fbpx

Gombo la 2 Salamu Mwafaka Namba 39, 40

Gombo la 2 Salamu Mwafaka Namba 39, 40

                                    

AMANI YA PEKEE YA MAWAZO

Hati miliki, Kimechapishwa tena 1949

Haki zote zimehifadhiwa

V. T. HOUTEFF

                                    

 

HAKI KWA NEEMA, HAKI KWA IMANI, NA HAKI YA KRISTO

ELIMU YA KIJANA MKRISTO — WAPI NA JINSI YA KUIPATA

                                    

1

ANDIKO LA SALA

Usiipime Kazi Ya Mungu Na Kigezo Cha Mwanadamu

Nitasoma kutoka katika Mafunzo ya Kristo kwa Mifano, ukurasa wa 78, aya ya kwanza: {2TG39: 2.1}

“Viongozi wakuu wa kutafakari mambo ya kidini katika kizazi hiki huvumisha sifa na kufanya ukumbusho wa wale waliopanda mbegu ya ukweli karne nyingi zilizopita. Je! Wengi hawakengeuki kutoka kwa kazi hii wakikanyagia chini ukuaji unaochipuka kwa mbegu ile ile leo? Kilio cha kale kinakaririwa, ‘Sisi tunajua ya kuwa Mungu alinena na Musa; bali mtu huyu [Kristo ndani ya mjumbe ambaye Amemtuma], hatujui atokako. Il-ivyokuwa katika vizazi vya mapema, kweli maalum kwa wakati huu hazipatikani kwa mamlaka ya kidini, ila kwa wanaume na wanawake ambao sio wasomi au werevu mno kuliamini neno la Mungu. ‘Maana, ndugu zangu, angalieni mwito wenu, ya kwamba si wengi wenye hekima ya mwilini, si wengi wenye nguvu, si wengi wenye cheo walioitwa; bali Mungu aliyachagua mambo mapumbavu ya dunia awaaibishe wenye hekima; tena Mungu alivichagua vitu dhaifu vya dunia ili aviaibishe vyenye nguvu.’” {2TG39: 2.2}

Andiko hili huagiza kuwaombea wale ambao wanaoangaliwa kuwa wenye hekima, kwa maana leo ilivyokuwa katika nyakati za zamani wanaoitwa eti viongozi wakuu wa dini kwa mkono mmoja wanavumisha sifa, wakifanya , kwa mfano, ukumbusho kwa watumwa wa Mungu wa karne nyingi za awali, ilhali kwa mkono mwingine wanawakanyagia chini wajumbe wa Mungu wa siku yao! Wao, pia, kwa kweli wanasema “Sisi tunajua ya kuwa Mungu alinena na Musa; bali mtu huyu hatujui atokako.” Tunapaswa kuomba kwamba watam-bue kosa lao la kuipima kazi ya Mungu na kigezo cha mwanadamu. Na tuombe, pia, kwamba sisi wenyewe tusi-tumbukie katika mazoea kama hayo. {2TG39: 2.3}

2

HAKI KWA NEEMA, HAKI KWA IMANI, NA HAKI YA KRISTO

ANDIKO LA HOTUBA NA V. T. HOUTEFF

MCHUNGAJI WA WADAUDI WAADVENTISTA WA SABATO

SABATO, JULAI 31, 1948

HEKALU LA MLIMA KARMELI

WACO, TEXAS

Yapo mazungumzo mengi kati yetu kuhusu “haki kwa neema” na “haki kwa imani,” pia juu ya “haki ya Kris-to.” Lakini mazungumzo haya yote yatakuwa na faida gani isipokuwa tufanye jambo ili kujua haki hizi ni nini, na jinsi ya kuzifanya ziwe zetu. Hatupaswi kwa hivyo kushindwa katika hili, na hatuwezi kushindwa iwapo tutamtafuta Bwana kwa moyo wote tunapojifunza kupitia mifano thabiti ambayo Roho wa Kweli ameweka mkononi wangu. {2TG39: 3.1}

Kwa kuanza uchambuzi nitasoma aya mbili za maandiko, kwanza kutoka katika Warumi, kisha kutoka katika Waebrania: {2TG39: 3.2}

Rum. 11:6 — “Lakini ikiwa ni kwa neema, haiwi kwa matendo tena: au hapo neema isingekuwa neema. Lakini ikiwa ni ya matendo, basi si neema tena; ama sivyo matendo si matendo tena.”

Tumeitwa katika uteuzi wa Mungu, lasema andiko, si kwa sababu ya matendo yetu mema, bali kupitia katika neema ya Mungu. Tumealikwa, kwa hivyo, kuwa Wakristo, wana wa Mungu, si kwa sababu tunastahili kufany-wa watoto Wake, ila kwa sababu yaupendeleo Wake kwetu. Hakika, hamna njia nyingine ambayo tunaweza

3

kuokolewa, kwa maana sisi sote tumetenda dhambi na, kwa hivyo, tunawezaje kuokolewa isipokuwa Yeye, kupitia kwa neema Yake, atusamehe dhambi zetu na kutuanzisha upya? Hii ndio huitwa kuzaliwa mara ya pili, jumla yake ni kwamba hatustahili sifa yoyote kuja katika nyumba ya Mungu. Sifa ni Yake. {2TG39: 3.3}

Kwa kuzaliwa kwetu kiasili sisi huzaliwa wenye dhambi, lakini kwa kuzaliwa kwetu kiroho tumezaliwa wenye haki. Maadamu tumezaliwa wenye dhambi huitumikia dhambi, ila maadamu tumezaliwa wenye haki hui-tumikia haki. Hivyo sio kwa matendo, bali kwa “neema” kwamba tuko jinsi tulivyo. {2TG39: 4.1}

Ebr. 11: 1 — “Basi imani ni kuwa na hakika ya mambo yatarajiwayo, ni bayana ya mambo yasiyooneka-na.”

Kwa imani, si kwa kuona, tunajua kwamba sisi ni wana wa Mungu, raia wa serikali Yake. Na kwa hivyo tunajitiisha kwa maagizo na sheria Zake. Kwa hivyo tunamheshimu na kumcha Yeye kama Mwokozi na Mfalme wetu. {2TG39: 4.2}

Hebu sasa kwa mfano turudi nyuma kwa siku ya Nuhu. Nuhu aliishi katika ulimwengu mwovu sana, mna-vyojua. Ulikuwa mwovu sana kwamba, jinsi Mungu alivyo mwenye huruma, hangaliweza kujizuia Mwenyewe uovu ulipokuwa ukiendelea. Mwishowe alimwamuru Nuhu kujenga safina, na akaahidi kwamba wote, iwe ni watakatifu au waovu, ambao wangeingia ndani ya safina wangepata ukombozi kutoka kwa gharika ya kutisha. Kwa sababu hawakustahiki upendeleo kama huo, walipewa, kwa hivyo, ukombozi kutoka kwa gharika kupitia tu “haki ya neema” — wangepokea sifa ya haki na kupewa uzima ambao hawakustahili. Hivyo tunaona “neema” ikichukua nafasi ya kuwaokoa wadhambi hata nyuma katika siku ya Nuhu. Na hivyo, “na dhambi ilipozidi, nee-ma ilikuwa nyingi zaidi.” Rum. 5:20. {2TG39: 4.3}

4

Katika wakati wa Abrahamu, pia, miaka 400 tu baada ya gharika dunia ilikuwa imezama kabisa katika ibada ya sanamu, na Mungu alimwamuru Abrahamu atoke katika nyumba ya baba yake, atoke katika nchi yake ya kuabudu sanamu, na aende katika nchi nyingine, nchi ambayo ingekuwa kwa ajili yake na watu wa Mungu tu. Na maadamu mtu yeyote, mzuri au mbaya, aliyejiunga kwa Abrahamu na Mungu wake waliruhusiwa kwa uhuru kuingia katika Nchi ya Ahadi kama vile walioishi kabla ya gharika walivyoruhusiwa kuingia ndani ya safina, wao pia, kwa hivyo, walipewa “haki kwa neema”; yaani, walipendelewa kuchukua msimamo wao kwa Mungu na Abrahamu, na kushiriki baraka, lakini sio kwa sababu ya matendo yao yoyote mazuri. Baada ya kuvumilia hadi mwisho, Abrahamu, ambaye imani yake haikushindwa, akawa baba wa wote ambao kupitia “haki kwa neema” hupata “haki kwa imani.” Hivyo unaona kwamba “haki kwa neema” hutuongoza hadi kwa “haki kwa imani,” ambayo thawabu yake ni, “haki ya Kristo.” {2TG39: 5.1}

Baadaye katika historia ukaja wakati kwamba awaye yote, mzuri na mbaya sawasawa, alijiunga na Kuhama kutoka Misri, aliokolewa kutoka kwa mabwana-kazi wa Farao na kwa jeshi lake lililowaandama. Ukombozi huu hawakuupata kwa sababu walistahili ukombozi, lakini kwa sababu ya “neema” ya Mungu kwao. (Angalia Eze-kieli 20:1-8.) Hivyo “wote…walikuwa chini ya wingu, wote wakapita kati ya bahari; wote wakabatizwa wawe wa Musa katika wingu na katika bahari; wote wakala chakula kile kile cha kiroho; wote wakanywa kinywaji kile kile cha kiroho: kwa maana waliunywea Mwamba wa kiroho uliowafuata: na Mwamba ule ulikuwa ni Kristo.” 1 Kor. 10:1-4. Naam, kupitia “haki kwa neema” hakuna aliyetengwa asishiriki baraka zilizotolewa wakati huo. {2TG39: 5.2}

5

Wakishapewa “haki kwa neema” ya kutosha kuivuka bahari, na wakishaingia jangwani, walipewa basi nafasi bora zaidi ya kudhihirisha “haki kwa imani.” Lakini ni wale tu ambao waliidhihirisha “haki kwa imani” waliishi na wakaingia katika Nchi ya Ahadi. Wale, hata hivyo, ambao hawakuitumia “imani” jangwani kuliko walivyofanya huko Misri waliangamia nyikani. {2TG39: 6.1}

Mwishowe, ukaja wakati wa waaminifu kuimiliki nchi. Na hivyo ikawa kwamba ni wale tu ambao yao “haki kwa imani” iliwategemeza, waliuvuka Mto Yordani. Wengine hawakuweza. Na kwa manufaa yetu Mtume ameuacha ushauri huu: “Basi, ikiwa ingalipo ahadi ya kuingia katika raha Yake, na tuogope mmoja wenu asije akaonekana ameikosa. Maana ni kweli sisi nasi tumehubiriwa habari njema vile vile kama hao; lakini Neno lile lililosikiwa halikuwafaa hao, kwa sababu halikuchanganyika na imani ndani yao walioisikia.” Ebr. 4:1, 2. {2TG39: 6.2}

