ya Wayahudi kwa Wakristo. {SR1P: 60.1}

Na mwisho, Abrahamu kutowapa urithi Hajiri na mwanawe, na kuwafukuza mara moja na milele, lilikuwa tazamio la mbele la Mungu kutowapa urithi na kuwatoa kwa nyumba Yake Wayahudi wa utu wa zamani ambao walishindwa kuongoka, kupatanishwa, kuzaliwa upya – walioshindwa kuuzika mwili wa zamani na kuinuka na wa kiroho kulingana na ahadi. {SR1P: 60.2}

Kwa hivyo, kamwe, Myahudi wa kimwili, sio zaidi ya mtu wa Mataifa wa kimwili, kurithi na watakatifu Ufalme wa Mungu — la, sio zaidi ya Ishmaeli kuurithi utajiri wa Ibrahimu — au hata kuwa na sehemu yoyote katika ahadi Zake za utukufu, isipokuwa wazaliwe mara ya pili, wazaliwe kwa Roho katika familia takatifu ya Mungu (Warumi 11:23). {SR1P: 60.3}

Baada ya kupitia vipindi hivi vitatu vya kanisa na ukuhani wake tofauti, sasa tunakuja kwa awamu ya pili ya elimu ya mifano, na hii tutaona haraka na kwa uhakika zaidi sasa tunapopitia onyesho la taipolojia la vizazi vyote kwa msaada wa ramani iliyo ambatanishwa, ambayo inaufunua vizuri ukweli endelevu na kutusihi kuupokea. {SR1P: 60.4}

60

61

Kwa njia ya ramani hii kanisa la Mungu linaonekana haraka katika vikundi vitano tofauti kwa vipindi. Ya kwanza viwili viko kwa mfano, na vitatu vya mwisho vitatu viko kwa akisi: {SR1P: 62.1}

(1) cha Nuhu, (2) cha Wazee wa imani, (3) cha Ufalme wa Muda, (4) cha Uinjilisti, (5) cha Ufalme wa Milele. {SR1P: 62.2}

Uzao wa elimu ya mifano wa “mwanamke” umezaliwa katika vikundi viwili vya asili –cha Nuhu na cha Mababu — na kinafikia ukomavu wa kiroho wakati wa akisi vikundi vitatu vinavyofuata; yaani, Ufalme wa Muda, Uinjilisti, na Ufalme wa milele. {SR1P: 62.3}

Katika safina asili watoto waliozaliwa kwa mwili: Kaini na Abeli, Ishmaeli na Isaka, Esau na Yakobo — mzuri na mbaya katika kila mfano. Na katika uakisi wanapata akisi wao kama ifuatavyo: {SR1P: 62.4}

Kwa mfano, katika historia yote ya kanisa wanaonekana akina Kaini kwa upande mmoja — wale wanaomwabudu Mungu, sio jinsi Anavyoamuru, ila kama wanavyotaka kulingana na hali. Na kwa upande mwingine wanaonekana akina Abeli — wale wanaomwabudu Mungu kwa usahihi kulingana na mapenzi Yake na ambao, kwa hivyo, kwa kufanya hivyo wanalengwa kwa hasira ya akina Kaini, ambao kwa hasira na wivu huwaua. Hivyo wafia dini. {SR1P: 62.5}

Kisha Neema ilimleta Sethi ili aendeleze sehemu ambayo Abeli ​​kwa hali ilivyokuwa alilazika kumwacha Kaini, mzaliwa wa kwanza, anawakilisha,

62

kulingana na kanuni ya Biblia, daraja la ukasisi, ambapo Abeli na Sethi, wadogo, lazima wanawakilisha daraja la waumini. {SR1P: 62.6}

Hivi walikuwa ukasisi na muumini, mnnafiki, mfia dini, na mtakatifu, walikuwa mfano tangu mwanzo wa jamii ya wanadamu. {SR1P: 63.1}

Isaka, mzawa wa kwanza kwa njia ya ahadi kupitia mapenzi ya Mungu, anaweza tu kuwakilisha daraja la wachungaji ambao wamewekwa katika ofisi takatifu kupitia haki ya kuzaliwa ya kiroho — “waliozaliwa mara ya pili,” walioteuliwa na Mungu. {SR1P: 63.2}

Ishmaeli, pia, akiwa mzaliwa wa kwanza wa Ibrahimu, lakini si kwa njia ya ndoa halali au ahadi, anawakilisha daraja la ukasisi wa utu wa kale ambao huongozwa kwa ofisi hiyo, si kwa njia ya haki ya kuzaliwa kiroho na wito kutoka kwa Bwana wa shamba la mizabibu, ila tu kupitia fursa. {SR1P: 63.3}

Kwa namna hii iliigizwa tabia ya marabi wa Wayahudi waliojipenda nafsi, Waishmaeli wa uakisi, waliowatesa mitume, akina Isaka wa uakisi. {SR1P: 63.4}

Esau na Yakobo wakiwa mapacha na wa mwisho katika mstari huu wa taipolojia, kwa hiyo wao ni kivuli cha vikundi viwili vya watu wanaoishi kwa wakati mmoja katika kipindi cha kanisa cha kufuata kile ambacho Isaka anawakilisha — cha mwisho, Esau wa Laodekia, akiwa wa kwanza kuzaliwa, anawakilisha ukasisi aa Esau ambao kwa kiasi kidogo kama mchuzi wa “ndengu” wanapoteza nafasi yao kwa wa’Yakobo washiriki. {SR1P: 63.5}

63

Na katika kuliongezea somo hilo, Roho ya Unabii zamani kwa nguvu aliwaonya mbeleni akina Esau, akisema: {SR1P: 64.1}

“Katika kupepetwa kwenye nguvu kutakakotukia hivi karibuni, tutaweza zaidi kupima nguvu za Israeli. Ishara zinaonyesha kwamba wakati unawadia ambapo Bwana atadhihirisha kwamba pepeta lake liko mkononi mwake, na ataisafisha sakafu yake kabisa …. {SR1P: 64.2}

“Wale ambao wametoa heshima kubwa kwa ‘sayansi inavyoitwa kwa uongo,’ hawatakuwa viongozi baadaye. Wale ambao wameamini kwa akili, ustadi, au talanta, hawatasimama baadaye kuwa viongozi wa askari. Hawakufululiza mwendo na nuru. Wale ambao wamejithibitsha kuwa sio waaminifu baadaye hawatakabidhiwa kundi. Katika kazi ya mwisho ya uchaji watu wakuu wachache hawatahusishwa. Wametosheka kwa ubinafsi, hawamtegemei Mungu, na hawezi kuwatumia. Bwana ana watumishi waaminifu, ambao katika mtetemo, wakati wa kupimwa watafunuliwa waonekane.” — Shuhuda, Gombo la 5, uk. 80. {SR1P: 64.3}

Sasa, badiliko la jina la Esau laonyesha kwamba akina Esau siku fulani, na si mbali sana, hawata kumbukwa na kusujudiwa kwamba ni wao wa kumaliza, ila zaidi watahofia kama Waedomu, kama wale wanaoangamia. Na badiliko la jina la Yakobo laonyesha kwamba wa-Yakobo basi hawatafukuzwa tena na kuogopa kama wa-Yakobo, kama wanyakuzi, wa kimwili, il zaidi wakaribishwe kama Waisraeli, wakuu watakatifu, watawala wenza wakisimama

64

na Mwana-Kondoo juu ya Mlima Zayuni (Ufu. 14: 1), katika kasri la Mfalme Mkuu. {SR1P: 64.4}

