15 Jul Gombo la 2 Salamu Mwafaka Namba 45, 46
Gombo la 2 Salamu Mwafaka Namba 45, 46
AMANI YA PEKEE YA MAWAZO
Hati miliki, Kimechapishwa tena 1950
Haki zote zimehifadhiwa
V. T. HOUTEFF
UKRISTO NI NINI? NI NANI ANAWEZA KUUSHIKA? NA NI NANI ANAWEZA KUUKOSA?
ZAWADI YA MIUJIZA HASWA KUPONYA NA KUNENA KWA LUGHA — LINI, VIPI, NANI?
1
ANDIKO LA SALA
Imani Na Sala
“Kupitia imani katika Kristo, kila upungufu wa tabia unaweza kujazwa, kila unajisi kusafishwa, kila kosa ku-rekebishwa, kila ubora kustawishwa. {2TG45: 2.1}
‘Ninyi mmekamilika ndani Yake.’ {2TG45: 2.2}
“Sala na imani imeungana kwa karibu, na inahitaji kujifunza pamoja. Katika sala ya imani ipo sayansi ya kiun-gu; ni sayansi ambayo kila mmoja atakayeweza kuyafanya kazi ya maisha yake kufanikiwa lazima aelewe. Kristo anasema, ‘Yoyote myaombayo, mkisali, aminini ya kwamba mnayapokea, nayo yatakuwa yenu.’ Yeye anaweka wazi kwamba kuomba kwetu lazima kulingane na mapenzi ya Mungu; lazima tuombe mambo ambayo Yeye ameahidi, na chochote tunachopokea lazima kitumike katika kutenda mapenzi Yake. Matakwa yakitimizwa, ahadi ni dhahiri. {2TG45: 2.3}
“Kwa msamaha wa dhambi, kwa Roho Mtakatifu, kwa tabia kama ya Kristo kwa hekima na nguvu ya kufan-ya kazi Yake, kwa zawadi yoyote ambayo Yeye ameahidi, tunaweza kuomba; kisha tuamini kwamba tunapokea, na kurudisha shukrani kwa Mungu ya kwamba tumepokea. {2TG45: 2.4}
“Tusihitaji kutafuta ushahidi wa nje wa ile baraka. Zawadi i katika ahadi, na tunaweza kufanya kazi yetu tukiwa na hakika kwamba lile ambalo Mungu ameahidi anaweza kulitekeleza, na ya kwamba zawadi hiyo, am-bayo tayari tunamiliki, itatambulika tunapoihitaji sana.” — Elimu, uk. 257, 258. {2TG45: 2.5}
2
UKRISTO NI NINI? NI NANI ANAWEZA KUUSHIKA? NA NI NANI ANAWEZA KUUKOSA?
ANDIKO LA HOTUBA NA V. T. HOUTEFF
MCHUNGAJI WA WADAUDI WAADVENTISTA WA SABATO
SABATO, MACHI 25, 1950
HEKALU LA MLIMA KARMELI
WACO, TEXAS
Ukristo wa kweli ni ukuaji. Ni kama mmea. Kristo Mwenyewe amewakilishwa kama Chipukizi (Isa. 11:1), na ufalme Wake kama mbegu ya haradali (Mat. 13:31, 32) ambayo baada ya kupandwa huwa mti, mkubwa wa aina yake. Lakini kwa sababu mti halisi lazima ujilishe chakula cha asili, vivyo hivyo mti wa kiroho lazima kwa hitaji ulijishe chakula cha kiroho, kwacho kama vile Chipukizi Lenyewe lilivyojilisha: {2TG45: 3.1}
“Kwa hiyo Bwana Mwenyewe atawapa ishara; Tazama, bikira atachukua mimba atazaa mtoto mwanamume, naye atamwita jina Lake Imanueli. Siagi na asali atakula, ili aweze kuyakataa mabaya na kuyachagua mema.” Isa. 7:14, 15. {2TG45: 3.2}
Hakika sote hukubali kwamba kifungu hiki cha Andiko ni utabiri wa Imanueli wa Mathayo 1:23 — Kristo katika ujio Wake wa kwanza. Ukweli, hata hivyo, kwamba Kristo alikula kila aina ya chakula halali, na hata alishtumiwa kuwa “mtu mlafi, na mnywaji wa divai” (Luka 7:34), alaye na “watoza ushuru na wenye dhambi” (Marko 2:16), hufanya uwe wazi kabisa kwamba lishe hii ya “siagi na
3
asali” si halisi. Isitoshe, ukweli kwamba siagi na asali havina uwezo wowote wa kumjaza mtu hekima na nia ya kuchagua wema na kuukataa uovu, la, si zaidi ya zifanyavyo bidhaa zingine za chakula, huonyesha kabisa kwamba hii “siagi na asali” ni mfano wa kitu maalum, kama vile nzi na nyuki wa Isaya 7:18 ni mfano wa Misri na Ashuru. Na ni nini kingine kinaweza kuwa ila chakula cha kiroho, aina ambayo hujenga tabia ya maadili, am-bayo humfanya mmoja “kuukataa uovu, na kuchagua wema?” Na ni kwa chanzo kipi kingine chakula kama hiki kingekuja isipokuwa Maandiko? Na nini kingine, isitoshe, asali ingeweza kuwakilisha ila Roho mwema wa Mungu ambaye hubariki kujifunza kwa uaminifu kwa kila mtu na imani sahili katika Neno? {2TG45: 3.3}
Ni dhahiri, kwa hivyo, nembo hii ya siagi na asali bila kukosea hutuambia kwamba Imanueli, Kristo, ali-wezeshwa kutambua na kushinda dhambi kwa usomaji Wake wa Biblia — kwa kumeng’enya yaliyomo Yake na kuyaruhusu kuwa sehemu Yake. Hii ilikuwa furaha Yake njema, jinsi asali ya mfano inavyofunua. Ndivyo il-ivyokuwa kwamba “Akawaambia, Mimi ninacho chakula msichokijua ninyi” (Yohana 4:32), na, “Imeandikwa, Mtu hataishi kwa mkate tu, ila kwa kila neno litokalo katika kinywa cha Mungu.” Mat. 4:4. {2TG45: 4.1}
Basi, ukweli ni dhahiri kwamba Ukristo ni mmea wa kiroho, unaojilisha Neno la Mungu jinsi unavyofunuliwa na Roho mwema wa Kweli. Kwa hivyo iwapo Kristo, Mfano wetu kwa njia hiyo “akazidi kuendelea katika hekima …, akimpendeza Mungu na wanadamu” (Luka 2:52), basi ni muhimu zaidi kwamba sisi, wafuasi Wake, tuishi kwa Neno lilo hilo, siagi na asali ile ile, ikiwa tutaweza kumiliki Ukristo wa kweli, unaodumisha uhai, na unaohifadhi maisha. Hakika tunaambiwa kikamilifu hivyo katika
4
aya zifuatazo za unabii wa Isaya: {2TG45: 4.2}
“Katika siku hiyo itakuwa kwamba, mtu atalisha ng’ombe mke mchanga, na kondoo wawili; kisha itakuwa kwa sababu wanyama hao watatoa maziwa mengi kwamba atakula siagi: kwa maana siagi na asali atakula kila mtu atakayesalia katika nchi.” Isa. 7:21, 22. {2TG45: 5.1}
Katika aya hizi Uvuvio unaelekeza umakini wetu kwa viumbe vitatu vinavyozalisha siagi — kondoo wawili na ng’ombe mke mchanga, na unaonya kimbele kwamba wale tu wanaokula bidhaa zao watakuwa na haki ya kuishi katika “nchi” — katika nchi ya watu wa Mungu. Hakuna wengine, la, si mwingine, atakuwa hapo. {2TG45: 5.2}
Kwa kuwa, kwa hivyo, ni wale tu ambao hula ile siagi, wale ambao kwa hivyo hujifunza kuukataa uovu na kuuchagua wema, wataruhusiwa kuishi katika nchi takatifu, yote yaliyodhahiri zaidi ni kwamba ile siagi ni mfa-no wa chakula cha kiroho. Na kwa sababu chanzo chake cha usambazaji ni kondoo wawili na ng’ombe mke mchanga, ni muhimu sana kwamba tuchunguze katika milki ya nembo hii ya Biblia kupata wao ni nini. {2TG45: 5.3}
Kondoo hao wawili, wa aina moja na si wachanga, kwa udhahiri ni nembo ya Maagano ya Kale na Jipya, Ne-no, ambalo huwezesha wapokeaji wake “kuchagua mema na kukataa mabaya.” Na yule ng’ombe akiwa mchanga, na kwa hivyo wa chimbuko la baadaye kuliko kondoo, na pia akiwa wa kimo kikubwa kuliko wao, kwa hivyo anaweza kuwa mfano wa maandishi yaliyovuviwa ya chimbuko la baadaye na ya kiasi kikubwa kuliko Biblia Yenyewe. Kama hayo tu kando na Biblia ni yale yanayotuletea “ushuhuda wa Yesu:…. kwa maana ushuhuda wa Yesu ndio Roho ya Unabii” (Ufu. 19:10) — ufasiri iliovuviwa wa Maandiko.
5
Ikumbukwe pia kwamba hii siagi na hii asali huzalishwa katika enzi ya Ukristo, katika wakati ambao kondoo wote wawili, Maagano yote, yako hai, na pia katika wakati ambapo Roho ya Unabii i kazini. {2TG45: 5.4}
Na Roho ya unabii ni nini? — Sura na aya iyo hiyo inatoa jibu: {2TG45: 6.1}
“Nami nikaanguka mbele ya miguu yake” [miguuni pa yule aliyemfunulia Yohana unabii] “ili nimsujudie. Akaniambia, Usiifanye hivi; mimi ni mjoli wako na wa ndugu zako walio na ushuhuda wa Yesu. Msujudie Mungu, kwa maana ushuhuda wa Yesu ndio roho ya unabii.” Ufu. 19:10. {2TG45: 6.2}
Hapa inaonekana kwamba wakati unabii huo ulifunuliwa kwa Yohana na mmoja wa ndugu zake, hivyo basi ulifunuliwa kwake Ushuhuda wa Yesu, Roho ya Unabii. Kichele, basi, mtumwa aliyevuviwa wa Mungu ambaye huleta ujumbe kwa ndugu zake, huleta Ushuhuda wa Yesu kwao. Kuelezea: Tuseme Bwana Yesu angetuma ujumbe wa kibinafsi kwako kupitia mjumbe, je! Ujumbe Wake haungekuwa ushuhuda Wake kwako? Na je! Mungu angemtunuku mjumbe huyo zawadi ya Roho Wake kukufunulia unabii ambao u katika Maandiko, je! Yeye hatakukujia na Roho ya Unabii? {2TG45: 6.3}
Kwa hivyo ni wazi kwamba “Ushuhuda wa Yesu” na “Roho ya Unabii” ni maneno visawe kwa ujumbe mwafaka uliotumwa kutoka kwa Mungu — “chakula kwa wakati wake.” Roho ya unabii, kwa hivyo, ni njia ya Mungu ya kuwasiliana kutoka Mbinguni moja kwa moja hadi kwa kanisa Lake katika nchi, na vile vile kulifunu-lia unabii uliotiwa muhuri. {2TG45: 6.4}
Jinsi ambavyo tumeona tayari kwamba kondoo hao wawili ni mfano wa Maagano ya Kale na Jipya
6
sasa tunaona pia kwamba “ng’ombe mke mchanga” ni mfano wa ufasiri iliovuviwa wa Biblia, Roho ya Unabii katika siku yetu. Ni dhahiri sasa kwamba bidhaa ya viumbe hivi vitatu lazima iwe lishe yetu ya kiroho iwapo tunatarajia “kusalia” na kuruhusiwa kuishi katika Nchi Takatifu, na ya kwamba hakuna maana kufikiri kwetu kusimama hukumuni katika njia nyingineyo. Na iwapo bado lipo shaka lolote juu ya hili, basi fikiria tafadhali lile mtume Petro anasema juu ya hiyo mada: {2TG45: 6.5}
“Nasi tuna lile neno la unabii lililo imara zaidi; ambalo mkiliangalia, kama taa ing’aayo mahali penye giza mwafanya vyema, mpaka kutakapopambazuka na nyota ya asubuhi kuzuka mioyoni mwenu. Mkijua neno hili kwanza, kwamba hakuna unabii wowote wa Maandiko upatao kufasiriwa kama apendavyo mtu fulani tu. Maana unabii haukuletwa popote kwa mapenzi ya mwanadamu, bali wanadamu walinena yaliyotoka kwa Mungu wakiongozwa na Roho Mtakatifu.” 2 Pet. 1:19-21. {2TG45: 7.1}
Je! Ulitia alama lile ambalo Uvuvio husema? Unatangaza wazi kwamba Maandiko hayafasiriwi kama apenda-vyo mtu fulani tu — si bila Roho wa Mungu ndani ya mtu, si na mtu peke yake, na si bila uteuzi wa Mungu mwenyewe. Na sababu iliyotolewa, unakumbuka, ni ukweli haswa kwamba unabii haukuletwa kwa mapenzi ya mwanadamu, bali kwa mapenzi ya Roho, kupitia “watu watakatifu wa Mungu.” Hii, ndugu, ni sheria na utarati-bu wa Mbingu. Na sisi ni nani kuibadilisha? Kuweka tumaini lako katika ufasiri wa apendavyo mtu tu kwa hivyo ni kuiuza nafsi yako kwa mwanadamu. Kuhusu zoea hatari kama hili, Bwana anaamuru: {2TG45: 7.2}
“Mwacheni mwanadamu, ambaye pumzi yake i katika mianzi ya pua yake; kwa maana hudhaniwaje kuwa ni kitu?” Isa. 2:22.
