fbpx

Gombo la 2 Salamu Mwafaka Namba 38

Gombo la 2 Salamu Mwafaka Namba 38

                                    

AMANI YA PEKEE YA MAWAZO

Hati miliki, Kimechapishwa tena 1949

Haki zote zimehifadhiwa

V. T. HOUTEFF

                                    

 

KANUNI ZA MSINGI ZA ELIMU

                                    

1

ANDIKO LA SALA

Hukumu Ni Ya Mungu

Nitasoma kutoka katika Mafunzo ya Kristo kwa Mifano, kuanzia kwa ukurasa wa 72, juu ya ukurasa, na kisha kwa ukurasa wa 73, aya ya mwisho: {2TG38: 2.1}

“Wengi ambao wanaofikiri kuwa wao ni Wakristo mwishowe watapatikana ni wapungufu. Wengi watakuwa mbinguni ambao majirani zao walidhani hawangeingia huko kamwe. Wengi huhukumu kwa mtazamo wa nje, lakini Mungu huhukumu moyo. Magugu na ngano zitakua pamoja hadi wakati wa mavuno; na mavuno ni mwi-sho wa wakati wa rehema….. Bila ya kujali onyo la Kristo, watu wametafuta kuyang’oa magugu. Kuwaadhibu wale waliodhaniwa kuwa watenda maovu, kanisa limetafuta nguvu za serikali. Wale waliotofautiana na mafun-disho yaliyowekwa wamefungwa jela, wameteswa na kuuawa, kwa uchochezi wa watu ambao walidai kuwa wanafanya kazi chini ya idhini ya Kristo. Lakini ni roho ya Shetani, si Roho ya Kristo, inayochochea matendo kama hayo. Hii ni mbinu ya Shetani mwenyewe kuuleta ulimwengu chini ya ufalme wake. Mungu amewakilish-wa vibaya kupitia kanisa kwa njia hii ya kuwashughulikia wale wanaodhaniwa kwamba ni wazushi. Si ku-wahukumu na kuwashutumu wengine, bali unyenyekevu na kutoutumaini ubinafsi, ndilo fundisho la mfano wa Kristo. Si zote zinazopandwa shambani ni nafaka njema. Ukweli kwamba watu wako kanisani hauthibitishi kwamba wao ni Wakristo.” {2TG38: 2.2}

Sasa tuombe kwa ajili ya nini? — Kwa mujibu wa andiko hili tunapaswa kuomba kwamba tusihukumu wen-gine; kwamba sisi kama Kanisa hushughulika tu na dhambi za wazi. Hebu tupige magoti. {2TG38: 2.3}

2

KANUNI ZA MSINGI ZA ELIMU

HOTUBA MAALUM ILIYOTOLEWA NA V. T. HOUTEFF,

MCHUNGAJI WA WADAUDI WAADVENTISTA WA SABATO

JUMAPILI JIONI, SEPTEMBA 8, 1946

HEKALU LA MLIMA KARMELI

WACO, TEXAS

Mith. 22:3, 6, 10, 15 — “Mwenye busara huyaona mabaya na kujificha; Bali wajinga huendelea mbele wakaumia…. Mlee mtoto katika njia impasayo, Naye hataiacha, hata atakapokuwa mzee…. Mtupe nje mwenye dharau, na ugomvi utatoka; Naam, fitina na fedheha zitakoma…. Ujinga umefungwa ndani ya moyo wa mtoto; Lakini fimbo ya adhabu itaufukuzia mbali.”

Wazazi wenye busara hutazama mbele. Wao waangalifu kuhakikisha mustakabali wa watoto wao. Hili wao hulifanya kwa kukazia kikiki ndani ya watoto wao kanuni zilizozalishwa na Mbingu ambazo kwazo watoto wanaweza kujenga kwa ufanisi taaluma ya maisha yao, maana juu ya kila msingi wowote ambao wazazi hu-waanzishia kujenga, huo ndio wa pekee ambao wanaweza kujenga juu yake. Msingi duni utawazuia milele kuto-ka kwa kitu chochote bora kuliko kile msingi wenyewe utakiruhusu, iwe katika safu ya dini au kazi. {2TG38: 3.1}

Wazazi wanapaswa kujua kwamba watoto wanapofikia kubalehe kwao, wanakuwa wa kujitegemea zaidi au kidogo, kujiwajibikia wenyewe. Wao hucheza, kwa mfano, kwa mujibu wa muziki wao wenyewe. Je! Ni muhi-mu jinsi gani, basi, kwamba wao mapema wamiliki maarifa muhimu yawapitishe salama katika miaka hiyo ya ujana. {2TG38: 3.2}

Kwanza kabisa, wanapaswa kidini

3

kufunzwa maadili mema, thamani ya wakati, jinsi ya kupata matokeo katika muda uliowekwa. Wanapaswa kuo-nywa kikamilifu kuhusu matokeo mabaya ya dakika zilizopotezwa. Hakika, wanapaswa kuongozwa ili wagun-due kwamba jumla ya dakika na masaa yanayotumika vizuri na maarifa wanayoyapata wakati wa ubalehe wao yataumba maisha yao yote. Wanapaswa kujua kwamba nyakati za miaka ya kubalehe ni nyakati muhimu zaidi katika maisha yao yote, na ya kwamba mara zikipotezwa, zimetoweka milele. Watoto hakika wanahitaji kuyajua sana mambo haya kabla waingie katika ubalehe wao. {2TG38: 3.3}

Hizi kanuni za msingi zinaonekana hata kwa uhalisi zaidi wakati mtu akizingatia kwamba tabia ni rahisi sana kufanyiza, lakini kivitendo haiwezekani kuikomesha. Hii ndio sababu watoto huwa jinsi wazazi walivyowalea. {2TG38: 4.1}

Isitoshe, wavulana na wasichana katika ubalehe wao wanazo nguvu nyingi kuliko wakati wowote baadaye, na kwa hivyo wanaweza kutekeleza zaidi katika miaka hiyo kuliko wanavyoweza baadaye katika urefu sawa wa wakati katika uwanja sawia wa kujitahidi na uzoefu. {2TG38: 4.2}