Baadaye, wakati kazi ya injili imekamilika na “uzao wa mwanamke” umekomaa kuwa Wakristo wazima (wanakuwa shoka la Bwana la vita — Yer 51:20) — na kuponda kichwa cha Joka, pia kuyapiga mataifa maovu — Dan. 2:44, 45), basi itaonekana dhahiri kwamba yale ambayo Adamu wa kwanza alipoteza kwa njia ya kujifurahisha tamaa, Adamu wa pili kwa njia ya kuwa na kiasi alirejesha, — Ufalme wa milele tena ukitawala dunia yote. (Dan 2:35). {SR1P: 65.1}

Basi litatoka chipukizi katika shina la Yese,” unasema Uvuvio, “na tawi litakalotoka katika mizizi yake [Mwokozi wa nyumba ya Yese] … wala hatahukumu kwa kuyafuata ayaonayo kwa macho yake, wala hataonya kwa kuyafuata ayasikiayo kwa masikio yake; bali kwa haki atawahukumu maskini, naye atawaonya wanyenyekevu wa dunia kwa adili…. {SR1P: 65.2}

“Na haki itakuwa mshipi wa viuno vyake, na uaminifu mshipi wa kujifungia. Mbwa-mwitu atakaa pamoja na mwana-kondoo, na chui atalala pamoja na mwana-mbuzi; ndama na mwana-simba na kinono watakuwa pamoja, na mtoto mdogo atawaongoza. Ng’ombe na dubu watalisha pamoja; watoto wao watalala pamoja; na simba atakula majani kama ng’ombe. Na mtoto anyonyaye atacheza penye tundu la nyoka, na mtoto aliyeachishwa atatia mkono wake katika pango la fira. Hawatadhuru wala hawataharibu katika

65

mlima wangu wote mtakatifu; maana dunia itajawa na kumjua Bwana, kama vile maji yanavyoifunika bahari. “Isa 11: 1-9. {SR1P: 65.3}

Na sasa, mpenzi msomaji, ukifahamu kwamba wakati wa karamu halisi ya chakula cha kiroho, “chakula kwa majira yake,” iko hapa hasa, wewe, naam umeongozwa kuuliza: Ni nini kilichoileta? Ni nini kilichofanya mabadiliko makubwa? {SR1P: 66.1}

Jibu kwa swali hili muhimu limepeanwa katika ufuatao

MPANGILIO WA SANJARI. {SR1P: 66.2}

“Basi wana wa Israeli kukaa kwao, maana, muda waliokaa ndani ya Misri, ulikuwa ni miaka mia nne na thelathini. ” Kut. 12:40. {SR1P: 66.3}

Msomaji hapa ndani ataona haraka kwamba matukio ya wakati wa kipindi hiki cha kukaa na mateso ya Abrahamu, Isaka, Yakobo, na Israeli, kwa kushangaza sana yanalingana na matukio kama hayo mwanzo wa kipindi cha Matengenezo ya Luther hadi ujumbe wa leo, kutiwa muhuri watu 144,000 . {SR1P: 66.4}

“Kipindi cha miaka mia nne na thelathini kuanzia kwa ahadi aliyopewa Abrahamu alipoagizwa kuondoka Ur ya Wakaldayo .. Miaka mia nne ya Mwanzo 15:13 ilianzia kwa kipindi kilichofuata. Tambua kwamba kipindi cha miaka mia nne sio tu wakati wa kukaa, lakini ni cha mateso. Hiki, kwa mujibu wa Maandiko, lazima kihesabiwe kuanzia miaka thelathini baadaye, karibu na wakati ambapo Ishmaeli, aliyezaliwa kwa mwili, alimtesa [Isaka] aliyezaliwa kwa

66

Roho. Wagal. 4:29.” — Mababu na Manabii uk.760, Nyongeza, Hati ya 6. {SR1P: 66.5}

Na kulingana na Wagalatia 3: 15-17, miaka 430 ilifika kikomo wakati wa kutoa sheria hapo Mlima Sinai. {SR1P: 67.1}

Mwanzoni mwa ulinganifu huu, tunakumbushwa kwamba Abrahamu alipoamua kumfuata Bwana kutoka Ur, ibada ya sanamu ilienea katika dunia ya Wakaldayo. Vivyo hivyo, ulidumumishwa na dunia ya wa Protestanti wakati ambapo Martin Luther aliamua kuwa kuhani badala ya wakili, ibada ya sanamu, ambayo alipinga, ilenea hata katika dunia yote ya Kikristo. Na fundisho ambalo alihubiri likiwa sawa na la Ibrahimu, “mwenye haki ataishi kwa imani,” tayari imeonekana kuwa Abrahamu na dunia ya wakati wake wanapata anapata vifani kwa Luther na dunia ya wakati wake. {SR1P: 67.2}

Baadaye pia, kuteta kwa Sara na Isaka dhidi ya Hajiri na Ishmaeli mwishoni mwa miaka thelathini tangu wakati Ibrahimu alipotoka Ur, inapata kifani chake mnamo mwaka wa 1530 B.K. Kuongoza awamu hii ya elimu ya mifano, historia yakumbusha kwamba yapata mwaka wa 1500 Luther aligundua Biblia ya Kilatini katika maktaba ya Chuo Kikuu cha Erfurt, na kujifunza kwa furaha yake kidogo kwamba Ilikuwa na zaidi ya sehemu muhimu katika matumizi ya kawaida. Miaka yake 30 ya kusoma na kuhubiri Biblia kulisababisha ungamo la Augsburg, hati iliyopitishwa kama imani ya Kiprotestanti na kuwasilishwa kwa

67

Barasa la Augsburg kwa Mfalme, Charles wa 4, mwaka wa 1530. {SR1P: 67.3}

Hivyo uamuzi wa Abrahamu wa kuishi kwa ajili ya Mungu badala ya Ur, unafanana na uamuzi wa Luther kuwa kuhani badala ya mwanasheria. Na kuteta kwa Sara na Isaka, kwamba Hajiri na Ishmaeli hawakuwa waaminifu kwa nyumba ya Ibrahimu na kwa hivyo hawangeweza kuwa tena sehemu yake, kamwe kuwa warithi wake, kunalingana na kuteta kwa Waprotestanti yaliyomo katika hati ambayo alipinga kuwa mazoea ya kanisa na wafuasi wake katika zama za Kati hayakuwa kulingana na Neno. {SR1P: 68.1}

Na tangu wakati Sarah alipoteta hadi wakati Musa alizaliwa, tumaini la ukombozi wa Israeli, ilikuwa miaka 320, ambayo, ikiongezwa kwa 1530 AD inatoa 1850, mwaka ambao ulizaliwa Ushuhuda wa kwanza kwa Kanisa, 144,000, Israeli wa leo. Kwa hiyo, ni wazi kwamba kuzaliwa kwa Musa, matumaini ya Israeli wa kale, hupata kifani chake katika kuzaliwa kwa Ushuhuda wa Kwanza, matumaini ya Israeli mamboleo. {SR1P: 68.2}

Kuendelea na matukio haya yanayofanana, tunakumbuka kwamba Musa akiwa na umri wa miaka 40 alijaribu kuwakomboa Israeli, lakini akashindwa, akakimbia. Kuongeza miaka 40 kwa 1850 AD, tunafika mwaka wa 1890, wakati dhehebu la Waadventista wa Sabato lilibuni

