fbpx

Mtoa Jibu Kitabu Namba 3

Mtoa Jibu Kitabu Namba 3

1

Hakimiliki 1944, na

V.T. Houteff

Haki Zote Zimehifadhiwa

Kwamba kila mtu aliye na kiu kwa ajili ya ukweli aweze kuupata, kijitabu hiki cha maswali na majibu ni kama utumishi wa Ukristo, kinatumwa bila malipo. Kinaweka tu dai moja, wajibu wa nafsi kwa mwenyewe kuyathibitisha mambo yote na kushikilia sana lililo jema. Nyuzi za pekee zilizounganishwa na toleo hili la bure ni ncha za dhahabu ya Edeni na kamba nyekundu za Kalvari — mahusiano ambayo hufunga. {ABN3: 2.1}

Majina na anwani za Waadventista wa Sabato zitathaminiwa. {ABN3: 2.2}

2

MTOA JIBU

Kitabu Namba 3

Maswali na Majibu kwa Mada za Ukweli wa Sasa

Katika Masilahi ya Ndugu Waadventista wa Sabato

na Wasomaji

wa

Fimbo ya Mchungaji

Na V.T. Houteff

Huyu “mwandishi,” mwenye elimu

ya ufalme wa

mbinguni, “hutoa

… vitu vipya na vya zamani.”

Mat. 13:52.

Sasa “mtakaseni Kristo Bwana mioyoni mwenu. Mwe tayari siku zote kumjibu kila mtu awaulizaye habari za tumaini lililo ndani yenu; lakini kwa upole na kwa hofu.”

1 Pet. 3:15.

3

 

YALIYOMO

 

Je! Ni Hekalu Gani Linatakaswa Na Ni Nini Kilicholitia Unajisi ? …..5

Je! Siku Huanza Lini? …………………………………………….…….7

Je! Mwaka Wa Kiebrania Huanza Lini? ……………………………….9

Je! Pasaka Na Mazishi Yalikuwa Siku Ile Ile? ………………………14

Je! Kazi Ya Fimbo Ya Mchungaji Ina Mfano? ………………………..19

Pepo Nne — Ni Nini? ……………………………………………………24

144,000 Au Umati Mkubwa? …………………………………………..26

Tuamini Au Tuwe Na Shaka? …………………………………………28

Je! Wote Wataufikia Wakati Wa Mapigo? ……………………..…….41

Je! Mapigo Yataanguka Laodekia Au Babeli? ………………………43

Je! Mnyama Ni Utawala Wa Serikali Ya Kiraia Na Ya Kidini?……..44

Je! Mbona Maono Yote Mawili Sio Sawa? …………………………..45

Ziwa La Moto Linawaka Au Limezimika Wakati Wa Millenia? …….46

Ni Sehemu Ndogo Tu Haijakanyagwa? ……………………..……….47

Nani Ambaye Alitoa Amri Ya Tatu? …………………………………..47

546 Au 547 K.K? …………………………………………………..……49

Wote Au Mabaki — Kina Nani? …………………………….…..……..51

Wachache Au Wengi Waokolewa? …………………………………..51

Utakuwa Upande Gani? ……………………………………………….54

Kuliokoa Kanisa Au Ulimwengu? ………………………………..……65

Kutakaswa Na Mungu, Au Na Shetani? ……………………………..69

Watoto Wachanga Na Wapagani Waokolewa

Au Wapotea? ……………………………………………………………71

Je! Kuwakusanya Watu Kutoka Mataifa Yote

Kutatia Ndani Watu Weusi? ……………………………………………74

Je! Mataifa Wataurithi Ufalme? ……………………………………….76

Je! Ni Nani Yeye Anayesita-sita? …..…………………..…………….76

Ndoa Au Useja? ………………………………………………………..79

Je! Sheria Imebatilishwa? …….…………………………………….…86

Je! Hatujaokolewa Tusizitunze Sheria? ……………………………..90

Ni Kwa Kusudi Gani Sanamu Isifanzwe? ……………………………92

Hatua Yako Itakayofuata Itakuwa Nini? ………………………….….94

4

 

MASWALI NA MAJIBU

JE! NI HEKALU GANI LINATAKASWA NA NI NINI KILICHOLITIA UNAJISI?

Swali Namba 48:

Je! Neno “kutakasa” lililonenwa katika Danieli 8:14 humaanisha utakaso wa hekalu la mbinguni? Ikiwa ni hivyo, ni nini kilicholitia unajisi? {ABN3: 5.1}

Jibu:

Ingawa hekalu la mbinguni na lile la duniani yapo katika maeneo mawili tofauti, bado moja kwa lazima hulihusisha lingine, kwa maana yote mawili hushughulikia dhambi zile zile na wadhambi wale wale. Hivyo, hekalu moja likitiwa unajisi kama tokeo litaathiri lile lingine. Kwa mfano, iwapo baadhi ya washiriki wa kanisa hapa duniani watakengeuka wakati mmoja baada ya kuongoka (walivyofanya Akani, Mfalme Sauli, Yuda, Anania na Safira, na wengine wengi ambao majina yao wakati mmoja yaliandikwa katika Kitabu cha Uzima lakini hata hivyo walishindwa kuendelea katika imani ikawa hawaustahili uzima wa milele), wao bila shaka wakati huo huo wangeyatia unajisi mahekalu yote mawili. Lile la duniani wanalitia unajisi kwa matendo na mvuto wao halisi; la mbinguni, likiwa na majina yao yasiyostahili katika vitabu vyake; kwa maana wakati hekalu la duniani huwahifadhi watu, la mbinguni huhifadhi kumbukumbu zao. {ABN3: 5.2}

Kwa hivyo wakati lipo hitaji la kulitakasa hekalu la duniani kutoka kwa waliokengeuka na wanafiki, lipo hitaji la kulitakasa hekalu la mbinguni kutoka kwa majina ya

5

wadhambi yaliyo katika vitabu vyake. Na jina sahihi kwa kazi kama hiyo ni Hukumu ya Upelelezi — kazi iliyoonyeshwa katika unabii wa Danieli (Dan. 7:9, 10) na katika mifano ya Kristo ya mavuno, juya, talanta, vazi la harusi, na mbuzi na kondoo. {ABN3: 5.3}

Hata hivyo, jinsi Biblia inavyofundisha wazi kwamba kazi hii maalum inatukia tu mara moja wakati wa rehema (Ebr. 9:26), inafuatia kwamba kumbukumbu za wale ambao wamekufa katika karne zote ndizo zitakazokuwa za kwanza kupitiwa upya mbele ya Mungu, Jaji Mkuu (Dan. 7:9, 10). Baada ya hizi kugaguliwa, basi uchunguzi wa kumbukumbu za walio hai utaanza. Na kama tunavyoambiwa kwamba yapo madaraja mawili ya watu kanisani (“ngano” na “magugu” — Mat. 13:30), ni dhahiri kwamba Hukumu ya Upelelezi (“mavuno”) ya wafu huathiri tu patakatifu pa mbinguni. Hili ni dhahiri maradufu inapokumbukwa kwamba “wafu hawajui neno lolote” (Mhu. 9:5) lakini wamelala bila fahamu wanapongojea makaburini mwao siku ya ufufuo. Lakini wakati Hukumu (“mavuno”) ya walio hai itaanza, basi lazima hekali la duniani litatakaswa kutoka kwa wanafiki, na hekalu la mbinguni kutoka kwa majina yao katika kumbukumbu zake. Mahekalu yote mawili kwa hivyo yanaathiriwa. Utakaso wa la duniani unaonyeshwa wazi na unabii wa Malaki: {ABN3: 6.1}

“Angalieni, namtuma mjumbe Wangu, naye ataitengeneza njia mbele Yangu; naye Bwana mnayemtafuta atalijilia hekalu Lake ghafula;

6

naam, yule mjumbe wa agano mnayemfurahia, angalieni, anakuja, asema Bwana wa majeshi. Lakini ni nani atakayestahimili siku ya kuja Kwake? Au ni nani atakayesimama atakapoonekana Yeye? Kwa maana Yeye ni mfano wa moto wa mtu asafishaye fedha, ni mfano wa sabuni ya mtu afuaye nguo; Naye ataketi kama asafishaye fedha na kuitakasa, Naye atawatakasa wana wa Lawi, atawasafisha kama dhahabu na fedha; nao watamtolea Bwana dhabihu katika haki.” Mal. 3:1-3. {ABN3: 6.2}

Aidha, kukanyagia chini ya miguu patakatifu na jeshi, na kuiangusha “kweli hata chini,” kulivyoonyeshwa katika Danieli 8:12, lazima pia kuzingatiwe. Kwa kuufanya ukuhani wa kipagani kuwa badala ya ukuhani wa Kristo, na wapagani wasio waongofu kuwa jeshi la Mungu, pia kwa kuanzisha sikukuu ya sherehe za kipagani kuchukua mahali pa Sabato ya Mungu, sio tu hekalu la mbinguni na la duniani bali pia mafundisho yalitiwa unajisi. Kwa hivyo wakati mahekalu hayo mawili yanapokuwa yakitakaswa kutoka kwa wadhambi, Ukweli wa Biblia unapepetwa kutoka kwa nadharia na maoni ya mwanadamu. {ABN3: 7.1}

SIKU HUANZA LINI?

Swali Namba 49:

Je! Siku ya masaa ishirini na manne huanza lini — machweo, wakati wa maawio, au usiku wa manane? {ABN3: 7.2}

Jibu:

Mzunguko wa masaa ishirini na manne huanzia machweo, kwa sababu wakati dunia ilikuja kuwapo na ikaanza kuzunguka

7

kwenye mhimili wake, haikuwapo nuru “juu ya uso wa vilindi vya maji,” na “Mungu akasema, iwe nuru; na ikawa nuru…. ikwa jioni ikawa asubuhi siku ya kwanza.” Mwa. 1:2, 3, 5. {ABN3: 7.3}

“Nuru” iliyoangaza siku ya kwanza, na ambayo kwayo Mungu aliutenga mchana kutoka kwa usiku (kuiweka dunia izunguke kwenye mhimili wake), haikuwa, hata hivyo, ile ya jua, kwa maana jua na mwezi haikuumbwa hata mpaka siku ya nne, wakati Aliposema “itawale mchana na usiku” (Mwa. 1:18), ambao Yeye alikuwa ameianzisha mapema. {ABN3: 8.1}

Ndivyo ilivyokuwa kwamba wakati dunia ilianza kuonyesha wakati wa milele kwa usiku wa kwanza wa juma la uumbaji, ambalo kwalo Sabato ya siku ya saba ya kila juma hupimwa; mwezi (sayari) ulianza kuonyesha wakati mwishoni mwa siku ya tatu na mwanzoni mwa usiku wa nne ambao kwa huo mwezi mwandamo hupimwa; na jua likaanza kuonyesha wakati mwishoni mwa usiku wa nne na mwanzoni mwa siku ya nne, ambalo kwalo mwaka hupimwa. Kwa hivyo, muda wa saa ambao hupima na kugawanya sehemu za juma, ni siku tatu mbeleni kwa muda wa saa ambao hupima na kuzigawanya sehemu za mwaka wa jua na mwezi mwandamo. Ili, kwa hivyo, ili watu Wake wakumbuke juma la uumbaji, tangu papo hapo muda wa wakati wa dunia ulianza, Mungu akaamuru: “Tangu jioni hata jioni, mtaiadhimisha hiyo Sabato yenu.” Law. 23:32. {ABN3: 8.2}

8

Kwa hivyo siku ya masaa ishirini na manne huanza na usiku, machweo; na wakati wa mchana wenyewe, kando na wakati wa usiku, huanza wakati wa maawio. {ABN3: 9.1}

JE! MWAKA WA KIEBRANIA HUANZA LINI?

Swali Namba 50:

Je! Unaweza kutuambia siku Mpya ya Mwaka wa Kiebrania, na siku za sikukuu zao takatifu, katika kalenda yetu ya Kirumi? {ABN3: 9.2}

Jibu:

Wakati akiliongoza jeshi la Kiebrania kutoka utumwani hadi kwa uhuru, Bwana alikuwa akiwaimarisha imara katika ukweli wa mambo yote, pamoja na ukweli wa siku ambayo mwaka huanza, siku ambayo mwezi huanza, na siku ambayo juma huanza. Bila shaka, dini ya Kiebrania ilikuwa ilihusika pakubwa na siku za juma, mwezi, na mwaka. {ABN3: 9.3}

Waebrania walipaswa kutakasa milele, (1) sio yoyote kwa saba, ila ya saba, siku ya kila juma, Sabato; (2) siku za kuanzia ya kumi na tano hadi ya ishirini na moja ya mwezi wa kwanza, juma la Pasaka; (3) siku ya hamsini baada ya mganda wa malimbuko kutolewa, Pentekoste; (4) siku ya kumi ya mwezi wa saba, Upatanisho; (5) siku za kuanzia ya kumi na tano hadi ya ishirini na moja ya mwezi huo huo, Sikukuu ya Vibanda; na (6) sikukuu za miezi mipya. Kwa hivyo Yule ajuaye Yote, Yeye aliyeziumba sayari na nyota anajua wakati ule Alipozianzisha kuzunguka kutawala siku, mwezi, na mwaka, aliamuru kwamba sikukuu takatifu

9

ziadhimishwe kwa mwezi ule ule na siku ile ile ambayo ziliwekwa wakfu kwanza. {ABN3: 9.4}

Naye akaagiza “na iwe mianga katika anga … nayo iwe dalili, na majira, na siku, na miaka” (Mwa. 1:14), kwa mizunguko ambayo Yeye aliwekea kila tarehe ya jua na ya kila mwezi, ili isiweze kusahaulika. Kisha kufanya salama maradufu dhidi ya hasara kama hiyo. Yeye “Akanena na Musa na Haruni katika nchi ya Misri, Akawaambia, mwezi huu utakuwa mwanzo wa miezi kwenu; utakuwa ni mwezi wa kwanza wa mwaka kwenu.” Kut. 12:1, 2. {ABN3: 10.1}

Hivi tunaona kwamba kidude Chake kikuu cha saa na kisichokosea cha dunia, mizunguko ya siku zote ya dunia yenyewe, hukazia kikiki siku na mwaka; ilhali mizunguko ya mwezi kwa dunia hufanyiza miezi. {ABN3: 10.2}

Lakini Mwaka Mpya wa Kirumi, Januari 1, hupata uasisi wake, sio katika mizunguko ya mfumo wa jua, lakini katika dhana za elimu ya hekaya. Ndiposa kwa sababu tarehe hailingani na aidha siku sare mchana na usiku ya masika au ya vuli, au aidha kwa majira ya joto au msimu wa baridi, basi iwapo wakazi wa dunia wapoteze hesabu ya siku, na wahitaji kuirejelea, wangekuwa hoi kufanya hivyo. {ABN3: 10.3}

Ili kuwazuia watu Wake kujiletea janga kama hilo, na kuwafanya waweze kuwa watambuzi kuhusu wakati mwaka huanza, Bwana alimpa Musa kalenda takatifu ya kila mwaka, ambayo haiwezi kupotea au kuhesabiwa

10

kimakosa maadamu dunia ingalipo. Alimwambia kwamba siku iliyotangulia Kutoka ilikuwa siku ya kumi na nne ya mwezi wa kwanza; na ya kwamba milele baadaye, walipaswa kusherehekea Pasaka usiku uo huo kila mwaka, usiku ulioifuata siku ya kumi na nne. Ndivyo Bwana alikuwa akiisimamisha tena kalenda ya uumbaji, akithibitisha tena kwamba mwaka huanza katika siku sare mchana na usiku ya masika, ambayo masika, msimu wa kwanza wa mwaka, huanzia, na ambayo jua na mwezi uliumbwa (siku ya nne tangu mwanzo wa uumbaji) — majira pekee katika wakati ambayo, kwa uhalisi haswa wa mambo, mwaka unaweza kuanzia. Na kwa hivyo ni kwamba Pasaka, Upatanisho, na Sikukuu ya Vibanda (sikukuu tatu muhimu sana katika mwaka), mbali na sherehe zingine, hudhibitiwa kwa mwaka wa jua na kwa mwezi mwandamo; Sabato ya kila juma kwa ile siku ambayo uumbaji ulianza; na mwaka wenyewe kwa siku sare mchana na usiku ya masika, ishara isiyoweza kusogezwa. {ABN3: 10.4}

Kuanza mwezi wake wa kwanza wa mwaka na mwezi mwandamo wa kwanza, kwenye, au baada ya, siku sare mchana na usiku ya masika, Machi 20-21, huweka siku ya kumi na nne, ile ambayo mwana-kondoo wa Pasaka alipaswa kuchinjwa, Aprili 3. Mwishowe, inaonekana kutowezekana kabisa kwa mwezi wa Kirumi kuwa na hata jambo ndogo kabisa la kufanya na kukazia kikiki wakati ama wa Pasaka au sadaka ya mganda, na kwa hivyo hauhusiki hata kidogo kuhesabu wakati wa aidha kusulubishwa au kufufuka kwa Kristo. {ABN3: 11.1}

11

Hii inaonekana zaidi kutoka kwa mchoro wa masimulizi ya matukio matakatifu ambayo yalikuja katika masika ya mwaka wa 31 B.K, mwaka ambao Kristo alisulubishwa, pamoja na matukio matakatifu ambayo yalikuja mwanzoni mwa mwaka wa 27 B.K, mwaka ambao Yeye alibatizwa, kama yanavyotazamwa kwa mchoro: {ABN3: 12.1}

12

Chati hii inatuwezesha kuona kwamba kama vile msimu mmoja wa jua hulingana na mwingine (siku sare mchana na usiku ya masika hulingana na siku sare mchana na usiku ya vuli, na mageuzi ya majira ya kiangazi, mageuzi ya majira baridi), kwa mtindo kama huo sikukuu takatifu za msimu mmoja hulingana na sikukuu takatifu za msimu mwingine: siku ya kumi ya mwezi wa kwanza, utengo wa mwana-kondoo mkamilifu kutoka kwa kundi (Kut. 12:3), sawa na siku ya kumi ya mwezi wa saba, kazi ya Upatanisho, utengo wa wenye haki kutoka kwa waovu, ukiashiria katika hafla zote mbili siku ya hukumu, siku ya kuwatenga watakatifu kutoka kwa waovu; siku ya kumi na sita ya mwezi wa kwanza, ambayo Yeye alisulubishwa, sawa na ya kumi na sita ya mwezi wa saba, siku ambayo Yeye alibatizwa, ikionyesha kwamba kaburi Lake la maji lilikuwa kivuli cha kaburi Lake mwambani; siku ya kumi na nane ya mwezi wa kwanza, ufufuo, ulilingana na siku ya kumi na nane ya mwezi wa saba, siku ya kwanza ya jaribu la nyikani; siku Zake arobaini za huduma ya ushindi kwa wanafunzi Wake, sawa na siku Zake arobaini za pambano la ushindi dhidi ya Shetani; na wanafunzi Wake kuihubiri injili baada ya Pentekoste, ikilingana na kuhubiri Kwake injili baada ya jaribu la nyikani. {ABN3: 13.1}

Kujua tarehe ya ubatizo Wake kama siku ya kumi na sita ya mwezi wa saba, tunahitaji tu kuzingatia, mbali na ulinganifu ukweli kwamba “neno la unabii lililo imara zaidi” huthibitisha kwamba Yeye alipaswa

13

kuhubiri miaka mitatu na nusu, na kisha “akatiliwe mbali.” Dan. 9:26. Na kwa kuwa Yeye alisulubishwa siku ya kumi na sita ya mwezi wa kwanza, lazima Alibatizwa kwa ajili ya ukasisi miaka mitatu na nusu mbeleni, siku ya kumi na sita ya mwezi wa saba. {ABN3: 13.2}

JE! PASAKA NA MAZISHI YALIKUWA SIKU ILE ILE?

