fbpx

Gombo la 2 Salamu Mwafaka Namba 15, 16

Gombo la 2 Salamu Mwafaka Namba 15, 16

                                    

AMANI YA PEKEE YA MAWAZO

Hati miliki, Kimechapishwa tena 1953

Haki zote zimehifadhiwa

V. T. HOUTEFF

                                    

 

LILE LITAKALOKUWA KATIKA BARAGUMU YA SITA WAKATI REHEMA INADUMU

KUSHINDWA KWA SHETANI MARA TATU KUNALETA “WAKATI WA TAABU MFANO WAKE HAUKUWAPO”

                                    

1

ANDIKO LA SALA

Dhambi Zinazopendwa Huzuia Ukweli

M.K.M. uk. 50 — “’Yeye pia aliyeipokea mbegu kati ya miiba huyo ndiye alisikiaye lile neno; na shughuli za dunia, na udanganyifu wa mali, hulisonga lile neno, likawa halizai. Mbegu ya injili mara nyingi huanguka kati ya miiba na magugu sugu; na ikiwa hakuna mabadiliko ya kimaadili moyoni mwa mwanadamu, iwapo tabia na mazoea ya zamani na maisha ya zamani ya dhambi hayajaachwa nyuma, iwapo tabia za Shetani hazijatengwa kutoka kwa nafsi, mmea wa ngano utasongwa. Miiba itakuwa ndiyo mmea, na itaiua ngano…. Iwapo moyo haujatiishwa kwa udhibiti wa Mungu, ikiwa Roho Mtakatifu hatendi kazi bila kukoma ili kumtakasa na kuiadili-sha tabia, tabia za zamani zitajifunua maishani…. Kristo aliyabainisha mambo ambayo ni hatari kwa nafsi. Kama yalivyoandikwa na Marko Yeye hutaja shughuli za dunia hii, udanganyifu wa mali, na tamaa za mambo men-gine. Luka hubainisha shughuli, mali, na anasa za maisha haya. Haya ndiyo hulisonga lile neno, mbegu ya kiroho inayokua. Nafsi huacha kupata lishe kutoka kwa Kristo, na maisha ya kiroho hufa moyoni.”{2TG15: 2.1}

Andiko hili hutuamuru kusali kwamba mbegu iliyopandwa mioyoni mwetu ianguke katika udongo mzuri, kwamba iweze kuota mzizi; kwamba tuwe huru kutoka kwa shughuli za maisha haya na kutoka kwa dhambi, kwa maana haijalishi unavutia kama nini Ukweli unaoingia masikioni mwa mtu, Hautafika kamwe moyoni iwapo iko dhambi yoyote inayopendwa. {2TG15: 2.2}

2

LILE LITAKALOKUWAKO KATIKA BARAGUMU YA SITA WAKATI REHEMA INADUMU

ANDIKO LA HOTUBA NA V. T. HOUTEFF

MCHUNGAJI WA WADAUDI WAADVENTISTA WA SABATO

SABATO, NOVEMBA 15, 1947

HEKALU LA MLIMA KARMELI

WACO, TEXAS

Mada ya uchambuzi wetu inapatikana katika Ufunuo, sura ya 10 na 11. Tutaanza na {2TG15: 3.1}

Ufu. 10: 1 — “Kisha nikaona malaika mwingine mwenye nguvu akishuka kutoka mbinguni, amevikwa wingu; na upinde wa mvua juu ya kichwa chake; na uso wake ulikuwa kama jua, na miguu yake kama nguzo za mo-to.”

Malaika huyu anazo sifa zote za nguvu ambayo hutuma chini “mvua ya masika,” na ambayo husababisha nafaka ya kiroho kukomaa kikamilifu, kwa saababu hiyo ndiyo maana ya wingu, na upinde wa mvua, huonye-sha. Kwa sababu upinde wa mvua hauonekani kamwe bila mvua, yule malaika kwa hivyo ndiye malaika anaye-leta mvua na mwangaza wa jua kwa ajili ya maendeleo ya kuyakomaza mazao ya mwisho. {2TG15: 3.2}

Ufu. 10: 2 — “Na katika mkono wake alikuwa na kitabu kidogo kimefunguliwa. Akaweka mguu wake wa ku-ume juu ya bahari, nao wa kushoto juu ya nchi..”

Kipo kitabu kimoja tu katika Bibilia ambacho kilipaswa kufunguliwa, na hicho ni kitabu cha Danieli (Dan. 12: 4). Na kwa kuwa kitu cha kwanza ambacho malaika alifanya ni kukifungua kitabu, uchambuzi unathibitisha kwamba yeye kwa kweli anaonekana kwenye eneo mwanzoni mwa wakati wa

3

mwisho, wakati ambapo kitabu kilipaswa kufunuliwa. (Ufu. 10: 2). {2TG15: 3.3}

Mnajua kwamba mwanadamu huanza kwa mguu wake wa kulia. Sasa, kwa sababu mguu wa kulia wa malaika ulikuwa juu ya bahari na mguu wake wa kushoto juu ya nchi, mfano huu unaonyesha kwamba anaanzia baharini, mkoa wa wanyama wa Danieli (Dan. 7), kisha juu ya nchi, mkoa wa mnyamma mwenye pembe mbili (Ufu. 13: 10-18). Kazi yake, kwa hivyo, inaanzia katika Nchi ya Kale, na inapaswa kujumuisha haswa ukweli wa kwanza ambao ulifunuliwa kutoka katika kitabu cha Danieli. Kwa ujumla ujumbe wake na nguvu zinathibitisha kwamba ni wa dunia yote — nchi na bahari. {2TG15: 4.1}

Ufu. 10: 3, 4 — “Naye akalia kwa sauti kuu, kama simba angurumavyo. Na alipolia, zile ngurumo saba zik-atoa sauti zao. Hata ngurumo saba zilipotoa sauti zao, nalikuwa tayari kuandika. Nami nalisikia sauti kutoka mbinguni ikisema, Yatie muhuri maneno hayo yaliyonenwa na hizo ngurumo saba, usiyaandike.”