68

Chama cha Kiroho cha Uhuru wa Kitaifa, ambacho pia kilishindwa kutimiza kusudi lake. {SR1P: 68.3}

Zaidi ya hayo, tarehe hii inayojulikana, 1890, ilifikiwa miaka miwili tu baada ya fundisho la “haki kwa imani” lililetwa mara ya kwanza kwa Dhehebu katika Mkutano wa kihistoria wa Kambi ya Minneapolis mwaka 1888, na kisha kukataliwa karibu na wale wote ambao walikuwapo. Kisha wakati wa miaka miwili iliyofuata, ulikataliwa na Dhehebu lote. (Angalia Kristo Haki Yetu, uk. 41-55, toleo la 1941; Shuhuda kwa Wachungaji, uk. 79, 80.) Hii ni moja ya sababu ambazo kanisa mwaka wa 1890 liliachwa kuingia na kukaa katika nyika ya uakisi miaka arobaini, sawia na jaribio la Musa kushindwa kuwatoa Israeli wa kale; pia kukimbia kwake kwenda nyikani. (Angalia Miaka Arobaini Nyikani, na Mzee Taylor Bunch, uk. 15-17.) {SR1P: 69.1}

Miaka arobaini baada ya jaribio la kwanza la kuwaokoa wana wa Israeli, hatimaye Musa alitumwa tena Misri na kisha akawezeshwa kuvunja nira ya Misri. Kuongeza miaka 40 kwa 1890 B.K, tunaletwa mwaka wa 1930, mwaka ambapo Fimbo ya Mchungaji, Gombo la 1, lilichapishwa mara ya kwanza, likitangaza katika dhehebu la Waadventista wa Sabato ya kwamba “Na mwaka wao niliowakomboa umewadia” siku ambayo “Bwana atapeleka mkono wake mara ya pili, ili ajipatie watu wake watakaosalia.” Isa. 63: 4, 11:11. Hivyo wito wa Musa

69

kwa kweli kuwaokoa Israeli kutoka utumwa wa Misri unalingana na kuwasili kwa Fimbo ya Mchungaji, ukidai utiifu kwa sheria ya Mungu, ukitangaza ukweli wa watu 144,000, na kutangaza kwamba huu ndio wakati wao kuokolewa kutoka kwa utawala wa Mataifa. {SR1P: 69.2}

Zaidi ya hayo, tangu wakati Abrahamu alipoamua kumfuata Bwana, hadi kuzaliwa kwa Yakobo, ulikuwa na miaka 85. Na tangu mwanzo wa Dhehebu la Waadventista wa Sabato, kuanzia njozi ya kwanza ya mwasisi wake, ambayo ilikuwa juu ya watu 144,000, hadi kuzaliwa kwa ujumbe wa Fimbo ya Mchungaji, pia ulikuwa na miaka 85. {SR1P: 70.1}

Ulinganifu huu wote hasa kwa wakati na lengo sasa unaweza kwa haraka na urahisi zaidi kufahamika katika —

MUHTASARI. {SR1P: 70.2}

Uamuzi wa Abrahamu kumtumikia Bwana mwaka wa 2083 B.U. (miaka kutoka kwa uumbaji) kulingana na kugeuka kwa Luther kziacha shughuli za kidunia hadi za kiroho mwaka wa 1500 B.K.; Kuteta kwa Sara dhidi ya Hajiri na Ishmael mnamo 2113 B.U. kunalingana na kuteta kwa Waprotestanti dhidi ya kanisa mnamo 1530 B.K.; kuzaliwa kwa Musa tumaini la Waisraeli wa kale, mwaka 2433 B.U., kunalingana katika mwaka 1850 B.K. na kuzaliwa kwa Ushuhuda wa Kwanza, tumaini la Israeli mamboleo — ukisimulia kuhusu watu 144,000, Israeli mamboleo. {SR1P: 70.3}

Na jaribio la Musa na kushindwa kuwakomboa Israeli mwaka 2473 B.U. linalingana na jaribio na kushindwa kwa Chama cha Uhuru wa Kiroho

70

cha Waadventista wa Sabato, na kukataa kwao ujumbe wa haki kwa Imani, — na kulisababisha pia Dhehebu mwaka wa 1890 B.K. kuingia na kukaa miaka 40 nyikani, hivyo kwa kusema. {SR1P: 70.4}

Mwishowe, kuwasili kwa Musa Misri na ufanisi wake kuliweka huru jeshi la Waebrania na kurudisha utaratibu na uhuru wa kiroho mwaka wa 2513 B.U., kunalingana na kuwasili kwa Fimbo ya Mchungaji mwaka wa 1930 B.K., na kwa jaribio lake kukamilisha uhuisho na matengenezo na kuwaweka huru Israeli wa sasa. {SR1P: 71.1}

(Katika mifano mingine ulinganifu wa matukio yanaweza kuwa, kwa kalenda yetu ya sasa, kuonekana kuwa mwaka mbele au mwaka nyuma, kwa ada na ukweli kwamba mwezi wa kwanza wa kalenda ya Musa upo katika mwezi wa nne wa mwaka wa kalenda ya sasa. Kwa mfano, tazama Mleta Jibu, Kitabu cha. 3 uk. 49, 50, toleo la 1944.) {SR1P: 71.2}

Kwa hivyo, mtu yeyote anaweza kuona kwamba miaka 430 ya asili na matukio yake yaliyosokotana kutoka wakati Abrahamu alipoondoka Ur hadi wakati Musa na fimbo ya Bwana alipoondoka Misri na kupeana sheria pale Mlima Sinai, ni sawa na miaka 430 ya uakisi tangu wakati Luther aliwacha kujifunza sheria na kuanza kujifunza Biblia, hadi mwaka ambapo Fimbo ya Mchungaji ilitangaza kutiwa muhuri watu 144,000, ukombozi wa Israeli mamboleo. {SR1P: 71.3}

Matukio haya yanayo uwiana sasa yanasimulia na kuonekana wazi zaidi kwenye ramani inayofuata: {SR1P: 71.4}

71

72

Matukio haya yote ya kisasa yakiwa sawa kikamilifu na ya kale kwa wakati na lengo, kwa hakika yanathibitisha ukweli kwamba kazi ya Fimbo ya Mchungaji iliagizwa mbeleni na Mungu na kwa wakati wake sasa jinsi ilivyokuwa kazi ya Musa na fimbo yake wakati wake. Moja ni ya baadaye kwa uzito kutia nguvu kuutambua muundo wa majaaliwa ya Mungu na kuyajua mbele maslahi ya milele ya msomaji kwa maelfu ya miaka kabla. {SR1P: 73.1}

Hivyo, kuzitwaa kabisa silaha za Adui wa myoyo, Mbunifu mkuu wa kweli hizi za taipolojia humuacha msomaji huru kufanya uamuzi wake mwenyewe iwapo ataendelea gizani au ajitokeze aingie katika Nuru ya Bwana, kutoendelea kustaajabu ni kanisa gani atajiunga, au ni nini ukweli na ni nini kosa. {SR1P: 73.2}

Aweze sasa kuangalia “Jinsi ilivyo mizuri juu ya milima Miguu yake aletaye habari njema, Yeye aitangazaye amani, Aletaye habari njema ya mambo mema, Yeye autangazaye wokovu, Auambiaye Sayuni, Mungu wako anamiliki!” Isa. 52: 7. {SR1P: 73.3}

Sasa swali ni “nini kilichofanya mageuzi makubwa,” “nini kilicholeta ukweli huu wa utukufu,” limejibiwa — kuwasili kwa wakati unaofaa kwa mjumbe huyu wa kimya aliyetabiriwa. {SR1P: 73.4}

