15 Aug Gombo la 2 Salamu Mwafaka Namba 35
Gombo la 2 Salamu Mwafaka Namba 35
AMANI YA PEKEE YA MAWAZO
Hati miliki, Kimechapishwa tena 1948
Haki zote zimehifadhiwa
V. T. HOUTEFF
BWANA HAKI YETU
1
ANDIKO LA SALA
Usiishi Kwa Ajili Yako Mwenyewe
Nitasoma kutoka katika Mafunzo ya Kristo kwa Mifano, ukurasa wa 67, aya ya kwanza na ya pili– {2TG35: 2.1}
“Ngano hukua, ‘kwanza jani, kisha suke, baada ya hilo nafaka kamili kwenye suke.’ Lengo la mkulima kwa kuipanda mbegu na taaluma ya kuukuza mmea ni kuzalisha nafaka. Yeye huwa na tumaini la chakula kwa mwenye njaa, na mbegu kwa mavuno kwa siku za baadaye. Hivyo Mkulima Mtakatifu huyatazamia mavuno kama thawabu ya kazi na kafara Yake. Kristo anatafuta kujitokeza Mwenyewe katika mioyo ya wanadamu; na Yeye hufanya hivyo kupitia wale wanaomwamini Yeye. Kusudi la maisha ya Mkristo ni kuzaa matunda, — kule kuitokeza tena tabia ya Kristo ndani ya mwamini, ili iweze kujitokeza tena ndani ya wengine. Mmea hauoti, haukui, au kuzaa matunda kwa ajili yake wenyewe, bali ‘humpa mpanzi mbegu, na chakula yule mlaji.’ Kwa hivyo hakuna mwanadamu anayefaa kuishi kwa ajili yake mwenyewe. Mkristo yuko duniani kama mwakilishi wa Kristo, kwa ajili ya wokovu wa nafsi zingine.” {2TG35: 2.2}
Tutaweza kuomba sasa kwamba tumruhusu Kristo ajitokeze Mwenyewe ndani yetu, na kwamba kupitia sisi Yeye aweze kutenda kazi kujitokeza Mwenyewe ndani ya wengine; kwamba tusiishi kwa ajili yetu wenyewe; ya kuwa tukumbuke kwamba Mkristo atakuwa mwakilishi wa Kristo katika mambo yote. {2TG35: 2.3}
2
“BWANA HAKI YETU”
ANDIKO LA HOTUBA NA V. T. HOUTEFF
MCHUNGAJI WA WADAUDI WAADVENTISTA WA SABATO
SABATO, APRILI 24, 1948
HEKALU LA MLIMA KARMELI
WACO, TEXAS
Andiko letu linapatikana katika Yeremia 23, kuanzia aya ya tano hadi ya nane, kwa jumla. {2TG35: 3.1}
Yer. 23:5 — “Tazama siku zinakuja, asema Bwana, Nitakapomchipushia Daudi Chipukizi la haki; naye ata-miliki mfalme, atatenda kwa hekima, naye atafanya hukumu na haki katika nchi.”
Hapa upo unabii wa ujio wa kwanza wa Yesu, Chipukizi la Haki, Ambaye atafanya hukumu na haki duniani. {2TG35: 3.2}
Aya ya 6 — “Katika siku zake Yuda ataokolewa, na Israeli atakaa salama, na jina lake atakaloitwa ni hili, BWANA NI HAKI YETU.”
“Katika siku zake;” yaani katika siku ambazo Chipukizi la Haki limeinuliwa, katika siku za Yesu, katika enzi ya Ukristo. Ni wazi, basi, siku fulani katika kipindi cha Ukristo, Uvuvio unafanya ijulikane, Yuda ataokolewa, na Israeli atakaa salama duniani. Ahadi hii, kwa hivyo, haijafanywa kwa Wayahudi wasioamini, ila kwa Wakris-to wanaoamini, kwa wale ambao wameifanya haki ya Bwana iwe yao. {2TG35: 3.3}
Walakini Wakristo hawa, tumeambiwa hapa, ni wazawa wa zote Yuda na Israeli
3
ambao kwa tokeo la kutawanywa kwao, na pia wao kujiunga na kanisa la Kikristo, katika karne nyingi wamepoteza utambulisho wao wa taifa. Kanisa la Kikristo, kwa hivyo, kulingana na Maandiko katika sehemu kubwa limefanyizwa na wazawa wa Yakobo, ambao uzao wake ulipaswa uwe kama mchanga wa bahari kwa umati. {2TG35: 3.4}
Wao watamwita Yesu BWANA NI HAKI YETU: Wataona wazi kwamba haki yao wenyewe ni matambara machafu, na wataifanya haki ya Kristo iwe yao kikamilifu. Vinginevyo wasingeweza kumwita Yeye “Bwana haki yetu.” {2TG35: 4.1}
Aya ya 7, 8 — “Kwa hiyo, angalia, siku zinakuja, asema Bwana, ambapo hawatasema tena, Aishivyo Bwana, aliyewatoa wana wa Israeli katika nchi ya Misri; lakini, Aishivyo Bwana, aliyewapandisha na kuwaongoza wazao wa nyumba ya Israeli kutoka nchi ya kaskazini, na kutoka nchi zote nilikowafukuza; nao watakaa kati-ka nchi yao wenyewe.”
Baada ya kuifikia siku kuu ya kukusanywa katika kipindi cha Ukristo, — ya kuokolewa kwao kutoka katika nchi zote, hadi kwa uakisi Kutoka kwa pili (Isa. 11:11), — kwa kawaida hawatasema, “aishivyo Bwana aliyetu-toa Misri,” au “aliyetutoa Babeli,” bali “aishivyo Bwana aliyetutoa katika nchi zote Yeye alikotufukuza.” Wanampa Yeye sifa kwa kutawanywa kwao, na kwa kukusanywa kwao, na pia kwa makao salama katika nchi yao wenyewe. Hawa, unaona, sio Wayahudi wasioamini, ila ni Wakristo walioongoka kabisa. Wao wataimiliki nchi. {2TG35: 4.2}
Zaidi ya hayo, wakati hili linapotukia hakutakuwa
4
na hofu na mauaji kati ya watu wa Mungu, — hakuna bunduki zilizofyatuliwa na mabomu yalioangushwa juu yao. Watu watakaa salama. “Wala hapana mwenyeji atakayesema, mimi mgonjwa; watu wakaao humo wa-tasamehewa uovu wao.” Isa. 33:24. {2TG35: 4.3}
“Kwa maana mimi, asema Bwana, nitakuwa ukuta wa moto kuuzunguka pande zote, nami nitakuwa huo utu-kufu ndani yake…. Imba ufurahi, Ee binti Zayuni; maana tazama, Ninakuja, Nami nitakaa kati yako, asema Bwana. Na mataifa mengi watajiunga na Bwana katika siku hiyo, nao watakuwa watu Wangu: Nami nitakaa katikati yako, nawe utajua ya kuwa Bwana wa majeshi Amenituma kwako.” Zek. 2:5, 10, 11. {2TG35: 5.1}
Jambo la muhimu sasa ni kujua ni nini haki ya Bwana na jinsi ya kuifanya iwe haki yetu sisi wenyewe, ili tuweze kufaa kwa Ufalme Wake. {2TG35: 5.2}
Bwana, hata hivyo, kwanza anatumaini kujua tulilo nalo dhidi Yake: {2TG35: 5.3}
Mika 6:3-5 — “Enyi watu Wangu, nimewatenda nini? Nami nimewachosha kwa habari gani? Shuhudieni juu Yangu. Kwa maana Nalikupandisha kutoka nchi ya Misri, na kukukomboa utoke katika nyumba ya utumwa, Nami naliwapeleka Musa, na Haruni, na Miriamu, watangulie mbele yako. Enyi watu Wangu, kumbukeni sasa alivyouliza Balaki, mfalme wa Moabu, na alivyojibu Balaamu, mwana wa Beori; kumbukeni toka Shitimu hata Gilgali, mpate kuyajua matendo ya haki ya Bwana.”
Kwa sababu hatuwezi kufikiri kuhusu jambo lolote ambacho tunaweza kuwa nalo dhidi ya Bwana, ingekuwa bora
5
tupate jibu la Balaamu kwa Balaki lilikuwa nini, ili kwamba tujifunze ilivyo Haki ya Bwana, na jinsi ya kuifanya iwe yetu wenyewe. Hebu tuende kwa hivyo tufungue kitabu cha Hesabu– {2TG35: 5.4}
Hes. 23:16, 17 — “Bwana akaonana na Balaamu akatia neno kinywani mwake, akasema, Umrudie Balaki, ukaseme hivi. Akafika kwake, [alipofika kwa Balaki] na tazama, amesimama karibu na sadaka yake ya ku-teketezwa, na wakuu wa Moabu pamoja naye. Balaki akamwambia, Bwana amenena nini?”
