15 Jun Gombo la 2 Salamu Mwafaka Namba 31, 32
Gombo la 2 Salamu Mwafaka Namba 31, 32
AMANI YA PEKEE YA MAWAZO
Hati miliki, Kimechapishwa tena 1948
Haki zote zimehifadhiwa
V. T. HOUTEFF
UREJESHO NA WAKATI
MTU AKIFA ATAWEZAJE KUISHI TENA? NA ATAKUWA KAMA NINI?
1
ANDIKO LA SALA
Fanya Kazi Yako; Mwachie Mungu Matokeo
Nitasoma kutoka katika Mafunzo ya Kristo kwa Mifano, ukurasa wa 64, kuanzia aya ya mwisho: {2TG31: 2.1}
“Kazi ya mpanzi ni kazi ya imani. Siri ya kuota na ukuaji wa mbegu yeye hawezi kuelewa. Lakini anayo imani katika vyombo ambavyo Mungu hutumia kusababisha mimea kunawiri. Kwa kuitupa mbegu yake ardhini, inaonekana anatupa nafaka ya thamani ambayo inaweza kutoa chakula kwa familia yake. Lakini anaacha tu ya sasa nzuri kwa ajili ya pato kubwa. Yeye hutupa mbegu, akitarajia kuikusanya maradufu nyingi katika mavuno mengi. Hivyo ndivyo watumwa wa Kristo wanapaswa kufanya kazi, wakitarajia mavuno kutoka kwa mbegu wanayopanda…. Katika kazi yetu ya maisha hatujui ni ipi itakayofanikiwa, hii au hiyo. Hii sio hoja yetu kutatua. Tunapaswa kufanya kazi yetu, na kumwachia Mungu matokeo.” {2TG31: 2.2}
Hebu tuombe kwa ajili ya imani, kisha twende kwa furaha katika shamba la mizabibu na kupanda mbegu am-bayo Bwana ametoa kwa neema, tukikumbuka ahadi Yake kwamba Neno Lake halitamrudia bure, bali kwamba litafanikiwa katika mambo yale Aliyolituma. Lazima tukumbuke, pia, kwamba imani ndio kipandio cha kwanza cha ngazi kwa wokovu, na ya kwamba bila imani hatuwezi kumpendeza Mungu. {2TG31: 2.3}
2
UREJESHO NA WAKATI
ANDIKO LA HOTUBA NA V. T. HOUTEFF
MCHUNGAJI WA WADAUDI WAADVENTISTA WA SABATO
SABATO, MACHI 13, 1948
HEKALU LA MLIMA KARMELI
WACO, TEXAS
Maandiko yetu yanapatikana katika sura ya tatu ya Matendo: {2TG31: 3.1}
Matendo 3:19-21 — “Tubuni basi, muongoke, ili dhambi zenu zifutwe, zipate kuja nyakati za kuburudishwa kwa kuwako kwake Bwana; Apate kumtuma Kristo Yesu, Ambaye mlihubiriwa tangu zamani: Ambaye ilim-pasa kupokewa mbinguni hata zije zamani za kurejeshwa kwa mambo yote, yaliyonenwa na Mungu kwa kin-ywa cha manabii Wake wote watakatifu tokea mwanzo wa ulimwengu.”
Hapa tunaambiwa kwamba mbingu lazima zimpokee Bwana, sio milele, bali hadi wakati wa “kurejeshwa kwa mambo yote.” Yeye, kwa hivyo, kwa wakati wa urejesho atarudi duniani. {2TG31: 3.2}
Je! Huku kurudi kutakuwa kusikotarajiwa? au Bwana atamtuma mtu fulani kwanza kuitengeneza njia Yake? Na ikiwa mtu atatangulia kuja Kwake, atakuwa nani? — “Akajibu, akawaambia, Kweli, Ni kweli Eliya yuaja kwanza, na kurejesha mambo yote.” Marko 9:12. Bwana, zaidi ya hayo, kupitia nabii Malaki anatangaza: {2TG31: 3.3}
Mal. 3:1; 4:5 — “Angalieni, namtuma mjumbe Wangu, naye ataitengeneza njia mbele Yangu; naye Bwana Mnayemtafuta atalijilia hekalu Lake ghafula.
3
naam, yule mjumbe wa agano mnayemfurahia, angalieni, anakuja, asema Bwana wa majeshi.… Angalieni, Nitawapelekea Eliya nabii, kabla haijaja siku ile ya Bwana, iliyo kuu na kuogofya.”