Kufikia hapa katika uchambuzi wetu tumeona kwamba Mungu hana ubaguzi, kwamba Yeye amejitahidi ku-waokoa watu wote nyakati zote kwa njia ile ile ambayo Yeye anajaribu kutuokoa sisi; ya kwamba Yeye hajifanyii majaribio — sio kutuokoa kwa njia moja na wengine kwa njia nyingine. {2TG39: 6.3}

Ufalme mwishowe ulianzishwa katika Nchi ya Ahadi na watu waliachwa waendelee katika “haki kwa imani.” Lakini kama nyakati za zamani “imani” ilififia tena, na taifa hilo lilikuwa la uovu usioweza kuvumilika, — la uovu sana hivi kwamba Mungu hakuweza kuvumilia tena liitwe kwa jina Lake likiwa linakaa katika nchi Yake. Mara moja hekalu na ikulu — vya kiroho na vya nje– vilitandazwa chini, na watu

6

wakuchukuliwa mateka. {2TG39: 6.4}

Mungu hata hivyo akawashikilia watu Wake jinsi ambavyo mama huwashikilia watoto wake, na baada ya mi-ongo saba, akiwa amewapatia mara tena haki kwa neema, Mungu aliwapa fursa ya kurejea katika nchi yao am-bapo walifurahia uamsho na matengenezo, lakini tu kwa muda kidogo. Badala ya kuendelea katika “haki kwa imani,” walianguka kutoka kwa “neema” na wakawa wabaya mara saba zaidi ya watangulizi wao. {2TG39: 7.1}

Hivyo ilikuwa kwamba iwapo wakati huo Mungu angaliweza kumwokoa mtu mmoja wa taifa Angeweza kufanya hivyo tu kwa kutoa nafasi nyingine ya “neema.” Mara hii Yeye alitoa zawadi ya Mwanawe wa pekee, Yesu Kristo, Mwokozi ambaye dhambi zetu sote ziliwekwa juu Yake. Na hivyo, wanyonge na waovu jinsi walivyokuwa wote Wayahudi na wa Mataifa, wote walialikwa kwa zawadi kubwa mno ya “neema,” ile neema ambayo uzima wa Mwana wa Mungu tu ndio unaweza kutoa. Mitume wenyewe hawakuwa kwa tendo lao jema lolote, bali kupitia zawadi hii ya “haki kwa neema,” walipewa fursa ya kushiriki “haki kwa imani.” {2TG39: 7.2}

Na kwa hivyo wasio waovu, waasi wa sheria ya Mungu, wamealikwa siku zote kupitia “haki kwa neema” kuingia katika “haki kwa imani,” haki ya pekee ambayo kwa kweli hupokea thawabu ya “haki ya Kristo” na ya uzima wa milele. “Sasa,” unasema Uvuvio, “mwenye haki ataishi kwa imani: naye akisitasita, roho Yangu haina furaha naye.” Ebr. 10:38. Mwenye haki, unaona, huishi kwa imani, lakini mwovu kwa neema. “Neema,” unaona, sio mguso wa mwisho wa wokovu. {2TG39: 7.3}

7

“Neema” ukiongeza “imani,” ukiongeza “haki ya Kristo,” ijara yake ni uzima wa milele. {2TG39: 8.1}

Sheria, zaidi ya hayo, haiokoi. Huihukumu dhambi na kudumisha haki. “Kwa sababu hakuna mwenye mwili atakayehesabiwa haki mbele Yake kwa matendo ya sheria; kwa maana kutambua dhambi huja kwa njia ya she-ria.” Rum. 3:20. Kwa kuwa tayari ni mdhambi, mwanadamu kwa hiyo sheria amehukumiwa kifo. Kwa “neema” tu, kwa hivyo, anaweza kuwekwa huru kutoka kwa hukumu ya sheria. Ndiposa, mdhambi, ni mvunja sheria, na mwenye haki ni mtunza sheria. “Neema,” kwa hivyo, humsamehe mdhambi, humtoa gerezani, kwa mfano, na humpa nafasi nyingine ya kushinda dhambi; lakini “imani” humdumisha akiwa huru. Jumla ya mambo ndio hii: “Haki kupitia neema” ni haki kupitia msamaha, ilhali “haki kupitia imani” ni haki kupitia mwenendo mwema, na hutiwa taji kwa “haki ya Kristo.” {2TG39: 8.2}

Kusisitiza: “Neema” husamehe dhambi zetu na kutuweka huru — hutupatia nafasi nyingine ya kuyafanya mai-sha yawe yanavyopaswa kuwa. Kwa hivyo, iwapo u chini ya “neema” haupo chini ya sheria, kwa sababu “nee-ma” imekufanya huru kutoka kwa adhabu ambayo sheria huweka. {2TG39: 8.3}

Baada ya kushindwa kufikia “haki kwa imani,” Wayahudi walianguka tena kutoka kwa “neema”; na kwa she-ria wakiwa wamehukumiwa kifo cha milele, walipewa tena “neema” — nafasi ya pili — kupitia kifo cha Mwana wa Mungu. Wale waliojitokeza kwa“neema,” walikuja katika kanisa la Kikristo tangu hapo wasalie huru, na ha-wangetenda dhambi tena isipokuwa kwa kosa, mkasa, au kwa ukosefu wa maono, dhambi ambazo tunasame-hewa iwapo hatuwezi kudumu

8

ndani yake. {2TG39: 8.4}

“Watoto wangu wadogo,” unasema Uvuvio, “nawaandikia haya, ili kwamba msitende dhambi. Na kama mtu akitenda dhambi, tunayemwombezi kwa Baba, Yesu Kristo mwenye haki: Naye ndiye kipatanisho kwa dhambi zetu: wala si kwa dhambi zetu tu, bali na kwa dhambi za ulimwengu wote. Na katika hili tuwajua ya kuwa tu-memjua Yeye, ikiwa tunashika amri Zake. Yeye asemaye, Nimemjua, wala hazishiki amri Zake, ni mwongo, wa-la kweli haimo ndani yake. Lakini ye yote anayeshika Neno lake, kwa kweli upendo wa Mungu umekamilishwa: kwa hivyo tunajua ya kuwa sisi tumo ndani yake.” 1 Yohana 2:1-5. {2TG39: 9.1}

Kanisa la Kikristo, ingawa, halikuendelea kwa muda mrefu katika “neema,” ila nalo, pia, katika nyakati lilian-guka chini sana kuliko kanisa la Kiyahudi. Lazima jambo lilihitajika kufanywa kwa ajili yake pia ikiwa yeyote wa washiriki wake angefanywa kuwa huru, na iwapo Mungu angeendelea kuwa na kanisa kwa dunia. Bila sha-ka, “kitu” hiki hakikuwa kingine isipokuwa Matengenezo ya Uprotestanti. Lakini kwa sababu sote tunajua kwamba Matengenezo hayajatimiza kusudi lake lililowekwa na Mungu, halijafikia umoja na imani ambayo Kani-sa lilifurahia siku ya Pentekoste, ni dhahiri kwamba jaribio lingine la uamsho na matengenezo ni hitaji la lazima kabisa. Ila ili kujua haya yote uhakika, lazima tulielekee “neno la unabii lililoimara,” kwa nabii Ezekieli. {2TG39: 9.2}

Ezek. 4:1, 2 — “Wewe nawe, mwanadamu, jipatie tofali uliweke mbele yako, kisha, chora juu yake mfano wa mji, yaani, Yerusalemu; ukauhusuru, ukajenge ngome juu yake, na kufanya boma juu yake; ukaweke makambi juu yake, na kuweka magogo ya kuubomoa yauzunguke pande zote.”

9

Hapa nabii aliamriwa kuuchora mji, Yerusalemu — mji mkuu wa kanisa. Yerusalemu huu, bila shaka, sio Ye-rusalemu halisi wa kijiografia, lakini mji ambao unawakilisha ule ambao Yerusalemu wenyewe ulisimamia — Ka-nisa lililotawanywa kote kote katika nchi za “Mataifa.” Zaidi ya hayo, Ezekieli mwenyewe aliambiwa kwamba mfano huu unalihusu kanisa likiwa limetawanyika kati ya Mataifa. (Tazama Ezek. 4:13.) Isitoshe, Ezekieli ali-amriwa kuuzingira, ili auteke! Sasa, kwa sababu Yerusalemu huu unawakilisha Kanisa likiwa kati ya Mataifa, na maadamu Mungu anamwagiza mtumwa Wake mwenyewe, nabii, kuuzingira, kuteta dhidi yake, na kuuteka, kwa hivyo ni dhahiri kwamba Kanisa, Yerusalemu ambao umeonyeshwa hapa, umeonyeshwa kama uliovutwa mbali na Mungu, na ya kwamba Mungu anajitahidi kuuokoa, kutekeleza matengenezo kati yake. Maana kwa kazi hiyo, basi, ndio kuuhusuru kwa Ezekieli. {2TG39: 10.1}

Mwishowe, kwa sababu kanisa la Kikristo, Yerusalemu, mbali na eneo lake halisi la kijiografia, lilishambuliwa hivyo kwa mara ya kwanza katika historia, au kuhusuriwa, na Martin Luther — na Mageuzi ya Uprotestanti — utimizo wa unabii huu bila shaka huanza na Luther. Ukweli huu utaonekana katika sura yote tunapoendelea kui-chambua aya kwa aya. {2TG39: 10.2}

Aya ya 3 — “Kisha ukajipatie bamba la chuma, ukalisimamishe liwe ukuta wa chuma kati ya wewe na mji huo; ukaelekeze uso wako juu yake, nao utahusuriwa, nawe utauhusuru. Hili litakuwa ishara kwa nyumba ya Israe-li. ”

Ukuta wa chuma, ulioonyeshwa kwa bamba la chuma, ni nembo kamili ya mtengo ambao

10

ulikuwepo kati ya Luther na ulioitwa eti Yerusalemu, Kanisa. Hii ilikuwa ishara, sio kwa Yuda, ufalme wa uaki-si wa kabila mbili kati ya Mataifa ila kwa Israeli, kwa washiriki wa ufalme wa uakisi wa kabila kumi wakiwa wametawanywa kati ya mataifa. {2TG39: 10.3}

Aya ya 4, 5 — “Tena lala chini kwa ubavu wako wa kushoto, ukaweke huo uovu wa nyumba ya Israeli juu yake; kwa kadiri ya hesabu ya siku utakazolala juu yake, kwa kadiri hiyo utauchukua uovu wao. Maana nimekuagizia miaka ya uovu wao iwe kwako hesabu ya siku, yaani, siku mia tatu na tisini; ndivyo utakavyouchukua uovu wa nyumba ya Israeli.”