Swali Namba 51:

Majuzi, juhudi nyingi zimefanywa kuweka kikiki siku maalum za juma ambazo hukumu, kusulibishwa, mazishi, na ufufuo wa Yesu ulifanyika; na urefu wa wakati Yeye alikuwa amesimama kwa hukumu, akining’inia msalabani, na kulala kaburini. Kauli zinazoletwa kama thibitisho kwenye mada hiyo zinanikanganya. Je! Unaweza kuzitatua? Na je! Yesu alikula pasaka siku ile ile Wayahudi waliila, au mapema? {ABN3: 14.1}

Jibu:

Pasipo kujali jinsi imefungwa katika siri inaweza kuonekana kwamba waandishi wa Injili waliiacha mada hii, mpangilio mmoja wa kweli umetolewa wazi na unasimama waziwazi; ambao ni, masaa ambayo matukio makuu yalifanyika. {ABN3: 14.2}

Injili zote hushuhudia kwamba Yesu alishikwa usiku ule ule Alikula Pasaka na wanafunzi Wake (Mat. 26:34; Marko 14:30; Luka 22:34). Yohana husimulia kwamba mara baada ya hapo “aliongozwa … hadi kwa Anasi” (Yohana 18:13), na Marko hufichua kwamba baadaye usiku ule Yeye aliletwa mbele ya “makuhani wakuu na baraza lote.” Marko 14:54, 55. “Na ilipopambazuka,” jinsi Injili zote zinavyokubaliana, Alifikishwa mwishowe mbele ya Sanhedrini. {ABN3: 14.3}

14

Ili kufanya kesi hiyo iwe halali, mahakama haikuweza (kwa sheria ya Kiyahudi) kukutana kabla ya jua kuchomoza, saa ya kumi na mbili, saa za kale. Ili kuwa sawa, wakati wa kesi haukuweza kuwa mapema zaidi ya 11:50 Alfajiri saa za kale (5:50 alfajiri saa za kisasa), kwa maana juma la Pasaka liliadhimishwa kutoka siku ya kumi na nne hadi siku ya ishirini na moja ya mwezi wa kwanza wa mwaka wa Kiebrania unaoanza na siku sare mchana na usiku ya masika (Machi 20-21), wakati wa mwaka ambapo mchana na usiku ni sawa. {ABN3: 15.1}

Baadaye, jinsi waandishi wote wa Injili huonyesha, Alipelekwa katika ukumbi wa hukumu wa Warumi, ambapo, kwa mujibu wa ushuhuda wa Yohana, Alihukumiwa mbele ya Pilato “saa sita.” Yohana 19:14. Na Marko husimulia kwamba Alisulubishwa “saa tatu” (Marko 15:25), ilhali Mathayo na Luka, pamoja na Marko, hushuhudia kwamba Alipokuwa akining’inia msalabani, giza liliifunika nchi kutoka saa sita hadi saa tisa (Mat. 27:45 Marko 15:33; Luka 23:44). Mwishowe, wote huungana kushuhudia kwamba Yesu alizikwa kabla ya saa kumi na mbili, machweo — kabla ya Sabato kuanza (Mat. 27:57-62; Marko 15:42-46; Luka 23:54-56). {ABN3: 15.2}

Chati inayofuata huwakilisha kipindi cha masaa arobaini na nane. Juu yake kila saa imeonyeshwa, na kumbukumbu kwa kila tukio imewekwa mkabala na saa ambayo tukio hilo lilifanyika. Takwimu za nje za chati huwakilisha kidude cha saa za kale; takwimu za ndani huwakilisha kidude cha

15

saa za kisasa. Sehemu zilizotiwa rangi huonyesha masaa ya usiku yaliyohusika, pia giza ambalo lilitukia Kristo alipokuwa akining’inia msalabani. {ABN3: 15.3}

16

Mtu angehitimisha kwamba matukio yanayohusiana na mateso ya Kristo, — kushikwa Kwake, kuhukumiwa, kusulubishwa, na kuzikwa, — yalitukia katika siku moja, basi, kama inavyoweza kuonekana wazi kutoka kwenye chati, haingalikuwapo “saa sita” ya kesi katika ukumbi wa hukumu wa Pilato; kwa kweli, haungekuwapo wakati hata mchache ungeruhusu kwa kesi hizo mbele ya majaji wa Warumi — Pilato na Herode! {ABN3: 17.1}

Na kudhani kwamba Luka 22:7-14 hurekodi Pasaka mbadala tu — kwamba Yesu na wanafunzi Wake walisherehekea pasaka kabla ya siku kufika — ni kuchukua msimamo unaotofautiana na “sheria” na vile vile na “ushuhuda” wa manabii na mitume (Isa. 8:20). Na laiti kama huu ungekuwa ukweli, Wayahudi ambao walikuwa wanahangaika kwa hamu ya kumtika Kristo tendo fulani la uhuni, wangeutumia sana, na kama tokeo lake mitume wangeliandika kulihusu. {ABN3: 17.2}

Ili kukidhi hitaji lisiloweza kutanguka la “sheria,” mwana-kondoo alipaswa achinjwe alasiri ya siku ya kumi na nne ya mwezi wa kwanza (Hes. 28:16), na sikukuu ilipaswa kusherehekewa siku ya kumi na tano (Hes. 28:17), usiku uliofuata siku ya kumi na nne (Kut. 12:8). Katika uthibitisho kamili wa ukweli huu Roho ya Unabii kwa mkazo

17

inasema: “Kwa siku ya kumi na nne ya mwezi wa kwanza wa Kiyahudi, siku ile ile na mwezi ule ule ambao kwa karne kumi na tano, mwana-kondoo wa Pasaka alikuwa amechinjwa, Kristo, baada ya kula Pasaka na wanafunzi Wake, alianzisha sherehe ile ambayo ilikuwa ya kukumbuka kifo Chake mwenyewe kama ‘Mwana-Kondoo wa Mungu, aichukuaye dhambi ya ulimwengu.’” — Pambano Kuu, uk. 399. {ABN3: 17.3}

Wakati juma la Pasaka lilidhibitiwa na mwezi, siku ambayo mganda ulipaswa kutolewa (mfano wa ufufuo — 1 Kor. 15:20; Tumaini la Vizazi Vyote, uk. 786) ilidhibitiwa na juma. Na kwa mujibu wa Law. 23:3, 11, mganda ulipaswa kutolewa siku iliyofuata Sabato ya siku ya saba, kwa maana Sabato ya aya ya 11, ni Sabato ya aya ya 3 — iliyo na uhusiano na ile ambayo Musa hutambulisha mada ya sikukuu. {ABN3: 18.1}

Maandiko, isitoshe, kamwe hayaiti siku ya sherehe “Sabato,” bali siku zote “sabato” au “sabato nyingi.” (Angalia Law. 23:23.) {ABN3: 18.2}

(Kwa maelezo ya kina kwa mada ya siku za juma la Pasaka, na ya kipindi cha “siku tatu mchana na usiku” — Mat. 12:39, 40 — Tazama Trakti Namba 10, Ishara ya Yona.) {ABN3: 18.3}

18

JE! KAZI YA FIMBO YA MCHUNGAJI INA MFANO?

Swali Namba 52:

Ikiwa “Fimbo ya Mchungaji” ni sawa kwamba “ambapo hakuna aina, hakuna ukweli,” basi mtu anaweza kuuliza, ni aina ya kazi ya “Fimbo” yenyewe? {ABN3: 19.1}

Jibu:

Katika Agano la Kale linaletwa kwa mtazamo Vuguvugu la kidini ambalo ni “mfano,” au kivuli, cha pacha katika Agano Jipya. Na kama vile Mungu jana alivyolianzisha na kuliongoza lile kuwakomboa watu Wake kutoka katika utumwa wa kikatili kwa mabwana wapagani, ndivyo pia atakavyofanya Yeye na lile lingine leo. Vivyo hivyo jinsi Yeye alivyoliagiza lile, ndivyo atakavyoliagiza lile lingine jinsi ya kutarajia kukombolewa na kusimamishwa katika nchi ya urithi wao, ufalme wa uhuru, amani, na wingi. Katika kuhakikishia hili, Anatangaza: “Basi mambo hayo yaliwapata wao kwa jinsi ya mifano, yakaandikwa ili kutuonya sisi, tuliofikiliwa na miisho ya zamani.” 1 Kor. 10:11. Na “Itakuwako njia kuu kwa mabaki ya watu Wake watakaobaki, watokao Ashuru, kama vile ilivyokuwako kwa Israeli, katika siku ile waliyotoka katika nchi ya Misri.” Isa. 11:16. {ABN3: 19.2}

Maandiko haya yanaonyesha wazi kwamba Vuguvugu la Kutoka la zamani lililoongozwa na Musa kupitia fimbo yake ya mchungaji, kutoka Misri hadi

19

Kanaani, huonyesha mbele kwa ukombozi wa mwisho wa watu wa Mungu kutoka katika utumwa wao wa muda mrefu kwa ufalme wa dunia hii, hadi kwa uhuru katika ufalme wa Mungu. Kwa hivyo hili Vuguvugu la Kutoka la mwisho na katika siku za mwisho linapaswa kuongozwa na Fimbo ya Mchungaji ya uakisi, likiwekwa huru kutoka kwa vifungo vyote vya kidunia — kutoka kwa dhambi na kwa wadhambi. {ABN3: 19.3}

Lakini ikumbukwe kwamba Vuguvugu la Kutoka, la mfano, lilikuwa katika sehemu mbili, sehemu ya kwanza iliongozwa na Musa, na ya pili Yoshua, na ya kwamba ilikuwa ya mwisho, iliyotakaswa, sehemu (ile ambayo ilikua baada ya kutangatanga nyikani kwa miaka arobaini, na baada ya wote isipokuwa wawili ambao walikuwa na umri wa zaidi ya miaka ishirini walipotoka Misri, walikuwa wamekufa) ambayo iliyoimilki nchi hiyo. {ABN3: 20.1}

Vuguvugu linaloongozwa na Fimbo leo ndilo Vuguvugu pekee katika Himaya ya Ukristo linalolingana na lile la mfano — Israeli ya siku ya Yoshua: kama hiyo, likiwavuta wafuasi wake kutoka tu kwa Vuguvugu mzazi, na likiwa na lengo lake la mara-tatu la ukombozi wa watu wa Mungu kutoka utumwani, kuimilki nchi na kuusimamisha ufalme. Na kama vile Israeli iliyotakaswa ya siku za Yoshua, kizazi kilichonusurika kutangatanga nyikani miaka arobaini, kilirithi kwanza uongozi wa mwisho wa Vuguvugu asili la Kutoka, na kisha nchi ya ahadi, hivyo Israeli iliyotakaswa leo (watu 144,000), wale ambao wataokoka kipindi cha miaka arobaini ya kutangatanga kutoka 1890-1930, na ambao wataokoka mchinjo wa Ezekieli 9, watakwezwa

20

kwa uongozi wa mwisho wa Vuguvugu la Kutoka la uakisi, kisha warithi “nchi ya ahadi,” na kuwa raia katika Ufalme wa milele. {ABN3: 20.2}

Hivyo tunaona kwamba haikuwa hadi baada ya wanung’uni kuondolewa, katika mfano, kwamba Yoshua alishika hatamu, na kuliongoza Vuguvugu la Kutoka hadi katika nchi ya Kanaani. Ndiposa, katika uakisi kipindi kabla ya Fimbo kuja kipindi cha Laodekia, ndicho ambacho ndani yake kunapatikana kutangatanga kwa asili, mashaka, na manung’uniko, yote mawili dhidi ya mwasisi na maagizo ya lishe (“matengenezo ya afya”) ya Vuguvugu, na matokeo ya laana na mchinjo. {ABN3: 21.1}

Matokeo ya haraka ya manung’uniko na malalamiko haya, na mashaka leo yamekuwa ya kuyapofusha macho ya wengi katika Vuguvugu la Ujio, na kuwasababisha wakengeuke wache kumfuata Kristo Kiongozi wao, na pole pole kurudi “kuelekea Misri.” — Shuhuda, Gombo la 5, uk. 217. Kwa hivyo, katika usambamba mwingine wa kutisha, jinsi Musa alivyoandika uzoefu wa kusikitisha wa ule mfano mwasisi wa dhehebu la Waadventista wa Sabato aliandika uzoefu wa kusikitisha zaidi wa uakisi, akitangaza mbali kurudi nyuma sana mwaka 1888: “Wengi walikuwa wamepoteza kumwona Yesu “ na “kutilia shaka na hata kutoziamini Shuhuda za Roho wa Mungu, kunatia chachu makanisa yetu kila mahali.” — Shuhuda, Gombo la 5, uk. 217. {ABN3: 21.2}

Kwa maneno mengine, kama kutoamini kwa

21

sehemu ya Israeli ya kale kuliwarudisha nyuma kutangatanga nyikani hadi wale wote wenye hatia walikuwa wameangamia vivyo hivyo kutoamini katika ujumbe wa Haki kwa Imani uliotangazwa katika Kongamano la Minneapolis kulilipeleka dhehebu la Waadventista wa Sabato katika kutangatanga nyikani miaka arobaini, hadi mwaka 1930, na kuwasili kwa ujumbe, kwa sauti ambayo kila mmoja lazima aidha afanye mapenzi ya Mungu au afe kama Akani na nyumba yake. Mungu awawezeshe Israeli ya leo, watoto wa wale ambao wameirudia historia ya Israeli ya zamani Shuhuda, Gombo la 5, uk. 160), waonywe kwa makosa ya baba zao, na watii mwito wa Saa Kumi na Moja. {ABN3: 21.3}

Elimu-mifano hii yenye uzito bado hufunua misambamba mingine muhimu: kama vile Vuguvugu la Kutoka lilifiliwa kiongozi wao aliyeonekana muda mfupi kabla ya kuingia katika nchi ya Kanaani, vivyo hivyo na Vuguvugu la Ujio lilifiliwa kiongozi wake aliyeonekana lilipokaribia mipakani mwa Ufalme; na kama vile Yoshua aliitwa wakati huo ili kuiongoza miguu ya mahujaji wachovu wa Mungu kwenda katika nchi yao, ndivyo pia lazima mwingine ainuke kwa wakati huu kuutimiza huo mfano, kuiongoza hadi nyumbani miguu ya watakatifu wa Mungu leo. {ABN3: 22.1}

“Kwa nabii, Bwana alimtoa Israeli kutoka Misri, na kwa mkono wa nabii alihifadhiwa.” Hos. 12:13. {ABN3: 22.2}

“Mtu fulani atakuja katika roho na nguvu ya Eliya, na atakapotokea,

22

watu wanaweza kusema: ‘… hauyafasiri Maandiko kwa njia sahihi.’” — Shuhuda kwa Wachungaji, uk. 475, 476. {ABN3: 22.3}

Katika maandishi yote ya historia ya kanisa tangu kwa Vuguvugu la Kutoka, ujumbe wa Fimbo ndio pekee unaoitisha Vuguvugu kama hilo, na ambalo kwa usahihi linalingana na mfano huo. (Angalia Trakti Namba 8, Mlima Zayuni Saa Kumi na Moja, na Trakti Namba 9, Tazama Navifanya Vitu Vyote Kuwa Vipya). {ABN3: 23.1}

Bila kukosea, kwa hivyo, nuru angavu inayoangaza kutoka kwa mfano, kutoka kwa shuhuda za manabii, na kutoka kwa historia, huutambua ujumbe wa Fimbo kama ndio pekee ulioti wakfu kuliongoza kanisa la siku za mwisho, lililowekwa huru kutoka kwa dhambi na wadhambi, kuingia katika nchi ya ahadi, wakati “nyakati za Mataifa zitakapotimia.” Luka 21:24. “Katika siku za wafalme hao Mungu wa mbinguni atausimamisha ufalme, ambao hautaangamizwa milele.” Dan. 2:44. Hiyo siku imekuja, na Fimbo ya Mungu i hapa kulitekeleza “vuguvugu kuu la matengenezo kati ya watu wa Mungu” — (Shuhuda, Gombo la 9, uk. 126), kupeana “uwezo na nguvu kwa Ujumbe wa Malaika wa Tatu” — (Maandishi ya Awali, uk. 277), ili kwamba, “likiwa limevikwa silaha za haki ya Kristo, kanisa … nzuri kama mwezi, safi kama jua, na la kutisha kama jeshi na mabango,” liweze “ kwenda ulimwenguni kote, likishinda na kushinda.” — Manabii na Wafalme, uk. 725. {ABN3: 23.2}

“Isikieni hiyo Fimbo, na Yeye aliyeiteua.” Mika 6:9. {ABN3: 23.3}

23

PEPO NNE — NI NINI?

Swali Namba 53:

“Shuhuda kwa Wachungaji,” uk. 444, husema: Yohana anaona nguvu za maumbile — tetemeko la ardhi, dhoruba, na ugomvi wa kisiasa — zikiwakilishwa kama ambazo zinazuiliwa na malaika wanne. “Lakini Trakti Namba 8, “Mlima Zayuni Saa ya Kumi na Moja, uk. 22, husema: “kwa sababu mataifa daima yamekuwa katika vita, kazi hii maradufu ya kudhuru haiwezi kuwakilisha mzozo wa kisiasa.” Taarifa hizi zinazokinzana zinawezaje kupatanishwa? {ABN3: 24.1}

Jibu:

Tuna uhakika kwamba ikiwa muulizaji atachunguza tena kwa makini Shuhuda kwa Wachungaji, uk. 444, ataona kuwa unajitahidi kuonyesha kwamba kusudi la Mungu katika kuzizuilia pepo, ni, jinsi kifungu kinavyosema wazi, “usalama wa kanisa la Mungu.” Mambo yakiwa hivyo, basi pepo hizo, zenyewe zikiwa ni mfano wa ugomvi, taabu, na vita, wakati zinapoachiliwa, zivume dhidi ya kanisa. Hili ni dhahiri kwa sababu kuzuiliwa kwazo tangu siku ya Yohana hadi saa hii, hakujawahi kamwe kuzuia na sasa hakuzuii vita kati ya mataifa yenyewe. Siku zote yamekuwa yakifanya vita moja kwa lingine, na leo yanahusika katika vita vya kufisha kote duniani visivyo na kifani katika historia yote, ingawa malaika bado wanazishikilia pepo. Lazima, kwa hivyo, ugomvi unaowakilishwa na pepo

24

kuvuma, kimsingi uwe wa kidini kwa kusudi, na kisiasa tu kwa utaratibu, na hivyo ni wa kidini-kisiasa, kama unavyoelezwa katika Trakti Namba 12, Dunia Jana, Leo, Kesho, uk. 38, 65, na katika Fimbo ya Mchungaji. Gombo la 2, uk. 114. Hitimisho hili limethibitishwa katika kifungu kifuatacho: {ABN3: 24.2}

“Wakati unakuja ambapo hatuwezi kuuza kwa bei yoyote. Amri itatangazwa kupiga marufuku mtu yeyote kununua au kuuza isipokuwa yule aliye na alama ya mnyama. Hili lilikaribia kutekelezwa huko California muda mfupi tangu wakati huo; lakini hili lilikuwa tu tishio la kuvuma kwa pepo nne. Bado zinashikiliwa na wale malaika wanne. Hatuko tayari. Kazi bado ipo inayopaswa kufanywa, na kisha malaika wataambiwa waziachilie, ili pepo nne ziweze kuvuma juu ya nchi. Huo utakuwa wakati wa maamuzi kwa watoto wa Mungu, — wakati wa taabu mfano wake haukuwapo tangu lilipoanza kuwapo taifa.” — Shuhuda, Gombo la 5, uk. 152. {ABN3: 25.1}

Trakti hiyo, katika maelezo yake kwa taarifa inayohojiwa, inasisitiza tu kipengee cha kidini cha hiyo taabu, katika jitihada za kuonyesha kwamba hiyo taabu sio ya lengo la kisiasa, — sio kuteka eneo, bali kuunda dini ya kimataifa ili kuulazimisha ulimwengu kuabudu sanamu ya mnyama. {ABN3: 25.2}

Katika nuru hii angavu, tunaona kwamba zote mbili Shuhuda kwa Wachungaji na mfululizo wa

25

Fimbo ya Mchungaji zinajitahidi kuonyesha kwamba ugomvi sio wa kisiasa tu au wa kidini tu, bali wa kidini na kisiasa. Ni muungano wa kanisa na serikali katika utendaji sawa. {ABN3: 25.3}

144,000 AU UMATI MKUBWA?

