fbpx

Gombo la 2 Salamu Mwafaka Namba 11, 12

Gombo la 2 Salamu Mwafaka Namba 11, 12

                                    

AMANI YA PEKEE YA MAWAZO

Hati miliki, Kimechapishwa tena 1953

Haki zote zimehifadhiwa

V. T. HOUTEFF

                                    

 

JINSI UFALME UTAKAVYOKUJA

UFUNUO — NI NINI?

                                    

1

WAZO LA SALA

Kuyaweka Mawazo Yetu Kwa Ufalme Wa Kristo

Tutaendelea kusoma kwetu kutoka katika Mafunzo ya Kristo kwa Mifano, ukurasa wa 44, aya ya mwisho– {2TG11: 2.1}

“Kwa sababu ndege wako tayari kuinyakua mbegu iliyo kando ya njia, hivyo Shetani yu tayari kuzinyakua mbegu za ukweli mtakatifu kutoka kwa nafsi. Anaogopa kwamba neno la Mungu linaweza kuwaamsha wasi-ojali, na kufanya kazi kwa moyo mgumu. Shetani na malaika zake wapo kwenye mikusanyiko ambayo injili huhubiriwa. Wakati malaika wa mbinguni wanajaribu kuvuta mioyo kwa neno la Mungu, adui yu macho ili kufanya kazi hiyo isiwe na matokeo. Kwa bidii iliyo sawa tu na maovu yake, hujaribu kuikomesha kazi ya Roho wa Mungu. Wakati Kristo anaivuta nafsi kwa upendo Wake, Shetani hujaribu kugeuza usikivu wa yule ambaye amevutwa kumtafuta Mwokozi. Huishughulisha nia na miradi ya kidunia. Huchochea kulaumiwa, au hupenyeza shaka na kutokuamini. Uchaguzi wa lugha ya mnenaji au mtindo wake yawezekana usiwafurahishe wasikilizaji, na wanaendelea kuzifikiria kasoro hizi. Hivyo ukweli wanaouhitaji, na ambao Mungu amewatumia kwa neema, haufanyi mguso wa kudumu.”{2TG11: 2.2}

Tunahitaji kuomba kwa ajili ya nini mchana huu? — Kwamba malaika waweze kutuzunguka ili Adui asiweze kupata fursa ya kuzinyakua mbegu za Ukweli wa Kiungu; kwamba tuyaweke mawazo yetu kwa Kristo na Ufalme Wake, hivyo hautakuwapo mwanya wowote kwa Yule Mwovu kupata kiingilio na hivyo kutudanganya kutenda dhambi. {2TG11: 2.3}

2

JINSI UFALME UTAKAVYOKUJA

ANDIKO LA HOTUBA NA V. T. HOUTEFF

MCHUNGAJI WA WADAUDI WAADVENTISTA WA SABATO

SABATO, OKTOBA 11, 1947

HEKALU LA MLIMA KARMELI

WACO, TEXAS

Wayahudi walikuwa wamejenga dhana potofu kuhusu namna Ufalme ungeweza kuwa, na jinsi na lini un-gepaswa kuja na hivyo wakati Bwana alipofunua dhana zao, walikasirika. Walikasirika sana, sio kwa sababu Ufalme ambao Mwokozi aliufunua haukuwa wa neema zaidi na halisi kuliko vile walivyowahi kufikiri, ila kwa sababu makosa yao yalifunuliwa! Hivyo watu waliopendelewa na Mbingu, Wayahudi, walirundika kosa juu ya kosa, na wakajiletea aibu na balaa. {2TG11: 3.1}

Wazo la Mkristo kuhusu Ufalme kwa kiasi fulani liwe na makosa, pia, na tushindwe kufaidika kutoka kwa makosa ya Wayahudi, basi anguko letu litakuwa kubwa zaidi kuliko lile la Wayahudi. Hebu kwa hivyo tuweke kando maoni yoyote ya zamani tunayoweza kuwa nayo, na tuupokee Ukweli wa Bwana uliofunuliwa ambao unatuletea wazo Lake la Ufalme upya leo: {2TG11: 3.2}

Mat. 13:24-26 — “Akawatolea mfano mwingine, akisema, Ufalme wa mbinguni umefanana na mtu aliye-panda mbegu njema katika konde lake. Lakini watu walipolala, akaja adui yake akapanda magugu katikati ya ngano akaenda zake. Baadaye majani ya ngano yalipomea na kuzaa, yakaonekana na magugu.”

Magugu masumbufu ambayo hukua zaidi na

3

thabiti kuliko ngano ambayo Shetani huyavuvia na kuyatumia hutunga nadharia potofu kuhusu mpango wa Mungu. Magugu, kwa mujibu wa mfano huo, yanafanana sana na ngano hivi kwamba hayawezi kugunduliwa isipokuwa baada ya kuzaa matunda; yaani, yanaweza kutambuliwa tu kwa matokeo ya mwisho yaliyozalishwa na matendo yao. {2TG11: 3.3}

Na matokeo haya yanaweza kuwa nini? Je! Ni nini kingine kutoka kwa maoni ambayo hayajavuviwa na Mbingu unaweza kutarajia Kanisani ila ubinafsi, majisifu, ubaguzi, udunia, chuki isiyo na sababu, chuki dhidi ya karipio na nuru kwa matendo yao maovu? Je! Sio lengo lao kujiinua wenyewe badala ya kumwinua Kristo na Ukweli Wake? {2TG11: 4.1}

“Lakini ufahamu neno hili, ya kuwa siku za mwisho kutakuwako na nyakati za hatari. Maana watu watakuwa wa kujipenda wenyewe, wenye kupenda fedha, wenye kujisifu, wenye kiburi, wenye kutukana, wasiotii wazazi wao, wasio na shukrani, wasio safi, wasiowapenda wa kwao, wasiotaka kufanya suluhu, wasingiziaji, wasi-ojizuia, wakali, wasiopenda mema, wasaliti, wakaidi, wenye kujivuna, wapendao anasa kuliko kumpenda Mun-gu; wenye mfano wa utauwa, lakini wakikana nguvu zake; hao nao ujiepushe nao. Kwa maana katika hao wamo wale wajiingizao katika nyumba za watu, na kuchukua mateka wanawake wajinga wenye mizigo ya dhambi, waliochukuliwa na tamaa za namna nyingi; wakijifunza siku zote, ila wasiweze kabisa kuufikia ujuzi wa kweli.”2 Tim. 3: 1-7. {2TG11: 4.2}

Mat. 13: 27-30 — “Watumwa wa mwenye nyumba wakaenda wakamwambia, Bwana, hukupanda mbegu nje-ma katika konde lako? Limepata wapi basi magugu? Akawaambia, Adui ndiye aliyetenda hivi. Watumwa wakamwambia, Basi, wataka twende tukayakusanye? Akasema, La; msije mkakusanya magugu, na kuzing’oa

4

ngano pamoja nayo. Viacheni vyote vikue hata wakati wa mavuno; na wakati wa mavuno nitawaambia wavunao, Yakusanyeni kwanza magugu, myafunge matita matita mkayachome; bali ngano ikusanyeni ghalani mwangu.”