7
Kwa sabababu ukweli uliofunuliwa unafunuliwa tu na Roho wa Kweli kwa wakati fulani, basi kwa mtu kuukataa ufunuo kama huo, “chakula kwa wakati wake” (Mat. 24:45), ni kutenda dhambi “dhidi ya Roho Mta-katifu.” Mat. 12:31. {2TG45: 8.1}
Kwa sababu sasa ni wazi kama mwangaza wa jua kwamba unaokunjua daima, Uliovuviwa ufasiri wa Maandiko ni Roho ya Unabii aliye hai daima, macho ya kanisa kazini (1 Sam. 9:9), basi kutokuwa na macho haya ya kiroho ni kujaribu kutembea, kana kwamba ni, katika giza kuu. {2TG45: 8.2}
Sayansi ya huo mchakato hupata ulinganifu wa karibu katika ile ya mkondo wa umeme unaotumika kote du-niani. Umeme hutenda kazi wakati waya yenye umeme (chanya) inapogusana na waya ya ardhini (hasi). Hivyo ni kwamba mawasiliano ya kanisa na chombo kilichochaguliwa na Mungu (waya ya ardhini) kilichounganishwa na Roho wa Mungu (waya yenye umeme) — ambavyo kwa pamoja huwakilisha chanya na hasi — ndio hulisisimua kanisa, na kwa hivyo kufungua njia ya mawasiliano kati ya kanisa na Mbingu. {2TG45: 8.3}
Katika busara ya mfano huu, inafuata kwamba Yesu Kristo ndiye mtambo mkuu wa umeme, na Baba ndiye kawi yake. Wakati, kwa hivyo, kanisa lote, si mshiriki aliyetengwa, linajiunganisha kwa Nyumba ya Umeme ya Mbingu, basi nchi itaangazwa kwa utukufu wa yule malaika (Ufu. 18:1). (Kwa sababu hii haswa “kuwekewa mikono” ni njia ya Kibiblia ya kupitisha Roho wa Mungu kutoka kwa mtu mmoja hadi kwa mwingine.) Kwa hivyo kanisa ambalo halina uhusiano huu muhimu na Mbingu ni kanisa lililokufa kiroho, ambalo lina uwezekano wa kuwa “nyonge, na lenye mashaka, na maskini, na kipofu, na uchi.” Ufu. 3:17. Hivyo hali kadhalika ni kila mtu mmoja mmoja ambaye hajaunganika na kanisa. Nguvu hii pekee inamwezesha
8
mshiriki mmoja mmoja wa kanisa kuyachagua mema na kuyakataa maovu, na kupita katika siku iliyo kuu na ya kuogofya ya Bwana. Kwa hivyo, imeonekana sasa upya kwamba lile linalohusu kanisa kama mwili, linamhusu mshiriki mmoja mmoja wa kanisa hilo. {2TG45: 8.4}
Hitimisho dhahiri kutoka kwa kweli hizi za maandiko ni kwamba watu pekee ambao watanusurika na ku-ruhusiwa kuishi katika Nchi Takatifu wakati wa “siku iliyo kuu na ya kuogofya ya Bwana” (Mal. 4:5) ni wale ambao huifanya kuwa shughuli yao kuu na zoea la kula kwa furaha (jinsi ile “asali” inavyoashiria) bidhaa za vi-umbe hivi vitatu vya kuzalisha siagi. {2TG45: 9.1}
Msiba utakaowapata wale ambao wanakataa siagi na asali, na ukombozi utakaokuja kwa wale ambao hujilisha, unaonyeshwa na Waufunuokatika mfano mwingine: {2TG45: 9.2}
“Nchi ikamsaidia yule mwanamke [kanisa], nchi ikafunua kinywa chake, ikayameza mafuriko [waovu] ali-yoyatoa joka katika kinywa chake. Yule joka akamkasirikia yule mwanamke, akaenda zake afanye vita juu ya uzao wake uliosalia [na wale ambao wamenusurika], wazishikao amri za Mungu, na kuwa na ushuhuda wa Yesu Kristo …. kwa maana ushuhuda wa Yesu ndio Roho ya Unabii.” Ufu. 12:16, 17; 19:10. {2TG45: 9.3}
Kifungu hiki hufichua kwamba masalia, wale ambao wamesazwa baada ya nchi kuyameza mafuriko ya joka ambayo sasa yanatisha kumgharikisha kabisa yule mwanamke (kanisa lililo hai milele), ndio wale kama kundi huzishika amri za Mungu, na kuwa na “ushuhuda wa Yesu Kristo.” Ni wakati huo, si sasa, kwamba masalia ka-ma kundi kwa kweli linazishika amri za Mungu, bado lina
9
Roho ya Unabii kati yake, na ni masalia kwa kweli, na si tena kwa matarajio tu au kwa maandishi. {2TG45: 9.4}
Kwa sababu utengo huu wa “magugu” kutoka kati ya “ngano” — “mavuno” — ni mamoja na kazi sawa na Hukumu ya walio hai, basi tofauti pekee kati ya Hukumu ya wafu na hukumu ya walio hai ni kwamba katika ya awali majina ya waovu yaondolewa vitabuni juu, ilhali katika ya mwisho waovu wanafagiliwa mbali kimwili kutoka kati ya washirika walio hai wa Kanisa. Si tu unabii na methali iliyozingatiwa hapa, bali pia mfano (upatanisho — Lawi 23:27, 29), pamoja na Maandishi ya Awali, uk. 118 na Shuhuda kwa Wachungaji, uk. 234, hufundisha ukweli ule ule. {2TG45: 10.1}
Hivi ndivyo ulivyo utakaso wa patakatifu (Dan. 8:14); hivi ndivyo ulivyo upatanisho wa uakisi (Pambano Kuu, uk. 399-402; 420-422; 428-430); Hivi ndivyo ilivyo hukumu ya walio hai; Hivi ndivyo ulivyo utakaso wa kanisa (Shuhuda, Gombo la 5, uk. 80). Huu ndio unaoleta mwisho wa dunia; na huu ndio unaorejesha umilele kwa Ukristo. {2TG45: 10.2}
Chini ya uangalifu maalum wa “Mkulima” asiyekosea kamwe, Ukristo, jinsi ambavyo tayari tumeona, ni mwunganisho wa mwanadamu na Uungu. Isitoshe, kwa kutumia siagi na asali ya kiroho, watakatifu wana-wezeshwa kuishi maisha ya mafanikio na ya manufaa hata sasa, na kwa hivyo wataziokoka hukumu za Mungu. {2TG45: 10.3}
Hivyo ni kwamba wakati Kristo Mwenyewe alijifunza kukataa uovu na kuchagua wema kwa kutumia hii siagi na asali, wafuasi Wake
10
sasa wanahakikisha waweze kuachwa hai na kupelekwa katika Nchi Takatifu, hata huko, tunaambiwa, wataji-lisha bidhaa za viumbe vitatu vilivyotajwa hapo awali vinavyozalisha siagi. {2TG45: 10.4}
Hapa inafaa kuuliza ni lini mapema katika mkondo wa wakati ambapo roho ya Ukristo ilichimbuka: {2TG45: 11.1}
“Mungu, Ambaye alisema zamani na baba zetu katika manabii kwa sehemu nyingi na kwa njia nyingi, mwisho wa siku hizi Amesema nasi katika Mwana Wake, Aliyemweka kuwa mrithi wa yote, tena kwa Yeye Aliufanya ulimwengu.” Ebr. 1:1, 2. {2TG45: 11.2}
Andiko hili hufunua kwamba Kristo si Mwokozi wetu tu bali ni Muumbaji wetu pia; kwamba Yeye hakuium-ba dunia yetu tu bali dunia zingine zote pia; na kwamba Yeye ni mmoja na Baba. Ni kwa sababu hii kwamba “Mungu (Baba) akasema (kwa mwana), na tumfanye mtu kwa mfano Wetu, kwa sura Yetu.” — Mwa 1:26. Na wakati vuguvugu la Kutoka lilikuwa njiani, wote “wakanywa…kinywaji kile kile cha roho: kwa maana wali-unywea Mwamba wa kiroho uliowafuata: na Mwamba ule ulikuwa ni Kristo.” 1 Kor. 10:4. {2TG45: 11.3}
Ni wazi, basi, kwa sababu nafsi inaoitwa sasa Kristo, imekuwa na watu wa Mungu tangu pambazuko la histo-ria, katika nyakati za Agano la Kale na Jipya, Ukristo duniani hujitambulisha Wenyewe na mwanzo wa uumbaji. {2TG45: 11.4}
Kwa hivyo Ukristo ulioanza na uumbaji, Kristo anaonyesha, ni kwa ulimwengu kile kuku alivyo kwa vi-faranga wake wachanga: “Ee Yerusalemu, Yerusalemu, uwauaye manabii, na kuwapiga kwa mawe wale wali-otumwa kwako, ni mara ngapi Nimetaka
11
kuwakusanya pamoja watoto wako, kama vile kuku avikusanyavyo pamoja vifaranga vyake chini ya mabawa yake, lakini hamkutaka! Angalieni, nyumba yenu mmeachiwa hali ya ukiwa.” Mat. 23:37, 38. {2TG45: 11.5}
Ukristo, zaidi ya hayo, ni kama mama, “maana Zayuni mara alipoona utungu, alizaa watoto wake.” Isa. 66:8. {2TG45: 12.1}
Ukristo, isitoshe, ni kama baba, “kwa maana Nimemjua,” asema Bwana, “ya kwamba atawaamuru wanawe na nyumba yake baada yake, waishike njia ya Bwana, wafanye haki na hukumu; ili kwamba Bwana Naye akamtimizie Ibrahimu ahadi Zake.” Mwa. 18:19. {2TG45: 12.2}
Ukristo, bado zaidi, ni kama kisima cha maji, kwa maana “ye yote atakayekunywa maji yale Nitakayompa,” alisema Kristo, “hataona kiu milele; bali yale maji Nitakayompa yatakuwa ndani yake chemchemi ya maji ya-kibubujikia uzima wa milele.” Yohana 4:14. {2TG45: 12.3}
Ukristo pia ni kama chumvi, kwa maana “Ninyi ni chumvi ya dunia” alitangaza Kristo, “lakini chumvi ikiwa imeharibika, itatiwa nini hata ikolee? haifai tena kabisa, ila kutupwa nje, na kukanyagwa na watu.” Mat. 5:13. {2TG45: 12.4}
Ukristo, tena, vivyo hivyo ni kama nyumba nzuri: “Ewe uliyeteswa, uliyerushwa na tufani, usiyetulizwa, tazama, Nitaweka mawe yako kwa rangi nzuri, Nitaweka misingi yako kwa yakuti samawi. Nami nitaifanya minara yako ya akiki nyekundu, na malango yako ya almasi, na mipaka yako yote ya mawe yapendezayo. Na watoto wako wote watafundishwa na Bwana; na amani ya