Hapa Maandiko huonyesha kwamba mtu fulani katika roho na nguvu ya Eliya nabii lazima ataonekana kwan-za, na hataitengeneza njia tu, bali pia atareyarejesha mambo yote. Kwa udhahiri, ujumbe wa Eliya utayarejesha mambo yote katika siku kuu na ya kuogofya ya Bwana, siku ya urejesho, siku ambayo Bwana atakuja kwa heka-lu Lake, Kanisa. Roho ya Eliya ilikuwa roho dhidi ya ibada ya sanamu, na nguvu yake ilikuwa nguvu ya ku-waangamiza wale walioongoza katika ibada ya sanamu, na kuleta utakatifu. {2TG31: 4.1}
Aya ya 2, 3 — “Lakini ni nani atakayestahimili siku ya kuja Kwake? Au ni nani atakayesimama atakapoon-ekana Yeye? Kwa maana Yeye ni mfano wa moto wa mtu asafishaye fedha, ni mfano wa sabuni ya mtu afuaye nguo; Naye ataketi kama asafishaye fedha na kuitakasa, Naye atawatakasa wana wa Lawi, atawasafisha ka-ma dhahabu na fedha; nao watamtolea Bwana dhabihu katika haki.”
Kwa ujio huu Yeye hatawapeleka watakatifu Wake katika majumba huko juu, lakini Atawatakasa wana wa Lawi — ukasisi; Atawaangamiza viongozi wa ibada ya sanamu. Kwa sababu utakatifu wa watumwa Wake un-astahili kwanza kurejeshwa, urejesho, kwa hivyo, unaanzia ndani ya Kanisa. Hivi ndivyo hali ya Edeni ya amani na usalama itakavyorejeshwa, maana tunaambiwa kwamba– {2TG31: 4.2}
Isa. 11:6-9 — “Mbwa-mwitu atakaa pamoja na mwana-kondoo, na chui atalala pamoja na mwana-mbuzi; ndama na mwana-simba na
4
kinono watakuwa pamoja, na mtoto mdogo atawaongoza. Ng’ombe na dubu watalisha pamoja; watoto wao watalala pamoja; na simba atakula majani kama ng’ombe. Na mtoto anyonyaye atacheza penye tundu la nyoka, na mtoto aliyeachishwa atatia mkono wake katika pango la fira. Hawatadhuru wala hawataharibu katika mlima Wangu wote mtakatifu; maana dunia itajawa na kumjua Bwana, kama vile maji yanavyoifunika bahari.”
Ndivyo ilivyokuwa Edeni, na ndivyo lazima iwe tena iwapo mambo yote yatarejeshwa, na ikiwa unabii huu utatimizwa. {2TG31: 5.1}
Aya ya 10 — “Na itakuwa katika siku hiyo, shina la Yese lisimamalo kuwa ishara kwa kabila za watu, yeye ndiye ambaye Mataifa watamtafuta; na mahali Pake pa kupumzikia patakuwa na utukufu.”
“Katika siku hiyo” — yaani, katika siku amani hii ya Edeni na usalama — wakati huo, sio baadaye, Ufalme wa Yuda na Israeli utarejeshwa (Ezek. 37:16-28) na kufanywa usimame kuwa ishara. Mataifa watautafuta. Urejesho huu wa Yuda na Israeli, kwa hivyo, unatukia katika wakati wa rehema, kwa maana Mataifa wataitafuta hiyo “ishara.” Kwa udhahiri, basi, Mataifa watakuwa bado wangalipo wakati ambapo amani na usalama wa Edeni utarejeshwa kwa watu wa Mungu katika siku kuu na ya kuogofya. {2TG31: 5.2}
“Basi kwa ajili yenu, Zayuni utalimwa kama shamba lilimwavyo, na Yerusalemu utakuwa magofu, na mlima wa nyumba utakuwa kama mahali palipoinuka msituni…. Lakini itakuwa katika siku za mwisho ya kwamba mli-ma wa nyumba ya Bwana utawekwa imara juu ya milima, nao utainuliwa juu
5
vilima; na watu watu wa mataifa watauendea makundi makundi. Na mataifa mengi watakwenda, na kusema, Njoni, twende juu mlimani kwa Bwana, na nyumbani kwa Mungu wa Yakobo; naye atatufundisha njia zake, nasi tutakwenda katika mapito yake: kwa maana katika Zayuni itatoka sheria, na neno la Bwana litatoka Ye-rusalemu.” Mika 3:12; 4:1,2. {2TG31: 5.3}