Swali Namba 54:

Je! Umati mkubwa (Ufu. 7:9) unawezaje kuwa kikamilisho cha watu 144,000 katika kujumuisha watakatifu walio hai? {ABN3: 26.1}

Jibu:

Licha ya ukweli kwamba “katika kazi ya kufunga” kwa dhehebu la Waadventista wa Sabato, ni watu 144,000 tu ambao wanapaswa kutiwa muhuri, kwa mujibu wa Shuhuda, Gombo la 3, uk. 266, bado mwanzoni mwa mwaka wa 1944, Dhehebu tayari lilikuwa limewahesabu washiriki wake zaidi ya nusu milioni, ilhali sehemu za eneo ambalo liko chini ya upanzi wa injili, zikilinganishwa na sehemu pana za wananadamu ambazo hata halijagusa, ni sawa na pembe ndogo sana. Kwa hivyo, kuzungumza kwa ulinganifu, wapo mamilioni kwa mamilioni ambao hawajawahi kusikia hata jina kama “Waadventista.” {ABN3: 26.2}

Iwapo kiwango cha ukuaji cha sasa cha Dhehebu kitaendelea hadi Ujumbe wa Ujio utakapokuwa umehubiriwa ulimwenguni kote, ushirika wake utakuwa umeongezeka kwa idadi kubwa Kristo atakapokuja. Hakika, kwa sababu hakuna hata uwezekano mdogo wa

26

kushuka kwa kiwango cha ukuaji wa sasa, ila kila uwezekano wa kuongezeka (jinsi walei huambiwa kwenye mimbari Sabato hata Sabato), ni hakika kwamba dhehebu, kwa kiwango chake cha sasa cha ukuaji, liendelee hadi kuja mara ya pili kwa Kristo, litakuwa wakati huo na idadi ya mamilioni. Na kama wangekuwepo tu 144,000 ambao watahamishwa bila kufa, basi mamilioni ya Waadventista wa Sabato walio hai wakati wa kufungwa mlango wa rehema, msiba kusema, wataangamia ama katika “mapigo saba ya mwisho” au kwa “mwangaza wa kuja Kwake”! Na iwapo “kazi ya kufunga kwa kanisa” humaanisha kwamba kati ya mamilioni ya washiriki hawa watakatifu 144,000 hakika watahamishwa bila kufa, basi ni nafasi gani finyu mshiriki yeyote anayo ya kuokolewa! Na isitoshe, katika tukio hilo, pamoja na magumu yanayowalemea dhidi yao kuokolewa, ni haki gani inayoweza kuwapo katika kuendelea kuleta waongofu zaidi na zaidi ili kuongeza ushirika wa kanisa? Kama hiki hakikuwa kitu kingine isipokuwa udanganyifu mkubwa — kuwafunika katika pambo la tumaini la wokovu! {ABN3: 26.3}

Kwa vile ni kinyume cha matakwa na juhudi za Mungu (Shuhuda, Gombo la 6, uk. 371) kuwaleta kanisani wale ambao hawajaokoka (magugu), basi fundisho kuu kwamba watakuwapo watakatifu walio hai 144,000 Kristo atapokuja kuwakusanya wote walio Wake, si kitu kingine isipokuwa kukiri

27

kwamba ongezeko la haraka la washiriki ni kazi ya Adui! {ABN3: 27.1}

Katika Ishara za Nyakati, Mei 3, 1927, yalitokea makala yaliyopewa kichwa, “Watu 144,000, Ushindi Wao na Tuzo Lao.” Katika makala hii, ambayo iliandikwa miaka mitatu kabla ya Fimbo la Mchungaji, Gombo la 1, kuchapishwa, Dhehebu lilifundisha kwamba watu 144,00, malimbuko ya watakatifu walio hai, watatiwa muhuri kwanza, nao watayaleta mavuno ya pili, “umati mkubwa” (Ufu. 7:9) ya watakatifu walio hai. {ABN3: 28.1}

Katika kuhama kutoka kwa msimamo huu, katika jaribio la kuupinga ujumbe wa saa ya sasa, Fimbo ya Mchungaji, wamejidunga wenyewe kwenye pembe za utata: kwa upande mmoja wakitoa uongo kwa fundisho lao la mwaka 1927, na kwa upande mwingine wakitoa tumaini la wokovu kwa washiriki wa kanisa! {ABN3: 28.2}

Kwa hivyo swali halipaswi kuwa ni jinsi gani umati mkubwa unaweza kuwa kikamilisho cha watu 144,000, lakini badala yake jinsi ambavyo hawawezi kuwa. {ABN3: 28.3}

TUAMINI AU TUWE NA SHAKA?

Swali Namba 55:

Ni vigumu kwangu kusonga mbele kwa bidii yote katika ufasiri wowote wa Biblia ambao madai yake hufanywa kwa Uvuvio. Je! mtu yeyote akifanya madai kama hayo haleti hatari kwa muundo wote wa

28

ujumbe wake, akifungua njia ili ufutwe mara moja kupitia kosa lo lote moja linaloweza kuwa ndani yake? {ABN3: 28.4}

Jibu:

Tatizo la muulizaji huchochewa na uhakika halisi kwamba ulimwengu wa Uprotestanti kwa muda mrefu umeshikilia wazo kwamba Mungu katika kizazi hiki hawezi kuajiri mnenaji aliyevuviwa kuyafasiri Maandiko na kutangaza mapenzi Yake bali huwekeza na kumuongoza kila Mkristo mmoja mmoja. Dhana hii, hata hivyo, inalipuka ulimwenguni kote wakati inapotazamwa katika nuru ya ukweli kwamba wale watu ambao hudai kuongozwa kibinafsi na Mungu, huhitilafiana kati yao kama vile madhehebu mbali mbali hayakubaliani moja kwa lingine. {ABN3: 29.1}

Kabla ya kuondoka Kwake, Mwokozi alitangaza: “Lakini…Atakapokuja, huyo Roho wa kweli, Atawaongoza awatie kwenye kweli yote; kwa maana hatanena kwa shauri Lake Mwenyewe, lakini yote atakayoyasikia atayanena, na mambo yajayo Atawapasha habari yake.” Yohana 16:13. Bila ubishi kwa hivyo, mapenzi ya Mungu ni kwamba tunayo Kweli yote na Kweli pekee. Na lazima ikumbukwe kwamba “hakuna unabii katika Maandiko upatao kufasiriwa kama apendavyo mtu fulani tu. Maana unabii haukuletwa popote kwa mapenzi ya mwanadamu; bali wanadamu walinena yaliyotoka kwa Mungu wakiongozwa na Roho Mtakatifu.” 2 Pet. 1:20, 21. {ABN3: 29.2}

Kwa kweli, neno lenyewe, Uvuvio, katika maana yake ya kitheolojia, humaanisha kutangaza

29

maagizo ya Mungu bila kutiwa unajisi na wanadamu. Kwa hivyo, pingamizi iwayo yote kwa Uvuvio, inaweza tu, kwa uchanganuzi wa mwisho, kuwa ni jaribio la kumwondoa Mungu asionekane na kuwaleta wanadamu mbele, kukatiza njia pekee ambayo Mungu anaweza kufasiri Maandiko, kuwasiliana na watu Wake — “kuufunua ukweli na kufichua makosa.” – Shuhuda kwa Wachungaji, uk. 107. “Bwana amejidhihirisha mara kwa mara katika majaliwa Yake,” inasema Roho ya Unabii, “kwamba hakuna kitu kingine isipokuwa ukweli uliofunuliwa, neno la Mungu, linaweza kumkomboa mwanadamu kutoka dhambini au kumlinda dhidi ya uasi.” — Shuhuda kwa Wachungaji, uk. 80. {ABN3: 29.3}

Hivyo, wazi kabisa, Neno la Mungu haliwezi kufasiriwa kwa njia apendavyo mtu fulani tu — bila msaada wa Uvuvio (2 Pet. 1:20, 21). Yeyote wanaojaribu kufasiri ujumbe ambao Bwana hutuma kwao, watajikuta wakimtumikia Shetani badala ya kumtumikia Kristo, na kwa kweli watasababisha wenyewe na wafuasi wao kuvunjikiwa meli ya imani. {ABN3: 30.1}

Ili kulinda imani ya waaminifu, Bwana huonyesha kwa njia ya mfano katika sura ya nne ya Zekaria, mbinu ambayo Yeye huwasilisha ukweli kwa watu Wake. Picha iliyoambatanishwa ni udhihirisho halisi wa kile nabii alionyeshwa. {ABN3: 30.2}

30

31

Hapa inaonekana kwamba kinara cha taa, kama kinavyofasiriwa na Ufunuo 1:20, ni nembo ya ushirika wa kanisa; mifereji inayochomoza kutoka kwenye bakuli la dhahabu hadi kwenye kinara cha taa, ni nembo ya ukasisi (Shuhuda kwa Wachungaji, uk. 188); miti ya mizeituni ni nembo ya Maandiko ya Agano la Kale na Jipya (Pambano Kuu, uk. 267); na mabomba mawili ya dhahabu, ambayo husafirisha mafuta ya dhahabu kutoka kwenye miti hadi kwenye bakuli, ni nembo ya wafasiri wa Biblia, wajumbe waliovuviwa kutoka kwa Mungu, kwa maana nembo hiyo kwa uthabiti huonyesha kwamba wao ndio pekee ambao Uvuvio huwawezesha kuteka mafuta kutoka kwenye mizeituni — kuyafasiri Maandiko. Na bakuli, chombo ambacho yale mabomba (wafasiri) humimina ndani yacho, chaweza tu kuwa maandishi ya Roho ya Unabii. {ABN3: 32.1}

Kama hitaji la kufuata na la kikawaida, Mungu atakuwa na mnenaji mmoja tu wa kuwafundisha watu Wake katika kusimamishwa kwa Ufalme Wake, jinsi Yeye hutuambia ki-nabii katika maneno waziwazi: “Nami nitaweka mchungaji mmoja juu yao, naye atawalisha, naam, mtumishi Wangu, Daudi; yeye atawalisha, naye atakuwa mchungaji wao. Na Mimi, Bwana, Nitakuwa Mungu wao, na mtumishi Wangu, Daudi, atakuwa mkuu kati yao; Mimi, Bwana, Nimesema haya. Nami nitafanya agano la amani nao, Nami nitawakomesha wanyama wakali kati yao; nao watakaa salama

32

jangwani, na kulala misituni. Nami nitawafanya wao, na mahali palipo pande zote za mlima Wangu, kuwa baraka, Nami nitaleta manyunyu kwa wakati wake; yatakuwako manyunyu ya baraka.” Ezek. 34:23-26. “Sauti ya Bwana inaulilia mjikwa mji, na mtu mwenye hekima ataliona jina Lako: isikieni hiyo Fimbo, na Yeye aliyeiagiza.” ‘’Walishe watu wako kwa fimbo yako, kundi la urithi wako, wakaao peke yao, mwituni katikati ya Karmeli; na walishe katika Bashani na Gileadi, kama siku za kale. Kama katika siku zile za kutoka kwako katika nchi ya Misri Nitamwonyesha mambo ya ajabu.” Mika 6:9; 7:14, 15 {ABN3: 32.2}

Kwa maana ujumbe katika Fimbo ya Mchungaji, tunatoa tu sifa kwa Yeye ambaye ni Wake. Na ikiwa yupo yeyote anayetaka hiyo sifa tujipe wenyewe, hufanya hivyo, sio kwa sababu wanatupenda au wanataka kutukweza juu yao wenyewe, lakini ni dhahiri kwa sababu pasipokujua wanaunga mkono sauti kutoka chini, ambayo humchukia Mungu na ufunuo wa Neno Lake, na ambayo daima huzungumza tu kuwajaribu watu wajiinue wenyewe badala ya Mungu, na hivyo kujidanganya kwa upofu na kuwaongoza wengine mbali kutoka kwa ukweli, yote kwa sababu huudhika kujisalimisha chini ya utawala wa Kristo sasa wakati “Anachukua mamlaka mikononi Mwake mwenyewe.” — Shuhuda kwa Wachungaji, uk. 300. {ABN3: 33.1}

Wacha wale ambao hupinga kujinyenyekeza kikamilifu kwa Uvuvio, wajiulize

33

wangalifanya nini kama wangeishi chini ya Musa na fimbo yake. Alijitambulisha mwenyewe kuwa mnenaji wa Mungu kama vile Fimbo ya leo hufanya. Kama tokeo, je! hawa wahalifu hawangeinuka na Kora dhidi ya Musa na Haruni, jinsi wanavyofanya sasa dhidi ya Fimbo, wakisema: “Ninyi inawatosha, kwa kuwa mkutano wote ni mtakatifu, kila mmoja miongoni mwao, Bwana Naye yu kati yao; n’nini basi kujitukuza juu ya mkutano wa Bwana? Hes. 16:3. {ABN3: 33.2}

Iwapo kama hao hawataki kwa moyo wote kuupokea ujumbe Uliovuviwa leo, je! wangeupokea ujumbe wa Mbatizaji, wa Kristo au wa mitume? La, hakika hapana, bila kujali taaluma yao. Na ikiwa hawatajitiisha kwa Uvuvio, watawezaje kuijua kweli? Na watawezaje kuingia katika Ufalme? Kwa maana Biblia husema: {ABN3: 34.1}

“Hakika Bwana Mungu hatafanya neno lo lote, bila kuwafunulia watumishi Wake manabii siri yake.” “Na kwa nabii Bwana alimtoa Israeli katika Misri, na kwa mkono wa nabii alihifadhiwa.” “Mwaminini Bwana, Mungu wenu, ndivyo mtakavyothibitika; waamini manabii Wake, ndivyo mtakavyofanikiwa.” Amosi 3:7; Hos. 12:13; 2 Nya. 20:20. {ABN3: 34.2}

“Nami nitaufanya ulimi wako ugandamane na kaakaa lako, hata utakuwa bubu, wala hutakuwa mwonyaji kwao;

34

kwa kuwa wao ni nyumba yenye kuasi. Lakini hapo Nitakaposema nawe, Nitafumbua kinywa chako, nawe utawaambia, Bwana Mungu asema hivi. Yeye asikiaye na asikie; naye akataaye na akatae; maana wao ni nyumba yenye kuasi.” Ezek. 3:26, 27. {ABN3: 34.3}

Ni maoni ya watu ambao hawajavuviwa ambayo yamelikatakata kanisa la Kikristo katika vipande vya kila aina na vipimo, na kulifanya “maskani ya mashetani, na ngome ya kila roho mchafu, na ngome ya kila ndege mchafu na mwenye kuchukiza.” (Ufu. 18:2), badala ya kulifanya kuwa maskani ya ukweli na wokovu, na makao ya watakatifu. {ABN3: 35.1}

Wacha wote wanaoshiriki hisia za muulizaji, watulie, na watafakari swali: Je! Ujumbe ambao haujavuviwa unawezaje kutoka kwa Mungu — kuwa ukweli — kuwa unaostahili kupokelewa? Ni wazi kwamba, kukataliwa mmoja anayedai Uvuvio kwa ujumbe wake, na tuhuma ya kuwa ndani yake dosari ya makosa, haipendekezwi na Yeye ambaye husema: “Msimzimishe Roho. Msitweze unabii. Jaribuni mambo yote; lishikilieni lililo jema.” 1 Thes. 5:19-21. {ABN3: 35.2}

“Kuliko hapo awali, tusiombe tu kwamba watumwa waweze kutumwa katika shamba kubwa la mavuno, ila tuwe na ufahamu safi wa ukweli, ili wajumbe wa kweli

35

watakapokuja, tuweze kuupokea ujumbe na kumheshimu mjumbe.” — Shuhuda, Gombo la 6, uk. 420. {ABN3: 35.3}

Katika siku ya Kristo, watilia shaka Uvuvio waliwashambulia wajumbe na ujumbe wao kwa wakati huo. Kwa upande mmoja walitafuta kosa kwa Yohana Mbatizaji kwa sababu lishe yake ilikuwa asali ya mwituni na mboga ya nzige (Mat 3:4). Kwa sababu yeye “hakuja akila wala kunywa,…wakasema, yu na pepo.” Mat. 11:18. Kwa upande mwingine, kwa sababu Kristo “alikuja akila na kunywa,” walimshutumu kuwa “mlafi Huyu, na mlevi, rafiki yao watoza ushuru na wenye dhambi” Mat. 11:19. Wakikana kwamba alitumwa na Mungu, wakamwuliza kwa dharau: “Unatenda mambo hayo kwa mamlaka gani? Tena ni nani aliyekupa mamlaka hii?” Luka 20:2. {ABN3: 36.1}

Na sasa kwa kanisa Lake katika siku hizi za mwisho, Roho Wake anatangaza: “Unabii lazima utimizwe.” Asema Bwana: “Angalieni, Nitawatumia nabii Eliya kabla haijaja siku ile ya Bwana, iliyo kuu na ya kuogofya.’ Mtu fulani atakuja katika roho na nguvu ya Eliya, na atakapoonekana, watu wataweza kusema: ‘Wewe ni mwenye bidii sana, huyafasiri Maandiko kwa njia sahihi. Hebu nikuambie jinsi ya kufundisha ujumbe wako.’” — Shuhuda kwa Wachungaji, uk. 475. {ABN3: 36.2}

Kwa watiao shaka kwa uwezekano wa ujumbe ambao hauna chochote isipokuwa ukweli, laja onyo: “Mungu na Shetani kamwe

36

hawafanyi kazi kwa ushirikiano. Shuhuda ama zinayo ishara ya Mungu au ile ya Shetani. Mti mzuri hauwezi kuzaa matunda mabaya….” — Shuhuda, Gombo la 5, uk. 98. “Tunaamini maono,” husema watiao shaka kwa Uvuvio, “lakini Dada White, kwa kuyaandika, aliweka ndani maneno yake mwenyewe, na tutaamini tu ile sehemu ambayo tunadhani ni ya Mungu, na hatutatii ile nyingine.” — Shuhuda, Gombo la 1, uk. 234. {ABN3: 36.3}

“Akawaambia, Enyi msiofahamu, wenye mioyo mizito ya kuamini yote waliyoyasema manabii.” Luka 24:25. “Na mtu ye yote akiondoa lo lote katika maneno ya unabii wa kitabu hiki, Mungu atamwondolea sehemu yake katika ule mti wa uzima, na katika ule mji mtakatifu, ambao habari zake zimeandikwa katika kitabu hiki.” Ufu. 22:19. {ABN3: 37.1}

Kwa ufananisho akiwaambia watu Wake kama kondoo na wachungaji, katika sura ya thelathini na nne ya Ezekieli, Bwana huuliza: “Je! Mwaona ya kuwa ni neno dogo ninyi kula malisho mema, hata mkawa hamna budi kukanyaga kwa miguu yenu yaliyosalia? Na kuwa mmekunywa maji yaliyo safi, nanyi hamna budi kuyatibua kwa miguu yaliyobaki?” Je! kweli wanafikiri inakubalika kupokea sehemu tu ya ukweli Yeye huwatumia, na kukanyagia miguuni mwao uliosalia? Kisha Anaongeza, “Na kwa habari za kondoo Zangu, wao wanakula hayo mliyoyakanyaga kwa miguu yenu, nao wanakunywa maji mliyoyatibua kwa miguu yenu.”