Sasa hebu tusikie jibu la Balaamu: {2TG35: 6.1}
Hes. 23:18, 19 — “Naye akatunga mithali yake, akasema, Ondoka Balaki, ukasikilize; Nisikilize, Ee mwana wa Zipori; Mungu si mtu, Aseme uongo; Wala si mwanadamu, Ajute; Iwapo Amesema, Hatalitenda? Iwapo Ame-nena, Hatalifikiliza?”
Haki ya Mungu, unaona, ni maadili Yake, ahadi Zake za hakika, Uwezo wake kutekeleza. Yeye huzihakikisha ahadi Zake; hazishindwi kamwe. Kuwa na Haki ya Bwana, kwa hivyo, ni kuwa na maadili na uaminifu Wake, na hizi hatuwezi kuwa nazo maadam tunapokuwa na shaka kwa Neno Lake, kwa maana kuwa na shaka sio jam-bo pungufu kumwita muongo! Kuwa na shaka ni kosa kubwa zaidi mtu anaweza kutenda! Hakuna mtu anayeweza kutomwamini Mungu na bado apokee baraka na ahadi Zake. Kuwa na Haki ya Bwana, kwa hivyo, ni kumwamini Yeye kabisa bila shaka. Na Anatarajia tuanzie wapi? — Yeye hutaka tuanze na lile jambo ambalo hututaabisha zaidi — mambo ya muda ya kesho. Anataka tujifunze kwamba hatuwezi kutumikia
6
nafsi na Mungu, pia: {2TG35: 6.2}
Mat. 6:24-26 — “Hakuna mtu awezaye kutumikia mabwana wawili; kwa maana atamchukia huyu, na kumpenda huyu; ama atashikamana na huyu, na kumdharau huyu. Hamwezi kumtumikia Mungu na ma-li. Kwa sababu hiyo nawaambieni, Msisumbukie maisha yenu, mle nini au mnywe nini; wala miili yenu, mvae nini. Maisha je! Si zaidi ya chakula, na mwili zaidi ya mavazi? Waangalieni ndege wa angani, ya kwamba ha-wapandi, wala hawavuni, wala hawakusanyi ghalani; na Baba yenu wa mbinguni huwalisha hao. Ninyi je! Si bora kupita hao? “
Aya hizi tatu hunena wazi wazi kwamba kuishi ili kutafuta riziki, na kuwa na wasiwasi jinsi utakavyokuwa kesho, sio kitu chochote kipungufu zaidi ya kutumikia mali (nafsi); ya kwamba huwezi kutumikia nafsi na Mun-gu kwa wakati mmoja; kwamba iwapo unamtumikia Mungu unapaswa kuwa huru kwa wasiwasi kuhusu siku zijazo kama ndege walivyo. Naam, unapaswa kuwa na imani hata zaidi kwa utunzi Wake, kwa maana wewe ni wa thamani kuliko walivyo nyuni. Unapaswa kujua kwa moyo wote kuwa maadamu unamtumikia Yeye, Hatakuacha wala kukutupa. {2TG35: 7.1}
Isa. 41:17 — “Maskini na wahitaji wanatafuta maji, wala hapana; ndimi zao zimekauka kwa kiu; mimi, Bwa-na, nitawasikia, mimi, Mungu wa Israeli, sitawaacha.”
Isa. 49:15 — “Je! Mwanamke aweza kumsahau mtoto wake anyonyaye, hata asimhurumie mwana wa tumbo lake? Naam, hawa waweza kusahau, lakini Mimi sitakusahau wewe.”
Mat. 6:27-34 — “Ni yupi kwenu ambaye akijisumbua aweza kujiongeza kimo chake hata mkono mmoja? Na mavazi, ya nini
7
kuyasumbukia? Fikirini maua ya mashamba, jinsi yameavyo; hayafanyi kazi, wala hayasokoti nami nawaam-bia, ya kwamba hata Sulemani katika fahari yake yote hakuvikwa vizuri kama mojawapo la hayo. Basi, ikiwa Mungu huyavika hivi majani ya kondeni, yaliyopo leo, na kesho hutupwa kalibuni, je! Hatazidi sana kuwavika ninyi, enyi wa imani haba? Msisumbuke, basi, mkisema, Tule nini? Au Tunywe nini? Au Tuvae nini? (Kwa maana hayo yote Mataifa huyatafuta:) kwa sababu Baba yenu wa mbinguni anajua ya kuwa mnahitaji hayo yote. Bali utafuteni kwanza Ufalme wa Mungu, na haki Yake; na hayo yote mtazidishiwa. Basi msisumbukie ya kesho; kwa kuwa kesho itajisumbukia yenyewe. Yatosha kwa siku maovu yake.”
Msisumbukie ya kesho, maana itajisumbukia yenyewe — kwa nini mvuke madaraja kabla kuyafikia? Kwa nini mhangaike ni jinsi gani mtashibisha tumbo zenu na namna mtajivika miili yenu kesho iwapo imeshughulikiwa leo? Kwa nini msumbuke kuhusu mahitaji yenu wenyewe, kwa nini msisumbuke jinsi ya kuuendeleza Ufalme wa Mungu? Kuutumia muda wa ziada kutengeneza mahema au kurekebisha viatu kwa ajili ya mapato ni sawa ikiwa hautasema, “Nitafanya hili na lile lingine na kupata pesa za kununua na kujenga hiki au kile.” Badala yake unapaswa kusema, “Mungu akitujalia, Nitafanya hili au lile, ili niweze kufika hapa au kufika pale, nitafanya hili na lile lingine kwa ajili ya maendeleo ya kazi Yake.” Lengo lolote nyuma ya tendo lako lazima liwe kwa ajili ya kuuendeleza Ufalme Wake. {2TG35: 8.1}
Kwa nini usiyafanye maslahi yako makuu yawe shughuli Yake? Mbona yasiwe Ufalme wa Mungu na haki
8
Yake, ili kwamba “hayo yote uzidishiwe”? Mbona ufanye kazi kujilisha mwenyewe? Kwa nini usimfanyie Mun-gu kazi na umruhusu Yeye akulishe na akuvike? Ana uwezo zaidi wa kukuruzuku kuliko utakavyoweza wakati wowote. Je! Mbona usimruhusu Yeye asimamie kazi yako, nyumba yako, mwili wako? {2TG35: 8.2}
Wakati unatenda amri Yake, Yeye atakufaa usishindwe. Mbona usifanye hivi na kuwa Mkristo kabisa? Kwa nini uwe Mkristo kwa jina, bali mtu wa Mataifa moyoni na imani? Usiifanyie nafsi kazi tena, mfanyie Mungu kazi na uwe huru kwa sumbuko, huru wa kujipatia mapato kwa njia yako mwenyewe. Wavuvi wa Galilaya wali-pokuwa wakivua kwa njia yao wenyewe walishindwa, lakini walipotupa juya pale Yesu alisema walitupe, papo hapo likajaa samaki. {2TG35: 9.1}
Ujue kwanza kwamba Mungu hapendezwi na shughuli yako ya ubinafsi, ila ndani yako na shughuli Yake ya kuokoa. Hakuna kwa hivyo haja wewe kuitumikia mali (nafsi), na wakati uo huo kutarajia baraka Zake kwa masilahi ya mali. Hakuna hata mtu katika dunia anayeweza kufanya kazi kwa ajili ya maslahi yake mwenyewe na bado atarajie kampuni yake kumusaidia, au kumudumisha katika nafasi ya kazi yoyote. Hakuna mwajiri anayewajiri watu kwa sababu anataka mwajiriwa wake apate mapato, ila kwa sababu yeye hutaka biashara yake itunzwe. Ujue kwamba shughuli ya Mungu ni ya umuhimu na yenye matokeo makubwa zaidi kuliko shughuli yoyote ya mwanadamu, na kwamba Mungu ni mwangalifu zaidi ya ambavyo mtu yeyote amewahi kuwa au atakavyokuwa. {2TG35: 9.2}
Mat. 11:28-30 — “Njoni Kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, Nami nita-wapumzisha. Jitieni nira Yangu, mjifunze Kwangu; kwa kuwa Mimi ni mpole na mnyenyekevu wa moyo; nanyi mtapata raha nafsini mwenu; kwa maana nira Yangu ni laini, na mzigo Wangu ni mwepesi.’’