Ni wazi kwamba baada ya kutapanywa kwa Wayahudi, na baada ya kwa Yerusalemu wa Kale, katika enzi ya Ukristo, katika siku za mwisho, kisha inakuwa kwamba urejesho wa mambo yote unatukia; na ukweli kwamba watu wengi wakati huo watajiunga na Bwana, urejesho kwa hivyo unatukia katika wakati wa rehema, katika siku kuu na ya kuogofya. “Ishara,” pia, itasimama wakati huo na kwayo Mataifa wataitafuta. Siku hiyo itakuwa kuu kwa wenye haki, na ya kutisha kwa wenye dhambi. {2TG31: 6.1}
Zekaria 14:4, 5 — “Na siku hiyo miguu Yake itasimama juu ya Mlima wa Mizeituni, unaoelekea Yerusalemu upande wa mashariki, nao mlima wa Mizeituni utapasuka katikati yake, upande wa mashariki na upande wa magharibi; litakuwako huko bonde kubwa sana; na nusu ya mlima ule utaondoka kwenda upande wa kaskazi-ni, na nusu yake itaondoka kwenda upande wa kusini. Nanyi mtakimbia kwa njia ya bonde la milima; kwa maana bonde lile la milima litaenea hata Aseli; naam, mtakimbia, kama vile mlivyokimbia mbele ya tetemeko la nchi, siku za Uzia, mfalme wa Yuda; na Bwana, Mungu wangu, atakuja, na watakatifu wote pamoja naye.”
“Katika siku hiyo.” Katika siku gani? — Katika siku ambayo mataifa yote yanakusanyika dhidi ya Yerusalemu ambao sasa upo, na kuleta anguko lake kutoka kwa utawala wa Mataifa. Siku hiyo miguu ya Bwana itasimama juu ya Mlima wa Mizeituni. Mlima wa Mizeituni utapasuka
6
katikati yake kuelekea mashariki na magharibi, kutakuwa na bonde kubwa sana; “Na nusu ya mlima ule utaondoka kwenda upande wa kaskazini, na nusu yake itaondoka kwenda upande wakusini.” Zek. 14:4. Ujio wa Bwana baada ya millenia, pia, utakuwa sawa na huu. Tazama Maandishi ya Awali, uk. 51, 52. {2TG31: 6.2}
Watumwa wa Mungu wakati huo watakimbia hadi kwenye bonde la milima, pale ambapo miguu ya Bwana itasimama, na watakatifu wote pamoja nao; yaani, “miguu” ya Bwana itafungua njia ya kurejeshwa kwa Ufalme, na ya kuwakusanya watu ndani yake. {2TG31: 7.1}
Isa. 11: 11-14 — “Na itakuwa katika siku hiyo, Bwana atapeleka mkono Wake mara ya pili, ili ajipatie watu Wake watakaosalia, kutoka Ashuru, na kutoka Misri, na kutoka Pathrosi, na kutoka Kushi, na kutoka Elamu, na kutoka Shinari, na kutoka Hamathi, na kutoka visiwa vya bahari. Naye atawatwekea mataifa bendera, atawakutanisha watu wa Israeli waliotupwa, atawakusanya watu wa Yuda waliotawanyika, kutoka ncha nne za dunia. Na wivu wa Efraimu utaondoka, na wale wanaomwudhi Yuda watakatiliwa mbali; Efraimu hatam-husudu Yuda, wala Yuda hatamwudhi Efraimu. Nao watashuka, watalirukia bega la Wafilisti upande wa ma-gharibi; nao pamoja watawateka wana wa mashariki; watanyosha mkono juu ya Edomu na Moabu; na wana wa Amoni watawatii.”
Hapa tunaona kwamba itakuwapo amani katika “bonde la milima” — amani kati ya mnyama na mnyama, na pia kati ya mwanadamu na mwanadamu, kwa sababu simba hatamdhuru mwana kondoo, na Yuda hatamwudhi Efraimu, na Efraimu hatamhusudu
7
Yuda. Yuda na Efraimu hata hivyo watakuwa vitani na nchi zinazoizunguka nchi, kwa maana watayarukia ma-bega ya Wafilisti, na kunyosha mkono juu ya Edomu na Moabu. Waamoni, hata hivyo, watawatii. {2TG31: 7.2}
Aya ya 15 — “Na Bwana atauangamiza kabisa ulimi wa bahari ya Misri; na kwa upepo Wake uteketezao ata-tikisa mkono Wake juu ya Mto, Naye ataupiga, uwe vijito saba, na kuwavusha watu wenye viatu vikavu.”
