fbpx

Gombo la 2021 Msimbo wa Nembo Nam 1-2-3

Cover for the first issue of the 2021 Symbolic Codes

Kwa Masilahi ya Dhehebu la SDA

“Kabila Kumi Na Mbili Waliotawanyika Ugenini”

Jarida hili ndogo limetiwa wakfu kujulisha habari na shughuli za matengenezo kwa waamini wa Ukweli wa Sasa; kujibu maswali kuhusiana na ujumbe wa kutiwa muhuri watu 144,000 (Ufu. 7:1-8) na umati mkubwa (Ufu. 7:9); kwa nabii za Isaya, Zekaria, Zefania, Mika, Hosea, Yoeli, Danieli, Ufunuo, Ezekieli, Yeremia, n.k., lakini kwa ukamilifu zaidi kwa vitabu vya kwanza vinane vilivyotajwa hapo juu; kwa mifano ya Kristo, kwa vivuli na nembo, na pia kwa maandishi ya Bi. E.G. White.

Hata hivyo, mgeni huyu wa kila robo mwaka anaahidi kujibu maswali kwa vifungu kama hivyo vya Maandiko jinsi tu ambavyo vimefunuliwa na Mungu na kutangazwa kwa mamlaka – yenye alama dhahiri ya ukweli. Kwa hivyo, ama atatoa jibu sahihi kwa maswali au sivyo akiri kutojua kwake kwa kusema “Sijui.

Lengo lake kuu ni kuufunua ukweli kwamba wakati umekuja Bwana audhihirishe uwezo Wake na kuliunganisha, na kulitakasa kanisa la Mungu – akiliita liamke kutoka kwa kitanda chake mavumbini na lijivike nguvu zake na zawadi ya mavazi yake mazuri, kwa maana “tokea sasa” hataingia ndani yako aliye najisi. (Isa. 52:1.) Kwa hivyo, anadai kwa udhahiri kwamba wajumbe wa “siku iliyo kuu na ya kutisha ya Bwana,” chini ya uangalizi wake, lazima watii kabisa matakwa, maagizo na ushauri wake wote ambao huwaletea mara kwa mara. Hatawafadhili wale wanaopuuza mamlaka yake matakatifu – kanisa linapaswa kuwa nuru kwa ulimwengu wote – zuri kama mwezi, – safi kama jua, na la kutisha kama jeshi lenye mabango. Isa. 62:1-7; Manabii na Wafalme, uk. 725.

Nembo zilizo kwa ukurasa wa jina la jarida ni nakala halisi ya Ufunuo, sura ya kumi na mbili na Tisa, na Isaya 7:21, ni nembo zinazofafanuliwa katika vitabu vyetu vinavyopatikana.

Mfariji huyu wa kila robo mwaka kwa furaha huwaita wa’S.D.A. ambao hufungua barua pepe zao au milango yao kukaribisha ziara yake. Hutoa kwa hiari wakati wake kuwahudumia wale wataokuwa warithi wa wokovu wala hakusanyi ada wala kutoza malipo kwa utumishi wake wa hisani. Huishi kwa zawadi za na sadaka za hiari – hamlemei mtu na huwafariji wote. Sala yake ya daima ni kwamba wateja wake wote wafanikiwe na kuwa na afya kama vile roho zao zifanikiwayo. (III Yohana 2.)

Eleza maswali yako kwa uwazi na dhahiri, ukitoa marejeo, na yatashughulikiwa mara tu zamu yayo kwa foleni inayosubiri itaruhusu.

Iwapo ungependa rafiki huyu aliyechapishwa aje nyumbani kwako siku zote, pia machapisho mengine bila fedha, tuma jina na anwani kwa info@gadsda.com au P.O. Box 23738, Waco, TX 76702.

Daudi Eliya Yezreeli

The 12 Tribes of Israel

Jan. – Feb. – Machi 2021 | Msimbo wa Nembo, Gombo 2021, Nam. 1, 2, 3 | Uk. 2 wa 28

Table Of Contents. Volume 2021 The Symbolic Code Nos. 4-5-6

Jan. – Feb. – Machi 2021 | Msimbo wa Nembo, Gombo 2021, Nam. 1, 2, 3 | Uk. 3 wa 28

DPPS And QESS Logo. Volume 2021 The Symbolic Code Nos. 4-5-6

Jan. – Feb. – Machi 2021 | Msimbo wa Nembo, Gombo 2021, Nam. 1, 2, 3 | Uk. 4 of 28

Advert Of Midweek Prayer Meeting. Volume 2021 The Symbolic Code Nos.
Historia Ya Shule Ya Watangulizi Uganda

Shule hii imeonyesha uweza wa Mungu kwa ndugu na dada zangu, jinsi ripoti ifuatayo itaonyesha.

Baada ya kugawanyika na Mt. Dale, washirika hapa Uganda tangu mwaka 2007, wakati baadhi waliamua kukomesha uhusiano na Mt. dale na wengine wakachagua kuendelea nao; tulifanya mipangilio ifuatayo:

Tukiwa na bidii ya kufanya kazi pamoja bega kwa bega na maagizo ya Mungu kuzuia kuzorota kwa maadili kulikokuwa kumekithiri kutuzunguka, tuliamua kwa neema ya Mungu kuanzisha shule chini ya majina SHULE YA MSINGI YA ULAWI WA MLIMA KARIMELI, chini ya kauli mbiu ELIMU YA KWELI, HUMFANZA MWANADAMU MKAMILIFU LEO NA MILELE. Na lengo la KUZALISHA URITHI WA WATU WENYE AKILI YA NGUVU SANA KWA MUNGU WETU.

Katika mkutano wa kwanza uliofanyika mwaka 2007, twamshukuru Mungu kwa sababu tulikuwa na wanafunzi kumi na wawili waliokuwa tayari kuanza. Mmoja wa washarika, Ndugu Ibrahim Sekabira, aliazimu kwa neema ya Mungu kufundisha katika shule hiyo. Shule ilianza na madarasa matatu na mwalimu mmoja tu ambaye alilipwa Dola 11 kama mshahara wake wa kila mwezi.

Madarasa yalikuwa ya msingi 1, 2, na 3. Wakati huo, shule ilikuwa ikiendeshwa nyumbani mwa Ndugu na Dada Walusimbi Fredie, na baadaye ikahamishiwa nyumbani mwa ndugu na dada Nsobya Steven.

Twamshukuru Mungu kwa sababu iliendeleza shughuli zake ingawa haikuwa imesajiliwa rasmi kwa kiwango cha kitaifa na hata bila uhusiano wowote ng’ambo maana mpasuko huo ulikuwa umetutenganisha na Mt. Dale.

Baada ya muda, tulimwajiri mwalimu wa pili, Dada Oliver Nakkazi, kumsaidia ndugu aliyekuwa amelemewa na jukumu kubwa. Dada huyu alipaswa kulipwa Dola 9 kama mshahara wake wa kila mwezi.

Ulipokuja mwaka 2009, Mungu alifanya uandalizi bora kwa shule hiyo wakati ndugu mmoja aitwaye Nsobya Steven alipochangia ardhi ya kujengwa majengo ya shule. Hii ilikuwa baraka kubwa kwa shule, na mipango ilianza mara moja kujenga

jengo la muda.

Baadaye Dada Oliver aliachishwa kazi ya kufundisha, na tukawaajiri walimu wengine watatu: Dada Martha Kabalwanyi, Ndugu Ibrahim Mpanga na Dada Specioza Ssekandi. Hao walifundisha kwa karibu miaka miwili tangu mwaka 2011. Kwa wakati huo, mzee wetu Dada Theopista Nankya alikuwa mhazini wa shule hiyo.

MAJENGO YA SHULE

Baada ya kupata ardhi hii, twamshukuru Mungu kwamba tuliweza kujenga jengo la muda lenye vyumba vitatu mbalimbali kukidhi madarasa tuliokuwa nayo. Jengo hili la muda hakika lilikuwa la muda kwa sababu mazulia ya hapa ya mafunjo yalivitenganisha.

Tulianza kulipanua jengo hili la muda mwaka baada ya mwaka kulingana na mahitaji yetu. Hili ndilo jengo la muda tuliloanza nalo;

Ulipokuja mwaka 2014 wakati ujumbe huu wa ajabu wa Kanisa la Saa ya 11 ulitujia, shule hiyo ilikuwa ikifanya kazi kati ya changamoto kadhaa na ukosefu wa habari kuhusu maswala maalum. Tulikuwa bado chini ya jengo lile lile la muda lililotumika kwa madarasa na kama mahali pa mikutano ya kanisa. Tulifanya warsha ya majuma mawili na Ndugu Maxwell Murunga na Ndugu Fidelis Mutale katika jengo lilo hilo la muda.

Baadaye tuliboresha hilo jengo tuliponunua mabati mapya na vigingi vya miti ili kujenga jengo thabiti. La kwanza lilikuwa katika hali mbaya iliyotishia afya, usalama wa wanafunzi, na hata utenda kazi wa walimu.

Katika mwaka 2015, tulikuwa tumeongeza madarasa na hata idadi ya wanafunzi shuleni. Tulikuwa na madarasa sita na wanafunzi 15 na walimu wanne.

Ilipofika mwaka 2016, walimu wawili waliajiriwa kuchukua nafasi ya wawili. Dada Annet Kusaasira aliajiriwa kuchukua nafasi ya Dada Martha na

Jan. – Feb. – Machi 2021 | Msimbo wa Nembo, Gombo 2021, Nam. 1, 2, 3 | Uk. 6 wa 28

Ndugu Kabugo Brian aliajiriwa kuchukua nafasi ya Dada Specioza Ssekandi. Katika mwaka huo, tulipomkaribisha Ndugu yetu David Owitti, pamoja na Ndugu Isaac Misiani, tuliendesha warsha ya siku saba katika jengo letu jipya la muda, na nyakati zingine tulikuwa tukikutana katika nyumba ya mhazini wa shule, haswa nyakati za mvua. Kwa wakati huo, tulianza kusikia kuhusu MPANGO WA USTAWI WA MIAKA MIWILI KWA UGANDA.

Baada ya warsha hiyo na Ndugu Owitti, mpango wa ustawi wa miaka miwili ulianzishwa. Washarika wote wa Uganda waliupokea kwa hamu kama jibu kutoka kwa Mungu wetu kuelekea vilio vyetu. Tumekuwa tukimlilia Yeye, haswa tukisihi kwa ajili ya majengo na ardhi ya kutosha kukidhi mahitaji ya shule na kanisa kwa ujumla.

MPANGO WA MAENDELEO YA MIAKA MIWILI

Mpangilio huu uliimarisha pakubwa imani yetu kwa Bwana. Mungu hakika anajua mahitaji ya watoto Wake, haswa kuwezesha kazi isonge mbele. Lililoonekana kuwa ndoto likawa uhalisi katika mwaka 2017. Wakati Baraza Kuu lilipoidhinisha mpango huo, jengo la fahari lilijengwa kwa shule ya Bwana hapa Uganda. Kuanzia mwanzo duni, kama tulivyoona kwa ripoti hii, Mungu alifanya muujiza mkubwa kwa kubuni mpango bora wa shule hii.

Hili ni jengo letu jipya, ambalo tunatumia kwa shule na ibada za kanisa wakati huu. Asifiwe Mungu wetu.

Ni ajabu hata kwa watu wote katika eneo hili kulingana na tulivyoanza. Hakuna aliyetarajia hili kutukia kwetu. Kwa kweli Mungu ameinua kiwango cha shule Yake.

Jina la shule Yake lilibadilishwa kutoka SHULE YA MSINGI YA ULAWI WA MLIMA KARIMELI kuwa SHULE YA WATANGULIZI UGANDA.

Shule hii hadi sasa imeweza kuandaa wanafunzi mbalimbali kufanya mitihani ya kitaifa –ambayo ilihitimisha elimu ya msingi

msingi katika nchi hii kwa miaka mitatu. Twamshukuru Mungu kwa sababu wanafunzi wamekuwa wakifanya vyema kwa kiwango cha kitaifa katika miaka hii yote mitatu. Hili pia limewashangaza watu wengi, lakini kwayote, tunamsifu Bwana kwa ufanisi huu. Shule nyingi hufanya mitihani, na wanafunzi wengine huishia kufeli, lakini shule hii ya Bwana, nataka kumshuhudia Yeye, haijawahi kuwa na mwanafunzi yeyote aliyefeli mitihani katika kiwango cha kitaifa katika miaka yote mitatu tumekuwa tukifuzu.

HALI YA SASA YA SHULE

Hivi sasa, mwaka 2021, tunashangilia katika Bwana. Shule iko katika jengo la fahari ambalo hutumika kwa malengo mawili, la madarasa na ukumbi wa ibada ya kanisa / mkutano.

Shule ina walimu wanne, mpishi mmoja, na mhazini.

Walimu wa sasa ni:

 1. Ndugu Ibrahim Sekabira akiwa mwalimu mkuu.
 2. Ndugu Kabugo Brian
 3. Ndugu Mpanga Ibrahim
 4. Dada Annet Kusaasira
 5. Dada Benah Nakyanzi akiwa mpishi
 6. Dada Nankya Teopista akiwa mhazini wa shule.

