fbpx

Gombo la 2 Salamu Mwafaka Namba 17, 18

Gombo la 2 Salamu Mwafaka Namba 17, 18

                                    

AMANI YA PEKEE YA MAWAZO

Hati miliki, Kimechapishwa tena 1953

Haki zote zimehifadhiwa

V. T. HOUTEFF

                                    

SERIKALI DUNIA NA WATU WA PEKEE AMBAO HAWATAISUJUDIA

SERIKALI YA MWISHO YA DUNIA YA KIKOMUNISTI AU YA KIBEPARI, IPI?

                                    

1

ANDIKO LA SALA

Udanganyifu Wa Mali

Alasiri hii nitaisoma kwenye ukurasa wa 52 wa Mafunzo ya Kristo kwa Mifano: {2TG17: 2.1}

“Kupenda mali kuna nguvu ya kupumbaza, ya udanganyifu. Mara nyingi wale ambao humiliki hazina za ulimwengu husahau kwamba Mungu ndiye anayewapa nguvu kupata mali. Wao husema, ‘Nguvu yangu na uwe-zo wa mkono wangu umenipatia utajiri huu.’ Mali zao, badala ya kuamsha shukrani kwa Mungu, huongoza kwa kujiinua nafsi. Wao hupoteza hisia za utegemezi wao kwa Mungu na wajibu wao kwa wanadamu wenzao. Bada-la ya kutambua mali kama talanta ya kutumika kwa utukufu wa Mungu na kuwainua wanadamu, huitazama ka-ma njia ya kujitumikia wenyewe. Badala ya kukuza ndani ya mwanadamu tabia za Mungu, mali inayotumiwa hivyo hukuza ndani yake tabia za Shetani…. {2TG17: 2.2}

“’Na tamaa za vitu vingine.’ Hivi sio lazima kwamba ni vitu vya dhambi ndani yake, ila ni kitu ambacho hu-fanywa cha kwanza badala ya ufalme wa Mungu. Chochote kinachovutia nia kutoka kwa Mungu, chochote kinachovutia hisia mbali na Kristo, ni adui kwa nafsi.” {2TG17: 2.3}

Tuweze sasa kuomba kwa ajili ya kutambua kwamba Mungu Ndiye hutupatia fursa ya kupata mahitaji yetu, na kwamba Yeye huwabariki wengine na mali bila kusudi lingine isipokuwa kwa matajiri kumtumikia Yeye katika umbile la kibinadamu. Katika andiko hili pia tunaidhinishwa kusali kwamba tuepuke kuitumikia nafsi, na tujifunze kumpa Mungu sifa kwa matendo yetu yote mema, na kuweka mzigo wa dhambi zetu dhidi ya Ibilisi. {2TG17: 2.4}

2

SERIKALI YA DUNIA NA WATU WA PEKEE AMBAO HAWATAISUJUDIA

ANDIKO LA HOTUBA NA V. T. HOUTEFF

MCHUNGAJI WA WADAUDI WAADVENTISTA WA SABATO

SABATO, DESEMBA 6, 1947

HEKALU LA MLIMA KARMELI

WACO, TEXAS

Danieli 7; Ufunuo 13, 17

3

Ufu. 13: 1-10 — “Kisha nikaona mnyama akitoka katika bahari, mwenye pembe kumi, na vichwa saba, na juu ya pembe zake ana vilemba kumi, na juu ya vichwa vyake majina ya makufuru. Na yule mnyama niliyemwona alikuwa mfano wa chui, na miguu yake ilikuwa kama miguu ya dubu, na kinywa chake kama kinywa cha sim-ba, yule joka akampa nguvu zake na kiti chake cha enzi na uwezo mwingi. Nikaona kimoja cha vichwa vyake kana kwamba kimetiwa jeraha la mauti, na pigo lake la mauti likapona. Dunia yote ikamstaajabia mnyama yule.”

“Wakamsujudu yule joka kwa sababu alimpa huyo mnyama uwezo wake; nao wakamsujudu yule mnyama, wakisema, Ni nani afananaye na mnyama huyu? Tena ni nani awezaye kufanya vita naye? Naye akapewa kinywa cha kunena maneno makuu, ya makufuru. Akapewa uwezo wa kufanya kazi yake miezi arobaini na miwili. {2TG17: 4.1}

“Akafunua kinywa chake amtukane Mungu, na kulitukana jina lake, na maskani yake, nao wakaao mbingu-ni. Tena akapewa kufanya vita na watakatifu na kuwashinda, akapewa uwezo juu ya kila kabila na jamaa na lugha na taifa. Na watu wote wakaao juu ya nchi wakamsujudu, kila ambaye jina lake halikuandikwa katika kitabu cha uzima cha Mwana-Kondoo, aliyechinjwa tangu kuwekwa misingi ya dunia. {2TG17: 4.2}

“Mtu akiwa na sikio na asikie. Mtu akichukua mateka, atachukuliwa mateka. Mtu akiua kwa upanga, atauawa kwa upanga. Hapa ndipo penye subira na imani ya watakatifu.”{2TG17: 4.3}

Hapa tumesoma maelezo ya mnyama

4

mmoja, lakini aya zilizosalia zinamleta mnyama mwingine kwa umakini wetu. {2TG17: 4.4}

Aya ya 11-14 — “Kisha nikaona mnyama mwingine, akipanda juu kutoka katika nchi; naye alikuwa na pembe mbili mfano wa Mwana-Kondoo, akanena kama joka. Naye atumia uwezo wote wa mnyama yule wa kwanza mbele yake. Naye aifanya dunia na wote wakaao ndani yake wamsujudie mnyama wa kwanza, ambaye jeraha lake la mauti lilipona. Naye afanya ishara kubwa, hata kufanya moto kushuka kutoka mbinguni uje juu ya nchi mbele ya wanadamu. Naye awakosesha wale wakaao juu ya nchi, kwa ishara zile alizopewa kuzifanya mbele ya huyo mnyama, akiwaambia wakaao juu ya nchi kumfanyia sanamu yule mnyama, aliyekuwa na je-raha la upanga naye akaishi.”