Naam, Bwana atafungua njia kwa ajili ya kuwakusanya watu Wake. Kutoka kwa leo, kwa hivyo, kutakuwa kama Kutoka kwa jana, kwa kiwango kikubwa tu zaidi. Watu wa Mungu katika siku hizi za mwisho wa-takusanywa kutoka kila nchi, sio kutoka nchi ya Misri. {2TG31: 8.1}
Aya ya 16 — “Itakuwako njia kuu kwa mabaki ya watu Wake watakaobaki, watokao Ashuru, kama vile il-ivyokuwako kwa Israeli, katika siku ile waliyotoka katika nchi ya Misri.”
Hivyo ndivyo ufalme wa Yuda na Israeli utarejeshwa, na kupewa amani na wingi. {2TG31: 8.2}
Mika 4:4 — “Bali wataketi kila mtu chini ya mzabibu wake, na chini ya mtini wake; wala hapana mtu ataka-yewatia hofu; kwa kuwa kinywa cha Bwana wa majeshi kimesema hivi.”
Na sasa hii ndiyo nuru ya Mungu, na hili ndilo ombi Lake: {2TG31: 8.3}
Isa. 2:5 — “Enyi nyumba ya Israeli, njoni, twende katika nuru ya Bwana.”
Ujumbe wa Eliya unaorejesha mambo
8
yote kwa kweli ni nyongeza kwa Ujumbe wa Malaika wa Tatu, na hakika utaufanya uumke kuwa kilio kikuu. Utawakusanya watu wa Mungu kutoka pembe nne za dunia, na kuwatoa kutoka Babeli wakati nchi inaangazwa kwa utukufu wa yule malaika (Ufu. 18:1-4). (Tazama Maandishi ya Awali, uk. 277.) {2TG31: 8.4}
Kama vile safina ya Nuhu ilihifadhi kila kitu chenye uhai ambacho kingekaa kwa dunia baada ya gharika, vivyo hivyo Ufalme uliyorejeshwa wa Yuda na Israeli utakusanya na kuhifadhi kutoka kwa mapigo kila kitu chenye uhai ambacho kitakaa kwa dunia mpya; Ufalme uliorejeshwa utakuwa safina katika siku yetu, na watu wake wataishi na kutawala miaka elfu na Kristo (Ufu. 20:4), na mwishowe kurudi wakati dunia itakapokuwa imeumbwa upya. {2TG31: 9.1}
Isa. 65:17, 18, 25 — “Maana, tazama, Mimi naumba mbingu mpya na nchi mpya, na mambo ya kwanza hayatakumbukwa, wala hayataingia moyoni. Lakini furahini, mkashangilie daima, kwa ajili ya hivi Nivi-umbavyo; maana, tazama, Naumba Yerusalemu uwe shangwe, na watu wake wawe furaha. Mbwa-mwitu na mwana-kondoo watalisha pamoja, na simba atakula majani kama ng’ombe; na mavumbi yatakuwa chakula cha nyoka. Hawatadhuru wala kuharibu katika mlima Wangu mtakatifu wote, asema Bwana.”
Bila shaka wale wanaotafuta kuingia katika safina hii ya usalama wataishi na kutawala na Kristo wakati wa miaka elfu moja, na wale ambao wanapuuza watalala bila pumzi katika “shimo la kuzimu” hadi kwa ufufuo wa baada ya millenia, kuamka tu kwa aibu na kudharauliwa milele, kupatwa na mateso ya mauti ya pili. {2TG31: 9.2}
Ni muhimu namna gani, basi, kwamba tusipate lepe la usingizi, ila kwamba tuamke na kujivika vazi la harusi
9
sasa ili tusije tukajikuta tukilia na kusaga meno yetu, hata vibaya zaidi kuliko walivyofanya walioishi kabla ya gharika nje ya safina mvua ilipokuja na umeme na radi zililipuka angani wakati vilindi vya maji vilivunjika. {2TG31: 9.3}
Tumeona sasa kwamba urejesho wa “mambo yote” unaanza na kuwakusanya watu katika Yuda, na ya kwam-ba Ufalme unakamilika wakati dunia imeumbwa upya. Hebu sisi kwa hivyo tufanye kile tunachoweza kusaidia kuijenga safina sasa na kuingia ndani yake na nafsi nyingi iwezekanavyo, kwa maana ufunuo wa Uvuvio wenyewe wa Ukweli huu unaonyesha kwamba tunakaribia siku ya urejesho wa mambo yote, kwamba huu ni ujumbe ya saa hii. {2TG31: 10.1}
10
Wazo Zito
Ee wazo zito! na linaweza kuwa
Saa ya Hukumu sasa imekuja,
Ambayo punde itakata shauri hatima yetu,
Na kutia muhuri adhabu ya kutisha ya mdhambi?
