fbpx

Mtoa Jibu Kitabu Namba 1

Mtoa Jibu Kitabu Namba 1

Mtoa Jibu Kitabu Namba1

MTOA JIBU

Kitabu Namba 1

Maswali na Majibu kwa Mada za Ukweli wa Sasa

Katika Masilahi ya Ndugu Waadventista wa Sabato

na Wasomaji

wa

Fimbo ya Mchungaji

Na V.T. Houteff

Huyu “mwandishi,” mwenye elimu

ya ufalme wa

mbinguni, “hutoa

… vitu vipya na vya zamani.”

Mat. 13:52.

Sasa “mtakaseni Kristo Bwana mioyoni mwenu. Mwe tayari siku zote kumjibu kila mtu awaulizaye habari za tumaini lililo ndani yenu; lakini kwa upole na kwa hofu.”

1 Pet. 3:15.

2

 

Hakimiliki 1944, na

V.T. Houteff

Haki zote zimehifadhiwa

Kwamba kila mtu aliye na kiu kwa ajili ya ukweli aweze kuupata, kijitabu hiki cha maswali na majibu ni kama utumishi wa Ukristo, kinatumwa bila malipo. Kinaweka tu dai moja, wajibu wa nafsi kwa mwenyewe kuyathibitisha mambo yote na kushikilia sana lililo jema. Nyuzi za pekee zilizounganishwa na toleo hili la bure ni ncha za dhahabu ya Edeni na kamba nyekundu za Kalvari — mahusiano ambayo hufunga.

3

YALIYOMO

 

Jambo La Utangulizi la Mtoa Jibu ………………………………5

Shida ya Laodekia ni Nini? ……………………………………..29

Mbona Hitaji La Uamsho Na Matengenezo? …………………35

Je! Ni Nini Ishara Ya Uvuvio? ………………………………….39

Je! Shetani Anafanya Mauzo Ya Jumla Au

Reja Reja Ya Udanganyifu? …………………………………….60

Je! Roho Anenaje Kwa Laodekia? …………………………….69

Je! Ukweli Hufanya Mgawanyiko? ……………………………..76

Kristo au Mtumwa Wake? ………………………………………77

Je! Lipo Hitaji la Mafuta ya Ziada? …………………………….79

Mvua ya Masika — Lini? …………………………………………81

Je! Kilio Kikuu Kimeanza? ………………………………………82

Je! Mvua ya Vuli Ni Nguvu ya Pentekoste? …………………..85

Unapohitaji Ukweli, Mbona Uombe Nguvu? ………………….88

Miaka Arobaini Bila Kujaza Tena? …………………………….93

Je! Fimbo ya Mchungaji Huweka Tarehe za Kinabii? ……….94

Hatua Yako Inayofuata Itakuwa Nini? …………………………95

Faharisi ya Maandiko ……………………………………………96

4

JAMBO LA UTANGULIZI LA MTOA JIBU

MNAJUA?

Ndugu wapenzi katika Laodekia, je! mnajua unabii hakika hutangaza wazi kwamba watu wa Mungu ndani ya kanisa la Laodekia wako katika hali ya hatari sana na hawajui? Vyema, Ndugu, iwapo mnalitambua au la, ikiwa mnaliamini au la, hivyo ndivyo suala lilivyo hasa. Na iwapo mnatarajia kuingia kwenye uzima wa milele, lazima muliamini, na hivyo bila kukawia. Lolote lingine mnaloweza kuamini au kutokuamini, jambo hili moja lazima muliamini, “kwa maana ni Shahidi wa Kweli anayesema, na ushuhuda Wake lazima uwe sahihi.” — Shuhuda, Gombo la 3, uk. 253. {ABN1: 5.1}

Na kumbukeni kwamba kwa watu wote, Walaodekia hawapaswi kuwa wa mwisho tu bali wasio na mwelekeo wa kukosoa, kwani wao wenyewe, anasema Shahidi wa Kweli, ni “wanyonge, na wenye mashaka, na maskini, na vipofu, na uchi,” bila hata kujishuku hivyo, lakini badala yake kwa furaha wakidhani kwamba wao “ni matajiri, na wamejitajirisha,” na “hawa haja ya kitu.” Ufu. 3:17. Vipi, basi, wanaweza kuwa katika nafasi hakika ya kujua chochote kuwahusu wengine! {ABN1: 5.2}

Tafakari, Ndugu, na mzinduke kwa uhai! Sauti hii, inayoteta nanyi muamke na kuepuka mitego ya Adui haiwezekani

5

kuwa sauti ya Adui! Kumbukeni kwamba Bwana “hutushangaza kwa kuzifunua nguvu Zake kupitia vyombo vya chaguo Lake mwenyewe, ilhali Yeye hupita kwa watu ambao tumewaangalia kama wale ambao nuru inapaswa kupitia ndani yao. Mungu hutaka tuupokee ukweli kwa sifa yake wenyewe, — kwa sababu ni ukweli.” — Shuhuda kwa Wachungaji, uk. 106. {ABN1: 5.3}

“Haijalishi nuru imetumwa kupitia kwa nani, tunapaswa kufungua mioyo yetu kuipokea katika unyenyekevu wa Kristo.… Sote tunapaswa kujua ni lipi linalofundishwa kati yetu; maana iwapo ni ukweli, tunauhitaji.” — Watendakazi wa Injili, uk. 301. {ABN1: 6.1}

“Hatari kubwa kwa watu wetu imekuwa ya kuwategemea wanadamu, na kuufanya mwili kuwa kinga yao. Wale ambao hawajakuwa na mazoea ya kuchunguza Biblia wenyewe, au kuupima ushahidi, wana imani katika viongozi, na hukubali maamuzi wanayofanya; na hivyo wengi watazikataa jumbe halisi ambazo Mungu hutuma kwa watu Wake, iwapo hawa ndugu viongozi hawatazikubali.” — Shuhuda kwa Wachungaji, uk. 106, 107. {ABN1: 6.2}

“Atawatumia watu kwa ajili ya kulifanikisha kusudi Lake ambao baadhi ya ndugu watawakataa kama wasiofaa kushirikishwa katika kazi.” — Mapitio na Kutangaza, Februari 9, 1895. {ABN1: 6.3}

Katika nuru ya maonyo haya, hautachukua wakati kwa uangalifu na kwa maombi

6

kuhakiki iwapo Mungu anaongoza katika kazi hii ya matengenezo? Yeye ameahidi kwa wote watakaofanya hivi, kwamba Yeye hatawaacha gizani bali Atawaongoza katika Kweli yote. Kwa hivyo hautamwamini kwa Neno Lake, na kumjaribu Yeye? {ABN1: 6.4}

Tunawasihi, kwa kuwa tayari “mashirika ya uovu yanaunganisha majeshi yao, na kujizatiti. Yanajiimarisha kwa vita vikuu vya mwisho. Mageuzi makubwa yatafanyika hivi karibuni katika ulimwengu wetu,” unasema Uvuvio, “na harakati za mwisho zitakuwa za kasi mno….Wakati unakuja ambapo katika udanganyifu na ufidhuli wao watu wataifikia hatua ambayo Bwana hataruhusu waipite, na watajifunza kwamba kuna kikomo cha uvumilivu wa Yehova.…Watu ambao hushikilia mamlaka ya serikali hawana uwezo wa kutatua shida ya ufisadi wa maadili, umaskini, ufukara, na uhalifu unaongezeka. Wanajitahidi bure kuweka shughuli za biashara kwa msingi salama zaidi….Hivi karibuni kila kitu kinachoweza kutikiswa kitatikiswa, ili vitu visivyoweza kutikiswa viweze kusalia…. {ABN1: 7.1}

“Haiwezekani kutoa wazo lolote la uzoefu wa watu wa Mungu ambao watakuwa hai duniani wakati utukufu wa mbinguni na marudio ya mateso ya zamani yamechangamana. Watatembea katika nuru inayotoka kwenye kiti cha enzi cha Mungu. Kwa njia ya malaika kutakuwa na

7

mawasiliano ya daima kati ya mbingu na nchi.” — Shuhuda, Gombo la 9, uk. 11, 13, 15, 16. {ABN1: 7.2}

Kwa mtazamo wa uhalisi huu mkuu ambao hata sasa unazuka mbele ya macho yetu, usiendelee, Ndugu Dada, kujificha gizani. Simama nuruni, usije ukajikwaa na kuanguka na usipatikane. Njooni, chukua wakati, na

Hebu Tusemezane. {ABN1: 8.1}

Kanisa la Laodekia, la mwisho kati ya makanisa saba (Ufu. 2, 3), likiwa mfano wa kanisa la Kikristo katika kipindi chake cha mwisho, wakati wetu, ujumbe kwalo ulionakiliwa ndio ujumbe wa mwisho kwa kanisa. Hivyo, kwa udhahiri, iwapo lipo somo lolote la Biblia muhimu kwa kanisa kulichambua, hakika ni ujumbe kwa Walaodekia. {ABN1: 8.2}

Ingawa wameridhika kwa mafanikio yao, Walaodekia ambao huamini na kumtii Mungu kwa Neno Lake hawatamhoji Yeye mintarafu hali yao ila, iwapo wanaiona au la, watakubali kwamba wako kwenye “udanganyifu wa kusikitisha,” “wanyonge, na wenye mashaka, na maskini, na vipofu na uchi.” Baada ya kufanya itikio hili kwa uaminifu, watafuata kwa utiifu ushauri wa Shahidi wa Kweli wanunue kutoka Kwake dawa ya macho ambayo Yeye pekee ndiye anayeweza kusambaza, waipake machoni mwao na waweze kuona. {ABN1: 8.3}

Wale, hata hivyo, ambao huegemea katika ulinzi

8

bandia wa ubinafsi wa kupuuza mambo, hawatamakinika kwa ushauri wenye onyo, na kama tokeo watapoteza kila kitu — watatapikwa nje! Hata sasa ni wachache mno wanahofia kamsa hii ya kitisho! Je! ni idadi ndogo sana inawachochea kujua taabu i wapi na wamesimamaje! Ni idadi ndogo sana, hakika, ambayo hata inawataabisha! Na idadi ndogo ilioje haina mwelekeo wa kuuliza kwa woga kwamba inaweza kukemea mwenendo wao mbaya na kuwanyima anasa za dhambi ambazo wanazipenda sana! Ajabu wachache bado wote pia kwelikweli. {ABN1: 8.4}

Kisha, pia, ikiwa imewekwa ndani yao hofu kuu ya manabii wa uongo, na kutoamshwa ndani yao tarajio lolote la wa ukweli (ingawa hawawezi kuwapo wa uongo pale ambapo hawapo wa ukweli), kwa hivyo wao wanakaribia kutofikiwa. Na nyuma ya mwenendo wao wa kutojali unaonekana ukweli kwamba “machungu ya wajibu na anasa za dhambi ni kamba ambazo Shetani huwafungia wanadamu katika mitego yake” (Shuhuda, Gombo la 5, uk. 53), ilhali nyuma ya hofu iliyoingizwa kwa kina kabisa ya manabii wa uongo, unaonekana uangalifu wa mlinzi wa bandia kuwazuia wasikutane na wajumbe ambao Mungu ametuma kwao. {ABN1: 9.1}

Hangaiko letu ndani, kwa hivyo, ni kwamba iamshwe shauku ndani yako, mpendwa Mlaodekia, kwenda kwa chanzo cha jambo hili, kuufanya hakika wokovu wako. Kwa hivyo hautakuwa mwenye busara na mwangalifu kabisa kukaa chini na mbeba-nuru huyu kwa unyenyekevu,

9

bila upendeleo, na kusoma kwa maombi ambayo lazima yakulipe mara nyingi zaidi ya yale uliyowekeza ndani yake? Kumbuka, ipo sheria ya takatifu inayogeuza kila juhudi ya uaminifu kuwa furaha, uzoefu wa kibinafsi na Mungu, na uzima wa milele. Kwa hivyo hautaanza sasa kujipima mwenyewe, sio tena kwa lile unalofikiri ulivyo au utakavyokuwa bali kwa lile Bwana anasema ulivyo na lazima uwe? Anza uchunguzi wako na yafuatayo

Maswali Saba. {ABN1: 9.2}

1. Laodekia ni nani?

2. Malaika huwakilisha nini?

3. Ni nini maana ya kuwa mnyonge na mwenye mashaka na maskini na kipofu na uchi?

4. Kuwa “vuguvugu” ni nini?

5. Mbona Mungu huhiari moja ama baridi au moto badala ya vuguvugu?

6. Dawa ya macho ni nini?

7. Iwapo Laodekia atashindwa kutubu, aibu yake itafunuliwaje? {ABN1: 10.1}

Ufunuo, sura ya 2 na ya 3, huelezea hali ya kila moja ya makanisa saba la mwisho ambalo ni Laodekia. Makanisa haya, inakubalika kwamba, hulionyesha kanisa la Kikristo katika vipindi saba tofauti; cha saba, Laodekia, kikilionyesha katika kipindi kabla tu ya “mavuno,”

10

cha mwisho ambacho “ngano na magugu” yamechangamana, na kile ambacho litapata utengo wa wabaya kutoka kwa wema (Mat. 13:30, 47-49). {ABN1: 10.2}

Kwa sababu katika kila sehemu yake, kanisa lazima liwe kweli kwa jina lake (pekee likiwa kitambulisho chake), kwa hivyo tutaliangalia swali:

Laodekia ni Nani? {ABN1: 11.1}

Laodekia linaweza kutambuliwa bila kukosea kati ya “mafundisho” mengi ya Ukristo kwa kazi ambayo linafanya — kutangaza hukumu. Kwa kweli, alama hii ya utambulisho imeonyeshwa wazi kwa jina lenyewe Laodekia, mseto wa maneno mawili ya Kiyunani lao na dekei, moja likimaanisha “watu,” pia “hunena,” lile lingine “hukumu,” mawili kwa maana moja watu wanaotangaza hukumu. Kanisa kwa hivyo, ambalo hutangaza, “Mcheni Mungu, na Kumtukuza; kwa maana saa ya hukumu Yake imekuja” (Ufu. 14:7), bila shaka ndilo linaloitwa Laodekia. Na linajulikana vile vile nje ya mizingo ya Waadventista wa Sabato kama ilivyo ndani, kwamba kanisa la Waadventista wa Sabato linajitahidi kuutangaza ujumbe wa hukumu wa Ufunuo 14:7, na kwa hivyo halipingwi katika madai yake kwa jina hilo, Laodekia. {ABN1: 11.2}

Maadamu, kwa hivyo, kanisa la Waadventista wa Sabato ndilo la pekee linalotangaza

11

hukumu, na kwa sababu kila mojawapo wa jumbe hizo saba umeelekezwa kwa malaika wa makanisa husika, ujumbe kwa Laodekia kwa hivyo umeelekezwa

Kwa Malaika wa Waadventista wa Sabato. {ABN1: 11.3}

Kwa mujibu wa Ufunuo 1:20, “vinara vya taa” huwakilisha makanisa, na “nyota” malaika (viongozi) ambao huyasimamia makanisa. Wakiwa ni wahudumu wa yale makanisa, malaika wanaonekana hivyo kuwa ukasisi, ambao jukumu lake ni kuhakikisha taa zimewashwa, zimejazwa mafuta, na zinawaka kwa uangavu, ili kanisa liweze kuangaza nuru kwa wote walio karibu. {ABN1: 12.1}

Kwa hivyo, kama malaika wa Laodekia, yeye ambaye ametumiwa ujumbe wa kukosoa, ni ishara ya ukasisi katika Laodekia, kwa hivyo anapaswa kuwa na wasiwasi zaidi kugundua shida i wapi, kwa maana yeye ni, asema Bwana.

Mnyonge, mwenye Mashaka, Maskini, Kipofu, na Uchi. {ABN1: 12.2}

Na Ukasisi ulio mnyonge, wenye mashaka, ulio mpofu, na uchi, ni kanisa gani (kinara cha taa) linaweza kudumu likiwaka? Na nuru yake ikiwa imezima au inakaribia kuzimika, litawezaje kuiangazia dunia jinsi Mungu ameliweka lifanye? Kupitia kwa macho ya Shahidi wa Kweli, kwa hivyo,

12

janga la Laodekia linaonekana wazi kabisa — “wahubiri wanaolala wanahubiri kwa watu wanaolala” (Shuhuda, Gombo la 2, uk. 337) ilhali ulimwengu wenye giza la dhambi unaendelea kutumbukia kuzimu katika giza lake! O, ni hali mbaya ya kusikitisha ilioje! Na bado inapuuzwa kabisa! {ABN1: 12.3}

Wote ukasisi na walei wakiwa katika hali inayosikitisha ya giza, itaonekana wazi kwamba ingawa kanisa la Laodekia ni la mwisho kwa mpangilio wa makanisa hayo saba, Mungu hawezi kupitia kwalo kuiangaza dunia na kuwaandaa watu Wake kwa ajili ya Ufalme likiwa gizani na likiwa halijajiandaa lenyewe. Kwa hivyo uhitaji wa mpangilio mpya, ukasisi mpya, jinsi ilivyotabiriwa katika Shuhuda, Gombo la 5, uk. 80, na katika Zefania 3:11, 12. {ABN1: 13.1}

Kisha itakuwa kwamba “wale tu, ambao wameyahimili na kuyashinda majaribu kupitia kwa nguvu zake Mwenye Uwezo wataruhusiwa kutenda sehemu kuutangaza [Ujumbe wa Malaika Watatu] utakapokuwa umeumuka kuingia katika Kilio Kikuu.” Mapitio na Kutangaza, Novemba 19, 1908. {ABN1: 13.2}

Katika nuru ya kweli hizi, ujumbe wa kinabii kwa malaika wa Laodekia lazima uletwe na kutangazwa na mtu mwingine isiyekuwa malaika mwenyewe. Lakini hili, kwa kweli, ni jambo ambalo hata ukasisi au walei hawatarajii au kutamani litukie. Kwa ajili ya waaminifu, hata hivyo, linafanyika. {ABN1: 13.3}

13

Hivyo kwa sababu Neno la Mungu husema kwamba ukasisi wa kanisa la Laodekia ni wa unyonge, wenye mashaka, maskini, kipofu, na uchi, na ya kwamba wao wala walei hawajui ukweli huu, unatoa usisitizo mzito kwa taarifa hizi: “wahubiri wanaolala wanahubiri kwa watu wanaolala!” (Shuhuda, Gombo la 2. uk. 337); “ujumbe wa Shahidi wa Kweli huwapata watu wa Mungu katika udanganyifu wa kusikitisha, hata sasa bado ni waaminifu katika udanganyifu huo.” — Shuhuda, Gombo la 3, uk. 253. {ABN1: 14.1}

Ingawa wako katika mashaka haya ya kutisha, ambayo yanapaswa kuwafanya watetemeke na kuogopa, na kutoa chochote ili watoke ndani yake, bado wanaendelea

Kuwa Wavuguvugu — Si Moto wala Baridi. {ABN1: 14.2}

Mtu anapojikuta katika hali ya hewa ambayo si baridi wala moto, bali vuguvugu, hali joto ambayo hutamaniwa na kutafutwa na wote, hapo hujinyoosha kama fukara ambaye amekuwa mwana-mfalme! Ndivyo ilivyo na Walaodekia, jinsi wanavyowakilishwa katika unabii, ingawa utajiri wao wanaoudhania si kitu ila mtego wa kifo! {ABN1: 14.3}

Kumwokoa mtu kutoka kwa udanganyifu wa kutisha kama huo ni kazi ambayo inahitaji hekima kubwa sio tu kwa sababu mwathiriwa kwa upofu amezoeshwa kwa hali ya hatari aliyomo, ilhali waokozi wake wanajaribu kumwokoa asiangamie, lakini pia kwa sababu huwaangalia kama maadui zake, manabii wa uongo, badala ya kama marafiki zake na wakombozi, wajumbe kutoka kwa Mungu! {ABN1: 14.4}

Mtoa Jibu Kitabu Namba1 14

Kutoka kwa safu ya maisha, ujumbe wa kuokoa ambao wao humwelezea, yeye huuchukia. Na kwa sababu hiyo kwa mwenendo wake dhidi yao, hupiga kelele: “Ondokeni, ondokeni, mimi ni tajiri na nimejitajirisha: sina haja ya kitu; nina ukweli wote. “Najua nini ni ukweli. Nimeridhika kwa nafasi yangu. Nimeweka vigingi vyangu, na sitasogezwa mbali na msimamo wangu, liwalo liwe, sitausikiliza ujumbe wa mjumbe huyu; kwa maana najua kwamba hauwezi kuwa ukweli.” — Shuhuda kwa Kazi za Shule ya Sabato, uk. 65; Mashauri kwa Kazi za Shule ya Sabato, uk. 28. {ABN1: 15.1}

