fbpx

Gombo la 2 Salamu Mwafaka Namba 03, 04

Gombo la 2 Salamu Mwafaka Namba 3, 4

                                    

AMANI YA PEKEE YA MAWAZO

Hati miliki, Kimechapishwa tena 1954

Haki zote zimehifadhiwa

V. T. HOUTEFF

                                    

 

UKARABATI WA NCHI YA MKRISTO NA UPASUAJI WA MOYO

WAFU NA WALIO HAI WANAJUMUISHA NYUMBA YOTE YA ISRAELI; GOGU ANAANGAMIA

                                    

1

ANDIKO LA SALA

Bibilia — Mamlaka Yasiyoweza Kukanushwa

Nitasoma kutoka katika “Mafunzo ya Kristo Kwa Mifano,” kuanzia ukurasa wa 38 na aya ya mwisho– {2TG3: 2.1}

“Waalimu wa Israeli hawakuwa wakipanda mbegu ya neno la Mungu. Kazi ya Kristo kama mwalimu wa ukweli ilikuwa tofauti kabisa na ile ya waalimu wa wakati Wake. Walizingatia mila, nadharia na ukisiaji wa kibinadamu. Mara nyingi yale ambayo mwanadamu alikuwa amefundisha na kuandika juu ya neno hilo, waliliweka mahali pa neno lenyewe…. Mada ya fundisho na mahubiri ya Kristo ilikuwa neno la Mungu. Alikutana na wauliza-maswali na dhihirifu, ‘Imeandikwa.’ ‘Maandiko yasemaje?’ ‘Unasomaje?’… Watumwa wa Kristo wanapaswa kufanya kazi iyo hiyo. Katika siku yetu, kama za zamani, kweli muhimu za neno la Mungu zimewekwa kando kwa nadharia na makisio ya wanadamu. Wachungaji wengi wanaodai kuamini injili hawaipokei Biblia yote kama neno lili-lovuviwa. Mtu mmoja mwenye busara huikataa sehemu moja; mwingine anahoji sehemu nyingine. Huusimamisha uamuzi wao kama bora kuliko neno; na Andiko ambalo wao hufundisha hutua juu ya mamlaka yao wenyewe. Usahihi Wake mtakatifu unaharibiwa…. Alionyesha Maandiko kama ya mamlaka yasiyoweza kutiliwa shaka, nasi tunapaswa kufanya vivyo hivyo. Bibilia inapaswa kuwasilishwa kama neno la Mungu wa milele, kama kikomo cha mabishano yote na msingi wa imani yote.” {2TG3: 2.2}

Tunahitaji kuomba alasiri hii kwa ajili ya msaada tusiweze kamwe kuliweka kando Neno la Mungu kwa nadharia na makisio ya wanadamu, ila siku zote kufundisha kweli dhahiri za Bibilia kwa mujibu wa Roho, mamlaka pekee isiyotiliwa shaka — mwisho wa mabishano yote, msingi wa imani yetu. Hebu tupige magoti. {2TG3: 2.3}

2

UKARABATI WA NCHI YA MKRISTO NA UPASUAJI WA MOYO

ANDIKO LA HOTUBA NA V. T. HOUTEFF

MCHUNGAJI WA WADAUDI WAADVENTISTA WA SABATO

SABATO, AGOSTI 23, 1947

HEKALU LA MLIMA KARMELI

WACO, TEXAS

Mada yetu ya alasiri hii ni ukarabati wa nchi ya Mkristo na upasuaji wa moyo. Mada hii tunaipata katika sura ya thelathini na sita ya Ezekieli. {2TG3: 3.1}

Ezek. 36: 1-10 — “Na wewe, mwanadamu, itabirie milima ya Israeli, useme, Enyi milima ya Israeli, lisikieni neno la Bwana. Bwana MUNGU asema hivi; Kwa sababu adui amesema juu yenu, Aha! Na, Mahali pa juu pa zamani [mahali pa ibada katika Nchi ya Ahadi] pamekuwa petu tupamiliki; basi tabiri useme, Bwana MUNGU asema hivi; Kwa sababu, naam, kwa sababu wamewafanya ninyi kuwa ukiwa, na ku-wameza pande zote, mpate kuwa milki kwa mabaki ya mataifa, nanyi mmeambwa kwa midomo yao wa-ongeao, na kwa masingizio ya watu; kwa sababu hiyo, enyi milima ya Israeli, lisikieni neno la Bwana MUNGU; Bwana MUNGU aiambia hivi hiyo milima na vilima, mifereji ya maji na mabonde, mahali pali-poharibika na kuwa ukiwa, na miji iliyoachwa [na watu Wake], ambayo imekuwa mateka, na kuzomewa na mabaki ya mataifa, walio karibu pande zote; basi Bwana MUNGU asema hivi; Hakika kwa moto wa wivu wangu nimenena juu ya mabaki ya mataifa, na juu ya Edomu yote [sasa Waarabu], waliojiandikia nchi yangu kuwa milki yao, kwa furaha ya mioyo yao yote,

3

kwa jeuri ya roho zao, ili waitupe nje kuwa mawindo; basi katika kutabiri habari za nchi ya Israeli, uiam-bie milima na vilima, mifereji ya maji na mabonde, Bwana MUNGU asema hivi; Tazama, nimenena kati-ka wivu wangu na hasira yangu, kwa sababu mmechukua aibu ya mataifa.”