Hivi sasa tuna wanafunzi 33 shuleni. Bwana ametusaidia kushinda changamoto ya karo ya shule. Tumekuwa tukipitia changamoto hii tangu mwanzoni mwa mwaka wa shule 2007. Kamati ya Ufadhili wa Elimu ya Kanisa la Saa ya Kumi na Moja imetoa karo ya shule kwa wanafunzi wetu wengi. Hili limeiwezesha shule kukidhi mahitaji yake ya kila siku.

Bwana aendelee kuibariki Kamati Kuu Tekelezi inapoongoza na kubuni njia za kukuza shule za Mungu katika nchi zote.

Tuendelee kumtumaini Bwana, maana Yeye ndiye wa kutuwezesha tufike katika ufalme Wake unaokuja hivi karibuni.

Ripoti imekusanywa na kuandikwa na kaka Ibrahim Sekabira – Mwalimu mkuu wa shule.

Jan. – Feb. – Machi 2021 | Msimbo wa Nembo, Gombo 2021, Nam. 1, 2, 3 | Uk. 7 wa 28

Guarnteed prosperity And Security

ILIYOANGAZIWA

Huu ni ujumbe wa kibinafsi kwako jinsi ya kufanikiwa na kufurahia maisha kwa kipimo kamili. Ustawi na usalama hapa umehakikishiwa — sera ya bima ambayo haijui kikomo. Kwa hiyo, ninawahimiza hii, na tumaini kwamba utafurahia na kupata faida kwa hiyo. Hivi ndivyo inavyofanya kazi:

“Angalieni namtuma mjumbe wangu,naye ataitengeneza njia mbele yangu;naye Bwana mnayemtafuta atalijilia hekalu lake ghafula;naam,yule mjumbe wa agano mnayemfurahia,angalieni,anakuja,asema BWANA wa majeshi.” Mal. 3:1.

Ahadi hapa ni kwamba Bwana atamtuma mjumbe, na kama vile sura ya nne ya Malaki ni tu kuendelea kwa hadithi ya sura ya tatu, huko tunaambiwa kwama mjumbe ni Eliya wa mfano (Mal. 4:5), mmoja ambaye ni “atatengeneza yote” (Mat. 17:11) na Uvuvio kwa kuongeza baadaye, na kwa ujumbe maalum kwa ukasisi wa Waadventista wa Sabato anaonya:

“Unabii lazima utimie. Bwana asema: ‘Angalieni, nitawatumia Eliya nabii kabla haijaja ile siku iliyo kuu na ya kutisha ya Bwana.’ Mtu fulani atakuja katika roho na nguvu ya Eliya, na atakapoonekana, watu wataweza kusema: “Wewe ni mwenye bidii sana, hauyafasiri maandiko

kwa njia inayofaa. Acha nikuambie jinsi ya kufundisha ujumbe wako.” — “Shuhuda kwa Wachungaji,” uk. 475, 476.

Yapo mambo makuu mawili ya kuzingatia katika nukuu hizi: (1) kwamba ujumbe na mjumbe aliyetajwa hapa ni wa mwisho kabisa; (2) ya kwamba atavirejesha vitu vyote, (3) ya kwamba ipo hatari kwa wengine kujifanya wapumbavu kwa kuthubutu kumwambia jinsi ya kufundisha ujumbe wake — wakidhani kuitwaa nafasi ya Mungu!

Aya hii ya Malaki tatu, kama utakavyoona kwa urahisi, ilitimizwa kwa sehemu tu, kimfano, na Yohana Mbatizaji, na ya kwamba utimilifu wake wa uakisi sio tu karibu sasa ila kwamba mbali na ujio wa kwanza wa Kristo ndio muhimu zaidi. Hebu sasa tuone mbona ni muhimu zaidi:

Ahadi ni kwamba Bwana atamtuma mjumbe, mtu fulani mwenye ujumbe, na kwamba pamoja Nao huyo mjumbe ataitayarisha njia ya Bwana kulijia Hekalu Lake. Kusudi la Bwana kuja, utakumbuka, ni kulitakasa Hekalu Lake, kanisa, na haswa Walawi — ukasisi:

“Lakini ni nani atakayestahimili siku ya kuja kwake? Au ni nani atakayesimama atakapoonekana yeye? Kwa maana yeye ni mfano wa moto wa asafishaye fedha, ni mfano wa sabuni ya afuaye nguo; naye ataketi kama asafishaye

Jan. – Feb. – Machi 2021 | Msimbo wa Nembo, Gombo 2021, Nam. 1, 2, 3 | Uk. 8 wa 28

na aitakasaye fedha, naye atawatakasa wana wa Lawi, atawasafisha kama dhahabu na fedha nao watamtolea Bwana dhabihu katika haki.” Mal. 3:2, 3.

La, sio kabla ya kazi hii kufanywa kwa ukasisi ndipo wanaweza kutoa dhabihu zinazokubalika kwa Mungu, unaona.

Ni dhahiri kwamba sura hii ya Malaki iliandikwa haswa kwa ajili ya watu waaminifu wa Mungu kwa wakati huu, katka wakati ambapo kutakaswa kwa kanisa kutafanyika, wakati ambapo samaki wazuri watawekwa vyomboni na wabaya “kutupwa.” — Mat. 13:47, 48. Baada ya utakaso kufanyika, unakumbuka, kwamba

“Ndipo sadaka ya Yuda na Yerusalemu itakuwa ya kupendeza kwa Bwana, kama siku za kale, na kama ilivyokuwa zamani.” Mal. 3:4.

“Nami Nitawakaribieni ili kuhukumu, nami Nitakuwa shahidi mwepesi dhidi ya wachawi, na dhidi ya wazinzi, na juu yao waapao kwa uongo, na juu yao wamwoneao mwenye kuajiriwa kwa ajili ya mshahara wake, wamwoneao mjane na yatima, na kumpotosha mgeni asipate haki yake, wala hawaniogopi Mimi, asema Bwana wa majeshi. Kwa kuwa Mimi Bwana, Sina kigeugeu; ndiyo maana ninyi hamkuangamizwa enyi wana wa Yakobo. — Mal. 3:5, 6.

Hapa uvuvio huelezea jinsi hukumu ya Walio hai inavyoanza, jinsi utakaso wa patakatifu hapa duniani utakavyofanyika (Danieli 8:14). Na baada ya kufunua kutowajibika kwa watu Wake kwa ajili ya wahitaji miongoni mwao, na kujinufaisha kwa kuwatumia wengine wakati wowote iwezekanavyo, kisha anahakikishia tena kwamba Yeye si kigeugeu; ya kwamba yeye ni yule yule Mungu asiyekosea na mwenye haki; ya kwamba amri na maagizo Yake ya kale ni ya milele; ya kwamba Yeye hajayabadilisha; ya kwamba atavirejesha vitu vyote. Yeye, kama utakavyoona, hatimaye anaifikia taabu yenyewe, kisha Anawasihi watu Wake wapokee suluhisho Lake.

Yeye asema:

“Tokea siku za baba zenu mmegeuka upande mkayaacha maagizo Yangu, wala hamkuyashika. Nirudieni Mimi, Nami nitawarudia ninyi, asema Bwana wa Majeshi. 

Lakini ninyi mwasema, Turudi kwa namna gani?” Mal. 3:7.

Kwa sababu watu Wake bado hawaoni ni wapi wameyaacha maagizo Yake, Yeye haswa huonyesha wazi na mara moja anajitetea kuchukua hatua:

“Je, Mwanadamu atamwibia Mungu? Lakini ninyi mnaniibia Mimi. Lakini ninyi mwasema, Tumekuibia kwa namna gani? Mmeniibia zaka na dhabihu. Nanyi mmelaaniwa kwa laana: maana mnaniibia Mimi, naam taifa hili lote. Leteni zaka kamili ghalani, ili kiwemo chakula katika nyumba Yangu, Mkanijaribu kwa njia hiyo, asema Bwana wa majeshi, mjue kama Sitawafungulia madirisha ya mbinguni, na kuwamwagieni baraka, hata isiwepo nafasi ya kutosha au la.” Mal. 3:8-10.

Kirai, “naam taifa hili lote” linamwibia Mungu ni hivyo kwa sababu ujumbe wa zamani, “Hukumu ya Wafu, (ambao Dhehebu la Waadventista wa Sabato liliitwa haswa kuutangaza), sasa umepitwa na wakati jinsi ulivyo ujumbe wa gharika ya Nuhu, na kwa vile maafisa wa Dhehebu tayari wameukataa ujumbe wa Hukumu ya walio hai lakini bado wanakusanya zaka za watu, wao kama taifa (kama Dhehebu) wanamwibia Mungu.

Zipo kweli nyingi za thamani zilizo katika Neno la Mungu lakini ni Ukweli wa sasa ambao Kundi linahitaji sasa. (“Maandishi ya Awali,” uk. 63).

Kumbuka kwamba sio kwa Walawi, au mahali fulani au watu wengine ila katika ghala la Mungu ndio humo zaka na matoleo yanapaswa kuletwa. Na sio kwa sababu nyingine yoyote isipokuwa kwamba ghala Lake liweze kuwa na utajiri wa kutoa chakula cha kiroho, “chakula kwa wakati wake.” Maneno haya kwa udhahiri na kwa uhakika huonyesha kwamba tegemeo pekee ambalo ujumbe wa kutakaswa kwa kanisa unao kwa kuidhamini kazi yake ni zaka na sadaka kutoka kwa watu Wake waaminifu; kwamba hakuna njia nyingine yoyote ambayo ujumbe ungeweza kutolewa; ya kwamba hakuna njia nyingine yoyote ambayo gharama zingelipwa. Hii ndio sababu Mungu haruhusu chombo [kisahani] kupitishwa sasa katika mikutano yetu, njia yoyote ya kuchanga pesa, na kuvisambaza vitabu vyetu kila mahali kama majani ya vuli bila fedha na bila thamani kwa watu. Kwa maneno mengine, vitabu, wachungaji,

Jan. – Feb. – Machi 2021 | Msimbo wa Nembo, Gombo 2021, Nam. 1, 2, 3 | Uk. 9 wa 28

na watenda kazi wa Biblia — wale wanaouleta ujumbe wa sasa langoni pako, wanapaswa kulipwa kwa zaka na sadaka ambazo huingia katika ghala la Bwana. Mungu, kwa hivyo, huwaomba watu Wake waaminifu kuitikia mwito Wake kwa furaha na wakidhi hilo hitaji kikamilifu. Haombi hili tu kwa ustawi wa ghala Lake, bali kwa ustawi wa watu Wake pia.

Kwa nini watangaza ujumbe lazima waje langoni pako ili kukuletea ujumbe? — Kwa sababu, jinsi unavyojua tayari, wachungaji wengi wamefunga milango ya kanisa na akili na mioyo ya walei dhidi ya ujumbe wa leo wa Bwana. Hili wametenda kwa kiwango kikubwa kuliko jinsi makuhani walivyofanya katika siku za Kristo. Bwana zamani sana katika wakati wa Yeremia aliona kimbele kwamba malaika (ukasisi) wa kanisa la Laodekia angefanya jambo hili ovu dhidi Yake na watu Wake ili kuwadumisha milele Walaodekia katika udanganyifu wao wa kibinafsi. Akizungumzia kutawanyika kwa Israeli ya kale kati ya mataifa, na kukusanywa kwa Israeli ya uakisi, katika sura ya kumi na sita ya unabii wa Yeremia Uvuvio hufafanua hivi:

“Tazama, Nitatuma watu kuwaita wavuvi wengi, asema Bwana, nao watawavua, na baada ya hayo Nitatuma watu kuwaita wawindaji wengi, nao watawawinda watoke katika kila mlima, na kila kilima, na pango za majabali.” (Yer. 16:16.)

Hapa unaambiwa wazi wazi kwamba katika wakati wa kukusanywa watumwa wa Mungu wanalazimika kwanza kuwavua watu Wake, kisha wawawinde. Kwa kuwa mawasiliano yetu ya kwanza nao yamekuwa kwa njia ya vitabu, hivyo, lazima iwe kuwavua. Ni hakika hivyo, pia, kwa sababu jinsi vinapotawanywa kila mahali kama majani ya vuli, samaki huja kuvichunguza, hupata ni vizuri kwa chakula, huuma na kunaswa, kwa mfano. Sasa, hata hivyo, tuko katika kipindi cha uwindaji, na tumeanza kuwawinda, iwe wako mjini au kijijini, katika maeneo rahisi kufikia, au katika maeneo magumu kufikia. Popote pale wanapoishi, lazima wawindwe, ingawa haitakuwa kazi rahisi sana kunasa nyumbani kitu kama Waadventista 300,000 au zaidi waliotawanyika nchini Marekani pekee, mbali na 500,000 au zaidi waliotawanyika katika nchi za kigeni. Hii unaona ni kazi kubwa ya gharama kubwa inayohitaji wawindaji wengi na magari ya bei ghali (ya dhamani ya chini

hayawezi kuhimili hiyo kazi), yanayokwenda mamia ya maelfu ya maili na kuhitaji mapipa mengi ya petroli na oili. Hii sio kazi ndogo, kwa ulinganisho haijawahi kuwapo kazi sawa na hii, na hivyo itachukua nguvu ya umoja wa kila mwamini wa Ukweli wa sasa kufanya yaendelee kwenda na kuiwezesha kazi ifanyike ili tuweze hivi karibuni kwenda katika nchi ya Utukufu.