Naam, ni hivyo; saa ya Hukumu
Inaharakisha kwa kasi kufunga kwake;
Basi Jaji, kwa uwezo mkuu,
Ashuke kulipiza kisasi kwa adui Zake.
Yeye aliyekuja duniani kufa,
Sadaka kwa dhambi ya wanadamu,
Na kisha akapanda juu sana,
Na muda mfupi atarudi tena,
Anasimama sasa mbele ya sanduku la agano,
Na kiti cha rehema, na makerubi.
Kudai damu Yake kwa ajili ya watakatifu, na kufanya
Ukumbusho wa mwisho wa dhambi yao.
Wakati muhimu ukaribu
Wakati sisi ambao jina lake tumekiri,
Kila mmoja kwa kura yake lazima asimame,
Na kupita mtihani wa mwisho, wa upekuzi.
Yesu! tunatumaini ndani Yako pekee;
Kwa rehema sasa tuangalie,
Kiri majina yetu mbele ya kiti cha enzi,
Na zifute dhambi zetu kutoka kwa kitabu Chako.
Ee Mwokozi Aliyebarikiwa! Tuweze kuhisi
Umuhimu kamili wa saa hii.
Vuvia mioyo yetu na bidii takatifu,
Na utusaidie kwa nguvu ya Roho Wako,
Ili tuweze, kwa nguvu Zako, kuwa imara,
Na kujasiri vita kwa ushujaa;
Kisha, juu ya Mlima Zayuni, kuungana na wimbo,
Na kueneza sifa za ushindi.
–R. F. Cottrell.
11
MTU AKIFA ATAWEZAJE KUISHI TENA? NA ATAKUWAJE ?
ANDIKO LA HOTUBA NA V. T. HOUTEFF
MCHUNGAJI WA WADAUDI WAADVENTISTA WA SABATO
SABATO, MACHI 20, 1948
HEKALU LA MLIMA KARMELI
WACO, TEXAS
“Maana ikiwa twaamini kwamba Yesu alikufa akafufuka, vivyo hivyo na hao waliolala katika Yesu Mungu atawaleta pamoja Naye. Kwa kuwa twawaambieni haya kwa neno la Bwana, kwamba sisi tulio hai na tutakaosa-lia hata wakati wa kuja kwake Bwana hakika hatutawatangulia wao waliokwisha kulala mauti. Kwa sababu Bwana Mwenyewe atashuka kutoka mbinguni pamoja na mwaliko, na sauti ya malaika mkuu, na parapanda ya Mungu: nao waliokufa katika Kristo watafufuliwa kwanza: kisha sisi tulio hai na tuliosalia tutanyakuliwa pamo-ja nao katika mawingu, ili tumlaki Bwana hewani: na hivyo tutakuwa na Bwana milele. Basi farijianeni kwa maneno hayo.” 1 The. 4:14-18. {2TG32: 12.1}
Hapa tunaona kwamba wale watakaokuja katika ufufuo wa kwanza hawataishi tena tu, bali hawatakufa tena. {2TG32: 12.2}
Sasa ili kupata jibu letu kwa swali, Mtu atawezaje kuishi tena? Kwanza tutafungua kitabu cha Mwanzo: {2TG32: 12.3}
Mwa. 2:7 — “Bwana Mungu akamfanya mtu kwa mavumbi ya ardhi, akampulizia puani pumzi ya uhai; mtu akawa nafsi hai.”