Mnyama huyu wa pili anainuka sio katika bahari, ila katika nchi. Naye anaitengeneza sanamu, mfano wa mnyama wa kwanza; yaani, anazifufua kanuni za serikali ya yule mnyama wa kwanza, kanuni zilizotenda kazi kabla ya yule mnyama wa kwanza kupokea jeraha lake la mauti. {2TG17: 5.1}

Aya ya 15-18 — “ Akapewa kutia pumzi katika ile sanamu ya mnyama, hata ile sanamu ya mnyama inene, na kuwafanya hao wote wasioisujudu sanamu ya mnyama wauawe. Naye awafanya wote, wadogo kwa wakubwa, na matajiri kwa maskini, na walio huru kwa watumwa, watiwe chapa katika mkono wao wa kuume, au katika vipaji vya nyuso zao; tena kwamba mtu awaye yote asiweze kununua wala kuuza, isipokuwa ana chapa ile, yaani, jina la mnyama yule, au hesabu ya jina lake. Hapa ndipo penye hekima. Yeye aliye na akili, na aihesabu hesabu ya mnyama huyo; maana ni hesabu ya kibinadamu. Na hesabu yake ni mia sita, sitini

5

na sita.”

Bibilia, tunaona, huiweka ile namba “666,” sio kwa mnyama wa kwanza, kama chui, ila kwa wa pili, yule mnyama mwenye pembe mbili, kwa maelezo ya mnyama wa kwanza hukoma katika Ufu. 13:10, na maelezo ya yule mnyama mwenye pembe mbili huanza na Ufu. 13:11 na kwishia na Ufu. 13:18. {2TG17: 6.1}

Chapisho la awali la dhehebu, lenye jina Neno Kwa Kundi Ndogo, na lililotolewa na waasisi wa dhehebu, pia kwa usahihi huweka namba “666” kwa mnyama mwenye pembe mbili (tazama ukurasa wa 19 wa Neno Kwa Kundi Ndogo.) {2TG17: 6.2}

Ufunuo ukiwa kikamilisho (Matendo ya Mitume, uk. 585) cha kitabu cha Danieli, ni muhimu tuguse kidogo kwa Danieli, sura ya saba haswa. {2TG17: 6.3}

Pembe ndogo katika awamu ya pili ya mnyama wa nne wa Danieli, huonyesha kuinuka kwa utawala wa kikatili na wa udhalimu, — utawala dhidi ya watu wa Mungu. Mfano wa mnyama kama chui wa Yohana katika sura ya 13, ambaye ni endelezo la mnyama wa nne wa Danieli, husimulia kinachotokea kwa utawala huo wa ushetani. {2TG17: 6.4}

Danieli huelezea kwamba wanyama wake wanne huwakilisha falme nne za dunia, mmoja ukifuata mwingine. Na imeeleweka kwa muda mrefu kwamba hizo ni Babeli, Umedi-Uajemi, Uyunani, na Rumi. Kumbuka kwamba mnyama kama chui wa Yohana ana kichwa cha simba (mnyama wa kwanza), miguu ya dubu (mnyama wa pili), mwili wa chui (mnyama wa tatu), na pembe kumi (mnyama wa nne). Na kwa hivyo, unaona, mnyama kama chui ni mnyama mseto wa wanyama wanne wa Danieli, mzawa wao. Lazima

6

kwa hivyo aiwakilishe dunia baada ya kuanguka kwa ufalme wa nne, baada ya Rumi ya Upagani {2TG17: 6.5}.

Zaidi ya hayo, pembe kumi ambazo hazina vilemba za mnyama wa nne wa Danieli zikiwa mfano wa wafalme ambao wangeinuka kutoka katika Ufalme wa Rumi, vilemba kwa mnyama kama chui vinaonyesha kwamba mnyama huyo anawakilisha kipindi ambacho wafalme walivitwaa vilemba vyao, kipindi baada ya kuvunjika kwa Ufalme wa Rumi ya Upagani. {2TG17: 7.1}

Bado zaidi, yule mnyama kama chui alimtukana Mungu na hema Yake kwa muda mrefu sawa na mnyama wa nne wa Danieli katika awamu yake ya pili, Rumi ya Upapa; yaani, “wakati na nyakati mbili na nusu wakati” (mi-aka 3 na miezi 6), miezi arobaini na miwili. Ni dhahiri, basi, kwamba mnyama kama chui alitawala wakati sam-bamba na mnyama dubwana katika awamu yake ya pili, awamu ya pembe ndogo yenye kichwa. Jeraha la mauti kwa mnyama kama chui kwa hivyo huwakilisha pigo la mauti ambalo alipokea kutoka kwa Matengenezo ya Up-rotestanti. Kwa hivyo kichwa chake kilichojeruhiwa kinawakilisha utawala wa pembe yenye kichwa (shirikisho la nguvu za serikali na za kidini) za mnyama wa Danieli aliyeondolewa nguvu zake za kiserikali — aliyeng’olewa pembe. {2TG17: 7.2}

Sasa, kwa sababu pembe za mnyama wa Yohana huaashiria mataifa, na kichwa chake kilichojeruhiwa huaashiria shirika la kidini lililotengwa kwa nguvu ya serikali, na maadamu vichwa vyake saba vyote vinafanana, isipokuwa jeraha kwa kimoja cha hivyo vichwa, inakuwa wazi kwamba vichwa, saba kwa idadi, huonyesha ma-kundi ya kidini, jumuiya ya Ukristo kwa ujumla. Pembe, walakini, kumi kwa idadi, huonyesha serikali za kiraia kwa ujumla. Kwa jumla pembe na vichwa kwa hivyo huwakilisha dunia ya leo kama vile kila mnyama wa wanne wa Danieli kwa mfululizo, huwakilisha dunia katika siku yao. {2TG17: 7.3}

7

Pembe na vichwa kwa ujumla zikiwa kwa mnyama wakati uo huo, hazikuja moja baada ya nyingine, au kwa namna kama hiyo kuanguka kama pembe katika Danieli sura ya 7 na ya 8, zinapaswa kusadikisha kila akili timamu kwamba pembe na vichwa huashiria makundi ya serikali na ya kidini, yote yakiwa hai kwa wakati uo huo, sio moja likifuata lingine. {2TG17: 8.1}

Makufuru yakiwa juu ya vile vichwa, sio juu ya zile pembe, humaanisha kwamba makundi ya kidini yali-yoonyeshwa humo hayamwabudu Mungu kulingana na Ukweli, kwamba sio kamili vile wanavyodai kuwa. Ufasiri halisi ambao Uvuvio huweka kwa neno “kukufuru” ni huu: “Najua makufuru ya hao wasemao ya kuwa ni Wayahudi, nao sio.” Ufu. 2: 9. {2TG17: 8.2}