Hamna shaka kwamba umri wa kubalehe wa mtoto yeyote ni hatari zaidi, pia. Nilivyosema hapo awali, wazazi wasingoje hadi tatizo liwasili, ila wanapaswa kuanza mapema kulizuilia. Ili kulitenda hili, wazazi lazima mapema katika maisha ya mtoto, kutambua ni nini kipaji asili cha mtoto, ili waweze kumfanya kwa wakati aamue itaka-yokuwa kazi au taaluma yake. Wanapaswa kumwezesha aweke lengo lake, na kisha kufanyiza ndani yake bidii ya kuiafikia. Wale ambao hawana lengo hawana lolote la kufanyia kazi kuliafikia. Wanaelea kama chelezo baha-rini, na hatua zao hazina malengo kama zile za kipepeo. Watoto

4

ambao wana lengo la kujitahidi kuliafikia, na ambao daima hudumu kwalo, wanakaribia hapo, na wanalazimika kuugeuza wakati wa utukutu kuwa wa faida. {2TG38: 4.3}

Watoto wanapaswa pia kufunzwa thamani ya dola. Badala ya kuruhusiwa kuingia katika tabia ya kutumia kila senti wanayoshika, wanapaswa kuelimishwa kuweka akiba kadiri wawezavyo. Mara wakishakuwa na mwonjo wa kuanza akaunti ya akiba, hata ingawa iwe kuanzia chini ya dola, wataendelea kwa bidii. Kwa njia hii, wao kuweka akiba itakuwa desturi ya kusisimua. Watoto ambao hawajafunzwa kupata ujira na kuweka akiba, na bado mwishowe wafanye jambo fulani wenyewe hawalitendi kwa sababu ya wazazi wao, ila bila kuwajali wao. {2TG38: 5.1}

Wapo maelfu ya watu, wengine katika kila jamii, ambao hawajui namna ya kutumia pesa au jinsi ya kusimamia nyumba. Hawa wa matokeo mabaya ya hasara, licha ya ni pesa ngapi wao huchuma, huwa hawana chochote kwa siku ya mvua. Siku zote wao ni maskini na daima katika deni, siku zote hutarajia hisani kutoka mahali fulani. {2TG38: 5.2}

Wafunze watoto wako kamwe wasinunue chochote ambacho hawana fedha kamili mapema, na hata wakati huo iwapo tu watahitaji bidhaa hizo kabisa. Chochote kinachonunuliwa kwa malipo ya wakati hugharimu zaidi. Na hilo, bila shaka, humaanisha bidhaa chache na kazi nyingi na wakati mgumu kwa mnunuzi. Katika visa vingi sehemu ya malipo huwa hayatekelezwi, na matokeo yake bidhaa hurejea kwa wamiliki halisi. Katika tukio kama hilo, mnunuzi hupata hasara ya jumla kwa uwekezaji wake wote. Madeni yasiyohitajika huvunja mamia ya nyumba kila mwaka. Wazazi wanapaswa kwa maagizo na kielelezo

5

wawaelimishe watoto wao dhidi ya mazoea ya kuvunja pochi na ya kuvunja nyumba. {2TG38: 5.3}

Wale ambao hujadili juu ya shida zao na wengine, mara nyingi hupokea maoni ya msaada na nuru kwa njia yao; hivyo basi wao huepuka hasara na aibu. {2TG38: 6.1}

Kuendelea na uchambuzi wetu, sasa nitasoma kutoka– {2TG38: 6.2}

Kumb. 11:13-28 — “Tena itakuwa, mtakaposikiza kwa bidii maagizo Yangu Niwaagizayo leo, kwa kumpenda Bwana, Mungu wenu, na Kumtumikia kwa mioyo yenu yote na roho zenu zote, ndipo Nitakapowapa mvua ya nchi yenu kwa wakati wake, mvua ya masika, na mvua ya vuli, mpate kuvuna nafaka yako, na divai yako, na mafuta yako.”

“Nami nitawapa nyasi katika mashamba yenu kulisha wanyama wenu wa mifugo, nanyi mtakula na kushiba. Jitunzeni nafsi zenu mioyo yenu isije ikadanganywa, mkageuka, na kutumikia miungu mingine, na kuiabudu; hasira za Bwana zikawaka juu yenu, Naye akafunga mbingu, kusiwe na mvua, wala nchi isitoe matunda yake; mkaangamia kwa upesi mtoke katika nchi nzuri awapayo Bwana.” {2TG38: 6.3}

“Kwa hivyo yawekeni maneno Yangu mioyoni mwenu na rohoni mwenu, yafungeni yawe dalili juu ya mikono yenu, nayo yatakuwa kama utepe katikati ya macho yenu. Nayo wafunzeni vijana wenu, kwa kuya-zungumza uketipo katika nyumba yako, na utembeapo njiani, na ulalapo, na uondokapo. Tena uyaandike juu ya miimo ya nyumba yako, na juu ya malango yako, ili siku zenu zifanywe nyingi, na za

6

vijana wenu nao, juu ya nchi Bwana aliwaapia baba zenu kuwa atawapa, kama zilivyo siku za mbingu juu ya nchi.” {2TG38: 6.4}

“Kwa kuwa kwamba mtayashika kwa bidii maagizo haya yote Niwaagizayo, kuyafanya, kumpenda Bwana Mungu wenu, na kutembea katika njia Zake zote, na kushikamana Naye; ndipo Bwana atakapowafukuza ma-taifa haya yote mbele yenu, nanyi mtamiliki mataifa makubwa yenye nguvu kuwapita ninyi.” {2TG38: 7.1}

“Kila mahali mtakapokanyaga kwa nyayo za miguu yenu patakuwa penu: tokea hilo jangwa na Lebanoni, na tokea mto Frati, mpaka bahari ya magharibi itakuwa ndio mipaka yenu. Hapatakuwa na mtu atakayeweza kusimama mbele yenu, Bwana, Mungu wenu, atawekea utisho wenu na kuhofiwa kwenu juu ya nchi yote mta-kayoikanyaga, kama Alivyowaambia.” {2TG38: 7.2}