Hapa tunaona kwamba ulikuwapo ukweli mwingine ambao ungalikuwa umeandikwa, lakini Yohana aliam-biwa asiuandike. Hatuwezi kujua ni ukubwa kadiri gani ukweli wa Ngurumo Saba unasheheni, ila ikiwezekana kama vile au zaidi ya Baragumu Saba. Bila kujali, hata hivyo, jambo moja linasimama wazi, nalo ni kwamba kutoziandika Ngurumo Saba kunaacha pengo katika mnyororo wa Ukweli. Na kwa sababu Ngurumo Saba hazikuandikwa, ukweli wazo hauwezi kufunuliwa kwa ufasiri, kwa maana hakuna chochote kilichoandikwa kuzihusu, na kwa hivyo hakuna chochote cha kufasiri kutoka kwazo. Iwapo, basi, tutawahi kuujua ukweli wa zile Ngurumo Saba, utaonyeshwa kwetu labda kwa njia ile ile kama Ufunuo ulivyoonyeshwa kwa Yohana.) {2TG15: 4.2}

4

Ufu. 10: 5-7 — “Na yule malaika niliyemwona, akisimama juu ya bahari na juu ya nchi, akainua mkono wake wa kuume kuelekea mbinguni, akaapa kwa yeye aliye hai hata milele na milele, yeye aliyeziumba mbingu na vitu vilivyomo, na nchi na vitu vilivyomo, na bahari na vitu vilivyomo, ya kwamba hapatakuwa na wakati baada ya haya; isipokuwa katika siku za sauti ya malaika wa saba atakapokuwa tayari kupiga baragumu; hapo ndipo siri ya Mungu itakapotimizwa, kama alivyowahubiri watumishi wake hao manabii.” (Mwanzoni mwa kuvuma kwa baragumu ya saba, Siri ya Mungu itatimizwa.)

Je! vipi kuhusu taarifa, “hapatakuwa na wakati baada ya haya”? — Jibu linapatikana katika Ufu. 10: 6, ambalo kwa kweli linathibitisha kwamba hapatakuwa na wakati baada ya haya kwa Siri ya Mungu kutimizwa; kwamba siku zinazosalia za baragumu ya sita, wakati hadi kwa kuvuma tarumbeta ya saba, ni wakati kwa ajili ya Siri ya Mungu, Injili ya Kristo, kutimizwa. Kwa kweli, tangazo hasa la kwanza la malaika wa saba ni kwamba falme za dunia hii zimekuwa falme za Bwana wetu, — kwamba kazi ya Injili imekamilika.) {2TG15: 5.1}

Ufu. 10: 8-10 — “Na sauti ile niliyoisikia kutoka mbinguni ilinena nami tena, ikisema, Enenda, ukakitwae kile kitabu kilichofunguliwa katika mkono wa yule malaika, aliyesimama juu ya bahari na juu ya nchi. Nikamwendea malaika yule nikamwambia kwamba anipe kile kitabu kidogo. Akaniambia, Kitwae, ukile, nacho kitakutia uchungu tumboni mwako, bali katika kinywa chako kitakuwa kitamu kama asali. Nikakitwaa kile kitabu kidogo katika mkono wa malaika yule, nikakila; nacho kikawa kitamu kama asali kinywani mwangu, na nilipokwisha kukila tumbo langu likatiwa uchungu.”

5

Kula kitabu ni, kwa mfano, “kumeza” semi zake. Utamu wa asali lazima uwe furaha ambayo hutoka kwa ahadi zake, na bila shaka uchungu huashiria kutokuweza kumeng’enya, kuelewa yote, na hivyo kuvunjika moyo. Haya, mnajua yalitimizwa katika siku za Vuguvugu la Waadventista wa siku ya Kwanza, ambapo kupitia ule uchambuzi wa kitabu cha Danieli, walipata kwamba kupatakasa Patakatifu (Dan. 8:14) kulianza mwaka wa 1844, lakini walikosa kuelewa utakaso haukumaanisha mwisho wa dunia na kurudi kwa Kristo. Kuvunjika moyo kulikuja baada ya tarehe iliyowekwa kupita na baada ya matarajio ya watu kutotimika.) {2TG15: 6.1}

Ufu. 10: 11 — “Wakaniambia, Imekupasa kutoa unabii tena juu ya watu na taifa na lugha na wafalme wengi.”

Baada ya kuvunjika moyo waliamriwa kutoa unabii tena; yaani, kuutangaza tena utakaso wa Patakatifu. Kazi hii walipaswa kuifanya miongoni mwa watu wengi, mataifa, lugha, na wafalme, bila shaka sio kwa wote.) {2TG15: 6.2}

Hivyo ilikuwa kwamba vuguvugu la Waadventista wa siku ya Kwanza lilipangwa upya na kuitwa tena, Waadventista wa Sabato. Jumuiya ya Waadventista wa Sabato, kwa hivyo, haitamaliza kazi. Ujumbe wake hau-endi kwa watu wote, kwa mataifa yote, lugha zote na wafalme wote. Vivyo hivyo, Kanisa, pia, litapangwa tena iwapo Injili ya Ufalme itahubiriwa kwa mataifa yote. “Uamsho na matengenezo lazima yafanyike chini ya msaada wa Roho Mtakatifu. Uamsho na matengenezo ni mambo mawili tofauti. Uamsho unaashiria upya wa maisha ya kiroho, kuzifanya hai nguvu za akili na moyo, ufufuo kutoka katika kifo cha kiroho. Matengenezo