Aya hizi, ambazo sasa zinaonekana katika mfumo wa ujumbe wa saa, zinaonyesha kwamba wakati wa Mataifa umekwisha, kwamba wateule wa Mungu watarejea na wamiliki nchi yao milele! {2TG3: 4.1}

Aya ya 11-14 — “Nami nitaongeza juu yenu mwanadamu na mnyama, nao watazidi na kuzaa; nami nita-wakalisha watu ndani yenu, kwa kadiri ya hali yenu ya kwanza, nami nitawatendea mema kuliko mema ya mianzo yenu; nanyi mtajua ya kuwa mimi ndimi Bwana. Naam, nitaleta watu watembee juu yenu, naam, watu wangu Israeli; nao watakumiliki, nawe utakuwa urithi wao, wala hutawafisha watoto wao tena tangu leo. Bwana MUNGU asema hivi; Kwa kuwa watu hukuambia, wewe nchi u mwenye kula wa-tu, nawe umekuwa mwenye kufisha watu wa taifa lako; basi hutakula watu tena, wala hutafisha watu wa taifa lako tena, asema Bwana MUNGU.”

Aya hizi haziwezi kupotoshwa kumaanisha

4

kurejea kwa Wayahudi kutoka Babeli, kwa sababu hapa imenenwa, nchi hiyo “basi hutakula watu tena, wala hutafisha watu wa taifa lako tena,” ilhali historia inaonyesha kwamba tangu kurudi kwa Wayahudi kutoka Babeli, nchi imewala watu — haijakuwapo amani ya kudumu. Zaidi ya hayo, sura hii inazungumza haswa kui-husu “nyumba ya Israeli,” ufalme wa kabila kumi, ambao haujawahi kurudi tena tangu ulipotawanywa na Waashuri. {2TG3: 4.2}

Aya ya 15-22 — “Wala sitakusikizisha tena aibu yao wasioamini, wala hutachukua matukano ya watu tena; wala hutalikwaza taifa lako tena, asema Bwana MUNGU. Tena, neno la Bwana likanijia, kusema, Mwanadamu, nyumba ya Israeli walipokaa katika nchi yao wenyewe, waliitia uchafu kwa njia yao na kwa matendo yao. Njia yao mbele zangu ilikuwa kama uchafu wa mwanamke wakati wa kutengwa kwake. Kwa hiyo nalimwaga hasira yangu juu yao, kwa ajili ya damu waliyoimwaga juu ya nchi, na kwa sababu wameitia uchafu kwa vinyago vyao. Nikawatawanya katika mataifa, wakatapanyika katika nchi nyingi; kwa kadiri ya njia yao, na kwa kadiri ya matendo yao, naliwahukumu. Nao walipoyafikilia ma-taifa yale waliyoyaendea, walilitia unajisi jina langu takatifu; kwa kuwa watu waliwanena, wakisema, Watu hawa ni watu wa Bwana, nao wametoka katika nchi yake. Lakini, naliwahurumia kwa ajili ya jina langu takatifu, ambalo nyumba ya Israeli walikuwa wamelitia unajisi katika mataifa waliyoyaendea. Kwa hiyo; waambieni nyumba ya Israeli, Bwana MUNGU asema hivi Sitendi hili kwa ajili yenu, Ee nyumba ya Israeli, bali kwa ajili ya jina langu takatifu, mlilolitia unajisi katika mataifa mliyoyaendea.”

Kwa maandiko haya sasa inaweza kueleweka kwamba Mungu hafanyi hivi kwa sababu watu Wake wa jana

5

au wa leo wamekuwa wazuri, lakini kwa sababu lazima alitetee jina Lake, na lazima Awajulishe mataifa kwamba waliweza kuwafukuza watu Wake kutoka katika nchi kwa sababu tu Yeye aliwaruhusu kufanya hivyo kwa sababu ya uovu wa watu Wake. {2TG3: 5.1}

Aya ya 23-27 — “Nami nitalitakasa jina langu kuu, lililotiwa unajisi katika mataifa, mlilolitia unajisi kati yao; nao mataifa watajua ya kuwa mimi ndimi Bwana, asema Bwana MUNGU, nitakapotakaswa kati yenu mbele ya macho yao. Maana nitawatwaa kati ya mataifa, nami nitawakusanya na kuwatoa katika nchi zote, na kuwarudisha katika nchi yenu wenyewe. Nami nitawanyunyizia maji safi, nanyi mtakuwa safi; nitawatakaseni na uchafu wenu wote, na vinyago vyenu vyote. Nami nitawapa ninyi moyo mpya, nami nitatia roho mpya ndani yenu, nami nitatoa moyo wa jiwe uliomo ndani ya mwili wenu, nami nita-wapa moyo wa nyama. Nami nitatia roho yangu ndani yenu, na kuwaendesha katika sheria zangu, nanyi mtazishika hukumu zangu, na kuzitenda.”

Ni dhahiri kuona kwamba kabla wewe na mimi kuwa tayari kuhamishwa bila kufa, lazima kwanza tuwe tayari kwenda katika nchi ya Ahadi, huko kutakaswa, huko mioyo yetu ya jiwe kuondolewa. Naam, njia pekee ya kuupata huu upasuaji wa moyo kufanywa juu yetu ni kumruhusu Bwana kwanza atukusanye kutoka kwa ma-taifa na kutuleta katika nchi yetu wenyewe. Kwa maana “basi,” asema Bwana, “Nitawanyunyizia maji safi,” na “nitawapa ninyi moyo mpya, nami nitatia roho mpya ndani yenu.” {2TG3: 6.1}

Mbele ya hili, ningependa kujua ni nani angaliweza kuishi na Kristo wakati wa miaka elfu bila kwanza ya kuwa alienda katika nchi, kutakaswa na huko kupokea moyo mpya? {2TG3: 6.2}

Aya ya 27-31 — “Nami nitatia roho yangu ndani yenu,

6

na kuwaendesha katika sheria zangu, nanyi mtazishika hukumu zangu, na kuzitenda. Nanyi mtakaa kati-ka nchi ile niliyowapa baba zenu, nanyi mtakuwa watu wangu, nami nitakuwa Mungu wenu. Nami nita-waokoeni na uchafu wenu wote; nitaiita ngano, na kuiongeza, wala sitaweka njaa juu yenu tena. Nami nitazidisha matunda ya miti, na mazao ya mashamba, msipate tena kutukanwa na mataifa kwa sababu ya njaa. Ndipo mtazikumbuka njia zenu mbaya, na matendo yenu yasiyokuwa mema, nanyi mtajichukia nafsi zenu kwa macho yenu, kwa sababu ya maovu yenu na machukizo yenu.”