Kwa kupinga kwamba wao si wanyonge (wasio na furaha), sio wenye mashaka (hawataabiki), si masikini (wasiohitaji ukweli), si vipofu (hawamo gizani au wasiokuwa na elimu), sio uchi (wasiokuwa na haki ya Kristo). Walaodekia wanampinga Shahidi wa Kweli, wanakataa ushauri Wake, na kuipuuza tiba Yake —

Dawa ya Macho. {ABN1: 15.2}

Kwa kuwa ni “dawa ya macho” pekee itakayowaponya maradhi yao ya kufisha ya Ulaodekia, kwa hivyo iwapo watashindwa kujipatia tiba hiyo (kwa kuutafuta ukweli kama hazina iliyofichika) na kujipaka (kutubu), watatapikwa nje. O, Ndugu, Dada, hautaitisha “dawa ya macho”? au utaendelea katika unyonge wako, mashaka, umaskini, upofu, na uchi, na hivyo kumlazimisha Yeye akutapike nje na

15

Kuifunua Aibu Yako? {ABN1: 15.3}

Ili aibu yenu, Ndugu, isifunuliwe kwa wote, kwa muda mrefu Mungu amejizuia kuufunulia ulimwengu dhambi ambazo mmezikuza na kuzificha. Sio milele, hata hivyo, Yeye atavumilia. Kwa hivyo kwa ajili ya nafsi zenu, msiendelee kubishana kwamba mnayo Kweli yote; koma kuongezea dhambi juu ya dhambi; tubuni, na mumrudie Yeye; Yeye atawapokea kwa furaha na kuwafanyia karamu alivyofanya yule baba katika mfano wa kumkaribisha nyumbani manawe mpotevu na kumfanyia karamu. {ABN1: 16.1}

Usiwe kama Myahudi. Bali fungua moyo wako; tupa nje kiburi chake, kuchukia kwake bila sababu, na majivuno ya ubinafsi wake; usiruhusu haya yakunyime maisha ya milele wakati wa mwisho kama huu. Iwapo utayarudia makosa ya Wayahudi, aibu yako na hasara yako itakuwa kubwa zaidi kuliko yao jinsi ilivyo nuru yako na fursa zako na upendeleo. Naam, zaidi ya kulinganishwa! Kwa hivyo usishindwe, tunakusihi, kumaliza ugonjwa wako wa muda mrefu na umaskini wa Ulaodekia, na usiendelee kudhani u

Tajiri, na Umejitajirisha. {ABN1: 16.2}

Kamwe hata usitangaaze kwamba unayo majengo yote, taasisi zote, fedha zote, watendakazi wote, waongofu wote ambao unahitaji! Majivuno yako ni kutokuwa na hitaji la ukweli zaidi! Mwenendo huu, kwa hivyo, Bwana asema, ndio njia

Mtoa Jibu Kitabu Namba1 16

ambayo unasema, “Mimi ni tajiri nimejitajirisha, na sina haja ya kitu.” Ndicho chanzo cha shida yako, na jambo ambalo Yeye hutarajia ukiri na kutubu. {ABN1: 16.3}

Dai la malaika (la ukasisi) la kimakosa la kuwa tajiri na kujitajirisha na kutohitaji kitu, halimfanyi kuwa muongo, lakini badala yake humuonyesha kuwa mwathirika wa ujinga na udanganyifu. Lakini fikra zake kwamba anao na anajua Ukweli wote, huifanya hali yake kuwa hatari zaidi kuliko ile ya muongo, kwa maana muongo hujua kwamba anadanganya. O, amka, Ndugu, Dada, amka! amka! {ABN1: 17.1}

Tenda Kama Alivyofanya Nathanieli.

Njoo uone! {ABN1: 17.2}

Kuona nini? Walaodekia, matajiri na waliojitajirisha, na hawahitaji kitu, na kisingizio kwamba hitaji la kutunza vitu vya kawaida vya maisha (Luka 14:15-19) huwakataza wao kuupokea mwaliko? {ABN1: 17.3}

Hakika la! {ABN1: 17.4}

Watazame walaodekia kutoka kwenye njia kuu na vichochoro — “maskini, na vilema, na vipofu, na viwete” (Luka 14:21), kwa furaha wanajipatia dawa! {ABN1: 17.5}

Lakini ole, sio wote wanaokuja, hukaa, kwa maana “Kila mtu alisikiapo neno la ufalme asielewe nalo, huja

17

yule mwovu, akalinyakua lililopandwa moyoni mwake. Huyo ndiye aliyepandwa karibu na njia.” Usiwe kama yeye, bali fanya juhudi inayohitajika kuujua Ukweli. Na wengine, “ikitukia dhiki au udhia kwa ajili ya lile neno,” mara huchukizwa. Hawa ndio wale “waliopandwa penye miamba.” Wala usiwe kama wao; kita mizizi katika Kweli. “Naye aliyepandwa penye udongo mzuri, huyo ndiye alisikiaye lile neno, na kuelewa nalo; yeye ndiye azaaye matunda, huyu mia, na huyu sitini, na huyu thelathini.” Mat. 13:19-23. {ABN1: 17.6}

Ingawa “mbaya” pamoja na “mzuri” bado wanakuja (kwa maana bado tuko katika kipindi ambacho ngano na magugu, samaki wazuri na wabaya huchangamana), hauhitaji kuwa magugu au “samaki wabaya.” Kuwa ngano, tenda kama “wazuri”: weka kando mawazo yako na njia zako, kisha mwamini Bwana, kwa maana husema: “…Mawazo Yangu si mawazo yenu, wala njia zenu si njia Zangu…Kama vile mbingu zilivyo juu sana kuliko nchi, kadhalika njia Zangu zi juu sana kuliko njia zenu, na mawazo Yangu kuliko mawazo yenu.” Isa. 55:8, 9. {ABN1: 18.1}

Na mwishowe, usiwe kama Mfarisayo anayeweza kuona kibanzi ndani ya jicho la ndugu yake, lakini asiweze kuiona boriti katika jicho lake mwenyewe (Mat. 7:3). Kwa maana baada ya yote “Wewe u nani?” anauliza Bwana. Je! Wewe mwenyewe sio Mlaodekia? Iweje “kumhukumu” wewe “mtumishi wa

18

mwingine? Kwa bwana wake mwenyewe yeye husimama au huanguka. Naam, atasimamishwa, kwa kuwa Bwana aweza kumsimamisha. “ Rum.14:4. {ABN1: 18.2}

Kamwe usimhangaikie yule mwenzio, Ndugu; hauna wakati wa kutosha wa kujitazama. Na isitoshe, usiupime Ukweli kwa fimbo ya mwanadamu, bali kwa Fimbo ya Mungu: “Isikieni hiyo Fimbo, na [Yeye] aliyeiteua” (Mika 6:9), anahimiza Bwana. {ABN1: 19.1}

Je! Hautatii ushauri Wake? Ikiwa utafanya hivyo, bila kukawia zaidi, tuma jina na anwani yako kwa ajili ya vitabu vya Ukweli wa Sasa — karamu ambayo, ingawa ni ya thamani ya kila kitu, haitakugharimu chochote. Na licha ya kuwa tiba pekee ya Ulaodekia wako, itakufurahisha na kuiridhisha nafsi yako yenye njaa na kitu chenye utajiri hakika na kisicho cha kawaida! {ABN1: 19.2}

Basi sisi sote kwa pamoja “tutakuwa na macho ya kiroho kuzitambua nyua za ndani za hekalu la mbinguni. Tutapata mada za wimbo na shukrani za kwaya ya mbinguni inayokizunguka kiti cha enzi. Wakati Zayuni itakapoamka na kuangaza, nuru yake itakuwa ikipenyeza zaidi na nyimbo za thamani za sifa na shukrani zitasikika kwenye mikutano ya watakatifu …. Tunapojipaka dawa ya macho ya dhahabu, tutauona utukufu mbele. Imani itapita katika kivuli kizito cha Shetani, na tutamwona Wakili wetu akitoa uvumba wa sifa Zake mwenyewe kwa niaba yetu.

19

Tutakapoliona hili jinsi lilivyo, jinsi Bwana anavyotamani tulione tutajawa na hisia za ukubwa na utofauti wa upendo wa Mungu.” — Shuhuda, Gombo la 6, uk. 368. Na kisha hatutaendelea kuhoji:

Ushauri wa Nani Unapaswa Kufuatwa? {ABN1: 19.3}

Sasa tunataka ujue kwamba tunathamini sana wasiwasi wako kwa ajili ya ustawi wetu wa kiroho, kama unavyoonyeshwa katika ukosoaji wako mwingi, na tunakuhakikishia kwamba tunatambua kuwa, iwapo tuna makosa, ushauri wako hakika ni wa thamani kwetu kama, iwapo tuko sawa, ulivyo ushauri wetu kwako. Kwa hivyo tuna imani kwamba utakubaliana nasi ili lazima tulitatue swali,

Nani Ni Nani? {ABN1: 20.1}

Kuanza uchunguzi wetu, ni muhimu katika haki kwa pande zote mbili, kuzingatia maarifa ya uzoefu wa kila mmoja. {ABN1: 20.2}

Kwa mtazamo wa uzoefu wetu mwingi kwa Ujumbe wa Malaika wa Tatu katika sehemu yake ya kwanza, na pia katika nyongeza yake ya sasa (Maandishi ya Awali, uk. 277), jinsi ilivyoletwa katika Fimbo ya Mchungaji, dhidi ya wako katika sehemu ya kwanza tu, tumelazimika kuamini kwamba uwezekano wa kuongozwa vibaya na malaika wa Walaodekia, ni mkubwa kuliko uwezekano wetu kuongozwa vibaya na Fimbo. {ABN1: 20.3}

Ungalikuwa katika nafasi, kama ile tuliyo ndani, kuwa na habari kamili katika jumbe zote,

20

— katika ule wa 1844 na ule wa leo, — basi uwezekano wako kuwa sawa na wetu kuwa wa makosa, dhidi ya uwezekano wako kuwa wa makosa na wetu kuwa sawa, ungesawazishwa sawasawa. Inavyowezekana, hata hivyo, unaufahamu ule wa awali tu, yamkini zaidi kwamba msimamo wetu unabeba asilimia kubwa ya uwezekano wa kuwa sawa kuliko wako. {ABN1: 20.4}

Isitoshe, iwapo Fimbo iko sawa au na mbaya “malaika wa kanisa la Laodekia” jinsi Bwana Mwenyewe ameweka wazi kabisa, yu katika udanganyifu wa kusikitisha, wa kuogofya, na wa kutisha (Shuhuda, Gombo la 3, uk. 253, 254 , 260), na karibu kutapikwa nje. {ABN1: 21.1}

Kwa mtazamo, kwa hivyo, wa jukumu kubwa linalofuata likiwa juu yetu, hatuwezi kutojibidiisha sana kwa ajili yako kuliko wewe ulivyo kwa ajili yetu. Wala huwezi kumudu kutokuwa mzingativu kwa ushauri wetu kwako kuliko tunavyoweza kuwa kwa wako kwetu. {ABN1: 21.2}

Na mwishowe, tukiwa tunaamini kwamba u mwaminifu kama sisi tulivyo, tuna imani kwamba utapima kwa uaminifu na kwa uangalifu kila neno lililo hapa ndani. {ABN1: 21.3}

Kuwa kwetu, kama unavyojua, wafuasi wasioyumba-yumba wa Biblia na uaminifu na maandishi ya Dada White, Waadventista wa Sabato kwelikweli tuna hakika kwamba maandiko yote ya bibilia na ya Dada White huiunga mkono Fimbo asilimia mia moja. Yote matatu, kwa hivyo,

21

tunaona yakiwa katika upatano kamili na Fimbo ikipeana “nguvu na msukumo” kwa ujumbe jinsi ulivvyotolewa tangu 1844. (Tazama Maandishi ya Awali, uk. 277.) {ABN1: 21.4}

Kwa mtazamo wa kudumisha usadikisho huu thabiti, unaweza kuelewa kwa urahisi kwamba kukataa kwako Fimbo kwa misingi kwamba haipatani na maandishi ya Dada White, sio kwetu uhalisi unavyoonekana kwako. {ABN1: 22.1}

Kisha, pia, tukiwa na kila sababu ya kuamini kwamba akili zetu ni timamu kikamilifu, sisi kwa hivyo tunayo kila sababu ya kuamini kwamba tunaweza kama wengine kwa werevu kusoma Biblia na maandishi ya Dada White. Kwa hivyo hebu sisi, kama Wakristo ambao wanataka sana kujua ukweli, kwa pamoja tuanze

Kuchunguza Yote Miwili Msimamo Wenu Na Wetu. {ABN1: 22.2}

Kwanza, si sahihi kwamba kitabu cha mwongozo cha Mkristo ni Biblia? Iwapo jibu lako kwa swali hili la msingi ni ndiyo, basi linatulazimisha kusoma maandishi ya Dada White katika nuru ya Biblia, sio Biblia katika nuru ya maandishi yake. Hili kwa kweli, yeye mwenyewe husema waziwazi:

“Wale tu ambao wamekuwa wanafunzi wa bidii wa Maandiko, na walioupokea upendo wa kweli, watakingwa kutoka kwa upotovu wenye nguvu ambao

22

utauteka nyara ulimwengu. Kwa ushuhuda wa Biblia hawa watamgundua mdanganyifu katika maficho yake. . . Je! watu wa Mungu sasa wamekita mizizi imara kwa neno Lake ya kwamba hawatajisalimisha kwa ushahidi wa hisia zao? Je! wao, katika mgogoro huo, watashikamana na Biblia, na Biblia tu?” Pambano Kuu, uk. 625. {ABN1: 22.3}

Kwa hivyo, ni wazi, kazi yake haipaswi kuzuiliwa kamwe kufasiriwa kwa njia kama hiyo ya kukinzana na Biblia lakini siku zote kuieleza waziwazi. Ikiwa unafuata bila kukengeuka kanuni hii kamili ya kufasiri, kamwe huwezi kuwa na uwezekano wa taabu yoyote na Fimbo au na ujumbe wowote ambao Bwana ataweza kutuma. {ABN1: 23.1}

Fasiri zenu za maandishi mengi ya Dada White, zinazojulikana sana, yamkini, zile zinazohusu Ufalme, kwa sababu huonekana kupingana na unabii wa Biblia, husababisha yule anayepokea maandishi yake kutilia shaka Biblia, na yule anayeshikilia Biblia kuwekwa dhidi ya maandishi yake, na hivyo kuleta mzozo na mafarakano kati ya ndugu. Fasiri kama hizo, zinazoegemea upande mmoja na zinazofanya mgawanyiko, kwa hivyo si za haki kwa Biblia na maandishi ya Dada White tu lakini pia kwenu wenyewe, na kisha kwa kazi ya Ukweli. {ABN1: 23.2}

Kwa hivyo, tunaamini, mtaona kwamba wakati mnajitahidi kimakusudi kuthibitisha Fimbo ni mbaya, kwa uhalisi bila kuja mnajitahidi kumthibitisha Dada White

23

kutopatana na Biblia — kazi ambayo ni ya kutawanya kutoka kwa Kristo badala ya kukusanya Kwake. {ABN1: 23.3}

Kwa sababu yote miwili msimamo wenu na wetu wa mafundisho lazima iwe katika mapatano kamili na Biblia, kwa hivyo tunawauliza mpatanishe msimamo wenu kwa Ufalme na Danieli 2:44; Yeremia 51:20; Hosea 3:4, 5; Isaya 2:1-4; Mika 4:1-6; Isaya 11:12-16; Yeremia 30:18, 21; 31:2-13; 32:37; Ezekieli 37:15-28. {ABN1: 24.1}

Tunaushikilia kuwa ni ukweli rahisi, unaojidhihirisha wenyewe kwamba kwa sababu jiwe (Dan. 2:34) ni nembo ya Ufalme, na ya kwamba wakati Linavipiga vidole vya ile sanamu, lazima Lisimamishwe kabla Livipige, jinsi Danieli alivyosema: “Katika siku za wafalme hawa [wafalme wa vidole: wafalme wa leo] Mungu wa mbinguni atausimamisha ufalme.” “Katika siku za wafalme hawa,” haziwezi kumaanisha baada ya siku zao. Na kama laula Ufalme usisimamishwe (uletwe kuwapo), Haliwezi kuyapiga mataifa. {ABN1: 24.2}

Ikiwa, zaidi ya hayo, Yuda na Israeli (falme zote mbili) hazikukusanywa pamoja katika ufalme mmoja, jinsi unabii unavyosema watakuwa (Ezek. 37:15-28), basi wanawezaje kuwa “shoka la vita” (Yer. 51:20)? Na unabii huo unawezaje kutimizwa? {ABN1: 24.3}

Vilevile ni wazi kwamba “siku nyingi” (Hos. 3:4, 5) ni miaka mingi tangu wakati Ufalme uliporomoka hadi Utakaposimamishwa tena mwishowe. Kwa hivyo neno “kurejea” haliwezi kumaanisha

24

chochote isipokuwa kwamba wale waliotawanywa “siku nyingi” ni lazima warudi katika nchi waliyochukuliwa mateka. {ABN1: 24,4}

Huu, zaidi, ni msimamo pekee, wenye upatano na mafundisho yote muhimu ya Biblia, ambayo hutoa uhakikisho wa kutimizwa unabii wa Isaya 2 na ule wa Mika 4. {ABN1: 25.1}

Tena: kutoka Isaya 11 tunaona kwamba Bwana “atapeleka mkono Wake tena mara ya pili ili kuwakomboa masalia ya watu Wake” (Isa. 11:11), na ya kwamba wakati Yeye atafanya hivyo, Atawaandalia njia kuu “kama vile ilivyokuwa kwa Israeli katika siku ile waliyotoka katika nchi ya Misri.” Isa. 11:16. {ABN1: 25.2}

Na Yeremia hushuhudia kwamba Bwana “atarudisha tena hema za Yakobo zilizohamishwa, na kuyahurumia makao yake; nao mji utajengwa juu ya magofu yake wenyewe …. na mkuu wao atatoka kati yao wenyewe naye mwenye kuwatawala atakuwa mtu wa jamaa yao.” Yer. 30:18, 21. {ABN1: 25.3}

Kwa Ezekieli, isitoshe, “Bwana MUNGU asema hivi; Tazama, Nitawatwaa wana wa Israeli kutoka kati ya mataifa walikokwenda, Nami nitawakusanya pande zote, na kuwaleta katika nchi yao wenyewe.” Ezek. 37:21. {ABN1: 25.4}

Bibilia ni aidha sahihi au yenye makosa. Iwapo unaamini kwamba ni sahihi, Iweke moyoni mwako, na uchukue msimamo Kwayo, angalau kwa vifungu kama hivi wazi vilivyonukuliwa hapa ndani — maandiko ambayo hayahitaji ufasiri. {ABN1: 25.5}

25

Na hakika ni kwamba Mungu hatakubali udhuru wa yeyote kujaribu kuzipiga chenga, ziko wazi kabisa na halisi. Wala hakuna mtu atakayefanikiwa kuziepuka hukumu za Mungu kwa kujaribu kwa mkono mmoja kuhepa kupitia anachofikiria kuwa mianya katika Fimbo, na kwa kujaribu kwa mkono mwingine kuweka katika maandishi ya Dada White, vizuizi vya kujificha nyuma yake. {ABN1: 26.1}

Majaribio ya ubatili kama hayo leo yatawaacha wahalifu kutokubalika zaidi (kwa kweli, sembuse) kuliko juhudi za ubatili za Wayahudi zilivyowaacha jana katika jaribio lao la kugundua mianya katika kazi ya Kristo kwa kutumia maandishi ya Musa. {ABN1: 26.2}

Ikiwa kisingizio cha mtu kiweze kuwa kwamba mafundisho ya Fimbo hayapatikani katika maandishi ya Dada White, hataondolewa lawama kwa kuikataa sauti yake kwa misingi hiyo kuliko Wayahudi kwa kupiga vita na kukataa Maandiko ya Agano Jipya kwa misingi kwamba hayapatikani katika maandishi ya manabii. {ABN1: 26.3}

Iwapo wewe ni mwamini wa dhati na mwaminifu katika Biblia na Roho ya Unabii, utatii ushauri huu: “… iwapo ujumbe unakuja ambao huelewi, vumilia machungu uweze kusikia sababu ambazo mjumbe anaweza kutoa.” — Shuhuda kwa Kazi za Shule ya Sabato, uk. 65, Mashauri kwa Kazi za Shule ya Sabato, uk. 29. {ABN1: 26.4}

26

Uadilifu wako katika kukataa ujumbe wa kutia muhuri kwa msingi kwamba unahitilafiana na maandishi ya Dada White, utapimwa kwa jibu lako kwake akikuhimiza uhojiane na mjumbe badala ya kuhojiana na maadui zake. {ABN1: 27.1}