9
Siku zote kumbuka kwamba Mungu hajakuita kwa zamu yako ya kazi ili kukulisha au kukufanya tajiri, ila ku-kuokoa na kuwaokoa wengine kupitia kwako. Kwa hivyo, lolote ufanyalo, lifanye kwa utukufu wa Mungu. Basi na wakati huo tu Atakuruzuku “hayo yote,” vitu ambavyo Mungu anaona vinafaa kutoa. Ataona kwamba una-pata mahitaji yako kwa njia moja au nyingine. Si kitu kipungufu kuliko imani ya Nuhu, ya Ayubu, na ya Danieli italipa bili hiyo, Ndugu, Dada, kwa sababu chochote kipungufu kwa hii ni tusi kwa Mungu. Na ni sawa kumwita Yeye mdanganyifu. Kutilia shaka ahadi za Mungu humnyang’anya kabisa mwenye shaka baraka na ahadi zote za Mungu. Ni wakati tu unapojifunza kumwamini Yeye atakuwa kwako “kama mahali pa kujificha kwa upepo, na mahali pa kujisitiri kwa dhoruba; Kama mito ya maji mahali pakavu, kama kivuli cha mwamba mkubwa kati-ka nchi yenye uchovu.” Isa. 32: 2. {2TG35: 10.1}
“Utafuteni kwanza Ufalme wa Mungu, na haki Yake; na hayo yote mtazidishiwa.” Ahadi hii ilikuwa njema wakati wa Daudi, na itakuwa njema sasa: {2TG35: 10.2}
Zab. 4:5 — “Toeni dhabihu za haki, na kumtumaini Bwana.”
Kwa uzoefu wa kibinafsi Daudi alijua uaminifu wa Mungu: Baada ya kufanya yote yaliyotakiwa kufanywa katika kumtumikia Mungu, alikuwa na imani kwamba wakati dubu na simba walipokuja kula wana-kondoo wake, Mungu angemwokoa iwapo angefanya yote awezayo kuwafanya waepuke. {2TG35: 10.3}
Zaidi ya hayo, akiwa na imani kwamba Mungu alikuwa amemwahidi ufalme, na akiwa ametiwa mafuta kuwa mfalme kwa watu wa Mungu, Daudi hakutilia shaka lolote. Kwa kutambua wajibu wake, bila woga alilikabili lile jitu Goliathi ambalo lilikuwa likimdharau Mungu na Ufalme
10
Wake, na alikuwa na imani kwamba lile jitu halingemdhuru. Kwa imani aliwaweka huru watu wake kutoka kwa nguvu ya lile jitu. Kwa imani alimshinda simba na dubu, na kuwaokoa wana-kondoo. Kwa imani alijua kwamba Sauli hangeweza kumuua, wala kumnyima kiti cha enzi. {2TG35: 10.4}
La, hakuna mnyama wala mwanadamu anayeweza kuwaua au kuwahadaa msikwezwe mkiyatenda maagizo ya Mungu, iwapo mnajua kwamba Yeye Aliye mlinzi wa Israeli halali usingizi wala kusinzia (Zab. 121:3, 4); kwamba Yeye anajua yote kuwahusu, marafiki zangu, kila wakati wa mchana na usiku; kwamba Yeye huchukua taarifa hata ya nywele ambazo huanguka kutoka kwa vichwa vyenu; kwamba lolote linalowakumba ni ila mapenzi yake Mungu kwa ajili ya manufaa yenu wenyewe. Nasema, iwapo mnajua na kuamini kwamba Yeye ndiye Mungu na Mlinzi wa miili na nafsi zenu, basi bila kujali kinachowapata, mtafurahi ndani yake na kumpa Mungu sifa kwa hilo, sio kunung’unika, ila kumtukuza hata katika majaribu na mateso yenu. {2TG35: 11.1}
Isa. 26:4 — “Mtumaini Bwana siku zote: maana Bwana YEHOVA ni mwamba wa milele.”
Ikiwa unamwamini Mungu kwa moyo wote, na iwapo ulimwengu utaanguka kutoka angani na kugongana na nyota, utapaa kwa furaha pamoja na Mungu. {2TG35: 11.2}
Hebu sasa tufungue 2 Wakorintho, sura ya kwanza, na tuone lile Paulo alijua kwa uzoefu kuhusu utunzi wa Mungu juu yake: {2TG35: 11.3}
2 Kor. 1:8, 9 — “Maana ndugu, hatupendi, msijue habari ya dhiki ile iliyotupata katika Asia, ya kwamba tulilemewa mno kuliko nguvu zetu, hata tukakata tamaa ya kuishi. Naam, sisi wenyewe tulikuwa na hukumu ya mauti katika nafsi zetu ili tusijitumainie nafsi zetu,
11
bali tumtumaini Mungu, awafufuaye wafu.”
Paulo alijifunza kwa uzoefu wa kibinafsi kwamba ni bure kumtumainia mwanadamu na nafsi, lakini kwamba ni ni mshahara mnono kumtumainia Mungu, kwamba Yeye pekee ndiye anayeweza kuulinda na kuutunza mwili na nafsi. {2TG35: 12.1}
Zab. 127:1 — “Bwana asipoijenga nyumba Waijengao wafanya kazi bure. Bwana asipoulinda mji Yeye aulindaye akesha bure.”
Watu wengi waaminifu wa Mungu walikuwa na uzoefu kama wa Paulo. Wakati, hata hivyo, hautaniruhusu kusema zaidi ya wachache. Tunapoingia katika imani ambayo Biblia hupendekeza, basi tuko tayari kuingia kati-ka uzoefu ambao Mungu anataka sisi mmoja mmoja tuwe ndani yake, ambao baada ya yote ni muhimu kwetu. Hebu nikupe kwanza wangu kama mfano halisi wa lile Mungu hufanya tunapomruhusu Yeye. {2TG35: 12.2}
Nilipokuwa nikiendesha hoteli ndogo katikati mwa magharibi zamani mnamo 1919, nilivutiwa sana katika dini, na kwa majaliwa nalijiunga na Waadventista wa Sabato. Waakati huo walikuwa wakikutana katika ukumbi uliokodishwa, sio wa kuvutia sana kwa ajili ya kanisa. Watu walionekana kuwa fukara sana. Mbali na mhubiri nalikuwa pekee yangu niliyelikuwa nikiendesha gari, naye alikuwa na Ford kuukuu ambalo nisingetoa dola moja kwa yake iwapo ningeliliendesha. {2TG35: 12.3}
Fikiri sasa kile kilichopita akilini mwangu, na unaweza kujua kwamba nalijiunga tu kwa kanisa kwa ajili ya Ukweli. Hakika, sikuwa na himizo lingine. Matumaini yangu ya kuwa tajiri siku fulani yakawa ndoto ya kuwa maskini zaidi. Naam, Ibilisi alinipa picha nzuri ya umaskini kama alivyompa
12
Bwana picha ya utukufu wa falme. Mimi hata hivyo naliazimu kukaa kwa Ukweli ambao nalikuwa nimejifunza bila kujali lililotokea. {2TG35: 12.4}
Kisha ukaja wakati naliuza hoteli na bila kukusudia nikaingia katika biashara ya mboga. Lakini baada ya muda naligundua kwamba sikutaka kuwa ndani yake, na nikaiuza kwa hasara. Kisha hiyo picha ya giza na weusi ya kuwa maskini unaokuja ikajipanua mara mia moja, lakini nalijitahidi kujiweka mwenye furaha katika Bwana. {2TG35: 13.1}
Wakati fulani baada ya kuliuza duka la mboga, naliondoka katika mji huo, na miezi sita baadaye nikatua Cali-fornia. Huko naliugua, na baada ya kufanya yote nalijua ya kufanya, mmoja wa wachungaji wastaafu wa Waadventista wa Sabato aliyeishi katika sehemu ile ile nilipokuwa naishi, akasema, “Hebu nikupeleke kwa Za-hanati ya Glendale, na nitakupendekeza uliye na msimamo mwema na imara kwa kanisa, na watakupa huduma nzuri na kadirio la chini, pia.” {2TG35: 13.2}
Tulipofika kwa upokezi, na baada ya yule mchungaji kumwambia yote aliyoweza kusema, karani wa zahanati aliniuliza ni arbuni ya namna gani ningeweza kuacha ili kulazwa. Nalisema, “Hundi.” (Kidogo ilinishangaza, kwa maana nalikuwa hospitalini hapo awali lakini kamwe sikuulizwa kulipa chochote kimbele, — la, sio hata baada ya kuruhusiwa kuondoka. Walinitumia ile bili kwa barua.) Alipotazama kwamba cheki imeandikwa benki ya Illi-nois, ilibidi nifafanue kwamba nalikuwa kiasi fulani mgeni magharibi na bado nalikuwa sijahamisha akaunti yangu ya benki. Karani aliichukua hundi kwa kusitasita, na nikapewa chumba, na kwa heshima nikamwambia kwamba ilinipasa nimsubiri daktari hadi atakapokuja. {2TG35: 13.3}