Ni bora sisi sote tukubali kushindwa kwetu kuliko kuukwepa Ukweli, kwa maana Ukweli ndio ambao utatuweka huru. {2TG17: 8.3}

Zaidi ya hayo, kwa sababu sisi hukubali kwamba Matengenezo yalisababisha pigo la mauti na likazalisha Up-rotestanti, na maadamu Uvuvio husema jeraha lilipona, haya yote yanathibitisha kitu ambacho iwapo tutaunga-ma, chaweza kuyaokoa maisha yetu yaliyo hatarini, na kutufanya tuwe wakuu kama yale maungamo yote kwa moyo ya zamani yalivyomfanya Daudi kuwa mkuu. Ni nini ambacho tunapaswa kuungama? — Ni hiki tu: Iwapo Uprotestanti ulimjeruhi mnyama kwa Matengenezo, basi kupona kwa lile jeraha hakuonyeshi chochote kipun-gufu kwamba Matengenezo yameshindwa kuliweka jeraha wazi, kwamba lengo la wanamatengenezo limekufa, na udikteta umeamshwa. Hakika, mfano huu hausemi chochote zaidi ya kile ujumbe wa kwa Walaodekia un-asema: {2TG17: 8.4}

8

“Kwa kuwa wasema, Mimi ni tajiri, nimejitajirisha, wala sina haja ya kitu; nawe hujui ya kuwa wewe u mnyonge, na mwenye mashaka, na maskini, na kipofu, na uchi. Nakupa shauri, ununue kwangu dhahabu ili-yosafishwa kwa moto, upate kuwa tajiri, na mavazi meupe upate kuvaa, aibu ya uchi wako isionekane, na dawa ya macho ya kujipaka macho yako, upate kuona.” Ufu. 3:17,18. {2TG17: 9.1}

Kwa mtu kuwa katika hali mbaya kama hiyo na wakati uo huo akibishana kwamba hahitaji chochote, kwa kweli ni kukufuru. {2TG17: 9.2}

Tofauti na yule mnyama wa kwanza, yule mnyama wa pili anakuja kutoka juu ya nchi. Bahari na nchi bila shaka huonyesha maeneo mawili tofauti. Tunajua kwamba wanyama wa Danieli 7, na mnyama kama chui wa Ufunuo 13, wanyama walioinuka kutoka baharini, wote chimbuko lao ni katika Nchi ya Kale, nchi ambazo jamii ya wanadamu ilianzia. Naam, ile “bahari” kwa usahihi ni mfano wa Nchi ya Kale kwa sababu bahari ni ghala la maji mengi, mahali ambapo maji huchimbuka, jinsi Nchi ya Kale ndio mahali ambapo jamii ya wanadamu ilianzia kuenea. {2TG17: 9.3}

“Nchi” basi, huashiria mahali mbali na “bahari” na kinyume cha kile bahari huwakilisha, — nchi inayojumuisha na wakazi ambao wamehama kutoka kwingine. Nchi kama hiyo tu au taifa mbali na Nchi ya Kale na yenye ushawishi kama ilivyoonyeshwa katika mnyama huyu mwenye pembe mbili anayeinuka baada ya kuundwa kwa mnyama kama chui, katika kipindi cha Uprotestanti, ni Marekani. Zaidi ya hayo, Marekani tayari ni utawala wa ulimwengu, na kwa hivyo hatuhitaji kuwa wa kukisia tena. Pembe mbili za yule mnyama

9

Huonyesha nguvu zake mbili za kisiasa zinazotawala — Wademokrasia na Wanajamhuri. Tabia yao kama ya mwana-kondoo inatoa taswira ya asiye na hatia, asiyedhuru, na mkarimu. Yule mnyama kunena kama joka hata hivyo hukataa katakata kuonekana kama pembe za mwana-kondoo. {2TG17: 9.4}.

Mnyama mwenye pembe mbili hutumia uwezo wote ambao yule mnyama wa kwanza, yule kama chui, alitu-mia, kumwonyesha tena kwamba ni utawala wa ulimwengu. Hakika, inahitaji utawala kama huo kuwalazimisha wakazi wote wa dunia kuabudu kama anavyoamuru, na kutekeleza sanamu ya utawala wa kanisa na serikali am-bao umepitwa na wakati kama wa Vizazi vya Kati vyenyewe. Naam, inachukua utawala kama huo kuushawishi ulimwengu, isipokuwa wale ambao majina yao yameandikwa katika Kitabu cha Uzima cha Mwana-Kondoo, kuusujudia. {2TG17: 10.1}

Aya ya 13-15 “Naye afanya ishara kubwa, hata kufanya moto kushuka kutoka mbinguni uje juu ya nchi mbele ya wanadamu. Naye awakosesha wale wakaao juu ya nchi, kwa ishara zile alizopewa kuzifanya mbele ya huyo mnyama, akiwaambia wakaao juu ya nchi kumfanyia sanamu yule mnyama, aliyekuwa na jeraha la upanga naye akaishi. Akapewa kutia pumzi katika ile sanamu ya mnyama, hata ile sanamu ya mnyama inene, na kuwafanya hao wote wasioisujudu sanamu ya mnyama wauawe.”

Hapa unaona kwamba muungano huu wa dunia, uliochochewa kuleta amani na maelewano kutoka kwa machafuko ya sasa, badala yake utaleta hata wakati wa taabu kubwa zaidi. Na kwa nini? — Kwa sababu ingawa mnyama anaweza kuleta Ukomunisti na Ubepari kwa makubaliano ya pamoja, na kuwasababisha

10

kuisujudia sanamu ya yule mnyama, bado wale ambao majina yao yameandikwa katika Kitabu cha Uzima cha Mwana-Kondoo hawatatii kamwe. Kutoka kwa hili unaona kwamba mpango wote umeelekezwa na nguvu isiyo ya kawaida ambayo kusudi lake ni kuwagomea watu wa Mungu. Wao hata hivyo wataokolewa. {2TG17: 10.2}

Wakati amri ya mnyama inapitishwa kwamba hakuna mtu anayeweza kununua au kuuza, na auawe kwa saba-bu ya kutotii, wakati huo Mungu pekee anaweza kuwalinda watu Wake, watu ambao majina yao yameandikwa katika kile “Kitabu.” Kama hii ndiyo ahadi Yake ya uaminifu: “Wakati huo Mikaeli atasimama, Jemadari mkuu asimamaye upande wa wana wa watu wako; na kutakuwa na wakati wa taabu, mfano wake haukuwapo tangu lilipoanza kuwapo taifa hata wakati uo huo: na wakati huo watu wako wataokolewa, kila mmoja atakayeoneka-na ameandikwa katika kitabu kile.” Dan. 12: 1. {2TG17: 11.1}

Aya ya 16, 17 — “Naye awafanya wote, wadogo kwa wakubwa, na matajiri kwa maskini, na walio huru kwa watumwa, watiwe chapa katika mkono wao wa kuume, au katika vipaji vya nyuso zao; tena kwamba mtu awaye yote asiweze kununua wala kuuza, isipokuwa ana chapa ile, yaani, jina la mnyama yule, au hesabu ya jina lake.”