“Angalieni, Nawawekea mbele yenu hivi leo baraka na laana; baraka, ni hapo mtakapoyasikiza maagizo ya Bwana, Mungu wenu, Niwaagizayo leo: na laana, ni hapo msiposikiza maagizo ya Bwana, Mungu wenu, mkikengeuka katika njia niwaagizayo leo, kwa kuiandama miungu mingine,msioijua.” {2TG38: 7.3}

Sasa tuunganishe andiko hili na– {2TG38: 7.4}

Kumb. 21:18-21 — “Mtu akiwa na mwana mkaidi, mshupavu, asiyetii sauti ya baba yake, wala sauti ya mama yake, nao wajapomwadhibu hawasikizi, ndipo babaye na mamaye na wamkamate, na kumpeleka kwa wazee wa mji wake, katika lango la

7

mahali pake; wawaambie wazee wa mji wake, Huyu mwana wetu ni mkaidi, mshupavu, hasikizi sauti yetu; ni mwasherati, tena ni mlevi. Waume wote wa mji wake na wamtupie mawe, afe; ndivyo utakavyoondoa uovu katikati yako; na Israeli wote watasikia na kuogopa.”

Naona vigumu kufikiri maneno haya yanahitaji ufasiri wowote. Yameandikwa waziwazi kama ambavyo mwandishi yeyote mzuri wa leo angeweza kuyaandika. Kwa kweli, naamini yameandikwa wazi zaidi kuliko ambavyo tungeweza kuyaandika. {2TG38: 8.1}

Unaona, kale, zamani sana katika nyakati za kale, Bwana alifanya zijulikane amri Zake na sheria Zake. Aliahi-di kwamba ikiwa watu Wake wangetii, Yeye angaliwafanya kuwa taifa kuu; kwamba wangeyamiliki mataifa makubwa na yenye nguvu kuliko wao; na ya kwamba mataifa yote, yangewaogopa. Aliwaambia waziwazi, hata hivyo, kwamba iwapo hawangetii, basi laana ingekuwa fungu lao. {2TG38: 8.2}

Aliwaagiza wawalee watoto watiifu. Wazazi waliamriwa kuwaleta kwa wazee iwapo wao wenyewe ha-wangeweza kuwafanya watoto wao watii, na wazee walipaswa kuwapiga mawe. Sababu iliyotolewa ilikuwa “Kwamba Israeli yote isikie na kuogopa,” — na kuacha uovu. Wakiwa na adhabu hii kwa mtazamo bila shaka walikuwa waangalifu sana jinsi walivyowalea watoto wao. {2TG38: 8.3}

Ikiwa tungalikuwa tunaishi katika wakati ambao Bwana aliwaamuru watu Wake, katika siku za Musa, hatungejua iwapo kweli Bwana alikuwa akimaanisha au alikuwa anaongea tu. Lakini kwa sababu karne nyingi zimepita, kwa tokeo la kutotii kwa Israeli ya kale tunaweza kuona kwamba Mungu hakufanya mchezo ila ali-maanisha. Naam, daima tangu

8

Wayahudi kama taifa walikosa kutii, wamepigwa teke kutoka kwa nguzo hadi kwa kigingi, na sasa katika miaka mitano iliyopita pekee, mamilioni wao wamechinjwa. Hata katika siku na kizazi hiki hamna nafasi kwa ajili yao mahali popote duniani. Ipo nafasi kwa kila mtu ila sio kwa Myahudi, na ni wazi kuona kwa nini. {2TG38: 8.4}

Wangalikuwa taifa kuu zaidi duniani, lakini sasa wao si taifa hata kidogo. Badala yake, wao ni mpira wa kan-danda kwa kila mguu kujaribu. Walitaka kuwa kama mataifa yaliyowazunguka, na mataifa daima tangu wakati huo yamewapiga mateke kutoka shimo moja la matope hadi jingine. Sasa tunaona kwamba Bwana hakuwa akidanganya. Alimaanisha tu lile Alilolisema, na Alilolinena kwa Wayahudi wakati huo, Analinena kwetu sisi leo. {2TG38: 9.1}

Ni sisi, si Wayahudi, ambao sasa wana chaguo la kufanya. Tunaweza kuchagua kuwa kama ulimwengu, na kufukuzwa hadi kuzimu pamoja nayo. Au tunaweza kuchagua kutenda lile ambalo Mungu huamuru, na kwa hivyo kuwa pamoja Naye katika ufalme Wake. Mojawapo wa chaguo hizi lazima sasa tufanye upesi. {2TG38: 9.2}

Sifikiri kama sisi hatujui lililo sahihi na lililo makosa. Wengi wetu tumejifunza Bibilia maisha yetu yote na tunayo angalau fikra nzuri ya yale ambayo huwa Inafuza. Tunalohitaji kufanya jioni hii, basi, ni kuamua iwapo sisi kama kikosi tutende lile Uvuvio hufundisha, au ikiwa tutajaribu kufanya hivyo kama mmoja mmoja. Wewe tuambie la kufanya katika swala la nidhamu: Je! Kila mtu afanye kama anavyoona inafaa, au tutakuwa na ki-wango ambacho sisi sote tunaweza kuongozwa? Je! Tunaenda kuamua la kufanya, na kulitenda, au tutaamua, na kamwe tusitende lile tunaloamua? {2TG38: 9.3}

9

Mambo ya dharura sana ni haya: Tutawezaje kuendesha shule? Na tutawavika vipi watoto wetu na sisi wenyewe? Je! Tujivike kama wakristo wanaoendelea au tujivike kamawa kidunia wanaoendelea? Je! Tutakuwa tukigombana juu yake, au sote tutaliona sawa? {2TG38: 10.1}

(Usharika: “Sisi sote tunapaswa kuona sawa.”) {2TG38: 10.2}

Je! Basi tuwe na kiwango cha kwenenda kwacho? {2TG38: 10.3}

(Usharika: “Naam”) {2TG38: 10.4}

Je! Tunapaswa kuwatenda nini wavulana na wasichana ambao wanaweza kuwa wakorofi, wasiotii, na wasio-wajali wazazi na waalimu wao? Je! Tuliache hilo kwa watoto kuamua, au tutafanya lile ambalo Bibilia hudai: Kwamba watoto waadabishwe nyumbani, na iwapo hilo halifanyi kazi, basi waletwe kwa wazee, waondolewe shuleni na kutoka kwa ushirika? Au wazazi waende nao? {2TG38: 10.5}