Naam, ni dhamana na kazi kubwa ikiwa na ahadi kubwa inayohitaji mamia kwa maelfu ya dola nyingi na watu wote wenye afya walio na ari ambao Yeye aweza kupata ili wawinde mamia kwa maelfu ya Waadventista wa Sabato “katika pango za majabali” kote duniani. Kusema jukumu kubwa sana hakufafanui mzigo huo, ila kwa udhahiri jinsi mchana ulivyo ni ukweli wa maana, ya kwamba hatuwezi kushindwa, na ya kwamba watu Wake watauitikia ujumbe na kuja kwa msaada wa Bwana dhidi ya wenye nguvu. Na tunastahili kushukuru sana kwamba kila mmoja amepewa pendeleo na fursa kwa njia moja au nyingine kushiriki “Vema, mtumwa mwema na mwaminifu.”

Katika nuru ya Ukweli uliofunuliwa unaona sasa wazi kwamba Mungu hupokea tu kile ambacho watu Wake wanaoipenda Kweli na wanaoutafuta Ufalme hutoa kwa hiari na kwa ukarimu. Yeye huchukia zawadi zinazopatikana kwa kuomba-omba, kushinikiza sana, na kufanya kampeni. Yeye hutoa changamoto kwa watu Wake wakamjaribu, sasa katika wakati wa kukusanywa, walete kwa moyo zaka na sadaka zao katika ghala Lake la Hukumu ya Walio Hai na waone kama Yeye hatawafungulia madirisha ya Mbinguni na kuwamwagia baraka hata isiwepo nafasi ya kutosha. Kisha Anahakikishia tena:

“Nami kwa ajili yenu Nitamkemea yeye alaye, wala hataharibu mazao ya ardhi yenu; wala mzabibu wenu hautapukutisha katika mashamba, asema Bwana wa majeshi. Na mataifa yote yatawaiteni heri: maana mtakuwa nchi ya kupendeza sana, asema Bwana wa Majeshi.” (Mal. 3:11, 12.)

Sasa wakati umekuja wa Bwana kuudhihirisha uwezo Wake, yeyote anayetaka mafanikio na kujulikana anaweza kupata,

“Kwa maana wakati umefika wa hukumu kuanza katika nyumba ya Mungu: na ikianza

Jan. – Feb. – Machi 2021 | Msimbo wa Nembo, Gombo 2021, Nam. 1, 2, 3 | Uk. 10  wa 28

School Of The Prophets Advert Of The Symbolic Code 2021 Nos. 4-5-6

kwetu sisi, mwisho wao wasioitii injili ya Mungu utakuwaje?” (1 Pet. 4:17.)

Ingawa tunaweza kuwa katika tabaka ambalo maneno yafuatayo huelezea, bado tunaweza kurudi Kwake na Atatusamehe na kuyafumbua macho yetu ili tuweze kuona sasa kwamba ipo tofauti kati ya yeye anayemtumikia Mungu na yeye Asiyemtumikia:

“Maneno yenu yamekuwa magumu juu Yangu, asema Bwana. Lakini ninyi mwasema, tumesema maneno juu Yako kwa namna gani? Mmesema, kumtumikia Mungu hakuna faida: na tumepata faida gani kuyashika maagizo Yake, na kwa kwenda kwa huzuni mbele ya Bwana wa majeshi? Na sasa twasema kwamba wenye kiburi ndio walio heri; naam, watendao uovu ndio wajengwao; naam, wamjaribuo Mungu ndio waponywao.” (Mal. 3:13-15.)

“Ndipo wale waliomcha Bwana waliposemezana wao kwa wao: naye Bwana akasikiliza, akasikia, na kitabu cha ukumbusho kikaandikwa mbele Yake kwa ajili ya hao waliomcha Bwana, na kulitafakari jina Lake. Nao watakuwa Wangu, asema Bwana wa Majeshi, katika siku ile niifanyazo vito Vyangu; nami Nitawaachilia, kama vile mtu amwachiliavyo mwanawe mwenyewe amtumikiaye. Ndipo mtakaporudi, nanyi mtapambanua kati ya mwenye haki na mwovu, na kati ya yeye amtumikiaye Mungu na yeye Asiyemtumikia.” (Mal. 3:16-18.)

Baada ya kumrudia Mungu na kuonja uzoefu huu mpya na Bwana, watu Wake waaminifu wanatamani kukutana pamoja na kuzungumza baraka zao wao kwa wao. Wakikumbuka furaha yao ya moyoni, na hamu yao ya kuueneza wema Wake mmoja kwa mwingine, Anaahidi kuandika kitabu cha ukumbusho wa milele.

Tunaweza sasa hakika kuzishika ahadi za Mungu na kuzifanya kuwa zetu. Ni pendeleo na fursa iliyoje sasa! Angalieni na mwone tofauti kati ya mbinu ya Mungu ya kuidhamini kazi Yake, na mfumo wa Kirumi ambao sasa unaendelezwa na kanisa: kupitisha kisahani [chombo], hotuba zenye nguvu, Siku Kubwa, Siku ya Vitabu, shinikizo kubwa, kampeni, kuuza, kunadi, Kukusanya Mavuno,

sadaka za siku ya kuzaliwa, vining’inizo vya mti wa Krismasi, kupima uzani wa watoto, mauzo ya Dorkasi, fedha za uwekezaji, na yale tusiyotakiwa kufanya! Kwa vile hakuna mojawapo wa mibinyo hii ni ya Kibiblia, na kwa vile yote ni ya asili ya Wapagani na kulaaniwa na Maandiko, haziwezi kutambuliwa kama sadaka za hiari. Chunguza uone.

Badala ya kutunza Sabato siku hiyo kutumiwa kuchangisha fedha, na badala ya nyumba ya ibada, kanisa hugeuzwa kuwa pango la wezi — chukizo kwa waangalizi, na linalovunja moyo sana kwa mshiriki kumwalika rafiki au jirani katika ibada ya kanisa. Je! Yupo yeyote anayestaajabu kwamba Mungu sasa hawaleti wengi kanisani (“Shuhuda,” Gombo la 6, uk. 371)?

Lilikuwa jambo la namna hii lililomwamsha Luther kuchukua hatua alipowaona makasisi [mapadre] wanaishi katika anasa kwa kuzitumia dhamiri za watu na kuwafanya maskini wawe hoi hohe hahe. Ibada ya kweli na mpango wa Mungu wa kuidhamini hiyo kazi lazima sasa urejeshwe.

Iwapo upo uamsho na matengenezo yanayohitajika katika safu yoyote hakika yanahitajika katika safu hii, na hakuna yeyote atakosa kushiriki kwayo ikiwa atalizingatia Neno la Mungu na iwapo atakataa kufuata machukizo yaliyotajwa hapo juu.

Ujumbe utafikilia kila nyumba ya Mwadventista wa Sabato na “hukumu katika nyumba ya Mungu” (1 Pet. 4:17) itaanza; kwa hivyo hakuna wakati wa kupoteza. Mambo haya yanapaswa sasa “kushughulisha akili yote, umakini wote.”

Sasa katika siku ya urejesho, Ndugu, Dada, Mungu anakuita uamke kwa ombi Lake:

“Piga kelele, usiache, paza sauti yako kama tarumbeta, uwahubiri watu Wangu kosa lao, na nyumba ya Yakobo dhambi zao.” (Isa. 58:1.)

Uwe mpole, lakini kwa vyovyote uisikitikie dhambi ya mdhambi na usijaribu kufunika dhambi. Kwa ajili yako mwenyewe, na kwa ajili ya maisha ya washarika yaache machukizo na uipokee alama ya ukombozi wa Mungu kutoka kwa silaha za kuchinjia za malaika. Soma Ezekieli tisa na Isa. 66:15-17, 19, 20.

Sauti ya Mungu
Barua ya Yezreeli Namba 9

Jan. – Feb. – Machi 2021 | Msimbo wa Nembo, Gombo 2021, Nam. 1, 2, 3 | Uk. 12  wa 28

Shuhuda

Wapendwa Kaka na Dada,

Nina langu ni Dada Dyenne Vreds, natoka Suriname. Nina wana watatu wa kupendeza Yoeli, Yonathani, na Yesse. Nitashuhudia kwa ufupi nilivyokutana na Ukweli wa Sasa na jinsi nimepata uzoefu wake.

Takriban miaka saba iliyopita, naliwasiliana na kina kaka na dada wa Kanisa la Saa ya 11 (Ndugu Iwan Kortram, Ndugu Lloyd van Niel, Dada Selma van Niel, Dada Phili van Niel, na Dada Helga Kortram). Nalikuwa nikijiunga na masomo ya mtandaoni na mikutano ya maombi. Sikujitolea wakati huo, lakini kwa namna fulani nalikuwa nimeshawishika kwamba ujumbe huu ulikuwa kweli.

Ilikuwa katika mwaka 2015 ambapo Ndugu Lennox Sam alikuja Suriname kwa mafunzo. Tulikuwa katika kundi la wanafamilia 25 waliokusanyika nyumbani kwa amu yangu. Ndugu Sam aliyafafanua maandiko vizuri sana. Aliyawasilisha kwa njia wazi, changamfu, na ya furaha ya kwamba hatukutaka yaishe. Alikuwa na bado ni mwalimu mzuri, pia mpole, wa kirafiki, na wa kuelewa. Siku hiyo sote tulibarikiwa na mafunzo na uwepo wake. Sote tulishawishika kwamba Mungu alimtuma, na sote tulitaka kujua zaidi kuhusu ukweli huu wa sasa.

Mwaka mmoja baada ya Ndugu Sam kuzuru Suriname, nalikuwa na matatizo ya kiafya, ukosefu wa kupumzika, mfadhaiko, na kufanya kazi kupita kiasi ilikuwa chanzo, kwa hivyo naliacha mojawapo wa kazi zangu. Naliendelea kufanya kazi, lakini hali ilizidi kuwa mbaya. Afya yangu ilikuwa hatarini, kwa hivyo ilibidi niache ile kazi nyingine na niitunze afya yangu. Dada Helga na Ndugu Iwan walinipa msaada. Nalifanya “Tiba ya Utumbo Mpana kutumia Maji.” Baada ya matibabu ya siku 10, utumbo wangu mdogo ulitakaswa katika kliniki yao. Walinisaidia sana na wakanipa ushauri mzuri kuhusu lishe yenye afya. Walinisimulia pia kuhusu ujumbe wa afya, ambao ni mada muhimu katika Ukweli huu wa Sasa. Naliponywa, na namshukuru Bwana kwa uponyaji wangu kwa msaada wa hawa ndugu na dada wapendwa walionisaidia katika mchakato huo wote.

Miaka ilipita, na bado, sikujifunza mwenyewe Ukweli huu wa Sasa vya kutosha. Hata ilifika hatua nikaanza kutilia shaka iwapo ujumbe wa Fimbo ya Mchungaji ulikuwa Ukweli wa Sasa, kwa sababu tu sikuelewa mada

fulani, ambazo zilinifanya niutilie shaka wote. Pia nalimwomba Bwana kwa bidii na kumuuliza anisadikishe tena. Nalimwomba pia iwapo Angewafanya washarika wote wa familia yangu, ambao pia waliujua ukweli huu, wauamini na kujifunza zaidi. Mungu alimtumia Ndugu Iwan, Ndugu Lloyd na Dada Helga. Mara moja kwa juma, walikuja nyumbani mwetu kutoa mafunzo ya Biblia. Roho Mtakatifu alikuwa anatenda kazi Yake. Na tukaanza kujisomea zaidi.

Mfululizo wa Magombo na Trakti za Fimbo ya Mchungaji “ na “Mfululizo wa Msimbo wa Nembo wa Fimbo ya Mchungaji” wa Ndugu V.T. Houteff una kurasa nyingi. Nalipokuwa nikiyatazama [magombo], nalihisi kwamba kamwe singeweza kusoma yote kabla ya kurudi kwa Kristo. Lakini asante Mungu kwa kunisaidia kujisomea mwenyewe. Twamshukuru pia kwa mafunzo ya Kidachi kwenye mtandao kutoka Ndugu Lloyd van Niel na vikundi vya kujifunza tulivyokuwa navyo kwenye mtandao Sehemu ya Suriname na Uholanzi na kikundi cha kusoma ambamo tunasoma pamoja Fimbo ya Mchungaji.

Ilikuwa pia baraka wakati Ndugu Jerry Cox alikuja Suriname katika mwaka 2018 kwa wasilisho la mafunzo ya majuma 2. Mafunzo hayo, ambayo yalikusudiwa waamini wa saa ya 9 wapate kujua zaidi kuhusu Ukweli wa Sasa, pia yalinisaidia kuelewa mambo fulani vyema, maswali mengi niliyokuwa nayo yakajibiwa. Namshukuru Bwana kwa hayo pia.