Bwana anajua jinsi ya kuokoa: Yeye aliwaruhusu watu Wake kutawanywa kwa mataifa yote ili kwamba An-apowarejesha nyumbani watalikumbuka tokeo la matendo yao ya uovu, na hivyo wauchukie uovu wao. {2TG3: 7.1}

Aya ya 33-36 — “Bwana MUNGU asema hivi; Siku ile nitakapowatakaseni na maovu yenu yote, nitaifan-ya miji ikaliwe na watu, na palipobomolewa pajengwe tena. Nchi iliyokuwa ukiwa italimwa, ijapokuwa ilikuwa ukiwa mbele ya macho ya watu wote waliopita. Nao watasema, Nchi hii, iliyokuwa ukiwa, imeku-wa kama bustani ya Edeni; nayo miji iliyokuwa mahame, na ukiwa, na magofu, sasa ina maboma, ina-kaliwa na watu. Ndipo mataifa, waliobaki karibu yenu pande zote, watajua ya kuwa mimi, Bwana, nime-jenga mahali palipoharibika, nami nimepanda mbegu katika nchi iliyokuwa ukiwa; mimi, Bwana, nimes-ema hayo; tena nitayatenda.”

Maajabu haya yote, unaona, Bwana atayatenda katika nchi ya Israeli na machoni pa mataifa. Haya ni kwa lazima matukio kabla ya milenia. {2TG3: 7.2}

7

Aya ya 37 — “Bwana MUNGU asema hivi, Tena kwa ajili ya jambo hili nitaulizwa na nyumba ya Israeli, ili niwatendee; nami nitawaongeza kwa watu kama kundi la kondoo.”

Wateule wa Mungu, aya hii inatangaza, watakuwa wanaomba kwa ajili ya utimizo wa maandiko haya. Unafanya nini, Ndugu, Dada? Je! Unaombea mambo haya? Au unapigana dhidi yake? Usidhubutu kusema, “Haijalishi,” kwa kuwa mwenendo kama huu wa kutoamini utakuweka nje ya Ufalme kwa hakika kama ulivyowaweka watu waalioishi kabla ya gharika nje ya safina. {2TG3: 8.1}

Aya ya 38 — “Kama kundi lililo tayari kutolewa sadaka, kama kundi la Yerusalemu katika sikukuu zake zilizoamriwa; ndivyo itakavyojazwa watu, miji ile iliyokuwa maganjo; nao watajua ya kuwa mimi ndimi Bwana.”

Je! bado kuna mashaka katika mioyo ya yeyote kati yenu? O, inawezekanaje liwepo shaka? Aya hizi, unaona, hazihitaji hakika ufafanuzi wowote. Hakuna fundisho wazi kabisa katika Bibilia. Hauwezi kuyafumba macho yako kwalo na bado utarajie kuhesabiwa kati ya waumini wa Neno la Mungu. {2TG3: 8.2}

Sasa tunaona kwamba lazima uwepo ukarabati wa nchi na upasuaji wa moyo — kwamba Ufalme wa Mungu unaanzia duniani machoni pa mataifa, kwamba utakuwa halisi kama kitu chochote, na kwamba hatakuwapo mdhambi ndani Yake, wala moyo wa jiwe ndani Yake. Je! huu sio wa kupendeza zaidi kuliko ule wa kudhani, uliofanywa wa kiroho sana, ufalme ambao huusikia mara nyingi? {2TG3: 8.3}

Eliya hakika yuaja kwanza na kurejesha mambo yote. Na mwishowe tutakuwa kile Adamu alikuwa mwanzoni, kuishi katika Bustani ya Edeni, na kula kwenye mti wa uzima. {2TG3: 8.4}

8

Itakuwa Salama Nawe

Tulia, Ee roho yangu,

Nyamaza kila hofu!

Baba yako anao uwezo mkubwa,

Naye Yu karibu daima.

 

Kamwe usinung’unikie fungu lako,

Chochote kinachoweza kutokea,

Ugonjwa au huzuni, hangaiko au uchungu,

Ni salama teule yote.

 

Mkono wa Baba wa kuadhibu

Unakuongoza;

Wala si mbali nchi ya ahadi.

Ambapo unavuma wimbo wa milele.

 

Ee, basi, nafsi yangu, tulia!

Subiri amri kuu ya mbingu;

Tafuta kufanya mapenzi ya Baba yako,

Itakuwa salama nawe.

— Thomas Hastings

9

WAZO LA SALA

Mafundisho Ya Watu Dhidi Ya Mafundisho Ya Roho

Alasiri hii nitasoma kutoka katika “Mafunzo ya Kristo Kwa Mifano,” ukurasa wa 40, aya 1 na ya 2. {2TG4: 10.1}

“… Katika mahubiri kutoka kwenye mimbari mingi ya leo hakuna udhihirisho wa uungu ambao huamsha dhamiri na kuleta uhai kwa nafsi…. Wapo wengi ambao wanamlilia Mungu aliye hai, wakitamani uwepo wa Mungu…. Liruhusu neno la Mungu linene kwa watu. Waruhusu wale ambao wamesikia mila na nadharia tu za watu na semi waisikie sauti yake Yeye ambaye neno lake linaweza kuihuisha nafsi kwa uzima wa milele. Mada pendwa ya Kristo ilikuwa upole wa baba na neema tele ya Mungu; Alizingatia sana utakatifu wa tabia Yake na sheria Yake; Alijidhihirisha Mwenyewe kwa watu kama Njia, Kweli, na Uzima. Wacha hizi ziwe mada za wachungaji wa Kristo. Wasilisha ukweli kama ulivyo katika Yesu. Fanya wazi mahitaji ya sheria na injili. Waambie watu ku-husu maisha ya Kristo ya kujikana nafsi na kafara; kudhalilishwa Kwake na kifo Chake; kufufuka Kwake na kupaa Kwake; Uombezi Wake kwa ajili yao katika nyua za Mungu; ahadi Yake, ‘Nitakuja tena, na kuwakari-bisha kwangu.’” {2TG4: 10.2}