Zamani kwa kweli waliwapiga mawe watoto waasi. Walitenda hili kwa sababu haingaliwezekana kanisa ku-wahifadhi wasiotii kati yake, na mataifa yaliyowazunguka hayangekuwa na wakaaji wageni, na kwa hivyo hakukuwa na lolote la kufanya isipokuwa kuwapiga kwa mawe. Leo, ingawa, wanaweza kuondolewa, na wanaporudiwa na fahamu zao, wanaweza kurejeshwa. {2TG38: 10.6}

Wazazi wana jukumu la kuona kwamba wavulana na wasichana wao wamefunzwa kutii; kwamba wana-waheshimu wazazi wao, wazee, na kila mtu katika jamii; na ya kwamba hawabishani na mtu yeyote. {2TG38: 10.7}

Je! Watoto wanapaswa kuwa na umri gani kabla hawajaachwa peke yao kufanya kama watakavyo? — maadamu

10

watoto wako katika nyumba ya wazazi wao, wanapaswa kuwa chini ya udhibiti wa wazazi wao. {2TG38: 10.8}

Iwapo tutakuwa na kiwango, lazima sote tuwe pamoja kwacho. Na ikiwa watoto watajua kwamba tunamaan-isha, kwamba hawawezi kuepuka, hawatajaribu kuweka chochote kwa mtu yeyote. Watoto wengi, hata hivyo, kwa kweli wamefunzwa kuwa wasiotii. Hili linaweza kuwaje? — Vyema, tangu wakati watoto ni vitoto vi-changa tu, wazazi huwaacha wawe na njia yao wenyewe. Kwanza watoto husema “Ndio,” wazazi husema “La” Kisha taabu huanza. Watoto hushinda ubishi kwa kilio, basi iwapo hakifanyi kazi, wao hupata matokeo kwa ku-gongagonga miguu yao kwa sakafu. Wanapoendelea kuwa watu wazima, hugundua njia mpya za kudai na ku-pata wanachotaka. Kwa kuwaruhusu watoto wao kuwashinda kwenye mchezo, kwa kweli wazazi huwafunza watoto wao kuwa wasiotii, wasio na heshima. Yaani dio sababu watoto wako tu jinsi ambavyo wazazi huwalea. {2TG38: 11.1}

Kamwe usimruhusu mtoto kuwa na njia yake dhidi yako, na hautawahi kuwa na taabu naye. “Lolote linalo-patikana kuwa haliwezekani kurekebisha, akili zenyewe hujifunza kulitambua na kujizoesha kwalo.” — Elimu, uk. 290. {2TG38: 11.2}

Je! Nyinyi wavulana na wasichana nyote mnaahidi kuikana dunia na “kujitokeza nyote” kwa ajili ya Bwana? Je! Mnakusudia kutolegeza msimamo kwa ya uovu, mazoea mabaya ya dunia? Je! Mnaazimia kufanya nyumba-ni, shule, na kanisa kuwa ufanisi? Kuwavutia wavulana na wasichana wengine katika mwelekeo sahihi? {2TG38: 11.3}

Iwapo sivyo, sasa tunawaonya kwamba mtafukuzwa shuleni na kutoka mahali hapa. Kama

11

kuna yeyote ambaye hawezi kutupatia jibu la nafsi yote, itakuwa bora kwenu kujiondoa sasa na kwenda mjini na katika shule ya umma. {2TG38: 11.4}

Hatujipumbazi. Leo tunamaanisha kama vile walivyokuwa wakimaanisha zamani za kale. Iwapo mnafikiria sheria hii ni ngumu sana kwa ajili yenu, semeni sasa. {2TG38: 12.1}

Je! Ninyi, wavulana na wasichana, mnaahidi kuwatii wazazi wenu na waalimu wenu? na kutomjibu mtu yeyote kwa dharau? {2TG38: 12.2}

Na je! Ninyi watu wazima mnaahidi kufanya kadiri mwezavyo kuwasaidia vijana? Je! Mnakubali kutoyapele-ka malalamiko yenu kuwahusu watoto au vijana kwa mtu yeyote ila kwa wazazi wao wenyewe? {2TG38: 12.3}

(Wote, wachanga na wazima, waliinua mikono yao kwa kukubali.) {2TG38: 12.4}

Je! Hamfikirii kwamba waamini wa Ukweli Ulioendelea wanapaswa kujivika kwa stara, kuvutia, na kupen-deza, kwa upatano na dini ya Kristo, ili kuwavutia watazamaji kuwaiga, wasigeuke kwa kuchukizwa? {2TG38: 12.5}

(Ushirika: “Naam”) {2TG38: 12.6}

Viwango vyetu vya mavazi kwa wanawake na wasichana, wanaume na wavulana, vimewekwa kwa ufahamu huu, na kumbuka sasa mmeahidi kuviweka kwa utendaji. {2TG38: 12.7}

Ni vyema kuzingatia kwamba hakuna kumbukumbu kwamba mtu yeyote alikuwa na fursa kutoka kwa namna Yesu alivyokuwa akijivika, kunena ama kwa ajili au dhidi Yake. Hii inaonyesha kwamba Yeye hakuwa bila ki-asi. Mbali na hilo, mavazi Yake lazima yalikuwa ya thamani kuwa nayo, la sivyo maadui Zake wasingejali

12

kuyapigia kura. {2TG38: 12.8}

Kanuni hii inapaswa kudhibiti namna tunavyojivika. Tunapaswa kujivika ili tuweze kukumbukwa, sio kwa kuvaa pambo la aina fulani, umbo, rangi, au kama hayo, ila kukumbukwa kwa kujivika vyema, bila umakini kutajwa haswa kwa kitu kimoja. Pia, mavazi yetu yanapaswa kuwa ya namna ambayo maskini sana hatajihisi kwamba hastahili kuwa mbele yetu, na ya kwamba mkwasi hatajihisi kuaibika katika ushirika wetu. {2TG38: 13.1}

Jumla ya mambo yote kwa kifupi ni hili: kwamba tujivike bila chochote kwa majivuno au wonyesho, ila kwa heshima na adabu. {2TG38: 13.2}