12
Katika andiko hili tunaambiwa kwamba Mungu alimuumba mtu kutoka kwa mavumbi ya ardhi. Kisha pumzi ya uhai ikapulizwa puani mwake, na hivyo akawa nafsi hai, kwamba pumzi na mwili pamoja ndio huifanya nafsi. Mchakato wa maendeleo ni sawa na mchakato wa kutengeneza barafu — halijoto ya chini na maji hutengeneza barafu kama vile mwili na pumzi huifanya nafsi. Kwa hivyo wakati pumzi inauacha mwili, mwanadamu sio tena nafsi hai — la, si zaidi ya barafu ni barafu baada yake kuwa maji. Mtu bila shaka hana nafsi iliyopo baada ya pumzi kuuacha mwili wake, maana mwili na pumzi kwa pamoja huifanya nafsi. {2TG32: 13.1}
“Najua” asema mwenye hekima, “kwamba, kila kazi aifanyayo Mungu, itadumu milele; haiwezekani kuizid-isha kitu, wala kuipunguza kitu; nayo Mungu ameifanya, ili watu wamche Yeye.” Muh. 3:14. {2TG32: 13.2}
Muh. 9:5,6 — “Kwa sababu walio hai wanajua ya kwamba watakufa; lakini wafu hawajui neno lo lote, wala hawana ijara tena; maana kumbukumbu lao limesahauliwa. Mapenzi yao na machukio yao, na husuda yao, imepotea yote pamoja; wala hawana sehemu tena katika jambo lo lote linalofanyika chini ya jua.”
Muh. 3:18-21 — “Nikasema moyoni mwangu, Ni kwa sababu ya wanadamu, ili Mungu awajaribu, nao waone ya kuwa wao wenyewe wafanana na wanyama. Kwa maana linalowatukia wanadamu linawatukia wanyama; jambo moja lawatukia; anavyokufa huyu ndivyo anavyokufa huyu; naam, wote wanayo pumzi moja; wala mwanadamu hana kitu cha kumpita mnyama; kwa maana yote ni ubatili. Wote huendea mahali pamoja; wote hutoka katika mavumbi; na hata mavumbini hurudi tena.
13
Ni nani ajuaye kama roho ya binadamu huenda juu, na kama roho ya mnyama huenda chini?”
Uvuvio unaona, kwanza hutuambia jinsi mwanadamu aliumbwa na jinsi alivyo, kisha Huuliza wazi: “Ni nani ajuaye kama roho ya mwanadamu huenda juu, na na kama roho ya mnyama huenda chini?” — Jibu la pekee am-balo linaweza kutolewa ni kwamba hakuna mtu ajuaye ila Mungu. Na kwa sababu Ametuambia kwamba mwili na pumzi pamoja, sio mbali mbali, huifanya nafsi, basi ni dhahiri kwamba mtu aliyekufa hana nafsi, kwamba mwili hurudi kwa mavumbi, na pumzi huirudia pumzi, kwa upepo. Isitoshe, linalomtukia mnyama lilo hilo humtukia mwanadamu. Wote wawili wanayo pumzi moja, hutangaza Uvuvio, na mmoja hana ukuu zaidi ya mwingine. {2TG32: 14.1}
Hili ndilo Mungu hunena kuihusu nafsi, na tunapaswa kumwamini Yeye badala ya kujipumbaza kwa nadharia ambazo hazijavuviwa za watu ambao kwa kimbelembele husema kwamba nafsi haifi kamwe, ingawa Mungu husema, “Nafsi ile itendayo dhambi, itakufa.” Ezek. 18:4. Hivyo, mwanadamu anapokufa, nafsi yake hutoweka kama ifanyavyo barafu wakati halijoto hupanda juu ya kiwango mgando. {2TG32: 14.2}
Ijayo ili kupata mtu atakakuwa kama nini anapofanywa kuishi tena maisha bila dhambi, tunapaswa kuona mwanadamu aliama nini kabla ya kutenda dhambi: {2TG32: 14.3}
Mwa 3:6-8 — “Mwanamke alipoona ya kuwa ule mti wafaa kwa chakula, wapendeza macho, nao ni mti wa kutamanika kwa maarifa, basi alitwaa katika matunda yake akala, akampa na mumewe, naye aka-la. Wakafumbuliwa macho wote wawili wakajijua kuwa wa uchi,
14
wakashona majani ya mtini, wakajifanyia nguo. Kisha wakasikia sauti ya Bwana Mungu, akitembea bustanini wakati wa jua kupunga; Adamu na mkewe wakajificha kati ya miti ya bustani, Bwana Mungu asiwaone.”