37

Na kwa sababu ya wale wanaopokea tu sehemu ya ujumbe ambao hufaa ladha zao zisizoongoka, ambazo hazipingani na nia zao potovu, Bwana anaonya kimbele: “Nitahukumu kati ya ng’ombe na ng’ombe.” {ABN3: 37.2}

Kati ya watu wa Mungu, daima limekuwapo daraja lenye mwelekeo wa kuhoji na kukosoa kila kitu katika “ukweli unaokunjua.” — Shuhuda, Gombo la 5, uk. 690. “Tunaamini hili na lile,” wao husema, “lakini hatutalipokea lile lingine.” Wengi wao hudhani ni alama ya werevu kuhoji na kukosoa, kuhukumu ujumbe ambao Mungu amewatumia. Nafsi hizi zenye ubinafsi ni za upumbavu sana na za upofu kwa ujinga wao hata ingawa karne hamsini na mkasa zaidi wa kibinadamu hukemea na kuonya sana dhidi ya mwenendo wao mbaya na unaoangamiza nafsi, bado wanabaki kuwa viziwi kwa kilio na vipofu kwa njia yao. Na kibaya zaidi mashaka yao na ukosoaji wao umezitawanya nafsi dhaifu kutoka kwa Kristo, na tokeo lake kwamba Mungu ametangaza hukumu: “Kwa kuwa mmesukuma kwa ubavu, na kwa mabega, na kuwapiga wenye maradhi kwa pembe zenu, hata mkawatawanyia mbali; basi Mimi nitaliokoa kundi Langu, wala hawatakuwa mateka tena; Nami Nitahukumu kati ya ng’ombe na ng’ombe.” Ezekieli. 34:21, 22. {ABN3: 38.1}

Mnaonywa, kwa hivyo, kwamba “jinsi wanafunzi walivyotangaza kwamba hakuna wokovu kwa jina lingine chini ya mbingu, waliloopewa wanadamu, vivyo hivyo, pia watumishi wa Mungu wanapaswa

38

kwa uaminifu na bila woga kuwaonya wale ambao hukumbatia tu sehemu ya kweli zinazounganika na ujumbe wa tatu, kwamba lazima wapokee kwa furaha jumbe zote jinsi Mungu amewapatia, au hawana sehemu katika jambo hilo.” Maandishi ya Awali, uk.188, 189. {ABN3: 38.2}

“’Shetani ana uwezo wa kupendekeza mashaka na kubuni pingamizi kwa ushuhuda mkali ambao Mungu hutuma, na wengi hufikiri kwamba ni sifa njema, alama ya werevu ndani yao, kuwa wasioamini, na kuhoji na kubishana. Wale wanaotaka kutilia shaka watapata nafasi ya kutosha. Mungu hapendekezi kuondoa fursa zote za kutokuamini. Yeye hutoa ushahidi, ambao lazima uchunguzwe kwa uangalifu na nia ya unyenyekevu na roho ya uelekevu; na wote wanapaswa kuamua kutokana na uzito wa ushahidi.’ ‘Mungu hupeana ushahidi wa kutosha kwa nia ya uelekevu, lakini yeye anayeacha uzito wa ushahidi kwa kuwa yapo mambo machache ambayo hawezi kuweka wazi kwa sababu ya uelewa wake hafifu, ataachwa katika mazingira baridi ya kutokuamini na mashaka ya maswali, na kuvunjikiwa meli ya imani.’” — Shuhuda, Gombo la 5, uk. 675, 676. {ABN3: 39.1}

Hakuna mtu anayethubutu kulinganisha haki zake na zile za Yesu, bado Yeye aliamini maandishi yote ya manabii, na wale wanaojiona kuwa wenye hekima sana, na kufikiri ni aibu sana, kuwaamini wote, Yeye huwaita “wapumbavu.” Luka 24:25. Wamejifanya wasioweza kuufahamu

39

kweli hizi sasa kama Wayahudi walivyojifanya wasiweze kuelewa mafundisho ya Yesu mintarafu “ufalme” wakati huo. {ABN3: 39.2}

Kila kizazi kimekuwa na umati wake ambao, badala wabatizwe kumfuata Kristo na Ukweli Wake, walibatizwa kumfuaza mwanadamu. Walijiunga na umati kanisani badala ya umati wa mbinguni. Kwa hivyo, Kristo ni mgeni kwao, na ukweli unapofunuliwa, wao huuita uongo, kisha huwafuata watu na kuukataa ukweli. Upumbavu huu umerudiwa mara kwa mara, na tokeo lake kwamba wachache waaminifu ambao wamemfuaza Kristo na ukweli Wake, wametupwa nje ya makanisa na kulazimishwa kuanza tena. Ndivyo ilivyo leo. Lakini kwa hawa waliotupwa nje wa Zayuni, inakuja sauti ya kufariji: “Lisikilizeni neno la Bwana, ninyi mtetemekao kwa sababu ya neno Lake; ndugu zenu wawachukiao ninyi, waliowatupa kwa ajili ya jina Langu, wamesema, na atukuzwe Bwana, tupate kuiona furaha yenu; lakini watatahayarika.” Isa. 66:5. “Jinsi ilivyo mizuri juu ya milima miguu Yake aletaye habari njema, yeye aitangazaye amani, aletaye habari njema ya mambo mema, yeye autangazaye wokovu, auambiaye Zayuni, Mungu Wako anamiliki! “ Isa. 52:7. {ABN3: 40.1}

“Mwaminini Bwana, Mungu wenu, ndivyo mtakavyothibitika; waamini manabii Wake, ndivyo mtakavyofanikiwa.” 2 Nya. 20:20. {ABN3: 40.2}

40

JE! WOTE WATAUFIKIA WAKATI WA MAPIGO?

Swali Namba 56:

Iwapo kanisa litatakaswa kabla rehema kufungwa kwa ulimwengu na kudumu safi baada ya hapo bila wadhambi wowote ndani yake, jinsi “Fimbo ya Mchungaji” hufundisha, basi unawezaje kupatanisha hili na “Maandishi ya Awali,” uk. 71, ambayo husema: Wengine “wataufikia wakati wa mapigo kuanguka, na kisha wataona ya kuwa walihitaji kuchongwa na kulinganishwa kwa ajili ya jengo”? {ABN3: 41.1}

Jibu:

Zipo taarifa zingine kutoka kwa mwandishi wa Maandishi ya Awali, ambazo zina uthibitisho mzuri zaidi kwamba Mungu, kabla ya wakati huo, atakuwa na kanisa safi na la kweli. (Angalia Pambano Kuu, uk. 425; Manabii na Wafalme, uk. 725; Shuhuda, Gombo la 5, uk. 80; Isa. 52:1, 2.) {ABN3: 41.2}

Kwa sababu taarifa hizi kadhaa zinahusu utakaso wa utangulizi ni za kweli kama ile iliyo katika Maandishi ya Awali ambayo huonekana kupinga utakaso, mtu hawezi kwa uaminifu kuzipuuza na kuizingatia hiyo tu. Tukumbuke siku zote kufuata sheria isiyoweza kukiukwa kwamba ufasiri wa taarifa moja iliyovuviwa lazima ipatane na taarifa zingine zote zinazohusiana. {ABN3: 41.3}

Baadhi ambao wanahangaika kuhatarisha Ukweli wa Sasa kwa uzito wa lile taarifa moja iliyovuviwa inaonekana kusema au kumaanisha, kwa ujeuri au kwa kutokujua sana

41

wanapuuza “uzito wa ushahidi.” Wengine wanafanya hivi kwa kutotazama mbele, ilhali wengine wanafanya hivyo ili kuziinua dhana zao fulani wanazozipenda. {ABN3: 41.4}

Msingi wa fundisho la hakuna utakaso wa utangulizi umejengwa, si kwa mwamba thabiti, ila kwa mchanga ule ule unaomomonyoka kama ule msingi wa dhana potovu kama hali ya wafu kuwa na ufahamu, mateso ya milele ya waovu, ubatizo kwa kunyunyizia, utakatifu wa Jumapili, na enzi ya millenia ya amani duniani. {ABN3: 42.1}

Kwa sababu, Ukweli ni endelevu, na kwa sababu utakaso wa kanisa ulikuwa haujafunuliwa taarifa hiyo katika Maandishi ya Awali ilipoandikwa, hatari iliyotabiriwa na ushauri uliotolewa humo haungewezekana kusemwa katika maneno mengine zaidi ya yale walioyaelewa kwa wakati huo. Wote hivyo walionywa wazi kimbele kwamba ikiwa wangeendelea kutenda dhambi, basi baada ya kufungwa kwa muda wa rehema kwa ulimwengu, mapigo, ambayo tayari walikuwa na uelewa fulani kuyahusu, yangekuwa malipo yao. Kwa hivyo iwapo Bwana angalikuwa amelielezea jambo hilo katika Maandishi ya Awali kama anavyofanya kupitia katika Fimbo leo, ingalimpasa kuwa alilifunua, kwa wakati huo, Maandishi ya Awali yalipokuwa yakiandikwa, ujumbe ambao unalihusu tu kanisa la leo, na ambao sasa tunapokea. {ABN3: 42.2}

Katika uchanganuzi wa mwisho, wadhambi wasiotubu ambao sasa wako kanisani, hawataweza

42

kamwe kuyaona mapigo saba ya mwisho, ilhali wengine, ambao sasa wako ulimwenguni, wakati wa Kilio Kikuu bado watapata nafasi ya “kuchongwa” kwa ajili ya jengo, na kuthaminiwa na “mawe yaliyo hai,” au sivyo wakione cha mtema kuni cha mapigo. {ABN3: 42.3}

Yeyeote hapaswi kuwa na ugumu wa kuliona hili sasa, kwa maana wale wote ambao Maandishi ya Awali kimsingi yalinena kwao tayari wamelala, ingawa mapigo bado yapo katika siku zijazo. Isitoshe, bado nuru zaidi itakuja mintarafu ukweli wa mapigo saba ya mwisho, na utakapokuja, tutaweza kuona tena kwamba tunayo “masomo mengi ya kujifunza, na mengi, mengi ya kuacha.” — Shuhuda kwa Wachungaji, uk. 30. {ABN3: 43.1}

JE! MAPIGO YATAANGUKA LAODEKIA AU BABELI?

Swali Namba 57:

Je! Mchinjo wa Ezekieli 9 hautatimizwa kwa mapigo saba ya mwisho? {ABN3: 43.2}

Jibu:

Mchinjo kama ulivyoelezwa katika unabii wa Ezekieli utaangamiza uhai wa wale waovu walio katika “nyumba ya Israeli na Yuda” (Ezek. 9:9) — kanisa; ilhali maangamizi ya mapigo yanawaangukia wote wanaopatikana katika “Babeli” (Ufu. 18:4) baada ya Bwana kutangaza “Tokeni kwake, enyi watu Wangu,” na baada ya wao kuitika na hivyo kujitenga

43

kutoka kwa walio Babeli. Maangamizi ya Ezekieli 9, kwa hivyo, yanawahusu tu washirika wake kama mfano au mtangulizi wa mapigo saba ya mwisho. {ABN3: 43.3}

Zaidi ya hayo, watu Wake, wale ambao wametiwa alama na malaika kwa mujibu wa unabii wa Ezekieli, hawajaitwa watoke ndani, ila badala yake wameachwa ndani. {ABN3: 44.1}

JE! MNYAMA NI UTAWALA WA SERIKALI YA KIRAIA NA YA KIDINI?

Swali Namba 58:

Je! “Kichwa” ambacho “kilitiwa jeraha la mauti” (Ufu. 13:3) hakiwakilishi utawala wa serikali ya kiraia na ya kidini ya Vizazi vya Kati? {ABN3: 44.2}

Jibu:

Wale ambao huelewa kwamba kichwa kilichojeruhiwa cha yule mnyama kama chui (Ufu. 13:1-3) huwakilisha Roma katika kipindi chake cha kidini bila shaka pia huelewa kwamba “pembe ndogo,” ambayo ilikuwa na “macho ya mwanadamu, na kinywa kilichonena maneno makuu” (Dan. 7:8), vile vile huwakilisha Roma kabla ya kichwa kujeruhiwa. Kuielewa mada hii kwa usahihi, ni muhimu kuuchunguza mfano huu wenye awamu mbili kuanzia chini hadi juu, kuanzia kwa mtazamo wa Danieli. {ABN3: 44.3}

Ikiwa na “macho ya mwanadamu” na “kinywa,” “pembe ndogo” kwa kweli ni pembe yenye kichwa,

44

jambo la kipekee kati ya serikali nyingi, uongozi mseto wa serikali za kiraia na za kidini zilizoshirikishwa katika kiongozi mmoja mwenye enzi kuu wakati wa Zama za Giza na za Kati, “utukufu uliokuwa wa Roma.” {ABN3: 44.4}

Kwa hivyo, shirikisho la zama za kati la tawala za kiraia na za kidini katika kanisa la Kirumi hutoa ufunguo wa ufasiri wa pembe na kichwa, ukithibitisha kwamba kichwa ambacho kilitiwa jeraha la mauti ni mfano wa sehemu ya kidini tu. Maana kwa yule mnyama kama chui, Rumi haiwakilishwi na ama pembe iliyojeruhiwa au kichwa chenye pembe, bali na kichwa kilichotiwa jeraha tu, ambacho huonyesha kwamba pigo liliathiri, sio nusu ya kiraia, serikali (pembe), lakini nusu tu ya kidini, kanisa (kichwa). {ABN3: 45.1}

JE! MBONA MAONO YOTE MAWILI SIO SAWA?

Swali Namba 59:

Iwapo Danieli 7:8, 25 na Ufunuo 13:3 zote hubashiri utawala huo huo, na ikiwa kanisa la Roma wakati wa Zama za Kati ndilo lle lililotabiriwa, kwa nini, katika maono ya Danieli, ni mseto wa utawala wa kiraia na wa kidini (pembe yenye kichwa), ilhali katika Ufunuo ni utawala wa kidini pekee (kichwa)? {ABN3: 45.2}

Jibu:

Kwamba utawala ule ule umefananishwa kwa wanyama wote wawili wanaonekana bila kokosea kutoka kwa ukweli kwamba wote “walimkufuru” kwa urefu sawa wa wakati: wa awali, kwa “wakati na nyakati mbili, na nusu

45

wakati” (Dan. 7:25); na wa mwisho, kwa” miezi arobaini na miwili” (Ufu. 13:5). Kipindi hiki pia kimeelezwa katika kitabu cha Ufunuo 11:3, na vile vile kimewakilishwa katika Ufunuo 12:14. kama “wakati, na nyakati mbili, na nusu wakati,” ambao kwa mujibu wa kanuni ya ufasiri ya Ezekieli 4:6, ni sawa na: “muda wa nusu wakati” au “nusu ya wakati” — 1/2 ya mwaka: katika jumla ni sawa na miaka 3 1/2, miezi 42, au siku 1260 (miezi 12 kwa mwaka, na siku 30 kwa mwezi, hesabu ya Biblia). {ABN3: 45.3}

Maono ya Danieli hutabiri tu kuanzishwa kwa shirikisho hilo la kanisa na serikali ya nchi, na kwa sababu hii haswa Yohana alipewa kuonyesha hatua yake ya mwisho, kuvunjwa kwayo tu. Kwa hivyo maono yote mawili hukamilisha yote — kuanzishwa na kuvunjwa. {ABN3: 46.1}

ZIWA LA MOTO LINAWAKA AU LIMEZIMIKA WAKATI WA MILLENIA?

Swali Namba 60:

Iwapo yule mnyama na nabii wa uongo wanatupwa katika ziwa la moto kabla ya millenia (Ufu. 19:20), na Ibilisi baada ya millenia (Ufu. 20:10), je! Moto huu utaendelea kuwaka kati ya matukio hayo mawili? {ABN3: 46.2}

Jibu:

Moto unaweza kuwa wa mfano, jinsi mengi ya Ufunuo yalivyo. Lakini uwe ni moto halisi au kitu kingine, sio lazima

46

Utawaka katika millenia yote, lakini unaweza kuwashwa tena baadaye. {ABN3: 46.3}

NI SEHEMU NDOGO TU HAIJAKANYAGWA?

Swali Namba 61:

Katika Trakti Namba 9, “Tazama Nivifanya Vitu Vyote Upya,” Toleo la 1942, uk. 38 ni taarifa: “Sehemu hiyo ya nchi mpya ambayo miguu ya waovu itakuwa imekanyaga…itatakaswa na moto utakaokuja “ukishuka kutoka mbinguni kwa Mungu.” Tumefundishwa kwamba katika ufufuo wa pili, waovu watatoka makaburini mwao kutoka kila sehemu ya nchi. Ikiwa ni hivyo, basi inawezekanaje kwamba watakanyaga sehemu yake ndogo tu? {ABN3: 47.1}

Jibu:

Sehemu ya nchi mpya ambayo miguu ya waovu haitakanyaga na kuitia unajisi, ndio ile sehemu ambayo Mji Mtakatifu umetua. {ABN3: 47.2}

NANI AMBAYE ALITOA AMRI YA TATU?

Swali Namba 62:

Nimejifunza kwa makini mfano wa hekalu jinsi unavyopatikana katika “Fimbo ya Mchungaji,” Gombo la 2, lakini siwezi kuona jinsi Dario anaweza kufanywa mwanzilishi wa amri ya tatu, isipokuwa uchukue msimamo kwamba alitoa amri mbili. Unawezaje kutatua utata huu? {ABN3: 47.3}

Jibu:

Biblia hutangaza kwamba Hekalu lilimalizika kwa amri ya Koreshi, Dario, na Artashasta, “katika mwaka wa sita wa kutawala kwa Dario Mfalme.” Ezra

47

6:14,15. Kwa sababu amri ya Artashasta ya Ezra 7, kulipamba hekalu, sio kulijenga (aya ya 27), ilifanywa baada ya hizo tatu zilizotajwa hapo awali, kwa hivyo haiwezi kuwa amri ya Artashasta ya Ezra 6:14. Hivyo, zilikuwapo amri tatu za kulijenga, na moja kuipamba: (1) moja ya Koreshi (Ezra 1:2-4); (2) moja ya Dario (Ezra 6:11, 12); (3) moja ya Artashasta, iliyoandikwa; (4) moja ya Artashasta, iliyoandikwa (Ezra 7:21- 26). {ABN3: 47.4}

Kwa hivyo ni kwamba amri ya Artashasta ya sura ya 7, ikiwa ya tatu kwenye kumbukumbu, imetofautishwa hivyo, kana kwamba kwa kweli inaweza kuwa ya nne. Basi, lazima zilikuwapo amri mbili za Artashasta. {ABN3: 48.1}

Ujenzi wa hekalu ulipomalizika “katika mwaka wa sita wa utawala wa Dario” (Ezra 6:15), sio katika utawala wa Artashasta, basi iwapo amri ya Dario sio ya tatu na ya mwisho, lazima ihitimishwe kwamba Dario ambaye alitawala wakati Hekalu lilipokamilishwa hakutoa amri. {ABN3: 48.2}

Iwapo mapunguzo yetu hayatakuwa sahihi, na ikiwa nuru zaidi juu ya mada hii inakuwa muhimu, ni hakika kwamba Bwana hatatuweka tusiijue. Kwa sababu wakati huu, hata hivyo, jambo linalopendeza haina mahangaiko yoyote, latosha jibu lililopeanwa. {ABN3: 48.3}

48

546 AU 547 K.K?

Swali Namba 63:

Katika Trakti Namba 3 “Hukumu na Mavuno,” Toleo la 1942, uk. 37, kuhesabu, kwa mujibu wa mchoro, huweka tarehe ya mwanzo wa unabii wa siku 2300 wa Danieli 8:14 kutoka 456 K.K, ilhali “Pambano Kuu,” uk. 328, huweka tarehe hiyo kutoka 457 K.K. Je! Unapatanishaje hizo mbili? {ABN3: 49.1}

Jibu:

Kushughulikia kipindi kirefu cha unabii kwa namba kamili tu, Trakti huhesabu kurudi nyuma miaka 2300 kutoka 1844, na hivyo kubainisha mwanzo wa hicho kipindi kama 456 K.K. Pambano Kuu, hata hivyo, inashughulikia ukweli kwamba kipindi hicho kilianza, sio katika mwezi wa kwanza wa mwaka kwa mujibu wa kalenda ya sasa, lakini badala yake katika mwezi wa saba (Oktoba yetu) ya mwaka kulingana na kalenda ya Musa (Kut. 12:2). {ABN3: 49.2}

Tofauti inaonekana kutoka mchoro unaofuata. Sehemu yake ya juu hushughulikia katika maneno ya ile trakti; sehemu yake ya chini, katika maneno ya Pambano Kuu. {ABN3: 49.3}

49

50

WOTE AU MABAKI — KINA NANI?