Tunahitaji kuomba kwa ajili ya msaada kujifunza jinsi ya kufunza alivyofanya Kristo, namna ya kuthamini ma-fundisho ya Roho juu ya mafundisho ya wanadamu, na jinsi ya kuliwasilisha Neno kama Lilivyo katika Yesu, tukiuweka wazi Ukweli. Hili ndilo hitaji letu kubwa. {2TG4: 10.3}

10

WAFU NA WALIO HAI WANAJUMUISHA NYUMBA YOTE YA ISRAELI; GOGU ANAANGAMIA

ANDIKO LA HOTUBA NA V. T. HOUTEFF

MCHUNGAJI WA WADAUDI WAADVENTISTA WA SABATO

SABATO, AGOSTI 30, 1947

HEKALU LA MLIMA KARMELI

WACO, TEXAS

Mada yetu leo inapatikana katika Ezekieli, sura ya 37 hadi ya 39. Sura hizi ni ndefu, na wakati hautaturuhusu kusoma kila aya, wala kutoa maelezo mengi juu yake. Na kwa hivyo hatutajaribu kushughulikia aya zote katika sura ya 38 na 39, wala kunena yote yanayoweza kusemwa. Aya ambazo tutaacha, hata hivyo, hakika hazihitaji maelezo yoyote, maana kwa nuru hii mkononi unapojifunza sura hizi kwa mapumziko yako ukweli wake uta-jitokeza wazi. {2TG4: 11.1}

Ezek. 37: 1-12 — “Mkono wa Bwana ulikuwa juu yangu, naye akanichukua nje katika roho ya Bwana, akaniweka chini, katikati ya bonde; nalo limejaa mifupa; akanipitisha karibu nayo pande zote; na tazama, palikuwa na mifupa mingi katika ule uwanda! Nayo, tazama, ilikuwa mikavu sana. Akaniambia, Mwana-damu, je! Mifupa hii yaweza kuishi? Nami nikajibu, Ee Bwana MUNGU, wajua wewe. Akaniambia tena, Toa unabii juu ya mifupa hii, uiambie, Enyi mifupa mikavu, lisikieni neno la Bwana. Bwana MUNGU aiambia mifupa hii maneno haya; Tazama, nitatia pumzi ndani yenu, nanyi mtaishi. Nami nitatia mishipa juu yenu, nami nitaleta nyama iwe juu yenu, na kuwafunika ngozi, na kutia pumzi ndani yenu, nanyi mta-ishi; nanyi mtajua ya kuwa mimi ndimi Bwana.”

11

“Basi nikatoa unabii kama nilivyoamriwa; hata nilipokuwa nikitoa unabii, palikuwa na mshindo mkuu; na tazama, tetemeko la nchi, na ile mifupa ikasogeleana, mfupa kwa mfupa mwenziwe. Nikatazama, kumbe! Kulikuwa na mishipa juu yake, nyama ikatokea juu yake, ngozi ikaifunika juu yake; lakini haikuwamo pumzi ndani yake. Ndipo akaniambia, Tabiri, utabirie upepo, mwanadamu, ukauambie upepo, Bwana MUNGU asema hivi; Njoo, kutoka pande za pepo nne, Ee pumzi, ukawapuzie hawa waliouawa, wapate kuishi. Basi nikatabiri kama alivyoniamuru; pumzi ikawaingia, wakaishi, wakasimama kwa miguu yao, jeshi kubwa mno. {2TG4: 12.1}

“Kisha akaniambia, Mwanadamu, mifupa hii ni nyumba yote ya Israeli; tazama, wao husema, Mifupa yetu ime-kauka, matumaini yetu yametupotea; tumekatiliwa mbali kabisa. Basi tabiri, uwaambie, Bwana MUNGU asema hivi; Tazama, nitafunua makaburi yenu, na kuwapandisha kutoka katika makaburi yenu, enyi watu wangu, nami nitawaingizeni katika nchi ya Israeli.” {2TG4: 12.2}

Hapa tunaona jinsi wafu watafufuliwa: Kwanza mifupa inakusanywa pamoja mfupa kwa mfupa. Ijayo nyama inaongezwa, kisha kufunikwa na ngozi, na mwishowe wanapewa pumzi. Katika Mwanzo tunaambiwa ya kwamba mwili wa Adamu ulitengenezwa kutoka kwa udongo, kisha pumzi ilipulizwa ndani ya pua lake na aka-wa nafsi hai. Kwa kuunganisha hewa na udongo mtu huyo akawa nafsi hai. Hivyo Maandiko hufunua kwamba ufufuo ni uumbaji mpya. Mwanadamu hupokea mwili mpya kutoka kwa wa zamani lakini ili kuwa mtu yule yule aliyeishi na kufa, kisha akafanywa hai tena, yeye lazima anapewa ufahamu wa zamani wa kiakili na kumbukum-bu ya ujuzi wa maisha yake. Hakika walio hai wanajua kwamba watakufa, lakini wafu hawajui neno lolote wa-kati wote wakiwa makaburini mwao. Mhu. 9: 5, 6. {2TG4: 12.3}

12

Aya ya 13, 14 — “Nanyi mtajua ya kuwa mimi ndimi Bwana, nitakapoyafunua makaburi yenu, na ku-watoa ninyi katika makaburi yenu, enyi watu wangu. Nami nitatia roho yangu ndani yenu, nanyi mtaishi, nami nitawawekeni katika nchi yenu, nanyi mtajua ya kuwa mimi, Bwana, nimesema hayo, na kuyati-miza, asema Bwana.”