Hapa tunaona kwamba hata maoni ya watumwa waaminifu zaidi wa Mungu kuhusu kuanzishwa kwa ufalme Wake na kuyang’oa magugu, sio sawa na mipango ya Mungu. Kazi hii ya utakaso ni ya malaika wa mbinguni pekee, wataifanya katika wakati wa mavuno baada ya kuamuriwa kufanya hivyo, sio kabla. {2TG11: 5.1}

Katika mfano huu pia tunaambiwa kwamba mavuno ya kiroho ni “wakati,” sio kazi ya dakika, na kwamba in-auleta mwisho wa dunia kama ilivyo kawaida wakati mavuno ya mwaka huleta mwisho wa hari. {2TG11: 5.2}

Hivyo, unaona, utengo wa ngano na magugu unatukia katika siku za mwisho na katika sehemu mbili tofauti: kwanza ndani ya nyumba ya Mungu (1 Pet. 4:17; Mat. 13:47,48), mishowe katika Babeli (Ufu. 18: 2-4). {2TG11: 5.3}

Katika ya awali magugu yanaondolewa miongoni mwa watu wa Mungu, ila katika ya mwisho watu wa Mun-gu wanaondolewa kati ya magugu — kutoka kwa maskani ya mashetani, ya kila roho mchafu, ya kila ndege mchafu na mwenye kuchukiza. {2TG11: 5.4}

Yapo mavuno mawili, pia: ya kwanza yanatoka katika kabila kumi na mbili za wana wa Israeli (Ufu. 7:2-8), Kanisa, na ya pili kutoka katika “mataifa yote” (Ufu. 7:9). {2TG11: 5.5}

Mat. 13: 31, 32 — “Akawatolea mfano mwingine, akisema, Ufalme wa mbinguni umefanana na

5

punje ya haradali, aliyoitwaa mtu akaipanda katika shamba lake; nayo ni ndogo kuliko mbegu zote; lakini ikii-sha kumea, huwa kubwa kuliko mboga zote, ikawa mti, hata nyuni wa angani huja na kukaa katika matawi yake.”

Mbegu ya haradali ikiwa ndogo zaidi ya mbegu zote mfano huu unaonyesha kwamba kile kitakachouanzisha Ufalme kitakuwa kidogo sana, kinyume na matarajio yote ya wanadamu. Pamoja na hayo, kama mmea wa haradali hukua mkubwa zaidi ya mimea yote, kwa hivyo Ufalme utakua na kuwa mkuu kwa falme zote. Hili likiwa kinyume na mipango yote ya wanadamu, ni kawaida kwamba wale ambao ni kama Nikodemo, na hen-delea kuaibika kutambuliwa na kitu kisichokuwa maarufu, kinachochukiwa, na kisicho na maana, kama tokeo lake wataachwa nje ya Ufalme. {2TG11: 6.1}

Mat. 13:33 — “Akawaambia mfano mwingine; Ufalme wa mbinguni umefanana na chachu aliyoitwaa mwa-namke, akaisitiri ndani ya pishi tatu za unga, hata ukachachwa wote pia.”

Ufalme umeonyeshwa hapa tena utaanza na kitu kidogo, lakini kitu hicho kidogo kitakuwa kama chachu nda-ni ya mkate. Je, chachu inaweza kuwa nini isipokuwa ujumbe usio na umaarufu ulioletwa na fulani mmoja aliye mdogo na kuuweka ndani ya Kanisa, mkate. Vyema, chachu i kwenye donge sasa. Iangalie tu ikichachisha donge zima. {2TG11: 6.2}

Mat. 13:44 — “Tena ufalme wa mbinguni umefanana na hazina iliyositirika katika shamba; ambayo mtu ali-poiona, aliificha; na kwa furaha yake akaenda akauza alivyo navyo vyote, akalinunua shamba lile.”

6

Wale watakaoingia kwenye Ufalme wanawakilishwa hapa kama watafutaji wa hazina kubwa, na wanapo-lipata eneo lake, shamba, huwa na hamu kubwa ya kulifanya liwe lao. Wao huwa na uhakika wa thamani yake, na hawahesabu kuwa si hatari kuuza vyote wanavyomiliki, viwe ni vingi au vichache, ili kuupata Ufalme. Kile wanachouza, kwa kweli, sio mashamba au nyumba tu, bali kitu chochote ambacho iwapo hakiuzwi kingewawe-ka nje ya Ufalme. Wanao uhakika kwamba wanafanya uwekezaji mzuri, kwamba watapata zaidi kuliko vile walivyowekeza. Kwa upande mwingine, wale walio wapumbavu, wasioijua thamani yake, huhisi hawatathubutu kufanya uwekezaji huo, na kwa sababu hiyo watakuwa wa kupoteza. {2TG11: 7.1}

Mat. 13:45,46 — “Tena ufalme wa mbinguni umefanana na mfanya biashara, mwenye kutafuta lulu nzuri; naye alipoona lulu moja ya thamani kubwa, alikwenda akauza alivyo navyo vyote, akainunua.”

Wale watakaourithi ufalme hapa tena wanawakilishwa kama wanaokitafuta kito cha thamani kubwa, Ukweli wa Ufalme. Na wanapokipata, wanahesabu kwamba sio mchezo wa kamari kuuza vitu vyote walivyo navyo ili kukifanya kiweze kuwa chao. Wanajua kwamba wanapata biashara, kwamba uwekezaji kama huo utawafanya wawe matajiri. {2TG11: 7.2}

Wote mtu aliyelinunua shamba lenye hazina kubwa, na mtu ambaye aliinunua lulu ya thamani kubwa waliuza vyote walivyokuwa navyo ili kufunga mauzo mbalimbali. Lakini ingawa yalichukua kila kitu walichokuwa na-cho, wote wawili walikuwa na vya kutosha kununua kile walichotaka. Hivyo ni kwamba haijalishi sisi ni nani, tajiri au maskini namna gani, iwapo tutaamua kuuza vyote na kuununua Ufalme, tutakuwa na vya kutosha

7

kuununua. {2TG11: 7.3}

Mat. 13:47,48 — “Tena ufalme wa mbinguni umefanana na juya, lililotupwa baharini, likakusanya samaki wa kila namna; hata lilipojaa, walilivuta pwani; wakaketi, wakakusanya walio wema vyomboni, bali walio wa-baya wakawatupa.”

Juya lazima liwakilishe Ukweli, ujumbe wa Ufalme. Linapotupwa baharini, ukichapishwa na kutumwa nje, unakusudiwa kuwanasa wema na wabaya. Lakini juya linapovutwa pwani, wabaya wakati huo wanatupwa nje kutoka kati ya wazuri, nao wazuri wanawekwa ndani ya vyombo, ndani ya Ufalme. Hivyo, kwa sababu tu mtu anavutiwa na Ukweli wenye nguvu, haimaanishi kwamba ameokolewa. Nafasi yake ya kudumu milele na Ukw-eli hutegemea kutii kwake matarajio ya Bwana kwake. {2TG11: 8.1}

Mat. 13:52 — “Akawaambia, Kwa sababu hiyo, kila mwandishi mwenye elimu ya ufalme wa mbinguni ame-fanana na mtu mwenye nyumba atoaye katika hazina yake vitu vipya na vya kale.”

Hapa Bwana anaonyesha wazi kwamba wajumbe wa Mungu wa Ufalme huleta kutoka kwa Neno mambo ya zamani na mapya: mambo yanayojulikana na mambo yasiyojulikana kwa wao. Hivyo ndivyo daima imekuwa katika ukunjuzi wa chuo na lazima iwe hivyo sasa. {2TG11: 8.2}

Luka 14:16, 17 — “Akamwambia, Mtu mmoja alifanya karamu kubwa akaalika watu wengi, akamtuma mtumwa wake saa ya chakula awaambie wale walioalikwa, Njoni, kwa kuwa vitu vyote vimekwisha kuwekwa tayari.”