12
watoto wako itakuwa nyingi.” Isa. 54:11-13. {2TG45: 12.5}
Muhimu zaidi, Ukristo ni upendo: “mkaenende katika upendo, kama Kristo naye alivyowapenda ninyi, tena Akajitoa kwa ajili yetu sadaka na dhabihu kwa Mungu kuwa harufu ya manukato.” Efe. 5:2. {2TG45: 13.1}
“Mpende jirani yako kama nafsi yako.” Mat. 22:39. “Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele.” Yohana 3:16. {2TG45: 13.2}
Kwa kuongezea, Ukristo ni kama upepo: hakuna yeyote isipokuwa Mungu na “aliyezaliwa mara ya pili” wana-jua unakotoka au unakokwenda, kwa maana “upepo [Ukristo] huvuma upendako, waisikia [ambaye hujazaliwa mara ya pili] sauti yake, lakini hujui unakotoka na unakokwenda: kadhalika [hauonekani kwa mtu ambaye hajazaliwa mara ya pili] na hali yake kila mtu aliyezaliwa kwa Roho.” Yohana 3: 8. {2TG45: 13.3}
Basi, haiwezekani kwa ambaye hajazaliwa mara ya pili kujua Ukristo wa kweli ni nini. Kwa sababu hii hasa Maandiko yanaonya kwa dhati: “… bali waovu watatenda mabaya: wala hataelewa mtu mbaya awaye yote.” Dan. 12:10. Acha mwenye dhambi, kwa hivyo, aiache dhambi yake, aombe Roho wa Kweli, na kisha ufahamu utamjia. “Mtafuteni Bwana maadamu Anapatikana, mwiteni maadamu Yu karibu. Mtu mbaya na aache njia yake, na mtu asiye haki aache mawazo yake; na amrudie Bwana, Naye atamrehemu na arejee kwa Mungu wetu, Naye atasamehe kabisa. Maana mawazo Yangu sio mawazo yenu, wala njia zenu si njia Zangu, asema Bwana. Kwa maana kama vile
13
mbingu zilivyo juu sana kuliko nchi, kadhalika njia Zangu zi juu sana kuliko njia zenu, na mawazo Yangu kuliko mawazo yenu.” Isa. 55:6-9. {2TG45: 13.4}
Lakini Ukristo bado ni zaidi ya haya yote. Ni chakula kwa wenye njaa, makao kwa waliotupwa, kabati ya mavazi kwa walio uchi, tabibu na nyumba ya wageni kwa wagonjwa. Kwa ufupi, ni kila kitu kwa kila mtu kati-ka nyumba ya Mungu. Na hapa kuna changamoto kwa wafuasi wake: {2TG45: 14.1}
“Je! Siyo kuwagawia wenye njaa chakula chako, na kuwaleta maskini waliotupwa nje nyumbani kwako? Umwonapo mtu aliye uchi, umvike nguo; wala usijifiche na mtu mwenye damu moja nawe?” Isa. 58:7. {2TG45: 14.2}
Changamoto hii, Ndugu, Dada, haiwezi kukabiliwa isipokuwa wote kwa hekima wasaidie kadiri wawezavyo, wakikumbuka kwamba hakuna juhudi isipokuwa ile inayodai kafara, itapewa thawabu. Kwa sababu alitoa yote, riziki yake, senti mbili za mjane maskini (Marko 12:41-44) zilifanya zaidi ya dola za matajiri zingeweza kutenda. Pia, mjane wa Serepta, alitumia tone lake la mwisho la mafuta na konzi yake ya mwisho ya unga kumlisha nabii wa Mungu, bila tumaini la kuweza kupata zaidi, lakini akiwa na tarajio la kufa njaa tu, bila kumhifadhia hata mwanawe mwenyewe. Kinyume cha hilo, hata hivyo, mafuta yake na pipa lake la unga halikuweza kuwa tupu kamwe (1 Fal. 17:12, 15, 16), na yeye na mwanawe waliendelea kuishi. {2TG45: 14.3}
Abrahamu alikuwa baba wa waminifu na rafiki wa Mungu kwa sababu alimtoa kwa madhabahu ya kafara yake bora na yake yote — mwanawe pekee. Mwa. 22:1-13. {2TG45: 14.4}
Katika siku yake, Yusufu alikuwa mwokozi wa ulimwengu,
14
na wa pili kwa Farao, sababu kwa ajili ya usafi wa moyo alijitoa mhanga kwa wadhifa wake wa bwana mkubwa kwa kifungo gerezani (Mwanzo 39:7-20). {2TG45: 14.5}
Musa alikuwa mkombozi mkuu na jemadari wa wakati wote kwa sababu alikitoa kafara kiti kikuu cha enzi katika siku yake kwa ajili ya uhuru wa ndugu zake (Ebr. 11:24, 25; Kut. 3:10). {2TG45: 15.1}
Mali na familia ya Ayubu iliongezwa maradufu kwa sababu alihimili mateso yake kwa uvumilivu wa Mungu (Ayubu 42:10). {2TG45: 15.2}
Samweli alikuwa nabii, kuhani, na mwamuzi kwa sababu ya uaminifu wake kwa bwana wake aliyeteuliwa na Mungu, Eli (1 Sam. 2:18; 3:18; 7:6). {2TG45: 15.3}
Eliya alihamishwa bila kufa kwa kuchagua kuwa mkimbizi kwa ajili ya Matengenezo (2 Wafalme 2:1, 11). {2TG45: 15.4}
Elisha alipewa sehemu maradufu ya Roho wa Mungu, kwa kuchoma madaraja yote nyuma yake kwa kuingia kwake katika ofisi ya kinabii ambayo aliitwa kwayo. Naam, alifanya isiwezekane mwenyewe kurejelea kilimo. Isitoshe, alimtumikia Eliya kwa uaminifu usiku na mchana, na kumtazama hadi “kisahani cha kupaa” kikatua ili kumnyakua, na hadi alipotoweka (2 Fal. 2:9-15). {2TG45: 15.5}
Daudi alifanywa kuwa mfalme kwa kuhatarisha maisha yake ili kuokoa maisha ya watu wa Mungu (1 Sam. 19:5; 2 Sam. 2:4). {2TG45: 15.6}
Sulemani alikuwa mwenye hekima na tajiri zaidi ya wafalme wote, kwa sababu ya kuchagua juu ya vyote vin-gine zawadi ya hekima kufanya uamuzi kwa watu wa Mungu kwa haki (1 Wafalme 3:11-13). {2TG45: 15.7}
15
Mitume walipewa thawabu ya majina yao kuandikwa kwenye misingi ya Mji Mtakatifu na wa Milele, kwa sababu hawakuyahesabu maisha yao kuwa bora kwa ajili ya injili (Ufu. 21:14). {2TG45: 16.1}
Luther alikuwa baba wa Uprotestanti, kwa kuthamini Matengenezo kuwa ya umuhimu mkubwa kuliko maisha yake mwenyewe. {2TG45: 16.2}
Henry Ford alikuwa mkwasi zaidi duniani katika wakati wake, kwa kujaribu kufanya kazi na kwa jili ya watu maskini wa ulimwengu zaidi ya washindani wake wote. {2TG45: 16.3}
Ndivyo inavyoinuka piramidi kubwa ya ukweli wa kihistoria kwamba watu ambao wamepata ufanisi mkubwa wa maisha ni wale ambao juhudi zao zimejikita, sio kwa maslahi ya ubinafsi, bali kwa kuwabariki wengine. Hakuna yeyote hata sasa ameweza kubadilisha sheria hii. Kwa nini tujaribu, basi, kujipumbaza kwa kujaribu kui-badilisha? Liwalo lote lengo katika maishani yako, iwapo unataka mafanikio, basi acha juhudi zako zielekezwe kwa manufaa ya wanadamu badala ya manufaa ya ubinafsi. Himizo la Kristo mwenyewe ni: “Bali utafuteni kwanza ufalme wa Mungu, na haki Yake; na hayo yote mtazidishiwa.” Mat. 6:33. {2TG45: 16.4}
Ndugu, Dada, usiendelee mpagani au mtu wa Mataifa; kuwa Mkristo kikamilifu. Usiwe kama wabinafsi, wenye kiburi, na wenye nia ya kidunia, kwa maana njia ya ushindani hukwishia kwenye paradiso ya mpumbavu. Ni njia kuu ya kwenda kuzimu. Iepuke. Tafakari tangazo la kutisha dhidi ya wachungaji wenye tamaa wa leo (Ezek. 34). {2TG45: 16.5}
Na sasa, tukirejea kwa Isaya 58, tunapata kwamba wakati Ukristo unaamka kwa hitaji hili kubwa na kufanya jambo fulani kulihusu, “ndipo”
16
Bwana anahidi, “nuru yako itakapopambazuka kama asubuhi, na afya yako itatokea mara; na haki yako itakutangulia. utukufu wa Bwana utakufuata nyuma ukulinde. Ndipo utaita, na Bwana ataitika; utalia, Naye atasema, Mimi hapa. Kama ukiiondoa nira, isiwepo kati yako, wala kunyosha kidole, wala kunena maovu; na kama ukimkunjulia mtu mwenye njaa nafsi yako, na kuishibisha nafsi iliyoteswa; ndipo nuru yako itakapo-pambazuka gizani, na kiwi chako kitakuwa kama adhuhuri. Naye Bwana atakuongoza daima, ataishibisha nafsi yako mahali pasipokuwa na maji, na kutia nguvu mifupa yako; nawe utakuwa kama bustani iliyotiwa maji, na kama chemchemi, ambayo maji yake hayapungui.” Isa. 58: 8-11. {2TG45: 16.6}
Sasa ukweli ulio wazi ni kwamba iwapo wakati unaweza kudumu, na ikiwa tutakaa katika njia ya Ukristo wa kweli ambapo nuru huangaza, basi lazima wote wafanye jambo kuhusu kazi hii iliyopuuzwa vibaya ya kuwatun-za wahitaji, kwa maana haiwezi kufanikishwa kutokea eneo moja la kati, lakini lazima igatuliwe kwa kila jimbo na nchi popote ujumbe wa saa hii “utatia mizizi chini na kuzaa matunda juu.” Isa. 37:31. {2TG45: 17.1}
“Ndipo Mfalme atawaambia wale walioko mkono Wake wa kuume, Njoni, mliobarikiwa na Baba Yangu, urithini ufalme mliowekewa tayari tangu kuumbwa kwa ulimwengu; kwa maana Nalikuwa na njaa mkanipa chakula, Nalikuwa na kiu, mkaninywesha: Nalikuwa mgeni, mkanikaribisha: Nalikuwa uchi, mkanivika: Naliku-wa mgonjwa, mkaja kunitazama: Nalikuwa kifungoni, mkanijia.” Mat. 25:34-36. {2TG45: 17.2}