6

yanaashiria kuwa na mpangilio mpya badiliko katika mawazo na nadharia, tabia na mazoea.’” — Kristo Haki Yetu, uk. 121, toleo la 1941.) {2TG15: 6.3}

Mpangilio mpya utatukiaje? — {2TG15: 7.1}

“Maana Bwana atakuja na moto, na magari yake ya vita kama upepo wa kisulisuli; ili atoe malipo ya ghadhabu yake kwa moto uwakao, na maonyo yake kwa miali ya moto. Kwa maana Bwana atatta na wote wenye mwili, kwa moto na kwa upanga wake; nao watakaouawa na Bwana watakuwa wengi. {2TG15: 7.2}

“Watu wale wajitakasao, na kujisafisha katika bustani, nyuma yake aliye katikati; wakila nyama ya nguruwe, na machukizo, na panya, watakoma pamoja, asema Bwana. {2TG15: 7.3}

“Nami nitaweka ishara kati yao, nami nitawatuma hao waliookoka kwa mataifa, Tarshishi, na Puli, na Ludi, wavutao upinde, kwa Tubali, na Yavani, visiwa vilivyo mbali; watu ambao hawajaisikia habari Yangu, wala kuuona utukufu Wangu; nao watahubiri utukufu Wangu katika Mataifa. {2TG15: 7.4}

“Nao watawaleta ndugu zenu wote kutoka mataifa yote, kuwa sadaka kwa Bwana, juu ya farasi, na katika magari, na katika machela, na juu ya nyumbu, na juu ya wanyama wepesi, mpaka mlima Wangu mtakatifu Ye-rusalemu, asema Bwana, kama vile wana wa Israeli waletavyo sadaka yao nyumbani kwa Bwana katika chombo safi.” Isa. 66:15-17, 19, 20. {2TG15: 7.5}

Katika aya hizi tunauona mchinjo ukitukia, mchinjo ambao unawaondolea mbali waasi wa Ukweli. Wale am-bao wanaokoka

7

mchinjo wa Bwana wanatumwa kwa mataifa ambao hawajauona utukufu wa Mungu, au kusikia sifa Yake, na watawaleta ndugu zao wote kutoka kwa “mataifa yote.” Kwa udhahiri, mchinjo huo u ndani ya Kanisa, kwa maana wale ambao wanaokoka wanatumwa kuhubiri kwa Mataifa ambao hawajui lolote kumhusu Mungu. Ku-watuma waaminifu kwa mataifa, baada ya kuchinjwa wale wasio waaminifu, kunadokeza umbele kupangilia upya. Na utume mwishowe utaenda, sio kwa mataifa mengi, ila kwa mataifa yote. Iwapo watawaleta ndugu zao kutoka kwa mataifa yote, basi lazima wawe wa mwisho, wale wa kumaliza kazi, “Siri ya Mungu,” kufunga re-hema na kuileta dunia kwa kikomo. {2TG15: 7.6}

Ufu. 11: 1 — “Nikapewa mwanzi kama fimbo; na mmoja akaniambia, Inuka, ukalipime hekalu la Mungu, na madhabahu, na hao wasujuduo humo.”

Kuwapima waabudu wa kweli ni hakika kuwahesabu. Na kwa hivyo unaona kwamba kufuatia Vuguvugu la Waadventista wa Sabato lazima kutakuwapo kuwahesabu watu wake. Na kwa sababu lipo kundi moja tu la kuhesabiwa, watu 144,000 (Ufu. 7:3), malimbuko (Ufu. 14:4), watumwa wa Mungu (Ufu. 7:3), inafuata kwam-ba wao ndio waliohesabiwa, ambao wanaokoka, na pia wanaotumwa kwa mataifa. Naam, wao ndio wanaoi-kamilisha Siri ya Mungu wanapowaleta ndugu zao kutoka kwa mataifa yote (Ufu. 7:9), mavuno ya pili. {2TG15: 8.1}

Aya ya 2 — “Na behewa iliyo nje ya hekalu uiache nje wala usiipime, kwa maana Mataifa wamepewa hiyo, nao wataukanyaga mji mtakatifu miezi arobaini na miwili.”

Waabudu, washiriki wa kanisa,

8

makabila ya Israeli, yatahesabiwa, lakini wale watakaolijaza behewa, wale wa Mataifa, wasioweza kuhesabiwa: “Baada ya hayo nikaona, na tazama, umati mkubwa sana, ambao hapana mtu awezaye kuuhesabu, watu wa kila taifa, na kabila, na jamaa, na lugha, wamesimama mbele ya kile kiti cha enzi, na mbele ya Mwana-Kondoo, wamevikwa mavazi meupe, wana matawi ya mitende mikononi mwao.” Ufu. 7: 9. {2TG15: 8.2}

Saba mara saba, arobaini na tisa, ilibainisha mwaka wa Yubile, ukombozi wa watu na wa nchi, mfano wa Ufalme kamili. Mbali na maana nyingine yoyote, miezi arobaini na miwili ikiwa ni saba sita tu, inaashiria kwam-ba mji mtakatifu, Yerusalemu, “hautakanyagiwa chini” muda wote hadi wakati wa Yubile ya uakisi, — Mataifa watafukuzwa watoke ndani yake kabla Siri ya Mungu kukamilika, kabla ya malaika wa saba kuanza kuvuma. {2TG15: 9.1}

Aya ya 3, 4 — “Nami nitawaruhusu mashahidi wangu wawili, nao watatoa unabii siku elfu na mia mbili na sitini, hali wamevikwa magunia. Hao ndio ile mizeituni miwili na vile vinara viwili visimamavyo mbele ya Bwana wa nchi.”