Hatimaye kwa kuwa umefahamishwa sawa sawa pale ambapo usalama wa mtu upo na hatari ya mtu inamuotea, wewe, msomaji mpendwa, bila shaka una hamu kujua ubora na kiwango cha chakula cha kiroho umekuwa ukila na

73

sasa unakula. Awamu hii ya taipolojia imefunuliwa kwa uaminifu zaidi na kwa usahihi katika

EZEKIELI NNE. {SR1P: 73.5}

“Wewe nawe, mwanadamu, jipatie tofali uliweke mbele yako, kisha, chora juu yake mfano wa mji, yaani, Yerusalemu.” Ezek. 4: 1. {SR1P: 74.1}

Ezekieli aliamuriwa kuchora mji juu ya kigae na kuuita Yerusalemu. Kitu ambacho mji huo ungechorwa kikiwa ni cha kudumu — kisichoweza kuoza — kinaashiria kwamba mji unaoangaliwa ni ule ambao utasimama milele: watu ambao hawatakufa kamwe. {SR1P: 74.2}

“Angalia Sayuni, mji wa sikukuu zetu; macho yako yatauona Yerusalemu umekuwa kao la raha; hema isiyotanga-tanga; vigingi vyake havitang’olewa, wala kamba zake hazitakatika. {SR1P: 74.3}

“Bali huko Bwana atakuwa pamoja nasi, mwenye adhama; mahali penye mito mipana na vijito, pasipopita mashua na makasia yake; wala hapana merikebu ya vita itakayopita hapo….. {SR1P: 74.4}

“Wala hapana mwenyeji atakayesema, Mimi mgonjwa; watu wakaao humo watasamehewa uovu wao.” Isa. 33:20, 21, 24. {SR1P: 74.5}

“Ukauhusuru, ukajenge ngome juu yake, na kufanya boma juu yake; ukaweke makambi juu yake, na kuweka magogo ya kuubomoa yauzunguke pande zote.” Ezek. 4: 2. {SR1P: 74.6}

Ku “uhusuru, inamaanisha, bila shaka, kuuvamia kwa na jeshi la watenda kazi ya matengenezo na kuulazimisha kujisalimisha —

74

Kuja kwa ujuzi wa ukweli ambao umefunuliwa hapa ndani. Kwa hivyo ni wazi,hatimaye, kwamba ujumbe wa sasa, na huo tu, unapaswa kuwasilishwa mbele ya watu wa Mungu. {SR1P: 74.7}

“Na kujenga ngome dhidi yake” — hakikisha kwamba hakuna yeyote atakayeokoka, mwema au mbaya. {SR1P: 75.1}

Kisha “kufanya boma”; usilegeze juhudi, na chukua tahadhari ili uuhifadhi mji. {SR1P: 75.2}

“Ukaweke makambi pia juu yake”; yaani, jenga mahali pa makaazi ya muda kwa ajili ya watenda kazi wako, Makao makuu ambapo utaendelezea kazi, na kufanya matayarisho ya kubaki pale mpaka umeutwaa mji. Hili ni kusudi la wakifu katika kukijenga Kituo cha Mlima Karmeli, hili ni lengo lake lililopewa. {SR1P: 75.3}

Pia “weka magogo ya kuvunjia boma vitani [viongozi wakuu] dhidi ya” mji “pande zote.” Chombo ambacho wanavunjia, bila shaka, ni ukweli dhahiri wa Biblia, wa kukata, na wa kushawishi. Na hili ni hitaji muhimu na dhahiri kuwa kwa kila tawi la kazi watu wenye uwezo wa kuongoza kwa busara. {SR1P: 75.4}

“Kisha ukajipatie bamba la chuma, ukalisimamishe liwe ukuta wa chuma kati ya wewe na mji huo; ukaelekeze uso wako juu yake, nao utahusuriwa, nawe utauhusuru. Hili litakuwa ishara kwa nyumba ya Israeli.” Ezek. 4: 3. {SR1P: 75.5}

Hiyo ni, wakati hili linafanyika katika nyumba ya uakisi ya Yuda, litasimama kama ishara ambayo nyumba ya uakisi ya Israeli itaonywa. {SR1P: 75.6}

Kisha itakuwa kwamba ” Na wana wa watu wangu watakapokuambia, wakisema,

76

Je! Hutatuonyesha maana ya mambo hayo utendayo? {SR1P: 75.7}

Waambie, Bwana MUNGU asema hivi; Tazama, nitakitwaa kijiti cha Yusufu, kilicho mkononi mwa Efraimu, na kabila za Israeli wenzake, nami nitawaweka pamoja nacho, yaani, pamoja na kijiti cha Yuda, na kuvifanya kuwa kijiti kimoja; navyo vitakuwa kimoja mkononi mwangu. {SR1P: 76.1}

“Navyo vijiti, ambavyo uliandika juu yake, vitakuwa mkononi mwako mbele ya macho yao” {SR1P: 76.2}

“Na mataifa watajua ya kuwa mimi ndimi Bwana, mimi niwatakasaye Israeli, patakatifu pangu patakapokuwa katikati yao milele.” Ezek. 37: 18-28. {SR1P: 77.4}

Jinsi mkuu wa majeshi anavyoweka uso wake dhidi ya taifa la adui kwa nia ya kulishinda, ndivyo Ezekieli wa uakisi alivyoamriwa kuanza huu “uhuisho na matengenezo” ya dharura miongoni mwa watu wa Mungu. {SR1P: 77.5}

“basi mtu awaye yote aisikiaye sauti ya tarumbeta, wala haonywi, upanga ukija na kumwondoa, damu yake itakuwa juu ya kichwa chake mwenyewe.” {SR1P: 77.6}

“Aliisikia sauti ya tarumbeta, wala hakuonywa; damu yake itakuwa juu yake; lakini kama angalionywa, angalijiokoa roho yake.” Ezek. 33: 4, 5. {SR1P: 77.7}

77

“Maana nimekuagizia miaka ya uovu wao iwe kwako hesabu ya siku, yaani, siku mia tatu na tisini; ndivyo utakavyouchukua uovu wa nyumba ya Israeli. Tena utakapozitimiza hizo, utalala kwa ubavu wako wa kuume, nawe utauchukua uovu wa nyumba ya Yuda; siku arobaini, siku moja kwa mwaka mmoja, nimekuagizia. Ezek 4: 5, 6. {SR1P: 78.1}

Katika uwasilishaji huu wa ki-mfano kuhusu hatima ya nyumba ya Israeli (ufalme wa kabila kumi) na wa nyumba ya Yuda (ufalme wa kabila mbili), wakati wa uhamisho wao kati ya watu wa mataifa, mbali na nchi yao, unasimama kwa ukuu kutazama ukweli kwamba akiwa amelala upande wake wa kushoto Ezekiel anaonyesha nyumba ya Israeli katika uovu wao kwa muda wa miaka 390, na kwamba akiwa amelala upande wake wa kulia yeye anaonyesha nyumba ya Yuda katika uovu wao kwa kipindi cha miaka 40. {SR1P: 78.2}

“Na tazama, nitakutia pingu, wala hutageuka toka upande mmoja hata upande wa pili, hata utakapozitimiza siku za mazingiwa yako.” Ezek. 4: 8. {SR1P: 78.3}