Wajibu wetu, hata hivyo, sio kutii agizo
17
hili tu, bali yote ambayo Uvuvio umeweka mbele yetu. Yote lazima yawe sehemu ya kuwa kwetu, kama kifan-yavyo chakula tunachokula, iwapo tutafurahia ahadi zote za Mungu, na kuwa warithi wa Ufalme wa milele. Huu ndio upande mwangavu wa ile picha. {2TG45: 17.3}
Lakini, kwa kusikitisha, upo upande wa giza pia. Karibu katika eneo la mbele ni baba Lutu. Kujichagulia kwa ubinafsi ardhi yote yenye rutuba ya tambarare, na kuviacha vilima tasa kwa baba yake mzee, Abrahamu, haikumzalishia mazao aliyotarajia. Hata ingawa alifanikiwa kwa muda, lakini mwishowe alipomaliza na Sodoma, alitoka maskini hohe hahe. (Mwa. 19:15-17). {2TG45: 18.1}
Farao na watu wake wakuu, wakijaribu kuwaweka watu wa Mungu utumwani milele, walifunikwa na Bahari ya Shamu, na kuzikwa wakiwa hai kati yake (Kut. 14:22, 23, 38). {2TG45: 18.2}
Kwa kumdanganya Nabothi atoke katika shamba lake la mizabibu na kwa kumuua, Ahabu, mfalme wa Israeli, na nyumba yake yote, walikufa kwa makali ya upanga (1 Wafalme 21). {2TG45: 18.3}
Wale ambao waliwatupa Waebrania watatu katika tanuru la moto, wao wenyewe waliangamizwa kwa miali yake (Dan. 3:22), kama vile wale watu wabinafsi, wenye choyo, wakatili waliomtupa Danieli ndani ya tundu la simba, wao wenyewe mwishowe waliangamizwa na wale hayawani wenye njaa. (Dan. 6:24). {2TG45: 18.4}
Hamani alisimamisha nguzo ambayo angetumia kumnyonga Mordekai, lakini aliishia kunyongwa kwayo yeye mwenyewe (Esta 7:10). {2TG45: 18.5}
Kwa kujichukulia utukufu na sifa kwa hotuba yake kuu, Herode aliliwa na chango (Matendo 12:23). {2TG45: 18.6}
18
Kwa bei ya sarafu chache za fedha, Yuda alimsaliti Mwalimu wake kuuawa, na kisha, wazimu ukamdhihaki kwa ujira huo mbaya, akajielekezea mkono wa tamaa na usaliti ambao ulitwaa huo ujira, na kwa huo akajiletea mwisho uliolaaniwa na wenye jeuri na kaburi la fukara, hata kabla ya Kristo kutundikwa msalabani (Mat. 27:5; Mdo. 1:18). {2TG45: 19.1}
Hakika “Mtu akichukua mateka atachukuliwa mateka, mtu akiua kwa upanga atauawa kwa upanga.” Ufu. 13:10. {2TG45: 19.2}
Hivyo sheria isiyotanguka ya kisasi bado hulipiza jicho kwa jicho na jino kwa jino. Aha! hivyo amini kweli, ki-la apandacho mtu, ndicho atakachovuna pia (Gal. 6:7). {2TG45: 19.3}
Mifano hii bora hugusa tu chuo cha historia. Maelfu ya mingine inaweza kuongezwa, kutosema chochote kwa ile asiyoweza kuhesabu mtu tangu pambazuko la wakati. {2TG45: 19.4}
Hivyo katika mwali huu unaofunua yote wa kurunzi inayopekua ukweli ya Mbingu zimewekwa kando kando “njia mbili za wasafiri” — njia ya uongo, yenye kujidai na legevu na pana, ambayo wengi wanaisafiria kwenda kwenye uharibifu; na njia ya kweli, isiyo ya kujidai na iliyosonga na nyembamba, ambayo wachache wanaisafiria hadi kwenye uzima. Na njia zote mbili sasa zimesimama zimejaa wingi wa nuru kutoka mwanzo hadi mwisho, msafiri anaweza kuona urefu wote wa kila njia, na kwa hivyo kujua nini cha kutarajia akisafiri kwa moja au ile nyingine. Mbona, basi, usichague kwenda kwenye njia inayoongoza hadi uzimani, usalama, na furaha, na milele uiepuke ile inayoongoza kwenye huzuni, umasikini na kifo? Mbona uendelee kujipumbaza kudiriki kujipatia ahadi za Mungu za uaminifu kwa kukimbia kutoka kwa lo hapa kwenda kwa lo huko, kutoka
19
kwa mtapeli huyu hadi kwa yule? Kwa nini usifuate baraka za maisha kwa njia ya Mungu? Bila shaka njia zote za Mungu ni kinyume na za mwanadamu, lakini iwapo zisingalikuwa hivyo, zingekuwaje bora zaidi kuliko zetu? “Maana mawazo yangu si mawazo yenu, wala njia zenu si njia zangu, asema Bwana.” Isa. 55:8. {2TG45: 19.5}
Mwishowe, Ukristo uliokomaa ni sura ya Mungu, ndani ya watu Wake wanapokuwa wamekomaa kabisa; — wanapokuwa wamekusanywa mmoja mmoja kutoka katika mataifa yote na kuletwa katika “nchi yao” (Ezek. 34:11-13); ambapo wakati damu yao imesafishwa, mioyo yao ya kijiwe imeondolewa kutoka ndani yao, na mi-oyo ya nyama pamoja na sheria ya Mungu iliyoandikwa juu yake wanapewa kwa ushindi na ubadilishaji wa fu-raha; wakati wote wanamjua na kumtumikia Bwana; kwa maana latangaza andiko: “Nami nitawapa ninyi moyo mpya, Nami nitatia roho mpya ndani yenu; Nami nitatoa moyo wa jiwe uliomo ndani ya mwili wenu, Nami nitawapa moyo wa nyama. Nami nitatia Roho Yangu ndani yenu, na kuwaendesha katika sheria Zangu, nanyi mtazishika hukumu Zangu, na kuzitenda.” Ezek. 36:26, 27. Hivyo inakuwa wakati huo na huko ndipo wana-tayarishwa kwa kuhamishwa bila kufa. {2TG45: 20.1}
Ni ipi sasa itakuwa na sisi — njia tukufu au isiyo tukufu, ya kumtumikia Mungu na wengine, au Shetani na ubinafsi? Kumtumikia Mungu na wanadamu ni ungwana, lakini kumtumikia Shetani na ubinafsi ni uovu. Je! Hatupaswi, basi, kuchagua kwa furaha kujilisha siagi na asali ya Mungu ili tuweze kujua tofauti kati ya wema na uovu, na tujifunze kuchagua mema na kukataa maovu? Je! Tutachagua kuhifadhiwa kutokana na maangamizo, na kupelekwa “katika nchi ya utukufu”? Mungu hukanya kwamba yeyote asiukatae mwaliko Wake wa neema zaidi. Sasa ni kwa kila mmoja kushikilia au kukosa kile
20
Ukristo ulio nacho kwa ajili yake. Ninakusihi uifanye iwe shughuli yako kuu kuzipata baraka zilizoahidiwa, ili uweze kuepuka maangamizo ya waovu, na wasioamini na wenye kutilia shaka, na “kuachwa” milele kufurahia ahadi: {2TG45: 20.2}
“Tena itakuwa ya kwamba yeye aliyebaki katika Zayuni, na yeye aliyeachwa ndani ya Yerusalemu, ataitwa mtakatifu, yaani, kila mmoja aliyeandikwa miongoni mwa hao walio hai ndani ya Yerusalemu:… Kisha kutaku-wa na hema kuwa uvuli wakati wa mchana kwa sababu ya hari, na kuwa mahali pa kukimbilia, na kujificha wa-kati wa tufani na mvua….Maana Bwana ameufariji Zayuni: amepafariji mahali pake palipokuwa ukiwa; amefan-ya jangwa lake kuwa kama bustani ya Edeni, na nyika yake kama bustani ya Bwana; furaha na kicheko zitaon-ekana ndani yake, kushukuru, na sauti ya sifa…. Nao waliokombolewa na Bwana watarejea, watafika Zayuni wakiimba; furaha ya milele itakuwa juu ya vichwa vyao; watapata shangwe na furaha; huzuni na kuugua zitakimbia.” Isa. 4:3, 6; Isa. 51:3, 11. {2TG45: 21.1}
21
ANDIKO LA SALA
Mti Tasa
Nitasoma kutoka katika Mafunzo ya Kristo kwa Mifano, uk. 217, 218, kuanzia aya ya kwanza: {2TG46: 22.1}
“Mti tasa hupokea mvua na mwangaza wa jua na utunzi wa mtunza bustani. Huvuta lishe kutoka mchangani. Lakini matawi yake yasiyozaa hutia ardhini giza tu, ili kwamba mimea yenye kuzaa matunda isiweze kunawiri chini ya kivuli chake …. {2TG46: 22.2}
“Kwa ule upendo usiochoka Kristo alihudumu kwa Israeli katika kipindi cha rehema iliyoongezwa…. Hivyo utunzi na kazi Yake kwako haijapungua, ila imeongezeka. Bado Anasema, ‘Mimi Bwana nalilinda; Nitalitia maji kila dakika; asije mtu akaliharibu, usiku na mchana.’{2TG46: 22.3}
“’Ikiwa utazaa matunda, vyema; na iwapo sivyo, basi baada ya hayo’ {2TG46: 22.4}
“Moyo ambao hauitikii vyombo vya Mungu huwa mgumu hadi usiweze tena kuwa mwepesi kwa mvuto wa Roho Mtakatifu. Kisha inakuwa kwamba neno linasemwa, ‘Ukate; kwa nini unafunika ardhi?’”{2TG46: 22.5}
Mfano huu huelezea kwamba Ukristo ni kama mmea; ni kama mti wa matunda. Isitoshe, hufafanua kwamba Mungu ni mvumilivu sana kwetu katika Ukristo wetu, kwa maana katika mfano huo baada ya mwaka wa tatu bila matunda Bwana angefikiria kuukata mtini tasa, na hata wakati huo bado alishawishika kungoja mwaka mwingine. Hivyo tunaona kwamba tumepewa wakati mwingi kutenda mema, — muda mwingi kuanza kuzaa matunda. Hakuna, hata hivyo, ilivyo katika mfano, mti usiozaa matunda ambao utanusurika baada ya mwaka wa nne wa mfano. {2TG46: 22.6}
22
ZAWADI YA MIUJIZA HASWA KUPONYA NA KUNENA KWA LUGHA — LINI, VIPI, NANI?