Wakati nabii Zekaria aliuliza ni nini mizeituni ya maono yake iliashiria, malaika akajibu, “Neno la Bwana.” Zek. 4: 6. {2TG15: 9.2}

Miti hiyo miwili ya mizeituni, basi, ni mfano wa Agano la Kale na Jipya, Bibilia (Pambano Kuu, uk. 267). Kuhusu nembo ya vinara vya taa Bwana Mwenyewe anaonyesha kwamba ni mifano ya makanisa (Ufu. 1:20). Vinara viwili kwa uhusiano na mizeituni ni kwa hivyo mifano ya makanisa ya Agano la Kale na Jipya,

9

makanisa ambayo yalitupatia Bibilia. {2TG15: 9.3}

Aya ya 5 — “Na mtu akitaka kuwadhuru, moto hutoka katika vinywa vyao na kuwala adui zao. Na mtu akitaka kuwadhuru, hivyo ndivyo impasavyo kuuawa.”

Kutoka kwa hili tunaona kwamba ingawa Bibilia ni rafiki bora kwa marafiki Zake, Ni adui wa kutisha kwa maadui Zake. Wakati Ukweli hauwezi kuokoa, unaua. {2TG15: 10.1}

Aya ya 6-11 — “Hao wana amri ya kuzifunga mbingu, ili mvua isinyeshe katika siku za unabii wao. Nao wana amri juu ya maji kuyageuza kuwa damu, na kuipiga nchi kwa kila pigo, kila watakapo.”

“Hata watakapoumaliza ushuhuda wao, yule mnyama atokaye katika kuzimu atafanya vita nao, naye atawashinda na kuwaua. Na mizoga yao itakuwa katika njia ya mji ule mkuu, uitwao kwa jinsi ya roho Sodoma, na Misri, tena ni hapo Bwana wao aliposulubiwa. {2TG15: 10.2}

“Na watu wa hao jamaa na kabila na lugha na mataifa wataitazama mizoga yao siku tatu u nusu,wala ha-waiachi mizoga yao kuwekwa kaburini. Nao wakaao juu ya nchi wafurahi juu yao na kushangilia. Nao wa-tapelekeana zawadi wao kwa wao, kwa kuwa manabii hao wawili waliwatesa wao wakaao juu ya nchi. Na baada ya siku hizo tatu u nusu Roho ya Uhai itokayo kwa Mungu akawaingia, wakasimama juu ya miguu yao; na hofu kuu ikawaangukia wwatu waliowatazama.” {2TG15: 10.3}

Sihitaji kusema zaidi juu ya aya hizi, kwa ajili yenu

10

mtapata maelezo ya kina kuzihusu katika Trakti Namba 2, Utata wa Onyo, uk. 47-48, toleo lililosahihishwa. {2TG15: 10.4}

Aya ya 12, 13 — “Wakasikia sauti kuu kutoka mbinguni ikiwaambia, Pandeni hata huku. Wakapanda mbingu-ni katika wingu, adui zao wakiwatazama. Na katika saa ile palikuwa na tetemeko kuu la nchi, na sehemu ya kumi ya mji ikaanguka; wanadamu elfu saba wakauawa katika tetemeko lile. Na waliosalia wakaingiwa na hofu, wakamtukuza Mungu wa mbingu.”

Bibilia huonyesha kwamba ila ni shimo moja la kuzimu lililofunguliwa, shimo ambalo nzige walitokezea (Ufu. 9: 2), na ilikuwa Nyota ya mbinguni ambayo ililifungua shimo ili kuwatoa mateka wake, — nzige ambao wangewadhuru watu wale tu ambao hawana muhuri wa Mungu katika vipaji vya nyuso zao, na kwa sababu walikuwa marafiki kwa watu wa Mungu, ukweli ni dhahiri: Nyota iliyowakomboa kutoka shimoni ni Kristo, na nzige ni wakristo, watu ambao waliokolewa kutoka kwa Uyahudi ulioasi. {2TG15: 11.1}

Zaidi ya hayo, ukweli kwamba Malaika wa Ufunuo 20:1 (adui mkubwa wa Shetani), Ndiye Aliye na ufunguo wa shimo la kuzimu, inafuatia kwamba Malaika wa Ufunuo 20:1 na Nyota ya Ufunuo 9:1 ni sawa, kwa maana Yule Ambaye alipewa ufunguo, Ndiye wa pekee angaliweza kuwa nao. {2TG15: 11.2}

Sasa tunaweza kuuliza ni nani mnyama wa shimo la kuzimu? Ikiwa Nyota iliyotoka Mbinguni na kulifungua shimo ni Kristo, na iwapo nzige waliotoka humo shimoni ni Wakristo, basi

11

hakuna njia ya kuepuka hitimisho kwamba yule mnyama aliyetoka kwenye shimo la kuzimu ni mfano wa Jumui-ya ya Wakristo. Hivyo ni kwamba Bwana alisulubiwa hapo. {2TG15: 11.3}

Sasa kwa sababu mji huo kiroho unaitwa Misri, humaanisha kwamba unawashikilia watu wa Mungu katika utumwa. Jina Sodoma linamaanisha kwamba watu wa kweli wa Mungu wataokolewa kutoka ndani yake kama vile Lutu alivyookolewa. {2TG15: 12.1}

Sehemu ya kumi ya ule mji lazima iweze kuwakilisha sehemu ya Bwana, zaka, kwa mfano. Mtetemeko kwa hivyo huwakilisha kupepetwa katika kanisa la Mungu. Masalia wanaompa Mungu utukufu, wanaweza tu kuwa waaminifu ambao watapona kupepetwa. Kanisa linatakaswa hivyo. Tetemeko hili, basi, ni ishara ya mchinjo wa Ezekieli tisa, na linaambatana na Isaya 66:16. {2TG15: 12.2}