Kuweka uovu wa mtu juu ya mtu mwingine, ni kumweka huru mdhambi kutoka kwa adhabu anayostahili. Ni tendo ambalo humpa mdhambi “haki” ambayo hajaipata, na hili ndilo Uvuvio huita “haki kwa neema.” Awali uovu wa Wayahudi uliwekwa juu ya Kristo, na taifa lilipewa nafasi ya kutoka nje ya kifungo chake cha kifo, kwa mfano, na kusimama huru katika Kristo. Wengi, lakini sio wote, wakati huo walijipatia hii “haki kwa nee-ma” na kuingia katika “haki kwa imani.” Hii “Neema” ile ile, unaona, ilitolewa tena kwa kanisa katika karne ya kumi na sita, maana kuuweka uovu wa nyumba yote ya Israeli juu ya Ezekieli humaanisha kichele sawa na kuyaweka maovu yetu sisi sote juu ya Kristo. {2TG39: 11.1}

Neema hii kupitia Ezekieli inaendelea siku — miaka 390 (Ezek. 4:6). Baada ya kipindi hiki cha wakati, nyum-ba ya Israeli, makanisa ya Kiprotestanti, yanaubeba uovu wao wenyewe; yaani, baada ya kipindi hiki cha muda kumalizika, basi “neema” hiyo iliyorefushwa inakoma na haitakuwapo nyingine. {2TG39: 11.2}

11

Ezekieli basi hazibebi dhambi zao tena. Wakati huo ndio muda ambamo wanapaswa kuishika sana “haki ya imani” iwapo watatuzwa “haki ya Kristo” pamoja na uzima wa milele. {2TG39: 12.1}

Aya ya 6, 7 — “Tena utakapozitimiza hizo, utalala kwa ubavu wako wa kuume, nawe utauchukua uovu wa nyumba ya Yuda; siku arobaini, siku moja kwa mwaka mmoja, nimekuagizia. Nawe utauelekeza uso wako, uelekee mazingiwa ya Yerusalemu, na mkono wako utakuwa haukuvikwa nguo, nawe utatoa unabii juu yake.”

Ezekieli alilala upande wake wa kulia, sio tu kwa uovu wa nyumba ya Israeli, lakini pia kwa uovu wa nyumba ya Yuda na hivyo kuubeba uovu wao, pia, kwa miaka arobaini. Na kwa hivyo nyumba zote mbili (Jumuiya ya Ukristo wote), wanapewa nafasi sawa, fursa sawa. Moja huja kwanza katika wakati, na ile nyingine mwisho. Miaka mia tatu na tisini ya “neema” inapeanwa kwa ya awali, na miaka 40 kwa ya mwisho, jumla ya miaka 430. Katika kipindi hiki cha wakati wanapaswa kushinda dhambi, na mwishowe kufikia “haki kwa imani,” na ku-tuzwa “haki ya Kristo.” Mwaka haswa ambao kipindi hiki cha miaka 430 huanzia, tutaona tunapoendelea na uchambuzi wetu. {2TG39: 12.2}

Aya ya 7, 8 — “Nawe utauelekeza uso wako, uelekee mazingiwa ya Yerusalemu, na mkono wako utakuwa haukuvikwa nguo, nawe utatoa unabii juu yake. Na tazama, nitakutia pingu, wala hutageuka toka upande mmoja hata upande wa pili, hata utakapozitimiza siku za mazingiwa yako.”

12

Kutovikwa nguo kwa mkono wa Ezekieli, bila shaka, humaanisha kwamba nguvu ya Matengenezo itaoneka-na, na dhambi za Yerusalemu zitafunuliwa — zitatangazwa dhidi yake. {2TG39: 13.1}

Isitoshe, mambo yaliyonenwa hapa hakika yatatukia, maana Ezekieli amefungwa chini ili asiweze kugeuka na kuupindua mfano. Hawezi kuinuka apendavyo, mpaka atimize amri ya Mungu, hadi amezikamilisha siku za ku-husuru kwake. Kisha mwishoni mwa wakati huu atasimama na tangu wakati huo na kuendelea kumwacha kila mtu auchukue uovu wake. Ezekieli, kwa hivyo, wakati amelala chini anawakilisha hali katika Matengenezo tan-gu wakati wa Luther hadi mwisho wa miaka 430. Kisha Ezekieli anasimama na kufanywa mlinzi: “Mwanadamu, Nimekuweka kuwa mlinzi kwa nyumba ya Israeli: basi ulisikie Neno hili kinywani Mwangu, ukawape maonyo Yangu.” Na kwa sababu unabii huu sasa umefunuliwa kwa mara ya kwanza, Ezekieli, bila shaka, ni mfano maalum wa juhudi hii ya mwisho ya uamsho na matengenezo, wa juhudi baada ya Ezekieli kukamilisha kulala chini na wakati yeye amesimama na yuafanya kazi. Kwa hivyo, juhudi ile ile ambayo Luther aliweka katika kar-ne ya kumi na sita itatekelezwa kwa namna kubwa sasa katika karne ya ishirini, maana hiyo ndio amri kwa nabii. {2TG39: 13.2}

Tofauti kati ya Matengenezo wakati wa miaka 430 na yale yaliyofuata, ni hii: Wakati wa miaka 430 “neema” ilidumu siku nyingi, ilhali baada ya kipindi hiki cha wakati kupita, na wakati Ezekieli amesimama, wale ambao wanashindwa kufikia “haki kwa imani” wenyewe watalipa gharama ya dhambi zao. Dhambi zao hazijaendelea kuwekwa kwa Ezekieli, na Ezekieli haendelei kulala chini na kutofanya kazi;

13

hawataendelea kusamehewa kwa sababu ya kutokujua baada ya onyo hilo kusikika masikioni mwao, kwa maana Ezekieli anaambiwa wazi: {2TG39: 13.3}

“Mwanadamu, Nimekuweka kuwa mlinzi wa nyumba ya Israeli; basi sikia neno hili litokalo katika kinywa Changu, ukawape maonyo haya yatokayo Kwangu. Ninamwambiapo mtu mbaya, hakika utakufa; wewe usimpe maonyo, wala husemi na huyo mtu mbaya ili kumwonya, kusudi aache njia yake mbaya na kujiokoa roho yake; mtu yule mbaya atakufa katika uovu wake; lakini damu yake nitaitaka mkononi mwako. Lakini ukimwonya mtu mbaya, wala yeye hauachi ubaya wake, wala njia yake mbaya, atakufa katika uovu wake; bali wewe umejiokoa roho yako. Tena, mtu mwenye haki aiachapo haki yake, na kutenda uovu, Nami nikiweka kikwazo mbele yake, atakufa; kwa sababu hukumwonya, atakufa katika uovu wake wala matendo yake ya haki aliyoyatenda hayata-kumbukwa; lakini damu yake nitaitaka mkononi mwako. Bali ukimwonya mwenye haki, kwamba yule mwenye haki asitende dhambi, tena ikiwa yeye hatendi dhambi, hakika ataishi, kwa sababu alikubali kuonywa; nawe umejiokoa roho yako.” Ezekieli. 3:17-21. {2TG39: 14.1}

Aya ya 9-11 — “Pia ujipatie ngano, na shayiri, na kunde, na dengu, na mtama, na kusemethi, ukavitie vyote katika chombo kimoja, ukajifanyie mkate kwa vitu hivyo; kwa kadiri ya hesabu ya siku utakazolala ubavuni mwako; yaani, siku mia tatu na tisini utaula. Na chakula chako utakachokula kitapimwa, shekeli ishirini kwa siku moja; utakila kwa wakati wake. Nawe utakunywa maji kwa kuyapima, sehemu ya sita ya hini; utayanywa kwa wakati wake.”

14

Nafaka zilizotajwa katika Ezek. 4:9 ni sita kwa idadi, na bila shaka ni mfano wa chakula cha kiroho, chakula ambacho kundi limelishwa katika ile miaka 390. Aina sita za nafaka hazimaanishi aina sita tu za kweli, mafun-disho, yaliyopeanwa kwa kundi katika kipindi cha miaka 390, lakini pia huashiria kutokamilika kwa Ukweli, maana namba saba, sio sita, huashiria namba ya Bibilia ya ukamilifu. Kwa sababu hiyo ni mafundisho ambayo wana-matengenezo walileta: {2TG39: 15.1}

(1) Fundisho la imani ambalo lililojenga dhehebu la Walutheri; (2) fundisho la Roho lililojenga dhehebu la Waprestiberi; (3) fundisho la neema ambalo lilijenga dhehebu la Wamethodisti; (4) fundisho la Ubatizo lili-lojenga dhehebu la Wabaptisti; (5) fundisho la ujio wa pili wa Kristo lililowajenga Waadventista wa Siku ya Kwanza; (6) fundisho la utakaso wa patakatifu pamoja na Sabato ya siku ya Saba lililowajenga Waadventista wa Sabato. (Madhehebu mengine yote pamoja na kuongeza, kuondoa, na mapunguzo, kwa udhahiri yamechipuka kutoka kwa madhehebu haya sita.) {2TG39: 15.2}

Mtu anaweza kuzusha hoja, ingawa ni ya kushindwa, kuhusu madhehebu yaliyotajwa hapa, lakini mtu hawezi kuzusha hoja yoyote dhidi ya ukweli kwamba haya mafundisho sita (nafaka) ni mafundisho makuu ambayo Up-rotestanti kwa ujumla umejengwa. Walakini, yawe haya au mafundisho mengine, ukweli kwamba ni sita tu, hu-maanisha kwamba ukweli wa saba utafunuliwa. Isitoshe, kweli hizi, unasema Uvuvio, ulipaswa kutolewa kwa wakati wake, kwa kipimo, — sio kila jambo linalohusu somo, — na Ukristo wote unajua kuwa hivi ndivyo ime-kuwa. {2TG39: 15.3}

Aya ya 12-15 — “Nawe utakila kama mkate wa shayiri,

15

nawe utakioka mbele ya macho yao juu ya mashonde yatokayo katika mwanadamu. Bwana akasema, Hivyo ndivyo wana wa Israeli watakavyokula chakula chao, hali kimetiwa unajisi, kati ya mataifa nitakakowafuku-za. Ndipo nikasema, Ee Bwana MUNGU, tazama, roho yangu haikutiwa unajisi; maana tangu ujana wangu hata sasa sijala nyamafu, wala iliyoraruliwa na hayawani; wala nyama ichukizayo haikuingia kinywani mwangu. Ndipo akaniambia, Tazama, Nimekupa mashonde ya ng’ombe badala ya mashonde ya mwanadamu, nawe utakipika chakula chako juu ya hayo.”