ANDIKO LA HOTUBA NA V. T. HOUTEFF,
MCHUNGAJI WA WADAUDI WAADVENTISTA WA SABATO
SABATO, APRILI 22, 1950
HEKALU LA MLIMA KARMELI
WACO, TEXAS
Halijawahi kabla kuwapo fundisho la miujiza, haswa kunena kwa lugha na uponyaji, ambalo huchochewa, ku-sisitizwa, na kutekelezwa kote kote katika Ukristo leo. Hata sasa kamwe halikuwapo shaka kuu kuhusu uhalali wa hayo maonyesho. Na wanapokabiliwa na wachochezi wa hii miujiza, wale ambao hawaiamini au kuipokea, wala kumiliki nguvu zake, hukimbilia kusema kuhusu chochote na kila kitu wanachoweza kufikiria katika juhudi zao za kukabili tukio hilo na kujifariji kwa mafanikio yao machache. Kuondoa moshi ambao umetokana na suala hili moto kati ya kambi hizi mbili hasimu za Wakristo, na kufunua ukweli juu ya mada hiyo, ambayo adui mkuu ameifunika kabisa, ndilo kusudi la Uvuvio hapa ndani. {2TG46:23.1}
Jambo kuu kwa ufahamu sahihi wa mada yote ni ukweli wa msingi kwamba siku ya Pentekoste wanafunzi walizungumza hakika katika lugha zote za watu ambazo zilikuwepo wakati huo. {2TG46: 23.2}
23
Kutoka kwa hatua hii muhimu, hakuna mtu anayeweza kuepa, na bado aiamini kumbu kumbu, au kujua ukw-eli uliomo: {2TG46: 24.1}
“ “Hata ilipotimia siku ya Pentekosti, walikuwako wote mahali pamoja. Kukaja ghafla toka mbinguni sauti kama uvumi wa upepo wa nguvu ukienda kasi, ukaijaza nyumba yote waliyokuwa wameketi. Kukawatokea ndimi zilizogawanyika kama ndimi za moto, uliowakalia kila mmoja wao. Wote wakajazwa Roho Mtakatifu, wakaanza kusema kwa lugha nyingine, kama Roho alivyowajalia kutamka. Na walikuwako Yerusalemu Waya-hudi wakikaa, watu wataua, watu wa kila taifa chini ya mbingu. Basi sauti hii iliposikiwa, makutano waliku-tanika, wakashikwa na fadhaa, kwa kuwa kila mmoja aliwasikia wakisema kwa lugha yake mwenyewe. Wa-kashangaa wote wakastaajabu, wakiambiana, Tazama hawa wote wasemao si Wagalilaya? Imekuwaje basi sisi kusikia kila mtu lugha yetu, tuliyozaliwa nayo? Warparthi, na Wamedi, na Waelami, nao wakaao Mesopotamia, na Uyahudi, na Kapadokia, Ponto, na Asia, Frigia, na Pamfilia, Misri, na pande za Libia karibu na Kirene, na wageni watokao Rumi, Wayahudi na waongofu, Wakrete na Waarabu, tunawasikia hawa wakisema kwa lugha zetu matendo makuu ya Mungu.” Matendo 2:1-11. {2TG46: 24.2}
Ingawa mada hii imekanganywa kwa mabishano, bado husimama wazi kutoka kwayo ukweli usiopingwa kwamba, bila kujali madai ya mtu yeyote, hakuna kikundi kingine cha watu, tangu wanafunzi waliopewa miujiza
24
kuiaga dunia, wameimiliki zawadi ambayo wote 120 walipokea siku ya Pentekoste. Kwa hivyo ukweli wazi ni kwamba karama hiyo hatimaye iliinua mabawa yake, kwa mfano, na ikatoweka kati ya wanadamu, kwa kweli kama walivyofanya wanafunzi wenyewe, na kwamba tangu siku hiyo kamwe haijajidhihirisha tena yenyewe. {2TG46: 24.3}
Je! Yupo yeyote atakayepinga dai hili, basi yote ambayo ni muhimu kupuuza ni kwa wao aidha kufunua vinywa vyao na kusema lugha zetu sisi sote leo, jinsi mitume walivyozungumza lugha za watu katika siku yao, au kutoa rekodi ya kihistoria ya udhihirisho kama huo tangu wakati huo. Lakini kwa kuendelea kutokuwepo kwa ushahidi kama huo, nini basi? Je! Zawadi hii itawahi kujidhihirisha tena yenyewe? Ikiwa ni hivyo, lini? Mbona si sasa? {2TG46: 25.1}
Ili kuyajibu maswali haya kwa njia ya kuridhisha, lazima kwanza tuangalie hali ambazo wanafunzi wa kwanza wa Kristo walipokea zawadi ya miujiza, kwa maana hali kama hizo ndizo zitaleta matokeo sawa. Kwanza kabisa, kila mmoja wa wanafunzi, itakumbukwa, walikuwa kwa nia moja mahali pamoja (Matendo 2:1) kabla ya kupokea zawadi hiyo. Kabla ya Pentekoste, walakini, walikuwa na wivu mmoja kwa mwingine na walikuwa wakitamani kupiku kila mmoja kwa cheo, ufahari, na mengine yote. Ukristo hata leo ni mbaya zaidi; kwa kweli, ni mbaya kuliko wakati mwingine wowote. Kamwe awali haujawahi kutukia mgogoro kama huo, kuzozana hivyo, kulaumu na kulaani, katika kujaribu kujiinua nafsi na kumwangusha mwingine. Hii si, haswa, kwa kuzingatia ukweli kwamba dhehebu moja halikubaliani
25
na lingine, maana wote wanajua kwamba zisingalikuwapo tofauti, hayangalikuwapo madhehebu. Badala yake, lililo la wasiwasi maalum ni ukweli kwamba ni nadra watu wawili ndani ya dhehebu moja kukubaliana kwa kauli zote za fundisho na kutenda. Mbali na kujaa mifarakano na migawanyiko, na ubaguzi wa kila aina, kila dhehebu katika Jumuiya ya Ukristo ni, kwa kuongezea, hupigwa kwa kila ugonjwa mwingine wa kiroho. Na ni nani anayeweza kukana? {2TG46: 25.2}
Muda mrefu kabla ya hali hizi za kusikitisha kustawi, Bwana alionya kimbele kwamba watu wangelala na kumruhusu Ibilisi kupanda “magugu” yake kati ya “ngano” (Mat. 13:25, 28). Kwa muda gani? — “Mpaka wakati wa mavuno.” Na “wakati wa mavuno,” asema Bwana, “nitawaambia wavunao, Yakusanyeni kwanza magugu, myafunge matita matita mkayachome; bali ngano ikusanyeni ghalani Mwangu.” Mat. 13:30. {2TG46: 26.1}
Kwa sababu ni hakikisho Kibiblia kwamba Mungu hatatoa zawadi ya miujiza kwa watu wengine isipokuwa wale ambao kama kikundi wanakuja kwa umoja, ambao wanakuja “kuona jicho kwa jicho” (Isa. 52:8), na maadamu Roho hawezi kuleta umoja na upatano sasa wakati magugu yamechangamana na ngano, basi wote wanaweza kujipatanisha kwa nidhamu ya kielimu na ukombozi ya kumngojea Bwana hadi “mavuno” — hadi magugu, wenye chokochoko wale waongo, wamesafishwa watoke. Wale ambao hawatangoja, bali si wavumili-vu kumiliki nguvu sasa ili wafanye maajabu, watajidanganya wenyewe kwa
26
zawadi ya ujanja. Wakitaka sana kupata zawadi ya nguvu ya kutenda miujiza ambayo ni maarufu badala ya karama zifanywe kuwapo kuharakisha mavuno, wanajiridhisha na ile bandia ambayo ni ya sasa, jinsi Farao alivyojiridhisha na nyoka wa miigizo ambao watu wake wakuu walileta dhidi ya nyoka wa Musa (Kut. 7:10-12). Iwapo hawa watenda-miujiza na wawinda-miujiza bandia wa leo hawatatubu upuzi huu, basi watalazimika kuli-pa adhabu kwa kucheza upumbavu. {2TG46: 26.2}
Je! Ni nini basi ukweli kuhusu zawadi hii? Je! Tunapaswa kuelewa kwamba kazi ya injili itafungwa bila hiyo? Uvuvio hautulii kimya juu ya swali hilo, ila, kama tutakavyoona, huweka wazi kwamba kazi ya injili haitafunga kamwe, “mavuno” hayataletwa ndani kamwe, bila dhihirisho la ulimwengu la karama ya Miujiza, pamoja na zawadi ya lugha. {2TG46: 27.1}
Lakini, unaweza kusema, ikiwa Malaika, si wanadamu, watawatenga wema kutoka kati ya wabaya, na hivyo kukamilisha “mavuno,” basi zawadi hiyo itakuwa ya kazi na manufaa gani kwa wanadamu, iwapo hakuna nafsi zaidi za kuokoa baada ya hapo? Ni hapa haswa katika sehemu hii iliyojaa mawingu njiani, ambapo kanisa li-nahitaji nuru ili lisije kwa upofu lijitumbukize ndani na kupoteza njia yake kwenye giza nene mbele. {2TG46: 27.2}
Ili kuingia kwenye mwali kamili wa nuru, lazima kwanza tukabili ukweli kwamba mavuno ya kabla ya Pen-tekoste yalitukia katika kanisa lililojidanganya lenyewe, la Kiyahudi; na kupitia nguvu ya kufanya miujiza ili-yoonyeshwa na
27
Kristo Mwenyewe, yalizalisha wanafunzi 120, malimbuko ya wale ambao watafufuliwa. Ilhali mavuno ya baada ya Pentekoste yalitukia kati ya mataifa; na kupitia nguvu ya kutenda miujiza iliyodhihirishwa na wanafunzi 120 waliojazwa na Roho, yalizalisha umati usioweza kuhesabika wa waongofu kwa Ukristo (Matendo 2:41, 47), matunda ya pili ya wale ambao watafufuliwa. {2TG46: 27.3}
Sasa kufanya muhtasari wa mifano kabla ya Pentekoste: (1) malimbuko yalihesabiwa; (2) yalikuja kutoka kwa kanisa lenyewe; (3) miujiza iliyofanywa wakati huo na Kristo Mwenyewe. {2TG46: 28.1}
Sasa tukija kwa mifano baada ya Pentekoste: (1) matunda ya pili hayakuhesabiwa; (2) yalikuja kutoka kwa mataifa; (3) miujiza ilifanywa wakati huo na wale waliohesabiwa (watu 120), malimbuko. {2TG46: 28.2}
Kwa hivyo, mavuno kabla ya Pentekoste ya uakisi yanafanyika katika kanisa lililojidanganya lenyewe, Laod-ekia, “nyumba ya Mungu”; na kupitia nguvu ya kufanya miujiza iliyodhihirishwa na Mbingu yenyewe katika ma-laika (Mat. 13:39), inazalisha watu 144,000, malimbuko ya wale ambao hawatakufa kamwe. Ilhali mavuno baada ya Pentekoste ya uakisi yanatukia kati ya mataifa; na kupitia nguvu ya kufanya miujiza iliyodhihirishwa na watu 144,000 waliojazwa Roho, inazalisha umati mkubwa ambao hakuna mtu awezaye kuuhesabu (Ufu. 7:9), matunda ya pili, ya wale ambao hawatakufa kamwe. {2TG46: 28.3}
Ukweli uu huu katika nyanja tofauti umeonyeshwa katika unabii wa Danieli: {2TG46: 28.4}
28
“…jiwe lilichongwa bila kazi ya mikono, nalo jiwe hilo likaipiga sanamu miguu yake,… na lile jiwe lililoipiga hiyo sanamu likawa mlima mkubwa, likaijaza dunia yote….na katika siku za wafalme hao Mungu wa mbinguni atausimamisha ufalme, nao…utavunja vipande vipande na kuziharibu hizi falme zote, nao utasimama milele na milele. Na kama vile ulivyoona ya kuwa jiwe lilichongwa mlimani bila kazi ya mikono, na na ya kuwa lilivunja-vunja kile chuma, na ile shaba, na ule udongo, na ile fedha na ile dhahabu; basi Mungu aliye mkuu amemjulisha mfalme mambo yatakayokuwa baadaye: na ndoto hii ni ya hakika, na tafsiri yake ni thabiti.” Dan. 2:34, 35, 44, 45. {2TG46: 29.1}
Nini hupiga sanamu? Je! Si lile jiwe ambalo Danieli hufunua ni nembo ya Ufalme wa Mungu uliorejeshwa? Kumbuka pia ukweli kwamba sanamu hiyo haipigwi kwa jiwe hadi baada ya (lile jiwe) limekatwa kutoka mli-mani, bila kazi ya mikono, na ya kwamba baadaye linakua na kuijaza dunia, na hivyo baadaye lenyewe kuwa mlima. Katika kufafanua wazi ukweli huu, nabii Isaya anaongeza: {2TG46: 29.2}
“Na itakuwa katika siku za mwisho, mlima wa nyumba ya Bwana utawekwa imara juu ya milima, nao utainuliwa juu ya vilima; na mataifa yote yatauendea makundi makundi. Na mataifa mengi watakwenda na kus-ema, njoni, twende mlimani kwa Bwana, nyumbani kwa Mungu wa Yakobo; Naye atatufundisha njia Zake, nasi tutatembea katika mapito Yake, kwa maana katika Zayuni atatoka