Mara baada ya Adamu na Hawa kula tunda lililokatazwa, badiliko la kushangaza lilitukia. Wao mara moja wakafahamu kwamba nuru ya uzima na uzuri ambayo walikuwa wamevikwa nayo imetoweka, wakajiona kuwa uchi, sura mbaya na wa aibu kwa jicho. Kwa sababu hiyo walijaribu kujifunika kwa majani na kujificha kati ya miti. Jani lile la kujifunika, hata hivyo, halikuwafunika ipasavyo, na kwa hivyo Bwana akawafanyia “mavazi ya ngozi.” {2TG32: 15.1}
Mtu atakuwaje iwapo ataishi tena? – Hakika sio mpungufu kuliko alivyokuwa hapo mwanzo kwa maana yote yaliyopotezwa yatarejeshwa. Wala hatastahili kuboreshwa, kwa maana kila kitu alichokiumba Bwana, Yeye Mwenyewe alitamka “ni chema sana.” Mwa. 1:31. Na kwa hivyo ikiwa mtu ataishi tena, atakuwa sawasawa jinsi Adamu alivyokuwa kabla ya kufanya dhambi. {2TG32: 15.2}
Sasa kwa ajili ya jibu kwa lile swali, “Atawezaje kuishi tena?” Tutaelekea kwa Ezekieli– {2TG32: 15.3}
Ezekieli 37:1-10 — “Mkono wa Bwana ulikuwa juu yangu, naye akanichukua nje katika roho ya Bwana, akaniweka chini, katikati ya bonde; nalo limejaa mifupa; akanipitisha karibu nayo pande zote; na tazama, palikuwa na mifupa mingi katika ule uwanda! Nayo, tazama, ilikuwa mikavu sana. Akaniambia, Mwanadamu, je! Mifupa hii yaweza kuishi? Nami nikajibu, Ee Bwana MUNGU, wajua wewe. Akaniambia tena, Toa unabii juu ya mifupa hii,
15
uiambie, Enyi mifupa mikavu, lisikieni neno la Bwana. Bwana MUNGU aiambia mifupa hii maneno haya; Tazama, nitatia pumzi ndani yenu, nanyi mtaishi. Nami nitatia mishipa juu yenu, nami nitaleta nyama iwe juu yenu, na kuwafunika ngozi, na kutia pumzi ndani yenu, nanyi mtaishi; nanyi mtajua ya kuwa mimi ndimi Bwana.”
“Basi nikatoa unabii kama nilivyoamriwa; hata nilipokuwa nikitoa unabii, palikuwa na mshindo mkuu, na tazama, tetemeko la nchi, na ile mifupa ikasogeleana, mfupa kwa mfupa mwenziwe. Nikatazama kumbe, kulikuwa na mishipa juu yake; lakini haikuwamo pumzi ndani yake. Ndipo akaniambia, Tabiri, utabirie upepo, mwanadamu, uwaambie upepo, Bwana MUNGU asema hivi; Njoo kutoka pande za pepo nne, Ee pumzi, uka-wapulizie hawa waliouawa, wapate kuishi. Basi nikatabiri kama alivyoniamuru, pumzi ikawaingia, wakaishi, wakasimama kwa miguu yao, jeshi kubwa mno.” {2TG32: 16.1}
Hapa tunajifunza kwamba mchakato wa ufufuo ni sawa na mchakato wa uumbaji: kwanza umbo la mtu, kisha kiumbe hai, mwili, ngozi, na mwisho pumzi, na tena anakuwa nafsi hai. Nafsi ya mtu au roho, unaona, hailetwi chini kutoka mbinguni, au juu kutoka kuzimu. Kwa kweli, sio nafsi hata kidogo, ila upepo kutoka kwa pembe nne za nchi hujaza mapafu yake kwa amri ya Mungu, na hivyo yeye tena huwa nafsi hai. Kisha, pia, nyenzo am-bazo mwanadamu aliumbwa kwazo mwanzoni, kwa hizo hizo ataumbwa tena, ili mfupa kwa mfupa uungane. Wakati ameumbwa tena hivyo au kufufuliwa, hata hivyo, lazima adumishe maarifa na kumbukumbu ambayo yeye
16
alikuwa nayo kwa kifo chake, vinginevyo mtu ambaye amefufuliwa hataweza kuwa mtu ambaye alikufa, na iwapo hilo halimhusu, basi ujuzi uliopatikana katika maisha haya utaweza kupotea. {2TG32: 16.2}
Jambo lijalo linalopendeza litakuwa ni kufahamu kwa nini kuna ufufuo mara mbili, miaka elfu mbali mbali (Ufu. 20:5, 6). Wacha tuelekee kwa Warumi: {2TG32: 17.1}
Rum. 8:10,11 — “Na Kristo akiwa ndani yenu, mwili wenu umekufa kwa sababu ya dhambi; bali roho yenu i hai, kwa sababu ya haki. Lakini, ikiwa Roho Yake yeye aliyemfufua Yesu katika wafu anakaa ndani yenu, Yeye aliyemfufua Kristo Yesu katika wafu ataihuisha na miili yenu iliyo katika hali ya kufa, kwa Roho Wake anayekaa ndani yenu.”