Kwa sababu ile keki ya shayiri iliyopiga na kuharibu hema ya Wamidiani ilitabiri msaada wa Mungu kwa ushindi wa Gideoni dhidi ya Wamidiani, hivyo nafaka ambazo huliwa kama mikate ya shayiri huashiria kwamba kweli zilizopokelewa zilikuwa za Roho, za asili ya Kiungu. Katika uokaji wake, hata hivyo, ndipo pale sehemu isiyofaa huingilia, maana Uvuvio huonyesha wazi kwamba hii iliokwa kwa “mashonde” badala ya kwa kuni, ikimaanisha kwa dhati kwamba kweli hizo zilitiwa unajisi na watu walipokuwa wakiziandaa kwa ajili ya kundi. Na ni kipi kingine kingeweza kuwa kuandaa isipokuwa kuongeza, kuondoa, kupunguza, kupotosha apendavyo mtu fulani tu, na matumizi mabaya ya watu ambao hawajavuviwa ambao huhutubu kwenye mimbari juu ya ma-fundisho haya, na ambao huandika zinazoitwa eti kweli safi za Bibilia na kuwakabidhi watu? {2TG39: 16.1}

Hakuna siri katika hili, kwa maana kila mtu anajua kwamba pepo za mafundisho zinazovuma kutoka pande zote, moja likipinga lingine, yote hayawezi kuwa ukweli safi wa Bibilia. Sehemu pekee ya kushangaza ni kwam-ba Uvuvio uliliona kimbele sana, na kwamba hakuna mtu aliyeligundua kabla Uvuvio Wenyewe kulifunua. {2TG39: 16.2}

Mungu, kwa kweli, hashiki hili

16

dhidi ya mtu yeyote, maana Yeye anasema: “Hivi ndivyo wana wa Israeli watakavyokula chakula chao hali ki-metiwa unajisi kati ya Mataifa, Nitakakowafukuza.” Ezek. 4:13. {2TG39: 16.3}

Hivyo unabii hutangaza kwamba hicho kimekuwa chakula cha kiroho ambacho kundi limelishwa kwa miaka 390, miaka ya wakati wa Matengenezo. Na ni nani anayeweza kukana? Je! Sisi, basi, bado tunashangaa ni dhehebu gani linaeneza Ukweli usiotiwa unajisi kwa washirika wake? Unabii hutangaza kwamba hamna, maana kama hicho kilipaswa kuwa chakula cha yote katika miaka 390! Na iwapo halipati Ukweli mpya uliovuviwa na Mbingu baada ya miaka 390 kupita, basi lazima lile chakula kilichookwa kwa “mashonde” milele, na kufa kwacho. {2TG39: 17.1}

Hili, nalisema tena, lisiwe la kushangaza kwa yeyote, kwa maana kila mtu anajua kwamba kwa sababu madhehebu yote hupingana moja dhidi ya lingine juu ya mafundisho, haiwezekani yote kuwa sawa. Inaweza, hata hivyo, kushangaza kujua kwamba hakuna hata moja ambalo ni sawa. {2TG39: 17.2}

Uhaba wa hata kweli hizi zilizonajisiwa na mwanadamu, unabii hutangaza, zimeletwa kwa ulimwengu wa Kikristo ili “washangazwe,” kwamba watambue umaskini wao, hitaji lao la ukweli kamili, ili kwamba wakati Roho wa Kweli atakapokuja, Atapata maadili ya kuitika mioyoni mwa wanadamu, vinginevyo waangamizwe katika uovu wao. {2TG39: 17.3}

Ili kupata haswa mwanzo wa kipindi cha miaka 430, lazima kwanza tupate mwaka ambao kipindi hicho kili-koma, mwaka ambao Ezekeli wa uakisi alisimama na kuanza kutoa onyo, mwaka ambao Roho wa Kweli al-ikikunjua chuo na kuuleta wingi wa Ukweli uliovuviwa na Mungu,

17

safi na usiotiwa unajisi (usiookwa kwa mashonde), wala si kwa wakati na kwa kipimo, — kweli ambazo tu-mekuwa tukijilisha kutoka kwa mfululizo huu wa masomo na ambazo Jumuiya hii imechapisha kwa wingi na kwa uaminifu katika Salamu Mwafaka na vitabu vingine, na kutawanywa kote duniani kama majani ya Vuli — tukio ambalo Kanisa halijawahi kuona! Na ninaposema kama majani ya Vuli, namaanisha kwa kweli hivyo, maa-na majani haya — naam, mamilioni — yanadondoshwa kote kote kati ya Walaodekia kwa wingi, bila fedha, na bila sharti. {2TG39: 17.4}

Ujumbe huu, jinsi baadhi yenu mnavyojua tayari, ulianza kukunjua mwaka wa 1930. Hivyo, tunapoondoa mi-aka 430 kutoka 1930, tunarejeshwa hadi mwaka 1500, wakati mwito kwa Martin Luther ulikuja, wakati alipoan-za kusoma Bibilia, wakati alipoanza kujiandaa kwa kazi ya Matengenezo. Ujumbe huu, kwa hivyo, ulipangwa na Mungu Mwenyewe na kuuweka nyuma katika wakati wa Ezekieli, yote kwa manufaa yako na yangu! Ni umakini ulioje alionao Mungu! Na tulioje tusiostahiki. {2TG39: 18.1}

Kwa sababu kipindi cha miaka 430 ambacho dhambi zetu ziliwekwa juu ya Ezekieli, kimepita, sisi wenyewe, si Ezekieli, kuanzia sasa tunawajibikia dhambi zetu iwapo sasa tutashindwa kutii ujumbe wa saa ya sasa na kuif-ikia “haki kwa imani.” Ilioje muhimu, basi, kwamba tusiipuuze fursa yetu sasa tuyapokee yale ambayo Mungu hutuma, na kuifikia “haki kwa imani” ili tuweze kutuzwa “haki ya Kristo.” Hivi tu ndivyo tunaweza kutarajia kuokoka silaha za kuchinja za malaika na tuishi na kutawala pamoja na Kristo katika miaka elfu. {2TG39: 18.2}

18

Kwa mujibu wa unabii huu mpya ambao umefunuliwa haitakuwepo nafasi nyingine, unaona, hakuna fursa nyingine kwa Walaodekia, nyumba ya Yuda. Ujumbe huu kwa Walaodekia, kwa hivyo, ni ujumbe wa mwisho, nafasi yao ya mwisho! Kutazama umbele wa watu wa utakaso huu nabii Isaya aliandika: “Amka, amka; jivike nguvu zako, Ee Zayuni; jivike mavazi yako mazuri, Ee Yerusalemu, mji mtakatifu: kwa maana tokea sasa ha-taingia ndani yako asiyetahiriwa wala aliye najisi…. Jinsi ilivyo mizuri juu ya milima miguu yake aletaye habari njema, yeye aitangazaye amani; aletaye habari njema ya mambo mema, yeye autangazaye wokovu; auambiaye Zayuni, Mungu wako anamiliki!” Isa. 52:1, 7. {2TG39: 19.1}

Kwa sababu tumeona kwamba miaka 430 ilimalizika mwaka wa 1930, tunapaswa sasa kujua ni lini miaka 390 ilikoma, wakati ambapo miaka 40 ya neema ilianza. Ili kuipata tarehe hii tunaondoa miaka 40 kutoka mwaka 1930, ambayo inaturejesha mwaka 1890. Ni nini kilitukia basi kuashiria mwanzo wa miaka 40? — Hili tu: dhehe-bu wakati huo liliukataa kabisa ujumbe ambao ungeufunua ukweli wa “haki kwa imani” na “haki ya Kristo,” ukweli haswa ambao ulianza tena kufunuliwa miaka mingi baadaye, Ukweli ambao sasa tunajilisha! Mungu kwa rehema yake, kwa hivyo, aliuweka uovu wao juu ya nabii Ezekieli katika miaka hiyo 40, — aliwapa nafasi kupitia “haki kwa neema” ili waweze kupata fursa sasa kuingia katika “haki kwa imani,” na hivyo kuvuna thawabu ya “haki ya Kristo.” {2TG39: 19.2}

Hapa tunaona kwamba historia hujirudia yenyewe: Israeli ya kale iliposikiza ripoti mbaya ambayo wapelelezi kumi walileta iliwasababisha kupoteza

19

imani katika nguvu ya Mungu, na kwa hivyo, walijirudisha nyuma miaka 40 kutoingia katika Nchi ya Ahadi. {2TG39: 19.3}

Vivyo hivyo, Dhehebu, unaona, tangu mwaka 1890 hadi mwaka 1930 limekuwa likitangatanga nyikani kwa mfano. Wamekuwa, tunaweza kusema, wamewekwa kwa hukumu. Hapa ndipo unaona dhahiri kwamba kutan-gatanga kwa jadi nyikani kulikuwa mfano. Hapa mfano hukutana na uakisi. Na wao kuikataa “haki kwa imani,” unang’amua, hakukumaanisha kwamba Mungu alishindwa na ya kwamba Yeye kwa hivyo asingaliweza tena kamwe kuleta kwetu Ukweli ule ule ambao ungekuwa wao miaka arobaini iliyopita. {2TG39: 20.1}

Isitoshe, kama wale ambao katika wakati wa Musa walikataa kustawi katika imani walikufa nyikani, hivyo wale watu ambao katika miaka ya 1888-1890 waliwajibika kwa kukataa kuendelea ndani ya Ukweli, walikufa kabla Mungu kurejea nao mara ya pili. Hatimaye, kama juhudi ya pili ya kale ya kuitwaa ile nchi ilifanikiwa mara tu baada ya Akani, mtenda dhambi wa mwisho katika siku hiyo, kupigwa mawe, hivyo juhudi ya pili ya leo lazima, pia, ifanikiwe mara tu baada ya kina Akani wa leo wameangamizwa na malaika wa Ezekieli Tisa. {2TG39: 20.2}

Ni kemeo lililoje hili kwa ndugu viongozi! Ni somo lililoje kwetu! Na nafasi ndogo ilioje wanayo ikiwa wa-taendelea kwa upofu kukaidi! Walei, hata hivyo, ambao hukutana na Ukweli huu wangeweza kuwa msaada mkubwa kwao iwapo badala ya kuridhia madai yasiyofaa ya upinzani kwamba walei waache kusoma maandiko haya kwa tishio la kupoteza ushirika, wao wenyewe wangedai kutoka kwa upinzani mafafanuzi bora, au angalau ya busara sawa,

20

ya maandiko tunayochanganua badala ya kukata tamaa. Ni upumbavu kuukataa Ukweli ili kulihifadhi jina lako katika Laodekia. Afadhali kuupokea Ukweli na ulihifadhi jina lako katika Kitabu cha Uzima cha Mwana-Kondoo. {2TG39: 20.3}