VIWANGO BORA VYA KIKRISTO VYA MAVAZI
YA WANAWAKE NA WASICHANA

Marinda/Magauni

Vifaa/Nyenzo. — Zinapaswa kuwa za ubora mzuri, za kudumu, mwafaka kwa hali ya hewa na kazi ya mtu. Hapana kitu cha mapambo au kupita kiasi. Vifaa vyembamba na vikubwa, chapa za wonyesho ni mwiko. {2TG38: 13.3}

Rangi. — Rangi zinapaswa kuwa za kumpendeza mtu binafsi. Michanganyiko ya rangi inapaswa kupatana, na isiwe ya wonyesho au ya tafrija. {2TG38: 13.4}

Mikono. — Katika hadhara, mikono inapaswa kuwa mirefu kabisa kufunika kiwiko wakati mikono imekun-jwa. Inapaswa kuwa ya

13

mtindo ambao hauachi wazi kwapa wakati mikono inapoinuliwa. {2TG38: 14.1}

Urefu wa Skati za Wanawake na Wanaobalehe. — Skati fupi karibu nusu moja ya urefu kati ya pia ya goti na kifundo cha miguu ni isiyo ya adabu, na hivyo haifai kwa mwanamke Mkristo. {2TG38: 14.2}

Urefu wa Skati ya wa Kabla Kubalehe. — Skati zafaa kufunika magoti. Usizifanye kuwa refu kumsababisha mtoto kutokuwa na starehe au kuchekwa bure. {2TG38: 14.3}

Kufaa kwa Mavazi. — Mavazi yanastahili kufaa vizuri, na sio kuning’inia kwa namna ya ovyoovyo. Yana-paswa kuwa ya starehe na safi, lakini lakini yasiyobana sana kuonyesha mistari ya mwili. {2TG38: 14.4}

Mistari ya shingo. — Mistari ya shingo haipaswi kuwa chini ya inchi 2 au 3 chini ya shimo la shingo, na ina-paswa kufaa ili isifunue matiti wakati mtu huyo anainama. {2TG38: 14.5}

Miundo. — Marinda yanastahili kutengenezwa kwa namna ya adabu, sio ya kidunia au ya upotovu. {2TG38: 14.6}

Vifungo, Mikanda, Mapambo. — Vifaa hivi vya nyongeza vinapaswa kuwa vya kutobadilika, safi, na vil-ivyosawazishwa, na vinavyopatana na rinda. Kisivaliwe chochote ili kuvutia mkazo kwa hicho kitu kimoja. {2TG38: 14.7}

14

Sweta

Isipokuwa kwa swala la wa kabla ya kubalehe, sweta za kuingizwa-juu sio za heshima zinapovaliwa bila koti au kabuti. Hata sweta za aina ya koti hazipaswi kutoshea kabisa ili kubana umbo la mwili. {2TG38: 15.1}

Suruali za Kazi

Hazipaswi kuvaliwa katika maeneo ya hadhara au njiani, ila tu katika kazi ambazo zinaweza kufanya mavazi yasiyofaa au hatari. Hata wakati huo yanapaswa kuwa ya mtindo iliyoundwa mahsusi kwa wanawake, sio kwa wanaume. Vaa masuruali aina ya skati. Wasichana wadogo wanaweza kuvaa ovaroli zilizotengenezwa kwa ajili yao. {2TG38: 15.2}

“Suti za kubadilisha za Mavazi”

Kiasi cha nguo kinapaswa kutawaliwa na kazi ya mtu binafsi na hali ya hewa, sio na mitindo ya kigeugeu inayobadilika daima. Kuwa na nguo nyingi tu ambazo ni muhimu kuziweka nadhifu na safi, wastani. {2TG38: 15.3}

Koseti (Nguo za ndani za kubana kiunoni hadi mapajani), Mikanda, nk.

Hizi hazipaswi kuvaliwa isipokuwa kwa agizo la tabibu kwa ugonjwa fulani. Mikanda ya Garter (soksi ndefu za wanawake zenye ukanda) ambayo haihitilafiani na mzunguko, ni sawa. {2TG38: 15.4}

15

Mavazi ya Harusi

Hijabu na marinda marefu hayapaswi kushutumiwa kwa harusi. Sehemu ya rinda inayokokotwa haifai. {2TG38: 16.1}

Suti za Kuoga, Kuota Jua, nk.

Kamwe kitu chochote kinachofunua mwili, kisivaliwe kwa uwepo wa wanaume na wavulana. Makundi mseto ya kuoga ni mwiko. {2TG38: 16.2}

Kofia

Mtindo. — Kofia ziwe za heshima na zilizosawazishwa, sio kwa kingo zilizopita kiasi, au kama sanduku la vidonge. Hazipaswi kuwa kubwa isivyofaa au ndogo za kuchekesha, bali za heshima na za kufaa. {2TG38: 16.3}

Mapambo. — Pamba kofia hiyo bila chochote kinachovutia uangalifu usiofaa kwacho. Utaji na mapambo mengine yanayonig’inia kwa wonyesho, hayastahili. Mapambo yanapaswa kufaa ila si ya kujionyesha. {2TG38: 16.4}

Rangi. — Rangi ya kofia inapaswa kupatana na nguo zingine, na haipaswi kuwa ya kumulika au ya kung’aa kwa umbali. {2TG38: 16.5}

Utaji/Dusumali kwa Hafla za Kidini

Utaji unapaswa kuwa unafaa kwa hafla husika, na ulio na maana kwa kusudi la utaji

16

kuliko kuwa kitu kilichonyakuliwa bila kukusudia. La mwisho ni la dharau. Wasichana wadogo wanapaswa kufunzwa kuvaa utaji mara tu wanapoweza kuelewa kuuhusu. {2TG38: 16.6}

Katika sehemu zingine za umma. — Kofia huonekana kuwa ya heshima zaidi kuliko kichwa kitupu mbele ya watu. {2TG38: 17.1}

Viatu

Muundo na Ubora. — Viatu vinapaswa kuwa vya kudumu na visivyobadilika. Epuka viatu visivyo na nafasi ya vidole na visivyo na visigino. Honekana visivyo na kiasi. Katika hafla maalum, sapatu zinaruhusiwa. {2TG38: 17.2}