Sio tu kwamba Yeye atawafufua watu Wake kutoka makaburini mwao, lakini pia Atawaleta katika nchi ya Is-raeli. Wafu kuishi tena kwa kweli ni muujiza lakini sio mkubwa zaidi kwa mdudu kujizika ardhini au kujifunikia ndani ya kifukofuko au kama hivyo, kisha kwenda katika hali ya kukosa fahamu, abadilishe umbo lake na kuwa kipepeo mzuri akivinjari hewani badala ya kutambaa ardhini. Hili na maajabu mengine hayaonekani kama miujiza kwa sababu ni matukio ya kawaida kila siku. Iwapo mwanzoni Mungu aliumba dunia kutoka kwa sufuri, Anaweza kumuumba tena mwanadamu kwa urahisi zaidi ambapo kwa kuanza, Yeye angalau anayo mifupa ya mwanadamu na ufahamu wake wa kiakili wa mema na mabaya. {2TG4: 13.1}

Aya ya 15-19 — “Neno la Bwana likanijia tena, kusema, Na wewe mwanadamu, twaa kijiti kimoja; ukaandike juu yake, Kwa Yuda, na kwa wana wa Israeli wenzake; kisha, twaa kijiti cha pili; ukaandike juu yake, Kwa Yusufu, kijiti cha Efraimu, na kwa nyumba yote ya Israeli wenzake; ukaviunge pamoja kwa ajili yako hiki na hiki viwe kijiti kimoja, viwe kimoja katika mkono wako. Na wana wa watu wangu watakapokuambia, wakisema, Je! Hutatuonyesha maana ya mambo hayo utendayo? Waambie, Bwana MUNGU asema hivi; Tazama, nitakitwaa kijiti cha Yusufu, kilicho mkononi mwa Efraimu,

13

na kabila za Israeli wenzake, nami nitawaweka pamoja nacho, yaani, pamoja na kijiti cha Yuda, na kuvi-fanya kuwa kijiti kimoja; navyo vitakuwa kimoja mkononi mwangu.”

Hapa tunaambiwa wazi wazi kwamba falme mbili za zamani, mifano, Yeye atazirejesha na kuziunganisha — na kwa hivyo kuleta uakisi. {2TG4: 14.1}

Aya ya 20, 21 — “Navyo vijiti, ambavyo uliandika juu yake, vitakuwa mkononi mwako mbele ya macho yao. Ukawaambie, Bwana MUNGU asema hivi; Tazama, nitawatwaa wana wa Israeli toka kati ya ma-taifa walikokwenda, nami nitawakusanya pande zote, na kuwaleta katika nchi yao wenyewe.”

Waaminifu kutoka kwa wazawa wa Israeli ambao walitapanywa katika mataifa yote, tunaambiwa kwa dhati, watakusanywa na kurejeshwa katika nchi yao. Wazawa hawa wa kabila za Yakobo hatupaswi hata hivyo kupotosha kwamba ni Wayahudi wa leo wasioamini ambao wanajaribu kupata umilki wa Palestina. Ufalme uliotabiriwa hapa, unakumbuka, utajumuishwa tu na waongofu kwa Kristo kutoka kwa zile kabila ambao walit-apanywa na kupotelea kati ya nchi za Mataifa, pamoja na wazawa wa wale waliojumuisha kanisa la Kikristo la kwanza, — ambao hawakujiita tena Wayahudi, ila Wakristo. Hawa, mbali na wale wa nchi za Mataifa ambao wa-tajiunga na Kristo, ni bila shaka watakaoujumuisha Ufalme huu wa kabla ya millenia katika Nchi ya Ahadi. {2TG4: 14.2}

Aya ya 22 — “Nami nitawafanya kuwa taifa moja katika nchi hiyo, juu ya milima ya Israeli; na mfalme mmoja atakuwa mfalme wao wote; wala hawatakuwa tena mataifa mawili, wala hawatagawanyikana kuwa falme mbili tena, hata milele.”

14

Faraja hii, unakumbuka, ni ya kudumu. Na kwa sabbu hamna wadhambi ndani Yake, ni dhahiri, kama il-ivyoonyeshwa mahali pengine kwenye machapisho yetu, ni tokeo la “Hukumu katika nyumba ya Mungu” (1 Pet. 4:17) — Hukumu ya Walio hai, utakaso wa kanisa, utengo wa samaki wabaya kutoka kwa wazuri (Mat. 13: 47, 48), kutakaswa kwa patakatifu (Dan. 8: 14) — mavuno ya malimbuko: watu 144,000 wanaosimama juu ya Mlima Zayuni na Mwana-Kondoo (Ufu. 14: 1) — “masalia.” Kisha unafuata kukusanywa ndani kwa mavuno ya pili. {2TG4: 15.1}

Maarifa yenu ya mambo haya, hata hivyo, hayatawafaidisha iwapo hamtafanya juhudi za kufa na kupona kuwa mmoja wa, au mmoja pamoja na watu 144,000. Ninyi, zaidi ya hayo, lazima muwe na mafuta haya ya ziada katika vyombo vyenu (Mat. 25: 1-12) sasa ambapo yanasambazwa bila gharama. Kuyapata baadaye haya-tawafaidisha, kwa maana watakaokuja wamechelewa watapata mlango umefungwa. Kubisha kwao mlangoni kutawasababisha wasikie tu Mwalimu akisema, “Ondokeni kwangu,” “Sikuwajua ninyi.” (Mat. 7:23). Hakika, lazima mjipatie mafuta haya ya kutoa nuru sasa ambapo Inaletwa milangoni mwenu iwapo Itawandea mema yoyote. {2TG4: 15.2}

Aya ya 23 — “Wala hawatajitia unajisi tena kwa vinyago vyao, wala kwa vitu vyao vichukizavyo, wala kwa makosa yao mojawapo; lakini nitawaokoa, na kuwatoa katika makao yao yote, ambayo wamefanya dhambi ndani yake, nami nitawatakasa; basi watakuwa watu wangu, nami nitakuwa Mungu wao.”