Utawala huu, unaona, utayadhibiti masoko ya dunia pia. {2TG17: 11.2}

Utabiri huu wa ki-mfano wa serikali ya dunia itakayoanzishwa, unaonyesha wazi kwamba serikali inayokuja ya dunia haitakuwa Umoja wa Mataifa, wala ya Ukomunisti, ila utawala wa kidini. Tunajua kwamba sio Ukomunisti, kwa sababu Ukomunisti u dhidi ya dini, na mnyama ni kwa ajili yake. {2TG17: 11.3}

Wakati hili linatimizwa, ambalo halipo tena

11

zaidi ya upeo wa macho, basi wale ambao majina yao yameandikwa katika “Kitabu cha Uzima” wataokolewa, bali wengine wote watakuwa wameipokea alama ya mnyama. Hakutakuwa na eneo la kati, au tabaka la kati. {2TG17: 11.4}

Tunapaswa sasa kuamua cha kufanya, ili tusije tukanaswa. Kwa sababu hii haswa nuru ya Ukweli imetujia sasa. {2TG17: 12.1}

Serikali ya dunia ambayo itatokea kwa “Umoja wa Mataifa” na “Umoja wa Mataifa,” haipo kwa kweli dunia yote, na bado itakuwapo “dunia mara mbili,” ila badala ya kuwa na Ubepari na Ukomunisti, watakuwapo wale wanaomsujudia yule mnyama na sanamu yake, na wale wanaomwabudu Mungu na majina yao kuandikwa kati-ka Kitabu. Wa mwisho ndio watu wa pekee ambao hawataisujudia serikali ya dunia ya baadaye. {2TG17: 12.2}

12

Wamebarikiwa ambao daima huishika

Njia safi na kamilifu;

Ambao kamwe hawaiachi njia takatifu

Ya amri za Mungu kupotea!

Wamebarikiwa, ambao kwa sheria zake za haki

Wamekuwa bado watiifu,

Na kwa bidii, juhudi za unyenyekevu

Neema yake wametafuta kushinda!

Umetuamuru kabisa, Bwana,

Kujifunza mapenzi Yako matakatifu;

Na bidii yetu yote kuajiri

Maagizo Yako kutimiza.

Ee basi mapenzi Yako matakatifu mno

Yaweze kwa njia zangu kuongoza;

Nami mwendo wa maisha yangu yote

Kwa maelekezi Yako niongozwe!

–Bila Jina.

13

ANDIKO LA SALA

Zingira Vijana Na Mivuto Mizuri

Ninasoma kutoka katika Mafunzo ya Kristo kwa Mifano, uk. 53: {2TG18: 14.1}

“Wakati akili ni changa na zenye nguvu nyingi, na rahisi kwa ukuaji wa haraka, lipo jaribu kubwa la kuuta-mani ubinafsi, kuitumikia nafsi…. Katika kipindi hiki cha kuiga cha maisha ya watoto wao, jukumu la wazazi ni kubwa mno. Linapaswa kuwa somo lao kuwazingira vijana kwa mvuto mzuri, mivuto ambayo itawapa mitazamo sahihi ya maisha na mafanikio yake ya kweli…. Kadri hamu ya anasa inavyozidi kupendelewa, ndivyo hukuwa imara. Maslahi ya vijana hawa hufyonzwa zaidi na zaidi katika burudani, hadi wanakuja kuiona kama kitu kikuu cha maisha. Wao huumba tabia za uvivu na kupendelea ubinafsi ambao hufanya karibu isiwezekane wao kuwa wakristo waaminifu.” {2TG18: 14.2}

Tumeshauriwa hapa kusali kwamba vijana wafunzwe na wakomae kuacha kuitumikia nafsi; kwamba wazazi wenyewe wajifunze hili, kwa maana katika hali nyingi misukumo ya wazazi huwaongoza watoto katika udunia na kiburi; kwamba wazazi na watoto wagundue kwamba kadiri hamu ya anasa inavyopendelewa, ndivyo huku-wa imara zaidi na huwa haiwezekani kuiridhisha zaidi; ya kuwa sisi sote tufahamu kwamba vijana wasipopewa mitazamo sahihi ya maisha na mafanikio yake ya kweli, watafyonzwa katika anasa na kuitazama kama kitu kikuu maishani. {2TG18: 14.3}

14

SERIKALI YA MWISHO YA DUNIA YA UKOMUNISTI AU YA UBEPARI — IPI?
Ufunuo 17, 18

ANDIKO LA HOTUBA NA V. T. HOUTEFF

MCHUNGAJI WA WADAUDI WAADVENTISTA WA SABATO

SABATO, DESEMBA 13, 1947

HEKALU LA MLIMA KARMELI

WACO, TEXAS

Ufunuo 17

15

Ufu. 17: 1-3 — “Akaja mmoja wa wale malaika saba, wenye vile vitasa saba, akanena nami, akisema, Njoo huku, nitakuonyesha hukumu ya yule kahaba mkuu aketiye juu ya maji mengi; ambaye wafalme wa nchi wamezini naye, nao wakaao katika nchi wamelevywa kwa mvinyo wa uasherati wake. Akanichukua katika Roho hata jangwani, nikaona mwanamke, ameketi juu ya mnyama mwekundu sana, mwenye kujaa majina ya makufuru, mwenye vichwa saba na pembe kumi.”