13
Basi, nalingoja siku hiyo yote, lakini hakuna nafsi iliyokuja ndani! Jioni, nilivyokuwa mgonjwa hivyo, nalivaa nguo zangu na kwenda kula chajio ndani ya chumba cha kulia. Kisha naliambiwa kwamba daktari alikuwa mba-li, lakini ataniona mara tu atakaporudi. Iliendelea hivi kwa siku nne, na hakuna nafsi ilioingia chumbani mwangu! Ningalikufa na hakuna mtu angalijua hadi labda siku kadhaa baadaye. Nadhani walitaka wapate pesa kutoka kwa benki na kujua kama salio langu lilikuwa zuri kabla wangeweza kunipa huduma! {2TG35: 14.1}
Hatimaye katika siku ya nne, kasisi wa Zahanati alikuja na udhuru kwa kuchelewa kwake kuniona. “Kama ningalijua kwamba wewe ni Mwadventista wa Sabato,” alielezea, “ningalikuwa nimekuona mapema.” Sikuwa nikimtarajia, ingawa, na haukufanya tofauti yoyote nami. Lakini nalisema moyoni mwangu, “Iwapo hukujua nil-ivyokuwa, ungaliweza kuja mapema.” {2TG35: 14.2}
Mwishowe daktari alikuja na baada ya uchunguzi kamili, naliambiwa kwamba nalikuwa mtu mgonjwa sana na nalipaswa nipate muuguzi maalum wa mchana na usiku kunitunza na kunipatia matibabu ya maji. Kwa idhini yangu muuguzi mwanafunzi akaingia ndani. Lakini wakati vivuli vya jioni vilipoenea angani, muuguzi alinambia kwamba ulikuwapo upungufu wa wauguzi maalum, na kwa hivyo yeye mwenyewe alikuwa anitunze usiku kucha iwapo ningemruhusu alete godoro lake ndani ya chumba changu. Wakati wote nalikuwa hapo, hata hivyo, kamwe hakuamka usiku kunitunza. {2TG35: 14.3}
Na kwa hivyo nalikuwa na muuguzi wa kibinafsi wa mchana na usiku, na mwishowe nilitozwa senti 50 kwa saa — dola sita kila siku kwake yeye kunitunza wakati wa mchana, na dola sita kila usiku kwa kulala na mimi chumbani! Hili pamoja na
14
matozo ya ziada yalikuwa yakikausha sana akiba yangu ambayo ilikuwa tayari imepungua. Na picha ya kufilisika na ya kuwa masikini ilikua kubwa na kubwa akilini mwangu mwenyewe, lakini nilipona ugonjwa wangu, na ni-kashukuru. {2TG35: 14.4}
Tukio hili la Zahanati, hata hivyo, lilileta picha nyingine ya kuvunja moyo akilini mwangu. Je! Zahanati hiyo ni mahali pa Mungu kwa ajili ya watu Wake wagonjwa? Nalijiuliza. Je! Watu hawa ni watu wa Mungu kweli? Jibu lililokuja kwa maswali haya lilikuwa hili: Zahanati ni ya Mungu, na kanisa ni la Mungu, lakini watu wanayoyaendesha ni vibaraka, wao ni makuhani, waandishi na Mafarisayo mamboleo, kwamba lipo hitaji la Wasamaria zaidi kati yao. Hapa ndipo mahali Kweli ya Mungu ipo, hata hivyo, na Mungu akinisaidia, nikasema, nitakaa nayo. Naam, Mungu alinisaidia, niliilinda imani, sikulalamika kuhusu chochote na nikadumu kanisani na kumbukumbu nzuri kama yoyote. {2TG35: 15.1}
Baada ya kutoka hospitalini, hata hivyo, nalikuwa mdhaifu na akaunti yangu ya benki ilikuwa karibu kwisha. Ilionekana kwangu, pia, kwamba hakikuwapo kitu ambacho ningeweza kujiingiza bila Sabato, kwamba ningean-gukia kwa rehema za ukarimu fulani, au vinginevyo kufa kwa njaa. Zaidi ya hayo, kwa miezi kadhaa sikuwa nimetuma zaka wala ahadi zangu za sadaka kanisani katikati mwa magharibi, kwa sababu hiyo nilikuwa na deni la kama $ 75. Nalifikiri wakati huo kwamba ikiwa nitashindwa kulipa deni hili sasa wakati nina pesa za kutosha kulipa, kamwe sitaweza kupata tena pesa nyingi kama hizo pamoja na lingeweza kukaa bila kulipwa milele. Afadhali nifilisike sasa, nalisema, na kuwa huru bila deni kuliko kufilisika baadaye na kuwa mwiwa milele. {2TG35: 15.2}
Akaunti yangu ya benki, nalifikiria, ilikuwa juu kidogo kwa deni langu. Nilipoandika hundi kwa salio lote
15
na kuipeleka kwa kanisa katikati mwa magharibi, niliachwa na $ 3.50 mfukoni mwangu, na bila matarajio ya ka-zi. Kisha naliandika kwa benki katikati mwa magharibi kwamba nalikuwa nikifunga akaunti yangu na kwamba wanapaswa kutuma hundi zilizobatilishwa na karatasi zingine kwa anwani yangu huko California. {2TG35: 15.3}
Kufikia hapo kwa maisha yangu, hata hivyo, meza ilipinduka kama vile ilivyompindukia Abrahamu baada ya kufanya yote isipokuwa amchinje mwanawe Isaka kwa madhabahu ya Mungu. Siku chache tu baada ya kui-andikia benki nalisikia kutoka kwao, na kwa mshangao wangu mkubwa walikuwa wametia ndani ya barua hundi ya karibu $ 350 kama salio langu la mwisho! Kamwe sikugundua jinsi ilivyotukia. {2TG35: 16.1}
Wakati huo huo nalipata kazi katika shirika la mitambo ya kufua, na wakati huo Waadventista wa Sabato walikuwa na mkutano wao wa marago 1923 huko Los Angeles. Na kwa hivyo naliamua kuhudhuria na kati ya vikao kujaribu kuuza mitambo ya kufua chapa Maytag katika kitongoji hicho. Na unafikiri nini? Niliuza mtambo kila siku na vifyonza vumbi kinyongeza. Hii iliendelea hivi wakati wote mkutano wa marago ulidumu, na hundi yangu ya kwanza kutoka kwa kampuni hiyo ilikuwa karibu $ 425. Lakini hili halikuwa yote, kisha tu mshangao mwingine ukanipata. Miaka kadhaa iliyopita, nalikuwa nimenunua hisa ambayo nilikuwa nimeamua haina tha-mani, lakini kwa mshangao wangu nalipokea barua ambayo shirika liliuliza ikiwa ningependa kuwauzia tena, na bei waliyotoa ilikuwa zaidi maradufu ya bei ambayo nilikuwa nimelipa! Hapa nalikuwa na uzoefu halisi wote wangu kama ilivyo ahadi katika Malaki 3:10. {2TG35: 16.2}
Zaidi ya hayo, shirika hili la Maytag lilikuwa jipya, na nilipoenda kuwafanyia kazi, walikuwa na eneo ndogo tu. Wakati wote nilipowafanyia kazi, hata hivyo, walifanikiwa na kukua kama Laban
16
wakati Yakobo alipokuwa akimfanyia kazi. Katika muda wa miaka mitatu walifungua ofisi za matawi kote kote maeneo jirani ya Los Angeles, na kisha wakasimamisha jengo lao ambalo lilionekana kama benki ndani na nje, nyumba nyingi pamoja kwenda chini na kitu kama futi sitini upana. Kuhusu jinsi ustawi wao uliisha nitawaambia baadaye kidogo. {2TG35: 16.3}