Baada ya raia wa falme za Yuda na Israeli kukusanywa kutoka katika nchi za mataifa na wao wenyewe kuwa taifa na ufalme “wakati huo” watatakaswa, na sio kabla yanena Maandiko. Kutoka kwa haya unaona kwamba hii ndio kazi

15

ya kupatakasa Patakatifu (Dan. 8: 14), utakaso wa kanisa (“Shuhuda,” Gombo la 5, uk. 80) — kulisafisha hekalu (Mal. 3: 1-3) — wakati wa mavuno kuzifuta dhambi na kasoro za waliotubu na kuwaondolea mbali ambao ha-wakutubu. Ni Hukumu ya Walio Hai ambayo inalisafisha kanisa. Inalitenga kutoka kwa ulimwengu, na kuli-wezesha lifae kwa ajili ya kuwakusanya watu (Ufu. 18: 4) — kulifanya liwe safina ya leo, mahali pa kimbilio kwa wote wanaotaka kuokoka mapigo. Baada ya hapo watakatifu wanadumu kuwa wasafi. Hawatendi dhambi tena. Wao ni watu wasafi na waaminifu wa Mungu milele. Haujawahi kamwe, kwa hivyo, kuja kwa watu wa Mungu ujumbe muhimu zaidi kuliko huu. {2TG4: 15.3}

Aya ya 24-28 — “Na mtumishi wangu, Daudi, atakuwa mfalme juu yao, nao wote watakuwa na mchungaji mmoja; nao wataenenda katika hukumu zangu, na kuzishika amri zangu, na kuzitenda. Nao watakaa katika nchi niliyompa Yakobo, mtumishi wangu, walimokaa baba zenu; nao watakaa humo, wao na watoto wao, na watoto wa watoto wao, milele; na Daudi, mtumishi wangu, atakuwa mkuu wao milele. Tena nitafanya agano la amani pamoja nao; litakuwa agano la milele pamoja nao; nami nitawaweka na kuwazidisha, na patakatifu pangu nitapaweka katikati yao milele. Tena maskani yangu itakuwa pamoja nao; nami nitakuwa Mungu wao, nao watakuwa watu wangu. Na mataifa watajua ya kuwa mimi ndimi Bwana, mimi niwatakasaye Israeli, pa-takatifu pangu patakapokuwa katikati yao milele.”

Kwa udhahiri, basi, mambo haya yote yanatukia mbele ya mataifa ili wapate kuona na kujua kile Mungu amewafanyia watu Wake. Hivyo watajua kuwa Yeye amewapenda. {2TG4: 16.1}

16

Ezek. 38: 1, 2 — “Neno la Bwana likanijia, kusema, Mwanadamu, kaza uso wako, umwelekee Gogu, wa nchi ya Magogu, mkuu wa Roshi, Mesheki, na Tubali, ukatabiri juu yake.”

Gogu hapa anasemekana kuwa mkuu, mfalme wa Mesheki na Tubali. Miji hii miwili, Mesheki na Tubali za-mani ilikuwa katika Asia, kusini mwa Bahari Nyeusi, ambapo Ufalme wa Uturuki upo sasa. {2TG4: 17.1}

Aya ya 8 — “Na baada ya siku nyingi utajiliwa; katika miaka ya mwisho, utaingia nchi iliyorudishiwa hali yake ya kwanza, baada ya kupigwa kwa upanga, iliyokusanywa toka kabila nyingi za watu, juu ya milima ya Israeli, iliyokuwa ukiwa wa daima; lakini imetolewa katika kabila za watu, nao watakaa salama salimini wote pia.”

“Siku nyingi” ambazo baadaye Gogu anajiliwa ni miaka elfu. Siku za mwisho ambazo Israeli wanarejea katika nchi yao, na wakati ambapo Gogu atakwenda kupingana nao ni kabla ya millenia. {2TG4: 17.2}

Aya ya 9 — “Nawe utapaa juu, utakuja kama tufani, utakuwa kama wingu kuifunika nchi, wewe, na vikosi vyako vyote, na kabila nyingi za watu pamoja nawe.”

Usemi, wa “kupaa, na kuja kama tufani,” hupendekeza kwamba mambo haya yatatukia katika wakati wa ndege. {2TG4: 17.3}

Aya ya 10-12 — “Bwana MUNGU asema hivi; Itakuwa katika siku hiyo, mawazo yataingia moyoni mwako, nawe utakusudia kusudi baya; nawe utasema, Nitapanda juu niiendee nchi yenye vijiji visivyo na maboma; nitawaendea watu wanaostarehe, wanaokaa salama, wote wakikaa pasipo kuta, ambao hawana makomeo wa-la malango; ili kuteka mateka, na kuwinda mawindo;

17

uugeuze mkono wako juu ya mahali palipoharibika, ambapo sasa panakaliwa na watu, na juu ya watu wali-okusanyika toka mataifa, waliopata ng’ombe na mali, wakaao katikati ya dunia.”

Kwa sababu nchi ya Israeli haitakuwa na kinga yoyote inayoonekana ya mwanadamu, itaonekana kwa Gogu kwamba hatakuwa na ugumu kuwanyag’anya watu nchi hiyo. {2TG4: 18.1}

Aya ya 13 — “Sheba, na Dedani, na wafanya biashara wa Tarshishi, pamoja na wana-simba wake wote, wa-takuambia, Je! Umekuja kuteka mateka? Umekusanya jeshi lako, ili kuwinda mawindo? Kuchukua fedha na dhahabu, kuchukua ng’ombe na mali, kuteka mateka mengi sana?”