Mnyama huyu anaonekana kuuwakilisha ulimwengu katika siku yake kama walivyo wanyama wote wa Dan-ieli na Ufunuo wanavyoonekana kuuwakilisha ulimwengu katika siku yao. {2TG18: 16.1}

Jangwa likiwa kinyume cha shamba la mizabibu huashiria kwamba eneo la yule mnyama sio katika Nchi ya Ahadi, sio katika shamba la mizabibu (Isa. 5:7), ila katika nchi za Mataifa, “nyikani” Kutokea eneo hili, kwa hivyo, imetengwa Nchi Takatifu. Na kwa ukweli kwamba mwanamke ameketi juu ya yule mnyama, akim-wendesha, inaonyeshwa kwa hakika kwamba anamtawala, na kwamba yule mnyama mwenyewe ni nembo ya utawala wa Babeli Mkuu. {2TG18: 16.2}

Pembe zake kumi huwakilisha nguvu za serikali za kiraia, kama vile pembe za mnyama yeyote wa mfano. Na iwapo kichwa kilichojeruhiwa cha yule mnyama kama chui wa sura ya 13 ni mfano wa shirika la kidini, kama inavyofundishwa na Dhehebu, basi vichwa vyake saba lazima vivyo hivyo viwakilishe makundi ya kidini! Hivyo ni kwamba mnyama huyu kwa ujumla, kama wanyama wengine wote wa Bibilia, huwakilisha ulimwengu wa Mataifa kwa ujumla wake — makundi ya kiraia na ya kidini (pembe

16

na vichwa). {2TG18: 16.3}

Kukufuru ni mtu kunene kijuujuu kumhusu Mungu, kutenda unafiki, kudai kuwa kitu fulani isipokuwa jinsi mtu alivyo hakika. Ufafanuzi wa Uvuvio ndio huu: “… Najua makufuru ya hao wasemao kwamba ni Wayahudi, nao sio, bali ni sinagogi la Shetani.” Ufu 2: 9. {2TG18: 17.1}

Aya ya 4-6 — “Na mwanamke yule alikuwa amevikwa nguo ya rangi ya zambarau, na nyekundu, amepambwa kwa dhahabu, na kito cha thamani, na lulu, naye alikuwa na kikombe cha dhahabu mkononi mwake, kilicho-jawa na machukizo, na machafu ya uasherati wake. Na katika kipaji cha uso wake alikuwa na jina lime-andikwa, la siri, BABELI MKUU, MAMA WA MAKAHABA NA MACHUKIZO YA NCHI. Nikamwona yule mwanamke amelewa kwa damu ya watakatifu, na kwa damu ya mashahidi wa Yesu. Nami nilipomwona ni-kastaajabu ajabu kuu.”

Mwanamke huyu hawakilishi kitu kipya, ila kitu kikongwe kama wakati wa wafia imani, kwa sababu yeye ndiye kisababishi cha kuuawa kwao. Je! Anaweza kuwa nini ila dini bandia ambayo ilichimbuka na dhabihu isiyokubalika ya Kaini? Tangu wakati huo amezaa madhehebu, amekuwa mama wa makahaba. Machukizo yake, unakumbuka, yamefanywa yavutie sana, yakisambazwa kutoka kwenye kikombe cha dhahabu kilichoshikiliwa mikononi ambayo imepambwa vizuri kwa vitu vya bei ghali mno vya dunia. {2TG18: 17.2}

Aya ya 7-13 — “Na yule malaika akaniambia, Kwani kustaajabu? Nitakuambia siri ya mwanamke huyu, na ya mnyama huyu amchukuaye, mwenye vile vichwa saba na zile pembe kumi. Yule mnyama uliyemwona aliku-wako, naye hayuko,

17

naye yu tayari kupanda kutoka kuzimu na kwenda kwenye uharibifu. Na hao wakaao juu ya nchi, wasi-oandikwa majina yao katika kitabu cha uzima tangu kuwekwa misingi ya ulimwengu, watastaajabu wam-wonapo yule mnyama, ya kwamba alikuwako, naye hayuko, naye atakuwako. Hapo ndipo penye akili zenye hekima. Vile vichwa saba ni milima saba anayokalia mwanamke huyo. Na wapo wafalme saba. Watano wamekwisha kuanguka, na mmoja yupo, na mwingine hajaja bado. Naye atakapokuja imempasa kukaa muda mchache. Na yule mnyama aliyekuwako naye hayuko, yeye ndiye wa nane, naye ni mmoja wa wale saba, naye aenenda kwenye uharibifu. Na zile pembe kumi ulizoziona ni wafalme kumi, ambao hawajapokea ufalme bado, lakini wapokea mamlaka kama wafalme muda wa saa moja pamoja na yule mnyama. Hawa wana shauri mo-ja, nao wampa yule mnyama nguvu zao na mamlaka yao.”

Hapa kuna mnyama ambaye umbo lake ni sawa na yule mnyama kama chui wa sura ya 13. Pembe za mnyama huyu mwekundu sana, ingawa, hazina vilemba, na hakuna hata kimoja cha vichwa vyake kimejeruhiwa. Pia, ba-dala ya kuwa na jina la Makufuru lililoandikwa tu kwa vichwa vyake, mwili wake wote umejaa majina ya ma-kufuru. {2TG18: 18.1}

Katika masomo yaliyopita tulijifunza kwamba mnyama kama chui huwakilisha dunia kutoka kwa anguko la Rumi ya Upagani hadi kwa wakati wetu (Pambano Kuu, uk. 442). Sasa, kwa sababu yule mnyama mwekundu sana pia anazo pembe kumi na vichwa saba, inaonekana tena kwamba yeye, pia, yuko katika mkondo wa wakati ni mfano wa dunia pamoja na tawala zake za serikali za kiraia na za kidini — pembe na vichwa. {2TG18: 18.2}

Kwa sababu kichwa chake hakijajeruhiwa kama vile kichwa cha mnyama kama chui, na maadamu jeraha la mnyama kama chui limepona, ni

18

wazi kwamba mnyama mwekundu sana huwakilisha dunia katika wakati jeraha limepona, katika wakati yule mnyama mwenye pembe mbili (Ufu. 13:11-18) anafanya sanamu ya mnyama kama chui katika hali yake ya kabla ya kutiwa jeraha. {2TG18: 18.3}