Ezekieli akiwa amefungwa bila kugeuka, anaonyesha kwa mfano uhakika na kutoweza kuiepuka adhabu ambayo watu wake kwa ajili ya uovu wao watabeba wakati wa kipindi cha miaka iliyotabiriwa.{SR1P: 78.4}

“Pia ujipatie ngano, na shayiri, na kunde, na dengu, na mtama, na kusemethi, ukavitie vyote katika chombo kimoja, ukajifanyie mkate kwa vitu hivyo; kwa kadiri ya hesabu ya siku utakazolala ubavuni mwako; yaani, siku mia tatu na tisini utaula….. Nawe utakila kama mkate wa shayiri, nawe utakioka mbele ya macho yao juu ya mashonde

78

yatokayo katika mwanadamu Bwana akasema, Hivyo ndivyo wana wa Israeli watakavyokula chakula chao, hali kimetiwa unajisi, kati ya mataifa nitakakowafukuza. “Ezek. 4: 9, 12, 13. {SR1P: 78.5}

Hii ndio adhabu ambayo itapimiwa kwa nyumba ya Israeli wakati wa miaka ya uhamisho wake kati ya Mataifa. Na wala historia takatifu au ya ulimwengu zimenakili kwamba watu wa Mungu daima walipasishwa kwa chakula kilichotayarishwa hivyo, ukweli huo umethibitishwa kikamilifu kwamba unabii huu wote ni mafumbo. Kwa hivyo, nafaka sita, zaweza kuwakilisha chakula cha kiroho tu kama vile nafaka za mazao mahali pengine katika Maandiko. Je! Vinaanza lini vipindi viwili (miaka 390 na miaka 40)? — Ni dhahiri si wakati ule Samaria, mji mkuu wa ufalme wa kabila kumi, ulivamiwa na Ashuru, wala wakati ule Yerusalemu, mji mkuu wa ufalme wa kabila mbili, ulizingirwa na Babeli, maana Ezekiel mwenyewe, sio mfalme wa Mataifa, atauhusuru Yerusalemu na kuuteka, usiokoke . {SR1P: 79.1}

Wala kipindi hicho hakikuweza kukamilika kwa kurejea Yuda kutoka Babeli hadi Yerusalemu walipokuwa wakijenga tena hekalu na mji, kwa kuwa Yuda ulikuwa uhamishoni miaka 70 tu, sio miaka 430. {SR1P: 79.2}

Na mwisho, kabila kumi, nyumba ya Israeli, hajawahi hata siku ya leo kurudi katika nchi yao. {SR1P: 79.3}

Mfano wote lazima uwe unabii wa kanisa katika kipindi

79

cha Kikristo. Na iwapo Ezekieli, mfano wa watumishi wa Mungu, bado hajauteka Yerusalemu, wakati wa ushindi wake bado ni wa baadaye. {SR1P: 79.4}

Lakini ni lini hasa kipindi kinaanza? — Jibu la pekee la akili ni: Wakati adhabu zinaanza kutekelezwa. Kwa hivyo, ni lazima tuhakikishe wakati ambapo watu wa Mungu waliotawanyika wamekuwa au wanapasishwa kula chakula kilichoandaliwa kama ilivyoelezwa katika Ezek. 4: 9 -13. {SR1P: 80.1}

Kwa kuwa nafaka ni mfano wa chakula cha kiroho, mafundisho, basi chombo kimoja ambacho zimewekwa mwanzo kinaweza tu kuwa mfano wa Biblia. Na inafuata kwa kujua kwamba katika hali yao ya asili, kabla ya kuokwa, lazima ziwakilishe mafundisho ambayo hayajafafanuliwa, yasioeleweka; na kinyume chake, wakati zimeandaliwa kuwa mikate na kuokwa, lazima ziwakilishe mafundisho yaliyotafsiriwa na kuchapishwa, tayari kusambazwa na kueleweka vyema — kuhubiriwa, kuaminiwa, na kuwa tabia. {SR1P: 80.2}

Katika kipindi cha miaka 390, Ezekiel alipaswa kula nafaka kidogo kidogo, “kwa kipimo,” na najisi, “zilizo okwa kwa moto wa mavi”. Moto kutoka kwa kuni au makaa ya mawe (chanzo asili) ni mfano wa nguvu za Roho Mtakatifu (Watenda Kazi wa Injili, uk. 22-23; Matendo 2: 3), kisha moto kutoka kwa mavi (chanzo ambacho si asili) lazima kiwe mfano wa nguvu ya kigeni kwa Roho Mtakatifu: hususan Shetani kuwavuvia wakala wa kibinadamu kushiriki katika tafsiri za “kibinadamu” za Maandiko — kitu kinachotia unajisi. {SR1P: 80.3}

80

Ukweli usioepukwa wa hitimisho hili umeonyeshwa kikamilifu zaidi kwa kuandika wazi vipindi vya kufuatana ambapo nyumba ya Israeli ilipokea mafundisho sita, yaliyo kwa mfano wa nafaka sita tofauti, ambazo zilipaswa kuendeleza maisha ya kiroho ya watu katika kipindi cha miaka 390. {SR1P: 81.1}

Inaeleweka sana kwamba kutoka wakati kanuni ya kanisa iliwekwa kwa Maandiko ya Agano Jipya hadi kwa wito wa Martin Luther, Ukweli ulitupwa chini (Dan 8:12), na kwamba ulianza kuinuliwa, kwanza na Walutheri ‘waliohubiri fundisho la Imani — mwanzo wa Matengenezo; kisha likafuatwa na sehemu kwa wakati, mtawalia na mahubiri ya Waprestiberi wakifudisha juu ya Roho Mtakatifu; na Wamethodisti wakihubiri fundisho la Neema; na Wabaptisti wa siku ya kwanza wakihubiri fundisho la Ubatizo; na Waadventista wa siku ya Kwanza fundisho la 2300 (Danieli 8:14), na kusababisha ufahamu sahihi wa ukweli wa Hekalu; na Wabaptisti wa Sabato wakihubiri ukweli wa Sabato. Mwisho Waadventista wa Sabato, na wao tu, waliyakumbatia mafundisho haya yote, kwa kutiwa Nuru na Mungu tu. {SR1P: 81.2}

Haya mafundisho sita, pamoja na masomo yanayohusiana nayo, ndio pekee yaliokuja kwa kanisa kutoka 1500 hadi 1930 B.K. Na jinsi hakuna mwanafunzi wa Biblia mwaminifu ataweza kuukataa ukweli kwamba kila moja kwa zamu limenajisiwa na tafsiri za kibinadamu,

81

Kuongeza na kuondoa (kuoka kwa moto wa mashonde), ukweli unasimama wazi zaidi kwamba nafaka sita ni mfano wa mafundisho haya sita, na kwamba kwa kufuatana yamehubiriwa tangu mwanzo wa Matengenezo ya Kiprotestanti. {SR1P: 81.3}

Sasa katika kuleta kwa mtazamo awamu nyingine ya kufanana, — kwamba kila nafaka ina tabia ya msingi ya mafundisho ambayo inawakilisha, — ukweli bado utaonekana katika miale inayong’aa zaidi. {SR1P: 82.1}

Kama ngano, nafaka ya kwanza katika mfano, kawaida ni ya kwanza kwa lishe ya kimwili, hivyo Imani, la kwanza kwa mafundisho katika Matengenezo, ni la kwanza naam, kanuni ya kwanza, katika chakula chake cha kiroho. Vivyo hivyo, kama vile bila ngano haiwezekani kukidhi mahitaji yetu ya kimwili, vivyo hivyo “bila imani haiwezekani kumpendeza” Yule Mtakatifu au kuanza maisha ya Kikristo. {SR1P: 82.2}