Mafanikio yangu yasiyotarajiwa katika kuuza mitambo ya kufua, bila shaka, yalitumiwa kama pampu ya ku-wakuza wauzaji wale wengine, na meneja wa mauzo akawa mdadisi sana kuihusu dini yangu. Mwisho nilipoongea naye alinambia: “Houteff, lazima iwe ajabu kuamini kama wewe, lakini unajua siwezi kamwe kuwa Mwadventista wa Sabato.” Kisha nikamuuliza kwa nini asiweze kuwa, naye akajibu “Kwa sababu iwapo nitaan-za kutunza Sabato kama wewe, nitaipoteza kazi yangu.” {2TG35: 17.1}
Nikasema, “Ni bora kupoteza kazi yako kuliko kuyapoteza maisha yako.” Na mazungumzo yakakoma. Lakini wakati mwingine nilipoingia ofisini naliona shada la maua lililokuwa likining’inia mlangoni, na kila kitu kilion-ekana kutia wasiwasi. Kisha naliambiwa kwamba Bwana Harney, meneja wa mauzo, alikuwa mgonjwa ghafla usiku uliopita na akafa mapema asubuhi hiyo. {2TG35: 17.2}
Yapata wakati huohuo karani mkuu wa uhasibu, pia, akapendezwa kujadili dini nami. Kadiri muda ulivyopita, nalijadili yale niliyokuwa nimejadili na Bwana Harney, na mwishowe yeye, pia, akasema, “Houteff, lazima iwe ajabu kuhisi unavyofanya, lakini siwezi kamwe kuwa Mwadventista wa Sabato.” {2TG35: 17.3}
Nikasema, “Mbona?” {2TG35: 17.4}
“Ah, singeweza kutunza Sabato na kazi yangu, pia,” alijibu. {2TG35: 17.5}
17
“Vyema,” nikasema, “ni bora kupoteza kazi yako kuliko kuyapoteza maisha yako, Bwana Barber.” {2TG35: 18.1}
Na hakika kabisa, wakati mwingine nilipoingia ofisini, nalimkuta kila mtu akiongea badala ya kufanya kazi! Kisha naliambiwa kwamba Bwana Barber, karani mkuu wa uhasibu, alipatikana amekufa asubuhi hiyo chumbani mwake! Amini au usiamini, lakini hili ndilo lililotukia kwa mabwana hao wote baada ya kuiuza imani yao kwa bei ya kazi! {2TG35: 18.2}
Baadaye kidogo, nalifikiri kwamba niweze kuwa na kitu changu badala ya kuendelea kufanya kazi ya Bwana Sleuter. Kwa hivyo nalikuwa nikitumia muda wangu mwingi kutafiti peremende za afya, na kwa vile nalikuwa nauza mtambo wa kufua sasa na wakati mwingine, sikuwa maarufu sana kwa kampuni hiyo. Na kwa vile nilikuwa nadai kampuni fedha kadhaa za uwakala, naliamua kujua mbona zilishikiliwa. Baada ya kujadili jambo hilo mara kadhaa na meneja wa mauzo alinituliza kila wakati kwa kuahidi “atalishugulikia.” Lakini siku moja nalisisitiza jambo hilo kwa bidii, na tokeo lake alisema, “Houteff, nimechoshwa kwa hili na sijali, unaweza kua-cha kazi.” Wakati mwingine niliingia ndani, nilipata habari kwamba Bwana Lisco, meneja wa mauzo, alifutwa kazi na ya kwamba Bwana Foster alikuwa ameichukua nafasi yake! Bwana Lisco, unaona, ndiye aliyepaswa kuacha kazi, sio mimi! {2TG35: 18.3}
Kisha nalikwenda kumwona meneja mpya kuhusu fedha zangu za uwakala. Aliahidi kulichunguza suala hilo na kunijuza wakati mwingine ningekuja ndani. Yeye, hata hivyo, alitenda jambo lile lile ambalo Bwana Lisco alifanya. Na wakati nilisisitiza suala hilo kwa bidii kama vile nilivyofanya kwa Bwana Lisco, yeye, pia, alisema, “Houteff, nimechoka na jambo hilo, na sijali ikiwa utaacha kazi.” Kipekee kabisa, hata hivyo, nilipoingia ndani, naliambiwa kwamba Bwana Foster, meneja wa mauzo, alikuwa ameachishwa kazi na hakuwa tena
18
katika kampuni! Mimi bado nilikuwa. {2TG35: 18.4}
Yapata wakati huu nalikuwa nimejenga biashara ya kutosha kwa peremende zangu za kiafya ili kunishughul-isha na nilikuwa karibu kuacha kazi kabisa. Kisha nikaenda kumwona Bwana Sleuter mwenyewe kuhusu fedha za uwakala nilizotaja awali, lakini akanikaribisha kwa ubaridi sana, na akanambia waziwazi kwamba sikuwa na chochote cha kutoa! Niondoke. Lakini katika muda wa karibu miezi sita, nafikiri ilikuwa, alipoteza shirika na mtu mwingine akaichukua kampuni! Hivi ndivyo kufanikiwa kwake kulikoma. {2TG35: 19.1}
Sio muda mrefu baada ya kwenda kufanya kazi kwa kampuni hii na nalipokuwa nikihubiri nalikutana na mwanamke ambaye mume wake alikuwa wa asili ya Kiyahudi, lakini alikuwa Mskandinavi, na Mwadventista wa Sabato. Alinambia kwamba mumewe aliipinga sana dini yake na wakati mmoja aliitupa Biblia yake kwenye jiko. Alitamani ningemsaidia mumewe kwa namna fulani abadili mwenendo wake. Nalimuuliza amwambie kwamba ningependa kumwona nyumbani kwake usiku uliofuata. Aliahidi kujaribu hilo na kisha anijulishe. {2TG35: 19.2}
Alikaa chini kwa masomo kadhaa pamoja nami nyumbani kwake na familia iliyokuwepo. Nalishangaa, hata hivyo, kumpata anapendezwa sana na yale yaliyowasilishwa, kinyume kabisa na lile mke wake alikuwa ame-nambia! Baada ya kumpa masomo matatu aliniita kando, akavuta mifuko ya suruali yake ndani nje na kunambia, “Unaona, nina familia kubwa ya kulisha na senti tatu tu mfukoni mwangu. Kabla hujanijia,” alielezea, “nalifanya kila kitu kupata kazi lakini nilishindwa. Katika kufadhaika kwangu,” aliendelea, “naliomba kwa mara ya kwanza katika maisha yangu. Nalimwomba Bwana amtume mtu anionyeshe la kufanya. Niliposikia unakuja,” akaongeza, “mimi
19
nalidhani lilikuwa jibu kwa ombi langu, na nalikuwa na hamu ya kukutana nawe. Na ndio sababu ulinipata niki-wa na nia wazi kwa dini yako. Lakini sasa, “ alisema, “najua kwamba Mungu ndiye aliyekutuma.” {2TG35: 19.3}
Nalimwuliza iwapo angependa kuuza mitambo ya kufua, naye akajibu, “niko tayari kufanya chochote unachopendekeza.” Nalimpeleka kwa kampuni ambayo nalikuwa nikiifanyia kazi, na akaenda kazini mara moja, akisafirisha akitumia gari lake mwenyewe. Mshahara wake, na mauzo machache mara kwa mara yalimletea zaidi ya $ 200 kila mwezi. {2TG35: 20.1}
Alimiliki nyumba aliyokuwa akiishi ndani yake, na kwa sababu maisha hayakuwa ya juu sana siku zile, aliwe-za kuweka akiba sehemu nzuri ya ujira wake. Baada ya muda akauza nyumba yake, akanunua konde la ekari ta-no akajenga nyumba mpya na tundu zuri la kuku kwa shamba hilo. Kisha akanambia kwamba alikusudia kufan-ya kazi kwa kampuni hiyo karibu miezi 18 zaidi, na kwa wakati huo atakuwa amemaliza kulipia nyumba na konde lake, au kiasi kidogo kumalizia, na kisha ataweza kutengeneza pato zuri kwa shamba lake la ekari tano. {2TG35: 20.2}
Vyema, yote yalionekana vizuri. Lakini Sabato moja asubuhi alikutana nami kanisani na akanambia kwamba kampuni hiyo ilipaswa kuchukuliwa siku hiyo. Alitaka kujua ikiwa ningeweza kwenda naye na kusikiliza hotuba wakati uhamisho ulikuwa ukifanywa. Nilijadiliana naye kwamba hapakuwa mahali pa kukaa katika Sabato, lakini akateta kwamba ikiwa asingekuwepo wanaweza kuajiri mtu mwingine kwa nafasi yake, na hangeweza kumudu kuipoteza kazi yake. Kwa hiyo alihudhuria mkutano wa shughuli. Muda mfupi baadaye, hata hivyo, kampuni hiyo mpya ilimwachisha kazi. Kwa hivyo hakuweza kudumisha malipo kwa rasilimali na kampuni ya mdhamini ikaifunga! Kisha mkewe akafa! {2TG35: 20.3}