Katika mfano huu imejulishwa kwamba katika

8

masaa ya kufunga ya muda wa rehema (wakati wa chajio, karibu na mwisho wa siku), Mbingu itatuma ujumbe kwa wale walioalikwa, kwa wale ambao tayari wanaifahamu Injili ya Kristo, kwa washiriki wa Kanisa. Mtumwa atawajulisha kwamba kila kitu ki tayari, kwamba sasa waje kwa karamu kuu ya jioni iliyosubiriwa kwa muda mrefu, — chakula cha jioni watakachokula katika jumba la Mwalimu (Ufalme), sio katika nyumba zao. {2TG11: 8.3}

Luka 14: 18-20 — “Wakaanza wote kutoa udhuru kwa nia moja. Wa kwanza alimwambia, Nimenunua sham-ba, sharti niende nikalitazame; tafadhali unisamehe. Mwingine akasema, Nimenunua ng’ombe jozi tano, nina-kwenda kuwajaribu; tafadhali unisamehe. Mwingine akasema, Nimeoa mke, na kwa sababu hiyo siwezi kuja.”

Wale waliotajwa hapa hawakuomba udhuru wa kutoipokea Injili ya Kristo, ila waliomba udhuru wa kutoingia kwenye jumba la Mwalimu, kutovichukua viti vyao mezani Pake! Naam, kwa mujibu wa mfano huo, wale wali-okuwa na pesa za kununua shamba, ng’ombe, na nyumba, pia kuoa wakati huo wa mwito wa mwisho kwa karamu ulipokuja, wote waliomba udhuru kwa nia moja. Lakini maskini na vilema, wale ambao walikuwa barabarani na kwenye vichochoro, kwa mfano, ambao hawakuwa na chochote chao wenyewe, na walikuwa na hitaji la kila kitu, walifurahi kuingia ndani kwa chakula cha jioni. {2TG11: 9.1}

Hii ni kawaida sana: Wale ambao wamejitosheleza na yale ambayo ulimwengu hutoa, hawajali kutoka ndani yake. Hapa unaona kwa nini ni rahisi ngamia kuliko ilivyo kwa mtu tajiri kupitia katika tundu ya sindano (Mat. 19:24). Wale ambao shida yao tu ni kujaribu kutajirika zaidi,

9

wale ambao wamejishughulisha sana na bidhaa za ulimwengu huu, hawawezi kuchukua muda wa kula chakula chajio cha Mwalimu. Hapa unafaa msemo wa zamani, “Karibu aokolewe, lakini kapotea kabisa.” Hapa inaoneka-na wazi kwamba kuupokea ukweli mmoja ila kuukataa unaofuata, haumfaidi yeyote kitu. Mwito wa mwisho kwa mtu ndio muhimu sana. {2TG11: 9.2}

Kwa nyakati ambazo kweli mpya zimeanzishwa, mamilioni wamepotea tu kwa sababu walikuwa wameridhika sana na kile walichokuwa nacho. Hawakuona hitaji la chochote bora, au sivyo walikuwa na kiburi sana kuupokea Ukweli usiokuwa maarufu kutoka kwa mmoja wa wajumbe aliyeteuliwa na Mungu. Hivyo ni kwamba wakati ambapo Mungu hutuma ujumbe, badala ya huo kuwa hatua yao ya kupanda juu kwa wokovu, umekuwa na bado ungali kwa wengi hatua ya kuporomoka kuelekea kuhukumiwa adhabu. Kwa hatua hii nabii aliagizwa: “…Enenda, ukawaambie watu hawa, Fulizeni kusikia, lakini msifahamu; fulizeni kutazama, lakini msione. Uunoneshe moyo wa watu hawa, ukayatie uzito masikio yao, ukayafumbe macho yao; wasije wakaona kwa macho yao, na kusikia kwa masikio yao, nakufahamu kwa mioyo yao, na kurejea na kuponywa.” Isa. 6: 9, 10. {2TG11: 10.1}

Luka 14:22, 23 — “Mtumwa akasema, Bwana, hayo uliyoagiza yamekwisha tendeka, na hata sasa ingaliko nafasi. Bwana akamwambia mtumwa, Toka nje uende barabarani na mipakani, ukawashurutishe kuingia nda-ni, nyumba yangu ipate kujaa.”

Ukweli kwamba katika mji walikuwamo wale ambao tayari walikuwa “wamealikwa” wakati mwito wa mwi-sho kwa karamu ya jioni ulipowajia, unathibitisha kwamba mji unawakilisha Kanisa. Kwa wao mtumwa ali-tumwa kwanza. Barabara kuu na mipakani, kwa hivyo, mahali ambapo mtumwa alikwenda baadaye, panawakili-sha ulimwengu, mbali na kwa mbali, kote kote kando na Kanisa. Lakini sehemu muhimu

10

zaidi na ya kusikitisha sana kukumbuka katika mfano huu ni ile ambayo imesimuliwa katika aya ifuatayo: {2TG11: 10.2}

Luka 14: 24 — “Maana nawaambia ya kwamba katika wale walioalikwa, hapana hata mmoja atakayeionja karamu yangu.”

Hili ndilo lililotukia: Mara tu walipoomba udhuru, rehema ilifungwa kwa wao, hawakuwa na nafasi nyingine ya kuonja chakula Chake chajio. Rehema, hata hivyo, ilibaki wazi kwa wale ambao walikuwa bado ha-wajaalikwa. Wale waliokuwa kwenye barabara kuu na mipakani bado wangaliweza kuokolewa. {2TG11: 11.1}

Kanisa huonekana linafahamu sana kuhusu wakati wa rehema kufungwa kwa ulimwengu, lakini halina ufahamu kwamba rehema kwa washiriki wake hufunga hasa kwa wakati wanapoukataa ujumbe uliotumwa na mbingu. Hapa inaonyeshwa kwa nini wanawali watano wapumbavu waliupata mlango umefungwa ingawa walikuwa wameyapata baadaye mafuta na kufika mlangoni: Rehema yao ilikuwa imefungwa wakati waliposhindwa katika fursa ya kwanza kuvijaza vyombo vyao na mafuta ya ziada, ujumbe wa ziada. {2TG11: 11.2}

Mat. 25:1-8 — “Ndipo [wakati mtumwa asiye mwaminifu anakatwa vipande. Mat. 24:51] ufalme wa mbinguni utakapofanana na wanawali kumi, waliotwaa taa zao, wakatoka kwenda kumlaki bwana arusi. Watano wao walikuwa wapumbavu, na watano wenye busara. Wale waliokuwa wapumbavu walizitwaa taa zao, wasitwae na mafuta pamoja nao; bali wale wenye busara walitwaa mafuta katika vyombo vyao pamoja na taa zao. Hata bwana arusi alipokawia, wote wakasinzia wakalala usingizi. Lakini usiku wa manane, pakawa na kelele, Tazama, bwana arusi yuaja; tokeni mwende kumlaki. Mara wakaondoka wanawa-li wale wote, wakazitengeneza taa zao. Wale wapumbavu wakawaambia wenye busara,

11

Tupeni mafuta yenu kidogo; maana taa zetu zinazimika.”

Hapa upo Ukweli ambao haupaswi kupitiwa kijuu-juu na mtu yeyote: Mafuta yanaweza tu kuwakilisha Ukw-eli wa ki-nabii uliofunuliwa, Ukweli unaoiangaza njia mbele yao. Mafuta kwenye chombo, kabla ya kumiminwa ndani ya taa, hata hivyo, hayawezi kuangaza njia ya mtu yeyote. Kwa hivyo mafuta kwenye vyombo vya ma-bikira hao watano lazima yawakilishe usambazaji wa ziada, Ukweli wa ziada, uliokuja kwao katika kipindi cha kusinzia na kulala. Maana wakati mwito ulipofanywa, “Tazama Bwana arusi,” wanawali wote kumi walipata ma-futa katika taa zao yameisha. Vyombo vya wenye busara, hata hivyo vilikuwa vimejaa na kwa hivyo waliweza kujaza tena taa zao. Kwa ulinganisho, wapumbavu waligundua kwamba sio tukwamba taa zao zilikuwa zim-ezimika, ila vyombo vyao vilikuwa vitupu, pia. Wao kisha wakaenda kuyatafuta mafuta, lakini hayakuwasaidia, maana walipata mlango umefungwa. Walikuwa wameridhika na yale waliokuwa nayo ndani ya taa zao, waki-dhani kwamba hawakuwa na hitaji la zaidi. Kinyume cha kudhani kwao hata hivyo katika kipindi cha kusinzia na kulala ghafla waliona taa zao zikizima. Kujikuta katika giza la kiroho na machafuko wakati huo wakawa nayo hamu ya kuyapata mafuta. {2TG11: 12.1}