Swali Namba 64:

Warumi 9:27 husema kwamba “mabaki” ya Israeli wataokolewa, lakini Warumi 11:26 husema kwamba Israeli “wote” wataokolewa. Sielewi hili. Unaweza kunisaidia? {ABN3: 51.1}

Jibu:

Warumi 9:27 inazungumza juu ya Israeli kama taifa, ambalo mabaki tu ndio wataokolewa; ilhali Warumi 11:26 inarejea kwa wateule wa Israeli kama mtu mmoja mmoja, wote ambao wataokolewa. {ABN3: 51.2}

WACHACHE AU WENGI WAOKOLEWA?

Swali Namba 65:

“Mpango wa wokovu ulikuwa umekamilishwa,” husema “Maandishi ya Awali,” uk. 281, “lakini wachache ndio walichagua kuupokea.” Taarifa hii hutumiwa sana dhidi ya fundisho la “umati mkubwa” jinsi linavyofundishwa na Wadaudi. Je! Utaitatua tafadhali? {ABN3: 51.3}

Jibu:

Ingawa wakati wa ukasisi Wake duniani Yesu aliomboleza kwamba “wengi wameitwa, lakini ni wachache waliochaguliwa” (Mat. 20:16), hata hivyo muda mrefu kabla, kupitia Isaya, Alikuwa ametangaza katika ahadi ya kinabii kwa kanisa: “Malango yako nayo yatakuwa wazi daima; hayatafungwa mchana wala usiku; ili watu wapate kukuletea utajiri wa mataifa, na wafalme wao wakiongozwa pamoja nao …. Mdogo atakuwa elfu, na

51

na mnyonge atakuwa taifa hodari: Mimi Bwana nitayahimiza hayo katika wakati wake.” Isa. 60:11, 22. {ABN3: 51.4}

“Na itakuwa katika siku za mwisho, mlima wa nyumba ya Bwana utawekwa imara juu ya milima, nao utainuliwa juu ya vilima; na mataifa yote watauendea makundi makundi. Na mataifa mengi watakwenda na kusema, njoni, twende juu mlimani kwa Bwana, nyumbani kwa Mungu wa Yakobo, Naye atatufundisha njia Zake, nasi tutakwenda katika mapito Yake maana katika Zayuni itatoka sheria, na neno la Bwana katika Yerusalemu. Naye atafanya hukumu katika mataifa mengi, atawakemea watu wa kabila nyingi; nao watafua panga zao ziwe majembe, na mikuki yao iwe miundu; taifa halitainua upanga juu ya taifa lingine, wala hawatajifunza vita tena kamwe. Enyi wa nyumba ya Israeli, njoni, tutembee katika nuru ya Bwana.” Isa. 2:2-5. {ABN3: 52.1}

Na kupitia nabii Zekaria, Yeye aliandika tena ahadi: “Mataifa mengi yatajiunga na Bwana katika siku hiyo.” Zek. 2:11. {ABN3: 52.2}

“Hata itakuwa, ya kwamba katika nchi yote mafungu mawili yatakatiliwa mbali, nao watakufa, asema Bwana; lakini fungu la tatu litabaki humo. Nami nitalileta fungu lile la tatu na kulipitisha kati ya moto,

52

Nami nitawasafisha kama fedha isafishwavyo, Nami nitawajaribu kama dhahabu ijaribiwavyo; wataliitia jina Langu, Nami nitawasikia; Mimi nitasema, watu hawa ndio Wangu; nao watasema, Bwana ndiye Mungu wangu.” Zekaria 13:8, 9. {ABN3: 52.3}

Isitoshe, wakati katika Maandishi ya Awali, uk. 281, mwandishi anasema, “lakini wachache ndio walichagua kuupokea,” katika Pambano Kuu, uk. 665, yeye huweka umati mkubwa wa Ufunuo 7:9 kama kundi tofauti na wafia imani na wengine wote ambao watafufuliwa, hivyo basi kuonyesha wazi kwamba “umati mkubwa” sio waliofufuliwa bali ni walio hai waliohamishwa bila kufa. Hili pia lathibitishwa na Mashauri kwa Walimu, uk. 532. {ABN3: 53.1}

Sasa, iwapo tutaufikia ukweli, lazima tuifasiri taarifa hiyo katika Maandishi ya Awali na ile iliyo katika Mathayo 20:16, kwa njia ya kupatana na Isaya 60:11, 22; Zekaria 2:11; 13:8, 9; Pambano Kuu, uk. 665, na vifungu vingine, ambayo vyote huonyesha kwamba kutakuwa na umati mkubwa. {ABN3: 53.2}

Hakuna mwanafunzi mwelekevu wa Biblia angejenga nadharia juu ya ufasiri ambao utampelekea kuweka kando maandiko mengine yote kwenye mada hiyo. Atatafuta kufanya uchanganuzi wake wa mwisho kwa njia ya kuwa katika upatano kamili na yote, au sivyo akiri kwamba hana nuru kwa mada hiyo. {ABN3: 53.3}

Katika nuru safi ya Biblia na ya vifungu vya Roho ya Unabii vilivyotajwa hapa, uzito wa ushahidi bila kupingwa

53

huongoza kwenye hitimisho kwamba umati mkubwa utaokolewa. Ukweli unadhihirika, basi, kwamba “wachache” humaanisha wale waliookolewa kwa kila mwito wa ujumbe katika vizazi vya zamani, ule wakati kabla ya “mavuno.” Lakini katika kufunga historia ya ulimwengu, wakati wa mavuno ya injili, kutakuwapo kukusanywa kukubwa kwa nafsi zilizokombolewa, “umati mkubwa ambao hakuna mtu anayeweza kuuhesabu.” Neno “mavuno” humaanisha uvunaji kama huo. {ABN3: 53.4}

Hivyo kwa ulinganisho na hesabu ya jumla ya waliopotea katika vizazi vyote, idadi ya jumla ya waliookolewa ni wachache; lakini bila kulinganisha, idadi ya jumla ya waliookolewa katika vizazi vyote, kwa hesabu halisi, ni wengi. Kwa ukweli huu yathibitisha maneno ya Ezekieli: “Basi, nilitabiri kama Alivyoniamuru, pumzi ikawaingia, wakaishi, wakasimama kwa miguu yao, jeshi kubwa mno.” Ezek. 37:10. {ABN3: 54.1}

Kwa sababu wokovu wa watu wengi hukinzana na mpango wa Ibilisi, basi, tusifanye kazi kwa ajili ya maslahi yake. {ABN3: 54.2}

UTAKUWA UPANDE GANI?

Swali Namba 66:

Je! Wadaudi hulionaje dhehebu la Waadventista wa Sabato? Je! Wao huchukua msimamo gani kuhusu maandishi ya Bi. E.G. White na Mlima Karmeli husimamia nini? {ABN3: 54.3}

Jibu:

Wadaudi Waadventista wa Sabato huamini kwamba kanisa la Waadventista

54

wa Sabato lilitiwa wakfu na mbingu na kutwikwa ujumbe maalum kwa ajili ya ulimwengu, lakini katika mkondo wa wakati liliruhusu lenyewe kuridhika, kuwa vuguvugu, na la kutojali katika kutekeleza majukumu yake matakatifu; na ya kwamba hivyo baada ya kukengeuka “kuacha kumfuata Kristo Kiongozi wake,” tangu wakati huo limekuwa “pole pole likirudi kuelekea Misri,” na tokeo la kusikitisha na baya sana kwamba “mwenendo wake wa kurudi nyuma umelitenga” na Mungu. — Kimenukuliwa, uk. 217. {ABN3: 54.4}

Tena Wadaudi huamini kwamba ukengeufu huu wa kutisha kumwacha Bwana unadhihirika wazi kabisa katika hiyo hali iliyogawanyika iliyofunuliwa katika dhehebu la Waadventista wa Sabato kwa mashindano yaliyo ndani yake “kati ya amri za Mungu na amri za wanadamu.” — Shuhuda, Gombo la 5, uk. 81. Hadi mwisho yatatatuliwe uwepo umoja na nguvu, lazima kabisa ili kanisa liweze kutimiza hatima yake ya upeo, Wadaudi bado huamini kwamba, kama ilivyoandikwa, “dhahabu itatenganishwa kutoka kwa takataka kanisani.” Katika maneno mengine, wao huamini kwamba kina Mamboleo, wale ambao wametoa heshima kubwa kwa “eti sayansi iitwavyo kwa uongo,’…wanaoamini katika akili, ustadi, au talanta” (Kimenukuliwa, uk. 80), watapepetwa kutoka kwa Wahafidhina — kutoka kwa wale ambao “wanasimama katika nuru … wakiugua na kulia kwa sababu ya machukizo yanayofanyika katika nchi.” — Kimenukuliwa, uk. 209. {ABN3: 55.1}

55

Ieleweke, hata hivyo, upesi kwamba, tofauti na wale wanaosisitiza wazi mitazamo yao ya umamboleo, Waadventista wa Sabato Mamboleo hushusha mielekeo hii, na kwa dhati hukiri kusimama kidete kwa misingi ya Uadventista wa Sabato, ingawa bila wao kujua pole pole huteleza zaidi na zaidi kutoka kwayo (Kristo Haki Yetu, Toleo la 1941, uk. 36). {ABN3: 56.1}

Kwamba kuteleza huku kunatambuliwa kama hatari halisi na wengine hata ndani ya kanisa, huonekana kutoka kwa makala yaliyochapishwa katika Mapitio na Kutangaza, Julai 2, 1936, yenye kichwa, “Umamboleo — Utumizi wa Kibinafsi:” {ABN3: 56.2}

“Kadiri tunavyotazama kwa wasiwasi kuenea upesi kwa Umamboleo kati ya makanisa mbalimbali ya Kiprotestanti, ni vyema kuyaangalia maisha yetu wenyewe, kuona iwapo kanuni na mienendo ile ile yawezekana haikuwa imeanza kutumika huko. Ilhali mafundisho na kanuni za Waadventista wa Sabato ni za Kihafidhina, ipo hatari kubwa kwamba sisi mmoja mmoja tunaweza kuwa Wamamboleo. {ABN3: 56.3}

“Ili kufahamu hatari hii vyema, inafaa kuzingatia tofauti muhimu kati ya Mhafidhina huliamini neno la Mungu kama mamlaka ya kukata maneno; ilhali Mmamboleo huamini katika ufasiri wa neno la Mungu kwa mujibu wa mawazo yake ya kibinadamu, na hivyo kuweka mawazo yale juu ya Mungu wa ufunuo. {ABN3: 56.4}

56

“Katika siku hizi za mwisho, Mungu hajazuilia ufunuo Wake kwetu kama watu kwa Maandiko tu, lakini pia ametupatia maagizo maalum kupitia kwa udhihirisho wa Roho ya Unabii…. {ABN3: 57.1}

“Kwa hivyo wakati makanisa maarufu huonyesha mienendo yao ya Umamboleo dhidi ya Biblia, inawezekana sisi kuonyesha mtazamo kama huo kwa jumbe maalum za Mungu kwetu. Kwa kweli, uhusiano wetu na Shuhuda ndio haswa mahali ambapo mtazamo huu utadhihirishwa kwanza.” {ABN3: 57.2}

Aina hii hatari ya umamboleo, inadhoofisha “imani ya watu wa Mungu katika Shuhuda” (Shuhuda, Gombo la 4, uk. 211), na polepole “kupanga upya” kanuni za msingi wa Dhehebu (Shuhuda kwa Wachungaji, uk. 48, 69, 70, 360, 372, 373, 409) ni ushahidi wa kuvunja moyo kwamba wale walio kwa uongozi wake ni Wamamboleo. Lakini wakionekana kutokuwa na hatia ya ukweli huo, na kukana kwao kuihusu, hufanya iweze kuwa vigumu sana kwetu kufanya lolote kuwasaidia, bila juhudi zetu kueleweka vibaya. Na kukazia hatia kwa kuanza kuteleza kutoka kwa misingi ya imani iliyowekwa na Mbingu leo, haiwezekani kama kumtafuta mwalimu wa kwanza wa Kiyahudi ambaye aliweka mahali pa “asema Bwana,” asema yeye mwenyewe au mtu mwingine yeyote. Hakika, yule wa kuajibishwa uasi huu haiwezekani kumtambua kama ilivyo tarehe ambayo kazi ya uovu ilianza. Uvuvio

57

husema: “Wapo leo ambao watawasilisha udanganyifu kama kweli za kupima, kama vile Wayahudi walivyowasilisha semi za wanadamu kama mkate wa mbinguni. Maneno yasiokuwa na thamani hupeanwa kwa watu wa Mungu kama fungu lao la chakula, ilhali nafsi zina njaa ya mkate wa uzima. Hadithi zilizotungwa kwa werevu zimebuniwa na wanadamu wanajaribu kufuma hizi hadithi kwenye utando. Wale ambao hufanya hivi siku moja wataona kazi yao kama inavyotazamwa na wapelelezi wa mbinguni. Wao huchagua kuleta kuni kwenye msingi, nyasi, na mabua, wakati wanalo neno la Mungu katika uthibiti wao na utajiri wote na nguvu, ambayo wanaweza kukusanya hazina za thamani za ukweli. Chakula kinachotayarishwa kwa ajili ya kundi kitasababisha ugonjwa wa kiroho, kuzorota, na kifo. Wakati wale wanaodai kuuamini ukweli wa sasa watapata fahamu zao wanapolipokea neno la Mungu jinsi linavyosema, wakati hawatajaribu kupotosha Maandiko, wataleta kutoka katika hazina ya moyoni mambo mapya na ya zamani, kuwaimarisha wenyewe na wale wanaowafanyia kazi.” — Mapitio na Kutangaza, Juni 18, 1901. {ABN3: 57.3}

Aidha, Wadaudi hushikilia kwamba imani kwamba Roho ya Unabii itakuwa kanisani hadi mwisho wa wakati, ni mojawapo wa jiwe la msingi la Uadventista wa Sabato. “Zawadi hii ya kinabii iliyotolewa,” hukiri Mzee A.G. Daniels, “ilipaswa kuwa na kanisa kutoka kwa Adamu hadi ujio wa pili wa Bwana na Mwokozi wetu Yesu Kristo atakapokuja kuwachukua waliokombolewa Wake

58

hadi Paradiso. Haikukoma na mitume, lakini inaweza kufuatiliwa kupitia karne nyingi hadi siku za mwisho za historia ya wanadamu, kabla tu ya kurudi kwa Bwana wetu. Wakati tukio hilo kuu la vizazi vyote litatukia, basi — na sio mpaka wakati huo — yatatimia yaliyonenwa na mtume Paulo: {ABN3: 58.1}

“‘…Bali ukiwapo unabii utabatilika; zikiwapo lugha, zitakoma; yakiwapo maarifa, yatabatilika. Kwa maana tunafahamu kwa sehemu; na tunafanya unabii kwa sehemu; lakini ijapo ile iliyo kamili, iliyo kwa sehemu itabatilika.’ — 1 Kor 13:8-10, A.R.V.” — Ya kudumu Zawadi Ya Unabii, uk. 6. {ABN3: 59.1}

Kwa sababu zawadi hii ya kinabii ilidhihirishwa kupitia kwa Dada White, kama ilivyothibitishwa kwa kweli, yeye lazima, wakati huo, aliandika chini ya Uvuvio wa Mungu, kama walivyofanya waandishi wa Biblia. Na, kwa hivyo, Uadventista wa Sabato halisi huegemea ukweli muhimu kwamba “hakuna unabii katika Maandiko upatao kufasiriwa kama apendavyo mtu fulani tu,” na hauwezi kueleweka zaidi sasa bila nuru maalum ya Mungu kuliko ambavyo unabii ungeeleweka katika wakati wa Danieli bila kutiwa nuru na malaika, aliyefafanua: “Nitakuonyesha yaliyoandikwa katika maandiko ya ukweli. Wala hapana anisaidiaye juu ya hao ila huyo Mikaeli Mkuu wenu.” Dan. 10:21. Hivyo tu, Mikaeli yule yule lazima amtume “mwalimu” kwetu leo;

59

vinginevyo yale mambo yapasayo amani yetu “yatafichwa machoni petu.” Luka 19:42. {ABN3: 59.2}

Mwamba huu thabiti wa fundisho ulipaswa daima kuwa msingi wa hakika wa Dhehebu, na kwa kiwango kwamba kanuni zake zimefuatwa kwa uaminifu imekuwapo nguvu kanisani. {ABN3: 60.1}

Baada ya kifo cha Dada White, mwaka 1915, zawadi ya Uvuvio, amilifu Roho ya Unabii, ikawa kimya, haikuendelea tena kujidhihirisha Yenyewe kwa muda. Wakati kanisa limekatwa kabisa kutoka kwa chanzo cha uhai wake, lilivyokuwa kanisa la Kiyahudi kutoka kwa kifo cha nabii Malaki hadi kuinuka kwa Yohana Mbatizaji, lingewezaje kudumisha nguvu na ukuaji wake? Kwa hivyo, sasa kama wakati huo, umefuata utapiamlo wa kiroho ule ule usioweza kuepukika na ulemavu, ukifuatana na msafara mrefu wa matatizo. {ABN3: 60.2}

Dhidi ya haya mandharinyuma ya giza kuporomoka kiroho na ugonjwa (unyonge, umaskini wa shida, upofu, na uchi), na mwisho unaokaribia (kutapikwa nje), inasimama wazi nakshi thabiti kazi maalum iliyochongwa ya Kituo cha Mlima Karmeli, kama kilivyofanya kilele kilichowaka moto cha Karmeli ya zamani kati ya ibada ya sanamu na uozo wa Israeli iliyo asi. Tena mfano unakutana na uakisi. Lakini kwa Israeli wa Mungu leo, malaika asema: “Ninyi mmetenda vibaya sana kuliko wao.” — Shuhuda, Gombo la 1, uk. 129. {ABN3: 60.3}

“Kama nyundo ya kuuvunja moyo mgumu; kama moto wa kuteketeza takataka” (Shuhuda, Gombo la 5, uk. 254), sauti ya Karmeli inapiga kelele kwa Laodekia onyo ambalo limepuuzwa: “Nimejaa huzuni wakati ninapowaza hali yetu kama watu. Bwana hajaifunga Mbingu kwetu, lakini mwenendo wetu wa kurudi nyuma umeendelea kututenga na Mungu. Kiburi, tamaa, na kuipenda dunia vimeiishi ndani ya moyo bila hofu ya kupigwa marufuku au kuhukumiwa. Dhambi za kuudhi na za kiburi zimekaa kati yetu. Hata hivyo maoni ya jumla ni kwamba kanisa linanawiri, na ya kwamba amani na ustawi wa kiroho upo katika mipaka yake yote.” {ABN3: 60.4}