Wale wanaokufa na Roho wa Kristo ndani yao, ndio wanaotokea kwa ufufuo wa wenye haki. Lakini wale ambao Roho wa Kristo hakai ndani yao watatokea katika ufufuo wa wasio haki, miaka elfu moja baada ya ufufuo wa wenye haki. {2TG32: 17.2}
Ufu. 20:6 — “Huo ndio ufufuo wa kwanza. Heri, na mtakatifu, ni yeye aliye na sehemu katika ufufuo wa kwanza; juu ya hao mauti ya pili haina nguvu; bali watakuwa makuhani wa Mungu na wa Kristo, nao wa-tatawala pamoja Naye hiyo miaka elfu.”
Iwapo aya hizi humaanisha kile zinachosema juu ya wenye haki, basi juu ya waovu kwa kweli zinasema: {2TG32: 17.3}
“Amelaaniwa na asiye mtakatifu yeye asiye na sehemu katika ufufuo wa kwanza: juu ya hao mauti ya pili ina nguvu; hawatakuwa makuhani wa Mungu na wa Kristo, nao hawatatawala pamoja Naye hiyo
17
miaka elfu.”{2TG32: 17.4}
Iwapo tutalipokea Neno la Mungu jinsi Uvuvio Unavyotupatia, na ikiwa sisi ni watendaji wa Neno Lake, tu-taishi tena, na kuwa mfano kamili wa Mungu kama vile Adamu na Hawa walivyokuwa. Hakika tutarejea katika Bustani ya Edeni. Bustani, pia, itanawiri tena kama awali, na mti wa uzima utazaa matunda yake kila mwezi. Na hivyo, unaona, mwanadamu ataishi tena, na hivyo kuishi milele. {2TG32: 18.1}
“Naye atafuta kila chozi katika macho yao; wala mauti haitakuwapo tena, wala maombolezo, wala kilio, wala maumivu hayatakuwapo tena; kwa kuwa mambo ya kwanza yamekwisha kupita. Na yYeye aketiye juu ya kile kiti cha enzi akasema, Tazama, nayafanya yote kuwa mapya. Akaniambia, Andika, ya kwamba maneno hayo ni amini na kweli. Akaniambia, Imekwisha kuwa. Mimi ni Alfa na Omega, Mwanzo na Mwisho. Mimi nitampa yeye mwenye kiu ya chemchemi ya maji ya uzima bure. Yeye ashindaye atayarithi haya; Nami nitakuwa Mungu wake, naye atakuwa Mwanangu.” Ufu. 21:4-7. {2TG32: 18.2}
“Lakini ijapo ile iliyo kamili, iliyo kwa sehemu itabatilika. Nilipokuwa mtoto mchanga, nalisema kama mtoto mchanga, nalifahamu kama mtoto mchanga, nalifikiri kama mtoto mchanga: tokea hapo nilipokuwa mtu mzima, nimeyabatilisha mambo ya kitoto. Maana wakati wa sasa tunaona kwa kioo kwa jinsi ya fumbo,wakati ule tutaona uso kwa uso: wakati wa sasa nafahamu kwa sehemu; wakati ule nitajua sana kama mimi ninavyojuliwa sana. Basi sasa inadumu imani, tumaini, upendo, haya matatu; na katika hayo lililo kuu ni upendo.” 1 Kor. 13: 10-13 {2TG32: 18.3}
Jumuiya ya Wadaudi Waadventista wa Sabato
(Ushirika Huru Unaojumuisha Kanisa)
Mlima Karmeli, Waco, Texas
S.L.P. 23738, Waco, TX 76702
+ 1-254-855-9539
www.gadsda.com
info@gadsda.com
Gombo la 2, Namba 31, 32
Kimechapishwa nchini Marekani
18