Hapa inaonekana kwamba ujumbe ambao Kanisa liko nao katika kipindi cha kusinzia na kulala hautoshi ku-wapeleka washiriki wake hadi mwisho. Wanauhitaji ujumbe wa ziada. {2TG11: 12.2}

Sasa ipo tofauti gani kati ya mafuta yaliyo ndani ya taa na mafuta yaliyo ndani ya chombo? — Hii tu: Mafuta yaliyo ndani ya taa, ambayo tayari huiangazia njia ya msafiri kuelekea katika jumba la Mwalimu, lazima ya-wakilishe Ukweli unaoendelea. Lakini mafuta yaliyo ndani ya chombo, lazima yauwakilishe Ukweli ambao utaiangaza njia ya mmoja baada ya Ukweli wa awali umeitimiza kazi yake. Kwa mfano,

12

baada ya mavuno (Hukumu ya Upelelezi) ya wafu kupita, kweli zingine muhimu zaidi lazima zianzishwe kwa ajili ya mavuno ya walio hai. Nasema kweli muhimu zaidi kwa sababu zinawahusu walio hai wenyewe, ku-wahusu wale ambao kesi zao zitapimwa kwa mizani, wale ambao binafsi watahukumiwa ama kama “ngano” au kama “magugu,” aidha kama “samaki” wazuri au “samaki” wabaya. {2TG11: 12.3}

Zaidi ya hayo, baada ya hukumu ya wafu ambayo Kanisa limekuwa likihubiri kwa idadi ya miaka, imekwisha, iwapo Kanisa wakati huo haliwezi kuupokea ujumbe mpya, ujumbe wa hukumu ya walio hai, halitakuwa na ujumbe, bila mafuta, kwa wakati wa hukumu ya walio hai. {2TG11: 13.1}

Maadamu mafuta yalikuwa yanapatikana kwa wanawali wote kumi, mfano huo unaonyesha wazi kwamba ujumbe wa hukumu ya walio hai unaletwa kwa Kanisa, ila ni nusu tu ya wanawali waliojipatia. Wakati hukumu ya walio hai itaanza na kilio kusikika, “Tazama, Bwana arusi yuaja: tokeni mwende Kumlaki,” wote wataamka, ila ni nusu yao tu watakaoingia. Wale nusu nyingine watakuwa wamefanya dhambi dhidi ya Roho Mtakatifu, watakuwa wameukataa Ukweli Wake! Kwa sababu hiyo watakapobisha mlangoni, jibu la Bwana arusi litakuwa, “Sikuwajua ninyi kamwe.” Upumbavu kama nini! na itakuwa kutamauka kama nini! {2TG11: 13.2}

Hili, unaona, sio nadharia ya mwanadamu, Ndugu, Dada. Ni ukweli bayana wa Mungu. Ni kesi ya kusikitisha kama nini kwa wale ambao sio tu wanavipuuza vyombo vyao wenyewe, lakini wanawazuia wengine kujipatia mafuta ya ziada sasa ambapo yanatolewa kwa wote. Hakika kutakuwapo kilio na kusaga meno isipokuwa wote

13

Walaodekia wavuguvugu sasa kwa fursa yao ya kwanza wabadilishe mawazo kuhusu kuwa tajiri na kujitajirisha na kutokuwa na haja ya kitu. {2TG11: 13.3}

Mat. 25:14-30 — “Maana ni mfano wa mtu atakaye kusafiri, aliwaita watumwa wake, akaweka kwao mali zake. Akampa mmoja talanta tano, na mmoja talanta mbili, na mmoja talanta moja; kila mtu kwa kadiri ya uwezo wake; akasafiri. Mara yule aliyepokea talanta tano akaenda, akafanya biashara nazo, akachuma faida talanta nyingine tano. Vile vile na yule mwenye mbili, yeye naye akachuma nyingine mbili faida. Lakini yule aliyepokea moja alikwenda akafukua chini, akaificha fedha ya bwana wake. Baada ya siku nyingi akaja bwa-na wa watumwa wale, akafanya hesabu nao. Akaja yule aliyepokea talanta tano, akaleta talanta nyingine ta-no, akisema, Bwana, uliweka kwangu talanta tano; tazama, talanta nyingine tano nilizopata faida. Bwana wake akamwambia, Vema, mtumwa mwema na mwaminifu; ulikuwa mwaminifu kwa machache, nitakuweka juu ya mengi; ingia katika furaha ya bwana wako. Akaja na yule aliyepokea talanta mbili, akasema, Bwana, uliweka kwangu talanta mbili; tazama, talanta nyingine mbili nilizopata faida. Bwana wake akamwambia, Vema, mtumwa mwema na mwaminifu; ulikuwa mwaminifu kwa machache, nitakuweka juu ya mengi; ingia katika furaha ya bwana wako. Akaja na yule aliyepokea talanta moja, akasema, Bwana, nalitambua ya kuwa wewe u mtu mgumu, wavuna usipopanda, wakusanya usipotawanya; basi nikaogopa, nikaenda nikaificha ta-lanta yako katika ardhi; tazama, unayo iliyo yako. Bwana wake

14

akajibu, akamwambia, Wewe mtumwa mbaya na mlegevu, ulijua ya kuwa navuna nisipopanda, nakusanya nisipotawanya; basi, ilikupasa kuiweka fedha yangu kwa watoao riba; nami nikija ningalipata iliyo yangu na faida yake. Basi, mnyang’anyeni talanta hiyo, mpeni yule aliye nazo talanta kumi. Kwa maana kila mwenye kitu atapewa, na kuongezewa tele; lakini asiye na kitu, hata kile alicho nacho atanyang’anywa. Na mtumwa yule asiyefaa, mtupeni mbali katika giza la nje; ndiko kutakuwako kilio na kusaga meno.”

Talanta katika mfano huu zinawakilisha bidhaa za Bwana, ujumbe Wake mwafaka kwa watu. Kila mmoja wa watumwa Wake amewakilishwa hapa kama ambaye amepewa kiasi fulani cha jukumu, lakini sio zaidi ya “uwezo wao”. {2TG11: 15.1}

Kutoka kwa mfano huu tunaona kwamba huduma yoyote ambayo haifikii kipimo cha 100% kwa ujazo, haiz-idishi maradufu ya talanta yake, haikubaliwi na Mungu. Huduma tepetevu sio huduma hata kidogo, ila ni hasara kubwa tu. {2TG11: 15.2}

Mat. 25:31-40 — “Hapo atakapokuja Mwana wa Adamu katika utukufu wake, na malaika watakatifu wote pamoja naye, ndipo atakapoketi katika kiti cha utukufu wake; na mataifa yote watakusanyika mbele zake; naye atawabagua kama vile mchungaji abaguavyo kondoo na mbuzi; atawaweka kondoo mkono wake wa ku-ume, na mbuzi mkono wake wa kushoto. Kisha Mfalme atawaambia wale walioko mkono wake wa kuume, Njoni, mliobarikiwa na Baba yangu, urithini ufalme mliowekewa tayari tangu kuumbwa ulimwengu; kwa maana nalikuwa na njaa, mkanipa chakula; nalikuwa na kiu, mkaninywesha; nalikuwa

15

mgeni, mkanikaribisha; nalikuwa uchi, mkanivika nalikuwa mgonjwa, mkaja kunitazama; nalikuwa kifungoni, mkanijia. Ndipo wenye haki watakapomjibu, wakisema, Bwana, ni lini tulipokuona una njaa, tukakulisha, au una kiu tukakunywesha? Tena ni lini tulipokuona u mgeni, tukakukaribisha, au u uchi, tukakuvika? Ni lini tena tulipokuona u mgonjwa, au kifungoni, tukakujia? Na Mfalme atajibu, akiwaambia, Amin, nawaambia, kadiri mlivyomtendea mmojawapo wa hao ndugu zangu walio wadogo, mlinitendea mimi. Kisha atawaambia na wale walioko mkono wake wa kushoto, Ondokeni kwangu, mliolaaniwa, mwende katika moto wa milele, aliowekewa tayari Ibilisi na malaika zake.”