Juu ya hayo, ukweli kwamba Siri ya Mungu inakamilika wakati malaika wa saba anaanza kuvuma, na pia ukweli kwamba kupepetwa kumeonyeshwa hapa kutukia wakati wa kuvuma kwa malaika wa sita, Ukweli unasimama wazi kwamba kupepetwa kunatukia kabla kazi ya Injili kukamilishwa. Roho ya Unabii katika siku yetu pia iliona umbele mpepeto huu: {2TG15: 12.3}

“Naliuliza maana ya mpepeto niliyouona, na nalionyeshwa kwamba utasababishwa na ushuhuda usiopinda unaoletwa mbele na ushauri wa Shahidi Mwaminifu kwa Walaodekia. Huu utakuwa na matokeo yake juu ya moya wa anayeupokea, na utamwongoza, kuinua kiwango na kutoa ukweli halisi. Wengine hawataustahimili ushuhuda huu wa moja kwa moja. Watainuka kuupinga, na hiki ndicho kitakachosababisha

12

mpepeto miongoni mwa watu wa Mungu.” — Maandishi ya Awali, uk. 270. {2TG15: 12.4}

Aya ya 14-19 — “Ole wa pili umekwisha pita, tazama ole wa tatu unakuja upesi.”

“Malaika wa saba akapiga baragumu; pakawa na sauti kuu katika mbingu, zikisema, ufalme wa dunia umekwi-sha kuwa ufalme wa Bwana wetu na wa Kristo wake; naye atamiliki hata milele na milele. {2TG15: 13.1}

“Na wale wazee ishirini na wanne, waketio mbele ya Mungu katika viti vya enzi vyao wakaanguka kifulifuli, wakamsujudia Mungu, wakisema, Tunakushukuru wewe, Bwana Mungu Mwenyezi, uliyeko na uliyekuwako, kwa sababu umeutwaa uweza wako ulio mkuu, na kumiliki. Na mataifa walikasirika, hasira yako nayo ikaja, na wakati ukaja wa kuhukumiwa waliokufa, na wa kuwapa thawabu yao watumwa wako manabii na watakatifu, na hao walichao jina lako, wadogo kwa wakubwa; na kuwaharibu hao waiharibuo nchi. {2TG15: 13.2}

“Kisha Hekalu la Mungu lililoko mbinguni likafunguliwa, na sanduku la agano lake likaonekana ndani ya hekalu lake. Kukawa na umeme, na sauti, na radi na tetemeko la nchi na mvua ya mawe nyingi sana.” {2TG15: 13.3}

Ikiwa unataka kuichambua sura ya kumi na moja ya Ufunuo katika maelezo yake yote, soma Trakti, “Kwa Makanisa Saba.” {2TG15: 13.4}

13

ANDIKO LA SALA

“Mahangaiko Ya Dunia Hii”

Nitasoma kutoka katika Mafunzo ya Kristo kwa Mifano, uk. 51, aya ya pili. {2TG16: 14.1}

“Hakuna daraja lililo huru kutoka kwa jaribu la hangaiko la kidunia. Kwa maskini, taabu na hali ngumu na ho-fu ya uhitaji huleta utatanishi na mizigo. Kwa matajiri huja hofu ya kupoteza na wingi wa mahangaiko ya wasi-wasi. Wafuasi wengi wa Kristo husahau funzo ambalo Yeye ametwagiza tujifunze kutoka kwa maua ya kon-deni. Huwa hawauamini utunzi Wake wa daima. Kristo hawezi kuubeba mzigo wao, kwa sababu hawamtwiki Yeye. Kwa hivyo mahangaiko ya maisha, ambayo yanapaswa kuwaelekeza kwa Mwokozi kwa ajili ya msaada na faraja, huwatenganisha kutoka Kwake.” {2TG16: 14.2}

Katika andiko hili tunaagizwa tusiibebe mizigo yetu wenyewe, ila tumruhusu Bwana aibebe kwa ajili yetu. Tungalikuwa na hisia ya farasi, tungalikuwa bora zaidi. Mnavyojua, farasi hawajali kuhusu mlo wao ujao. Kusudi lao pekee ni kuyahudumia mapenzi ya bwana wao. Wao wote huacha mzigo wa chakula na malazi kwa mabwana zao. Wanajua kwamba wanastahili ujira wao. {2TG16: 14.3}

Farasi, mnaona, wanayo imani zaidi kwa mabwana zao kuliko Wakristo wengi walivyo nayo kwa Mungu. {2TG16: 14.4}

Sasa tupige magoti na tuombe kwamba tutaweza kuyatambua haya kabisa na kwamba tutaweka imani yetu kamili katika Bwana wetu. Tunaye Bwana mwema, nasi ni wana Wake, sio farasi Wake, kumbuka. {2TG16: 14.5}

14

KUSHINDWA KWA SHETANI MARA TATU KUNALETA “WAKATI WA TAABU MFANO WAKE HAUKUWAPO”

ANDIKO LA HOTUBA NA V. T. HOUTEFF

MCHUNGAJI WA WADAUDI WAADVENTISTA WA SABATO

SABATO, NOVEMBA 29, 1947

HEKALU LA MLIMA KARMELI

WACO, TEXAS

Mada yetu alasiri hii inapatikana katika Ufunuo 12, na imeonyeshwa kwenye chati ifuatayo– {2TG16: 15.1}