“Kanisa limekengeuka na kuacha kumfuata Kristo Kiongozi wake, na badala yake linarudi pole pole kuelekea Misri. Lakini wachache wametiwa hofu au kushangaa kwa upungufu wao wa nguvu za kiroho.Shaka na hata kutoziamini Shuhuda za Roho wa Mungu, kunatia chachu makanisa yetu kila mahali. Shetani anatazamia iwe hivyo. Wachungaji wanaohubiri ubinafsi badala ya Kristo wanatazamia iwe hivyo. Shuhuda hazisomwi na haziwekwi maanani. Mungu amenena kwenu. Nuru imekuwa ikiangaza kutoka kwa neno Lake na katika Shuhuda, na zote mbili zimedunishwa na kupuuzwa. Matokeo ni dhahiri kwa ukosefu wa usafi na moyo wa ibada na imani thabiti miongoni mwetu.” — Shuhuda, Gombo la 5, uk. 217. {ABN3: 61.1}

“Sasa ni wakati ambao tunapaswa kuungana kwa karibu na Mungu, ili tuweze kufichwa wakati ukali wa ghadhabu Yake

61

inamwaga juu ya wanadamu. Tumetanga mbali na mipaka ya zamani. Hebu turudi. Ikiwa Bwana ni Mungu, mtumikie: iwapo ni Baali, mtumikie. Unachagua kuwa upande gani?” — Shuhuda, Gombo la 5, uk. 137. {ABN3: 61.2}

Na sasa inaendelea kuvuma zaidi na zaidi sauti ya Karmeli, kupitia mfululizo wa machapisho ya Fimbo ya Mchungaji, “sauti ya Bwana … kwa mji, na,” asema Mungu Mwandishi, “mtu wa hekima ataliona jina lako: isikieni hiyo Fimbo, na Yeye aliyiagiza.” Mika 6:9. {ABN3: 62.1}

“Walishe watu wako,” Anaamuru, “kwa fimbo yako, kundi la urithi wako, wakaao pekee yao mwituni, katikati ya Karmeli.” Mika 7:14. {ABN3: 62.2}

Kwa hivyo kuwaokoa waaminifu katika Laodekia kutoka kwa njaa na kifo cha kiroho, kuwahuisha, kuwarejesha, na kuwahami tena kwa pambano la mwisho, Bwana ameituma Fimbo. {ABN3: 62.3}

Wakati kazi hii ya urejesho imekamilishwa kwa mujibu wa Mathayo 17:11, na mambo ya Umamboleo “yamekatiliwa mbali” kama ilivyoamriwa katika Ezekieli 9 na katika Shuhuda, Gombo la 5, uk. 80, wakati huo utaonekana kanisani utimizo wa haraka wa maneno ya Kristo: “Mvua ikanyesha, mafuriko yakaja, pepo zikavuma, zikaipiga ile nyumba;” na ikasimama. Mat. 7:25. {ABN3: 62.4}

Kama waasisi wa mapema wa kanisa la Adventista, wale wanaotii Fimbo ndio

62

warejeshaji wa “mapito ya zamani;” wao hutambua matokeo mabaya yanayohusika katika kwenda kinyume na nuru yoyote ambayo Bwana huchagua kutuma kwa watu Wake. Na kwa vile ujumbe wa Fimbo umeamsha shauku kwa hitaji la “matengenezo kati ya watu wa Mungu,” sisi kama Wadaudi hatungekuwa tu waongo kwa amana yetu lakini pia tungekuwa tunapitia “upande ule mwingine,” tukiruhusu kanisa letu pendwa la Waadventista wa Sabato kujikokota mavumbini, ndugu zetu wapotee, na ulimwengu unaotuzunguka uangamie kwa “kukosa maarifa,” iwapo hatungezinduka kulionya kanisa kuhusu hatari inayokuja. {ABN3: 62.5}

Bidii yetu isiyokuwa na ubinafsi na juhudi ya kuwasaidia ndugu wote Mamboleo Waadventista wa Sabato, bila kujali jamii yao, utaifa, au nafasi zao za kijamii, ni ushahidi tosha wa upendo wetu kwao na kujitolea kwa ajili yao. Tunaamini pamoja na mtume Paulo kwamba wote ni watoto wa Adamu watoto waliofanywa kuwa katika familia ya Mungu kupitia kwa Bwana na Mwokozi wetu Yesu Kristo. {ABN3: 63.1}

Ingawa tunatambua ukuu wa lengo letu, lakini pamoja na ujasiri kamili kwa Kiongozi wetu, Ambaye hajawahi kushindwa kufanikisha awamu yoyote ya kusudi la Mungu, tunaikabili kazi yetu kwa ujasiri na imani, tukiamini kwamba “tunaweza kukwea na kuimiliki ile nchi” ya urithi wetu, na mwishowe kuingia katika Kanaani ya mbinguni, ambako “ maziwa na asali “yatatiririka milele. {ABN3: 63.2}

63

Kwa sababu ya hitaji, basi, Kituo cha Mlima Karmeli kimejengwa kama kituo cha shughuli za mafunzo na kuwafanya watendakazi wafae kuupeleka ujumbe huu maalum kwa kanisa; kuwaelimisha vijana wanaostahili; kuwatunza maskini anayestahiki, wakongwe, wajane, na mayatima; na kwa kuwahudumia wagonjwa na wadhaifu kulingana na mpango wa Mungu. Kimekuwa na maagizo ya Mungu maradufu kwacho: “Piga kelele, usiache, paza sauti yako kama tarumbeta, uwahubiri watu Wangu kosa lao, na nyumba ya Yakobo dhambi zao.” Isa. 58:1. {ABN3: 64.1}

“Pigeni tarumbeta katika Zayuni, takaseni saumu, kusanyeni kusanyiko kuu; kusanyeni watu, litakaseni kusanyiko, kusanyeni wazee, kusanyeni watoto, na hao wanyonyao maziwa; Bwana arusi na atoke chumbani mwake, na bibi arusi katika hema yake.” Yoeli 2:15, 16. {ABN3: 64.2}

Wakati kimekamilisha hii “kazi ya kufunga kwa kanisa” (Shuhuda, Gombo la 3, uk. 266), wakati huo wale ambao wameshinda kila “jaribu katika nguvu zake Mwenye Uwezo,” ambao wameugua na kulia na kuokoka kuangamizwa “watakuwa kama Daudi, na nyumba ya Daudi itakuwa kama Mungu, kama malaika wa Bwana mbele yao.” Zek. 12:8. Wadaudi kweli kweli! — “watu wakuu tena wenye nguvu” (Yoeli 2:2), “likiwa limevikwa silaha za haki ya Kristo,… ‘zuri kama mwezi, safi kama jua, la kutisha kama jeshi lenye mabango,… likienda mbele duniani kote, likishinda

64

na kushinda.” — Manabii na Wafalme, uk 725. {ABN3: 64.3}

Kwa njia hii Wadaudi Waadventista wa Sabato watawakusanya watakatifu wote katika nyumba ya Bwana. {ABN3: 65.1}

Mzigo mkubwa wa Mlima Karmeli ni kuifanya kazi hii nyingi haraka iwezekanavyo, ili tuweze basi kurudi nyumbani katika pumziko letu la milele, kutoendelea tena kufungwa na minyororo ya dhambi. {ABN3: 65.2}

KULIOKOA KANISA AU ULIMWENGU?

Swali Namba 67:

Iwapo, kwa saa hii ya mwisho, tunatoa bidii yetu yote kwa wokovu wa kanisa, ulimwengu wote utafikiwa vipi? {ABN3: 65.3}

Jibu:

Utume wa kuokoa ulimwengu hauwezi kuwa muhimu zaidi kuliko utume wa kuliokoa kanisa. Kuongeza ushirika wa kanisa chini ya hali za sasa za uvuguvugu wa Ulaodekia, hakuwezi tena kuuendeleza Ufalme wa Kristo kuliko vile kungalifanywa chini ya hali za ndani ya kanisa la Kiyahudi katika siku za ujio Wake wa kwanza. Kuelewa hali halisi katika kanisa hilo, Yohana Mbatizaji na Kristo mwenyewe na hata mitume mwanzoni, walijishughulisha kufanya kazi, sio kwa ulimwengu kwa ujumla, bali kwa manufaa ya ndugu zao kanisani. {ABN3: 65.4}

Kama mwondoko uleule kutoka kwa Kristo uko ndani ya kanisa sasa kama ulivyokuwa

65

wakati huo (Shuhuda, Gombo la 5, uk. 217), itachukua juhudi kubwa zaidi kuwaokoa watu kutoka kwa “udanganyifu wa kusikitisha” wa Ulaodekia (Shuhuda, Gombo la 3, uk. 253), kuliko ikiwa wangalikuwa katika ukafiri. Kwa maana katika Laodekia wamefanywa kuamini kwamba wanayo kweli yote inayohitajika kuwa nayo, kwamba wao ni matajiri wamejitajirisha, na hawana haja ya kitu — wokovu wao umehifadhiwa milele maadamu wanao ushirika kanisani! Kwa hivyo ipo hatari kubwa ya wao kupoteza nafsi zao ndani ya kanisa wakati likiwa “vuguvugu” na karibu kutapikwa nje, kuliko iwapo wataendelea kukaa ulimwenguni hadi kanisa liamke kutoka kwa kulala kwake, na kujipaka dawa ya macho (Ukweli) — lione kwa usahihi, litende haki, na liongoze na kulisha kundi vyema. {ABN3: 65.5}

Kila mshiriki mwaminifu aulize swali, iwapo kanisa lenyewe halijaokolewa (Shuhuda, Gombo la 3, uk. 253), halimfuati Kristo Kiongozi wake (Shuhuda, Gombo la 5, uk. 217) na “limekuwa kahaba” (Shuhuda, Gombo la 8, uk. 250), linawezaje kuwaokoa wengine? Hitaji kubwa kwa hivyo kwanza ni kuwaokoa wale walio kanisani, kisha wale walio ulimwenguni. Ile “kazi maalum ya utakaso, ya kuondoa dhambi, kati ya watu wa Mungu” (Pambano Kuu, uk. 425), “kazi ya kufunga kwa kanisa, katika wakati wa kutiwa muhuri watu mia na arobaini na nne elfu” (Shuhuda, Gombo la 3, uk. 266), lazima ije kwanza, kisha itafuata ya kutiwa muhuri wale wa ulimwenguni. {ABN3: 66.1}

66

Watu na raslimali ambazo tayari zimetumika kwa kazi ya umishonari kwa ulimwengu ni nyingi sana kuliko raslimali chache zilizopo za kuupeleka ujumbe kwa Walaodekia, ingawa kanisa linalo hitaji kubwa zaidi kuliko ulimwengu. {ABN3: 67.1}

Hata hivyo, kuupeleka ujumbe kwa kanisa hakuathiri kazi ya utume kwa ulimwengu, maana wakati Wadaudi hufanya kazi kwa maslahi ya kanisa, Dhehebu huupeleka ujumbe wa zamani kwa ulimwengu. Lakini iwapo Wadaudi pia watumie wakati wao na fedha kushughulikia masilahi ya mataifa, basi kanisa na ulimwengu vitatumbukizwa kuzimu. Kwa hivyo, ili kuuokoa ulimwengu, lazima kwanza tutafute kuliokoa kanisa kutokana na uharibifu ulio karibu sana, kama walivyofanya Yohana Mbatizaji, Kristo, na mitume, katika siku zao. {ABN3: 67.2}

Baada ya kanisa kuamka na kukoma kuota kwamba “ni tajiri, na limejitajirisha,” ligundue kwamba linahitaji kila kitu badala ya “sufuri,” lijivike nguvu zake kwa kumwelekea Kiongozi wake, lijivike mavazi ya haki Yake, na kutoruhusu aliye najisi kuingia tena ndani yake (Isa 52:1), kisha haki yake itatoka kama mwangaza na wokovu wake kama taa iwakayo. Na mataifa wataiona haki yake, na wafalme wote wataona utukufu wake (Isa. 62:1, 2). Basi litaweza kuokoa

67

hakika. Kisha “malango yako nayo yatakuwa wazi daima; hayatafungwa mchana wala usiku; ili watu wapate kukuletea” wewe “utajiri wa mataifa, na wafalme wao wakiongozwa pamoja nao. Kwa maana kila taifa na ufalme wa watu wasiotaka kukutumikia” wewe “wataangamia; naam, mataifa hayo wataharibiwa kabisa.” Isa. 60:11, 12. {ABN3: 67.3}

Hebu waamini wote wa Ukweli wa sasa, kwa hivyo, waufuatilie mkondo huu hadi kwa kilele chake cha furaha: “Imba, ufurahi, Ee binti Zayuni; maana, tazama, Naja, Nami nitakaa kati yako, asema Bwana. Na mataifa mengi watajiunga na Bwana katika siku ile, nao watakuwa watu Wangu; Nami nitakaa kati yako, nawe utajua ya kuwa Bwana wa majeshi amenituma kwako.” Zek. 2:10, 11. {ABN3: 68.1}

Bado zaidi, si kwamba ni sisi, bali Kristo Ambaye “anachukua mamlaka katika mikono Yake mwenyewe” (Shuhuda kwa Wachungaji, uk. 300), sio wajibu wetu kumwambia ni kazi gani inapaswa kufanywa, na ni ipi inapaswa kuachwa bila kufanywa, lakini hebu kila mfuasi Wake atambue kwamba Yeye “atatenda katika kazi hii ya mwisho kwa namna iliyo kinyume sana kwa utaratibu wa kawaida wa mambo, na kwa njia ambayo itakuwa kinyume na mpango wowote wa wanadamu.” — Shuhuda kwa Wachungaji, uk. 300. {ABN3: 68.2}

Usiwe kama daraja ambalo “linahoji na kukosoa kila kitu ambacho huinuka katika kukunjua kwa ukweli” (Shuhuda, Gombo la 5, uk. 690), lakini uwe kama wale “ambao huruhusu Mbingu iongoze.” — Shuhuda kwa Wachungaji, uk. 475. {ABN3: 68.3}

68

Amri kwetu ni: “Piga kelele usiache, paza sauti yako kama tarumbeta, uwahubiri watu Wangu kosa lao, na nyumba ya Yakobo dhambi zao.” Isa. 58:1. {ABN3: 69.1}

“Piteni, piteni, katika malango; itengenezeni njia ya watu; tutieni, tutieni barabara; toeni mawe yake; twekeni bendera kwa ajili ya kabila za watu. Tazama, Bwana ametangaza habari mpaka mwisho wa dunia, mwambieni binti Zayuni, tazama, wokovu wako unakuja; tazama, thawabu Yake i pamoja Naye, na malipo Yake yako mbele Yake.” Isa. 62:10, 11. {ABN3: 69.2}

KUTAKASWA NA MUNGU, AU NA SHETANI?

Swali Namba 68:

Je! Kanisa litatakaswa kabla ya utekelezwaji wa amri ya mnyama kama ilivyotabiriwa katika Ufunuo 13:15-17? Au je! Amri hii kali itakuwa njia ya kulitakasa kanisa kwa kuwapepeta kutoka kwalo wale ambao sio waaminifu kwa Ukweli? {ABN3: 69.3}

Jibu:

Iwapo ni kweli kwamba amri ya huyo mnyama ni kuwapepeta nje watu ambao hawajaongoka (magugu) waliomo kanisani, basi mtu lazima ahitimishe kwamba yule mnyama sio nembo ya utawala wa kanuni kama ya joka, bali shirika lililotumwa na mbingu, lililotumwa kuyatupa nje magugu ambayo joka ameleta ndani! {ABN3: 69.4}

Kutoka kwa Ezekieli 9 tunaona kwamba sio “mnyama”, ila malaika wanapaswa kutekeleza hili. Baada ya

69

yule aliye na kidau cha wino wa mwandishi kiunoni mwake kutia alama kwa wale ambao huugua na kulia kwa sababu ya machukizo yanayofanyika kati yao, watano wenye silaha za kuchinjia wanafuata ili kuwachinja wote walioachwa bila alama. Na utakaso huu mkubwa, jinsi unabii wenyewe na Shuhuda hutaarifu haswa, unatukia kanisani. (Tazama Shuhuda kwa Wachungaji, uk. 445; Shuhuda, Gombo la 3, uk.266, 267; Shuhuda, Gombo la 5, uk. 210, 211; pia Trakti Namba 1, Viunganishi vya Biblia.) {ABN3: 69.5}

Ni lengo lililopangwa kimbele na Shetani kulichafua kanisa kwa kuzidisha badala ya kupunguza washirika wasio waaminifu. Na ikiwa amri yake kali ni kulitakasa kanisa, basi ni kwa kusudi gani Bwana “analijia ghafla hekalu Lake … na … kuketi kama asafishaye fedha na kuitakasa” (Mal. 3:1-3); mbona ujumbe wa kusababisha upepeto (Maandishi ya Awali, uk. 270); na kwa nini malaika wa Ezekieli 9, wale “watakaotokea” ili “kuwatenga waovu kutoka kati ya wenye haki”? Mat. 13:49. {ABN3: 70.1}

Je! Huu mzigo wa kazi ya utakaso, ni ya Shetani au ya Bwana? Shetani hafanyi chochote kulitakasa kanisa, lakini anafanya kila kitu kulichafua. {ABN3: 70.2}

Kwa hivyo amri ya mnyama na utekelezwaji wake mkali, sio kwa kusudi la kulitakasa kanisa, lakini ni kwa kusudi la kuzuia njia ya kutoka

70

Babeli, kwa hivyo kuushika ulimwengu mateka. Hili analifanya haswa kusitisha mtiririko thabiti wa umati wa waongofu kwa la wakati huo kanisa ambalo tayari limesafishwa na kutakaswa. Licha ya, hata hivyo, juhudi kubwa ya Adui kuwazuilia Babeli, waaminifu watatoka. Watatii ushauri wa Bwana: “Mtu awaye yote akimsujudu huyo mnyama na sanamu yake, na kuipokea chapa katika kipaji cha uso wake, au katika mkono wake, yeye naye atakunywa katika mvinyo wa ghadhabu ya Mungu iliyotengenezwa, pasipo kuchanganywa na maji, katika kikombe cha hasira Yake; naye atateswa kwa moto na kiberiti mbele ya malaika watakatifu, na mbele ya Mwana-Kondoo.” Ufu. 14:9, 10. {ABN3: 70.3}

WATOTO WACHANGA NA WAPAGANI WAOKOLEWA AU WAPOTEA?