Vile vile, kama shayiri, nafaka ya pili katika mfano, ni ya pili katika lishe ya mwanadamu ya kimwili, hivyo Roho Mtakatifu, fundisho la pili katika Matengenezo, ni sehemu ya pili, kanuni ya pili, katika chakula chake cha kiroho. Baada ya kusikia sana Mmidiani akisimulia kuwa katika ndoto aliona keki ya shayiri ikivingirisha ndani ya hema yake na kuipindua, Gideoni mara moja alielewa keki ya shayiri iliwakilisha kazi ya Roho — ufunuo kwake kwenda dhidi ya Wamidiani. {SR1P: 82.3}

Maharagwe, aina ya tatu katika mfano, kawaida ni ya tatu kwa lishe ya mtu kimwili:

82

vile vile Neema, fundisho la tatu katika Matengenezo, ni sehemu ya tatu, kanuni ya tatu, katika chakula chake cha kiroho. {SR1P: 82.4}

Na jinsi dengu, aina ya nne ya chakula katika lishe ya kimwili, hazipendwi ulimwenguni kote kama maharagwe, vilevile Ubatizo wa kuzamishwa, fundisho la nne katika Matengenezo, na hivyo sehemu ya nne, kanuni ya nne, katika chakula cha kiroho, zinaheshimiwa kidogo sana na kutokuwa mazoea kuliko Neema. {SR1P: 83.1}

Nafaka ya tano, mtama, aghalabu haujulikani wala hautumiwi, na kwa ujumla huonekana kuwa wa thamani kidogo, manyasi ya mwitu tu, ingawa kwa kweli ni muhimu kwa nyasi na nafaka. Hivyo kwa kile unachowakilisha: Siku 2300, kufunua mwanzo wa Hukumu, fundisho la tano katika Matengenezo, sehemu ya tano, kanuni ya tano katika chakula cha kiroho cha Mkristo, inajulikana na inaaminiwa na wachache tu. {SR1P: 83.2}

Kusemethi, nafaka ya sita, “aina ya ngano ya kudumu, ilijulikana katika nyakati za mwanzo,” inawakilisha kikamilifu fundisho la sita katika Matengenezo, kanuni ya sita katika dini ya Kikristo — Sabato ya Siku ya saba ikihusiana na hekalu, ya zamani, ya kudumu, mafundisho mawili ya Biblia ambayo yanaadhimishwa kwa uchache. {SR1P: 83.3}

Hatua ya mwisho katika sayansi ya kutengeneza keki ni kuoka, kisha kuandalia; na hatua ya mwisho katika maandalizi ya mafundisho ni kuyaandika, kisha kuyahubiri. {SR1P: 83.4}

83

Ingawa nafaka ni uumbaji wa Mungu, kuonyesha kwamba mafundisho ambayo zinawakilisha ndani yake zenyewe ni ukweli wa Mungu, lakini Ezekieli katika maono akioka mikate ya mfano juu ya moto wa mashonde, yanaonyesha kwamba mafundisho haya yamenajisiwa – kufafanuliwa visivyo, yameongezwa na kuondolewa kwayo — kama, kukatwa vipande vidogo, kisha kuandaliwa. {SR1P: 84.1}

Kuwaweka chini nyumba ya Israeli kwa chakula kama hicho wakati wa miaka 390, na nyumba ya Yuda kwa saumu wakati wa miaka 40 iliyofuata, Mungu aliwaadhibu wote wawili kwa uovu wao. {SR1P: 84.2}

Saumu ndefu ya Yuda hatimaye inapokwisha, basi bila shaka wataanza kupokea mkate safi, ukweli usiotiwa unajisi, kwa haraka na kwa kiasi kikubwa jinsi mahitaji yao yatakavyoitisha, na kuanzia hapo watakula chakula na kunywa maji daima bila kipimo wala mshangao. Haya watapata kuona, lakini hata baada ya miaka 430 kukamilika, wakati ambapo mji utatekwa na watu kuwekwa huru kutoka kwa nira ya mabwana wao wote — wanafiki, wanaochukiza, na wasiomcha Mungu. {SR1P: 84.3}

Na mwishowe, wakati Yerusalemu, nchi yao, nchi ya ahadi, imewekwa huru kutoka kwa utawala wa Mataifa, “nyakati za Mataifa zinapotimia,” basi watoto hawa waliookolewa wa “mateka wa binti Sayuni” waliohamishwa (Isaya 52: 2) , “kurejea, na kumtafuta Bwana Mungu wao, na Daudi mfalme wao, nao watamcha Bwana na wema Wake.” Hos. 3: 5. Kisha watahakikishiwa daima

84

hata kwa usambazwaji mkubwa zaidi wa safi, usiotiwa unajisi (Uvuvio) Ukweli. {SR1P: 84.4}

Basi mimi nitaliokoa kundi langu, asema Bwana, wala hawatakuwa mateka tena; nami nitahukumu kati ya mnyama na mnyama. Nami nitaweka mchungaji mmoja juu yao, naye atawalisha, naam, mtumishi wangu, Daudi; yeye atawalisha, naye atakuwa mchungaji wao. Na mimi, Bwana, nitakuwa Mungu wao, na mtumishi wangu, Daudi, atakuwa mkuu kati yao; mimi, Bwana, nimesema haya. Ezek. 34: 22-24. {SR1P: 85.1}

Ukweli kwamba watu wa Mungu tangu mwaka wa 1930 wamekuwa wakipokea usambazaji unaoongezeka wa ukweli safi (uliofunuliwa na Mungu) kwa mikono ya mmoja, ni ushahidi ndani yake kwamba siyo tu karamu iliyotiwa unajisi na miaka 390 imekwisha, ila pia saumu ya miaka 40. Hakuna haja tena, kwa hivyo, yeyote kujilisha keki zilizookwa juu ya mashonde, au kufunga saumu. {SR1P: 85.2}

Sasa, kwa kuondoa miaka 430 kutoka 1930 B.K., tunapata 1500 A.D., wakati Roho aliongoza Matengenezo ya Kiprotestanti. Na kama vile nafaka zilizonajisiwa (mafundisho) kwa miaka 390 yalihubiriwa kwa mikutano ya Waprotestanti, na ila pia kwa saumu ya miaka 40 (kutokuwepo kwa Ukweli endelevu) ilitukia katika Dini ya Waadventista wa Sabato. Kweli mbili zinajitokeza wazi: kwanza, kwamba Waprotestanti katika mfano huu wanaitwa “nyumba ya Israeli”; na pili kwamba Waadventista wa Sabato wanaitwanyumba ya Yuda

85

Mtengano ambao Mungu alileta katika ufalme wa Sulemani kwa kweli unaashiria mtengano ambao upo kati ya watunza Sabato na watunza Jumapili. {SR1P: 85.3}

Sikiliza mjumbe wa Bwana, akiwaonya watunza-Sabato kuhusu kuzidisha saumu ambayo wangepaswa kupata: {SR1P: 86.1}

“Nimeagizwa kutoka kwa Mungu kukwaambia kwamba hakuna mshale mwingine wa nuru kupitia Shuhuda utaangaza kwenye njia yako, mpaka utakapoweka kwa matumizi ya vitendo nuru ambayo umepewa tayari.” — Shuhuda, Gombo la 2, uk. 606. {SR1P: 86.2}