Hapa imeonyeshwa kwamba watu wenye ubinafsi hawataingia kamwe katika Ufalme wa Mungu. Ni wale tu ambao wanajitahidi kufanya kitu kwa ajili ya wengine, na haswa kwa wale ambao ni wa nyumba ya imani, ndio watakaowaingia katika furaha ya Bwana wao. {2TG11: 16.1}

Kwa kweli ujio huu wa Bwana uliotajwa katika aya hizi sio ule ambao watakatifu watamlaki Yeye angani, ila kwa hakika ni ule ambao Yeye atakutana nao kwa hukumu duniani, “hukumu ya walio hai.” Yeye ataketi juu ya kiti cha enzi cha utukufu Wake, kwenye kiti cha enzi cha Kanisa Lake, Ufalme Wake, na kutoka hapo Ata-hukumu na kuutenganisha ulimwengu wote. Wengine atawaweka kulia Kwake, na wengine kushoto Kwake. {2TG11: 16.2}

Wacha sasa tuutazame utengo ndani ya Kanisa kwa mujibu wa Ufunuo. {2TG11: 16.3}

Ufu. 3: 14-16 — “Na kwa malaika wa kanisa lililoko Laodekia andika; Haya ndiyo anenayo yeye aliye Amina, Shahidi aliye mwaminifu na wa kweli, mwanzo wa kuumba kwa Mungu. Nayajua matendo yako, ya kuwa hu baridi wala hu moto; ingekuwa heri kama ungekuwa baridi au moto. Basi, kwa sababu

16

una uvuguvugu, wala hu baridi wala moto, nitakutapika utoke katika kinywa changu.”

“Malaika”, yule anayelisimamia kanisa, hawezi kuwakilisha daraja lolote isipokuwa ukasisi wa kanisa, wa-tumwa Wake. Wale ambao wameridhika (vuguvugu), ambao huhisi hawahitaji kitu chochote, hawana haja ya ujumbe wa ziada kwa hukumu ya walio hai, kama hawa Yeye atawatapika nje isipokuwa watubu. Kazi hii, unaona, inawakilisha kulitakasa hekalu Lake. {2TG11: 17.1}

Sasa tunamgeukia Malaki– {2TG11: 17.2}

Mal. 3: 1 — “Angalieni, namtuma mjumbe wangu, naye ataitengeneza njia mbele yangu; naye Bwana mnayemtafuta atalijilia hekalu lake ghafula; naam, yule mjumbe wa agano mnayemfurahia, angalieni, anaku-ja, asema Bwana wa majeshi.”

Aya hii hujulisha watu wawili, Bwana na mjumbe Wake. Katika lugha ya leo aya hii ingalisomwa kama ifu-atavyo: {2TG11: 17.3}

“Tazama, Namtuma mjumbe Wangu, yule mjumbe wa agano naye ataitengeneza njia mbele Yangu; naye Bwana mnayemtafuta na Mnayemfurahia atalijia hekalu Lake ghafla; Tazama, Atakuja, asema Bwana wa majeshi.”{2TG11: 17.4}

Aya ya 2-4 — “Lakini ni nani atakayestahimili siku ya kuja kwake? Au ni nani atakayesimama atakapooneka-na yeye? Kwa maana yeye ni mfano wa moto wa mtu asafishaye fedha, ni mfano wa sabuni ya mtu afuaye nguo; naye ataketi kama asafishaye fedha na kuitakasa, naye atawatakasa wana wa Lawi, atawasafisha kama dhahabu na fedha; nao watamtolea Bwana dhabihu katika haki. Wakati ule

17

ndipo dhabihu za Yuda na Yerusalemu zitakapopendeza mbele za Bwana, kama katika siku za kale, na kama katika miaka ya zamani.”

Kwa udhahiri aya hizi zinatabiri kwamba Bwana atamtuma nabii Eliya kabla ya siku ile iliyo kuu na ya kuo-gofya ya Bwana, kabla ya hukumu ya washiriki walio hai katika kanisa Lake kuanza, kabla ya mtengo wa “magugu” kutoka kwa “ngano,” “samaki” wabaya kutoka kwa wazuri. Wakati huo Yeye anawatakasa wana wa Lawi — ukasisi. Mungu anatuhakikishia kwamba kabla kazi hii kuanza, Atamtuma mjumbe Wake, mjumbe wa ahadi, nabii Eliya. {2TG11: 18.1}

Ufu. 18: 1-4 — “Baada ya hayo naliona malaika mwingine, akishuka kutoka mbinguni, mwenye mamlaka kuu; na nchi ikaangazwa kwa utukufu wake. Akalia kwa sauti kuu, akisema, Umeanguka, umeanguka Babeli ule mkuu; umekuwa maskani ya mashetani, na ngome ya kila roho mchafu, na ngome ya kila ndege mchafu mwenye kuchukiza; kwa kuwa mataifa yote wamekunywa mvinyo ya ghadhabu ya uasherati wake, na wafal-me wa nchi wamezini naye, na wafanya biashara wa nchi wamepata mali kwa nguvu za kiburi chake. Kisha nikasikia sauti nyingine kutoka mbinguni, ikisema, Tokeni kwake, enyi watu wangu, msishiriki dhambi zake, wala msipokee mapigo yake.”

Aya hizi zinaonyesha mtengo ambao utatukia katika mahali panapoitwa eti ulimwengu wa Kikristo. Ila tia alama kwamba malaika anatangaza anguko la Babeli katika wakati wa Kilio Kikuu cha malaika, katika wakati ambapo dunia inaangazwa na utukufu wa malaika. Kisha inakuwa kwamba watu wa Mungu kwa kweli wanait-wa watoke Babeli. {2TG11: 18.2}

18

Zaidi ya hayo, ili Mungu awaite watu Wake watoke Babeli kwa sababu ya dhambi zake, inamaanisha kwamba lazima Yeye awalete mahali ambapo hakuna dhambi, — ndani ya Kanisa Lake lililotakaswa, Ufalme Wake, ma-hali ambapo hamna dhambi, na ambapo haipo hatari ya mapigo. Kwa udhahiri, basi, utakaso wa Kanisa unatukia kwanza, na kisha watu Wake waliosalia wanaitwa kutoka Babeli. {2TG11: 19.1}

Kumbuka sasa, hivi ndio jinsi Ufalme utakavyokuja. {2TG11: 19.2}

“Kwa hiyo imetupasa kuyaangalia zaidi hayo yaliyosikiwa, tusije tukayakosa. Kwa maana ikiwa lile neno lili-lonenwa na malaika lilikuwa imara, na kila kosa na uasi ulipata ujira wa haki; sisi je! Tutapataje kupona, tusipojali wokovu mkuu namna hii;…”? Ebr. 2:1-3. {2TG11: 19.3}

19

ANDIKO LA SALA

Msiwe Wasikilizaji Wa Penye Miamba

Alasiri hii tutaanza kusoma kwenye ukurasa wa 46 wa Mafunzo ya Kristo Kwa Mifano: {2TG12: 20.1}