Nchi hizi jirani na watu wanaomwuliza Gogu kuwaambia kazi yake, kwa wazi hawashirikiani naye. {2TG4: 18.2}

Aya ya 14-17 — “Basi, mwanadamu, tabiri, umwambie Gogu, Bwana MUNGU asema hivi; Katika siku ile wa-tu wangu, Israeli, watakapokaa salama, hutapata habari? Nawe utakuja kutoka mahali pako, kutoka pande za mwisho za kaskazini, wewe, na watu wa kabila nyingi pamoja nawe, wote wamepanda farasi, kusanyiko kubwa, na jeshi kuu; nawe utapanda juu uwajilie watu wangu, Israeli, kama wingu kuifunika nchi; itakuwa katika siku za mwisho, nitakuleta upigane na nchi yangu, ili mataifa wanijue, nitakapotakaswa kwako, Ewe Gogu, mbele ya macho yao. Bwana MUNGU asema hivi; Je! Wewe ndiwe niliyemnena zamani za kale, kwa vinywa vya watumishi wangu, manabii wa Israeli, waliotabiri siku zile kwa muda wa miaka mingi, ya kwamba nitakuleta upigane nao?”

18

Ni wazi, Ufalme huu wa Israeli unasimamishwa katika siku za mwisho, katika siku za kabla ya millenia, kwa maana baada ya Ufalme kusimamishwa, Gogu anaanzisha vita dhidi Yake. Hakika, hili haliwezi kuwa baada ya millenia, maana wakati huo mataifa yote kutoka pembe nne za dunia, Gogu na Magogu pamoja nao, watauzun-guka, sio milima ya Israeli, ila Yerusalemu mpya. Zaidi ya hayo kwa wakati huo watakaouawa hawatazikwa bali watachomwa wawe majivu (Ufu. 20: 9, 10; Mal. 4: 1). {2TG4: 19.1}

Aya ya 23 — “Nami nitajitukuza, na kujitakasa, na kujidhihirisha, mbele ya macho ya mataifa mengi; nao wa-tajua ya kuwa mimi ndimi Bwana.”

Ezek. 39: 1-7 — “Na wewe, mwanadamu, tabiri juu ya Gogu, useme, Bwana MUNGU asema hivi, Tazama, mimi ni juu yako, Ewe Gogu, mkuu wa Roshi, Mesheki, na Tubali; nami nitakugeuza na kukuongoza, nami nitakupandisha toka pande za mwisho za kaskazini; nami nitakuleta juu ya milima ya Israeli; nami nitaupiga upinde wako, utoke katika mkono wako wa kushoto, na mishale yako nitaiangusha, itoke katika mkono wako wa kulia. Utaanguka juu ya milima ya Israeli, wewe, na vikosi vyako vyote, na watu wa kabila nyingi walio pamoja nawe; nami nitakutoa na kuwapa ndege wa kila namna walao nyama, na wanyama wa nchi, uliwe na wao. Utaanguka katika uwanda; kwa maana mimi nimenena neno hili, asema Bwana MUNGU. Nami nitapele-ka moto juu ya Magogu; na juu ya watu wote wakaao salama katika visiwa; nao watajua ya kuwa mimi ndimi Bwana. Na jina langu takatifu nitalifanya kuwa limejulikana kati ya watu wangu Israeli; wala sitaliacha jina langu takatifu kutiwa unajisi tena; nao mataifa watajua ya kuwa mimi ndimi Bwana, na Aliye Mtakatifu kati-ka Israeli.”

Gogu, unaona, atashindwa kuwanyang’anya watu wa Mungu. Badala yake ataangamia katika milima ya Is-raeli. {2TG4: 19.2}

19

Aya ya 8-15 — “Tazama, linakuja, nalo litatendeka, asema Bwana MUNGU; hii ndiyo siku ile niliyoinena. Hao wakaao katika miji ya Israeli watatoka, nao watafanya mioto kwa silaha za vita na kuziteketeza, ngao, na vigao, na pinde, na mishale, na mafumo, na mikuki, nao watazitumia kama kuni kwa muda wa miaka sa-ba; hata hawataokota kuni mashambani, wala hawatakata kuni msituni; maana watafanya mioto kwa silaha zile; nao watawateka nyara watu waliowateka wao, na kunyang’anya vitu vya watu walionyang’anya vitu vyao, asema Bwana MUNGU. Tena, itakuwa katika siku hiyo, nitampa Gogu pa kuzikia katika Israeli, bonde la wapitao, upande wa mashariki wa bahari; nalo litawazuia wapitao; na huko watamzika Gogu na watu wake jamii yote; nao wataliita, Bonde la Hamon-Gogu. Na kwa muda wa miezi saba nyumba ya Israeli watakuwa wakiwazika, wapate kuisafisha nchi. Naam, watu wote wa nchi hiyo watawazika; itakuwa ni sifa kwao katika siku ile nitakapotukuzwa, asema Bwana MUNGU. Nao watawachagua watu wa kufanya kazi ya daima, wa-takaopita kati ya nchi, ili kuwazika waliosalia juu ya uso wa nchi, ili kuisafisha; miezi saba itakapokwisha kupita watatafuta. Na hao wapitao kati ya nchi watatafuta; na mtu ye yote aonapo mfupa wa mtu, ndipo atakapoweka alama karibu nao, hata wazishi watakapouzika katika bonde la Hamon-Gogu.”