Unakumbuka kwamba pembe za mnyama wa nne wa Danieli hazikuwa na vilemba, na pembe za mnyama ka-ma chui wa Yohana zilikuwa na vilemba, na tena kwamba pembe za mnyama mwekundu sana hazina vilemba. Uvuvio kwa njia ya wanyama hawa wa mfano huonyesha vipindi vitatu vya wakati, kimoja kikifuata kingine: (1) kipindi kabla ya wafalme wa Ulaya kupokea taji zao; (2) kipindi ambacho walivikwa vilemba; (3) kipindi cha wafalme wasio na vilemba ambamo Babeli Mkuu anatawala kwa ukuu. {2TG18: 19.1}

Ukweli kwamba karibu wafalme wote waliovikwa vilemba wa dunia wameondolewa madarakani ni uthibit-isho ndani yake wenyewe kwamba kipindi Namba 2, kipindi cha mnyama kama chui (pembe zilizovikwa taji) kinakaribia kupita, na kwamba kipindi Namba 3, Kipindi cha mnyama mwekundu sana (pembe zisizokuwa na taji) kinakaribia kuingizwa. Ili kuufanya mpito, dhiki ya sasa ya mataifa kwa hivyo haiwezi kuepukika. {2TG18: 19.2}

Aya ya 14-18 — “Hawa watafanya vita na Mwana-Kondoo, na Mwana-Kondoo atawashinda, kwa maana Yeye ni Bwana wa Mabwana, na Mfalme wa Wafalme, na hao walio pamoja naye ndio walioitwa, na wateule, na waaminifu. Kisha akaniambia, Yale maji uliyoyaona, hapo aketipo yule kahaba, ni jamaa na makutano na mataifa na lugha. Na zile pembe kumi ulizoziona, na huyo mnyama, hao watamchukia yule kahaba, nao wa-tamfanya kuwa mkiwa na uchi, watamla nyama yake, watamteketeza kabisa kwa moto. Maana Mungu ametia

19

mioyoni mwao kufanya shauri lake, na kufanya shauri moja, na kumpa yule mnyama ufalme wao hata mane-no ya Mungu yatimizwe. Na yule mwanamke uliyemwona, ni mji ule mkubwa, wenye ufalme juu ya wafalme wa nchi.”

Tena, ukweli kwamba pembe kumi (wafalme) wanayo nia moja (tofauti na wafalme wa vidole wa Danieli 2:42,43), lakini hawana ufalme wao wenyewe, mbali na ukweli kwamba mwanamke humtawala mnyama, na pia ukweli kwamba viongozi wa Kikomunisti (wafalme wasio na vilemba) wa mataifa na wanayo nia moja (hufanya kazi kwa pamoja kwa kusudi moja), — kweli hizi zote huonyesha kwamba ingawa Ukomunisti unaonekana kama dola ijayo ya kuitawala dunia, unabii huu wa ki-mfano huonyesha kwamba dunia itatawaliwa na ujao mfumo wa kidini wa kimataifa, na Babeli Mkuu, mpinzani wa dini ya Kristo, na wa bandia kwa mwanamke katika Ufunuo sura ya 12. Mnyama mwekundu sana, kwa hivyo, ni mfano wa serikali ya dunia ambayo itatotokea kupitia mageuzi katika Umoja wa Mataifa mwishowe. {2TG18 20.1}

Kwa maana wale ambao hawana sehemu katika ufufuo wa kwanza, wadhambi wote ambao hawakutubu tan-gu mwanzo wa dunia hadi kwa Millenia, watafufuliwa baada ya miaka 1000, wakati huo hakika watagundua kwamba majina yao hayakuandikwa “katika Kitabu cha Uzima”, — la, hakuna hata mmoja wao, hata tangu kuwekwa msingi wa dunia. Ukweli unadhihirika wazi kwamba wakati huo tu ndipo watakapomwona yule mnyama katika awamu zake tatu (“alikuwako, naye hayuko, naye atakuwako”); yaani, “yuko” kabla ya Millenia; “naye hayuko” wakati wa Millenia; “naye yuko” baada ya Millenia. {2TG18: 20.2}

Yeye “hayuko” wakati wa miaka 1000 kwa sababu

20

mwanzoni mwa miaka 1000, yule mnyama na nabii wa uongo “wanatupwa katika ziwa la moto,” basi “waliosa-lia,” wengine wote ambao hawakutoka ndani ya himaya ya Babeli, “wanauawa kwa upanga” wa “Mfalme wa wafalme, na Bwana wa mabwana.” Ufu. 19:21,16. {2TG18: 20.3}

Kwa muhtasari, akiwa ameishi kabla ya Millenia, na pia baada ya Millenia, na kuwa amekufa wakati wa Mil-lenia, yule mnyama anaonekana katika awamu tatu, katika vipindi vitatu: kabla millenia ambapo “yuko” katika millenia ambapo “naye hayuko” na baada ya millenia, ambapo “yuko.” {2TG18 21.1}

Naye “Atapanda kutoka kuzimu” (kutoka shimoni, ambamo Shetani mwenyewe atakuwa amefungwa kwa miaka 1000), na kisha “kwenda kwenye uharibifu” (Ufu. 17:8); yaani, kwa muda mfupi atawekwa kwa mauti yake ya pili ambayo hakuna ufufuo. {2TG18: 21.2}

“Yeye ndiye wa nane, naye ni mmoja wa wale saba”; yaani, wapo wanyama wanne katika Danieli 7, wawili katika Ufunuo 13, na moja katika sura ya 17 — wanyama saba kwa ujumla. Bali yule wa saba anaishi mara mbili, na kwa hivyo baada ya ufufuo wake “yeye ndiye wa nane,” lakini “ni mmoja wa wale saba.” Kisha anaenda kwenye uharibifu, — anapata mauti ya pili. {2TG18: 21.3}

Taarifa, “na wapo wafalme saba,” huonyesha kwamba wafalme hawa sio mfano; yaani, wao sio pembe, wala wao sio vichwa. Pembe zote na vichwa vyote viko sasa kwa mnyama, ilhali “wafalme saba” hawapo pale ki-mfano — watano wameanguka, mmoja yupo, na mwingine hajaja bado. {2TG18 21.4}