Urefu wa Visigino. — Kwa ajili ya afya, visigino vinapaswa kuwa chini ya inchi 2. Visigino virefu hutishia afya. {2TG38: 17.3}

Rangi. — Vaa rangi zinazofaa. Viatu vyeupe havifai mashambani na vijijini ambako njia hazijawekwa lami. Viatu vyeusi huonekana vya kuvaliwa muda mrefu, na vinafaa zaidi kwa mtenda kazi wa injili kuliko rangi zin-gine za viatu. {2TG38: 17.4}

Mapambo. — Mapambo yanapaswa kukifaa kiatu, na sio ya wonyesho au kuning’inia kuvutia umakini. {2TG38: 17.5}

Soksi Ndefu

Nyenzo na Uzito. — Soksi zinaweza kuwa pamba, hariri, rayon au nailoni, aina yoyote inayofaa zaidi kwa hafla au kazi hiyo. Soksi nyembamba zimeshutumiwa. {2TG38: 17.6}

17

Vaa uzito wa utumishi. {2TG38: 18.1}

Zilizosokotwa hadi Chini ya Magoti. — Hazifai zinapoonekana. Usiuweke mwili kwa wonyesho. {2TG38: 18.2}

Soksi za Polisi. — Mwiko iwapo miguu imefunuliwa. Ni sawa kwa watoto wachanga katika hali joto ya hewa. {2TG38: 18.3}

Bila Soksi. — Umeshutumiwa isipokuwa bila viatu. {2TG38: 18.4}

Kuvika Nywele

Upswept. — Ni sawa ikiwa sio kupita kiasi. {2TG38: 18.5}

Nywele za Urefu Wastani Zinazoning’inia — Zinaruhusiwa kwa wasichana iwapo zimewekwa safi. {2TG38: 18.6}

Nywele zilizofupishwa. — Mwiko kwa wanawake na wanaobalehe; ni sawa kwa vitoto vichanga na wasichana wadogo ikiwa ni lazima, lakini afadhali nywele ziachwe zikue. {2TG38: 18.7}

Nywele za asili za Singa au za Mawimbi-mawimbi. — Zipange kiasilia na kwa unadhifu iwezekanavyo. {2TG38: 18.8}

Nywele Zilizonyooka. — Usijaribu kufanya kitu cha kupita kiasi kwa nywele zako ambacho Mungu haku-kusudia. Panga ziwe safi na kwa unadhifu. {2TG38: 18.9}

Kusuka kwa Kudumu, Kusuka kwa Vidole na Vifungu vya Nywele, nk. — Zote kama hizi zisizo za asili ni mwiko. {2TG38: 18.10}

Kuvuta Nywele kwenye “Panya,” Roller, nk — Sawa iwapo inahitajika. {2TG38: 18.11}

18

Bizimu (Vishikio) za Nywele. — Ni sawa iwapo vinahitajika, lakini rangi ya bizimu ikiwezekana ipatane na rangi ya nywele. Usitumie chochote cha kung’aa au cha wonyesho kuvutia kuona. {2TG38: 19.1}

Tepe (Kamba/Ugwe). — Inaruhusiwa kwa wasichana wadogo kushikilia nywele zao. {2TG38: 19.2}

Vito

Saa za Kiwiko/Mkononi. — Kwa maana kamili, saa ya kiwiko ni bangili iliyo na kidude cha saa juu yake, na haipaswi kuvaliwa njiani au hadharani. {2TG38: 19.3}

Vipini vya Mavazi. — Vyema, ikiwa vinatimiza kusudi, na sio vya wonyesho au madoido/urembo. Vito vya kujirembesha vimeshutumiwa. {2TG38: 19.4}

Vito Vingine vya Mapambo. — Mikufu ya shingo, mikufu ya shingo, vibweta, bangili, vipuli, pete/bizimu, etc., vyote vimeshutumiwa. {2TG38: 19.5}

Vipodozi

Poda ya uso, poda ya kuoga, mafuta ya kioevu, vikausha ngozi, krimu baridi ni sawa iwapo vinahitajika, na ikiwa havinunuliwi kupita kiasi. Lakini namna ya poda nyekundu, rangi ya mdomo, penseli ya nyusi za macho, wanja, marashi, rangi za kucha za vidole, kucha nyeupe, nk. vimeshutumiwa {2TG38: 19.6}

Usafi wa Kibinafsi

Viondoa harufu, dawa za kuondoa nywele zinaweza kuruhusiwa iwapo zinahitajika kabisa, na ikiwa kitu chochote cha madhara hakitumiki. Dawa za kudhibiti jasho sio za kiafya. {2TG38: 19.7}

19

VIWANGO BORA VYA KIKRISTO VYA MAVAZI
YA WANAUME NA WAVULANA

Suti

Mtindo. — Suti zinapaswa kukatwa kwa namna ya kiheshima–bila chochote cha tafrija au kupita kiasi. Hasa suti zinazopaswa kuvaliwa kwenye mimbari ziwe nadhifu na za adabu. Angalia kwamba suti hiyo inafaa vizuri na haining’inii kwa namna isiyofaa. {2TG38: 20.1}

Nyenzo. — Ubora wa nyenzo unapaswa kuwa wa kudumu, na wa kuzingatia hali ya hewa na kazi. {2TG38: 20.2}

Rangi. — Rangi halisi ambazo hazimuliki, zinapaswa kutumika. Iwapo koti lazima liwe la rangi moja na suruali ndefu za rangi nyingine, uangalifu unapaswa kuzingatiwa ili rangi zipatane vyema, na zisionekane za kicheko. Kwa ujumla, michanganyo kama hiyo inapaswa kuepukwa. Kamwe haipaswi kuvaliwa kwenye mimba-ri. {2TG38: 20.3}

Mashati

Mashati ya Michezo na Ukosi (Kola) Uliowazi. — Mashati ya michezo ya ukosi uliowazi yanaweza kutumika wakati wa kusafiri mashambani au kwa hafla kama hizo. Kanisani au njiani, walakini, hayafai. Ukosi haupaswi kuvaliwa chini kabisa kuliko kifungo cha kwanza. {2TG38: 20.4}