29
sheria, na neno la Bwana katika Yerusalemu.” Isa. 2:2, 3. {2TG46: 29.3}
Hivyo kadiri hilo jiwe, lililochongwa kimiujiza kutoka kwa mlima mmoja, linabadilika kimiujiza kuwa mlima mwingine, kisha kuijaza dunia yote, linafunua mchakato wa unabii kubadilika kuwa historia: kwamba lile jiwe (kwa sababu litakua) ni nembo ya malimbuko katika ufalme; ya kuwa ufalme mchanga huanza na watu 144,000 “watumwa wa Mungu” (Ufu. 7:3); kwa sababu hiyo kanisa la Laodekia (kwa kuwa ni la mwisho ambalo ngano na magugu huchangamana, watu 144,000, malimbuko, yanavunwa) kwa lazima ni mlima ambao jiwe, malimbu-ko ya ufalme, yanakatwa au kuchukuliwa kutoka kwalo. {2TG46: 30.1}
Zaidi ya hayo, inaonekana kwamba wao kukatwa bila kazi ya mikono, bila msaada wa kibinadamu, ni wazi huonyesha ukweli kwamba wamechumwa na malaika; kwamba kuongezeka kwao, wakati huo, jinsi ukuaji wa jiwe huonyesha, ni matokeo yanayofuata ya kukusanywa kwa mavuno ya pili kutoka katika mataifa yote, na kusababisha mlima au ufalme, kuijaza dunia yote; na kwamba kazi hii ya kimiujiza ya kulichonga jiwe, ya kuten-ganisha watu 144,000, kitovu cha ufalme, ni kutakaswa kwa kanisa. {2TG46: 30.2}
Mwishowe, kwa sababu jiwe, ambavyo limeonekana, limekatwa — ufalme mchanga kusimamishwa — “katika siku za wafalme hao” (wafalme wa vidole), si baada ya siku zao, na maadamu “watumwa wa Mungu” watu 144,000 wanasimama juu ya Mlima Zayuni (Ufu. 14:1), inafuatia kumalizia kwamba ufalme wa jiwe mwanzoni mwake
30
unasimamishwa katika Nchi Takatifu, wakati wafalme wa vidole wangalipo. {2TG46: 30.3}
Pasipo shaka, kwa hivyo, watu 144,00 watumwa wa Mungu wasiokuwa na uongo. (Ufu. 14:5), wanaounda serikali ya Mungu mwanzoni mwake, jiwe ambalo linaipiga sanamu hiyo, na ambalo baadaye linakuwa mlima mkubwa ambao unaijaza dunia yote, ni chombo katika kuzipindua mwishowe serikali zote za dunia. Kwa hivyo, ni nani wengine wakati huo katika dunia yote, ni nani wengine hakika ila kwa wao, yaweza kuwa yaliandikwa: {2TG46: 31.1}
“… ni watu walioishara; … hao ni wakuu tena wenye nguvu; mfano wao haukuwako kamwe, wala hautaku-wako baada ya hao, hata katika miaka ya vizazi vingi.” Zek. 3:8; Yoeli 2:2. {2TG6: 31.2}
“Na hayo mabaki ya Yakobo yatakuwa kati ya kabila nyingi mfano wa umande utokao kwa Bwana, mfano wa manyunyu yatokayo kwa Bwana, mfano wa umande katika manyasi, yasiyomngojea mtu, wala kukawilia wanadamu…. Mkono wako na uinuliwe juu ya adui zako, na adui zako wote wakauliwe mbali…. Fungu la Yakobo siye kama hawa; maana Ndiye aliyeviumba vitu vyote; na Israeli ni kabila ya urithi Wake: Bwana wa majeshi ndilo jina Lake. Wewe u shoka Langu na silaha Zangu za vita; kwa wewe Nitavunja-vunja mataifa, na kwa wewe Nitaharibu falme; na kwa wewe Nitamvunja-vunja farasi na yeye ampandaye; na kwa wewe Nitalivunja-vunja gari la vita na yeye achukuliwaye ndani yake; na kwa wewe Nitawavunja-vunja mwanamume na mwanamke; na kwa wewe Nitawavunja-vunja mzee na mtoto, na kwa wewe Nitawavunja-
31
vunja kijana mwanamme na kijana mwanamke; Na kwa wewe Nitamvunja-vunja mchungaji na kundi lake; na kwa wewe Nitamvunja-vunja mkulima na jozi yake ya ng’ombe; na kwa wewe Nitawavunja-vunja maliwali na maakida.” Mika 5:7, 9; Yer. 51:19-23. {2TG46: 31.3}
Nani atathubutu kuhoji kwamba katika unabii hawa ndio wale watu na hili ndilo kanisa ambalo linakamilisha kazi — watu pekee na kanisa pekee ambalo litamiliki karama zote za roho, kuanzia karama ya unabii hadi karama ya maongozi na karama ya miujiza; kwamba zawadi hizi wamepewa kwa kufanikisha kazi yao ya kutia taji ya kuangaza nchi kwa utukufu (Ufu. 18:1), ya “kuhubiri injili hii ya ufalme katika ulimwengu wote kuwa ushuhuda kwa mataifa yote,” hivyo kuwakusanya watu wa Mungu, mavuno ya pili, bila magugu (“watu Wangu”), kutoka Babeli (Ufu. 18:4). Kutoka katika kila taifa na kabila na lugha na jamaa (ambao Babeli inatawala), wanawaleta “ndugu zao” ndani ya kanisa lililotakaswa (Isa. 66:19, 20), ufalme wa Mungu duniani katika uchanga wa urejesho wake. {2TG46: 32.1}
Kuona kinabii katika siku nyingi za kale siku hii tukufu ya ushindi kwa watu na kanisa la Mungu, na kwa “in-jili ya milele,” Uvuvio kwa shangwe ulitangaza: {2TG46: 32.2}
“… Miujiza mikubwa ilifanywa, wagonjwa waliponywa, na ishara na maajabu yaliwafuata waamini. Mungu alikuwa katika kazi hiyo, na kila mtakatifu, bila hofu kwa matokeo, alifuata masadikisho
32
ya dhamiri yake mwenyewe, na kuungana na wale waliokuwa wakizishika amri zote za Mungu; na kwa nguvu wakatangaza nchi za mbali ujumbe wa tatu….” — Maandishi ya Awali, uk. 278. {2TG46: 32.3}
“Na katika siku zile wanadamu watatafuta mauti, wala hawataiona kamwe; nao watatamani kufa, nayo mauti itawakimbia.” Ufu. 9:6. {2TG46: 33.1}
“… panga zilizoinuliwa kuua watu wa Mungu zilivunjika na kuanguka dhaifu kama majani….” — Maandishi ya Awali, uk. 285. {2TG46: 33.2}
“Bwana asema hivi; Mimi nimerudi Zayuni, Nami nitakaa katikati ya Yerusalemu; na Yerusalemu utaitwa mji wa kweli; na mlima wa BWANA wa majeshi utaitwa mlima mtakatifu…. Naam, watu wa kabila nyingi na ma-taifa hodari watakuja Yerusalemu kumtafuta Bwana wa majeshi, na kuomba fadhili za Bwana. Bwana wa majeshi asema hivi; Katika siku hizo itakuwa kwamba watu kumi wa lugha zote za mataifa, wataushika upindo wa nguo yake yeye aliye Myahudi, wakisema, Tutakwenda pamoja nanyi, kwa maana tumesikia kwamba Mungu yu pamoja nanyi.” Zek. 8:3, 22, 23. {2TG46: 33.3}
Kwa hivyo kuangazia haswa swala la lugha, unabii wa Zekaria hufichua kwamba katika wakati wa ku-kusanywa, katika wakati ambapo Mungu Mwenyewe analiita kanisa “mji wa kweli,” “mlima mtakatifu,” wakati ambamo mataifa yatakwenda kumtafuta Bwana na kuwaalika wengine kuja pamoja nao, wakati huo inakuwa kwamba kanisa lote, kila askari
33
mwamilifu katika jeshi la injili, atakuwa na karama ya lugha, jinsi inavyoonyeshwa wazi kwa uthibitisho kwam-ba “watu kumi wa lugha zote za mataifa” Maana ya ulimwengu ya hii namba huthibitishwa kwa vidole kumi vya sanamu kubwa ya Danieli 2, na pembe kumi za yule mnyama wa Danieli 7 na wa Ufunuo 13:1, na watumwa kumi wa mfano wa talanta kumi (Luka 19:12-25), na kwa wanawali kumi (Mat. 25:1-12) ambao ni mfano wa kanisa lote, ilhali wanawali watano wenye busara (“ngano”) na wanawali watano wapumbavu (“magugu”) bado wamechangamana. Katika mifano hii na jinsi ilivyo katika mingine yote, namba kumi kiidadi ni nembo ya Ulimwengu mzima. {2TG46: 33.4}
Kama vile unavyokata kauli unabii wa Zekaria kuhusu zawadi halisi ya kunena kwa lugha, ni wa Yoeli, Mika, Yeremia, Maandishi ya Awali, na unabii wa Ufunuo kuhusu zawadi zingine za miujiza, ikiwemo kinga kwa kifo, itadhihirishwa kati ya watu wa Mungu. Kuendelea na unabii wa Yoeli, tunaona karama zinapeanwa kwa wazee na wana: {2TG46: 34.1}
“Furahini, basi, enyi wana wa Zayuni, mkamfurahie Bwana, Mungu wenu; kwa kuwa Yeye huwapa ninyi mvua ya masika, kwa kipimo cha haki, Naye huwanyeshea mvua, mvua ya masika, na mvua ya vuli, kama kwanza…. Hata itakuwa, baada ya hayo, ya kwamba nitamimina Roho Yangu juu ya wote wenye mwili; na wana wenu, waume kwa wake, watatabiri, wazee wenu wataota ndoto, na vijana wenu wataona maono.” Yoeli 2:23, 28. {2TG46: 34.2}
34
Hapa pia, kwa maneno wazi umewekwa ukweli kwamba baada ya, si kabla, mvua ya masika na ya vuli (zote mbili ni mfano wa kweli mpya zinazokuja moja kwa moja kutoka kwenye Kiti cha Enzi cha Mungu, kabla ya mavuno), katika wakati wa “mavuno” makubwa, wakati wa watu kukusanywa, hizi karama za miujiza zitare-jeshwa. Tokeo la Mungu kuwarejesha limeonyeshwa kwa picha wazi wazi na wote wawili Isaya na Mika katika maneno yao karibu yanayofanana: {2TG46: 35.1}
“Lakini itakuwa katika siku za mwisho, ya kwamba mlima wa nyumba ya Bwana utawekwa imara juu ya mili-ma, nao utainuliwa juu ya vilima; na watu wa mataifa watauendea makundi makundi. Na mataifa mengi wa-takwenda na kusema, Njoni, twende juu mlimani kwa Bwana, na nyumbani kwa Mungu wa Yakobo; Naye ata-tufundisha njia Zake, nasi tutakwenda katika mapito Yake; kwa maana katika Zayuni itatoka sheria, na neno la Bwana litatoka Yerusalemu.” Mika 4:1, 2. {2TG46: 35.2}
Katika nyongeza ya ushuhuda wa mifano hiyo, hapa, kutoka vinywani mwa mashahidi takribani saba (Yo-hana, Mika, Yoeli, Danieli, Zekaria, Isaya, Kristo Mwenyewe) ni “neno la Unabii lililo imara,” likifunua wakati uliowekwa rasmi wa karama ya miujiza. {2TG46: 35.3}
Kwa muhtasari, ushuhuda wao mwaminifu ni kwamba kudhihirishwa tena kwa hizo zawadi, miongoni mwa wanadamu, kutakuwa (1) baada, si kabla ya, mvua ya vuli kumiminwa; (2) baada ya jiwe “kuchongwa kutoka mlimani,” si kabla; (3) wakati ambapo Bwana anayakusanya mavuno ya pili kutoka
35
“mashariki” na kutoka “magharibi”; (4) wakati Zayuni na Yerusalemu “inaitwa mji wa kweli, mlima wa Bwana wa majeshi mlima mtakatifu” (ufalme mtakatifu); (5) wakati “wenyeji wa mji mmoja,” watakwenda kwa mwingine, wakisema, “Njoni twende upesi kuomba mbele ya Bwana, na kumtafuta Bwana wa majeshi: Nitakwenda pia.” {2TG46: 35.4}
Kwa hivyo Bwana atawaweka huru Wake kutoka kwa dhambi na wenye dhambi, kuwatenga siku zote, na kuwapatia nguvu zote za kutenda miujiza. Je! Yeye anafanya hivi kwa sababu wamekuwa wema? au kwa ajili ya jina Lake? Hili ndilo jibu Lake mwenyewe: {2TG46: 36.1}
“Kwa hiyo; waambieni nyumba ya Israeli, Bwana MUNGU asema hivi Sitendi hili kwa ajili yenu, Ee nyumba ya Israeli, bali kwa ajili ya jina Langu takatifu, mlilolitia unajisi katika mataifa mliyoyaendea. Nami nitalitakasa jina Langu kuu, lililotiwa unajisi katika mataifa, mlilolitia unajisi kati yao; nao mataifa watajua ya kuwa mimi ndimi Bwana, asema Bwana MUNGU, Nitakapotakaswa kati yenu mbele ya macho yao. Maana Nitawatwaa kati ya ma-taifa, Nami nitawakusanya na kuwatoa katika nchi zote, na kuwarudisha katika nchi yenu wenyewe. Nami nita-wanyunyizia maji safi, nanyi mtakuwa safi; Nitawatakaseni na uchafu wenu wote, na vinyago vyenu vyote. Nami nitawapa ninyi moyo mpya, Nami nitatia roho mpya ndani yenu, Nami nitatoa moyo wa jiwe uliomo ndani ya mwili wenu, Nami nitawapa moyo wa nyama. Nami nitatia Roho Yangu ndani yenu,