20
Mtu yeyote anaweza kuona kwamba matukio haya yote mfululizo ya siku, yaliyofungamana kwa ukaribu mo-ja kwa lingine bila kitu kingine chochote kati yake, haingewezekana yawe bahati mbaya, ila ya Majaliwa kabisa. {2TG35: 21.1}
Sasa hebu niwasimulie muujiza mwingine ambao ulitukia karibu na wakati huo. Jumatano moja niliendesha gari hadi kwa sehemu ya biashara ya Los Angeles. Baada ya kumaliza shughuli yangu alasiri kabisa, na nilipokuwa nikitembea kwenda ng’ambo ya barabara, naliona mwanamke akiendesha kunielekea. Lakini nilipokuwa nikitembea karibu katikati ya barabara, sikuona hatari yoyote kwa sababu ilikuwapo nafasi ya kutosha kwa ajili yake kupita. Yeye hata hivyo alipindua gari lake moja kwa moja kuja kwangu. Naam, alinigon-ga kutokea kushoto kwangu, akiwa na msisimko kupita kiasi hakuweza kulisimamisha gari lake kabla ya kufika katikati ya nyumba nyingi pamoja. Na hivyo aliendelea kwenda kutoka kwenye kona ya barabara hadi katikati mwa kijia. Ni nini kilinipata gari liliponigonga? Je! Lilinibwaga tambarare njiani, na kupita juu yangu? La, hili halikutukia kwa sababu jambo fulani kubwa lilifanyika: {2TG35: 21.2}
Mkono usioonekana ulinibeba mbele ya gari, miguu yangu ikiteleza kwa wepesi barabarani na upande wangu wa kulia mbele, na upande wangu wa kushoto ukiegemea radieta ya gari! Baada ya kwenda karibu nusu ya um-bali kabla lile gari kusimama, kitu fulani kikaniketisha kwa bamba la gari, na nikauweka mkono wangu wa kushoto kuizunguka taa kubwa ya mbele ya kushoto ya gari! Kisha nalisema moyoni, “Sasa mwanamke unaweza kuendelea ikiwa hilo ndilo bora unaweza kufanya.” Aliposimama, nikaiweka miguu yangu ardhini na nikatoka kwa hilo gari. {2TG35: 21.3}
Wakati huohuo naligundua kwamba penseli niliyokuwa nayo mfukoni mwa koti langu ilikuwa imevunjwa vipande vipande nusu ya dazeni kutoka kwa athari, lakini mbavu zangu zilikuwa
21
hazijaguzwa! Kufikia wakati huo lile gari nami tulikuwa tumezungukwa na watu, na polisi watatu wakimtafuta mtu ambaye gari lilimgonga. Lakini kwa sababu hawakumpata mtu amelala barabarani, au amebanwa chini ya gari, naliwaambia kwamba ni mimi ambaye nilikuwa nimegongwa! Walitaka kunipeleka hospitalini, na nilipowaambia kwamba sikuwa nimeumia, nalimsikia mmoja akisema, “Lazima ameumia ila ana msisimko sana na hajui hali yake.” {2TG35: 21.4}
Kisha wakanifanya niinue miguu na mikono juu na chini, mara kadhaa, halafu mmoja akapiga kelele, “Ame-umbwa kwa mpira!” Mwanamke huyo alishtakiwa kuendesha gari kwa maili 30 kwa saa. Kisha nikatembea mi-pangilio mitatu ya nyumba pamoja hadi kwa gari langu, na kuelekea kwenye mkutano wa maombi katika kanisa la Exposition Park, ambapo katika msimu wetu wa shuhuda naliwaambia kuhusu ile ajali na matokeo. Bado tun-aishi katika siku za miujiza, mnaona. {2TG35: 22.1}
Baada ya haya yote na uzoefu mwingine, basi ukaja ujumbe ambao sasa tunajitahidi kuupeleka kwa Walaode-kia. Maadui wa ujumbe wakati huo hawakuacha chochote bila kupinduliwa wakitafuta jambo dhidi yangu, ba-dala ya kuhakikisha kwamba hawakuwa wanaukataa Ukweli. Walijaribu kwa vyovyote kubandika jambo fulani juu yangu na kukomesha shughuli zangu, lakini hawakupata lolote na kama ada karibu washiriki 30 wa kanisa hilo walidumu katika mikutano yangu maalum kila Sabato alasiri. Kisha ukaja wakati ambapo wazee wa kanisa walikataa kuturuhusu tutumie kanisa kwa mikutano yetu, na wakatufanya sote tutoke. Lakini mmoja wa kina dada ambaye alikuwa akiishi katika nyumba kubwa mkabala na kanisa hilo akatoa mahali kwa mikutano, na palikuwa kizaazaa kikubwa kati ya watu pande zote za majengo ya kanisa. Baadhi walikuwa kwa ajili yetu na wengine walikuwa dhidi yetu. Hivyo
22
ilikuwa kwamba ile nyumba iliyokuwa mkabala na kanisa ilijaa alasiri hiyo na wengi walisikiliza wakiwa nje kupitia madirishani. Maadui walishindwa kuvunja mikutano yetu, na ushindi ulikuwa wetu. {2TG35: 22.2}
Baadaye walitukataza kuhudhuria ibada zao za kanisa, na walianza kuwaondoa kwa ushirika wale ambao bado walitaka kuhudhuria mikutano yetu. Walijaribu kunihamisha nchini, pia, ila wakashindwa. Kisha walijaribu kupata amri ya korti dhidi ya yeyote kati yetu kwenda kanisani siku ya Sabato, lakini wakapoteza. Wakati mmo-ja waliwaita polisi ili wanikamate kwa tuhuma za uongo kwamba nalikuwa nikivuruga mikutano, lakini baada ya maafisa katika kituo cha polisi kusikia kisa changu na mashtaka ya shemasi dhidi yangu, aliwaamuru wale askari wawili waliotuleta kwenye kituo kutuweka ndani ya gari lao tena, na kuturudisha kanisani pale waliponikamata! {2TG35: 23.1}
Baada ya hili wazee walijaribu kuniweka katika hifadhi ya wenye kichaa. “Meneja wa jiji” la Glendale mwenyewe (Mwadventista wa Sabato) alikuwa amekuja kwa kanisa hili asubuhi hiyo ya Sabato kuweka mashtaka na kuniona nikichukuliwa na kufungiwa katika ile hifadhi. Baada ya kuzungumza nami kwa dakika chache, hata hivyo, afisa huyo hakufanya lolote ila kunambia kwamba hatanisumbua tena! Kisha meneja wa jiji mwenye pauni 200 alijihisi mdogo kuliko uzani wangu wa ratili 135. {2TG35: 23.2}
Walitenda mambo haya yote yasiyofaa na mengine mengi; zaidi ya hayo, walinena na kuhutubu dhidi yangu. Na ingawa sikuwa na yeyote ila Bwana wa kunilinda wakati wowote, bado katika haya yote ushindi ulikuwa wangu! {2TG35: 23.3}
Tulipoihamisha ofisi yetu kutoka California hadi
23
Texas, ambapo hatukuwa na rafiki wala mwamini katika ujumbe, wazee wa kanisa walifurahi, na wakafikiri kwamba kazi yetu ingekufa wakati huo hakika. Walakini ilikua zaidi kuliko hapo awali, ingawa hili lilitukia katikati ya mshuko wa kiuchumi, mnamo 1935, wakati mamia na maelfu ya biashara zilikuwa zikifilisika, na am-bapo watu wakwasi walikuwa wanaanza kuwa maskini. Bali sisi ambao tulianza bila chochote, tulikua na kufan-ikiwa. Sisi, zaidi ya hayo, kamwe hatukuchukua michango katika mikutano yetu iwayo yote popote kamwe hatukufanya wito wowote wa pesa. Hili bado lina nguvu. Kisha, pia, vitabu vyetu vya bure ambavyo huenda nje kila juma kwa juma hujumlisha mamia na maelfu ya dola juma baada ya juma, na mwaka baada ya mwaka, mbali na gharama ya kuijenga Taasisi. {2TG35: 23.4}