Lile kwa baadhi yenu linaweza kuonekana kuwa linaweka fundisho hili au lile la Fimbo kupingana na maandishi ya Dada White, halionekani kuwa ukweli kama lilivyo kwa namna zote huweka taarifa ya Bwana katika Mathayo 10:23 kinyume kabisa na ahadi Zake. “Hamtamaliza,” maandiko yasema, “miji ya Israeli, hata ajapo Mwana wa Adamu.” Lakini mitume hawakwenda kuhubiri injili sio kwa miji ya Israeli tu bali pia kwa “kila kiumbe kilicho chini ya mbingu” (Kol. 1:23), na bado Mwana wa Adamu “hajaja,” ingawa miaka 1900 imepita tangu wakati huo. Lazima Kristo alikuwa amenena ukweli, lakini haueleweki, kama vile mambo mengi yanayohusiana na Ukweli wa Sasa hayaeleweki, na kwa hivyo katika hali nyingi yanapotoshwa. {ABN1: 27.2}

Wakati Musa aliandika sehemu ya kwanza ya Biblia hakupewa upendeleo wa kuandika Ukweli wote ambao Mungu alikusudia kuufunua kwa watu Wake. Baadaye katika kipindi cha Agano la Kale alikuja Isaya, Yeremia, Ezekieli, n.k. Kisha katika kipindi cha Agano Jipya akaja Yohana Mbatizaji, Kristo, mitume, wana-matengenezo, Miller, na Dada

27

White, kila mmoja kwa zamu yake wakafundisha ukweli ambao, hata hivyo, haungeweza kuthibitishwa na maandishi ya Musa. Hii ndiyo sheria ya Mungu ya kuukunjua ukweli. Na kwa hasara ya mtu mwenyewe atakataa kukiri kwamba inafanya kazi hivyo leo kama zamani, hata ingawa ujumbe leo umetolewa wote kutoka kwa waandishi waliovuviwa kabla yake. {ABN1: 27.3}

Ingawa yapo mengi zaidi ya kusemwa juu ya mambo haya, inatosha mistari hii kwa sasa, kwa maana isipokuwa kwa ajili ya maisha yako uyajibu, mengi yatakuwa tu ya kukuchosha na kuupoteza wakati kwa upande wetu. {ABN1: 28.1}

Sala yetu ya moyo mnyoofu na tumaini la dhati, kwa hivyo, ni kwamba, wakati wa thamani, usioweza kukombolewa uliowekwa katika juhudi hii ya nia njema na kuzijali sana nafsi zenu, itakuwa njia ya kuwaleta ninyi mfurahi katika tumaini tukufu ambalo Fimbo huweka mbele yenu. Mioyo yenu iweze kuitikia “sauti ya Bwana,” ambayo bado “inaulilia mji, … isikieni hiyo Fimbo, na Yeye Aliyeiteua.” {ABN1: 28.2}

Iwapo mmeamua sasa kulitii agizo hili, na lile lililo katika Shuhuda kwa Kazi za Shule ya Sabato, uk. 65, kustahimili machungu kusikia sababu ambayo mjumbe anaweza kutoa, na kuuliza maswali kwa ujumbe huo, ikiwa ni kuhusiana na Biblia au maandishi ya Dada White, mnahakikishiwa kwamba tutawakaribisha tusikie kutoka kwenu, na kwa furaha tutafanya kadiri ya uaminifu wetu kutatua lolote linalohusika. {ABN1: 28.3}

28

MASWALI NA MAJIBU

SHIDA YA LAODEKIA NI NINI?

Swali Namba 1:

Ni nini shida ya Laodekia na dawa ni nini?

Jibu:

Kuelezea hali yake kwa lugha ya leo, Uvuvio unatangaza: {ABN1: 29.1}

“Ujumbe kwa kanisa la Laodekia ni wa kushtua na kuleta mashtaka, na unawahusu watu wa Mungu kwa wakati huu …. {ABN1: 29.2}

“Watu wa Mungu wamewakilishwa katika ujumbe kwa Walaodekia kama walio katika nafasi ya usalama wa kimwili. Wako shwari, wanajiamini kuwa katika hali ya upeo wa mafanikio ya Kiroho…. {ABN1: 29.3}

“Ni udanganyifu mkubwa jinsi gani ulioje unaoweza kuja kwa akili za wanadamu kuliko kujiamini kwamba wao wako sawa, ilhali wote wamekosa! Ujumbe wa Shahidi wa Kweli huwapata watu wa Mungu katika udanganyifu wa kusikitisha, hata sasa bado ni waaminifu katika udanganyifu huo. Hawajui ya kwamba hali yao ni mbaya machoni pa Mungu. Ilhali wale wanaohutubiwa wanajidanganya kwamba wako katika hali ya juu kiroho, ujumbe wa Shahidi wa Kweli huvunja usalama wao kwa mashtaka ya kushtua na ya kushangaza kuhusu

29

hali yao halisi ya upofu wa kiroho, umaskini, na unyonge. Ushuhuda, unaokata hivyo na mkali, hauwezi kuwa kosa, kwa sababu ni Shahidi wa Kweli anayenena, na ushuhuda Wake lazima uwe sahihi.” — Shuhuda, Gombo la 3, uk. 252, 253. {ABN1: 29.4}

“Naliuliza maana ya upepeto nilioona, na nalionyeshwa kwamba utasababishwa na ushuhuda usiopinda unaoletwa mbele na ushauri wa Shahidi wa Kweli kwa Walaodekia. Huu utakuwa na matokeo yake juu ya moyo wa anayeupokea, na utamwongoza, kuinua kiwango na kutoa ukweli halisi. Wengine hawataustahimili ushuhuda huu wa moja kwa moja. Watainuka kuupinga, na hili ndilo litakalosababisha upepeto miongoni mwa watu wa Mungu.” {ABN1: 30.1}

“Naliona kwamba ushuhuda mzito wa Shahidi Mwaminifu haujapokelewa hata nusu. Ushuhuda wa kicho ambao juu yake hatima ya kanisa inaning’inia umeheshimiwa kimzaha, ikiwa si kupuuzwa kabisa. Ushuhuda huu sharti ufanye toba ya ndani; wote wanaoupokea kweli kweli watautii, na kutakaswa.” — Maandishi ya Awali, uk. 270. {ABN1: 30.2}

“… mwenendo wetu wa kurudi nyuma umeendelea kututenga na Mungu. Kiburi, tamaa, na kuipenda dunia vimeiishi ndani ya moyo bila hofu ya kupigwa marufuku au kuhukumiwa. Dhambi za kuudhi na za kiburi zimekaa kati yetu. Hata hivyo maoni ya jumla ni kwamba kanisa linanawiri, na ya kwamba amani na ustawi wa kiroho upo katika mipaka yake yote.” {ABN1: 30.3}

30

“Kanisa limekengeuka na kuacha kumfuata Kristo Kiongozi wake, na badala yake linarudi pole pole kuelekea Misri. Lakini wachache wametiwa hofu au kushangaa kwa upungufu wao wa nguvu za kiroho. Shaka na hata kutoziamini Shuhuda za Roho wa Mungu, kunatia chachu makanisa yetu kila mahali. Shetani anatazamia iwe hivyo. Wachungaji wanaohubiri ubinafsi badala ya Kristo wanatazamia iwe hivyo. Shuhuda hazisomwi na haziwekwi maanani. Mungu amenena kwenu. Nuru imekuwa ikiangaza kutoka kwa neno Lake na katika Shuhuda, na zote mbili zimedunishwa na kupuuzwa. Matokeo ni dhahiri kwa ukosefu wa usafi na moyo wa ibada na imani thabiti miongoni mwetu.” — Shuhuda, Gombo la 5, uk. 217. {ABN1: 31.1}

Kwamba Laodekia ni jina la ki-mfano kwa dhehebu la Waadventista wa Sabato, kila Mwadventista wa Sabato anajua, lakini hata sasa hakuna mtu anayejali kufanya chochote kulihusu! Badala yake, wote wameridhika kwamba wanayo kweli yote ya kuwapeleka ndani! {ABN1: 31.2}

Ili kuongeza muda wa hali yao ya uvuguvugu kwa muda usiojulikana, nguvu ya Shetani imefunika kikamilifu kifuniko cha chupa ya joto kilichoundwa kwa utando usiyoruhusu kweli ipenye wa kuchukia bila sababu, kujiamini nafsi, na hofu kwamba mtu fulani anajaribu sana kuwadanganya kwa neno au kwa kitabu. Hivyo wengi wetu, kama Waadventista wa Sabato, hatujadili au kusoma kweli za Biblia ambazo haziungwi mkono na mtu yeyote ambaye hajaidhinishwa na malaika wa Laodekia — makasisi wa baraza. Kwa sababu hiyo, watu kama hao hawawezi

31

kufikiwa na ujumbe kutoka mbinguni leo kwa urahisi kuliko Wayahudi katika siku yao. Walakini, Yeye Ajuaye yote aliamuru: {ABN1: 31.3}

“Na kwa malaika wa kanisa lililoko Laodekia andika; Haya ndiyo anenayo Yeye aliye Amina, Shahidi aliye mwaminifu na wa kweli, Mwanzo wa kuumba kwa Mungu. Nayajua matendo yako, ya kuwa hu baridi wala hu moto; ingekuwa heri kama ungekuwa baridi au moto. Basi, kwa sababu una uvuguvugu, wala hu baridi wala moto, Nitakutapika utoke katika kinywa Changu. Kwa kuwa wasema, Mimi ni tajiri, nimejitajirisha, wala sina haja ya kitu; nawe hujui ya kuwa wewe u mnyonge, na mwenye mashaka, na maskini, na kipofu, na uchi. Nakupa shauri, ununue Kwangu dhahabu iliyosafishwa kwa moto, upate kuwa tajiri, na mavazi meupe upate kuvaa, aibu ya uchi wako isionekane, na dawa ya macho ya kujipaka macho yako, upate kuona.” Ufu. 3:14-18. {ABN1: 32.1}

Kwa hivyo katika Ufunuo 2:5 wakati Bwana anakikaripia kundi moja la viongozi, akiwaonya kwamba wasipotubu na kufanya matendo yao ya kwanza Yeye atawajilia upesi na kukiondoa kinara cha taa katika usimamizi wao, Yeye aifanya hatima hiyo iwe kwa masharti ya itikio lao wenyewe kwa kemeo Lake la ukali. {ABN1: 32.2}

Lakini baadaye, kwa uongozi wa Laodekia (malaika), Yeye hufanya amri kali

32

zaidi, bila masharti, waziwazi, yenye makali na taarifa ya mwisho, kwamba Yeye atawatapika nje hivyo kuileta serikali ya kanisa la Laodekia kwa kikomo cha ghafla na chenye msiba. Kwa wakati huu haswa, basi, kanisa litapitia usafishwaji kamili wa nyumba, mageuzi ya utawala na mpangilio, hata kama zamani za kale Ufalme “uliraruliwa kutoka” kwa Sauli na akapewa Daudi (1 Sam. 15:28). {ABN1: 32.3}

Na kama vile Daudi, mwana wa nane wa Yesse, hakuchaguliwa hadi baada ya ndugu zake saba katika mapitio mtawalia mmoja baada ya mwingine, kwa hivyo “nyumba ya Daudi” (Zek. 12:8; Shuhuda, Gombo la 5, uk. 81), kanisa lililowekwa huru kutoka kwa “magugu,” kanisa la nane kwa urithi katika Agano Jipya, halingeweza kutokea hadi mfululizo wa yale saba yangekuwa yamepita moja moja. (Angalia Trakti Namba 8, Mlima Zayuni Saa Kumi na Moja.) {ABN1: 33.1}

Dhahiri, “malaika” na kanisa linaloambiwa, lazima huwakilisha makundi mawili — ukasisi na walei. Lakini yule anayeambiwa moja kwa moja na kushutumiwa ni malaika, yule anayewasimamia walei. Wa Shahidi wa Kweli “wa kushtua na wa kuleta mashtaka” kwa hivyo, ingawa hauwaepushi walei, ni moja kwa moja na haswa kwa ajili ya ukasisi. Hivyo hasa wao, zaidi ya yote, wachukue tahadhari na kuweka moyoni vyema maadili mema makuu kwamba Bwana Mchungaji hatamwacha kondoo yeyote kutotunzwa kwa uangalifu, aanguke kuzimu, iwapo Yeye anaweza kumsaidia. {ABN1: 33.2}

33

Lakini kwa sababu, kama wachungaji wadogo, kwa muda mrefu na kwa kuhuzunisha wamekuwa wa kutojali hivyo, Bwana miaka kadhaa iliyopita aliahidi kwamba Yeye muda usiokuwa mrefu “atalisimamia kundi Mwenyewe.” — Shuhuda, Gombo la 5, uk. 80. {ABN1: 34.1}

Katika utabiri wa mageuzi haya kamili kutoka kwa ulegevu wa Ulaodekia, Roho wa Kweli kwa uzito anathibitisha: “Mungu atatumia njia na mbinu ambazo zitaonekana kwamba Yeye anachukua mamlaka mikononi Mwake. Watendakazi watashangazwa …” — Shuhuda kwa Wachungaji, uk. 300. {ABN1: 34.2}

Tena, tunasoma kwamba Mungu atawaweka kando wale ambao “wamejitosheleza kwa unafsi, wasiomtegemea Mungu,” na ambao “Yeye hawezi kuwatumia,” na atawafunua waonekane “wale wa thamani waliofichwa sasa ambao hawajamsujudia Baali.” — Shuhuda, Gombo la 5, uk. 80, 81. {ABN1: 34.3}

Hivyo hata kwa usahihi zaidi historia takatifu hujirudia yenyewe kuliko historia najisi. Na maneno ya kutisha yasiyoweza kutanguliwa ya nabii Samweli kwa Sauli, huja yakipiga kengele katika vizazi vingi hadi chini na ukomo maradufu kwa Walaodekia: {ABN1: 34.4}

“Bwana amekurarulia ufalme wa Israeli, naye amempa jirani yako, aliye mwema kuliko wewe. Tena Yeye aliye Nguvu za Israeli hatanena uongo, wala hataona majuto; maana Siye mwanadamu, hata ajute.” 1 Sam. 15:28, 29. {ABN1: 34.5}

Uvuguvugu wa Ulaodekia — dhana ya kuridhika ya kuwa tajiri na kujitajirisha,

34

ya kuwa na ukweli, na hata kuongeza juu yake — si kitu kipungufu kuliko kinaya halisi. Ni kwa sababu hiyo kwamba Walaodekia “ni wanyonge na wenye mashaka, na maskini, na vipofu, na uchi” (Ufu. 3:17), kimakosa wakiamini kwamba wao ni matajiri na wamejitajirisha. Lakini mahututi kama walivyo udanganyifu huu, hauhitaji kuua iwapo tu watajinyenyekeza na “kununua” ile “dawa ya macho” waliyopewa ili waweze kuuona uchi wao, kisha watubu, watafute msamaha, na wastawi katika ukweli. Lakini, ole, uvuguvugu wao (kuridhika), si moto au baridi (kutoridhika), hali ambayo hufanya iwe vigumu kwao kuitambua hali yao kama ilivyokuwa kwa Wayahudi katika wakati wa Kristo. {ABN1: 34.6}

MBONA HITAJI LA UAMSHO NA MATENGENEZO?

Swali Namba 2:

Ikiwa kanisa ni chombo kinachopendwa zaidi na Mungu kwa nchi (Shuhuda kwa Wachungaji, uk. 20) na ikiwa Yeye analiongoza, mbona hitaji la “uamsho na matengenezo”?

Jibu:

Kwa sababu kanisa ni chombo kinachopendwa zaidi na Mungu kwa nchi, Yeye mara kwa mara hulishauri, hulikemea, na kuliadhibu ili kulileta lidumishe kiwango cha juu ambacho Yeye ameliwekea. Na ingawa historia yake ni kumbukumbu moja ndefu, ya kusikitisha rekodi ya kutenda dhambi na kutubu, kutenda dhambi na kutubu, bado Bwana amelivumilia katika uvumilivu wa milele na uvumilivu wa upendo wa Mungu

35

ulioonyeshwa kwa uzuri sana katika mfano wa mwana mpotevu. Na mwishowe katika upendo huu usiyoelezeka, Yeye “alijitoa Mwenyewe” (Gal. 1:4) kwa ajili yake kama mtu wa Mwana Wake wa pekee. Lakini dhabihu hii kuu bila kujali, halijawahi kamwe kuuthamini kabisa upendo Wake usiokuwa na mwisho kwalo. Hata sasa, Mwokozi anatangaza kwa kusikitisha kwamba Yeye analo neno dhidi yake, na hulishauri kwa maneno mazito litubu na kukaa pamoja Naye katika kiti Chake cha enzi (Ufu. 3:14-21), akielezea wazi hatima isiyoweza kuepukika ya wote wanaoshindwa kutii shauri Lake (Ufu. 3:16). Lakini, kwa kusikitisha, halijatii, na kwa hivyo Yeye “analeta dhidi ya wachungaji na watu shtaka zito la unyonge wa kiroho, akisema, “Nayajua matendo yako, ya kuwa hu baridi wala hu moto ingekuwa heri kama ungekuwa baridi au moto.’” — Kristo Haki Yetu, Toleo la 1941, uk. 121. {ABN1: 35.1}

Hivyo Mungu, kwa Upendo Wake usio na mipaka, wenye kutambua yote kwa ajili ya kanisa Lake, anaitisha uamsho wa kiroho na matengenezo ya kiroho. Hili lisipotukia, wale ambao ni wavuguvugu wataendelea kukua wa kumchukiza Bwana zaidi, mpaka atakapokataa kuwatambua kama watoto Wake. {ABN1: 36.1}

“’Uamsho na matengenezo lazima yafanyike chini ya msaada wa Roho Mtakatifu. Uamsho na matengenezo ni mambo mawili tofauti. Uamsho huashiria upya wa maisha ya kiroho, kuzifanya hai nguvu za akili na moyo, ufufuo

36

kutoka katika kifo cha kiroho. Matengenezo huashiria kuwa na mpangilio mpya badiliko katika mawazo na nadharia, tabia na mazoea. Matengenezo hayawezi kuzaa matunda mazuri ya haki isipokuwa yameunganishwa na uamsho wa Roho. Uamsho na matengenezo lazima yafanye kazi yake iliyowekwa rasmi, na katika kufanya kazi hii ni lazima uchangamane.” — Kristo Haki Yetu, uk. 154. {ABN1: 36.2}

Katika taarifa hizi zilizovuviwa, kweli tatu zasimama kwa ujasiri mtulivu: (1) Mungu anatuma mwito huu ulio wazi kwanza kwa wachungaji, na kisha kwa walei; (2) Yeye anatoa tamko halisi kwamba atawatapika kutoka kinywani Mwake wote watakaoshindwa kutii, na kuingia katika “uamsho wa kiroho na matengenezo ya kiroho”; na (3) Yeye anaweka wazi kwamba vuguvugu kama hili humaanisha “mpangilio mpya, badiliko katika mawazo na nadharia, tabia na mazoea.” Ni wazi, basi, kanisa lazima lipate uzoefu wa badiliko mara matatu kabla lionekane zuri “kama mwezi, safi kama jua, na la kutisha kama jeshi na mabango,” likienda “katika ulimwengu wote, likishinda na kushinda.” — Manabii na Wafalme, uk. 725. {ABN1: 37.1}

Mungu atalitawala katika kanisa Lake sasa kama Alivyofanya wakati wa Musa: “Serikali ya Israeli ilikuwa na sifa za jumuiya kamili, ya ajabu pia kwa ukamilifu na urahisi wake. Mpangilio ukionyeshwa kwa ubora katika ukamilifu na upangaji wa kazi zote zilizoumbwa na Mungu zilidhihirika katika uchumi wa Waebrania.

37

Mungu alikuwa kitovu cha mamlaka na serikali, Mfalme wa Israeli. Musa alisimama kama kiongozi wao anayeonekana, ambaye aliteuliwa na Mungu, kutekeleza sheria hizo kwa jina Lake. Kutoka kwa wazee wa makabila baraza la sabini baadaye lilichaguliwa kumsaidia Musa katika maswala ya jumla ya taifa. Kisha wakaja makuhani, waliotafuta ushauri kwa Bwana katika patakatifu. Akida, au wakuu, walitawala juu ya makabila. Chini yao walikuwa viongozi wa maelfu, na viongozi wa mamia, na viongozi wa hamsini, na viongozi wa makumi?’ na, mwisho kabisa maafisa ambao wangeweza kuajiriwa kwa kazi maalum.” — Mababu na Manabii, uk. 374. {ABN1: 38.2}

Iwapo “kanuni zile zile za kicho na haki ambazo zilikuwa zinawaelekeza watawala kati ya watu wa Mungu wakati wa Musa na wa Daudi, zingefuatwa pia na wale waliopewa usimamizi wa kanisa jipya lililopangiliwa la Mungu katika kipindi cha injili” (Matendo ya Mitume, uk. 95), na ikiwa mwanadamu hawezi kuboresha kwa utawala wa serikali ya Mungu, basi mbona tusiufuate mtindo wake? Kwa hivyo hitaji la “uamsho na matengenezo.” {ABN1: 38.1}

Kama warejeshaji wa kila taasisi Takatifu, tunayo furaha kuwatangazia wasomaji wa Ukweli wa Sasa, kwamba mbali na vitabu vya “uamsho,” wanaweza pia kupata kile cha “matengenezo,” chapisho letu la mpangilio, Ulawi wa Wadaudi Waadventista wa Sabato. {ABN1: 38.2}

38

NI NINI ISHARA YA UVUVIO?