“Naye aliyepandwa penye miamba, huyo ndiye alisikiaye lile neno, akalipokea mara kwa furaha; lakini hana mizizi ndani yake, bali hudumu kwa muda. Ikitukia dhiki au udhia kwa ajili ya lile neno, mara huchukizwa. {2TG12: 20.2}

“Mbegu iliyopandwa penye miamba hupata kina kidogo cha mchanga. Mmea huota haraka, lakini mzizi hau-wezi kuupenya mwamba ili kupata lishe ya kudumisha ukuaji wake, na punde hunyauka. Wengi ambao hufanya madai ya dini ni wasikilizaji wa penye miamba. Kwa sababu mwamba ni msingi wa tabaka la dunia, ubinafsi wa moyo wa asili huwa msingi wa udongo wa shauku zao njema na matarajio yao. Kupenda ubinafsi hakujanyenyekezwa. Hawajauona uovu uliokidhiri wa dhambi, na moyo haujanyenyekezwa chini ya hisia ya hatia yake. Daraja hili linaweza kushawishiwa kwa urahisi, na kuonekana kama waongofu waangavu, lakini wanayo dini ya juujuu tu.”{2TG12: 20.3}

Lipo daraja la watu ambao ni wepesi sana kuuona Ukweli wa Sasa, lakini ambao, mara tu mateso, dhihaka, usumbufu na majaribu yanapoinuka, mara moja huikana misimamo yao. Ukweli hauna mzizi ndani ya kama ha-wa, na punde hunyauka kutoka kwa akili na mioyo yao. Hebu sasa tupige magoti na tuombe kwa ajili ya kina cha udongo mioyoni mwetu, ili tuweze kushikilia sana imani yetu, masadikisho yetu, katika hali yoyote. {2TG12: 20.4}

20

UFUNUO — NI NINI?

ANDIKO LA HOTUBA NA V. T. HOUTEFF

MCHUNGAJI WA WADAUDI WAADVENTISTA WA SABATO

SABATO, OKTOBA 18, 1947

HEKALU LA MLIMA KARMELI

WACO, TEXAS

Ili kuupokea Ufunuo, kitabu cha mwisho cha Bibilia, Yohana alichukuliwa mara mbili katika Roho. Ili kuona hili tutasoma Ufunuo 1: 10, na 4: 2. {2TG12: 21.1}

Ufu. 1:10 — “Nalikuwa katika Roho siku ya Bwana, na nikasikia sauti kuu nyuma yangu, kama sauti ya baragumu.”

Hii ni mara ya kwanza kwa Yohana katika Roho, na alipokuwa ndani Yake aliupokea Ufunuo sura ya 1, 2, na 3. {2TG12: 21.2}

Ufu. 4: 2 — “Na mara nalikuwa katika Roho: na tazama, kiti cha enzi kimewekwa mbinguni, na mmoja ameketi juu ya kile kiti.”

Hii ni mara ya pili ya Yohana katika Roho, wakati ambapo aliupokea Ufunuo sura ya 4 hadi 22. {2TG12: 21.3}

Aya tisa za kwanza za sura ya 1 zina utangulizi wa Yohana kwa kile kitabu, na ni muhtasari mfupi wa yale aliyoyaona. Aya zilizosalia za sura ya 1 zina utangulizi wa Bwana kwa Ufunuo, baada ya hapo katika sura ya 2 na ya 3 amepewa ujumbe maalum wa kupelekwa kwa yale makanisa saba. Haya yote ndio Yohana aliona wakati alipokuwa katika Roho mara ya kwanza. {2TG12: 21.4}

Sasa tunakuja kwa Ufunuo sura ya 4 na ya 5, tunasoma yale Yohana aliona mara yake ya pili katika Roho. {2TG12: 21.5}

21

Ufu. 4 — “Baada ya hayo naliona, na tazama, mlango ukafunguka mbinguni, na sauti ile ya kwanza nili-yoisikia kama sauti ya baragumu ikinena nami, ikisema, Panda hata huku, nami nitakuonyesha mambo am-bayo hayana budi kuwako baada ya hayo. Na mara nalikuwa katika Roho; na tazama, kiti cha enzi kimewekwa mbinguni na mmoja ameketi juu ya kile kiti; na yeye aliyeketi alionekana mithili ya jiwe la yaspi na akiki, na upinde wa mvua ulikizunguka kile kiti cha enzi, ukionekana mithili ya zumaridi. Na viti ishirini na vinne vilikizunguka kile kiti cha enzi, na juu ya vile viti naliona wazee ishirini na wanne, wameketi, wamevikwa mavazi meupe; na juu ya vichwa vyao walikuwa na taji za dhahabu. Na katika kile kiti cha enzi kunatoka umeme na sauti na ngurumo. Na taa saba za moto zilikiwaka mbele ya kile kiti cha enzi, ndizo Roho saba za Mungu. Na mbele ya kile kiti cha enzi kulikuwa na mfano wa bahari ya kioo, kama bilauri; na katikati ya kile kiti cha enzi, na pande zote za kile kiti, walikuwako wenye uhai wanne, wamejaa macho mbele na nyu-ma.

“Na huyo mwenye uhai wa kwanza alikuwa mfano wa simba, na mwenye uhai wa pili alikuwa mfano wa ndama, namwenye uhai wa tatu alikuwa na uso kama uso wa mwanadamu, na mwenye uhai wa nne alikuwa alikuwa mfano wa tai arukaye. Na hawa wenye uhai wanne kila mmoja alikuwa na mabawa sita; na pande zote na ndani wamejaa macho; wala hawapumziki mchana wala usiku, wakisema, Mtakatifu, Mtakatifu, Mtakatifu, Bwana Mungu Mwenyezi, aliyekuwako na aliyeko na atakayekuja. Na hao wenye uhai wanapompa yeye aketiye juu ya kile kiti cha enzi utukufu na heshima na shukrani, yeye aliye hai hata milele na milele, ndipo hao wazee ishirini na wanne huanguka mbele yake Yeye aketiye juu ya kile kiti cha enzi, nao humsujudia Yeye aliye hai hata milele na milele, nao huzitupa taji zao mbele ya kile kiti cha enzi, wakisema, Umestahili wewe, Bwana wetu na Mungu wetu kuupokea utukufu na heshima na uweza; kwa kuwa wewe ndiwe uliyeviumba vitu vyote, na

22

Kwa sababu ya mapenzi yako vilikuwako, navyo vikaumbwa.” {2TG12: 22.1}

Ufu. 5 — “Kisha nikaona katika mkono wa kuume wake yeye aliyeketi juu ya kile kiti cha enzi kitabu kilicho-andikwa ndani na nyuma, kimetiwa muhuri saba. Nikaona malaika mwenye nguvu akihubiri kwa sauti kuu, N’nani astahiliye kukifungua kitabu, na kuzivunja muhuri zake? Wala hapakuwa na mtu mbinguni, wala juu ya nchi, wala chini ya nchi, aliyeweza kukifungua hicho kitabu, wala kukitazama. Nami nikalia sana kwa kuwa hapakuonekana mtu astahiliye kukifungua hicho kitabu, wala kukitazama. Na mmojawapo wa wale wazee akaniambia, Usilie; tazama, Simba aliye wa kabila ya Yuda, Shina la Daudi, yeye ameshinda apate kukifungua kile kitabu, na zile muhuri zake saba.