Na leo baada ya kupitia jinamizi la kudhani ningaliweza kuishi maisha ya umaskini, nilivyoelezea awali, mkopo wangu hauna mipaka, na hundi ninazoandika jumla yazo ni maelfu ya dola wiki baada ya wiki, na mwa-ka baada ya mwaka, ingawa mimi sina hati ya dhamana, similiki mali yoyote, na sina akaunti ya kibinafsi! Tena, mimi huwalipa makatibu wangu kiasi ambacho mimi hujilipa mwenyewe na wafanyikazi wangu wengine hu-walipa maradufu kiasi hicho. Naam, ipo miujiza mikubwa leo kama ilivyowahi kuwa. {2TG35: 24.1}
Yakobo, pia, hakuwa na haki yake mwenyewe ila alikuwa na bidii kubwa na heshima kwa haki ya Bwana. Esau, hata hivyo, ambaye hakujali haki ya Bwana aliiuza haki yake ya mzaliwa wa kwanza kwa mchuzi wa ndengu tu. Lilikuwa kama nini patano la Yakobo! Kama tokeo, hata hivyo, Yakobo akawa mkimbizi. Usiku wa kwanza mbali na nyumbani, hata hivyo, Mungu alikutana naye, na baada ya kumpa njozi, Yakobo aliweka tegemeo lake lote kwa Mungu na akaahidi kuwa mwaminifu katika majukumu yake yote. {2TG35: 24.2}
24
Kwanza alipokuwa Padan-Aramu, Yakobo hakuwa na chochote ila imani na bidii. Alikuwa tu mfanyakazi mzuri, ni hayo tu. Sifa hizi Labani alizitambua mara moja ndani ya Yakobo, na kama tokeo Labani hakujitolea tu kumpa binti yake Raheli kuwa mkewe, lakini hata akabuni mpango wa kumlazimisha kuwatwaa mabinti wote wawili — Raheli na Lea — wasichana pekee katika familia! Isitoshe, ingawa Yakobo alilipia sana kwa ajili yao miaka kumi na minne ya kufanya kazi ngumu kwa uaminifu, yeye katika miaka sita iliyofuata akawa mkwasi! Basi kwa kurejea nyumbani, kwa moyo wote, kwa uaminifu, na kwa dhamiri huru akamwambia Labani: {2TG35: 25.1}
“Miaka hii ishirini nimekaa kwako; kondoo wako na mbuzi wako wake hawakuharibu mimba, wala waume katika wanyama wako sikuwala.” Mwa. 31:38. {2TG35: 25.2}
Bado zaidi, alipoulizwa alichotaka kwa kazi yake baada ya miaka kumi na minne kukamilika, alichagua ujira ambao Mungu angelipa, sio Labani. Kwa maana alimwambia Labani: {2TG35: 25.3}
Usinipe chochote, lakini ruhusu nipite kati ya kundi lako lote la leo, na kuondoa kutoka humo ng’ombe wote wenye doa, wa madoadoa, na hudhurungi, kondoo na mbuzi, na uwapeleke safari ya siku tatu mbali na wale wengine ili isiwepo nafasi ya wao kuchangamana. Hadi leo, kondoo na ng’ombe wote, walio na doa au wasio na doa watakuwa wako, lakini baada ya hapa wote watakaozaliwa na doa kutoka kwa wasio na doa (inavyooneka-na haiwezekani) watakuwa wangu kwa kukutumikia! {2TG35: 25.4}
Labani alifurahishwa vyema na mkataba huo na Yakobo akaenda kufanya kazi. Mungu alibariki kazi za Yakobo licha ya kutowezekana kimaumbile, na ndani ya
25
miaka sita alikuwa mkwasi! Mbona? — Kwa sababu Yakobo alimtumikia Mungu kwa moyo wote, na alimwa-mini Yeye kabisa kwa maisha yake. Hakutaka chochote isipokuwa kile Mungu angemruhusu apate. Alijua kwambamaadamu anamfanyia Bwana kazi, Bwana hatamwacha kwa njaa wala uchi. Alijua kwamba iwapo Mungu aliyavika hivyo majani ya kondeni, Yeye angemvika na kumlisha katika shamba Lake la mizabibu. {2TG35: 25.5}
Kwa sababu Yakobo alikuwa akitajirika upesi sana, na kwa sababu babake mkwe alimtaka akae muda mrefu, na pia kwa sababu Yakobo alikuwa bado anamwogopa Esau, kwa nini alimwacha Labani, na mbona alianza ku-rejea nyumbani? — Jibu ni rahisi, kwa sababu Mungu alimwuliza kurejea, akisema: {2TG35: 26.1}
Mwa. 31:13 — “Mimi ni Mungu wa Betheli, huko ulikotia mafuta nguzo, na kuniwekea nadhiri: sasa on-doka, toka katika nchi hii, urudi mpaka nchi ile uliyozaliwa.”
Kutoka kwa kumbukumbu hii, unaona, Yakobo alikuwa mwaminifu kwa kazi yake, na alikuwa mwangalifu siku zote kwa amri ya Mungu. Je! Sisi ni kama Yakobo? Au sisi ni kama Yuda Iskariote? Yakobo, sasa unajua, alichukua utunzi kamili wa biashara ya Labani, na akafuata maelekezo ya Mungu wakati wote. Lakini Yuda Is-kariote alichukua utunzi kamili wa maslahi yake ya ubinafsi kwa gharama ya Zawadi ya Mungu, na badala ya kufuata maelekezo ya Bwana, alifuata yake. Sasa, hata hivyo, linganisha mwisho wa Yakobo na ule wa Yuda’. Kazi ya mmoja iliishia kwa utukufu na kazi ya mwingine iliishia kwa aibu na msiba. {2TG35: 26.2}
Unamfanyia nani kazi, Ndugu, Dada? kwa ajili yako mwenyewe au kwa ajili ya Mungu? — Unasema, “Kwa Mungu,” na ninatumai uko sawa, lakini kumbuka, kama nilivyosema awali, kwamba hakuna kampuni ya biashara
26
itakayomdumisha mfanyakazi ambaye havutiwi sana katika ufanisi wa kampuni yake jinsi alivyo katika kiwango cha mshahara wake. Isitoshe, hakuna kampuni inayovutiwa na shughuli binafsi ya mfanyakazi. Inavutiwa katika shughuli yake yenyewe. Shughuli ya Mungu, hata hivyo, ni muhimu zaidi, na ya matokeo muhimu sana kuliko shughuli ya mtu yeyote. Yeye, pia, havutiwi hata kidogo na shughuli yako ya ubinafsi, Anavutiwa na shughuli Yake ya kuziokoa nafsi. Huwezi, kwa hivyo, kufanya masilahi yako mwenyewe ya umuhimu wa kwanza na Yake kuwa ya pili, na wakati uo huo utarajie kuvuna ahadi Zake, na kumtarajia Yeye ajibu maombi yako. Iwapo hivi ndivyo ilivyo, basi unajiita eti Mkristo kwa uongo. Kwa mujibu wa Mathayo 6:32, wewe bado ni mtu wa Mataifa uliyedanganyika. {2TG35: 26.3}
Kuwa Mkristo machoni pa Mungu sio lazima ujisifu, ila msifu Mungu na wema Wake. Usijigambe kamwe kwa maslahi na mafanikio yako, ila ujivunie ya Mungu. Usijaribu kamwe kuendeleza shughuli yako, bali kila wakati jaribu kuendeleza ya Mungu. Kamwe usiombe nuru ujue la kufanya, na mahali pa kwenda ili kwamba shughuli, masilahi yako yaweze kufanikiwa, ila badala yake omba nuru ili Mungu akusaidie kufanya jambo hilo au kwenda mahali utaweza kuhudumu kwa kazi Yake, kwamba Yeye akuongoze na kukufunza jinsi ya kuuen-deleza ufalme Wake. Kisha, wakati huo tu, utapata kwamba hautakosea kamwe! Nia yoyote ile isipokuwa hii itakupeleka pale ambapo Mungu hataki uende, na pale ambapo utalazimika kuubeba mzigo wako mwenyewe bila Yeye. {2TG35: 27.1}
Nimeona watu kadhaa wakiapa kwa mbingu na nchi kwamba Mungu amewaongoza hapa au pale, ndani ya hili au lile lingine. Lakini wakati mambo hayakuwafurahisha, basi walijiondoa wakiapa kwa bidii kwamba laiti Mungu hakuwa amewaongoza