15

Ufu. 12: 1-6 –“Na ishara kuu ilionekana mbinguni; mwanamke aliyevikwa jua, na mwezi ulikuwa chini ya mi-guu yake, na juu ya kichwa chake taji ya nyota kumi na mbili. Naye alikuwa ana mimba, akilia, hali ana utun-gu na kuumwa katika kuzaa. Ikaonekana ishara nyingine mbinguni; na tazama, joka kubwa jekundu, alikuwa na vichwa saba na pembe kumi, na juu ya vichwa vyake vilemba saba. Na mkia wake wakokota theluthi ya nyota za mbinguni, na kuziangusha katika nchi. Na yule joka akasimama mbele ya yule mwanamke aliye tayari kuzaa, ili azaapo, amle mtoto wake. Naye akazaa mtoto mwanamume, yeye atakayewachunga mataifa yote kwa fimbo ya chuma. Na mtoto wake akanyakuliwa hata kwa Mungu, na kwa kiti chake cha enzi. Yule mwanamke akakimbilia nyikani, ambapo ana mahali palipotengenezwa na Mungu, ili wamlishe huko muda wa siku elfu na mia mbili na sitini.”

Sote kwa kiasi tunakubali, najua, kwamba mwanamke huyu wa Ufunuo 12 ni nembo ya Kanisa; kwamba Joka ni nembo ya Shetani; na kwamba mtoto humwakilisha Kristo. Lakini kwa kadri hatuwezi kukubaliana kama mwanamke ni nembo ya kanisa la Agano la Kale au Jipya au ya yote mawili, ni muhimu kwamba tujifunze ili tuone jicho kwa jicho. {2TG16: 16.1}

Sasa, maswali yanainuka kwa kawaida, iwapo Kristo Ndiye Aliyezalisha kanisa la Kikristo, basi anawezaje kuwa mama Yake? Na je! Kristo hakuzaliwa angalau miaka thelathini kabla kanisa la Kikristo kuwapo? Je! yai huwa halitagwi kabla ya kifaranga kuanguliwa? Na mwishowe, je! sio kweli kwamba ikiwa hatutafanya kosa kwa msingi wa uongo kwamba tutajikuta mbali na mbali zaidi kutoka kwa ukweli

16

juu ya mada? — Kwa hakika. Basi, hebu, tufanye wa uhakika msingi ambao tunajenga juu yake. {2TG16: 16.2}

Sote tunajua kwamba Kristo alizaliwa, sio kwa kanisa la Kikristo, ila kwa la Kiyahudi. Hili likiwa hivyo, basi tunawezaje kuuepuka ukweli kwamba mwanamke huyu aliyevikwa taji yenye nyota kumi na mbili kimsingi ni kanisa la Kiyahudi ambalo liliona utungu na kumzaa “Mkombozi wa ulimwengu” katika kipindi cha Agano la Kale? {2TG16: 17.1}

Zaidi ya hayo, kabla mtoto hajazaliwa, na kabla Injili ya Kristo kuja kwa Kanisa, alikuwa amevikwa jua, na mwezi ulikuwa chini ya miguu yake. Hakuna kwa hivyo hata udhuru mdogo kwa mtu kuhitimisha kwamba yule mwanamke huwakilisha Kanisa lililovikwa na Injili ya Kristo. Na ikiwa vazi lake la jua haliwakilishi Injili ya Kristo, basi linawakilisha nini? {2TG16: 17.2}

Kwa sababu alikuwa amevikwa jua kabla ya kuzaliwa kwa Kristo, na kabla ya Injili kuja, basi mavazi yake ya jua lazima yawe ni Bibilia, Neno la Mungu lililomvika vazi katika kipindi cha manabii. {2TG16: 17.3}

Je! Ni nini kinachowakilishwa na mwezi chini ya miguu yake? — Ukweli kwamba mwezi wa mbingu za mbingu huakisi nuru kutoka jua hadi kwa dunia, mwezi wa nembo kwa sababu ya kuwa chini ya miguu ya mwanamke, na jua likiangaza moja kwa moja juu yake, sio kwa kuakisi kupitia kwa mwezi, humaanisha kwamba njia yake ya kupitisha nuru, ya mwezi, ilikuwa inatoweka, haikuwa inahitajika tena, kwamba jua lenyewe, chanzo cha nuru yake, likiangaza moja kwa moja juu yake, lilimfunika kwa miale yake miangavu. Je! Mwezi basi ungaliweza kuwakilisha nini ila kipindi kabla ya Bibilia kuja, kipindi

17

kabla ya Musa, ambacho Neno la Mungu halikuangaza moja kwa moja kwa watu kama linavyofanya leo (kwa maana hawakuwa na Bibilia siku hizo), bali liliakisiwa kwao kupitia kwa watu wa Mungu, wawasiliani, yaani, manabii kabla ya Musa hawakuziandika jumbe za Mungu ila walizipitisha kwa masimulizi. {2TG16: 17.4}

Ingawa huyu mwanamke aliyevikwa taji ya nyota kumi na mbili huwakilisha kitu fulani katika wakati wa Agano la Kale, jinsi ambavyo tumeona tayari, yeye hata hivyo anaonekana kuwakilisha kitu fulani katika wakati wa Agano Jipya. Hili tunaliona kutoka kwa ukweli kwamba baada ya mtoto kuzaliwa, na baada ya kanisa la Kikristo kutokea, mwanamke huyo alipewa mabawa ya tai mkubwa, na hivyo akawezeshwa kuruka hadi nyi-kani, huko kulishwa “kwa wakati, na nyakati, na nusu wakati.” Zaidi ya hayo, yeye kuliacha shamba la mizabibu (nchi yake — Palestina) na kwenda nyikani (nchi za watu wa Mataifa, kwa maana ndivyo nyika huwakilisha ki-mfano kwa ulinganisho na shamba la mizabibu) tena kunaonyesha kwamba aliendelea kuwapo baada ya mtoto wake kuzaliwa. {2TG16: 18.1}