Lazima tung’amue kabisa kwamba Mungu kupitia huu

21

mfano hufanya muhtasari wa historia ya dunia yote, kwa maana mnyama, kama nilivyosema hapo awali, ni mfa-no sio wa dunia kabla ya millenia lakini pia wa dunia ya uovu baada ya millenia. Wafalme saba wa falme “tangu msingi wa ulimwengu kabla ya gharika; (1) Dunia ya kale kabla ya gharika; (2) Milki ya zamani ya Babeli; (3) Milki ya Umedi na Uajemi; (4) Milki ya Uyunani; (5) Milki ya Rumi. Hawa wameanguka. (6) Yule ambaye yupo, ni dunia ambayo dhiki ya sasa ya mataifa itazalisha (kabla ya millenia), na ambayo mnyama mwenyewe, katika awamu yake ya kwanza, ndiye mfano. Na (7) yule hajaja bado, ni dunia baada ya miaka 1000, ambayo mnyama mwenyewe, katika awamu yake ya tatu, pia ni mfano. {2TG18: 21.5}

Hivyo pamoja na mfano huu dunia ya dhambi imewakilishwa tangu mwanzo hadi mwisho wake kabisa. Mnyama huyu, kwa hivyo, ni muhtasari wa ki-mfano wa dunia yote. {2TG18: 22.1}

Ile “saa moja” ni dhahiri ule wakati kutoka saa kumi na moja hadi saa kumi na mbili za masaa ya mfano kama yalivyowekwa katika Mathayo 20:6. {2TG18 22.2}

Namba kumi katika mfano huu, kama kwingineko katika Bibilia, hubeba maana ya ulimwengu wote. Wafalme kumi hawana ufalme wakati ambapo mwanamke anamwendesha mnyama, lakini kwa pamoja na mnyama wa-takuwa na mamlaka kama wafalme. Kirai, “bado,” kinamaanisha kwamba baada ya saa moja wataupokea ufalme wao. {2TG18: 22.3}

Aya ya 14 — “Hawa watafanya vita na Mwana-Kondoo, na Mwana Kondoo atawashinda, kwa maana Yeye ni Bwana wa Mabwana, na Mfalme wa Wafalme, na hao walio pamoja naye ndio walioitwa, na wateule, na waaminifu.“

22

Wafalme hawa watakuwa wapinga dini na kwa hivyo wapinga Ukristo. Mwishowe watafanya vita na Bwana na walioitwa Wake, wateule, na waaminifu, lakini “Mwana-Kondoo atawashinda” wafalme. {2TG18: 23.1}

Mwanamke, alivyoonyeshwa hapo awali, ni ishara ya mfumo shirikisho wa kidini ambao zile pembe sio tu haziko katika mapatano lakini pia ni maadui zake. Kwa sababu hiyo, baada ya saa ya ki-mfano kupita, wanamtoa kwa yule mnyama, na kumfanya kuwa ukiwa, na kumchoma kwa moto. Kisha inakuwa kwamba wanaupokea ufalme wao “kwa majira na wakati.” Dan. 7:12. {2TG17: 23.2}

Aya ya 17 — “Maana Mungu ametia mioyoni mwao kufanya shauri lake, na kufanya shauri moja, na kumpa yule mnyama ufalme wao hata maneno ya Mungu yatimizwe.”

Mwito wa kutoka Babeli (Ufu. 18:4), ni mwito kwa watu wa Mungu kutoka katika eneo lake la kijiografia. {2TG18: 23.3}

Sura ya kumi na nane ni endelezo la ya kumi na saba, kwa hivyo tutaichambua pia: {2TG18: 23,4}

Ufu. 18:1 — “Baada ya hayo naliona malaika mwingine, akishuka kutoka mbinguni, mwenye mamlaka kuu; na nchi ikaangazwa kwa utukufu wake.”

Baada ya mambo gani? — Baada ya mnyama mwekundu sana kutokea na wakati ambapo yule mwanamke, Babeli, ameketi juu yake. Ni wakati huo ndipo nchi itaangazwa na utukufu wa yule malaika, na ujumbe wa saa hiyo. {2TG18: 23.5}

Aya ya 2-4 — “Akalia kwa sauti kuu, akisema, Umeanguka, umeanguka Babeli ule mkuu;

23

umekuwa maskani ya mashetani, na ngome ya kila roho mchafu, na ngome ya kila ndege mchafu mwenye kuchukiza; kwa kuwa mataifa yote wamekunywa mvinyo ya ghadhabu ya uasherati wake, na wafalme wa nchi wamezini naye, na wafanya biashara wa nchi wamepata mali kwa nguvu za kiburi chake. Kisha nikasikia sauti nyingine kutoka mbinguni, ikisema, Tokeni kwake, enyi watu wangu, msishiriki dhambi zake, wala msipokee mapigo yake.”

Sauti ya mbinguni, Roho wa Kweli, inasikika ikiwaita watu wa Mungu watoke Babeli baada ya nchi kuangazwa na utukufu wa yule malaika. Ili watu wa Mungu watoke ili wasizishiriki dhambi zake wala wasiya-pokee mapigo yake, lazima waitwe kuingia mahali pasipokuwa na dhambi, na hivyo kuokolewa kutoka kwa mapigo ya Babeli. Kwa sababu hiyo wanaenda katika kanisa lililotakaswa lisilokuwa na dhambi, na nchi ambayo haimo katika hatari ya mapigo. {2TG18: 24.1}

Aya ya 5-7 — “Kwa maana dhambi zake zimefika hata mbinguni, na Mungu amekumbuka maovu yake. Mlipeni kama yeye alivyolipa, mkamlipe mara mbili kwa kadiri ya matendo yake. Katika kikombe kile alichokichanganyisha, mchanganyishieni maradufu. Kwa kadiri alivyojitukuza na kufanya anasa, mpeni maumivu na huzuni kadiri iyo hiyo. Kwa kuwa husema moyoni mwake, Nimeketi malkia, wala si mjane, wala sitaona huzuni kamwe.”