27
ndani yake! Na tena kuapa kwa bidii kama vile hapo awali kwamba Mungu anawaondoa ndani yake, na hadi katika kitu fulani bora! Walijihisi tena kuwa vyema kwamba Mungu alikuwa akiongoza katika hatua zao, ingawa ilikuwa kinyume cha lile walifikiri Yeye alikuwa amewaongoza ndani yake hapo awali! {2TG35: 27.2}
Wengine wamejihisi kwamba Mungu alikuwa amewafungulia njia ya kufanya hili au lile lingine kwa ukweli kwamba waliweza kupata pesa za safari, au kupata mnunuzi wa kitu kimoja au kingine, kupata hiki na kupata kile. Bado wengine walinambia kwamba walifungua Bibilia bila utaratibu, na ya kwamba macho yao yalitua kwa aya ambayo iliashiria kibali cha Mungu kwa hatua yao. Ndugu mmoja alinambia kwamba alikuwa ameigeuza sarafu na mwingine alikuwa ameupata mshale wa Kihindu ukielekeza kwa mwelekeo aliopaswa kwenda! Haya yote nimeyaona yakikosa kufaulu ingawa ishara hizi zilishikiliwa kama vithibitisho vizuri vya mapenzi ya Mungu katika maswala husika. {2TG35: 28.1}
Niruhusu niwaambie kwamba ishara hizi zenyewe ndani yake ni dhana ya ufidhuli wa upeo zaidi, ndoto na kamari, sio ishara za Mungu hata kidogo. Isitoshe, mipango ya mtu yeyote ambayo ina msingi kwa maslahi ya ubinafsi, ya msingi kwa ni wapi na jinsi gani mtu anaweza kuboresha miradi yake ya faida wakati anajidai kuwa Mkristo, — nawaambia kwamba hii yote ni miradi, sio mipango ya Mungu hata kidogo, bila kujali njia itavyofun-guka, au kitakachotukia. Ukweli ni kwamba Mungu kamwe hapewi nafasi ya kuelekeza katika mambo haya, maana kumpa Yeye fursa hiyo, Anasema, “Bali utafuteni kwanza Ufalme wa Mungu, na haki Yake; na hayo yote mtazidishiwa.” {2TG35: 28.2}
Basi, unapoufanya Ufalme wa Mungu
28
maslahi yako makuu, basi kwa uhakika utajikuta katika mahali sahihi kwa wakati unaofaa, ukitenda jambo sahihi ukivuna baraka bora za Mungu. Basi unaweza kutulia kwa uhakika kwamba Yeye atakufungulia njia na ku-kupeleka pale unahitaji kuwa hata iwapo Yeye atakuinua kutoka kisimani, na kuwaambia Waishmaeli wakupeleke hadi Misri na kukuweka ufanye kazi katika nyumba ya Potifa. Yeye anaweza hata kukupeleka gere-zani kabla Akuketishe pamoja na Farao kwenye kiti cha enzi. Au Yeye anaweza kusababisha ukimbie kutoka Misri na akufanye uwachunge kondoo pande zote za Mlima Horebu. Anaweza kukuleta dhidi ya Bahari ya Shamu wakati ambapo Wamisri wanakuandama. Anaweza kukuleta jangwani ambapo hakuna maji au chakula. Simba na dubu wanaweza kuja kuwanyakua kondoo wako, Goliathi kuwaua watu wako, na mfalme anaweza kukutupa katika tanuru ya moto, au katika tundu la simba. {2TG35: 28.3}
Naam, mamia na maelfu ya mambo yanaweza kutukia, lakini yeye anayemwamini Mungu na kufanya kazi Yake vyema atapata hivi vyote vinavyojulikana eti vizuizi au misiba kuwa ukombozi wa ajabu, na njia za kufan-ikiwa, vyote vikitimiza mipango ya ajabu ya Mungu, na njia ya Mungu kuelekea kukwezwa kwako kutoka kwa jambo moja kubwa hadi kwa lingine. Unapokuwa katika utunzi wa Mungu na kwa udhibiti Wake kamwe usiseme Ibilisi alifanya hili au lile bila kujali ni nini, kwa maana hawezi kufanya chochote isipokuwa ameruhusi-wa kukifanya. Sku zote mpe Mungu sifa. {2TG35: 29.1}
Nalikuja Marekani, sio kwa sababu nalitaka, lakini kwa sababu Mungu alitaka nije. Na kwa sababu sikujua ka-zi yangu ya siku zijazo, na kwa vile Mungu wakati huo hangeweza kunifanya nielewe zaidi kuliko vile alivyoweza kumfanya Yusufu aelewe safari yake ya kwenda Misri, nilifukuzwa wakati huo nje ya nchi kwa mtutu wa bunduki kama vile Musa alivyofukuzwa kutoka Misri, ingawa sikuwa
29
nimefanya chochote kujiletea taabu. Na unafikiri ni nani aliyewaongoza waasi kunitimua nje ya nchi? Si mwingine ila Askofu wa kanisa la Orthodoksi la Ugiriki wa jimbo hilo! Na unadhani ni wapi alipoidhamini kampeni yake ya kuniandama? Kanisani Jumapili asubuhi akiwa katika mavazi yake kamili na karibu futi ishirini kutoka pale niliposimama! {2TG35: 29.2}
Wakati huo sikujua kwenda mbali kwangu kutoka nyumbani hadi katika nchi ya mbali kama hiyo kulihusu ni-ni, lakini sasa najua kama vile Yosefu alivyojua kwamba tumaini la nduguze kuushinda mpango wa Mungu kwa ajili yake ulikuwa ni mpango wa Mungu kumpeleka Misri. Na hivyo badala ya kuuzuia mpango huo, hakika wa-lisababisha mpango huo utekelezwe! {2TG35: 30.1}
Wakati mambo yanaenda kinyume cha mapenzi na nia ya mtu leo, Wakristo wengi humpa Ibilisi sifa. Ni wa-kati tu mambo yanapokwenda kulingana na wanavyotaka wao humpa Mungu sifa! Balaamu, pia, alifurahi wa-kati njia ilifunguliwa kwake kwenda kwa Balaki, lakini malaika wa Bwana alipoizuia barabara ambayo alikuwa akisafiri kwayo, basi Balaamu, akapata kichaa kama mbwa na kumpiga punda. {2TG35: 30.2}
La, hakuna chochote ila wewe mwenyewe unaweza kuushinda mipango ya Mungu kwa ajili yako. Wawe ni marafiki zako au maadui zako, wawe ni wanyama au wafalme, utawapata wote bila kujua au kwa kujua wakitenda kazi kwa ajili ya manufaa yako badala ya madhara kwako ikiwa unayatekeleza maagizo ya Mungu. Mbingu ni rasilimali kubwa kama nini! Na ni nani anayeijua! {2TG35: 30.3}
Kumbuka sasa, kwamba chochote kitakachoweza kusimama njiani mwako, iwe ni Bahari ya Shamu au Mto Yordani, uwe ni mlima au liwe ni jangwa, kitakuwa haswa ngazi yako ya kupandia. {2TG35: 30.4}
Kama hii ndio haki ya Bwana
30
Bwana, na unaweza kuipata kwa gharama ya haki yako mwenyewe. Kisha utapata njia za Bwana zikiwa juu zaidi kuliko zako kama vile Mbingu ilivyo juu sana kuliko nchi. Hili litakapotukia, ndipo wewe tu utasema kwa ufahamu, “Bwana ni Haki yetu.” {2TG35: 30.5}
“Utamlinda yeye ambaye moyo wake umekutegemea Wewe: kwa kuwa anakutumaini. Mtumainini Bwana siku zote; maana Bwana YEHOVA ni mwamba wa milele: kwa kuwa Yeye umewashusha wakaao juu; mji ule ulioinuka, Yeye aushusha; Yeye aushusha hata nchi; Yeye huuleta hata mavumbini. Mguu utaukanyagia chini, naam hata miguu yao walio maskini, na hatua zao walio wahitaji.” Isa. 26:3-6. {2TG35: 31.1}
31
Jumuiya ya Wadaudi Waadventista wa Sabato
(Ushirika Huru Unaojumuisha Kanisa)
Mlima Karmeli, Waco, Texas
S.L.P. 23738, Waco, TX 76702
+ 1-254-855-9539
www.gadsda.com
info@gadsda.com
Gombo la 2, Namba 35
Kimechapishwa nchini Marekani
32