36
na kuwaendesha katika sheria Zangu, nanyi mtazishika hukumu Zangu, na kuzitenda. Nanyi mtakaa katika nchi ile niliyowapa baba zenu, nanyi mtakuwa watu Wangu, Nami nitakuwa Mungu wenu.” Ezek. 36:22-28. {2TG46: 36.2}
Kumbuka jinsi aya hizi zinaifanya hiyo picha kuwa wazi — kwamba lile Mungu huwafanyia watu Wake, Yeye hafanyi kwa sababu wanalistahili, bali kwa ajili ya jina Lake mwenyewe; kwamba Yeye halifanyi kabla, ila baada ya, Yeye kuwatoa katika nchi zote na kuwaleta katika nchi yao; ya kwamba Yeye wakati huo na hapo anawasafisha na kuibadilisha mioyo yao. Yote ambayo huonyesha kwamba maadamu watu Wake wamechang-amana na magugu, na wanaishi kati ya Mataifa, kamwe hawawezi kustahili kuhamishwa bila kufa. Ni wazi, kwa hivyo, nchi ya baba zetu itakuwa chumba chetu bora kabisa cha kutuvika mavazi tufae kwa jamii ya viumbe wasafi, wasio na dhambi, wa milele. {2TG46: 37.1}
Je! Tunaona, basi, wazi kama tunavyopaswa, kwamba kushindwa kutii ukweli wa tukio hili muhimu zaidi katika historia yote ya kanisa, ni kupoteza zawadi ya miujiza, kufanywa tufae kuhamishwa bila kufa, na haki ya kuishi na kutawala na Kristo katika miaka elfu? Tusithubutu kumruhusu Adui atudanganye kuhusu kustahiki moyo mpya kwa Mbingu. {2TG46: 37.2}
Huku kukusanywa ndani hakika kutakuwa kutoka kwa pili, na kutakuwa sawa vile Bwana amesema: {2TG46: 37.3}
“Na itakuwa katika siku hiyo,
37
Bwana atapeleka mkono Wake mara ya pili, ili ajipatie watu Wake watakaosalia, kutoka Ashuru, na kutoka Misri, na kutoka Pathrosi, na kutoka Kushi, na kutoka Elamu, na kutoka Shinari, na kutoka Hamathi, na kutoka visiwa vya bahari…. kama vile ilivyokuwako kwa Israeli, katika siku ile waliyotoka katika nchi ya Misri.” Isa. 11:11, 16. {2TG46: 37.4}
“Nami nitampa mashamba yake ya mizabibu toka huko, na bonde la Akori kuwa mlango wa tumaini; naye ataniitikia huko, kama siku zile za ujana wake, na kama siku ile alipopanda kutoka nchi ya Misri.” Hos. 2:15. {2TG46: 38.1}
“…badala ya kumtolea yote Kristo, wengi wamechukua kabari ya dhahabu na vazi zuri la Kibabeli, na kuvificha kambini. Ikiwa uwepo wa Akani mmoja ulitosha kudhoofisha kambi yote ya Israeli, je! tunaweza kushangazwa kwa mafanikio madogo ambayo huambatana na juhudi zetu wakati kila kanisa na karibu kila fa-milia i na Akani?” — Shuhuda, Gombo la 5, uk. 157. {2TG46: 38.2}
Kwa hivyo ndio sababu ya utakaso wa kanisa ulio karibu sana, kuangamizwa kwa kina Akani wa leo, katika maandalio ya uakisi kuvuka Yordani. {2TG46: 38.3}
Sasa inapaswa kuangaliwa namna kazi hii ya (“kupepeta”), kutenganisha, itakavyoanza, na pia jinsi kanisa litakavyoisikia kuhusu hilo. Miaka kadhaa iliyopita, Roho wa Mungu alifunua ukweli katika maono: {2TG46: 38.4}
“Naliuliza maana ya kupepeta
38
nilioona,” alitangaza mpokeaji wa maono hayo, “na nalionyeshwa kwamba utasababishwa na ushuhuda usiopinda unaoletwa mbele na ushauri wa Shahidi Mwaminifu kwa Walaodekia. Huu utakuwa na matokeo yake juu ya moyo wa anayeupokea, na utamwongoza, kuinua kiwango na kutoa ukweli halisi. Wengine hawataustahimili ushuhuda huu wa moja kwa moja. Watainuka kuupinga, na hili ndilo litakalosababisha upepeto miongoni mwa watu wa Mungu.” — Maandishi ya Awali, uk. 270. {2TG46: 38.5}
Katika maono haya, tunatambulishwa kwa ujumbe imara ambao unapaswa kupelekwa kwa Walaodekia, na yaani utaanzisha upepeto kati ya watu wa Mungu. Kisha katika maono na ushuhuda unaofuata, tumepewa kuo-na tokeo la utukufu kwa upepeto huu. {2TG46: 39.1}
“…Miujiza mikubwa ilifanywa, wagonjwa waliponywa, na ishara na maajabu yaliwafuata waamini. Mungu alikuwa katika kazi hiyo, na kila mtakatifu, bila hofu kwa matokeo, alifuata masadikisho ya dhamiri yake mwenyewe, na kuungana na wale waliokuwa wakizishika amri zote za Mungu; na kwa nguvu wakatangaza nchi za mbali ujumbe wa tatu.” — Kimenukuliwa, uk. 278. {2TG46: 39.2}
“Waambieni walio na moyo wa hofu, Jipeni moyo, msiogope; tazama, Mungu wenu atakuja na kisasi, na malipo ya Mungu; atakuja na kuwaokoa ninyi. Ndipo macho ya vipofu yatafumbuliwa, na masikio ya viziwi yatazibuli-wa. Ndipo mtu aliye kilema ataruka-ruka kama kulungu, na ulimi wake
39
aliye bubu utaimba; maana katika nyika maji yatabubujika; na vijito jangwani.” Isa. 35:4-6. {2TG46: 39.3}
“… Haiwezekani kutoa wazo lolote la uzoefu wa watu wa Mungu ambao watakuwa hai duniani wakati utu-kufu wa mbinguni na marudio ya mateso ya zamani yamechangamana. Watatembea katika nuru inayotoka kwenye kiti cha enzi cha Mungu. Kwa njia ya malaika kutakuwa na mawasiliano ya daima kati ya mbingu na nchi. Na Shetani, akiwa amezungukwa na malaika waovu, na akidai kuwa ni Mungu, atafanya miujiza ya kila aina, kuwadanganya yamkini, wateule. Watu wa Mungu hawatapata usalama wao katika kufanya miujiza; kwa maana Shetani ataghushi miujiza ambayo itafanywa. Watu waliojaribiwa na kupimwa na Mungu watapata nguvu zao katika ishara iliyonenwa katika Kut. 31:12-18 ….”– Shuhuda, Gombo la 9, uk. 16. {2TG46: 40.1}
Akitabiri siku hii kuu ya nguvu ya Mungu, “nabii wa injili,” pia, huelekeza macho yetu kwa wale ambao, kwa kutii “ushuhuda usiopinda,” wanaokoka masaibu ya kupepetwa, na kuona uso kwa uso mandhari hayo ya ajabu ya utukufu ujao: {2TG46: 40.2}
“Angalia Zayuni, mji wa sikukuu zetu; macho yako yatauona Yerusalemu umekuwa kao la raha; hema isiyotanga-tanga; vigingi vyake havitang’olewa, wala kamba zake hazitakatika. Bali huko Bwana atakuwa pamoja nasi, mwenye adhama; mahali penye mito mipana na vijito,
40
pasipopita mashua na makasia yake; wala hapana merikebu ya vita itakayopita hapo….. Wala hapana mwenyeji atakayesema, Mimi mgonjwa; watu wakaao humo watasamehewa uovu wao.” Isa. 33:20, 21, 24. {2TG46: 40.3}
Kisha kwa picha hii iliyo tukufu tayari, Uvuvio bado unaongeza sehemu nyingine ya kuangazia na ya kutia moyo: {2TG46: 41.1}
“Na itakuwa ya kwamba mtu awaye yote atakayeliita jina la Bwana ataponywa; kwa kuwa katika mlima Zayuni na katika Yerusalemu watakuwako watu watakaookoka, kama Bwana alivyosema; na katika mabaki, hao awaitao Bwana…. Bali Yuda atadumu milele, na Yerusalemu tangu kizazi hata kizazi.” Yoeli 2:32; Yoeli 3:20. {2TG46: 41.2}
“Bali katika mlima Zayuni watakuwako wenye kuokoka, nao utakuwa mtakatifu; na nyumba ya Yakobo wa-tamiliki milki zao…. Tena waokozi watakwea juu ya mlima Zayuni ili kuuhukumu mlima wa Esau; na huo ufalme utakuwa ni mali ya Bwana.” Obad. 1:17, 21. {2TG46: 41.3}
Unabii huu mara mbili wa ukombozi na za matukio yanayofuatana, huonyesha wazi nguvu ya kufanya maaja-bu ambayo itawawekeza wale ambao wataistahimili inayojongea upesi “siku ile ya Bwana iliyo kuu na ya kuo-gofya.” {2TG46: 41.4}
Na sasa kadiri siku ile “inaharakisha kwa kasi” (Shuhuda, Gombo la 5, uk. 80), kuwameza kwa uharibifu Walaodekia ambao hupuuza ujumbe ambao husababisha kupepetwa, kwa kweli hakuna ila wagonjwa, maskini,
41
waliotupwa nje, na wale kutoka njiani na vichochoro, watakuwa wapole na wanyenyekevu kabisa kuitikia maonyo, kupata uzoefu wa nguvu ya kubadilisha ya neema ya Mungu kwa mioyo yao, kupewa utakaso endele-vu wa haki kwa imani, na kuwa miongoni mwa waliokusanywa, jinsi Uvuvio unavyofichua zaidi: {2TG46: 41.5}
“Naye atawatwekea mataifa bendera, Atawakutanisha watu wa Israeli waliotupwa, Atawakusanya watu wa Yuda waliotawanyika, kutoka ncha nne za dunia.” Isa. 11:12. {2TG46: 42.1}
“Akamwambia, Mtu mmoja alifanya karamu kubwa akaalika watu wengi, akamtuma mtumwa wake saa ya chakula chajio awaambie wale walioalikwa, Njoni, kwa kuwa vitu vyote vimekwisha kuwekwa tayari. Wakaanza wote kutoa udhuru kwa nia moja. Wa kwanza alimwambia, Nimenunua shamba, sharti niende nikalitazame; ta-fadhali unisamehe. Mwingine akasema, Nimenunua ng’ombe jozi tano, ninakwenda kuwajaribu; tafadhali unis-amehe. Mwingine akasema, Nimeoa mke, na kwa sababu hiyo siwezi kuja. Yule mtumwa akaenda, akampa bwana wake habari ya mambo hayo. Basi, yule mwenye nyumba akakasirika, akamwambia mtumwa wake, Toka upesi, uende katika njia kuu na vichochoro vya mji, ukawalete hapa maskini, na vilema, na vipofu, na viwete.” Luka 14:16-21. {2TG46: 42.2}
“…Waovu watatenda maovu; wala hataelewa mtu mbaya awaye yote; bali wao walio na hekima ndio watakaoe-lewa.” Dan. 12:10. {2TG46: 42.3}
42
Ni nani wenye hekima kuelewa? Je! Wewe, Ndugu, Dada? Je! Utachukua hatua sasa, ilhali wakati ungalipo? Je! utaikabili taswira hiyo na kuwa tayari kukutana na hali hiyo? Je utafanya? Kabla ya Roho wa Mungu kukua-cha? na Adui kupata manufaa ya mwisho juu yako? Je! Utang’amua kwamba anapomdang’anya tajiri kwa ubatili na kumponda maskini kwa masumbuko, atatumia kila silaha aliyonayo kuwavunja moyo, kuwakatisha tamaa, na kuwatawanya wale wote wanaoupokea mwaliko wa rehema wa Bwana kwa karamu Yake? {2TG46: 43.1}
Isitoshe, hakika kama aishivyo Ibilisi, ataajiri kila chombo ama kuongeza kwa Ukweli wa Mungu, au kuondoa kwa Huo, akiongeza ubaya na kuvunja moyo, haswa akizingatia hali mbaya na mateso ya watakatifu, ili kufunga anguko lao ikiwezekana. Kimsingi atategemea mawili ya mashirika yake yenye nguvu na yenye ufanisi — kupita kiasi — moja kusukuma kulia na lingine kushoto: Katika juhudi za kuwatawanya wengi iwezekanavyo kutoka kwa njia ya katikati ya nuru atajaribu kulisukuma kundi moja hadi katika moto wa ukaidi, na kulitumbukiza kundi lingine ndani ya maji ya barafu ya bila kujali. Kufikia hapa atatafuta kulishawishi kundi la awali kwamba mateso na misiba yao ni matokeo dhahiri ya utiifu usio kamili kwa ukweli wa sasa, na atalidhihaki kundi la mwi-sho kama lenye msimamo mkali katika mwenendo wao wa imani. {2TG46: 43.2}