Swali Namba 69:

Je! Watoto wachanga na wapagani wanaokufa bila kupata fursa ya kusikia injili ya Kristo na kumpokea Yeye kama Mwokozi wao, wataokolewa? Iwapo wanaweza kuokolewa hivyo katika ujinga wao, mbona basi wote wasiweze kuokolewa? {ABN3: 71.1}

Jibu:

Kama wasioijua injili wangeokolewa katika ujinga wao, basi ingalikuwa bora zaidi ya kwamba kanisa liuache ulimwengu wote bila habari ya injili, ili wote waweze kuokolewa. Lakini hapana! hakuna mtu anayeweza kuokolewa bila injili. {ABN3: 71.2}

71

Kuhusu wokovu wa watoto wachanga na watoto ambao wazazi wao wameokolewa, Roho ya Unabii husema: {ABN3: 72.1}

“Malaika ‘wanawakusanya wateule kutoka kwa pepo nne, kutoka mwisho mmoja wa mbingu hadi mwingine.’ Watoto wachanga wanachukuliwa na malaika watakatifu hadi kwa mikono ya mama zao. Marafiki waliotengwa kwa muda mrefu na kifo wameunganishwa, asilani wasiachane tena, na kwa nyimbo za furaha wanapanda pamoja hadi kwa mji wa Mungu.” — Pambano Kuu, uk. 645. {ABN3: 72.2}

“Ndivyo imani ya mwanamke huyu ilipewa thawabu. Kristo, Mtoaji mkuu wa Uhai, akamrejesha mtoto wake kwake. Vivyo hivyo waaminifu Wake watapewa thawabu, kwa ujio Wake, kifo kinapoteza uchungu wake, na kaburi limeporwa ushindi ulilodai. Kisha Atawarejeshea watumwa Wake watoto ambao wamechukuliwa kutoka kwao na kifo. “Bwana asema hivi, Sauti imesikiwa Rama, kilio, na maombolezo mengi, Raheli akiwalilia watoto wake; asikubali kufarijiwa kwa watoto wake, kwa kuwa hawako, Bwana asema hivi, Zuia sauti yako, usilie, na macho yako yasitoke machozi; maana kazi yako itapata thawabu,… nao watakuja tena toka nchi ya adui; ndivyo asemavyo Bwana. Na lipo tumaini katika mwisho wako, asema Bwana, ya kuwa watoto wako watarudi tena katika mpaka wao wenyewe.” — Manabii na Wafalme, uk. 239. {ABN3: 72.3}

Na kuhusu wokovu wa watoto ambao wazazi wao wamepotea, Bwana anaamuru: {ABN3: 72.4}

72

“Waueni kabisa, mzee, na kijana, na msichana, na watoto wachanga, na wanawake; lakini msimkaribie mtu ye yote mwenye hiyo alama; tena anzeni katika patakatifu Pangu. Basi, wakaanza kwa wazee waliokuwa mbele ya nyumba.” Ezek. 9:6. {ABN3: 73.1}

“Kisha Yoshua, na Israeli wote pamoja naye, wakamtwaa Akani, mwana wa Zera, na ile fedha, na lile joho, na ile kabari ya dhahabu, na wanawe, na binti zake, na ng’ombe zake, na punda zake, na kondoo zake, na hema yake, na vitu vyote alivyokuwa navyo, wakavileta juu hata bonde la Akori.” Yoshua akasema, “Mbona umetufadhaisha hivi? Bwana atakufadhaisha wewe leo. Ndipo Israeli wote wakampiga kwa mawe, kisha wakawateketeza kwa moto, na kuwapiga kwa mawe.” Yos. 7:24, 25. {ABN3: 73.2

Kutoka kwa vifungu hivi vilivyovuviwa, tunaona kwamba watoto wachanga na watoto wanaokolewa tu kwa sababu ya uaminifu wa wazazi wao. Ni jukumu zito lililoje, la ajabu, na la kutisha! {ABN3: 73.3}

Mintarafu mtumwa wa kipagani, tunasoma: “Naliona kwamba bwana wa mtumwa atawajibikia nafsi ya mtumwa wake ambaye amemweka bila kujua; na dhambi za mtumwa huyo zitajiliwa kwa bwana wake. Mungu hawezi kumpeleka mbinguni mtumwa ambaye amewekwa katika ujinga na kudunishwa, bila kujua lolote kumhusu Mungu au Biblia, asiyeogopa chochote isipokuwa kiboko cha bwana wake, na kushikilia nafasi ya chini kuliko wanyama.

73

Lakini Yeye humfanyia jambo bora zaidi ambalo Mungu mwenye huruma anaweza kufanya. Anamruhusu kuwa kama hakukuwa.” — Maandishi ya Awali, uk. 276. {ABN3: 73.4}

Ni dhahiri, kwa hivyo, kwamba wale ambao hawakuwa na fursa ya kujifunza ukweli wa wokovu, hawatapata adhabu ile ambayo waovu walio na habari watapata, ingawa hawawezi kupewa uzima wa milele. {ABN3: 74.1}

JE! KUWAKUSANYA WATU KUTOKA KWA MATAIFA YOTE KUTATIA NDANI WATU WEUSI?

Swali Namba 70:

Je! andiko, “Kushi itamnyoshea Mungu mikono yake mara” (Zab. 68:31), humaanisha kwamba jamii za watu weusi zitamwelekea Mungu? {ABN3: 74.2}

Jibu:

Ijapokuwa hakuna watu ambao wameokolewa kama taifa, andiko linalohojiwa, likichukuliwa na vifungu vinavyofanana, kwa kweli huonyesha kwamba kutakuwa na kukusanywa kukubwa kutoka Kushi. Ni ukusanywaji kama huo kutoka katika kila taifa, jamaa, lugha, na watu wa ulimwengu ambao ndio watajumuisha “umati mkubwa” wa Ufunuo 7:9. “Wakuu watatoka Misri” (Zab. 68:31) maandiko yasema. “Na mataifa mengi watakwenda na kusema, njoni, twende juu mlimani kwa Bwana, na nyumbani kwa Mungu wa Yakobo; Naye atatufundisha njia Zake, nasi tutakwenda katika mapito Yake; kwa maana katika

74

Zayuni itatoka sheria, na neno la Bwana litatoka Yerusalemu.” Mika 4:2. {ABN3: 74.3}

“Na Mataifa wataona haki yako, na wafalme wote watauona utukufu wako; nawe utaitwa jina jipya, litakalotajwa na kinywa cha Bwana.” Isa. 62:2. {ABN3: 75.1}

Akitazama mbele kwa ukusanywaji huu mkubwa, nabii anauliza swali: “Ni nani hawa warukao kama wingu, na kama njiwa waendao madirishani kwao!” Ndipo Bwana anajibu: “Hakika yake visiwa Vitaningojea, na merikebu za Tarshishi kwanza, ili kuleta wana wako kutoka mbali, na fedha yao na dhahabu yao pamoja nao, kwa ajili Yake Mtakatifu wa Israeli, kwa kuwa Amekutukuza wewe. Na wana wa wageni watajenga kuta zako, na wafalme wao watakuhudumu; maana katika ghadhabu Yangu Nalikupiga, Lakini katika upendeleo Wangu Nimekurehemu. {ABN3: 75.2}

“Malango yako nayo yatakuwa wazi daima; hayatafungwa mchana wala usiku; ili watu wapate kukuletea utajiri wa mataifa, na wafalme wao wakiongozwa pamoja nao. Kwa maana kila taifa na ufalme wa watu wasiotaka kukutumikia wataangamia; naam, mataifa hayo wataharibiwa kabisa. Utukufu wa Lebanoni utakujia wewe, mberoshi na mtidhari na mteashuri pamoja; ili kupapamba mahali Pangu patakatifu;

75

Nami Nitapatukuza mahali pa miguu Yangu. Na wana wa watu wale waliokutesa watakuja kwako na kukuinamia; nao wote waliokudharau watajiinamisha hata nyayo za miguu yako; nao watakuita, mji wa Bwana, Zayuni wa Mtakatifu wa Israeli.” Isa 60:8-14. “Kwa maana siku ya Yezreeli itakuwa kuu.” Hos. 1:11. {ABN3: 75.3}

JE! MATAIFA WATAURITHI UFALME?

Swali Namba 71:

Je! Israeli ya kiroho hufanyizwa na Mataifa? Je! Niko sawa kusema kwamba uhusiano wa Mataifa kwa Israeli ni ule wa mwingizo? {ABN3: 76.1}

Jibu:

Utakuwapo mti mmoja tu wa familia katika Ufalme, mti wa Yakobo, ambao Mataifa wamepandikizwa, kama inavyoonekana kutoka Warumi 11. {ABN3: 76.2}

Hili limeonyeshwa zaidi na mji mtakatifu ambao hauna lango la Mataifa, lakini kila mojawapo wa malango kumi na mbili ina jina moja la makabila kumi na mawili ya Israeli. Kwa hivyo, Mataifa huokolewa kupitia mwingizo — kupandikizwa ndani ya mzeituni wa asili, na hivyo kufanywa raia asili wa Israeli wanaurithi Ufalme. {ABN3: 76..3}

JE! NI NANI YEYE ANAYESITA-SITA?

Swali Namba 72:

Je! Unaweza kufafanua Mika 4:6, 7? {ABN3: 76.4}

76

Jibu:

“Katika siku ile, asema Bwana, Nitamkusanya yeye anayesita-sita, Nami Nitamrudisha yeye aliyefukuzwa, na yeye Niliyemtesa. Nami Nitamfanya yeye aliyechechemea kuwa mabaki, na yeye aliyetupwa mbali kuwa taifa lenye nguvu, na Bwana atawamiliki katika mlima Zayuni tangu sasa na hata milele.” Mika 4:6, 7. {ABN3: 77.1}

Aya hizi zinaleta kwa mtazamo mataifa matatu: “yeye anayesita-sita,” “yeye aliyetupwa,” na yeye “aliyeteswa.” {ABN3: 77.2}

Katika mfano wa mpanzi wa mbegu, tunaambiwa kwamba “naye aliyepandwa penye miamba, huyo ndiye alisikiaye lile Neno, [bila kusita-sita] akalipokea mara kwa furaha; lakini hana mizizi ndani yake, bali hudumu kwa muda; ikitukia dhiki au udhia kwa ajili ya lile Neno, mara huchukizwa;… Naye aliyepandwa penye udongo mzuri, huyo ndiye alisikiaye lile Neno, na kuelewa nalo; yeye ndiye azaaye matunda, huyu mia, na huyu sitini, na huyu thelathini.” Mat. 13:20, 21, 23. {ABN3: 77.3}

Tofauti kati ya aina mbili za udongo ni kwamba mbegu kwenye miamba, udongo usio na kina huota haraka, ilhali mbegu kwenye mzuri, udongo wa kina huota polepole. {ABN3: 77.4}

Kutoka kwa somo hili la mfano tunaona kwamba “yeye anayesita-sita” ndiye aliyepokea mbegu katika udongo mzuri, kanisa la Kikristo.

77

Na ndilo linalohitaji kukusanywa kwa sababu limetawanyika na kugawanyika katika mitengano. Wakati huo, likiwa limekusanyika, litajumuisha “masalia” wa mwanamke. Ufu 12:17. {ABN3: 77.5}

Yeye “aliyetupwa mbali” hawezi kuwa mwingine isipokuwa ufalme wa makabila kumi, na yeye “aliyeteswa” ni ufalme wa makabila mawili, Yuda, kama itakavyoonekana kwa kusoma sura ya tatu ya Mika. {ABN3: 78.1}

“Yeye anayesita-sita,” kanisa la Kikristo, Bwana atalifanya kuwa masalia: Atawatenga watoto wake haramu, magugu, kutoka kwake. “Na yeye aliyetupwa mbali,” ufalme wa makabila kumi, Ataufanya kuwa “taifa lenye nguvu; naye Bwana atawamiliki katika Mlima Zayuni tangu sasa hata milele.” Mika 4:7. Na kwa Yuda “kusanyiko la watu litakuwa.” Mwa. 49:10. {ABN3: 78.2}

Wazawa wa hawa watatu — wake “yeye anayesita-sita” (kanisa la Kikristo la kwanza pamoja na Mataifa waliongoka); ya “yeye aliyetupwa mbali” (waliotawanywa wa Israeli — ufalme wa makabila kumi); na yeye “aliyeteswa” (ufalme wa makabila mawili, Yuda) — wanajumuisha kanisa la Ufalme. {ABN3: 78.3}

Ndivyo raia ambao ni shina la Ufalme, wataongoka na kukusanywa kutoka katika kanisa la Kikristo na kutoka kwa wazawa wa falme mbili za zamani, Israeli na Yuda, kisha kuletwa kwa Mlima Zayuni, kwa sababu “Bwana ayapenda

78

malango ya Zayuni kuliko maskani zote za Yakobo. Umetajwa kwa mambo matukufu, Ee mji wa Mungu. Nitataja Rahabu na Babeli miongoni mwao wanaonijua. Tazama Filisti, na Tiro, na Kushi; huyu alizaliwa humo. Naam, mintarafu Zayuni itasemwa, huyu na huyu alizaliwa humo. Na Yeye Aliye juu Ataufanya imara. Bwana atahesabu, Awaandikapo mataifa, huyu alizaliwa humo. Selah. “ Zab 87:2-6. {ABN3: 78.4}

NDOA AU USEJA?

Swali Namba 73:

Paulo husema: “Ndugu, muda uliobaki si mwingi; basi tokea sasa, kwamba wote walio na wake wawe kana kwamba hawana.” “Ila nipendalo ni kwamba watu wote wawe kama mimi nilivyo.” 1 Kor. 7:29, 7. Humaanisha nini? {ABN3: 79.1}

Jibu:

Kulielewa kwa usahihi fundisho la mtume la ndoa na useja, kama lilivyowekwa katika aya zinazohojiwa, na ili kupata mtazamo sahihi kwa lengo lake na kwa mambo ambayo anajadili, ni muhimu kwanza kuitazama sura hiyo kwenye mpangilio kamili. {ABN3: 79.2}

1 Wakorintho 7:1 hufichua kwamba alikuwa ameipokea barua, na jibu lake kwayo (katika sura hii) huonyesha kwamba miongoni mwa waumini katika kanisa la Korintho, kulikuwa na kutoridhika na ukosefu wa uelewa kwa uhusiano wa ndoa.

79

Wengine hawakuridhika na fungu lao la maisha ya upweke; wengine walikuwa wamechoka na fungu la maisha yao ya ndoa; ilhali bado wengine walihoji kama waweze kuwaacha waume au wake zao wasioamini, na wafunge ndoa upya. {ABN3: 79.3}

Kujitahidi siku zote kuwatendea watu wote mema, na kuzuia uwezekano wowote wa makabiliano katika kanisa hilo changa, Paulo kwa busara na kwa uwazi anaelezea manufaa yote ya mali asili ya ndoa na ya mali asili ya upweke. {ABN3: 80.1}

Kuhusu wale ambao hawajaoa na wajane, anasema: “Ni heri wakae kama mimi nilivyo. Lakini ikiwa hawawezi kujizuia, na waoe; maana ni afadhali kuoa kuliko kuwaka tamaa.” 1 Kor. 7:8, 9. {ABN3: 80.2}

“Na kwa wale waliofunga ndoa” — kwa wale wanandoa ambao kila mmoja wao alimwamini Kristo, na kwa wale wanandoa ambao mmoja wao hakuamini — anaandika: “Nawaagiza, wala hapo si mimi, ila Bwana, Mke asiachane na mumewe: … tena mume asimwache mkewe. Lakini watu wengine nawaambia mimi, wala si Bwana, ya kwamba iwapo ndugu mmoja ana mke asiyeamini, na mke huyo anakubali kukaa naye asimwache. Na mwanamke, ambaye ana mume asiyeamini, na mume huyo anakubali kukaa naye, asimwache mumewe.” 1 Kor. 7:10-13. {ABN3: 80.3}

Katika hotuba hii fupi, tunaona kwamba mtume hatetei useja, lakini anahimiza wazi wazi kwamba ili “kuepuka zinaa,

80

… kila mwanamume awe na mke wake mwenyewe, na kila mwanamke awe na mume wake mwenyewe. “1 Kor 7: 2. {ABN3: 80.4}

Huwasihi wote waume na wake ambao ni waamini, lakini ambao hawaishi pamoja vyema, kujaribu ikiwa inawezekana kuishi kwa amani na kila mmoja. Na pale ambapo mmoja ni mwamini kwamba aaminiye anapaswa kujaribu kumwongoa mwenzi asiye amini (1 Kor. 7:14). Anaongeza, hata hivyo, kwamba ikiwa yule asiyeamini ataondoka, “ndugu au dada hayuko chini ya kifungo katika masuala kama hayo.” 1 Kor. 7:15. {ABN3: 81.1}

Kwa uelekevu sawa, hufundisha kwamba iwapo wawili wa imani sawa waamue kutengana, hawapaswi kufunga ndoa na mwingine, lakini wajaribu kupatana (1 Kor. 7:11). Bado ana furaha, hata hivyo: “Umefunguliwa? Usitafute mke.” 1 Kor. 7:27. “Kila mtu na akae katika hali ile ile aliyokuwa nayo alipoitwa” (1 Kor. 7:20), na ajifunze kuridhika jinsi “Nimejifunza, kuwa radhi na hali yoyote ile niliyo nayo.” Filip. 4:11. {ABN3: 81.2}

Hali ya sasa ya maisha ikiwa ni ya muda mfupi, aliwahimiza kwa wakati uliopo kuweka matumaini yao, sio kwa mambo ya ulimwengu huu, bali kwa utukufu wa ulimwengu ujao, maana “jicho halijayaona, wala sikio halijayasikia, wala hayakuingia katika moyo wa mwanadamu, mambo ambayo Mungu amewaandalia wampendao.” 1 Kor. 2:9. {ABN3: 81.3}

Wakati hali hii ya furaha, takatifu imefikiwa, basi itakuwa kwamba “wale walio

81

na wake na wawe kama hawana; na wale waliao kama hawalii; na wale wafurahio kama hawafurahi; na wale wanunuao, kama hawana kitu. Na wale wautumiao ulimwengu huu, kama hawautumii sana; kwa maana mambo ya ulimwengu huu yanapita.” 1 Kor 7:29-31. {ABN3: 81.4}

Yaani, wale ambao sasa wanao wake hawatanufaika nao zaidi katika maisha ya baadaye kuliko kama hawakuwa nao; wala wale wanaonunua sasa, wakati huo hawatamiliki zaidi ya wale ambao hawanunui kitu sasa; lakini wote — waliofunga ndoa na wapweke, wale wanaoomboleza na wale wanaofurahi, wale wanunuao na wale wasionunua — wakati huo watakuwa katika hali sawa, ili kwamba wote wafurahi pamoja, “kwa maana mambo ya ulimwengu huu yanapita.” “Basi hivyo amwozaye mwanamwali wake afanya vema; na yeye asiyemwoza atazidi kufanya vema. {ABN3: 82.1}

“Mwanamke hufungwa maadamu mumewe yu hai, lakini ikiwa mumewe amefariki, yu huru kuolewa na mtu ye yote amtakaye; katika Bwana tu. Lakini heri yeye zaidi akikaa kama alivyo; ndivyo nionavyo mimi, nami nadhani ya kuwa mimi nami nina Roho wa Mungu.” 1 Kor. 7:38-40. {ABN3: 82.2}

Hakuna popote katika ushauri huu wa ndoa kwamba Paulo analazimisha agizo na mfano wake kwa kupendelea kabisa mali asili moja ya maisha kupita nyingine, wala kukomesha manufaa ya haki za ndoa iliyotakaswa

82

yaliyohakikishwa kwa agano la ndoa. {ABN3: 82.3}

Wale ambao huamua wenyewe kuongozwa kuchagua ndoa, na ambao wameazimia kwenenda katika kicho kwa utukufu wa Mungu, ni lazima watafunga ndoa “tu katika Bwana:” hawatajitwalia aidha makafiri au waamini wasio waongofu wa kidunia na wasiomcha Mungu. Wenye hekima watakumbuka siku zote utambuzi kwamba mavazi na tabia za kidunia haziwezi kumvutia Mkristo wa kweli na kwa hivyo haziwezi kuleta muungano wa kweli wa Ukristo wenye furaha, na wa kudumu. Wataweka mapenzi yao tu kwa mtu ambaye ni mwaminifu, anayejitahidi, mwenye bidii na mwamilifu anayejali sana mambo ya kiroho mfuasi wa Ukweli wa Sasa. {ABN3: 83.1}