Namshukuru Bwana kwa uvumilivu Wake na kuyajibu maombi yangu yote kwa sababu nafurahia kusoma katika Fimbo ya Mchungaji na kuidurusu mwenyewe. Pamoja na mafunzo ya Ndugu Sam kwenye mtandao, na mafunzo mengine yote mtandaoni, nazielewa nabii na maandishi yote vyema zaidi. Hunipa furaha na amani moyoni mwangu na pia kunifariji katika nyakati ngumu.

Jisomee Ukweli wa Sasa na chini ya uongozi wa Roho Mtakatifu. Bwana atayajibu maswali mengi, na nabii zitafafanuliwa. Sijasoma yote, bali namshukuru Mungu kwa yale nimesoma hadi sasa.

Ninashukuru sana kwa kaka na dada wote ambao walinisaidia na sisi sote kuelewa na kuufafanua Ukweli wa Sasa. Na naomba kwamba kila mtu ambaye atakutana na Ukweli huu wa

Jan. – Feb. – Machi 2021 | Msimbo wa Nembo, Gombo 2021, Nam. 1, 2, 3 | Uk. 13  wa 28

Sasa atabarikiwa. Na ya kwamba tutaishi kwa ukweli huu atabarikiwa. Na ya kwamba tutaishi kwa ukweli huu ili sisi sote tujiandae kwa ajili na kuwa katika Ufalme wa Mungu unaokuja hivi karibuni! Mungu awabariki ninyi nyote!

Dada Dyenne Vreds,
Nusu-Mviringo ya Magharibi, Suriname, Lelydorp.

HISTORIA YA UKWELI WA SASA – ST. LUCIA. W.I.

Hamna awazaye kuwazuia wateule wasiupokee Ukweli wa Sasa

Ukweli wa sasa ulinijia, na Katibu wa Waco (2500) aliniomba niutupe alipokuwa akimdunisha aliyeutuma, Ndugu Lennox Sam. Namshukuru Mungu haikuwa nia yangu kuyatupilia mbali mambo kabla kuyakagua. Haukuwa wakati wangu kula hii siagi na asali, kwa hivyo kompyuta yangu haingecheza hizo DVD.

Kwa miaka mitatu, nilikitunza kifurushi hicho. Katika wakati huo, nalitembelewa mara tatu kwa ujumla, kila juma na wachungaji wawili kutoka Makao Makuu ya Waco. Nilijadili na kuwaelezea yote niliyokuwa nayo, lakini Bwana alikiweka kifurushi hicho kikiwa kimefichwa nyumbani mwangu. Kamwe sikukumbuka lolote kuhusu hizo DVD.

Ee, Lisifuni Jina Lake Takatifu, wakati mwafaka ulikuwa umekuja, nikanunua kicheza DVD kisha bila kujua kilichokuwa katika DVD hizi, nalianza kula uhondo, sikuweza kukoma kuzicheza maana maudhui yake yalikuwa matamu na ya kweli. Baada ya kuzicheza kama mara kumi, ilibidi nimtafute Ndugu Sam, kumhoji, na hapa nipo leo, bado nashangilia na kula uhondo wa Ukweli wa Sasa wa kizazi changu.

Ni kama karibu kufa na kurejeshwa kuwa hai. Wakati nilipokea Ukweli kutoka kwa Ukasisi wa Mganda wa Kutikiswa, yalikuwa marudio ya yaliyotokea nilipokuwa Mwaadventista wa Sabato. Yalinikumbusha kujitolea kwangu tangu mwanzoni kwamba “bidii niliyokuwa nayo ulimwenguni kabla ya kukutana na Yesu, nitakuwa nayo na zaidi kwa kazi ya Mungu katika safari yangu ya Mkristo.”

Katika mwaka 2013 niliposikia kwamba itakuwapo warsha barani Afrika, naliomba iwepo moja pia St. Lucia, nayo hakika ilianzisha safari ya Ukweli wa sasa kisiwani humo. Ilinilazimu kuzuru na kumwalika kila Mdaudi kisiwani humo ambaye

ningeweza kumfikia, wote waamilifu na wasiofanya kazi; ni uzoefu ulioje kukutana na Wadaudi wengi wasiofanya kazi ambao kamwe sikuwajua hapo awali.

Warsha hiyo ilikuwa baraka, haswa kwangu, Ndugu Annius Jn. Marie na Dada Patricia Verpret, walisafiri kutoka Martinique ili wajifunze zaidi Ukweli moja kwa moja kutoka kwa Ndugu Sam.

Ndugu Annius anashuhudia kama ifuatavyo: “Nalikuwa Mwadventista mwakani 2008, na nikajulishwa ujumbe wa Fimbo mwakani 2010 nalijifunza kwa kukatiza-katiza hadi mwakani 2013 wakati Ndugu Sam alikuja St. Lucia. Baada ya Ndugu Sam kuondoka St. Lucia, niliota ndoto, na katika ile ndoto, sauti ilinambia yale mtu huyu anasema ni Ukweli, na tangu hapo, nalisadikishwa kwamba huu ni Ukweli. Kati ya wote katika wilaya yangu, mimi pekee ndiye niliyeupokea.”

Tumekuwa na upinzani mwingi katika kipindi cha miaka saba iliyopita. Wengi wamekuja na kwenda jinsi tunavyojua kwamba Ukweli haujawahi kuwavutia walio wengi. Hata hivyo, hadi sasa, sisi wanne wamekita mizizi kikamilifu, na kadi za usharika. Ndugu Annius Jn. Marie, Ndugu Simon Cox na malkia wake Shemida Cox nami Ndugu Jerry Cox. kama “samaki huja kuvichunguza, hupata ni vizuri kwa chakula, huuma na kunaswa, kwa mfano. {JL9: 5.2}”

Kaka Jerry Cox

Isaiah 2:22. Volume 2021 The Symbolic Code Nos. 1-2-3. First Quarter

Jan. – Feb. – Machi 2021 | Msimbo wa Nembo, Gombo 2021, Nam. 1, 2, 3 | Uk. 14  wa 28

Salamu katika Yesu Kristo, Kina Kaka, na Dada zangu,

Namshukuru Mungu kwa ujumbe wa Fimbo ya Mchungaji, ambao hujumuisha mfululizo wa kanuni ambazo watu wanapaswa kujua ili waingie katika Ufalme wa Mungu. Naliupokea ujumbe huu huko Haiti katika mwaka 2006 kutoka kwa Dada aliyetoka Merekani. Nalifurahi kuusikia ujumbe huu katika kila mkutano, na kadiri muda ulivyoendelea kupita, nilisoma kwa bidii trakti zote mbali mbali za mfukoni nilizokuwa nazo. Maswali kadhaa yalinijia akilini nilipokuwa nikisoma, lakini mengi yalishughulikiwa bila kuniridhisha nilipoyauliza.

Katika mwaka 2008 nalisafiri kwenda Chile nikiwa na trakti zote za mfukoni nilizokuwa nazo na nikasimama dhidi ya magumu yote nikizisoma na kuzisoma tena hadi nilipokutana na Dada Patricia Verpret, ambaye nilianza kujifunza naye. Baada ya mwaka au miwili, aliwasilisha kwangu Ukweli kuhusu Mganda wa Kutikiswa ulioletwa na Ndugu Lennox Sam, wakati huo nilianza kupata majibu kwa maswali yote niliyokuwa nayo.

Kwa miaka mingi nalikuwa nikimshukuru Mungu kwa baraka Zake zote. Sasa nasonga mbele katika ujumbe wa Ukweli wa Sasa. Ninawasilisha Fimbo ya Mchungaji kwa kina Ndugu na Dada ambao hawakuujua ujumbe huo. Sasa tunazo familia tatu na Dada mmoja wanaojifunza ujumbe wa Ukweli wa Sasa na kulidhamini Kanisa la Saa ya 11 kupitia zaka na sadaka. Najua kwamba, jinsi ambavyo uvuvio husema, vito vingi vinavyopatikana katika Kanisa la saa ya 9 lazima vikusanywe, na Bwana, katika Kanisa la saa ya 11. Mungu anasubiri ushirikiano wetu kuvileta.

Nalibariki Jina la Bwana kwa sababu Yeye ndiye Bwana na Muasisi wa ulimwengu wote, na Yeye siku zote anayo mipango ya kuwaokoa watoto Wake, jina Lake lihimidiwe!

Kaka. Jean Edvard Louis,

Santiago, Chile

MWENDO WOTE MWOKOZI WANGU ALINIONGOZA

KIPINDI CHA KIMORAVIA

Nalizaliwa na kulelewa katika familia iliyohudhuria Kanisa la Kimoravia, na haikuwa mpaka mamangu,  ambaye alikuwa mwamini mwaminifu, alienda kupumzika kaburini mwake ya kwamba Bwana alituongoza kutoka katika Kanisa la Jumapili

moja kwa moja hadi katika ujumbe wa Fimbo ya Mchungaji Rod. Kabla ya tukio hili, nalikuwa mwamini mlipa zaka mwaminifu nikishiriki na wanangu kila shughuli iliyofanyika katika Kanisa hilo la kutunza Jumapili. Hata hivyo, sikuridhika na nikapata kwamba mikutano yao ilikuwa zaidi na zaidi mikutano ya kijamii, na hakika hatukuwa tunakua kiroho.

KIPINDI KATIKA DAVIDIA

Bwana katika Majaliwa Yake alikuwa tayari amemweka Dada ambaye alikuwa m’S.D.A. katika familia yetu. Tulipojiuliza ni lini tutamwona tena mama yetu mpendwa, majibu yalitoka katika Biblia. Hili lilisababisha mafunzo ya Biblia na Ndugu Mdaudi, na kati ya watoto sita, wanne kati yetu tulikuwa washarika wa Kituo cha Mlima Karmeli, Mt. Dale, mwaka 1998. Tulipitia dhoruba zote za mada zenye utata, ambazo bado zinawakanganya wengine leo, lakini Bwana alitushikilia kwa nguvu kwa lile tulilolijua lililkuwa Ukweli wa Sasa

KIPINDI CHA KANISA LA SAA YA KUMI NA MOJA

Katika mwaka 2015, Bwana alitupata tunastahiki kupewa uelewa wa Ukweli endelevu. Ujumbe wa Fimbo ya Mchungaji isiyotiwa unajisi bila makapi ya utungwaji wa kibinadamu ndio ninaojilisha hata leo.

Bwana aendelee kutuongoza kwenye Njia ya Kifalme hadi katika Ufalme Wake, maana Yeye hakika ajua jinsi ya kuokoa.

Dada. Phili Kortram van Niel

Suriname

WA UJASIRI WENYE USHUJAA

Sifa kwa Bwana na Mwokozi wetu, Ambaye ametumiminia upande huu kwa wingi na baraka Zake sisizokoma! Naandika mistari hii michache kuwaletea habari kutokea Eneo la Lumakanda /Eldoret, Kenya. Mabwana kazi wa Baraza la mtaa wamewaka hasira na wanawatenga na kanisa waamini wa Fimbo ya Mchungaji. Likiwa msingi wa mwamba wa lango la Ukweli wa Sasa ndani ya Kenya, Baraza la mtaa la Kaskazini-Magharibi watu wana hofu kwamba hivi karibuni chachu ‘yenye sumu’ ya ujumbe itayachachisha makanisa yao kila mahali.

Ndugu Gilbert na Ndugu Lumumba tayari mara kadhaa wameshtakiwa mbele ya

Jan. – Feb. – Machi 2021 | Msimbo wa Nembo, Gombo 2021, Nam. 1, 2, 3 | Uk. 15  wa 28

polisi mikutano ya baraza la kanisa kujibu mashtaka ya uonevu kutoka kwa Wazee dhidi yao. Lakini, katika matukio hayo yote, Mungu amewajalia fadhila na wanadamu! Ingawa ni azimio alilokusudia adui kuwaponda wajumbe wa Ukweli, tunaomba sala zenu tuishinde roho ya maridhiano na uvuguvugu inayoenea kote katika safu za makanisa yetu na tusimame imara chini ya bendera Jemedari Immanueli ili tuuwasilishe Ukweli wa Sasa.

Ndugu. Michael Chivolo Murunga

Eneo la Eldoret/Lumakanda,

Kenya.