Kuzingatia kauli hizi zote kwa ujumla, zinaonyesha hakika kwamba mwanamke huyo ni mfano wa Kanisa la Mungu lililo hai daima kwa nyakati zote, na kwamba ndilo Ukweli Wake wa kuokoa, Mke wake wa kweli, Ukweli uliomzaa Kristo na ambao huwazaa “Ndugu” Zake wote (wafuasi Wake), “masalia wa uzao wake.” Ufu. 12:17. {2TG16: 18.2}

Wakati ambapo ahadi ya Mwokozi ajaye ilifanywa, ndipo wakati huo joka lilijua kwamba Kanisa lingemzaa “mtoto mwanamme,” na kutokea wakati huo alimchunguza kwa ukaribu, akitumaini kumuangamiza Mkombozi wa dunia mara tu Yeye anapozaliwa. Hili alijitahidi kulitimiza

18

kupitia kwa Herode, aliposababisha umati wa watoto wachanga kuchinjwa. Mtoto Kristo, hata hivyo aliokoka, na Ibilisi akakumbana na kushindwa kwake kwa kwanza katika uhusiano huu. {2TG16: 18.3}

Sasa Joka likiwa limeimarishwa na vichwa saba na pembe kumi, humaanisha kwamba lilidhibiti tawala zote za kiraia na kidini katika siku hiyo (kwa maana namba “kumi” ya mfano humaanisha dunia yote nzima, jinsi am-bavyo hufanya vidole kumi vya Danieli 2, pembe kumi za wale wanyama wengine wa Bibilia, na wanawali kumi wa Mathayo 25). {2TG16: 19.1}

Zile pembe huwakilisha tawala zote za kiraia, ilhali vichwa huwakilisha tawala zote za kidini, kwa maana namba ya Bibilia “saba” humaanisha ukamilifu. Juu ya hayo, ukweli kwamba lile Kanisa (Wayahudi), chombo pekee kupitia kwacho kilimfanyia Mungu kazi hadi wakati huo, kilimsulubisha Bwana, ndani yake ni uthibitisho wa kutosha kwamba Kanisa lilikuwa limeasi, kwamba lilikuwa kichwa cha saba cha Joka, na kwamba hivyo ndivyo Joka lilivyokuwa limejihami kwa pembe kumi na vichwa saba, — kwa mamlaka yote ya kiraia na ya kidini. Na, hivyo, mnaona, Joka pamoja na pembe zake na vichwa huwakilisha dunia iliotekwa na Ibilisi. {2TG16: 19.2}

Hivyo ni kwamba dunia ilikuwa imepotea katika siku hiyo, na hivyo ilikuwa kwamba Kristo alikuja kuikom-boa. Ili kufanya yote haya Yeye alianzisha mpangilio mpya wa kanisa. Katika nuru hii tunamwona Kristo, Mkombozi wa ulimwengu, na utume Wake hata muhimu zaidi kuliko vile tumewahi kuuona hapo awali. {2TG16: 19.3}

Mchoro wa Joka kutoka mbinguni theluthi ya nyota (malaika, Ufu. 12:9) kwa mkia wake, sio kwa makucha yake, humaanisha kwamba mwanzoni mwa uasi wa Shetani wa ulimwengu mzima malaika walijitolea kumfuata kiongozi mwasi,

19

na kuungana naye katika kazi yake ya uovu dhidi ya familia ya wanadamu. {2TG16: 19.4}

Ufu. 12:7-17 — “Kulikuwa na vita mbinguni; Mikaeli na malaika zake wakapigana na yule joka, yule joka naye akapigana nao pamoja na malaika zake; nao hawakushinda, wala mahali pao hapakuonekana tena mbinguni. Yule joka akatupwa, yule mkubwa, nyoka wa zamani, aitwaye Ibilisi na Shetani, audanganyaye ulimwengu wote; akatupwa hata nchi, na malaika zake wakatupwa pamoja naye. Nikasikia sauti kuu mbingu-ni, ikisema, Sasa kumekuwa wokovu, na nguvu, na ufalme wa Mungu wetu, na mamlaka ya Kristo wake; kwa maana ametupwa chini mshitaki wa ndugu zetu, yeye awashitakiye mbele za Mungu wetu, mchana na us-iku. Nao wakamshinda kwa damu ya Mwana-Kondoo, na kwa neno la ushuhuda wao; ambao hawakupenda maisha yao hata kufa. Kwa hiyo shangilieni, enyi mbingu, nanyi mkaao humo. Ole wa nchi na bahari! Kwa maana yule Ibilisi ameshuka kwenu mwenye ghadhabu nyingi, akijua ya kuwa ana wakati mchache tu. Na joka yule alipoona ya kuwa ametupwa katika nchi, alimwudhi mwanamke yule aliyemzaa mtoto mwana-mume. Mwanamke yule akapewa mabawa mawili ya tai yule mkubwa, ili aruke, aende zake nyikani hata ma-hali pake, hapo alishwapo kwa wakati na nyakati na nusu ya wakati, mbali na nyoka huyo. Nyoka akatoa katika kinywa chake, nyuma ya huyo mwanamke, maji kama mto, amfanye kuchukuliwa na mto ule. Nchi ikamsaidia mwanamke; nchi ikafunua kinywa chake, ikaumeza mto ule alioutoa yule joka katika kinywa chake. Joka akamkasirikia yule mwanamke, akaenda zake afanye vita juu ya wazao wake waliosalia, wazishi-kao

20

amri za Mungu, na kuwa na ushuhuda wa Yesu.”