Na hitaji sawa la muhimu kwa ufanisi wa hii bora zaidi lakini iliyo ngumu shughuli ya maisha ni kwamba wala mtu asiingie ndani yake mapema, bila kufanya maandalizi muhimu kamili. Kwa hivyo, hakuna kijana mvulana Mdaudi mcha Mungu ambaye anaweza kimaadili kuruhusu kutafakari ndoa isipokuwa aweze kuwa ambaye, mapema katika maisha ameamua ni biashara au taaluma gani inayomfaa, ameweka lengo lake, na aidha amelifikia au yu karibu kulifikia, amejenga nyumba na kuipamba au anazo raslimali za kufanya hivyo, au angalau amejenga au ana uwezo wa kujenga moja. {ABN3: 83.2}

Kujaribu kuchukua magumu, mazito, na majukumu

83

ya kufadhaisha kuisimamisha nyumba kwa mpangilio wa Mungu, bila kufanya maandalizi yote muhimu yaliyotajwa hapa, mmoja anaweza kutarajia kidogo kukuza nguvu za mwili, kiakili na kiroho ambazo Mkristo amekusudiwa na Mungu kupata. Kupuuza hili, atafanya maisha yawe magumu na ya laana, na kwa gharama ya kuhuzunisha atakua msumbufu wa ardhi badala ya baraka kwa nchi. Badala ya kuwa muungwana anayejitegemea, atakuwa mnyonge wa kuwategemea wengine; badala ya kuwa mvuto wa kuinua jamii, atakuwa yule anayeidhoofisha; badala ya kuwatosheleza watoto wake fursa ya usalama unaofaa, akiwapatia malezi na mafunzo ambayo kila mwanadamu anastahili, atakuwa baba wa watoto wa bahati mbaya, wanaoishi kwa uwezekano wote kufikia mwisho duni wa wasiofaa. {ABN3: 83.3}

Kila kijana mvulana Mdaudi mcha Mungu ataepuka msiba kama huu kwa kujiandaa kikamilifu kwa ajili ya uzoefu huu mkubwa maishani kabla ya kujitosa ndani yake. Atakumbuka kwamba kabla Bwana hajamleta mwanadamu awepo, Yeye aliiumba nchi makao ya mwanadamu, na kisha akaipamba kwa nuru, hewa, chakula, na maji, na kichaka, mti na nyasi, na ndege, mnyama wa mwitu, na ng’ombe. Na akijua hili, atafanya vilevile. {ABN3: 84.1}

Licha ya kufikia sifa hizi zote muhimu za ustahili, mume mtarajiwa anayekuza mafanikio ya ndoa, hatachukua hatua ya ndoa kabla

84

hajahitimu kufanya majukumu ya mke nyumbani iwapo ataweza kuwa mgonjwa, adhoofike kimwili au afe, au yamjie majukumu mengine kwa sababu isiyotarajiwa. {ABN3: 84.2}

Kwa upande mwingine, hakuna kijana mwanamke Mdaudi mcha Mungu ambaye anaweza kimaadili kuruhusu kutafakari ndoa isipokuwa amepata ujuzi wa nyumbani na kuweza kutekeleza kila jukumu la nyumbani. Iwapo anaweza kuidumisha nyumba ikiwa safi na maridadi na kwa mpangilio; iwapo anaweza kwa ustadi kupika, kufua, na kushona; ikiwa anaweza kuwatunza wagonjwa na kufanya huduma ya kwanza; iwapo anaweza kwa busara kuwatunza watoto; ikiwa anaweza kuotesha kiunga cha mboga kuokoa pesa na kusambaza kwa meza yake mboga nyingi ambazo zimetoka kuchumwa (maana zinapochumwa, siku kadhaa kabla zitumike, hupoteza vitamini nyingi kupitia oksijeni); — iwapo anaweza kufanya haya yote, basi anastahili heshima ya kuwa mke mwema; amepata saruji ya muungano thabiti, wa kudumu. Hata hivyo, ingawa, wa kuheshimu na kuheshimiwa jinsi ni lazima aweze kuwa, lazima pia awe na biashara au taaluma fulani iwapo mumewe awe mgonjwa au kuwa mlemavu au afe yeye anaweza kuiongoza nyumba na kutunza mahitaji yake na kuyakabili matatizo yake. {ABN3: 85.1}

Mwishowe, wote watafikiri vema na ukweli kwamba ni mara chache kwa chombo cha mwanamme mchanga kiakili, kimaadili, na kitaaluma kinafaa kwa majukumu ya ndoa kabla ya kufika katika umri wa miaka ishirini na minne — siku ya ukuaji kamili wa mwanamme

85

na ustawi, na ya kwamba mwanamke mchanga ni mara chache vivyo hivyo kuwa tayari kabla kufikisha umri wa miaka ishirini — siku ya ukuaji kamili na ustawi wa mwanamke. {ABN3: 85.2}

JE! SHERIA IMEBATILISHWA?

Swali Namba 74:

Paulo anaandika: “Mtu mmoja afanya tofauti kati ya siku na siku, mwingine aona siku zote kuwa sawasawa. Kila mtu na athibitike katika akili zake mwenyewe. Yeye aadhimishaye siku, huiadhimisha kwa Bwana; naye alaye, hula kwa Bwana, kwa maana amshukuru Mungu; tena asiyekula, hali kwa Bwana, naye pia amshukuru Mungu.” Rumi. 14:5, 6. {ABN3: 86.1}

Katika nuru ya andiko hili, je! si kweli kwamba mtu huokolewa kwa imani bila kujali imani yake ya mafundisho labda katika Sabato na lishe? {ABN3: 86.2}

Jibu:

Baada ya kutarajia haswa swali hili, Uvuvio kupitia kwa Paulo na watendakazi wenzake walilijibu mara moja: {ABN3: 86.3}

“Basi, je! Twaibatilisha sheria kwa imani hiyo? Hasha: kinyume cha hayo, twaithibitisha sheria.” Rumi. 3:31. “Maana mtu awaye yote atakayeishika sheria yote ila akajikwaa katika neno moja, amekosa juu ya yote.” Yakobo 2:10. “Kwa maana huku ndiko kumpenda Mungu, kwamba tuzishike amri Zake: Na amri Zake si nzito.” 1 Yohana 5:3. “Heri wazifuao nguo zao, wawe na amri kuuendea huo mti

86

wa uzima, na kuingia mjini kwa malango yake.” Ufu. 22:14. {ABN3: 86.4}

“Ndugu zangu yafaa nini, mtu akisema ya kwamba anayo imani, lakini hana matendo? Je! Ile imani yaweza kumwokoa?…Vivyo hivyo na imani, isipokuwa ina matendo, imekufa, imekufa nafsini mwake….Wewe waamini ya kuwa Mungu ni mmoja, watenda vema: mashetani nao waaamini na kutetemeka. Lakini wataka kujua, wewe mwanadamu usiye kitu, kwamba imani pasipo matendo haizai?…Maana kama vile mwili pasipo roho umekufa, vivyo hivyo imani bila matendo imekufa.” Yakobo 2:14, 17, 19, 20, 26. {ABN3: 87.1}

Tena: baada ya kuandika, “Lakini ijapokuwa sisi, au malaika wa mbinguni, atawahubiri ninyi injili yoyote isipokuwa hiyo tuliyowahubiri, na alaaniwe” (Gal. 1:8), Paulo hangaliweza kamwe kuwa aligeuka na kutetea kwamba mtu anaweza kuokolewa kwa injili yake mwenyewe, kwa lile yeye mwenyewe anafikiri au kufanya. {ABN3: 87.2}

Hakuna mtu mwenye akili timamu anayeamini maandishi ya Paulo kama sehemu ya Maandiko Matakatifu anayeweza kujisadikisha kwa ukweli kwamba wakati mmoja Paulo angeiinua sheria na wakati ujao aikanyagie chini. Naam, kwa hivyo, ufasiri wa mmoja kwa maandishi ya mtume lazima uwe wa kuyafanya yapatane. {ABN3: 87.3}

Katika Warumi 14:5, 6 anajaribu kusahihisha shutuma sisizo za haki kwa kuwahimiza waamini kwamba kila mtu lazima ashawishike katika dhamiri yake mwenyewe, na ya kwamba

87

wajibu wa Mkristo ni kutunza, kunena, na kufundisha Ukweli, si kudai utiifu wake kwa huo; si kuwadharau wale wanaokula au wale wasiokula, au wale wanaoidhamisha siku moja kuliko nyingine; lakini kuwaruhusu wote washawishike kikamilifu katika dhamiri zao. Kwa ufupi jukumu la Mkristo ni kuwa mhisani, kuwa Mkristo kweli kweli, kuwa na nia yake mwenyewe, lakini kuwa tayari kuyaacha maoni yake kwa “Bwana asema hivi.” {ABN3: 87.4}

Kwamba Sabato na vile vile amri zingine zote ni za milele, za kutunzwa hata akhera, kila mmoja anaweza kuona kwa urahisi kutoka kwa maandiko yafuatayo: “Na itakuwa, mwezi mpya hata mwezi mpya, na sabato hata sabato wanadamu wote watakuja kuabudu mbele Yangu, asema Bwana.” Isa. 66:23. Na kutazama mbele kwa wakati wa “siku iliyo kuu na ya kutisha ya Bwana,” wakati tu ulio mbele yetu, Bwana huwaonya watu ambao watakuwa wanaishi kwa wakati huo: “Ikumbukeni torati ya Musa mtumishi Wangu, Niliyomwamuru huko Horebu kwa ajili ya Israeli wote, naam amri na hukumu. Mal. 4:4. {ABN3: 88.1}

“Bwana asema hivi, shikeni hukumu, mkatende haki; kwa maana wokovu Wangu u karibu kuja, na haki Yangu kufunuliwa. Heri afanyaye haya, na mwanadamu ayashikaye sana; azishikaye sabato asizivunje, auzuiaye mkono wake usifanye uovu wo wote. Wala mgeni, aambatanaye

88

na Bwana, asiseme hivi, hakika yake Bwana atanitenga na watu Wake; wala towashi asiseme, mimi ni mti mkavu. Kwa maana Bwana awaambia hivi matowashi, wanaozishika sabato Zangu, na kuyachagua mambo Yanipendezayo, na kulishika sana agano Langu; Nitawapa hawa nyumbani Mwangu, na ndani ya kuta Zangu, kumbukumbu na jina, lililo jema kuliko kuwa na wana na binti; Nitawapa jina lidumulo milele, lisilokatiliwa mbali. Na wageni, walioandamana na Bwana ili wamhudumu, na kulipenda jina la Bwana, kuwa watumishi Wake; kila aishikaye sabato asiivunje, na kulishika sana agano Langu; Nitawaleta hao nao hata mlima Wangu mtakatifu, na kuwafurahisha katika nyumba Yangu ya sala; makafara yao na dhabihu zao zitakubaliwa juu ya madhabahu Yangu; kwa maana nyumba Yangu itaitwa nyumba ya sala kwa mataifa yote. Bwana Mungu, akusanyaye waliofukuzwa katika Israeli asema pamoja na hayo Nitamkusanyia na wengine, zaidi ya hao walio wake waliokusanywa.” Isa. 56:1-8. {ABN3: 88.2}

Kwa hivyo sio Sabato tu bali pia sheria yote inapaswa kutunzwa sasa na hata milele na wote Myahudi na wa Mataifa, imani haiondolei mbali sheria ya Mungu, lakini badala yake huithibitisha milele, na humwezesha mtu kuitunza. {ABN3: 89.1}

Wale ambao wameongoka kikweli kwa Mungu kupitia haki ya Kristo, huwa hawapati

89

ugumu kutii sheria. Hupendezwa kutenda mapenzi ya Mungu. {ABN3: 89.2}

Na mwishowe, watakapoingia katika nchi ya ahadi na Mungu awape mioyo mipya na kuziandika amri Zake kwayo (Ezek. 36:23-29), wakati huo kwa waliotakaswa kujasiri kutenda dhambi, litakuwa jaribio kubwa la mara elfu kuliko lilivyokuwa kwa Yusufu huko Misri alipopiga kelele dhidi ya jaribu: “Nawezaje…kuufanya uovu huu mkubwa, nimkosee Mungu”? (Mwa. 39:9), na haiwezekani kabisa kuliko ilivyokuwa kwa Kristo. Hakika, dhambi itakuwa chukizo kwa kawaida kwetu sisi wakati huo jinsi kifo kilivyo sasa. Kristo hufanya hilo liwezekane kwa kuziosha dhambi zetu katika damu Yake ya thamani, akiumba ndani mwetu asili isiyo ya dhambi, “moyo mpya,” anapotutoa kutoka kati ya mataifa, na kutuleta katika “nchi yetu” wenyewe. Ezek. 36:24. {ABN3: 90.1}

JE! HATUJAOKOLEWA TUSIZITUNZE SHERIA?

Swali Namba 75:

Je! Ni sheria gani Wagalatia 3:13 hutaja? Je! Kuokolewa kutoka kwa laana ya sheria ya dhambi humaanisha ukombozi wa kutozitunza zile amri kumi? {ABN3: 90.2}

Jibu:

Sheria iliyozungumziwa katika Wagalatia 3:13 ni sheria ya amri kumi (Kut. 20:). Humfundisha mtu kwamba utiifu wake kwayo humletea baraka nyingi za: kudumisha uaminifu wake kwa Mungu na kwa mwanadamu; ikilinda

90

dini yake (Kut. 20:3-7) ikiwa imejengwa kwa Ukweli; daima ikimkumbusha kwamba Mungu aliumba mbingu na nchi kwa siku sita za kufanya kazi, ikimhifadhia fursa ya kuwa na Mungu wakati akipumzika kwa Siku Yake Takatifu — ya saba (Kut. 20:8-11); kuwafunza watoto kuheshimu wazazi wao (Kut. 20:12), ikimzuia mtu kuua (Kut. 20:13); ikihifadhi usafi wa moyo ndani ya wote, lakini haswa kuwalinda wanawake (Kut. 20:14); kutia ndani ya mtu uaminifu (Kut. 20:15) na kukuza uadilifu wa hali ya juu; kumkinga kutoka kwa udanganyifu (Kut. 20:16); na kumwokoa kutoka kwa utamanifu (Kut. 20:17). Ni kioo cha Mkristo, na ngao yake. {ABN3: 90.3}

Fundisho, kwa hivyo, ambalo huondoa utiifu kamili kwa sheria ya Mungu, maneno pekee ambayo Yeye ametujalia kwa vidole Vyake mwenyewe na kuinena hadharani kwa sauti Yake mwenyewe (Kut. 31:18; Kumb. 4:13, 14) ), kwa matokeo linaruhusu ibada ya miungu mingine, na hivyo kwa athari sio tu kuwafundisha Wakristo kumdhalilisha Baba wa uumbaji wote lakini hivyo basi pia huhimiza wazazi wote kuvunjiwa heshima, mbali na kukonyeza jicho kwa mauaji, uzinzi, kutofuata haki, kusema uongo, na kutamani. {ABN3: 91.1}

Kwa hivyo, ikiwa imekiukwa, sheria huleta laana; ikiwa itatunzwa isikiukwe, huleta baraka. (Angalia Kut. 20:5, 6; Ufu. 22:14.) Hakuna mtu, hata hivyo bila uongofu kamili anaweza aidha kuwa na mzigo au nguvu ya kuitunza isikiukwe. {ABN3: 91.2}

91

NI KWA KUSUDI GANI SANAMU ISIFANZWE?

Swali Namba 76:

Je! Amri ya pili ya Sheria kumi haikatazi mtu kuchonga, kusubu, kupaka rangi, au kuchora picha ya mfano wa kitu chochote kilicho mbinguni au duniani? {ABN3: 92.1}

Jibu:

Ili kuwa na hakika, amri ya pili hukataza kufanza mfano kwa kitu chochote, iwe ni cha mbinguni au cha duniani, kwa kusudi la kumwabudu Mungu. Wengine, hata hivyo, huchukua msimamo uliokithiri kwamba inakataza kufanza mfano wa aina yoyote kwa kitu chochote kwa sababu yoyote, hata kwa kusudi la kuelezea wazo. Kukemea hivi aina yoyote ya picha, iwe ni ya mandhari, ya ukutani, ya minara ya ukumbusho, ya upigaji picha, ya ujenzi, au yoyote, itakuwa ni kuharamisha chombo chote cha sanaa ya picha na sayansi — utekelezwaji wa msingi wa mfumo wa elimu ya ustaarabu. {ABN3: 92.2}

Walakini, ikiwa hilo ndilo kusudi la mapenzi Matakatifu ya amri, basi lazima tuitii bila kuhoji, na tutakuwa bora zaidi bila kujali matokeo. {ABN3: 92.3}

Biblia Yenyewe, hata hivyo, hufunua kwamba amri hiyo haikatazi kufanza mfano wowote ila kwa madhumuni ya ibada. Na hata Hutoa sababu ya lile katazo. Katika maandishi ya Musa, tunasoma: {ABN3: 92.4}

92

“Bwana akasema nanyi kutoka kati ya moto; mkasikia sauti ya maneno, lakini hamkuona umbo lo lote; sauti tu…Jihadharini nafsi zenu basi; maana hamkuona umbo la namna yo yote siku ile Bwana aliyosema nanyi kutoka kati ya moto; msije mkajiharibu nafsi zenu, mkajifanyia sanamu ya kuchonga, mfano wa sura yo yote, mfano wa mwanamume au mwanamke, mfano wa mnyama ye yote aliye duniani, au mfano wa ndege ye yote arukaye mbinguni, au mfano wa kitu cho chote kitambaacho juu ya ardhi, au mfano wa samaki ye yote aliye majini chini ya nchi; tena usije ukainua macho yako hata mbinguni, na ulionapo jua, na mwezi, na nyota, jeshi la mbinguni lote pia, ukashawishwa na kuviabudu, na kuvitumikia, ambavyo Bwana, Mungu wako amewagawanyia watu wote chini ya mbingu zote.” Kumb. 4:12, 15-19. {ABN3: 93.1}

Isitoshe, katika hekalu la Sulemani, mifano ya uumbaji wa Mungu ulitumika. Kwa mfano, Sulemani “akafanya kiti cha enzi kikubwa cha pembe, akakifunikiza kwa dhahabu iliyo safi. Kiti kile kilikuwa na daraja sita, tena na kikao cha miguu cha dhahabu, navyo vilikuwa vimeshikamana na kiti; na mikono huko na huko mahali pa kuketi, na simba wawili wakisimama kando ya hiyo mikono. Na simba kumi na wawili wamesimama juu ya daraja sita, huko na huko.” 2 Nya. 9:17-19. {ABN3: 93.2}

93

Tena akafanya bahari ya kuyeyuka, “na chini yake palikuwa na mifano wa ng’ombe, walioizunguka pande zote.” 2 Nya. 4:3. {ABN3: 94.1}

Kisha, pia, “makerubi yalinyosha mabawa yao juu ya mahali pa sanduku, makerubi yakalifunika lile sanduku na miti yake kwa juu.” 2 Nya. 5:8. {ABN3: 94.2}

Je! Hii haikuwa mifano ya viumbe ambavyo Mungu aliumba? Je! Bwana hakuongoza katika ujenzi huo? Amri, kwa hivyo, hukataza kujifanyia sanamu ya kubuni ya Mungu au ya kitu chochote kwa kusudi la ibada. {ABN3: 94.3}

(Italiki zote ni zetu)

======

HATUA YAKO ITAKAYOFUATA ITAKUWA NINI?

Sasa ikiwa umefurahia, umethamini, na kufaidika na safari hii ya maswali na majibu kupitia Kitabu Namba 3, na iwapo unatumaini kuendelea, basi tuma ombi kwa Kitabu Namba 4. Kitatumwa kama utumishi wa Kikristo bila malipo au wajibu. {ABN3: 94.4}

94

FAHARISI YA MAANDIKO

>