Ndugu. N. Getanda

Kuelekea mishoni mwa mwaka 2009, Nalitumwa kazini maili kadhaa mbali kutoka nyumbani. Sikupenda mahali hapo, lakini wafanya kazi wenzangu walinibembeleza niende. Nilipofika, tulitumwa katika maeneo mbali mbali, na nikaachwa kusimama peke yangu. Mbali kutoka nyumbani, marafiki, na tunaojuana, Sikuwa na wa kutegemea isipokuwa Mungu. Imani yangu ndani Yake iliimarika, nikahusiana Naye nilipokuwa kijana wa karibu miaka 21. Siku moja nilihitajika kufanya kazi siku ya Sabato, jambo ambalo sikuwahi kufanya tangu utoto wangu. Sikuwa na nyumba, nililala kwenye sakafu ya ofisi ya kampuni bila blanketi au godoro, sikuwa na chakula kizuri, na sikumiliki kitu chochote; lakini niliishi na tumaini kwamba siku moja nitamiliki kitu kutoka kwa kazi hii – kwa hivyo nilikuwa na kila udhuru nifanye kazi siku ya Sabato, jinsi wengi walivyoniambia. Huu ulikuwa mtihani wa Ukristo. Nalikataa, na msimamizi wangu kwa ghadhabu alinambia nichague ama Sabato au kazi. Nalimwambia kwamba nalikuwa nikimjulisha tu na ya kwamba sikuwa nikitafuta ruhusa yake ili niende kuabudu. Akatiwa wazimu kwa hasira, na kwa vile ilikuwa kampuni ya usalama, kutotii amri kungemaanisha kufutwa kazi mara moja. Naliazimu moyoni mwangu kwamba Mungu wa Abrahamu, Isaka, na Yakobo, Ambaye nalimfahamu tangu utotoni mwangu, anapaswa kupewa utiifu, kwa hivyo nalikaidi amri hizo nikaenda kanisani.

Jumapili asubuhi, niliporudi kazini, msimamizi alinambia kwamba nimsubiri meneja wangu siku ijayo, na alipowasili, akiwa amepashwa habari ya kesi yangu, alinikasirikia sana akaniambia kwamba

atanipa funzo; lakini wadhani nini? Mambo yalitendeka kinyume. Kesi yangu ilipowasilishwa mbele ya halmashauri kuu, iliamuliwa kwamba kesi yangu haikuwa kati ya zile zinazohitaji kufutwa. Uaminifu huu uliongoza kukwezwa kwangu hadi kiwango cha msimamizi.

Nikiwa katika ofisi hii baada ya kupandishwa cheo, Ndugu mmoja alinipata nasoma kitabu cha Tumaini la Vizazi Vyote na Pambano Kuu, ambavyo nilijua kama maandishi pekee ya Dada E. G. WHITE. Vilikuwa hazina yangu; Nilivisoma na kuvisoma tena. Kwa hivyo katika uaminifu wangu, fundisho la Mathayo 20 pekee lilikuwa limeyafumbua macho yangu baada ya muda pamoja naye. Kwa hivyo naliupokea ujumbe wa fimbo ya Mchungaji mwaka uo huo na kuwa Mdaudi baadaye.

Sehemu ya kusisimua zaidi ya safari hii ni kwamba kamwe sikujua kwamba vilikuwapo vikundi kadhaa vya Wadaudi. Baada ya kujiunga na Jumuiya ya Njia 2500 Mlima Karmeli kama Mdaudi, tulikuwa tukipokea mafunzo na miongozo kadhaa ya kusoma, Msimbo wa Nembo, n.k. Siku moja naliona nukuu kumhusu Ndugu Sam Lennox na uchambuzi wake wa mavuno na dondoo kadhaa chache zilizoambatanishwa katika makala yetu ya kila robo, ilibidi nizisome. Kisha nikamwambia Ndugu aliyeniletea kwamba yale niliyokuwa nimesoma yana maana sana kuliko yale ambayo nimekuwa nikisoma kutoka kwa makala ya robo mwaka.

Hatukufuatilia zaidi kwa sababu kamwe hatukujua jinsi ya kumfikia. Ingawa wazo hilo lilitupiliwa mbali, baadaye tulipokea wasilisho lake la video lililoitwa SIKU YA KUTOA HESABU. Nikiwa na ari ya kujua, nilisikiliza bila upendeleo, na Kweli na hoja zilizowasilishwa zilikuwa sisizopingwa. Ukweli halisi tu ndio uliowekwa mbele. Baadaye aliitwa, na tulikuwa na mkutano wa ana kwa ana, na hakika tunatangaza kwenu nyote, kwamba ukweli wa wa kwanza wa malimbuko, siku ya kutoa hesabu, na mganda wa kutikisa, ni ukweli wa sasa; fanya uchunguzi wako mwenyewe kabla hujachelewa sana: Yeremia 8:20.

Shukrani kwa kufufua tena mfululizo wa Msimbo wa Nembo.

Mungu awabariki.

Kaka Nelson Getanda, Kenya, Afrika.

Next Issue. The Bride Groom Cometh.

Jan. – Feb. – Machi 2021 | Msimbo wa Nembo, Gombo 2021, Nam. 1, 2, 3 | Uk. 16  wa 28

Pembe ya Mhazini

wa Kamati Kuu Tekelezi

TUKUMBUKE……

Katika Msimbo wa Nembo Gombo la Kumi Namba Mbili, wa mwisho, kabla ya nabii wa Mungu kulala, yafuatayo yaliletwa kwa umakini wa washarika wa Kanisa la Saa ya 11:

“…Bwana hutarajia watu Wake kwa furaha kuiunga mkono kazi Yake, kwanza kwa zaka na sadaka zao, na kisha kwa kuuza vyote iwapo wataingia katika uzima wa milele. Ilifafanuliwa kwamba yeye ambaye huzingatia kwa uaminifu matakwa Yake ya kwanza, zaka, na sadaka, mwishowe, kwa furaha, atapiga hatua kwa kuuza vyote wakati Mungu anatoa amri. Hivyo yeye ataweza kulinunua shamba lenye hazina kubwa.” {10SC2: 11.3}

Utaratibu wa Kurejesha Zaka

Hapa zipo njia mbili ambazo zaweza kutumika kurejesha zaka zako kwa Makao Makuu ya Amerika:

 1. Kutumia Wavuti Mtandaoni: kulipa ukitumia Stripe au Paypal
 2. Kutuma kwa Njia ya Posta kwa S.L.P. 23738, Waco, TX 76702

Hapa njia kadhaa zaweza kutumika kurejesha zaka zako katika Shamba la Afrika: Kenya, Uganda, na Zambia:

 1. Mpesa: kutuma fedha ukitumia simu hadi kwa Mhazini
 2. Kuweka kwenye Benki; na
 3. Kutumia wakala kutuma fedha.

Hapa zipo njia mbili zinazoweza kutumika kurejesha zaka katika field ya Kifaranza, Holland/Suriname:

 1. Kuweka katika akaunti ya benki; na
 2. Uhamisho kutoka benki hadi benki.

Mhazini Mkuu

–Dada Patricia Verpret

Ripoti ya Nyimbo

BARAKA KUU AU LAANA YA KUTISHA

Muziki ni moja wapo ya zawadi nzuri ambazo Bwana amekuwa radhi kutupatia. Nyimbo za mbinguni zinaweza kubadilisha mihemko yetu, kutuchangamsha, kututia moyo, kutujenga, na pia ni njia ya kutufundisha masomo bora ya kiroho. Awali, wakati wa siku za waasisi Waadventista, Roho wa Kweli ilituonya kwamba “Muziki, usipotumiwa vibaya, ni baraka kubwa; lakini ukitumiwa vibaya, ni laana ya kutisha.” Shuhuda, Gombo la 1 uk. 497. “Muziki ulibuniwa kutumikia kusudi takatifu, kuinua mawazo kwa yaliyo safi, ya uungwana, na kuinua, na kuamsha rohoni ibada na shukrani kwa Mungu.” Wazee wa Imani na Manabii, uk. 594.

Kamati ya Nyimbo ilianzishwa katika mwaka 2018 kuhariri nyimbo ambazo washarika wa kanisa wanatunga. Kwa sababu ya utamu wa Ukweli wakati huu, washarika wa kanisa wamehimizwa kusimulia Ukweli katika nyimbo. Kamati hukutana kwa wastani mara mbili kwa juma kuhariri nyimbo. Wanakamati wanamshukuru sana Mungu kwa upendeleo huu wa kumfanyia Kristo kazi katika kazi hii ya uungwana, na uzoefu uliopatikana ni wa thamani hakika kwa maisha yetu ya Kiroho. Wafuatao ni washarika wa sasa wa Kamati ya Nyimbo na maelezo yao ya mawasiliano.

Jan. – Feb. – Machi 2021 | Msimbo wa Nembo, Gombo 2021, Nam. 1, 2, 3 | Uk. 17  wa 28

HymnalCommittee.

Baada ya miaka miwili ya kazi, Kamati imependezwa kutangaza kutolewa kwa hati ya nyimbo za Kanisa la Saa ya Kumi na Moja. Nyimbo hizo bado hazijachapishwa katika kitabu, lakini toleo la pdf la kugawiza (toleo 21001) lilitolewa mapema mwaka huu wa Kigregoria kwa washarika wa kanisa. Tuliligawiza kwenye vikundi vikuu vya mitandao ya kijamii ya Kanisa la Saa ya Kumi na Moja. Pamoja na nyimbo hizo kipo kiunganishi cha mtambo wa google kinachosheheni rekodi za hizo nyimbo ili washarika wajifunze kuziimba. Lengo kuu la nyimbo hizi ni kuimba Ukweli wetu wa sasa unapoendelea na kukua mtamu zaidi. Kwa hivyo, kila msharika wa kanisa ajiunge nasi kutoa sifa na shukrani kwa Mungu wetu kwa neema na rehema Zake ambazo Ametuwezesha kumfanyia hii kazi. Twawahimiza washarika wa kanisa kwa furaha kuiunga mkono kazi hii kwa kujifahamisha hizi nyimbo upesi na kuziimba mara kwa mara na kwa uhuru wakati wa ibada ya familia, vikao vya maombi, ibada ya Sabato, ibada za kibinafsi, n.k. Himizo maalum lawaendea viongozi katika nchi na maeneo mbali mbali kuhakikisha kwamba wanaimba hizo nyimbo katika mikutano ya kanisa. Tazamio letu, tukiwa kamati, tuko tayari kufanya yote ambayo Bwana atatuvuvia na kutuelekeza kutenda. Tunakusudia kuendelea kuhariri nyimbo, na toleo lijalo tunatarajia litolewe kabla au mwishoni mwa mwaka huu wa kifedha. Tunataka pia tuendelee kufanya kazi kwenye wavuti wa muziki na kuizindua punde kwa neema ya Mungu. Tunapanga kutangaza hizi nyimbo kwa njia bora zaidi na kuwahimiza washarika zaidi kuzitunga. Kamati pia inapokea mashairi, na tutayapangilia na kuyaweka kwa wavuti. Mwisho, Kamati inawahimiza washarika waandike nyimbo kwa ajili ya watoto, na kuzirahisisha iwezekanavyo kwa akili zao zinazokua. Mungu awe na kazi hii na awabariki nyote. Amina.

Kiunganishi cha Mtambo wa Google kwa rekodi za nyimbo: https://bit.ly/3u9M6hZ

VIFAA:

 • Blenda

KINYWAJI CHENYE AFYA CHA KITUNGU SAUMU

VIUNGO:

 • 4-5 vidole vya kitunguu saumu.
 • 3 vijiko vya mezani vya mafuta ya nazi au mizeituni.
 • 0.1 lita (1/3 ya kikombe) ya maji.
 • 1 lita (vikombe 4.2) ya maziwa ya soya, malozi au nazi.
 • 2-3 vijiko vya mezani vya Asali halisi, au 3 vya sukari ya mtende, au tende 3.
 • 15 malozi matamu.
 • 2-3 malozi machungu.
 • 1 kipande kizito cha tangawizi.
 • ½ kijiko cha chai cha chumvi ya Himalaya, Celtic, au ya Bahari.
 • 1 kijiko cha chai cha mbegu za malenge.
 • 1 kijiko kidogo cha mbegu za alizeti.
 • Mfinyo 1 Pilipili kali.

KUANDAA:

Hatua ya 1: Yachemshe maziwa.

Hatua ya 2: Ongeza viungo hivi vya sharubati katika *blenda: vitunguu saumu vilivyogobolewa, mafuta, malozi, mbegu za malenge, mbegu za alizeti, tangawizi na maji, na uvichanganye vizuri pamoja.

Hatua ya 3: Ongeza asali, pilipili, chumvi, na uchanganye.

Hatua ya 4: Mwisho, ongeza maziwa na uchanganye.

Hatua ya 5: Mimina mara moja kwenye bilauri za kunywea.

Hatua ya 6: Shukuru kwa kinywaji na ufurahie.

 

KWA AFYA YAKO!

Kinywaji hiki ni tiba yenye kawi na kitaongeza kinga ya mwili haraka.