Swali Namba 3:

Ni nini ufasiri kama apendavyo mtu fulani tu? Ni kwa namna gani mmoja huvuviwa? Na Uvuvio hufanya kazi kupitia kwa nani? {ABN1: 39.1}

Jibu:

“Kila andiko, lenye pumzi ya Mungu, lafaa kwa mafundisho, na kwa kuwaonya watu makosa yao, na kwa kuwaongoza, na kwa kuwaadibisha katika haki; ili mtu wa Mungu awe kamili, amekamilishwa apate kutenda kila tendo jema.” 2 Tim. 3:16, 17. {ABN1: 39.2}

“Mkijua neno hili kwanza, ya kwamba hakuna unabii katika maandiko upatao kufasiriwa kama apendavyo mtu fulani tu. Maana unabii haukuletwa po pote kwa mapenzi ya mwanadamu; bali wanadamu walinena yaliyotoka kwa Mungu, wakiongozwa na Roho Mtakatifu.” 2 Pet. 1:20, 21. {ABN1: 39.3}

Umethibitishwa usemi, Maandiko yote, (sio tu sehemu Yake), yamevuviwa. Ukielezwa kwa kukana, hakuna sehemu Yake inayoweza kufasiriwa apendavyo mtu, kwa sababu kwamba Hayakuja kutoka kwa wanadamu bali kwa Mungu. Na yanaweza kufasiriwa na wanadamu tu kwa kadiri na wakati Roho wa Mungu anaamuru. Kwa sababu hiyo, kila nukta na neno la Maandiko na ufasiri Wake ni wa Uvuvio, na hivyo kuwa wa faida kabisa kumwongoza mtu wa Mungu kimafundisho, kumkemea na kumrekebisha, na katika haki kumfunza, hadi kwa ukamilifu wa imani na matendo. {ABN1: 39.4}

39

Basi hebu tufanye agano na Bwana kwamba tangu sasa hatutapokea au kuendeleza kama ukweli uliofasiriwa apendavyo mtu fulani tu wa Maandiko. Na kudumisha kwa uelekevu kutoikiuka ahadi hii ya kicho kwa Bwana, lazima kwanza, tuelewe

Ishara ya Uvuvio. {ABN1: 40.1}

Katika maana yake Kimaandiko, Uvuvio hufafanuliwa kama “ushawishi wa Mungu wa moja kwa moja na wa ghafla unaotumika kwa roho au nafsi ya mwanadamu” (Kamusi ya karne Mpya); kwa maneno mengine, Ni kazi maalum ya Roho wa Mungu. Ni, kwa hivyo katika udhihirisho Wake wa njia nyingi, hufanya kazi, sio utendaji kazi wa akili yenyewe, bali kwa uwezo wa Roho. Ili kupata uelewa sahihi wa mchakato huu, hata hivyo, mtu lazima auone katika mtazamo wa kihistoria, ukitenda kazi kati ya wanadamu tangu mwanzo wa uumbaji. {ABN1: 40.2}

Kwa mfano Wake Mungu alimuumba Adamu, na akampa enzi “akatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na wanyama, na nchi yote pia, na kila chenye kutambaa kitambaacho juu ya nchi.” Mwa. 1:26. {ABN1: 40.3}

Kwa hivyo, kwa sababu Yeye alimumba Adamu kuwa mfalme wa milki ya kwanza ya dunia, na viumbe vyote hai raia ndani yake, uwezo asilia wa Adamu kuvitawala, na utiifu wavyo asilia kwake, huonyesha kwamba uumbaji wote,

40

mwanadamu na wanyama, ndege na vitu vitambaavyo, vilishawishiwa au kujaliwa na Mungu — vilivuviwa. Kwa hivyo Adamu alipoukagua uumbaji wote wa wanyama kama ulivyopita mbele yake, hakutumia muda wowote kujifunza maumbile ya hao viumbe ili kuvitambua, ila mara moja alivipatia kila aina jina lake; navyo, kwa zamu, vikamtambua mara moja kama mfalme wao — vikajitiisha kwake. Werevu huu bora (kama walivyojaaliwa katika Mathayo 10:19) huonyesha wazi kwamba uumbaji wote ulishawishiwa na uwezo ulio juu na zaidi ya wake wenyewe. Kwa ufupi, uelewa wa Adamu na wa wanyama ulikuja kwa njia ya Uvuvio. {ABN1: 40.4}

Uvuvio, kwa sababu hiyo, haujazuilia mafunuo Yake, kwa mwanadamu pekee. Na historia takatifu huonyesha kwamba wala haujazuiliwa kwa maono (Dan. 7:2), au ndoto (Mwa. 28:12), au mawasiliano yasiokuwa ya moja kwa moja (Kut. 40:35; 28:30), au mazungumzo ya moja kwa moja ya ana kwa ana (Mwa. 18:2) na viumbe vitakatifu, au kwa mtindo mwingine wowote wa usemi. Badala yake Huja “kwa njia nyingi.” Kwa hivyo, Mungu “kwa sehemu nyingi… alisema zamani na baba zetu.” Ebr. 1:1. {ABN1: 41.1}

Ukweli huu wa msingi ulikuwa, labda, umeonyeshwa vyema katika kazi ya Nuhu, haswa katika upeo wake, wakati werevu maalum ulipeanwa kwa walioteuliwa washirika wa wanyama walioumbwa, ili kutoka karibu na mbali waweze kupata njia yao hadi ndani ya safina na kudumisha amani mmoja na mwingine. (Tazama Mwanzo 7:1-4.) {ABN1: 41.2}

41

Lakini baada ya kunusurika gharika, wazawa wa familia ya Nuhu mara moja walisahau somo hilo la thamani sana. Kwa hivyo ikawa kwamba watu walioishi baada ya gharika walikuwa wameamua kuamini kwamba ingekuwapo gharika ya pili kwa ulimwengu wote jinsi watu walioishi kabla ya gharika hawakuamini ingekuwapo ya kwanza. Kwa hivyo kutoamini katika uvuvio wa Nuhu kulitangazwa baada ya gharika kama ilivyokuwa hapo kabla, na tokeo kwamba katika juhudi za kupata usalama wa maisha, watu walijaribu kujenga mnara wa Babeli, jengo refu la kwanza ulimwenguni na ukumbusho wa mapema kwa upumbavu wa kazi ya mwanadamu ya kustaajabisha kupata wokovu wake bila msaada wa Uvuvio wa Mungu. Mwenendo huu wenye matusi wa wajenzi dhidi ya ahadi ya Bwana kupitia Nuhu, uliamsha kutopendezwa Kwake hivi kwamba Akafuta kutoka kwa kumbukizi zao lugha ambayo alikuwa amewapa kupitia kwa Adamu na, badala yake, akavuvia ndani yao lugha zote tofauti za dunia, pamoja na tokeo lake wajenzi walichanganyikiwa kati yao na hawakuweza kuendelea kujenga (Mwa. 11:7-9). {ABN1: 42.1}

Katika tukio hili la ajabu ambalo lilibadilisha sana mwenendo wa jamii ya wanadamu, tunaona namna nyingine ya Uvuvio ukifunua kwamba wakati mtu mmoja au kikundi cha watu wanaweza kufanya kazi kwa makusudi kuhitilafiana na Mungu, Yeye anaweza kuwapa zawadi Yake, kuvuruga mikakati yao ya uovu (Mwa. 11:1-9) ilhali Akiendeleza

42

kusudi Lake la milele na kupata sifa kwa jina Lake (Zab. 76:10). {ABN1: 42.2}

Mfano mwingine wa udhihirisho huu wa ajabu unaonekana katika uhalifu wa nia ya uovu ya Balaamu. Bwana aliudhibiti ulimi wa Balaamu hata ingawa akili zake zilikuwa zimepotoka kulaani Israeli, aliweza kutamka baraka tu (Hes. 22, 23, 24). {ABN1: 43.1}

Hebu hii “mifano” iwe ukumbusho wetu wa daima kwamba mtu yeyote ambaye atadiriki kufanya kazi dhidi ya mapenzi yaliyofunuliwa ya Bwana hatafaulu na kufedheheka. {ABN1: 43.2}

Katika siku za baada ya gharika Bwana alitokea na kumwambia Abramu: “Nitawapa uzao wako nchi hii.” Mwa. 12:7. Kisha miaka kadhaa baadaye “watu watatu walisimama mbele yake,” mmoja wao akamwambia, “Sara mkeo atapata mwana wa kiume.” Mwa. 18:2, 10. Hivyo kupitia wakala wa Mungu, kwa njia fulani tofauti na ile iliyowadhibiti Adamu na Nuhu, Abrahamu aliwezeshwa (alivuviwa) kuelewa yatakayotukia siku za baadaye kwa ajili yake na wazawa wake. {ABN1: 43.3}

Kisha, pia, ulikuwapo wakati Balaamu (ambaye, kwa kisa cha Mfalme Balaki, alikuwa njiani kuelekea Moabu) alimcharaza punda wake mwaminifu, ambaye wakati huo alipokea zawadi ya kunena, akamwambia bwana wake mnyanyasaji: “Nimekutenda nini, hata ukanipiga mara tatu hizi?” Hes. 22:28. Hicho kiumbe bubu, tunaona,

43

kiliwezeshwa (kilivuviwa) kuzungumza kwa Uwezo uliokiumba. Kwa hivyo, itakuwa vyema, hakika kwa kila mtu kutii yale ambayo Bwana husema na kutenda bila kujali vipi, lini, wapi, au kupitia kwa nani Yeye husema au kutenda. {ABN1: 43.4}

Tena, miaka mingi kabla Israeli kuingia Misri, Mungu kwa majaliwa Yake (Mwa. 45:5) alimshawishi Yakobo kutengeneza kanzu ya rangi nyingi kwa mwanawe mdogo, Yusufu. Hili likionekana kuwa ubaguzi, pamoja na ndoto ya Yusufu na ufasiri wa baba yake kuihusu (Mwa. 37:10), uliwachochea wale ndugu waliokuwa na wivu kumuuza kama mtumwa, achukuliwe mbali hadi Misri ili kuzuia kuchukua mahali pao katika ushawishi au nafasi. Lakini huko Misri Bwana kwa wakati Wake mwenyewe alimwinua kwenye kiti cha enzi cha pili cha ufalme, kisha akaleta miaka ya wingi, pia miaka ya njaa, kama njia ya kuihamisha nyumba yote ya Yakobo kuingia Misri. {ABN1: 44.1}

Katika jaribio lao la kutamausha kutaka kumwondolea mbali Yusufu ili waepuke kutawaliwa naye, ndugu zake walifaulu tu (kuchochea uwezo ulio makini daima wa Majaliwa) kumwinua hadi kwenye kiti cha enzi cha utawala wa Misri, na kujishusha chini kwa aibu miguuni pake. Hapa upo ushahidi uliotiwa alama kwamba yeye anayejaribu kuyashinda makusudi ya Mungu hufanikiwa tu kuyashinda yake na kuyaendeleza ya Mungu. {ABN1: 44.2}

44

Wakati, akiwa kama mkimbizi kutoka Misri, Musa alikuwa akichunga kondoo za baba mkwe huko Midiani, “malaika wa Bwana akamtokea ndani ya mwali wa moto katikati ya kijiti; akatazama, na, kumbe, kile kijiti kiliwaka moto, nacho kijiti hakikuteketea.” Kut. 3:2. Kwa udhihirisho huu, Musa alivuviwa ili kuwaweka huru Israeli kutoka katika utumwa wao mgumu wa Wamisri. Na kisha kama kiongozi wa Waebrania wakati wa miaka yao arobaini ya kutangatanga nyikani, aliwasiliana na Bwana uso kwa uso (Kut. 34:30-35), na akaondoka uso wake uking’aa kwa utukufu. Hivyo uzoefu wake ulikuwa wa ajabu kwa ule wa wengine kabla yake. {ABN1: 45.1}

Farao na Nebukadnezza walikuwa na ndoto. Yusufu na Danieli walizifasiri (Mwa. 40:8-12; 41:25-38; Dan. 2:28; 4:20, 24). Danieli nabii, Yohana Waufunuo, na watu wengine watakatifu wa Mungu walikuwa na maono. Kila mmoja alikuwa mpokeaji maalum wa Uvuvio katika namna tofauti, na kwa kiwango kikubwa au kidogo. {ABN1: 45.2}

Kutoka kwa mifano hii na mingineyo mingi, tunaona kwamba Uvuvio hutenda kazi kwa njia mbali mbali maajabu Yake kutekeleza. Kupitia mwanadamu na kupitia wanyama, kwa kweli kupitia uumbaji wote, kazi Yake inaonekana katika namna nyingi. Baadhi wameusikia kwa sauti inayosikika, wote kupitia mawakala wanaoonekana (Kut. 34:30-35) na mawakala wasioonekana (Kut. 3:2). Wengine wameushuhudia kupitia maonyesho halisi,

45

ndoto, maono, majaliwa, talanta ya usemi wa ajabu na wa ghafla. {ABN1: 45.3}

Katika utendaji wote, kwa hivyo, tii udhihirisho wowote usio wa kawaida katika kanisa la Mungu, bila kujali chanzo, uwe ni wa binadamu au wa katili, wa mdogo au kubwa, mwafrika au mzungu, tajiri au maskini. Bila upendeleo linganisha kazi yake kwa Maandiko, na iwapo inapatana nayo, ikiwa inapata msingi wake na utabiri humo, kuwafanya watu wawe waaminifu kwa sheria na kwa manabii, na kuongeza nuru kwa ukweli wa sasa, upokee kwa gharama yoyote iwe pesa, mali, wadhifa, marafiki, na jamaa, kwa maana ni uhai wako mwenyewe. Yeye atakayethibitika mwaminifu katika wajibu huu atapata mara mia kwa kafara ambayo imemgharimu kuwa mwaminifu kwa sauti ya Bwana (Mat. 19:29). {ABN1: 46.1}

Lakini kuwa mkweli, na hivyo kujiokoa kutoka kwa dhambi isiyosamehewa, mtu lazima awe macho kila wakati. Na hili anaweza kulifanya tu kwa maombi akiichunguza ile roho ambayo inadai kuja kwa jina la Bwana. Akishindwa kufanya hili, anasimama katika hatari kubwa ya kukataa ombi la Roho Mtakatifu (Uvuvio), na hivyo kwa utepetevu kutupilia mbali maisha yake mwenyewe. {ABN1: 46.2}

“Ujumbe unapokuja katika jina la Bwana kwa watu Wake,” asema Roho wa Ukweli, “hakuna mtu anayeweza kujizuia kutofanya uchunguzi wa madai yake. Hakuna mtu anayeweza kujimudu kusimama nyuma katika mwenendo wa kutojali na

46

kujiamini na kusema: ‘Najua nini ni ukweli. Nimeridhika kwa nafasi yangu. Nimeweka vigingi vyangu, na sitasogezwa mbali na msimamo wangu, liwalo liwe, sitausikiliza ujumbe wa mjumbe huyu; kwa maana najua kwamba hauwezi kuwa ukweli’ Ilikuwa kutokana na kuufuata mwenendo huu hasa kwamba makanisa maarufu yaliachwa katika sehemu ya giza, na ndiyo sababu jumbe za mbingu hazijawafikia.” — Shuhuda kwa Kazi za Shule ya Sabato, uk. 65; Mashauri kwa Kazi za Shule ya Sabato, uk.28. {ABN1: 46.3}

Uvuvio huonyesha wazi kabisa kwamba mjumbe wa Bwana asithubutu kwa njia yoyote afanye ubunifu juu ya ufunuo (Ufu. 22:18-20), ingawa mara nyingi abarikiwe kuuelezea kwa maneno yake mwenyewe. Kuhukumiwa kwa kiwango sawa, hakuna mtu yeyote aweze kuthubutu kuhitilafiana na kazi ya mwandishi aliyevuviwa. Utaratibu huu wa busara siku zote huhitimisha kwamba wakati jambo katika maandishi ya mmoja halieleweki, basi mwandishi mwenyewe anapaswa kuulizwa kulihusu, iwapo yu hai. Vinginevyo, ni Roho yule yule wa Uvuvio, Mwandishi asilia wa maandishi, anayeweza kufafanua lolote linalohusika. Hakika, “ujumbe unapokuja,” jinsi Uvuvio unavyosema, “vumilia ili uweze kusikiza sababu ambazo mjumbe anaweza kutoa, ukilinganisha andiko kwa andiko, ili uweze kujua iwapo zinaidhinishwa na Neno la Mungu au la.”– Shuhuda kwa Kazi za Shule ya Sabato, uk.

47

65, 66; Mashauri kwa Kazi za Shule ya Sabato, uk. 29. {ABN1: 47.1}

Katika jambo lolote sio utaratibu wa maadili na salama kumsihi mpinzani wa maandishi ya mtu kuangazia sehemu yake iwayo yote. Mwana-demokrasi asingefikiri kumsihi Mwana-jamhuri kuangazia jukwaa la Udemokrasia, au kinyume chake, iwapo kila mmoja alitaka kujua ukweli. Kumbuka kwamba Hawa aliweka imani katika ufasiri wa Adui kwa Neno la Bwana (tendo ambalo lilimwongoza yeye na Adamu katika uasi na anguko lao, na tokeo la kufukuzwa kwao kutoka Paradiso) ndio iliyoleta laana ya dhambi na kifo kwa uumbaji wote wa dunia. Badala yake, ni kwa ajili yetu sasa kujiepusha na kizuizi hiki kielekeacho shimoni cha zamani na hapo kukifanya kiwe ngazi ya kupandia hadi kwa Ufalme. {ABN1: 48.1}

Kumbuka, pia, kwamba mazoea ya kulinganisha taarifa zilizonyafuliwa kutoka kwa muktadha wazo kimsingi ni mabaya, na huongoza leo kwa upotovu mwingi na utumizi mbaya wa ukweli jinsi ufanyavyo upindaji kimakusudi wa ushindani wa Shetani kwa Kristo: “Ukiwa ndiwe Mwana wa Mungu, jitupe chini, kwa maana imeandikwa, Atakuagizia malaika Zake, na mikononi mwao Watakuchukua, usije ukajikwaa mguu Wako katika jiwe.” Mat. 4:6. {ABN1: 48.2}

Kutoka kwa vidokezo vilivyotolewa hadi hapa, tunaona wazi kabisa kwamba bidhaa za mwisho za Uvuvio huangukia moja wapo ya makundi mawili —

48

aidha Uvuvio wa maneno au Uvuvio wa mawazo. Kuonyesha waziwazi: malaika hutokea na kumwambia mmoja, “Bwana kwa wakati kama huo na kama ule Atafanya hivi na vile kwa watu Wake. Waambie ujumbe huu, na uwaonyeshe kutoka kwa Maandiko ya kweli, maana manabii wameyanena humo tangu zamani.” Ujumbe wa malaika lazima ufikishwe na uaminifu kwa wazo hilo; ingawa ni dhahiri uchaguzi wa maneno, mbali na nukuu, ni lazima huachiwa mjumbe. Kwa hivyo, wakati wowote anapouona uwezekano wa kufanya wazo lililovuviwa lisimame wazi wazi na kwa uwezo, mjumbe yu chini ya wajibu mkubwa wa maadili kusahihisha lugha yake. Ni hivyo tu ndipo mtiririko wa maoni yaliyovuviwa yataendelea kung’aa na kuwa mazuri. {ABN1: 48.3}

Bado zaidi, zipo hali zinazohusiana na vipengele fulani vya kila ujumbe ambavyo hulazimisha maelezo zaidi. Maelezo kama hayo, hata hivyo, hayawezi kuwa makuu kuliko nuru inayoangaza kwa wakati huo. Na nuru inaweza kuja tu kutoka ndani ya ujumbe wenyewe, au, tena, inaweza kutoka kwa ufahamu uliowekewa mpaka wa kawaida kwa wakati “huo wa sasa” — uelewa ambao mjumbe mwenyewe huushiriki. {ABN1: 49.1}

Kisa kama hicho kilikuwa cha Yohana Mbatizaji. Alivuviwa kutangaza tu kuja kwa Mfalme, Yohana alikabiliwa na swali mintarafu kuanzishwa