Nasema ni upumbavu kuukataa Ukweli tu kwa maneno ya anavyosema hivi mtu badala ya kumwendea Mun-gu kwa sala na kutenda kulingana na kusadiki kwako mwenyewe kupitia Roho aongozaye katika Kweli yote. Kutenda vinginevyo ni kuukana muunganisho wowote wa kibinafsi na Mbingu, na kuiweka imani yako kwa mwanadamu, kuufanya “mwili kuwa kinga yako.” Isa. 2:22. Usiruhusu, kwa hivyo, adui anene uende nje ya Ukweli huu, haswa usoni pa ukweli kwamba upinzani hauna chochote kuthibitisha, chochote cha mamlaka, au rasmi, hauna chochote cha kuchukua nafasi yake. Na ni upumbavu ulioje kwa mtu kujaribu kuuhakiki Ukweli kwa akili ya upinzani! Ni jambo la busara kana kwamba ungeweza kutafuta maoni ya mwanasiasa wa Ujamhuri kuhusu tumaini lako la kuupigia Udemokrasia kura! Itaweza kuwapo busara kutafuta msaada kwa mtu ambaye haegemei upande mmoja, lakini kamwe hakuna hekima yoyote kwenda kwa mtu ambaye anaupinga vikali Ukw-eli huu jinsi makuhani, waandishi, na Mafarisayo walivyoyapinga mafundisho ya Kristo. {2TG39: 21.1}

Iwapo huoni kila jambo kwa udhahiri ambavyo ungependa, kwa nini usiupokee ushauri wa Roho ya Unabii? Acha nikusomee aya chache: {2TG39: 21.2}

“… Iwapo ujumbe unakuja usiouelewa, vumilia ili uweze kusikiza sababu ambazo mjumbe anaweza kutoa, ukilinganisha maandiko kwa maandiko, ili uweze kujua iwapo zinaidhinishwa na Neno la Mungu au la. Ikiwa utaamini kwamba msimamo uliochukuliwa hauna msingi katika Neno la Mungu,

21

ikiwa msimamo unaoshikilia juu ya suala hauwezi kupingwa, basi wasilisha sababu zako thabiti, kwa maana msimamo wako hautatikiswa kwa kukutana na makosa. Hakuna wema au ubabe kuendeleza vita gizani kuya-fumba macho yako usije ukaona, kuyaziba masikio yako usije ukasikia, kuufanya mgumu moyo wako katika upumbavu na kutokuamini usije ukanyenyekezwa na kukiri kwamba umepokea nuru kwa mambo fulani ya ukw-eli.” — Mashauri kwa Kazi za Shule ya Sabato, uk. 29. {2TG39: 21.3}

“Nuru ya thamani itangaza kutoka katika Neno la Mungu, na mtu yeyote asidhanie kuamuru ni nini kitakacholetwa au kutoletwa mbele ya watu katika jumbe za kuangazisha Atakazotuma, na hivyo kumzimisha Roho wa Mungu. Iwayo yoyote nafasi yake ya mamlaka, hakuna mtu aliye na haki ya kuizimisha nuru kutoka kwa watu. Ujumbe unapokuja katika jina la Bwana kwa watu Wake, hakuna mtu anayeweza kujizuia kutofanya uchunguzi wa madai yake. Hakuna mtu anayeweza kujimudu kusimama nyuma katika mwenendo wa kutojali na kujiamini na kusema: ‘Najua nini ni ukweli. Nimeridhika kwa nafasi yangu. Nimeweka vigingi vyangu, na sitasogezwa mbali na msimamo wangu, liwalo liwe, sitausikiliza ujumbe wa mjumbe huyu; kwa maana najua kwamba hauwezi kuwa ukweli’ Ilikuwa kutokana na kuufuata mwenendo huu hasa kwamba makanisa maarufu yaliachwa katika sehemu ya giza, na ndiyo sababu jumbe za mbingu hazijawafikia.” — Kimenukuliwa, uk. 28. {2TG39: 22.1}

“Bado upo ukweli wa thamani sana ambao utafunuliwa kwa watu katika wakati huu wa hatari na giza, lakini ni kusudi la Shetani aliloazimia kuzuia nuru ya kweli isiangaze

22

ndani ya mioyo ya wanadamu. Iwapo tungetaka kuwa na nuru ambayo imeandaliwa kwa ajili yetu, tunapaswa kuonyesha tumaini letu kwa ajili yake kwa kulichunguza kwa bidii neno la Mungu. Kweli za thamani ambazo zimekuwa hazijulikani kwa muda mrefu zitafunuliwa kwa nuru ambayo itadhihirisha thamani yake takatifu; kwa maana Mungu atalitukuza neno lake, kwamba liweze kuonekana katika nuru ambayo hatujawahi kuiona awali. Ila wale wanaodai kuupenda ukweli lazima waweze kutanua uwezo wao, ili waweze kuelewa mambo ya kina ya ne-no, ili Mungu atukuzwe na watu Wake waweze kubarikiwa na kuelimishwa. Kwa mioyo ya unyenyekevu, ili-yojishusha kwa neema ya Mungu, mnapaswa kuja kwa jukumu la kuyapekua Maandiko, tayari kuupokea kila mwali wa nuru takatifu, na kutembea katika njia ya utakatifu.” — Kimenukuliwa. uk. 25. {2TG39: 22.2}

Isitoshe, huoni kamwe dunia yote kwa kutupia jicho. Huona tu sehemu yake kwa wakati. Vivyo hivyo huwezi kutarajia kuona Ukweli wote mara moja, ila mchache tu kwa wakati mmoja. Shikilia huo mchache, na unapoen-delea kusali na kuchmbua, wote utakuwa wazi kama jua na utaanza kuelewa mada yote kwa ukamilifu. {2TG39: 23.1}

Ndugu, Dada, usiipite tena fursa yako. Tenda sasa ufanye amani na Mungu. Yakimbie sasa machukizo, na uuchukue msimamo wako kwenye mkono wa kulia wa Mungu iwapo unataka baraka Zake na uzima wa milele. “Leo kama mtaisikia sauti Yake, msifanye migumu mioyo yenu.” Ebr. 4:7. Tambua kwamba Mungu Mwenyewe anasema nawe, ya kwamba haya si maneno ya mwanadamu, si hekaya, kwamba huu ni ujumbe ambao umesalia ukiwa umetiwa muhuri katika karne nyingi, na ambao sasa umefunuliwa na kuletwa kwako kama maua mapya yaliyofunikwa umande wa majira ya hari. {2TG39: 23.2}

23

Mojawapo wa sehemu muhimu zaidi za uchambuzi huu, unaona, ni ukweli kwamba katika miaka 430 — kuto-ka 1500 hadi 1930 — uovu wetu sote umewekwa juu ya nabii wa Mungu. Nasema, kwa sababu ya “neema” hii nyingi ambayo imekuwepo katika hiyo miaka, tumeruhusiwa kuwa hapa leo. Wanadamu, hata hivyo, wame-tumia fursa ya “neema” ya Mungu, na wamekuja kufikiri kwamba Yeye ameiacha nchi, kwamba Ametuacha tu-fanye kama tunavyoweza, na tuendelee kadri tuwezavyo. Sote tutabadilisha nia zetu mara tu kuonya umbele kwa Mungu kutakuwa kumekamilika. {2TG39: 24.1}

Kwa hivyo, wale Walaodekia ambao wangeweza kujitokeza kwa fursa ya kushiriki karamu hii mpya na isiyotiwa unajisi ya “chakula kwa wakati wake,” ambao wangeweza sasa kwa mwito wa mwisho washikilie “haki kwa neema” waliyopewa tayari, — wote wanaweza ingia katika “haki kwa imani” ambayo itapewa thawabu ya “haki ya Kristo,” na hivyo kuvikwa taji kwa uzima wa milele. Bila shaka, wengine wote watalazimika kuubeba uovu wao wenyewe na kulipia adhabu yao wenyewe. Wataangamia. {2TG39: 24.2}

Kweli, unafikiri hauna haja ya kitu, lakini Mungu Ajuaye hakika anasema kwamba wewe ni “mnyonge, na mwenye mashaka, na maskini, na kipofu, na uchi,” unahitaji kila kitu. Je! Hutauchukua ushauri Wake na kuyapaka macho yako dawa ili uweze kuona? {2TG39: 24.3}

Mwishowe, wakati ujumbe wa onyo umekwishawafikia watu, basi wale ambao hawatafaidika nao, ambao hawatafanya matengenezo, — watakaoshindwa “kuugua na kulia dhidi ya machukizo yote kati yake,” — kisha inakuwa kwamba wale ambao sasa hawawezi kufikia “haki kwa imani,” watajikuta hawana “alama.” wao ndipo-sa

24

watalipia adhabu ya dhambi zao, kuangamia chini ya silaha za kuchinja za malaika. (Soma Ezekieli Tisa; Shuhu-da kwa Kanisa, Gombo la 3, uk. 266, 267; Shuhuda kwa Kanisa, Gombo la 5, uk. 210, 211.) {2TG39: 24.4}

Kwa udhahiri, nyumba ya Yuda, tangu mwaka 1930 inasimama katika hitaji lile lile kama vile nyumba ya Is-raeli ilisimama baada ya mwaka 1890. Wote sasa wanahitaji ujumbe wa leo iwapo wanatarajia kuwa na makao katika ufalme wa Mungu. Zaidi ya hayo, ni wazi kuona kwamba lile nyumba ya Yuda ilishindwa kutekeleza baada ya mwaka 1890 lazima sasa tulitimize dhidi ya magumu makubwa na kwa wakati mfupi. {2TG39: 25.1}

Mafunzo ambayo yanafundishwa katika sura hii ni haya: Kwanza imeonyeshwa kwamba kipindi cha “haki kwa neema” sasa kimepita; ya kuwa sasa tumefika wakati ambapo usalama wetu upo tu katika kutenda “haki kwa imani,” iwapo tunatarajia kutuzwa “haki ya Kristo,” na kuvikwa taji ya uzima wa milele. Funzo la pili hu-fundisha kwamba Kanisa bado hata sasa halijapata Ukweli wote, na ule lililonao umechafuliwa, “umeokwa kwa mashonde.” Hivyo hitaji kubwa kwamba tupate Ukweli Uliovuviwa kutoka kwa Kiti cha Enzi cha Mungu; maa-na tukiwa nao tumeokolewa, na bila huo tumepotea. {2TG39: 25.2}