Wa pekee watakaovumilia hadi mwisho watakuwa wale ambao kwa uangalifu huzichunguza hatua zao zizipeperushwe ama kwa nyongeza zake, au
43
kuondoa kwake kutoka, kwa kazi za Uvuvio. {2TG46: 43.3}
Walio na habari, hata hivyo, watafurahi badala ya kusukumwa na kushinikizwa kufa moyo. Hakuna chochote, hata mateso ya Ayubu, yatawavunja moyo, kwa maana watakuwa na hekima na wataelewa: wataijua kweli, nayo kweli itawaweka huru kutoka kwa mitego ya Shetani. Watakumbuka kwamba yule mtu kipofu (Yohana 9:1-3) alizaliwa kipofu, si kwa sababu ya dhambi ya mtu mwingine, bali tu kwamba Mwana wa Adamu atukuzwe ndani yake. Watakumbuka, pia, kwamba Lazaro na Dorkasi waliugua na kufa, si kwa sababu waliku-wa wadhambi wakuu wa siku ile, bali ili tu kwamba Mwana wa Mungu aonyeshe kwamba Yeye anazo nguvu si tu za kuponya wagonjwa ila pia kuwafufua waliokufa kwa mapenzi Yake. Watatambua kwamba mateso na hali mbaya ambazo zimewajia, haijawavuta mbali kwa Mungu, ila badala yake yamewavuta karibu Kwake; kwamba wao ni heri kuingia katika ufalme, maskini, viwete, wachechemeao, na vipofu, kuliko kwenda kwa uharibifu, matajiri wa majumba, ardhi, ng’ombe, na afya au chochote. {2TG46: 44.1}
Kwa machozi ya shangwe kuhusu Yeye kumsamehe dhambi zake kubwa, Mariamu Magdalene akaisafisha miguu ya Mwokozi wake, na kuifuta kwa nywele zake, kisha akakivunja kibweta cha marhamu ya thamani, akatia mafuta kichwani Mwake kwa mafuta yake. Wakati yote hayo yalipokuwa yakifanyika, mikono ya tamaa ya Yuda ilikuwa ikitetema kwa bei yake ili kunenepesha pochi yake, ingawa kwa wakati uo huo alikuwa kwa ujanja akidai upendo wa kina kwa maskini! Taaluma hii ya kinafiki, wakati akiegemea kifua chake,
44
kwa mfano “pamoja na sauti za njiwa,” alitaka kupasisha kama upendo wa kweli kwa wengine, kwa kumshtumu Mariamu kwa ubadhirifu na hasara, na Yesu kwa ubatili na uharibifu. {2TG46: 44.2}
Walio na habari na wenye kufahamu watawatambua ndugu waongo kama hao kati yao, na watajua kwamba ikiwa Mungu anawataka waaminifu Wake wawe wagonjwa, wataugua kwa furaha kwa ajili Yake; kwamba iwapo Anawataka wawe na afya, watalisifu jina Lake takatifu kwa afya na nguvu kuwawezesha kutenda jambo kwa ajili ya wanyonge, walemavu, wagonjwa, na wanaoteseka; kwamba ikiwa Anawataka wafe, basi hawawezi kuishi na watakufa kwa furaha; kwamba iwapo Yeye anataka waishi, hawawezi na hawatataka kufa; kwamba chochote Atakacho, hiki ndicho na atakichukua kwa furaha. Tumaini lao litakuwa katika Yeye tu. Wataziba masikio yao kwa wote ambao kwa njia moja au nyingine hutafuta kuikataa kazi ya Ukweli leo; hawatasikiliza fitina; watakuwa na imani kwamba Mungu ndiye kiongozi wa kazi, kwamba Yeye Mwenyewe anaishughulikia kazi Yake. Watajua kwamba wote watakaobaki katika mashimo ya uongo na udhalimu mwishowe wataingia kwenye “shimo la kuzimu” la uharibifu. {2TG46: 45.1}
Mafunzo, pia, kutoka kwa majaribu ya Ayubu yatakuwa ya kujifunza, matumaini, na imani kwa ajili yao. Wa-taelewa, na kuzingatia vyema ukweli, kwamba walikuwapo kina Ayubu kabla ya Ayubu wa Biblia, kwamba walikuwapo Ayubu tangu kwake, kwamba wapo kina Ayubu leo, na kwamba watakuwapo kina Ayubu hadi Ufalme utakapokuja. Imani yao kwa Mungu itakuwa katika kweli na
45
imani, iwe kwa pigo au ole, katika ugonjwa au kifo, na hakuna kitakachoweza kuwatoa kwa ujumbe wa Mbingu wa siku hiyo. Watajua kwamba utakuwa ama maisha yao au kifo chao, na kwa uzima wataambata. Ha-watapatikana wakinung’unika, wakitilia shaka, wakimtuhumu, au kukata tamaa, maana lolote fungu lao wakiwa ndani ya ukigo wa Mungu, watajua kwamba ni mapenzi Yake kwao. Kila mmoja wao kwa moyo na roho na kwa hakika watasema: {2TG46: 45.2}
“Nitayainua macho yangu niitazame milima, Msaada wangu utatoka wapi? Msaada wangu u katika Bwana, Ali-yezifanya mbingu na nchi. Asiuache mguu wako usogezwe; Asisinzie akulindaye; Naam, hatasinzia wala hatalala usingizi, Yeye aliye mlinzi wa Israeli. Bwana ndiye mlinzi wako; Bwana ni uvuli mkono wako wa kuume. Jua hal-itakupiga mchana, Wala mwezi wakati wa usiku. Bwana atakulinda na mabaya yote, Atakulinda nafsi yako. Bwana atakulinda utokapo na uingiapo, Tangu sasa na hata milele.” Zab. 121:1-8. {2TG46: 46.1}
Katika nuru iliyoongezeka sasa inayoangaza kwa swala la kubishaniwa sana la lugha na miujiza mingine, yeyote asiendelee tena gizani, akose, au achangayikiwe kuhusu asili, sifa, na kusudi la nguvu ya kweli ya kuten-da miujiza, na wakati wa udhihirisho wake. La kusikitisha kusema, hata hivyo, umati wa watu ambao hawana habari na waliofahamishwa visivyo wataendelea kunaswa wanapodakia ndoano zenye chambo za ahadi za miujiza zikining’inia kwa
46
mwaliko kutoka kwa wale wanaoitwa eti watenda kazi wa miujiza hapa, pale, na kila mahali, na hivyo kutoka kwa mbaya hadi mbaya zaidi, wakiponda muda wao na pesa zao, uhai wao na afya yao, tumaini lao na imani yao. {2TG46: 46.2}
Hakuna watakatifu watakaosali, kisha wastaajabu iwapo Mungu amesikia na kujibu sala zao. Watajua na kufurahi katika imani kwamba Yeye amesikia na kuwajibu kwa njia Yake mwenyewe, hata ingawa litakuwa kinyume kabisa na lile waliloliomba. Watafanya lile wanaloweza katika njia ya Mungu, wapokee msaada ambao Yeye hutoa, na kujua kwamba ni “heri kumkimbilia Bwana kuliko kuwatumainia wanadamu.” Zab. 118:8. {2TG46: 47.1}
Kwa sababu wakati wa Mungu kulikweza kundi lolote la watu wenye wonyesho wa nguvu ya kufanya miujiza bado haujafika, ingawa hakika unajongea upesi sana, na kwa sababu ninyi ndugu mnajua unabii kuhusu mada hii, basi iwapo mtatii, mtakuwa na bahati na furaha namna gani kujiokoa kutokimbia hapa na pale kutafuta nguvu ya kufanya miujiza ambapo hakuna ya kweli. {2TG46: 47.2}
Ikiwa ninyi, ndugu, mkikaa ndani ya ukigo wa Mungu wa ufunuo uliovuviwa, na kutembea Naye kama alivyofanya Henoko wa zamani, mtakuwa Naye kando yenu kila hatua ya njia. Kwa hivyo mzigo wako wowote, mwachie Yeye, Naye Mwenyewe atakubebea ili ushinde. Ujue ya kwamba amesikia maombi yako, na kwamba atakupa ombi lako Anavyoona inafaa kutekeleza mpango Wake
47
kwa ajili yako na kwa injili Yake leo. {2TG46: 47.3}
Wadaku wa miujiza na wawindaji wa miujiza, wakaidi wote, kumbuka, wanaweza kuwa wataka mapinduzi hatari, tayari kuhujumu kila kitu kisicho sawa na fikira zao. Vinywa vilegevu na vinavyotoa sauti vitajaribu kuti-kisa imani yetu sisi sote. Wale, ingawa, ambao hubeba mzigo mzito wa kulisha kundi “chakula kwa wakati wake” watakuwa walengwa wakuu wa Ibilisi. Kwa wakati kama huu, hawa wafuasi wa Mungu waliojitolea wa-tafaidika zaidi na ushauri wa Bwana: {2TG46: 48.1}
“Msimwamini rafiki, msimwekee kiongozi tumaini; ilinde milango ya midomo ya kinywa chako ili mkeo alalaye kifuani mwako asijue habari. Kwa maana mwana humwaibisha babaye, na binti huondoka ashindane na mamaye; na mwanamke aliyeolewa hushindana na mavyaaye; adui za mtu ni watu wa nyumbani mwake mwenyewe. Lakini mimi, nitamtazamia Bwana; nitamngojea Mungu wa wokovu wangu; Mungu wangu atanisikia.” Mika 7:5-7. {2TG46: 48.2}
Itagunduliwa kwamba kutakuwa na sauti maelfu, zingine kutoka kwa wanaojidai ni waamini, na zingine kutoka kwa wale wanaopigana dhidi ya imani ya watakatifu, sauti moja ikishutumu jambo moja, na nyingine ikishtumu jambo lingine, na lile mmoja anakemea, mwingine analiidhinisha. Lakini zinaposhikiliwa karibu na nuru ya neno la Mungu, falsafa zao mkorogo zote na manung’uniko, mipango yao iliyotengenezwa ya wana-damu na maoni ya kimwili, yataonekana kuwa tu ni ghasia za chuki, wivu, kiburi, maoni ya kibinafsi,
48
kinyongo, kijicho, siasa, uchoyo, ubaguzi, na kila ubinafsi mwingine. Hawa kwa kusikitisha, waliojituma wenyewe, wakiwa bado kwenye giza la kiroho, bila shaka hujiwazia kwamba wanamtumikia Mungu kwa bidii na nguvu. Lakini siku moja watagundua kwa kitisho kwamba wamekuwa wakifanya kazi dhidi ya Bwana, kama Sauli wa Tarso alivyojigundua mwenyewe. Maombi ya watakatifu yaweze kuwaamsha, na kuwaweka watende kazi kwa ajili ya Bwana, jinsi sala za Stefano zilimfanya Sauli kuwa mtume mkuu Paulo kwa wote Myahudi na Myunani. Na yeye aliye na sikio, aweze kusikia yale anenayo Roho, na ashike sana alicho nacho asije adui kwa hila akichukue kutoka kwa mkamato wake. {2TG46: 48.3}
49
Ili kuleta furaha hii isiyoneneka ya ahadi za Mungu, tarajio la vizazi, masomo haya yanachapishwa na kutum-wa bila malipo au wajibu kwa wote wanaotaka kuwa nayo. Tuma jina na anwani yako kwa Shirika la Uchap-ishaji la Ulimwengu, Kituo cha Mlima Karmeli, Waco, Texas. {2TG46: 50.1}
50
Usiyakose Manufaa Juu Ya Hili
Iwapo haujatuma kwa ajili ya nakala yako iliyotangazwa na iliyojadiliwa sana kijitabu cha afya cha kurasa 96 (“Kabari Inayoingia”) ambacho kimefanya uamsho mkubwa katika dunia ya Waadventista na ambacho kimeli-weka Shirika la K.I. katika mwangaza, usikikose iwapo afya, nyumba, na furaha yako inamaanisha kitu kwako. Kwa maoni yetu kitabu hiki ndicho bora hatujawahi kuona juu ya suala hili. Kwa kweli tunahisi kwamba ki-metumwa na Mungu, na kwamba nakala yake inapaswa kuwa katika kila nyumba. Tumejulishwa kwamba sasa unaweza kukipata bila kuagizia. Tuma jina lako, anwani, na jina la kanisa ambalo wewe ni mshiriki (unaombwa kuchapisha), na senti 15 kwa sarafu au stempu kwa Shirika La Kabari Inayoingia La Marekani, Kituo cha Mlima Karmeli, Waco, Texas, Marekani na kitatumwa kwako. {2TG46: 51.1}
51
Jumuiya ya Wadaudi Waadventista wa Sabato
(Ushirika Huru Unaojumuisha Kanisa)
Mlima Karmeli, Waco, Texas
S.L.P. 23738, Waco, TX 76702
+ 1-254-855-9539
www.gadsda.com
info@gadsda.com
Gombo la 2, Namba 45, 46
Kimechapishwa nchini Marekani
52