49

kwa ufalme. Alijibu akizingatia uelewa wa kawaida ambao yeye na watu walikuwa nao kuhusu ufalme — kwamba Mfalme akija bila shaka Yeye atausimamisha ufalme Wake na hivyo kuwaweka huru watu Wake kutoka kwa nira ya Warumi. Lakini Kristo alipoonekana hatimaye, Yeye alifafanua kwamba wakati wa ufalme kusimamishwa, na wa nira ya Warumi kuondolewa kutoka kwa mabega ya watu Wake, ulikuwa bado haujafika. Na “wenye hekima” kweli hawakuwa na shaka kwa mafundisho haya yaliyopingana, bali waliupokea ukweli kwa furaha katika umbo lake la kuendelea, na waliendelea kupata mafanikio ya juu na ya juu zaidi ya kiroho, ilhali wale waliojikwaa kwa utofauti huu labda walimkataa Yohana kama nabii wa uongo na wakampokea Yesu kama Kristo, au walimpokea Yohana kama nabii wa kweli na kumkataa Yesu kama Kristo wa uongo, na kwa hivyo wakateleza zaidi na mbali zaidi kurudi nyuma na kwenda chini hadi hawakuwa tena wafuasi wa Kristo au Yohana. {ABN1: 49.2}

Njia za Uvuvio hazibadiliki, ni zile zile jana, leo, na kesho. Maswali mintarafu ukweli uliofunuliwa kwa hivyo lazima yajibiwe kwa njia ile ile leo kama yalivyokuwa katika wakati wa Yohana. Na hivi sasa kama wakati huo, wakosoaji, makafiri, na wanaotilia shaka watapata kulabu nyingi za kuning’inishia mashaka yao. Lakini vivyo hivyo sasa kama wakati huo, watiliao shaka watanaswa katika ujanja wao wenyewe. {ABN1: 50.1}

50

Uvuvio, isitoshe, siku zote huwaletea wajumbe wa Mungu katika mapatano kamili, kamwe si kwa mgawanyiko. Ukweli huu mkuu unaonekana umefafanuliwa vizuri katika uzoefu wa mtume Petro, Myahudi, na Kornelio, Jemadari wa Kirumi, na Mtu wa Mataifa. Bwana alijua kwamba Petro hatampokea mtu wa Mataifa, na ya kwamba Kornelio hangeweza kamwe kujitokeza kwa Myahudi. Kwa hivyo wote walipewa maono ya kuwaagiza la kufanya. (Tazama Matendo 10.) Na kutii maono ya mbinguni ambayo kwayo waliheshimiana, wao bila shida waliingia katika umoja wa heshima. {ABN1: 51.1}

Kisha upo uzoefu wa ajabu wa Paulo. Alipokuwa akifanya kazi ya uovu ya kuwatesa Wakristo, Bwana alikutana naye barabarani akielekea Dameski, akamwongoa, na kumpa maagizo ya mahojiano na Anania. Lakini akijua kwamba Anania, alimjua vyema Paulo kama mtesi wa waaminifu, hangeweza kamwe kumpokea wa mwisho kwa kukiri kwake uongofu na urafiki, Bwana alimpa Anania maono vile vile, alimufunulia uongofu wa Paulo. Na kwa hivyo wao, pia, kama Petro na Kornelio hapo awali, hawakuwa wakaidi kwa maono yao ya mbinguni (Matendo 26:19). {ABN1: 51.2}

Katika siku za Musa, wengine waliibuka wakidai kuwa Bwana alikuwa akinena kupitia kwao na pia kupitia kwa Musa (Hes. 16:2, 3). Uchochezi wao, hata hivyo, badala ya kuleta utaratibu na upatano

51

baina yao wenyewe na Musa, ulileta machafuko na vurugu, na matokeo mabaya kwamba maelfu walipoteza maisha yao (Hes. 16:32, 35, 49). Kama Bwana alikuwa amenena na watu hao, hakika angalikuwa amemjuza Musa jambo hilo. Lakini haswa ukosefu wa ufunuo wowote kama huo, ulifanya dhahiri kwa Musa kwamba Bwana hakuwa anawainua Kora, Dathani, na Abiramu kama walivyodai Yeye alikuwa akifanya, lakini badala yake kwamba wao kama wa mafarakano na walaghai, walikuwa wakijikweza wenyewe. Iwapo Musa, kama mtumwa wa Mungu, angalikubali madai yao, hakika yeye angekutana na adhabu kama vile “mtu wa Mungu” ambaye, alishawishiwa na “nabii mzee” kuiacha njia na kula mkate naye, wakati Bwana alikuwa amemwamuru asifanye hivyo, aliuawa na simba. Somo la kicho! Usizitii sauti za wanadamu kinyume na ya Mungu. (Tazama 1 Wafalme 13.) {ABN1: 51.3}

Wale, zaidi ya hayo, ambao Bwana hukweza, daima huogopa kujiweka mbele. Ingawa Daudi, kwa mfano, alikuwa ametiwa mafuta na Samweli kuwa mfalme juu ya Israeli, kamwe hakujaribu kukitwaa kiti cha enzi. Kwa kweli, hakufanya hata kujulikane kukwezwa kwake. Na kisha katika hatari ya kufa mikononi mwa Sauli mwenyewe, hata alimlinda. Katika uadilifu huu mzuri, Daudi alionyesha upendo, unyenyekevu, upole, na haki iliyozalishwa (iliyovuviwa) na Roho wa Mungu. Yake ilikuwa subira ya utulivu, upole,

52

uvumilivu ambao huja na maarifa ya hakika kwamba Mungu anaongoza. Akijua kwamba Bwana alikuwa amemtia mafuta kuwa mfalme, alisubiri kwa furaha hadi Bwana alipoona inafaa kumweka kwenye kiti cha enzi. {ABN1: 52.1}

Kutoka kwa hii mifano na mingineyo mingi, tunaona kwamba Mungu sio tu hutuma wakala mmoja kubadilisha, kuweka upya, au kutangua ujumbe ambao amemwagiza wakala mwingine, bila Yeye kwanza kufanya jambo hilo lijulikane na wote wawili, lakini pia kwamba Yeye kamwe haheshimu kuwakweza wale wanaotafuta kujiinua na kuikuza nafsi, bali kwamba huwakweza kwa msimu unaofaa wale wanaojinyenyekeza chini ya mkono Wake hodari (1 Pet. 5:6). {ABN1: 53.1}

Kama mantiki inayofahamika kwa awamu zilizotangulia za mada ya Uvuvio, itatambulika kwamba wote wanaongoka na kuwa watiifu kwa Bwana ni wapokeaji wa mnururisho Mtakatifu. Maana hakuna yeyote isipokuwa Roho Mtakatifu anaweza kumshawishi mmoja kwa Ukweli, kumsadikisha dhambi zake, kumpa toba, na kumtia nguvu kutii sheria za Mungu, kanuni Zake na maagizo Yake. Mwanadamu mwenyewe hawezi kuyatekeleza mabadiliko haya kama vile chui asivyoweza kubadilisha madoadoa yake. {ABN1: 53.2}

“Iwapo unaona dhambi yako, usingoje kujifanya bora. Ni wangapi hapo ambao hufikiri si wazuri kabisa kuja kwa Kristo. Je! Unatarajia kuwa bora kupitia juhudi zako mwenyewe?” ‘Je!

53

Mkushi anaweza kuibadilisha ngozi yake, au chui madoadoa yake? basi nanyi pia tenda wema, ambao mmezoea kutenda maovu.’ Upo msaada kwa ajili yetu ndani ya Mungu tu. Hatupaswi kungoja ubembelezi wenye nguvu, fursa bora, au tabia takatifu. Hatuwezi kufanya lolote sisi wenyewe. Lazima tuje kwa Kristo jinsi ambavyo tulivyo.” — Njia Salama, uk. 35, 36. {ABN1: 53.3}

“Hauwezi kufanya upatanisho wa dhambi zako za zamani, hauwezi kuubadilisha moyo wako, na kujifanza kuwa mtakatifu. Lakini Mungu ameahidi kukufanyia haya yote kupitia kwa Kristo. Wewe amini ahadi hiyo. Ungama dhambi zako, na ujikabidhi kwa Mungu. Unataka kumtumikia Yeye. Hakika unapolitenda hili, Mungu atalitimiza neno Lake kwako. Iwapo unaamini ile ahadi, — amini kwamba umesamehewa na kutakaswa, — Mungu hutoa ukweli; umepona, jinsi Kristo alivyompa aliyepooza nguvu kutembea mtu huyo alipoamini kwamba amepona. Ni hivyo ikiwa unaamini.” — Njia Salama, uk. 55. {ABN1: 54.1}

Hivyo kila mfuasi wa kweli wa Kristo amevuviwa katika fungu lake mwenyewe — mmoja kufasiri, mwingine kuchambua, na bado mwingine kufunza, na bado mwingine kupambanua, na wote kutenda na kujinyima kwa ajili Yake. {ABN1: 54.2}

Vivyo hivyo na kila Mkristo wa kweli amewezeshwa na Mungu kuteseka au kufurahi. Kwa hivyo, lolote linalotukia kwake, yawe ni mateso na huzuni, au hali-njema na furaha, mtoto anayemwamini Mungu hudiriki tu kumpa

54

Bwana sifa na hakuna mwingine kwa fungu lake. Na kumbuka kwamba “Jaribu halikuwapata ninyi, isipokuwa lililo kawaida ya wanadamu; ila Mungu ni mwaminifu; ambaye hatawaacha mjaribiwe kupita mwezavyo; lakini pamoja na lile jaribu atafanya na mlango wa kutokea, ili mweze kustahimili.” 1 Kor. 10:13. {ABN1: 54.3}

“Naam, hatasinzia wala hatalala usingizi, Yeye aliye mlinzi wa Israeli. Bwana ndiye mlinzi wako; Bwana ni uvuli mkono wako wa kuume. Jua halitakupiga mchana, Wala mwezi wakati wa usiku. Bwana atakulinda na mabaya yote, Atakulinda nafsi yako. Bwana atakulinda utokapo na uingiapo, Tangu sasa na hata milele.” Zab. 121:4-8. {ABN1: 55.1}

Kwa hivyo msiwe wakung’unika kama walivyokuwa wale “walioidharau ile nchi ya kupendeza,” na “wala hawakuliamini neno Lake. Bali wakanung’unika hemani mwao, wala hawakuisikiliza sauti ya Bwana. Ndipo alipowainulia mkono Wake, ya kuwa atawaangamiza nyikani.” Zab. 106:24-26. {ABN1: 55.2}

Lakini kuwa kama mtume mwaminifu: “Si kwamba nasema haya kwa kuwa nina mahitaji; maana nimejifunza kuwa radhi na hali yo yote niliyo nayo. Najua kudhiliwa, tena najua kufanikiwa; katika hali yo yote, na katika mambo yo yote, nimefundishwa kushiba na kuona njaa,

55

kuwa na vingi na kupungukiwa. Nayaweza mambo yote katika Yeye anitiaye nguvu. “ Filp 4:11-13. {ABN1: 55.3}

Lakini wakati upo mtiririko kutoka kwenye bakuli ya dhahabu (Zek. 4:2.) Kwamba Uvuvio ambao humwezesha mmoja kuwa Mkristo wa kweli, upo mtiririko kutoka kwenye pipa la kuzimu huo uvuvio mwingine ambao hutenda kazi kumfanza mmoja kuwa Mkristo wa uongo. Mmoja huokoa, mwingine huangamiza. Tukihitaji mwingi kama tunavyofanya ili tuweze kuwa wa ufahamu kamili na heshima kwa mmoja, Mungu, sisi kwa wakati uo huo kuwa na hitaji lililosawazishwa la kuwa hai kikamilifu kwa bandia wake —

Uvuvio wa Shetani. {ABN1: 56.1}

Inasikitisha, nguvu hii ya kishetani sikuzote imekuwa katika vizazi vyote ikifanikiwa kwa utukutu miongoni mwa uongozi wa kanisa. Bila kujua, umejiingiza siku zote katika kufuata ubunifu na juhudi za Shetani kubomoa (kupanga upya) kazi ambayo walidhani kwamba wanaijenga. {ABN1: 56.2}

Kwa ujio wa kwanza wa Kristo, viongozi wa kanisa walivuviwa sana na roho ya Shetani hivi kwamba, jinsi historia ya kanisa inavyofichua, nyakati zingine walitenda kama mashetani, kama watu ambao walikuwa wamerukwa na akili zao. Walikufa ganzi kwa mvua ya Ukweli ilivyonyesha katika siku hiyo, makuhani, waandishi, na Mafarisayo kwa kawaida walikuwa wamejazwa bidii ya kuwazuilia watu manyunyu ya

56

Ukweli. Hivyo ilikuwa kwamba walitumia kila njia iliyowezekana kuweka mwavuli, kwa mfano, juu ya vichwa vya watu, ili kuzuia hata tone la manyunyu ya vuli ya kuokoa maisha isiwanyeshee. Kwa hivyo ingawa matone ya Ukweli yalikuwa yakinyesha kuwazunguka pande zote kuliko hapo awali, waliridhika kubaki kwa ukame chini ya mwavuli wa kasisi unaokinga Ukweli. {ABN1: 56.3}

Ilikuwa katika masaa hayo ya giza ya historia ya mwanadamu, kwamba Ukweli na makosa, nuru na giza, uhuru na utumwa, viliunganishwa katika lile ambalo labda lilikuwa pambano kuu zaidi la wakati wote. Hadi Pentekoste, ni watu 120 tu kati ya mamilioni walioishi wakati huo waliokolewa kutoka kwenye ulanguzi wa kiroho kote nchini. Na baada tu kubatizwa na Roho Mtakatifu na kujazwa nguvu katika Pentekoste waliwezeshwa kuwasaidia wegine waliokuwa na kiu kutoka katika mzingo wa Shetani. {ABN1: 57.1}

Akiwa ameshindwa katika juhudi hii ya kuuzima Ukweli milele, Shetani upesi akafufua juhudi zake. Vyaja Vizazi vya Giza, na anaonekana tena akivuvia uadui dhidi ya Ukweli na wafuasi wake. Akawaachilia mashetani wake wote kwa ghadhabu yao yote juu ya kanisa, akaileta “dhiki kuu, ambayo haijatokea namna yake tangu mwanzo wa ulimwengu hata sasa, wala haitakuwapo kamwe.” Na kama siku hizo zisingalifupishwa, asingeokoka mtu ye yote, “lakini kwa ajili ya wateule siku hizo”

57

zilifupishwa (Mat. 24:21, 22) na Matengenezo. Kwa hivyo, mwingilio wa Mungu tu ulimzuia kuizimisha sauti ya Matengenezo na kuzidhoofisha nguvu zake. Hivi ndivyo ambavyo imekuwa siku zote, ilivyo leo, na itakavyokuwa mwisho mchungu. {ABN1: 57.2}

Kama tokeo, licha ya nuru yote inayoangaza sasa, umati mkubwa kwa upumbavu unaendelea kusongamana chini ya dari ya Shetani, kwa wakati uo huo wakisaidia kuvuta na kushikilia umati wa wengine chini yake pamoja nao. Walakini

Ahadi za Mungu Husimama Imara. {ABN1: 58.1}

“Sikilizeni, enyi mbingu, Nami nitanena; Na nchi isikie maneno ya kinywa Changu. Mafundisho Yangu yatadondoka kama mvua, Maneno Yangu yatatona-tona kama umande; Kama manyunyu juu ya majani mabichi; Kama matone ya mvua juu ya mimea.” Kumb. 32:1, 2. {ABN1: 58.2}

“Furahini, basi, enyi wana wa Zayuni, mkamfurahie Bwana, Mungu wenu; kwa kuwa Yeye huwapa ninyi mvua ya masika, kwa kipimo cha haki, Naye huwanyeshea mvua, mvua ya masika, na mvua ya vuli, kama kwanza. Na sakafu za kupepetea zitajaa ngano, na mashinikizo yatafurika kwa divai na mafuta …. Hata itakuwa, baada ya hayo, ya kwamba Nitamimina Roho Yangu juu ya wote wenye mwili; na wana wenu, waume kwa wake, watatabiri, wazee wenu wataota ndoto, na vijana wenu wataona maono; tena juu ya watumishi wenu, wanaume kwa wanawake, katika

58

siku zile, Nitamimina Roho Yangu.” Yoeli 2:23, 24, 28, 29. {ABN1: 58.3}

“Ndipo mtu aliye kilema ataruka-ruka kama kulungu, na ulimi wake aliye bubu utaimba; maana katika nyika maji yatabubujika; na vijito jangwani. Na mchanga ung’aao mfano wa maji utakuwa ziwa la maji, na nchi yenye kiu itakuwa chemchemi za maji; katika makao ya mbweha, walipokuwa wamelala, patakuwa na majani, pamoja na matete na mafunjo.” Isa. 35:6, 7. {ABN1: 59.1}

Licha ya Shetani kujitahidi kuifunika dunia yote na kifaa chake kinachokinga Ukweli, “Lakini itakuwa katika siku za mwisho, ya kwamba mlima wa nyumba ya Bwana utawekwa imara juu ya milima, nao utainuliwa juu ya vilima; na watu wa mataifa watauendea makundi makundi. Na mataifa mengi watakwenda na kusema, Njoni, twende juu mlimani kwa Bwana, na nyumbani kwa Mungu wa Yakobo; Naye atatufundisha njia Zake, nasi tutakwenda katika mapito Yake; kwa maana katika Zayuni itatoka sheria, na neno la Bwana litatoka Yerusalemu. {ABN1: 59.2}

“Naye atafanya hukumu kati ya watu wa kabila nyingi, Naye atawakemea mataifa wenye nguvu walio mbali; nao watafua panga zao ziwe majembe, na mikuki yao iwe miundu; taifa halitainua upanga juu ya taifa lingine, wala hawatajifunza vita tena kamwe. Bali wataketi kila mtu chini ya mzabibu wake, na chini ya mtini wake; wala hapana mtu atakayewatia hofu; kwa kuwa kinywa cha

59

Bwana wa majeshi kimenena hayo. Kwa maana mataifa yote watakwenda, kila moja kwa jina la mungu wake, na sisi tutakwenda kwa jina la Bwana, Mungu wetu, milele na milele.” Mika 4:1-5. {ABN1: 59.3}

JE! SHETANI ANAFANYA MAUZO YA JUMLA AU REJA REJA YA UDANGANYIFU?