Amewalipa watu wa Mungu kwa maovu, na sasa atalipwa maradufu. Amejisifu kwa kuitawala dunia, na akasema moyoni mwake kwamba yeye si “mjane,” ya kwamba Mungu ni mumewe, lakini anajikuta amekosea. {2TG18: 24.2}

24

Aya ya 8-13 — “Kwa sababu hiyo mapigo yake yatakuja katika siku moja, mauti, na huzuni, na njaa, naye atateketezwa kabisa kwa moto. Kwa maana Bwana Mungu aliyemhukumu ni mwenye nguvu. Na hao wafalme wa nchi, waliozini naye na kufanya anasa pamoja naye, watalia na kumwombolezea; wauonapo moshi wa kuungua kwake; wakisimama mbali kwa hofu ya maumivu yake, wakisema, Ole, ole, mji ule ulio mkuu, Babeli, mji ule ulio na nguvu! Kwa kuwa katika saa moja hukumu yako imekuja. Nao wafanya biashara wa nchi walia na kumwombolezea, kwa sababu hapana mtu anunuaye bidhaa yao tena; bidhaa ya dhahabu, na fedha, na kito chenye thamani, na lulu, na kitani nzuri, na nguo ya rangi ya zambarau, na hariri, na nguo nyekundu; na kila mti wa uudi, na kila chombo cha pembe, na kila chombo cha mti wa thamani nyingi, na cha shaba, na cha chuma, na cha marimari; na mdalasini, na iliki, na uvumba, na marhamu, na ubani, na mvinyo, na mafuta ya mzeituni, na unga mzuri, na ngano, na ng’ombe, na kondoo, na farasi, na magari, na miili na roho za wana-damu.”

Ameweka kila kitu mikononi mwake, na mikono yake imewekwa ndani ya kila kitu, lakini sasa utukufu wake umefikia kikomo. {2TG18: 25.1}

Aya ya 14-21 — “Na matunda yaliyotamaniwa na roho yako yamekuondokea; na vitu vyote vilivyo laini na vitu vya fahari vimekupotea; wala watu hawataviona tena kamwe. Na wafanya biashara ya vitu hivyo, wali-opata mali kwake, watasimama mbali, kwa hofu ya maumivu yake; wakilia na kuomboleza, wakisema, Ole, ole, mji ule mkuu! Uliovikwa kitani nzuri, na nguo ya rangi ya zambarau, na nguo nyekundu, na kupambwa kwa dhahabu, na kito cha thamani, na lulu; kwa kuwa katika saa moja utajiri mwingi namna hii

25

umekuwa ukiwa. Na kila nahodha na kila aendaye mahali popote kwa matanga, na mabaharia, nao wote watendao kazi baharini, wakasimama mbali; wakalia sana, walipouona moshi wa kuungua kwake, wakisema, Ni mji upi ulio mfano wa mji huu mkubwa! Wakatupa mavumbi juu ya vichwa vyao, wakalia, wakitokwa na machozi na kuomboleza, wakisema, Ole, ole, mji ule ulio mkuu! Ambao ndani yake wote wenye merikebu ba-harini walipata mali kwa utajiri wake; kwa kuwa katika saa moja umekuwa ukiwa. Furahini juu yake, enyi mbingu, nanyi watakatifu na mitume na manabii; kwa maana Mungu amehukumu hukumu yenu juu yake. Na malaika mmoja mwenye nguvu akainua jiwe, kama jiwe kubwa la kusagia, akalitupa katika bahari, akisema, Kama hivi, kwa nguvu nyingi, utatupwa Babeli, mji ule mkuu, wala hautaonekana tena kabisa.”

Vurugu kama nini! na mwisho wake wenye kuaibisha wakati zile pembe kumi zinamshika Babeli, makao ma-kuu ya wenye kujidai, utawala mkuu wa dunia yote. Sasa ni wakati na fursa yetu kujiandaa kwa pepo nne ziachiliwe, na kuandaa kimbilio, mahali pasipokuwa na dhambi kwa ajili ya kukusanywa kwa watu, na kwa ajili ya kukamilisha kazi ya injili ulimwenguni kote. {2TG18: 26.1}

Aya ya 22-24 — “Wala sauti ya wapiga vinanda, na ya wapiga zomari, na ya wapiga filimbi, na ya wapiga baragumu, haitasikiwa ndani yako tena kabisa; wala fundi awaye yote wa kazi yo yote hataonekana ndani yako tena kabisa; wala sauti ya jiwe la kusagia haitasikiwa ndani yako tena kabisa; wala nuru ya taa haitamulika ndani yako tena kabisa; wala sauti ya bwana-arusi na bibi-arusi haitasikiwa ndani yako tena kabisa; maana hao wafanya biashara wako walikuwa wakuu wa nchi, kwa kuwa mataifa yote walidanganywa kwa uchawi wako. Na ndani yake ilionekana damu ya manabii, na ya watakatifu, na ya wale

26

wote waliouawa juu ya nchi.”

Tunaona kwamba mfumo huu wa serikali umeundwa pasipo kusudi lingine isipokuwa kuwafanya wafuasi wake matajiri kwa jina la dini, zoezi ambalo huzidi aina zote za ibada ya sanamu. {2TG18: 27.1}

Iwapo mioyo yetu imejikita kwa mali, ikiwa upendo wetu kwa fedha unakuwa mkubwa kuliko upendo wetu kusaidia kuuanzisha Ufalme, basi hakuna tumaini. Wa namna hii watajikuta kwa sumaku wamevutwa chini nda-ni ya Babeli. Lazima tukumbuke kwamba kupenda fedha ndilo shina la maovu yote; kwamba ni rahisi kwa ngamia kupita katika tundu la sindano kuliko tajiri kuingia katika Ufalme. Lakini, cha kusikitisha kusema, licha ya onyo hili la kicho, tunaona hata watu wengi walio na ufahamu katika mambo ya Mungu hunaswa kwa fedha ya aibu kama hii. {2TG18: 27.2}

Ikiwa tunayo dola wakati tunapoihitaji, pia kuwa na uhakika wa mavazi yetu ya kila siku , chakula, na kitanda cha kulalia, tunapaswa kujihisi tajiri. Tuweze kuhisi kana kwamba tunazo dola milioni moja katika benki. Naam, ikiwa tunautafuta kwanza ufalme wa Mungu na haki Yake na kuijali shughuli ya Bwana, bila kuwa wazembe katika chochote na waangalifu katika kila kitu, basi haya yote tutazidishiwa (Mat. 6:31-33). {2TG18: 27.3}

Tumeona kwa hivyo tena kwamba serikali ya mwisho ya dunia haitakuwa ya Ukomunisti wala ya Ubepari, ila ya kidini na itakayopendelea sana Ubepari kuliko Ukomunisti. {2TG18: 27.4}

27

Jumuiya ya Wadaudi Waadventista wa Sabato

(Ushirika Huru Unaojumuisha Kanisa)

Mlima Karmeli, Waco, Texas

S.L.P. 23738, Waco, TX 76702

+ 1-254-855-9539

www.gadsda.com

info@gadsda.com

Gombo la 2, Namba 17, 18

Kimechapishwa nchini Marekani

28

>