25

ELIMU YA KIJANA MKRISTO — WAPI NA JINSI YA KUIPATA

ANDIKO LA HOTUBA NA V. T. HOUTEFF

MCHUNGAJI WA WADAUDI WAADVENTISTA WA SABATO

SABATO, NOVEMBA 13, 1948

HEKALU LA MLIMA KARMELI

WACO, TEXAS

Elimu yenye usawaziko ya kijana Mkristo i katika awamu tatu: ya maadili, ya utakatifu, na ya kidunia. Hizi hupatikana katika shule tatu tofauti: ya nyumbani, shule ya kanisa, na shule ya umma. {2TG40: 26.1}

Kila moja ya shule hizi ina jukumu lake muhimu kutekeleza kwa ustawi wa mtoto. Shule ya umma humfun-disha mtoto jinsi ya kuishi katika jamii. Shule ya kanisa humfunza jinsi ya kuingia katika uzima wa milele. Lakini shule ya nyumbani, mbali na kumfunza mienendo ya maadili, huweka msingi kwa awamu zote za elimu. {2TG40: 26.2}

Isitoshe, mtoto sio tu huanzia maisha nyumbani, lakini pia hutumia wakati wake mwingi humo. Shule ya nyumbani, kwa hivyo, huchangia jukumu muhimu sana katika kufinyanga maisha ya mtoto. Kutoka kwa hili tunaweza kuona upesi mbona nyumba iliyovunjika au isiyo na mpangilio, isiyojali haiwezi kamwe kukidhi mahitaji ya mtoto. Ni kwa muujiza tu ambapo mtoto aliyelelewa katika nyumba kama hiyo anaweza kuwa raia mzuri, anayetii sheria za taifa, na mshirika anayeheshimiwa kanisani. {2TG40: 26.3}

Naam, nasema, kwa muujiza tu anaweza kupanda hadi kileleni pa ngazi katika jumuiya ya dunia, kutosema chochote kuhusu nafasi yake finyu katika jumuiya ya Mbinguni. {2TG40: 26.4}

26

Hebu nifafanue kazi ya nyumbani: Mkulima hupanda mbegu ardhini, na hali zinazofaa hufanya iweze kuota na kuchomoza jani lake dogo kupitia udongo. Mwanzoni, hata hivyo, mmea mdogo hujilisha katika utomvu wa ile mbegu wakati ikipekecha jani lake dhaifu juu na kuzamisha mizizi yake midogo kuelekea chini. Hivyo ukiwa ndani ya ganda (nyumba) ni mmea mdogo (mtoto) ukiwezeshwa kuanza kubadilika wenyewe ili kujipatia chaku-la kutoka mchangani na mwangaza wa jua kutoka angani kudumisha uhai. Kanuni i hii hufanya kazi ndani ya nyumba: Mtoto akiwa nyumbani lazima aanzishwe polepole na kisha kuwekwa mwenyewe kikamilifu na wazazi wake. Iwapo wazazi watashindwa kutekeleza jukumu hili kwa mtoto wao, basi mtoto hatasimama kwa nafasi nzuri katika maisha ambayo Muumba ameagiza kwamba anapaswa kuwa nayo. {2TG40: 27.1}

Mifano ya Nyumba Nzuri

Katika hatua hii nitasoma kwenu jambo kuhusu shule za nyumbani zilizofanikiwa: {2TG40: 27.2}

Mwa 18:16-19 — “Kisha watu hao wakaondoka huko wakaelekeza nyuso zao Sodoma. Abrahamu akaenda pamoja nao awasindikize. Bwana akanena, Je! Nimfiche Abrahamu jambo Nilifanyalo, ikiwa Abrahamu atakuwa taifa kuu, hodari, na katika yeye mataifa yote ya dunia watabarikiwa? Kwa maana Nimemjua ya kwamba atawaamuru wanawe, na nyumba yake baada yake waishike njia ya Bwana, wafanye haki na huku-mu, ili kwamba Bwana Naye akamtimizie Abrahamu ahadi Zake.”

Ulikuwa ukarimu wa Abrahamu ambao ulileta baraka kubwa kama hiyo nyumbani kwake — wale wageni wa-tatu wa Mbinguni Ambao walithibitisha tena ahadi ya mrithi. Na tendo lake la kuwakaribisha

27

na kuwaonyesha njia ya kuelekea mjini kwa kutembea umbali fulani nao, lilisababisha malaika kumwambia utume wao wa kusikitisha kuhusu Sodoma. Hakuna nyumba, kwa hivyo, inapaswa “msisahau kuwafadhili wa-geni: maana kwa njia hii wengine wamewakaribisha malaika pasipo kujua.” Ebr. 13:2. {2TG40: 27.3}

Katika aya ambazo tumesoma muda mfupi uliopita, tunaambiwa kwamba Abrahamu alipaswa kuwa taifa kubwa na hodari kwa sababu angewaamuru watoto wake na nyumba yake kumfuata Mungu, kuishika njia ya Bwana, kutenda “haki na hukumu.” Mungu alitambua kwamba nyumba ya Abrahamu ingekuwa shule ya nyumbani ya kielelezo, na hivyo huyu Babu wa Vizazi vingi akawa “rafiki wa Mungu,” na “baba wa waaminifu.” Mungu, unaona, huwaheshimu wazazi ambao huendesha nyumba zao vyema, ambao huamuru nyumba zao kum-fuata Yeye. {2TG40: 28.1}

Tuchunguze sasa tuone ni kwa kiwango gani shule ya nyumbani ya Abrahamu ilikuwa ya kielelezo? — Mwanawe, Isaka, unajua, alikuwa karibu na umri wa miaka kumi na saba tu neno la Bwana lilipomjia Abrahamu kwamba anapaswa kumtoa mwanawe wa pekee. Baba alitii agizo hilo kwa uaminifu, na akampeleka Isaka kwenye safari hiyo ya kupimwa ya kihistoria na pia ya kuelimisha. Hadi dakika ya mwisho kabisa ndipo kijana akaambiwa kwamba yeye ndiye angekuwa mhanga wa kafara. Lakini je! Alikasirika au alipinga alipoambiwa? — La, hakika. Badala yake, alifanya yote aliyoweza kumfariji baba yake, na kwa hiari na kwa moyo mkunjufu akajilaza mwenyewe kwa madhabahu! {2TG40: 28.2}

Je! Haya yote yanamaanisha nini? — Yanamaanisha kwamba Isaka alikuwa amepokea malezi makamilifu nyumbani kwake, na kwa hivyo aliuheshimu uamuzi wa

28

baba na dini. Alikuwa mtiifu kwa Mungu wake, na mwenye imani. Akijua kwamba njia ya Mungu ilikuwa kwa maslahi yake bora, aliamua kwamba itakuwa vyema kufa kuliko kukosa kumtii Mungu au baba yake. {2TG40: 28.3}

Sasa tutaenda zaidi na tutafute mfano katika nyumba ya Isaka mwenyewe ili tuone alikuwa mzazi na mwali-mu wa namna gani. Esau na Yakobo walikuwa wanawe pacha, mnajua, na wote wawili walilelewa katika nyum-ba yake. Ikiwa utasoma kati ya aya katika kisa hiki maarufu cha Bibilia, utawapata waalimu wawili na jozi mbili za wanafunzi nyumbani mwa Isaka: Isaka alimpenda Esau, na Rebeka alimpenda Yakobo. {2TG40: 29.1}

Yakobo alikuwa msaada kwa mama yake, na kwa hivyo akajifunza jinsi ya kuandaa chakula ambacho kiliku-wa cha kupendeza na kitamu. Ndivyo aliweza kuandaa bakuli la mchuzi ambalo liliuzwa bei ya juu kuliko chakula kingine chochote kilichowahi kuuzwa. Mbali na kujifunza sanaa ya upishi, alipendezwa sana na dini, na akajiweka wa kufaa kukaa kwenye kiti cha enzi cha wazee wa imani. {2TG40: 29.2}

Kwa upande mwingine, Esau alipendezwa tu na vitu visivyodumu, na akajinyima urithi wake kwa kiti cha en-zi kwa ajili ya michezo na tamaa isiyodhibitiwa ya kula. Badala ya kuwa stadi katika majukumu yake ya kidini, akawa stadi wa kuwinda. Ndiposa urithi kwa kiti cha enzi cha waze wa imani hakikuwa na maana tena kwake kuliko bei ya bakuli la mchuzi. {2TG40: 29.3}

Ndani ya vijana hawa wawili tunaona malengo mawili yanayopingana maishani — mmoja alijiingiza michezoni, mwingine katika dini. Isaka alikuwa anajua vyema hili, lakini kwa sababu alimpenda sana Esau kuli-ko alivyompenda Yakobo, na maadamu Esau alikuwa mwanawe mkubwa, hakuona sababu ya

29

kwamba Esau asiipate hiyo baraka na kukaa kwa kiti cha enzi cha mababu. Rebeka, hata hivyo, alikuwa mwepesi kugundua kwamba Esau hakufaa kwa nafasi hiyo, na ya kwamba Yakobo angetenda vyema kwayo. Hivyo ilikuwa kwamba kwa upande mmoja Isaka alimwagiza Esau kuandaa karamu na aje kwake kubarikiwa, kwa upande mwingine Rebeka alimshauri na kumsaidia Yakobo kumwiga Esau na kuipata hiyo baraka kwa ku-tumia fursa ya uhafifu wa kuona wa macho ya baba yake. Udanganyifu huu, bila shaka, ulifaulu jinsi ulivyofan-ya kwa sababu Majaliwa yalikuwa kazini. {2TG40: 29.4}

Sasa, hebu tuone lile tumejifunza kuhusu mafunzo ya Esau na mafunzo ya Yakobo: Kwa sababu Isaka aliku-wa amefungamana sana kwa Esau, na Rebeka kwa Yakobo, na maadamu Esau alikuwa mshindwa na Yakobo alifanikiwa, je! haiwezi kuhitimishwa kwamba Rebeka alifanikiwa kumfunza vizuri Yakobo, ilhali Isaka alipuuza hitaji la Esau la kumjua Mungu na majukumu ya nyumbani ambayo yalikuwa yake? {2TG40: 30.1}

Kutoka kwa ulinganisho huu nina uhuru kusema kwamba Isaka kwa njia fulani alikuwa baba wa kutelekeza, na ya kwamba Rebecca alikuwa mama imara na mwangalifu sana. Kweli, lazima alikuwapo aina moja ya nyenzo kumlea Yakobo na nyingine kumlea Esau, lakini Esau angekuwa amekemewa; na iwapo kemeo halingemsaidia, basi asingeweza kupewa baraka. Hapana, uthabiti haupaswi kamwe kutoa nafasi kwa anasa. {2TG40: 30.2}