Swali Namba 4:

Je! Shetani hutupa kikwazo maalum mbele ya kanisa kama mwili, au huwashambulia tu washirika wake mmoja mmoja? {ABN1: 60.1}

Jibu:

Tangu siku ile ya kutisha ndani ya Edeni alipopenyeza dhambi duniani na kusababisha anguko la mwanadamu, Shetani ametupa katika njia ya kila vuguvugu la ukombozi, kikwazo tofauti ambacho kwacho umati wa watu umesafiria na kuanguka. Hakika kabisa, kwa hivyo lazima itarajiwe kwamba anayo hatari fulani tofauti kama hiyo iliyowekwa njiani mwetu leo. Sisi, hata hivyo, tukiwa katika kizazi hiki na manufaa makubwa ya kujua mitego mbalimbali ambayo imesababisha vifo kwa umati wa watu katika Mavuguvugu ya zamani, tutapata hukumu na adhabu kubwa iwapo tunashindwa kutambua wetu. Na isitoshe, ikiwa tutashindwa, tutashuhudia kwa ulimwengu wote kwamba sisi ni wanyonge wa wanyonge. Lazima tusimame — tusimame dhidi ya mtego maalum wa werevu ambao haujawahi kuwekwa na Yule

60

Mwovu! Lakini tutafanyaje hili iwapo hatujui ni nini au ni wapi ulipo? {ABN1: 60.2}

Ili kupata pale ambapo hatari haswa inavizia, hebu tuangalie kwa ufupi kuikumbuka tena mitego ya awali, katika vipindi ambavyo ilitukia, kuanzia Vuguvugu la kwanza lililoandikwa la kanisa: {ABN1: 61.1}

Vuguvugu la Nuhu liliwekwa rasmi kujenga safina likiwa kama onyo la gharika iliyokuwa ikija na kama kimbilio kutoka kwayo. Kikwazo maalum cha kujikwaa ambacho Shetani alitupa kwenye njia ya umati wakati huo, alikibuni kutoka kwa ukweli kwamba katika maumbile yote hakuna mwanadamu aliyekuwa ameona kitu chochote kilichoazima ushahidi hata wa mbali kuhusu uwezekano wa kutukia ishara kama mvua. Hivyo, kwa kuegemea maarifa yao finyu ya maumbile na uwezo wake, walidhihaki na kudharau sayansi ya Nuhu na onyo lake la maangamizo, na wakaendeleza “kula na kunywa, wakioa na kuolewa, hata siku ile aliyoingia Nuhu katika safina, wasitambue, hata Gharika ikaja, ikawachukua wote.” Mat. 24:38, 39. {ABN1: 61.2}

Kuinua kwao sayansi ya wanadamu na kupuuza sayansi ya Mungu, kwa hivyo, ndio uliokuwa mtego maalum ambao uliwachukua watu walioishi kabla ya gharika. Hatima yao kwa uzito hutuonya kwa uangalifu tuepuke makosa yao. {ABN1: 61.3}

Katika Vuguvugu la Abrahamu, baba wa waaminifu aliitwa kuondoka katika miji ya ulimwengu wa zamani, kwa tumaini

61

kwamba siku fulani Vuguvugu hilo lingeweza kuimiliki nchi ya ahadi kwa ushindi. Akiwa anaufahamu kamili ukweli huu, Shetani alifanya kazi kwa nguvu kulikengeusha hilo Vuguvugu liingie katika miji ya mataifa njiani. Kwenye kizuizi hiki cha kujikwaa Lutu alianguka kwacho, pamoja na tokeo kwamba mwishowe Bwana alipomwondoa kwenye maangamizi ya Sodoma, kama kinga kilichonyakuliwa kutoka motoni, alitoka ndani fukara hohe hahe. {ABN1: 61.4}

Kwa hivyo miji ya kidunia ilikuwa mchanga wa kuwazamisha watu wa kwanza walioishi baada ya gharika. Tusije tukapoteza vyote mule, kama Lutu. {ABN1: 62.1}

Vuguvugu la Musa liliongozwa kutoka Misri ili kumiliki nchi ya ahadi, na humo kuwa ufalme. Kwa ujanja akifanikisha majaribu yake kwa mielekeo yao waliorithi, Shetani aliwavuvia wale waliokuwa watu wazima walipoondoka katika nchi ya Farao, kwa manung’uniko yasiyokoma, kulalamika, kutafuta ofisi na kuasi, na mwishowe kuwaogopa majitu wakazi wa nchi ya ahadi. Wakishindwa kuona kwamba nguvu yao ilikuwa mkono hodari wa Bwana, walilazimika kutangatanga kwa muda wa miaka mirefu arobaini nyikani, na humo kuiacha ikauke mifupa ya wote isipokuwa wawili wa washirika wao ambao walikuwa na umri mkubwa walipoondoka Misri. {ABN1: 62.2}

Kutoamini, shingo gumu, kutokuwa na imani kwa uongozi wa Mungu, na kutafuta ofisi, kwa hivyo, lilikuwa dubwana lenye vichwa vinne lililowameza watu wa Kutoka. Na

Mtoa Jibu Kitabu Namba 1 62

hivi vitamla kila mwamini wa Ukweli wa sasa anayepotelea kwenye mapango yao. {ABN1: 62.3}

Vuguvugu la Kanani chini ya Yoshua liliondolewa wadhambi wote na kuagizwa kuimiliki nchi, kuwafukuza mataifa nje, na kuusimamisha ufalme wa milele. Akijua kwamba mwendelezo wake ulitegemea utiifu wao kwa maagizo ya Bwana kupitia manabii Wake, Shetani aliwachochea watu kuwadhihaki wajumbe wa Mungu, kuyadharau maneno Yake, na kuwatumia vibaya manabii Wake, “hadi ghadhabu ya Bwana ikawaka dhidi ya watu Wake, hata kusiwe na kuponya” (2 Nya. 36:16), na akawaachilia warudi tena utumwani. {ABN1: 63.1}

Hivyo kwa raia wa ufalme, manabii walikuwa mwamba mkuu wa kujikwaza — mwamba ambao juu yake hakuna kizazi kabla au tangu wakati huo kumekuwa huru kutojikwaza. Wenye hekima leo, kwa hivyo, “hawataudharau unabii.” 1 Thes. 5:20. {ABN1: 63.2}

Vuguvugu la Mitume lilitokezwa kutangaza kuhamishwa kwa utumishi wa patakatifu pa duniani hadi kwa “hema ya mbinguni, ambayo Bwana aliiweka, na wala si mwanadamu” (Ebr. 8:2), na kubatiza “kwa jina la Baba, na la Mwana, na la Roho Mtakatifu” (Mat. 28:19) wote ambao wanapaswa kutubu dhambi zao. Lakini ili kuvuruga kusudi lake, Shetani alianza kufanya kazi kutengeneza udanganyifu mwingine, na baada ya kuondoka kwa mitume alifanikiwa haraka kusababisha kanisa likose kuuona kabisa

63

ukweli wa ukuhani wa Kristo na ukweli wa ubatizo, na kuanzisha badala yazo ukuhani wa uongo wa kidunia na ubatizo wa watoto wachanga. {ABN1: 63.3}

Kwa hivyo wakiwa wameongozwa kutoamini na kupuuza utumishi wa patakatifu na ubatizo, haswa wokovu wao wenyewe, kanisa la Kikristo lilianguka kupitia mlango wa mtego wa Shetani hadi kwenye makosa. Na mlango huo bado umewekwa ili kuchukua miguu ya wasio waangalifu — wote ambao hupuuza au kuchukulia kihivi-vivi ukweli unaoendelea daima uliofunuliwa katika ujumbe maalum wa leo wa kutiwa muhuri. {ABN1: 64.1}

Mavuguvugu ya Waprotestanti yaliinuliwa kutangaza na kutumia uongozi wa Biblia, kwa sababu ulimwengu kabla ya matengenezo ulikuwa umefungwa gizani kwa sheria ya dini ya mwanadamu ambaye hakuvuviwa, kutowaruhusu watu wa kawaida haki ya kumiliki Biblia, na kuwafanya wautegemee ufasiri wake apendavyo tu kuihusu. Kwa hivyo yakaja makanisa ya Uprotestanti katika ufuatano wayo, ili kurejesha Ukweli uliokanyagiwa chini, kila moja likiteta dhidi ya dhuluma hizi na unyakuzi wa haki za binadamu, kila moja likiitwa kuufanya ulimwengu wa Ukristo ujue hitaji la Uvuvio wa kweli na uhuru wa dini, haki ya kumiliki Biblia na kujisomea wenyewe, na jukumu la kuifanya Biblia na Biblia pekee, kuwa kanuni ya imani yao. {ABN1: 64.2}

Akiwa ameazimia, hata hivyo, kuyaua Matengenezo, Shetani daima tangu mwanzo wayo amefanya kazi kusababisha kila

64

mshiriki wa kanisa kujifurahisha katika ufasiri wa apendavyo mtu tu wa Maandiko na katika nadharia za ziada za Kibiblia. Kwa hivyo, Uprotestanti leo hujikuta wenyewe ukifuata sio tu katika njia ya fasiri za Biblia ambazo hazijavuviwa za mtu mmoja bali katika njia za fasiri ambazo hazijavuviwa za maelfu ya watu! Na tokeo yake ni kwamba Himaya ya Wakristo imejaa madhehebu na mchafuko usio na kifani katika historia — uthibitisho kwamba kazi kubwa ya mababa waasisi wa Matengenezo ya Uprotestanti imepotoshwa na kugeuzwa kuwa jeshi la kudhoofisha la kuvuruga kusudi maalum la Mungu kwa kanisa leo. {ABN1: 64.3}

Hivi tunaona kwamba Matengenezo, ambayo, mwanzoni yalikuwa chini ya maelekezo ya watu waliovuviwa, yaliliinua kanisa kutoka katika bwawa moja la matope, baadaye chini ya maelekezo ya watu ambao hawakuvuviwa, walilitumbukiza ndani ya lingine, ambamo limekuwa likihangaika tangu wakati huo. Na isipokuwa tuuruhusu Ukweli utukwamue kutoka kwa bwawa hili hatari la machafuko, hatuwezi kumshinda Adui wa Uvuvio katika juhudi zake zisizochoka na zenye nguvu kwa kuvipotosha vifaa vya wokovu wetu kuwa silaha za maangamizi yetu. {ABN1: 65.1}

Vuguvugu la Waadventista wa Sabato liliteuliwa kutangaza kazi ya patakatifu: “Mcheni Mungu, na kumtukuza, kwa maana saa ya hukumu Yake [mavuno] imekuja” (Ufu. 14:7) kuondoa katika Kitabu cha Uzima cha Mwana-Kondoo, majina ya wote ambao hawakuvijaza vyombo vyao mafuta ya

65

ziada (Mat. 25:3), na wale ambao hawakuwa wamejivika vazi la harusi (Mat. 22:11), pia wale ambao hawakuwa wamezidisha talanta zao mara mbili (Mat. 25:14-30); na pia kuondoa magugu kutoka kati ya ngano (Mat. 13:30). {ABN1: 65.2}

Utangazaji huu mintarafu wafu ulikuwa wa kuwaandaa walio hai kwa hukumu yao inayokaribia. Kwa sababu hii, Shetani ametumia kila chombo kuwapumbaza Waadventista kuwa wasikilizaji na wahubiri tu lakini sio watendaji wa Neno; kwa kulipa zaka za mnanaa na bizari na jira, kwa mfano, lakini kuyaacha mambo makuu ya sheria. Kwa ufupi, amewafanya kuwa wanyonge na wenye mashaka na maskini na vipofu na uchi kwa kushindwa upande mmoja kuwa waaminifu katika kutenda yale wanayowafunza wengine kufanya, na kwa kushindwa kwa upande mwingine kujizuia wasitende yale wanayowafunza wengine wasifanye. Na ili kuwazuia wasiamke kutoka kwa huu “udanganyifu wa kutisha” (Shuhuda, Gombo la 3, uk. 254), yeye huwadumisha kuwa wavuguvugu, kwa utulivu wakiota kwamba wao ni matajiri wa ukweli na hawana haja ya chochote, ingawa kwa kweli wako kwa shida na wanahitaji kila kitu. {ABN1: 66.1}

Wazi wazi, basi, uvuguvugu na maono ya uongo ya kuwa tajiri ni makosa ya kipekee kwa Walaodekia, na ni hatari ambazo ikiwa hazitatambuliwa na kuondolewa hatimaye zitasababisha Mungu awatapika kutoka kinywani Mwake (Ufu. 3:16). Hivi tena

66

kwa huruma Bwana anawasihi waamini wa Ukweli wa sasa watembee nuruni na waepuke uvuguvugu, wasije wakarudi nyuma kwa kufikiri wao ni matajiri na wamejitajirisha na hawahitaji chochote, na tena kuwa maskini na wahitaji wa kila kitu. Hivyo tunaona kwamba wakati Shetani hajaweza kumpindua kila mshirika binafsi, hata hivyo, ameweza, kupindua kila Vuguvugu hadi leo. {ABN1: 66.2}

Vuguvugu la saa kumi na moja, likiwa la mwisho kabisa, kwa hivyo liko kwenye hatari kubwa zaidi ya yote. Ni uharaka gani, basi, kwamba tuwe macho ili tusije, pia, tukaanguka! Vuguvugu hili, hata hivyo, likiwa ni juhudi ya mwisho ya injili, lazima “litoe uwezo na msukumo” kwa Ujumbe wa Malaika wa Tatu na “kuiangaza nchi kwa utukufu wake” (Ufu. 18:1); lazima lishinde, ingawa kila vuguvugu kabla yake limeshindwa. Limekusudiwa, si kutoa “utabiri tena” kwa “mataifa mengi” (Ufu. 10:11), bali kwa “mataifa yote.” Na kwa sababu litakwenda kwa watu ambao hawajaisikia habari Yake, na kuwaleta katika nyumba ya Bwana watakatifu wote “kutoka katika mataifa yote” (Isa. 66:19, 20), ndiposa lilipangiwa tangu zamani kudumu. Ili kutekeleza kusudi hili lililopangwa kimbele, Mungu sasa anachukua mamlaka mikononi Mwake (Shuhuda kwa Wachungaji, uk. 300), ili kulitakasa kanisa kwa kuondoa ndani yake magugu, na kulihifadhi likiwa huru kwayo tokea sasa, ili liweze kusimama juu ya Mlima Zayuni na Mwana-Kondoo (Ufu. 14:1). {ABN1: 67.1}

67

Hakika, katika uhalisi haswa wa hali hiyo, Vuguvugu la Saa ya Kumi na moja lazima lishinde, kwa maana, likiwa ni la mwisho, lile ambalo litayaleta ndani mavuno, basi likishindwa, kila mtu duniani leo atabaki amepotea milele. Maradufu, kwa hivyo, ni sababu kwamba Bwana anakusudia lisimame. Hivyo, Wadaudi wameitwa kwa “Ufalme kwa wakati kama huu.” {ABN1: 68.1}

“Kwa maana,” latangaza Neno, “Bwana atateta na wote wenye mwili kwa moto na kwa upanga Wake: nao watakaouawa na Bwana watakuwa wengi…. Nami nitawatuma hao waliookoka kwa mataifa…. Nao watahubiri utukufu Wangu katika mataifa. Nao watawataleta ndugu zenu wote kutoka katika mataifa yote kuwa sadaka kwa Bwana.” Isa. 66:16-20. {ABN1: 68.2}

“Nao [Mataifa] watawaita watu watakatifu, waliokombolewa na Bwana. Isa. 62:12. {ABN1: 68.3}

“Lakini ni nani atakayestahimili siku siku…? Au ni nani atakayesimama atakapoonekana Yeye? Kwa maana Yeye ni mfano wa moto wa mtu asafishaye fedha, ni mfano wa sabuni ya mtu afuaye nguo.” Mal. 3:2. {ABN1: 68.4}

Sababu zaidi, basi, kwamba wafuasi wake lazima wapimwe na kuthibitishwa wanastahili. Nini, kwa hivyo, hatari ya kwanza na kubwa inayowakabili waamini wa Ukweli wa sasa leo? {ABN1: 68.5}

Pamoja na wisho wa safari ndefu kwa mtazamo, kazi haijawahi kuwa kubwa sana, wakati

68

wa kuitekeleza haujawahi kuwa mfupi sana, na watendakazi hawajawahi kuwa wachache sana, kama sasa. Unavyojidhihirisha, kwa hivyo, ni ukweli kwamba bidii kuu ya Shetani saa hii lazima iwe ya kusababisha wakati upotezwe na kazi isifanywe. {ABN1: 68.6}

Amka, basi, Ee mwamini wa Ukweli wa sasa! Inuka upesi kwa kazi iliyowekwa, na “lolote mkono wako utakalolipata kulifanya, ulifanye kwa nguvu zako.” Mhu. 9:10. Usiruhusu tena muda upotezwe, kwa maana kila wa thamani ni muhimu kwa wokovu wa nafsi yako mwenyewe na kwa nafsi za wengine. {ABN1: 69.1}

JE! ROHO ANENAJE KWA LAODEKIA?

Swali Namba 5:

Je! Laodekia katika uvuguvugu wake hawasilishi katika njia kamili hali hatari ambayo mtume Paulo huonya dhidi yake anaposema: “anayejidhania kuwa amesimama na aangalie asianguke”? {ABN1: 69.2}

Jibu:

Historia takatifu hurudia-rudia na funzo la kuhuzunisha kwamba watu wanapokwenda kombo, walivyofanya Israeli wakati wa Eliya na tena katika wakati wa Kristo, hawawi tena na hisia kwamba wamekosa. Vivyo hivyo kurudia-rudia ni funzo baya hata zaidi kwamba watu kama hao siku zote wamezipotosha juhudi za Mungu kuwaleta kwa utambuzi wa makosa yao. Hivyo mara tu wanapoongozwa kuasi kutoka kwa mafundisho ya manabii, na

69

kunaswa na uongozi mpya wa wanadamu wenye sumaku, ukombozi na kurekebishwa kwao huwa vigumu kuwezekana. (Tazama Manabii na Wafalme, uk. 122,126.) {ABN1: 69.3}

Katika njia mbalimbali, udhaifu wa kufisha ambao umekuwa sifa ya kila Vuguvugu, kutoka lile la Israeli hadi lile la Laodekia, umekuwa katika “kuweka msingi tena wa kuzitubia kazi zisizo na uhai.” Ebr. 6:1. Na lile ambalo bado ni la msingi, na la dharura zaidi kwenye suala, ni kwamba kila Vuguvugu vivyo hivyo lilishindwa kustawi kutoka kwa ujumbe mmoja hadi uliofuata, na kuendelea kufikia lengo lake la ufanisi bora katika maarifa ya Mungu. Badala yake, kila moja lilianguka kutoka vimo virefu vya uzoefu wake wa mapema, hadi chini kwa umaskini wa kiroho, kwa sababu lilishindwa kuambatana na Ukweli. Kila Vuguvugu lililoitwa na Mungu lilikwama pale ambapo kwa kinaya lilijiridhisha lenyewe kwamba lilikuwa bado katika hatua zilizotakaswa hadi kwa Mlima wa Ukamilifu, kwamba “lilikuwa linanawiri, na ya kwamba amani na mafanikio ya kiroho” yalikuwa “katika mipaka [yake] yote” (Shuhuda, Gombo la 5, uk. 217), ilhali katika uhalisi, kinyume kabisa ulikuwa ndio ukweli. Hivyo linafuata Laodekia, likiwaza liko sawa wakati ambapo lote limekosea. {ABN1: 70.1}

Kamwe katika historia ya ujeuri ya ulimwengu huu uliogharikishwa kwa dhambi hatari kubwa na hitaji kubwa limelikabili kanisa. Katika hatari hii inayoifunika kotekote, “Mungu anasema nini kuwahusu watu Wake? — ‘Lakini watu hawa ni watu walioibiwa na kutekwa;

70

wote wamenaswa katika mashimo, wamefichwa katika magereza; wamekuwa mawindo, wala hapana aokoaye; wamekuwa mateka, wala hapana asemaye, Rudisha. (Tazama pia Isaya 43.) Huu ni unabii ambao utatimizwa.” — Shuhuda kwa Wachungaji, uk. 96. {ABN1: 70.2}

“Ni udanganyifu mkubwa ulioje unaoweza kuja kwa akili za binadamu kuliko kujiamini kwamba wao wako sawa, ilhali wao wote wamekosa!” — Shuhuda, Gombo la 3, uk. 252, 253. {ABN1: 71.1}

Tena imeandikwa katika Mithali 29:18 (pambizo), “Pale mbapo hakuna maono, watu huangamia.” {ABN1: 71.2}

Hapa katika onyesho pana zaidi ipo picha ya watu ambao hakika wamepoteza “maono” yao (uongozi wa Mungu uliotolewa na sauti hai ya karama ya unabii iliyo kati yao), lakini ambayo hawaitambui. La kushangaza zaidi, ni wazi wameanzisha uvumbuzi wao wenyewe (visanamu) kama mbadala wa mambo ya Mungu. Wamefanya hili pole pole hivi kwamba hawalijui kwa sababu wapo wengi hawajajipatia magombo ya Roho ya Unabii — “jicho lao” haswa. Na ambapo wengine wamekuwa na magombo haya ya maono yakitapakaa kuwazunguka pande zote, wameyaacha yakae bila kusomwa au kupuuzwa na kwa hivyo “kutothaminiwa.” — Shuhuda, Gombo la 5, uk. 217. Kwa hivyo ni kwa maana hii zaidi ya nyingine yoyote kwamba wamekuwa vipofu — hawatarajii tena hata ukweli wowote

71

uliofunuliwa zaidi kupeana uwezo na msukumo kwa ujumbe wao (Maandishi ya Awali, uk. 277). Bado wanajidanganya kwamba wako katika mzingo wa ndani wa neema ya Mungu! {ABN1: 71.3}

“Ujumbe wa Shahidi wa Kweli huwapata watu wa Mungu katika udanganyifu wa kusikitisha, hata sasa bado ni waaminifu katika udanganyifu huo. Hawajui ya kwamba hali yao ni mbaya machoni pa Mungu. Ilhali wale wanaohutubiwa wanajidanganya kwamba wako katika hali ya juu kiroho, ujumbe wa Shahidi wa Kweli huvunja usalama wao kwa mashtaka ya kushtua na ya kushangaza kuhusu hali yao halisi ya upofu wa kiroho, umaskini, na unyonge. Ushuhuda, unaokata hivyo na mkali, hauwezi kuwa kosa, kwa sababu ni Shahidi wa Kweli anayenena, na ushuhuda Wake lazima uwe sahihi.” — Shuhuda, Gombo la 3, uk. 253. — {ABN1: 72.1}

Iwapo michakato ya kuwaza ya Walaodekia haikuwa katika hitaji kubwa la marekebisho kamili ya kiroho na mwelekeo mpya, hawangeweza “kufikiri kwamba wote wako sawa ilhali wote wamekosea,” hufikiri kwamba wao ni “matajiri” ambapo kwa uhalisi wako “maskini” sana — fukara wa ukweli na haki! {ABN1: 72.2}