20

Mikono. — Kwa mavazi na mivalio ya mimbari, mikono ya mavazi inapaswa kuvaliwa kwa urefu kamili. Mikono iliyokunjwa au mifupi inaweza kuvaliwa ikiwa hafla hiyo itahitaji AU kwa ajili ya urahisi. Mashati yasiyokuwa na mikono ni mwiko mbele ya umma. {2TG38: 21.1}

Mashati Yaliyovaliwa Nje ya Suruali Ndefu. — Mashati yaliyovaliwa nje ya suruali ndefu huwatambulisha walioyavaa kama ni wazembe au wanajaribu kuonekana wa tafrija au kitu fulani — wasichokijua. Wao hujiondoa kwa heshima. {2TG38: 21.2}

Uchi bila Shati. — Kwa umma au mbele ya wanawake au wasichana, mwanamume anapaswa kuvaa shati ki-la wakati. Wafunze wavulana wachanga kufanya vivyo hivyo. {2TG38: 21.3}

Tai

Muundo. — Aidha tai ya uta au ya-nne mkononi inaweza kuvaliwa — yoyote ambayo ni bora kwa suti au hafla. Usivae chochote kupindukia. {2TG38: 21.4}

Rangi na Miuundo. — Tai haifai kuwa ya tamasha au ya kumulika, bali inapaswa kuvutia na ipatane kwa suti na iwe ya kumfaa anayeivaa. Rangi za kutazamisha na mifumo ya wonyesho haistahili. {2TG38: 21.5}

Vitu vya Ziada

Nje ya Mfuko wa Kifua. — Kujivika kitambaa au kalamu na kalamu ya mkaa nje ya mfuko wa kifua haifai kwa lolote isipokuwa kuvutia, kuimarisha

21

majivuno. Usiidunishe hivyo tabia yako, bali viweke katika mifuko ya ndani ambamo vinafaa kuwa. {2TG38: 21.6}

Saa za Kiwiko. — Kwa maana kamili, saa ya kiwiko ni bangili iliyo na kidude cha saa juu yake, na haipaswi kuvaliwa njiani au hadharani. Iwapo unaona ni lazima kubeba kidude cha saa, tumia saa ya mfukoni. {2TG38: 22.1}

Vipini vya Tai na Bizimu za Tai. — Vipini vya tai ni mwiko. Ikiwa inahitajika kuvaa bizimu ya tai, tumia mo-ja inayoweza kufichwa ndani ya mikunjo ya tai. Usivae chochote cha wonyesho. {2TG38: 22.2}

Minyororo ya Saa. — Minyororo ya saa kwa wonyesho haifai kabisa kama ilivvyo bizimu ya tai, pete, au bangili. Iweke mbali isionekane. {2TG38: 22.3}

Vinginevyo

Pete, ya sikio, ya pua (hazama/kishaufu), nk — Pete na vito vingine vimeshutumiwa. {2TG38: 22.4}

Mishipi ya Kushikilia Mikono ya Shati. — Mishipi ya mikono si ya kiafya iwapo imevaliwa ikibana sana hata kuhitilafiana na mzunguko. Ikiwa inahitajika kuivaa, usitumie chochote kinachoonekana wazi. Ni bora, hata hivyo, kufupisha mikono ya shati lako. {2TG38: 22.5}

Dusumali/Leso (Kanga). — Kamwe usivae dusumali kwa wonyesho tu. Chagua rangi zinazopatana na mava-zi mengine yote — chochote kisiwe cha kujionesha. {2TG38: 22.6}

Soksi Zilizosokotwa hadi Chini. — Soksi zinapaswa

22

kutegemezwa ifaavyo, vinginevyo huonekana duni na ovyo. {2TG38: 22.7}

Viatu. — Chagua viatu vya ubora wa kudumu na muundo na rangi halisi. Viatu vyeupe havifai mashambani na vijijini ambako njia hazijawekwa lami. Huonekana kuwa visivyo vya adabu kwenye mimbari na huvutia umakini usiofaa kwa miguu. Viatu vyeusi huonekana vya kuvaliwa muda mrefu, na vinafaa zaidi kwa mtenda kazi wa injili kuliko rangi zingine za viatu. {2TG38: 23.1}

Suti za Kuoga na Kaptura/Chupi. — Hizi ni sawa kwa hafla sahihi, lakini vikundi mseto vya kuoga ni mwiko. {2TG38: 23.2}

Nywele. — Panga nywele kiasili na kwa unadhifu iwezekanavyo, ukiondoa vitu vyote vya bandia kama ny-wele ndefu zilizofumwa za kudumu, nk. Iwapo nywele ni kavu, tumia mafuta ambayo hayana marashi sana, kitu ambacho ni cha manufaa kwa nywele na sio tu kwa “harufu.” {2TG38: 23.3}

Kuonekana kwa Jumla. — Usianguke katika mazoea yasio ya unadhifu (ya uzembe): Dumisha nywele fupi, ndevu zilizonyolewa (usipovaa masharubu), na mavazi nadhifu na masafi kadiri shughuli inavyoruhusu. Mungu anawahitaji wawakilishi Wake kujivika kwa njia ya kuipongeza dini yao kwa wote walio juu na chini, kwa mata-jiri na maskini. Usivae kwa kupindukia wala kwa matambara. Kaa katikati ya njia chini ya hali zote. {2TG38: 23.4}

23

Kumbuka

Hivi ni viwango vya sasa vya mavazi, na Wadaudi wote wanapaswa kufuatana nazo. Isipokuwa ni kwa saba-bu ambazo hazijaonekana mapema, tofauti yoyote kutoka kwa viwango hivi, wakati vinasimama dhahiri, humjumuisha mkosaji na wanafiki. {2TG38: 24.1}

 