Ifuatayo tutachungulia katika shule ya nyumbani ambayo Yakobo mwenyewe aliendesha, na tuone matokeo yalikuwa nini. Kuzingatia kweli kwamba familia yake ilikuwa kubwa (watoto kumi na watatu kwa ujumla) kuli-ko familia za mababu zake; kwamba wanawe wote

30

walikubaliwa kuwa wazazi wa raia wa kanisa la milele; ya kwamba mwanawe, Yusufu, alijidhibiti kikamilifu, alikuza roho ya rehema, alimheshimu baba yake, akashikamana na maagizo ya Mbingu, na akapata kibali kwa Mungu na kwa mwanadamu; — Nasema kwamba kwa kweli hizi zote tunajua ya kuwa Yakobo aliipatia familia yake mafunzo bora iwezekanavyo. Kwa kumalizia, alimlea mmoja mkuu na mungwana kabisa ambaye ulimwen-gu haujawahi kuona. {2TG40: 30.3}

Naamini kwamba wakati hautaturuhusu kuangalia shule nyingine nzuri ya nyumbani, nyumba ambayo Musa alizaliwa. {2TG40: 31.1}

Kujua kwamba Abrahamu na uzao wake wangekaa katika nchi ya ugenini miaka 430 tu, mama ya Musa aling’amua kwamba wakati wa ukombozi kutoka utumwa wa Wamisri ulikuwa umekaribia katika siku yake. Lakini amri ya Farao ilidai kila mtoto Mwebrania wa kiume atupwe katika Mto Nile, na hivyo licha ya hilo ali-azimia kumficha mwanawe aliyetoka kuzaliwa. Labda, alifikiri, anaweza kuwa ndiye atakayeliongoza jeshi la Waebrania kutoka Misri na kuingia katika nchi ya ahadi, na ikiwa ni hivyo, Mungu angemwokoa. {2TG40: 31.2}

Miezi mitatu baadaye, hata hivyo, alipata kwamba hangeweza tena kumficha Mtoto Musa, na kwa hivyo ba-dala ya kubeba hatari isiyoweza kuepukwa ya kumpoteza, alitengeneza kisafina kidogo, akamweka mtoto mchanga ndani yake, na akakiweka kwa utunzi wa Mungu kwenye Mto Nile. Mungu alichukua hatamu kwa hali hiyo na mtoto akaishi. Sasa angalia muujiza: Mara tu binti mfalme alipomwona yule mtoto, alijua kwamba ni mtoto wa Kiebrania, lakini badala ya kumuacha auawe jinsi Farao alivyokuwa ameamuru, akamlea! Isitoshe, Majaliwa yalipanga kwamba yule mtoto anapaswa kulelewa katika nyumba ya Mwebrania. Hivyo

31

ilikuwa kwamba Mtoto Musa kwa Majaliwa alirudishwa kwa mama yake mwenyewe kumtunza, na gharama zote za nyumbani zililipwa kutoka katika hazina ya mfalme! {2TG40: 31.3}

Uthibitisho baada ya kushuhudia miujiza hii yote, yule mama alijua yakini kwamba Musa angekuwa mkom-bozi. Na mafunzo ya nyumbani aliyopewa katika miaka hiyo kumi na miwili na mama yake, Musa hakusahau hata kati ya askari wa kiti cha enzi kikuu cha ufalme duniani cha siku yake. {2TG40: 32.1}

Hakika, mafunzo ambayo mtu hupokea nyumbani, unaona, ndio msingi wa mustakabali wake wote. {2TG40: 32.2}

Mifano ya Nyumba Mbaya

Katika tofauti iliyopo wazi kwa nyumba hizi nzuri, nitavuta uaangalifu wako kwa shule ya nyumbani moja au mbili mbaya, na matokeo yake. {2TG40: 32.3}

Kwanza ninafikiri kuihusu nyumba ya Lutu. O, Naam, najua kwamba Lutu alikuwa mtu mkuu katika Sodo-ma, lakini hakuna mtu ambaye angesikiza rai yake usiku ule Sodoma ingepunguzwa kuwa moshi na majivu ya pepo kupeperusha mbali na kwa Bahari ya Chumvi kutulia juu yake. Hapana, si hata watoto wake mwenyewe ambao walikuwa katika nyumba zao wangemsikiliza. Mabinti zake wawili tu waliokoka moto mkubwa, eti kwa sababu malaika waliwanyakua watoke kama kinga kutoka motoni. {2TG40: 32.4}

Kushindwa kulioje ilikuwa nyumba ya Lutu! Hasara ilioje! Sababu mbili zilikuwa msingi wa yote yaliyom-pata: kwanza, kwa sababu alijenga hema yake kuelekea Sodoma; na pili kwa sababu hakujali kuilea nyumba yake katika kumcha Mungu. Isitoshe,

32

laiti Lutu angekuwa ameziongoza kwenye Kweli na haki hata nafsi kumi kutoka kwa idadi kubwa ya Sodoma, angaliweza kuiokoa Sodoma na Gomora kutoka kwa maangamizi. {2TG40: 32.5}

Hebu ninene nawe kuihusu nyumba nyingine mbaya, ile ya Eli, kuhani wa kale wa Israeli. Yeye, jinsi alivyofanya Lutu, alifanya nyumba yake kushindwa kabisa, ingawa mara kwa mara alionywa kuhusu kupuuza kwake. {2TG40: 33.1}

1 Sam. 2:27-35 — “Kisha mtu wa Mungu akamwendea Eli, akamwambia, Bwana asema hivi, Je! Mimi sikujidhihirisha nafsi Yangu kwa nyumba ya baba yako, walipokuwa katika Misri, wakiitumikia nyumba ya Farao? Je! Sikumchagua yeye katika kabila zote za Israeli, ili awe kuhani Wangu, apande madhabahuni Kwangu; na kufukiza uvumba, na kuvaa naivera mbele Yangu? Nami sikuwapa watu wa mbari ya baba yako dhabihu zote za wana wa Israeli zilizotolewa kwa moto? Kwa nini basi mnaipiga teke dhabihu Yangu na sa-daka Yangu nilizoziamuru katika maskani Yangu; ukawaheshimu wanao kuliko Mimi, mpate kujinenepesha kwa sadaka zote za watu Wangu Israeli zilizo njema? Kwa sababu hiyo, Bwana, Mungu wa Israeli, asema, Ni kweli, Nalisema ya kuwa nyumba yako, na nyumba ya baba yako itakwenda mbele Yangu milele; lakini sasa Bwana asema, Jambo hili na liwe mbali nami; kwa maana wao wanaoniheshimu Nitawaheshimu, na wao wanaonidharau watahesabiwa kuwa si kitu. Angalia, siku zinakuja, Nitakapoukata mkono wako, na mkono wa mbari ya baba yako, hata nyumbani mwako hatakuwako mzee. Nawe utalitazama teso la maskani Yangu, katika utajiri wote watakaopewa Israeli; wala nyumbani mwako hatakuwako mzee milele. Tena mtu wa kwako, ambaye sitamtenga na madhabahu yangu, atakuwa mtu wa kukupofusha macho,

33

na kukuhuzunisha moyo; tena wazao wote wa nyumba yako watakufa wapatapo kuwa watu wazima. Na hii ndiyo ishara itakayokuwa kwako, itakayowapata wana wako wawili, Hofni na Finehasi; watakufa wote wawili katika siku moja. Nami nitajiinulia kuhani mwaminifu, atakayefanya sawasawa na mambo yote niliyo nayo katika moyo Wangu, na katika nia Yangu; Nami nitamjengea nyumba iliyo imara; naye atakwenda mbele ya masihi Wangu milele.”

Aya hizi hufichua kwamba Eli alikemewa kwa uzembe wake wa kutoiamuru nyumba yake kumfuata Mungu. Alikuwa hata ameonywa mapema kwa matokeo yasiyoweza kuepukika ya utepetevu wake; kwamba nyumba yake, uzao wake wote, ungekufa katika umri wa ujana iwapo angeendelea hivyo. Lakini Eli hakufanya chochote kulihusu swala hilo, na hivyo aliathirika kwa matokeo ambayo alikuwa ameonywa kuyahusu. {2TG40: 34.1}

Je! Mambo haya hayajaandikwa kwa tujifunze kwayo, kwa ajili ya mifano yetu? Mbona, basi, zipo nyumba nyingi ambazo zimevunjika leo kama tokeo la mafunzo mabaya ya nyumbani, au hamna mafunzo, kuliko zil-ivyovunjika katika siku za Eli? Na, ajabu kama inavyoonekana, janga hili hutokea mara kwa mara kuliko isivyo katika nyumba ambazo wazazi ni waangalifu sana kwamba watoto wao wasiingie katika shule ya umma ila wapate elimu yao yote katika shule ya kanisa. Hakika, kosa halipo kwa shule ya kanisa yenyewe, bali kwa ukw-eli kwamba wazazi hutarajia kwamba shule ya kanisa ichukue majukumu ya uzazi — kutenda yale ambayo waza-zi wenyewe hushindwa kufanya. Na hebu nikuambie kwamba iwe shule ya kanisa au shule ya umma, wala yoy-ote haiwezi kuchukua nafasi ya shule ya nyumbani. {2TG40: 34.2}

Mbali na hilo, kwa sababu shule za kanisa kwa kiasi kikubwa ni mambo ya familia, kwa kiwango kikubwa hu-ongozwa na wazazi wenyewe, shule hizi tayari

34

zimethibitisha kushindwa vibaya! Ikiwa unaitilia shaka taarifa hii ya kutisha, basi wachunguze washiriki wako wa kanisa, na kwa mshangao wako utapata kwamba wengi wao ni tunda la shule ya umma, na kwamba waliofuzu wengi wa shule ya kanisa wako nje duniani. Baada ya kusikia maelezo haya, dada mmoja alichunguza kanisa lake na akapata kwamba asilimia 70 walielimishwa katika shule ya umma; asilimia 27 katika shule za um-ma na za kanisa; na asilimia 3 katika shule ya kanisa tu! {2TG40: 34.3}

Hii si yote: Utapata kwamba washiriki wa kanisa ambao wameongoka nusu, hawajaongoka, kwa kawaida, iwapo si kabisa, ni tunda la shule ya kanisa. Bado zaidi, utapata kwamba mabingwa wakuu dhidi ya Ukweli mwafaka, dhidi ya “chakula kwa wakati wake,” na waenezaji wa machukizo ndani ya kanisa, kwa ujumla ni tunda la shule ya kanisa! {2TG40: 35.1}

Uzoefu wangu kwa miaka katika kazi ya injili umenithibitishia kwamba yale ninayosema ni kweli. Usinielewe vibaya; Simtuhumu mtu yeyote. Najaribu kumsaidia kila mmoja wenu kwa faida yenu wenyewe mwamke kwa hali hiyo, na kulitii Neno la Mungu. Hivi karibuni vyombo vya dola vinaweza kuanza kuwatia gerezani wazazi, pia, kufuatia kukamatwa na makosa ya watoto, iwapo nyumba zitaendelea kama zinavyofanya sasa. {2TG40: 35.2}