Kwa hivyo, si chochote ila ujumbe wenye “uponyaji katika mabawa yake” utaponya akili ya Mlaodekia ugonjwa wake wa kiroho. Katika saa hii hatari ya kanisa, “Wale ambao wamekuwa waoga na wasiojiamini, watajitangaza wazi kwa ajili ya Kristo na

72

ukweli wake. Wale dhaifu sana na wa kusitasita kanisani, watakuwa kama Daudi — tayari kutenda na kuthubutu.” — Shuhuda, Gombo la 5, uk. 81. Mbona? — Kwa sababu wanayo ahadi kwamba “watu wa nyumba ya Daudi, na wenyeji wa Yerusalemu, watafunguliwa chemchemi kwa dhambi na kwa unajisi.. {ABN1: 72.3}

“Kisha itakuwa katika siku hiyo, asema Bwana wa majeshi, nitakatilia mbali majina ya sanamu katika nchi, yasikumbukwe tena; pia nitawafukuza manabii, na roho ya uchafu, watoke katika nchi.” Zek. 13:1, 2. {ABN1: 73.1}

“Kwa kuwa katika siku hiyo kila mtu atatupa sanamu zake … ambazo mikono yenu imezifanya zikawa dhambi kwenu … Mwelekeeni Yeye Mliyemwasi sana enyi wana wa Israeli.” Isa. 31:7, 6. {ABN1: 73.2}

“Katika siku hiyo Bwana atawalinda wenyeji wa Yerusalemu; na yeye aliye dhaifu miongoni mwao atakuwa kama Daudi siku hiyo; nayo nyumba ya Daudi itakuwa kama Mungu, kama malaika wa Bwana mbele yao.” Zek. 12:8. {ABN1: 73.3}

Sauti ya Roho kupitia Isaya sasa pia inapiga kelele kwa sauti: “Amka, amka, jivike nguvu zako, Ee Zayuni; Jivike mavazi yako mazuri, Ee Yerusalemu, mji mtakatifu; Kwa maana tokea sasa hataingia ndani yako asiyetahiriwa, wala aliye najisi …. Jinsi ilivyo mizuri juu ya milima

73

miguu yake aletaye habari njema, yeye aitangazaye amani, aletaye habari njema ya mambo mema, yeye autangazaye wokovu, auambiaye Zayuni, Mungu Wako anamiliki!” Isa 52:1, 7. {ABN1: 73.4}

Sauti iyo hiyo kupitia Nahumu pia inasihi: “Tazama, juu ya milima iko miguu yake aletaye habari njema, atangazaye amani. Zishike sikukuu zako, Ee Yuda, uziondoe nadhiri zako; kwa maana yule mwovu hatapita kati yako tena kamwe; amekwisha kukatiliwa mbali.” Nah. 1:15. {ABN1: 74.1}

Lakini katika historia yake yote, kanisa kwa ujumla halijawahi kuupokea ujumbe kutoka mbinguni. Mwito kwa hivyo huja kwa kila mshiriki binafsi. Kila mmoja lazima ajiamulie mwenyewe. Hakuna mtu anayepaswa kuruhusu kushawishiwa na mwingine. Na “hakuna mtu anayeweza kujizuia kutofanya uchunguzi wa madai yake…. Ilikuwa kutokana na kuufuata mwenendo huu hasa kwamba makanisa maarufu yaliachwa katika sehemu ya giza, na ndiyo sababu jumbe za mbingu hazijawafikia.” — Shuhuda kwa Kazi za Shule ya Sabato, uk. 65; Mashauri kwa Kazi za Shule ya Sabato, uk. 28. {ABN1: 74.2}

“Lakini tunaona kwamba Mungu wa mbinguni wakati mwingine huwaagiza watu kufunza lile ambalo huangaliwa kama ni kinyume na mafundisho yaliyowekwa. Kwa sababu wale ambao wakati fulani

74

walikuwa ghala la ukweli wakawa wasio waaminifu kwa jukumu lao takatifu, Bwana aliwachagua wengine ambao wangeweza kuipokea mianga miangavu ya Jua la Haki, na wangetetea kweli ambazo hazikuwa kulingana na mafundisho ya viongozi wa kidini. Na kisha viongozi hawa katika upofu wa akili zao, hutoa udanganyifu kamili kwa kile kinachodhaniwa kuwa ni gadhabu ya haki dhidi ya wale ambao wameweka kando hadithi zilizotungwa kwa werevu. Hutenda kama watu ambao wamepatwa na wazimu. Hawauangalii uwezekano kwamba wao wenyewe hawajalielewa Neno kwa usahihi. Hawatafumbua macho yao kutambua ukweli kwamba wamefasiri na kutumia vibaya Maandiko, na wamejenga dhana za uongo, na kuziita mafundisho ya msingi ya imani.” — Shuhuda kwa Wachungaji, uk. 69, 70. {ABN1: 74.3}

Kwa sababu Walaodekia tayari wako katika udanganyifu mkubwa, basi kwa yeyote kati yao kukataa kulichunguza dai la ukweli akiogopa kudanganywa kwa kufanya hivyo, ni kupumbaza akili. Kuchunguza na kuchambua ni wokovu pekee wa mtu — tumaini lake la pekee la kutoka katika udanganyifu wake wa “kusikitisha,” “wa kutisha,” “wa kuogofya” (Shuhuda, Gombo la 3, uk. 253, 254, 260), na tumaini lake pekee la kumlinda kumzuia kutumbukia kuzimu. Kwa hivyo lazima asome kuliko hapo awali! Na kwa kufanya hivyo atapata kwamba huu ni mwanzo wa ujumbe haswa ambao lazima awe nao

Mtoa Jibu Kitabu Namba 1 75

ili kuondoa magamba kutoka ndani ya macho yake na kuvifunua visivyoonekana, lakini hata hivyo halisi, ni vifungo vya uvuguvugu na kujiinua nafsi ambavyo Adui humshikilia akiwa mfungwa. {ABN1: 75.1}

JE! UKWELI HUFANYA MGAWANYIKO?

Swali Namba 6:

Je! Mbona kwa uelekevu usikubali kwamba ujumbe wowote unaokuja kutoka kwa Mungu haupaswi kusababisha mgawanyiko na utengano kati ya watu Wake? Je! Si ukweli kwamba “Fimbo ya Mchungaji” husababisha yote mawili, uthibitisho wa kutosha kwamba haiwezi kuwa na ujumbe wa saa hii? {ABN1: 76.1}

Jibu:

Ni hakika kweli kwamba ufunuo wowote mpya wa ukweli kutoka kwa Neno la Mungu haupaswi kamwe kusababisha mgawanyiko na utengano. Lakini ukweli wa kusikitisha ni kwamba kinyume siku zote umekuwa ukweli. {ABN1: 76.2}

Ili kujiridhisha mwenyewe muulizaji anahitaji kujiuliza: Je! Ni mara ngapi Mungu ametuma jumbe kwa kanisa Lake ambazo hazikuleta shida na utengano miongoni mwa watu Wake? Iwapo mahitimisho yanaunga mkono kauli yake, basi kama Wakristo lazima bila shaka tubadilishe msimamo wetu na tukubali kwamba Fimbo haina ujumbe kutoka kwa Mungu. Ikiwa, hata hivyo, historia ya kanisa inadunisha mantiki yake, basi bila shaka tutamtarajia yeye, kama Mkristo mwaminifu na anayeutafuta ukweli, akiri kwamba hoja yake haijapinga Fimbo. {ABN1: 76.3}

76

Kama jumbe zote zilizotumwa na mbingu kuutangulia, ujumbe wa Fimbo ni, kwa mujibu wa unabii wa Ezekieli katika sura ya 9, na Shuhuda kwa Wachungaji, uk. 445, umewekwa “kwa kuanguka na kuinuka wengi katika Israeli” (Luka 2:34), umehesabiwa kikamilifu kuleta mpepeto, utengo wa magugu kutoka kati ya ngano katika ushirika wa kanisa! (Tazama pia Maandishi ya Awali, uk. 270.) {ABN1: 77.1}

Ukweli kwamba ujumbe wa Fimbo huleta utengano, ni ushahidi mmoja zaidi katika uthibitisho kwamba katika athari hii ya msingi, angalau, uko sambamba na jumbe zingine zote kutoka kwa Mungu. Hili kwa hivyo huongeza kiunganishi kingine kwenye mnyororo wa dhahabu wa Ukweli ambao hauwezi kuchafuliwa au kuvunjwa. “Uzito wa ushahidi” ni kigezo cha haki na cha mwisho kinachostahili kwa Mkristo ambaye lazima ajifanyie uchunguzi kuhusu ukweli unaodai kuwa. {ABN1: 77.2}

KRISTO AU MTUMWA WAKE?

Swali Namba 7:

Je! Unawezaje kupatanisha “Watendakazi wa Injili,” uk. 44, aya ya 2, na “Fimbo ya Mchungaji,” Gombo la 2, uk. 240, aya ya 2, zilizowasilishwa kwa kulinganishwa kama ifuatavyo: {ABN1: 77.3}

“Mjumbe sio Bwana Mwenyewe, … yeye ndiye atakayeiandaa njia ya Bwana.” — “Fimbo ya Mchungaji,” Gombo la 2, uk. 240. {ABN1: 77.4}

“Kristo, Mjumbe wa agano alileta habari njema ya wokovu.” — “Watendakazi wa Injili, uk. 44. {ABN1: 77.5}

77

Jibu:

Tukiwa kwa ukurasa wa 44, Watendakazi wa Injili hutumia jina “Mjumbe wa Agano” kwa Kristo, kwenye ukurasa wa 20 hulitumia kwa Musa. Katika ulinganisho, maandishi haya yanaonekana kama ifuatavyo: {ABN1: 78.1}

“Musa alipochaguliwa kama mjumbe wa agano, neno alilopewa lilikuwa, “Uwe wewe kwa ajili ya watu mbele ya Mungu.’” — Watendakazi wa Injili, uk. 20. “Kristo mjumbe wa agano, alileta habari njema ya wokovu.” — Watendakazi wa Injili, uk. 44. {ABN1: 78.2}

Hali ya kuwa Watendakazi wa Injili hulitumia neno hilo kwa wote Musa na Kristo, Kristo Mwenyewe hulitumia kwa Yohana Mbatizaji. Alisema “kwa umati wa watu habari za Yohana … Mlikwenda nyikani kuona nini? Nabii? naam, Ninawaambia, na aliye mkuu zaidi ya nabii. Maana huyu ndiye aliyeandikiwa haya, Tazama, Mimi, namtuma mjumbe Wangu mbele ya uso wako, atakayeitengeneza njia Yako mbele Yako. Na ikiwa mtayapokea, yeye ndiye Eliya, atakayekuja. Mat. 11:7, 9, 10, 14. {ABN1: 78.3}

Kwa sababu Mungu alikuwa amefanya maagano yaliyonenwa na yaliyoandikwa na watu Wake wa zamani kwamba angewatumia Musa, Yohana, na Kristo, walikuja katika utimizo wa maagano hayo. Na kila mmoja baada ya kuuleta ujumbe, kila mmoja kwa wakati wake alikuwa Mjumbe wa Agano. Walakini, maneno ya Malaki huonyesha wazi kwamba Mjumbe wa Agano ni, kwa maana kamili nabii Eliya (Mal. 3:1-5; 4:5), mjumbe wa mwisho anayeitayarisha

78

njia ya Bwana. (Angalia Shuhuda kwa Wachungaji, uk. 475.) {ABN1: 78.4}

Katika uchanganuzi wa mwisho, hata hivyo, jina Mjumbe wa Agano ni la Roho Mtakatifu. Kwa mfano, 1 Petro 3:18-20 husema kwamba Kristo aliwahubiria watu walioishi kabla ya gharika na “Roho” yule yule ambaye “Alimuhuisha.” Lakini alipokuwa akihubiri katika Roho kupitia mtu Nuhu, sio Yeye Mwenyewe, kwa hivyo Yeye aliufunua ukweli kwamba Roho Mtakatifu yu ndani ya wajumbe Wake sawa. {ABN1: 79.1}

Hivyo “watu watakatifu wa Mungu walinena wakiongozwa na Roho Mtakatifu.” 2 Pet. 1:21. Likielezwa kwa muhtasari mfupi, neno Mjumbe wa Agano humaanisha Roho Mtakatifu (Kristo asiyeonekana) ndani ya mwakilishi anayeonekana wa Mbingu — awe ni Musa, Yohana, Kristo, Eliya, au mtu mwingine yeyote. {ABN1: 79.2}

JE! LIPO HITAJI LA “MAFUTA YA ZIADA”?

Swali Namba 8:

Nimeambiwa kwamba mahali fulani katika maandishi yake, Dada White alisema: “Tunayo nuru yote ambayo tunahitaji hadi Yesu atakapokuja.” Je! Unaweza kutoa dondoo? {ABN1: 79.3}

Jibu:

Tunajua hakuna taarifa kama hiyo. Isitoshe, tamshi lolote kama hilo litakuwa kinyume kabisa na kila jambo Dada White ameandika kwa mada hii, kama inavyoonekana haraka kutoka kwa mbili tu za shuhuda zake kwa jambo hili: {ABN1: 79.4}

79

“Nimeulizwa swali, ‘Je! Unafikiri kwamba Bwana anayo nuru nyingine zaidi kwetu kama watu?” Najibu kwamba Yeye anayo nuru ambayo ni mpya kwetu, na bado ni nuru yenye thamani ya zamani ambayo itaangaza kutoka kwa Neno la ukweli. Tunavyo tu vimulimuli vya mishale ya nuru ambayo bado haijakuja kwetu. Hatuitumii zaidi nuru ambayo Bwana ametupatia tayari, na hivyo tunashindwa kupokea nuru iliyoongezeka; hatutembei katika nuru ambayo tayari imeangazwa juu yetu.” — Mapitio na Kutangaza, Juni 3, 1890. {ABN1: 80.1}

“Sote tunapaswa kujua nini kinachofundishwa kati yetu; kwa maana iwapo ni ukweli, tunauhitaji…. Haijalishi ni kupitia kwa nani nuru imetumwa, tunapaswa kufungua mioyo yetu kuipokea katika unyenyekevu wa Kristo…. O, tutende kama watu wanaotaka nuru! “Bwana hutuma nuru kwetu kuhakiki sisi ni wenye roho ya namna gani. Hatupaswi kujidanganya.” “Hatupaswi kwa nukta kufikiri kwamba hakuna nuru zaidi, hakuna ukweli zaidi, utakaopeanwa kwetu.” — Watendakazi wa Injili, uk. 301, 302, 310. {ABN1: 80.2}

Ni wazi, kwa hivyo, hapawezi kuwapo hata kidokezi katika maandishi ya Dada White kwamba tayari tunayo Kweli yote na hatuhitaji chochote zaidi. Lakini ipo ndani ya Biblia angalau mitazamo-kimbele miwili ya watu ambao hufikiri ki-makosa hawana hitaji la chochote zaidi: (1) wanawali watano wapumbavu, ambao hufikiri mafuta ndani ya taa

80

zao yanatosha kuwapa nuru angavu hadi katika Ufalme, lakini ambao, wakiwa wamekosea, wanashindwa kufikia lengo lao (Tazama Mathayo 25:1-13); (2) Walaodekia, wanaofikiri hawana hitaji la chochote, ingawa Bwana husema wanahitaji kila kitu, na ambao hivyo hujihukumia maangamizi watapikwe kutoka katika kinywa Chake. (Tazama Ufunuo 3:14-18.) {ABN1: 80.3}

Mtu yeyote ambaye huendelea juu ya dhana kwamba Dada White amesema, “Tunayo nuru yote ambayo tunahitaji hadi Yesu aje,” ni, isipokuwa aisalimishe dhana hiyo upesi, kujihukumu kwa hatima ya aidha mwanamwali mpumbavu au Mlaodekia asiyetubu. {ABN1: 81.1}

MVUA YA MASIKA — LINI?

Swali Namba 9:

“Maandishi ya Awali,” uk. 15, hunena kuhusu Mungu kutangaza siku na saa ya kuja kwa Yesu, na kuwamiminia watakatifu Roho Mtakatifu. Je! Haya yote hayatukii kwa wakati wa mapigo saba ya mwisho, kabla tu ya Ujio wa pili? Iwapo ni hivyo, basi hayaonyeshi kwamba “mvua ya masika” itamiminwa kwa watu wa Mungu baada ya kufungwa muda wa rehema? {ABN1: 81.2}

Jibu:

Kweli, tunaelewa kutoka kwa kifungu kinachozungumziwa kwamba kuelekea mwishoni mwa pigo la saba, Mungu atatangaza siku na saa ya kuja kwa Kristo, na ya kwamba wakati huo Yeye atamimina Roho Wake kwa watakatifu Wake. Hata hivyo, hatuelewi kwamba huu umiminwaji utakuwa aidha “ya masika”

81

au “mvua ya vuli” ya ukweli, au bado ni nguvu iliyotabiriwa katika Yoeli 2:23, 28, ila badala yake ni udhihirisho wa mwisho wa Roho wa Mungu sio kutufunulia Ukweli zaidi wa Injili, au kutuwezesha kuutangaza kikamilifu kabisa, lakini tu kutubatiza tuweze kufaa kumwona Yesu uso kwa uso, “jinsi Yeye alivyo.” {ABN1: 81.3}

JE! KILIO KIKUU KIMEANZA?

Swali Namba 10:

Dada White aliandika mnamo 1892 kwamba Kilio Kikuu cha Ujumbe wa Malaika wa Tatu kilikuwa tayari kimeanza; tafadhali eleza mbona wengine hudai kwamba bado ni cha baadaye. Na nini hukifanya kiweze kuwa”kikuu”? {ABN1: 82.1}

Jibu:

Lazima iwepo alama ya kutofautisha kati ya sauti ya ujumbe kabla ya Kilio Kikuu, na sauti ya ujumbe katika Kilio Kikuu; vinginevyo hakingeitwa “kikuu.” {ABN1: 82.2}

Ujumbe unaumuka hadi kwa Kilio Kikuu kwa msingi wa “nyongeza” ambayo huupatia “uwezo na nguvu” — Maandishi ya Awali, uk. 277. Hitimisho la pekee linaloweza kukubaliwa, kwa hivyo, ni kwamba kwa sababu kanisa kamwe halijaupokea ujumbe wa nyongeza, na kwa sababu haujawahi kuja mmoja (mwingine tofauti na ule katika machapisho ya Fimbo ya Mchungaji) ambao ungeweza kupeana “uwezo na nguvu” kwa ujumbe wa zamani, Kilio Kikuu hakikuweza kuanza wakati wowote uliopita kwa huu. {ABN1: 82.3}

82

Isitoshe, “machukizo” kanisani hayajazuilia Kilio Kikuu tu lakini pia yamekizimisha kilio hafifu ambacho hutangulia. Hakika, “malaika wa kanisa la Walaodekia,” akiwa hafai hata kukamilisha kuutangaza ujumbe huo katika kilio chake hafifu, lazima hafai kabisa kuutangaza katika Kilio Kikuu. Ni wazi, iwapo sasa hawezi kutubu upesi na kuupokea ujumbe wa nyongeza ambao utaanzisha Kilio Kikuu, basi sio tu kwamba hatasaidia kuutangaza bali hata “atatapikwa nje.” {ABN1: 83.1}

“… wale tu ambao wameyastahimili majaribu katika nguvu za Yule mwenye Uwezo,” huonya Roho ya Unabii, “wataruhusiwa kushiriki katika kuutangaza [Ujumbe wa Malaika Watatu] wakati utakapokuwa umeumuka na kuingia katika kilio kikuu.” — Mapitio na Kutangaza, Novemba 19, 1908. {ABN1: 83.2}

Kwa hivyo wakati kilio hafifu kinatangazwa na wale ambao, wameshinda, na vile vile na wale ambao hawajashinda majaribu, Kilio Kikuu kitatangazwa tu na wale wameshinda. {ABN1: 83.3}

Ingawa Kilio Kikuu kingalikuwa kilianza mwaka 1892, kilizimwa wakati kanisa liliukataa ujumbe wa Haki kwa Imani mwaka 1888. Hivyo, kile chuo ambacho kilikuwa na ujumbe wa “nyongeza” ambao ungepeana “uwezo na nguvu” kwa Ujumbe wa Malaika wa Tatu, kwa wakati huo kilikoma kukunjua. Na kwa sababu hiyo, badala yake

83

kuwa nuru ya ulimwengu, kanisa lenyewe likaingia gizani. Kuona hili, Roho wa Kweli alifanya tangazo la kutisha la angamizo kwa Walaodekia wasiotubu, ilhali akitoa ahadi ya furaha ya utukufu wa baadaye kwa wote watakao amka na kutembea katika nuru inayotokea kwenye kiti cha enzi. {ABN1: 83.4}

“Je! atawezaje yeyote wa ndugu zetu kujua wakati nuru hii itawajia watu wa Mungu?” lilikuwa swali la kufagilia wakati huo lililoulizwa na Uvuvio. Na jibu lililovuviwa lilikuwa: “Hata sasa hakika hatujaiona nuru ambayo inajibu maelezo haya. Mungu anayo nuru kwa watu Wake, na wote watakaoipokea watauona uovu wa kukaa katika hali ya uvuguvugu.” — Mapitio na Kutangaza, Aprili 1, 1890. {ABN1: 84.1}

“Katika udhihirisho wa nguvu ambayo itaangaza nchi kwa utukufu wake, watakiona tu kitu ambacho katika upofu wao watafikiri ni hatari, kitu ambacho kitaziamsha hofu zao na watajikaza kuupinga. Kwa sababu Bwana hafanyi kazi kulingana na matarajio na mawazo yao, wataipinga kazi. Mbona, wanasema, hatupaswi kumjua Roho wa Mungu, wakati ambapo tumekuwa kazini kwa miaka mingi sana?” — Shule ya Mafunzo ya Biblia, 1907. (Imechapishwa tena katika Mapitio na Kutangaza, Novemba 7, 1918.) Taarifa hii huonyesha wazi Kilio Kikuu katika siku za baadaye kutoka mwaka 1918. {ABN1: 84.2}

84

“Upendo wa Kristo, upendo wa ndugu zetu, utashuhudia kwa ulimwengu kwamba tumekuwa na Yesu na tumejifunza Kwake. Wakati huo ujumbe wa malaika wa tatu utaumuka hadi kwa kilio kikuu, na nchi yote itaangazwa kwa utukufu wa Bwana.” — Shuhuda, Gombo la 6, uk. 401. {ABN1: 85.1}

JE! MVUA YA VULI NI NGUVU YA PENTEKOSTE?