Zaidi ya hayo, Yerusalemu, basi ikumbukwe, ni mji mkuu wa Yuda. Hivyo kuuhusuru kwa sasa “mji” (dhehebu la Waadventista wa Sabato) inakuwa ishara kwa watunza Jumapili; yaani, kumeundwa ili kuwaamsha kwa ufahamu wa jinsi Bwana anapaswa kuabudiwa, na pale ambapo ukweli wa kuokoa unapatikana; wa kuanza kwa “siku kuu na ya kutisha ya Bwana,” na hukumu Yake, pia kuwaleta kwa ufahamu kwamba iwapo “inaanza katika nyumba ya Mungu,” utakuwaje “mwisho wao wasiotii Injili ya Mungu? ” 1 Pet. 4: 17. {SR1P: 86.3}

Hakuna sasa tena haja ya mwaminifu-mtafuta ukweli kutembea kuzurura kutoka kanisa hadi kanisa, kutafuta kwa kupapasa kupitia msitu usio na mwisho wa giza nene wa vitabu vya dini za kidunia katika kutafuta kanisa sahihi na fundisho sahihi. Yote mawili sasa yametambulika wazi, yakimpa changamoto atakayevichukua

86

vyombo vya Bwana, kuwa safi, kutokigusa kile ambacho kimeokwa kwenye moto wa “mashonde” – kile ambacho hakijavuviwa na Roho wa Kweli — na daima kuwa mwangalifu sana ya kuwa hakuna ukweli mpya uliofunuliwa ulipelekwa kwa kanisa wakati wa miaka arobaini kuanzia 1890 hadi 1930, na hivyo kila mtu anayejidai kwa ujumbe kutoka mbinguni katika kipindi hicho alikuwa ni muongo. {SR1P: 86.4}

Lakini kwa saumu ya muda mrefu sasa imekatizwa na ukweli mpya, mwingi na ambao haujatiwa unajisi kwa hekima ya mwanadamu, walio na njaa sasa wanakula kwenye meza ya wingi ya Fimbo (Mika 7:14), ambayo wewe, msomaji mpendwa, sasa umeketi na kwa furaha umealikwa kuendelea kukaa muda wote wa karamu uliosalia. {SR1P: 87.1}

Hautafanya hili? Ikiwa ungependa, basi tu ulifanye lijulikane, na wingi wote, usio na mshindani, karamu ya kuokoa maisha itawekwa mara mbele yako bila kipimo na bila kununua! {SR1P: 87.2}

Mwenyewe hasa sasa umewasili kwa wakati wa kudumu “uhuisho na matengenezo” –

KINA MAMA, SASA FANYA MWITO WENU WA MWISHO. {SR1P: 87.3}

Na Bi. E. Hermanson

“Lakini mtumwa yule mbaya akisema moyoni mwake, Bwana wangu anakawia; akaanza kuwapiga wajoli wake, na kula na kunywa pamoja na walevi; bwana wake mtumwa huyo atakuja siku asiyodhani, na saa asiyojua, atamkata vipande viwili,

87

na kumwekea fungu lake pamoja na wanafiki; ndiko kutakuwako kilio na kusaga meno.”Mat. 24: 48-51. {SR1P: 87.4}

Uvuvio unafundisha kwamba kula kwake na kunywa na walevi hakumaanishi tu kunywa divai. Mtu anaweza kulewa kwa kushirikiana na roho ya ulimwengu, na pia kwa kushughulika sana “masumbuko ya maisha haya.” Luka 21:34. {SR1P: 88.1}

Na kufanya yote haya ni kusema moyoni, “Bwana wangu anakawia.” “tule, tunywe, kwa maana kesho tutakufa” Mat. 24:48; Isa. 22:13. {SR1P: 88.2}

Nikiwa mshiriki wa dhehebu la Waadventista wa Sabato, na mama wa watoto watatu, nia yangu imekuwa ni kuwafundisha kuweka upendo wao, sio kwa njia za ulimwengu ila juu ya Njia ya Kweli na Haki. Mama waaminifu wanajua kwamba kazi na wajibu sio mwepesi au rahisi. Na kwa hakika haujapunguzwa na ushawishi wa kidunia kutoka ndani ya kanisa, unaofanya kazi ya kujenga mimba ya udanganyifu kwa kile ambacho Mungu anatarajia kwa watoto wake. {SR1P: 88.3}

Shughuli kama zile zilizo orodheshwa katika matangazo yafuatayo, yaliyotolewa na Kanisa la Waadventista wa Sabato la Ukumbusho wa White la Los Angeles, California, ni mifano ya ushawishi ule: {SR1P: 88.4}

HABARI ZA CHAMA

Kitivo cha Kati ya wa Elimu ya Juu–Waliohitimu Awali Kukutana Kuogelea: … Jambo kuu la kutazamwa jioni lilikuwa maonyesho ya kupiga mbizi na Georgia Coleman, bingwa wa kitaifa kwa wanawake wa kupiga mbizi…. {SR1P: 88.5}

88

Chama cha Karamu ya jioni Novemba: Hiki chaahidi lishe ya aina yake. Watatu-pamoja na msomaji kutoka chama cha Wanawake cha Glee cha U.S.C. atakuwa kivutio kikuu. Bill Hunter, Mkurugenzi wa Wanariadha wa U.S.C. atatusimulia machache juu ya michezo. Pata tiketi zako mapema. {SR1P: 89.1}

MATUKIO YAJAYO

Nov. 24: Chama cha Karamu ya jioni.

Nov. 25: Wadogo dhidi ya Wafanyakazi Mchezo wa Besiboli.

Nov. 28: Mashindano ya michezo ya Golfu Mechi itakuwa kwenye Montebello Park.

Desemba 2: Kitivo dhidi ya Watumishi Mchezo wa Besiboli.

Desemba 9: Kitivo dhidi ya Wadogo Mchezo wa Besiboli, saa 1:00.

Wafanyakazi timu ya 1 dhidi ya Wafanyakazi timu ya 2, saa 11:00.

Desemba 16: Wakubwa dhidi ya Wadogo Mchezo wa Besiboli.

Desemba 21-26: Karamu ya Likizo ya kijumba melini, Ziwa la Dubu Mkubwa.

Hotuba ya Afya, Y.M.C.A., Ijumaa, saa 2:00 usiku {SR1P: 89.2}

HABARI ZA JUMUIA

Kitivo-Wenye elimu ya Juu Shindano Mchezo Golfu: Ijumaa asubuhi Novemba 28, Chama cha Golfu Bustani ya Montebello…. {SR1P: 89.3}

Kitivo-wazima mchezo wa Besiboli Jumanne iliyopita ulisababisha alama 3-13. Hii, hata hivyo, haifai kwa hakika kuwakilisha u karibu wa shindano ikilinganishwa na makabiliano yaliyopita. Michezo michache zaidi na kitivo watakuwa wakishikilia yao wenyewe, hata hivyo, H____ S____ na W___ hawatakawia mbio nyingi za nyumbani. H____ inashikilia rekodi hadi sasa ….  — “Matangazo ya kila wiki,” Novemba 14 na 21, 1930.  {SR1P: 89.4}

Ndani ya nuru ya onyo wazi la Uvuvio, ratiba kama hizi hazina nafasi katika

89

Taasisi zetu ikiwa tunapaswa kuwavutia watoto wetu na vijana katika mafundisho wazi, yasiyopinda ya Mwokozi wetu. Fikiria hilo, wachungaji na walimu Waadventista wa Sabato wanafadhili mipango kama hii! Akili changa kwa kawaida hazifahamu upande mzito wa maisha, na kwa tarehe na hafla nyingi ambazo huwekwa mbele yao daima kwa njia hii, wanawezaje kupendezwa kujitahidi kuingia kupitia mlango ulio mwembamba? {SR1P: 89.5}