Kwa sababu aya hizi hazihitaji maelezo, tunapita hadi kwa {2TG4: 20.1}

Aya ya 22-29 — “Basi, nyumba ya Israeli watajua ya kuwa mimi ndimi Bwana, Mungu wao, tangu siku hiyo na baadaye. Nao mataifa watajua ya kuwa nyumba ya Israeli walihamishwa, na kwenda kifungoni, kwa saba-bu ya uovu

20

wao; kwa sababu waliniasi, nami nikawaficha uso wangu; basi nikawatia katika mikono ya adui zao, nao wakaanguka kwa upanga, wote pia. Kwa kadiri ya uchafu wao, kwa kadiri ya makosa yao, ndivyo nil-ivyowatenda, nami nikawaficha uso wangu. Kwa sababu hiyo, Bwana MUNGU asema hivi, Sasa nitawarejeza watu wa Yakobo waliohamishwa, nitawahurumia nyumba yote ya Israeli; nami nitalionea wivu jina langu ta-katifu. Nao watachukua aibu yao, na makosa yao yote walioniasi, watakapokaa salama katika nchi yao wenyewe, wala hapana mtu atakayewatia hofu; nitakapokuwa nimewaleta tena kutoka kabila za watu, na ku-wakusanya kwa kuwatoa katika nchi za adui zao, na kutakaswa kati yao mbele ya macho ya mataifa mengi. Nao watajua ya kuwa mimi ndimi Bwana, Mungu wao, kwa kuwa naliwahamisha, waende utumwani kati ya mataifa, na mimi nikawakusanya, na kuwaingiza katika nchi yao wenyewe; wala sitawaacha tena huko kamwe, hata mmojawapo; wala sitawaficha uso wangu tena; kwa maana nimemwaga roho yangu juu ya nyumba ya Israeli, asema Bwana MUNGU.”

Sijui sura yoyote katika Bibilia iliyo wazi zaidi kuliko sura hizi za Ezekieli. Hazihitaji ufafanuzi kwa vyovyote. Lakini licha ya hayo Dhehebu huzipuuza kana kwamba hazipo katika Bibilia. Na hata sasa, badala ya kufundisha utimizo wa hivi karibuni wa sura hizi, kusimamishwa kwa Ufalme, wachungaji wanatenda yote wanayoweza kuwapotosha walei na kuyazongazonga Maandiko kwa fumbo! Kwa hivyo upo ushahidi juu ya ushahidi kwamba malaika wa kanisa la Laodekia ni kipofu, lakini bado hajui. {2TG4: 21.1}

Sasa kwenye hii njia panda, hatima ya milele ya watumwa wote wa Mungu inapaswa kutatuliwa. Sasa lazima wachukue aidha hatua ambayo Paulo alilazimika kuchukua njiani

21

akielekea Dameski, au hatua ambayo Yuda alichukua katika chumba cha juu baada ya Mwalimu kumtawadha miguu. Hii ni, unaona, sio unenaji wa mwanadamu; ni wa Mungu, wa Bibilia. {2TG4: 21.2}

Sasa umepewa fursa ya kuwa Danieli, Ayubu, Stefano, Luther, Miller, au White. Natumai kwamba hakuna mtu kati yenu atachagua kuwa mwandishi au Mfarisayo. Walikuwa werevu wa kutafuta kosa, lakini wapumbavu sana kuuona Ukweli. Kama hawa unajua hawajawahi kumuongoza mtu yeyote kwenye Kweli, lakini daima wamewaweka hata mataifa yote mbali Nayo. Ni werevu katika taaluma yao ya uovu. {2TG4: 22.1}

Usiyakose Manufaa Juu Ya Hili

Iwapo haujatuma kwa ajili ya nakala yako iliyotangazwa na iliyojadiliwa sana kijitabu cha afya cha kurasa 96 (“Kabari Inayoingia”) ambacho kimefanya uamsho mkubwa katika dunia ya Waadventista na ambacho kimeli-weka Shirika la K.I. katika mwangaza, usikikose iwapo afya, nyumba, na furaha yako inamaanisha kitu kwako. Kwa maoni yetu kitabu hiki ndicho bora hatujawahi kuona juu ya su-ala hili. Kwa kweli tunahisi kwamba ki-metumwa na Mungu, na kwamba nakala yake inapaswa kuwa katika kila nyumba. Tumejulishwa kwamba sasa unaweza kukipata bila kuagizia. Tuma jina lako, anwani, na jina la kanisa ambalo wewe ni mshiriki (unaombwa kuchapisha), na senti 15 kwa sarafu au stempu kwa Shirika La Kabari Inayoingia La Marekani, Kituo cha Mlima Karmeli, Waco, Texas, Marekani na kitatumwa kwako. {2TG4: 22.2}

22

Wingu na Moto

Kama zamani wakati majeshi ya Israeli

Walilazimishwa nyikani kukaa,

Wakimwamini Mungu wao kuongoza njia

Kwa nuru kamili ya siku.

 

Huku na huko kama meli isiyo na tanga,

Sio dira ya kuwaongoza kupitia bonde,

Bali ishara ya Mungu wao ilikuwa karibu daima.

Hivyo mioyo yao ikizimia kuchangamshwa.

 

Siku zote za kutanga-tanga kwao walilishwa

Hadi kwa nchi ya ahadi waliongozwa;

Kwa mkono wa Bwana, kwa uongozi hakika,

Wakaletwa pwani ya Kanaani.

 

Hivyo ishara ya moto usiku,

Na ishara ya wingu mchana,

Ikipaa juu, mbele tu,

Wanaposafari njiani mwao,

Itakuwa mwelekezi na kiongozi,

Mpaka tupite nyikani,

Maana Bwana Mungu wetu Katika wakati Wake mwema

Ataongoza kwenye nuru mwishowe.

–C. A. Miles

23

Jumuiya ya Wadaudi Waadventista wa Sabato

(Ushirika Huru Unaojumuisha Kanisa)

Mlima Karmeli, Waco, Texas

S.L.P. 23738, Waco, TX 76702

+ 1-254-855-9539

www.gadsda.com

info@gadsda.com

Gombo la 2, Namba 3, 4

Kimechapishwa nchini Marekani

24

>