Jambo kuu linalopaswa kukumbukwa katika aya hizi ni kwamba baada ya Joka na malaika zake kutupwa kutoka Mbinguni (kushindwa kwa pili kwa Shetani), na baada ya kulitesa Kanisa, na alipokuwa amepaa kuingia nyikani, Joka likamfuata huko, lakini badala ya kumtesa, likatoa “maji kama mafuriko nyuma yake,” likitumaini kumfanya achukuliwe nayo. Kwa maneno mengine, baada ya kuona kwamba hangaliweza kuzuia ukuaji wa Ka-nisa la Kikristo kwa kuwatesa wafuasi wake, lilibadilisha mbinu zake na badala yake likawalazimisha Wapagani kujiunga nalo, likitarajia kulisababisha kufanywa kuwa la upagani — “kuchukuliwa.” {2TG16: 21.1}

Joka, hata hivyo, litakosa tena shabaha, kwa maana nchi itafunua kinywa chake na kuumeza mto kama mafu-riko; yaani, Uvuvio hakika unatabiri kwamba wale hujiunga na Kanisa kwa kusudi lingine isipokuwa kufuata na kutekeleza Ukweli, watatolewa kwa muujiza, watamezwa na nchi, kwa mfano. Na hili litakapotukia Shetani atakuwa amekutana na kushindwa kwake kwa tatu. Kwa muhtasari, hapa ni kushindwa kwake mara tatu: Nam-ba 1 — Kushindwa kummeza mtoto; Namba 2 — Kushindwa vita Mbinguni; Namba 3 — Kushindwa kulipagani-sha Kanisa kwa kuligharikisha na wasio waongofu. {2TG16: 21.2}

Wakati atakapokutana na kushindwa kwake kwa tatu, wakati magugu aliyoyapanda yamechomwa (kwa maa-na kama mafuriko wanamezwa na nchi, lakini kama magugu wanachomwa na malaika), wakati huo inakuwa kwamba Kanisa litaonekana “zuri kama mwezi, safi kama jua, la kutisha kama jeshi lenye bendera, litasonga mbele dunani kote

21

likishinda na kushinda.” — Manabii na Wafalme, uk. 725. {2TG16: 21.3}

Baada ya kukutana na kushindwa nguvu hivi, na baada ya kuona kwamba Kanisa limewekwa huru kuutoka kwa mafuriko yake, hasira ya Joka itazidishwa. Atamkasirikia huyo mwanamke na “kufanya vita juu ya wazao wake waliosalia, wazishikao amri za Mungu, na kuwa na ushuhuda wa Yesu Kristo” (Ufu. 12:17), “Roho ya Un-abii” (Ufu. 19:10). {2TG16: 22.1}

Bila shaka, waliosalia ni wale ambao wamesazwa baada ya nchi kukifunua kinywa chake na kuyameza mafu-riko. Wao kama kundi huzishika amri za Mungu, na wanayo Roho ya Unabii aliye hai, Roho ambaye ali-andikisha Maandiko, Ambaye amewaongoza watu wa Mungu katika Kweli yote kupitia vizazi vyote, na Am-baye bado anawaongoza. Hivyo ni kwamba hasira ya Joka, na utakaso wa Kanisa, uliosababishwa na Joka kushindwa mara ya tatu, kutaleta wakati wa taabu ambayo haikuwahi kuwapo: {2TG16: 22.2}

“Wakati huo Mikaeli atasimama, Jemadari mkuu asimamaye upande wa wana wa watu wako; na kutakuwa na wakati wa taabu, mfano wake haukuwapo tangu lilipoanza kuwapo taifa hata wakati uo huo: na wakati huo wa-tu wako wataokolewa, kila mmoja atakayeonekana ameandikwa katika kitabu kile.” Dan. 12: 1. {2TG16: 22.3}

Hakuna kitu duniani ambacho kina thamani kama majina yetu kuwa yameandikwa kwenye kile kitabu. Na humo yanaweza kuwamo majina yetu iwapo tutachagua kumfuata Roho wa Kweli na kuzishika amri za Mungu. Hapa tumeona kwamba wale wanaofikiri kwamba sheria, amri hizo kumi, “zimetanguliwa,” kwamba maisha yao hayafai kupatana na

22

sheria; na wale ambao hufikiri kwamba Roho ya Unabii ni jambo la zamani, kwamba Mungu ameiacha dunia kujiendesha kadri iwezavyo, kwamba Yeye hajijisumbui tena kumtuma nabii; kwamba wote hawa watajikuta katika muungano na Babeli Mkuu, kiti cha Joka, na badala ya kuweka majina yao katika kile Kitabu, watakuwa na alama ya mnyama, na watashiriki sehemu kuwatesa waliosalia ambao wanashika Amri za Mungu, na kuwa na ushuhuda wa Yesu Kristo. {2TG16: 22.4}

Sasa ni wakati wa wote kuamua ama kumezwa na nchi — kutupwa motoni — au kuokolewa na Mikaeli, Mkuu wetu. {2TG16: 23.1}

Hebu kwa hivyo tuchague ukombozi badala ya kushindwa. “Mpendeni Bwana, ninyi nyote mlio watakatifu wake wote; Bwana huwahifadhi waaminifu, humlipa atendaye kiburi malipo tele.” Zab. 31:23. {2TG16: 23.2}

23

Jumuiya ya Wadaudi Waadventista wa Sabato

(Ushirika Huru Unaojumuisha Kanisa)

Mlima Karmeli, Waco, Texas

S.L.P. 23738, Waco, TX 76702

+ 1-254-855-9539

www.gadsda.com

info@gadsda.com

Gombo la 2, Namba 15, 16

Kimechapishwa nchini Marekani

24

>