Swali Namba 11:

“Fimbo ya Mchungaji” husema kwamba mvua ya vuli ni Roho ya Unabii, na kwamba mvua ya masika ni ujumbe unaohusiana kwa karibu kabla ya Pentekoste, au “mwalimu wa haki,” ambao kanisa sasa linapokea, na kwamba “nguvu” ya Pentekoste bado ni jambo lingine. Lakini “Tumaini la Vizazi Vyote” husema kwamba “mvua ya vuli” ilikuwa “kumiminwa kwa Roho katika siku za mitume,” na “mvua ya masika,” umiminwaji wa Pentekoste yenyewe, utatukia katika siku za mwisho. Je! Ni lipi la kuamini? {ABN1: 85.2}

Jibu:

Vitabu vyote vinajaribu kusema yale ambayo Biblia husema, na ili kuleta upatano lazima tujifunze tena mada hiyo moja kutoka kwa moja Biblia, haswa kutoka kwa unabii wa Yoeli: “Furahini, basi, enyi wana wa Zayuni, mkamfurahie Bwana, Mungu wenu; kwa kuwa Yeye amewapa ninyi mvua ya masika, kwa kipimo cha haki, Naye atawezesha ishuke kwenu mvua, mvua ya masika, na mvua ya vuli, katika mwezi wa kwanza. Yoeli 2:23. {ABN1: 85.3}

85

Hakuna mtu anayepaswa kushindwa kuona kwamba unabii wa Yoeli unahitaji kutimizwa maradufu. Ingawa wale ambao wameahidiwa mvua ya masika, wanaambiwa kwamba tayari wamepewa mvua ya vuli, wakati mvua ya masika inanyesha juu yao, huleta pamoja nayo mvua ya vuli, zote zikija juu yao katika mwezi wa kwanza. Maana ya pambizo kwa mvua huiita “mwalimu wa haki.” Sasa, iwapo mvua ya vuli inarudia na kunyesha tena na mvua ya masika katika mwezi uo huo, basi ukweli unasimama wazi kwamba mvua ya vuli katika siku za mitume ndio ile ambayo Tumaini la Vizazi Vyote huzungumzia, na kwamba mvua ya vuli ambayo hunyesha katika mwezi wa mvua ya masika, ndio ambayo Fimbo huzungumzia. {ABN1: 86.1}

Katika ufalme wa maumbile, mvua ya vuli hupasua na kuotesha mbegu na mvua ya masika hulileta jani katika ukuaji kamili. Hivyo katika ufalme wa kiroho, “mvua ya vuli” lazima imaanishe ujumbe uliotumwa kutoka mbinguni kuotesha mbegu ya kiroho, na “mvua ya masika,” ujumbe uliofuata wa kukomaza nafaka kwa mavuno ya kiroho. Hivyo katika kumleta mpokeaji kwa ukomavu kamili wa haki, mvua ya vuli na ya masika huwakilisha walimu wawili wa haki. Katika matumizi kamili, kwa hivyo zile mvua mbili za siku za mwisho sio tu kumiminwa kwa wa kwanza ukweli kabla ya Pentekoste, mafundisho ya Kristo katika siku Yake, mfano, lakini pia ni umiminwaji wa kwanza wa ukweli wa mwisho kabla ya Pentekoste,

86

Ukweli uliostawi katika siku yetu, uakisi. Kwanza lazima uwepo ufunuo wa ukweli wa Pentekoste kabla iweze kutolewa nguvu ya Pentekoste kuutangaza: “Hata itakuwa baada ya hayo [baada ya mvua ya vuli na ya masika],” asema Yeye Ajuaye yote, “kwamba nitamimina Roho Yangu juu ya wote wenye mwili.” Yoeli 2:28. {ABN1: 86.2}

Kwa hivyo, udhihirisho huu mara mbili wa Roho Mtakatifu huonekana kuwa hautengani. Wa kwanza huwaendeleza watu kwa kuwafundisha katika haki; wa pili huwakomaza kikamilifu, na kuwavika nguvu ya kuutangaza ukweli katika haki. Kwa matokeo, anapeanwa katika awamu ya kwanza ya kazi “mwalimu wa haki” ambaye hulifunza jeshi la walimu wadogo wa haki kwa ajili ya kuitekeleza awamu ya pili. {ABN1: 87.1}

Kwa sababu ungeweza kuwapo ufunuo wa ukweli katika wakati wa mitume,’ wa Dada White, na katika siku yetu Tumaini la Vizazi Vyote ni sahihi kwa kusema kwamba, kwa wakati huo (kilipoandikwa), mvua ya vuli ilikuwa ni “mvua” ya ukweli katika siku ya mitume. Lakini kama ilivyo leo mvua ya vuli sio tu ukweli wa siku za mitume lakini pia ule wa siku ya Dada White, Fimbo i sahihi kwa kusema kwamba maandishi yake ni “mvua ya vuli” leo, na ya kwamba mvua ya masika, jinsi Yoeli huonyesha, hutumika moja kwa moja kwa ujumbe wa mwisho — ujumbe wa leo (Yoeli 2:23). Hivyo tu (mvua ya vuli ikiwa ni maandishi ya Dada White, na “mvua ya masika” ikiwa ni

87

Fimbo) mvua ya vuli na ya masika zinaweza kunyesha kwa wakati mmoja, kama inavyotakikana na Yoeli 2:23 Na nguvu ya Roho, ikiwa andamo kwa mvua ya vuli na ya masika, kwa hivyo bado ni ya baadaye. {ABN1: 87.2}

UNAPOHITAJI UKWELI, MBONA UOMBE NGUVU?

Swali Namba 12:

Kuambiwa waombe kwa ajili ya umiminwaji wa Roho Mtakatifu, maelfu kwa maelfu wamefanya hivyo kwa bidii, lakini bila kufanikiwa. Kwa nini? {ABN1: 88.1}

Jibu:

Mara kwa mara Mavuguvugu mengi yenye bidii ya kibinafsi na ya makundi ya Kikristo yamezindua maombi ya kusisimua ya masafa marefu katika juhudi walioamua, ya uvumilivu ili kuleta utimizo wa kumiminwa kwa ahadi ya Roho Mtakatifu, hata “mvua ya masika.” Kwa sababu, ingawa, juhudi hizi za misimu zimemalizikia siku zote katika huzuni, kuvunjika moyo na kufadhaika, maelfu ya nafsi zimekanganyikiwa na kupumbazika akili, zimeacha imani yao kabisa, na labda kuzama katika ukafiri. {ABN1: 88.2}

Bado hakuna mwanafunzi wa Maandiko atakayekataa kwamba Biblia hakika hutangaza ahadi ya mmoja udhihirisho wa nguvu ya Roho Mtakatifu, kukabithiwa waamini wote umiminwaji maalum wa nguvu kama ile mitume walipokea siku ya Pentekoste, — naam, hata kubwa zaidi. {ABN1: 88.3}

88

Basi jibu kwa swali, Mbona sasa hatuipokei ile Nguvu? Bila shaka ni, Kwa sababu matakwa ya kuipokea bado hayajaafikiwa. Wakati yanapotimizwa ahadi hii hakika ya Mungu itatimizwa mara moja, kama ilivyokuwa hata kwa mitume. {ABN1: 89.1}

Kwa hivyo, chochote sasa kinachomzuia Mkristo kutoipokea zawadi hii kuu ya zawadi zote, kizuizi lazima ki kwake na sio kwa Mungu. {ABN1: 89.2}

Ipo ahadi ya Mfariji, Roho wa Kweli (Yohana 16:7-13), na ahadi ya “mvua ya masika” Yoeli 2:23, 28. Mfariji huyu aliyeahidiwa, mitume walimpokea siku ya Pentekoste, na Angekaa pamoja nao milele; yaani, hata na warithi wao. Lakini ilivyokuwa katika urithi wa mitume, watu wa maadili ya kwanza ya mitume walikoma, polepole Msaidizi akatoweka. Na ingawa kwa nyakati tofauti Amejitokeza tena katika umbo la Roho wa Kweli, nguvu na uwepo Wake wa Pentekoste tangu wakati huo haujawahi kutolewa tena. Udhihirisho huu wa Roho katika Nguvu (Yoeli 2:28), unapaswa, hata hivyo kutofautishwa na udhihirisho wa Roho katika Kweli (Yoeli 2:23) {ABN1: 89.3}

Haswa jina, “mvua ya masika,” lenyewe huonyesha kwamba udhihirisho huu hasa unatukia katika “siku za mwisho” — wakati wetu. Na kupitia Zekaria nabii, Uvuvio unaonyesha kwamba kuna wakati uliowekwa

89

kwa ajili ya mvua ya masika, unahimiza: “Mwombeni Bwana mvua wakati wa masika; naam Bwana afanyaye umeme, Naye atawapa manyunyu ya mvua, kwa kila unyasi kondeni.” Zek. 10:1. {ABN1: 89.4}

Kifungu kinachohusiana na Yoeli 2:23, maana ya pambizo, huweka wazi kwamba “mvua ya masika,” ujumbe wa mwisho, ni “mwalimu wa haki,” ukimletea mpokeaji maarifa kamili ya Ukweli, haki. Kwa hivyo wakati Wakristo kwa udharura wameombwa sana kuomba na kuugua kwa ajili ya Roho wa Kweli nyakati zote, wanaagizwa kwa udharura zaidi kuomba kwa ajili yake sasa! {ABN1: 90.1}

Kama ilivyo katika hali asili ya mambo, mvua ya masika haiji tu kufanya ngano ikue lakini pia huleta ukomavu kamili, hivyo, kwa ulinganifu wa kiroho, huyu Mwalimu wa Haki lazima awalete watakatifu kwa kimo kamili cha watu ndani ya Kristo Yesu (Efe. 4:13) — kuwafanya wastahili kwa Ufalme. {ABN1: 90.2}

Lakini awamu ya pili, ile nguvu iliyoahidiwa (Yoeli 2:28) ambayo itakuja “baadaye,” baada ya “mvua ya masika,” ndio ambayo Wakristo wengi huomba bila kuzingatia kwamba ipo awamu ya kwanza (Yoeli 2:23) — “mwalimu wa haki,” umiminwaji wa mwisho wa Ukweli wa Sasa ambao lazima upatikane kabla umiminwaji wa mwisho wa nguvu uweze kutekelezwa. {ABN1: 90.3}

Ni dhahiri kwamba sehemu ambayo huja “baadaye,” nguvu ya Pentekoste, huja

90

kumwezesha mpokeaji kuutangaza ukweli wa mwisho; na nguvu hii haitakuja mpaka kanisa kama kundi “kila unyasi kondeni” (Zek. 10:1), sio kundi hapa na kundi huko, kwa furaha limefyonza kwa ajili ya ukuaji wake wa kiroho mvua yote ambayo Mwalimu wa Haki, ambaye sasa amekuja, ameileta. {ABN1: 90.4}

Lakini swali kuu hapa linalotukabili ni: Je! Ni lini “kila unyasi” kila mshiriki wa kanisa ataupokea Ukweli na nguvu hii ya utukufu? Je! Mtakatifu na mnafiki watashiriki sawa? Uvuvio unajibu: {ABN1: 91.1}

“Kwa moto na kwa upanga Wake Bwana atateta na wote wenye mwili: nao watakaouawa na Bwana watakuwa wengi…. Nami nitawatuma hao waliookoka kwa mataifa…. Nao watautangaza utukufu Wangu katika mataifa. Nao watawataleta ndugu zenu…. mpaka kwa Mlima Wangu mtakatifu Yerusalemu, asema Bwana, kama vile wana wa Israeli waletavyo sadaka yao katika chombo safi nyumbani mwa Bwana.” Isa. 66:16, 19, 20. {ABN1: 91.2}

Kwa hivyo, katika wakati kati ya “mvua ya masika” ya ukweli na “kumiminwa” kwa nguvu ya Roho, watatiwa muhuri idadi ya waliowekwa wakfu ambao wataokoka kutoka kati ya “waliouawa na Bwana.” Kwa maneno mengine, kwa mavuno ya malimbuko, wakati wadhambi wote wametupwa nje ya kanisa, na wenye haki kuachwa peke yao kama walivyokuwa wanafunzi 120 katika chumba cha juu, basi na

91

wakati huo tu ndipo Bwana anaweza hatimaye kuimimina nguvu ya Roho Wake kwa wote, ili wote (wote “waliokoka” watatabiri, waote ndoto, na kuona maono. {ABN1: 91.3}

“Tena itakuwa ya kwamba yeye aliyebaki katika Zayuni, na yeye aliyeachwa ndani ya Yerusalemu, ataitwa mtakatifu; yaani, kila mmoja aliyeandikwa miongoni mwa hao walio hai ndani ya Yerusalemu; hapo Bwana atakapokuwa ameuosha uchafu wa hao binti za Zayuni na kuisafisha damu ya Yerusalemu kati yake, kwa roho ya hukumu na kwa roho ya kuteketeza. Tena juu ya makao yote ya mlima Zayuni, na juu ya makusanyiko yake, Bwana ataumba wingu na moshi wakati wa mchana, na mwangaza wa miali ya moto wakati wa usiku; kwa maana juu ya utukufu wote itatandazwa sitara. Kisha kutakuwa na hema kuwa uvuli wakati wa mchana kwa sababu ya hari, na kuwa mahali pa kukimbilia na kujificha wakati wa tufani na mvua.” Isa. 4:3-6. {ABN1: 92.1}

Ni baada tu ya utakaso huu mkuu kanisani (ulioelezewa pia katika sura ya tisa ya Ezekieli) ndiposa masalia watawezeshwa kupeleka yenye mwangaza kamili, kurunzi ya Ukweli kwa ulimwengu wote wa Mataifa. Kutoka Zayuni wakati huo itatokea sheria, na neno la Bwana kutoka Yerusalemu. Kazi wakati huo itakamilika, “itafupishwa katika haki,” na Bwana ataonekana kwa utukufu — kila jicho likimwona. (Ufu. 1:7). {ABN1: 92.2}

92

MIAKA AROBAINI BILA KUJAZA TENA?

Swali Namba 13:

Inawezekanaje kuwa kweli kwamba hakuna ukweli endelevu uliotolewa kwa kanisa katika kipindi cha miaka arobaini kutoka mwaka 1890 hadi 1930, wakati maandishi mengi ya Dada White yalichapishwa kutoka mwaka 1890 hadi 1915? {ABN1: 93.1}

Jibu:

Ingawa maandishi mengi ya Dada White yalichapishwa katika kipindi kilichotajwa hapo juu, bado uchunguzi makini utafunua kwamba iwapo ufunuo wowote mpya wa ukweli mwafaka wa Biblia, “chakula kwa wakati wake,” ulichapishwa ndani ya hicho kipindi, ulifunuliwa kwake kabla ya mwaka 1890. Kwa kweli, mapema tangu mwaka 1871, yeye mwenyewe alitangaza kukoma kwa nuru kupitia Shuhuda: “Nimeagizwa kutoka kwa Mungu kukwaambia kwamba hakuna mshale mwingine wa nuru kupitia Shuhuda utaangaza kwenye njia yako, mpaka utakapoweka kwa matumizi ya vitendo nuru ambayo umepewa tayari.” — Shuhuda, Gombo la 2, uk. 606. {ABN1: 93.2}

Kwa hivyo Shuhuda zozote alizoandika kati ya tarehe zinazozungumziwa (1890 na 1915) hazikuwa dhahiri za kuufunua ukweli mwafaka wa Biblia, lakini kimsingi kutoa ushauri, himizo, kemeo, na maagizo katika haki kwa jaribio la kuwaokoa Walaodekia wasitapikwe nje. Maandishi yake mengine yoyote yaliyosalia, katika nyanja zake za kinabii, yalikuwa siri hadi miaka

93

arobaini ilipomalizikia kwa kuwasili Fimbo la Mchungaji. {ABN1: 93.3}

Kwa muda mrefu bila mafuta ya kiroho, chombo cha kanisa kilicho na Ukweli kilihitaji kujazwa mafuta mapya, ili nuru yake iweze kuangazia njia yake yote kuelekea katika Ufalme, lisije likaanguka kutoka kwenye njia iliyosonga na nyembamba mwishoni kabisa mwa safari yake refu. Hivyo katika upendo Wake mkuu na rehema, Bwana ametuma Fimbo ya Mchungaji kukusanya na kutumia kivitendo nuru ambayo imetolewa tayari. Kwa hivyo, sasa, anaamuru Bwana, “Isikieni hiyo Fimbo, na Yeye Aliyeiagiza?” Mika 6:9. {ABN1: 94.1}

JE, FIMBO YA MCHUNGAJI HUWEKA TAREHE ZA KINABII?

Swali Namba 14:

Katika taarifa ifuatayo, “Wakati Mungu anaisafisha njia kwa ajili ya mapigo saba ya mwisho kwa kuwalaza baadhi ya watu Wake kaburini, Amefanya vivyo hivyo kwa tukio litakalotukia mwaka 1931 (ikiwa tarehe hiyo itakuwa sahihi),” Je! “Fimbo ya Mchungaji,” Gombo la 1, uk. 219, inamaanisha kufundisha kwamba hukumu ya wafu ilifungwa mnamo 1931 au karibu nao? {ABN1: 94.2}

Jibu:

Katika taarifa inayohojiwa, Fimbo haina dondoo kwa Hukumu ya Upelelezi. Ujumbe hauweki tarehe, ama kamili au ya makisio, kwa ajili ya kufungwa kwa hukumu ya wafu, au kwa mwanzo wa Hukumu ya walio hai. Wakati wa kukoma kwa tukio moja na mwanzo

94

wa lingine, hauwezi kujulikana hadi moja limepita na lingine liwe limeanza. {ABN1: 94.3}

Kuhusu tarehe na tukio linalounganishwa na mwaka 1931, hatuna nuru zaidi kwa wakati huu kuliko unayopatikana katika Fimbo ya Mchungaji, Gombo la 1, uk. 108-114, na Gombo la 2, uk. 275. Ilikuwa mwishoni mwa 1930 na mwanzoni mwa 1931 ya kwamba uchapishaji wa ujumbe katika Fimbo ulifanyika, ukifunua ukweli wa watu 144,000 ukiitisha matengenezo. Kwa hivyo, ijapokuwa haikueleweka mbeleni ingekuwaje asili ya tukio hilo, lakini utimilifu wa wakati ulipokuja na hakuna tukio lingine lilitokea ila hili, hivyo basi lilitambuliwa kwamba ni lile lililotabiriwa katika Ezekieli 4 kuhusiana na mwisho wa miaka 430 ya unabii wakati “chuo” kilikuwa kikunjue zamu nyingine. {ABN1: 95.1}

(Italiki zote ni zetu.)

======

HATUA YAKO ITAKAYOFUATA ITAKUWA NINI?

Sasa ikiwa umefurahia, umethamini, na kufaidika na safari hii ya maswali na majibu kupitia Kitabu Namba 1, na iwapo unatumaini kuendelea, basi tuma ombi kwa Kitabu Namba 2. Kitatumwa kama utumishi wa Kikristo bila malipo au wajibu. {ABN1: 95.2}

95

FAHARISI YA MAANDIKO

>