Kushughulikia maswala ya anasa, mtumishi wa Bwana anasema, “Naliambiwa na Mwelekezi wangu: ‘Angalia, na tazama ibada ya sanamu ya watu Wangu, ambao nimekuwa nikisema, na kuamka mapema, na kuwaonyesha hatari zao. Nikaona kwamba wangezaa matunda.’ Walikuwapo baadhi waliokuwa wakijitahidi kufanya kwa ustadi, kila mmoja akijaribu kumshinda mwingine kukimbia kwa kasi ya baiskeli zao. Palikuwa na roho ya ugomvi na ushindani kati yao kuhusu ni nani aliyepaswa kuwa mkuu zaidi. Roho ilikuwa sawa na ile iliyodhihirishwa katika michezo ya besiboli kwenye uwanja wa chuo. Akasema Mwongozi wangu: ‘Mambo haya ni makosa kwa Mungu. Kote karibu na mbali watu wanaangamia kwa ajili ya mkate wa uzima na maji ya wokovu.'” — Shuhuda, Gombo la 8, uk. 52. {SR1P: 90.1}

Kwa nini kuwapeleka vijana kwa Y.M.C.A.? Je, haingewezekana hotuba ya afya ifanywe katika kanisa letu au katika kumbi za shule? {SR1P: 90.2}

90

Kwa nini mashindano ya Klabu ya Golfu asubuhi ya Ijumaa? Je! Hatukuambiwa katika Maandiko kuwa Ijumaa ni siku ya maandalio ya Sabato, si siku ya anasa? Kama sheria, iwapo mtu anafanya maandalizi mazuri, hakuna wakati mwingi wa kupoteza katika kucheza kitu chochote. {SR1P: 91.1}

Hatuwezi kuwa na pingamizi kwa uogeleaji, lakini ni athari gani ya onyesho la ujuzi wa michezo ya ubingwa na majadiliano ya namna hii kuhusu “Michezo” kwa vijana? Je, yatajenga ari kubwa ndani yao kumtumikia Kristo? Makapi ni nini kwa ngano? {SR1P: 91.2}

Tunawezaje kama kina mama kuwatunza watoto wetu mbali na ulimwengu iwapo kitivo cha shule kinawapeleka kwenye taasisi za kidunia ambamo wao hutupwa ndani ya mahusiano na machafuko mseto? Je, tunaishi kulingana na kanuni ambazo Dhehebu letu la Waadventista wa Sabato lilianzishwa? {SR1P: 91.3}

Roho wa Kweli sasa anahimiza tena: “Kwa maana sisi tu hekalu la Mungu aliye hai; kama Mungu alivyosema, ya kwamba, Nitakaa ndani yao, na kati yao nitatembea, nami nitakuwa Mungu wao, nao watakuwa watu wangu. Kwa hiyo, Tokeni kati yao, Mkatengwe nao, asema Bwana, Msiguse kitu kilicho kichafu, Nami nitawakaribisha. 2 Wakor. 6:16, 17. {SR1P: 91.4}

Hali haijabadilika bora hata baada ya Fimbo kuteta kwanza, inathibitishwa na taarifa zaidi zifuatazo: {SR1P: 91.5}

91

SAA YA WACHEZAJI WASIO WA KULIPWA

ONYESHO LA AJABU SANA

la

1 9 4 3

UKUMBI WA PAULSON

Cor. Jimbo la Michigan

JUMAMOSI. USIKU OKT. 9 saa 2:00 usiku

ZAIDI YA DOLA ZA MAREKANI 50.00 ZITAPEANWA

KWA WASHINDI

MASAA MAWILI YA –

KUCHEKA !!!

MACHOZI!!!

BARIDI !!!

KUPIGA MAYOWE !!! na

MASTAAJABU !!!

Kliniki Kufaidika na Mapato

Kutoka kwa Hafla hii ya Tamasha

Inadhaminiwa na

WANAWAKE WA KUSAIDIA WA C.M.E.

92

Fikiria kuiweka nyumba ya Mungu kwa matumizi ya kipagani kama haya! Ajabu yoyote kwamba Mungu anasema: {SR1P: 93.1}

“Ni nani anayeweza kusema ukweli, ‘Dhahabu yetu imejaribiwa kwa moto, mavazi yetu hayajatiwa doa na ulimwengu’? Nalimuona Mwalimu wetu akionyesha mavazi ya kile kinachoitwa utakatifu, akawavua, akatandaza wazi uchafu uliokuwa chini yake. Kisha akaniambia: Je, hauoni jinsi walivyojifunika kwa hila unajisi na uozo wa tabia? “Je, mji mwaminifu umekuwaje kahaba?” Nyumba ya Baba yangu imefanywa kuwa ya biashara, mahali ambapo uwepo wa Mungu na Utukufu umetoweka, Kwa sababu hii kuna udhaifu, na nguvu inakosekana. “– Shuhuda, Gombo la 8, uk. 250. {SR1P: 93.2}

Kwa sababu hii, labda, kama ilivyo kwa nyingine yoyote, kanisa linahitaji ujumbe wa Shahidi wa Mwaminifu, ambao pekee unaweza kutuchochea na kutuwezesha kuinuka kwa maombi na kufunga ili kujiokoa wenyewe na watoto wetu kutoka kwa kinachojulikana anasa za kizazi hiki, ambazo Ibilisi anatafuta kuwadanganya na kuwaharibu hata wateule. {SR1P: 93.3}

Mkubwa ni mzigo wa moyo wangu kwamba kila Mu-adventista wa Sabato mtiifu ataisikia Sauti ambayo sasa inalia kati yetu “kuigeuza myoyo ya baba iwaelekee watoto, na moyo wa watoto iwaelekee baba zao.” Mal. 4:6. {SR1P: 93.4}

93

Na jinsi viongozi wameshindwa, hata baada ya kuteta vikali hivi kurekebisha maovu yaliyopo, ni wakati kwamba waumini waaminifu kikamilifu waamke kwa uzito wa hali hiyo na kufanya kile wanachoweza kuleta suluhu. {SR1P: 94.1}

Wandugu wanahitaji nuru juu ya suala hilo, na Bwana amepeana hakikisho kuwa “hata kama watu wetu wote wanaoongoza wataikataa nuru na ukweli, mlango huo utasalia kuwa wazi. Bwana atawainua watu watakaopeana kwa watu ujumbe wa wakati huu.” — Shuhuda kwa Wachungaji, uk. 107. {SR1P: 94.2}

Wazazi, kwa nini msiwe wale watu? Na iwapo huwezi kuanza sasa basi unaonywa kwamba “wakati unaofaa” hautakuja, na kwamba fursa yako itakuwa imetoweka milele. {SR1P: 94.3}

KUMBUSHO

Sasa kwa kuwa umemaliza kusoma na kujifunza yaliyomo katika kijitabu hiki, tunakukumbusha, msomaji mpendwa, kwamba hiki na vijitabu vingine vya mfululizo vya Fimbo ya Mchungaji vinatumwa bila malipo kwa Waadventista wa Sabato, na kwamba kama utatutumia majina na anwani ya wengi utakavyo, wachapishaji watakuwa na furaha na kwa upesi kuwaandalia ujumbe wa saa. {SR1P: 94.4}

94

>