Mwandishi mashuhuri na mwenye mamlaka juu ya uhusiano na shida za kijamii, Leon J. Sauli, anasema haya katika kitabu chake kinachoitwa, Ukomavu wa Kihisia. “Hamna watoto wa shida, wazazi wa shida na mazingira ya shida tu.” {2TG40: 35.3}

Na iwapo mimi sasa nimekuwa adui wenu kwa sababu huwaambia ukweli, basi ninyi wenyewe hamtayathibit-isha mambo haya? {2TG40: 35.4}

35

Mfumo Wa Mungu Wa Elimu

Tumeona sasa matokeo ya shule nzuri za nyumbani na shule mbaya za nyumbani, lakini tutasaidiwa zaidi kwa kutazama ndani ya mfumo wa elimu ambao Uvuvio ulipendekeza, na kwa kuufanya uwe mfumo wetu wa kufundisha watoto. Ni huu: {2TG40: 36.1}

Kut. 12:22-27 — “Nanyi twaeni tawi la hisopu, mkalichovye katika ile damu iliyo bakulini na kukipiga kizingiti cha juu, na miimo miwili ya mlango, kwa hiyo damu iliyo katika bakuli; tena mtu ye yote miongoni mwenu asitoke mlangoni mwa nyumba yake hata asubuhi. Kwa kuwa Bwana atapita ili awapige hao Wamisri; na hapo Atakapoiona hiyo damu katika kizingiti cha juu, na katika ile miimo miwili, Bwana atapita juu ya mlan-go, wala hatamwacha mwenye kuharibu aingie nyumbani mwenu kuwapiga ninyi. Nanyi mtalitunza jambo hili kuwa ni amri kwako na kwa wanao milele. Itakuwa hapo mtakapoifikilia hiyo nchi, Bwana atakayowapa, ka-ma alivyoahidi, ndipo mtakapoushika utumishi huu. Kisha itakuwa, hapo watoto wenu watakapowauliza, N’ni-ni maana yake utumishi huu kwenu? Ndipo mtawaambia, Ni dhabihu ya pasaka ya Bwana, kwa kuwa alipita juu ya nyumba za wana wa Israeli huko Misri, hapo alipowapiga Wamisri, akaziokoa nyumba zetu. Hao watu wakainama vichwa na kusujudia.”

Yosh. 4:5-7 — “Naye Yoshua akawaambia, Haya, piteni ninyi mtangulie mbele ya sanduku la Bwana, Mungu wenu, mwende pale katikati ya Yordani, mkatwae kila mtu wenu jiwe moja begani mwake, kwa kadiri ya hesabu ya kabila za wana wa Israeli; ili kwamba jambo hili liwe ishara kati yenu, hapo watoto wenu wataka-powauliza ninyi katika siku zijazo,

36

wakisema, Ni nini maana yake mawe haya? Ndipo mtakapowaambia, Ni kwa sababu maji ya Yordani yalitindika mbele ya sanduku la agano la Bwana; hapo lilipovuka Yordani, hayo maji ya Yordani yalitindika; na mawe haya yatakuwa ni ukumbusho kwa wana wa Israeli milele.”

Mungu, tunaona, Huweka ukumbusho kwa mambo muhimu ya maisha ili kuchochea maswali. Wazazi wana-paswa kufanya vivyo hivyo ili kuanzisha kupendezwa katika mambo ambayo wanataka watoto wao wafun-dishwe. {2TG40: 37.1}

Kumb. 6:4-9 — “Sikiza, Ee Israeli; Bwana, Mungu wetu, Bwana ndiye mmoja. Nawe mpende Bwana, Mungu wako, kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa nguvu zako zote. Na maneno haya Nina-yokuamuru leo, yatakuwa katika moyo wako; nawe uwafundishe watoto wako kwa bidii, na kuyanena uketipo katika nyumba yako, na utembeapo njiani, na ulalapo, na uondokapo. Yafunge yawe dalili juu ya mkono wako, nayo yatakuwa kama utepe katikati ya macho yako. Tena yaandike juu ya miimo ya nyumba yako, na juu ya malango yako.”

Mambo muhimu ya maisha yanapaswa kuwekwa daima mbele ya watoto, na siku zote kwa njia ya kupendeza, — kamwe si kwa njia ya kuwafanya wachoshwe na dini, na kamwe si kwa njia ambayo itasababisha somo kuwa la kuchosha. {2TG40: 37.2}

Mti Mbaya Hauwezi Kuzaa Tunda Zuri

Wote wazazi na watoto wanapaswa daima kukumbuka kwamba Mungu anahesabu juu yao, atarajia, na ya kwamba wao wenyewe wanaweza kujenga au kuzuia

37

mistakabali yao. Hili tunaona vyema katika yafuatayo: {2TG40: 37.3}

Kwa sababu kazi ya Yesu ilikuwa ya umuhimu mkubwa na ya matokeo makuu, Mungu alikuwa mwangalifu sana kuhusu uzazi wa Yesu. Kwa sababu hii aliuchagua ukoo wa Abrahamu (mti mzuri), wa Isaka, Yakobo, Yuda, Yesse, Daudi, na kwa njia ya nasaba ya ukoo hadi kwa Yusufu, ambaye alikuwa mume wa Mariamu. Hata ingawa Yusufu angekuwa tu baba mlezi wa Yesu, Mungu alikuwa mwangalifu kumchagua. {2TG40: 38.1}

Na kwa uangalifu kama ule aliokuwa nao Mungu kuhusu ni nani angepaswa kuwa baba mlezi wa Yesu, Alikuwa mwangalifu zaidi katika uteuzi wa mama wa Yesu. Hivyo Mungu alimchagua mama wa Mwokozi kutoka kwa nasaba ya Yusufu, mwana wa Yakobo. {2TG40: 38.2}

Je! Najuaje ulivyokuwa uzazi wa nasaba ya Yesu? — Vyema, ukoo wa baba Yake mlezi najua kutoka kwa mfuatano ambao Mtakatifu Mathayo hutoa. Na nasaba ya mama Yake naijua kutoka kwa unabii wa Musa am-bao nitasoma sasa: “Yusufu ni mti mchanga wenye kuzaa, mti mchanga wenye kuzaa kribu na chemchemi; ma-tawi yake yametanda ukutani; wapiga mishale walimtenda machungu, wakamtupia, wakamwudhi; lakini upinde wake ukakaa imara, mikono yake ikapata nguvu kwa mikono ya Mwenye Enzi wa Yakobo; (Kutoka huko ni mchungaji, jiwe la Israeli).” Mwa. 49:22-24. {2TG40: 38.3}

Sio tu ukoo wa wazazi wa Yesu uliteuliwa kwa uangalifu, ila pia imeteuliwa nasaba ya kila mmoja wa watu wa Mungu waliokabidhiwa majukumu mazito. Kwa nini, nawauliza ninyi, tahadhari kama hizo zinaweza kuchukuliwa ikiwa wazazi hawabebi sehemu muhimu zaidi

38

katika maisha ya watoto? {2TG40: 38.4}

Lazima sasa ikumbukwe, basi, kwamba mtoto hupata elimu yenye usawaziko katika shule tatu — ya nyumba-ni, shule ya kanisa, na shule ya umma, shule yake ya umuhimu zaidi ni nyumbani, maana mtoto kwa kiasi kikubwa huwa ambavyo nyumba humlea. {2TG40: 39.1}

Matokeo

“Itakuwa, utakapoisikia sauti ya Bwana, Mungu wako, kwa bidii, kutunza kuyafanya maagizo Yake yote nikuagizayo leo, ndipo Bwana, Mungu wako, atakapokutukuza juu ya mataifa yote ya duniani, na baraka hizi zote zitakukujilia na kukupata, usikiapo sauti ya Bwana, Mungu wako.” {2TG40: 39.2}

“Utabarikiwa katika mjini, na utabarikiwa na mashambani. Utabarikiwa uzao wa tumbo lako, na uzao wa nchi yako, na uzao wa wanyama wako wa mifugo, maongeo ya ng’ombe wako, na wadogo wa kondoo wako. Litabarikiwa kapu lako na chombo chako cha kukandia unga. Utabarikiwa uingiapo, utabarikiwa naa utokapo.” Kumb. 28:1-6. {2TG40: 39.3}

Itaweza kukutendea vyema nafsi yako iwapo utasoma nyumbani kuhusu jukumu la wazazi kama lilivyowe-kwa katika Mashauri kwa Walimu, uk. 158, 159; Shuhuda kwa Kanisa, Gombo la 3, Uk. 143, 144; na wajibu wa watoto katika Kutoka 20:12; 2 Kor. 6:14-18; 1 Kor. 6:15-20. {2TG40: 39.4}

39

KWA AJILI YA WAHITAJI NG’AMBO

Simu nyingi kutoka ng’ambo zimepigwa kwetu kwa ajili ya mavazi, lakini hatuwezi kutosheleza mahitaji ya daima. Na kwa hivyo ikiwa una nguo yoyote ya akiba katika hali nzuri ambayo ungependa itumike kwa kazi inayofaa, basi tuma mchango wako kwa Shirika la Uchapishaji la Ulimwengu, Kituo cha Mlima Karmeli, Waco, Texas. {2TG40: 40.1}

40

MWITO WA MAANDISHI YA DADA WHITE

Maombi ya dharura yamepokelewa kutoka nchi za kigeni ya nakala za Shuhuda kwa Kanisa, Maandishi ya Awali, na maandishi mengine ya Dada E. G. White. Kwa sababu tunayo shauku ya kutosheleza maombi yote kama hiyo ya ndugu na dada ambao hawawezi, ama kwa sababu ya eneo la mashambani au kwa sababu ya ukosefu wa pesa, kujipatia vitabu vya Dada White na Biblia, tunaweza kuthamini sana ukitutumia nakala zozote za ziada ambazo unaweza kuwa nazo. (Tuma kwa: Shirika la Uchapishaji la Ulimwengu, Kituo cha Mlima Kar-meli, Waco, Texas.) {2TG40: 41.1}

41

MAELEZO

42

MAELEZO

43

Jumuiya ya Wadaudi Waadventista wa Sabato

(Ushirika Huru Unaojumuisha Kanisa)

Mlima Karmeli, Waco, Texas

S.L.P. 23738, Waco, TX 76702

+ 1-254-855-9539

www.gadsda.com

info@gadsda.com

Gombo la 2, Namba 39, 40

Kimechapishwa nchini Marekani

44

>