Jan. – Feb. – Machi 2021 | Msimbo wa Nembo, Gombo 2021, Nam. 1, 2, 3 | Uk. 18  wa 28

Wadaudi Vijana na Vijana Watu Wazima

Jumuiya ya Vijana na Watu Wazima Vijana Wadaudi, kifupi DYAYA, ilisikika mara ya kwanza wakati wa maadhimisho ya Siku ya Siku mwaka 2018 kutoka kwa Mchungaji Lennox Sam. Ilikuwa kaulimbiu ya mwaka uliokuwa mbele, kutenda kazi kwa na Vijana na Watu Wazima Vijana wetu. Jumuiya ya DYAYA ilianzishwa ili iwape Vijana na Watu Wazima Vijana jukwaa la kukutana na kuhimizana kudumisha imani, kujifunza Ukweli wa Sasa na kuwa nguvu amilifu katika safari ya Ufalme wa Mungu. Katika mwaka 2020 DYAYA iliwekwa chini ya mwavuli wa Idara ya Uchungaji, na mkutano wa siku kumi ulifanyika kuanzia 19 Agosti hadi 29, 2020. Nchi mbali mbali ziliombwa kuwasilisha majina ya viongozi waliopendekezwa kwa DYAYA ili wachukue ofisi isivyo rasmi hadi watakapothibitishwa na Ndugu Sam. Majina yaliyowasilishwa ni kama ifuatavyo,

DIVISHENI YA KENYA:

Mwenyekiti:  Kaka  Brian Gisore (Eneo La Rongai)

Katibu: Dada Diana Onyiego (Eneo La Shauri Moyo)

Mwakilishi wa Vijana: Kaka Antony Muela (Eneo La Masii)

DIVISHENI YA ZAMBIA:

Mwenyekiti: Kaka Brighton Chakwila (Eneo La Lusaka)

Katibu: Kaka Lameck Moyo (Eneo La Monze)

Mwakilishi wa Vijana: Kaka Leon Chongwe (Eneo La Mazabuka)

DIVISHENI YA  UGANDA:

Mwenyekiti: Kaka Ibrahim Sekabira (Eneo La Kampala)

Katibu: 

Mwakilishi wa Vijana: Dada Irene Mugala

THE WESTERN HEMISPHERE:

Mwenyekiti: Kaka Denny Vreds (Lelydorp, Suriname)

Katibu: Dada Edwina Henry (Florida, USA)

Mwakilishi wa Vijana: Hamna kwa sasa

Jumuiya ya DYAYA hujumuisha Vijana waamilifu (wakiwa kati ya miaka 12 na 20, kwa ujumla) na Watu Wazima Vijana (wakiwa kati ya miaka 21 na 34, kwa ujumla) wa Kanisa la saa ya 11 ambao wako tayari kufunzwa kulingana na mapenzi ya Mungu na kuwatayarisha kwa utumishi ili waweze kwenda na kuwafikia wengine.

SHUGHULI

Shughuli za Vijana na Watu Wazima Vijana Wadaudi Kanisani zimekuwa mtandaoni haswa. Tarehe 11 Septemba 2020, tuliunda kikundi cha WhatsApp kwa Vijana na Watu Wazima Vijana wote. Jumapili ya pili ya kila mwezi, Vijana na Watu Wazima Vijana hukutana kujadili mada anuwai wanazopendezwa nazo na kushiriki uchambuzi na majadiliano kutoka kwa Neno la Mungu. Vikao hivi vimekuwa msaada mkubwa kwa wale wanaovihudhuria. Husaidia pakubwa kuwasaidia kuelewa jinsi ya kusoma na

kuuwasilisha Ukweli.

Kila siku saa 12 maawio kwa saa za Afrika Mashariki, saa 11 maawio kwa saa za Afrika ya Kati, ikiwa ni saa 3 usiku kwa saa za Amerika Pana Kati, Usomaji wa Andiko na sala kwa dakika tano husambazwa katika kikundi cha WhatsApp. Usomaji huu hufanywa kwa zamu kati ya washarika. Usomaji huenda mbali kuwahimiza washarika, na wakati uo huo, husaidia wasomaji kuwa na utangamano.

KUTOKA KATIKA DIVISHENI

Tawi la Divisheni ya Kenya la Jumuiya ya DYAYA linafanya kazi kwa Utaumishi wa Muziki. Wale wanaopendezwa na wanaweza kuja pamoja kuunda kikundi cha WhatsApp. Lengo lao ni kuimba na kurekodi nyimbo zenye Ujumbe wa Ukweli wa Sasa. Wanajitahidi sauti na video zirekodiwe hivi karibuni, fedha zinakusanywa kufanikisha hilo.

Jan. – Feb. – Machi 2021 | Msimbo wa Nembo, Gombo 2021, Nam. 1, 2, 3 | Uk. 19 wa 28

Tawi la Divisheni ya Zambia limekuwa na mikutano ambapo limeweka mipango yao ili kutambua kusudi la Jumuiya na limeorodhesha hatua anuwai za kuifanikisha. Malengo kadhaa yameorodheshwa hapa chini:

   1. Kuishi kupatana na Ukweli;
   2. Kutembeleana na mara nyingi kupiga simu na kutuma ujumbe wa “Aisee” kwa kila mmoja;
   3. Kumwongoa kila m’DYAYA wa nchi ya Zambia kwa kikundi cha WhatsApp;
   4. Kumhimiza kila mmoja asome vitabu vya E.G. White vilivyochapishwa kwa ajili ya waamini vijana, kama vile MYP, AH, na MCP;
   5. Kujihusisha katika shughuli za mapumziko ili tusishawishiwe katika anasa za dhambi;
   6. Kupanga mikutano ya kambi ya DYAYA ili kujuana na kubadilishana ujuzi, shuhuda, na uzoefu;
   7. Kuwahimiza washarika wa DYAYA wakamilishe kusoma Fimbo kwa kutoa habari za kila juma kuhusu mafanikio yao ya kusoma na tarehe ya mpango wao kukamilisha;
   8. Kuwashirikisha kiutendaji Vijana wetu katika shughuli za kanisa kama vipindi vya kuikaribisha Sabato;
   9. Kuhimizana wanapokosea wakati wanawasilisha ujumbe, badala ya kuwavunja moyo;
   10. Kusisitiza umuhimu wa kuwa na Kristo ndani yetu na kuwa na masomo kuhusu wongofu;
   11. Kwa kupitia misingi yetu ya imani katika mikutano yetu na kufanya majadiliano kwa Zoom juu ya mada tofauti kama Muziki Mtakatifu, Ushairi Matakatifu, Historia Takatifu, masomo ya Kompyuta, na misingi ya Kilimo.

Kama DYAYA,

Tunathubutu kuwa ‘Danieli’,

Tunathubutu Kusimama Peke Yetu,

Tunathubutu Kuwa na Kusudi Imara,

Tunathubutu kufanya lijulikane;

HATA TUNAVYO

Simama Kama Jasiri,

Nyuso zetu kumkabili Adui.

KUZAA WATOTO

Watoto ndio urithi wa Bwana, na tunawajibika Kwake tunavyoisimamia mali Yake. . . Katika upendo, imani, na sala, wazazi watende kazi kwa familia zao, hata kwa furaha wanaweza kuja kwa Mungu wakisema, “Tazama, mimi na watoto hawa niliopewa na Bwana.” {AH 159.2}

Nyumba bila watoto ni mahali pa ukiwa. Mioyo ya wakazi iko hatarini kuwa ya ubinafsi, ya kuthamini sana kupenda starehe zao, na kushauriana na tamaa zao na yanayowafaa. Wao hujikusanyia huruma, lakini wanayo kidogo ya kuwaonyesha wengine. {AH 159.3}

Mwaka uliopita, kama tokeo la Tiba ya asili kutoka katika Zahanati Zeri ya Gileadi, kati ya wanandoa wetu wasio na watoto mmoja alizaa mwana-kondoo wao wa kwanza; tunatumaini Tiba zingine nyingi zenye mafanikio. Tangu wakati huo tumepata matokeo mazuri kwa wanawake waliotamani kupata watoto kwa Tiba hii

UKUAJI WA WANAWAKE WAGUMBA UNAONGEZEKA KWA KASI

Mojawapo ya sababu za kawaida zinazosababisha utasa wa kike ni:

Kushindwa kutaga mayai, husababishwa na chanjo katika umri mdogo – haswa barani Afrika. Hii ni mojawapo wa sababu za kawaida ambazo hutukia kwa 40% ya wanawake walio na matatizo ya ugumba. Kutotaga mayai kwaweza kuwa tokeo la sababu kadhaa, kama:

 • Hali za uraibu na mazingira.
 • Matatizo katika mzunguko wa hedhi.
 • Matatizo ya muundo katika mfumo wa uzazi.
 • Maambukizi.
 • Yai kushindwa kukomaa ipasavyo.
 • Endometriosisi.
 • Ugonjwa wa kifuko cha mayai chenye uvimbe mwingi uliojaa maji.
 • Kimsingi uzalishaji haba wa kifuko cha mayai.
 • Vichembechembe kama nyuzinyuzi [fibroids] katika mji wa mimba.
 • Magonjwa ya kinga nafsia.

Katika Msimbo wa Nembo ujao, tutashughulikia mengi kwa mada hii.

Jan. – Feb. – Machi 2021 | Msimbo wa Nembo, Gombo 2021, Nam. 1, 2, 3 | Uk. 20 wa 28

Mapainia

Mapainia Wa Kweli Katika Kurejea Waco

Mnamo 1986, Jumuiya ya Wadaudi huko Mountaindale, NY, iliungana na Jumuiya ya Wadaudi ya Yucaipa, California. Hawakuwa na nakala za Msimbo wa Nembo zilizochapishwa na Ndugu Houteff, na Msimbo pekee waliokuwa nao ni ule uliochapishwa na Dada Houteff. Muda fulani baada ya kuungana, Msimbo wa Nembo uliochapishwa na nabii ulionekana. Ndani yake, Ukweli wa eneo la Waco kudumu ulipatikana, Ukweli ambao haukupokelewa na idadi kubwa ya walei na hakuna mmoja wa viongozi.

Kikao cha Mountaindale cha mwaka 1988 kiliwasilisha “Suala la Waco,” kama lilivyoitwa, na kikateua kamati ya kutafuta ukweli kupeleleza ardhi ya Waco na kuripoti kwa Kikao kijacho mwaka 1990. Ni wazi kwamba, matokeo ya uchunguzi wao hayakuunga mkono kurejea Waco ingawa ripoti hiyo ilisema kwamba haikuandikwa kumshawishi yeyote kwa ajili au dhidi ya “Suala la Waco.” Hata hivyo, ilisema ilipata fununu kwa msharika wa zamani wa Baraza Kuu la Ndugu Houteff na kutoa ripoti ovu dhidi ya kuhamia Waco. Wadaudi wachache tu waliokuwa na roho ya Yoshua na Kalebu walipiga kura kurejea Waco baada ya kusoma matokeo ya ile iliyoitwa eti kamati ya kutafuta ukweli. Kikao cha Mountaindale cha mwaka 1990 kilipiga kura dhidi ya kuhamia Waco.

Hata hivyo mwaka 1988, wawili kati ya walimu wa Mountaindale walikuwa wamefundisha ukweli wa Eneo kwa waongofu wapya kadhaa huko Boston, Massachusetts, yaani: Ndugu Carl na Dada Joyce Huggins, Dada Alethia Blount, Ndugu Noah na Dada Katherine Peniston, kati ya wengine, hata kabla ya ripoti ya kuegemea upande kutafuta ukweli kuchapishwa, Bwana alitia ndani ya mioyo ya waongofu hawa wapya ari ya kutii Fimbo na kurudi katika eneo la makao ya kudumu la kuutangaza

ujumbe wa kutia muhuri kwa Walaodekia. Kwa hivyo, wakiwa wamechochewa na Roho wa Ukweli wa Eneo uliokataliwa, mapainia wa kweli wa kurejea Waco walijipanga katika mwaka 1988 kama Jumuiya na wakaanza kufanya maandalio ya kureja Waco. Hivyo, ghala la Bwana lilihamishwa kwa kukataliwa Ukweli wa eneo.

Agosti 28, 1989, Jumuiya mpya iliyoundwa ilinunua nyumba iliyoko 2239 Lake Ridge Circle, Waco, Texas, 76710, kwa Mlima Karmeli wa uakisi. Ghala la Mungu lilikuwa limerudi nyumbani. Akiwa Mtunza Hazina wa kwanza wa Jumuiya mpya, Dada Alethia Blount alihamia Waco kuisimamisha kambi na kochi iliyotumika kuketi na kulalia na sufuria, viokamikate, na vyombo vichache vya kupakulia na kulia. Ndugu na Dada Huggins baadaye walijiunga na Dada Blount huko Waco. Mapainia hawa waaminifu kwa imani walidai mali ya Mlima Karmeli kwa kazi ya Mungu walipokuwa wakitembea humo Sabato hata Sabato, wakimwomba Bwana alirejeshe eneo hili kwa watu Wake. Waliona bayana mambo yasiyoonekana kuwa yanayoonekana mwaka 1991 Waprestiberi walipoamua ulikuwa wakati wao kuuza mali yao ya kanisa la Mlima Karmeli na wahamie kwa eneo lao jipya. Wakala wa orodha aliwajuza mapainia kabla mali hiyo kuwekwa sokoni ili wengine waione. Alikuwa yule yule wakala aliyewasaidia kupata nyumba kwenye Lake Ridge Circle.