“Kisha Nikaona, na tazama, katikati ya kile kiti cha enzi na wale wenye uhai wanne, na katikati ya wale wazee, Mwana-Kondoo amesimama alikuwa kana kwamba amechinjwa, mwenye pembe saba na macho saba, ambazo ni Roho saba za Mungu zilizotumwa katika dunia yote. Akaja akakitwaa kile kitabu katika mkono wa kuume wake Yeye aliyeketi juu ya kile kiti cha enzi. Hata alipokitwaa kile kitabu, hao wenye uhai wanne na wale wazee ishirini na wanne wakaanguka mbele ya Mwana-Kondoo, kila mmoja wao ana kinubi, na vitasa vya dhahabu vilivyojaa manukato, ambayo ni maombi ya watakatifu. Nao waimba wimbo mpya, wakisema, “Wastshili wewe kukitwaa hicho kitabu, na kuzifungua mihuri zake; kwa kuwa ulichinjwa, ukamnunulia Mungu kwa damu yako watu wa kila kabila, na lugha, na jamaa, na taifa; ukawafanya kuwa ufalme na makuhani kwa Mungu wetu, nao wanamiliki juu ya nchi. {2TG12: 23.1}

“Nikaona, nikasikia sauti ya malaika wengi pande zote za kile kiti cha enzi na za wale wenye uhai

23

na za wale wazee: na hesabu yao ilikuwa elfu kumi mara elfu kumi, na maelfu ya maelfu; wakisema kwa sauti kuu, “Astahili Mwana-Kondoo aliyechinjwa kuupokea uweza, na utajiri, na hekima, na nguvu, na heshima, na utukufu na baraka. Na kila kiumbe kilichoko mbinguni na juu ya nchi, na chini ya nchi, na kama vile vilivyo ba-harini, na vitu vyote vilivyomo ndani yake, nalivisikia vikisema, Baraka, na heshima, na utukufu na uweza una Yeye aketiye juu ya kiti cha enzi, na kwa Mwana-Kondoo hata milele na milele. Na wale wenye uhai wanne wakasema, Amina. Na wale wazee ishirini na wanne wakaanguka chini, wakamwabudu Yeye aishiye milele na milele.”{2TG12: 23.2}

Sura ya 4 na ya5, tunaona, zinasheheni eneo la tukio maalum lililosababisha Kitabu kufunguliwa. Kile kili-chotoka ndani ya Kitabu ni, kwa maana kamili, Ufunuo wa Yesu Kristo, wa Yule Ambaye alistahili kukifungua kile Kitabu. {2TG12: 24.1}

Hivyo ni kwamba “Ufunuo wa Yesu Kristo” huanza na sura ya sita na kuisha na sura ya mwisho ya Kitabu, sura ambazo ndani yake yameandikwa mambo ambayo kufunuliwa kwa ile mihuri saba ilifichua. Naam, Ufunuo unajumuisha mambo yaliyofungwa kwa mihuri saba. {2TG12: 24.2}

Ni wazi sasa kwamba Ni “Ufunuo wa Yesu Kristo aliyopewa na Mungu”; yaani, Mungu alimpa Yesu kile Kitabu. Yesu akakichukua, akaifungua mihuri ambayo kilikuwa kimefungwa nayo na kuyaweka wazi mambo ambayo hakuna mtu angaliweza kuyafichua isipokuwa Yeye. Mihuri Saba, kwa hivyo, hushughulikia “Ufunuo wote wa Yesu Kristo Aliyopewa na Mungu,” na unajumuisha mambo ambayo yalitoka ndani ya kile Kitabu. Ufunuo, zaidi ya hayo,

24

u katika sehemu saba, kwa sababu kila moja ya mihuri ilifichua sehemu fulani ya Ufunuo: Muhuri wa kwanza ulifichua mambo yaliyoandikwa katika sura ya sita, aya ya pili; Muhuri wa pili ulifichua mambo ya aya ya nne; Muhuri wa tatu ulifunua mambo ya aya ya tano na ya sita; Muhuri wa nne ulifichua mambo ya aya ya 7 na ya 8; Muhuri wa tano ulifunua mambo ya aya ya tisa hadi ya kumi na moja; Muhuri wa sita ulifichua mambo ya aya ya kumi na mbili hadi sura ya nane; Muhuri wa saba ulifichua mambo ya sura ya nane hadi ya ishirini na mbili, kwa jumla. Kwamba sura hizi zote ni endelezo la sura ya sita inaonekana kwa ukweli kwamba kila sura inaanza na kiunganishi “Na.” {2TG12: 24.3}

Ufunuo, basi, umegawanywa katika sehemu saba. Na kwa hivyo tunapozungumza juu ya Mihuri Saba, kwa uhalisia tunauzungumzia Ufunuo. {2TG12: 25.1}

Wa mwisho kwa mihuri, wa saba, umegawanywa katika migawo mingine saba, Baragumu Saba, ambazo huanza na sura ya nane, na dhahiri huisha pamoja na sura ya kumi na moja. {2TG12: 25.2}

Jambo la pili la kuzingatia ni tukio ambalo lilisababisha kile Kitabu kufunguliwa. Kwa ufahamu tayari, nimezalisha tena mchoro wa tukio hilo. Ninaweza kutaja kwamba nimekuwa mwangalifu sana kuuchora sawa-sawa vile Yohana anavyolielezea. {2TG12: 25.3}

25

Kwa ukosefu wa nafasi, hata hivyo, maelfu ya malaika kukizunguka kiti cha enzi wanakosa kwenye mchoro. Huu ndio mchoro hapa: {2TG12: 26.1}

MAMBO AMBAYO HAYANA BUDI KUWAKO “UPESI”

UFUNUO SURA YA NNE NA YA TANO

26

Ni tukio gani ambalo lilisababisha mihuri ya kile Kitabu kufunguliwa? — Ili kupata jibu kwa swali hili, kwanza tunapaswa kuzingatia washiriki katika mkutano. Hapo tunamwona Mmoja kwenye kiti cha enzi, kisha Mwana-Kondoo, kisha wazee, na maelfu ya malaika pande zote za kile kiti cha enzi, pia “wanyama” ambao wenyewe wanashuhudia kwamba wao ni wawakilishi wa waliokombolewa, kwa maana husema, “Kwa kuwa ulichinjwa, ukamnunulia Mungu kwa damu yako watu wa kila kabila, na lugha, na jamaa, na taifa.” Ufu. 5: 9. {2TG12: 27.1}

Ni nini kingine ambacho kusanyiko kama hili lingaliweza kuwakilisha isipokuwa Hukumu. Hapo tunamwona Jaji wa Haki, Wakili wetu mkuu, ameketi kwenye kile kiti cha enzi, kisha Mwana-Kondoo, na jopo la majaji ishirini na wanne, pia mashahidi malaika, na wanyama wanne wanaowakilisha waliokombolewa. Zaidi ya hayo, Ufunuo wenyewe unatangaza kwa mkazo kwamba tukio hilo ni Hukumu katika kikao, kwa maana unasema: “Mcheni Mungu, na kumtukuza; kwa maana saa ya hukumu Yake imekuja: Msujudieni yeye aliyezifanya mbingu na nchi na bahari na chemichemi za maji.” Ufu 14: 7. {2TG12: 27.2}

Nabii Danieli, pia, ambaye kitabu chake ni kikamilisho cha Ufunuo, alipewa picha ya Hukumu. Alimuona Mzee wa Siku ameketi kwenye kile kiti cha enzi, pia viti vya enzi ambavyo kwa udhahiri huketi wazee ishirini na wanne. Aliona pia maelfu ya malaika, na “Mmoja kama Mwana wa adamu”, Mwana-Kondoo, akaletwa mbele ya Mzee wa Siku. {2TG12: 27.3}

Katika ulinganisho wa unabii wa Danieli na Ufunuo wa Yohana unasimama kama ifuatavyo: {2TG12: 27.4}

27

Maono ya Danieli (Danieli 7) Maono ya Yohana (Ufunuo)

1. “Nikatazama hata viti vya enzi vikawekwa.” Dan. 7: 9. 1. “Kisha nikaona viti vya enzi.” Ufu 20: 4 {2TG12: 28.1}