UNYENYEKEVU KATIKA MAVAZI

“Katika hotuba Yake mlimani, Kristo anawahimiza wafuasi Wake wasiruhusu akili zao zivutwe sana katika mambo ya kidunia. Yeye husema wazi: ‘Huwezi kumtumikia Mungu na mali. Kwa sababu hiyo Nawaambieni, Msisumbukie maisha yenu, mle nini au mnywe nini; Wala miili yenu, mvae nini. Maisha je! Si zaidi ya chakula, na mwili zaidi ya mavazi?’’ Na mavazi kwa nini kuyasumbukia? Fikirini maua ya mashamba, jinsi yameavyo; hayafanyi kazi, wala hayasokoti; Nami nawaambia ya kwamba hata Sulemani katika fahari yake yote hakuvikwa vizuri kama mojawapo la hayo.’ {2TG38: 24.2}

“Maneno haya yamejaa maana. Yalitumika katika siku za Kristo, na yanatuhusu katika siku yetu. Yesu hapa analinganisha uzuri wa maua ya kondeni na mapambo bandia ya mavazi. Yeye anatangaza kwamba utukufu wa Sulemani haungaliweza kustahimili kulinganishwa na mojawapo ya maua katika uzuri wa asili. Hapa lipo somo kwa wote walio na shauku kujua na kutenda mapenzi ya Mungu. Yesu

24

ameona masumbuko na ibada inayopewa mavazi, na ameonya, naam, ametuamuru, tusiweke mawazo mengi juu yake. Ni muhimu kwamba tuwe waangalifu kutii maneno Yake. Sulemani alikuwa ameshughulisha mawazo ya maonyesho ya nje hivi kwamba alishindwa kuinua akili zake katika muunganisho wa daima kwa Mungu wa hekima. Ukamilifu na uzuri wa tabia ulipuuzwa katika jaribio lake la kupata uzuri wa nje. Aliuza heshima na uadilifu wa tabia yake katika kutaka kujitukuza mwenyewe mbele ya ulimwengu, na mwishowe akawa dikteta, akidhamini maisha yake ya gharama ya juu kwa ushuru wa kuwaponza watu. Yeye mwanzo alianza kupotoka moyoni, kisha akaasi kutoka kwa Mungu, na mwishowe akawa mwabudu sanamu. {2TG38: 24.3}

“Tunapoona dada zetu wakiacha unyenyekevu wa mavazi, na kuukuza upendo kwa mitindo ya ulimwengu, tunahisi kutaabishwa. Kwa kuchukua hatua katika mwelekeo huu, wanajitenga na Mungu na kupuuza mavazi ya ndani. Hawapaswi kujihisi kwamba wana uhuru kutumia wakati waliopewa na Mungu katika mapambo ya-siyohitajika kwa mavazi yao. Ingalikuwa bora zaidi utumike kuyachunguza Maandiko, na hivyo kupata ufahamu kamili wa unabii na masomo ya utendaji ya Kristo. {2TG38: 25.1}

“Kristo ni mfano wetu. Lazima tuuweke Mtindo huo daima mbele yetu, na tutafakari dhabihu isiyo na kikomo ambayo imetolewa ili kutukomboa kutoka kwa utumwa wa dhambi. Iwapo tunajikuta tumeshutumiwa tuna-pojitazama kwenye kioo, hebu tusiendelee zaidi katika uasi, ila tutazame mema pande zote, na tuyafue mavazi yetu ya tabia katika damu ya Mwana-Kondoo, yapate kuwa bila mawaa. Hebu tupige kelele, alivyofanya Daudi alivyosema, Unifumbue macho yangu,

25

niyatazame maajabu yatokayo katika sheria Yako.” Kwa wale ambao Mungu amewakabidhi wakati na raslimali kwamba ziweze kuwa baraka kwa wanadamu, lakini ambao wameziponda zawadi hizi bila sababu juu yao wenyewe na watoto wao, watakuwa na hesabu ya kutisha kukutana nayo katika mahakama ya Mungu. {2TG38: 25.2}

. . . . .

“Wale kati ya watunza Sabato ambao wamejitiisha kwa mvuto wa dunia, watapimwa. Hatari za siku za mwi-sho ziko juu yetu, na majaribu yako mbele ya watu wanaodai kuwa wa Mungu ambayo wengi hawakutarajia. Usahihi wa imani yao utathibitishwa. Wengi wameungana na walimwengu kwa kiburi, ubatili, na kutafuta anasa, wakijihadaa kwamba wanaweza kufanya hayo na waendelee kuwa Wakristo. Lakini ni anasa hizi ambazo hu-watenga kwa Mungu, na kuwafanya watoto wa ulimwengu. Kristo hajatupatia mfano kama huu. Wale tu ambao hujikana nafsi, na kuishi maisha ya kiasi, unyenyekevu, na utakatifu, ni wafuasi wa kweli wa Yesu; na kama hao hawawezi kufurahia jumuiya ya wapenda dunia.” — Shuhuda kwa Kanisa, Gombo la 4, Uk. 628, 629, 632, 633. {2TG38: 26.1}

Jinsi ya Kupata za Ziada

Wakati ambapo unaagiza nakala za ziada za “Trakti za Vuli,” tafadhali bainisha gombo na namba ya somo ba-dala ya tarehe au jina. Hili litawezesha kuingiza agizo lako bila kukawia. {2TG38: 26.2}

26

Hizi ndogo kila Juma, ambazo hazikugharimu chochote, ni za thamani isiyokadirika kwako. Soma na uziweke kwenye maktaba yako, kwa maana wakati hakika utakuja utakaposhukuru kuwa umezihifadhi nakala zako. {2TG38: 27.1}

 

KWA AJILI YA WAHITAJI NG’AMBO

Simu nyingi kutoka ng’ambo zimepigwa kweti kwa ajili ya mavazi, lakini hatuwezi kutosheleza mahitaji ya daima. Na kwa hivyo ikiwa una nguo yoyote ya akiba katika hali nzuri ambayo ungependa itumike kwa kazi inayofaa, basi tuma mchango wako kwa Shirika la Uchapishaji la Ulimwengu, Kituo cha Mlima Karmeli, Waco, Texas. {2TG38: 27.2}

27

Jumuiya ya Wadaudi Waadventista wa Sabato

(Ushirika Huru Unaojumuisha Kanisa)

Mlima Karmeli, Waco, Texas

S.L.P. 23738, Waco, TX 76702

+ 1-254-855-9539

www.gadsda.com

info@gadsda.com

Gombo la 2, Namba 38

Kimechapishwa nchini Marekani

28

>