Wakati ule ule, katika Jumuiya ya Mountaindale, taabu ilikuwa ikitokota kwa mtu fulani mwenye ushawishi mkubwa ambaye alikuwa karibu kufurushwa. Akitishika kwa ukosefu wa ajira na akijua kwamba waanzilishi huko Waco daima walikuwa wakiwasihi wajiunge nao, alitambua fursa nzuri, akapanga ujanja bora sana wa kisiasa, na Kikao cha dharura kikaitwa,

Jan. – Feb. – Machi 2021 | Msimbo wa Nembo, Gombo 2021, Nam. 1, 2, 3 | Uk. 21 wa 28

na kura ya kuhamishia Jumuiya huko Waco ikapatikana. Hawa walikuwa watu wale wale ambao hawakutaka kuhama katika mwaka 1988 na 1990. Mbona Kikao maalum cha mwaka 1991 kilipiga kura kuhamisha Makao Makuu hadi Waco? Jibu ni fursa nzuri, lakini lile mwanadamu alikusudia kwa masilahi ya kibinafsi; Mungu alilitumia kwa masilahi Yake.

Mapainia waliokuwa Waco walifurahi sana kuwaza kwamba ndugu zao wengine walikuwa wameupokea Ukweli wa Eneo, bila kujua haikuwa hivyo, ila kwa fursa nzuri, kwa furaha waliwakabidhi wageni kila kitu na kujitiisha chini ya uongozi wao. Wote walikuwa wanaishi kwenye 2239 Lake Ridge Circle. Waliwakaribisha kwa furaha na kutoa nafasi kwa viongozi wao wapya, bila kujua kwamba punde uongozi ungeingilia mali hiyo bila kusema, ingawa waliishi katika nyumba moja! Wageni wa mwaka 1991 walitoa bei ya $ 250,000.00. Wabrestiberi mwishowe waliamua $ 285,000.00 na wakaweka rehani mbili: moja kwa $ 210,000.00 na ya pili kwa $ 20,000.00. Mmoja wa waamini asili wa mwaka 1988 wa Ukweli wa Eneo alikopa arabuni kutoka kwa mama yake kukamilisha huo mpango. Hakuna hata mmoja wa mapainia aliyealikwa kwa meza ya kuikomboa kihistoria sehemu ya Mlima Karmeli wa uakisi. Uongozi wa Waishmaeli wa 1991 hawakupenda historia

jinsi Mungu alivyoiandika, kwa hivyo waliiandika upya na kwa kiburi wakasimulia hivyo mbele ya jalada la Msimbo wa Nembo wa kwanza uliochapishwa na Jumuiya ya Waco katika mwaka 1991 ulioitwa “Kuiandika Upya Historia.”

Mungu aliwatoa Mountaindale, sio kwa ajili yao kuwa wafisadi kuzidi walivyokuwa huko Mountaindale, ila badala yake wasonge mbele katika Ukweli, wamwinue Kristo, na kukiinua kiwango juu; badala yake, waliufuata mfano wa Wayahudi baada ya kurejea kutoka uhamishoni Babeli. Tena, Bwana akatuma Ukweli mwingine unaohusu wakati wa sasa katika mwaka 2003, Akiwajuza watu Wake kwamba lazima kuwepo kutakaswa kwa Wadaudi kwanza kwa vile sisi ni wa kwanza wa malimbuko ya mavuno. Katika mwaka 2007, viongozi wa makundi kadhaa ya Wadaudi mwishowe walipoukataa Ukweli huo, Bwana alihamisha Ghala Lake hadi kwa “Wavesheaf Ministries”.

Mapainia watatu waliotajwa hapo juu waliokuwa wa kwanza kuhamia Waco waliupokea Ukweli wa Kutakaswa kwa Wadaudi. Kwa huzuni, Dada Huggins alilala katika mwaka 2009 na alizikwa kando ya waasisi wa mwaka 1935. Ndugu Huggins na Dada Blount bado wanashangilia katika Kweli. Ukasisi wa Mganda wa Kutikisa sasa unajulikana kama Jumuiya ya Wadaudi Waadventista wa Sabato, iliyo kilimani Mlima Karmeli wa uakisi Waco, Texas.

KUZUIA KWA MUNGU AU CHANJO YA MWANADAMU – IPI?

TUFANYE NINI KWA KORONA AU KWA KIRUSI KINGINE CHOCHOTE? IWE NI MAUMIVU YA MAUMBILE AU MIPANGO YA MWANADAMU?

Usafi: soma ukurasa wa 97 hadi wa 102 katika trakti Ulawi wa Wadaudi Waadventista wa Sabato.

Na usisahau kwamba vitu muhimu zaidi kwa afya ni maji safi, mwangaza wa jua, hewa mpya safi, na mazoezi ya nje ya nyumba. {EW: 45.2}

“Hewa safi, mwangaza wa jua, kujinyima, pumziko, mazoezi, lishe sahihi, matumizi ya maji, imani katika nguvu za Mungu — hizi ndio tiba za kweli. Kila mtu anapaswa kuwa na maarifa kuhusu nguvu za tiba asilia na jinsi ya kuzitumia. Ni muhimu kuelewa kanuni zinazohusika kuwatibu wagonjwa na kuwa na mafunzo ya kivitendo ambayo yatamwezesha mtu kutumia maarifa haya kwa usahihi.” {MH 127.2}

Make friends. Uwe mchangamfu na mtulivu nyakati zote. Kumbuka kwamba “moyo uliochangamka ni dawa nzuri; bali roho iliyopondeka huikausha mifupa.” Mit. 17:22. Hofu, hasira kali, mizigo mizito na wasiwasi, huongeza utoaji wa kioevu cha kumeng’enya, na kusababisha tumbo la tindi kali na vidonda vya tumbo. {EW: 81.1}

“Uhusiano uliopo kati ya akili na mwili ni wa ndani. Wakati kimoja [kiungo] kimeathirika, kingine husikitika. Hali ya akili huathiri afya kwa kiwango kikubwa zaidi kuliko vile wengi huwaza. Magonjwa mengi ambayo wanadamu huugua ni tokeo la

(Yameendelezwa uk. 26)

Jan. – Feb. – Machi 2021 | Msimbo wa Nembo, Gombo 2021, Nam. 1, 2, 3 | Uk. 22 wa 28

Maisha ya Familia na Afya

Wapenzi, familia pendwa ya Kanisa la Saa ya Kumi na Moja, tunayo furaha kuwaletea habari na maendeleo kutoka kwa Idara ya Maisha ya Familia na Afya.

““Fundisho la matengenezo ya afya yanasemekana kuwa ‘mkono wa kulia na mkono wa Ujumbe wa Malaika wa Tatu,’ na ya kwamba kazi ya matibabu ni ‘mkono wa kulia wa ujumbe.’” {SR2: 179.2}

IDARA ILIKUJA KUWEKO FEBRUARI 2019.

Tangu wakati tulipoanza, tumepata baraka za Bwana kila daima katika juhudi zetu za kuondoa maradhi ya wagonjwa kati yetu.

Bwana alitoa neno Lake kwa Israeli ya kale kwamba iwapo wangeshikamana Naye kabisa na kufanya matakwa Yake yote, Yeye angewaondolea magonjwa yote ambayo alikuwa Amewaletea Wamisri, lakini ahadi hii ilitolewa kwa sharti la utiifu. Kama Waisraeli wangetii agizo walilopokea na kunufaika na manufaa yake, wangekuwa kielezo cha afya na ufanisi kwa ulimwengu. Waisraeli walishindwa kutimiza kusudi la Mungu na kwa hivyo hawakuweza kupokea baraka ambazo zingekuwa zao.

Sisi tunaoitwa Israeli ya Kiroho leo tumepewa fadhila kupokea baraka hizi zote zilizoahidiwa Israeli ya kale.

“… Uaminifu kama huo leo ​​utazalisha matokeo kama hayo. Kwetu, imeandikwa, ‘Bali ninyi ni mzao mteule, ukuhani wa kifalme, taifa takatifu, watu wa milki ya Mungu; mpate kuzitangaza fadhili zake Yeye aliyewaita mtoke gizani mkaingie katika nuru Yake ya ajabu.’” 1 Petro 2:9. {CD 26.3}

 

IDARA HII INA VITENGO VIFUATAVYO:

ZAHANATI ZERI YA GILEADI

Hii ni zahanati ya mtandaoni ambamo washarika wa Kanisa wanaweza kuja wakiwa wagonjwa au kutumia wakati fulani kukusanya maarifa zaidi juu ya lolote wanalotaka kujua mintarafu ya afya.

Zahanati hii imegawanywa katika sehemu mbili, moja kwa kina dada na nyingine kwa kina kaka.

JIKO LA HEWANI

“Upishi sio sayansi duni, ni mojawapo wa zilizo muhimu zaidi katika maisha ya utendaji. Ni sayansi ambayo wanawake wote wanapaswa kujifunza, na inapaswa kufundishwa katika njia ya kuyafaidi madaraja maskini. Ili kufanya chakula cha kupendeza na wakati uo huo kuwa rahisi na chenye lishe, huhitaji ustadi; lakini lawezekana. Wapishi wanapaswa kujua jinsi ya kuandaa chakula rahisi kwa njia rahisi na ya kiafya, ili kiweze kuwa chenye ladha zaidi, na pia cha kuleta afya, kwa sababu ya kurahisishwa.” 378 {CCh 222.5}

Jikoni kwetu, chakula chenye afya huandaliwa na Kamati:

 • ambayo huhakikisha kwamba chakula cha kuleta afya, chenye ladha na michanganyiko sahihi ya vyakula inaandaliwa;
 • ambayo pia hutoa ushauri nasaha katika vikundi anuwai vya WhatsApp vya shirika; na
 • ambayo hutunza mapishi na kubuni “Mapishi ya Saa ya Kumi na Moja,” ambayo hutoka kwa washarika wetu katika Sehemu tofauti.

VIKOSI VYA MAOMBI

LENGO LETU

Kuinyenyekeza mioyo yao mbele ya Mungu kwa sala ya kusihi na kufunga kwa niaba ya familia yao ya Kanisa la Saa ya Kumi na Moja, marafiki, na wagonjwa kati yao, ili waweze kupokea neema Yake ya msamaha, wamkaribie Yeye na Kumsihi awafungulie hazina Yake.

Kwa mwaka sasa, kila Jumatano asubuhi, Wanakikosi hukusanyika kuanzia 12 hadi 1 Asubuhi APK ili kuomba mbele ya Kiti cha Enzi cha Rehema cha Bwana na haja za maombi ambayo yalikusanywa

Jan. – Feb. – Machi 2021 | Msimbo wa Nembo, Gombo 2021, Nam. 1, 2, 3 | Uk. 23 wa 28

katika juma kutoka kwa washarika wa kanisa, familia, na marafiki.

Maombi yanajibiwa, na mara moja kwa mwezi, sadaka ya shukrani, sifa, na shuhuda hutolewa kwa Bwana.

KUTAFUTA WAKUJITOLEA KATIKA IDARA YA AFYA

“Bwana anawaita wakujitolea waingie katika jeshi Lake. Wanaume na wanawake wagonjwa wanahitajika wawe wanamatengenezo wa afya. Mungu atashirikiana na watoto Wake kuhifadhi afya zao, iwapo watakula kwa uangalifu, wakikataa kuweka mizigo isiyohitajika tumboni. Kwa neema Ameitengeneza njia ya asili kuwa hakika na salama, pana ya kuwatosha wote kutembea kwayo. Ametoa kwa ajili ya riziki yetu mazao ya nchi halisi na yanayoleta afya.” {CD 39.3}

“Yeye asiyetii maagizo ambayo Mungu ametoa katika neno Lake na katika matendo Yake, yeye asiyetii amri takatifu, ana uzoefu wenye kasoro. Yeye ni Mkristo mgonjwa. Maisha yake ya kiroho ni dhaifu. Anaishi, lakini maisha yake hayana manukato. Yeye hupoteza nyakati za thamani zenye neema.” {CD 39.4}

MPANGILIO

Bado kwa sasa tunaendelea kuipangilia Idara ya Afya.

Kaka yangu mpendwa, dada yangu mpendwa, njoo tufanye kazi pamoja katika Shamba la Mizabibu la Bwana.

Je, wewe ni mwenye bidii? Je! Unao uzoefu wa kufanya kazi kama mmishonari wa utabibu? Wasiliana nasi, na Bwana atakuwa pia na kazi kwa ajili yako kufanya katika idara hii muhimu.

WANAKAMATI WA IDARA YA AFYA NI:

Dada Helga Kortram (Mkurugenzi)
Dada Edna Twara (Naibu Mkurugenzi)
Kaka Lloyd van Niel (Katibu)
Dada Phili van Niel (Mhazini)
Dada Huguette Suivant (Msharika)
Dada Josseline Samy (Msharika)
Dada Lungowe Mwiya (Msharika)
Dada Sylvia Kayanga (Msharika)
Kaka Iwan Kortram (Msharika)
Kaka Lennox Sam (Mshauri).