2. “Na mmoja aliye Mzee wa Siku ameketi.” Dan. 7: 9. 2. “Na mmoja ameketi juu ya kile kiti cha enzi.” Ufu 4: 2. {2TG12: 28.2}

3. “Mto kama wa moto ukatoka ukapita mbele Yake.” Dan. 7:10. 3. “Kisha nikaona kitu kama mfano wa bahari ya kioo iliyochangamana na moto.” Ufu. 15: 2. {2TG12: 28.3}

4. “Mmoja aliye mfano wa Mwana wa adamu akaja… akamkaribia Mzee wa Siku, wakamleta karibu naye.” Dan. 7:13. 4. “Katikati ya kile kiti cha enzi na wale wenye uhai wanne… Mwan-Kondoo amesimama.” Ufu 5: 6. {2TG12: 28.4}

5. “Vitabu vikafunuliwa.” Dan. 7:10. 5. “Na vitabu vikafunguliwa.” Ufu. 20:12. {2TG12: 28.5}

6. “Maelfu elfu wakamtumikia, na elfu kumi mara elfu kumi wakasimama mbele Yake.” Dan. 7:10. 6. “Nikasikia sauti ya malaika wengi pande zote za kile kiti cha enzi… na hesabu yao ilikuwa elfu kumi mara elfu kumi, na maelfu ya maelfu.” Ufu 5:11. {2TG12: 28.6}

7. “Hukumu ikawekwa, na vitabu vikafunguliwa.” Dan. 7:10. 7. “Saa ya hukumu Yake imekuja.” “Kisha ni-kawaona wafu, wakubwa kwa wadogo, wamesimama mbele ya Mungu; na vitabu vikafunguliwa: na kitabu kingine kikafunguliwa, na ambacho ni cha uzima: na hao wafu wakahukumiwa katika mambo hayo yali-yoandikwa katika vile vitabu, sawasawa na matendo yao.” Ufu 20:12. {2TG12: 28.7}

28

Tofauti ya pekee, unaona, ni kwamba Danieli alionyeshwa Hukumu ikiwa ikiwekwa, ilhali Yohana aliiona katika kikao kamili. {2TG12: 29.1}

Ufunuo, zaidi ya hayo, katika aya zifuatazo tena na tena unajaribu kutufanya tuone kwamba hafla iliyoonye-shwa hapo ni Hukumu katika kikao: {2TG12: 29.2}

“Mcheni Mungu,na kumtukuza; kwa maana saa ya hukumu Yake imekuja.”{2TG12: 29.3}

“Kisha nikaona viti vya enzi,” anatangaza Yohana, “nao wakapewa hukumu.” Ufu. 20: 4. {2TG12: 29.4}

Yohana kwa kweli aliuandika kama unabii, lakini unapotukia kwa uhalisia basi chombo cha Mungu duniani, Roho ya Unabii Kanisani itatangaza kwamba tukio hilo kweli limetendeka. {2TG12: 29.5}

Kwa sababu kumbu kumbu za wote waliokufa na walio hai lazima zipitiwe na Jopo la Hukumu, Ujumbe wa Malaika wa Kwanza (Ufu. 14: 6), lazima utangazwe katika vipindi vyote viwili, katika kipindi cha

29

hukumu kwa wafu, na kwa kilio kikuu katika kipindi cha hukumu kwa walio hai. Utumizi wa moja kwa moja wa Ujumbe wa Malaika wa Kwanza, kwa hivyo, pia mwito wa kutoka Babeli, utatangazwa kwa kweli katika siku ambayo nchi itaangazwa kwa utukufu wa malaika. (Angalia Ufu. 18: 1-4). Ufunuo, kwa hivyo, utaeleweka vyema zaidi katika wakati wa hukumu kwa walio hai. {2TG12: 29.6}

Nuru ambayo sasa huangaza kwenye njia yetu ni ushahidi usio na shaka kwamba tunaujongea wakati wa hukumu kwa walio hai, wakati ambapo “atakapokuja Mwana wa Adamu katika utukufu wake, na malaika wa-takatifu wote pamoja naye, ndipo atakapoketi katika kiti cha utukufu wake: na mataifa yote watakusanyika mbele yake, naye atawabagua kama vile mchungaji awabaguavyo kondoo na mbuzi.” Mat. 25: 31-33. {2TG12: 30.1}

Sasa kwa sababu Ufunuo hufichua shughuli za Hukumu ya jamii yote ya wanadamu, na maadamu ilifunguli-wa na kile Kitabu kilichofungwa na mihuri saba, na pia kwa sababu Ufunuo, kama ulivyoonyeshwa awali, unajumuisha mambo ambayo yalikuwa katika Kitabu kilichofungwa mihuri, basi ni busara kwamba Ufunuo una-sheheni ramani fupi ya historia ya wanadamu tangu mwanzo hadi mwisho wa dunia. {2TG12: 30.2}

Yaliyomo ndani ya Mihuri Saba kwa hivyo huwafahamu wanadamu wote; na lazima yaanze na Adamu, mtu wa kwanza juu ya nchi. Ukweli huu unaonekana tena haswa kutoka kwa ukweli kwamba mambo ambayo mihuri mitano ya kwanza ilifichua yameshughulikiwa katika aya moja, mbili, au tatu mtawalia (ilhali mihuri miwili ya mwisho ambayo inasheheni mambo yanayoihusu Hukumu kwa walio hai, kwa watu ambao lazima wajue kwam-ba kesi zao ziko kwenye hukumu) ni mirefu sana: Kumbu kumbu ya mambo ambayo muhuri wa sita hufichua ni

30

aya 22 kwa urefu, na muhuri wa saba ni sura 15 kwa urefu. {2TG12: 30.3}

Mnaona, marafiki zangu, kwamba yale tulionayo katika uchambuzi huu sio nadharia, sio wazo la mtu bunifu la ki-njozi na lisiloaminika, ila ni Ukweli wote wa Mungu. Hii ni Bibilia kweli kweli, na ni funzo kama nini, pia! {2TG12: 31.1}

Vipi, basi, wewe na mimi tunawezaje kumudu kuruhusu wokovu wetu uponyoke kutoka kwa mkamato wetu? Je! Tunawezaje kuwa wasiojali na wasiokuwa na msimamo kwa maneno haya ya kicho katika historia yote ya mwanadamu? Je! Hatupaswi kujiandaa kukutana na Mungu wetu kwa amani? Je! Hatupaswi sasa kama wana-wali wenye busara kuvijaza vyombo vyetu kwa mafuta haya yenye kutoa nuru ili tuweze kuzijaza tena taa zetu? Au je! sisi kama wapumbavu tutaipuuza fursa yetu, na hivyo kuzuiwa kuwasili penye “mlango” kabla ufungwe dhidi yetu? Ni la kutisha kama nini hata wazo la kusikia Mwalimu kutoka ndani akisema, “Ondokeni kwangu, Sikuwajua ninyi kamwe.” {2TG12: 31.2}

Ni kwa sababu tumekuja kwa wakati wa kumkumbuka Mungu kama huu kwamba masomo haya kupitia gha-rama kubwa na kupitia kafara kuu, yanatawanywa kama majani ya vuli kote kote Laodekia. {2TG12: 31.3}

Kwa nini mtu yeyote aweze kujidanganya kuhusu uzima wa milele, uliovikwa taji ya furaha na shangwe? Mungu hukataza kwamba yeyote kati yetu asipatwe jinsi mfano huo huwawasilisha wanawali watano wap-umbavu. {2TG12: 31.4}

31

Jumuiya ya Wadaudi Waadventista wa Sabato

(Ushirika Huru Unaojumuisha Kanisa)

Mlima Karmeli, Waco, Texas

S.L.P. 23738, Waco, TX 76702

+ 1-254-855-9539

www.gadsda.com

info@gadsda.com

Gombo la 2, Namba 11, 12

Kimechapishwa nchini Marekani

32

>