Idara ya Uchungaji

“Bila kukosea, kwa hivyo, nuru angavu inayoangaza kutoka kwa mfano, kutoka kwa shuhuda za manabii, na kutoka kwa historia, huutambua ujumbe wa Fimbo kama ndio pekee uliowekwa wakfu kuliongoza kanisa la siku za mwisho, lililowekwa huru kutoka kwa dhambi na wadhambi, kuingia katika nchi ya ahadi, wakati, ‘nyakati za mataifa zitakapotimia.’ Luka 21:24. ‘Katika siku za wafalme hao Mungu wa mbinguni atausimamisha ufalme, ambao hautaangamizwa milele’ Dan. 2:44. Hiyo siku imekuja na Fimbo ya Mungu I hapa kulitekeleza ‘vuguvugu kuu la matengenezo kati ya watu wa Mungu.’ – (Shuhuda, Gombo la9, uk. 126), kupeana ‘ uwezo na juhudi kwa Ujumbe wa Malaika wa Tatu.’ – (Maandishi ya Awali, uk. 277), ili kwamba, ‘likiwa limevikwa silaha za haki ya Kristo, kanisa… zuri kama mwezi, safi kama jua, na la kutisha kama jeshi lenye mabango,’ liweze ‘kwenda ulimwenguni kote, likishinda

na kushinda.” – Manabii na Wafalme, uk. 725. {ABN3: 23.2}

Katika nuru ya taarifa hii, Idara ya Uchungaji tangu ilipoanzishwa imewahudumia kondoo sio tu kupitia mafunzo ya kibinafsi ya Biblia lakini pia kupitia uenezaji wa Fimbo isiyotiwa unajisi kupitia video, mitandao ya kijamii, n.k. Mikutano ya Maombi katikati ya juma hufanyika kila Jumanne saa 2 usiku, Shule ya Manabii kila mwezi Sabato ya pili saa 1 asubuhi, na kila juma Amerika Pana mafunzo ya Sabato Alasiri saa 9 alasiri (zote zikiwa ni saa za Amerika Pana ya Kati, APK). Waadventista na Wadaudi wote hualikwa na kuruhusiwa kuuliza maswali kila baada ya wasilisho, isipokuwa katika Mkutano wa Maombi, ambamo kushiriki huwa mwishoni katika sifa, shukrani, na shuhuda.

Vitambulisho vya Webina vya mikutano hii ni kama ifuatavyo (hakuna nenosiri):

Jan. – Feb. – Machi 2021 | Msimbo wa Nembo, Gombo 2021, Nam. 1, 2, 3 | Uk. 24 wa 28

Mkutano wa Maombi Katikati ya Juma: 989 2478 5827
Shule ya Manabii: 940 2826 1432
Nusu-Mviringo ya Magharibi Sabato Alasiri: 940 4716 3414

Ushauri nasaha wa mchungaji kwa ubatizo, ndoa, mahimizo ya kwa mtu binafsi, n.k., hufanywa mara kwa mara, na sasa, washarika wa Kanisa wanapokea ziara sibayana za mchungaji Jumapili ya mwisho kila mwezi. Kwa vile kuhudumu sio tu kazi ya mchungaji aliyewekwa wakfu, ndugu, dada, na vijana hushiriki kwa pamoja na kibinafsi katika kazi hii kuu ya matengenezo. Hakika, idara hii haifumbi macho kwa mahitaji ya kiroho au ya kimwili ya wakongwe, wagonjwa, maskini, wajane, na mayatima.

Msharika yeyote wa Kanisa anaweza kuomba ushauri wa uchungaji wakati wowote kwa kuwasiliana na katibu wa Idara ya Uchungaji kwa mdsec@gadsda.com.

“Hakika,… Yeye alichagua kuwa na wajenzi waaminifu washikilie upanga kwa mkono mmoja na matofali kwa mkono mwingine (Neh. 4:17, 18). Kazi yao ilikuwa ngumu sana, ikiwa haikuwa ngumu kuliko yetu, lakini walikuwa waaminifu kwayo, na hatuwezi kumudu kuwa waaminifu wapungufu kuliko wao. Naam, walifanya kazi nyingi ya kujenga na kufundisha. Hawakufundisha dini tu, bali kujenga, pia.” {1TG9: 13.3}

Katibu wa Idara ya Uchungaji
Dada Phili Kortram-van Niel

Maisha ya Familia

Idara hii ilianza Februari 2019 pamoja na Idara ya Afya na zikaunganishwa kufanyiza Idara ya Maisha ya Familia na Afya (FLHD).

Lengo la kuzishauri na kuzisaidia familia za Kanisa la Saa ya Kumi na Moja limeonekana kuwa ufanisi mkubwa na kanisa lilipata uzoefu wa baraka tele za Bwana kutoka kwa kazi ya utumishi huu.

“Wanawake vijana wanapaswa kufunzwa upishi kikamilifu. Ziwazo zote hali zao maishani, hapa yapo maarifa ambayo yanaweza kutumika kivitendo. Ni tawi la elimu ambalo lina mvuto usiopinda katika maisha ya mwanadamu, haswa maisha ya wapendwa. Wengi mke na mama ambaye hajapata elimu sahihi, na asiye stadi katika idara ya upishi, kila siku analisha familia yake chakula kilichotayarishwa vibaya ambacho hatua kwa hatua na kwa hakika kinaharibu viungo vya kumeng’enya, kinafanya damu kuwa duni, na mara kwa mara kuleta mashambulizi makali ya ugonjwa wenye uvimbe, na kusababisha kifo cha mapema.” – “Mashauri kwa Afya,” uk. 145. {2SC3,4: 16.2.3}

Kwa sababu ya maonyo haya, tulianza na Jiko la Hewani, ambalo ni njia ya kuwasaidia washarika wa Kanisa letu la Saa ya Kumi na Moja kukuza ujuzi katika sehemu muhimu ya shughuli zao za kila siku za kifamilia zinazoitwa upishi. Madarasa ya upishi mtandaoni hivi karibuni yatakuwa sehemu ya utumishi wetu.

NDOA

“Jinsi ilivyo kwa taasisi ya Sabato, vivyo hivyo lazima Mungu airejeshe ile ya ndoa. Maneno ya Kristo: ‘Kwa maana katika ufufuo hawaoi, wala hawaolewi, bali huwa kama malaika wa Mungu Mbinguni’ (Mat. 22:30), hufichua kwamba tumepoteza mtazamo wa maana ya kweli ya taasisi ya ndoa. Na kwa sababu Mungu bado hajatujuza kikamilifu hali ya maisha yetu ya baadaye, sisi, sasa hivi, hatuezi kuelewa kabisa ama ndoa au uhusiano wa kifamilia baada ya ufufuo.” {3SC2: 7.2.3}

Huwa tunapanga mafunzo kuhusu Ndoa, Kupanga Uzazi, n.k., Jumapili ya mwisho kila mwezi. Tunasoma siku zote pia katika Nyumba ya Mwaadventista na vifungu muhimu katika Msimbo wa Nembo mintarafu ya maisha ya familia ili kufikia kiwango kinachohitajika cha Ufalme unaokuja hivi karibuni.

Jan. – Feb. – Machi 2021 | Msimbo wa Nembo, Gombo 2021, Nam. 1, 2, 3 | Uk. 25 wa 28

KUISHAURI FAMILIA YA KANISA LA SAA YA KUMI NA MOJA

Kitengo hiki ni kimojawapo cha sehemu muhimu za Idara ya Maisha ya Familia. Akiwa mchungaji na mratibu wa Idara ya Maisha ya Familia na Afya, Ndugu Sam kwa sasa anakutana na familia na waamini wote wa kanisa. Wale ambao wamekutana na Ndugu Sam walifurahia mkutano wao wa kwanza na wanatazamia miadi yao ijayo naye.

(Mungu au Mwanadamu, Yupi? Yameendelezwa kutoka uk. 20)

mfadhaiko. Huzuni, wasiwasi, kutoridhika, kujuta, hatia, kutokuaminiana, zote huwa huvunja nguvu za uhai na kukaribisha kuoza na mauti… Ujasiri, tumaini, imani, huruma, upendo, kuboresha afya na kudumisha uhai. Moyo uliotulia, roho iliyochangamka, ni afya kwa mwili na nguvu kwa nafsi.” — Ukasisi wa Uponyaji, uk. 241. {EW: 81.2}

Fuata mpango wa afya themanini / ishirini, na chochote kinachoweza kuliwa kibichi, usipike. Utakase mfumo wako wa kumeng’enya chakula angalau mara mbili kwa mwaka.

BIDHAA HIZI ZA CHAKULA NI KIUA VIJISUMU ASILIA NA VITAKASA MWILI AMBAVYO LAZIMA VISIKOSEKANE KABISA NYUMBANI MWETU: KITUNGUU SAUMU; BIZARI; TANGAWIZI; LIMAU; PILIPILI KALI;

MAKAA.

Rejea katika Mapito ya Zamani.

“Bwana asema hivi, simameni katika njia kuu, mkaone, mkaulize habari za mapito ya zamani, I wapi njia iliyo njema? Mkaenende katika hiyo, nanyi mtajipatia raha katika nafsi zenu. Lakini walisema, hatutaki kwenda katika njia hiyo.” Yeremia 6:16

“Tumetangatanga mbali na mipaka ya zamani. Turudi. Ikiwa Bwana ni Mungu, mtumikie; iwapo ni Baali, mtumikie. Unachagua kuwa upande?” — Shuhuda, Gombo la 5, uk. 137. {ABN2: 71.2}

“Kanisa limekengeuka na kuacha kumfuata Kristo Kiongozi wake, na badala yake linarudi pole pole kuelekea Misri!” Na ya kwamba “Mji mwaminifu umekuwaje kahaba;” na ya kwamba “Nyumba ya Baba Yangu imefanywa nyumba ya biashara, mahali ambapo uwepo wa Mungu na utukufu umetoweka.” Tazama, “Shuhuda kwa Kanisa,” Gombo la 5, uk. 217; Gombo la 8, uk. 250; Gombo la 5, uk. 211. {3SC11-12: 10.2.5}

“Tokea siku za baba zenu mmegeuka upande mkayaacha maagizo Yangu, wala hamkuyashika. Nirudieni Mimi, Nami nitawarudia ninyi, asema Bwana wa majeshi.” Mal. 3:7.

Kumb. 7:15. “Na Bwana atakuondolea magonjwa yote, wala hatatia juu yako maradhi yoyote mabaya uyajuayo ya Misri, lakini atayaweka juu ya [wote] wakuchukiao.”

Matukio Yajayo

Shule ya Manabii ya Walimu, Sabato ya kwanza ya kila mwezi
Saa 1 asubuhi saa za Kati, Tuma Barua pepe kwa mwaliko, Rekebisha kulingana na eneo lako

Shule ya Manabii kwa washiriki wote, Sabato ya 2 ya Kila Mwezi
Saa 1 asubuhi saa za Kati, Rekebisha kulingana na eneo lako
Nambari ya Zoom: 940 2826 1432, Hamna Nenosiri.

Fundisho la Sabato Mchana, Saa 9 alasiri saa za Kati, Rekebisha kulingana na eneo lako
Nambari ya Zoom: 940 4716 3414, Hamna Nenosiri

Mkutano wa Maombi wa Jumanne Jioni, Saa 2 Usiku saa za Kati
Nambari ya Zoom: 989 2478 5827, Hamna Nenosiri

Wana-Mfalme na Makuhani Wadaudi (DPPS) Jumatano ya 2 na ya mwisho
Saa 2 usiku saa za Kati, Nambari ya Zoom: 964 6277 5768, Passcode: 1

Jumuiya ya kina dada ya Malkia Esta (QESS) Saa 2 usiku saa za Kati, Jumatano ya 1 na ya 3.
Nambari ya Zoom: 959 0403 4695, Passcode: 7

Shule ya Manabii ya Walimu, Sabato ya kwanza ya kila mwezi
Saa 9 alasiri saa za Afrika Mashariki, Tuma Barua pepe kwa mwaliko, Rekebisha kulingana na eneo lako

Shule ya Manabii kwa washiriki wote, Sabato ya 2 ya Kila Mwezi
Saa 9 alasiri saa za Afrika Mashariki, Rekebisha kulingana na eneo lako
Nambari ya Zoom: 940 2826 1432, Hamna Nenosiri

Fundisho la Sabato Mchana, Saa 4 Usiku saa za Afrika Mashariki, Rekebisha kulingana na eneo lako
Nambari ya Zoom: 940 4716 3414, Hamna Nenosiri

Mkutano wa Maombi wa Alhamisi Asubuhi, Saa 10 Alfajiri saa za Afrika Mashariki
Nambari ya Zoom: 989 2478 5827, Hamna Nenosiri

Wana-Mfalme na Makuhani Wadaudi (DPPS) Alhamisi ya 2 na ya mwisho
Saa 10 alfajiri saa za Afrika Mashariki, Nambari ya Zoom: 964 6277 5768, Nenosiri: 1

Jumuiya ya kina dada ya Malkia Esta (QESS) Saa 10 alfajiri saa za Afrika Mashariki, Alhamisi ya 1 na ya 3.
Nambari ya Zoom: 959 0403 4695, Nenosiri: 7

Siku 10 za Maombi — Aprili 11-20, 2021
Saa 2 usiku saa za Kati, Kila usiku kwa siku kumi, Nambari ya Zoom: 918 8260 8708, Hamna Nenosiri linalohitajika

Jan. – Feb. – Machi 2021 | Msimbo wa Nembo, Gombo 2021, Nam. 1, 2, 3 | Uk. 26 wa 28

Advert Of
Picture
>